Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Sita wafa katika ajali, 45 wajeruhiwa Singida

$
0
0
WATU sita wamekufa na wengine 45 kujeruhiwa katika ajali mbili tofauti za barabarani zilizotokea juzi na jana mkoani Singida.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka alisema mjini hapa jana kuwa ajali ya kwanza ilitokea Juni 11 mwaka huu saa 1.30 usiku eneo la Manga nje kidogo ya mji huu kwenye Barabara Kuu ya Singida – Mwanza.

Alisema ajali hiyo ililihusisha basi lenye usajili wa namba T174 CAV Scania la Kampuni ya Nice Line linalomilikiwa na Enock Mwita wa jijini Mwanza ambalo lilikuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Mwanza.

Dereva wa basi hilo aliligonga kwa nyuma gari la mizigo lenye namba za usajili RAT 317N/ RL 0754 aina ya Benz lililokuwa limeegeshwa pembeni mwa barabara hiyo na kusababisha vifo vya abiria watatu papo hapo. Wengine wawili walifia hospitalini na kusababisha majeruhi 37.

Kwa mujibu wa Kamanda Sedoyeka, dereva huyo ambaye alikimbilia kusikojulikana baada ya ajali kutokea, alikuwa kwenye mwendo kasi. Katika ajali nyingine iliyotokea Juni 12 saa 12.15 asubuhi katika eneo la Kindai kwenye barabara kuu ya Singida – Dodoma nje kidogo ya mji huu, gari aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T 998 CWG liliacha njia na kupinduka kisha kusababisha kifo cha abiria mmoja na majeruhi wanane.

Alisema abiria wa gari hilo walikuwa wakisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Kahama mkoani Shinyanga kwa ajili ya kuhudhuria mazikoi ya ndugu yao na gari lao lilipofika eneo la ajali kwenye kona kali dereva wake, Paul Bundala alishindwa kulimudu kutokana mwendo kasi.

Baadhi ya waliokufa katika ajali hiyo ni Shija Masanja,Yohana Chimole na Febronia Kway. Miili ya waliotajwa na wengine watatu ambao majina yao hayajatambuliwa imehifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Singida ambapo pia wamelazwa majeruhi.

TANZIA: Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Issa Shaaban Simba amefariki asubuhi ya leo.

$
0
0
Muda mfupi uliopita nimepata taarifa kuwa kiongozi mkuu wa waislamu nchini Tanzania Mufti Issa Bin Shaaban Simba amefariki dunia.

Hakika ni majonzi na pigo kubwa kwa Waislam na watanzania kwa ujumla.

Amezaliwa Shaaban na ameondoka ndani ya mwezi wa Shaaban,
Innalilah wainailah Rajiun.

Mwenyezi mungu ampe kauli thabiti na amjaalie pepo ya kheri na kumsamehe madhambi yake.
The Grand Muft of Tanzania has passed away.

Chanzo: Abdul Mohamed

Wema Sepetu na Jokate Mwegelo Waongea Lugha Moja Kusherehekea Ushindi wa Alikiba!

$
0
0
Alikiba na Jokate wanadaiwa kuwa na uhusiano. Wema amekuwa upande wa Kiba tangu kuachana na Diamond na wengi wamekuwa wakikichukulia kama ni kisasi.
Baada ya ushindi huo warembo hao walitumia Instagram kutoa pongezi zao.
“Hongera sana cherie @officialalikiba kwa kujishindia tuzo sita jana usiku kwenye kiba Tanzania music awards (KTMA) sorry Kilimanjaro Tanzania music awards 2015. Teh teh the,” aliandika Jokate.
“Ni kitu cha kumshukuru Mungu ulikaa kimya miaka 3 ila ukarudi na wimbo mmoja ukatuteka tena. Kusema ukweli tukiachilia mbali ushabiki ‘mwana’ ulituliza akili na ukafanya vizuri sana nchini. Mashabiki wanakupenda. Sana. Mpole hivi, mcheshi, mstaarabu. Na unajua mziki. Tunakuombea sasa hii iwe motisha ya wewe kufika mbali zaidi. Ndio kwanza safari imeanza. Uzuri unaomba mungu so najua hata kutupa. Ila kaza mwana we kazaaa!!! We are behind you,” aliongeza.
Naye Wema aliandika: Nilitaka zote saba ila hata 6 pia sio mbaya…. #KingKiba…. Umetisha.”
Jokate pia amepost picha akiwa na Wema na kuandika: It’s a beautiful and powerful thing when strong girls come together. emojiemojiemoji️. With The Sweetheart @wemasepetu.”

