Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Baba Lowassa, Sumaye na Babu Kingunge Sheria ni Msumeno

$
0
0
Sheria zetu za nchi haziruhusu kujadili matokeo ya urais mahakamani, so to say, huwezi kuyaquestion kokote isipokuwa kwa wananchi. Na ukishitaki kwa wananchi utasababisha uvunjifu wa amani, na hakuna mtanzania hata mmoja atakayekubali ujinga huo wa kuvunja Amani.

Twende mbele, turudi nyuma. Wakati sheria hizi zinatungwa, au zinafanyiwa marekebisho, Lowassa, Kingunge na Sumaye walikuwa CCM wakiyapinga mapendekezo ya wapinzani kutaka matokeo ya urais yajadiliwe mahakamani; wakaisimamia katiba mbovu iliyopinga uwepo wa tume huru ya uchaguzi.

Leo sheria zile walizozisimamiawakiwa CCM ndiyo zimewatafuna. Wameonja joto ya jiwe walilolirusha wenyewe. Hawana tena uwezo wa kushitaki kuhusu matokeo waliyoyapata, na sisi hatupo tayari kuandamana.

Hapa wanalazimika kukubali kukubaliana na wasiyokubaliananayo, maana wakati yanatengenezwa waliyatetea. "Walitega mtego mtego ambao umewanasa wenyewe".

Nampongeza sana Mbowe kwa kuwakaribisha hawa wanaCCM ndani CDM. Angalau wale waliobaki CCM watajifunza kutetea maslahi ya nchi badala ya kutetea maslahi ya chama na maslahi binafsi.

By COARTEM/JF

Vyama 6 Yyamtaka Mwenyekiti ZEC Ajiuzulu......Maalim Seif atoa Wito kwa Rais Kikwete Na Dk Shein

$
0
0
Mgombea wa Urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amemuomba Rais Jakaya Kikwete na Rais Ali Mohamed Shein kubeba dhamana ya uongozi katika siku hizi chache zilizobaki za uongozi wao kwa kusimamia katiba na sheria za nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mtendeni Maalim Seif amesema marais hao wawili kuheshimu maamuzi ya Wazanzibari waliyoyafanya tarehe 25 Oktoba na kuwataka washirikiane nae katika kuinusuru Zanzibar.

“Nawaomba sana Rais Kikwete na Rais Shein kukwepa matumizi ya nguvu na badala yake tushirikiane kutunza amani na haki za wananchi. Mimi niko tayari kushirikiana nao kama ambavyo nimekuwa nikifanya mara zote. Tushirikiane kuiepushia Zanzibar na Tanzania fedheha ya kimataifa”. Alisema Maalim Seif.

Akizungumzia kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi iwapo ni halali au sio halali Maalim Seif amesema lile lilikuwa ni tamko binafsi la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Jecha Salum Jecha ambapo Chama Cha Wananchi (CUF) kimetiwa nguvu na tamko la Makamishna wawili wa Tume waliothibitisha kwamba tamko lile ni lake binafsi.

“Ni kwamba hakukuwa na kikao cha Tume kilichokaa kuamua yaliyosemwa na Jecha, na kwamba hakuna misingi ya kikatiba na kisheria ya tamko lile” alisema Maalim Seif na kuongeza kwamba.

“Jana jopo la wanasheria wa CUF lilikutana kuangalia kwa kina kama kuna misingi ya kikatiba na kisheria ya tamko lile binafsi la Jecha Salim Jecha, na limetoa hoja za msingi zifuatazo kwa kuanzia muundo wa Tume ambapo Kifungu 119(1) kinaanzisha Tume ya Uchaguzi yenye wajumbe saba (7) akiwemo Mwenyekiti wao.

Alisema (1) Kifungu 119 (10) kinatamka kuwa: “Kiwango cha mikutano ya Tume ya Uchaguzi ni Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wane na kila uamuzi wa Tume ni lazima uungwe mkono na Wajumbe walio wengi”.

Aidha alisema (1) Kwa sababu Tume haikukaa kwa pamoja ikiwa na Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti na angalau wajumbe wengine wanne, na kwa sababu maamuzi yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Tume yalikuwa ni yake peke yake, maamuzi hayo kikatiba ni batili na hayana nguvu zozote.

Maalim Seif ambaye ni Katibu Mkuu wa CUF alisema waangalizi wote wa uchaguzi ikiwa ni pamoja na SADC, AU, Commonwealth Observer Team, European Union Election Observation Team, Waangalizi kutoka Uingereza na Marekani, na TEMCO, wote walisema mbali na dosari ndogo ndogo uchaguzi ulikuwa huru, wa haki na amani.

Aidha aliwaambia waandishi wa habari kwamba Mwenyekiti wa ZEC mwenyewe naye pia alisema uchaguzi ulikuwa huru na wa haki ambapo Mwenyekiti huyo huyo alisimamia kazi ya uhakikiwa matokeo na kutia saini fomu za matokeo yaliyohakikiwa na kuthibitishwa za majimbo 31 ya Unguja na kuyatangaza matokeo hayo kabla.

“Kwa nini ghafla ilipofika siku ya tatu ambayo ni jana aligeuka na kukataa kuendelea na uhakiki na badala yake kudai eti kulikuwa na mambo kadhaa ya kufanya uchaguzi huo usiwe huru na wa haki? Tena dosari zenyewe za tamko lake eti ni pamoja na wajumbe wake kuvua mashati na kutaka kupigana” alisema Maalim.

