Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live

Mashabiki wahisi Ivan bado yupo moyoni mwa Zari baada ya mama kijacho huyo kupost ujumbe huu

$
0
0
Zari the Bosslady anatarajiwa kuwa mama wa mtoto wa Diamond Platnumz miezi michache ijayo lakini bado anahisi mume wake wa zamani, Ivan ni baba mzuri na anajivunia kwa vile anavyowalea watoto wao watatu waliowapata.

Mrembo huyo wa Uganda alipost picha ya Chris Brown akiwa na mwanae Royalty kwenye tuzo za Billboard wiki iliyopita pamoja na picha ya Ivan akiwa na watoto wao watatu na kuandika: Tag all men who are proud dads.”

Pamoja na mashabiki wengi kumsifia kwa ukomavu wake hasa katika namna anavyomzungumzia ex wake, wapo waliohisi kuwa amekosea kuandika hivyo na kwamba huenda bado anampenda.

“Hahahahahaha….zari yo mazing of all dads u include yo Ex,” aliandika Mackenzie Safari Shamirah aliyejibiwa na Zari, “and since when did our differences strip him of his fatherhood?”

Rakeem Jonez aliandika: This ain’t cool at all…if u want dat old thing back..then leave our diamond alone..it won’t surprise us coz u’ve always been dat hoe..he can be with anywoman that he wants to be with..he’s only with u bcoz of dat baby and he’s not acting crayz bcoz of u..it’s bcoz of that unborn baby..only her.”

Huss Deezy aliandika: Zari, you would lie to every body that you are happy with diamond but the fact remains that the kids u have with Ivan are ur soul and source of joy until u die. U could run from them but u won’t hide the fact is Ivan is the true man for you and u will sit one day and say I told u the truth. The happiness you think u are in ryt now with diamond is your few years to come painful tears of pain. I will be there to remind you dear.”

Zari alijibu: Run from them???? Hahahhold on I ran from my kids? Really since when? last I checked I woke up with them today b4 school I wake up with em every other day when when am SA…..did I miss something or does someone live in my house to know me more than I do myself….. people move on am not the 1st one. And as for my kids they are always priority to me and they live with me.”

Naye Moses Mulwana alichombeza: it’s so hurting to see ur wife going out with someone else but all my thanks goes to Ivan, for sure u are indeed a great man who have handled things in a professional way.

Zarinah Tlale alimjibu Moses: It hurts even more seeing men treat women like shit and expect them to sit around coz they have kids like their world ended. Gone r days hun, gon are the days.”

Bongo5

Adam Juma 'Hanscana na Nisher ' Watakuua Kwa Pressure'

$
0
0
Juzi kupitia ukurasa wake wa Instagram Director Mkongwe Adam Juma aliweka post ambayo ni wazi alionyesha kukerwa na mambo mbalimbali ambayo yanaendelea katika tasnia ya filamu na muziki kiujumla, ambapo kwa tafsiri
ya haraka haraka Adam anaonyesha wazi kuwa kuna watu ambao wapo muda mfupi katika tasnia hiyo na kujiona kama wamemaliza kila jambo wakati yeye ni mkongwe ila anazidi kuijifunza kila siku, jambo ambalo anaamini litamfanya aendelee kuwepo siku zote ukilinganisha na watu ambao wameridhika na mafanikio ya muda mfupi na kujisahau na kudai kuwa kamwe hawatatoka.

"Watanzania wabishi sana, miaka mitatu tu mtu anaanza kujifanya anajua kumpita mungu,,, kwa style hii hakuna atakae toka i swear to god!!!! Mimi kila siku najifunza ili siku moja nifanye kazi ninayoipenda kwa umakini sio kutengeneza video tu!!!! Wengine wanaona kushika kamera na kushot ndio mwisho, tunafanya kazi na watu wengine njee tunajifunza sana vitu mkiona nimenyamaza mnaona kama mimi fala vile, ngoja sasa.

Baada ya kutoa kauli ambayo kwa mashabiki wameipokea kama Adam amepaniki kutokana na ukali wa maneno ambayo alitumia kufikisha ujumbe huo, baada ya kuweka ujumbe wake huo katika Ukurasa wa Facebook wa East Africa Radio/ www.facebook.com/EARadio mashabiki walitoa maneno yao kwa Adam ikiwa pamoja na kumshauri kuwa yeye ni mtu mzima anaweza kufikisha ujumbe kwa namna nzuri pasipo kutoa makwazo kwa watu kutokana na heshima ambayo tayari kajijengea nyuma kwa kufanya kazi nzuri na kuleta changamoto na uboreshaji katika tasnia hiyo kwa miaka kadhaa huko nyuma.

Adorn Leonidas nadhani ni hasira tu, mtu akiwa na hasira anaweza kuongea chochote. Namshauri aturie tu atawatukana wangapi?
Lakini baadhi ya mashabiki wao wanaamini kuwa huenda maneno yaliyomtoka Adam Juma ni kwa sababu ya changamoto anayoipata kutoka kwa waongozaji wadogo katika tasnia hiyo ambao kwa sasa wanafanya vizuri, na kufunguka mambo mengi kutokana na ushindani wao wenyewe na hapa ndipo mashabiki hao walipoamini kuwa vijana hao wanampa sana Changamoto Adam na kuandika haya.

"Michael Dilunga Hanscana na Nisher watakupa presha broo fanya kazi, Ronaldinho alikuwa anaupiga mpira mwingi sana lakini sasa hivi kafunikwa na kina Messi. wanaokulewa watakuelewa tuu siku zote fanya kazi mkubwa achana na maneno kama hayo

"Riziki Rajab Hanscana anawaumiza kichwa kama Kiba vile huku upande wa pili"

"Ebbyno Chiboko ujuwe nini ..! Mtu anae karibiwa na kifo utamjuwa tu..uropokaropoka tu hovyo...
Kama kuna alie mzinguwa nae aende kimyakimya tu akamzinguwe..kutafuta mashahidi hiyo ni kesi."

"Prince Hans Maxwell Huyo muoga tuu hana lolote kama haogopi kwanini asimtaje, mbona 2Pac alimchana makavu Big, F..k Big, F..k Bad boys, F..CK Mob deep na akamalizia if u are down with bad boys F..ck u too.

Shafii Mahmoud usibishane na kuamua kuchimba biti, piga kazi bhana maneno ya nini Adam!

