Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Diamond Azidi Kukata Watu Kidomo.... Ashinda tuzo mbili za African NAFCA

$
0
0
Diamond Platnumz anaendelea kufanya vizuri kimataifa baada ya kuibuka mshindi wa tuzo mbili za African NAFCA.

Muimbaji huyo ameshinda vipengele vya msanii wa mwaka anayependwa pamoja wimbo wa mwaka unaopendwa ‘Nana’ aliomshirikisha Flavour.

Kupitia Instagram, Diamond ameandika:

I would love to say thank you to everybody who Voted for me on @africannafca Awards…am so grateful, i wouldn’t have Made it without you…hare are our Trophies….i will always make sure i work hard to make My Africa Proud..also wanna Thank @africannafca for keep Supporting African talents….please, don’t forget to Vote for me on @MtvEma awards.

Wafanyakazi waliofichua ukweli kuhusu kikao cha Dr. Slaa Serena Hotel wafukuzwa kazi

$
0
0
Kama mnavyokumbuka mwezi huu tarehe 1 aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema Dr Slaa aliitisha kikao cha waandishi wa habari pale Serena Hotel, ambapo mkutano huo ulirushwa LIVE na vituo vya televisheni vipatavyo vitano na radio kadhaa nazo zikarusha mkutano huo moja kwa moja.

Katika mkutano huo alitangaza rasmi kujivua Ukatibu Mkuu wa Chadema na uanachama pia wa Chama hicho na kueleza kuwa anastaafu kabisa shughuli za siasa na kwa hiyo akaeleza kuwa hana nia ya kujiunga na chama chochote cha siasa.

Hata hivyo katika kikao hicho ambapo alitumia zaidi ya saa 1 kuongea ambapo alikitumia kikao hicho karibu chote kuporomosha mashambulizi mfululizo kwa chama chake cha Chadema na vyama vinavyounda Ukawa na kumshambulia Edward Lowassa kwa nguvu zake zote na kumuita fisadi mkubwa na kukilaumu chama chake kwa kumpokea Lowassa na kupewa fursa ya kugombea Urais kwa tiketi ya chama cha Chadema kuwa ni sawasawa na kukihamisha choo kutoka chumbani na kukipeleka sebuleni.


Baada ya kikao hicho kwisha kesho yake ikatumbukizwa clip kwenye mitandao ya kijamii ambapo mfanyakazi mmoja wa kike wa Hoteli hiyo aliyatambulika kwa jina la Neema alisikika akielezea namna kikao hicho kilivyoandaliwa na kugharimiwa gharama zote na KITENGO na namna Dr Slaa alivyokuwa amepangiwa chumba katika Hoteli hiyo na KITENGO siku moja kabla na kuwa siku hiyo kabla ya kufanyika kikao hicho Dr Slaa alilala hotelini hapo akiwa na 'mchumba' wake Josephine Mushumbusi.

Dada huyo jasiri na shujaa aliendelea kueleza kwenye clip hiyo namna watu wa KITENGO wakishirikiana na idara ya usalama wa Hoteli hiyo ambavyo walikuwa wakimuingiza kwa kificho hotelini hapo Dr Slaa na mkewe pamoja na Dr Mwakyembe ambaye alikutana na Dr Slaa na kuongea naye kwa masaa matatu kabla ya kikao chake hicho na waandishi wa habari kwa kupitia 'mlango wa nyuma' ambao kwa kawaida hutumika tu na wafanyakazi wa Hoteli hiyo.

Taarifa ambazo zimepatikana ni kuwa Mfanyakazi huyo Neema pamoja na Afisa Mkuu wa Usalama wa Hoteli hiyo pamoja na Msaidizi wake upande wa Usalama, tayari wamashafukuzwa kazi kwa 'maagizo' toka mamlaka za juu za nchi yetu.

Inasemekana pia kuwa wafanyakazi hao hawakupewa hata fursa ya kutoa utetezi wao kwa tuhuma hizo kwenye kikao cha Nidhamu kama ilivyo utaratibu wa kawaida wa Hoteli hiyo na ambavyo pia ni kinyume kabisa cha principle kuu ya Natural Justice ya right to be heard.

Hivyo basi kutokana na taarifa hizo za kutimuliwa kwa wafanyakazi hao kujulikana hivi sasa upo umuhimu mkubwa wa wakereketwa wa haki za binadamu,viongozi wanaounda muungano wa Ukawa na wananchi wengine kwa ujumla wao kulifuatilia kwa karibu suala hilo na kuhakikisha kuwa uonevu huo uliofanywa na serikali hii ya Sisiem dhidi ya wafanyakazi hao unakomeshwa na wafanyakazi hao warejeshwe kazini.

