Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104803 articles
Browse latest View live

Penny: Natamani Mtoto lakini sina wa Kuzaa nae

$
0
0
Aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ Penniel Mwingilwa amesema sasa anatamani kuzaa lakini tatizo lipo kwa mwanaume wa kuzaa naye.

Penny alitoa tamko hilo baada ya Diamond kunukuliwa jana (Alhamisi) na gazeti la Amani kuwa, alimpa mimba mara mbili binti huyo lakini zikayeyuka katika mazingira ya kutatanisha.

Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni Penny alisema, sasa hivi anapomuona mtoto anachanganyikiwa na kujikuta akitamani naye kuitwa mama hivyo akimpata mwanaume sahihi wa kutimiza ndoto yake hiyo hatafanya ajizi

Kiukweli sasa ndiyo ule wakati wa kuzaa, natamani sana mtoto lakini sasa wa kuzaa naye yuko wapi? Hapo ndiyo tatizo maana siyo kuzaa na mtu ili mradi mtoto awe na baba,” alisema Penny.

URAIS:January Makamba awaita wasanii wa Bongo Movie Serena Hotel leo

$
0
0
Katika hali ya kushangaza, naibu waziri wa Sayansi na Teknolojia January Makamba amewaandalia chakula cha jioni wasanii wa Bongo Movie leo jumatatu usiku Serena Hotel, imefahamika. Mualiko huo unaoratibiwa kwa karibu na msanii JB, unatarajiwa kuambatana na maombi ya bwana Makamba kwa wasanii wamuunge mkono katika ndoto yake ya Urais 2015. Kila msanii atakayeshiriki ameandaliwa bahasha maalum ya pesa za Xmas na Mwaka Mpya 2015. 

Baadhi ya wasanii wanatajwa kutumika kuvuta pesa kutoka kwa wagombea zaidi ya mmoja, wakitumia mchakato wa Urais kama mwanya wa kujipatia pesa za bila jasho. JB anatajwa pia kuwa mtu wa karibu wa Edward Lowassa, hivyo kuzua sintofahamu juu ya ushiriki wake katika kuwashawishi wasanii wenzie wa Bongo Movie kukutana na kumuunga mkono January Makamba. 
Hongereni wasanii kwa kutumia vema fursa.

Mke wa Mtu Adakwa Akijiuza Mitaani, Adai Anatafuta Pesa ya Christmas

$
0
0
Stori: Dustan Shekidele, Morogoro 
Ni aibu iliyoje! Tabia ya wanawake kujiuza kwa kisingizio cha kusaka fedha kwa ajili ya Sikukuu ya Krismasi imewatokea puani wanawake zaidi ya kumi akiwemo mke wa mtu baada ya kunaswa mawindoni na kutiwa nguvuni.

Tukio hilo la aibu lilitokea katika msako maalum wa polisi waliotoa kolabo kwa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers, uliofanyika katika eneo ‘korofi’ la ltinga, Msamvu Kata ya Mwembesongo mkoani hapa, wikiendi iliyopita.

Awali, Kamanda wa OFM mkoani hapa alipokea malalamiko lukuki kutoka kwa wananchi waishio jirani na eneo hilo waliokuwa wakiwalalamikia wanawake hao kugeuza vibanda vyao vya simu kuwa gesti na kuvitumia kufanyia ngono usiku na kuzagaa kwa kondom kila sehemu.

Kabla ya msako, OFM iliwashauri kupeleka malalamiko hayo kwenye serikali ya mtaa na polisi.
Kabla ya kufanya oparesheni hiyo, shushushu wetu alifanya upelelezi na kubaini kwamba ni kweli wanawake hao huvitumia vibanda hivyo kama gesti.

Baada ya kujiridhisha, OFM na jeshi la polisi walipofika eneo hilo majira ya saa 5:00 usiku na kuwanasa wanawake hao kisha kuwasukumiza kwenye difenda na kwenda kuwasweka lupango kusubiri sheria ichukue mkondo wake.

