Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104808 articles
Browse latest View live

CCM Wayapuuza MAFURIKO ya Lowassa......Nape Asema Hata Mrema Alikuwa Kivutio. Ataka Gari la WAGONJWA Lipelekwe Kwa Lowassa Mapema

$
0
0
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesisitiza kuwa kitashinda Uchaguzi Mkuu mwaka huu kwa sababu kina mtandao mkubwa wa wanachama kuanzia ngazi ya chini na kwamba kufurika kwa wananchi katika mikutano ya Mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa sio ushindi, kikisema kura ni mahesabu.

Aidha, kimesema kuwa mgombea huyo wa Chadema na umoja wa vyama vinne vya upinzani (Ukawa), amedanganywa na wapambe wake kuihama CCM na kumkejeli ikisema gari la wagonjwa linapaswa kuwekwa nyumbani kwake siku ya uchaguzi kwani CCM itapata ushindi wa uhakika asubuhi.

Akitoa taarifa kuhusu kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika jana katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisisitiza kuwa ushindi wa chama hicho tawala na kikongwe hauna shaka kutokana na mtandao wake kuanzia ngazi ya chini.

Akijibu swali kuhusu kufurika kwa wananchi katika mikutano ya mgombea huyo wa Chadema, Nape alisema:

“Kwa walioanza siasa jana ndio watashituka. Mwaka 2010 Slaa (Dk Willibrod) katika mkutano wake wa mwisho wa kampeni Mbeya alipata watu wengi kuliko wale aliopata Edward. Lakini kura alizopata Mbeya utashangaa.

“Kupata watu wengi mkutanoni hakutushangazi kwani kura ni mahesabu, hawa (Chadema na mgombea wao) wanatoka pointi moja kwenda nyingine. CCM ina mtandao, ukiondoka mjumbe wa nyumba kumi anapitia watu wake anasafisha nyayo zenu,” alisema kiongozi huyo.

Nape aliongeza kuwa wapinzani wote wametoka ndani ya CCM kuanzia kwa Augustino Mrema mwaka 1995 na hadi katika chaguzi nyingine zilizofuta na zote wapinzani walishindwa, na hata safari hii CCM itashinda.

Akimgeukia Lowassa, Nape alisema Waziri Mkuu huyo aliyejiuzulu, amedanganywa na wapambe wake na kuondoka chama tawala, na kwamba licha ya kuhamia huko, CCM itamshinda asubuhi na kuwataka wanaotishia kukihama kufanya hivyo na si kuleta shinikizo.

“Katika mchakato wa uchaguzi si wote watakaoridhika na matokeo kwa sababu kuna wengi wanajiandaa kushinda na sio kushindwa, na matokeo yanapokuwa hivyo, wanakuwa hawaridhiki na hapo ndipo wanazungumzia kwenda upande wa pili, na hasa kwa shinikizo la wapambe.

“Hili limetokea kwa Edward, amekwenda upande wa pili, amedanganywa na watu, tutampiga. Ushindi wa CCM ni wa uhakika, sio wa matumaini. Matumaini yapo Angaza, CCM ni ya uhakika. Tutashinda asubuhi. Tumesema ni mpambano kati ya wagombea na makapi,” alisema Nape na kuongeza:

“Zipo mechi ambazo unajua hii utashinda. Yanga na Lipuli ya Iringa unajua matokeo yake. Tunataka mgombea mwenzetu apelekewe ambulance (gari la wagonjwa) nyumbani kwake, kwani ushindi kwetu ni uhakika.

” Kuhusu wanaolalamika na kutishia kuhama, alisema malalamiko hayawezi kutolewa barabarani kwani chama hicho kina utaratibu wake na yale yote yaliyolalamikiwa yakiwamo ya udiwani, yamefanyiwa kazi.

 “Tulisema wakati ule wa mchakato wa kutafuta mgombea wa urais kuwa hatutafanya kazi kwa shinikizo. Tunajua uimara wa chama chetu, kama kuna watu wanataka kwenda upande wa pili waende. Lakini CCM haiwezi kufanya kazi kwa vitisho na shinikizo.

"Tatizo ni kwamba kunatokea wagombea 12, halafu unasema lazima uwe wewe. Kuna watu (wanaotaka kuhama) wanafanya hivyo kwa shinikizo la viroba na hela,” alisema Nape.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Agosti 18

$
0
0




















Morning Guys..Nimewawekea Vichwa vya habari vya Magazeti ya Leo Hapa vilivyomake Headlines siku ya Jana...

Unaweza pia Kutembelea Page yetu ya Instagram kwa Kubonyeza Hapa: @udaku_special 

Askari Magereza Aliyepanga Mauaji Stakishari Auawa

$
0
0
MAPYA tena! Aliyekuwa askari magereza wa Gereza la Dondwe, Wilaya ya Mkuranga, Pwani, Juma Rashid ambaye Uwazi liliwahi kumripoti kuwa, ndiye ayechora ramani yote ya uvamizi na mauaji ya askari wa Kituo cha Polisi  Stakishari, Dar imebainika kwamba ameuawa, Uwazi linazidi kukokotoa.
Uchunguzi wa kina uliofanywa na gazeti hili umebaini kwamba askari huyo ndiye yule aliyeuawa siku ya tukio lililojiri Julai 12, mwaka huu nje ya kituo cha Stakishari ambaye alijulikana kwa jina maarufu la Osama.

HAIKUJULIKANA
Hata hivyo, baada ya muaji hayo, taarifa zilienea kwamba, aliyeuawa eneo la tukio ni mmoja wa majambazi hao bila kujulikana kuwa ndiye askari magereza mstaafu mpaka hivi karibuni ambapo, mke wake, Fatuma Hassan (37) alipoanika ukweli kwa gazeti hili.

Uchunguzi zaidi umebaini kuwa, siku chache kabla ya tukio la uvamizi huo, marehemu Osama alionekana kwenye baa moja iliyopo maeneo ya Stakishari na kuwanunulia pombe baadhi ya polisi huku akichunguza sehemu zinazohifadhiwa silaha na jinsi gani polisi wanavyokaa katika lindo pia ni siku gani inafaa kwa uvamizi ambapo alibaini ni Jumapili.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, timu ya Uwazi ilifunga safari hadi kwenye Kijiji cha Dondwe na kufikia nyumbani kwa marehemu Osama ambaye aliacha kazi akiwa na cheo cha koplo na kufanya mahojiano na mke wake, Fatuma.

Mwanamke huyo ambaye alianza kwa kukiri kwamba marehemu Osama alikuwa mumewe, alisimulia maisha yake na mwanaume huyo hadi anauawa. Alikuwa na haya:
“Tulifunga ndoa na Juma mwaka 1999 huko Kigoma alikokuwa akifanyia kazi katika Gereza la Kwitanga. Tulipendana sana. Mume wangu alikuwa mpole, msikivu, sikutegemea kama angeweza kuuawa katika mazingira kama haya ya aibu.
“Mwaka 2009, akatakiwa kuja kuripoti Gereza la Ukonga (Dar) halafu akapangiwa kuja hapa Gereza la  Dondwe (ni tawi la Gereza la Ukonga).”