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Tarehe 16 Juni 2015

$
0
0






















Habari  Zilizopo  Katika  Magazeti  ya  Leo  Jumanne  ya  Tarehe 16 Juni 2015

Linah Kutoa 'Tamko Kali' kwa mahasimu na Kumuhusu WEMA SEPETU Kumchukulia Bwana Ake

$
0
0
Star wa muziki Linah Sanga amesema kuwa bado ana dukuduku kubwa moyoni ambalo anajipanga hivi karibuni kulianika hadharani kwa njia ya tamko rasmi ambalo atalitoa kwa njia hiyo hiyo ya mtandao.


Linah
Baada ya kupitia kipindi kigumu cha misukosuko ya kusemwa na vilevile kutukanwa mitandaoni na kulalamika sana, star wa muziki Linah Sanga amesema kuwa bado ana dukuduku kubwa moyoni ambalo anajipanga hivi karibuni kulianika hadharani kwa njia ya tamko rasmi ambalo atalitoa kwa njia hiyo hiyo ya mtandao.
Kwa mujibu wa Linah kupitia mahojiano exlusive tuliyofanya naye, amesema kuwa tamko hilo kwa sehemu linahusiana na tuhuma za kulalamika kuibiwa bwana, kitu ambacho kinaendelea akiwa haoni sababu ya kuendelea kukaa kimya zaidi, na kuumia roho.
Linah amesema kuwa, kwa sasa anajipanga kuandaa waraka huu na kuanzia siku yoyote kutoka sasa, mambo yote kutoka moyoni mwa mrembo huyu anayetikisa chati za muziki ndani na nje ya Tanzania, yatakuwa hadharani.

Wema Sepetu Atoa Sababu kwanini HATOMSAMEHE Kajala Masanja

$
0
0
Kwa muda mrefu sasa hivi watu wanaofatilia habari za mastaa wa bongo wanafahamu kwamba Waigizaji Wema Sepetu pamoja na Kajala ambao walikua marafiki mpaka Wema akamuokoa Kajala kwenda Jela kwa kumlipia faini ya MILIONI 13, hawapatani sasa hivi hata wakikutana hawasalimiani.

Wema Sepetu alikutana na Zamaradi Mketema kwenye show ya CloudsTV (TAKE ONE) na kuongea mengi kuhusu Kajala na kwanini hatomsamehe, kwenye hizi video mbili hapa chini kuna Part I na Part II Wema akiongea yote.
PARTY 2

Watanzania tumwombee na tujitokeze kumsaidia mwanamuziki Banza Stone kwani yupo katika hali mbaya

$
0
0

Akizungumza katika kipindi cha jioni cha E-FM kinachoongozwa na Gadner G. Habash mama mzazi na kaka wa damu wa mwanamuziki fundi na bora wa kizazi cha kati cha watanzania Ramadhani Masanja a.k.a mwalimu wa walimu / Banza stone wamesema kuwa mwanamuziki huyo sasa ni siku ya tatu " hatoi kauli " na " hataki tena kunywa dawa " na " hali yake sasa inazidi kudhoofika " hali inayopelekea wao kukata tamaa na kumwachia mwenyezi mungu. 

Hata hivyo mama mzazi wa banza stone aliwashukuru sana wafanyakazi wa kituo cha redio cha e fm na msanii mwenziye muumini mwinjuma kwa kuwa wamekuwa bega kwa bega kujitokeza mara kwa mara kumtembelea na kumsadia mwanamuziki huyo mahiri ambaye binafsi nakiri kuwa huyu jamaa hakika ni " fundi " ktk medani za uimbaji na utunzi na hili halina ubishi.