Lowassa Amvunja Miguu Magufuli...Apata Mapokezi Makubwa yakushangaza Jimboni Kwa Magufuli Chato

$
0
0
Ukitaka kujuwa Magufuli ni mzigo kwa Ccm ni mkutano Lowassa aliofanya Chato leo.
Watu hawamtaki magufuli kila mtu lowassa na mabadiliko.
Ina maana kama Lowassa amepata ushindi mkubwa namna hii nyumbani kwa Pombe nani tena wakumzuia asiingie ikulu.

Sheria ya Makosa Ya mtandao yanasa watano Ambao Hutengeneza Message FEKI Za Wanasiasa

$
0
0
Kamanda Kova
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linawashikilia watu watano kwa tuhuma za kutumia vibaya mitandao ya kijamii kufanya uhalifu wa  kutengeneza habari za uongo na uzushi dhidi ya viongozi au watu maarufu.

Akizungumza  na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleimani Kova alisema watu hao wamekuwa wakitumia vibaya majina ya watu maarufu hasa wanasiasa.

Kova alitaja majina ya wanasiasa yanayotumiwa vibaya kuwa ni mgombea ubunge Jimbo la Kibamba, John Mnyika na mgombea urais wa Chadema chini ya mwamvuli wa Ukawa, Edward Lowassa na wakuu wa vyombo vya ulinzi na  usalama.

Aliwataja watuhumiwa hao, kuwa ni Joel Lumbay (32), Omar Suleiman wote wakazi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Michael Nickson (32) mkazi wa Tegeta, Patrick Natala  na Maxmillian Msacky wakazi wa jijini Dar es Salaam.

Alisema watu hao, wamekuwa wakituma ujumbe mbalimbali  wakionesha viongozi hao walikuwa wanajadili jambo fulani dhidi ya kundi au chama  kingine cha siasa kwa kutumia mitandao.

“Wana tabia ya kutengeneza ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwa lugha iliyozoeleka kama ‘kuchati,’  lakini mawasiliano hayo hayapo… yanakuwa yametengenezwa ili kutimiza malengo yao. Jambo hili ni kosa la jinai na linaweza kuchochea chuki  katika makundi ya watu,” alisema Kova.

Alisema jeshi hilo linaendelea kuwasaka watu hao kwa kushirikiana  na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

“Kiongozi  au mtu yeyote atakayeona  ameathirika na mbinu  chafu za kihalifu  asisite kutoa taarifa kwa vyombo  vya dola ili hatua za kisheria zichukuliwe mara moja,” alisema.

Mitambo ya Kuzalisha Umeme wa gesi Yawashwa.....Tatizo la Umeme Kukatika Kuisha LEO.

$
0
0
Mitambo ya Tanesco
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema kazi ya kuunganisha mabomba ya gesi kutoka Kinyelezi I kwenda katika mitambo ya Ubungo I na II, jijini Dar es Salaam imekamilika.

Aidha, kazi ya kuwasha mashine 10 za mtambo wa Ubungo I imekamilika na  inategemewa tatizo la kukatika umeme litafikia tamati kuanzia leo.

Akizungumza na mtandao huu jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Uhusiano wa Tanesco, Adrian Severin, alisema kazi ya kuwasha mitambo hiyo inahitaji umakini mkubwa  kutokana na mfumo unaotumika kuwa mpya.

Alisema kazi ya kuunganisha mabomba ya gesi imekamilika na tatizo lililokuwapo la kukatika umeme lilitokana na matengenezo ya mfumo mpya yaliyokuwa yakiendelea kwa ajili ya kuwashwa kwa mitambo hiyo mipya.

Aliwataka wananchi wawe na subira wakati kazi hiyo ikiendelea na hadi kufikia leo itakuwa imekamilika na umeme utapatikana kwa uhakika baada ya kuanza kuzalishwa kwa kutumia gesi kutoka Mtwara.

 “Kuanzia leo (jana) umeme umeanza kurudi kupatikana kwa uhakika katika mikoa mbalimbali pamoja na jiji la Dar es Salaam kutokana na mafundi kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwasha genereta 10 za Ubungo I, hivyo mpaka kesho (leo) uzalishaji umeme utakuwa umeongezeka,” alisema na kuongeza:

“Watanzania wategemee umeme wa uhakika baada ya kuanza kuzalisha umeme wa gesi ya Mtwara kwani  kazi ya kuunganisha bomba la kusafirisha nishati hiyo imekamilika hivyo inatuhakikishia nchi kuwa na umeme wa uhakika hata kama mabwawa ya maji yanayotumiwa kuzalisha umeme yatakuwa yamekauka.”

