Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live

Mzee Kingunge Ngombale Mwiru Amekishukia Chama cha CCM...Adai ‘Kimechanganyikiwa’.

$
0
0
Aliyekuwa kada mkongwe wa CCM, mzee Kingunge Ngombale Mwiru amekishukia chama chake hicho cha zamani na viongozi wake wa sasa kwa madai kuwa ‘kimechanganyikiwa’.

Akiongea leo katika mkutano wa kufunga kampeni za vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa baada ya kumnadi mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa, Mzee Kingunge alidai kuwa mwenendo wa kampeni na matamko ya viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho huku akitoa mfano wa lugha kali pamoja na matusi yaliyotumika kwenye majukwaa ya kampeni.

Mzee Kingunge alimsihi Rais Jakaya Kikwete kutotumia nguvu ya dola kuzuia sauti ya wananchi walio wengi ambao alidai wameamua kumuingiza Ikulu Edward Lowassa.
 
Alimshauri Rais Kikwete kujipanga kukabidhi kwa amani madaraka kwa mgombea urais atakayeshinda ambaye anaamini ni Lowassa kama alivyokabidhiwa nafasi hiyo kutoka kwa rais wa serikali ya awamu ya tatu, Benjamin Mkapa.

“CCM imekuwa na utaratibu wa kukabidhi madaraka kwa amani, Mwinyi alimkabidhi madaraka Mkapa kwa amani, Mkapa naye alimkabidhi yeye kwa amani, sasa nay eye afanye hivyo.”

Alisema kuwa kuna dalili kwamba Rais Kikwete anataka kuyapinga matakwa ya wananchi walio wengi kwa kuchakachua matokeo na kufanya hujuma kwenye mchakato wa uchaguzi kwa kutumia nguvu ya dola hivyo akamsihi aache kwa kuwa ataliingiza taifa kwenye machafuko.

Mwanasiasa huyo mkongwe alionesha kusikitishwa na kauli zilizotolewa na Rais Kikwete kwa kuwachukulia wapinzani kama ‘adui’ na kwamba wapigwe. Alisema mchezo wa siasa ni ushindani na sio uadui.

Mzee Kingunge aliwakumbusha wananchi kuwa mwalimu Nyerere aliwahi kumtangaza adui wa Tanzania anayefaa kupigwa kuwa ni Idd Amin na sio wananchi wa Tanzania.

“Nyerere alikaa na wazee wa Dar es Salaam, akasema tumpige adui Idd Amin, akatangaza apigwe na kweli tukampiga,” alisema na kudai kuwa alishangaa kumsikia Rais Kikwete akitangaza kuwa wapinzania ni maadui na wapigwe.

Mzee Kingunge alitangaza kuitosa CCM na kuhamia upande wa Mabadiliko akidai kuwa viongozi wa sasa wa CCM wamepoteza dira na chama hicho kimekosa muelekeo na kimekata pumzi, hivyo hakiwezi tena kuwafikisha watanzania kwenye kilele cha mafanikio.

Haji Duni agundua janja ya CCM,waliopangwa kuchakachua matokeo watajwa

$
0
0
Mgombea Mwenza wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,Haji Duni amesema kuwa wamegundua njama iliyopangwa na Chama cha Mapinduzi CCM pamoja na Tume ya uchaguzi kwamba kura zikitoka kwenye vituo zipite kwenye mtandao na kuziiba kwa kutumia wataalamu wao wa TEHAMA.

Ameyasema hayo mapema leo wakati wa kufunga kampeni kwa vyama vinavyounda umoja huo zilizofanyika katika viwanja vya jangwani jijini Dar es Salaam

Duni  amesema kuwa CCM imetayarisha wataalam wawili ambao watafanya kazi hiyo na kwamba UKAWA watajitahidi kuweka kumbukumbu iliyosahihi ya matokeo ya kura zao zote ili kuepusha wizi unaotaka kufanywa.