Kinachonisikitisha sana ni kwamba hata wanamuziki wenzake tu ni kama vile wamemsusa mwenzao ukiachilia mbali huyo muumini mwinjuma na inasemekana kuwa hata wakipigiwa simu hawapokei na wengi wao wanajifanya wapo busy kwenye ma concert yao wakati ukweli ni kwamba wengi wao tunao humu humu mjini.

Hasira yangu kubwa ipo kwa wale mapedeshee wa mjini ambao nakumbuka walikuwa wakimfuata banza stone na kumpigia magoti kuwa awataje katika nyimbo zake kwa mfano " papa antibiotique muzee wa jamii forum mutu ya fedha mingi " ( wakati ukweli hata hizo hela sina ) lakini sasa hata kumsikia tu huyu jamaa aliyekuwa akiwafagilia hawataki na wanamkwepa.

Uchungu wangu mwingine naupeleka kwa marafiki zake ambao wakati ameugua mara ya kwanza na kupata nafuu ndiyo walikuwa wa kwanza kwenda kumchukua na kumpeleka kula nae bata huku wakimpa mipombesigarana powder huku wao wakidhani kuwa wanamsaidia kumbe ndiyo wamemfikisha hapa alipo sasa.

Jazba zangu za mwisho nazielekeza kwa wanahabari wa tanzania ambao nina uhakika wengi wao wameweza sana kutengeneza majina yao kupitia mgongo wa banza stone haswa kwa kupata habari zenye mvuto kutoka kwake na nakumbuka kuna tv nyingi sana zilikuwa zinamtumia banza stone kama chambo chao ktk kuvutia watazamaji wao lakini sijaona mwandishi yoyote aliyediriki hata kumpa coverage banza stone juu ya hii hali yake mbaya ya kiafya.

Hitimisho:
Najua wengi sasa tunasubiria tu kwa hamu labda Israeli afanye yake kwa Banza stone ili sasa tuanze kushindana kuvaa sutimadela,miwani huku tukienda na magari yetu ya kifahari msibani, kujifanya ku pledge mahela mengi huku tukitafuta coverage ya kutosha ktk media kwa kujifanya tunamjua sana banza stone na kutoa machozi ya kinafiki nakizandiki.

Chonde chonde watanzania wenzangu hali yaBanza stone ni mbaya....narudia nimbaya......na namalizia kusema kuwa nimbaya na naomba uzi wangu huu umguse kila mtu na tujitokezeni kwenda kumjulia tu hali na tuache ushamba kuwa kwenda kumwona mgonjwa ni mpaka uende na kitu ila kwenda kwako tu na maneno yako ya hekima,utu na busara kwa Banza stone kunaweza kumsaidia na akarudi katika hali yake ya kawaida.

Ewe Mwenyezi Mungu mpe nafuu na mjalie afya njema mwanamuziki wetu kipenzi Ramadhani Masanja (Banza stone ) kwani bado tunamujhitaji katika tasnia hii ya muziki wa dansi. 

Amina / Amen.

Nawasilisha..

Source: Jamii forums

Crazy Fans of Wema, Kiba and Jokate to vote for Davido

$
0
0

Hivi watanzania mna masaibu gani. Kuna watu wanadai diamond ana dharau, sasa hyo dharau mnaiona mashabiki wa Wema tu. Nimepita pita kitaa kuuliza watu na wanasema hawana tatizo na Diamond.

Ila nimekuja kujua kumbe chanzo cha chuki ni mimba ya zari na kuachana na wema. Washabiki wa wema hawajakubali hali ya wema kutokuwa na raisi wa wasafi, pia Wema nae bado ana kisasi, na ndo mana anaendesha kampeni ya kumpigia kura Davido na sio mtanzania mwenzake Diamond.

