Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live

Picture of the day-Cute or Not?


Kazi anayotaka kufanya mtoto wa kwanza wa Obama yajulikana yawashangaza wengi

$
0
0
Mtoto wa kwanza wa rais wa Marekani Malia Obama ’17’ ameanza harakati zake za kutaka kuwa mwigizaji na muongozaji a filamu.

Malia ameonekana huko Brooklyn na kundi la watayarishaji na waigizaji wa “Girls” hivi karibuni huku mashabiki wakifahamishwa kuwa hatacheza kwenye filamu hii ila ndio anajifunza mambo hayo.

Malia alionyesha kupenda kuwa mwigizaji na hata kuonekana kwenye tamthilia ya Halle Berry “Extant.”

David Silinde ATOA Siri ya Miswada ya Gesi na Mafuta Kuharakishwa Kupitishwa BUNGENI....Kumbe ni Shinikizo

$
0
0
Mbunge wa Kasulu mjini Moses Machali amesema kuwa yeye na wenzake wanawaachia kazi ya mapambano bungeni wabunge wa UKAWA waliobaki bungeni kuhahakikisha miswada mitatu ya gesi na mafuta haijadiliwi.

Mbunge wa Kasulu mjini Moses Machali amesema kuwa yeye na wenzake wanawaachia kazi ya mapambano bungeni wabunge wa UKAWA waliobaki bungeni kuhahakikisha miswada mitatu ya gesi na mafuta haijadiliwi.

Machali ametoa kauli hiyo katika mahojiano na EATV kufuatia adhabu aliyopewa yeye na wenzake watano ya kutohudhuria vikao vitano vya bunge kutokana na madai ya kuvunja kanuni kwa kumzuia spika kufanya kazi yake.

“Sisi tuliopewa adhabu ndiyo hatutakiwi zaidi, kwahiyo tunawaachia wenzetu wapigane”
Machali amesema hakubaliani na adhabu waliyopewa kwa kuwa utaratibu na kanuni hazikufuatwa wakati wa kusikilizwa

“Kanuni zinasema mtu anapoitwa kuhojiwa anatakiwa kuwa na wakili wake lakini sisi hatujapewa fursa ya kwenda na mawakili……. Mpaka muda huu (saa 3 usiku) hatujaamua nini cha kufanya”
Machali amesema haijawahi kutokea duniani kote miswada mitatu muhimu kama hiyo ikawasilishwa kwa wakati mmoja.
wabunge waliosimamishwa pamoja na Machali ni Pauline Gekul, Tundu Lissu, John Mnyika na Felix Mkosamali.

Ikumbukwe pia Waziri wa Nishati na madini alisema kuwa ni muhimu miswada hiyo ikapitishwa sasa ili kuwahi soko la gesi la dunia.
Katika hatua nyingine mbunge wa Mbozi Magharibi Davidi Silinde amesema seikali ina mpango wa kuwaburuza wabunge kwa kupitisha miswada muhimu kwa taifa kwa muda mfupi bila kuwapa fursa wabunge wausome.

Amesema mapendekezo ya kambi rasmi ya upinzani ni kwamba miswada hiyo iachwe hadi katika bunge la mwezi wa nne ili wananchi na wabunge wapate nafasi ya kuelewa kilichomo.
Silinde amesema kuwa kulazimishwa kwa miswada hiyo ni shinikizo kutoka nchini Marekani kupitia miradi ya MCC.

Chuchu nje nje: Huddah Apost Picha za Aibu Kwenye Instagram!

$
0
0
Huddah Monroe anafahamika kwa maisha yake controversial hivyo si jambo la ajabu kwa followers wake wa Instagram kumuona akila bata kwenye beach za Ulaya huku akiwa na nguo inayoonesha nipples zake! Jionee mwenyewe!


This is Zari Before Dating Diamond Paltnumz.. See Phtotos Here

$
0
0

Zari Hassan, a Ugandan socialite has never dissapointed the socialites’ family, if she needs the D, she goes for it. Here is the list of men who are alleged to have slept with socialite Zari according to evibe.ug in Pictures:


Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya July 4

$
0
0



























Habari  Zilizopo  Katika  Magazeti  ya  Leo  Jumamosi  ya  July 4

Ray C: Sitanii Niliposema natafuta Mwanaume wa Kunioa

$
0
0
Ray C amedai kuwa hafanyi utani kufuatia tangazo lake la kutafuta mume wa kumuoa.


