Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live

Mkoa wa Arusha Waongoza Kwa Watu Binafsi Kumiliki Bastola..

$
0
0
Mkoa wa Arusha umetajwa kati ya mikoa ya pembezoni nchini ambayo inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanaomiliki silaha za moto, hasa bastola.

Katika maeneo ya burudani katika jiji la Arusha kumekuwapo na matukio ya watu kutishiana kwa bastola jambo ambalo limesababisha ulinzi kuimarishwa katika maeneo haya na baadhi ya wateja kuzuiwa kuingia ndani na silaha hizo.

Uchunguzi wa kina uliofanywa na Mwananchi umebaini kuwa idadi kubwa ya vijana katika jiji la Arusha wanamiliki bastola, baadhi kihalali na wengine kinyume cha sheria.

Kwa wanaomiliki kihalali ni wale waliofuata utaratibu za kisheria za umiliki, ambao unaanzia ngazi ya kijiji au mtaa, kujadiliwa na baadaye kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, kamati ya mkoa na hatimaye makao makuu ya polisi.

Hata hivyo, kati ya wanaomiliki kihalali, kuna kundi ambalo linamiliki bastola hizo kihalali kupitia mawakala ambao hulipwa kati ya Sh1.5 milioni hadi Sh2 milioni.

Uchunguzi umebaini kuwa watu wengi wanaomiliki silaha hizo kinyume cha sheria ndiyo wanazitumia katika matukio ya uhalifu.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas licha ya kukiri vijana wengi kumiliki bastola katika jiji hilo, alisema wengi wanaozimiliki wamezipata kwa kufuata sheria.

Hata hivyo, katika kudhibiti silaha hizo, alisema jeshi hilo kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama limesitisha kutoa vibali vya umiliki wa bastola.

Tumesitisha kutoa vibali vya bastola lakini tunatoa vibali vya silaha nyingine kwa mahitaji maalumu, lakini silaha zilizopo mikononi mwa watu ni zile ambazo zilitolewa kipindi kirefu cha nyuma,” alisema.

Alisema baadhi ya waliopata bastola kipindi cha nyuma ni wafanyabiashara na wachimbaji wa madini katika maeneo ya Mererani kulingana na biashara zao.

Hata hivyo, alisema silaha hizo zilitolewa kihalali lakini baadhi ya wamiliki wamekuwa si waangalifu katika utunzaji na hivyo kufanya baadhi kuwafikia watu wasio waaminifu.

Katika matukio ya ujambazi ambayo yanatokea hapa Arusha, silaha ambazo tunakamata ni zile ambazo zilizotolewa kihalali lakini wamiliki wake waliibiwa au kupoteza,” alisema.

Alisema uhakiki wa silaha ambao umekuwa ukifanywa na jeshi hilo na kwa kiasi kikubwa umesaidia kuziondoa bastola mikononi mwa watu wasio waaminifu.

Kuuzwa kwa silaha

Mwananchi imebaini kuwa, baadhi ya wamiliki wa silaha hasa bastola wamekuwa wakiuza mitaani kutokana na hali ngumu ya maisha.

Joram Kaaya mkazi wa Ngulelo alilieleza gazeti hili kuwa kipindi cha nyuma vijana wengi wa Mirerani walinunua silaha kihalali kutokana na biashara zao lakini sasa kutokana na kuporomoka biashara ya madini ya Tanzanite wamekuwa wakiuza.

Bastola zinauzwa kati ya Sh1,000,000 hadi 2.5 milioni kutoka kwa wamiliki lakini wanakueleza kufuata taratibu za umiliki, kwa kuandika barua ya umiliki wa silaha ngazi ya mtaa na kwenda polisi kabla ya kukabidhiwa silaha na kitabu chake,” alisema.

Mkazi mmoja wa Arusha, aliyeomba kuhifadhiwa jina, lake alikiri kuwapo kwa madalali wa silaha ambao wamekuwa wakifuata taratibu za umiliki wa silaha.

Mimi mwenyewe nimenunua bastola yangu kwa mtu lakini kabla ya kumiliki nilifuata taratibu zote za kipolisi na kiserikali na nimekuwa nikiilipia kila mwaka,” alisema.

Hata hivyo, Kamanda Sabas alikemea utaratibu wa kununua silaha mitaani akisema ni kuvunja sheria.

Ni makosa kisheria, kuuza na kununua silaha mitaani ambao watakamatwa watafikishwa katika vyombo vya sheria, kuna taratibu za umiliki kwa ambao wanahitaji silaha ni vyema kuzifuata,” alisema.

Silaha kutoka nje

Wakati polisi wakieleza kuwapo udhibiti mkubwa katika uingiaji wa silaha katika njia haramu, taarifa zilizolifikia Mwananchi zinaeleza kuwa wapo watu wanaziingiza kutoka nje ya nchi kupitia njia za panya.

Silaha hizo, zinaelezwa kuingizwa kwa kubadilishana na bidhaa mbalimbali kama vyakula, mifugo na fedha.

Katika Wilaya ya Ngorongoro pekee, ambayo ipo mpakani na nchi jirani na Kenya, mara kadhaa polisi, wamekuwa wakikamata silaha zinazomilikiwa kinyume cha sheria ambazo zinamilikiwa na makundi ya wafugaji na wakulima ambao wamekuwa wakipigana mara kwa mara kugombea ardhi.

Mwaka juzi silaha zaidi ya 80 zilikamatwa katika operesheni ya polisi katika wilaya ya Ngorongoro pekee na kumekuwapo na taarifa za wakazi wengi wa wilaya hiyo kumiliki silaha kinyemela.

Wilaya nyingine zenye wamiliki wengi wa silaha ama halali au haramu ni Arumeru na Longido huku wilaya za Monduli na Karatu zikiwa hazijaathiriwa sana na kuzagaa kwa silaha.


Mwili wa Mwanafunzi Mtahiniwa wa Kidato cha Mne Aliyesombwa na Mafuriko Waopolewa

$
0
0
 Miili ya watu wawili waliokufa maji baada ya kusombwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zilizonyesha mwanzoni mwa wiki hii jijini Mwanza, ukiwamo wa mwanafunzi, imeopolewa kwenye mwalo wa Ziwa Victoria.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo, alisema miili iliyoopolewa ni wa mwanafunzi huyo wa Shule ya Sekondari ya Nyamanoro, Zainabu Shaaban (18) aliyekumbwa na mkasa huo wakati akienda kufanya mitihani taifa ya kidato cha nne na wa mwendesha bodaboda, Ibun Rashid.