Ila tu nisisitize; Jokate, Wema na Mange, nyie na washabiki wenu mpigien Davido wenu, ila msitake kufanya watanzania wengine wamchukie Diamond bila sababu. Sisi watanzania wengine tutampigia kura.

Na naona Vanesa nae ashaanza kuingia team Wema, mana anajipigia promo yeye mwenyewe na kumuacha Diamond, badilika dada.

Vote for Diamond ana Vanesa, MTV Awards.

By Mdau


This is new Car of Diamond Platnumz Given By his Baby Zari

$
0
0
Gift from Zari to Diamond Platnumz...
Diamondplatnumz Captioned The Above Pic as Follows:
Thanks alot baby it's Finaly Here ���� @zarithebosslady

Baba Haji, Lemutuz Watifuana, Kisa Mchango wa Harusi

$
0
0

Staa wa Bongo Movies, Adam Haji ‘Baba Haji’ amemtolea uvivu ‘The King Of All Bongo Social Media Network’ Lemutuz kutokana na tukio la udhalilishaji  alilolifanya dhidi yake!

Lemutuz ambaye amezoeleka kwa kutoa hisia na mtazamo wake juu ya mambo mbali mbali mtandaoni, mapema wiki iliyopita alimnanga Baba Haji kupitia ukurasa wke kwenye mtandao wa instagram akidai kuwa  amekuwa akisumbua kuhusu michango ya harusikiasi cha kubadili staili ya kudai michango hiyo.

Kutokana na kitendo hicho Baba Haji alishindwa kuvumilia  na kuamua kuandika waraka wa kumjibu kumjibu Lemutuz kupitia mtandao huo huo wa instagram ambapo wasomaji wengi walimuunga mkono na kumshambulia Le Mutuz

Waraka wa Baba Haji ulisema hivi;

Harusi ni jambo la kheri sana kwa wenye kujua, yaani kwa wale ambao Mwenyezi Mungu aliowapa hali ya kulijua hilo! Kiukweli hatuwezi kubisha kwamba ktk Africa watu sote hushauriana na kuchangiana kufanikisha fanction (shughuli) na sio Mahari au maulidi ambayo nimefanya ili kubariki ndoa yangu, na imekuwa kawaida sana kwa miaka ya zamani kabla kuzaliwa kwangu 1980 na hadi sasa.

Wajinga (Kina Lemutuz) wasiojua wenye hila na gilba na inda hupotosha sana watu kwakua tu wao wazazi wao walituibia pesa za mlipa kodi na kwenda kusoma USA au Ulaya na eti wakachukua mila za huko ambazo ni za kiyunani kwa udhalilishaji dhidi yangu eti nilikusumbua kwa simu kukuomba mchango na kisha nikabadili style ya kukufuatilia unichangie mtu mzima ovyo muongo sana wewe huna utu kabisa umejaa nafsi ya kizembe na ujinga uliopitiliza.

Sidhani kama una akili timamu na sidhani kama unalilinda jina la mlezi wako abilisi wa mguu mmoja chago mtembea upande upande.

Baada ya Baba Haji kuweka waraka huu, maoni ya wasomaji wengi yalimshambulia Lemutuzi kwa kile alichokifanya na kumtuliza Baba Haji kwa udhalilishaji aliofanyiwa na mtanzania mwenzake anayejifanya kakulia Marekani.

Picha: Baba Haji akiwa na mkewake siku ya harusi yao.

KIU

Team Diamond vs Team Alikiba: Kinachoendelea Instagram Kinatutia Aibu Watanzania!

$
0
0

Upinzani kati ya Diamond Platnumz na Alikiba sasa unaelekea kubaya. Kiukweli nimesikitishwa sana na kile ambacho ninakiona kikiendelea kwenye Instagram kati ya kambi hizi mbili.