LISTEN: Tanzania's King of Bongo Flava Music, Diamond Platnumz, Sets His Sights on Conquering the World

$
0
0
LISTEN: Tanzania's King of Bongo Flava music, Diamond Platnumz, sets his sights on conquering the world 

Mose Iyobo: Aunt Ezekiel Amekwamisha safari ya London

$
0
0
Staa maarufu wa filamu Bongo Aunt Ezekiel akiwa na mpenzi wake Moses Iyobo.

Dansa wa mwanamuziki Naseeb Abdul ‘Diamond’ Mose Iyobo, ambaye pia ni mpenzi wa staa maarufu wa filamu nchini Tanzania,Aunt Ezekiel, amefunguka kuwa hajajumuika na dansa wenzake kwenda jijini London, Uingereza kutokana na hali ya mpenzi wake.

Mose, amesema kuwa alishindwa kujumuika na wenzake akihofia hali ya mpenzi wake na kudai kuwa anapenda kuwa na mrembo wake karibu hadi hatua za mwisho za kujifungua kwake.

Ameongeza kuwa anashindwa kwenda mbali sana kutokana na hali ya mpenzi wake kwa kuwa anakuwa na wasiwasi sana hivyo hata London, ameshindwa kwenda kwani anatamani kuona hatua kwa hatua ya mpenzi wake hadi kumpata mtoto wao.

Anti Lulu Awatishia Wake za Watu

$
0
0
Staa wa Bongo Movies na mtangazaji mwenye vituko vingi na kujiachia kwa sana amekuja na mpya nyingine ya kuwakanya wanaomtukana katika mitandao ya kijamii kila anapoweka picha zake.

 Anti Lulu amesema asilimia kubwa ya watu wanamtukana anapoweka picha zinazomuonesha maumbile yake  ni wanawake.

"Asilimia kubwa ya wanawake ndio wanaongoza kunitukana nikiweka picha zangu za Mungu alivyoniumba ..mapaja yangu,hips zangu ma**ko yangu...sasa sijui kwanini mwatukana nyie wanawake angalieni nisiwabebee mabwana au wanaume zenu kwa mlioolewa,mimi mmakonde na Mbondei..mtalia na kusaga meno" aliandika hivyo katika ukurasa wake wa facebook.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Tarehe 22 May 2014

$
0
0

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Tarehe 22 May 2014




















Habari  Zilizopo  Katika  Magazeti  ya  Leo  Ijumaa  ya  Tarehe  22  May 2014

Mwigulu awaomba radhi wanafunzi elimu ya juu

$
0
0
SIKU moja baada ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kile cha St Joseph vyote vya   Dar es Salaam kuanza mgomo kutokana na kukosa fedha za kujikimu, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amewaomba radhi.

 Nchemba aliomba radhi bungeni jana baada ya Mbunge wa Viti Maalum, Ester Bulaya (CCM) kuomba muongozo, akihoji sababu za Serikali kushindwa kupeleka fedha hizo vyuoni.

 “Mheshimiwa Spika, naomba nipewe mwongozo ni kwa sababu gani serikali imeshindwa kupeleka fedha huku ikijua wazi kwamba wanafunzi hao ni watoto wa masikini,

Katika taarifa yake, Nchemba alisema kutokana na kuchelewa huko aliwaomba radhi wanafunzi ambao wanasoma kwa kutegemea mkopo wa serikali huku akizitaka mamlaka husika kuhakikisha fedha hizo zinawafikia wanafunzi mara moja. Alisema  Hazina imekwisha kuidhinisha fedha hizo.

 “Juzi hazina ilikamilisha miamala ya fedha ambazo zinahitajika katika vyuo hivyo na mamlaka zinazohusika zilipaswa kufikisha fedha hizo jana kwa wahusika (wanafunzi),” alisema Nchemba na kuongeza:

 “Ni muda mrefu migomo haijatokea kutokana na ukweli kuwa mtiririko wa utoaji wa fedha haukuwa na matatizo. 

 “Hakuna hata wa kulikuza suala hili kwa sababu msingi wake ulikuwa ni wa halali lakini kwa sasa limepatiwa ufumbuzi,” alisisitiza.

 Kuchelewa kutolewa fedha hizo za mkopo kumesababisha wanafunzi wa vyuo hivyo kugoma kuanzia juzi  hadi watakapopewa fedha hizo za kujikimu.

Bulaya katika taarifa yake alisema wanafunzi zaidi 7,000 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) juzi waligoma kuingia darasani kwa sababu ya kukosa fedha za kujikimu huku wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo cha Mtakatifu Joseph kilicho Mbezi, Dar es Saam wakisimamishwa masomo.
Mwisho

Actress Aunty Ezekiel Gives Birth To a Baby Girl

$
0
0
Actress Aunty Ezekiel and boyfriend Moze Iyobo have been blessed with a baby girl. Aunty gave birth this night and one of celebs who took to social media to congratulate her include Diamond Platnumz and Zamaradi Mketema.



Soma Dhana Nzima ya kubemenda mtoto, mitazamo, ufafanuzi na ushauri

$
0
0
Kuna hili suala linaloitwa 'kubemenda' mtoto, watu wanadai kuwa sperms huwa zinaleta madhara kwenye maziwa ya mama na kumdhoofisha mtoto kiafya na wengine wanasema ukimshika mtoto baada ya sex pia ina madhara. kiukweli suala la Kubemenda ni imani potofu (myth) na hakuna uhusiano wa sperms na maziwa ya mama katika kudhoofisha afya ya mtoto; iwe kwa kushirikiana tendo la ndoa au kumshika mtoto baada ya sex.

Je, nini maana ya kubemenda mtoto? 

Kwanza hii imani potofu inaeleza kwamba kubemenda mtoto ni pale wanandoa wanapojihusisha na tendo la ndoa baada ya mtoto Kuzaliwa (pale mke anapokuwa tayari kiafya kwa tendo la ndoa baada ya kujifungua) kwa maana kwamba sperms huharibu maziwa ambayo mtoto ananyonya, si kweli hakuna uhusiano wowote kati ya maziwa ya mama na sperms katika kuathiri afya ya mtoto.
Pili kubemenda mtoto ni kitendo cha wanandoa kujihusisha na tendo la ndoa na mke kushika mimba miezi mwili tu au mitatu tu baada ya kujifungua na kupelekea kuzaa mtoto mwingine baada ya mwaka na matokeo yake mtoto aliyetangulia Kuzaliwa huwa dhaifu kiafya (huchelewa kutembea) na huitwa ni mtoto ambaye amebemendwa, kitu ambacho ni imani potofu kwani kuna wanandoa wengi tu wamezaa watoto waliopishana mwaka na wote wana afya njema kabisa.