AANZA KUBADILIKA TABIA
“Akiwa hapa Dondwe, ghafla mume wangu alianza kubadilika tabia, akawa anafuga ndevu tofauti na taratibu za kazini kwake. Akaonywa na viongozi wake lakini hakubadilika.
“Lakini pia alinitaka mimi nianze kuvaa nguo za kufunika mwili  mzima mpaka mikono na kubaki uso tu. Hilo sikukubaliana nalo.

“Tuliendelea kuishi mpaka mwaka 2012, akasema anataka kuacha kazi. Mimi sikukubaliana naye kwa sababu tuna watoto, yeye akasema lazima aache kazi. Nilimuuliza anataka kufanya kazi gani na kwa nini aliamua kuacha kazi? Akasema aliamua hivyo kwa sababu imani ya dini yake haikuwa ikimruhusu kufanya kazi ya uaskari ambayo aliitafsiri kuwa ni ya ukafiri.
“Kweli. Siku ilifika, akaandika barua ya kuacha kazi, lakini pia akaniandikia mimi talaka moja kwa sababu sikumuunga mkono kwenye matakwa yake.”
“Maisha yalianza kuwa magumu. Akawa anauza maji mitaani kwa kubeba madumu kwenye baiskeli. Baadaye akanunua pikipiki ya magurudumu matatu, akaendelea na biashara hiyo.”

MKE ARUDI KWAO
“Ilinibidi mimi niondoke kurudi kwetu Singida. Baadaye nilikwenda kwao kuwaeleza ndugu zake akiwemo baba yake mzazi. Walishangaa sana, aliitwa lakini hakwenda. Wakanishauri nirudi hapa Dondwe ili niwatunze watoto. Majirani zangu hapa nao walinipigia simu wakisema nirudi, watoto wanateseka.
“Nilirudi, lakini nilipofika ikawa kila mmoja analala katika chumba chake. Hakunijali kwa chakula wala kwa mavazi.
“Kitu kilichonishangaza ni kwamba, aliniambia kuwa anataka kuwatoa watoto kwenye shule za serikali na kuwapeleka za dini. Nilikwenda kwa mtendaji wa kijiji nikamweleza. Aliitwa ofisini lakini hakwenda. Kuanzia hapo akaacha kuwahudumia.”
MAAJABU ZAIDI

“Mimi nilianza kuamini mume wangu hakuwa yule baada ya watu aliokuwa akiswali nao, walipokuwa wakija hapa nyumbani aliwaambia mimi si mke wake. Isitoshe hata baba yake mzazi alipofariki dunia Aprili mwaka huu hakwenda.”

STAKISHARI
“Nakumbuka siku hiyo ya tukio la kule Stakishari, aliondoka hapa jioni akisema anasafiri kwenda kwao Singida. Nilimuuliza mbona unaondoka na pikipiki, utaitunza wapi? Akasema ataiacha kwa ndugu zake wa Dar.
“Hata hivyo, nilipata wasiwasi. Lakini sikuwa na la kusema. Aliondoka zake. Ilipofika usiku nilimpigia simu ikawa haipatikani. Kwa kweli sikupata usingizi. Kesho yake nikapiga tena simu pia hakupatikana.
“Niliamua kuwapigia simu kwao, wakasema hawana taarifa ya ujio wake. Jioni nikampigia dada yake ambaye yupo Singida mjini, akasema hawajamuona.

MAMBO HADHARANI
“Nilikuwa najiuliza maswali mengi sana lakini bila majibu. Baada ya siku kama tatu kupita, ikatangazwa na jeshi la polisi kwamba kuna jambazi mwenye madevu ameuawa na picha yake ikawa mtandaoni. Mtendaji wa kijiji chetu, Said Mohamed Mfume naye akawa amepata taarifa hizo akaniita ofisini kwake.
“Mtendaji akaniambia kwamba kuna picha ya mtu aliyeuawa katika tukio la Stakishari anafanana na mume wangu lakini hakunionesha. Picha hiyo ilisambaa hadi kwao Singida.
“Kuna ndugu yangu akaja mpaka hapa Dondwe akanionesha hiyo picha, nikagundua ni yeye mume wangu. Katika magazeti waliandika jina la Ustadhi Rashid.
“Marafiki zake nao baada ya kupata taarifa walikuja hapa na kuniambia eti mume wangu ameuawa lakini ni kama amepata shahada. Wakimaanisha kwamba amekufa kishujaa katika kutetea dini.”

MKE AENDA STAKISHARI
“Ilitulazimu kwenda Kituo cha Polisi Stakishari ili kupata taarifa kamili. Kufika wakaniweka ndani siku tano kwa mahojiano. Hivi ninavyozungumza na wewe  simu yangu bado iko pale kituoni.
“Niliporudi hapa nyumbani, niliwaambia watoto juu ya kifo cha baba yao, kwa kweli walijisikia vibaya sana ingawa alikuwa hawataki waziwazi.”

MWILI WACHUKULIWA
“Agosti 4, mwaka huu, mimi na watu wengine hapa  tulikwenda kuuchukua mwili Muhimbili. Kufika tukapata taarifa kwamba kuna watu walikwenda jana yake kuutaka mwili lakini walizuiwa. Mimi  nilijua ni wale marafiki zake.

“Baada ya kuuchukua mwili tulishindwa mahali pa kwenda kuuzika kutokana na tukio alilolifanya. Ilibidi tukamzike kwenye Makaburi ya Kijiji cha Mazinda, Mbuyuni, Chanika ambako kuna dada yangu kaolewa huko. Mumewe alisema kumzikia Dondwe haitatoa picha nzuri kutokana na aina ya kifo.

“Agosti 8, mwaka huu, tulikwenda kujengea kaburi lake, tukakuta kifuu cha nazi kilichoandikwa maneno ya Kiarabu. Ilinishangaza sana mimi. Hivyo ndivyo ilivyokuwa au ninavyomjua marehemu Rashid Juma baba wa watoto wangu wanne.”
Baadhi ya askari magereza wa Gereza la Dondwe ambao walikuwa wakifanya kazi na marehemu walipohojiwa na Uwazi walisema wanamtambua marehemu ambapo kazini alikuwa akitumia jina la Antony Gembo.

La Juma Rashid lilikuwa la dini lakini aliamua kuacha kazi kwani alibadilika akawa tofauti na taratibu za kijeshi. Alipoambiwa ajirekebishe aliamua kuacha kazi lakini cha kushangaza hakuchunguzwa anakwenda kufanya kazi gani na kwa nini alikuwa na kiburi hicho cha kuacha kazi.
Baadhi ya wanakijiji waliohojiwa kuhusiana na maisha ya marehemu huyo walisema hakuna aliyejua angeweza kujiunga na tabia hiyo ya kihalifu na hata siku alipouawa haikujulikana mara moja kuwa ni yeye.