Katika hali ya kushangaza, mmoja wa wanawake hao alikuwa akiomba msamaha kwa madai kwamba ni mke wa mtu hivyo mumewe akijua ishu hiyo atamtoa roho.
“Jamani mimi ni mke wa mtu, mume wangu alivyo mkali akijua nimekutwa huko atanimaliza,” alisikika mwanamke huyo.
GPL

Moshi Ndio Habari ya Mjini Week Hii..Jionee Umati wa Wasafiri Stand Kuu ya Mabasi ya Mikoani Ubungo

$
0
0
Wiki hii ya Christmas Pale Ubungo stand kuu ya Mabasi ya kwenda Mikoani Hapatoshi, Wasafiri ni wengi kweli Hasa wa Kwenda Mkoa wa Moshi kama ilivyokuwa Kawaida ya Wachaga kipindi hiki cha sikukuu hukitumia kwenda kusalimia Ndugu na Jamaa Huko kwao ....Mbuta Nanga..Ruwa Mangi

Profesa Tibaijuka Kufukuzwa Kazi..Rais Asema Atupe Nafasi , Prof Muhongo Awekwa Kiporo

$
0
0
Leo Rais Kikwete Akiwa anahutubia Wazee wa Dar es Salaam Amesema Kutokana na Sakata La IPTL Amemwambia Prof Anna Tibaijuka Awape Nafasi waweze kuchagua Mtu mwingine katika nafasi yake Serekalini kwa kukiuka maadili ya uongozi Baada ya kupokea Pesa nyingi kwenye account yake na kuzitumia huku akijua ni fedha zenye utata mkubwa..Awali Pro Tibaijuka alitangaza kwa waandishi wa habari kuwa hawezi kujiuzulu kwa swala hilo..

Pia Rais Amesema Kuhusu Profesa Muhongo Amemuweka kiporo ila ndani ya siku mbili hizi atatoa Maamuzi yake

Je una Maoni yoyote kuhusu Kauli hizo za Jakaya Kikwete?

Majanga Mwisho wa Mwaka: Ndege Nyingine Yapotea Ikiwa na Abiria 162

$
0
0
NDEGE ya AirAsia, QZ8501 iliyokuwa na watu 162 ikitokea Indonesia kwenda Singapore imepoteza mawasiliano leo asubuhi.

Kati ya watu hao 162, abiria walikuwa 155, marubani 2 na wafanyakazi wa ndege hiyo 5. Watu 157 ni raia wa Indonesia, 3 raia wa Korea Kusini, 1 kutoka Malaysia na 1 raia wa Singapore.

Imeelezwa kuwa kabla ya ndege hiyo kupoteza mawasiliano, rubani aliomba kubadili uelekeo wa kawaida kutokana na hali mbaya ya hewa.

Ndege hiyo ilifanyiwa matengenezo kwa mara ya mwisho Novemba 16, 2014 kama ilivyokuwa imepangwa.

Rubani wa ndege hiyo ana uzoefu wa saa 6,100 angani huku msaidizi wake akiwa na uzoefu wa saa 2,275.
Miongoni mwa abiria 155 waliokuwa kwenye ndege hiyo, 138 ni watu wazima, 16 watoto na 1 mama mjamzito.

QZ8501 imetoka Indonesia saa 11: 27 alfajiri na ilitarajiwa kuwasili Singapore saa 2:37 asubuhi.

Thea: Hatuvai Vimini Kusaka Mabwana, Vimini ni ‘Kiki’ tu ya Mjini

$
0
0
MWIGIZAJI Ndumbagwe Misayo maarufu kama Thea, amesema wasanii huvaa sketi fupi ‘vimini’ wakilenga kwenda na wakati na si kujipitisha mbele ya wanaume.

Thea aliiambia Mwanaspoti, kuwa ni kama wanatekeleza wimbo wa mwanamuziki Bwana Misosi ‘Nitoke Vipi’, lakini haimaanishi kwamba wavaaji wote ni wahuni.

“Vimini ni ‘kiki’ tu mjini, watu wengi wanaamini ni sehemu mojawapo ya uvaaji au Nitoke Vipi kama Bwana Misosi alivyosema. Kuna watu wanaamini waigizaji tunaovaa au wanaovaa vimini wanafanya hivyo ili kutafuta biashara, ukweli ni kwamba hakuna kitu kama hicho, kama wapo basi ni kumi kwa mmoja,” alisema Thea.

“Vimini ni ‘kiki’ tu ya mjini. Watu wanaweza kununua filamu kwa sababu wanataka kuona paja la mtu Fulani. Hapo unakuwa umeuza filamu si mwili.”

