Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live

Tofauti ya Askari Wetu na Wenzetu..Katika Majanga ya Mafuriko

$
0
0
Askari Wetu Wakisaidiwa Kuvuka Maji 
 Tofauti ya Askari Wetu na Wenzetu..Katika Majanga ya Mafuriko
 Askari wa Wenzetu Wakisaidia watu Kuvuka 


Hapa Nimeweka Taarifa ya Wizara ya Mawasiliano Kuhusu Sheria Ya Makosa ya Mitandao kuanza Kutumika

$
0
0

Ndugu Wananchi,

Ndugu Waandishi wa Habari,

 Kukua kwa kasi kwa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kumeleta mafanikio mengi katika nyanja mbalimbali za maisha ya kila siku. Mafanikio haya yanathibitika kwa kuongezeka kwa huduma za mawasiliano, huduma za kifedha na matumizi ya mitandao ya kijamii. 
  
Aidha, mafanikio hayo yameleta changamoto nyingi katika jamii. Changamoto hizo ni pamoja na kuibuka kwa makosa mapya ya jinai na pia mbinu mpya za kutenda makosa ya zamani.

Ndugu Wananchi,

 Makosa hayo hujumuisha uhalifu wa Mitandao ambao simu za mkononi, kompyuta au mifumo ya kompyuta hutumika kama nyenzo za kutenda uhalifu huo.
 

Mifano ya makosa hayo ni kama ifuatavyo:

1. Kumekuwepo na wizi wa fedha kwa njia ya mtandao,

2. Kumekuwepo na ugaidi kupitia kwenye mitandao,

4. Kuwepo na mmomonyoko mkubwa wa maadili,

3. Kumekuwepo na uharibifu wa miundombinu muhimu ya Taifa kwa makusudi, Kwa mfano kukatwa kwa makusudi Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano. [Hii imepelekea kuisababishia Serikali na Sekta binafsi hasara na kusababisha kukosekana kwa huduma mbalimbali za kiuchumi na za kijamii].

Ndugu Wananchi,

Kama mnavyofahamu kwenye kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililopita, Serikali ilipeleka Mswada wa kutunga sheria ya uhalifu wa mtandao (Cyber Crimes) na Sheria hiyo ilipitishwa na Bunge. 
  
Madhumuni ya kutunga sheria hii kama sheria nyingine zilizotungwa na Bunge hapa nchini ni kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii hasa kwenye matumizi ya TEHAMA.

Ndugu Wananchi,

Ndugu Wandishi wa Habari,

 Tanzania siyo nchi ya kwanza kutunga sheria  kama hii. Kuna nchi mbalimbali duniani zimetunga sheria kama hii, kwa mfano nchi ya Uingereza (UK Computer Misuse Act, 1990), India (IT Act, 2000), Malaysia (Computer Crime Act 2. ) Uganda (Computer Misuse Act, 2010), Korea ya Kusini (Information and Communications Network Act na Information and Communication Infrastructure Protection Act),  Singapore (The Computer Misuse and Cybersecurity Act), Maturities (Computer Misuse and Cybercrime Act, 2003), Afrika ya Kusini, Marekani (Computer Fraud and Abuse Act, 1984)  na nyingi nyinginezo.

Ndugu Wananchi sasa mmepata pahala pa kukimbilia, kwani mukitendewa uhalifu kupitia mitando sheria hii itawasaidia kupata haki zenu. Ninawashangaa sana wale wanaopinga kutungwa kwa sheria hii hapa Tanzania.
  
Haikubaliki hata kidogo kuona Wantanzania wengine wanakumbana na uhalifu kupitia Kwenye mtandao na wachache kwa faida zao binafsi wanataka Serikali ikae kimya. 
  
Sheria hii haina tofauti na sheria za nchi nyingine nilizozitaja hapo awali. Sheria hii imetungwa kwa mazingira ya nchi yetu ya Tanzania.

Ndugu Wananchi,

 Sheria hii  sasa imeshasainiwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kupitia hatua zote za kuiboresha.
  
Hatua ya MWISHO ilikuwa ni ile ya marekebisho yaliyofanywa na Bunge ambapo baadhi ya vifungu vilivyolalamikiwa  viliboreshwa. 
  
Kwa hivyo wananchi sasa tuipokee sheria hii na kuitumia. Sheria hii ni nzuri na itasaidia sana kuwalinda wananchi, mitandao na miundombinu yetu muhimu ya kitaifa.

Katika kuitumia sheria hii na kama ilivyo kwa sheria nyingine yoyote, patakapoonekana kuna mapungufu, marekebisho yatafanyika. Kwa hivyo kama kuna mtu yeyote mwenye maoni ya kuiboresha sheria hii anaweza kuleta  maoni Serikalini hapa Wizarani.
  
Ninarejea tena: Waheshimiwa Wabunge, Waheshimiwa Mabalozi, wadau mbalimbali wa  Sekta ya Mawasiliano, waandishi wa habari, wana-bloggers, na wananchi kwa ujumla kama kuna yeyote mwenye maoni ya kuboresha kifungu chochote cha sheria hii alate maoni hayo hapa Wizarani.

Serikali kupitia Wizara yangu itapokea maoni au ushauri huo, tutayatafakari na kuyafanyia kazi kwa kina. Haitosaidia sana kusema huko pembeni, jukwaa zuri la kuleta maoni ni kupitia Wizara yangu.

Ndugu Wananchi, na

Ndugu Waandishi wa Habari,

Hii haitokuwa sheria ya kwanza kufanyiwa marekebisho kama itaonekana kuna umuhimu wa kufanya hivyo.

Ahsanteni na Ninawashukuru sana kwa  kunisikiliza.

Watu Watano Wathibitishwa Kufariki Dunia Jijini Dar es Salaam Kutokana na Mafuriko

$
0
0

JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA
WIZARA YA MAMBO YANDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA

PRESS RELEASE
08/05/2015

WATU WATANO WATHIBITISHWA KUFARIKI DUNIA JIJINI DAR ES SALAAM KUTOKANA NA MAFURIKO
Watu watano wameripotiwa kupoteza maisha jijini Dar es Salaam kutokana na athari za mafuriko kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha jiji. Mvua hizo zinazonyesha kwa siku tatu mfululizo zimesababisha vifo vya watanzania hawa katika maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam kama ifuatavyo:
Mnamo tarehe 06/05/2015 majira ya saa moja kamili usiku huko maeneo ya Magomeni Kinondoni jijini Dar es Salaam mtu mmoja jina SHABAN S/O IDD, Miaka 73, Mkazi wa Manzese alisombwa na maji ya mto ng’ombe alipokuwa akijaribu kuvuka mto huo. Mwili wake ulipatikana siku iliyofuata 07/05/2015 akiwatayari amekwishafariki dunia na umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala.

Kifo kingine kilitokea tarehe 07/05/2015majira ya  saa sita kamili mchana huko maeneo ya Mwananyamala Mbuyuni Kata ya Mwananyamala, OysterBay, Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo mtu mmoja aitwaye MASUMBUKO S/O DOUGLASS @ LIMAMU, Miaka kati ya 50-55, mkazi wa Mwananyamala Mbuyuni, alianguka na kufariki dunia ghafla wakati anatoa maji yaliyoingia nyumbani kwake. Uchunguzi wa awali umebaini kuwa marehemu alikuwa na tatizo la ugonjwa wa kifafa hivyo wakati akihangaika kutoa maji, ugonjwa huo ulimpata na kuanguka kwenye maji na kufariki dunia baada ya kukosa msaada wa haraka. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi.

Mtu mwingine mwanaume RASHIDI S/O HASSAN, Miaka 36, Mkazi wa maeneo ya Mvuruhani Pemba Mnazi Kigamboni jijini Dar es Salaam alizama katika mkondo wa maji unaoelekea baharini tarehe 06/05/2015. Mwili wake ulipatikana tarehe 07/05/2015 ukiwa unaelea majini umbali wa mita 500 toka eneo alilozama.

Kifo kingine kimetokea tarehe 06/05/2015 huko Yombo Makangarawe ambapo mtoto aitwaye GLORIA D/O MREMA, mwaka mmoja na miezi mitatu alipotea baada ya watoto wenzake kumuacha wakati wakicheza pamoja. Juhudi za kumtafuta zilifanyika bila mafanikio hadi mwili wake ulipopatikana ukiwa unaelea majini katima mto mzinga akiwa tayari ameshapoteza maisha.  Mwili umehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke

Kifo kingine kimetokea tarehe 08/05/2015 saa moja kamili asubuhi huko maeneo ya Kinondoni Mkwajuni, Kata ya Mkwajuni Wilaya ya Kinondoni ambapo mtu mmoja mwanaume ambaye jina lake halikufahamika mara moja anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka (40-45) mkazi wa Kinondoni Mkwajuni, alikutwa amefariki dunia. Mwili umehifadhiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi.