Infact nahisi ushabiki huu una hasara nyingi kuliko faida kwenye industry yetu. Kwa leo sitaongelea jinsi ushabiki wa wasanii hawa wawili wenye nguvu unavyofanya wasanii wengine wanaofanya vizuri nchini kutoangaliwa, bali nitazungumzia kusikitishwa na kile kinachofanyika Instagram ambapo mashabiki wa Alikiba wameanzisha kampeni ya kuhakikisha kuwa Diamond anakosa tuzo kwenye MTV MAMA pamoja na mashabiki wa Diamond kumtukana Davido bila hatia!

Kwanini lakini tunafanya hivi? Hivi kweli tunaamua kujidhalilisha kiasi hiki? Majirani zetu wanatucheka, wanatubeza, wanatushangaa kweli kweli! Ushindani huu wa ndani kati ya wasanii hawa wawili kwanini uondoe utaifa wetu? Ushabiki gani huu?

Diamond Platnumz amechaguliwa kuwania vipengele vitatu kwenye tuzo za mwaka huu za MTV MAMA, iwapo akishinda, ushindi wake si wa familia yake na mashabiki wake peke yake, ni ushindi wa nchi nzima.
Kitendo kinachofanywa na maadui zake ambao infact ni mashabiki wa Alikiba na Wema Sepetu cha kuhamasishana kuwapigia kura Davido na Wizkid ili washinde na kumkomoa Diamond si kizuri.

Ni vyema linapokuja suala la kimataifa, tuweke tofauti zetu pembeni na tuwe kimoja. Kama hili haliwezekani, ni vyema kukaa tu kimya kuliko kuhamasishana kuwapigia kura wapinzani ili msanii wa Tanzania akose.

Haya, jana nimeshuhudia kitu kingine cha ajabu kabisa kwenye Instagram. Davido aliweka post kuonesha nominations nne alizopata.

From nowhere, comments nyingi zikawa ni kati ya Diamond vs Davido! Kwanini? Hii ni page ya msanii wa Nigeria ambaye anawataarifu mashabiki wake kuhusiana na nominations zake sasa huu ushabiki wa Diamond na yeye unatoka wapi tena?

Mbona tunatiana aibu kiasi hiki? Mbona tunaonekana malimbukeni na wageni wa mitandao? Hatuna kazi za kufanya ama nini hiki? Ndio, hadi wanaijeria wanatushangaa na kutuona kama wageni wa hivi vitu? Ugomvi wa Diamond na Davido ulishaisha siku nyingi sasa kwanini mashabiki wanalazimisha uendelee kuwepo?

Kama unampenda Diamond si unajua jinsi ya kumpigia kura, sasa kwanini uende kwenye page ya mtu ambaye wala hana time na masuala hayo na kuanza kumchafulia tu post yake?

Kiukweli tunatiana aibu. Tubadilike!

Bongo5

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Tarehe 17 Juni 2015

$
0
0









Habari  Katika Magazeti ya  Leo

Mwanamuziki Linah Sanga Bado Ana Dukuduku na Wema Sepetu

$
0
0
Siku chache baada kuenea kwa taarifa za kuporwa bwana na Wema Sepetu, staa wa Bongo Fleva Esterlinah Sanga ‘Linah’ amefunguka kuwa bado ana dukuduku kubwa moyoni ambalo anajipanga hivi karibuni kulianaika hadharani kwa njia ya tamko rasmi ambalo atalitoa kwa njia hiyo hiyo ya mtandao

Kwa mujibu wa linah ,amesema kuwa tamko hilokwa sehemu linahusiana na tuhuma za kulalamika kuibiwa  bwana, kitu ambacho kinaendelea akiwa haoni sababu ya kuendelea kukaa kimya zaidi na kuumia roho.

Linah amesema kuwa kwa sasa anajipanga kuaandaa waraka huo na siku yoyote kuanzia sasa mambo kutoka moyoni mwa staa huyo yatakuwa hadharani.

Linah amesema anatarajia kumtangaza rasmi mpenzi wake mpya kutoka nchini Nigeria “ Nampenda sana  mpenzi wangu  nitaamua kumuweka wazi ili mashabiki wangu watanbue uhusiano wangu  mpya ni  wa msanii mkubwa sana  nampenda  hii sio project  ni kitu ambacho ni kweli  nimechoka na masimango ya Watanzania’.

