Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Florah Mvungi Amkataza H:Baba Kucheza Mpira...Adai Atakosa Haki yake ya Msingi Kama Mke

$
0
0
Mwigizaji wa filamu za Kibongo,Frolah Mvungi amemkataza mume wake,msanii wa Bongo Fleva,H: Baba kucheza mpira.

H: Baba amesajiliwa na klabu ya Toto African ya jijini Mwanza hali inayomfanya kuwa mbali na familia yake ambayo ipo jijini Dar,na ndiyo sababu kubwa iliyotajwa kukatazwa na mkewe kuichezea timu hiyo.

Kwa mujibu wa msanii huyo alisema kuwa mkewe alikaa kikao na ndugu zake waliopo jijini Mwanza kuzungumzia suala hilo kama atakubali abaki kucheza mpira atacheza lakini akibaki na msimamo wake basi ataacha kucheza na kurudi Dar.

‘’Unajua wife anacholalamika kuwa nitakuwa mbali na familia kwahiyo atakosa haki yake ya msingi kama mke,’alisema H: Baba.

Picha: Wema Sepetu na Steve Nyerere Wakiwa Ikulu ya Dodoma na Rais Kikwete

$
0
0
Hizi ni baadhi ya picha za mastaa wabongo movies, Wema Sepetu na Steve Nyerere zilizo trend siku ya leo kwenye mtandao wa instagram wakiwa na Rais Kitwete Ikulu ndogo, Dodoma.

“Wakati nyie mnaongea upuuzi… Yangu yaninyookea….. Alhamdulillah… Wa moja havai mbili… Abadan asilan…. Earlier today… Ikulu… Dodoma… Thank u Mr.President”-Wema aliandika hayo kwenye moja ya picha hizo.

Kwa maneno hayo, inawezekana mastaa hawa wakawa wamepata shavu kutoka kwa Rais.

Nisha Akana Kukamatwa na Madawa ya Kulevya

$
0
0
Msanii wa tasnia ya Bongo movie nchini Salama Jabu alimaarufu kama Nisha ameibuka na kuwatoa hofu watanzania pamoja na mashabiki wake kuwa hajakamatwa na madawa ya kulevya kama ambavyo taarifa zinavyosambaza katika mitandano ya kijamii.

Nisha kwa sasa yupo nchini China amekanusha taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram baaada ya kuona akiulizwa sana na kupewa pole na watu wake wa karibu. Nisha amesema huwa si kawaida yake kujibu au kutolea ufafanuzi mambo ambayo huwa ni uzushi lakini kutokana na uzito wa uzushi huu wa kukamatwa na madawa ya kulevya ilibidi atoe ufafanuzi huu.


"Naomba leo niweke wazi hili suala lililoandikwa na kusambaa kuwa nimekamatwa China na madawa, huwa napenda kupuuzia vitu ila wacha niongee leo ili nisiwape watu presha na maswali mengi na kuwaweka njia panda, mimi sijakamatwa, sijawahi kukamatwa na wala sitaweza kukamatwa kwa ajili ya ujinga kama huo wa madawa ya kulevya kwanza siyapendi lakini pili hata niwe masikini vipi siwezi kujiingiza kwenye janga hilo," alisema Nisha.


Mbali na hilo Nisha ameeleza jambo ambalo limemtokea alipofika nchini China katika uwanja wa ndege na kusema kuwa kutokana na nchini za Afrika hususani Nigeria na Tanzania kuhusishwa sana na biashara za madawa ya kulevya hivyo kumekuwa na ulinzi mkali jambo ambalo lilimfanya akagulie kwa zaidi ya saa tatu.

"Kilichotokea ni hiki kutokana na Watanzania kuharibu sana na scandals za kukamatwa na madawa ya kulevya, (wengi mnalijua hilo) ukiwa unavuka border ukionekana tu passport yako ni ya Tanzania basi unasachiwa sana. Ni kweli walinisachi kwa zaidi ya masaa matatu. Hilo kwa Watanzania wanaovuka kwenda Hong Kong nadhani mmenielewa, si mimi tu yoyote Mtanzania au Wanigeria au taifa lolote lenye historia ya nchi yao kukamatwa na unga lazima shughuli ikupate lakini hawajanikuta na kitu I'm ok," aliongeza Nisha.