Pamoja na vifo hivyo kuripotiwa, pia mtu mmoja ajulikanae kwa jina la MABULA S/O MOSSES, Miaka 65, Mkulima, Mkazi wa Vingunguti,  Buguruni wilaya Ilala amevunjika mguu wake wa kulia sehemu ya chini ya goti baada ya kuangukiwa na ukuta wa Godown la FIDA S/O HUSSEIN lililopakana na nyumba yake. Pia ukuta huo umesababisha uharibifu wa vitu mbalimbali. Majeruhi amepekwa Hospitali ya Amana kwa matibabu.
Katika kata ya Mchikichini, taarifa ya mafuriko inaonyesha takribani nyumba 60 hadi 70 zimefunikwa na maji hadi juu ya mapaa ambapo wakazi wake tayari walikuwa wamehama kufuatia agizo la Serikali kuwa wahame maeneo hayo. Pia takribani watu 30 hadi 35 wamejihifadhi katika shule ya Srkondari Mchikichini.
Katika Kata ya Jangwani, zipo nyumba zinazokadiriwa kufikia 90-100 zimefunikwa na maji hadi juu ya paa. Wakazi takribani 250-300 walihama mapema kufuatia taarifa hiyo ya Serikali. Aidha watu wanaokadiriwa kati ya 25-30 nao wamejihifadhi katika Shule ya Sekondari Mchikichini.  
Aidha, maeneo yaliyoathirika zaidi kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha ni Keko, Chang’ombe maduka mawili, Yombo Vituka, Vingunguti, Africana, Msasani Bonde la Mpunga, Eneo la Jangwani, Manzese, Kigogo, Mburahati, Boko Basihaya, na maeneo mengine ambayo taarifa zake bado hazijapokelewa
Barabara zinazounganisha katikati ya Jiji na pembezoni zimeharibika na hivyo kusababisha kutolewa maelekezo barabara hizo kufungwa ili kupunguza madhara ambayo yangeweza kutokea.
Aidha, madaraja mbalimbali yameharibika h
ivyo kukata mawasiliano kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine. Kwa mfano daraja la linalounganisha Mbagala na Mtoni Kijichi maarufu kama njia ya ng’ombe. Daraja lingine ni lile la Kinyerezi ambalo halipitiki baada ya kusombwa na maji.
Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Serikali limejiandaa kwa hali ya dharura itakayojitokeza. Pia Jeshi la Polisi limejipanga kukabili foleni kwa kuhusisha askari wa vikosi mbalimbali ili kukwamua tatizo hilo ambalo limesababishwa na uharibifu wa miundombinu.
Aidha nawataka wananchi wote kuchukua tahadhari ya hali ya juu hasa wale waishio maeneo ambayo ni mikondo ya maji au watumiaji barabara zinazopitiwa na mikondo hiyo. Wananchi wanaombwa kutoa taarifa za mapema na haraka pindi wanapoona au kugundua kuna maeneo au jambo  linalohatarisha maisha yao na ya watu wengine.
NB: Wakati huo huo zimepokelewa taarifa za kupatikana kwa miili ya watu watatu waliofariki ambayo inafanyiwa uchunguzi katika hospitali mbalimbali jiji Dar es Salaam ili kujua kama vifo hivyo vimetokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha jiji. Taarifa kamili zitatolewa kuhusu wajihi wa watu hao na wako katika hospitali gani
 
S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

Kajala Aapa Kutousahau Msaada wa Wema Sepetu

$
0
0
Kajala Masanja amesema kuwa pamoja na kuwa hawana waelewano mazuri na rafiki yake wa zamani Wema Sepetu, hawezi kusahau wema aliomfanyia wa kumtolea shilingi milioni 13 kwenye huku yake miaka kadhaa iliyopita.

Kajala amesema hafikirii kuzirudisha fedha hizo kwa Wema ambaye amekuwa akieleza kujuta kuutoa msaada huo.

Sio kwamba natamani kumrudishia milioni 13, kwa sababu mimi najua yeye alinisaidia kipindi mimi naHitaji na hakuna mtu yoyote alitokea kunisaidia kipindi hicho,” Kajala aliiambia Global TV.

Kweli nashukuru mpaka kesho kwa sababu alitoa msaada ambao siwezi kuusahau hata kama tuna ugomvi kiasi gani. Sasa kwa sababu yeye alisaidia kwa moyo mmoja na akikaa akiongea anajuta kwanini alinisaidia kumlipia Kajala inakuwa inamfutia hata zile baraka alizozipata.

Hii ndiyo Sababu ya Mwigizaji Ray Kutooa Hadi Sasa..Japo Umri Unazidi Kumtupa Mkono

$
0
0
Staa mkongwe wa Bongo Movies, Vincent Kigosi ‘Ray’ amefungukia sababu za kutooa licha ya kwamba umri umekwenda.

Akizungumza na gazeti la  Ijumaa katika mahojiano maalum, Ray alisema amekuwa akipangua mawazo ya kuoa kila wakati kutokana na ugumu wa kumpata mwanamke ambaye hatampa stress kama zinazowapata baadhi ya watu.

Alisema, kwa kuwa suala la kuoa ni jambo nyeti, halihitaji kukurupuka na hicho ndicho kimemfanya mpaka leo asiingie kwenye maisha ya ndoa.

“Unajua hili suala la ndoa ni sensitive ‘nyeti’ sana, halihitaji kukurupuka, linakutaka ukiingia kwenye uhusiano umchunguze vizuri huyo uliyempata ili kujiaminisha kwamba, hatakusumbua.

Hilo ndilo linalonifanya niwe singo mpaka leo, najua wengi wananishangaa lakini kwa kifupi ugumu wa kumpata mweza sahihi ndiyo sababu ya kutooa mpaka leo,” alisema Ray.

Alipoulizwa kwamba, ina maana kwa wapenzi wake waliopita wakiwemo Ruth Suka ‘Mainda’, Blandina Chagula ‘Johari na Hans Chuchu hakuna aliyeona anafaa kuwa mke, msanii huyo alicheka sana kisha akasema: “Wewee, acha mambo yako.”

Sakata la Escrow: IKULU Yasema Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini Ndugu Eliakim C. Maswi Hana HATIA

$
0
0
MATOKEO YA UCHUNGUZI WA AWALI KUMHUSU NDUGU ELIAKIM C. MASWI, KATIBU MKUU, WIZARA YA NISHATI NA MADINI
_________________________________________________

1.0    Utangulizi

1.1  Katika mkutano wake wa 16 na 17, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na mambo mengine, lilijadili Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali iliyotokana na Taarifa ya Ukaguzi wa Akaunti ya Tegeta Escrow uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

1.2 Baada ya majadiliano, Bunge lilipitisha maazimio kadhaa yaliyoelekezwa kwa Serikali kwa ushauri na utekelezaji.
 
Mojawapo ya maazimio hayo yalimtaja Ndugu Eliakim C. Maswi, ambaye ndiye Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, kuwa amehusika kijinai au kimaadili katika miamala iliyotokea katika akaunti ya Tegeta Escrow.

1.3 Wakati anahutubia Taifa kupitia Wazee wa Dar es Salaam tarehe 22 Desemba, 2014, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisema ifuatavyo:-

“Kuhusu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, kwa vile ni Mtumishi wa Umma, anatawaliwa na Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma. Hivyo, nimeshaelekeza Mamlaka kuchunguza tuhuma zake na hatimaye ikibainika ana makosa hatua za kinidhamu zitachukuliwa.”

1.4 Tuhuma dhidi ya Ndugu Eliakim C. Maswi zimeshughulikiwa katika ngazi mbili tofauti. Amechunguzwa na Sekretarieti ya Maadili ya Umma, kisha baada ya hapo alichunguzwa pia na Kamati ya Uchunguzi wa Awali iliyoundwa na mamlaka yake ya nidhamu.

2.0    Sekretarieti ya Tume ya Maadili

2.1 Kifungu 18 (2) (c) na (3) cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma kinaipa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma mamlaka na uwezo wa kuchunguza tuhuma yoyote ya kuvunjwa kwa maadili ya uongozi wa umma yanayotawaliwa na Sheria hiyo. 
 