Vyanzo vyetu vilieleza kwamba, marehemu kabla  hajabadilika tabia alikuwa akiswali katika nyumba moja ya ibada. Baada ya muda kukatokea kundi la watu ambao ni marafiki zake kutoka kijiji jirani.
Hata hivyo, waumini wa madhehebu waliyokuwa wakiswali waliwashtukia kutokana na elimu ya dini waliyokuwa wakiitoa ambayo ilikuwa ya kihalifu zaidi, wakatimuliwa.
Inadaiwa kuwa, baada ya kutimuliwa, watu hao wakiwa na marehemu walielekea Kijiji cha Mandikongo ambapo kulikuwa na ngome yao. Na ndiko ambako baada ya uvamizi wa Stakishari, jeshi la polisi lilikuta bunduki 15 na shilingi zaidi ya milioni mia moja na sabini elfu zikiwa zimefukiwa ardhini.
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar, Suleimani Kova (pichani), aliliambia gazeti hili kwamba baadhi ya watuhumiwa wa tukio hilo wameshakamatwa.

MTENDAJI WA KIJIJI
Mtendaji wa Kijiji cha Dondwe, Mfume alipohojiwa na waandishi wetu alikiri kumtambua marehemu kwani alikuwa mkazi wake na mke wake walikuwa wakifika ofisini kuelezea mambo aliyokuwa akifanyiwa na marehemu.

Ugumu wa Lowassa Kuingia Ikulu Oct 2015 Huu Hapa

$
0
0
WAKATI wafuasi wa vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi ( Ukawa) wakiwa na shangwe kutokana na kumpata Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kama mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba, ugumu wa kiongozi huyo kuingia ikulu umebainishwa, Uwazi lina habari kamili.


aliyekuwa waziri mkuu wa kwanza wa serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete, alijiunga na Chadema mwishoni mwa Julai mwaka huu baada ya jina lake kukatwa wakati wa mchakato wa kutafuta mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), nafasi ambayo ilitua kwa Dk. John Pombe Magufuli.

Ugumu wa kwanza unaotajwa, ni uwezekano wa kutopigiwa kura na wafuasi wote wa Chadema, ambao kuingia kwa kada huyo wa zamani wa CCM, kuliwagawa, kwani wapo waliokubali kwa roho moja ujio wake na wengine ambao hawakupendezwa kabisa na jambo hilo. Mgawanyo huo, unapunguza kura ambazo angeweza kuzipata endapo wanachama hao wangekuwa kitu kimoja kama awali.

Ingawa aliripotiwa kuwa na wafuasi wengi akiwa CCM, ushahidi unaonesha kuwa siyo mashabiki wake wote wamefurahishwa na hatua yake ya kuhamia upinzani, hivyo idadi kubwa ya wapiga kura aliokuwa akiwategemea, wameamua kuachana naye na wao kuendelea kubakia chama tawala.
Ugumu mwingine, unatokana na ukweli kuwa licha ya Chadema kujizatiti hadi vijijini, lakini haina mtandao mpana kama ilivyo kwa CCM, hivyo hata ile ‘amsha amsha’ inayoonekana mijini hivi sasa, haiko vijijini, ambako chama tawala bado kina mizizi na kina wapiga kura wengi maeneo hayo.
Jambo lingine linalotajwa kuwa ni gumu kwa Lowassa kuingia ikulu, ni ukweli kuwa kujiweka kando kwa viongozi wawili waliokuwa na mashabiki wengi, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa na Mwenyekiti wa Cuf, Profesa Ibrahim Lipumba kumewachanganya mno wafuasi wao na hivyo kuwa njia panda.

Ukimya wa Dk. Slaa, anayeaminika kufanya kazi kubwa ya kuwashawishi watu kuipenda Chadema, umewafanya baadhi ya wafuasi wake kutokuwa na mwelekeo, hivyo kuweka uwezekano mkubwa wa watu hao ama kupiga kura kwa wagombea wa vyama vingine au wasipige kabisa, kitu kitakachopunguza kwa kiwango kikubwa idadi ya kura za Lowassa kuelekea ikulu.

Urais Waivuruga ACT-Wazalendo ya Zitto Kabwe.......Waliyemchukulia Fomu ya Urais Akataa, Asema Hajajiandaa Kisaikolojia

$
0
0
Hali ya hewa ndani ya Chama cha ACT- Wazalendo ambacho kinaongozwa na Zitto Kabwe, imechafuka, baada ya Kamati Kuu kumpitisha na kumchukulia fomu ya urais, Prof. Kitila Mkumbo, huku mwenyewe akisita kulipokea jukumu hilo.

Kufuatia hatua hiyo, Prof. Kitila ameandika katika mtandao wa kijamii kuwa hajaandaliwa kisaikolojia kupeperusha bendera ya chama hicho katika nafasi ya urais na jukumu hilo wapewe viongozi wengine waandamizi.

Tofauti na ilivyozoeleka kwa wagombea kwenda na wafuasi wao Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kuchukua fomu za kugombea urais, kwa upande wa ACT – Wazalendo, Katibu Mkuu, Samson Mwigamba, jana alikwenda Nec kumchukulia  fomu Prof. Kitila ambaye inadaiwa viongozi wakuu wa chama hicho wamekutana naye kwa mazungumzo ya kumshawishi akubali kupeperusha bendera ya chama hicho kuelekea Ikulu.

Mapema asubuhi jana Prof. Kitila alifika ofisi za chama hicho Kijitonyama na kuondoka na majira ya saa 5:00 asubuhi wafuasi zaidi ya 100 wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali walivamia ofisi hiyo na kumbana Mwigamba kuwaeleza kwanini chama hicho kinachelewa kuweka wazi mchakato wa mgombea wake wa urais.

Habari zinasema kuwa licha ya Prof. Kitila kutokuwapo kwenye kikao cha Kamati Kuu (CC) kilichopitisha uamuzi wa kumtaka apeperushe bendera ya chama hicho katika nafasi ya urais, lakini ulipitishwa uamuzi wa kwamba abebe jukumu hilo zito.

Wakati Kamati Kuu ikiamua hivyo, hadi jana alasiri hapakuwapo na makubaliano na Prof. Kitila, lakini viongozi wakuu wa chama walikuwa kwenye mazungumzo naye.

Akizungumza na mtandao huu jana, Mwigamba alisema alichukua fomu hiyo saa 4:00 asubuhi, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Kamati Kuu iliyokutana Agosti 15, mwaka huu.

Alisema pamoja na azimio hilo, Kamati Kuu ilipitisha majina ya wagombea ubunge nchi nzima, wagombea udiwani na kupokea ripoti ya wataalamu washauri juu ya ushiriki katika harakati za uchaguzi wa rais.

“Baada ya kupokea taarifa na mapendekezo yao tukajiridhisha kwa mustakabali wa taifa, chama kinahitaji kusimamisha mgombea urais, ndipo nilipoagizwa kwenda kuchukua kwa sababu muda unaenda zianze kujazwa ili Ijumaa ambayo ndiyo siku ya mwisho zirudishwe,” alisema Mwigamba.

Alisema Kamati Kuu imeamua hivyo kwa kuwa Prof. Kitila ni mwadilifu, mzalendo wa kweli, anaweka mbele maslahi ya Taifa na kwamba ana sifa zote za kuliongoza taifa na mgombea mwenza atakuwa ni Mwandishi wa habari mkongwe, Hawra Shamte.

Hata hivyo, Hawra, alipoulizwa kuhusu maamuzi hayo ya Kamati Kuu, alisema hana taarifa zozote na kwamba hadi jana jioni hakuarifiwa chochote.