Severin alisema gesi ya kutoka Mtwara inategemewa kuendesha mtambo wa Ubungo II wenye uwezo wa kuzalisha MW 105, mitambo ya Symbion MW 112 na Kinyerezi I, MW 150).

Alisema mtambo wa Ubungo I utaendelea kuzalisha umeme kwa kutumia gesi ya Songosongo na kwamba Ubungo II ndiyo utumia gesi ya Mtwara kwa kuwa inatosha kuendesha mitambo hiyo.

Severine alisema uzalishaji wa umeme kwa kutumia gesi utaisaidia serikali kuokoa takribani dola za Marekani bilioni moja kwa mwaka, ambazo zilikuwa zinatumiwa kununua mafuta mazito ya kuzalisha

What is Wrong with these Hon. Lowassa’s Pictures which went viral on social media?

$
0
0


Guys what’s wrong with these Hon. Lowassa’s Pictures which went viral on social media?


Mchezaji wa Yanga Canavaro Kuchukuliwa Hatua za Kinidhamu Baada ya Kupiga Picha na Jezi ya Yanga Kuonyesha Akimsupport Magufuli

$
0
0
Headlines za uchaguzi mkuu 2015 bado zinazidi kuchukua nafasi, tumekuwa tukiona watu maarufu kama wasanii wa filamu na Bongofleva wakionyesha hisia zao kwa wagombea wawapendao. Ila kwa wachezaji mpira wa miguu ni tofauti kidogo kulingana na sheria za vilabu vyao pamoja na mikataba yao.

Baada ya kuonekana kwa picha ya nahodha wa klabu ya Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Nadir Haroub Cannavaro akimsuport moja kati ya wagombea Urais wa mwaka 2015, kumekuwa na stori nyingi sana kuhusiana na sheria ya wachezaji kuonesha hisia zao kwa vyama wavipendavyo hususani wakiwa wamevaa jezi za vilabu vyao.

katibu mkuu wa Yanga Dk Jonas Tiboroha Kazungumza kuhusiana na Cannavaro kuvaa jezi za Yanga na kupiga picha akionyesha hisia zake kwa mgombea huyo.

Mimi nafikiri Cannavaro angekwenda akiwa amevaa nguo zake za kawaida na kuonyesha kumsuport Magufuli au mwingine isingekuwa na tatizo. Sisi tunachozungumzia ni yeye kuvaa jezi ya klabu na yenye nembo ya mdhamini wetu halafu unaonyesha kushabikia siasa, Cannavaro amekosea hivyo kama klabu tumekaa chini na tutaangalia hatua za kinidhamu zipi zichukuliwe

Utafiti wa CCM kwamba Magufuli Anaongoza kwa 69.3% Unapingana na Uhalisia Uliopo...

$
0
0
January Makamba Akiongea na Waandishi wa Habari
Nimekuwa nikifuatilia hali halisi ya mwamko wa kisiasa katika sehemu mbalimbali nchini, mijini na vijijini hata katika mitandao ya kijamii na kujionea jinsi UKAWA ikiungwa mkono na watu wengi mno.

"Utafiti wetu wa ndani, tulioufanya kwa kipindi cha siku kumi zilizopita katika majimbo 246 kati ya majimbo 269, unaonyesha kwamba Dr. Magufuli atapata ushindi wa asilimia 69.3 Tunaamini kwamba asilimia hizi zitaongezek kadri Watanzania wengi zaidi wanavyopata fursa ya kumsikiliza Dr. Magufuli na kusikiliza Ilani na sera za CCM"

inaonekana utafiti huu ulifanyika katika majukwaa ya kampeni za CCM kwa sababu matokeo yao yanapingana na hali halisi zikiwemo tafiti za maoni kupitia mitandao mbalimbali, kama vile


Inaonekana utafiti huu ulifanyika katika majukwaa ya kampeni za CCM kwa sababu matokeo yao yanapingana na hali halisi zikiwemo tafiti za maoni kupitia mitandao mbalimbali, kama vile

1. Poll - EasyPolls.net

2. Online Pre-election Polling, 2015 Tanzania Election : Open Discussion Forums

3. VOTE ONLINE FOR TANZANIA PRESIDENT | #VOTE4TPO | Mayocoo , Special Voting portal

Ninaamini uchaguzi ukifanyika leo CCM haiwezi kupata kura zaidi ya 25%.

