Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

AJABU:Mwanaume Apandikiziwa Uso wa Mtu Mwingine Baada ya Uso wake Kuaribika na Kuwekewa Sura ya Mtu aliyekufa

$
0
0
Picha ikimwonyesha Norris kabla hajapata ajali, alivyopata ajali na baada ya kuwekewa uso mwingine wa marehemu
Ajali nyingi duniani zimekua zikisababisha vifo vya watu wengi huku zikiacha wengine wakiwa na ulemavu wa maisha ambao huwasababishia kupoteza mwelekeo wa maisha yao na kukata tamaa kabisa.
Pamoja na wengi kubaki na ulemavu, lakini pia madaktari wamekuwa kijitahidi kadri wawezavyo kuwarudisha watu hao katika hali zao lakini moja ya tukio la kushangaza ni la kijana Richard Norris ambaye alipata ajali mbaya na kumpelekea kuharibika vibaya sura yake.

Unaambiwa baada ya ajali hiyo kijana huyo alishindwa kutoka nyumbani kwa takribani miaka 15 na amini usiamini kijana huyo alifanyiwa upasuaji wa kihistoria uliochukua masaa 36 na kupandikizwa uso mpya wa mtu ambaye alishafariki baada ya kupata ajali.

Upasuaji huo ulifanyika katika hospitali ya University of Maryland Medical Center na ulifanikiwa kwa kiasi kikubwa na sasa kijana huyo anaendelea vyema akiwa mwenye furaha.

Kwa kawaida kwa sababu ya maadili ya utabibu watu waliopewa mabaki ya viungo vya wafu hawaruhusiwi kukutana na jamaa au ndugu wa marehemu, lakini Norris hakuweza kujizuia kukutana na Aversano, kutoka Maryland ambaye ni dada wa marehemu.

Waziri Nyalandu na mkewe Faraja kwenye jarida la bang time hii !

$
0
0

Bang ni miongoni mwa Majarida ya Tanzania ambayo yamekuwepo kwenye headlines kwa muda mrefu ambapo time hii kuna toleo jipya ambalo Waziri wa mali asili Lazaro Nyalandu na mke wake ndio wamecover.

Humo ndani wanazungumzia maisha yao, pia Waziri anazungumzia ishu yake ya kuutaka Urais wa Tanzania, amewazungumzia vijana wa Tanzania na mengine mengi hivyo ukiipata nakala yako utakutana pia na wengine akiwemo mtangazaji Sporah

Baada ya Jana Lowassa Kutangaza nia Urais 2015..January Makamba Nae Aja na Mpya...

$
0
0
Tume ya taifa ya uchaguzi imeshatangaza kwamba uchaguzi mkuu utafanyika October 2015 ambapo sasa ni headlines zake zinachukua nafasi kwa watu mbalimbali kutangaza nia za kugombea nafasi ya juu ya Urais.
Post hii inamilikiwa na January Makamba ambae ni Mbunge wa Bumbuli Tanga na anautaka Urais pia ambapo May 30 2015 aliandika :

  •  ‘Wiki ijayo tutataarifu ni lini na kwa namna gani tutazungumza na Watanzania, kuchukua fomu, kuanza safari za mikoani kukutana na Watanzania

Sentensi 18 za Edward Lowassa akitangaza kugombea Urais Arusha

$
0
0
May 30 2015 inakuwa siku ambayo inaingia kwenye Historia kubwa kwenye ishu za siasa Tanzania.. bado miezi michache ufanyike uchaguzi mkuu, mmoja ya watu ambao walitajwa sana na kuwa kwenye headlines kubwa kwenye vyombo  vya habari ni Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa.

Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid katikati ya Jiji la Arusha ulishuhudia kwa mara nyingine kujaa kwa watu ambao walikuja kushuhudia Mbunge huyo akitangaza nia ya kugombea Urais mwaka huu.


  • “Watanzania wanahitaji mabadiliko, nina uwezo wa kusimamia mabadiliko hayo.. Mwalimu Nyerere alisema Watanzania wasipoyapata mabadiliko hayo ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM. sina shaka tukijipanga vizuri ndani ya CCM tunaweza kuwapa Watanzania mabadiliko wanayoyataka”  Edward Lowassa.
  • “Nchi yetu inahitaji viongozi wenye sifa hizi.. uongozi wenye uthubutu usioogopa kufanya maamuzi magumu, uongozi usioyumba.. aweze kuwaunganisha Watanzania na kutoa utofauti kati ya walionacho na wasionacho“ Edward Lowassa.
  • “Nina hamu, nina shauku na nina uwezo wa kuiongoza Tanzania… ninaamini nina kila kigezo cha kuibeba dhamana ya nchi yetu.. Katika vitu ninavyojivunia ni pale nilipoenda kupigana vita ya Kagera, nilishiriki kikamilifu nikiwa miongoni mwa askari wa mbele kuikomboa nchi yetu, muwaulize wengine waliwahi hata kufika Kagera?” Edward Lowassa.
  • “Kwa wingi wa rasilimali tulizonazo tuna kila sababu ya kutokuwa ombaomba… Haya ninayoyaeleza ndio msingi wa utendaji wa serikali nitakayoiongoza nikichaguliwa.. nimeamua kugombea Urais ili kupambana na umaskini.. Uongozi wangu utaleta mchakamchaka wa maendeleo” Edward Lowassa.
  • “Najua Watanzania wangapi wanaishi kwa bodaboda, mama ntilie.. hawa ni rafiki zangu hawatafukuzwa barabarani.. ni raia wa Tanzania wanaostahili kula kama wewe“
  • “Kwenye michezo tumechoka kuwa kichwa cha mwendawazimu, tutaibadili hali hii kwa kasi sana“  Edward Lowassa.

Nancy Sumary na Dada Yako Nakaya Kunani ? Je ni Kweli Kuna Beef Kati ya Hawa Ndugu Wawili?