Matukio hayo yalitokana na mvua hizo zilizonyesha Novemba 2, mwaka huu kwa saa tano huku zikiharibu miundombinu, mali na nyumba kujaa maji.

Mkumbo alisema miili hiyo iliopolewa kwa ushirikiano wa polisi na wananchi na kwamba ilikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya maziko.

Awali, akizungumza nyumbani kwake, mama mlezi wa mwanafunzi huyo, Anastazia Alex alisema alitoka nyumbani akiwa na mwanafunzi mwenzake, Asnaty Ally kwenda shule na wakati wakivuka daraja aliteleza na kusombwa na maji.

Wakati wanatoka hapa (nyumbani) mvua haikuwa kubwa, ila waliondoka wamevaa nguo za nyumbani, zile za shule waliziweka kwenye mfuko ili zisilowane kabla hawajafika shuleni. Inasemekana aliteleza kwenye daraja akaanguka, akaanza kupiga yowe kuomba msaada,” alisema Alex.

Alisema kutokana na muda huo mvua kuwa iliendelea kunyesha, hakuweza kupata msaada hadi mwenzake alipokwenda kutoa taarifa shuleni.

Mkuu wa Sekondari ya Nyamanoro, Praxeda Kaijage alisema walipata taarifa hizo kwa mwanafunzi huyo baada ya kufika shuleni hapo.

Alisema baada ya kutoa taarifa kwa walimu, walianza kufuatilia kwa kushirikiana na familia yake. “Tulipewa taarifa na mwanafunzi mwenzake aliyekuwa naye (Asnaty) kuwa ameteleza kwenye daraja, akachukuliwa na maji, tulichukua hatua haraka kwenda eneo la tukio ila hatukuona kitu, tulifanya jitihada za kuwasiliana na familia tukawa tunamtafuta ila hatukufanikiwa,” alisema Mwalimu Kaijage.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyamanoro Kaskazini, Shija Salileje alisema waliitisha mkutano na kushirikiana kumtafuta mwanafunzi huyo kwenye mitaro hadi ziwani. Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela, John Wanga alisema licha ya kutoa boti mbili, waliagiza watendaji wa kata, mtaa na wenyeviti kumtafuta mwanafunzi huyo na kuhakikisha anapatikana.

Mwanamke Ashambuliwa Kwa Kuzungumza Kiswahili Marekani

$
0
0
Mwanamke aitwaye, Asma Jama ameshambuliwa nchini Marekani kwa kuongea Kiswahili.

Jama alikuwa amekaa na familia yake kwenye mgahawa wa Applebee huko Minnesota, akikata kiu na juice huku mazungumzo yakiendelea kabla ya kujeruhiwa vibaya mdomoni. Mwanamke aliyekuwa amekaa jirani yake alimponda na glasi nzito ya bia mdomoni.

Sababu? Jama alikuwa akizungumza Kiswahili na familia yake.

Siamini baada ya miaka yote hii mtu ananipiga sababu niko tofauti,” alisema Jama. “Mtu ananipiga kwasababu nilikuwa nikizungumza lugha ya kigeni.”

Shambulio lilimwacha Jama na majeraha usoni pamoja na mdomo kuchanika kiasi cha kushonwa nyuzi 17.

Jodie Burchard-Risch, 43, na mume wake, walikuwa wamekaa kwenye mgahawa huo jirani na Jama, aliyekuwa ameketi na binamu na watoto wa nduguze. Wawili hao walichukizwa baada ya kumsikiliza Jama na familia yake wakizungumza lugha ngeni.



Jama alisema wawili hao waliwaambia waende nyumbani. “Walisema ukiwa Marekani unatakiwa kuzungumza Kiingereza.”

Jama, ambaye ni msomali, alihamia Minnesota mwaka 2000 kutoka Kenya. Anazungumza lugha: Kiingereza, Kiswahili na Kisomali.

Jumatatu hii, Burchard-Risch alishikiliwa kwa kosa la shambulio.

Kutokana na shambulio hilo, Jama anadai hana amani tena na anafikiria kuhama Minnesota. Amesema anaweza kuungana na dada yake aliyehama Minnesota mwezi June na kwenda Dallas.

Taarifa Kuhusu Mkutano wa Chadema Uliyopangwa Kufanyika Viwanja vya Jagwani Ambapo Lowassa Atahutubia Hii Hapa

$
0
0
Taarifa inatolewa kwa wapenzi, mashabiki, wafuasi na wanachama wa CHADEMA, wanaUKAWA na umma wa Watanzania wote wapenda mabadiliko kwa ujumla kuhusu mkutano mkubwa wa hadhara wa kesho katika Viwanja vya Jangwani, jijini Dar Es Salaam ambao umeshatangazwa kwa njia mbalimbali za upashanaji habari, umeahirishwa hadi hapo maelekezo na utaratibu mwingine utakapotolewa baadae.
Ni vyema kuwataarifu ujumbe huu mapema maelfu ya Watanzania ambao tunajua wamejiandaa kuhudhuria kwa wingi kusikia 'neno kutoka kwa Rais wa Mioyo ya Watanzania' na viongozi wakuu wa vyama vinavyounda UKAWA juu ya uelekeo wa nchi kwenye mkutano huo ambao pia ulilenga kuwatambulisha wabunge wote wa UKAWA na kuwashukuru Watanzania kwa namna walivyounga mkono agenda za MABADILIKO kwenye mapambano makubwa ya ushindi wakiwa begabega na Jemadari Lowassa, Babu Duni, wagombea ubunge na udiwani wa UKAWA.

Nani Unahisi Atakuwa Waziri/Waziri Mkuu wa 2015-2020?

$
0
0
Baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kumtangaza rais mteule wa awamu ya tano, nani unahisi atateuliwa na mheshimiwa John Pombe Magufuli kuwa Waziri Mkuu ?

Magufuli, Kama Kweli Unapinga Ufisadi Mteue Kafulila Kuwa Mbunge

$
0
0
Najua kwa mujibu wa katiba ya nchi najua una viti kumi vya Rais. Naomba sana umteue kafulila Kuwa mbunge ili dhamira ya kupinga ufisadi ifanyike kwa vitendo pia atakusaidia kukamata majizi na mafisadi yaliyotufikisha hapa na pia imani yako kwa watanzania itaongezeka maradufu

Maskini..Lowassa Asalimu Amri Kwa Polisi...Atoa Ujumbe Huu Hapa Kwa Wafuasi Wote wa Ukawa Kuhusu Mkutano Wake

$
0
0
Maskini..Lowassa Asalimu Amri Kwa Polisi Kuhusu Mkutano aliokuwa aufanye kuongea na Wananchi...Atoa Ujumbe Huu Hapa Kwa Wafuasi Wote wa Ukawa Kuhusu Mkutano Wake

Baraza Kuu La CUF Lakataa Kurudia Uchaguzi Zanzibar!

