Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live

GARI AINA YA ISUZU INAUZWA BEI NAFUU KABISA..

$
0
0
 NI GARI AINA YA ISUZU KAMA UNAVYOINA KWENYE PICHA INAUZWA KWA SHILINGI 16 MILION ...GARI NI TANI 2.6 , CC 4000, YA MWAKA 1996...MAELEWANO YAPO ...GARI IPO DAR ..KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA NUMBER 0713583548 AU 0684885434
PICHA ZAIDI HIZI HAPA CHINI:







DR.SLAA:BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI LIMECHOKA KABLA HALIJAANZA FANYA KAZI

$
0
0
Katibu mkuu wa Chadema Dr. Willbrod Slaa amesema kwamba baraza jipya la mawaziri lililoteuliwa na kutangazwa jana na katibu mkuu kiongozi limechoka kabla halijaanza kufanya kazi.

Aidha Dr. Slaa amesema kuwa uteuzi wa Mwigulu Nchemba kama naibu waziri wa fedha (sera) ni mkakati wa CCM kujichotea fedha za uchaguzi mkuu ujao hivyo tutarajie EPA nyingine.

Uteuzi wa Mwigulu Nchemba, Dr. Asharose Migiro, Adam Malima, Saada Mkuya, Jenista Mhagama na kurejeshwa kwa Dr. Shukuru Kawambwa kumezua manung'uniko mengi huku wengi wakihoji uwezo wao kiutendaji.

Dr Migiro anakuwa waziri wa katiba na sharia huku akielezwa kama miongoni mwa waliobeba maslahi ya CCM kwenye mchakato wa katiba mpya hususan kwenye madaraka ya rais na muundo wa muungano. Saada, Nchemba na Malima wamekabidhiwa wizara nyeti ya fedha na uchumi ambapo imedaiwa kuwa uwezo wao kiutendaji hauwezi kuiletea ufanisi wizara hiyo huku wengi wakitilia shaka uteuzi wa Nchemba kiuadilifu ambapo amekuwa akionyesha chuki za wazi kwa Chadema na viongozi wake na kukosa kabisa staha pale anapochangia bungeni.

Kawambwa na Jenista wamepewa jukumu la kuongoza elimu ambapo Kawambwa alionyesha dhahiri kushindwa vibaya kuongoza sekta hiyo nyeti kabla ya uteuzi mwingine wa jana.

WAZIRI NYALANDU AANZA NA MKWARA MZITO

$
0
0

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, ameweka wazi kwamba atamshughulikia mtu yeyote atakayebainika kujihusisha na biashara haramu ya ujangili, hata kama ni kigogo na kwamba haogopi mtu.

Nyalandu ambaye kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa huo, alikuwa Naibu Waziri wa wizara hiyo chini ya Balozi Khamis Kagasheki, aliyasema hayo jana mara baada ya kupokelewa kwa shangwe na watumishi wa makao Makuu ya wizara hiyo yaliyopo jijini Dar es Salaam.

My take: Huyu jamaa apewe tu ushirikino tuone impact yake

NAWAOGOPA WANAWAKE WAZURI..TATIZO SIJUI NINI

$
0
0
Nawaogopa wanawake wazuri, tatizo sijui nini?
Pamoja na ujanja wangu wote ktk nyanja mbali mbali lakini linapo kuja swala la mapenzi nishindwa kujielewa sijui Kwanini Nawaogopa wanawake wazuri (Watanashati/ Warembo) Tangu nibaleh na kujiingiza na maswala ya mahusiano sijawahi kujipa ujasiri wa kusimamisha PINI na kuitupia vina. Sio kama siwataki hapa ukweli Nawaogopa sana wanawake wazuri. Wanawake wangu sikuzote ni wakawaida sana tena wengine kiukweli hawanifikii hata kwa hadhi (kuku wa kienyeji) Imefika wakati Rafiki zangu wananiita wa Mizoga kwa kupenda wanawake wabovu.