Tuhuma dhidi ya Ndugu Eliakim C. Maswi zilizomo kwenye maazimio ya Bunge zinatawaliwa na Sheria hiyo.

2.2 Katika kutekeleza majukumu yake, Sekretarieti ya Maadili ya Umma ilifanya uchunguzi wa awali na kisha kumhoji Ndugu Eliakim C. Maswi tarehe 19 Desemba, 2014.

2.3 Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma haijabaini kuwepo kwa maslahi binafsi katika uamuzi uliofanywa na Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini wa kuruhusu fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow kutolewa. 
 
Aidha, hawakubaini ukiukwaji wowote wa maadili ya viongozi wa umma uliofanywa na Ndugu Eliakim C. Maswi. 
 
Waliona kuwa yote aliyoyafanya yalizingatia matakwa ya Sheria, ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na ridhaa ya TANESCO. Hivyo, Sekretarieti ya Maadili haikuona msingi wowote wa kuendelea na shauri la Ndugu Eliakim C. Maswi, na wamelihitimisha.

3.0 Kamati ya Uchunguzi wa Awali ya Mamlaka ya Nidhamu

3.1 Kwa mujibu wa Kifungu 4(3) (d) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 (kama ilivyorekebishwa) Katibu Mkuu Kiongozi ndiye Mamlaka ya Nidhamu ya Makatibu Wakuu.

3.2 Kwa kuzingatia Azimio husika la Bunge, na kwa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Katibu Mkuu Kiongozi aliunda Kamati ya Uchunguzi wa Awali dhidi ya Ndugu Eliakim C. Maswi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, chini ya Kifungu cha 36 cha Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003 kinachotamka ifuatavyo:-
 
“Where it is necessary to institute disciplinary proceedings against a public servant, the disciplinary authority shall make preliminary investigations before instituting disciplinary proceedings.”

3.3    Kwa mamlaka aliyonayo chini ya Kanuni 35(2)(b) na Kanuni 37 ya Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003, Katibu Mkuu Kiongozi alimpumzisha Bwana Eliakim C. MASWI kutekeleza majukumu yake ya kazi ya Katibu Mkuu ili kupisha uchunguzi wa awali. 
 
Uchunguzi wa awali ulifanyika chini ya Kanuni ya 36 ya Kanuni za Utumishi wa Umma zilizotajwa, pamoja na Kifungu 4(3) (d) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002, kama ilivyorekebishwa.

3.4 Kwa mamlaka aliyonayo chini ya Kanuni zilizotajwa kwenye ibara 3.3 hapo juu, Katibu Mkuu Kiongozi aliteua Kamati ya Uchunguzi wa Awali na kuipa Hadidu za Rejea zifuatazo:

3.4.1 Kubainisha wajibu na madaraka halisi ya Katibu Mkuu, Wizaraya Nishati na Madini, kwenye uendeshaji wa TANESCO kwa ujumla, na hususan kwenye kufungua, kuendesha na hatimaye kufungwa kwa akaunti ya Tegeta Escrow.

3.4.2 Kubainisha na kupata maelezo ya kina juu ya kuhusika kwa Bwana Eliakim C. Maswi katika mchakato na mtiririko mzima wa akaunti ya Tegeta Escrow, tangu kufunguliwa hadi kufungwa.

3.4.3 Kubainisha na kupata maelezo ya kina iwapo kuna jambo lolote ambalo Bwana Eliakim C. Maswi alilifanya au ambalo alipaswa  kulifanya lakini hakulifanya, linalomstahilisha achukuliwe hatua za nidhamu.

3.4.4  Kubainisha na kupata maelezo ya kina iwapo katika hatua yoyote ya mchakato na mtiririko wa tangu kufunguliwa hadi kufungwa kwa akaunti ya Tegeta Escrow, Bwana Eliakim C. Maswi alifanya  jambo lolote linalodhihirisha matumizi mabaya ya mamlaka yake kama Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, kwa namna iliyosababisha hasara ya aina yoyote ile kwa Taifa la Tanzania.

3.4.5  Kubainisha na kupata maelezo ya kina iwapo katika hatua yoyote tangu akaunti ya Tegeta Escrow ilipofunguliwa hadi ilipofungwa, Bwana Eliakim C. Maswi hakuchukua tahadhari ya kutosha kulinda maslahi ya umma na kusababisha kupotea kwa fedha za umma kwa uzembe au matumizi mabaya ya madaraka.

3.4.6 Kubainisha iwapo kuna mahali popote katika mchakato wa akaunti ya Tegeta Escrow ambapo Bwana Eliakim Chacha Maswi alifanya jambo lolote linaloashiria kitendo cha kijinai, au kukiuka maadili ya viongozi wa umma.

3.4.7 Kuandaa taarifa ya uchunguzi wa awali kwa msingi wa Hadidu za Rejea zilizomo humu na kuiwasilisha kwa Katibu Mkuu Kiongozi. Taarifa hiyo, pamoja na mambo mengine, ipendekeze hatua za kuchukuliwa kwa kila eneo ambalo Kamati itabaini umuhimu wa hatua kuchukuliwa.

3.5   Mapendekezo ya Kamati ya Uchunguzi wa Awali

3.5.5 Kamati haijabaini kosa lolote ambalo linaweza kusababisha Ndugu Eliakim Chacha Maswi, Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, kufunguliwa mashtaka ya kinidhamu kwa kukiuka Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298 ikisomwa pamoja na Kanuni zake za mwaka 2003 kwa kuruhusu Benki Kuu ya Tanzania kutoa fedha zilizokuwa katika Akaunti ya Tegeta Escrow.

4    Hitimisho la Uchunguzi wa Awali

4.4 Uchunguzi wa Awali uliofanywa na Sekretarieti ya Maadili umebaini kuwa Ndugu Eliakim C. Maswi hana makosa yoyote ya kimaadili katika mchakato wa fedha za akaunti ya Tegeta Escrow.

4.5  Hali Kadhalika Uchunguzi wa Awali uliofanywa na Kamati ya Uchunguzi wa Awali iliyoundwa na Katibu Mkuu Kiongozi umebaini kuwa Ndugu Eliakim C. Maswi, “hakutenda au kuhusika na jambo lolote linaloashiria vitendo vya jinai au kukiuka Maadili ya Viongozi wa Umma”.

4.6   Ushahidi wa vielelezo uliotolewa kwenye Sekretarieti ya Maadili na kwenye Kamati ya Uchunguzi wa Awali umejitosheleza kuthibitisha kwamba Ndugu Eliakim C. Maswi alitenda kazi yake kwa kiwango kinachoridhisha kwa kufanya mawasiliano na mamlaka mbalimbali na kwa nyakati tofauti kwa lengo la kuhakikisha na kujiridhisha kwamba kufungwa kwa Akaunti ya Tegeta Escrow kunafanyika kwa usahihi.

4.7 Hakuna ushahidi wowote kuwa Ndugu Eliakim C. Maswi alikuwa miongoni mwa waliopata mgao wa fedha au fadhila yoyote kutokana na kufungwa Akaunti ya Tegeta Escrow.

4.8 Kwa nafasi yake ya mamlaka ya nidhamu Katibu Mkuu Kiongozi, ameridhika kuwa Ndugu Eliakim C. Maswi hana makosa yoyote aliyoyafanya katika mchakato wa akaunti ya Tegeta Escrow yanayostahili adhabu. 
 
Hivyo, mchakato wa kinidhamu, kimaadili na kijinai dhidi yake umefikia mwisho wake. Mwenye mamlaka ya uteuzi atatafakari taarifa hizi na kuamua cha kufanya kuhusu ajira yake baadaye.
 
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
8 Mei, 2015

SAKATA LA OPARESHENI TOKOMEZA: Ikulu Yasema Mawaziri WOTE Waliofukuzwa Kwa Kashfa Hiyo Hawana HATIA

$
0
0
TAARIFA YA KUKAMILIKA KWA KAZI YA TUME YA UCHUNGUZI WA MALALAMIKO YALIYOTOKANA NA UTEKELEZAJI WA OPERESHENI TOKOMEZA
___________________________________________ 

1.0    Utangulizi:

1.1 Tarehe 01/05/2014, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliunda Tume ya Uchunguzi kuhusu malalamiko yaliyotokana na utekelezaji wa Operesheni Tokomeza. Aliteua Makamishna watatu ambao ni Mhe. 
 