$
0
0
Baraza Kuu la Chama cha Wananchi (CUF), limekutana na kusisitiza kuwa hawatarudia uchaguzi wa Zanzibar.

Mkutano huo ulifanyika jana mjini hapa ambapo walijadili mkwamo wa kisiasa nchini na juhudi zinazoendelea katika kukabiliana na hali hiyo.

Naibu katibu mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazrui alikaririwa akisema baada ya kikao hicho, “Wanaosema uchaguzi urejewe waachieni wenyewe, sisi katika CUF hakuna habari hiyo. Kwa sasa kutangaza matokeo ya uchaguzi ndiyo msimamo wetu, ili mshindi atangazwe na kuapishwa .” alisema Mazrui

Awali Kaimu Mwenyekiti wa Taifa wa CUF, Twaha Taslima akiwa na safu ya juu ya uongozi wa chama hicho, walisema kuna haja ya kuendelea kutafuta haki ya Wazanzibari kwa kuitaka Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kutangaza matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka huu, ili mshindi ajulikane na aweze kuapishwa.

Taslima alisema pia baraza hilo lilibariki juhudi za mgombea urais wa Zanzibar kupitia CUF akiungwa mkono na Ukawa, Maalim Seif Sharif Hamad kutafuta suluhisho la mkwamo huo baada ya Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya uchaguzi wa visiwani humo hatua iliyopingwa taasisi za ndani na za kimataifa.

Juhudi hizo ni pamoja na mazungumzo ya Maalim Seif na wanadiplomasia wakiwamo mabalozi mbalimbali waliopo nchini, yaliyofanyika katika Ofisi za Ubalozi wa Canada, Mtaa wa Mirambo Na. 50, jijini Dar es Salaam.

Aliongeza kuwa, Maalim Seif pia alizungumza faragha kwa saa moja na Rais mstaafu, Jakaya Kikwete, Ikulu Dar es Salaam.

Katika juhudi hizo, Maalim Seif aliliarifu Baraza Kuu jinsi alivyoishawishi jumuiya ya kimataifa isimame pamoja na ukweli, kwamba kilichotendeka Zanzibar ni kupinduliwa kwa demokrasia hivyo kutaka wananchi wapewe haki yao.

Tumesikia na kushuhudia kauli za mataifa zikishinikiza Serikali na hata utawala mpya ulioingia madarakani, katika Jamhuri ya Muungano kwamba maamuzi ya Wazanzibari yaheshimiwe kwa ZEC kumtangaza mshindi ili aweze kuapishwa,” alisema Maalim Seif. Huku akinukuu taarifa ya Pongezi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerr kwa Rais mpya Dk John Magufuli.

Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ambayo bado ipo katika muundo wa Umoja wa Kitaifa aliongeza kuwa , “Tunashukuru dunia nzima inatuunga mkono kwa jambo hili”.

Kabla ya kikao hicho kilichoanza saa 8.30 mchana kilitanguliwa na Kamati Tendaji ya Taifa ya CUF ambacho kilizungumzia uteuzi wa viti maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Chanzo: Mwananchi

Hatimaye Salva Rweyemamu Aondoka Rasmi Ikulu. Kukabidhi Ofisi Kesho Nov 9, 2015

$
0
0
I depart the State House a Happy Man - Salva

One of the most admirable attributes of this digital age sweeping our lives, is the capacity it has created for would be volunteers, who are in no way in shortage, in our society, to create and disseminate discriminatory information regarding other people.

A good example is the nonsense information that has been doing the rounds in the last few hours about my departure, or imminent departure, from my position as the Presidential Communications Director at the State House.

The truth of the matter is that during my eight plus years at the State House, I have signed numerous contracts, the last of which expired on September 11, this year, 2015 and it was renewed for a further 62 days.

The end of this contract, as far as I am concerned, is Tuesday, November 10, this year 2015. I will officially hand over office tomorrow, Monday, Tuesday 9, 2015 to Ms. Premi Kibanga, my very able assistant for all those years. In fact today, Sunday, I was clearing my office and preparing my handover notes.

I leave the State House a very happy person and I would like to thank President Dr. John Pombe Joseph Magufuli and the 4th President of our country HE Jakaya Mrisho Kikwete for their trust in my capacity to be their assistant and the opportunity they gave me to serve our people and our country at this level.

I would also like to thank all the State House staff under the leadership of, first Chief Secretary Philomen Luhanjo and now Ambassador Ombeni Yohana Sefue, for their unwavering support over all these years. They have been exceptional.

Finally, I owe huge gratitude to my friends and colleagues in the media. Their invaluable support over the years has been the pillar and strength of my work at the State House during the Kikwete Administration. I thank you all.

Salva Rweyemamu
November 8, 2015

Samattha Mfungaji Bora, TP Mazembe Mabingwa Africa

$
0
0
Nyota wa Tanzania na timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Samatta amefunga goli moja kwenye ushindi wa magoli 2-0 iliyoupata timu yake ya TP Mazembe kwenye mchezo wa marudiano wa fainali ya vilabu bingwa Afrika dhidi ya USM Alger mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Stade TP Mazembe Lubumbashi, Congo DR.

Ushindi huo umeifanya TP Mazembe ichukue kombe la vilabu bingwa barani Afrika kwa mara ya tano lakini ikiwa ni mara ya kwanza kwa wachezaji wa kimataifa wa Tanzania wanaokipiga kwenye klabu hiyo Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.

Samatta na Ulimwengu wameweka rekodi ya kuwa watanzania wa kwanza kunyanyua kombe la klabu bingwa barani Afrika huku nyota wengine waliong’ara zamani kwenye medani ya soka wakishindwa kufanya hivyo.

Mazembe ilishachukua kombe hilo mwaka 1967, 1968, 2009, 2010 na mwaka huu 2015 imefanya hivyo.

Kipindi cha kwanza cha mchezo huo hakikua na mashambulizi mengi kwa timu zote mbili hasa kwa upande wa TP Mazembe ambao walionekana kama wanalinda ushindi wao walioupata kwenye mechi ya awali nchini Algeria. Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa sare ya bila kufungana.