$
0
0
Nasikia Habari ya Mjini ni kuwa Hawa Ndugu wawili wa Damu Nancy Sumary na Dada yake Nakaya Kwa sasa Haziivi Hata Kidogo...Je Kunani Ama ni Uzushi tu ...Embu kwa Anaye jua A-Z atujuze....Maana Sitaki Kuamini Jinsi walivyokuwa wanapendana..eti sasa kila mtu kivyake....

Lucy Komba: Shida Kuubwa Tuliyonayo Wasanii...'Ukiwa na Kijana Utaambiwa Hufanani Nae Ukiwa na Mbabu Utaambiwa wa Nini'

$
0
0
SHIDA KUUBWA TULIYONAYO WASANII ukiwa na mwanaume kijana utaambiwa hufanani nae, ukiwa na mbabu utaambiwa vijana wote waliojaa mjini mbabu wa nini, ukiwa na kijana ambaye hana hela utaambiwa na umaarufu wote huo umekosa mwanaume mwenye hela, ukiwa na tajiri utasikia anasura mbaya lakini pesa sabuni ya roho, ukiwa na mzungu mzee utaambiwa huna lolote usubiri madakesi tu, ukiwa na mzungu kijana utaambiwa mzungu gani hana hela.

Sasa je tufanyaje? Tuchagulieni nyie basi wa kufanana na sie. Lakini mimi naangalia moyo wangu unavyoniambia siangalii ya binadamu hasa sisi weusi maneno hayakauki.

By Lucy Komba on Instagram

Mwigulu Nchemba Kutangaza Nia ya Kugommbea Urais Leo Saa 9 Alasiri Chuo cha Mipango, Dodoma

$
0
0
Mwigulu  Nchemba  Kutangaza  Nia  ya  Kugommbea  Urais  Leo  Saa  9  Alasiri.

Kama  kawaida, Mpekuzi  itakuwa  hewani  kukupatia  dondoo  muhimu za  sera  yake.

Itarushwa Live na Star TV

Hawa walisherekea kifo cha Mwalimu Nyerere, leo wanamtumia kuutaka urais!

$
0
0
Tuachane na Josephat Gwajima anayejiita ni mchungaji japo sijui nani alimtunuku uchungaji na kwavigezo vipi, yeye hana tofauti na sigara kali

Aliyekuwa anaamini Kingunge ni kiongozi wa kitaifa atafakari upya,Jiulizeni kwa nini hakupata nafasi ya juu kama Mzee Kawawa enzi ya mwalimu?

Ni Kingunge huyuhuyu alifukuzwa ukuu wa mkoa singida na Mwalimu Nyerere, leo anajivika chanda cha Mwalimu.

Lowa alifukuzwa uanachama wa TANU kwakosa la kuiba pesa ya ujenzi wa ofisi za umoja wa vijana wa Tanu jijini Arusha yeye akiwa ni katibu wa vijana mkoa,

Ni Moringe na baadhi ya wazee waliopiga magoti kumuombea punguzo la adhabu na hivyo akapewa adhabu ya kuwepo Lumumba tu bila kazi yoyote kwa mda wa mwaka mzima.

Katibu wa vijana TANU Taifa ndugu Elly Anangisye alifukuzwa moja kwa moja na ubunge wa Rungwe akavuliwa.

Alipofariki tu Mzee Nyeree, Lowasa na kundi lake walifanya party na kupongezana, wengine walipigiana simu hata kabla hajafa kuwa kikwazo kimeondoka,

Leo kutangaza nia ya urais wanamtaja Mwalimu kama mbeleko.

Rip J.K Nyerere

BY Yericko Nyerere/JF

LULU MICHAEL Afyatuka Aamua Kumtolea Uvivu HUSNA MAULID...'Acha Kutafuta Kiki za Kisen** Kupitia Mimi'

$
0
0
Haya haya...mwenzenu uswahili niliacha Sema Naomba leo niuridie kdgo ️na Tafadhali kwa ndugu,jamaa,Marafiki ️na yyte. Mwenye uwezo ww kumfikia Mtu anaitwa HUSNA MAULIDI mtanisaidia ku munch ️na kumfikishia huu ujumbe....

ANGALIZO:Post hii itakaa kwa dk5tu....sihiitaji Post Virus in my New n fresh Page...!
Mwambieni na YEYE nilishamwambia ANIACHE mana inaonekana hawezi kukaa muda bila kunitaja au kuniongelea..!

️Ni hivi huu ni mwaka wa pili probably umekuwa UNAONGEA SANA on social media Lkn mm Nakaa kimya...Sio mjinga mwenzio...nakuepuka usijekuwa unatafuta pa kufia bureee...2nd stop competing wth me shooo tuko tofaaaaaaaaaautiiiiii my friend😭😭😂
Hivi ushangai mtu hana Muda ️na ww LKN we hakukauki mdomoni..!
Me sikutukani ila naomba ujumbe ukifie tu....ungefanya kama hujawahi kuniona wala kunijua tokea umezaliwa mana me nishafanikiwa kwa hilo..hakuna kipengele ulichobaki kwenye akili yangu hata kwa bahati mbaya..!

I thnk ukiacha kutafuta Kiki za kisen** kupitia mm bdo utakuwa wewe tu n nothing will change...!Oky bi dada
Angalizo:sio kama sijui matusi,na maneno ya shombo ninayo pia ila nimeamua kutumia Busara tu...!

Written By Lulu Michael

Huyu MBUTA NANGA Unaweza Kumuona Fyatu na Kichaa..Lakini ni Mzima na Anajua Anachokifanya kwa Uchizi Wake

$
0
0
Ebhana eeeh! Huyu mdada unaweza kumuona fyatu, kichaa, kichwa ngumu na yote unayotaka. Lkn ni mzima kabisa ana akili timamu na anajua anachokifanya. Na anawapata wengi sana....mtamtukana, mtampost na pia mtaangalia kazi zake halafu yeye ndo furaha yake!!! Mi huwa namchukulia kama comedian simchukulii serious sana!