Tanuru la Filamu

WEMA SEPETU Kugombea Ubunge Mwaka Huu..Tuliwaambiwa Vitu Vizuri Vyaja Kutoka kwa Wema Mtulie

$
0
0
Miss Tanzania 2006 na muigizaji wa filamu, Wema Abraham Sepetu jana June 16 kupitia kipindi cha Ala za Roho ya Clouds FM alifunguka kuhusiana na kuchukua fomu ya ubunge wa viti maalumu mkoani Singida pamoja na ishu ya kutoka na boyfriend wa msanii Linah.

Akizungumza na Diva Loveness wa Ala za Roho, Wema Sepetu alisema:

”Sasa hivi niko singida kwenye maandalizi ya kuchukua fomu kwasababu nagombea ubunge wa viti maalumu mkoa wa singida, kwa hiyo nimekuja huku kuja katika kuhamasisha vijana wajitokeze kujiandikisha kwenye daftari la kupigia kura.
 
"Nimekuja kujiandikisha huku kwa sababu mama yangu ni mtu wa singida so nimejiandikisha tayari tukutane 15 tena kuja kuchukua fomu kwasababu fomu zinatoka  tarehe 14 mwezi wa saba so inshallah tuombe uzima, kampeni zimeshaanza zile ndogo ndogo nashukuru Mungu naendelea vizuri nahitaji support kwa jamii"

Baada  ya  Maelezo  hayo Diva  alimuuliza  Wema  swali:
 
“…I Know about kampeni za chini chini ambazo ulikuwa unafanya kwa muda mrefu kwaajili ya kugombea Ubunge na umepiga picha kwa Raqay tayari ukiwa na mavazi ya CCM si ndio kampeni pale iko pale pale au??…”

Majibu  Ya Wema  Sepetu:
“…. Yes nimefanya so ama nilikuwa nazungumza na mangement yangu ambayo yupo Martin kadinda na pia yuko Petiman  ambaye yupo katika suala zima la kampeni yangu.
 
"Watanzania wajue tu yes  nitachukua fomu ya kugombea Ubunge wa viti maalumu ya mkoani Singida and tutaona uko mbele itakavyokuwa kwasababu hiki ni kinyang’anyiro naingia, ni kama vile naingia kwenye mapambano yaani vitaani so kuna kupata na  kukosa .
 
"Sifikiri kukosa kwasababu mtu ukifikiri kukosa unajiweka kwenye negative side sana lakini najua kwa nguvu za watanzania na kwa nguvu za wananchi wa Singida wataweza kuniamini na kunipa kura zao."

Katika mahojiano hayo Diva alimuuliza tena  Wema Sepetu kuhusu ishu ya kuwa na mahusiano na boyfriend wa Lina ambapo  Wema  alijibu:

"Huwezi amini hizo habari si za kweli kwasababu tulikuwa tunafanya project  zinakuja ila nimeshangaa kuona kwanini Linah ameenda on air kwenye kipindi na kuzungumza hizo habari kuwa natembea na boyfriend wake naomba watu waelewe kwamba sikweli…”

Shehe Amuonya Shilole Kuhusu Swala La Mavazi..Soma Hapa

$
0
0


Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salim, amemjia juu staa wa sinema na Bongo Fleva, Zuwena Mohammed a.k.a Shilole au Shishi Baby baada ya kutangaza kuwa anasali swala tano, kauli ambayo inalenga kudhalilisha Uislam kutokana na skendo zake hasa kukaa mtupu, jambo ambalo ni kukiuka maadili ya binti wa Kiislam.

Hivi karibuni, huku akiwa na skendo ya kutia aibu Ulaya, Shilole alidai yeye ni Muislam safi na kwamba ni swala tano, jambo lililoibua mjadala mzito kwa mashabiki wake kwa kuwa alichokisema hakiendani na muonekano wake.
Akizungumza na gazeti hili baada ya kuibuka kwa ishu hiyo, shehe huyo aliamua kuingilia akieleza kwamba sifa za Muislam anayesali swala tano haziendani kabisa na yeye na anapaswa kujitazama upya.