Akizungumzia suala la baraza la Wawakilishi jipya Maalim Seif alisema Kifungu 92(1) cha Katiba ya Zanzibar kinaeleza kwamba maisha ya Baraza la Wawakilishi ni miaka mitano tokea lilipoitishwa mkutano wake wa mwanzo hivyo Kifungu 90(1) kinaeleza kwamba mkutano wa mwanzo wa Baraza la Wawakilishi utafanyika si zaidi ya siku 90 tokea Baraza lilipovunjwa kwa ajili ya kuitishwa uchaguzi.

Kuna masuali kadhaa ya kujiuliza alisema Maalim Seif ikiwemo ni “Rais yupi ataitisha Baraza?, Wawakilishi wapi wataitwa (wakati hawapo)?, Yote haya yanaleta mgogogro wa kikatiba ambao umesababishwa na mtu mmoja anayeitwa Jecha Salim Jecha kwa sababu tu ya kufuata maelekezo ya chama chake cha CCM”. Alihoji Maalim Seif huku akionekana kuongea kwa kujiamini.

Hata hivyo alisema kuna suali la muundo wa mpito ambapo kama uchaguzi utarejewa, kama anavyotaka Mwenyekiti wa Tume, jambo ambalo alisema halikubaliki kwa sababu ya kukosa misingi ya kikatiba na kisheria, ina maana kuwa serikali itakuwa haipo.

Akitoa sababu za kutokuwepo Maalim Seif alisema kwanza muda wa Urais ni miaka mitano kuanzia tarehe aliyochaguliwa kwa mujibu wa kifungu 28(2) cha Katiba, Ingekuwa tamko la Jecha Salim Jecha ni halali, basi maana yake hakuna Rais anayefuata kwa sababu ya kufutwa kwa uchaguzi, hivyo hakutakuwa na kiapo cha kumuapisha rais mpya. Kwa msingi huo, msharti ya kifungu cha 28(1)(a) hayana nafasi katika mtafaruku huu uliosababishwa na mtu mmoja.

“Hiyo maana yake, kipindi hicho sasa kitakuwa tete na haijulikani kikatiba ni nani ataongoza nchi? Tunasema hivyo kwa sababu vifungu vya Katiba 33(1) na (2) havitumiki hapa kwa suala la kuwa wazi kwa kiti cha Urais na kukaimiwa kwa nafasi hiyo”. Aliongeza.

Alisema hiyo ni kwa sababu nafasi ya Urais haipo kwa sababu itakuwa imemaliza muda wake ifikapo tarehe 2 Novemba, 2015, siku ambayo Urais wa Dk. Ali Mohamed Shein unakamilisha miaka mitano kamili.

Halikadhalika Maalim Seif alitaka kujua jee katika suala hilo suluhisho ni nini? “Kutokana na hoja tulizozieleza hapo juu, ni wazi kwamba tamko la Jecha Salim Jecha ni lake binafsi na kama tulivyotangulia kusema, halina misingi ya kikatiba na kisheria.

Kwenye taarifa yake alisema kuwa “… kwa uwezo nilionao …”. Masuala ya kujiuliza ni uwezo upi? Chini ya kifungu kipi cha Katiba au Sheria ya Uchaguzi?” alihoji.

Katika kutilia nguvu hoja yake hiyo ya kisheria Maalim Seif alisema kwa kifupi, ni kwamba Mwenyekiti wa ZEC uwezo huo hana kikatiba na kisheria na kwa msingi huo, maamuzi yake hayo ni batili.

Kufuatilia masuali hayo ambayo majibu yake yapo kisheria Maalim Seif alisema CUF inasisitiza kile kinachodaiwa na waangalizi wote wa uchaguzi waliotoa taarifa zao kwamba uamuzi wa Mwenyekiti wa ZEC ni uamuzi wake binafsi pekee na haukuwa uamuzi wa Tume, kwani hakukuwa na kikao chochote cha Tume kilichokaa kufikia uamuzi huo.

Alisema uamuzi huo uwekwe upande na Jecha Salim Jecha amepoteza sifa ya uadilifu ambayo ni msingi mkuu wa kazi ya Tume ya Uchaguzi katika kusimamia maamuzi ya Wazanzibari ambao kikatiba (kwa mujibu wa kifungu cha 9(2) (a) ndiyo wenye mamlaka ya kuwaweka madarakani viongozi wa Serikali.

“Hivyo, anapaswa awajibike kwa hatua yake ya kuiingiza nchi katika mgogoro pasina sababu yoyote na ajiuzulu” alisema Maalim Seif huku akionekana na furaha katika mkutano huo wa waandishi wa habari.

Aidha alishauri Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar waendelee na kazi ya kukamilisha uhakiki na majumuisho ya matokeo ya uchaguzi kwa majimbo 14 yaliyobaki na kisha kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa Rais wa Zazibar.

Alisema baada ya ukamilishaji huo alisema mshindi wa nafasi ya Urais wa Zanzibar aapishwe, Viongozi wa CUF na CCM washirikiane kuunda Serikali mpya ya Umoja wa Kitaifa itakayoiongoza Zanzibar katika miaka mitano ijayo.

“Kwa maana hiyo, kitumike kifungu 42(6) cha Sheria ya Uchaguzi kinachoeleza kwamba kama kuna matatizo yoyote katika vituo vya kupigia kura a na matokeo hayawezi kutolewa ndani ya siku tatu; basi Tume iendelee kuhesabu na kuhakiki kura na kutangaza matokeo ndani ya siku tatu nyengine na shughuli za kiserikali ziweze kuendelea” aliongeza.