Hizo videos zake na ukichaa wake kila kitu kinaishia kumuingizia pesa....yaan very ceative. Na anapata wateja ni balaa anauza dozens and dozens...hizo chupi akishusha mzigo bongo watu watakimbilia kununua na kuuzia watu kama sio yeye aliyetengeneza.

Kila mmoja wetu kuna mahali ni dhaifu na mahali ana nguvu fulani.....dada @mbutanangablog ukiweza kujitahidi kujizuia hasira zako kwa wanaokuudhi. Utakuwa ni dada ambaye wengi wataiga mfano na kujivunia unatoka Tanzania...bila hivo wengi tutaendelea kukichukulia kimzaha tu...kumbe kuna kitu kikubwa cha thaman ndani yako.

By Mrekebishatabia Instagram

Gwajima: Asiyempenda Lowassa Akale Limao!!!

$
0
0
Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Askofu Josephati Gwajima amesema kwamba mwananchi  au mwanasiasa  yeyote asiyempenda Mbunge wa Monduli Edward Lowassa akale limao

Askofu Gwajima alisema hayo juzi  mara baada ya Edward Lowassa kumaliza hatuba yake wakati akitangaza  nia ya kutaka kugombea  urais katika uchaguzi mkuukwa  tiketi  ya  Chama cha Mapinduzi, CCM.

Kabla ya kumaliza hotuba yake wananchi walimshinikiza Edward Lowassa amsimamishe Askofu Gwajima  ndipo Lowassa alimuita na kumpa maiki aongee na wananchi waliofurika katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid  jijini Arusha.

Askofu Gwajima  alianza kwa kuomba mwenyezi Mungu aibariki safari ya Matumaini ya Mbunge wa Monduli Edward Lowassa na mwisho kabisa kuwapa mjumbe mzito wananchi kuwa mwenye Chuki na Lowassa akale limao.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya June 1, 2015

$
0
0

January Makamba: Taifa liko njia panda, Wananchi Chagueni Kiongozi Atakayeleta Maendeleo

















January Makamba: Taifa liko njia panda, Wananchi Chagueni Kiongozi Atakayeleta Maendeleo

Makalio Makubwa ya Agness Masogange Lasababisha Ajali

$
0
0
Agness Masogange
Imelda mtema
Makubwa! Lile kalio la haja la muuza nyago maarufu kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva, Agness Gerald ‘Masogange’ limesababisha ajali kati ya bodaboda na Bajaj maeneo ya Sinza-Mori baada ya mrembo huyo kushuka kwenye gari akielekea saluni.

Shuhuda wa tukio hilo alisema kuwa bodaboda ilikuwa ikitokea upande wa Baa ya Meeda na Bajaj ilikuwa ikitokea upande mwingine ambapo muendesha bodaboda alitumia muda mwingi akimtazama Masogange aliyekuwa akikatiza huku akilitingisha wowowo ndipo jamaa huyo akasababisha ajali.


Yaani aliposhuka Masogange tu kwenye gari yule mwendesha bodaboda hakuwa anaangalia mbele kabisa wakati Bajaj ilikuwa ikija kwa kasi hivyo akashindwa kuikwepa akaivaa na kumrusha dereva wa bodaboda upande mwingine kwa kishindo,” alisema shuhuda.
Agness Masogange Akionyesha Makalio yake

Mpashaji wetu alizidi kuweka wazi kuwa baada ya ajali hiyo kutokea, watu walikusanyika kitendo ambacho hata Masogange kilimshtua na kumfanya asimame kuangali tukio hilo.

Hata hivyo, shuhuda huyo alisema madereva hao walielewana na kuyamaliza palepale.

Baada ya gazeti hili kupata ‘ubuyu’ huo, lilimtafuta Masogange ambapo alikiri kutokea kwa ajali hiyo lakini mwanzo hakujua kama yeye alikuwa chanzo cha ajali hiyo.

Unajua mimi nilivyosikia kishindo na watu wakipiga makelele sikujua kama  nilikuwa chanzo hadi niliposikia watu wanaanza kunong’ona maana hata mimi nilikuwa nashangaa na kujikuta nikicheka tu kwani sikujua wowowo langu lilisababisha shida,” alisema.ge.

Miss Tanzania Amchokoza Zari, Yadaiwa Ana Mahusiano ya Kimapenzi na Mwanamuziki Diamond Platnumz

$
0
0
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa katika pozi na miss huyo.
Musa mateja
Madai mazito! Mshiriki wa Kinyang’anyiro cha Miss Tanzania 2011/12 ambaye alianza harakati za kunyakua taji hilo akitokea Mkoa wa Shinyanga na baadaye kutwaa Taji la Miss Kanda ya Ziwa, Glory Samwel anadaiwa kumchokonoa Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kwa kile kinachodaiwa kuwa ana ukaribu wa ‘kimalovee’ na mpenzi wa Zari, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Chanzo cha ‘unyunyuzi’ huo kilitonya kwamba, mlimbwende huyo amekuwa akionekana mara kwa mara akijivinjari na Diamond jambo ambalo wadau wamelishtukia na kubaini kuwa ana mpango wa kuingilia penzi la Zari na kusambaratishia uchumba wa wawili hao.

Ijumaa Wikienda lilinyetishiwa habari hizo hivi karibuni na kuamua kuzifanyia kazi hatua kwa hatua, ambapo liliweza kujiridhisha kwa baadhi ya matukio ya picha ambazo mrembo huyo amekuwa akipiga na Diamond.

Mbali na picha pia kuna matukio ya sherehe za ‘bethidei’ ambazo Diamond alionekana akiwa karibu na mrembo huyo.

Ukiachilia mbali uchunguzi huo, mwanahabari wetu alimtafuta mrembo huyo kwa lengo la kutaka kujiridhisha juu ya madai hayo ambapo alikiri kuwa na ukaribu na Diamond huku akifafanua kwamba uhusiano wake na jamaa huyo si wa kimapenzi kama wengi wanavyomchukulia.

Hizo picha za karibu zaidi ni zile ambazo tulipiga kwenye bethidei ya meneja wa Diamond aitwaye Salaam, ambayo ilifanyika pale nyumbani kwake (Salaam) Kijitonyama (Dar) hivi karibuni.