HATIMAE CHAGGA BARBIE AMALIZA BEEF AMSAMEHE PREZZO KWA MOYO WAKE WOTE

$
0
0
We had barely recovered from Chagga Barbie's vicious first salvo at Prezzowhen she opened a can of worms exposing her former lover.

In the midst of a stream profanity, she revealed that Prezzo was broke and mocked him for his $8000 Chrysler.

This is how part of what she said “ Range unazo couple sio au nikale ka $8000 crossfire Chrysler ka 2002 kaliko na miles 150,000 plus hapa wivu ulikuwa unakusumbua”

After spilling all this vitriol,she finally cooled off and said that she had forgiven him in this statement

"Am thankful to have family and few friends that support me unconditional, was advised from day one to stay away from him but bse of Power of Love I end up not listening, I followed my heart but @the end I saw it all on my own eyes. Wanna take time to apologize to everyone, I just learn a lesson in a hard way but am thankful too that I cleared my chest. #LoveCanMakeUsActCrazy Prezzo ur not my enemy, I forgive u from my heart n may God be with u n give u everything u have ever wish for. #Peace"

MTANDAO WA KUMTOA JACK PATRICK WAUNDWA

$
0
0

Na Erick Evarist
FAMILIA ya modo wa Bongo, Jacqueline Patrick aliyenaswa kwa msala wa madawa ya kulevya Macau- China inadaiwa kuunda mtandao kwa ajili ya kufanikisha zoezi la kumchomoa mrembo huyo mikononi mwa vyombo vya sheria.

Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na familia hiyo (jina lipo), familia hiyo imeanza mchakato huo hivi karibuni hasa baada ya kudadisi kuhusiana na sheria za eneo alilokamatiwa (Macau) kutokuwa kali kisheria tofauti na maeneo mengine ya nchi hiyo kama Hong Kong.

“Wameandaa mikakati thabiti kwani wamegundua Macau ni tofauti na maeneo mengine ya China ambayo ukikamatwa na madawa ya kulevya na kuthibitika kuwa na hatia, hakuna msalie mtume, ni kitanzi tu. Macau sheria zao si kali sana, wanaweza wakafanikiwa kumchomoa hata kwa njia za panya,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

“Kinara wa mtandao huo ni Jux yule wanayesema ni mpenzi wake Jack ambaye kwa sasa yupo China. Ndiye ambaye juzijuzi hapa aliposti picha mpya za Jack na kusababisha watu wajue mrembo huyo kaachiwa huru.”

Paparazi wetu alimtafuta dada yake Jack ambaye hakupenda kutaja jina lake  ambapo alisema inawauma kutojua hatima ya ndugu yao hivyo wameona bora wajipange kwenda kufuatilia sakata hilo kupitia kwa Jux waliyemtaja kama ni rafiki wa Jack.

“Tunasikia maneno mengi tofautitofauti, inatuuma sisi kama ndugu hivyo tutajichanga na tutawatuma ndugu wawili ili waweze kwenda kushughulikia suala la ndugu yetu. Katika mkakati huu tumepata na baadhi ya marafiki wa Jack ambao kwa sasa sitawataja,” alisema dada huyo.

Hata hivyo, imeelezwa ndugu hao wametahadharishwa kuwa makini kwani licha ya kusikia sheria za Macau si kali sana wasidharau kwani huenda wakawekewa mtego na kujikuta wameingia katika matatizo kama watajaribu kutumia mlango wa ‘uani’ kumtoa Jack.

Source:Global Publishers

BAADA YA PREZZO KUACHWA NA TOTO LA KICHAGA..SASA HUDDAH ATANGAZA KUMTAKA TENA PREZZO

$
0
0
Mpenzi wa zamani wa Prezzo ameonyesha kuguswa na tukio la Prezzo kupigwa chini na Toto la Kitanzania Chagga Birbie na kuanza kupost Message kwenye twitter za kuonyesha kumpa kampani Prezzo na kusema anamtaka warudiana kuwa anammiss Kitandani...Makubwa...
Jisomee mwenyewe mtiririko wa message zake


But on the real Baby .What did u do to the fatso? I miss you @AMB_Prezzo .I'm still your ride or die.I'm coming home .Don't u worry.