Katika hatua nyengine Malaim Seif alirejea tena kauli yake ya kuhimiza Amani na kuwataka wafuasi wake na wananchama wa CUF na Wazanzibari wote kwa ujumla kuendelea kuwa watulivu na kutunza amani ya nchi yetu huku wakitambua kwamba tutayasimamia maamuzi yao waliyoyafanya tarehe 25 Oktoba, 2015.

Baadhi ya wafuasi wa CUF wakiwa wamekusanyika nje ya ofisi za CUF Mtendeni kusikiliza kauli za viongozi wao kuhusu maamuzi watakayochukua baada ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi

Rais Kikwete Alivyomkaribisha Kumpongeza Dk. Magufuli Baada ya Matokeo ya Urais Kutangazwa

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza kwa furaha mshindi wa kinyang'anyiro cha Urais kwa tiketi ya CCM na Rais Mteule Dkt John Pombe Joseph Magufuli wakifurahia matokeo mara baada ya Mwenyekiti wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva  kutangaza kutangaza rasmi matokeo ya uchaguzi mkuu Ikulu jijini Dar es salaam ambako walifuatilia kwa pamoja matangazo hayo ya moja kwa moja kupitia vituo vya televisheni  jana  jioni Oktoba 29, 2015


Mama Salma Kikwete akimpongeza mshindi wa kinyang'anyiro cha Urais kwa tiketi ya CCM na Rais Mteule Dkt John Pombe Joseph Magufuli mara baada ya Mwenyekiti wa Tais kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu Ikulu jijini Dar es salaam ambako walifuatilia kwa pamoja matangazo hayo ya moja kwa moja kupitia vituo vya televisheni jana jioni Oktoba 29, 2015


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza kwa furaha mshindi wa kinyang'anyiro cha Urais kwa tiketi ya CCM na Rais Mteule Dkt John Pombe Joseph Magufuli mara baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva kutangaza kutangaza rasmi matokeo ya uchaguzi mkuu Ikulu jijini Dar es salaam ambako walifuatilia kwa pamoja matangazo hayo ya moja kwa moja kupitia vituo vya televisheni jana jioni Oktoba 29, 2015



Kauli ya Mwanamuziki Diamond Platnumz Baada ya John Magufuli Kushinda Urais wa Tanzania

$
0
0
"(Happy birthday Dr. john Pombe Magufuli...and many Congratulation for Being our New Tanzania's President...) Heri ya kuzaliwa na Pongezi nyingi zikufikie Dr. John Magufuli Pombe pamoja na Uongozi mzima na wanachama wote wa Ccm kwa kuweza kufanikiwa kuiongoza tena Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.. Lakini pia niwashukuru na kuwapongeza Vyama vyote vya upinzani kwani naamini amshaamsha mliyoifanya Mwaka huu itasaidia kuongeza kasi za utendaji wa viongozi wetu pendwa na Nchi yetu kupata Maendeleo zaidi... hakika uchaguzi wa Mwaka huu ulikuwa ni wakipekee... Ni muda wa wote sasa kushirikiana kwa pamoja na Kuijenga Nchi...Kumbuka: hakuna ataekuletea Maendeleo chumbani kwako! amka tuwajibike maana Hata Punda hajasoma lakini hakosi kazi" Diamond Platnumz

Dr. Magufuli Akabidhiwa Rasmi CHETI Cha Ushindi wa Kiti cha Urais

$
0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva amemkabidhi cheti cha ushindi wa kiti cha urais, Dk John Pombe Magufuli  na  mgombea  mwenza  wake  Samia  Suluhu  katika  Ukumbi wa Diamond Jubilee  asubuhi  hii.

Katika  tukio  hilo, Wagombea urais wa Chadema Edward Lowassa na Hashim Rungwe wa Chauma wamesusia sherehe hizi  za kukabidhiwa cheti cha ushindi Dk John Magufuli wa CCM.

Dk Kitila Mkumbo Atoa Neno Baada ya Ushindi wa Magufuli..“Huu Uchaguzi Ulikuwa ni Tofauti na ile ya Miaka iliyopita...."

$
0
0
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ualimu cha Chang’ombe (Duce), Dk Kitila Mkumbo alisema Dk Magufuli alipitia njia ngumu kupata mafanikio hayo.
“Amepambana na ushindani mkubwa,” alisema Dk Kitila aliyeongea na Mwananchi baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo ya uchaguzi ambao ulikuwa ni vita baina ya Dk Magufuli na Lowassa, ambaye ni Waziri Mkuu wa kwanza kukihama chama tawala na kugombea urais kwa tiketi ya upinzani
“Huu uchaguzi ulikuwa ni tofauti na ile ya miaka iliyopita. Sasa ana kazi kubwa ya kutuunganisha ili tuwe wamoja tushiriki kufanya kazi kwa maendeleo ya nchi yetu.”

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki Moon aipongeza Tanzania Kwa Uchaguzi Huru na Haki

$
0
0
Salam za pongezi kitaifa na kimataifa zaanza kutolewa kwa Rais mteule wa awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Taifa la Tanzania.

Mapema leo baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kumaliza hafla ya kumkabidhi Rais mteule cheti cha ushindi katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es Salaam.Tanzania ilianza pokea salamu za pongezi toka kwa Katibu Mkuu wa umoja wa mataifa (UN) Ban Ki -Moon liyetuma salamu zake za pongezi.

Pia, aipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuratibu na kusimamia vyema zoezi zima la Uchaguzi, ukusanyaji matokeo ya Uchaguzi kutoka katika vituo mbalimbali, ujumlishaji matokeo kusanywa, pamoja na usomaji matokeo hayo uliokuwa wa wazi, huru na haki.