Nisha amewataka baadhi ya waandishi wa mitandao ya kijamii zikiwepo website pamoja na blogs mbalimbali kuwa na uhakika na taarifa mbalimbali wanazoziweka ili kuepusha kusambaza uzushi ambao unaweza kuleta mshtuko kwa watu wengine na kusababisha matatizo.

EATV.TV

Dk Slaa Aikana Account ya Twitter Inayomzushia mazito Kuhusu yeye na Chadema Kumkubali Lowassa

$
0
0
Wakati kukiwa na taarifa zinazosambaa mtandaoni zikimuhusisha Dk Willibrod Slaa na akaunti ambayo imekuwa ikitoa msimamo wake wa kujitenga na shughuli za siasa pamoja na Ukawa, katibu huyo mkuu wa Chadema amekanusha taarifa hizo akisema hajawahi kuwa na akaunti ya twitter.

Dk Slaa, aliyekuwa anatajwa kuwa mgombea urais wa Chadema, hajaonekana hadharani katika matukio makubwa ya kichama tangu Chadema na Ukawa walipomkaribisha waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa na kumteua kuwa mgombea urais anayeungwa mkono na vyama vinne vinavyounda umoja huo.

Mara ya mwisho kuonekana kwenye shughuli za chama hicho ni katika kikao cha Kamati Kuu wakati Lowassa alikaribishwa kufanya majadiliano na kujibu hoja za wajumbe.

Lakini baada ya hapo Dk Slaa hakuonekana wakati wa kutambulishwa kwa Lowassa kwa waandishi wa habari, tukio la kuchukua na kurudisha fomu za urais ndani ya chama na tukio la juzi la kuchukua fomu za urais kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Wakati hayo yakiendelea, kuna akaunti ya twitter yenye jina la “Dr Willibrord Slaa” ambayo imekuwa ikitoa kauli mfululizo zikiwa na ujumbe mbalimbali unaoendana na mazingira aliyomo sasa mwanasiasa huyo.

 Agosti 10, kulitumwa ujumbe zaidi mara 10, mmojawapo ukijaribu kuwaaminisha watu kuwa hiyo ni akaunti halisi ya Dk Slaa.

“Ndugu zangu Watanzania, hii ni akaunti yangu rasmi, bila shaka yoyote na naomba ninachoandika hapa kifikishwe kwa Watanzania popote walipo,” unasema ujumbe huo.

Taarifa nyingine zilizotumwa kwenye akaunti hiyo ya twitter ni pamoja na ile iliyoeleza kuwa   Dk Slaa ameomba ulinzi kutoka nchi na mashirika ya kimataifa na atazungumza kupitia runinga na redio pindi atakapopata ulinzi.

Akizungumzia sakata  hili jana, Dk Slaa alisema hajawahi kutuma taarifa yoyote kwenye mitandao ya kijamii.

“Sijawahi ku-operate (kuendesha) kitu chochote kwenye akaunti ya twitter, sina akaunti kama hiyo,” alisema Dk Slaa.

Mbali na kukanusha kumiliki na kuendesha akaunti hiyo, Dk Slaa alirudia kauli yake ya wiki iliyopita kuwa atatoa msimamo wake muda muafaka utakapofika, baada ya kuulizwa swali kuhusu hatma yake ndani ya Chadema na kisiasa kwa ujumla.

“Subira yavuta heri, sasa ili uipate hiyo heri unatakiwa kuvumilia. Kwa hiyo wakati ukifika nitazungumza tu na Watanzania,” alisema.

Alipoulizwa ni wapi alipo kwa sasa, alisema yupo Dar es Salaam anapumzika, lakini akasisitiza kuwa ipo siku ataweka wazi mustakabali wake kisiasa.

Dk Slaa alisema yeye na mke wake Josephine Mushumbusi wanatarajia kusafiri kwenda nje ya nchi katika siku chache zijazo, ingawa hakuweka wazi nchi anayotarajia kuitembelea, lakini akasema atarejea baada ya wiki moja.

Diamond Asema Alilipwa Shilingi Milioni 100 ili Kutumbuiza Jukwaa Moja na Alikiba Katika Show ya ‘Kiboko Yao’

$
0
0
Mashabiki wengi wa muziki wa Bongo wanatamani siku moja kuwaona Diamond na Alikiba wanafanya kazi pamoja, kama ambavyo Wizkid na Davido ambao wameahidi kuachia joint yao siku si nyingi baada ya kuthibitisha kuwa hakuna beef kati yao.