Alisema wakati mgombea huyo anakutana na viongozi wakuu wa chama hicho, fomu hiyo itaendelea kusambazwa mikoani ili kusaka wadhamini na kwamba walianza kufanya hivyo jana.

“Tofauti yetu na wengine hatutakuwa na ziara kwenye kusaka wadhamini, nimeenda na wanachama wengine watatu kuchukua fomu na sikuwa na msururu wa watu na hivyo hivyo kwenye kusaka wadhamini itakuwa kimya kimya,” alisema Mwigamba.

Alipoulizwa juu ya utayari wa Prof. Kitila kupeperusha bendera hiyo, alisema: “Hatuna wasiwasi, tunaamini atakubali uamuzi wa Kamati Kuu, anajua ni wajibu kubeba jukumu chama kinapomuhitaji.”

Aidha, Mwigamba alisema kama itashindikana kwa Prof. Kitila, ni lazima chama hicho kisimamishe mgombea mwingine katika nafasi hiyo.

Kitila: Sina Maandalizi
Katika kundi la mtandao wa kijamii la chama hicho la Whatsaap, lijulikanalo kama ACT Taasisi Imara, Prof. Kitila aliandika taarifa ya kuwashukuru wanachama na viongozi kwa imani yao kwake, lakini alisema hawezi kubeba jukumu hilo.

“Naomba niwashukuru nyote kwa imani kubwa mliyonayo juu yangu katika kukiwakilisha chama katika nafasi ya urais, naishukuru Kamati Kuu kwa imani yake kwangu hata kufikia hatua ya kupitisha azimio la kuniomba kugombea urais kwa chama chetu. Jana CC (Kamati Kuu) ilituma ujumbe maalum nyumbani kwangu kwa ajili ya kuzungumza na familia na jamaa zangu juu ya ombi hilo,” alisema katika andiko hilo na kuongeza:

“Nimekuwa nikitafakari tangu Alhamisi nilipoombwa rasmi kutafakari uwezekano wa mimi kugombea baada ya juhudi zetu za kutafuta mgombea kushindikana. Nimefanya mawasiliano mapana ndani ya familia, chama, chuoni ninapofanyia kazi, kanisani kwangu na kwa watu na taasisi mbalimbali ninazohusiana nazo.”

Alisema baada ya tafakari na mawasiliano mapana (consultations), ameona hana utayari na maandalizi ya maana ya kisaikolojia, kifamilia na kisiasa kumuwezesha kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu ujao.

“Najua nimewaangusha sana katika uamuzi wangu huu, lakini naamini kwamba mtaheshimu uamuzi wangu na kwamba hamtaacha kuthamini mchango wangu katika chama kwa sababu ya kukataa kugombea urais,” alisema na kuongeza:

“Nasikitika kwa tuhuma ambazo baadhi ya wanachama wetu wanarusha katika mitandao ya kijamii na sehemu nyingine. Nathamini na kuheshimu haki ya wanachama kuonyesha hasira kwa jambo wasilolipenda…nawasihi wanachama wajizuie kuzusha mambo yatakayochochea chuki ndani ya chama na kukatishana tamaa.”

Aidha, alishauri wanachama wengine waandamizi waombwe wachukue jukumu hilo na kuwataja kuwa ni Mwenyekiti wa ACT – Wazalendo na Katibu Mkuu, Mwigamba na kwamba wakati hayo yakitafakariwa wasisahau malengo mapana ya chama waliyojiwekea katika uchaguzi huo.

Alisema mafanikio waliyofikia ni kuweka wagombea ubunge na udiwani kata na majimbo mengi nchini.

Mwigamba alipoulizwa juu ya taarifa hiyo, alijibu: “Sina simu ya whatsaap ila naenda kwenye kikao hadi leo (kesho) nitawapa taarifa.”

Wafuasi wakusanyika
Baadhi ya mabango yaliyokuwa yamebebwa na wanachama na wafuasi wa ACT-Wazalendo yalikuwa na ujumbe wa ‘wamenunuliwa’ na mgombea wa Chadema, Edward Lowassa ili wasisimamishe mgombea urais.

Wafuasi hao walikaa kwa saa nne nje ya ofisi hizo wakiimba nyimbo mbalimbali.

Mabango mengine yalisomeka: “Viongozi hatuwaelewi mmekaa muda mrefu bila kutuambia mgombea urais ni nani wakati muda unaisha, kama hamsimamishi mgombea ni bora mfunge ofisi, tusijihusishe tena na siasa, liko wapi azimio la Tabora?”

Lowassa Adai CCM Itapata Laana Kubwa Kwa Walichomfanyia Mzee Kingunge Bila ya Huruma...

$
0
0
SIKU mbili baada ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), kumvua Ukamanda Mkuu, mwanasiasa mkongwe nchini, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, uamuzi huo umepokewa tofauti na mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Edward Lowassa.

Tamko la UVCCM ambalo lilitolewa na Katibu Mkuu wa umoja huo,Sixtus Mapunda, lilisema wamefikia uamuzi huo kutokana na tabia, mwenendo wa Mzee Kingunge aliounesha hivi karibuni tofauti na maadili pamoja na taratibu za CCM.

Umoja huo ulipendekeza vikao vya CCM, kuuangangalia upya uanachama wake na kuchukua hatua kubwa zaidi.

Bw. Lowassa ambaye pia ni mgombea urais anayeviwakilisha vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), alisema CCM itapata laana kama itaridhia kuondolewa kwa Mzee Kingunge.

Akiwahutubia mamia ya wafuasi wa UKAWA katika Viwanja vya Kibandamaiti, Mjini Zanzibar, jana ambako alikwenda kutambulishwa na kutafuta wadhamini, Bw. Lowassa alisema Mzee Kingunge ni mmoja kati ya wazee muhimu ndani ya CCM.

"Nasikitika sana kwa hatua kali alizochukuliwa Mzee Kingunge, kama isingekuwa yeye, CCM isingefika hapo ilipo, watapata laana," alisema.
 

Mapokezi yake
Lowassa aliwasili Zanzibar jana asubuhi akitokea jijini Mwanza kwandege ya kukodi akiwa na viongozi wengine wa UKAWA pamoja na mgombea mwenza, Bw. Juma Duni Haji.

Baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar, msafara huo ulipokewa na Katibu Mkuu wa CUF Taifa ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.

Akihutubia mkutano huo, Lowassa aliwaambia Wazanzibar kuwa atahakikisha anazingatia taratibu za kisheria ili Masheikh wa Jumuiya ya Mihadhara ya Kiislamu (Uamsho) wanaoshikiliwa katika mahabusu jijini Dar es Salaam, wanapata haki zao.

Ahadi hiyo ya Lowassa ilisababisha umati huo kulipuka kwa furaha na vifijo huku ukimuita `Rais, Rais, Rais.

Alisema kwa mara zote alizokwenda Zanzibar, hajawahi kushuhudia umati mkubwa kama aliouona jana.

Lowassa alisema amekwenda Zanzibar kuomba dhamana ya wananchi na kurudia kauli yake kwamba anawania urais kwa kuwa anauchukia umaskini.