Ni kweli watu wengi wananituhumu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Diamond lakini si kweli maana ninajuana naye kawaida tu,” alisema Glory.

Kwa upande wa Diamond aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa ni kweli anamfahamu Glory ila si mpenzi wake na anachokijua ni shabiki wake kama ilivyo kwa wengine.

Alisema hata picha alizopiga naye hakuna picha za hovyo maana zilipigwa hadharani.

Glory ni shabiki wangu wa kawaida tu kama ilivyo kwa mashabiki wangu wengine, suala la kupiga naye picha halimaanishi ni demu wangu,” alisema Diamond.

Mchezaji Mrisho Khalfan Ngassa Atoa Rasmi Sauzi Afrika Akiwa na Mkewe 'Nimekuja huku kuhamia rasmi sasa, tunakwenda kuangalia nyumba'

$
0
0
Ngassa na Mkewe Radhia
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa amewasili nchini Afrika Kusini leo tayari kwa maisha mapya katika klabu mpya, Free State Stars ya Bethlehem.
Mchezaji huyo wa zamani wa Kagera Sugar, Azam FC na Simba SC, Ngassa ametua Johannesburg leo asubuhi na kuunganisha safari kwa gari la dogo la Free State kwenda Bethlehem.
Ngassa ametua na mkewe, Radhia Enea Mngazija na watakwenda kukagua nyumba aliyopewa na mwajiri wake, tayari kuanza maisha mapya.

Nimekuja huku kuhamia rasmi sasa, tunakwenda kuangalia nyumba mimi na bibie (Radhia). Unajua mambo ya nyumba ni ya akina mama. Sasa yeye akisema ameipenda nyumba, nawaambia safi, tunaingia,”amesema.

Hata hivyo, Ngassa atarejea Dar es Salaam wiki ijayo kwa ajili ya kujiunga na kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars kinachokwenda kucheza na Misri mechi ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika katikati ya mwezi.

Nadhani sitakuwa na muda mrefu, viongozi niliwaambia kabisa natakiwa kwenye kambi ya timu ya taifa. Kwa hivyo wanajua. Natarajia kurudi wiki ijayo tu kujiunga na timu ya taifa,”amesema.
Ngassa amejiunga na FS mwanzoni mwa mwezi huu kwa Mkataba wa miaka minne, kama mchezaji huru baada ya kumaliza Mkataba wake Yanga SC.

Mwanamuziki SHETTA Aibua Tena Vita ya Maneno Kati ya BIKIRA wa KISUKUMA na Mwaandaji wa Instagram Partyz Freeconic Ideas

$
0
0
Hawa ni marafiki wawili waliowahi kufanya kazi pamoja lkn kwasababu ya kutoelewana kibiashara wakatengana kila mmoja akaenda njia yake. Seth yeye now yuko EFM radio na Fred yuko na Freeconic Ideas kampuni yake.

Jana radio ya EFM waliandaa event ya miaka 16 ya msanii Juma Nature ambapo Bikira wa Kisukuma akaipigia kampeni kwa maneno hayo juu kuhusu kuwepo kwa msanii Shetta ukumbi Dar Live....ilionekana ni maneno ya kuudhi kwa mwenzake ambaye pia alikuwa na event ya Instagram Party na Shetta naye alikuwepo sehemu hiyo pia.

Nimechunguza pande zote mbili kuona tatizo nilichogundua hapa ni lugha ya biashara kila mmoja amvutie msikilizaji au anayehudhuria, kila mmoja kwa namna yake kufanya matangazo kuhamasisha watu kuhudhuria events zao.

Seth na Fred nyie bhana hamjakutana barabarani isifike hatua mkaanza kuwapa watu faida mtandaoni, kama kuna mtu bado ana wivu na kinyongo na mwenzake muonane muweke peace na ikibidi mshirikiane kwa mambo mengine yanayohusu events.

Mmeanza kazi kwa kuijenga IG party pamoja wakati hamna kitu mpaka hatua nyingine Seth kuweka bond gari yake ili mpewe pesa, kwa kile cheo cha afisa Masoko aliweka nguvu kubwa kutafuta masponsors ambao ndio hao hao mko nao pamoja mpaka hivi sasa na mengine mengi khs kampuni ya @freconic_ideaz Leo hii nadhan si busara kuitana kwenye mitandao nyie ni ndugu mnaweza kuonana na kuyazungumza kama kuna kitu kilibaki.

By Mrekebishatabia

Haya Ndio Madhara ya Wapenzi Kunyonyana Sehemu za Siri kwa Kutumia Midomo Wafanyapo Mapenzi

$
0
0
ZAIDI ya nusu ya vijana Duniani wanakumbwa na magonjwa mbalimbali yanayotokana na maambukizi ya virusi vinavyotokana na ngono zembe.

Kwa muujibu wa utafii uliofanywa na jopo la Madaktari nchini Marekeni umebaini kwamba, vijana wengi hususan Barani Afrika wanakumbwa na magonjwa ya kuambukiza kutokana na tabia ya kufanya ngono zembe na kunyonyana sehemu mbalimbali za miili yao.

Utafiti huo umebaini kwamba, vijana wengi wanapenda kuiga tabia  zinazofanywa na baadhi ya watu mbalimbali wanaoigiza muvi mbalimbali duniani zikiwemo muvi za ngono.

Madaktari hao katika utafiti wao wamebaini kwamba, vijana wengi hupenda kunyonyana ndimi zao,sehemu za siri,makwapani sehemu za makalio kwenye matiti bila kujali kwamba, mwili wa binadamu unazalisha bakteria nyingi kila kukicha na kwamba bakteria hizo, huwa sumu pale zinapoingia kwa binadammu mwingine.

Katika hatua nyingine utafiti huo pia umebaini kwamba, kuna baadhi ya wanawake wanapenda kunyonya ndimi za watoto wao wakati wa kuwalisha vyakula, ama kuwabiga mabusu kila wakati bila kujali usafi wa vinywa vyao, kiasi cha kusababishi maambukizi ya magonjwa ya ngozi kwa watoto wao.