  • “Hahaaha yaani leo nimeipata fresh, simu na msg ni nyingi sana wengi wanadhani natania!Niko serious jamani!endeleeni na maombi huwezi jua u could be the lucky one,” ameandika kwenye Instagram.



  • “Ila ishu ya kutumia simu moja kidogo imeleta tafrani so inaonyesha michepuko ni mingi kwenye ndoa ila najua nikimpata wangu tutarekebibishana kuhusu hilo najua tutaenda sawa tu.”
  • “Mpaka nimeshapata [maombi] mia tano leo tu kwahiyo naona muda si mrefu ntatangaza harusi ingawa wako kwenye mchujo,” amefafanua.

Jose Chameleone Aahidi Kumpiga Jeki Wema Kwenye Safari yake ya Kuwania Ubunge

$
0
0
Jose Chameleone yupo tayari kumsaidia Wema Sepetu kwenye harakati zake za kuwania nafasi ya ubunge wa viti maalum mkoani Singida.

Petit ambaye ni mmoja wa watu walio karibu na Wema amepost screeshot kwenye Instagram ya mazungumzo na Chameleone kwenye WhatsApp.

“S/O to my bro Jchameleone kwa kuonesha support pale inshallah atakapochukua mama form ya kugombea Ubunge Viti maalum.. Tutakuwa nae kwenye campaign mwanzo mwisho.. Thank u so much bro.. Lets support Wema Sepetu,” aliandika Petit kwenye picha hiyo chini:


Mwigizaji wa Bongo Movies Esha Buheti Akiri Kuchepuka Nje ya Ndoa

$
0
0
Mwigizaji Bongo, Esha Buheti, licha ya kuwa ndani ya ndoa, amekiri kuchepuka na mcheza mpira mmoja ambaye hakutaka kuweka wazi jina lake.

Akizungumza na na gazeti la Ijumaa, Esha aliweka wazi hisia zake kuwa kwa sasa ana kifaa kipya chenye hadhi na amekuwa akitupia picha zake mitandaoni kisha anazitoa.

“Najua wambeya watataka kumchunguza mpenzi wangu wa sasa ndiyo maana namuweka mtandaoni kisha nafuta harakaharaka,” alisema Esha.

Esha alifunguka kuwa, pamoja na ‘kidumu’ alichonacho bado yuko kwenye ndoa yake na anamheshimu mumewe aliyezaa naye mtoto mmoja.

Diamond Platnumz Asalimu Amri Kwa Baba Yake....Baada ya Kumchunia Kwa Muda Mrefu

$
0
0
ULE msemo usemao ‘wagombanao ndiyo wapatanao’ umetimia kwa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ baada ya kuwa na mgogoro kwa muda mrefu na baba yake, Abdul Jumaa ‘Baba D’ ambapo anadaiwa kusalimu amri na sasa wanaelewana, Risasi Jumamosi linakuwa la kwanza kukunyetishia.

TUJIUNGEA NA CHANZO

Chanzo makini ambacho ni rafiki wa karibu wa Baba D, mapema wiki hii kililieleza gazeti hili kwamba, kwa sasa Diamond amesalimu amri kwa baba yake kwani amekuwa akimsikiliza na kumsaidia pale anapokuwa na shida tofauti na ilivyokuwa awali.

“Angalau sasa Diamond anamsaidia baba yake kwani hata akimpigia simu anamsikiliza na anampa fedha ndogondogo za matumizi tofauti na zamani,” kilinyetisha chanzo hicho kwa sharti kuu moja tu la kutochorwa jina gazetini.


NYUMBANI KWA BABA D

Baada ya kupata ‘news’ hizo, gazeti hili lilimfungia safari baba Diamond hadi nyumbani kwake, Magomeni jijini Dar ambapo alikiri kwamba mwanaye Diamond kwa sasa anamsikiliza na hata akiwa na shida anamsaidia japokuwa bado anasumbuliwa na mguu na anahitaji matibabu ya kina zaidi kwani inatoa maji na kuvimba.

SHUKRANI KWA GLOBAL

“Nawashukuru hata ninyi Magazeti ya Global kwani mmechangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya mwanangu. Kwa sasa ananisadia hata nikimpigia simu ananisikiliza tofauti na zamani,” alisema baba Diamond.