MAJANGA:MANCHESTER UNITED YAFUNGWA TENA NA SUNDERLAND KWA MATUTA

$
0
0
TIMU ya Manchester United imeendelea kusuasua katika michuano mbalimbali baada ya kuondolewa na Sunderland katika nusu fainali za michuano ya Kombe la Ligi maarufu kama Capital One Cup iliyopigwa Old Trafford.

Manchester imetupwa nje ya mashindano hayo kwa mikwaju ya penalti baada ya matokeo ya awali kuwa sare ya 3-3 na Sunderland kushinda kwa penalti 2-1.

Baada ya matokeo hayo, Sunderland inayoshika nafasi ya pili kutoka mkiani ikiwa na pointi 18 juu ya Cardiff City katika Ligi Kuu ya England, itakutana na Manchester City Machi 2 mwaka huu katika fainali itakayopigwa uwanja wa Wembley.

MCHUMBA WA LULU MICHAEL SI SIRI TENA!

$
0
0
Hamida Hassan, Mayasa Mariwata na Galdness Mallya
HAYAWIHAYAWI hatimaye yamekua! Siku chache baada ya sexy lady wa sinema za Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ kutangaza sifa za mwanaume atakayemchumbia, amejitokeza mtu anayetaka kuchukua jumla na si siri tena, Amani limenyetishiwa.

SIFA ZAKE
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa familia ya staa huyo anayekimbiza sokoni na filamu yake ya Foolish Age, mchumba huyo anaitwa Johnson lakini ni maarufu kwa jina la JR na pia ni Mkristo kama ilivyo kwa Lulu.

JR ni mfanyabiashara kigogo wa jijini Dar mwenye ‘mahela’ ya kufa mtu.
Pia mchumba huyo ni bosi wa kampuni kubwa ya uandaaji, usambazaji wa kazi za sanaa Bongo.

ALISHAKWENDA KWA AKINA LULU
“Kwa taarifa yenu, tayari JR anafahamika vizuri kwa akina Lulu kwani alishakwenda kujitambulisha na kuna maneno kwamba ndiye aliyempangia nyumba kubwa, Tegeta jijini Dar.

“Unajua yule jamaa aliona fursa akaitumia. Baada ya Lulu kutoka mahabusu kwa matatizo ya kifo cha mwandani wake, Steven Kanumba ndipo JR akafanya juu chini kumnasa hadi akafanikiwa,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:

“Muda siyo mrefu zitasikika cherekochereko za Lulu kuolewa.
“Ukweli ni kwamba hata mama Lulu (Lucresia Karugila) amemkubali yule mchumba kwani ndiye anayemfanya Lulu aonekane kama alivyo kwa sasa.

“Sasa hivi Lulu anaishi kwenye bonge la nyumba kule Tegeta (Dar) na suala la usafiri si ishu. Anabadili tu magari. Kusema kweli kwa sasa bidada mambo yamemwendea vizuri.
“Anachoogopa tu yasitokee kama yale ya Clement wa Wema Sepetu.”

AMANI LASAKA WAHUSIKA
Baada ya kumwagiwa upupu huo, gazeti hili liliwasaka wahusika mmoja baada ya mwingine ili kupata mbivu na mbichi za ishu hiyo.

MAMA LULU
Kwa kuwa ni jambo la kifamilia, gazeti hili lilipozungumza na mama Lulu, Lucresia Karugila alisema si jambo baya kwa mwanaye kuwa na mchumba hivyo anamkubali (huyo mchumba) huku akiweka wazi kuwa hana kipingamizi chochote.