Kipindi cha pili Mazembe walianza kusaka ushindi na wakafanikiwa kupata goli la kuongonza lililofungwa na Mbwana Samatta kwa mkwaju wa penati dakika ya 75 baada ya Roger Assale kuangushwa na beki wa USM Alger akiwa kwenye eneo la hatari.

Goli hilo limemfanya Samatta kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo kwa kufikisha jumla ya magoli nane na kumpiku Bakry ‘Al Medina’ Babiker wa Al Merreikh ambaye wamekua wakichuana kwa muda mrefu.

Wakati dakika zikiwa zinaelekea ukingoni Mbwana Samatta alitengeneza goli jingine ambalo lilifungwa na Roger Assale ambalo lilimaliza kabisa ndoto za USM Alger kutwaa ubingwa huo kwa mara ya kwanza.

TP Mazembe wamekuwa mabingwa kwa jumla ya magoli 4-1 dhidi ya USM Alger, mchezo wa fainali ya kwanza uliochezwa Algiers, Algeria ulimalizika kwa Mazembe kushinda kwa magoli 2-1 huku mchezo wa marudiano ambao umepigwa jijini Lubumbashi, Congo DR ukimalizika kwa TP Mazembe kushinda kwa magoli 2-0.

Ubingwa huo unawapa Mazembe tiketi ya kushiriki fainali za vilabu bingwa duniani zitakazofanyika December mwaka huu nchini Japan.

TP Mazembe inaungana na mabingwa wa Ulaya Barcelona na mabingwa wa Copa Libertadores River Plate ambao tayari wamejihakikishia nafasi kwenye fainali hizo huku mabingwa wa Oceania klabu ya Auckland City pamoja na mabingwa wa Amerika Kusini Club America wakiwa tarari kwenye orodha hiyo.

Bingwa wa Asia kati ya Al-Ahli au Guangzhou Evergrande Taobao na J-League wataungana wataungana na vilabu vingine na kufanya jumla ya vilabu nane vitakavyocuana kwenye fainali hizo.
Source:Shafih Dauda

Zijue Saa 72 za Dk Magufuli Akiwa Ikulu..Afanya Kazi Usiku na Mchana

$
0
0
Baada ya Rais John Magufuli kuanza kwa kishindo maisha ya Ikulu kwa kutekeleza kauli mbiu yake ya “hapa kazi tu”, watu walioongea na gazeti hili wameonyesha kuridhishwa, lakini baadhi wakimpinga na wengine kumkosoa.

Akiwa kwenye kampeni za kuutaka urais kwa tiketi ya CCM, alisema ataanza kazi mara baada ya kuapishwa, na atafanya kazi usiku na mchana.

Katika siku nne za kwanza, Rais huyo wa Serikali ya Awamu ya Tano pia ametoa maagizo kadhaa, ikiwemo kuitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuhakikisha inakusanya kodi hasa kwa kuwabana wafanyabiashara wakubwa, kuziba mianya ya ukwepaji kodi na kutangaza elimu bure kuanzia mwakani.

Rais Magufuli alitoa agizo hilo baada ya kufanya kikao na makatibu wakuu, naibu makatibu wakuu, Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade kwa lengo la kutoa mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Tano.

Alisema mabalozi wa Tanzania wanaowakilisha nchi huko nje, ndiyo watakaotakiwa kufanya shughuli zote kwenye nchi wanazofanya kazi hadi hapo atakapolitolea suala hilo uamuzi mwingine.

Wasemavyo wasomi

Wengi waliozungumza na gazeti hili walimsifu Rais Magufuli kutokana na kuagiza walipa kodi, hasa wafanyabiashara wakubwa wadhibitiwe, kusimamisha safari za nje, wakisema fedha zitakazookolewa zitasaidia katika kutekeleza ahadi ambazo yeye na chama chake walizitoa wakati wa kampeni.

“Ingawa kitaalamu huwezi kupima utendaji kwa siku tatu, Rais Magufuli ameanza kazi kwa kutoa maagizo ili kuhakikisha anatekeleza aliyoahidi kama kutoa elimu bure ya msingi hadi sekondari,” alisema Profesa Lugano Kusiluka wa Chuo Kikuu Huria (OUT).

“Sasa ni wajibu wa watendaji wa serikali kutekeleza.”

Sifa kama hizo zilitolewa na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Charles Marwa, ambaye alisema hatua ya kuanzia kuwabana walipa kodi wakubwa ni mwanzo mzuri, akishauri Dk Magufuli aanze kuwabana maafisa wa juu wa TRA ndipo ashuke kwa maafisa wa chini kudhibiti kodi.

Suala la kodi pia lilizungumziwa na Dk Alexander Makulilo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye alisema baadhi ya wafanyabiashara wakubwa ndiyo wakwepaji wakubwa wa kodi.

“Wakati wafanyakazi wenye mishahara mikubwa ndiyo wanaolipa kodi kubwa serikalini, baadhi ya wafanyabiashara wakubwa ndiyo wanaoongoza kukwepa na kusamehewa kodi,” alisema.

Alitaka juhudi kubwa ifanyike katika kuhakikisha wafanyabiashara hao hawakwepi kodi wala kupewa misamaha.

Kwa upande wake, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, George Shumbusho alisema Dk Magufuli ameanza kazi vizuri kutokana na kuchukua hatua zinazolenga kuhakikisha Serikali inakuwa na fedha.

Alisema chama chake cha CCM kilitoa ahadi nyingi kwa wananchi wakati wa kampeni na hivyo ili kutimiza ahadi hizo ni lazima kodi zikusanywe na kubana matumizi ya Serikali.

Dk Benson Bana, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, pia alipongeza uamuzi wa kudhibiti walipa kodi akisema kama kila mmoja angekuwa analipa, nchi isingekuwa na utegemezi katika bajeti kama uliopo sasa.

“Wafanyabiashara wengi hawalipi kodi, wanashirikiana na wafanyakazi wenye dhamana ya kukusanya kodi kukwepa kodi, wanagawana fedha za Watanzania. Kama Rais Magufuli ameliona hilo, basi huo ni mwanzo mzuri,” alisema.

Dk Bana pia alisema Rais anatakiwa kuangalia eneo la matumizi ya magari kwa watumishi wa Serikali na kushauri walipwe posho ya mafuta badala kutumia magari ya kifahari ambayo alisema yanatafuna fedha nyingi za walipa kodi.

“Wanaotakiwa kutumia magari ya Serikali ni mawaziri na manaibu wao, makatibu wakuu, manaibu wao na wakurugenzi waandaliwe utaratibu mwingine wa kupewa posho ya usafiri ili watumie magari binafsi,” alisema.