Hata hivyo katika nyongeza yake, aelezea "concern" yake juu ya zoezi la Uchaguzi Zanzibar.


Soma Hapa:



HUDDAH MONROE reveals the rough S*X she is enjoying with French men like wild animals

$
0
0


Huddah Monroe has decided to share unnecessary details about the kind of s*x she is enjoying with French men while on vacation in Paris and here is her experience;

French people love kissing! Eww! The rough the s£x the better! Biting and scratching like wild animals. Can’t stand a humble man! Lord help. Have you ever watched lions f**k? I just think lions have the best s£x ever! Animals don’t turn me on. Lions only.  – Huddah Monroe


Edward Lowassa Awe Kielelezo cha Kuigwa Katika Kutimiza Malengo Yetu

$
0
0
Mara kadhaa nilikuwa na mtazamo hasi juu ya mh.Lowassa Mwaka jana mwezi wa Feb nilipata bahati ya kuwa na mazungumzo na mmoja wa washauri wa masuala ya kisiasa wa chama cha mapinduzi ambaye ni proffessor mstaafu wa chuo kikuu cha Dar es salaam ninamwamini sana na ni mkweli katika mazungumzo ya hapa na pale tuligusia swala la Richmond Maelezo yake na hitimisho lake baada ya kusoma ripoti ya mwakyembe hakuona sehemu ambayo Lowassa alihusika. Tokea siku ile nilibadili mtazamo wangu juu yake kwasababu kabla nilimuona ni fisadi na mtu asiyefaa kuwa kiongozi. Japo haindoi ukweli kuwa lowassa ana uchafu wake na yeye lakini ni nani basi msafi amponde jiwe? iwe ndani ya chadema au ccm?

Pamoja na mambo yote aliyopitia nimependa ambavyo amekuwa na msimamo katika kusimamia lengo lake na hili ni moja ya sifa ambayo kiongozi anapaswa awe nayo. kuna tofauti kati ya uchu wa madaraka na kutimiza ndoto na malengo uliyojiwekea. uchu wa madaraka ni pale ambapo mtu amepewa dhamana ya uongozi kwa muda mrefu na bado anataka kuendelea hata kama wale ambao anawaongoza hawamtaki katika nafasi ile.

Lowassa aliutamani urais toka angali kijana hii ilikuwa ni ndoto yake. aliutaka kwaajili ya haya anayotuambia au kwa maslahi yake hilo jibu analo yeye na MUNGU pekee. baada ya kushindwa 1995 walijiwekea mkakati na miaka 10 baadaye Lowassa alimuachia rafiki yake na akamsaidia mpaka akawa Rais wa nchi hii, Lowassa alizawadiwa uwaziri mkuu kama njia ya kuja kushika majukumu ya Urais 2015. hapo katikati yalitokea ya kutokea na makubaliano yao yakaingia shimoni. marafiki wakawa maadui wakubwa. huku mmoja lengo lake likiwa ni kuwa Rais wa nchii hii. Rafiki yake alifanya kila jitihada kuhakikisha lengo na adhma ya rafiki yake haitimii.

Katika hatua ambazo tunaweza kusema rafiki yake ali win mchezo ni hatua za awali ndani ya chama. pamoja na nguvu ya ushawishi na wafuasi wengi lowassa hakufua dafu. pamoja na kushindwa huko bado Lowassa hakukata tamaa sababu yeye ndoto yake ilikuwa ni kuwa Rais wa nchi hii na alijiandaa kwa kila hali ili ndoto yake itimie.Lowassa akavunja mwiko ambao haujawahi vunjwa toka CCM izaliwe tena akiwa mtu aliyewahi kushika wadhifaa wajuu kabisa. Lowassa hakuwa tayari kuona mtu mmoja anakuwa kikwazo katika kutimiza ndoto yake. aliaamua kumkwepa huyo mtu ali atimize ndoto zake kwa mrango mwingine.

Lowassa alifanikiwa na Lowassa amegombea urais. Lowassa anadai ameibiwa kura kama madai yake yana ukweli mbele za MUNGU Lowassa ni Rais wa Nchi hii hata kama ataenda monduli Kuchunga ng'ombe. na kama basi ameshindwa kihalali basi lowassa atakuwa ameshindwa kutimiza ndoto yake lakini ameshindwa dakika za mwisho katika kupigania ndoto zake. hili ni funzo kubwa kwetu weka pembeni kashfa,mienendo na tabia zake binadamu wa aina yake ni wachache haswa kwenye nchi yetu.

Jipime mwenyewe ulipokuwa mtoto mdogo ulikuwa na ndoto ya kuwa nani ukiwa mkubwa? Je leo unaiishi ndoto hiyo? kama ndio hongera kwasababu wewe ni miongoni mwa wachache waliofanikiwa kuishi ndoto zao kama hapana ni ulikabili vipi changamoto zilizokufanya usitimize?.

Kama we ni mdogo basi jifunze na uchukue hatua kabla wakati haujakuacha.

Kama watanzania tunapaswa kujiuliza je Rais mteule aliwahi kuota kuwa Rais alijiandaa na kupambana kufikia ndoto hii? Kama ni kwa bahati basi tutegemee nini? na kama kweli alijiandaa na kupigania ndoto yake basi tutegemee nini kwa hili pia

 By Major Mwendwa

Lembeli Aeleza Hatma Yake Baada Ya Kushindwa, Ajibu Tetesi Juu Yake

$
0
0
Aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Kahama, James Lembeli ameelezea kinachoendelea katika maisha yake ya kisiasa hasa baada ya kushindwa katika uchaguzi wa mwaka huu akiwa ndani ya chama chake kipya cha Chadema.