By Simplicity/JF

Ujue Ukweli wa Edward Lowassa Kukimbia Midahalo ya Urais

$
0
0
Lowassa na Magufuli
Vyama vyote vya siasa vimekubali kufanya mdahalo wa wagombea wa Urais kwenye vyombo vya habari lakini vyama vinavyounda UKAWA vimekataa kushiriki kwenye midahalo hiyo kwa kutoa sharti moja la kutomshirikisha mgombea wao na badala yake waende wenyeviti wa vyama.

Utaratibu wa dunia nzima kwenye midahalo wanahudhuria wagombea na siyo wenye viti wa vyama... Yaani Rais Kikwete aache majukumu yake ikulu halafu aende kwenye vyombo vya habari kufanya midahalo wakati kwenye midahalo wanazungumzia sera za chama husika na sasa aliyebeba sera za CCM ni Ndugu Magufuli.

Baada ya kufanya uchunguzi sababu zifuatazo zimebainika kuwa ndiyo vigezo vya kumfanya mgombea wa UKAWA ndugu Lowassa kususia midahalo hiyo
1. Afya yake ni dhaifu na haimruhusu kukaa muda mrefu bila kupewa dawa ya kumuongezea nguvu. kwenye mikutano yake ya kampeni hajawahi kuzungumza zaidi ya dakika 15, sasa atawezaje kuhudhuria mdahalo akaongea zaidi ya nusu saa?

2. Amehusika sana kwenye kashfa nyingi za ubadhilifu wa mali za umma na hana uwezo wa kukataa ukweli huo, hata alipoulizwa na waandishi wa habari huko Dodoma alikataa kulijibu hilo swali, na endapo atahudhuria kwenye mdahalo wowote hilo swali hawezi kuliepuka

3. Chama chake hakina sera nzuri, anakosa kitu cha kuongea awapo mbele ya watu kwakua chama chake hakijaandaa ilani nzuri yenye sera za kumkomboa Mtanzania. Wakati wenzake wanatoa sera za kupunguza gharama za ujenzi yeye anamwaga sera za kuwatoa jela akina Babu Seya na kubomoa nyumba za nyasi nchi nzima kwa muda wa siku 100

By Aisha Idd

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Tarehe 17....Wema Uso kwa Uso na Zari Akubali Mwaliko Aliopewa na Mama Diamond...

$
0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Tarehe 17....Wema Uso kwa Uso na Zari Akubali Mwaliko Aliopewa na Mama Diamond...





















Aunt Ezekiel: Nina Haki ya Kuhama Chama

$
0
0
MWIGIZAJI mahiri wa filamu nchini, Aunt Ezekiel, amedai kutishiwa amani baada ya kufanya maamuzi yake kisiasa ambapo amehamisha ushabiki wake kutoka chama kimoja na kwenda chama kingine.

Licha ya mrembo huyo kudai kupokea vitisho mbalimbali, pia alidai amehama chama hicho na kujiunga na kingine

kutokana na kukubali sera za chama hicho.

“Sera za chama nilichohamia zimenivutia na wala sikulazimishwa na mtu wala sijapokea fedha wala gari kuhamia

huko kama inavyosemekana, bali nafsi na mapenzi pamoja na haki yangu ndiyo yaliyonipeleka huko.

“Nashangaa maamuzi yawe yangu bado watu wanitumie jumbe za vitisho, mimi ni raia kama walivyo wengine,

umaarufu wangu usiwe sababu,” alisema Aunt, ambaye awali alikuwa akivaa magwanda yanayoaminika kuwa jezi ya chama alichokihama

Chanzo:Mtanzania

Magufuli Aibuka na Msemo wa UKAWA....Adai M4C ni ‘Magufuli for Change’

$
0
0
John Magufili Katika Kampeni
Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli amesema maana na neno M4C, linalotumiwa na Chadema ni "Magufuli for Change” akimaanisha ndiye atakayeleta mabadiliko.

Dk Magufuli alitoa kauli hiyo jana katika Kata ya Nguruka, Jimbo la Kigoma Kusini mkoani Kigoma, alipohutubia mkutano wa hadhara wa kampeni ambapo aliwabeza wapinzani kuwa hawawezi kurudi kwa wananchi kuangalia shida zao.

Mkiangalia hizi picha za wagombea, mimi nimevaa shati, mwingine amevaa suti. Sasa huyu mwenye suti anaweza kukubali kuja kupata shida na nyinyi huku?” alihoji na kuongeza:

Wanasema M4C, mnajua maana yake?” aliuliza mgombea huyo na kujibu mwenyewe, “maana yake ni ‘Magufuli for Change’.