Ameongeza kuwa kila wakala lazima apatiwe nyaraka ya matokeo ya kura iliyotiwa saini,

Aliwataja wataalam hao kuwa ni Mr Mkanyanga na Sesy Francis ambao ndio wamekabidhiwa kuiba kura katika kituo cha Kurasini karibu na makao makuu ya uhamiaji.

“Wakileta mchezo tutawaambia wananchi wakakizunguke alafu tutaona kama hodari ni Rais Kikwete au wananchi …..Kikwete umeambiwa ukabidhi nchi kama ulivyopewa kwa amani na akuna Jeshi linaloweza kupiagana na umma,”amesema Duni.

Kikwete: Lowassa Ndio Mhusika wa Kashfa ya Richmond

$
0
0
Akiongea leo Mwanza kwenye kufunga kampeni za ccm Mh.Jk amesema ni kweli alishiriki kwenye makubaliano ya kutafuta kampuni ya kufua umeme baada ya Mabwawa kukauka nchi, lakini hakushiriki kutafuta kampuni gani ilete umeme, hivyo hahusiki kwa namna yoyote kwa ujio wa Richmond.

Hivyo waziri Mkuu ndio mhusika mkuu wa Richmond!

Kikwete aweka wazi kuwa waziri mkuu kipindi hicho ndio muhusika mkuu kwenye Richmond, baraza la mawaziri pamoja na yeye walihusika nawalikubaliana kuwa kuna upungufu wa umeme na mitambo ikanunuliwe lakini hakuhusika kampuni gani ya kwenda kuleta hiyo mitambo .

Alisisitiza sheria za manunuzi zifuatwe lakini waziri mkuu wa wakati huo hakufata na aliunda tume ya manunuzi ya kwake mwenyewe .
 By thehunk/JF

Hali ilivyo Sehemu Mbali Mbali za Kupigga Kura..Wengi Walalamika Majina yao kutokuwepo..na Wengine Wasema Utaratibu wa Kupiga Kura Upo Slow Sana

$
0
0
Mdakuzi Wako nimetembea vituo mbali mbali maeneo ya Boko, Bunju, na Mabwepande na Wananchi Wengi walio katika vituo hivyo wamedai kuwa zoezi la upigaji linaenda taratibu sana kiasi huenda mpaka saa kumi watu wasimalize kupiga kura...pia baadhi ya wapiga kura majina yao hajaonekani ....zaidi ya hapo zoezi linaenda vizuri .....

LOWASSA Apiga Kura...Huu Ndio Mtazamo wake Baada ya Kupiga Kura...Asema Haya

$
0
0
Mgombea urais kupitia Chadema Edward Lowassa atoa mtazamo wake mara baada ya kupiga kura....

Lowassa amesema hatokubaliana na matokeo kama uchaguzi hautokuwa wa haki.

Mgombea Mmoja wa Urais 2015 Ashindwa Kupiga Kura..Sababu Hizi Hapa

$
0
0
Mgombea Urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama cha TLP Macmillan Lyimo ameshindwa kutekeleza haki yake ya msngi na ya kikatiba ya kupiga kura leo baada ya kukosekana kwa fomu namba 19 inayo mruhusu kupiga kura kwa kuwa hayupo kituo chake cha kupigia kura cha Dar es Salaam alichojiandikisha awali ambapo kwa sasa yupo jijini Arusha.

Mbali  na  kukosekana  kwa  fomu  hiyo, Mgombea  huyo  pia  hakuwa  na  kitambulisho  chake  cha  kupigia  kura

Hapa Nakuletea Kionjo cha Nyimbo ya ALI KIBA na CRISTIAN BELLA....Haki ya Hii Nyimbo ni Noma

$
0
0
Hakika Hii Nyimbo Lazima ije Kushika hasa....Yaaani hizi Sauti ni utamu mpaka kisogoni...
Bonyeza Play usikilize....