“Nataka kuwahakikishia Watanzania popote kwamba mabadiliko yataletwa na vyama vya upinzani. Nimetembea sehemu mbalimbali nimeona wananchi wanataka mabadadiliko ya uongozi,” alisema.

Kuhusu Katiba, alisema yeye ni muumini wa Serikali Tatu zitakazosaidia kuimarisha Muungano na kwamba msimamo wake huo aliouonyesha tangu miaka ya 90 wakati wa harakati za kundi la G55.

Alisema suala hilo litafafanuliwa vizuri wakati wa uzinduzi wa ilani ya uchaguzi Jumamosi wiki hii na wakati wa kampeni.

Hata hivyo, Lowassa alisema njia ya kuiondoa CCM madarakani, ni kwa kupiga kura na wananchi wajiandae pia kulinda kura.

Masheikh  waliofungwa
Alisema Masheikh mkoani Mwanza walimwomba azungumzie jambo hilo na kwamba atakachofanya atakapoingia madarakani, atazingatia taratibu za kisheria kufuatilia stahili zao.

Bayport Yaanzisha Huduma Mpya ya Bima ya Magari, Pikipiki na Bajaj

$
0
0
Mratibu wa Bima kutoka Bayport Financial Services, Ruth Bura, katikati akizungumza katika uzinduzi wa huduma mpya ya Bima ya Magari, pikipiki na Bajaj kwa kushirikiana na Kampuni ya NIKO Insurance. Kulia ni Meneja Uendelezaji wa Biashara wa NIKO Insurance, Jabir Kigoda na kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Niko, Mannaseh Kawoloka.


Bayport yaanzisha huduma mpya ya bima ya magari, pikipiki na bajaj

Na Mwandishi Wetu, Dar es SalaamTAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mambo ya mikopo, imezindua huduma mpya ya bima ya magari, pikipiki na bajaj, ikiwa na lengo la kurahisisha masuala ya usafiri kwa wateja wao ili kukwamua zaidi. Kuanzishwa kwa huduma hiyo mpya kumetajwa kuwa kutachangia kwa kiasi kikubwa wamiliki wa vyombo hivyo vya usafiri waliokuwa wakishindwa kulipa bima kwa wakati na wakati mwingine mteja kupata ajali hali ya kuwa hana huduma ya bima inayoweza kumlinda.


Oparesheni Meneja wa Bayport Financial Services, Charles Mgeta, kushoto akizungumza jambo katika uzinduzi wa huduma mpya ya Bima ya Magari, pikipiki na bajaj. Anayefuata ni Afisa Mtendaji Mkuu wa NIKO Insurance, Mannaseh Kawoloka.

1.Afisa Mtendaji Mkuu wa NIKO Insurance, Mannaseh Kawoloka katikati akizungumza jambo katika uzinduzi wa huduma mpya ya bima ya magari, pikipiki na bajaj inayoendeshwa na Taasisi ya Bayport Financial Services. Kulia kwake ni Mratibu wa bima hiyo, Ruth Buran a kushoto kwake ni Meneja Oparesheni wa Bayport, Charles Mgeta. Picha zote na Mpiga Picha Wetu.
Wakati shughuli ya uzinduzi wa huduma mpya ya bima ya magari, pikipiki na bajaj kutoka Bayport Financial Services kwa kushirikiana na NIKO Insurance ukiendelea Makao Makuu ya Bayport leo asubuhi.
Meneja Madai wa Niko Insurance, David Mshuza, akiafuatiwa na Cecilia Peter na Lester Chinyang'anya. Picha zote na Mpiga Picha Wetu.

Akizungumza leo asubuhi jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Bima hiyo kutoka Bayport Financial Services, Ruth Bura, alisema huduma yao wanayoshirikiana na NIKO Insurance ina lengo kubwa la kumrudisha mteja wao (mkata bima), katika hali aliyokuwa nayo kabla ya kupata ajali hiyo.

Alisema mara kadhaa baadhi ya Watanzania wamekuwa wakikimbizana na askari wa usalama barabarani kwa sababu hawana bima kwenye vyombo vyao vya usafiri, ila kwa kupitia huduma yao mpya, sasa kila mtu anaweza kujiunga na bima kwa njia rahisi, wakiamini kuwa ni sehemu yao ya kuhakikisha wateja wao wanakuwa kwenye usalama ili watimize wajibu wao kufanya kazi na kukuza uchumi wao na wa Tanzania kwa ujumla.
“Ili mtu aweze kujiunga na huduma yetu ya Bima kutoka Bayport Financial Services, kwanza anatakiwa kujaza fomu yetu ya mkopo na ile fomu ya udhibitisho wa bima, bila kusahau nyaraka za umiliki wa gari lake ili tujiridhishe na umiliki wake.


“Baada ya hapo, gari lake litapigwa picha tano kila pembe, ikiwa ni nyuma na mbele na kwenye injini na tukimaliza hatua hiyo, mteja wetu atapatiwa mkataba wa bima pamoja na ‘sticker’ kuonyesha kuwa yupo kwenye bima, huku huduma hiyo ikiwa ni rahisi kwa sababu gharama za bima kwa mwaka ni kuanzia Sh 354,000 pamoja na VAT,” Alisema.


“NIKO tunajisikia faraja kubwa kushirikiana na wenzetu Bayport Financial Services kutoa huduma bora na kiwango cha juu, hususan kwa kupitia huduma hii mpya ya bima ya magari, tukiamini kuwa itawafanya Watanzania wote watembee kifua mbele, maana ile presha ya kukimbiana na watu wa usalama barabarani itakuwa imepatiwa ufumbuzi,” alisema Kigoda.


Bayport Financial Services ni taasisi ya kifedha inayotoa huduma mbalimbali za mikopo ya fedha, mikopo ya bidhaa, bila kusahau mradi wa mikopo ya viwanja vya Vikuruti unaoendelea na kuwafanya Watanzania watembee kifua mbele, huku taasisi hiyo ikifanikiwa kuwa na matawi 80 Tanzania Bara, hivyo kutoa huduma bora na kwa njia rahisi kwa kupitia matawi yao au mtandao wao wa www.kopabayport.co.tz.



Naye Meneja Uendelezaji wa Biashara wa NIKO Insurance, Jabir Kigoda, alisema kuwa huduma hiyo ni nzuri na rahisi inayoweza kuwanufaisha wateja na Watanzania wote, hivyo wanapaswa kuichangamkia ili kuwaweka katika usalama wao na wa vyombo vyao vya usafiri.


CCM Yatangaza Kamati ya Kampeni za Uchaguzi Yenye Watu 32 Chini ya Abdulrahman Kinana

$
0
0
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa jana Agosti 17, 2015 katika kikao chake cha siku moja kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dokta Jakaya Mrisho Kikwete imekamilisha kazi ya uteuzi wa Wagombea Ubunge katika majimbo mawili ya Singida Mashariki na Kiteto.

Wagombea ubunge walioteuliwa kupeperusha bendera ya CCM katika majimbo hayo ni pamoja na Ndugu Jonathan Njau (Singida Mashariki) na Ndugu Emmanuel Papian John (Kiteto).