Muimbaji wa nyimbo za injili Rose Muhando Katika Utapeli Mwingine Siku ya X-Mass

$
0
0
Habari zilizoenea kwenye magazeti na mitandao ni kwamba Muimbaji wa nyimbo za injili Rose Muhando safari hii amemtapeliAlex Msama baada ya kupokea fedha kwa makubaliano ya kushiriki Tamasha la Krismasi kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa lakini siku ya tukio, Ijumaa iliyopita, mwanadada huyo hakutokea!
“Hii ni mara ya pili, kwenye uzinduzi wa albamu ya msanii John Lisu pale Diamond Jubilee (Dar), Rose alipokea shilingi milioni moja kutoka kwa Msama lakini siku ya uzinduzi hakutokea. Kusema ukweli huu utapeli wa Rose wa kuchukua fedha za watu halafu hatokei sasa imekuwa too much. Nimesikia habari kwamba ameogopa kutokea uwanjani hapa ambako tamasha lilifanyika kwa kuhofia mimba yake kuonekana maana kwa sasa ni kubwa.” Kimesema chanzo hicho cha habari
Una lipi la kumwambia Rose juu ya jambo hili? na unalizungumziaje jambo hili?

Sugu 'Tanzania Nchi Pekee Haijashusha Bei ya Mafuta'

$
0
0
Tanzania ndiyo nchi pekee ambayo bado inayowauzia wananchi wake mafuta kwa bei ya juu licha ya kuwa bei ya mafuta katika soko la dunia kushuka kwa Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi ameyasema hayo wakati akiongea na Wananchi wa Halmashauri ya mamlaka ya mji mdogo wa Kyela na kusema kuwa kumekuwepo na bei kubwa ya mafuta nchini ikilinganishwa na nchi nyingine.
Mh. Mbilinyi, amedai kuwa bei hiyo ya mafuta ni kubwa ukilinganisha na nchi nyingine duniani ambazo gharama za mafuta imeshuka zaidi ya nusu kutoka na kupatika kwa wingi kwa bidhaa hiyo kwa sasa duniani.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mbeya, Joseph Mwachembe maarufu kwa jina la China amesema kuwa katika maeneo ambayo Chadema imeshinda kuongoza serikali za mitaa na vijiji, viongozi wake watafanya kazi kwa kuzingatia matakwa ya wananchi na sio maelekezo kutoka serikali ku.
Nao viongozi wa Ukawa mkoani Mbeya wamesema kuwa muungano wa vyama vinavyounda umoja huo umeonesha mafanikio makubwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na moto huo huo utaendelea mpaka kwenye uchaguzi mkuu ujao. ya asilimia 50.


Hili ni Fundisho Kwa Wanaume Wanaopenda Kutongoza Kila Mwanamke, Ona Kilichomtokea Huyu Jamaa

$
0
0
Hii ni fundisho tosha kwa wanaume mnaopenda kutongoza tongoza kila wanamke : huyo jaama kilicho mtokea baada ya kutongoza ni hicho hapo mkionacho kwenye picha , badilikeni siyo kila mwanamke ni wakumtongoza tu mtakuja kukutana na mashetani shauri yenu.....!!

Mtoto wa Miezi Mitatu Awa Mwathirika Dawa za Kulevya

$
0
0
Mtoto mwenye umri wa miezi mitatu, mkazi wa Buza, Dar es Salaam amebainika kuwa mwathirika wa dawa za kulevya.

Damu na mkojo vya mtoto huyo (jina tunalihifadhi) vilichukuliwa na kupimwa katika maabara ya Hospitali ya Mwananyamala na baada ya saa mbili, majibu yalitoka na kuthibitisha kwamba alikuwa na chembechembe za dawa za kulevya aina ya heroini.

Taarifa za kitabibu zinaonyesha kuwa kuwapo kwa heroini mwilini mwa mtu, huweza kuonekana katika mkojo ndani ya siku mbili hadi nne iwapo dawa hizo zilitumiwa na mhusika kwa kati ya saa mbili hadi tano.

Hatua ya kumfanyia vipimo mtoto huyo wa kiume, inatokana na jitihada za gazeti hili kutaka kufahamu jinsi utumiaji wa dawa za kulevya kwa wanawake wajawazito na wale wanaonyonyesha unavyoweza kumwathiri mtoto akiwa tumboni au anayenyonya maziwa ya mama mwathirika.

Mtaalamu wa tiba katika Hospitali ya Mwananyamala, Dk Elifasi Mritu anasema: “Ni kweli ukitumia dawa za kulevya wakati unanyonyesha au wakati wa mimba, mtoto naye huathirika.”