Alisema hivi sasa inawezekana bosi akawa anaishi Bunju na dereva wake Mbagala ambako ndiko gari linakolala, hali ambayo alisema inasababisha kuwa na gharama kubwa za uendeshaji.

Profesa wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, George Shumbusho alisema iwapo Serikali ya Dk Magufuli itawategemea wafanyabiashara wadogo walipe kodi, haitaweza kutekeleza ahadi zake kwa sababu hakutakuwa na fedha.

Edward Porokwa, ambaye ni mkurugenzi wa shirika la PINGOs Forums, alisema kutaka walipakodi wakubwa walipe kodi, ni jambo zuri ambalo litaondoa misamaha ya kodi inayoliangamiza taifa.

Safari za nje hazina tija

Wachambuzi hao pia waliangalia agizo la kusitisha safari za nje hadi kwa kibali maalumu na kutaka shughuli ambazo zingefanywa na watendaji waliopo hapa nchini, zifanywe na mabalozi.

Mabalozi sasa watakuwa na majukumu zaidi katika kuwakilisha nchi nje,” alisema Martine Masawe, mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe ambaye alimsifu Rais kwa uamuzi wa kusitisha safari za nje.

Alisema njia hiyo itapunguza matumizi makubwa ya nchi na kufanya fedha kuwa na matumizi katika masuala ya kusaidia vipaumbele vilivyopo.

Maoni hayo yanalingana na ya Dk Alexander Makulilo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)aliyesema safari za nje zimekuwa zikitumia fedha nyingi za walipakodi wakati kuna mabalozi wanaowakilisha nje ya nchi.

Nashauri yeye ndiye awe mfano kwa kupunguza safari zake nje kwa sababu Rais na ujumbe wake hutumia gharama kubwa katika safari za nje,” alisema.

Lakini Dk Bana alikwenda mbali zaidi kwa kusema Rais anatakiwa kushikilia msimamo wake kwa kuwa suala la safari za nje limekuwapo tangu Serikali ya Awamu ya Kwanza.

“Ikulu ndiyo ilikuwa inatoa vibali kwa watumishi wanaosafiri kwenda nje ya nchi, lakini usimamizi umekuwa mbaya na kusababisha watumishi kusafiri mara kwa mara nje ya nchi kwenye mikutano ambayo wakifika wala hawachangii chochote,” alisema Dk Bana ambaye amebobea kwenye sayansi ya siasa.

Ameanza kazi vizuri kwa sababu eneo la safari za nje linapoteza fedha nyingi wakati watumishi wengi wanakwenda huko kwa ajili ya kufanya manunuzi.

Pia Faraja Christotoms, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), alimtahadharisha kuwa maagizo hayo yasiwe nguvu ya soda.

Kasi aliyoanza nayo siyo mbaya, tunaomba tu isiwe kama nguvu ya soda,” alisema.

Hata Rais (wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya) Kikwete alianza hivyo hivyo kwa kutembelea wizara mbalimbali. Lakini hawa ni watu wawili tofauti. Tumpe muda tuone, labda ana dhamira nzuri na nchi yake.

Hoja za wanaomkosoa

Maagizo na utendaji wa Rais katika siku zake nne za kwanza hayajakosa wakosoaji.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Paul Losolutie alisema agizo la kutoa elimu bure linahitaji kwenda sambamba na vifaa vya elimu.

“Hata kama watasema elimu bure wakati bado shule hazina madawati na walimu hawalipwi vizuri itakuwa haina maana kusema elimu ni bure wakati wanafunzi katika fomu zao za kujiunga na shule wataambiwa waje na mchango wa maabara, madawati, mafyekeo, walinzi na majembe,” alisema.

Alishauri utekelezaji wake uwe ni pamoja na kufuta michango ya wazazi, akisema kwa sasa ada ya shule hizo ni Sh 20,000, lakini michango ya mwanafunzi anayeingia kidato cha kwanza inafikia Sh300,000 jambo ambalo ni mzigo kwa mzazi kuliko ada.

Mwanafunzi wa Chuo cha Mipango Dodoma, Godrick Ngoli, alisema uamuzi wa kutoa elimu bure ni mzuri, lakini ingefaa zaidi baraza la mawaziri kushirikishwa kwanza ili kupanga mipango ya utekelezaji wake kwa pamoja.

Mwingine aliyemkosoa ni Profesa Semboja ambaye alisema Dk Magufuli alitakiwa kwanza kuhakikisha mifumo yote ya Serikali inafanya kazi vizuri kwa namna inavyotakiwa.

Alisema iwapo Rais atafuatilia kila kitu, itafikia wakati atachoka na kuona mzigo mkubwa.

Alimshauri atumie siku 100 za kwanza kusoma mifumo inavyofanya kazi na kuwapa majukumu watendaji wake ili kurekebisha kasoro atakazokuwa amezibaini.

Urais ni taasisi, na siyo kwamba Rais atafanya kila kitu mwenyewe. Rais Magufuli ahakikishe anakuwa na timu nzuri ya watendaji ambayo itamsaidia kusimamia yale yote anayotaka yafanyike bila yeye kusema neno,” alisema.

Pia, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Paul Rosolutie alitilia shaka utekelezaji wa elimu bure na kusema suala hilo linahitaji muda wa kutosha ili kuweka mipango ya utekelezaji wake bila kuathiri huduma nyingine muhimu kwa shule za umma.

Hata zile Sh20,000 wanazolipa wanafunzi zilikuwa hazitoshi kutatua matatizo ya shule na Serikali inashindwa kupeleka fedha za wanafunzi. Sidhani kama hilo lilifanyika, vinginevyo itakuwa ni mzigo mkubwa kwa watendaji wa Serikali katika kulitekeleza,” alifafanua.

Wapinga kusitishwa safari

Marwa wa Chuo Kikuu cha Mzumbe pia alipinga uamuzi wa kusitisha safari za nje akisema utasababisha matatizo kwa kuwa makubaliano mengi ya nchi huhusisha mawaziri na watumishi wa Serikali.

Sasa kusema mabalozi ndiyo watakuwa wanawakilisha nchi katika baadhi ya mambo haitawezekana,” alisema.

Marwa alitoa mfano Rais aliyepita aliyesitisha safari zote za nje isipokuwa kwa kibali cha Serikali wakati akiingia madarakani mwaka 2005, lakini akakumbana na ugumu katika utekelezaji wa agizo hilo, na badala yake safari zikaongezeka.

Maoni ya wananchi

Wananchi wengine walioongea na Mwananchi pia walisifu hatua ambazo Dk Magufuli ameshachukua hadi sasa.