Upande wa Diamond amesema kuwa yupo tayari kufanya chochote katika muziki endapo kina maslahi kwake. Kuthibitisha hilo ametoa mfano kuwa alikubali kushiriki tamasha la ‘Kiboko Yao’ lililofanyika Leaders Club mapema mwaka huu ambalo na Alikiba pia alitumbuiza, kwasababu lilikuwa na maslahi mazuri kwake.

“Unajua mi nafanya biashara, na kitu chochote ambacho kwangu mi kinakuwa kina maslahi mi siwezi kukataa kukifanya.” Diamond ameaimbia 255 ya XXL ya Clouds Fm.

Baba Tiffah ameongeza kuwa alilipwa shilingi milioni 100 ili kutumbuiza kwenye tamasha hilo.

Nakupa mfano hapa katikati kulikuwa na show ilivyokuja mi nikawaambia hii show ni biashara kwangu mi sikatai lakini you have to pay me, show mi nimelipwa milioni 100 ndo nimetumbuiza, siamini kama kuna msanii wa kiTanzania alishawahi kulipwa milioni 100, hili swala si umetengeneza kama beef, tuifanye kibiashara, nikalipwa milioni 100, nisiwe mnafiki milioni 100 sababu show hizo natozaga nikiwa na show nje labda Kenya , Rwanda naweza nikapiga show milioni 120, 130 lakini ilikuwa mara ya kwanza Tanzania milioni 100, lakini kwasababu ilikuwa beef na sio kwamba show haikulipa, ililipa kwasababu ilikuwa imeshatengeneza tension yaani flani na flani kwahiyo tuzitumie hizi vitu kimaslahi zaidi.

Kwa Mara ya Kwanza Serekali Yasifia Maandamano ya Chadema, Yadai Maandamono ya LOWASSA Yalikuwa ya Amani

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe amesema wamefurahishwa na amani iliyotawala wakati wa maandamano ya kumsindikiza mgombea wa urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Edward Lowassa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuchukua fomu juzi.

Waziri Chikawe alisema jana kuwa alishuhudia umati mkubwa wa watu wakiimba na kucheza katika hali ya amani na hilo ni jambo zuri linalopasa kuendelea wakati wote.

Alisema anatarajia hali hiyo itaendelea hata mikoani mgombea huyo akienda.

“Tumefurahi, kulikuwa na amani ya kutosha, watu walikuwa wengi zaidi ya ilivyokuwa kwa CCM,” alisema Waziri Chikawe.

Waziri Chikawe alikiri maandamano hayo kusimamisha shughuli katika baadhi ya maeneo ikiwamo ofisi yake ambayo haikupokea wageni kwa saa kadhaa.

Wakati huohuo, Chikawe alionya: “Tunaomba wanasiasa na mashabiki wao wasitembee na silaha kwenye mikutano yao, waziache mahali salama nyumbani na pia wawaache polisi wafanye kazi yao ya kuwalinda wote.”

Waziri Chikawe alisema mabomu ya machozi yanayotumika kazi yake siyo kuua au kuumiza watu bali kuzuia wasifanye vurugu.

Hata hivyo, Waziri Chikawe alisisistiza ushiriki wa viongozi wa vyama vya siasa ni muhimu katika kufanikisha hilo.

Alisema wanasiasa wanapaswa kujiheshimu kwa kukwepa kampeni za uchochezi na kauli zinazoweza kusababisha fujo.

Zari: Ujauzito Ujao na Mimi Nitapiga Picha za Utupu Kama Kim Kardashian

$
0
0
Selfie ya utupu aliyoshare Kim Kardashian kwenye akaunti yake ya Instagram ili kuwajibu waliodhani anafake ujauzito (Ingia hapa), imempa ‘wazo’ Zari The Boss Lady a.k.a mama Tiffah la kufanya hako kamchezo atakapopata ujauzito mwingine na Diamond.

Kupitia Instagram Zari alishare picha ya utupu aliyopost Kim Kardashian na kuandika “mlisema nilikuwa mtupu kwenye photoshoot ya tumbo la ujauzito???? Hivi ndivyo picha ya utupu inavyokuwa”. Aliongeza “wakati ujao na mimi nitapiga za utupu”. Aliongeza kuwa Diamond ameanza kufikiria kupata naye mtoto wa pili.