Alipoulizwa jina la mwanaume huyo na kwamba ni kigogo mwenye fedha nyingi, mzazi huyo alitoa ruksa aulizwe Lulu mwenyewe.

“Mimi sina sababu ya kumkataa mwanaume ambaye wamekubaliana na mwanangu, kikubwa ni makubaliano, namkubali,” alisema mama Lulu.


HUYU HAPA LULU
Kwa upande wake Lulu mambo yalikuwa hivi;
Amani: Mambo vipi Lulu?
Lulu: Poa, naongea na nani?
Amani: (akatajiwa jina la mwandishi) kwanza hongera kwa kupata mchumba.
Lulu: Nani kawaambia?

Amani: Kwa kazi yetu hii hatushindwi kujua. Je, ni kweli umepata mchumba?
Lulu: Ndiyo lakini nisingependa sana kulizungumzia hilo.
Amani: Anaitwa nani?
Lulu: Siwezi kumtaja leo (Jumanne iliyopita). Nitawatajia tu ninyi subirini. Itakuwa surprise (mshangao), siku si nyingi nitamuanika.

Amani: Je, ni kweli ni maarufu kwa jina la JR? Au wewe tutajie hata jina la mwanzo tu.
Lulu: Nimeshasema jamani nitawatajia kwani ninyi mna haraka gani?
Amani: Je, ni kweli ni mmiliki wa kampuni ya burudani? (anatajiwa kampuni).
Lulu: Hayo yote yatafahamika kwenye utambulisho. Naomba niishie hapo ‘coz’ sina cha zaidi kuhusu ishu hiyo jamani subirini siku si nyingi.


MAMA KANUMBA
Baada ya kujiridhisha kuwa sasa Lulu ana mchumba rasmi, ‘kijumbe’ wetu alimfikishia taarifa aliyekuwa mama mkwe wa staa huyo wakati akiwa na Kanumba, mama Kanumba, Flora Mtegoa ili naye atie neno.

Mama Kanumba hakuwa na kipingamizi juu ya suala hilo zaidi ya kuchekelea huku akiweka wazi kuwa Lulu kwa sasa anaweza kuolewa.
“Mimi sina tatizo kabisa, namjua. Lulu anaweza kuolewa na nimempa baraka zote,” alisema mama Kanumba ambaye kwa sasa ni shosti mkubwa wa mama Lulu.

JR SASA
Hata hivyo, gazeti hili halikuishia hapo kwani lilisaka namba ya simu ya kiganjani ya mwanaume huyo ambapo ilipopatikana, alipigiwa, mambo yakawa hivi:
Amani: Habari yako mkuu JR?
JR: Safi, nikusaidie nini?

Amani: Mimi…(akatajiwa jina la mwandishi na kampuni) wewe ndiye JR mmiliki wa kampuni ya…(anatajiwa jina la kampuni).
JR: Kwanza mimi siyo JR ni GR. Huyo JR ni mdogo wangu.
Amani: Mbona sisi tumetajiwa JR ambaye anamiliki kampuni ya...(anatajiwa tena jina la kampuni).
JR: Oke, ndiyo mimi nikusaidie nini?

Amani: Taarifa tulizonazo ni kwamba una uhusiano na Lulu? Yaani wewe ndiye mchumba wake?
JR: Ndiyo, sitaki maswali (tusi na kukata simu).  
Tangu kitokee kifo cha Kanumba ambaye alikuwa na uhusiano wa siri na Lulu, bidada huyo hajawahi kuwa na mwanaume hadi huyo mchumba aliyejitokeza.

DIAMOND NA WEMA SEPETU NDANI YA SHUKA MOJA KWA BED...WACHA MUVI IENDELEEE.

$
0
0
HILO MUVI WE WACHA LIENDELEE...MI NILIKUA NAPITA TU MDAU...USIKU MWEMA JAMANI.

WANAUME TUMEUBWA MATESO..KAZI KAZI ...