Mwenyekiti wa Kampuni za Ulinzi, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Kasimir Kubaja alisema  kuzuia safari za viongozi nje ya nchi ni safi kwa sababu zinatumia fedha nyingi za kigeni wakati ukweli wapo mabalozi ambao wangeweza kutekeleza majukumu hayo.

Hata hivyo Kubeja alimshauri Rais Magufuli kufuatilia kwa ukaribu suala la wazabuni serikalini akisema fedha nyingi zinaibwa katika manunuzi.

Naye mhandisi wa umeme wa mjini Mbeya, George Mwang’ombe alisema kitendo cha kusitisha safari za nje kwa viongozi ni kizuri, lakini kiende sambamba na kupiga marufuku magari ya Serikali kwenda kwenye baa, kuzuia posho za vikao vya ndani  na kuwabana watendaji wa halmashauri wafanye kazi za wananchi.

Mwang’ombe pia alishauri Serikali itoe fedha za uendeshaji kwenye shule za sekondari na za msingi ili kuepusha ukata utakaosababishwa na kutolewa elimu bure.

Mkurungezi wa asasi ya Kukuza Utawala na Uwazi Tanzania (IGT), Edwin Soko alisema Rais amefanya vizuri kufuta safari za nje na kwamba njia hiyo itamfanya aweze kutimiza ahadi zake, kama kutoa Sh50 milioni kwa kila Kijiji, kujenga barabra za kisasa pamoja na kununua meli mpya.

Ofisa Ustawi wa Jamii, Mwanza, Davis Justine alisema Dk Magufuli amefanya vizuri kuagiza wafanyabiashara wakubwa wabanwe na kulipaa kodi na kufuta safari za nje, kwa kuwa zilikuwa zinapoteza fedha nyingi ambazo zingewekezwa katika sehemu nyingine zingeleta maendeleo.

Sharon Sauwa, Lauden Mwambona, Lilian Lucas, Ngollo John, Peter Elias, Mussa Juma na Raymond Kaminyoge.


Niko Tayari Kukamatwa Kwa Kujitangaza Mshindi wa Uchaguzi Zanzibar-Maalim Seif

$
0
0
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema yuko tayari kukamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka, kama kitendo chake cha kujitangazia ushindi ni kosa.

Maalim Seif alikuwa akizungumza na viongozi wa majimbo, makatibu wa matawi, wajumbe wa mkutano mkuu, wajumbe wa kamati za utendaji za ngazi zote na watendaji wa chama hicho.

Alisema haoni hatua yake ya kuitaka Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imtangaze kuwa mshindi haina matatizo kwa kuwa ana uhakika kuwa ndiye aliyeshinda kwenye uchaguzi.      

Nilichosema ni ZEC initangaze kwa kuwa nilishinda uchaguzi. Je, hapo kuna ubaya gani ati? Nishitakini basi, nasema niko tayari, nishtakini. Nitakuja mahakamani kujitetea, mnamtisha nani! Mnamtisha nani hapa?” alihoji.

Maalim Seif aliwania urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF akiungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), akichuana vikali na mgombea wa CCM, Dk Mohamed Shein.

Hadi sasa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) haijamtangaza mshindi na badala yake imefuta matokeo ya kura za nafasi hiyo pamoja na za uchaguzi wa wawakilishi, ikisema uchaguzi utarudiwa tena ndani ya siku 30.

Hata hivyo, CUF imepinga ikitaka ZEC imtangaze mshindi kwa madai kuwa chama hicho ndicho kilichoibuka na ushindi.

Jana, Maalim Seif, ambaye ameshagombea urais wa Zanzibar mara tano, alirudia wito wake wa kuitaka ZEC imtangaze kuwa mshindi ili aapishwe na kuanza kazi, ikidai anataka kuanza kuijenga upya Zanzibar. Pia alisisitiza msimamo wake wa kushirikiana na CCM katika utawala wake kwa kuwa Katiba ya Zanzibar inaelekeza chama kinachoshinda kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).

Sijui wenzetu wanachohofia ni nini na mara hii sisi (CUF) tumeshinda viti 27 na wao idadi hiyo hiyo ya viti 27 vya Baraza la Wawakilishi, tutakuwa na idadi sawa kwa sawa ya mawaziri tuongoze nchi pamoja,” alisema Maalim Seif.

Kiongozi huyo wa CUF alihoji sababu za Rais Shein kutokubali kushindwa akihoji anaona ubaya gani kuridhia.

Tukae pamoja tuunde Serikali akiwa Makamu wa Kwanza wa Rais au kama hataki CCM wamteue mtu yoyote tuongoze nchi. Mbona mimi niliridhia kuwa Makamu wa Kwanza?” alihoji.

Maalim Seif alisema hakuna namna yoyote ya kupindua uamuzi wa wananchi walioufanya kupitia masanduku ya kura.

Alisema wanachokifanya ZEC ni kuchelewesha kukamilisha uhakiki wa kura kwa majimbo 14 yaliyobakia na kumtangaza mshindi wa urais, na hivyo kuishauri ZEC kukamilisha kazi ili serikali mpya ianze kufanya kazi ya watumikia wananchi.

Alisema tayari dunia nzima wanamfahamu rais aliyechaguliwa na wananchi wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu uliopita, na kuwataka wanachama wa CUF kuacha kusikiliza kile alichokiita proganda za CCM zinazoeleza kurejewa kwa uchaguzi.

Akizungumzia madai ya ongezeko la kura katika kisiwa cha Pemba, Maalim Seif alisema hayo hayana ukweli kwani hakuna hata ‘kituo kimoja kilichozidishwa wapiga kura 350 kama ZEC ilivyopanga, akisema vingine vilikuwa na wapigakura chini ya idadi hiyo.

Mapema akizungumza katika mkutano huo, mkurugenzi wa mipango na uchaguzi wa CUF, Omar Ali Shehe alisema chama hicho kimepata ushindi mkubwa kwa nafasi za uwakilishi na udiwani.

Alisema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 chama hicho kilipata wawakilishi wanne na madiwani saba kisiwani Unguja, lakini katika uchaguzi wa 2015 kimepata wawakilishi tisa na madiwani 15.

Kiongozi huyo alisema CCM imepoteza kata zote tatu za udiwani katika kisiwa cha Pemba na kukifanya chama hicho kushindwa kupata mjumbe katika Baraza la Wawakilishi, ubunge na udiwani.