BABA D ATOA NENO

Mzazi huyo wa staa wa Ngoma ya Nana alikwenda mbele zaidi na kumtaka mwanaye Diamond alete heshima kwa familia kwa kuoa kama ameamua kuwa na Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ambaye kwa sasa ana ujauzito wake.

Baba D alimtaka mwanaye huyo afunge ndoa na Zari kihalali kwani kila kunapokucha wanawake wazuri wanazaliwa, asije akaishia kuvishavisha wanawake pete za uchumba tu bila kuoa.

“Diamond amepata fedha akiwa kijana, ni bahati iliyoje hiyo! Anatakiwa sasa atulie na mwanamke mmoja kama amemchagua Zari basi wafunge ndoa halali maana baadhi ya wanaume huwa tuna tabia moja, kwamba, mwanamke akishazaa tunamuona mvuto wake umeisha.

“Hivyo, hata kwa Diamond inaweza kutokea baada ya Zari kujifungua, akamuona hivyo na akakutana na mwanamke mwingine mzuri ambaye hajazaa, akaamua kuwa naye tena na kumsahau huyo (Zari) lakini akiwa kwenye ndoa ni afadhali,” alisema baba Diamond.


AMKUMBUKA WEMA

Hata hivyo, katika mazungumzo hayo maalum, baba Diamond alimkumbuka aliyekuwa mpenzi wa mwanaye, Wema Sepetu kwamba ni mwanamke mzuri na anayefaa japokuwa mwanaye ameamua kuwa na Zari ambaye pia ni mzuri ila anamkumbuka sana Wema kwani ndiye aliyewahi kutambulishwa na akawa anamjali.

DIAMOND AENDELEA KUTISHA NIGERIA

Baada ya kusikia upande wa baba, gazeti hili lilimtafuta Diamond ili kuthibitisha ishu hiyo ambapo alijibu kwa kifupi kuwa yupo Nigeria akiendelea na kampeni ya kuomba kupigiwa kura kwenye Tuzo za MTV-Mama’s.

HUKO NYUMA

Diamond na baba yake walikuwa kwenye mgogoro wa muda mrefu ambapo mzazi huyo alikuwa akilalamika kwamba mwanaye huyo hakuwa akimjali na hata alipokuwa akijaribu kumpigia simu alikuwa hampi ushirikiano.
GPL

Hatuoni Sababu ya Kutokuchukua Ubingwa - SIMBA

$
0
0
Klabu ya Simba imesema hakuna sababu ya wao kushindwa kuchukua kombe la Ligi kuu Soka Tanzania Bara kutokana na kujiimarisha katika nafasi mbalimbali kwa kusajili wachezaji wenye viwango vya juu.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Afisa habari wa Simba Sc, Haji Manara amesema, wanavijana ambao msimu uliopita hawakuweza kufanya vizuri ambapo kwa msimu ujao watafanya vizuri kwasababu wameshajiandaa vya kutosha na wamekomaa ambao wataungana na wachezaji wazoefu ili kukiimarisha zaidi kikosi hicho.

Manara amesema, usajili wa safari hii umeiweka timu sawa kwa ajili ya kujiweka tayari kuchukua Ubingwa kwani wamejipanga kila eneo kwa ndani na nje ya Uwanja.
Kwa upande wa Usajili, Klabu hiyo imefanikiwa kumsajili Mganda Hamis Kiiza Diego mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuitumikia katika mechi za msimu ujao wa Ligi kuu Soka Tanzania Bara.

Pipi Adai yeye na Mume wake Hutumia Simu Moja

$
0
0
Muimbaji wa Bongo Flava, Pipi amedai kuwa yeye na mume wake hutumia simu moja.

Pipi alikuwa akiongea na kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM.

“Unajua kama mtu sio mwaminifu katika ndoa yako hiyo ndio itakuwa tabu na mtu akiamua kucheat anaweza hata bila simu japo watu wengine wanaona ni wivu lakini hiyo ni misingi ambayo tumejiwekea tokea tulivyoana,” alisema.

“Mimi na mume wangu tuna miaka kumi sasa hivi maana tokea tulivyokuwa hatujafunga ndoa hadi sasa hivi ni miaka kumi inafika. Mimi na mume wangu tuna misingi mizuri ya uaminifu, na wala hatuna mambo mengi kwa hiyo hatuna sababu ya kufichana, kwangu mimi naona ni kawaida tu hata yeye,” aliongeza.