“Kwa kuwa yeye mwenyewe ndiye kasema, hatuwezi kumbishia, isipokuwa kwa jinsi alivyo ukianzia suala la mavazi ni wazi anaidhalilisha dini ya Kiislam kwa sababu Muislam ambaye ni mcha Mungu kwa kiasi hicho, anatakiwa ajisitiri kimavazi.


“Kama haitoshi ukitazama hata matendo yake mfano ile shoo aliyoenda kufanya kule Ubelgiji (Ulaya) na kuonekana sehemu ya matiti haikustahiki kabisa kwani ameenda kinyume na matakwa ya dini yake, inawezekana tukawa tunamlaumu lakini huenda akawa hana mafunzo ya kutosha ya kidini na kujua anapaswa awe vipi ili kuendana na sheria za Dini ya Kiislamu hususan kwa mtu ambaye ameamua kujitakasa na maovu na kumsujudia Mungu,” alisema shehe huyo anayeheshimika.

Alisema hapendi ‘kumjaji’ mtu aliyeamua kubadilika kwa kuacha mambo ya dunia na kumfuata Mungu, hivyo alimpa mwaliko maalum Jumapili afike kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar ambako kulikuwa na mafunzo maalum yaliyotolewa kwa Waislam wote kwa ajili ya kujiandaa na Mwezi Mtukufu wa Ramadhani (haikujulikana kama Shilole alikwenda).

Source : Global Publisher

Audio: Wema Akiongelea Uamuzi wa Kuwania Ubunge wa Viti Maalum: Msikilize Hapa

$
0
0


Wema Sepetu anaingia kwenye siasa rasmi mwaka huu kwa kuchukua fomu ya kuwania ubunge wa viti maalum mkoani Singida kwa tiketi ya CCM. Msikilize akizungumza kwa kina kwenye mahojiano aliyofanya na Diva kwenye kipindi ch Ala za Roho, Clouds FM


WEMA SEPETU Atakwa Kujifunza Kuweka Breki Mdomoni Anapoongea

$
0
0
SALAMU nyingi zikufikie mrembo usiyechuja umaarufu tangu mwaka 2006, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ vipi uko poa? Mishemishe zinakwendaje?
Ukitaka kujua afya yangu, mimi namshukuru Mungu kwani ni mzima, hofu na mashaka ni kwako wewe uliye mbali na upeo wa macho yangu. Kitambo kidogo kimepita sijakuona lakini naamini u-mzima wa afya.
Mbali na kukusalimia, dhumuni la barua hii ni kutaka kukumbusha juu ya umuhimu wa mdomo wako kuwa na staha. Kuna vitu vya kuzungumza lakini kuna ambavyo vinapaswa kuwekwa ‘spea’.

Binafsi sikufurahishwa na namna ambavyo ulimpa maneno makali aliyekuwa rafiki yako, Kajala Masanja kupitia kipindi cha televisheni wiki iliyopita.Si busara kumtusi mwenzako hadharani kiasi kile. Hata kama amekukosea kiasi gani, wewe ni mtu maarufu unapaswa kuhakikisha kile unachokizungumza kitakuwa na matokeo gani mbele ya jamii inayokuzunguka.
Ugomvi wenu wewe na Kajala una historia ndefu, kibusara hakukuwa na sababu ya kuendeleza mjadala ambao hata watu tayari walishaanza kuusahau. Vitabu vya dini vinatufundisha, kusamehe na kusahau.

Nilishawahi kukuandikia barua huko nyuma, nilikusihi usamehe hili suala liishe. Nilisema hivyo kwa sababu mara kadhaa Kajala ameshaonesha nia ya kutaka yaishe lakini wewe ukaendeleza vita. Kwa nini usimsamehe? Mbaya zaidi hata huyo mwanaume ambaye inasemekana alikuibia naye nimetonywa kuwa ameshaachana naye.