Kabla ya mkutano huo, alielezea kauli ya kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la CUF kilichokutana chini ya mwenyekiti wake, Twaha Taslima, akisema kiliishauri ZEC kutengua uamuzi wa mwenyekiti wake, Jecha Salim Jecha wa kufuta uchaguzi mkuu wa Zanzibar, kwa vile hana mamlaka ya kikatiba na wala Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar hampi nguvu ya kufuta uchaguzi huo.

Jecha amekuwa akidaiwa kufanya uamuzi huo bila ya kushirikisha viongozi wenzake wa ZEC.

Kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar, matokeo ya uchaguzi wa Rais yanatakiwa kutolewa siku tatu baada ya wananchi kupiga kura na yanaweza kucheleweshwa kwa siku tatu zaidi iwapo kutatokea matatizo katika kuhesabu kura.

Dk Helen Kijo-Bisimba Mkurugenzi wa LHRC Apata Ajali Mbaya..Hizi Hapa Picha za Ajali Hiyo

$
0
0
MKURUGENZI wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Helen Kijo-Bisimba amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akitembelea kuacha njia na kupinduka jijini Dar es Salaam.

Gari hiyo yenye namba za usajili T336 CTT aina ya Toyota LandCruiser GX V8, lilipinduka jana asubuhi, baada ya kuacha njia katika Narabara ya Ali Hassan Mwinyi, jijini Dar es Salaam.

Gari hilo lililokuwa likiendeshwa na dereva wa mkurugenzi huyo, lilipinduka kwenye eneo maarufu la taa za Aga Khan likiwa na abiria watatu, akiwemo Bisimba.

Akizungumza katika mahojiano na Radio One jana, Mkurugenzi Msaidizi wa LHRC, Imelda Urio alisema Bisimba amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan wakati abiria wengine waliruhusiwa baada ya matibabu.

Baada ya Kupata Ubunge Professor J Asema Mipango Kuhusu Music Wake..Kama Ulizani Ataacha Muziki Basi Soma Hii Ushangae

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Mikumi, Joseph Haule aka Professor J, amesema baada ya kushinda kiti cha ubunge atafanya muziki wake kwa ufanisi kushinda kipindi cha nyuma.

Jay amesema umefika wakati wa yeye kufanya collabo na wasanii wakubwa. “Naendelea kufanya sanaa yangu na huenda nikaifanya kwa ufanisi mkubwa zaidi,” Jay aliiambia East Africa Radio wiki iliyopita.

“Unaweza ukasikia watanzania wanafanya kazi na akina Eminem na Jay Z, kwahiyo nategemea kufanya kwa next level kwa sababu naamini exposure nitakayoipata watu wategemee vitu vizuri zaidi. Nitafungua milango, kwenye muziki wa Bongo Flava tunaenda kufungua ukurasa mwingine kwa ajili ya watanzania.”

Ushauri Kwa Rais Dr John Magufuli Kuhusu Kutumia Lugha ya Kiswahili Ndani na Nje ya Nchi Kwenye Mikutano

$
0
0
Ili kuipa hadhi na kuitangaza lugha yetu ya taifa, nashauri rais wetu mpya atumie Kiswahili katika shughuli zote rasmi za kitaifa na kimataifa. Cha msingi ni kuwa na wakalimani mahiri katika shughuli za kimataifa. Hii itainua hadhi na heshima ya nchi yetu badala ya kuendelea kuthamini lugha za kigeni. Tumekuwa watumwa mno wa lugha ya kiingereza mpaka kufikia hatua kudhani kuwa mtu anayeongea kiingereza vizuri ndiye aliye elimika wakati si kweli. Elimu ni uwezo siyo kuongea kiingereza. Hiki kiingereza cha "izi, wozi, wea, kongrugesheni, ameizingi, wati?, yu no, no problemu hakitusaidii kitu. Na kwa ujinga wetu tunafundishana kwa lugha tusiyoijua vizuri matokeo yake watoto wanafeli halafu tunawaona wajinga kumbe sera zetu ndio mbovu. Wachina, wakorea, wajerumani, wareno, wafaransa mbona wanatumia lugha zao na wanapiga hatua kubwa sana katika uchumi na sayansi. Sisi na kiingereza chetu cha kuombea maji tumefika wapi zaidi ya kutudhalilisha?

Maoni yangu haya hayana maana kuwa sitambui uwezo mkubwa wa kiingereza alio nao dr. Nataka aendeleze pale mwenzake alipoachia mwenzake, kwani alianza kwa kuhutubia kwa kiswahili kwenye mkutano wa AU lakini baadaye akaacha. Mimi nashauri Dr. sasa ajikite pamoja na mambo mengi kuitangaza lugha ya kiswahili kimataifa kwa yeye mwenyewe kuitumia badala ya kiingereza. Huwa naona viongozi wa nchi nyingine kama za kiarabu pamoja na kuwa wanajua kiingereza lakini utakuta wanazaunguza kiarabu na kisha wasiojua kutafsiriwa. Wakalimani sasa hivi tunao wengi, ni vizuri wakatumika vizuri kuikuza lugha yetu ya taifa. Ukweli ni kuwa unapotumia lugha mama au lugha ya taifa una kuwa na uhuru na uwezo mkubwa sana wa kujieleza na kuelezea kuliko unapotumia lugha za kigeni. Kwa watanzania wengi lugha yetu ya mama ni kiswahili.
By Tulimumu

Edward Lowassa wa Ukawa Ajitokeza na Kumkosoa Dr John Magufuli, Amuhoji Maswali Matatu