Akiongea katika taarifa rasmi kwa wananchi wa jimbo hilo, Lembeli amesema kuwa hivi sasa atajikita zaidi katika shughuli za chama chake pamoja na shughuli alizokuwa akizifanya kabla ya kuwa mbunge wa jimbo hilo.

Alisema kuwa ataendelea kufanya kazi zake na mashirika ya kimataifa kama mjumbe wa Bodi mbalimbali. Pia, ataendelea kufanya kazi ya kusimamia radio yake (Kahama FM) ambayo amedai kuwa taarifa zilizosambazwa kuwa ameiuza kulipa deni la mkopo aliopewa kuendesha kampeni sio za kweli.

Pia, Lembeli amewashukuru wananchi waliojitokeza kumuunga mkono na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika masuala ya maendeleo na ataendeelea kushirikiana nao kukamilisha miradi mbalimbali aliyokuwa ameanza kuitekeleza kwa juhudi zake binafsi.

Kadhalika, Lembeli amekanusha taarifa zilizokuwa zimesambazwa kuwa alikamatwa na jeshi la polisi mara tu baada ya Jumanne Kishimba wa CCM kutangazwa kuwa mshindi.

Kuhusu afya yake, alisema kuwa yeye ni mzima tofauti na habari zinazoendelea kuenea kuwa ni mgonjwa hasa baada ya kupata ajali ya gari na matokeo kutangazwa

Angalizo kwa Mbowe, Mnyika, Kubenea, Mdee, Tundu Lissu

$
0
0
Ni dhahiri kuwa sasa uchaguzi umekamilika mara baada ya tume kumtangaza mshindi wa urai ndgu yetu John Joseph Pombe Magufuli kuwa ndiye rais mteule kwa mjibu wa matokeo.

Ushauri wangu kwamba kwa upande wa wabunge wa viti maalum naomba watoke hata kule ambako CDM haikushinda lakini imefanya vizuri. Kuna kushinda lakini pia kuna kufanya vizuri sana japo hukushinda. Hii inaweza kuwa karata ya kukiimarisha chama kwa kuwa si kwamba baada ya kushindwa wanachama wa CHADEMA ndo wamehamia CCM, hapana, bado wapo kabisa na cha kushangaza hawana imani na CCM na mteule Magufuli wenyewe bado wanaamini mabadiliko hayatatoka CCM hata siku moja ila ni mpaka upinzani uingie madarakani.

Hivyo basi, kwa kuwapa nafasi ya mbunge viti maalumu bila shaka italeta nguvu mpya ya mshikamao na mbunge huyo kazi yake nyingine itakuwa ni kuendelea kufungua matawi mapya huku akiyaimarisha yale yaliyopo tayari.

Mungu bado anaipenda CHADEMA na wana CHADEMA wote popote walipo ndani na nje ya nchi na ndiyo maana tumeona kabisa kuwa safari hii Chadema kimepata nafasi ya kuunda na kuongoza halimashauri nyingi yakiwemo na majiji makubwa mfano Arusha, Mbeya na pengine Jiji kuu la Dar. Hii ni fursa kubwa mno kuliko wakati wowte w uwepo wake ktk siasa za Tanzania.

Ombi lakini pia angalizo: Hakikisheni kuwa kwa mara ya kwanza Jiji la Dar limekuwa chini ya upinzani, na mfanye juu chini na uzalendo kabisa kuwa mgombea wa CCM hapati nafasi ya kuwa Mayor kwakuwa madiwani wengi na wabunge wengi Dar Es Salaam wanatoka upinzani.

Hivyo siasa ni mahesabu yalichanganyikana na science bila kusahau technique na akili-maarifa. Kulichukua Jiji kuu kama Dar ni nafasi ya heshima sana kwa chama pinzani kwa kuwa jiji hilo ndiyo sura ya nchi nzima. Hivyo basi fanyeni kazi usiku na mchana ili kuwaletea kile wananchi walichokikosa toka CCM na ndo kaana wakawakataa kwa njia ya kura. kwa kutumia mapato ya Jiji, Boresheni miundo mbinu, elimu, afya na nafasi za biashara kwa watu wenye hali ya chini maana hawa ndo walioichoka CCM, matumaini yao ni kwenu.

Hivo hivo na kwenye halimashauri za wilayani mfano Ukerewe, Arumeru Tunduma na kwinginepo fanyeni kiume mkawe hodari kwa vitendo na mipango yenu yote ilete matokeo bora kwa watu husika. Jengeni shule za secondari za kisasa zenye maabara na mazingira safi, jengeni shule za msingi safi na zenye ubora kwa watoto huku mkijali maisha ya waalimu kwa kuwajengea nyumba kwa kuwa hela mnazo za halimashari.

Naamini kufikia 2020 mtakuwa mmeshapata mtaji mkubwa mno mtakao uhubiri kwa watanzania huku mkitoa mifano ya kazi zenu kwenye zile halimashauri mlizoongoza kwa miaka mitano ijayo.

Hii itakuwa karata nzuri isiyohitaji maneno mengi bali iliyojaa vitendo na utimilifu wa ahadi walizonadi wagombea. Watu washachoshwa na maneno matamu ya CCM yasiyo na vitendo, basi ninyi mtakuwa mfano bora endapo mkizifanyia hayo niliyoshauri hapo juu halimashauri zenu yakiwemo na mjii, naamini uchaguzi ujao mtakuwa na nafasi kubwa sana ya kuongoza halimashauri kam siyo zote basi thelui tatu ya wilaya zote nchi nzima. Na hapo ndipo CCM itapoteza nguvu kabisa kuanzia serikali za mitaa hadi ngazi za wilaya na majiji, na huu ndo utakuwa mwisho wa CCM.