Kuhusu filamu hizo madakati hao walisema kwamba, watu wanaoigiza katika picha mbalimbali wanakuwa chini uchunguzi wa watalaam wa afya, kabla na baada ya kurekodi filamu, tofauti na watu wanavyo dhani kwamba wale kweli ndiyo tabia yao na pengine ni watu waliokutana na kuanza kunyonyana ovyo.

Mashabiki Wamshauri Mwigizaji LULU MICHAEL Haya Kutokana na Bifu Alilonalo na HUSNA MAULID Lililosababishwa na Kuchukuliana Mabwana

$
0
0
Mwigizaji Lulu Michael Jana alishindwa kuvumilia na Kumtolea Uvivu Mrembo Husna Maulid Akitaka Amkome na Kuacha Kumuongelea, Lulu Alitoa Meneno Makali ambayo yamefanya baadhi ya Mashabiki wake Kumshauri ...

Hawa ni Baadhi ya Mashabiki waliomshauri kupitia Instagram:

mrekebishatabia @elizabethmichaelofficial mumy! We sasahivi focus kwa unayoyafanya...kama ni shule, kazi nk.....Haujaanza kusemwa leo na ulinyamaza kimya maisha yakaendelea, naona unaanza kuzua majadiliano kwenye social networks.... hapa ndo sasa unachokonoa watu kuongea mengi na media kuandika. Fanya yako kwa bidii itasaidia kuziba yale mengine. 12

cjthefqueen @elizabethmichaelofficial ningekushauri siku nyingine kabla hujaruhusu hasira zikucontrol mamii kaa chumbani ufikirie mangapi mazito umepitia then pima maumivu ya yale ulopitia na maumivu ya kusemwa na mtu mmoja halafu ukipata jibu piga goti sali na useme Asante Mungu. ...... Chukua cm yako n listen to the song u lv the most basi utakuwa umeepusha shirki hapo.


good_belle Huyo lulu mnamuonea buree husna ndo kaanza au hamjaona kuna smtimes mtu unachoka inabid tu hana moyo wa chuma huyuu 3

joyjovlyne_movingshop_tz Love u bby n fanya yako dear n by da way best wishes Roho wa Mungu akutangulie n kil dem wd success mamiii@elizabethmichaelofficial 4h

liliousbyt  la mjinga au mpumbv ni kukaa kimya, kujibishn ny ni kuonkn wote ni matahira tuuu aliponymz tk kipnd kile we all see how class she is but nau haya jan husna kajibu vile na leo yeye atajibu hivi and then wat next? Na we all know for other side who is guilty n not guilty inspite of all this bull shit!! So mi naona @mrekebishatabia ameongea point kwanza ana mitihn focus na kusoma na mitihn uvune mavuno mazr hp bdye na si kujibishn mtandaoni 7


staystrong_lizymichael Wataongea tu ila watanyamaza coz watz tumeumbiwa hivyo, as she said ni miaka kama miwili kavumilia matusi na maneno yote, sometimes kusema au kuongea chochote katika yanayoendelea kunafanya utoe dukuduku lako moyoni na maisha yanaendeleaa, kasema kamaliza I hope hata nafsi yake iko safiiiiiiiii @mrekebishatabia @elizabethmichaelofficial  13h
Read more at http://websta.me/n/mrekebishatabia#SwFViPkMc1U4vz6s.99

Mwanamuziki AY Ayapa Kisogo Mapenzi, Aamua Kuwa Single Boy..'Sasa ni Mwaka Mzima Umepita Bila.....'

$
0
0
AY ameamua kujipa mapumziko marefu ya kutokuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi.

Rapper huyo alikiambia kipindi cha Mlimanidotcom cha Mlimani TV kuwa ana mwaka mmoja na nusu sasa bila kuwa kwenye uhusiano wowote.

Sasa hivi nimeingia kwenye break karibia mwaka mmoja na nusu,” alisema AY.

Kila mtu ana uamuzi wake na kila mtu ana mipango yake katika maisha so kwa upande wangu nimeona nifocus sana kwenye kazi na ndio maana mnaona matokeo ya kazi inavyofanyika. Sometimes vitu kama hivyo vinakusogeza mbele, sometimes inaweza ikakudiscourage uwaka slow katika kazi zako. Ikitokea imetokea ila sasa hivi nipo kama baiskeli.

Ukweli wa Sakata Zima la Richmond Na Jinsi Lowassa Alivyohusishwa na Sakata Hilo

$
0
0
Kwa  mara  ya  kwanza  Waziri  Mkuu  wa  Zamani, Edward  Lowassa  amefunguka  na  kueleza  ukweli  halisi  wa  sakata  zima  la  Richmond  lililomfanya  achukue  uamuzi  wa  kujiuzulu  wadhifa  wake  wa  uwaziri  mwaka  2008.

Katika  maojiano  maalumu  na  Mpekuzi,Lowassa  amewaka  wazi  kuwa  anapata  shida  kujua  kama  tupo  makini  kusimamia  ipasavyo  mambo  yanayohusu  maisha  yetu,kwani  masihara  ya  kisiasa  yaliyoratibiwa  na  baadhi  ya  wabunge  ndiyo  yaliyosababisha  serikali  kupitia  Tanesco kushindwa  katika  kesi  ya  kuvunjwa  kwa  mkataba  wa  Richmond/Dowans  katika  mahakama  ya  kimataifa  ya  usuluhishi  wa  mizozo  ya  kiuwekezaji (ICC)  iliyopo  Paris  nchini  Ufaransa  na  kutakiwa  kulipa  mabilioni  ya pesa.

Pamoja  na  mambo  mengine, Lowassa  ambaye  ametangaza  nia  ya  kuwania  nafasi  ya  Urais  amezungumzia  kwa  kina  urafiki  wake  na  Rais  Jakaya  Mrisho Kikwete  pamoja  na  utajiri  wake.