Dr. Magufuli Tayari Keshapiga Kura, Chato......Kasema Matone ya Mvua Yamemnyeshea na Hiyo ni Ishara Kwamba Atashinda

$
0
0
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Magufuli amepiga kura katika jimbo la Chato mapema asubuhi hii na kueleza kuwa amepata dalili nzuri alipofika kwenye kituo hicho cha kupigia kura.

Akiongea na waandishi wa habari baada ya kupiga kura, Dkt. Magufuli alieleza kuna dalili nzuri za ushindi kwa upande wake hasa baada ya matone ya mvua kuanza kudondoka punde alipofika kwenye kituo hicho.

Hata hivyo, Dkt. Magufuli hakutoa maelezo kuhusu matarajio yake na maoni yake kuhusu mchakato mzima wa kampeni pamoja na kutoeleza atayapokeaje matokeo ya aina yoyote.

Alito jibu la ufupi linaloashiria kuwa, “nitaeleza baada ya kuapishwa.”

Dkt. Magufuli aliwahimiza watanzania kuendelea kujitokeza kwa wingi kumchagua kiongozi wanaemtaka kwa ngazi zote za urais, ubunge na udiwani na kumtanguliza Mungu katika uamuzi wao.

“Mimi nimetimiza wajibu wagu kama raia, na nawashauri wenzangu wajihimu wakapige kura kwa kuwa hilo ndilo jukumu letu, wawachague marais, wabunge na madiwani.”

Aidha, Dkt. Magufuli alieleza kuridhishwa na mazingira ya zoezi la kupiga kura katika kituo hicho.

Rais Kikwete Naye Keshapiga Kura....Kasema Tarehe 5 Atakabidhi Nchi

$
0
0

Rais Jakaya Kikwete amesema kuwa Tarehe 5 Mwezi November 2015 atakuwa Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais ameyasema hayo alipokuwa akipiga kura leo katika jimbo la Chalinze-Msoga ambapo aliambatana na mkewe Mama Salma Kikwete 

Polisi Wavamia Kituo cha Kukusanya Matokeo ya Uchaguzi cha Ukawa na Kukamata Watu Wanaokiendesha

$
0
0
Polisi jijini hapa jana usiku walivamia kituo cha kukusanya matokeo ya nchi nzima cha Chadema kilichopo Kijitonyama na kuwakamata watu wote wanaokiendesha.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa chama hicho, Tumaini Makene alisema tukio hilo lilitokea saa nne usiku wakati vijana hao wakiendelea kukusanya matokeo hayo.

Alisema kituo hicho kilichokuwa kikiendeshwa na vijana 800 na wengine maelfu waliokuwa mikoani wakituma matokeo, kilianza kazi hiyo jana asubuhi kikilenga kukusanya matokeo yote, kuyajumlisha na kujua mshindi kabla ya matokeo ya jumla ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Kituo chetu kinafanya kazi ile ile kama inayofanywa na kituo cha CCM kilichopo maeneo ya Mlimani City, tunashangaa polisi kuwakamata watu wetu,” alisema Makene.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura alisema kwa sasa polisi wanafanya operesheni nyingi na watu mbalimbali wanakamatwa, hivyo asingeweza kujua kama watu hao pia wamekamatwa katika operesheni hiyo.



John Magufuli, Edward Lowassa Waendeleza Tambo..Kila Mmoja Adai Atashinda...

$
0
0
By Waandishi Wetu, Mwananchi
Dar/mikoani. Wagombea urais jana walikuwa miongoni mwa mamilioni ya Watanzania waliojitokeza kupiga kura, huku Dk John Magufuli wa CCM na Edward Lowassa wakiendeleza tambo za ushindi.

Baadhi ya wagombea urais walitumia haki yao ya kidemokrasia nyumbani kwao na waliobaki wapiga kura jijini Dar es Salaam.