$
0
0
Tupia Neno Moja tu kwa huyu Mwanaumeeee

HALI YA MWIGIZAJI JOHARI SI SHWARI..ALAZWA HOI HOSPITALINI

$
0
0
Mwana Dada na mwigizaji mkongwe Blandina Chagula maarufu Johari ni mgonjwa na amelazwa katika moja ya hospitali maarufu hapa jijini.


Kwa mujibu wa blogu ya mwigizaji Deogratious Shija, ndugu wa karibu wa Johari ameshindwa kuweka wazi ni hospitali gani ambayo Johari amelazwa na kusema kuwa wanashindwa kusema mahali alipolazwa Johari kutokana na usumbufu wa waandishi wa habari " kwakweli Johari anaumwa sana na tunaomba dua zenu tu" Alisema ndugu huyo wa johari. Jamani tumumkumbuke katika dua muigizaji huyu na wagonjwa wengine wote mahospitalini. Ameni

ZA DARAJA LA DUMILA LILIOHARIBIKA KUTOKANA NA MVUA-SERIKALI YAIFUNGA BARABARA YA MOROGORO -DODOMA KWA MUDA

$
0
0



Mvua kubwa iliyonyesha wilayani Mvomero, Morogoro usiku wa kuamkia jana imesababisha madhara makubwa ikiwemo kukatika kwa daraja la Dumila linalounganisha barabara za Morogoro na Dodoma na kusababisha safari za wananchi kukwama.

CCM YAKANUSHA KUANZISHA HOJA YA MAWAZIRI MIZIGO

$
0
0
Chama Cha Mapinduzi CCM chasema haikua hoja yake kumtaka Rais kuwafukuza wale walioitwa “MAWAZIRI MIZIGO” bali kuchukua hatua za kurekebisha mapungufu yaliyokuwepo chini ya mamlaka yao. 

Chasema Kufukuza inaweza kuwa ni njia ya kutatua tatizo lakini sio njia pekee.

Je uonavyo wewe, kufukuza mawaziri ni njia sahihi ya kutatua matatizo uliyonayo?

LULU "NIKIONA POMBE HUWA NAIPA SHIKAMOO KWA JINSI ILIVYONIFANYA"

$
0
0
MSANII wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema kuwa sasa hivi anaiogopa na kuiheshimu sana pombe akiamini kwamba ndiyo chanzo cha maisha kuharibika.

Kwa mujibu wa tovuti ya GPL hivi , Lulu alisema tangu ametoka gerezani ameamua kujiweka pembeni na kilevi hicho na kwamba bora aitwe mshamba.

“Kiukweli nikiiona pombe kuna wakati naipa shikamoo kwani ndiyo kichocheo cha kila baya hapa duniani, watakaoniona mshamba kwa kubadilika kwangu wanione hivyohivyo,” alisema Lulu.

Msanii huyo kipindi cha nyumba alikuwa hakamatiki kwa kilevi na kuna wakati aliwahi kuzimika alipofakamia pombe za ofa alipokuwa ndani ya Ukumbi wa Maisha Club, jijini Dar.

NISHA ABEMBELEZA PENZI LA NEY WA MITEGO

$
0
0
STAA wa sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ anadaiwa kubembeleza penzi kwa staa wa muziki wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Ijumaa lina full mchongo.

Mnyetishaji wetu alivujisha mawasiliano baina ya wawili hao waliowahi kuwa wapenzi kisha kumwagana ambapo yalionyesha kuwa Nisha analitamani upya penzi la staa huyo.



Mbali na mawasiliano ya ujumbe wa maandishi, chanzo hicho kilicho karibu na mastaa hao kilikwenda mbali zaidi kwa kuvujisha picha ambazo zilionesha Nisha akimtumia Nay huku akichombeza na meseji tofauti za kumtega.