Balozi Jaji (Mst) Hamisi Amiri Msumi (Mwenyekiti wa Tume), Mhe. Jaji (Mst) Stephen Ernest Ntashima Ihema (Kamishna), Mhe. Jaji (Mst) Vincent Kitubio Damian Lyimo (Kamishna) na Ndugu Frederick Kapela Manyanda (Katibu wa Tume).

1.2  Operesheni Tokomeza ilikuwa Operesheni iliyobuniwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa lengo jema na muhimu la kupambana na ujangili unaotishia urithi wetu wa wanyama pori, hususani tembo, faru, nyati, twiga, pundamilia n.k.

2.0  Hadidu Rejea kwa Tume

2.1Kuchunguza namna Operesheni Tokomeza ilivyotekelezwa;

2.2.Kuchunguza iwapo maafisa waliotekeleza Operesheni Tokomeza walizingatia sheria, kanuni, taratibu na hadidu rejea walizopewa;

2.3.Kuchunguza iwapo maafisa waliotekeleza Operesheni Tokomeza walivunja sheria, kanuni, taratibu na hadidu rejea walizopewa;

2.4.Kuchunguza iwapo kuna watu waliokiuka sheria yoyote wakati wa utekelezaji wa Operesheni Tokomeza na iwapo hatua zilizochukuliwa na maafisa wa Operesheni Tokomeza dhidi ya wakosaji hao na mali zao zilikuwa sahihi;

2.5.Kupendekeza hatua zinazostahili kuchukuliwa dhidi ya maaafisa wa Operesheni Tokomeza waliokiuka sheria, kanuni, taratibu na hadidu rejea za Operesheni Tokomeza; na

2.6.Kupendekeza mambo yanayopaswa kuzingatiwa katika kupanga na kutekeleza Operesheni nyingine kama hii ili kuzuia na kuepuka malalamiko mengine kama yaliyotokea kwenye Operesheni Tokomeza.

3.0    Kukamilika kwa kazi ya Tume

3.1  Tume imekamilisha kazi yake na kukabidhi taarifa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, tarehe      10 Aprili, 2015. Kwa maagizo ya Rais tumeisoma na kuichambua taarifa hiyo vya kutosha. 
 
Kwa hakika Tume imefanya kazi kubwa sana, na nzuri sana ya uchunguzi na uandishi wa taarifa. Kazi imefanywa kwa weledi na umakini wa hali ya juu na kwa lengo dhahiri la kutenda haki. Katika siku 265, Tume ilitembelea wilaya 38 katika mikoa 20 na kuhoji jumla ya mashahidi 259. 
 
Mikoa iliyohusika ni Kigoma, Katavi, Rukwa, Mbeya, Kagera, Geita, Shinyanga, Simiyu, Mara, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Iringa, Morogoro, Pwani, Tabora, Singida, Manyara, Arusha na Tanga.

3.2 Tume imejitahidi kuwahoji wote waliokuwa na malalamiko, kuwahoji mashuhuda, kuwahoji watuhumiwa, na kukusanya ushahidi wa aina mbalimbali ili ama kuthibitisha makosa pale yalipofanyika na kupendekeza hatua za kuchukua, au kujiridhisha kuwa tuhuma na malalamiko hayakuwa ya msingi.
 
 Kazi hiyo imefanywa vizuri na kurahisisha kazi ya Serikali ya kuchukua hatua zinazostahili.

4.0    Operesheni Tokomeza ilivyotekelezwa 

4.1   Tume ilibaini kuwa katika kipindi cha mwezi mmoja cha utekelezaji wa Operesheni Tokomeza iliyoanza tarehe 4 Oktoba, 2013, mafanikio mengi yalipatikana, ikiwemo:

4.1.1 Watuhumiwa 1,030 wa makosa mbalimbali yanayohusu ujangili na uvunaji haramu wa misitu walikamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria;

4.1.2   Kukamatwa kwa meno ya 211 yenye uzito wa kilo 522, meno ya ngiri 11, mikia ya wanyama mbalimbali 36, ngozi za wanyama mbalimbali 21, pembe za swala 46, mitego ya wanyama 134, ng’ombe 7,621 waliokuwa wanachungwa ndani ya hifadhi na misitu, baiskeli 58, pikipiki 8 na magari 9;

4.1.3  Katika kipindi cha Operesheni kulikamatwa jumla ya bunduki za kijeshi 18, bunduki za kiraia 1,579, risasi 1,964, mbao vipande 27,913, mkaa magunia 1,242, magogo 858 na misumeno 60.

4.1.4  Operesheni ilifanikiwa kupunguza kasi ya mauaji ya tembo kutoka tembo wawili kwa siku hadi tembo wawili kwa mwezi wakati wa Operesheni;

4.2 Operesheni ilisitishwa rasmi tarehe 01/11/2013 ili kupisha uchunguzi wa malalamiko yaliyojitokeza. Baada tu ya kusitishwa kwa Operesheni wafugaji wengi wamerudisha mifugo yao katika maeneo ya hifadhi yaani Mapori ya Akiba, Hifadhi za Taifa, Hifadhi za Misitu na Maeneo Oevu na ujangili ukaanza kurejea. 
 
Aidha watuhumiwa waliokuwa wametoroka kukimbia Operesheni wameanza kurejea kwenye makazi yao.

5.0 Vitendo vya Ukiukwaji wa Sheria, Kanuni, Taratibu na Hadidu Rejea

5.1 Tume imebaini kuwa katika utekelezaji wa Operesheni kulikuwa na matukio ya ukiukwaji wa Sheria, Kanuni, Taratibu na Hadidu Rejea. Ukiukwaji huu umesababisha madhara kwa wananchi mbalimbali ikiwemo vifo, madhara ya mwili na kadhalika.

5.2  Tume ilichunguza matukio 15 ya vifo, na kuridhika kuwa vifo tisa (9) kati ya hivyo vilisababishwa na mateso ambapo watendaji kwenye Operesheni walitumia nguvu kubwa kupita kiasi dhidi ya watuhumiwa wakati wa ukamataji au kuhoji.
 Kabla ya vifo watu hao walikuwa chini ya ulinzi wa askari wa Operesheni na kuna ushahidi wa kitabibu (medical reports), ushahidi wa kimazingira na ushahidi wa kuona, unaohusisha vifo vya marehemu hao na mateso kutoka kwa askari wa Operesheni. 
 
Tume haikupata ushahidi wa kuhusisha vifo sita (6) vilivyobaki moja kwa moja na Operesheni Tokomeza.

5.3 Tume ilichunguza madai ya mateso yaliyosababisha madhara kwenye miili ya wahusika. Walalamikaji walieleza Tume kwamba waliteswa ili waoneshe silaha au nyara zilipofichwa au wakiri kujihusisha na ujangili au ujambazi na wataje washirika wao wa mtandao wa ujangili. 
 
Kulikuwa pia na malalamiko ya udhalilishwaji. Malalamiko hayo yalitoka kwenye wilaya ishirini na mbili (22) za mikoa mbalimbali. 
 
Yapo matukio ambayo walalamikaji waliweza kuleta mbele ya Tume uthibitisho wa kuteswa, na walionesha makovu na kutoa vyeti vya matibabu na PF 3 walizopewa baada ya kuumia.

5.4 Tume imebaini kuwepo matendo mbalimbali ya ukiukwaji wa sheria, kanuni, taratibu na hadidu rejea uliofanywa na baadhi ya askari wa Operesheni na maafisa wengine walioshiriki katika utekelezaji wake, ikiwemo matukio yanayoashiria rushwa na udanganyifu mbalimbali.

5.5 Tume ilishughulikia pia tuhuma za wizi, upotevu na uporaji wa mali. Walalamikaji wa kundi hili walieleza Tume kuwa wakati wa utekelezaji wa Operesheni, waliibiwa au kupoteza fedha na mali zao wakati na baada ya kukamatwa au kupekuliwa na askari wa Operesheni. 
 
Tume ilichunguza jumla ya matukio ishirini na tatu (23) ya aina hiyo na kubaini kuwa malalamiko mengi yalitokana na askari wa Operesheni kutofuata sheria, kanuni na taratibu za ukamataji, kuhoji na upekuzi maungoni mwa watuhumiwa na kwenye nyumba zao.
 
Kasoro zilizoonekana ni pamoja na kutoshirikisha viongozi au watu huru katika upekuzi na kutojazwa hati za upekuzi mara baada ya upekuzi. Kasoro nyingine ni askari wengi kuingia kwenye nyumba kwa wakati mmoja. 
 