Ukweli  juu  ya  Sakata  la  Richmond

Swali: Utakumbuka  kwamba  ulijiuzulu  uwaziri  mkuu  kutokana  na  sakata  la  Richmond. Leo  hii  ni  miaka  saba imepita, unaweza  kutueleza  uhusika  wako  katika  sakata  hili?

Jibu: Waswahili  wanasema  ukweli  unajitetea  wenyewe.Lakini  nianze  kulijibu  hili  kwa  kueleza  maana  halisi  ya  dhana  ya  kuwajibika.  Si  kosa  hata  kidogo  kujiuzulu  wadhifa  wa  kisiasa  kunapotokea  mkanganyiko  wa  mambo  kwa  namna  ile  ilivyotokea. Uongozi  ni  dhamana.

Mimi  sio  kiongozi  wa  kwanza  hapa  nchini  na  nje  ya  nchi  kuwajibika  yanapotokea  mambo  ya  namna  hiyo. Rais  wetu  mstaafu  mzee  Ali  Hassan  Mwinyi  alipata  kuwajibika  kwa  njia  ya  kujiuzulu  uwaziri  wa  mambo  ya  ndani  baada  ya  Raia  kuuawa  na  polisi  mkoani  Shinyanga  miaka  ya  70.

Naamini  kwa  dhati  kabisa  kwamba  watanzania  walio wengi  sasa  wanajua  zaidi  ukweli  kuhusu  sakata  la  Richmond  ambalo  lilisababisha  nijiuzulu  uwaziri  mkuu.

Pengine  niseme  tena  leo, kwamba  niliwajibika  kisiasa  kwa  sababu  kuu  mbili:

1:Kulinda  heshima  ya  chama  changu  na  serikali  kama  nilivyosema  wakati  ule.

2: Nilijiuzulu  ili  ku 'register'  masikitiko  yangu  kwa  namna  kamati  teule  ya  bunge  ilivyolitaja  jina  langu  sana  na  tena  kwa  namna  ya  kunituhumu  kwa  mambo  ambayo  sikuyafanya, wakifanya  hivyo  pasipo  kunipa  haki  ya  msingi  ya  kusikilizwa (Natural  Justice).

Sakata  la  Richmond  ni  kielelezo  kizuri  au  mfano  mzuri  wa  kihistoria  wa  namna  magomvi  ya  kisiasa  yanavyoweza  kuliingiza  taifa  katika  gharama  au  hasara  kubwa

Ni  jambo  la  bahati  mbaya, kwamba  kasoro  za  kimaamuzi  na  kiutendaji  zilizotokea  wakati  wa  mchakato  wa  kutafuta  suluhu  ya  dharura  iliyokuwa  ikikusudiwa  kulinusuru  taifa  katika  madhila  kubwa  iliyokuwa  ikitokana  na  ukame  mkali  ulioikumba  nchi  yetu  katika  kipindi  cha  kati  ya  mwaka 2005  na  2007, yaligeuzwa  kwa  sababu  tu  ya  kuendekeza  ugomvi  wa  kisiasa  na  kuwa  kile  kilichopewa  jina  la  "Kashfa  kubwa  ya  Ufisadi".

Ni  lini  na  wapi  kulipata  kuwa  na  rushwa  katika  mkataba  ambao  serikali  ambayo  mimi  nilikuwa  waziri  mkuu  wake, ilifikia uamuzi  wa mkusudi  kabisa  wa  kukataa  kuilipa  hata  senti  moja  kampuni  ambayo  ilionyesha mwelekeo  wa  kusuasua  baada  ya  kushinda  zabuni  ya  kuleta  mitambo  ya  kuzalisha  umeme  wa  dharura  wa  megawati 120. Nasema  hakuna  hata  senti  moja  ya  serikali  ilitumika  kuilipa  Richmond.

Ikumbukwe  kwamba  uamuzi  wa  kukataa  kuilipa  Richmond  hata  senti  moja  ulifikiwa  serikalini  baada  ya  jambo  hilo  kujadiliwa  katika  ngazi mbalimbali  serikalini  kabla  ya  bunge  kuunda  kamati  teule.

Si  hivyo  tu, ukweli kwamba  mkataba  uliopipa  Richmond  kuzalisha  na  kuiuzia Tanesco  Umeme  ulifuata  taratibu  zote  za  kiserikali  na  kwa  kuzingatia  misingi  wa  mikataba  mingine  ya  mikataba  ya  dharura  ya  namna  ile  ambayo  ishakuwepo,ni  kielelezo  kingine  cha  namna  jambo  hilo  lilivyoshughulikwa  kwa  ushabiki mkubwa  wa  kisiasa.

Leo  hii  ninapolazimika, tena  kwa  uchungu  na  masikitiko  makubwa  kulijibu  swali  hilo, huku  nikitambua  kwamba  ugomvi  wa  kisiasa  ulioratibiwa  na  baadhi  ya  wabunge  ndio  uliosababisha  serikali  kushindwa  katika  kesi  ya  kuvunjwa  kwa  mkataba  wa  Richmond/Dowans  hata  kutakiwa  kulipa  mabilioni  ya  pesa, napata  shida  kujua  iwapo  kweli  tupo  makini  katika  kusimamia  ipasavyo  mambo  yanayohusu  taifa  letu.

Nina  imani  watanzania  ambao  wamekuwa  wakifuatilia  mwenendo  wa  bunge  tangu  wakati wa sakata  la  Escrow  ni  mashahidi  kwamba  wabunge  kadhaa  kutoka  CCM na  upinzani  kwa  nyakati  tofauti  wameonekana  kuanza  kupata  picha  na kutambua  kuwa  kulikuwa  na  njama  za  makusudi  za  kutafutana  na  kuumizana  kisiasa  wakati  wa  sakata  la  Richmond.

Kauli  ambazo  zimetolewa  kwa  nyakati  tofauti  na  hivi  majuzi  na  kiongozi  wa  kambi  ya  upinzani  bungeni, Freeman Mbowe  kuhusu  kile  ambacho  kilitokea  wakati  wa  mzozo  wa  Richmond  ni  ushahidi  wa  hicho  ninachokisema.