Wooooooiiiii did I hear that I was naked in my baby bump photoshoot???? Well well well, this is what naked looks like. Smh!!!! Way to go Kimmy next time am stripping too….. Baba T is thinking about a lil brother already”– Aliandika Zari.

Mgombea Urais John Magufuli Amesema Akishinda Urais Atagawa Kompyuta kwa Kila Mwalimu Nchi Nzima

$
0
0
Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, John Magufuli amesema akishinda Urais atagawa Kompyuta mpakato(Laptop) kwa kila mwalimu nchi nzima. Amesema atachukua hatua hiyo ili kuinua kiwango cha Elimu Nchini. Pia ahaidi Mil. 50 kila Kijiji kukuza Uchumi akishinda Urais. Source: Raia mwema

Nini maoni yako hapo

XXL ya Clouds FM yawapatanisha Q Chillah na TID, ‘no beef’ tena… Full interview iko hapa.. (Audio)

$
0
0
Inawezekana hukua unaamini kuwa kuna siku  jamaa hawa wawili ambao walikua wakiwakilisha ‘Top Band‘, Q Chief na TID wasingeweza kukaa pamoja na kumaliza tofauti zao na hii imetokana na kuingia kwenye headlines sehemu mbalimbali kuwa hawako sawa, taarifa ikufikie kuwa TID na Q Chief kwa sasa wako fresh na wanarudi pamoja kimuziki tena.

chiiiKwenye interview ya kukumbuka album zilizopita kwenye XXL ya Clouds FM August 13 waliwaita Q Chief na TID, yamezungumzwa mengi sana kwenye interview hii ikiwemo album nyingine itakayotoka itakayowaunganisha Q Chief na TID, Nimekurekodia interview yote mtu wangu.

Bonyeza play kusikiliza interview yote.

Polisi Wazuia Msafara wa LOWASSA Kushiriki Mazishi ya Mzee Kisumo

$
0
0
Polisi  wakiwa  tayari  kwa  lolote  baada  ya  kuzuia  msafara  wa  LOWASSA
Polisi mjini Mwanga, mkoani Kilimanjaro umezuia msafara wa mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa uliokuwa unaelekea Usangi kuhudhuria mazishi ya kada wa CCM, Peter Kisumo.

Vyanzo vya kuaminika toka mjini Mwanga vinasema, polisi walizuia msafara huo kutokana na kujumuisha idadi kubwa ya magari ya viongozi waandamizi wa Ukawa na wabunge wanaounda umoja huo jambo ambalo polisi hawakuafiki.

Taarifa zinasema, tukio hilo lililotokea katikati ya Mwanga na Usangi lilizusha mjadala wa zaidi ya dakika 30, polisi wakitaka Lowassa aende mazishini peke yake huku magari mengine yaliyoambatana naye yarejee yalikotoka jambo ambalo halikuafikiwa na mwanasiasa huyo.

Baada ya polisi kusisitiza kutoruhusu msafara mzima uende mazishini mgombea huyo aliamua yeye na maofisa wengine alioambatana nao kurudi Mwanga akisisitiza asingeweza kwenda peke yake akiwaacha watu aliambatana nao.


Mabalozi Mia Moja wa CCM Monduli, Wahamia CHADEMA

$
0
0
Mabalozi wa mashina miamoja na kumi wa CCM mwenyekiti katibu kata wajumbe wa kamati ya siasa ya kata pamoja na wenyeviti wa mitaa minne katika kata ya Monduli mjini mkoa Arusha wamehama CCM na kuhamia Chadema.

Tukio ilo limetokea Monduli mjini leo majira ya saa sita mchana wakati viongozi hao walipo kusanyika na kutoa kauli ya kuhama CCM na kuhamia Chadema huku wakieleza sababu zinazo wafanya kufikia maamuzi hayo.

Kwa upande wao wenyeviti wa serikali za mitaa wajumbe wa nyumba kumi na katibu wa CCM kata ya Monduli Anna Erinest wameitaka jamii itambue kuwa hayo ni maamuzi yao binafsi na hayahusiki na shinikizo la mtu yoyote kama inavyo daiwa na baadhi ya watu kila wanaohama udaiwa wameshinikizwa.