Baada ya kuzinasa meseji hizo ambazo chanzo kilidai kimeziiba kutoka katika moja ya simu ya mastaa hao, paparazi wetu aliingia mzigoni kuwasaka mastaa hao ili kujua kama wana mpango wa kurudiana.



Wa kwanza kupatikana alikuwa ni Nisha ambaye alisema: “Dah, ni kweli ninawasiliana na Nay kama rafiki wa kawaida tu.



“Nay ana demu wake na mimi nina bwana wangu.”
Kwa upande wa Nay wa Mitego alipata kigugumizi kidogo kulizungumzia hilo lakini akakiri kupata meseji hizo za mitego lakini akadai hakuna kinachoendelea kati yao.



CREDIT GPL

MSANII RICHIE WA BONGO MOVIES AKIRI KUTAPANYA FEDHA ZA BONGO MOVIES

$
0
0
MKONGWE katika anga la filamu za Kibongo, Single Mtambalike ‘Richie’ amekiri kutumia vibaya madaraka wakati wa uongozi wake kama mweka hazina wa Klabu ya Bongo Movie msimu uliopita.

Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar, Richie alisema kulikuwa na mfumo mbovu wa jinsi ya kutumia pesa“Kuna mazuri tulifanya pia mabaya yapo hususan mfumo mbovu wa jinsi ya kutumia pesa, kiongozi yeyote aliweza kuchukua pesa bila kuhojiwa na hata mimi nilikuwa natumia vibaya,” alisema Richie.

BAADA YA LULU KUPATA MCHUMBA..SINTAH AJITOKEZA NA KUMPA DARASA LA MAPENZI

$
0
0


Ninakutakia kila la kheri ila kuwa muangalifu na wanaume maana kuna wa aina mbili masikini na matajiri, wale masikini watakupenda kwa dhati wakiwa hawana ila siku wakipata utawajua wao nani, ama uongo wadau?

na wale matajiri watajua umependea pesa zao na hata kama umempenda kwa dhati mambo ya manyanyaso na nk yatahusika, esp matajiri watakuhonga kila kitu make sure hata akikununulia kijiko kiwe katika jina lako Elizabeth Michael.

the best maana sasa umekuwa yaliyopi
ta si ndwele tugange yajayo, one more thing, mfiche mtarajiwa wako we anza kumtangaza anaitwa J haaa kuna makubimbiri yanan’gaa macho kazi yao kusubiri kutongozwa halafu yalivyokuwa mahayawani yenyewe yanakuja kwa nia moja tu ya kuharibu na kusepa so TAKE CARE……. 

Unstoppable

PENNY AAMUA KUFUNGUKA KUHUSU KUVUNJIKA MAPENZI YAO NA DIAMOND..HUU NDIO UKWELI NA NINI KINAENDELEA SASA

$
0
0
Mtangazaji na meneja wa vipindi wa kituo cha runinga cha DTV, Penniel Mwingila aka VJ Penny, amesema kuwa yeye na mpenzi wake, staa wa ‘My Number One’, Diamond Platnumz, wamepeana nafasi ili kila mmoja kutafakari anachotaka maishani.

Kauli ya Penny kwenye mahojiano maalum na Bongo5 TV, inajibu maswali ya wengi kuhusiana na kama wawili hao wapo pamoja au wameachana baada ya Diamond na mpenzi wake wa zamani, Wema Sepetu kurudiana tena. Katika interview hiyo, Penny ameongea pia kuanzia historia yake, namna alivyoingia kwenye utangazaji, alivyokutana na Diamond, mapenzi yao yalivyokuwa, alivyojisikia baada ya kuona picha za Wema na Diamond, maisha yake ya sasa na mipango yake ya mwaka huu.

Akizungumzia kuhusu alivyojisikia baada ya kuona picha za Diamond akiwa na Wema, Penny amesema yeye pia alishangaa kama watu wengine walivyoshangaa kuziona.