Kauli ya Dk Mritu ambaye ni daktari katika kitengo cha tiba ya methadone hospitalini hapo, inaungwa mkono na Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Akili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Frank Mushi ambaye anasema mama anayetumia dawa za kulevya akiwa mjamzito humwathiri pia mtoto.

Mama wa mtoto azungumza

Mama wa mtoto, Zena maarufu Zerish, mkazi wa Yombo Buza alikiri kwamba alipata ujauzito wakati akitumia dawa za kulevya na kwamba hadi sasa anavuta dawa hizo huku akiendelea kumnyonyesha mtoto huyo.

Anasema baada ya kujifungua hakukaa ndani kwa siku 40 kama wafanyavyo wanawake wengi wa Kitanzania, kwa sababu mwili wake ulikuwa unahitaji ‘unga’ vinginevyo hali yake huwa mbaya.

Anasema baada ya kujifungua alianza kuzunguka huku na kule akiwa na mtoto mgongoni, huku akiwa amebeba mfuko wake wa plastiki wenye mahitaji muhimu ya mtoto kama nepi na nguo.

Anasema anapovuta au kujichoma dawa, mtoto wake pia hupata ‘stimu’ kwa sababu hupata dawa hizo za kulevya kupitia maziwa anayonyonya na hivyo wote wawili kulala fofofo sehemu yoyote ile.

Hata hivyo, kwa Zerish na mwanaye, anapofikia hali ya kuwa ‘alosto’ (wakati dawa za kulevya zinapoisha mwilini na hivyo kuhitaji tena), huwa ni adhabu kali mno.Anasema dawa zinapoisha mwilini na mtoto naye huwa katika hali hiyo na hivyo hulia sana. Hali hiyo humfanya akimbie kutafuta dawa ili ‘kujinusuru’ yeye na mwanaye.

Uwezekano wa tiba

Dk Mushi anasema watoto wanaoathirika kwa dawa kupitia mama zao, hulia sana na kujinyonganyonga hali inayoashiria wanapata maumivu ya tumbo.

“Lakini tumaini lipo kwa watoto hao, kwani hupewa dawa aina ya morphin ambayo hukata ulevi huo taratibu. Baada ya muda hupona kabisa,” anasema.

Hata hivyo, alisema iwapo mtoto ataendelea kunyonya maziwa bila kupata tiba huku mama naye akitumia dawa hizo, huweza kuwa mtumiaji wa dawa hadi anapokuwa mkubwa.

Katika hospitali za Muhimbili na Mwananyamala, wanawake wenye watoto walio na uraibu wa dawa za kulevya hutakiwa kuhudhuria kliniki kila siku bila kukosa.

Mwanamke anayetumia dawa za kulevya hutibiwa kwa dawa aina ya methadone na mtoto hupewa morphin.

Check Hii Video Mvua ilivyodhalilisha Uwanja wa NDEGE Dar Salaaam ...Wavuja Kinomaa

$
0
0
Aibu Kubwa Imetokea Katika Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere Dar  baada ya Mvua Kubwa Anayonyesha Kuvuja Ndani ya Sehemu ambapo Abiria wa Mataifa mbali Mbali ukaguliwa Tickets zao Kabla ya kuingia Kwenye ndege, tukio hilo limeshuhudiwa na Raia mbali Mbali Kutoka nchi tofauti waliokuwa wakifanya ukaguzi waTickets zao..

Angalia Video ya Aibu Hapa:

Lisemwalo:Mahusiano ya Wastara na Bond

$
0
0
Tukiwa tunaelekea kuumaliza mwaka huu wa 2014 niameona sio mbaya nikawapa ubuyu huu, wa kile kinachodaiwa kuwa mwigizaji wa filamu za hapa bongo, Wastara Juma sasa hivi anatoka na mtangazaji na mwigizaji Bond Bin Sinnan.

Mbali na wawili hawa kuwa na mahusiano ya kizazi, kwani walishaigiza pamoja filamu kama “Uamini Fudhaifu” iliyotoka mwaka huu ambayo ina dhima ya mapenzi na vichekesho, inasemekana  kwamba wawili hawa wameshavuka mstari na kutengeneza mausianao ya mtu na mpenzi wake.

Mitandaoni

Madai haya ya wawili hawa kuwa katika mahusiano yameanzia huko mitandaoni ususani mtandao wa Instagram, ambapo wawili hawa kwa mara kadhaa waneonekana wakipiga picha pamoja kwa mtindo wa “selfie” na kuacha maswali mengi kwa mashabiki wao ambao wengi wanauliza kunani? Lakini mara zote wamekuwa hawatoi majimbu. Hii ikapelekea watu wajiongeze kwa kuwaunga mkono na kuwatakia mahusiano mema na wengine wachache wakiponda.