Naomba kuwasilisha kwenu wadau na wapenda nchi yetu si kwa ushabiki usiyo na ufahamu wa hali halisi ya Taifa letu ilivyo, kwamba CCM imetumia hila hasa kwa wale walioishia elimu ya msingi wengi wao wanaishi vijiji kwa utafiti wa TWAWEZA ulivyoonyesha.

By Obsaver

Zari Amvua Tiffah Hiziri iliyowekwa Mkononi Mwake na Bibi yake Mama Diamond

$
0
0
DIAMOND upoo! Zarinah Hassan a.k.a Mama Tiffah amechukua uamuzi mgumu wa kumvua mwanaye Tiffah ile dawa aliyokuwa amefungwa mkononi ‘hirizi’, hali iliyowafanya watu wengi wabaki na vingi viulizo.

Awali, Tiffah alivishwa hirizi hiyo siku chache baada ya kuzaliwa na Diamond akaizungumzia kuwa, ni utamaduni wa kawaida ambao kwa mila za Kibongo siyo tatizo.

Hata hivyo, wakati Diamond akitoa ufafanuzi huo baada ya watu kuibua maneno kuwa ‘hirizi’ hiyo inahusiana na mambo ya kishirikina, Zari alidaiwa kutokubaliana na uamuzi huo na ikadaiwa kuwa, alishindwa kugoma ili kutomkwaza mama Diamond ambaye ndiye aliyefanya zoezi hilo.

Baada ya Tiffah kudumu na ‘dawa’ hiyo kwa miezi michache (kitu ambacho si cha kawaida), Zari alipokwenda Sauzi alifanya maamuzi magumu ya kwenda kinyume na utamaduni na mzazi mwenzake na kuamua kuivua ‘hirizi’ hiyo.


Ushahidi wa Zari kufanya hivyo unaonekana kwenye picha za hivi karibuni alizoposti kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo moja inamuonesha Tiffah akiwa kavaa ‘hirizi’ hiyo na nyingine hana.

Kufuatia uamuzi huo, baadhi ya Wabongo walionesha kumshangaa Zari huku wakimponda kuwa alichokifanya siyo sawa.

Unajua ule ni utamaduni wa bwana wake, alitakiwa auheshimu hata kama kwao mambo hayo hayapo. Kitendo cha yeye kwenda Sauzi na kumvua Tiffah ile dawa ni kuonesha dharau, amemdharau Diamond na mama yake pia, siyo sawa,” alisema shabiki wa Diamond aliyejitambulisha kwa jina la Mariam.

Diamond hakuweza kupatikana mara moja kuzungumzia uamuzi wa mzazi mwenzake huyo.

Source:Global Publishers

Video: Young D akizungumzia kutengana na meneja wake na tetesi za kuvuta unga kwenye XXL

$
0
0
Tazama mahojiano ya Young Dee kupitia kipindi XXL ya Clouds Fm, alipokuwa akizungumzia kuhusu kutengana na label yake ya zamani MDB. Hii ni baada ya boss wa kampuni hiyo Max Rioba kudai kuwa rapper huyo alizingua. Itazame interview yote hapa Kama hukupata nafasi ya kuisikiliza iliporuka wiki iliyopita.

How Does DIAMOND Feel When Eating This, Look at ZARI’s thayos (PHOTOs)

$
0
0


How does DIAMOND feel when eating this, Look at ZARI’s thayos (PHOTOs)

Tamko: CUF yaipa ZEC siku tatu kukamilisha mchakato wa uchaguzi ........Isipofanya Hivyo Wananchi Wataamua Wenyewwe

$
0
0
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesema hakuna malalamiko yoyote yaliyowasilishwa katika siku ya upigaji kura.

Maalim Seif ambaye ni Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo taarifa kuwa mawakala wa CCM wameitwa pamoja na maofisa wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) katika kiwanda cha Makonyo Wilaya ya Chake Chake, kwa ajili ya kujazishwa fomu za malalamiko ili ziweze kutumika kudai kuwa yalikuwepo malalamiko katika zoezi hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Chama hicho zilizoko Mtendeni Mjini Zanzibar, Maalim Seif amesema njama hizo za CCM wameshazigundua na kawatozikubali.

Amesema njia pekee ya kuondosha utatanishi wa uchaguzi huo ni kukamilisha uhakiki wa majumuisho na kutangaza matokeo ya uchaguzi huo.

Amesema kwa upande wake pamoja na Chama chake, wataendeleza jitihada za kulipatia ufumbuzi suala hilo kwa kushirikiana na Jumuiya ya Kimataifa, ili kukamilisha uhakiki wa majumuisho ya kura kwa majimbo 14 yaliyobaki na hatimaye kutangazwa mshindi wa Urais si zaidi ya tarehe 02/11/2015.

Hata hivyo amesema iwapo hakutokuwa na hatua zozote zilizochukuliwa kukamilisha uchaguzi huo na kuheshimu maamuzi ya wananchi walio wengi hadi ifikapo tarehe 01/11/2015, viongozi wa CUF wataondoa mkono wao na kuwaachia wananchi waweze kutafuta haki yao kwa njia za amani.

Katika hatua nyengine Maalim Seif ameelezea kusikitishwa na vitendo vinavyofanywa na vikosi vya ulinzi na usalama kwa kuwatesa na kuwapiga raia wasiokuwa na hatia katika makaazi yao.