“Mimi ni mtu ambaye utaniambia ‘fulani amefariki’ na sitakiamini mpaka nione kabisa huyu hapa amekufa,” amesema Penny. “Nilipoziona picha nilishtuka kidogo, kibinadamu nilikuwa ‘Ohh Mungu wangu kipi kinaendelea’. Lakini sijui.. Mungu wa ajabu sana, niliichukulia kwa uzito mdogo kadri nilivyoweza, ilipita tu kama ‘shaaa’.. na dakika inayofuata (Diamond) anasema ‘ohh ni movie’. Mimi nilikuwa kama nyie, amini usiamini ‘Ni movie okay vizuri, baby anafanya movie’. Kwa kawaida nilitakuwa kuipokea tofauti lakini ni kama nilishikwa na ganzi kwa muda, sikutaka kujiumiza. Kuna ‘buttom’ ambayo nikiruhusu iniumize nitaumia, nikiamua kitu kinipite na siwezi hata kujisumbua. Alirejea, maisha yakaendelea, nimekaa nasubiri movie hiyo.”

Penny amesema pamoja na yote hayo, maisha yaliendelea kama kawaida kati yao kama vile hakuna kilichotokea.

“Alirejea kutoka kwenye safari yake ya movie na tuliendelea kuwa pamoja kwasababu mimi nilikuwa nani kuhukumu tofauti? Hicho ndicho kitu nawaambia watu, sikuwepo hivyo kama anasema alikuwa anafanya movie nitamuamini kwasababu sikuwepo. Napenda kuona vitu mwenyewe, mimi ni mtu wa hivyo, nahukumu vitu pindi nionapo mwenyewe. Maisha yaliendelea, tuliendelea kuwa sisi. Nilikuwa na vitu vilivyokuwa vikizunguka kwenye mawazo yangu nje na ndani.. ‘hivi ndivyo natakiwa kuwa?’ Watu wanadhani nina moyo wa jiwe, nina moyo, nina akili, saa zingine inabidi nikae nifikirie, nini hiki, nini kile. Mambo yalikuwa sawa lakini tofauti kidogo kuzingatia ukweli kwamba sikujua nini cha kufikiria, sikujua nini cha kufanya na nilitakiwa kuchukua muda wangu kuhakikisha kuwa sifanyi kosa lolote. Na nilikuwa bado pembeni yake, bado nikimsupport chochote alichokuwa akikifanya iwe movie, nyimbo zake mpya au chochote, niliendelea kuwepo kwaajili yake kuwa girlfriend wake, rafiki yake wa dhati, mkono wake wa kulia.”

Hata hivyo Penny amesema ilifika wakati ambapo waliona bora ‘kupumzisha’ uhusiano wao kutokana na hali halisi ya mabadiliko yaliyokuwa yamejitokeza.

“Kama uhusiano wowote ulivyo, kuna mwanzo na mwisho na watu wanaachana kwa sababu nyingi. Nilihisi kwamba nahitaji kumpa nafasi, wote ni vijana na wakati mwingine tunahitaji nafasi kugundua vitu vipya, kuona kipi hasa unachokihitaji kwenye maisha. Unajua ukimruhusu ndege afanye vitu mbalimbali then atajua kama ‘mti huu ndio unanifaa, mti huu haunifai. Hivyo nilihisi kwamba wote tulihitaji hicho, tulihitaji ‘space’ hivyo nikampa nafasi na mimi nakuchukua nafasi. Huwa nawaambia watu kuwa vyovyote ilivyo, yeyote atakayekuwa naye, nipo pembeni yake nikimshangilia kwasababu ni kweli (Diamond) ni mtu mzuri ndani. Achana na watu wanavyomuona chizi chizi, sahau msanii unayemjua, ana roho nzuri na anajua anachokitaka. Ni ngumu kuacha iende.. kama ni rahisi kuacha iende basi hujampenda huyo mtu.”