Nyumba ya Jay Dee Kupigwa Mnada Baada ya Kushindwa Kulipa Deni la Mkopo

$
0
0
Baada ya Judith Wambura Habash kushindwa kulipa mkopo aliokopa,nyumba yake iliyopo Mivumoni,Kinondoni imewekwa sokoni kwa ajili ya kupigwa mnada.

Mtakumbuka kuwa sasa hata Bar yake ya M.O.G imefungwa muda sasa.

Tumuombee Anaconda maana anapita kwenye wakati mgumu sana sasa hivi

Chachu Ombara/ Jamii Forums

Jerry Muro, Kwa Kiingereza chako hiki, hakika umejidhalilisha na kuwatia aibu mno Walimu wako wote

$
0
0
Akiwa Anazungumza Kwa Madaha Katika Kituo Cha Magic FM Kipindi Katika Kipindi Chao Cha MICHEZO Huku Muda Mwingi Akitumia Kuiponda Simba Na Haswa Viongozi Wake Na Haswa Akimlenga Msemaji Mwenzie Haji Manara Kuwa Hajui Kuongea Kiingereza Na Ndiyo Maana Simba Haiendi Mbali Kusajili Wachezaji Anaowaita Yeye " Wa Kimataifa " Na Wanaishia Tu Kusajili Wachezaji Wa Nchi Za Karibu Wanaoongea Kiswahili ( Hapa Akimaanisha Wa Uganda, Kenya Na Burundi ).

Baada Ya Hapo Jerry Muro Nae Tena Mbele Ya Waandishi Wa Habari Akazungumza Kiingereza Hiki Nitakachokiandika Hapa Na Alichokuwa Anataka Kumaanisha Kisha Tutajua Je Ni Kweli Anajua Kiingereza au Ni Wale Wale? Halafu Hapo Hapo Anasema Kuwa Ana MASTER'S DEGREE Ya Public Administration Lakini Hatuambii Kasoma Lini, Wapi Na Kamaliza Lini Na Huku Akiwa Amesahau Kuwa Wapo Watu Wanaomjua A To Z au KINDAKINDAKI Kuliko Hata Anavyojijua Yeye ILA Tumeamua Tu Kumfichia Siri Kwa Kumuheshimu Kwakuwa Tu Ni Mwana Tasnia Mwenzetu.

Kiingereza Chake Ni Hiki kifuatacho Na Nitaomba Sana Kama Huna Background Nzuri Ya Kiingereza SANIFU Tusipotezeane Muda Kwa Kubishana Bali Nataka Watakaochangia Basi Wawe Kweli Ni Wazuri Ktk Communication Skills Na Matumizi Ya Lugha Yenyewe Ambayo Msemaji Wa Yanga Jerry Muro Anasema Anaijua Huku Akidai Viongozi Wa Simba Hawakijui.

Yanga Tuko Vizuri............Yeye Akasema............Yanga We Are Much Okey.
Yanga Tuko Tayari..........Yeye Akasema............Yanga We Are Arleady.

Wataalam Wa Lugha, Wajuvi Wa Kiingereza Cha Kuzungumza Na Kuandika Na Hata Wale Mliosoma Vizuri Sana Communication Skills Naombeni Mnisaidie Je Kusema " Yanga We Are Much Okey " Na " Yanga We Are Already " Ni Kiingereza Sahihi Na Ambacho Mtu Wa Caliber Ya POPOMA Jerry Murro Anaweza Kujivunia Nacho?

Na Namalizia Tu Kwa Kumkumbusha Jerry Muro Kuwa Msemaji Mwenzie Wa Simba Sports Club Haji Manara Ni Msomi ALIYETUKUKA Vizuri Tu Na Haishii Tu Kuongea Kiingereza Kizuri Lakini Kwa Faida Yake Na Wengine Msiojua Haji Manara Pia Ni Linguist Tena ALIYETUKUKA.
JF

Wife Kaniroga Nikienda nje Haisimami, Ndani inasimama, Help Pls

$
0
0
Nimekua na mgogoro mkubwa na wife wangu kwa Muda flani sasa, nisingependa kuutaja maana nilishautaja mgogoro huo hapa na tulishaufunga mjadala huo