Katika mkutano huo, mgombea huyo alimtaka mgombea ubunge wa chama hicho katika jimbo hilo, Hasna Mwilima amwachie matatizo ya jimbo hilo ayashughulikie mwenyewe.

Matatizo yanayowakabili wananchi wa jimbo hilo ni bei ya tumbaku, kukosekana kwa umeme na maji na upandishaji hadhi kituo cha afya cha Nguruka kuwa hospitali ya Wilaya ya Uvinza.

Dk Magufuli alisema kazi ya kwanza atakayompa waziri wake wa kilimo, itakuwa ni kutafuta soko la zao la tumbaku kwa mikoa ya Tabora na Kigoma ili wananchi wauze kwa bei nzuri.

Mchagueni Hasna Mwilima ili akawawakilishe bungeni, lakini kwa matatizo haya niachieni mimi. Haiwezekani mpaka sasa Nguruka hamna umeme,” alisema mgombea huyo.

Akiwa katika Jimbo la Kigoma Kaskazini, alimtambulisha mgombea ubunge wa jimbo hilo, Peter Serukamba na kuwataka wananchi kumchagua ili akashirikiane na Serikali yake bungeni.

Lakini ilipofika zamu ya mgombea ubunge wa jimbo la Kigoma Mjini, Dk Amani Kabourou, hali ilibadilika na kutokea minong’ono ya wananchi kama ishara ya kumkataa pale alipopewa nafasi ya kuwasalimia.

Dk Kabourou alianza kuzungumzia mipango yake endapo atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa mara nyingine, hata hivyo wananchi walisikika wakisema ‘hapana, hapana’ huku wakinyoosha mikono juu kuonyesha ishara ya kumkataa mgombea huyo.

Wakati Dk Magufuli alipojaribu kumnadi mgombea huyo, wananchi walianza tena kupiga kelele, wakisema ‘hatumtaki...’ jambo lililomfanya Dk Magufuli kutomwombea kura na kuendelea kuzungumzia mambo mengine.

Ray Awapa Makavu UKAWA

$
0
0
Vincent Kigosi ‘Ray’ 
Staa wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ ameendelea kushusha maneno kwa chama kinachounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) baada ya kufunguka hadharani kuwa hawakuwa na sera ambazo zingemfanya aendelee kubaki.

Staa huyo ambaye kwa sasa amerudi Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema kurudi kwake CCM hakumaanishi kama amehongwa kama watu wanavyoendelea kusambaza habari hizo bali amekwenda kutokana na kuvutiwa na sera.

“Naomba nieleweke kuwa dhamira yangu ya kubaki Ukawa ndiyo ilikuwa ikinisuta. Nikiwa kama mmoja wa wasanii, nimevutiwa na sera za CCM hasa kwa upande wa wasanii ambapo Mgombea Urais, Magufuli (John Pombe) alisema moja ya sera zao ni kujali maslahi kwa wasanii na kuwafungulia mfuko maalum utakaowashughulikia,” alisema Ray.

LOWASSA: Asanteni Chato Kwa Mahaba Yenu.....Mnanifanya Nideke

$
0
0
Mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, anayeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Watanzania (Ukawa), ameipenya ngome ya mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, wilayani kwake Chato na kupata mapokezi makubwa.

Mkutano wa jana ulikuwa wa kwanza kufanyika mjini hapo akiwa ametokea Morogoro, mkutano mwingine aliufanya mjini Geita.

"Nikiutazama huu umma nashtuka sana, hapa ni nyumbani kwa Magufuli. Wazanzibari wanasema haya ni mahaba nami nayapokea. Mnanifanya nideke na hapa ni nyumbani kwa Magufuli, watakaonipa kura wanyooshe mikono juu...mikono namna hii inanipa faraja, nimepokea mahaba yenu," alisema Lowassa.

Akizungumzia matatizo elimu Chato alisema atapiga marufuku michango ya wanafunzi na kuanzia Januari watoto wote watasoma bure na elimu bora.

Alisema hatasahau kilimo na akasema wakulima wataruhusiwa kuuza mazao yao popote wanapotaka bila kubugudhiwa.

Alisema atahakikisha pia wakazi wa Chato wanapata maji toka Ziwa Victoria kama alivyowafanyia wakazi wa Mkoa wa Shinyanga ambao wanapata maji toka ziwa hilo.

Aidha, alisema atafufua kiwanda cha kuchambua pamba kichopo wilayani hapa ambacho kimekufa wakati wa CCM.