Aidha, Tume imebaini walalamikaji wengine waliongeza chumvi katika ushahidi wao kuhusu idadi ya mali na fedha zilizopotea au kuibiwa na hivyo ushahidi wao kutoaminika au kuthibitika.

5.6 Tume ilichunguza malalamiko ya kubakwa wakati wa utekelezaji wa Operesheni. Matukio yaliyochunguzwa na Tume yalikuwa katika Kijiji cha Iputi, Wilaya ya Ulanga, Mkoa wa Morogoro na Kijiji cha Mwantimba Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu na Wilayani Sikonge. 
 
Hata hivyo wote waliodai kubakwa hawakujitokeza mbele ya Tume kutoa ushahidi wao, hivyo Tume haikuweza kuchunguza malalamiko yao. 
 
Alijitokeza mlalamikaji mmoja Wilayani Ulanga, Morogoro, lakini Tume haikuridhika na maelezo yake, ambayo hayakutosheleza kubainisha kosa kwenye utekelezaji wa Operesheni Tokomeza.

5.7 Tume ilibaini kuwa wapo watuhumiwa waliofikishwa mahakamani na kutiwa hatiani na wengine kuachiwa. Tume imeona kuwa hatua hii ilikuwa sahihi kisheria. Lakini Tume ilibaini pia kuwa baadhi ya watuhumiwa hawakufikishwa mahakamani. 
 
Badala yake maafisa wa Operesheni walijichukulia mamlaka ya kutoa adhabu kwa watuhumiwa kama vile kukamata na kuzuia mali zao, kuchoma moto nyumba na mali zilizokuwa kwenye maeneo ya hifadhi, kuua au kujeruhi mifugo iliyokutwa kwenye maeneo ya hifadhi au kuuza kwa mnada ng’ombe waliokamatwa kwenye maeneo ya hifadhi. 
 
Hatua nyingine inayolalamikiwa ni kuchukua bunduki zinazomilikiwa kisheria.

5.8  Tume imebaini kwamba katika baadhi ya maeneo askari wa Operesheni walichoma nyumba moto kwa madai ya nyumba hizo kujengwa kwenye hifadhi. 
 
Malalamiko hayo yalitoka katika Wilaya za Mlele na Mpanda, Mkoa wa Katavi, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya; Wilaya za Nkasi na Sumbawanga, Mkoa wa Rukwa; na Wilaya ya Simanjiro, Mkoa wa Manyara. 
 
Katika uchunguzi wa matukio haya Tume imebaini yafuatayo:

  • Wanakijiji hawakupewa taarifa ya kutosha kuhamisha mali zao kabla ya kuchoma nyumba zao;
  • Baadhi ya wanakijiji walipoteza vyakula na mali zao katika zoezi hilo la uchomaji moto;
  • Kuna vijiji vilivyosajiliwa lakini sehemu ya vitongoji vyake viko ndani ya Hifadhi za Taifa;
  • Kuna maeneo ya hifadhi au ushoroba (buffer zone) ambayo hayana alama za mipaka kati ya hifadhi  au ushoroba na vijiji husika;
  • Kuna nyumba ambazo hazikuwa kwenye eneo la hifadhi au ushoroba na hivyo zilichomwa moto kinyume cha sheria. 
  • Baadhi ya matukio na malalamiko ya kuchomewa moto nyumba yalitokea kabla ya Operesheni.

5.9  Uchunguzi wa Tume umebaini kuwepo kwa tatizo kubwa la wafugaji kutoka nje ya nchi na wafugaji wenyeji kuingiza mifugo yao katika Mapori ya Akiba, Hifadhi ya Misitu, Maeneo Oevu na Hifadhi za Taifa. 
 
Maeneo yaliyoathirika sana na tatizo hili ni Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Pori la Akiba la Kigosi – Moyowosi, Pori la Akiba la Maswa, Mapori ya Akiba ya Biharamulo – Burigi – Kimisi na Pori la Akiba la Kijereshi.

Katika baadhi ya maeneo imethibitika kwamba wapo ng’ombe waliouawa kwa kupigwa risasi baada ya kukutwa ndani ya hifadhi.
   
Aidha, Tume imeridhika kwamba kuna ng’ombe wa walalamikaji waliokamatwa na kuuzwa kwa mnada. Uuzaji wa ng’ombe katika tukio hili haukuzingatia utaratibu wa kisheria.

5.10 Tume ilipata ushahidi kwamba katika maeneo mbalimbali askari wa Operesheni walikamata au kuchukua bunduki, risasi pamoja na vitabu vyake hata kwa silaha zinazomilikiwa kihalali. 
 
Maeneo ambayo yalikuwa na malalamiko ya watu kuchukuliwa silaha zao ni mikoa saba (7) ambayo ni Katavi, Mbeya, Lindi, Morogoro, Tabora, Manyara na Pwani ambapo jumla ya watu sitini na mbili (62) walijitokeza mbele ya Tume kulalamika tukio hili.

6.0  Hatua Zitakazochukuliwa na Serikali

6.1  Baada ya kupitia kwa kina taarifa ya Tume, pamoja na mapendekezo ya Tume, Serikali itafanya yafuatayo:

6.1.1  Hatua za kimashtaka zitaendelea kwa shauri la mauaji ambalo upelelezi wake umekamilika na hatua za kiuchunguzi zitaendelea kwa mashauri mengine nane (8) ya mauaji ambayo upelelezi wake haujakamilika;

6.1.2  Hatua za kisheria na kiutawala zitachukuliwa dhidi ya watuhumiwa waliothibitika kuwatesa watu 15 wakati wa Operesheni;

6.1.3 Hatua za kiuchunguzi zinazofanywa na TAKUKURU kuhusu tuhuma za rushwa na udanganyifu zilizothibitika zitaendelea;

6.1.4 Silaha zinazodaiwa kumilikiwa kihalali zitafanyiwa uhakiki na ukaguzi wa kina kuhusu umiliki na matumizi yake na endapo hakutakuwa na sababu nyingine za kisheria za kuzuia urejeshwaji, wamiliki warejeshewe silaha zao kwa mujibu wa sheria na taratibu;

6.1.5 Mali ambazo zimethibitika kuchukuliwa wakati wa Operesheni kwa tuhuma za kuhusishwa na uvunaji haramu wa mazao ya misitu zirejeshwe endapo hakutakuwa na sababu za kisheria kuendelea kuzishikilia;

6.1.6 Serikali itafanya uhakiki wa vijiji ambavyo vimesajiliwa na vimo ndani ya hifadhi ili kutatua migogoro ya ardhi kati ya hifadhi na vijiji. Aidha, Serikali itahakikisha kunakuwa na ushirikiano wa karibu kati ya Msajili wa vijiji au mamlaka husika  na Wizara ya Maliasili na Utalii ili kuepuka kusajili vijiji ndani ya maeneo ya hifadhi;

6.1.7 Wizara ya Maliasili na Utalii itatayarisha kanuni zitakazoweka utaratibu wa kuwaondoa watu waliovamia na kujenga makazi katika hifadhi;

6.1.8 Sheria zote zinazolinda maeneo ya hifadhi zitafanyiwa marekebisho ili kuongeza adhabu kwa kosa la kuingiza mifugo kwenye Hifadhi bila kujali uraia wa wamiliki wa mifugo hiyo;

6.2 Kwa vile Tume imejiridhisha na faida kubwa na mafanikio ya Operesheni    Tokomeza, Serikali itaendelea na Operesheni kama hizo kadri     itakavyojitajika ili kuokoa maliasili za Taifa, ikiwemo wanyama, hifadhi     na misitu. 
 
Hata hivyo ushauri wa Tume juu ya kuboresha upangaji,     usimamizi na utekelezaji wa Operesheni hizo itazingatiwa kikamilifu.

7.0    Mawaziri Waliojiuzulu
Tume ilijiridhisha kuwa Mawaziri wote waliojiuzulu, yaani Mhe. Dkt. Emmanuel J. Nchimbi, Mb., Mhe. Balozi Khamis Kagasheki, Mb., Mhe. Mathayo D. Mathayo, Mb., na Mhe. Shamsi V. Nahodha, Mb.,hawakuhusika moja kwa moja na makosa yoyote ya utekelezaji kwenye Operesheni Tokomeza. Hivyo, waliwajibika kisiasa tu na hakuna hatua nyingine inayostahili dhidi yao.