Kutokana na huo mgogoro nikalazimika kutafuta farijiko pembeni, farijiko hilo ni staff mwenzangu kazini ambae alikua alikua historia ya mgogoro wangu

Mwanzo nilienda kujipumzisha tu kwa Muda ili kupata Muda Wa kupumua kuondoa stress lakini baadae nikanogewa nikawa nalala huko siku mbili hadi tatu ndo narudi home

Sijajua wife alitumia mbinu gani kumbaini mbaya wake, maana nilishangaa tu katia team kazini na kuanzisha varangati
Hata nyumbani kwa huo mchepuko sijui kapajuaje, nilistukia tu siku moja tumejipumzisha ndani akatia Tim pale na kuanzisha fujo akinitaka turudi nyumbani la sivyo pale pangegeuka Syria, ilikua ni aibu kubwa nikalazimika kutii na kuondoka nae

Tulipofika home nilikua na hasira sana nikamwambia hata afanyeje mm nitaendelea tu na yule mwanamke wangu apende asipende nae akanijibu kwamba tutaona nani mshindi, kwamba nikiendelea na huyo mwanamke nitaona kitachonipata

Kweli bana, nilikaa siku kadhaa bila kwenda, siku nilipoenda kwa mchepuko nikashangaa uume hausimami, tulijaribu kila namba lakini wapi
Kila siku tukawa tunajaribu bila mafanikio

Tulikua na siku nyingi hatujafanya mapenzi na wife kwa sababu ya ugomvi, cha kushangaza ghafla tu usiku akaanza kunitomasa na kunifanyia romance ya nguvu, huku akinibembeleza tudumishe ndoa yetu Mara tusimpe shetani nafasi sijui na blah blah nyingi hadi tukajuana bila shida

Kesho yake niliporudi kwa mchepuko haisimami tena, ndipo nikakumbuka ile kauli kwamba "" tutaona""
Tumejaribu na kujaribu na mchepuko wangu lakini wapi
Hadi umeenda sehem na kuambiwa ni wife wangu ndo amefanya vile so mtaalam kamwambia ni lazima niende nikatibiwe la sivyo nitakua sitembei na mwanamke mwingine yoyote yule zaidi ya wife na ikitokea tumeachana ndo balaa kabisa
Yaani ametengeneza dawa nisimamishe kwake tu

Lakini cha ajabu huyu mke wangu hujidai mtu Wa dini kwa kuimba mimba vijinyimbo vya kina rose mhando Muda wote

Wakuu mnanishaurije? Niende kwa huyo daktari Wa mchepuko wangu nikatibiwe?

Nimethibitisha kwamba ni mke wangu maana kawa mtu mwema sana kwangu tangu shida hii inipate, akifanya vyote tulivyokua tukifanya zamani mwanzo Wa ndoa

Nimetafuta binti mwingine kabisa ili nijaribishe ikawa vile vile niliporudi home mambo safi

Wakuu nahitaji msaada Wa haraka pls

Ugomvi wangu na wife uliotufikisha hapa hatukawahi kuumaliza na nilimtimua kurudi kwao ndipo akarudi kwa kufosi ndipo nikatafuta demu pembeni

Help pls

Kama Lowassa ni Fisadi, Rais Kikwete tamka Hadharani

$
0
0
Kama Lowassa ni fisadi na mwizi wa mali za watanzania.

Mwenyekiti wa CCM JK simama hadharani na utamke wazi wazi la sivyo tunaposema CCM ni chama cha mafisadi kwa miaka yote msipingane na Sisi.

Au La na mwenyekiti wa CCM utakuwa upo kwenye cheni moja na EL
Mnaogopa nini kumtaja kama ni fisadi?

Na kwanini mtumie vijana wa ngazi za chini kama Makonda na Nape kwenye chama chenu kumwandama na nyie mkiwa kimya?

Tunaitaji matamko ya
1.Mwenyekiti wa CCM
2.Makamu mwenyekiti CCM
3.Katibu Mkuu CCM

Sio Mavuvuzela wa chama,la sivyo nyote ni mafisadi na wezi tu mnaooneana aibu kwa kuzidiana ufisidi.

Siri ya Mbuzi wa Kinondoni Makaburini...Je ni Kweli ni wa Kichawi ?