Wakazi hao walimuahidi kura za ndiyo na kumuangusha Dk. Magufuli mapema asubuhi Oktoba 25, mwaka huu.

Alifanya mkutano huo katika eneo la stendi ya zamani ya mabasi mjini hapa jana.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, alisema wapinzani hawana nia ya kuleta vita na vurugu.

"Sisi hakuna vita, tutawaondoa CCM kwa amani kabisa," alisema na kuongeza: "Chini ya CCM hakuna maendeleo."

Aidha alimtaka Dk. Magufuli kutoka CCM kama anaona kitanda chao kina kunguni na yeye hawezi kukilalia.
Mapema Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, alisema yupo tayari kurudi tena mahabusu ya Segerea tena na tena hadi Oktoba 25, mwaka huu.

Alisema lengo la serikali kumbambikia kesi na kumnyima dhamana, ilikuwa ni kuwatisha wananchi ili wakiona waziri mstaafu kama yeye anapelekwa mahakamani na Segerea, watishike na kuingiwa na woga zaidi ili waachane  na Ukawa.

"Lengo lilikuwa watu waone mimi kama waziri mstaafu na mwanasheria maarufu nimefunguliwa mashitaka, wananchi waogope kujiunga na Ukawa," alisema.

Aliwaomba wakazi wa hapa hata kama wanaipenda CCM kukumbuka hali itakavyokuwa kwa watoto wao chini ya CCM.

Alisema wakumbuke pale wanapokwenda hospitali na kukosa dawa, watoto wao kukosa elimu na ajira, hivyo matatizo hayo yawafanye kuachana na CCM.

Alisema serikali atakayoiunda Lowassa itakuwa na uwezo mkubwa wa kuongoza kuliko ilivyo kwa Serikali hii ya CCM.

Alisema Dk. Magufuli haijui CCM kwa sababu hajawahi kuwa hata balozi wa nyumba kumi, hivyo hawezi kuwa kiongozi.

Alisema alijiunga na CCM mwaka 1991, lakini akiikumbuka CCM ya wakati huo na hii iliyoshika dola sasa, hazifanani kabisa.

"Kilichobaki kwa CCM hii ya sasa ni rangi ya kijani, alama ya rangi ya njano za jembe na nyundo, basi.

"Hiki siyo tena chama cha wakulima na wafanyakazi, ni chama kilichokosa maadili ya uongozi kiasi cha kuwasafisha watuhumiwa wa Escrow na Epa.

"Ilifikia hatua sisi nafsi zetu zilitusuta, nikiwa nawaangalia watoto wangu nilikuwa napata uchungu kuhusu hatma yao chini ya dola ya CCM,"alisema.

Bila kuwataja majina, alisema CCM imewapitisha baadhi ya wanachama  wao waliokuwa wakituhumiwa na ufisadi wa Escrow na EPA kugombea ubunge.
Kwa upande wake, Richard Tambwe Hizza, alisema huu ni mwaka ambao Mungu ametaka Lowassa awe rais.

Alisema Ukawa wana uwezo wa kuwaletea wananchi maendeleo tofauti na CCM.

'Mkitaka kujua CCM ni watu wa ovyo, mliona jinsi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wote walivyoimba, 'Tuna imani ni Lowassa, lakini Rais Jakaya Kikwete, hakutaka kuwasikiliza," alisema.

Aliwataka wananchi wasigombane huko mitaani bali waelimishane.

Alisema hawawezi kuwaacha Watanzania wakiwa katika hali mbaya namna hii.

Alisema amezunguka nchi hii na kuona jinsi watu wanavyomkubali Lowassa utadhani walikuwa wanaishi nyumba moja.

"Mwaka huu Nyerere atafufuka na kumshuhudia Lowassa akiapishwa kuwa rais," alisema.

Alisema wananchi watakaoipigia kura CCM Oktoba 25, atatakiwa kujipima kwa kwenda hospitali.

Katika hatua nyingine, aliyejitambulisha kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Tanzania Wilaya ya Chato, Lucas Michael, alipanda jukwaani na kusema katika Halmashauri ya Wilaya ya Chato, ndiyo pekee ambayo walimu wanalazimika kujinunulia chaki.

Alisema walimu wilayani humo wananyanyasika na hata walimu wastaafu wanashindwa kurudi makwao baada ya halmashauri kushindwa kuwapatia fedha za nauli.

Aliwataka walimu wenzake mbali na kufundisha popote walipo wasiwe waoga, wawafundishe wanafunzi ukweli.