Siwezi Kumsamehe Mke Wangu, Ametembea na Mkurugenzi wa Ofisini Kwake

$
0
0
Baada ya kupoteza kazi yangu niliyumba sana, niliwaza nitaishije bila kazi hapa mjini, hata hivyo nilijipa moyo kwamba kwa kuwa wife ana kazi Basi mambo madogo madogo hayatasumbua wakati huo nami nitakua nakazana kutafuta kazi nyingine.

Kumbe nilikua nimekosea kuwaza hivyo, ilianza taratibu kama mzaha wife kuchelewa kurudi na kuja kuanzia saa tano usiku na kuendelea kwamba wamelazimika kufanya overtime.

Baada ya wiki kadhaa visingizio vikaisha akawa hana cha kusingizia tena, anakuja usiku ule ule mwingi bila kunisemesha chochote na kupitiliza chumbani kulala moja kwa moja bila kula wala kuoga.

Nikajiuliza, kwa biologia ya wanawake ilivyo na joto la Dar inawezekana wife akarudi na kulala tu bila kuoga? Na chakula je ina maana analala na njaa? Nikasema nitapata tu majibu ya maswali Haya, only time will tell.

Hadi napoteza kazi yangu sikua namiliki Gari wala wife hakua nalo, baada ya hizi harakati za kurudi usiku mwingi na kutoshinda home weekend nzima hatimaye wife """"" akanunua Gari""""" Toyota IST.

Nilikua naumia rohoni kwa suspicion but sikujua where and how to start investigation on that particular matter hadi siku moja tulienda pamoja na wife kwenye Gari lake na mdogo wake wa kike aliyekuja toka Jana yake.

Mimi niliomba nikae nyuma wao mbele, kabla hatujaondoka nashangaa kuiona chupi ya wife bikini pembeni ya miguu yangu ndani ya Gari, kwa kifupi ile safari ilikufa.

Nilimtoa ndani ya Gari kwa kipigo kikali sana nikitaka kujua kulikoni hiyo chupi kuwepo humo, hakawa hana cha kujitetea, nikamfungua chumbani na nikachukua simu zake zote nikawa nazo sebuleni, tangu kufunga ndoa sikuwahi kumpiga zaidi ya siku hiyo.

Hapo sebuleni nilipitia meseji zote kwenye simu zake, baada ya zoezi hilo nililidhika beyond reasonable doubt my wife was seeing someone else.

Na mtu huyo alikua ni mkurugenzi wake kazini, na hiyo kampuni anayofanya wife ni ya huyo bosi, nikamfungulia saa tatu usiku na kumpa simu zake nikaendelea na mambo mengine.

Sikupata usingizi siku hiyo, nilikaa kwenye TV nikibadilisha Chanel mbali mbali, saa nane usiku alinifuata sebuleni na kupiga magoti akaniomba msamaha kwa machozi kwamba hatorudia, haelewi kwa nini alifanya vile, sikumjibu nikamwambia arudi alale.

Nika conclude kwamba sina mke, nikaazimia kwamba nisilete fujo, kwa hali niliyonayo nijifanye ---- tu huku moyoni nikijua sina mke, halaf niendelee ku fight nikifanikiwa niachane nae niendelee na maisha yangu.

Wife ali pretend kwamba ametubu na ameachana na yule jamaa, lakini kwa siri aliendelea nae, hakujua kama mimi najua yule mpenzi wake ndie bosi wake kazini, alikua amenidanganya kwamba ni mteja wa kampuni yao na kwamba hawaonani tena.

Kunipumbaza, kwa mara ya kwanza, ilikua ni Ijumaa, akaja na bahasha akanipa ilikua na million mbili za elfu kumi kumi, kaniambia amepata kazini baada ya kufanya deal, nikazipokea nikaziweka benki, Ili kuni fool kila siku mbili tatu au wiki alikua ananiletea pesa, laki tano na kuendelea nami nikawa natunza pesa nikikusanya mtaji.

Nikaanza kufanya shughuli zangu za kibiashara, kidogo kidogo mambo yangu yamekua mazuri kwa pesa hizo hizo za uzinzi wa wife, yeye kwa kipindi chote anaamini kwamba amenifanya ----, akienda kulala kwa hotels na huyo jama, wakati mwingine akiaga anakwenda safari kikazi kumbe yupo humu humu Dar, nami nikajifanya mjinga nikajiimarisha.