Nyinyi mlishibana kama marafiki wa kuambiana kila kitu, la kwako la Kajala na la Kajala la kwako watu wanashindwa kuwaelewa kama kweli mlishibana kwa nini msikae na kuanza ukurasa mpya?
Sijawahi kumsikia Kajala anakuzungumzia vibaya lakini wewe kila siku unamsema. Unafikiri yeye hana mabaya yako? Akiyaanika hadharani utafurahi? Haiwezi kuwa sawa.Nakulaumu wewe zaidi katika hili maana historia inaonesha haudumu na marafiki. Uliwahi kuwa na urafiki na kina Jack wa Chuz, Rose Ndauka, Jamila na wengine kibao lakini wote uliwaacha njiani.
Kama hiyo haitoshi, Aunt naye mmedumu kwenye ushosti kwa muda mrefu lakini naye pia miezi kadhaa iliyopita mlitofautiana na sina hakika kama hadi sasa mpo sawa kama zamani japo mlipatanishwa.
Nikusihi, badilika. Kuwa na staha, chunga sana kauli zako kwani wewe unaheshimika katika jamii.

Nikushukuru kwa kunisoma!
Mimi ni kaka yako,
-
Erick Evarist

DAVIDO Atoa Mpya Kwa Vimbele mbele wa Tanzania Wanaomvotia Yeye MTV Awards, Awaomba Wamvutie Diamond Platnumz yeye Hana Shinda na Vote za Tanzania

$
0
0
Hii kali soma ka screenshot chini....
Imeandika "Tanzania Thanx 4 voting but i don want distabance in my acc plz vote Diamond not me Plz"


Davido msanii wa Nigeria, baada ya kuchoshwa na kufatiliwa na Tanzanians ambao hawataki mTanzania mwenzetu Diamond Platnumz ashinde kura kisa kumsaidia wema anayelilia maoenzi na kiba anayetaka kupaa.

Watanzania hawa wamefikia kutia aibu nchi yetu kwa kuandika maneno ya ajabu na hata kutukanana humo humo. Wanamuomba pia mengi wakijua ni single man...aibuuuuuuuu

Amewajibu na kwa mie hata sishangai alichoandika, watu wanadhani wananchi wa nchi zingine ni wajinga kama wao.

Uwiiiiiii mmetia aibu ujumbe huo

Mwanamuziki Fid Q Chukua Tahadhari, Umeshuka Sana Kimuziki

$
0
0
Fid Q uwezo wako unashuka sana, Fid Q wasasa si Fid Q wa miaka michache iliyopita
Fid Q naheshimu sana uwezo wako wa kuandika japo flow yako si nzuri sana.

Kuhusu kuandika Joh Makini hakwambii kitu lakini flow yako si mbaya sana.

Rudi nyuma angalia ni wapi umekwamba Fid Q, mpaka leo hii umepiga show za fiesta
zisizozidi hata tatu, show kubwa ya Dar hujatia mguu kabisa.

Kidogo watu tumeanza kukusahau, unahitaji kufanya kazi ya ziada ili urudi pale ulipokuwa.

Fid Q rudi zako, enzi zile unaandika mwanza mwanza. Kinyume na hapo tuzo za Kili za 2015 utazisikia bombani.

By MCHUNGUZI HURU (Associate Professor)

Basi la Timu ya Taifa, Taifa Stars Lapigwa Mawe na Mashabiki Wenye Hasira

$
0
0
Watu wasiojulikana wamelishambulia kwa mawe basi la timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars maeneo ya Kariakoo, jijini Dar es Salaam.

Basi hilo lililokuwa limebeba baadhi ya wachezaji wa timu hiyo waliokuwa wakitoka mazoezini uwanja wa Karume, lilishambuliwa kwa mawe na watu wanaosadikiwa kuwa mashabiki wenye hasira.
 
Taifa Stars juzi ilifungwa mabao 3-0 na Misri katika mechi yake ya kwanza ya Kundi G kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika 2017 mjini Alexandria.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images