Aidha Kamati Kuu imefanya uteuzi wa Kamati ya Kampeni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015 ambayo itaongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

Wajumbe wa Kamati hiyo ni kama ifuatavyo;-

1.    Ndugu Abdulrahman Kinana        -    Mwenyekiti
2.    Ndugu Rajab Luhwavi     -    Makamu Mwenyekiti – Bara
3.    Ndugu Vuai Ali Vuai      -     Makamu Mwenyekiti - Z’bar
4.    Ndugu Sofia Simba
5.    Ndugu Mohamed Seif Khatib
6.    Ndugu Asha-Rose Migiro
7.    Ndugu Samwel Sitta
8.    Ndugu Nape Nnauye
9.    Ndugu Mwigulu Nchemba
10.    Ndugu Harrison Mwakyembe
11.    Ndugu January Makamba
12.    Ndugu Amina Makillagi
13.    Ndugu Christopher Ole Sendeka
14.    Ndugu Stephen Wasira
15.    Ndugu Abdallah Bulembo
16.    Ndugu Hadija Aboud
17.    Ndugu Mohamed Aboud
18.    Ndugu Lazaro Nyalandu
19.    Ndugu Issa Haji Ussi
20.    Ndugu Waride Bakari Jabu
21.    Ndugu Mahmoud Thabit Kombo
22.    Ndugu Shamsi Vuai Nahodha
23.    Ndugu Maua Daftari
24.    Ndugu Stephen Masele
25.    Ndugu Pindi Chana
26.    Ndugu Shaka Shaka
27.    Ndugu Makongoro Nyerere
28.    Ndugu Bernard Membe
29.    Ndugu Sadifa Juma Khamis
30.    Ndugu Antony Diallo
31.    Ndugu Livingston Lusinde
32 .    Ndugu Ummy Mwalimu

Imetolewa na:-


Hackers Waigeuza Akaunti ya Instagram ya Fid Q Kuwa ya Wema Sepetu!

$
0
0
Kama unaitafuta akaunti ya Instagram ya Fid Q kuanzia jana bila mafanikio basi fahamu kuwa hackers wameitaifisha, kufuta picha zake zote na kuigeuza kuwa ya Wema Sepetu.

Akaunti hiyo ina followers zaidi 160,000.

“Account hii imekuwa hacked jana usiku ila mimi nimegundua leo asubuhi,” Fid ameiambia Clouds FM.

Niligundua baada ya kuingia katika account ikawa inanigomea. Mimi nilikuwa nimeandika mwanaharakati, sasa naona wameamua kubadili na jina na kuandika jina la Wema Sepetu,” alisema.

Zari The Bosslady Awajibu Ivan na King Lawrenc, ‘Visasi Hufanywa na Vilaza’

$
0
0
Hatimaye Zari The Bosslady ameamua kumjibu ex wake Ivan na swahiba wake King Lawrenc ambao wamekuwa wakimtupia madongo kuwa mtoto wake Tiffah si wa Diamond, ni wao.

King Lawrence alienda mbali zaidi kwa kutumia kampuni ya wanasheria kumtaka achukue vipimo vya DNA vya kichanga hicho chenye zaidi ya followers 80k kwenye Instagram.

Zari ametumia Instagram kuwajibu kwa kudai kuwa wanachofanya wawili hao ni visasi ambavyo anaamini hufanywa na vilaza!

Visasi hufanywa na vilaza,” ameandika Zari kwenye Instagram.

BO$$LADY anafahamu kuwa huzuni aliyonayo mtu mwenye chuki wakati akiangalia furaha na mafanikio yake ni adhabu tosha. Inabidi niyageuzie mgongo mambo yate ya kijinga yanayoendelea. Naendelea kuwaua kwasababu watu hutaka kuzima taa inayowaka zaidi kwao,” ameongeza.

Diamond tayari ametoa majibu yake kufuatia hatua hiyo ya Ivan na Lawrenc.

Mpenzi Wangu Simuelewi, na Nimekuta Picha yake FB imewekwa na Msichana

$
0
0
Nina mpenzi wangu tunakaribia kumaliza mwaka sasa. Kukutana kwetu ni mara chache sana kutokana na masomo.

Kusema kweli tokea tumeanza mahusiano sijawahi pokea hata shs 10 toka kwake. Hapo mwanzo tulikuwa tunawasiliana vizuri kipindi nikiwa chuo kutokana na pesa ninayotumiwa na mama yangu nikifunga chuo mawasiliano yanapungua sababu kutokuwa na pesa ya kununua vocha.

Nikimuelezea hiyo hali anasema haiwezekani Sasa kabadilika, nikimuuliza anasema yupo kawaida.

Kinachonitatiza ni kwamba juzi kati nilikuta picha yake FB imepostiwa na mdada fulani, comments zinaonyesha huyo dada na aliyeko kwenye picha ambaye ni mpenzi wangu ni wapenzi.

Kumuuliza mpenzi wangu anadai hajui ni kwanni huyo dada kapost hiyo picha na kwamba sio wapenzi ila wanafahamiana.

Jamani nisaidieni maana roho inauma sana

Enyi Wanawake Mlioolewa Kuweni Makini sana na Waume Zenu Unapoleta Mdogo Wako wa Kike

$
0
0
Hili jambo ni kuwatahadharisha wanawake ambao wapo ndani ya ndoa na kuwaonya wanaume wote walio ndani ya ndoa waache tabia ya huyu jamaa, pia kutaka ushauri wenu

Kuna binti mmoja tuko kwenye mahusiano kwa mda lengo akimaliza chuo na yakiwa majaliwa ya muumba tufunge ndoa, sasa alipokuja hapa Jijini Dar akawa anaishi kwa dada yake ambaye kuolewa.

Sasa huyo mwanaume amekua akimsumbua sana mpenzi wangu (ambaye ni shemeji yake) kumtaka kimapenzi, hili tatizo limekua likitusumbua akili sana na mpenzi wangu kwa sababu ya kuonyesha msimamo amekua akimtukana bila sababu.

Uzuri ni kwamba sms zote zipo na kila mazungumzo mpenzi wangu anayarecod na mengine yapi kwenye simu yangu ananitumia WhatsApp, yani anavyomtukana wakati mwingine na kumwambia yani unawapa wanaume wengine huko nnje unaninyima mimi.

Uzuri ni kwamba tuko karibu sana na mpenzi wangu kwasababu tunaishi mtaani mmoja kwa hiyo wakati mwingi yupo kwangu akitoka chuo kabla ya kurudi kwao, kwahiyo tumekua tukimrecod huyo baba tukiwa wote bila yeye kujua, na wakati huu sasa hamuheshimu huyo shemeji yake na kujibu anavyotaka na huyo shemeji yake ana umri wa miaka 40-45 na kuendelea.

Cha kusikitisha zaidi amekuja mdogo wake huyo mpenzi wangu aliemaliza secondary yani hata vichichu ndo vimeanza jamaa kaanza kukisumbua nasema kitoto coz ndo kamefikisha 18 juzi, sasa kamelalamika kwa mpenzi wangu kua jamaa anakasumbua balaa.