Tatu kubemenda ni kitendo cha mwanandoa mmoja kutoka nje ya ndoa (sex) na akirudi ndani huendelea na tendo la ndoa na matokeo yake mtoto wa ndani ya ndoa huwa dhaifu, pia ni imani potofu hakuna kitu kama hicho. Jambo la msingi ni kufuata ushauri wa kitaalamu ambao ni wiki sita baada ya kujifungua. Je, kuna ukweli wowote kuhusiana na hii imani potofu Iwe wanandoa kujihusisha na tendo la ndoa baada ya mtoto Kuzaliwa au kuzaa mwingine baada ya mwaka au hata kutoka nje hakuna uhusiano na mtoto aliyezaliwa kama suala la usafi na lishe bora litazingatiwa kwa mtoto anayehusika.

Je, kulikoni mababu zetu wakaweka imani kama hiyo kwa wanandoa? 

Kama zilivyo imani zingine potofu kama vile mwanamke mjamzito kutokula mayai mababu zetu walikuwa na somo ndani yake, inawezekana walitaka kuhakikisha wanandoa wanashiriki vizuri katika kulea mtoto kwa pamoja bila kupendekeza tabia za uchafu na kujirusha nje na ndani ya ndoa bila utaratibu. Pia labda mababu zetu walihofia kitendo cha mwanamke kutoa maziwa (chuluzika) wakati wa tendo la ndoa hasa anapofika kileleni (tangu akifungue hadi miezi 8 hivi) na wakawa wanahofia kinaweza kuathiri kiwango cha chakula cha mtoto hivyo ili kuzuia ni kutunga imani (potofu) kwamba mtoto ataathirika kwa mke na mume kushiriki tendo la ndoa.

Je, ili mtoto asionekane amebemendwa wanandoa wanahitaji kufanya kitu gani? 

Ni vizuri kufahamu kwamba hakuna uhusiano wa sperms kuharibu maziwa ya mama wakati wa kumnyonyesha mtoto hivyo wanandoa kushiriki tendo la ndoa halina uhusiano wowote na mtoto kuwa na afya mbaya kiasi cha kuchelewa kutembea. Mtoto anahitaji watoto chakula bora chenye viini-lishe vyote vinavyohitajika ili kukua vizuri pia mama anahitaji kujiweka mazingira safi (kuwa msafi) wakati ananyonyesha, ahakikishe anasafisha chuchu zake na mikono yake au kuzingatia usafi kimwili kabla ya kumnyonyesha mtoto iwe baada ya sex au muda wowote.

Je, kulikoni mababu zetu wakaweka imani kama hiyo kwa wanandoa?

Kama zilivyo imani zingine potofu kama vile mwanamke mjamzito kutokula mayai mababu zetu walikuwa na somo ndani yake, inawezekana walitaka kuhakikisha wanandoa wanashiriki vizuri katika kulea mtoto kwa pamoja bila kupendekeza tabia za uchafu na kujirusha nje na ndani ya ndoa bila utaratibu. Pia labda mababu zetu walihofia kitendo cha mwanamke kutoa maziwa (chuluzika) wakati wa tendo la ndoa hasa anapofika kileleni (tangu akifungue hadi miezi 8 hivi) na wakawa wanahofia kinaweza kuathiri kiwango cha chakula cha mtoto hivyo ili kuzuia ni kutunga imani (potofu) kwamba mtoto ataathirika kwa mke na mume kushiriki tendo la ndoa.

Je, ili mtoto asionekane amebemendwa wanandoa wanahitaji kufanya kitu gani? 

Ni vizuri kufahamu kwamba hakuna uhusiano wa sperms kuharibu maziwa ya mama wakati wa kumnyonyesha mtoto hivyo wanandoa kushiriki tendo la ndoa halina uhusiano wowote na mtoto kuwa na afya mbaya kiasi cha kuchelewa kutembea. Mtoto anahitaji watoto chakula bora chenye viini-lishe vyote vinavyohitajika ili kukua vizuri pia mama anahitaji kujiweka mazingira safi (kuwa msafi) wakati ananyonyesha, ahakikishe anasafisha chuchu zake na mikono yake au kuzingatia usafi kimwili kabla ya kumnyonyesha mtoto iwe baada ya sex au muda wowote. Huwezi kusikia takataka za neno kubemenda katika nchi zilizoendelea kama Canada, Sweden, Australia, Ujerumani nk why? Ni traditions (Myth).

Chanzo: sayi manyanda

Wanafunzi wa Kitanzania Wafukuzwa Kenya

$
0
0
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, mamia ya wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma katika shule za msingi nchini Kenya, wameripotiwa kufukuzwa nchini humo.

Tayari 50 kati yao, wamerejeshwa nchini huku wengine kadhaa wakiwa bado wamekwama katika eneo la Narok Magharibi. Baadhi ya walioathirika ni wale ambao wako katika hatua za mwisho za kuhitimisha elimu yao ya msingi katika darasa la nane.

Vijana hao wanatarajiwa kufanya mitihani yao ya kumaliza shule Oktoba mwaka huu ; na kufukuzwa kwao kunawaweka katika wakati mgumu zaidi kimasomo.

Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Hashim Mgandilwa alikiri kuwepo na tatizo hilo na alilieleza gazeti hili jana kuwa: “Ni kweli wanafunzi wetu waliokuwa wanasoma Kenya wamefukuzwa nchini humo na 44 kati yao wamesharudi nchini, ila tuna wasiwasi kwamba mamia wengine watakuwa bado wamekwama huko na tuko mbioni kuwafuatilia zaidi.”

Meneja wa Baraza la Wafugaji katika Tarafa ya Ngorongoro, Peter Metele naye alikiri kuwepo kwa tatizo hilo na kuongeza kuwa yeye ndiye
anayefanya kazi ya kwenda kuwachukua wanafunzi waliotimuliwa Kenya.

Imeelezwa kuwa chanzo cha kutimuliwa kwa watoto hao ni msuguano, ulioibuka baada ya kufanyika kwa operesheni maalumu ya kuwaondoa wahamiaji haramu kutoka nchi jirani ya Kenya, wanaodaiwa kuvamia maeneo ya Loliondo na Sale.

Hadi sasa watoto 27 wamehifadhiwa kwenye nyumba ya kulala wageni ya Cobra katika eneo la Wasso, Loliondo. Wengine takribani 10 wamepelekwa kwenye kata ya Arash na waliobakia wako majumbani mwao.