Nilipozipata hizi, mzee wa ubuyu ni kaamua kuingia huko istagram kujionea, Ebwana ehh!!!.

Nilipopitia ukurasa wa Bond, nilikuta zaidi ya nusu za picha zake zote alizoweka ni zile amepiga na mwanadada Wastara au za wastara peke yake (baadhi hizo hapo juu)

Nikaingia kwa Wastara, huku nako nikamkuta, Bond na huko ndiko moto unapowaka wa wa wawili kukwa kwenye mahusinao kwani “comment” nyingi za mashabiki zinaonyesha kuwa hii ndio PROJECT mpya.

Bado wote wawili hawajasema lolote hadi sasa..sasa waswahili wansema, Lisemwalo?....

Kama ni kweli, Napenda kuwatakia kila la kheri, kwani ni jambo jema.

~By Mzee wa Ubuyu
via BongoMovies

Samantha Apokelewa Kwa Mikono Miwili na Familia ya Idris Mshindi wa Big Brother

$
0
0
Mapenzi urafiki wa Idris Sultan na mrembo wa Afrika Kusini aliyekuwa swahiba wake wa karibu kwenye shindano la Big Brother Africa, Samantha, umefika kwenye hatua ya juu zaidi.

Samantha ambaye bado yupo nchini amepokelewa kwa mikono miwili na familia ya Idris.

“They’ve only been good to me and I can’t say thank you enough. How people can love you this much but only no you a few weeks is beyond me,” ameandika Samantha kwenye picha akiwa na familia ya Idris.

“God bless your beautiful hearts . Thank you ! Thank you ! Thank you.”


Download Wimbo Mpya wa Kushirikiana wa Vanessa Mdee, Aika, Nahreel, Avid na Barnaba.

$
0
0
Download Hapa Wimbo mpya wa kushirikiana wa Vanessa Mdee aka. V Money, Aika, Nahreel, Avid na Barnaba, Wimbo Umetengenezwa na Producer Nahreel

Download Wimbo Mpya wa Grace Matata Akishirikiana na Maua Sama-Hello

$
0
0
HELLO! is a duet featuring Grace Matata and Maua Sama. The song is written and composed by Maua Sama and Grace Matata, produced and mixed by Ema the Boy at Classic Sound Studio and mastered by Will HD.

Kijana Auwawa Kwa Kupigwa Risasi Akiwa Club Jijini Dar

$
0
0
Kijana mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja,  usiku wa kuamkia leo amepigwa risasi ya shingo na watu wasiojulikana wakati akiingia Club Maisha ilioko Oyster Bay jijini Dar es salaam. 

Tukio hilo lilitokea majira ya saa tano(5) usiku  ambapo kijana huyu akiwa na rafiki zake wanne(4) wakiwa ndio wanashuka kwenye gari yao waliyokuja nayo, walijikuta wamevamiwa na watu wawili wasiojulikana na yeye kupigwa risasi ya shingo kisha watu hao kutokomea kusikojulikana. 

Shuhuda wa tukio hilo alisema aliwaona watu wawili walioshuka kwenye gari ndogo nyeusi ilifunga breki kwa kasi kwani walionekana walikuwa mwendo kasi sana, kisha kuwavamia watu waliokuwa wanashuka kwenye gari ilikuwa imepaki muda mfupi baada ya kufika eneo hilo.

 shuhuda huyo aliendelea kwa kusema alisikia sauti ndogo ya kitu kilicholia "pyuuu!!!" bila ya kuelewa ni nini na kisha kufuatiwa na kelele nyingi za watu hao waliokuwa wamevamiwa. 
Waliotenda tukio hilo walitoweka mara moja eneo la tukio baada ya watu kujaa eneo ambalo kijana huyo alipigwa risasi alikuwa ameanguka chini. 

Polisi walifika eneo la tukio na kukuta kijana huyo ameanguka chini na damu nyingi zikiwa zimemtoka sehemu za shingoni na kifuani huku akiwa amewekewa nguo shingoni ili damu isiendelee kutoka ambapo ilisemekana ilikuwa ikitoka nyingi sana.


 Walimpakia kwenye gari yao kumuwahisha katika hospitali ya jirani ya mwananyamala, lakini kijana huyo alifia njiani akikimbizwa kuelekea hospitali.