Kwamba  leo  hii  mh. Mbowe  anaposema,acha  nimnukuu;
"Kuendekeza  makundi  na  vita  vya  kisiasa  ndani  ya  CCM  na  serikali  yake  kwa  gharama  ya  taifa  hili  sasa  linadaiwa  sh. bilioni 120  baada  ya  kushindwa  kwenye  kesi  ya  Richmond/Dowans  katika  mahakama  ya  kimataifa  ya  usuluhishi (ICC)  huko  Paris"

Mh. Mbowe  haishii  hapo  bali  anakwenda  bali  zaidi  na  kusema  iwapo  ukweli  hautawekwa  bayana,"huko  mbeleni  jambo  hilo  litaligharimu  taifa  mabilioni  haya  ya  fedha  ambayo  yangeweza  kuepukika  kama  ukweli, uwazi  na  haki  vingetawala  mchakato  mzima  wa  kashfa  ya  Richmond."

Ni  wazi  kwamba  anachokisema  Mbowe  hapa  ni  kwamba  swala  hili  lilishughulikuwa  katika  misingi  isiyo  bayana  na kwamba  haki  haikutendeka.

Ukweli  mchungu, leo  hii  mitambo  ileile  iliyoletwa  na  Richmond  na  Dowans  ambayo  ingeweza  kununuliwa  na  Tanesco  kama  baadhi  ya  wataalamu  walivyoshauri, badala  yake  inamilikiwa  na  kampuni  ya  kimarekani  ya Symbion  baada  ya  mkataba  kuvunjwa  kinyume  cha  sheria.

Wakati  tukiugulia  maumivu  ya  makosa  yetu,Rais  wa  Marekani  Barack  Obama  na  aliyekuwa  Waziri  wa  mambo  ya  nje  wa  taifa  hilo  kuwa, Hillary Clinton,kwa  nyakati  tofauti  wakati  wa  ziara  zao  hapa  nchini  walisifia  ubora  wa  mitambo  hiyo  kuwa  ni  ya  kisasa  kabisa  tofauti  na  kile  kilichoelezwa wa  wale  wanaoendekeza  siasa  za  makundi  ambao  walidai  kuwa  mitambo  hiyo  haiwezi  kuwasha  hata  hata  kibatari.

Lakini  kubwa  na  muhimu  katika  yote  hayo  ni  hukumu  ya  Mahakama  ya  ICC  ambayo  ilisomwa  na  majaji  watatu  ambao  weledi  na  uzoefu  wao  mkubwa  kisheria  si  wa  kutiliwa  shaka, mmoja  akitokea  katika  Supreme  Court  ya  Marekani, mwingine  wa  mahakama  ya  Rufani  ya  Uingereza  na  watatu  kutoka  Mahakama  ya  Rufani  ya  Uganda.

Majaji  hao  watatu  katika  hukumu  yao  walitamka  bayana  kuhusu  kufuatwa  kwa  taratibu  zote  za  kisheria  katika  kuipa  ushindi  Richmond/Dowans  katika  zabuni yake  na  kutokuwepo  kwa  wingu  lolote  la  shaka  juu  ya  vitendo  vya  Rushwa  katika  mchakato  mzima  wa  zabuni  hiyo. Vinginevyo  tusingeshindwa  kesi  hii  na  kuligharimu  taifa  mabilioni  haya.

Ukisoma  Ripoti  ya  kamati  ya  Dr  Harrison  Mwakyembe, kuna  sehemu  inaeleza  bayana  kwamba  mwaka 2004,zaidi  ya mwaka  mmoja  kabla  serikali  ya  awamu  ya  nne  ambayo  mimi  nilikuwa  waziri  mkuu  wake  haijaingia  madarakani,kampuni  hiyo  hiyo  ya  Richmond  ilishinda  zabuni  kubwa  ya  kujenga  bomba  la mafuta  kutoka  Dar  es  Salaam  hadi  Mwanza.

Huu  ni  ushahidi  wa  kwanza  muhimu  kwamba  hii  kampuni  ilishakuwa  miongoni  mwa  kampuni  za  kiukezaji  miaka  kadhaa  kabla  ya  mimi  sijawa  waziri  mkuu.

Ukweli  huu  uliothibitishwa  hadi  katika  kamati  teule  ya  Mwakyembe  ni  ushahidi wa  kwanza  wa  wazi  kwamba  eti  mimi  Lowassa  ndiye  niliyekuwa  mmiliki  wa  kampuni  hiyo  ambayo  hata  wawekezaji  wake  sijapata  kuwajua  au  hata  kukutana  nao  hazikuwa  sahihi.

Lakini  tukumbuke  kwamba  madai  haya  yalithibitika  kuwa  siyo  sahihi  baada  ya  mahakama  ya  kimataifa  ya  usuluhishi  kutamka  kwamba  Richmond  ilikuwa  kampuni  iliyosajiliwa  Marekani  kwa  miaka  mingi  na  kwamba  ilishinda  zabuni  ya  kuzalisha  umeme  wa  dharura kihalali.

Kwangu  mimi  jambo  muhimu  katika  sakata  hili  lilikuwa  ni  uamuzi  wa  bodi  ya  tenda  ya  Tanesco  na  wizara  ya  Nishati  ambayo  katika  rekodi  zake  ilikuwa  ikiifahamu  vizuri  Richmond  kutochukua  tahadhari  mapema, yaani  kufanya  due deligence  ipasavyo, kwa  kuangalia  uwezo  wa  kifedha  wa  kampuni  husika  kabla  ya  kuipa  ushindi. 

Sasa  naingiaje  Lowassa  hapo  au  familia  yangu?  Hakika  haya  ni  masihara, Mungu  anajua.