$
0
0
Kumekuwa na "story" nyingi juu ya mbuzi wanaolala maeneo ya Kinondoni makaburini,na wakati wa mchana kuzunguka huku na kule kuanzia Kinondoni muslim,studio,mpaka maeneo ya Biafra na Morrocco(?),hawa ni mbuzi wasio na mchungaji wala "mmiliki",huzunguka hapa na pale ktk kujitafutia malisho ktk majalala na maeneo ya makazi ya watu.

Wenyeji wengi wa Kinondoni wanasema mbuzi hao walianza kuonekana mmoja mmoja lkn sasa wamekuwa wengi na kuzunguka wakiwa ktk kundi.Hawachinjiki wala kukamatika,wengine huwahusisha na "masalia" ya mbuzi wa "kafara" ambapo watu wengi wanaoamini juu ya kafara huja nyakati za usiku ktk maeneo ya makaburi na kutoa kafara au kuwaacha kama njia ya kutawanya "mikosi" na "mabalaa".

Zipo habari za kikundi cha mateja kujikusanya na kuwakamata hao mbuzi na kuwauza kwa wapika supu,kitu kilichopelekea mateja wengi kupukutika kwa kifo na magonjwa ya hatari,na wale wanunuzi kupata mauzauza ya ajabu..kiasi mpaka sasa,licha ya njaa za mateja,lkn huwezi kukuta teja anawakamata na kuwauza.

Mbuzi Hawa Wanaitwa gusa unate...Je kwa wajuzi na wajanja wa Kinondoni,kuna ukweli gani juu ya mbuzi hawa??ni nani kweli mmliki wa hii mifugo?

Vurugu zimetokea leo Zanzibar baada ya Wanachama wawili wa CUF kupigwa risasi na watu waliofunika Nyuso zao

$
0
0
Hali ya hatari imetanda katika wingu la Zanzibar mchana huu kufuatia Wanachama wawili wa CUF (majina yao bado hayajafahamika) kupigwa risasi na watu waliofunika nyuso zao kwenye kituo cha kuandikishia wapiga kura Makunduchi.

Waathirika wamewahishwa hospitali ya Arahma kuwahi matibabu ya haraka.

Taarifa zaidi zaja...

'Bao la Mkono' latua Tume ya Uchunguzi.....Mdomo wa Mponza NAPE na Kusababisha Vikao vya NEC kusimamishwa

$
0
0
Wakizungumza kwenye mkutano kati ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na viongozi wa vyama vya siasa kuhusu maadili ya Uchaguzi jana, baadhi ya viongozi hao walitaka mkutano huo usitishwe hadi pale CCM itakapomuonya Nape Wakizungumza kwenye mkutano kati ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na viongozi wa vyama vya siasa kuhusu maadili ya Uchaguzi jana, baadhi ya viongozi hao walitaka mkutano huo usitishwe hadi pale CCM itakapomuonya Nape

Dar es Salaam. Kauli ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye bado inawaumiza vichwa wapinzani nchini baada ya viongozi hao jana kuitamkia wazi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), kuwa hakuna haja ya kujadili maadili wakati CCM tayari kimesema ‘kitafunga bao la mkono.’ Wakizungumza kwenye mkutano kati ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na viongozi wa vyama vya siasa kuhusu maadili ya Uchaguzi jana, baadhi ya viongozi hao walitaka mkutano huo usitishwe hadi pale CCM itakapomuonya Nape.

Wa kwanza kuibua mada kuhusu Nape, ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha NLD, Dk Emmanuel Makaidi ambaye alisema hakuna haja ya kuendelea na mkutano huo hadi NEC, Msajili wa Vyama vya Siasa na IGP wakemee kauli hiyo. “Hivi tutayazungumziaje maadili, mbona CCM kimeshaonyesha kuwa hakitafuata maadili, kuna haja gani ya kuzungumzia wakati wameshasema watafunga hata kwa goli la mkono?” alisema Dk Makaidi. Awali akiwa katika ziara ya Kinana wilayani ya Sengerema, Nape alikaririwa akisema kuwa ana uhakika CCM itashinda baada ya kuona mwitikio mkubwa wa Watanzania katika ziara hizo. “Rangi inayoenda Ikulu ni hii (anaonyesha shati lake la kijani ambayo hutumiwa na chama hicho).