"Walimu kokote kule mliko kafanyeni uamuzi sahihi, bila woga na wakati ndiyo huu wa kufanya maamuzi ya mabadiliko," alisema.

Mgombea ubunge wa Jimbo la Chato, Dk. Benedickt Lukanima, alimweleza Lowassa kuhusu matatizo ya maji ingawa wana ziwa, matatizo ya elimu bora kwa watoto wao na dawa hospitalini.

Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, alisema wamekubaliana na wenzake kurudi tena hapa kuzungumza mambo ya Chato.

Hata hivyo, wananchi walipaza sauti zao wakimtaka azungumze wakati huo naye akasema, namna pekee ya kuing'oa na kuizika CCM ni lazima ianzie hapa Chato.

"Ili nchi hii  iishi, tunahitaji kuizika CCM na mahali pa kuanzia ni hapa Chato," alisema.

Huku baadhi ya vijana wakiwa wanapitisha mfano wa jeneza lililokuwa limezungushwa bendera ya CCM, Lissu alisema Ukawa wamekuwa wakipata matusi na kejeli nyingi na namna pekee ya kuiondoa madarakani ni kumng'oa Dk. Magufuli na kuizika CCM.

Watu Kelele Fisadi Fisadi Richmond Richmond. Ninajiuliza Kwani Kazi ya TAKUKURU au PCCB ni Nini? Mbona Hakamatwi

$
0
0
Fisadi
Watu kelele fisadi fisadi Richmond Richmond. Ninajiuliza kwani kazi ya TAKUKURU au PCCB ni nini? Nilidhani baada ya ripoti ya Mwakyembe hawa PCCB wangeifanyia kazi kuweza kufungua mashtaka. Kama chombo kama hiki akijaona umuhimu huo ufisadi ni upi? Serikali ni ile ile ya awamu ya nne na bado ina muda wa kuhakikisha wanatumia chombo chao PCCB kupata ukweli wa Richmond mbona nayo imekaa kimya? au inaamini hakukuwepo na wizi wa kodi za wananchi? Watanzania tusichanganywe na vitu visivyo na ushahidi wa kutosha au ushahidi butu. Nadhani neno ufisadi au Richmond ni lugha ya kampeni kama ilivyokuwa "Maisha bora kwa kila Mtanzania". Achana nao wanaosema ni fisadi sikiliza Sera chagua kiongozi anayekufa. ##‪#‎Kiona‬ Mbali***

Kwa Wanaume: Usithubutu Kumsomesha Mke, Mchumba Ama Mpenzi

$
0
0
Kusomesha ni jukumu la mzazi, sio mume, mchumba au boyfriend. Kozi pekee wanayotakiwa kusomeshwa hawa wenzetu ni cookery (mapishi), driving kwa ajili ya kuendesha lile gari la mkopo apeleke watoto shule na kuendea sokoni na sayansi kimu tu, zingine unajitafutia presha.

Wengi wamelizwa huko vyouni, wanakutana na watu wa kila aina kuanzia serengeti boys mpaka veterans wa mapenzi wenye hela zao na wanaojua Kujali...Msichana Atajifanya Mgumu Mwaka wa kwanza tu akishazoea ni Mteremko wa Kitonga hasa wake za watu, wengine ndio dharau zinaanzia hapo na ndoa au penzi kuisha.

Mwenye masikio na asikie na Mwenye Kubisha hili aje Hapa...

By Mdukuzi

Jengo Refu zaidi kuliko yote Afrika Mashariki Limefunguliwa Jijini Dar na Rais Kikwete

$
0
0
Jengo refu zaidi lililokamilika Afrika Mashariki na Kati lazinduliwa nchini Tanzania.

PSPF Towers ni moja ya majengo machache marefu barani Afrika na ndiyo jengo refu zaidi lililokamilika Afrika Mashariki na Kati, likiwa na urefu wa mita 147.

Majengo mengine marefu Afrika ni Carlton Centre (mita 223) lililopo Afrika Kusini, Hassan II Mosque (mita 210) lililopo Moroko, Ponte City (mita 173) lililopo Afrika Kusini, Necon House (Mita 160) lililopo Nigeria, Marble Tower (mita 152), Pear dawn (mita 152), Pear dawn (mita 152), Met Life Centre (mita 150) na 88 on field (mita 147) yote ya Afrika ya kusini.

Jengo hilo lililozinduliwa na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, ujenzi wake ulitumia miaka minne tangu mwaka 2011 hadi 2015 limegharimu shilingi bilioni 139.20 za Tanzania lina maeneo ya ofisi na nyumba za makazi 88. Pia katika jengo hili kuna sehemu ya mgahawa, mabenki, bwawa la kuogelea, Sehemu za kufanyia mazoezi, maegesho ya magari na sehemu nyingine muhimu.