Kila jambo lina mwanzo na mwisho, mkurugenzi kapata msichana mpya kazini inaonekana mke wangu katemwa, yupo tu nyumbani namuacha hapo asubuhi naenda kwa business zangu narudi jioni, nikimuuliza kulikoni analia tu, yupo frustrated, ndipo nikapata chanzo kikanieleza yaliyotokea huko kazini kwao, mapenzi na bosi yamefikia mwisho.

Nimeishi kwa mateso rohoni kwa miaka 4, huku nikificha hasira yangu, nikishiriki tendo la ndoa, ili kumhadaa huyu mzinzi bila yeye kujua, sikuwahi kupata wazo la kufumania kwa kua nilikua nitaharibu mpango wangu.

Wiki hii najiandaa kuhamia kwangu ingawa ni vyumba viwili na sitting room but it is my home, naenda kuanza upya
Nasamehe mtoto pia, nitapata mwingine, kwanza sina imani kama ni wangu, nitaondoka na begi tu.

Yote Tisa, kumi nimepona rohoni, nasikia amani sana.

Kusamehe ni msamiati kwangu kwa sasa, hatua hii niliipanga miaka minne nyuma.

Ama kweli poteza kazi ndo utajua sura halisi ya mkeo

  By Jean pierre oberoi

Majina Rasmi ya Wagombea Ubunge CCM 2015 Yatajwa-Anna Tibaijuka na Job Ndugai Ndani

$
0
0
Majina ya walioteuliwa kugombea ubunge wa majimbo na uwakilishi wa viti maalum kupitia CCM katika majimbo yote Tanzania yametoka rasmi , yupo Iddi Azzan anagombea Jimbo la Kinondoni, Prof. Anna Tibaijuka anagombea jimbo la Muleba Kusini.
Nape Nnauye anagombea jimbo la Mtama., Nimrod Mkono anagombea jimbo la Butiama, Ndugu Ridhiwani Kikwete anagombea Chalinze na Job Ndugai ameteuliwa kugombea Kongwa.

Kujua wote walioteuliwa kuwakilisha majimbo na viti maalum Bonyeza Link Hii Hapa chini:





Attachment: 

Benard Membe Afunguka Kwa Mara ya Kwanza Baada ya Kuanguka Mbio za Urais- CCM

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amefunguka kwa mara ya kwanza  na kuweka wazi kilichotokea mjini Dodoma na kusababisha ashindwe katika uteuzi wa kuwania urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Membe amekuwa kada wa tatu kueleza hadharani jinsi uteuzi huo ulivyoendeshwa ambao Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, aliibuka kidedea kati ya makada 42 waliojitokeza kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa.

Makada wengine waliojitokeza hadharani kuelezea mchakato huo ni Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Mark Mwandosya, ambao kwa nyakati tofauti walieleza sababu mbalimbali zilizosababisha kushindwa kwao.

Membe akizungumza jijini Dar es Salaam jana katika kongamano la pili la Watanzania waishio ughaibuni (Diaspora), alisema mchakato huo ulikuwa ni sawa na timu mbili za mpira wa miguu zilizokuwa zinapambana uwanjani.

Alisema unaweza ukapata timu nzuri sana ya mpira kwenye ligi na ikashinda michezo yote bila kufungwa goli hata moja.

Aliongeza kuwa lakini mwishoni timu hiyo inapotoka sare na timu nyingine ambayo ni dhaifu kwenye fainali, timu hizo zinakwenda kwenye penalti kwa kuwa mshindi lazima apatikane.

Membe alieleza kuwa wakati wa upigaji penalti timu hiyo ambayo ilitarajiwa kuibuka na ushindi kwa kuwa ilicheza mpira safi ikafungwa penalti zote tano na hiyo timu ambayo haikutegemewa ikashinda mabao yote.

Alisema kuwa kwenye ‘football jargon’ kitendo hicho cha timu iliyocheza mpira vizuri na kudhaniwa ingeibuka na ushindi, lakini ikashindwa kwenye penalti, timu hiyo imekufa kifo cha ghafla.

Membe aliendelea kueleza kuwa timu hiyo itakuwa imepigwa kifo cha ghafla na kueleza kuwa inapopigwa kifo cha namna hiyo timu hiyo haiwezi kutegemewa isimame na ielezee kilichotokea.