Wakati mgombea wa CCM, Dk John Magufuli akipiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Magufuli, Kata ya Muungano mkoani Geita, mgombea wa Chadema anayeungwa mkono na Ukawa, Edward Lowassa alikuwa jimboni kwake Monduli.

Mgombea wa ACT-Wazalendo, Anna Mghwira alipiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Kibaoni mkoani Singida, huku Hashim Rungwe wa Chaumma alipiga kituo cha Shule ya Msingi Ushindi, Mikocheni B, jijini Dar es Salaam.

Fahmi Dovutwa alipiga kura eneo la Kagera, Magomeni jijini Dar es Salaam, Jankeni Kasambala wa NRA (Minazi Mirefu, KIwalani), Chief Yemba wa ADC (Buguruni), na Macmillan Lyimo TLP aliyepiga kura kituo cha Njiapanda, Vunjo baada ya kutokea sintofahamu ya kitambulisho chake cha mpigakura.

Magufuli Chato

Baada ya kupiga kura, Dk Magufuli aliwataka Watanzania kumtanguliza Mungu kwa kila jambo kwa kuwa yeye ndiye muweza wa kila kitu na kuwasisitiza kuendelea kuilinda na kuitunza amani ya nchi.

Magufuli aliyeongozana na mkuu wa mkoa wa Geita, Fatma Mwasa, mkuu wa wilaya ya Chato, Shaban Ntarambe na kamanda wa polisi wa mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo, alisema anaamini ana baraka za Mungu kutokana na kuanza kuonyesha baada ya kumaliza kupiga kura.

Kwa mujibu wa Ofisa uchaguzi jimbo la Chato, Gaston Misungwi, wananchi 186,688 wamejiandikisha kupiga kura kati yao wanawake ni 94,056 na wanaume ni 92,832 huku vituo vya kupigia kura ni 521.

Lowassa: Nitashinda

Mjini Monduli, Lowassa baada ya kupiga kura kituo cha Ngarashi, Monduli alisema ana uhakika atashinda uchaguzi na hatakubali matokeo kama kutakuwapo wizi wa kura.

Hata hivyo, alisema upigaji kura ulikuwa unakwenda vizuri katika maeneo mengi ya nchi.“Nina uhakika wa kushinda kama uchaguzi ni huru na haki na sitakubali matokeo iwapo hautakuwa huru wala haki,” alisema Lowassa aliyeambatana na mkewe Regina.

Mgombea mwenza wa Lowassa, Juma Duni Haji alipiga kura kituo cha Bwawani saa 5:30 asubuhi.

Maalim Seif

Kwa upande wake, mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Shariff Hamad alisema ni Mungu pekee yake anayefahamu kitakachotokea Zanzibar ikiwa uchaguzi hautakuwa huru na haki.

Alisema hayo baada ya kuulizwa nini hatima ya Zanzibar ikiwa uchaguzi huo hautakuwa huru na haki.

“Kama nikishindwa katika uchaguzi ambao ni huru na haki nitampongeza aliyeshinda, lakini kama nitashindwa na uchaguzi ambao si huru na haki, sitakubali matokeo,” alisema Maalim.

Maalim Seif alisema hayo jana baada ya kupiga kura katika kituo Namba 13 cha Mtoni Kidatu, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Mgombea TLP ajichanganya

Katika hatua nyingine, mgombea urais wa TLP, Macmillan Lyimo jana alitoa maelezo yaliyojichanganya, awali akisema ameshindwa kupiga kura baada ya kwenda kituoni bila kitambulisho, lakini baadaye akatoa kauli nyingine tofauti.

Lyimo alifika kituo cha Ghala Njipanda saa 2:30 asubuhi na kutakiwa kujaza fomu maalumu kwa wagombea urais endapo mgombea anapiga kura tofauti na kituo alichojiandikishia.