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
8 Mei, 2015

Kioja..Aunty Lulu Adai Makalio Yake Makubwa Yanamtesa Sana..Wavulana Wanamfuata Kutaka Kamchezo Kabaya

$
0
0
MWIGIZAJI Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ ametoa kioja cha aina yake baada ya kuibuka na kusema kuwa makalio yake yanamtesa akidai anasumbuliwa sana na wanaume wanaovutiwa nayo faragha.

Akipiga stori na Risasi Jumamosi, Aunty Lulu alisema wanaume wengi wamekuwa wakimiminika kutaka baada ya kusambaziana kuwa mwigizaji huyo analitumia umbo lake ndivyo sivyo.

Nawaomba wanaume waache kunifatafata jamani wananikosesha amani kwani mimi nimefundwa  najua madhara ya hako kamchezo kabaya, siwezi kuthubutu hata  mara moja,” alisema Aunty Lulu

~Global Publishers

Despite Being The No.1 Victim, Wema Sepetu Criticizes And Rejects Cyber Bullying/Crime Law Just For Freedom of Speech To Tanzanians

$
0
0
Wema Sepetu, Diamond Platnumz, Lulu Elizabeth Michael and Kajala Masanja are Tanzanian celebrities who have been experiencing cyber bullying at the high degree. But Wema Sepetu, one of the most influential celebs in Tanzania has criticized negatively the Cyber Bullying/crime bill saying that if it turns to be law it will be deny freedom of speech to Tanzanians and politicians want it just because they will benefit from it by hiding their wrong doings. Below is what Wema Posted on Instagram......



However, Wema seems to get influency from Mange Kimambi to reject the bill because Mange posted nice article on her blog rejecting the bill and reasons why it should not pass as law, Mange and Wema are like sisters because Mange is the one who discovered Wema through Miss Dar Indian Occean in 2006 and eventually Wema Became Miss Tanzania the same year.

Anyhow, this law is not good, it will not be appropriate to a country which prioritize good and transparent governance

Photo: A Glimpse of Jacqueline Wolper's Closet Which Looks Like a Boutique At Her Home !

$
0
0
Forget about Lulu and Wema Sepetu, Jacqueline Wolper is the Tanzanian celeb with huge budget per year just for buying clothes and other fashion items. The actress likes to wear and she looks stylish everyday. Here is a glimpse of her closet......remember it is still not exposed fully! . And below is what she captioned with the photo......
"Good morning farm, am getting ready to go to work...as always the hardest part of starting my day is finding what to wear...look at me"

Pamoja na Kukanusha Mara Nyingi ..Watu Wadai Wema Sepetu Anatumia Madawa ya Kulevya "Unga"

$
0
0
PAMOJA na mwenyewe kukanusha kuwa si mtumiaji wa madawa ya kulevya (unga), watu wanazidi kusema eti supastaa wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu ‘Madam’ anatumia unga, Risasi Jumamosi limesheheni data.


UBUYU WAVUJISHWA
Kwa mujibu wa chanzo makini, Wema amekuwa akitumia kilevi hicho kwa muda mrefu huku akifanya jambo hilo kwa siri kubwa.“Hivi hamna habari ya Wema kubwia unga? Mbona kila mtu anajua, watu wengi tu wanafahamu lakini wanashindwa namna tu ya kumueleza mwenyewe ili aache maana kila mtu anamhofia si unamjua naye Madam mtu wa kumaindimaindi,” kilisema chanzo hicho.

MITANDAO YAKAZIA MADAI
Kama hiyo haitoshi, kwa nyakati tofauti, watumiaji mbalimbali wa mitandao ya kijamii wamekuwa wakidai kuwa staa huyo anabwia unga licha ya kuwa hawana ushahidi wa moja kwa moja.“Mimi sijawahi kumuona lakini kuna watu wake wa karibu tu wananihakikishia kwamba Wema anatumia madawa ya kulevya, ila naamini mwenyewe anaujua ukweli wote wa haya yanayosemwa,” ilisomeka sehemu ya maoni mtandaoni.

RISASI LAMFUNGIA KAZI
Baada ya kupata madai hayo, Risasi Jumamosi lilimfungia kazi Madam ili kuweza kumsikia anazungumziaje tuhuma hizo nzito.

Jumatano iliyopita, mwanahabari wetu alikwenda nyumbani kwa mwigizaji huyo mwenye mvuto wa kipekee, Mtaa wa Bwawani-Kijitonyama lakini bahati mbaya alikuwa ametoka kwenda kurekodi na hata alipofanya subira hadi jioni, bado hakurejea huku simu yake ikiita bila kupokelewa.

JITIHADA ZAIDI
Siku iliyofuata, mwanahabari wetu aliyeambatana na mmoja wa wahariri wa Global Publishers, walitia timu kwa mara nyingine nyumbani kwa Madam lakini pia mwigizaji huyo alikuwa ametoka lakini bahati nzuri alipopigiwa simu alipokea, mambo yalikuwa hivi:Risasi: Wema tumekutafuta sana hapa nyumbani kwako bila mafanikio tuna ishu ya msingi kweli tunataka kujua kutoka kwako?

Wema: Poleni, ishu gani?
Risasi: Tumepokea habari kuwa wewe unatumia madawa ya kulevya,  umewahi kusikia hizi habari?
Wema: Ndiyo hizo habari nimewahi kuzisikia. Nakumbuka nilianza kuzisikia tangu kipindi kile mimi natembea na CK (yule kigogo wake), walivumisha sana lakini hakuna ukweli wowote.

ADAI WAMEMPONZA
“Tena imefika wakati wananikosesha hadi amani, imenifanya hadi niwe nakaguliwa kupindukia bila sababu za msingi, juzi hapa wakati naenda Mwanza (kwenye shoo ya Instagram), walinibana sana pale Air Port hadi nikataka kuachwa na ndege.


AISHI KWA TAHADHARI
“Yaani kwa sasa nimelazimika kuweka hadi ulinzi mkali pale nyumbani, maana huwezi jua watu wasionipenda wanaweza kuja wakanibambikia nikaonekana natumia kumbe sijui hata ukoje. Sasa hivi kila atakayeingia lazima akaguliwe, ahojiwe ndipo aingie.

ATAJA KUHUSISHWA NA ROMMY
“Kuna wakati walinitaja kuwa natumia kwa kuwa nina ukaribu na Rommy Johnson (binamu yake msanii Diamond) kitu ambacho nilikikanusha na ninaendelea kusema hakuna ukweli wowote.

MAMA’KE ARIPOTI POLISI
“Ili kuwataka watu wasinihusishe kwa namna yoyote na kujihadhari, tuliongea na mama, akaenda kutoa taarifa polisi Mabatini ili nisije kupata tatizo lolote linalohusishwa na madawa ya kulevya.”

RAFIKI ZAKE WANENA
Mwanahabari wetu aliwavutia waya marafiki wa Wema, Aunt Ezekiel na Martin Kadinda ambaye ni meneja wa mwigizaji huyo ambao kwa pamoja walidai hawajawahi kumuona Madam hata siku moja akibwia unga achilia mbali kukaa karibu na wabwiaji.

“Sijawahi kumuona Wema hata siku moja anatumia hivyo vitu (unga), watakuwa wanamzushia ili watimize azma yao ya kumchafua si unajua si wote wanampenda?,” alisema Aunt huku Martin akikazia:“Hakuna kitu kama hicho, Madam hatumii bwana, sisi tupo naye, tunafanya naye kazi siku zote, hatujawahi kumuona, huo ni uzushi tu.”

~Global Publishers

Askofu Gwajima Asimamisha Mvua Dar "Mvua imekoma kuanzia sasa na haitaharibu tena, na ninaiamuru ardhi imeze maji yote yaliyojaa juu ya nchi".

$
0
0
Askofu Gwajima....." Watu wa utabiri wa hali ya hewa wanasema mvua itanyesha zaidi LAKINI mimi nasema HAPANA mana tumezijua Hila zake shetani"

Katika mahubiri yake jana jioni tarehe 08/05/2015 siku ya Ijumaa, Askofu Mkuu wa Makanisa ya Ufufuo na Uzima alifundisha juu ya somo liitwalo "VITA VYA HALI".

Katika somo hilo Askofu Gwajima alibainisha wazi ya kuwa sio kila mabadiliko ya hali ya hewa yanayotokea duniani ni matokea ya nguvu za kiasilia za dunia yaani Nature au ni mabadiliko ya majira ya mwaka bali wapo watu pia wenye uwezo wa kubadili hali ya hewa kwa njia za kichawi na kusababisha mafuriko makubwa, vifo, uharibifu Wa mali na hasara zinazoweza kuwarudisha watu nyuma.