Tuna uhakika na ushindi wa Rais. Kwa namna yoyote ile, CCM itarudi Ikulu hata kama ni kwa bao la mkono… bao ni bao tu ili mradi refa hajaona,” alisema Nape. Hata hivyo, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva aliwatoa wasiwasi wanasiasa hao akiwaambia kuwa Nec itafanya uchaguzi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu na hivyo kauli ya Nape haiwahusu. “Maadili tunayoyatengeneza yataanza kutumika kuanzia Agosti 22, wakati wa kampeni, lakini iwapo kuna vurugu zinatokea baina ya vyama sisi wala Nec hatuhusiki,” alisema. Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa akichangia kipengele cha wahusika wa maadili aliitaka Nec kuliweka Jeshi la Polisi kupitia IGP kusaini na kuwa mhusika katika masuala ya maadili ya uchaguzi.

 Hiki kipengele cha 1.3 kinawataja wahusika wa maadili kuwa ni vyama vya siasa, wagombea, Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Nec pekee. “Kutokana na uzoefu tulionao katka chaguzi zilizopita, Jeshi la polisi ni washiriki wakubwa katika masuala ya uchaguzi, kama jeshi hilo halitasaini maadili hayo basi kutakuwa na matatizo makubwa katika uchaguzi huo,” alisema. Awali akifungua mkutano huo Jaji Lubuva alivitaka vyama vya siasa kufuata maadili, sheria na kanuni za uchaguzi, na katika kipindi chote cha kuanza kwa kampeni hadi siku ya uchaguzi. Chanzo:
 Mwananchi

Wabunge wengine 35 nao wamepigwa stop kuingia Bungeni kwa siku tano kuanzia leo July 4 2015

$
0
0
Kumekuwa na story nyingi tofauti toka ndani ya Kikao cha Bunge Dodoma, kwa muda wa siku tatu mfululizo zimetokea vurugu, Kikao kikaahirishwa kwa siku mbili mfululizo.

Alhamisi July 02 2015 Mbunge John Mnyika aliomba mwongozo kuomba Bunge lisiendelee kwa vile ishu ya kujadili Miswada mitatu kwa siku moja ilikuwa inakiuka Kanuni za Bunge, ukatokea mvutano na baadae Spika AnneMakinda akaahirisha Bunge.


Ijumaa July 03 2015 hali ikawa hivyohivyo tena, wakati Waziri George Simbachawene anasoma Muswada, ikatokea mvutano mwingine, zikaanzishwa kelele Bunge likaahirisha tena.. Kikao cha Jioni Spika Anne Makinda akarudi na list ya majina ya Wabunge ambao wamesimamishwa Bungeni kutokana na maamuzi ya Kamati ya Maadili ya Bunge.


Leo July 04 2015 Kikao kimeanza tena saa tatu asubuhi, Mbunge Ezekiel Wenje akaomba Spika atoe ufafanuzi wa kwanini Mbunge Silinde hayuko kwenye list ya waliotajwa kusimamishwa lakini Askari wa Bunge wamemzuia asiingie kwenye Kikao?

Majibu ya Spika hayakuwaridhisha baadhi ya Wabunge, zikaanza tena kelele… Spika akataja list ya Wabunge wengine ambao wanasimamishwa kuhudhuria Vikao vya Bunge kwa siku tano kila mmoja.

List ya Wabunge wote iko hapa.

Ezekiel Wenje

Mussa Kombo

Masoud Abdallah Salim

Rebecca Ngodo

Sabrina Sungura

Khatib Said Haji

Dr. Anthony Mbassa

Maulidah Anna Valerian Komu

Kulikoyela Kahigi

Cecilia Pareso

Joyce Mukya

Mariam Msabaha

Grace Kiwelu

Israel Natse

 Mustapha Akonaay

Konchesta Rwamlaza

Suleiman Bungura

Rashid Ali Abdallah

Ali Hamad

Riziki Juma

Rukia Kassim Ahmed

Azza Hamad

Khatibu Said Haji

Kombo Khamis Kombo

Ali Khamis Seif

Haroub Mohammed Shamisi

Kuruthum Jumanne

Mchuchuli

Amina Mwidau

Mkiwa Kimwanga

Salum Baruhani

Marry Stellah Malaki

Rashid Ally Omary

Mwanamrisho Abama

Lucy Owenya
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live




Latest Images