Amesema matukio hayo yamekuwa yakiripotiwa zaidi katika Wilaya za Magharibi “A na B”, na katika tukio la hivi karibuni amesema nyumba za raia wasiokuwa na hatia zimechomwa moto katika kisiwa cha Tumbatu na kuwafanya wananchi kuanza kupoteza uvumilivu.

Rais Mteule, Dr. Magufuli Aikosoa CCM.....Awataka Wanafiki Walioko Ndani Ya CCM Wajisalimishe Mapema

$
0
0
Rais Mteule Dk John Magufuli ameamua kufunguka kuhusu ugumu aliokabiliana nao wakati wa mchakato wa kampeni akieleza kuwa  uchaguzi wa mwaka huu umekuwa na changamoto kubwa kutokana na hujuma zilizofanywa na wanafiki waliojificha ndani ya Chama cha Mapinduzi(CCM).

Amesema amekerwa na hali hiyo kiasi cha kushindwa kuvumilia kuizungumzia jana, hasa baada ya kuona  uchaguzi umekwisha, hivyo ni vyema wanafiki hao wakajisalimisha kwa kutubu  kwa kuwa wamekigharimu chama hicho na kusababisha kiwe kwenye  wakati mgumu.

Amesema kwamba asiposema atakuwa ni  mnafiki kwa sababu uchaguzi umekwisha bora wawekwe wazi kwa sababu anaona ni bora kuishi na mchawi kuliko mnafiki, alimuomba Mwenyekiti  wa chama hicho Jakaya asiwahurumie wanaokihujumu, hivyo kusababisha washindwe kufika kwenye malengo.

“Nisiposema nitakuwa mnafiki msema kweli ni mpenzi wa Mungu watubu wajirekebishe ni mara kumi kuwa na mpinzani kutoka nje kuliko ndani ya chama,mipango yenu mtaipanga mchana usiku wataitoa nje ni afadhali uwe na mchawi atakuroga ufe kuliko mnafiki ndani, ” amesema  Maguli  katika  hafla  ndongo  ya  kumpongeza  baada  ya  kukabidhiwa  cheti  na  kuongeza:

“ Lakini ukweli utabaki kuwa ukweli  wewe ni mwenyekiti lakini ulikaa na wanafiki ndani ya CCM, ndiyo wametufanya wakati mwingine tufike hapa tulipofika, ndiyo wametufanya tufike hapa tulipo , leo kwa hiyo nakuomba ukitengeneze chama chetu vizuri ukishamgundua mnafiki usikae naye fukuza kesho, nimeona hili nilizungumze lakini unisamehe sana kwa sababu ningebaki nalo moyoni ningenisababishia kiungulia,ambacho nimekiona wakati nazunguka nikiwa kwenye kampeni,”

Kuanza kazi haraka
Magufuli  amewahakikishia wananchi kuwa  mara baada ya kuapishwa siku hiyo hiyo atanza kufanya kazi, kwa kuwa hakuomba nafasi hiyo kwa majaribio bali kuwatumikia wananchi kwa dhati.

Pia ameomba ushirikiano mzuri kutoka kwa wananchi ili waweze kufanikisha yale ambayo wameahidi wakati wa kampeni yeye na na Makamu Rais Samia Suluhu Hassan,  ili waweze kutimiza wajibu wa kuwatumikia  bila kinyongo na kuyatimiza yake waliyoahidi wakati wa kampeni.

“Kwa hiyo niwaombe  ndugu zangu watanzania wote bila kujali vyama vyetu tunaomba sana ushirikiano wenu , tusipopata ushirikiano wetu hatuwezi kuyatimiza kwa wakati, tisipopata ushirikiano mzuri kutoka kwenye mtatuchelewesha mara unataka kufanya hizi mara kuna maandamano yakashindwe, yakalegee  yakabaki huko huko yalikoanzia, kwa sababu sisi tunataka tufanye kazi,” alisema Dk Magufuli na kushangiliwa.

Aliongeza  kusema“ Katika kuzunguka kwetu kwa  wananchi wameona kuna kero nyingi za maji, umeme, miundombinu, wananchi wanataka zitatuliwe haraka, niwaombe watanzania bila kujali  vyama naomba ushirikiano wenu mzurI, ili tufanikishe hayo tuliyoahidi wakati wa kampeni,” alisisitiza.

Amsifu JK
Rais huyo Mteule alimsifu  Rais wa awamu ya nne Dk Jakaya Kikwete  akisema kwamba ni wa tofauti kwani licha ya kumtembeza katika maeneo karibu yote ya Ikulu , lakini pia amekuwa na busara za kukubali na kuendeleza madaraka ya kupokezana.

“ Nataka niseme mheshimiwa Rais una moyo wa pekee, Mungu akujalie sana viongozi wengi Afrika wanapokaribia kuondoka madarakani wengine huwa wanatengeneza hata katiba tofauti ili katiba ili waendelee kubaki madarakani, lakini wewe upo tayari kuondoka hata leo,” alisema.

Dk Magufuli alisema anaamini kwamba wananchi wataendelea kumuombea, kumlinda kwa kuwa amethamini Tanzania Kwanza, hivyo ataendelea kuhitaji busara zake pale itakapobidi atakapoingia madarakani.

Awali akitoa maoni yake mara baada ya Dk Magufuli kukabidhiwa cheti cha ushindi, Mratibu wa Taifa wa ULINGO, Dk Ave Maria Semakafu alisema anaamini wanawake wengi wamefurahishwa na ushindi huo kwa sababu kwa umewezesha pia kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi kuwa na Makamu wa Rais mwanamke Samia Suluhu Hassan.