Sasa wakuu hapa nifanyeje coz huyo mtu kuna siku nahisi kuna siku atambaka kama sio mpenzi wangu basi ni hako kadogo kake, hebu tafakari mkewe yupo na wanaishi wote humo ndani lakini jamaa kakomaa na wadogo zake, huyo baba pamoja mke wake wanajua mimi nina mahusiano na huyo binti.

Ila hawajawahi kuniuliza, tunakaa mtaa mmoja na tinasali kanisa moja, nishaurini nifanyeje coz ushahidi wa record anavyokomaa upo na naweza kuvuruga hata ndoa yao, na pia nawahurimia hawa madogo coz sijui itakuaje na dada yao.

Na nyie wanaume hebu tuachieni hawa wadogo zao tioe acheni tamaa mana hao wadogo zake usipeme, dada yao hata nusu hawafikii.

WANAWAKE KUENI MAKINI NA WAUME ZENU MNAPOWALETA WADOGO ZENU WAZURI KULIKO NYIE KUISHI NA NYIE, sio wote nimeleta tahadhari

Aliyemuoa Mwanamuziki Meninah ni Mtoto wa Profesa Muhongo

$
0
0
Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo sasa ni baba mkwe wa muimbaji wa ‘Shaghala Bhaghala’, Meninah Atick aliyefunga ndoa na mwanae, Abdukarim Haule.

Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania mahaba ya mtoto huyo wa Waziri Muhongo, Peter Haule yamemfanya abadili dini na kuwa Abdulkarim Haule ili aweze kumuoa Meninah ambaye ni muislamu. Wawili hao walifunga ndoa huko Kigamboni wikiendi iliyopita.

Japo hajasema chochote kuhusu ndoa yake zaidi ya picha zinazoashiria ndoa yao, Meninah ameandika kwenye Instagram:

Usichague msichana ambaye ni mzuri duniani, chagua anayekupa furaha duniani, maisha ni mafupi na huwezi jua kesho kuna nini, fanya mazuri, asante Mungu kwa kila njia ninayopitia, nazidi kukumbuka kwa kubadilisha maisha yangu na kutumaini milele

HATIMAYE Mrembo Machachari wa Kenya Huddah Monroe Atulizwa Kwa Kuvishwa Pete ya Uchumba

$
0
0
Huddah Monroe
MREMBO kutoka nchini Kenya, Huddah Monroe, ameanza kuionesha pete ya uchumba aliyovishwa wiki iliyopita.

Mwanamitindo huyo mwenye umaarufu mkubwa nchini humo, ameamua kuvunja ukimya wake na kuionesha pete hiyo kupitia akaunti yake ya Instagram.

“Kila kitu kipo wazi, lakini muda ukifika watu watamjua nani aliyenivisha pete hii, lakini kwa sasa watu wanatakiwa wajue nina pete ya uchumba.

Kwa sasa naweza kusema sihitaji usumbufu kutoka kwa mwanamume yeyote, huu ni muda wangu wa kutulia na kufanya maisha na mume wangu mtarajiwa,” alieleza Huddah.

Kisuma na Safari Resort Baa za Wiki Kwenye Shindano la Tusker Fanyakweli Kiwanjani

$
0
0
 Mshereheshaji wa promosheni ya Fanyakweli Kiwanjani Gadner G. Habash akiongea na mkazi wa Yombo Vituka, Vicky Omary (katikati) kabla ya kumkabidhi zawadi mbalimbali kama bia za bure, fulana na mfuko ndani ya baa ya Kisuma iliyopo Mwembeyanga Tandika ambapo kampeni ya Tusker Fanyakweli ilifunga kambi kiwanjani hapo baada ya baa hiyo kuibuka mshindi wa wiki. (Kulia) ni balozi wa bia hiyo Bi. Veronica Mbilinyi.

Dj wa E-fm anayetambulika kwa jina la Dj Spar, akiporomosha burudani ya muziki ndani ya baa ya Kisuma iliyopo Temeke jijini Dar wakati wa hafla ya kuipongeza baa hiyo iliyoibuka mshindi wa wiki wa kampeni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani. Lengo la kampeni hiyo likiwa ni kuhamasisha baa mbalimbali za mitaa tunayoishi kufanya kweli wanapotoa huduma kwa wateja.

 Mkazi wa Temeke Bi. Anna Sylvester (Katikati) akipokea zawadi ya polo shirt baada ya kushiriki kwenye kampeni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani alipojumuika na marafiki zake kuipongeza baa ya wiki ya Kisuma iliyopo Tandika jijini Dar es salaam baada ya baa hiyo kuibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Fanya kweli kiwanjani wiki hii.(Wa kwanza kulia) ni rafiki yake aliyefahamika kwa jina la Tatu Mohammed, (Wa pili kulia) ni Mshereheshaji wa shughuli hiyo Gadner G. Habash sambamba na wasimamizi wa bia hiyo toka SBL.

 Bi. Catherine Bonventure (Katikati) Mkazi wa Temeke akipokea zawadi ya kalamu pamoja na bia za bure kutoka kwa mshereheshaji wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani Gadner G. Habash (Kulia) kwenye kiwanja cha Kisuma wakati wa kuipongeza baa hiyo ya Tandika jijini Dar es salaam baada ya baa hiyo kuibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker lengo lake likiwa ni kuhamasisha baa mbalimbali za mitaa tunayoishi kufanya kweli kwa kwa wateja wakati wa utoaji huduma. (Kushoto) ni balozi wa bia hiyo Bi. Veronica Mbilinyi.

Mkazi wa Mwembeyanga Bi. Sikudhani Idd (katikati) akipokea zawadi yake ya bia za bure, mfuko pamoja na Tisheti alivyopewa wakati wa hafla ya kuipongeza baa ya Kisuma ya Mwembeyanga Tandika mara baada ya baa hiyo kuibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker toka kampuni ya bia ya Serengeti. (Kushoto) ni Mshereheshaji wa promosheni ya Fanyakweli Kiwanjani Gadner Habbash na (kulia) ni balozi wa bia hiyo Bi. Veronica Mbilinyi.


Mshereheshaji wa promosheni ya Tusker Fanya kweli kiwanjani akizungumza na mkazi wa Kimara na mpenzi wa bia ya Tusker Bi. Grace Mweleke wakati wa promosheni ya Fanyakweli kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker ilipofunga kambi kiwanjani hapo kuipongeza baa ya Safari resort ya Kimara iliyoibuka mshindi wa wiki wa promosheni hiyo.

Ridhiwani Kikwete: Sasa Kumekucha.... Nikiangalia Hiki Kikosi Naamini Kabisa Kuna Chama Kitamficha Mgombea Wake Ndani

$
0
0
Baada ya CCM Kutoa List ya Team Ambayo itahakikisha CCM inashinda Urais 2015 , Mtoto wa Rais Ridhiwani Kikwete Ameandika Meneno haya :

"Sasa kumekucha.... Nikiangalia hiki kikosi naamini kabisa kuna Chama kitamficha mgombea wake ndani ili wengine wafanye yale ya matumizi halali ya Madodoki ya Chuma .... Nani msiniulize. Huu ndiyo mziki wa Magufuli, sidhani kama Mtauweza"

Je Kwa Maoni yako ni Mgombea Yupi Atafichwa Ndani ? 