“Naomba leo nitumie nafasi hii kwa mara ya kwanza kuelezea kilichotokea mjini Dodoma katika uchaguzi wa nafasi ya urais kwa Chama Cha Mapinduzi na nadhani sitaulizwa tena,” alisema Membe.

Mfano huo huenda ukahusishwa na wanachama wa CCM waliokuwa wanamuunga mkono Membe kama timu iliyokuwa inatumainiwa ingeshinda mchakato huo, huku Dk. Magufuli akielezwa kama timu ambayo haikudhaniwa kushinda kinyang’anyiro hicho kutokana na kutokuwa na makundi yaliyokuwa yanamuunga mkono.

Membe alikuwa na kundi kubwa la wafuasi akimfuatia Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

Lowassa na Membe walikuwa miongoni mwa makada sita ambao walipewa adhabu ya kufungiwa mwaka mmoja kuanzia Februari, mwaka jana hadi Mei, mwaka huu, baada ya kubainika kuwa walianza kampeni mapema kabla ya wakati kinyume cha kanuni za chama hicho

Irene Uwoya Apitishwa na CCM Kuwa Mbunge Viti Maalum Kupitia Tabora

$
0
0
Mwigizaji wa filamu za Kibongo,Irene Uwoya apitishwa na Halmashauri Kuu ya CCM (NEC )kuwa mbunge viti maalum vijana mkoa wa Tabora.

Wengine waliopitishwa ni namba 1. Halima Bulembo 2. Zainab Katimba 3. Mariam Ditopile 4. Mary Kangoye 5. Kizigo 6. Irene Uwoya.

Hongera sana Uwoya.

Steve Nyerere Afungukia Madai Kuhamia Ukawa!

$
0
0
STAA wa uchekeshaji na filamu Bongo, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’ amefungukia madai ya kujiondoa Chama Cha Mapinduzi na kujiunga na umoja wa UKAWA akisema kushindwa kwake katika kura za maoni hakuwezi kuondoa heshima yake kwa Mwenyekiti wake, Jakaya Kikwete.

Akizungumza na gazeti hili juzi, Steve alisema Rais Kikwete amefanya mambo mengi sana kwa wasanii, kiasi kwamba ni mtu asiye na hisani pekee anaweza kuhama CCM kwa sababu ya kushindwa katika kura za maoni au ushawishi wa namna yoyote.

“Kikwete na CCM wamefanya mambo makubwa sana kwa wasanii, leo unaniambia mimi nihamie Ukawa, hivi wakati Lowassa (Edward, mgombea wa Ukawa) alipokuwa waziri mkuu aliwafanyia nini wasanii? Mimi kushika nafasi ya tano kwenye kura za maoni ni ushindi kwangu, kama ilivyo kwa Wema (Sepetu) kushika nafasi ya tano ni ushindi, kwa nini tuhame?” alisema msanii huyo.

Steve alitoa kauli hiyo kufuatia swali aliloulizwa kutokana na uvumi kuwa yeye na wenzake walikuwa mbioni kujiunga na Ukawa baada ya kushindwa kwenye kura za maoni za CCM hivi karibuni.

Chanzo: GPL

Profesa Lipumba Awasili Nchini Akitokea Rwanda

$
0
0
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea Rwanda jana. Picha na Said Khamis

NORA Ananga Wasanii Wanaotumika Kisiasa! Adai Hawaitambui Thamani yao...Kila Mwaka Wanatumika na Kuachwa Solemba

$
0
0
Nora wa Bongo Movies
Msanii wa ‘long time’ kwenye ulimwengu wa filamu, Nuru Nassoro ‘Nora’ amewananga wasanii ambao wanakubali kutumika kisiasa katika kipindi hiki bila kujua madhara watakayopata baada ya uchaguzi.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Nora alisema kuwa, anawashangaa baadhi ya wasanii kukubali kununulika wakati wakijua kuwa, baada ya uchaguzi watamwagwa.
“Jamani mimi nashangaa kuona wasanii tunatumika kwa kiasi hiki, thamani yetu hatuitambui kabisa, kila baada ya miaka mitano tunatumika kisha tunaachwa solemba, yaani dah!” alisema Nora.