Katika kudhihirisha mambo hayo Askofu Gwajima alitolea mfano mtu mmoja aliyewahi kuishi duniani aitwaye Nicolas Tesla ambaye alikua na uwezo mkubwa juu ya kubadili na kutawala(control) hali ya hewa.

Baadaye nikaunganisha ujumbe wa Askofu Gwajima na nikagundua jambo hili ni kweli kabisa baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Sadick kutangaza kuwa MVUA HIZI ZINASAIDIA SANA KUWAONDOA WATU MABONDENI pasipo kuwaza kuwa watu hawa ndio walipa kodi wake na ndio wanaomlipa mshahara wake!

Kwa maneno yale sasa tunaamini ya kuwa Sio kila mvua, mafuriko, ajali za moto, ajali za magari au kiangazi ni mambo ya asili bali mengi hutengenezwa na wanadamu(wachawi) na mashetani ili kuwaangamiza wengine.

Kabla ya kumaliza Ibada hiyo jana jioni majira ya saa moja na nusu, Askofu Gwajima ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu wa Jeshi la Bwana la Ufufuo na Uzima aliyaongoza majeshi yote kwenye maombi ya kusambaratisha mvua na mafuriko yote na hali kuwa ya kawaida.

Maarifa makubwa aliyonayo Askofu Gwajima juu ya mambo ya rohoni na mwilini umefanya watu kuzijua hila za wachawi na mashetani wenye nia ya kuangamiza watu na kuwafanya masikini kwa njia ya maji..

"Mvua imekoma kuanzia sasa na haitaharibu tena, na ninaiamuru ardhi imeze maji yote yaliyojaa juu ya nchi"... alisema Askofu Gwajima katika kumalizia ibada.

JE Thamani ya Yamoto Band ni Nyumba na Gari ?

$
0
0
Saidi fella ni mfanyabiashara Katika tasnia ya Muziki na mafanikio ya hii band kwa asilimia zote yeye ndio kayawezesha. Kwa hili nampa Hongera sana

Kilichonifanya niandike huu uzi ni Tukio ambalo limetokea jana ikiwa ni siku ya kuzaliwa ya kiongozi wa band hiyo Aslay, katika siku hiyo ndugu Fella alitoa zawadi ya gari dogo kwa kijana wake. Sambamba na hili Fella ameshatangazia uma kuwa Nyumba za hawa vijana watakabidhiwa mwezi wa saba na pengine Rais akawa mgeni rasmi. Nimpongeze tena Fella kwa hatua hii nzuri

Ninachojiuliza hapa na kilichopelekea kuandika huu uzi ni Je nini thamani ya mziki wa hawa vijana? Mimi sio mtaalam wa kutathimini mziki ila kitu kimoja ambacho nina uhakika ni kuwa hawa vijana wana kipaji kikubwa chenye thamani zaidi ya hili gari na hizo Nyumba watakazopewa. Najua utajiuliza iweje niseme hivi Wakati hizo Nyumba sijaziona, naongea haya kwa uzoefu wa Fella kwani amekuwa akiwanunulia Nyumba wasanii wake Temba na Chege,

Mara ya mwisho nilimuona Fella akimkabidhi Temba Nyumba aliyomnunulia nje ya mji. Kimsingi ile Nyumba ilikuwa ni ya kawaida sana na ni Nyumba ambayo ilikuwa chakavu kwa kiasi fulani. Thamani ya Temba na Chege Sidhani kama ni sawa na Nyumba ya namna ile. Kutokana na hilo ndio maana naamini hata hawa vijana wa Yamoto nao watapewa Nyumba za ubora wa kawaida ambayo si linganifu na thamani ya vipaji vyao.

Kwanini Fella uwanunulie Au kuwajengea Nyumba wasanii wako? Kwanini usiwape hela zao wafanye yao wewe ubaki kuwasimamia na kuwakumbusha umuhimu wa kufanya maendeleo. Wasanii wako sio Watoto kiasi kwamba washindwe kusimamia ujenzi Au ununuzi wa Nyumba zao. Kitendo hiki cha kuwajengea Au kuwanunulia Nyumba kinaficha Mengi juu ya gharama halisi za manunuzi.

Mbona dimond Nyumba yake hamjamjengea Au kumnunulia? Hili ni swali ambalo nawaachia Yamoto band,Chege na Temba. Ifike mahali msanii awe mwajiri wa manager na sio kinyume chake, ndio maana Diamond anafanikiwa sababu yeye kawaajiri Fela na Babu Tale japo mbele ya Jamii huwa anajishusha ili ionekane kama Hao wawili ni maboss zake

By xfactor

New Couple Alert? Alikiba & Jokate Mwegelo (Details)

$
0
0
Kuna tetesi zinavuna kuwa Jokate Mwegelo na Alikiba ni wapenzi!

Tetesi hizo zimekuwepo kwa muda sasa japo wawili hao bado hawajaweza kuthibitisha muungano wao.

Mtangazaji namba moja kwa udaku nchini, Soudy Brown wa Clouds FM alijaribu kumtafuta Jokate kutaka kutegua kitendawili hicho lakini kama ilivyotarajiwa, Jokate aliishia kuangua kicheko tu na kutotoa jibu.

Wafuatiliaji wa mambo wameenda mbali zaidi na kudai kuwa wawili hao wamekuwa wakionekana pamoja kwenye sehemu kadhaa ikiwemo nyumbani kwa Alikiba.

Wengine wamefuatilia baadhi ya picha zao mitandao ya kijamii na kugundua kuwa Jokate amewahi kuivaa kofia ya mkeka ya Alikiba!

Bongo5 binafsi haijaweza kuthibitisha uwepo wa uhusiano huo.

Shilole Posted Her Video On Instagram Talking Broken English..Seriously !

$
0
0
Shilole Posted Her Video On Instagram Talking Broken English .. See Video Below


MKE Alininyanyasa Sana Nilipofukuzwa Kazi, MUNGU Ameniona, Sasa Yamegeuka

$
0
0
Siku moja nisiyopenda kuikumbuka nilitwa ofisini kwa bosi wangu na kukabidhiwa barua ya kufukuzwa kazi
Hiyo ilikua ni baada ya uchunguzi wa miezi kdhaa wa kosa nililokua nimelifanya bahati mbaya. Miezi mitatu nyuma nilimuingizia pesa mteja kimakosa kwenye akaunti yake kiasi cha million mia tatu na hamsini ambazo alitakiwa kuwekewa Mteja mwingine halali kupata pesa hizo.

Kama humu ndani Kuna banker ataelewa nachokisema, kwamba makosa kama haya benki ni kawaida sana. Ukigundua kosa kama hili unawahi una reverse hiyo entry una m-credit anaetakiwa shida ni kama uliemwekea kimakosa akawahi kuzichukua ndipo yanakukuta yaliyonikuta mimi.

Baada ya kufukuzwa kazi mke wangu alibadilika kabisa
Nilishuhudia yafuatayo:-

(1) Alitamka mimi ni mjinga ndio maana nimefukuzwa kazi.

(2) Chake kikawa chake tu.

(3) Akawa anawaambia wazi watoto kuwa kitu fulani kimenunuliwa na yeye na sio mimi.

(4) Muda wa kurudi home ukabadilika sasa anarudi usiku mwingi, nampa kipigo cha nguvu anazira na kukimbilia kwao, kwenye usuluhishi anawaambia wasuluhishi kwamba mimi namuonea wivu kwa kuwa ana kazi mimi sina.

(5) Niliuza Gari zangu mbili ili nipate mtaji wa kufanya biashara hivyo nikawa sina Gari nilijua maadam wife ana Gari tutatumia wote maana hata yeye wakati hana Gari alikua akitumia magari yangu.

Kinyume na matarajio hakutaka kabisa niguse Gari lake mimi nikawa mtu wa miguu.Majirani wakawa wanashangaa mfumo wetu wa maisha.

(6) Life yetu ya bedroom ikawa imekufa no intimacy no love making nothing. Alianza kidogo kidogo leo mara aseme anaumwa, kesho kachoka, hadi mwezi unaisha. Nikaamua isiwe tabu nikaacha kuulizia tena, nae akawa amepotezea moja kwa moja.