“Tumewahifadhi kwenye nyumba za kulala wageni kwa sababu kuna wale wanaotoka vijiji vya mbali sana na tunataka tujitahidi kufanya mazungumzo na viongozi wa upande wa Kenya ili waruhusiwe kurejea mashuleni, iwapo tutafanikiwa basi iwe rahisi kuwarudisha Kenya,” alisema Mwenyekiti wa Baraza la Wafugaji wa Ngorongoro, Metili.

Imedaiwa kuwa wanafunzi waliofanikiwa kurejeshwa ni wale wanaodhaminiwa na Baraza la Wafugaji na wale waliopelekwa na taasisi mbalimbali, ambao ilikuwa rahisi kutumiwa usafiri, ila kwa waliopelekwa na wazazi wao, bado wamekwama Kenya.

“Tulishafanya mazungumzo ya awali na viongozi wa upande wa Kenya siku ya tarehe 12 Mei mwaka huu, lakini ingawa tulikubaliana mengi, ikiwemo wafanyabiashara wetu kuruhusiwa kupeleka bidhaa Kenya inaonekana kuwa wananchi wa Narok wao wana maamuzi yao tofauti na serikali yao hivyo wanasisitiza kuendeleza mzozo, na sasa wameamua kuongeza tatizo kwa kuwatimua watoto,” alisema Mkuu huyo wa Wilaya.

Kwa upande wake, Katibu wa Baraza la Wafugaji, Ngorongoro, James ole Moringe alisema baraza hilo pia linafanya jitihada za kukutana na viongozi wa Narok na walimu wa huko ili kupata mwafaka wa suala hilo.

Akisimulia, mmoja wa wanafunzi hao, Lilian Peter (14) anayesoma darasa la Nane katika

Shule ya Ilkerin-Loita, alisema Chifu wa eneo hilo alifika shuleni kwao na kuwaita walimu ofisini, kisha baadaye Mwalimu Mkuu, Abel Githinji alianza kuingia madarasani na kuwatoa wanafunzi wote wa Kitanzania huku akiwaagiza wafungashe virago.

Wengi wa wanafunzi hao ni wale wanaotoka kwenye tarafa mbalimbali za wilaya ya Ngorongoro, ambayo imepakana moja kwa moja na Kaunti au Jimbo la Narok, Kenya.

Mwanafunzi mwingine, Naini Petey ambaye anasema wenzao wanaosoma shule nyingine ya Naikara, pia walifukuzwa na wengi wao bado wamekwama nchini Kenya, wakisubiri wazazi au wafadhili waende kuwachukua.

Juhudi za gazeti hili kuwapata mawaziri wenye dhamana ya mahusiano ya kimataifa, Bernard Membe wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Dk Harrison Mwakyembe wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, hawakupatikana katika ofisi zao, kwa njia za simu na hata bungeni Dodoma kuweza kuzungumzia suala hilo.

Chanzo: Habari Leo

Did Wema Sepetu Disclose The Woman Who Might Cause Zari And Diamond’s Break Up?

$
0
0
This Is Diamond Platnumz Rumored Girlfriend Who Lives In London !

Wema and her following are seriously looking for a way to piss off Diamond and his wife. It’s evident that sooner than later this parties will clash badly.

The war already began amongst their fans, so the clock is ticking before the celebrities blow up at each other faces. The reason am assuming this is because there are some photos being circulated by Wema Sepetu’s fan page.

This photos apparently belong to the woman behind Wema and Diamond’s split. The fan page has been tagging Zari on the other womans photos with the caption “Muke mdogo”.



As petty as it sounds this seems to have gotten to Zari who replied with a strong quote directed to her haters.

As for now I am not sure who runs the Wema fan pages but question is, how would these pages have personal information about Wema and her ex if she is not involved with the whole scandal herself?

Al Shabaab Wavamia Tena Kenya, Watoa Onyo Kali Kwa Wananchi

$
0
0
Mamlaka nchini Kenya imesema kuwa walinda usalama wamekabiliana na washukiwa wa kundi la wapiganaji wa kiislamu la Al- Shaabab, katika wilaya ya Ijara katika kaunti ya Garissa Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.

Mapema, wapiganaji hao waliokisiwa kuwa zaidi ya 50 kutoka Somalia, wanasemekana kushambulia kambi za polisi katika eneo la Yumbis, takriban kilomita 30 kutoka Daadab.

Wavamizi wa Al-Shabaab waliteka vijiji vitatu na kupeperusha bendera yao Kaskazini Mashariki mwa Kenya kwa muda kabla ya maafisa wa polisi nchini kenya kuwasili na kuwatimua. Vijiji vilivyovamiwa ni Ramu iliyoko Mandera, na vijiji vya Yumbis na Holugho vilivyoko Garissa.

Walioshuhudia wamesema kuwa wapiganaji hao waliikejeli serikali ya Kenya na wakawaonya wanavijiji kwa kuendelea kushirikiana na serikali ya Kenya.

Japo viongozi nchini Kenya wamesema kuwa maafisa wa usalama wamewafukuza  wanavijiji wenyeji wa Yombis wanaodai kuwa bado wapiganaji hao wako

Tundu Lissu Aishambulia Serikali Bungeni....Asema Rais, Mawaziri Wamekithiri Kwa Ahadi Hewa

$
0
0
MSEMAJI wa Kambi Rasmi ya Upinzani na mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, ameichachafya serikali akidai imekithiri kwa ahadi hewa ambazo zimekuwa zikitolewa na Rais Jakaya Kikwete na mawaziri kuhusiana na Kura ya Maoni ya Katiba Pendekezwa.

Lissu alitoa kauli hiyo jana katika Mkutano wa 20 wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma wakati akiwasilisha mapendekezo ya kambi pinzani kuhusu makadirio ya matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria.

Lissu alisema Rais Kikwete wakati akikabidhiwa katiba pendekezwa aliwaahidi Watanzania kuwa katiba hiyo ingepigiwa kura ya maoni Aprili 30, mwaka huu lakini hadi sasa ahadi hiyo haijatekelezwa.

Alisema leo ni wiki ya 3 tangu Rais awaahidi Watanzania juu ya upigaji wa kura ya maoni lakini mpaka sasa haijulikani siku wala tarehe ya kura ya maoni kutokana na ubabaishaji uliopo ndani ya Serikali.

Lissu alisema ni dhahiri hakuna uhakika wowote kufanyika kura ya maoni juu ya katiba mpya kutokana na sheria iliyopo ya kura ya maoni ya mwaka 2015.

Alisema kwa sasa kuna uhakika wa Rais kuondoka madarakani bila ya katiba mpya aliyowaahidi Watanzania kupatikana katika kipindi cha takribani miaka mitano iliyopita.