Kudumu kwa rekodi ya urefu ya PSPF Towers lenye minara miwili na ukubwa wa mita za mraba 73,000, kutategemea kukamilika kwa majengo mengine yanayochipua kwa kasi katika Afrika.

Serikali Yakanusha Rais Kikwete Kutumia Shilingi trilioni 4 kwa ajili ya Safari za Kikazi nje ya nchi uongozi wake wa miaka 10

$
0
0
Kikwete
Wizara imesikitishwa na taarifa za uongo zilizotolewa katika vyombo vya habari kuwa Mhe. Jakaya Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uongozi wake wa miaka 10 ametumia Shilingi trilioni 4 kwa ajili ya safari za kikazi nje ya nchi, ambazo ni wastani wa bajeti nzima ya wizara kwa miaka mitano (5).

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inapenda kutoa ufafanuzi kuwa tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete aingie madarakani mwaka 2005, kiasi kikubwa kabisa cha bajeti kuwahi kutengwa kwa ajili ya safari za Viongozi Wakuu yaani Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu ni shilingi bilioni 50 ambazo zilitengwa kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015 kwa ajili ya Idara ya Itifaki. Kwa miaka mingine yote wastani umekuwa ni kati ya shilingi bilioni tano hadi 25 kulingana na mahitaji ya idara hiyo.

Ifahamike kuwa kiasi hicho cha shilingi bilioni 50 ni bajeti nzima ya Idara ya Itifaki, ambapo kuna fungu maalum kwa ajili ya ziara za viongozi. Fungu hilo linagharamia makundi makuu matano kama ifuatavyo:

1.Kundi la Rais wakiwemo Wasaidizi, Mawaziri au Wakuu wa Taasisi na Walinzi;
2.Kundi la Makamu wa Rais wakiwemo Wasaidizi, Mawaziri au Wakuu wa Taasisi na Walinzi;
3.Kundi la Waziri Mkuu wakiwemo Wasaidizi, Mawaziri au Wakuu wa Taasisi na Walinzi;
4.Kundi la Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka nje ya nchi wanapotembelea Tanzania; na
5.Kundi la Wajumbe Maalum wanaokuja nchini kuleta taarifa muhimu kwa Rais.

Makundi yote haya hugaramiwa na Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje ndani ya bajeti ya Idara ya Itifaki kifungu cha Ziara za Viongozi.

Aidha uandaaji wa bajeti ya Wizara chini ya Idara ya Sera na Mipango unahusisha wadau wengine nje ya Wizara kama vile Kamati ya Bunge ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na hupitishwa kila mwaka na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tunapenda kuwaatahadharisha wananchi juu ya watu wanaotoa taarifa za uongo kwa madhumuni ya  kujenga chuki dhidi ya Serikali.  Ikumbukwe kuwa ziara za viongozi zinazoratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje zina mafanikio makubwa kwa nchi na Watanzania kwa ujumla.

Wizara inaandaa taarifa  ndefu ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara, changamoto na mafanikio yaliyopatikana ndani ya kipindi cha miaka kumi ya uongozi wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambayo itatolewa kwa umma kwa lengo la kutoa elimu zaidi.

MWISHO.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
17 Septemba 2015

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa...Ikiwemo ya Lowassa Kudaiwa Kukodi Makomando wa Israel

Baada ya Kuwa Mpweke Muda Mrefu Penny Aibuka na Kusema Akipata Mwanaume Bora Anazaa Soon

$
0
0
Penniel Mingilwa ‘Penny’
Na imelda mtema
Hosti wa Kipindi cha Bongo Star Search, Penniel Mingilwa ‘Penny’ amefunguka kuwa suala la kupata mtoto lipo kwenye akili yake lakini litatimia tu endapo atapata baba bora.

Akizungumzia maisha yake ya kimapenzi kwa sasa Penny alisema kuwa, hawezi kuyaanika kwa sasa ila ukweli ni kwamba hamu ya kuitwa mama anayo na anaamini akimpata mwanaume sahihi anayeweza kumudu jukumu la kuwa mzazi, atazaa na kuyaacha maisha yaendelee.

“Kwa maneno haya mtu anaweza kudhani nabagua lakini ninachotaka mimi ni kuwa na baba wa mwanangu anayejua maana ya familia nisije kumuumiza mtoto wangu bure,” alisema Penny.
Source:GPL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images