Uhusiano  Wake  na  Rais  Kikwete

Swali:Jina  lako  limetajwa  kwa  muda  mrefu  pengine  kuliko  ilivyo  kwa  mwanasiasa  mwingine  yeyote  ndani  na  nje  ya  CCM  juu  ya  kuwa  mgomea  Urais  katika  uchaguzi  mkuu  wa Oktoba  mwaka  huu.
  1. Je,unafikiri  ni  kwa  nini  imekuwa  hivyo?
  2. Je,umejiandaa  kukabiliana  na  mikiki ya  Urais?
  3. Iwapo  jibu  lako  ni  ndiyo,nini  hasa  ambacho  wewe  unadhani  unastahili  zaidi  pengine  kuliko  kwa  mgombea  mwingine  yeyote  kubebeshwa  dhamana  hiyo  kubwa  na  nzito?
  4. Unaweza  kutuambia  ni mambo  gani  hasa  umepanga kulifanyia  taifa  hili  iwapo  CCM itakuteua  kuwa  mgombea  wake  wa  Urais  na  watanzania  wakakuchagua  kuwa  kiongozi  wao  mkuu?
  5. Kwa  miaka  mingi  sasa  jina  lako  limekuwa  likitajwa  sambamba  na  Rais  Kikwete.Unaweza  ukawaeleza  watanzania  wewe  na  Kikwete  mlikutana  lini  na  wapi?

Jibu: Ni  kweli  kwamba  jina  langu  limehusishwa  sana  na  Rais  Kikwete  kwa  wema  na  kwa  ubaya. Kwa  wema  kwamba  tumefanya  naye  kazi  ndani  ya  CCM,kabla  sote  wawili  hatujapata  fursa  ya  kuitumikia  serikali

Katika  hadhira  na  hususani  nje  ya  CCM, uhusiano  wangu  na  mh.Rais  Kikwete  ulianza  kuonekana  mwaka 1995,wakati  yeye  na  mimi  tulipokubaliana  pamoja  na  tena  baada  ya  kushauriana  kwa  kina  na  hatimaye  tukafikia  uamuzi  wa  kutangaza  nia  pamoja  ya  kuchukua  fomu  na  kukiomba  chama  chetu,chama  cha  mapinduzi  kiteue  mmoja  wetu  kubeba  bendera  ya  chama  ya  kugombea  urais.

Tulipotangaza  uamuzi  wetu  huo, tuliwaahidi  watanzania  mbele  ya  vyombo  vya  habari  kwamba, yeyote  ambaye  angeshinda, yule  mwenzake  aliyeshindwa  angemuunga  mkono  kwa  nguvu  zake  zote.

Kimsingi  kile  ambacho  siku  zote  nimekuwa  nikiita  safari  ya  matumaini  kilianza  na  ndoto  hiyo  ambayo  sote  wawili   tuliijenga  katika  misingi  ya  kutambua  kuwa"Uongozi  ni  wajibu  na  kuwa  kiongozi  ni  kuwa  mtumishi  wa  watu",.

Tangu  wakati  huo, tumeendelea  kuwa  karibu  kirafiki,kisiasa  na  kikazi  na  Rais  Kikwete,tukishirikiana  vyema  katika  kujadili, kuanisha  na  kutafuta  majibu  ya  changamoto  mbalimbali  za  kiungozi  katika  taifa  letu.

Uamuzi  huo  ndiyo  ambao  ulisababisha  wakati  fulani  nilipokuwa nikiongea  na  wanahabari  miaka  kadhaa  baada  ya  kujiuzulu  uwaziri  mkuu  nitoe  kauli  ambayo  ilipewa  tafsiri  tofauti  na  wanasiasa  na  wachambuzi  mbalimbali  wa  masuala  ya  kisiasa  pale  niliposema;" Mimi  na  Rais  Kikwete  hatukukutana  barabarani".

Ni  imani  hiyo  niliyoijenga  katika  misingi  mama  ya  kufahamiana  na  kuaminiana  ndiyo  ambayo  wakati  wa  mchakato  wa  kumtafuta  Rais  wa  Nne  wa  Tanzania  kwa  moyo  wa  dhati  kabisa  nilimuunga  mkono  mwenzangu  katika  harakati  hizo  na  wenzangu  tuliokuwa  na  mawazo  hayo  wakaniteua  mimi  kuwa  mwenyekiti  wa  kamati  ya  ushindi  ambayo  ilikuwa  na  kazi  kubwa  na  ngumu  ya  kuratibu  harakati  za  kumhakikishia  mgomea  wetu  huyo ( Rais  Kikwete)  anateuliwa  kubeba  bendera  ya  kugombea  kwa  tiketi  ya  CCM. Jambo  jema  katika  hili  tulifanikiwa  na  tukashinda.

Kilichofuata  baada  ya  hapo  wengi  wanakifahamu,mheshimiwa  Rais  alinipa  heshima  kwa  ridhaa  yake  mwenyewe  Disemba  2005  kuwa  Waziri  mkuu  wake  wa  kwanza  katika  Serikali  yake.

Hili  la  kwamba  ni  rafiki  yangu, ni  swala  ambalo  hata  yeye  mwenyewe  mheshimiwa  Rais  amepata  kulielezea  hadharani mara  kadhaa  tangu  mwaka  1995  na  baadaye  akafanya  hivyo  mwaka  2005  alipokuwa  akirejesha  fomu  yake  ya  kuomba  ridhaa  ya  CCM  alipotutaja  mimi  na  Rostam Aziz  kuwa  ni  marafiki  zake.

Waliosoma  maandiko  yake  watakuwa  wanakumbuka  kwamba  yeye  mwenyewe  amepata  kuandika  kwa  mkono  wake  kwamba, aliniteua  kuwa  waziri  mkuu  si  kwa  sababu ya  urafiki  wetu  bali  kwa  kutambua  uwezo  na  uchapakazi  wangu.

Kwangu  hilo  ni  jambo  la  faraja  na  kutia  moyo  sana.Naamini  maelezo  hayo  yanajibu  kwa  sehemu  kubwa kile  ambacho  kila  mara  kimekuwa  kikirejewa  kuhusu  urafiki  wangu  na  Rais  Kikwete.
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>