Msimamizi msaidizi wa kituo hicho, Aliko Mkumbo alimkabidhi fomu hiyo na kumtaka aijaze na kisha ampe kitambulisho, ndipo Lyimo alipojipapasa na kugundua hakuwa nacho.

Kutokana na hali hiyo, msimamizi huyo alimweleza kuwa asingeweza kupiga kura bila kuwa na kitambulisho cha mpiga kura, na Lyimo aliafiki, akisema anakwenda kukitafuta.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya kituo hicho, Lyimo alisema uamuzi wa msimamizi huyo ulikuwa ni sahihi na kwamba yeye alijiandikishia Dar es Salaam na sio jimbo la Vunjo.

Hata hivyo baadaye, Lyimo alibuka na kudai kuwa hakukuwa na fomu Namba 19 inayojazwa kwa mpigakura nje ya kituo alichojiandikisha, jambo ambalo NEC imeeleza kuwa ilikuwapo.

Baadaye mgombea huyo alipiga kura saa 6:00 mchana kwa kile alicholiambia gazeti hili kuwa ni baada ya kuitwa na msimamizi msaidizi wa uchaguzi kuwa fomu imepatikana.

Ajitetea aliifichia siri NEC

Baadaye Lyimo alisema si kweli kwamba hakuwa na kitambulisho cha mpigakura, bali alitaka kuifichia siri NEC kutokana na kutokuwapo fomu Namba 19.

“Nilitumia hekima tu kutoka pale, lakini inabidi niseme ukweli kwa vile tayari dunia nzima imeshajua sijapiga kura,” alisema.

Mgombea huyo alisema msimamizi msaidizi wa kituo hicho, amechukua namba yake ya simu kwamba pale watakapokuwa wameshapata fomu hiyo, wangemwita apige kura.

“Niko hotelini nasubiri waniite. Hii Tume imekaa kinamna namna. Kama mimi mgombea urais inakuwa hivi, watu wa kawaida inakuwaje? Wameniambia ‘we katulie mahali tutakuita’,” alisema.

Ilipofika saa 5:21 asubuhi, mgombea huyo alimpigia simu mwandishi wetu na kumjulisha kuwa tayari Tume wamemwambia aende kupiga kura kwa vile wameshapata fomu hiyo.

Lyimo alifika katika kituo hicho tena saa 5:50 na kwenda moja kwa moja kwa Msimamizi Msaidizi ambaye alimkabidhi fomu Namba 19 na kuijaza kisha kupewa karatasi ya kupigia kura.

Kura ya mlinzi

Kabla ya kupiga kura, kulitokea ubishani kati ya msimamizi msaidizi na Lyimo, baada ya msimamizi huyo kumzuia mlinzi wake ambaye ni polisi kupiga kura ya rais.

“Huyu ni sajini wa polisi, kwa nini asipige kura ya rais? Asipopewa fursa na mimi sitapiga kura,” alisema Lyimo hali iliyomfanya msimamizi huyo kuwasiliana kwa simu na mamlaka ya juu yake.

Hata hivyo, baada ya kuzungumza kwa simu, bado msimamizi huyo alishikilia msimamo kuwa maelekezo ni kwamba asingeweza kupiga kura lakini wakati huo, Lyimo tayari alikuwa amepiga kura.

Msimamizi wa Uchaguzi majimbo ya Vunjo na Moshi Vijijini, Fulgence Mponji alikanusha madai ya mgombea huyo kuwa katika kituo hicho hakikuwa na fomu Namba 19.

“Yeye hakujiandikishia Vunjo wala hakujiandikishia Mkoa wa Kilimanjaro. Utaratibu lazima ujaze fomu Namba 19, sasa yeye alipopewa aijaze akasema ooh ngojeni nakuja,” alisema.