Mbunge huyo machachari alisisitiza; "Ndani ya utawala wa Rais Kikwete unaonesha dhahiri kuwa ameshindwa kukamilisha mchakato huo pamoja na chama chake CCM.

"Hata kama tume ya uchaguzi itaweza kukamilisha jukumu lake la kuandikisha wapiga kura nchi nzima bado hakuna uhakika wa kufanyika kwa kura ya maoni kutokana na matakwa ya sheria ya kura ya maoni 2015."

Alisema Sheria hiyo iliweka utaratibu mgumu wa uendeshaji wa kura ya maoni ambapo kila hatua inayotakiwa kuchukuliwa haiwezekani kuahirishwa kwa kuongezewa muda.

Aakizungumzia haki za binadamu, Lissu alisema kwa kiasi kikubwa ukiukwaji wa haki za binadamu umeongezeka kwa Watanzania.

Alisema mauaji na mashambulizi dhidi ya viongozi wa kidini na waumini wao kufanyiwa ukatili sehemu zao za ibada hakuna mtu yeyote aliyeadhibiwa katika kesi hizo.

"Serikali haijatoa taarifa yoyote juu ya wahusika na wauaji wa mashambulio mbalimbali yaliyofanyika nchini, yakiwemo ya Daud Mwangosi pamoja na shambulio la Dkt.Ulimboka hadi sasa hayajajulikana hatma yake,"alisema Lissu.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Kigoma, Felix Mkosamali alisema ni aibu kwa nchi katika kura ya maoni kwani sheria yake bado haitekelezeki na haiwezekani kwa mazingira ya sasa yalivyo inashangaza waziri wa sheria kutangaza kuwepo kwa kura hiyo.

Mkosamali alisema hii ni aibu kwa nchi kuendeshwa bila ya kuwa na uhakika nayo wala kuwa na ratiba au sheria inayoeleweka kwani hata katiba hiyo ikilazimika kupigiwa kura inakuwa haina umuhimu kwa wananchi wake.

"Kwa hili serikali imeshafeli tangu mwanzo mchakato huu wa katiba ni mchakato ambao ukiutafakali unashangaza hasa kwa chama cha CCM kushauriana na vyama vingine kwani katiba za wenzetu ni nzuri na zenye mashiko kwa jamii yao,"alisema Mkosamali.

Akizungumzia Sheria iliyopo sasa nchini, Mkosamali alisema  Sheria zinazotekelezwa nchini ni asilimia 30 mambo mengi yanaendeshwa kiholela bila kufuata sheria.

Alisema hali ya watu kutumia sheria mikononi imeweza kuongezeka kutokana na jamii kutoamini serikali ambapo mara nyingi wanapowafikisha watuhumiwa polisi wanaachiwa.

Mkanda wa Ngono Wa Jini Kabula Wasambaa Mitandaoni

$
0
0
Staa aliyejizolea umaarufu mkubwa kupitia Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’, anadaiwa kurekodiwa mkanda wa ngono na kusambazwa katika mitandao ya kijamii.

Chanzo cha habari hii kimeeleza kwamba, tukio hilo lilitokea hivi karibuni baada ya mtu anayedaiwa kuwa ni mchumba wa staa huyo kumrekodi video hiyo na baadaye walipopishana kauli, akaamua kuisambaza kwa njia ya CD.

Mtandao huu umeshuhudia baadhi ya picha zinazodaiwa kuwa zilikatwa kutoka katika video hiyo ndipo mwanahabari wetu alipomtafuta  Jini Kabula ili kujua nini kilimsibu hadi akarekodiwa video hiyo.

Alisema kwa mazingira ya tukio hilo, anashindwa hata ajibu nini maana haelewi kilichotokea hadi mkanda huo ukasambaa kiasi hicho na kumsababishia matatizo kwa ndugu zake.

“Kiukweli nashindwa hata nikujibu nini maana kama aibu tayari imeshanikuta, hivyo sioni kama naweza kuongea kitu chochote kwa sasa kikanisafisha, kikubwa namwachia Mungu maana sina tena pa kuuficha uso wangu kwa hiki kilichotokea, yaani yamenikuta,” alisema Jini Kabula ambapo alipobanwa zaidi kuhusu aliyemrekodi, alijibu kuwa ni mchezaji wa timu ya Yanga pasipo kumtaja jina.

Mpekuzi Blog

Kidoa Ayasifia Makalio Yake, Ampa Makavu Agness Masogange

$
0
0
Video Queen anayekuja kwa kasi Bongo, Asha Salumu `Kidoa’ amempa makavu laivu muuza sura mwenziye Agnes Gerald ‘Masogange,’ akimponda kuwa kalio lake siyo orijino kwani wakati mwingine hulijaladia.

Kidoa amesema amekuwa akimshangaa mrembo  huyo kwa kujianika mtandaoni akionekana ana kalio kubwa kumbe siyo orijino.

“Masogange cha mtoto kwangu, ni kweli kalio analo lakini siyo kubwa kama linavyoonekana kwenye picha anazopiga. Nasikia huwa anajaladia kwa kuvaa taiti zenye masponji, sasa atashindana na mimi?” alihoji Kidoa.

Mama Avua Nguo Kumlaani "Serengeti Boy" Aliyegoma Kumlipa Baada Ya Kumpa Penzi

$
0
0
Mama mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja amefanya aibu ya mwaka baada ya kusaula (kuvua) nguo zake na kubaki mtupu, kisa kikidaiwa ni kumlaani ‘serengeti boy’ wake aliyemfanyia kitu mbaya.


Kwa mujibu wa chanzo chetu, mwanamke huyo mbali ya kuwa na mtu wake amedaiwa kuwa na tabia ya kuchepuka na wanaume tofauti ambapo amekuwa akifanya hivyo kwa kupanga chumba katika moja ya gesti  iliyopo Sinza kwa Remmy, jijini Dar.

Inadaiwa kuwa tukio hilo lililotokea hivi karibuni, mwanamke huyo kama kawaida yake alipata mteja ambaye ni mdogo kwake kiumri, ambaye pia ni mkazi wa eneo kulikotokea varangati hilo.
“Walikubaliana na huyo kijana kupumzika kwa muda na yule mwanamke katika chumba alichopanga, baada ya kumaliza mambo yao kijana aligoma kumpa hela ndipo mtiti ulipoanzia,” kilisema  chanzo hicho na  kuongeza;

 ”Tulishangaa kuona watu wakivutana huku mwanamke akiwa na kanga moja, ndipo kijana akapata upenyo na kuchoropoka na mwanamke yule akaanza kuvua nguo huku akisema anamlaani kutokana na umri wake kuwa mdogo na kumdhulumu chake.
“Watu walimsihi lakini akawa hasikii zaidi ya kuendelea kuvua na kuamua kumfuata yule kijana kwao huku akiendelea kuvua njia nzima, alipofika kwa yule kijana alianza kugonga geti kwa fujo huku akitoa maneno ikiwemo ya kumlaani.