“ Tumefungua ukurasa mpya kwani miaka 20 ya tamko la Mkutano wa wanawake  Duniani wa mwaka 1995 Beijing, tumekuwa na mrejesho mzuri kuhusu mwitikio wa Serikali kuweka ushiriki sawa wa nafasi za uongozi badala ya kuwafanya wanawake wawe watu wa kupiga kura kwa kuchagua viongozi wa ngazi mbalimbali lakini sasa nao wanachaguliwa, wanaaminika na kupewa nafasi kubwa ya uongozi kama hii,” alisema Dk Semakafu .

Alisema uchaguzi wa mwaka huu umekuwa ni wa kihistoria katika mambo mengi licha ya ushindani wa kisiasa lakini wanawake wawili walikuwa ni wagombea akiwamo Anna Mgwira aliyekuwa akigombea nafasi ya urais kupitia chama cha ACT Wazalendo.

“ Binafsi nilikuwa nafuatilia kwa karibu kampeni zao kulikuwa na mwitikio mkubwa wa watu walikuwa wakiwasikiliza na hakukuwa na hali ya udhalilishaji wa kuona kwamba hawastahili kwa sababu tu wao ni wanawake ,” alisema

Dk. Cheni Aipasukia Serikali Ijayo

$
0
0
MUIGIZAJI nguli nchini,Mahsein Awadh Said ‘Dk Cheni’ hivi karibuni ametoa ya moyoni kwa kusema kuwa serikali
ijayo iache mambo ya blabla bali itimize ahadi ambazo imekuwa ikitoa kwa wasanii ikiwa ni pamoja na kulinda haki
na masilahi yao.

Akizungumzia jinsi alivyouona uchaguzi, Dk Cheni alisema ameridhika na matokeo lakini akatoa rai kwa wale waliochaguliwa kuwaangaili wasanii kwa jicho la pili ili nao waweze kunufaika kwa kazi zao.

“Wakati wa blaablaa umepita, waliyoahidi kuhusu wasanii wayafanyie kazi, tunataka kunufaika na kile tunachokifanya, naamini serikali itaundwa na watu makini na kero zetu zitashughulikiwa ipasavyo,” alisema Dk. Cheni.

Chanzo: GPL


Why Would A LADY do This in The Gym? A Must Watch VIDEO for men.

$
0
0

Some ladies have perfected the skill of tempting men but this bootylicious lady has decided to take things to another level.

One even wonders whether she had gone to the gym for a work-out or to s3duce men.
Just click play and see what she did.


Mengi Azomewa Diamond Jubilee, Aokolewa na Membe

$
0
0
Mzee yamemkuta leo pale kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee leo.Ameokolewa na Mh Membe ambaye amemtoa kwa gari lake(pichani).Lakini pia Mwandishi Sam Maela wa ITV leo mchana kapata mshike mshike wa kushiba pale Lumumba,ilibidi aokolewa na polisi.Jamani haste haste.Kuna maisha baada ya Uchaguzi.Lile lilikuwa gemu tu.Mwacheni huyo Mzee,
 SOURCE - JAMII FORUMS

38 Kizimbani Kwa Kufanya Vurugu Mbagala Wakati wa Uchaguzi

$
0
0
Dar es Salaam. Watu 38 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi  K isutu wakikabiliwa na mashtaka manne likiwamo la kutoa vitisho vya shinikizo kwa msimamizi  atoe matokeo ya Ubunge ya Mbagala bila ya kufuata utaratibu na  kuchoma maboxi 11 ya kupigia kura  na karatasi za kupigia kura zenye thamani ya Sh 2.2 milioni.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali  Mwandamizi, Joseph Maugo akishirikiana na Wakili wa Serikali, Genis Tesha  walidai mbele ya Hakimu Mkazi, Emilius Mchauru kuwa Oktoba 27,2015 katika eneo la Mbagala Majimatitu  kwa nia ya uhalifu walifanya mkusanyiko na kuleta hisia ya uvunjifu wa amani.

Alidai kuwa washtakiwa hao walifanya kosa hilo kinyume na kifungu cha 74 na 75cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho 2002.

Katika shtaka la pili, wanadaiwa kuwa Oktoba 27,2015  huko Mbagala Majimatitu, kinyume  na kifungu cha 79 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho 2002 washtakiwa  hao walikusanyika  na kufanya waliyodhamiria kuyafanya na kusababisha uvunjifu wa amani na kuleta hofu katika jamii.

Maugo katika shtaka la tatu, washtakiwa hao kwa pamoja kinyume na kifungu cha 326(1) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho 2002 walichoma maboxi 11 ya kupigia kura na karatasi za kupigia kura zenye thamani ya Sh 2.2 milioni mali ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Wakili huyo wa Serikali katika shtaka la nne  alidai kuwa siku hiyo ya tukio washtakiwa  hao, walitoa vitisho na kumshinikiza msimamizi wa uchaguzi  atoe matokeo ya ubunge ya Mbagala bila ya kufuata utaratibu wa sheria.

Washtakiwa hao wanadaiwa kufanya kosa hilo kinyume na kifungu 89B (1)(b) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho 2002.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, washtakiwa wote walikana  na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi  wa kesi bado haujakamilika.

Hakimu Mchauru alimtaka kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao wanaaminika ambao kila mmoja atasaini bondi ya Sh 2 milioni hata hivyo washtakiwa hao walipelekwa rumande baada ya kushindwa kukamilisha masharti hayo.

Kesi imeahirishwa hadi Novemba 12, 2015  kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.

By Tausi Ally, Mwananchi


Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images