Bifu la Diamond na Alikiba Limeisha? Meneja wa Diamond Apiga Picha ya Pamoja na Alikiba

$
0
0
Kitu ambacho mashabiki wengi wa Music Tanzania na hata nje ya Nchi wangependa kusikia kinaweza kikawa kimekaribia,  Meneja wa Diamond, Salaam amepiga picha ya Pamoja na mpinzani mkubwa wa msanii wake, Alikiba.

Haijajulikana nini kinaendelea lakini inawezekana labda ugomvi wa wasanii hao wawili umefikia mwisho na labda tutegemee chochote kutoka kwa hao wasanii wawili. Kweli mbongo mpe picha story ataandika mwenyewe

Picha hiyo inaonekana imepigwa jana, ukiangalia vizuri kwenye hiyo picha utamwona Ne-yo kwa nyuma, Kwahiyo iko wazi kuwa meneja wa Diamond yupo Kenya pamoja na Alikiba. Kitu kingine cha kutegemea ni collabo ya Diamond na Ne-yo, Diamond alikutana na Ne-yo mwezi uliopita Afrika kusini na aliahidi kuwa kuna kitu kinafata kwahiyo inawezekana meneja wa Diamond yupo Nairobi kwa ajili ya kukamilisha collabo hiyo.

Alikiba ameenda jijini humo kwa ajili ya  Coke Studio ambapo pia ataungana na wasanii wengine wa Afrika kushirikiana na Msanii wa Marekani.

CCM Yateka Mchakato wa Kumpata Mgombea Urais ACT-Wazalendo..Yaliyotabiriwa Yametimia

$
0
0
|Hatimaye Profesa Kitila Mkumbo akataa kuwa msaliti wa safari ya mabadiliko.
|CCM wahaha kutafuta mgombea mbadala.
|Zitto Kabwe aingia makubaliano na CCM.

Yale yaliyotabiriwa kwa muda mrefu kwamba chama cha ACT Wazalendo (chini ya kiongozi Mkuu Zitto Kabwe) ni Mpini wa CCM kumaliza upinzani nchini, HATIMAYE YAMETIMIA. Habari zilizopo ni kwamba kumetokea sintofahamu kubwa ndani ya Chama Cha ACT Wazalendo baada ya aliyetarajiwa kubeba bendera ya chama hicho kwa tiketi ya Urais, Profesa Kitila Mkumbo kuamua kupingana na viongozi wenzake ndani ya chama hicho na kukataa kuwa msaliti wa vuguvugu la mabadiliko linaloendelea kufagia siasa za Tanzania, hasa baada ya Edward Lowassa kuteuliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA huku mgombea huyo wa UKAWA (Edward Lowassa) akiendelea kukipa Chama cha mapinduzi (CCM) mgombea wake John Magufuli wakati mgumu kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.

Hatua ya Profesa Kitila Mkumbo kuamua kukataa kuwa msaliti wa vuguvugu la mabadiliko yanayotakiwa na wananchi walio wengi imetishia uwezekano wa chama cha ACT Wazalendo kukosa mgombea wake wa Urais.Kutokana na hali hiyo, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeamua kuingilia kati na kusisitiza kwamba ni lazima ACT Wazalendo isimamishe mgombea wake kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba. Lengo kuu ni kuhakikisha kwamba ACT Wazalendo inapunguza kura za Ukawa (Lowassa) huku kiongozi mkuu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akiwa tayari ameshaingia katika makubaliano na CCM kutekeleza mradi huo.

Kwahiyo wakati wowote kuanzia sasa, ACT Wazalendo itamtangaza mgombea wake wa urais na sasahivi kazi ya kumpata mgombea huyo wa Urais (ACT Wazalendo) inasimamiwa na Chama Chama Mapinduzi (CCM).

Kwa karibia miaka miwili sasa kumekuwepo na mjadala mkubwa humu Jamiiforums kuhusu jinsi gani chama cha ACT Wazalendo chini ya Zitto Kabwe kimekuwa kinatumiwa na Chama Tawala (CCM) Kama mpini wa kumaliza upinzani nchini. Hatimaye yametimia, na Mjadala wa kina juu ya jinsi gani tumefika hapa unapatikana kwenye uzi wa Nguruvi3 kwa kubofya hapa:

Duru za siasa: Chama cha ACT -Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani

MODS, tafadhali msiondoe au kuunganisha uzi huu na mwingine kwani katika mazingira ya sasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba, uzi huu unajitegemea, lakini muhimu zaidi, utasaidia umma kuelewa jinsi gani CCM inajaribu kila njia kuhujumu UKAWA kuelekea Oktoba 25.

Chanzo: Mchumbuzi Kutoka Jamii Forums

Lowassa: Nitamtoa Babu Seya Gerezani

$
0
0
Nimestuka Lowassa kudharau utawala wa sheria. Babuseya alikata rufaa mahakama kuu ya Tanzania na kushindwa kwa kosa la ubakaji na udhalilishaji watoto.

Je Lowassa hautambui mhimili wa mahakama? Je utaachia wafungwa wote?

Lowassa ataleta mgongano wa kidola.

Chanzo: Raia Tanzania

Kila Kitu Wazi.. na DiamondPlatnumz Kaonyesha Anamsupport Mgombea Urais Gani 2015.

$
0
0
Ni mwaka wa Uchaguzi Tanzania ambapo upinzani mkubwa unaonekana kwenye Wagombea wawili ambao ni John Pombe Magufuli atakaegombea kupitia CCM na Edward Lowassa aliyechukua fomu ya CHADEMA kwenye headlines za muungano wa vyama vya upinzani (UKAWA)

Tayari mpaka sasa tumeona baadhi ya mastaa wa Tanzania wakiweka wazi watu wanaowakubali kati ya hawa wawili, miongoni mwao ni Wema Sepetu aliyeweka wazi kumsupport Magufuli, mwigizaji Jackline Wolper na Aunty Ezekiel wanamsupport Edward Lowassa na sasa ni Diamond kaweka wazi.

Diamond anamsupport John Pombe Magufuli na kayaandika haya>>> Iwe Msanii, Mtangazaji, ama Mwanamichezo, ila Kila Mtanzania anahaki ya Kuchagua kiongozi anaeamini ni Bora, Mchapa kazi, Mwenye Afya na Msimamo ili kutuendelezea Nchi yetu… Kwa Uchunguzi na tathmini niliyoifanya tangu hizi mambo za Kampeni zianze nimegundua na kuamini kuwa huyu ndio Jembe

Kwenye sentensi ya pili Diamond akaandika >>> ‘Nitakuandikia na kukupostia ushahidi kukuthibitishia kwanini nimeona John Magufuli Pombe ndie anaefaa… unapohisi na wewe una fact za kumtetea umtakaye karibu uniambie hapo halaf na mi nikumwagie zangu, ila usijisumbue Matusi coz hayatokusaidia wala kunisaidia kunibadilisha akili yangu kwa sababu sanasana ntakuona Huna akili Maana nishayazoea, nipe fact zako nami nikupe zangu ili pamoja Tujenge nchi….. #HapaKaziTu #Ccm

Viewing all 104808 articles
Browse latest View live


Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>