“Pamoja na makelele na kusaula kote nguo zake lakini hakuambulia kitu zaidi ya kuonesha sehemu zake za siri na baadaye aliamua kuondoka."

GPL

Lowassa Na Wenzake Sasa Wako Huru....Adhabu Yao Imekwisha LEO......Taarifa Kamili Iko Hapa

$
0
0
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari wa Sekretarieti kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi mjini Dodoma leo tarehe 22 Mei 2015.

                       TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kamati Kuu imepokea na kutafakari taarifa ya Kamati ya Usalama na Maadili ambayo ilipitia adhabu waliyopewa wanachama sita waliokiuka kanuni za Maadili na kupewa Onyo Kali, adhabu iliyodumu kwa kipindi kisichopungua miezi 12.

Wanachama hao sita ni;-
i. January Makamba
ii. Willium Ngeleja
iii. Steven Wasira
iv. Bernard Membe
v. Edward Lowassa
vi. Fredrick Sumaye

Kamati Kuu imepokea na kukubali pendekezo la Kamati ya Usalama na Maadili ya kumalizaka kwa kipindi cha adhabu kwa wanachama hawa. Kwahiyo adhabu hiyo kwa sasa imemalizika, na wanachama hao wameruhusiwa kuendelea na shughuli zao katika Chama.

Hata hivyo Kamati Kuu inawataka wanachama hawa na wale wengine wenye nia ya kugombea Urais kupitia CCM Kuzisoma , Kuziheshimu na Kuzizingatia Kanuni za Maadili za CCM na kanuni zingine zinazoongoza mchakato ndani ya Chama, ili wasikumbwe na adhabu itokanayo na kuzivunja kanuni hizo.

Wale wote wanaotaka kugombea, yaani waliokuwa kwenye adhabu na wengine watakaojiingiza kwenye kampeni mapema na hivyo kukiuka maadili na miiko ya Chama, taarifa za kukiuka kwao zitatumiwa wakati wa kuchuja majina ya wagombea utakapofika.

Taarifa hizo zitatumika katika kuwapima na kuamua iwapo wana sifa za kutosha na wanafaa au hawafai katika kupata uteuzi wa nafasi wanayoiomba.

Imetolewa na;-
Nape Moses Nnauye
Katibu wa Itikadi na Uenezi
22/05/2015

Hii Ndo Siri ya Taarifa ya TV zote Kulazimishwa Kujiunga TBC Saa Mbili Jioni

$
0
0
Mwaka juzi kulikuwa na sintofahamu kuhusu nani achinje iliyosababisha kifo cha mchungaji moja kanda ya ziwa. Wakati sarakasi hiyo ikiwachanganya watanzania, katibu wa Bunge Thomas Kashillah aliibuka na kusema Bunge halitaoneshwa tena kwenye Runinga. Mjadala ukahama kutoka uchinjaji na kuwa Bunge kutooneshwa. Serikali ikafanikiwa, kombe likafunikwa na mwanaharamu akapita.

Mwaka 2013 mvua kubwa kuliko hii ya mwaka huu ilinyesha na kusababisha mamia ya watu kulala njiani na njaa wakiwa na watoto. Njia zote za kuingia Dsm zilifungwa na maji na matokeo yake watu wakawa na hasira na serikali kutosimamia miundo mbinu vizuri jambo lililosababishia wao kupata madhara yale. wakati hayo yakipamba kwenye vyombo vya habari ghafla tukaambiwa Makamu wa Rais, waziri magufuli na mkuu wa mkoa wa Dsm wameanguka na helikopta. kama kwaida Mjadala ukahama kwa walioanguka na helikopta. Mwanaharamu akapita tena. Ikumbukwe kuwa hakuna kati ya walioanguka na helikopta aliyenda hospitali wala picha ya helikopta iliyoanguka haikuonekana mpaka leo kama kaburi la Daudi Balali wa EPA iliyoibuliwa na Dr Dlaa.

Wakati wa Bunge la katiba, Tundu Lissu na UKAWA waliibua madudu mengi kuhusu muungano hasa pale walipohoji lilipo kaburi la waasisi wa muungano amabao ni Hanga na wenzake. Wakati mjadala huo ukishika kasi Dodoma, ghafla serikali ikaibuka na ugonjwa wa Dengue. Tukaambiwa wamekufa watu wawili mara watatu wakati malaria inaua zaidi ya watu watatu kila siku achilia mbali hao watatu hata kama ni zaidi ya watatu waliokufa mara moja na Dengue. Baada ya hoja ya Muungano kupita Dengue nayo ikayeyuka bila maelezo ya kutosha.

Je, watu wameshajiuliza kwanini magaidi feki wa amaboni walikuja wakati hoja ya ESCROW ikivuma? Tuliambiwa kuna askari wetu wamekufa. Je, akina nani kwa majina na walizikwa wapi na lini? Nani ameona picha hata moja ya askari wetu?

Mifano ya usanii huu wa serikali kuibua hoja ili kujilinda au kufunika udhaifu wake ni mingi sana.
Huko nyuma nilishaandika zaidi ya mifano kumi ya namna hii. Mifano hii michache inatosha kujenga hoja yangu. Kwa nini nimeyaeleza yote hayo??

Jana jioni nilimsikia kwenye ITV mwenyekiti wa MOAT ndugu Reginald Mengi akilalamikia serikali kutaka kupeleka mswada wa uhuru wa habari ambao moja ya kipengele chake kinavilazimisha vyombo vyote vya habari vikiwepo ITV, STAR TV, Chanel ten nk vijiunge na TBC saa mbili usiku kwa taarifa ya habari. kwamba vyombo vingine (TV zingine) havipaswi kuwa na taarifa yao ya habari wenyewe badala yake sheria itawalazimisha wajiunge na TBC. Je, hili linawezekana??