Amesema kila anapoulizwa maswali ya ni nani kati yake na Diamond aliyemwacha mwenzake, hujibu hajui kwakuwa wamepeana tu nafasi ya kila mtu kufanya mambo yake na kuongeza kuwa bado wanaendelea kuwasiliana huku akiwa na furaha na chochote (Diamond) anachofanya.

Penny amesema japo ameendelea na maisha yake lakini bado anachukua muda kufikiria nini anachohitaji maishani na hadi sasa hajafikiria kuwa na mwanaume mwingine. “Bado, sio kwamba sitongozwi, wanaume wanakuja lakini najaribu … hakuna mwanaume mkamilifu, najaribu kutafuta mwanaume anayeweza kuwa mkamilifu kidogo najua yupo sehemu.”


Ameongeza kuwa anatamani kurejea katika maisha ya kawaida na kuwa na uhusiano na mwanaume asiye maarufu kwakuwa kuwa na uhusiano na mtu mwenye jina kulimfanya achunguzwe muda wote na kujikuta akikosa maisha ‘faragha’.

“Napenda kurejea kwenye maisha niliyokuwa nayo ‘it was much fun’, napenda maisha yangu ya faragha.”

Penny amesisitiza kuwa mwaka 2014 ameupanga kuwa mwaka wa kufanya kazi zaidi na anaamini utakuwa wa ushindi kwake.


“Nilijiambia mwenyewe siku ya January 1 kuwa ‘mwaka huu ni mwaka wa ushindi kwangu’ na naenda kushinda, vyovyote vile naenda kushinda, naenda kuweka nguvu yangu yote, kwahiyo kuna mengi yanakuja, mengi.”

Source:Bongo5.com

MWANAFUNZI IFM AKUTWA AMEFARIKI CHUMBANI, SOMA KILICHOTOKEA HAPA

$
0
0
Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Ibrahim Jackson (24), amekutwa akiwa amekufa katika chumba cha kupumzikia kilichopo chuoni hapo bila mwili wake kuwa najeraha lolote.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi, alisema tukio hilo lilitokea saa 11:30 juzi jioni katika chumba namba 118 jengo namba D kilichopo mtaa wa Shaban Robert.
NIPASHE lilifika IFM na kuzungumza na Mshauri wa Wanafunzi, Emmanuel Mushi, ambaye alisema kuwa marehemu alikuwa anasomea Shahada ya Usimamizi wa Kodi akiwamwaka wa pili.
Alisema marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kifafa kwa muda mrefu kabla hata hajajiunga na IFM.
Alisema juzi jioni marehemu aliomba funguo kwa ajili ya kwenda kupumzika katika chumba kinachotumiwa kulala nawanafunzi kutoka nje ya nchi pindi wanapofika chuoni hapo kwa ajili yamasomo.
“Nyaraka zake zinaonyesha marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kifafa kwa muda mrefu, hata kabla hajajiunga na chuohiki, kwa hapa chuoni ugonjwa huo ulikuwa unamtokea mara kwa mara,” alisema Mushi.
Aliongeza kuwa mara baada ya kupewa funguo alikwenda kupumzika katika chumba hicho na baadaye alikutwa amefariki huku mwili wake ukiwa umelala kitandani.
Alisema baada ya tukio hilo walitoa taarifa katika kituo cha polisi napolisi walifika katika chumba hicho na kumpeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa uchunguzi zaidi.
Mushi alisema wamewasiliana na wazazi wake waliopo wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya na taratibu za kuusafirisha mwili huo zitafanyika leo.
Mmoja wa marafiki wa karibu wa marehemu, Peter Alphonce, aliliambia NIPASHE kuwa alikuwa na marehemu siku moja kabla ya kifo chake wakicheza mpira na walimaliza kucheza vizuri na kuagana kuelekea hosteli.
“Nilikuwa naye jana (juzi) tukicheza mpira, hadi saa kumi tulipomaliza aliniaga na kuelekea katika MachavaHostel ndiko anakolala,” alisema Alphonce.
@NIPASHE.
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live




Latest Images