Hata wazazi wangu aliwa mistreat sana wakawa hawaji tena kwangu, mama yangu akawa ananitumia vitu kwa njia basi kutoka nyumbani kama mchele, maharage, unga na kadhalika ili na mm nionekane nachangia.Wakuu siku ya kufa nyani miti yote huteleza. Kila nilichojaribu kukifanya ili nijinasue kinakwama, nakuta mtaji wote unakata naanza moja.Ilikatika miaka minne nikiwa kwenye hali hii maana nilipata matatizo 2010. Mwaka Jana kuna Dada mmoja tulisoma wote primary school akaamua kunisaidia, huyu dada tulikutana Posta accidentally tukapeana contact
mimi nilishamsahau ila yeye alinikumbuka.

Baadae akaniunganisha na mumewe ambae ni HR manager kwenye shirika fulani, nikamwelezea ukweli wote na akaniingiza kaziniWife sikumwambia kuwa nimepata kazi akaanza kuona nakuja na mahitaji ndani, nikawa naondoka zangu alfajiri narudi usiku mwingi. Nikaita mafundi wakabomoa ukuta wote wa fensi uliokua umeoza waliiba sana cement wakati wa ujenzi ukajengwa upya, vitu vyote vilivyochoka ndani nikabadilisha. Wife alishangaa sana ila akashindwa kuniuliza maana hadi hapo tulikua hatuongeleshani zaidi ya salam za asubuhi na jioni tu basi.

Wana jf siwezi kuwaficha sehemu niliyopata naingiza hela Mara kumi ya ile kazi yangu ya benki, hii sikutokana na mshahara bali njia mbali mbali katikati ya mwezi kitengo chetu tupo wanne,hali ikiwa nzuri huwa tunagawana hadi laki mbili kila siku, kama hali ni mbaya tunagawana laki moja kwa siku hii ni mbali na ile tunayogawana mwisho wa mwezi kama million 3 each person mshahara ni mdogo tu ni laki saba tu kwa mwezi.Maana mshikaji alisema anaweza kuniingiza kazini ila kama mfanyakazi wa kawaida kwa kuwa benki nilifukuzwa hakukua na reference wala background check so nikaamua kufuta kwenye CV kuwa nilifanya bank.

Nimeanza mchakato wa talaka kupitia mwanasheria mmoja rafiki yangu, mwezi January mwaka huu amemwandikia barua ya kumtaarifu uamuzi huo na copy Ustawi wa jamii pia, baadae tutafungua shauri la talaka.Kinyume na matarajio yangu wife kwa kuwa alishañichoka na hakuna kinachoendelea kati yetu nilijua angekubali tu. Cha ajabu hivi sasa kupitia wazee wake wameniita kikao zaidi ya Mara 6 sasa ili tusuluhishe tofauti zetuKawa mpole sana, alidhan nitaendelea kuteseka milele

Wakuu sasa sipo nyumbani kwa hasira ya mambo aliyonitendea hivi sasa sipo nyumbani nimepanga upande wa nyumba nimeanza ujenzi ili nihamie. Kila siku lazima nipite kwa watoto niwaone ndo niondoke. Nimesimama njia panda, mm binafsi nilishaamua simtaki tena huyu mwanamke ila wazee na viongozi wa dini tunakoabudu wanasema turudiane juzi mke wangu alinipigia magoti tukiwa kikaoni kwamba nimsamehe, nifute kusudio la kuomba talaka mahakamani. Wazazi wangu hawataki kusikia kabisa neno msamahakwa matendo aliyotufanyia.


NB: Nimetaja kipato ili kuwapa mwanga na uelewa wa tatizo isichukuliwe vinginevyo

Nimesikia amepata matatizo kazini ila sina uhakika na taarifa hizo

Naomba ushauri wenu

By Christo devries/Jamii Forums

Wema Sepetu: Ray, Steve Nyerere Wanafiki Wakubwa

$
0
0
Staa wa Bongo Movies, Wema Sepetu ‘Madam’ juzikati alijikuta akivunja ukimya kwa kusema kwamba, wasanii wenzake Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na Vincent Kigosi ‘Ray’ ni wanafiki wakubwa baada ya kumtosa kwenye Pati ya Instagram iliyofanyika hivi karibuni jijini Mwanza.

Akizungumza na paparazi wa GPL, Wema alisema alikubaliana na mastaa hao kutoenda kwenye Shoo ya Zari All White Party iliyofanyika Mlimani City jijini Dar badala yake waongozane naye jijini Mwanza lakini wakamgeuka.

“Sitaki kabisa nisikie mtu ananiambia habari ya Steve Nyerere au Ray maana ni wanafiki wakubwa, hawawezi kuniahidi kutokwenda pati ya Zari lakini wakaenda na wasije Mwanza kama walivyoniahidi,” alisema Wema.Paparazi wetu baada ya kupata malalamiko ya Wema, alimsaka Steve ili aweze kuzungumzia unafiki wao, akafunguka:

“Kweli mimi na Ray tuliahidi kuungana na Wema kwenye shoo yake ya Mwanza ila siku ya mwisho tulikwama baada ya kupungukiwa fedha ya nauli, hivyo tukashindwa kabisa na tusingeweza sisi kwenda huko kwa kumtegemea yeye atulipie kila kitu.Tukaona twende kwa Diamond ambaye naye alitualika.”

Ray hakuweza kupatikana mara moja kuzungumzia tuhuma hizo.

Globalpublishers

Mchumba wa Shilole Nuhu Mziwanda Atoa Kali Nyingine ya Mwaka...Hii Sasa Kutafuta Kick

$
0
0
Imenibidi kushare nanyi labda mtaelewa post ilivyoandikwa sijui ni kiingereza au kifilipino
tueleweshane wapendwa

Nuhu Ameandika Hivi kwenye caption ya hiyo picha hapo Juu : She is my angel to me and inside my heart is draw she is name by natural ink from the God , love of me mziwanda to she is so not aproched with others girls 

Baada ya Wema Kupromote Watu Wampigie Kura Ali Kiba Kill Awards, Diamond Aibuka na Kuziponda Vibaya Tuzo Hizo ya Kill Awards

$
0
0
Ki ukweli nahisi hawa wawili bado wanawindana japo wameachana , ni kama wanafuatiliziana nyendo zao na kujaribu kuumizana kwa njia moja ama nyingine huku wakijaribu kuonyesha kila mmoja ame move on ...

Embu ona hiii : Wema Sasa amekuja na nguvu zote ana mtangaza Ali Kiba Kwenye Instagram yake na Kuomba watu wampigie kura kushinda Kill Music Awards wakati akijua kabisa Ali Kiba na  Diamond haziivi ...

Baada ya Muda Diamond Anaibuka na Kuziponda Vibaya Tuzo za Kill Awards Kama Univyosomeka Hapa Chini:

Mwigizaji Lulu Michael Amganda Van Vicker!

$
0
0
Staa mrembo wa Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ anadaiwa kumganda mwigizaji kutoka nchini Ghana, Van Vicker gazeti la leo la Risasi limeripoti.

Habari kutoka chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa Lulu kilidai kwamba, mwanadada huyo amekuwa na mawasiliano ya karibu na Van Vicker tangu walipokutana Septemba, 2013 kwenye Jengo la Akade, Posta jijini Dar ambapo jamaa huyo alitua nchini kurekodi filamu na mastaa wa Bongo.

“Kwa taarifa yenu Lulu sasa hivi mambo yake na Van Vicker ni bambam na wanawasiliana usiku na mchana, nadhani kuna kitu kikubwa kinakuja. Yaani Lulu amemganda jamaa japokuwa sijajua kamili kama wana project gani.
“Kama mtakumbuka kipindi kile Van Vicker alikuja Bongo kucheza filamu ya Hashim Kambi (mwigizaji wa Bongo) ndiyo walifahamiana.

“Inawezekana anataka kufanya naye kazi kama Wema (Sepetu) ambaye hivi karibuni alikwenda Ghana na picha zikasambaa wakifanya yao,” alisema mtu huyo kwa sharti la kutochorwa jina gazetini.

Baada ya kumwagiwa ‘ubuyu’ huo, gazeti hilo lilizungumza na Lulu juu ya ishu hiyo ambapo alikiri kuwa ni mtu wake wa karibu na kwamba ni kweli amekuwa akiwasiliana naye.“Van Vicker ni mtu wangu, nimekuwa nikiwasiliana naye, kusalimiana na kuulizana maendeleo ya kazi zetu za sanaa,” alisema Lulu.
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>