Mimi kama MIKAEL AWEDA sidanganyiki na hili. Nina wasi wasi nalo. Siamini kabisa nikirejea mifano tajwa hapo juu. Kwa maoni yangu taarifa hii imeletwa ili kubadilisha au kusahaulisha au kufunika mjadala wa ufisadi wa zaidi ya trilioni moja ulioibuliwa na Chadema baada ya kuchambua ripoti ya CAG. Kwa hiyo, taarifa hii imeletwa makusudi wakati bunge na vyombo vya habari vikijadili ufisadi huu wa serikali. Nijuavyo, Bungeni wakishamaliza taarifa hii ya TV zote kujiunga na TBC saa mbili jioni nayo itayeyeka kama taarifa ya Dengue, hoja ya kashilillah ya Bunge kutooneshwa na TV au helikopta kuanguka bila majeruhi wala picha yake kuonekana.

Nihitimiasha kwa kusema kuwa ninahitaji muda zaidi kuamini hili vinginevyo mwana wa Aweda hadanganywi na janja ya kufunika wizi wa matrilioni yaliyoibwa na viongozi wa serikali kwa kuibua hoja mbadala.

Nawasilisha
Mikael Aweda
0784 583 330
22/05/2015

Ushauri: Jinsi ya Kununua Gari iliotumika Ndani ya Tanzania

$
0
0
Baada ya kusikia watu wengi 'wakiumizwa' na 'kupigwa' wakiwa kwenye harakati za kutafuta usafiri uliotumika nchini, nimeona sio mbaya nikitoa ushauri ni jinsi gani unaweza kuepuka majanga kwenye zoezi hilo.

Naandika kama mnunuzi au muuzaji wa aina hio ya magari, kwahio siegemei upande wowote na ninachokiandika hapa sio sheria naweza kuwa sahihi au nisiwe sahihi ila ni imani yangu lipo litakalosaidia baadhi ya watu.

Njia muhimu za kufuata ili kupata gari unalotaka ni kama ifuatavyo:

1.Fanya utafiti mdogo juu ya gari unayoitaka: Uliza ujue gari unayoitaka inauzwa kiasi gani[makadirio]. Ukiweza kujua bei ya showroom au ukiagiza mwenyewe Japan halafu linganisha na bei utakayopewa hapa. Hili ni muhimu kwa sababu nimeshuhudia watu wananunua magari yaliyotumika Tanzania kwa bei ambayo ukiagiza mwenyewe unalipata kutoka japan au ukiongeza kidogo tu unapata la showroom.

2.Usiwe na haraka: Usiwe na haraka kabisa kwenye kutafuta gari. Utaletewa kila aina ya gari na usipokuwa makini utanunua gari bovu. Angalia taratibu angalau magari matano tofauti kwenye chaguo lako ndipo uamue, madalali watakusumbua ili mradi tu wapate cha juu.

3.Epuka madalali: Kama unaweza epuka madalali. Tafuta gari kwa kuuliza watu ulio karibu nao, ndugu jamaa na marafiki au unaofanya nao kazi au biashara. Hii ni nzuri chochote kikitokea una pa kuanzia. Madalali wengi hawajali maslahi yako wala ya muuzaji cha muhimu kwao ni cha juu tu. Gari ya 4m dalali atakuuzia 5-6m.

4.Tafuta Fundi: Ukilipenda gari lolote tafuta fundi akusaidie kulikagua,hata kama una idea na magari kuna vitu hutaviona ila fundi atakusaidia. Kuwa makini kuna mafundi huwa wanabonyezwa wakufiche hitilafu halafu baadae wanarudi kupewa chao ukishauziwa kanyaboya.

5.Epuka gari iliopigwa rangi: Epuka gari iliopigwa rangi siku chache kabla ya kuwekwa sokoni, wazoefu wanajua gari za aina hio ndio umuhimu wa fundi unapokuja. Gari inaweza kuwa imegongwa hivyo imenyooshwa na wanakuzuga kwa rangi inayong'aa. Siku hizi rangi hata 200,000 unapiga gari nzima ila ukinunua hilo baada ya mwezi rangi inababuka yote.

6.Epuka gari iliooshwa engine:Ukikagua gari ukiona imeoshwa engine ogopa sana. Mara nyingi gari zinaoshwa engine kuficha 'leakage',yaani oil na vitu vingine vinavyovuja kutoka sehemu mbalimbali za engine.

7.Jaribu gari wewe mwenyewe: Ni muhimu kuendesha na kuijaribu gari wewe mwenyewe hata ukienda na fundi. Ipitishe njia mbovu usikie jinsi ilivyo chini,chochote kinachogonga kuwa makini,usisikilize ukiambiwa ni tatizo dogo, kwanini hakurekebisha. Ingawa yapo matatizo madogomadogo ila kuwa makini.

8.Usiangalie Namba: Usibabaishwe na namba, eti hii C,D etc. Kuna gari namba A ziko vizuri kuliko namba C. Muhimu ni hali ya gari husika kwa muda huo.

9.Nenda TRA kujiridhisha: Ni muhimu kujua ukweli na status ya gari na mwenye gari. Jiridhishe anaekuuzia ndio mwenye gari. Akuonyeshe nyaraka zote halisi hata za kodi aliolipia.

10.Mwisho kabisa ukilipenda gari fanyeni makabidhiano kwa kuandikishana kwa mwanasheria. Ukiweza lipia benki na ubaki na risiti kama ushahidi wa malipo kupitia akaunti yake. Epuka kubeba cash kumpelekea muuzaji mahali alipo.

Haya machache naamini yanaweza kuwa msaada kwa watu wanaonunua magari yaliyotumika nchini,wengine mnaweza kuongezea mawili matatu na kurekebisha nilipokosea.

BATULI: Kanumba Kama Kaacha Laana Kwenye Filamu Za Bongo

$
0
0
APRILI 7 mwaka 2012 tasnia ya filamu ilipatwa na majonzi makubwa kutokana na kifo cha aliyekuwa mwigizaji nguli, Steven Kanumba, ambaye alikuwa kipenzi cha wengi ndani na nje ya nchi.
Licha ya wengi kutokuamini kwa muda huo, baada ya muda ikagundulika kweli amefariki, hivyo majonzi zaidi yakarindima, huku kila mtu akisema lake kuhusu kifo hicho.
Baada ya mazishi yake mashabiki walijipa matumaini kwamba tasnia hiyo licha ya kumpoteza mwigizaji huyo ingeendelea vema kutokana na kuwa na idadi kubwa ya waigizaji wenye sifa kama za Kanumba, lakini hadi leo mwaka wa tatu tasnia hiyo inaonekana kupoteza mvuto.
Mwigizaji, Yobnesh Yussuf ‘Batuli’, alipotembelea Kampuni ya New Habari (2006) Ltd , aliongeza chachu ya kutaka kujua zaidi anamkumbukaje Kanumba ambaye waliwahi kufanya kazi kwa ukaribu.
“Wasanii wengi hatujui tatizo ni nini, ndiyo maana naweza kusema kama ameacha laana kwa kuwa tumekutana mara kwa mara kuzungumzia jambo hilo, lakini kama tumeshindwa tumejitahidi na hakuna aliyeweza kufikia mvuto na uwezo wake kwa mashabiki, ndiyo maana tunaonekana kama tunapoteza mwelekeo na kifo chake ni kama kimeacha laana kwa filamu za Tanzania,’’ anaeleza Batuli.
Batuli, mwenye watoto wawili ambaye amezaa mapema kwa hofu ya uzuri wake kuisha kabla ya kupata motto, anasema wakati mwingine wanajikuta wakisema kwamba kwa sasa wanasubiri muujiza ya Mungu ndiyo kutokee mapinduzi mapya katika filamu za bongo, maana kwa sasa hali imeyumba.