TCRA Watoa ADHABU Kwa Kituo cha Televisheni cha ITV

$
0
0
Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) imetoa  adhabu ya onyo  kali  na  kukitaka  kituo cha  ITV kuomba radhi mara mbili mfululizo kwenye taariifa zake za habari baada ya kukiuka sheria ya utangazaji nchini ya Mwaka 2005.

Hukumu hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na kamati ya maudhui ya utangazaji, katika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Margaret Munyagi (pichani) wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo  Muyangi  alisema kamati hiyo imebaini kituo cha  ITV kulikiuka sheria hiyo ya utangazaji nchini kwa kurusha taarifa ambayo ingeweza kuleta machafuko nchini.

Alidai katika kipindi cha Habari zilizotufikia muda huu kilichorushwa siku ya Jumatatu ya tarehe 10 mwezi huu majira ya saa 2.22 asubuhi , ITV  Walitangaza  “Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limepiga marufuku maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema wakati wa kumsindikiza Lowassa kwenda kuchukua fomu ya Urais."

Alisema katika kipindi hicho Mtangazaji wake alisikika akisema Jeshi hilo limezuia maandamano hayo baada ya kubaini yanauvunjifu wa amani huku Mtangazaji huyo akimnukuu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova akidai ndo amesema hivyo,Wakati taarifa hiyo ilikuwa ya upotoshaji kwani jeshi hilo halikuwa limetoa taarifa hizo..

Bi Muyangi  alisema baada ya ITV kurusha taarifa hiyo ya kwanza juu kuzuiliwa  huko kwa maandamano, ndipo siku hiyo hiyo  tena katika kipindi hicho cha Habari zilizotufikia mda huu majira ya saa tatu asubuhi kilirushwa taarifa inayosema Jeshi la Polisi limeruhushu maandamo ya Chadema kutoka Makao makuu wa Chama cha Wananchi CUF Buguruni Jijini Dar es Salaam kwenda Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC.

Muyangi alidai katika taarifa hiyo ilisikika sauti ya Kamanda Kova juu ya kuruhusu maandamono hayo,tofauti na taarifa ya kwanza ambayo haikuweka uthibitisho wa Kamanda Kova.

Alisema baada ya Mamlaka hiyo kubaini makosa hayo,Kamati hiyo iliwasiliana na Mkurugenzi wa ITV Bi Mhavile na mkurugenzi wa Redio one Deogratus Rweyunga pamoja na Mhariri wa ITV Steven Chuwa ili kutaka  ufafanuzi ambapo wote kwa pamoja walikiri kosa hilo huku wakisema Mtangazaji huyu alitoa taarifa kwenye Mitandao ya Kijamii ambayo ilikuwa inakataza maandamano hayo ambapo alishindwa  kuithibitisha kama taarifa hiyo  ni ya kweli au la.

Aidha, Bi Muyangi alisema baada ya Kamati hiyo kusikiliza pande zote,ndipo wakatoa hukumu kwa kupitia sheria ya Utangazaji ya mwaka 2005 ambayo inakataza kituo chohote cha Utangazaji kurusha taarifa zinazoleta mchanganyiko katika jamii,

Mrema asema UKAWA umepoteza mwelekeo

$
0
0
Mwenyekiti wa taifa wa TLP Augustine Mrema amewatahadharisha watanzania kuwa macho juu ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ambao umepoteza mwelekeo na kuyumba kisiasa na kudai kuwa hawafai kuingia ikulu na kuongoza nchi.

Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha TLP , Augustino Lyatonga Mrema
Mrema ametoa tahadhari katika eneo la njiapanda baada ya kurejea ofisi ya msimamizi wa uchaguzi wilaya ya Moshi kuchukua fomu za kugombea ubunge katika jimbo la Vunjo huku akisindikizwa na wafuasi wake.
Amesema, kitendo cha ukawa kumkashifu hadharani waziri aliyestaafu Mh
Edward Lowasa kuwa ni fisadi na baadaye kumpokea na kumteua kuwa mgombea wa urais ukawa imeonyesha udhaifu mkubwa na kwamba watanzania wa sasa si wakuburuzwa.
Mh. Mrema amesema kuwa haiwezekani mtu alieachwa na chama na kuonekana hafai kutokana na tuhuma za ufisadi kicha CHADEMA ndio wakaona anafaa kuwa mgombea huko ni kuonyesha kutokuwa na msimamo ndani ya hivyo ni vigumu kuwapa uongozi wa nchi.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images