Precision Air Watangaza Nafasi za Kazi Kwa Watu Kumi..Changamkia Deal Haraka

$
0
0
JOB VACANCY
Precision Air Services Plc is a fast growing private Tanzanian airline which operates in Partnership with Kenya Airways, with its strategies to expand wings beyond East Africa and Africa. In order to keep our services at a higher level and meet our customers’ maximum satisfaction We wish to invite applications from suitably qualified candidates to fill in this
challenging position.
POSITION: RESERVATION AND TICKETING SALES AGENT (10 POSTS)
REPORTS TO: INDOOR SALES SUPERVISOR
DUTY STATION: DAR ES SALAAM – 9 POSTS: ARUSHA - 1 POST

ROLE PURPOSE To provide efficient and effective customer focused Passenger Ticket Sales & Reservation

KEY ACCOUNTABILITIES / RESPONSIBILITIES
• Make ticket reservations, confirmations, reconfirmations and seat selection for clients on PW flights in compliance with the carrier policies, procedures and customer expectations.
• To give fare quotes to all PW clients including group quotations and bookings.
• To ensure daily sales reports and sales dispatches are submitted in accordance to company procedures
• Give clients flight details and information and details.
• Handle and issue E- tickets on behalf of the company and accordance to company procedures.
• Handle flight disruptions, advising clients, reissue and revalidate electronic tickets
• Handle telephone & email enquiries as regards travel information.
• To protect and enhance revenue collection to meet carriers expectations and customer expectations
• Any other duties as may be assigned by your supervisor

KEY PERFORMANCE INDICATORS
• Meets the set passenger ticket sales targets
• 100% accuracy in fare quotation and collection of monies.
• Telephone answered within 3 rings
• Response to emails within working

COMPETENCIES
• Integrity
• Team player
• Proactive/ result oriented
• Pleasant & presentable
• Communication / interpersonal skills
• Resilient
• Self motivated
• Customer Service in Airline environment

KNOWLEDGE, SKILLS, EXPERIENCE
• IATA/UFTAA Foundation/consultants diploma
• Certification in relevant computer application
• Experience in delivering service in demanding consumer environment
• Fluency in appropriate foreign languages an added advantage

Closing Date: Not later than 02nd January 2015. Mode of Application: If you feel you meet the above requirements please send your application and CV to the address below. Only short‐listed applicants will be contacted.
Director of Human Resources and Administration
Precision Air Services Plc Mail Box 70770 Dar es Salaam Tanzania
E‐mail: pwrecruit@precisionairtz.com

Mapenzi Moto Moto: Diamond Kula Sikukuu ya Mwaka Mpya Rwanda na Mpenzi Wake Mpya

$
0
0


Mambo yazidi Kuwa Mazuri Upande wa Diamond na Zari kwani Mapenzi yao ni Moto Moto , Kwa sasa wanafuatana kama Kumbi kumbi kila Diamond anapofanya Show za nje lazima Mtoto Zari Awe Pembeni , Baada ya Kuwasha moto Juzi Huko Rwanda akiwa na Zari Sasa ni zamu ya Rwanda , Diamond Ameweka Picha Akiwa na Zari na Kuandika Haya hapa Chini:                                                      "Jus touched down Rwanda...Damn! i can not wait to spend my New year's eve here!"

Wema Sepetu. Aongea Kuhusu Mapenzi ya Diamond na Zari 'Such a Good Couple. Wivu wa nini, I Wish Him all the Best and Ammmm'

$
0
0
U Heard ya jana December 29 iko hapa, Gossip Cop alihudhuria shughuli ya kutambulisha msanii mpya ambaye atakuwa kwenye Management ya Endless Fame iliyofanyika Tegeta Dar siku ya jana December 28, akapata nafasi ya kuzungumza na Wema na jinsi anavyojisikia kuhusu uhusiano wa Diamond na Zari.
Wema alisema anachukulia fresh, hana tatizo lolote na yoyote kati ya wawili hao kwa sasa ameendelea na mambo yake.
“... Aisee nawapenda… such a good couple. Wivu wa nini, I wish him all the best and ammmm… I wish him happiness …” Wema Sepetu.
Kwa bahati mbaya wakati wakijiandaa kutoka ukumbini hapo baada ya mahojiano hayo Wema alipata jeraha baada ya kubanwa kidole na mlango wa gari.
Viewing all 104803 articles
Browse latest View live




Latest Images