Imeandikwa na Raymond Kaminyoge, Salma Said, Rehema Matowo, Daniel Mjema na Zephania Ubwani



Breaking News:Diamond Awa Msanii wa Kwanza Afrika Kushinda ‘Worldwide Act Africa/India’ Kwenye Tuzo za MTV EMA

$
0
0
Diamond Platnumz ameiletea sifa na heshima kubwa Tanzania kwa mara nyingine, kwa kushinda tuzo kubwa ya ‘Best Worldwide Act Africa/India’ kwenye tuzo za MTV Europe Music Awards 2015 zilizotolewa Milan, Italy usiku wa Jumapili Oct.25.


Hii ni kwa mara ya kwanza kwenye historia ya tuzo za MTV EMA toka vipegele vya Worldwide Act vilipoongezwa kwenye tuzo hizo mwaka 2011, tuzo ya ‘Best Worldwide Act Africa/India’ imekuja Afrika mwaka huu.

Diamond ambaye pia ni mshindi wa kipengele cha ‘Best African Act’ kwenye tuzo hizo, alikuwa akichuana na mwigizaji na mwanamuziki maarufu wa India, Priyanka Chopra aliyewahi kuwa pia Miss World mwaka 2000.

Ushindi wa Diamond ni mkubwa kwasababu hakuwa anaiwakilisha Tanzania pekee, bali bara zima la Afrika.

Hawa ni washindi wa miaka iliyopita wa kipengele alichoshinda Diamond mwaka huu:

2011 – Abdelfattah Grini (Morocco)
2012 – Ahmed Soultan (Morocco)
2013 – Ahmed Soultan (Morocco)
2014 – Mohammed Assaf (Palestina)

Kauli Hii ya JANUARY MAKAMBA Yawashangaza Wengi "Dkt. John Pombe Magufuli kutangazwa Rais Mteule tarehe 29 Oktoba 2015"

$
0
0

 Kauli Hii ya JANUARY MAKAMBA Kwenye Twitter Yawashangaza Wengi  "Dkt. John Pombe Magufuli kutangazwa Rais Mteule tarehe 29 Oktoba 2015"

Ameandika Hivi Jana Usiku:


ZEC Imetangaza Matokeo ya Urais Zanzibar Katika Majimbo Manne Mpaka Sasa.......CCM imeshinda matatu, CUF 1

$
0
0
Hadi sasa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar imeshatangaza matokeo ya kura za urais kwa majimbo manne kati ya 54. 

Majimbo hayo ni Kwahani, Fuoni, Kiembesamaki na Malindi. Dk. Shein wa CCM anaongoza kwenye majimbo matatu ya Kwahani, Fuoni na Kiembesamaki huku Maalim Seif wa CUF akiongoza kwenye jimbo la Malindi.
 
1. UCHAGUZI ZANZIBAR: URAIS JIMBO LA MALINDI
ACT - 4
TADEA - 3
ADC - 10
FP - 6
CCK - 3
CCM - 2,334
CHAUMA - 7
CUF - 5,667
MAKINI - 3
JAHAZI -2
NRA - 0
TLP - 1
SAU - 2
DP - 1
 
2. UCHAGUZI ZANZIBAR: URAIS JIMBO LA FUONI
CCM - 889
CUF - 429
ADC- 3
TLP - 4
SAU- 3
DP- 2
NRA - 1
MAKINI - 1
CHAUMMA - 1
ACT - 0
TADEA- 0

  
3. UCHAGUZI ZANZIBAR: URAIS JIMBO LA KIEMBE SAMAKI
CCM - 4413
CUF - 2986
CHAUMA- 13
ACT -5
ADC- 4
FP- 4
MAKINI-2
DP- 2
JAHAZI -2
SAU-1
NRA -2

Video: Kura FEKI Zakamatwa Shuleni Bukoba Zikiwa Zimepigwa kwa Ajili ya Wagombea wa CCM

$
0
0
Wilayani Bukoba, karatasi za kupigia kura ambazo ziliwekewa alama ya vema kwenye sehemu za wagombea wa udiwani, ubunge na urais, jana  ziligundulika nyuma ya bweni la Shule ya Sekondari ya Kahororo.