Tatizo nini?
Batuli anasema zipo changamoto nyingi zinazowafanya wasifikie mafanikio aliyokuwa nayo Kanumba katika filamu, likiwemo la kutokuaminiwa na wafadhili kunakotokana na baadhi ya waigizaji maarufu wenye majina makubwa katika tasnia hiyo kudhulumu wafadhili hao kiasi kwamba hawataki kufanya kazi na waigizaji wengine wa filamu.
“Wapo wafadhili wameshatoa fedha nyingi kwa baadhi ya masupastaa wetu ili watengeneze filamu zenye ubora na kiwango cha juu ili kuleta hamasa katika soko la filamu kama ilivyokuwa enzi za Kanumba, lakini hakuna aliyethubutu hadi leo, wengi wao wametumia kwa maslahi ya pombe, mapenzi na mambo mengine, wamesahau kwamba walipewa fedha kwa ajili ya kufanyia mapinduzi ya filamu,’’ anaeleza.
Licha ya hayo, Batuli bado anaamini kwamba Kanumba alikuwa na vitu vingi vya ziada vilivyomfanya apendwe ndani na nje ya nchi, vikiwemo uthubutu wake, kujitambua na kuwa na uchungu wa mafanikio.
“Kanumba alikuwa hakurupuki, alikuwa hakati tamaa, hata alipokuwa akichekwa aliamini ipo siku atapigiwa vigelegele, alikuwa mbunifu na mpenda kukosolewa asiye na woga wa kufanya lolote analoona ni fursa kwake,’’ anaendelea kumuelezea.
Anasema: “Kuna kipindi alikuwa anajipanga kwenda kuigiza na waigizaji wa Nigeria, aliponiambia mpango wake huo nilicheka kwamba anakwenda huko ataongea Kiingereza gani, lakini sikuamini jibu lake alisema watajua huko huko, kweli alikwenda na akaigiza na waigizaji wa Nigeria ambao ni maarufu.
“Nakumbuka tulikuwa tukikutana naye kwenye masomo ya Kiingereza, alipokwenda Big Brother watu walicheka Kiingereza chake, lakini hakukata tama, alizidi kujifunza na kujituma, hatimaye akacheza filamu ya “Moses” na mwigizaji maarufu nchini Nigeria, Ramsey Noah, tena kwa Kiingereza kizuri, kila mmoja akaikubali filamu hiyo na ujio wake wa kutangaza soko kimataifa,’’ anaeleza Batuli huku akidai kwamba ni vigumu kuziba pengo la Kanumba.
Haki miliki
Akizungumzia haki miliki, Batuli anaeleza kwamba ni jambo baya linalowaumiza wasanii kwa kuwa baadhi ya wasambazaji wananunua hakimiliki za wasanii, hivyo wakifariki dunia hukosa haki zao nyingi za msingi.
“Mfano mzuri ni kwa Kanumba, kama kungekuwa na hakimiliki ya kazi zake nadhani filamu zake zingeendelea kuuzwa na fedha zingesaidia familia yake, lakini nadhani kwa sasa hali si hivyo, ushauri wangu ni kwamba wanunuaji wa kazi za wasanii wasinunue hakimiliki za kazi zao ili wawasaidie kupiga hatua ya kimaendeleo,’’ anaeleza.
Mapenzi
Batuli anasema alikuwa anafahamu kwamba mwigizaji mwenzake, Nice Mohamed ‘Mtunisi’ alikuwa akimpenda muda mrefu lakini alikuwa mzito kumtamkia.
“Mtunisi aliniogopa, domo zege, wajanja walimuwahi lakini baada ya kusikia nimeachana na mume wangu wa mwanzo akaja kwa gia zote, nikamkubali tukawa wapenzi, lakini hatukupata mtoto,” anaeleza.
“Lakini kwa muda wote wa miaka miwili ya mapenzi yetu alikuwa akinitenda mno, alinidanganya mengi, ilifika kipindi aliniletea dada wa ndani kumbe ni mke mwezangu, nilipochunguza nikagundua kwamba ana mke aliyekuwa akiishi Kimara na pia nilisikia tetesi za kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki, Pauline Zongo, nilipomuuliza alikataa.”
Anasema anakumbuka maisha ya Mtunisi kama maigizo, hakuwahi kumwambia kama alikuwa na mke, lakini alipofanya uchunguzi wake akagundua kwamba alikuwa na mke Kimara, alipomfuatilia yule mwanamke akaja moto akiwa na gazeti lake lililoandikwa habari zangu kuhusu Mtunisi, lakini baada ya kumtuliza na kuzungumza, tukatambua kwamba mwanamume huyo alikuwa akituchezea bila kujijua.
“Mtunisi alikuwa ndani, alipotoka akanipiga kibao, akidai nimekwenda kumfanyia fujo, hapo akaongeza hasira, mimi na yule mwanamke wake tulimchangia tukampiga sana, hatasahau na mapenzi yakaishia hapo, kila mtu akawa na maisha yake sina cha kukumbuka, zaidi najutia kupoteza muda wangu kwake,’’ anaeleza Batuli.
Kuasili watoto
Akielezea maisha ya kuwa na watoto zaidi, anasema anatamani watoto zaidi lakini wa kike tena wawe mapacha.
“Napenda mtoto wa kike kwa kuwa nina watoto wawili wa kiume, nitazungumza na wataalamu wa masuala ya uzazi kama nitafanikiwa sawa lakini nikishindwa nitaasili mtoto wa kike,’’ anaeleza.
Gazeti la Mtanzania,22 May 2015
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live




Latest Images