Karatasi hizo zilikuwa zimesambaa nyuma ya bweni la wanafunzi wa kidato cha sita, hali iliyowafanya wanafunzi wahisi kuwapo kwa karatasi zaidi ndani ya mabweni.

 Mmoja wa wanafunzi alisema karatasi hizo zilisambaa nyuma ya bweni hilo baada ya mwanafunzi mmoja kuzirusha kupitia dirishani kutokana na kutuhumiwa kutumiwa na mmoja wa wagombea kwenye jimbo hilo lenye ushindani mkali kati ya Chadema na CCM.

Mmoja wa walimu, Charles Rushinge alisema aligundua karatasi hizo wakati akikagua mazingira ya shule na baadaye kutoa taarifa kwa vyombo husika kwa ajili ya kuchukua hatua.

Hata hivyo, pamoja na kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi kufika shuleni hapo kushuhudia tukio akiwa na baadhi ya maofisa usalama, bado hakuwa tayari kutoa ufafanuzi wa idadi ya karatasi za kura na chanzo cha tukio hilo.

Tukio hilo liliibuka huku yakiwepo malalamiko mengi katika vituo vya Kata ya Kashai kuwa kuna karatasi zimenyofolewa kutoka kwenye baadhi ya vitabu vya kupigia kura, ikiwa ni pamoja na kituo cha Zahanati ya Kashai na Shule ya Msingi na Mafumbo.

Mkurugenzi wa uchaguzi wa Jimbo la Bukoba Mjini, Aron Kagurumjuri aliwataka wananchi wapige kura na kudai alipokea vitabu kutoka NEC vikiwa vimefungwa kwenye maboksi, hivyo tatizo la karatasi hizo za kura si lake....Tazama  Video  hiii

Mabomu ya Machozi Yarindima Mwanza Kuwatawanya Wafuasi wa Chadema Walioingia Barabarani Kushangilia Ushindi

$
0
0
Polisi mkoani Mwanza jana walitumia mabomu ya machozi  kuwatawanya watu wanaoaminika kuwa wafuasi wa Chadema  walioingia mitaani kushangilia wakiamini wagombea wao wanaongoza katika matokeo ya awali.

Tukio hilo lilitokea kwenye kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi Mlimani, eneo la Butimba, Ghana na Shule ya Msingi Buzuluga kwenye majimbo ya Nyamagana na Ilemela.

Taarifa toka jijini Mwanza zinasema kundi la watu waliokuwa vituoni wakisubiri kubandikwa kwa matokeo hayo, lililipuka kwa shangwe, nderemo na shamrashamra baada ya matokeo hayo kubandikwa na wasimamizi wa uchaguzi wakiamini wagombea wao wanaongoza.

Baafa  ya  hali  hiyo, polisi waliingilia kati na kufyatua mabomu ya machozi kutawanya wafuasi hao.

Katika uchaguzi wa mwaka huu, mgombea ubunge wa Chadema na mbunge anayemaliza muda wake katika jimbo la Nyamagana, Ezekiel Wenje anachuana vikali na aliyekuwa Meya wa jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula wa CCM.

Katika jimbo la Ilemela, mbunge anayemaliza muda wake, Highness Kiwia wa Chadema anatetea nafasi yake kwa kupambana na mgombea wa CCM, Anjela Mabula.

Uchaguzi wa urais, ubunge na udiwani umefanyika jana Oktoba 25, mwaka huu ambapo takribani Watanzania milioni 22.7 wamejiandikisha kwenye daftari la kudumu kwa upande wa Tanzania Bara huku kwa upande wa Zanzibar zaidi ya wapigakura laki tano wamejiandikisha.

Wassira Chali Hongera Sana Ester Bulaya

$
0
0
 Kwa Habari nilizozipata ni kuwa Wassira Chali Hongera Sana Ester Bulaya kwa kuchukua Ubunge jimbo la Bunda Kupitia Chadema

Meseji Kutoka Jamii Forums Baada ya Kuvamiwa na Website yao Kutopatikana Jana Masaa 7

$
0
0
Tunafarijika kuwafahamisha kuwa tumerejea hewani baada ya kupata mashambulizi ya makusudi yenye kulenga kuzuia upatikanaji wa huduma kwa watumiaji wa JamiiForums (DDOS Attack) kwa takribani masaa 7, kuanzia saa 7 mchana hadi saa 2 usiku.

Mashambulizi haya yaliyolenga kuidhoofisha miundombinu yetu, yamefanywa kwa kupangwa na kwa kiwango tulichobaini kuwa yalifanywa na wataalamu waliobobea katika masuala ya mashambulizi ya kimtandao.

Tunalaani kwa nguvu zetu zote kitendo hiki na vingine vya mwelekeo kama huu vyenye kulenga kunyamazisha sauti za wananchi.

Timu yetu ya wataalamu itaendelea kufanya kazi kwa umakini zaidi katika kipindi hiki cha Uchaguzi na tunaomba ushirikiano wa wanachama na wadau wa JamiiForums pale mtakapoona huduma zetu zinasuasua kwa namna yoyote ile katika upatikanaji. Wasiliana nasi kupitia support@jamiiforums.com

Tunawashukuru sana kwa uvumilivu wenu katika kipindi hiki na tunawatakia kila la heri katika mchakato wa Uchaguzi Mkuu.

Maxence M. Melo,
K.n.y Uongozi wa JamiiForums

Kufuatia Kazi Nzuri Iliyotuka Inayofanywa na ITV, Mnaonaje Mzee Mengi Akabidhiwe Kuiendesha TBC?

$
0
0
Kufuatia Kazi Nzuri na Iliyotuka Inayofanywa na vyombo vya habari vya IPP, in particular, kituo cha televisheni cha ITV, katika uchaguzi huu, Jee Mnaonaje Kama tukiishauri serikali ijayo, imkabidhi Mzee Reginald Mengi, Jukumu zito la Kuiendesha TBC?!.

Najua wazo langu hili litapata upinzani, toka kwa watu wanaojiita wazalendo, kwa kuleta hoja, huwezi kuibinafsisha TBC kwa sababu ni taasisi nyeti!. Hili sio jambo la ajabu, Tanzania tumeisha binafsisha taasisi mbalimbali na nyingine ni nyeti zaidi ya TBC mfano, City Water, TTCL, Tanesco, TRL, ATC etc.

Swali hili ni kufutia ITV kuwa ndio tegemeo pekee la taarifa za matokeo ya Uchaguzi Mkuu, as if ITV ndio TV ya Taifa, jukumu ambalo lingepaswa kubebwa na TBC!. Kama hoja ni uzalendo, ni nani mzalendo halisi wa taifa hili kati ya ITV na TBC?!.

Hongera sana ITV, Hongera Mzee wetu, Reginald Abraham Mengi, hongera menejiment ya ITV ikiongozwa na Iron Lady, Joyce Mhavile, na Hongera kwa News team yote ya ITV ambayo ni hakuna kulala, mnafanya kazi 24/7, hivyo na sisi huku majumbani mwetu, tunakesha na nyinyi!.

Mungu awabariki sana!.

Maoni Huru Kutoka Kwa Pasco /Jamii Forums

Kauli ya Kwanza ya Ester Bulaya Baada ya Kumngo'a Wasira Ubunge Jimbo la Bunda

$
0
0
Hakuna kisichowezekana chini ya jua, asante wanabunda,kwakuniamini, hatimaye ameng'oka.mungu wangu asante kwa kunisiimamia. Nimeshinda nasubiri kutangaza rasmi.
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live




Latest Images