$
0
0
Aliyekuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),
Edward Lowassa, amehoji maswali matatu kwa Rais Dk. John Magufuli.Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana, Lowassa amemtaka Rais Magufuli baada ya kusema hakuna mtoto atakayelipa ada kuanzia Januari, mwakani, atamke mustakabali wa wanafunzi walioko shuleni kama wataguswa na hatua hiyo au la.
Lowassa amesema kwa upande wake ahadi ya elimu bure aliyokuwa akiinadi wakati wa kampeni, ilikuwa ni kuanzia shule ya awali hadi chuo kikuu na kwamba hata wale walioko mashuleni, wangeguswa na hatua hiyo.
“Niliahidi watoto wote walioko na watakaoanza shule kuanzia kindergarten (shule ya awali) hadi chuo kikuu, serikali yetu ingegharimia. Na nilitangaza kufuta michango yote shuleni ili kumpunguzia mzigo mwananchi,” alisisitiza Lowassa ambaye amekataa kuyatambua matokeo ya ushindi wa Dk. Magufuli akidai kuwa yeye ndiye aliyeshinda kwa asilimia 62 ya kura zote zilizopigwa.
Kuhusu suala la mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, Lowassa amesema yeye alishaweka wazi kuwa elimu ingekuwa bure hadi chuo kikuu.
“Vijana hawa wanahangaika na mikopo na nasikia ni asilimia 17 tu kati ya wanafunzi 70,000 ndiyo waliopata mikopo. Sera ya Chadema na Ukawa kwa ujumla, ni kufuta kabisa shida hizi kwa serikali kufadhili elimu yao,” alifafanua Lowassa katika taarifa yake hiyo. Kwa msingi huo, Ukawa kupitia kwa aliyekuwa mgombea wao wa urais, Lowassa, umewataka wananchi kutofautisha ahadi ya elimu bure iliyotolewa na Rais Magufuli na ile iliyotolewa na Ukawa.
Lowassa alisema Magufuli ametoa maelekezo kwa watendaji wa serikali kuweka mikakati ya kutekeleza ahadi yake kuanzia Januari, mwakani kwamba hakuna mtoto atakayelipa ada.
Hata hivyo, amesema hajaeleza waziwazi hatma ya wanafunzi walioko mashuleni kama wataguswa na hatua hiyo au la.

Babu Seya Atua Mahakama ya Afrika......Awasilisha Hoja Tatu, Alia na Serikali Kuvunja Sheria

$
0
0
Hatimaye mwanamuziki, Nguza Viking  maarufu kama Babu Seya na mwanae, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’, wametua katika Mahakama ya Haki za Binadamu Afrika (AFCPHR)  Arusha.

Wanamuziki hao wamekata rufaa dhidi ya adhabu waliyohukumiwa  mwaka 2004 ya kutumikia kifungo cha maisha gerezani.

Kupitia shauri lao lililowasilishwa mahakamani na kupewa namba 006/ 2015, wanaiomba Mahakama ya Afrika kutoa uamuzi kuwa haki zao zilivunjwa.

Kwa sababu hiyo   wanaomba waachiwe huru na kulipwa fidia.

Katika shauri hilo pia wameomba wawezeshwe kupata msaada wa  sheria na.

Pia wanataka Mahakama hiyo  iteue wataalamu watakaotoa ufafanuzi wa hoja za kesi yao na kuisaidia   kufikia   wajibu wake.

Miongoni mwa hoja za walalamikaji hao zilizowasilishwa mahakamani hapo ni pamoja na kwamba mwenendo wa shauri lao haukufanyika kwa kuzingatia haki,.

Vilevile wanadai hati ya mashtaka dhidi yao ilikosewa kuandikwa tarehe ambayo tuhuma za makosa yao zilidaiwa kufanywa hivyo wakashindwa   kutayarisha utetezi wao.

Pia   wanadai  mahakama iliyowatia hatiani ilijielekeza katika  ushahidi wa upande wa mashtaka pekee usioshirikisha ushahidi mwingine.

Wanadai kwamba Serikali ya Tanzania kupitia maofisa wake, ilivunja misingi ya haki za binadamu na sheria za kimataifa.

Wanadai pia kwamba mlalamikiwa alivunja Ibara 1,2, 3, 5, 7(1)b), 13 na 18(1) ya Mkataba wa Afrika kuhusu Ubindamu na Haki za Binadamu.

Malalamiko mingine ni kuwa baada ya kukamatwa hawakuelezwa mapema kuhusu mashtaka waliyokuwa wakituhumiwa nayo.

Wanadai kwa sababu hiyo waliwekwa chini ya ulinzi kwa siku nne bila kuwa na mawasiliano na kupata fursa ya kuonana na mwanasheria au mtu mwingine ye yote.

Wanadai  wakiwa chini ya ulinzi polisi waliwatesa na kuwatukana na  baadaye ofisa mmoja wa polisi aliwaeleza kuwa wanatuhumiwa kwa ubakaji.

Walalamikaji hao   raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), walikuwa wakiishi na kufanya kazi ya muziki  Dar es Salaam.

Wanadai kwamba  mashtaka dhidi yao yalitungwa na hivyo hukumu iliyotolewa haikujikita katika ushahidi wenye nguvu katika sheria.

Nguza na wanawae watatu walikamatwa Oktoba 12, mwaka 2003 na kufikishwa kituo cha Polisi cha Magomeni   Dar es Salaam.

Baadaye walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Oktoba 16 mwaka 2003.

Watuhumiwa hao pamoja na mwingine aliyejulikana kwa jina la Mwalimu walishtakiwa kwa tuhuma  10 za ubakaji.

Pia walikabiliwa  na mashtaka 11 ya kunajisi watoto 10 wenye umri wa miaka sita na nane. Watuhumiwa wote walikana mashitaka yao.

Baada ya kusikilizwa kesi hiyo, Mahakama ya Kisutu  Dar es Salaam ilitoa hukumu Juni 25, mwaka 2004.

Iliwatia hatiani kwa kifungo cha maisha jela huku mtuhumiwa wa tano,   Mwalimu akiachiwa huru.

Walikata rufaa Mahakama ya Rufaa Tanzania Oktoba 30  mwaka juzi ambako wafungwa wawili Francis Nguza na Nguza Mbango walishinda rufaa yao.

Hata hivyo, Babu Seya na Papii Kocha walijigonga mwamba na kurudishwa  jela kwa kuhukumiwa kifungo cha maisha.

Walivyotiwa mbaroni
‘Babu Seya’ na ‘Papii Kocha’ walihukumiwa kifungo cha maisha jela mwaka 2004 baada ya kupatikana na hatia ya ubakaji na kuwanajisi watoto wa Shule ya Msingi Mashujaa,   Sinza   Dar es Salaam.

Babu Seya na wanawe walidaiwa kutenda makosa 10 ya kubaka watoto hao wa shule ya msingi waliokuwa na umri kati ya miaka sita na minane.

Mahakama iliwatia hatiani kwa makosa mengine 11 ya kulawiti watoto wa kike wenye umri huohuo kati ya Aprili na Oktoba 2003.

Juni 25, 2004, Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam aliwatia hatiani Babu Seya na wanae kwa   hatia ya kubaka na kulawiti.

Januari 27 mwaka 2005, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Thomas Mihayo alitupilia mbali rufaa yao iliyokuwa ikipinga hukumu dhidi yao.

Hukumu hiyo ilitolewa na aliyekuwa Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Addy Lyamuya aliyewatia hatiani kwa makosa yote waliyokuwa wameshitakiwa nayo Juni 25, mwaka 2004.

Awali mwaka 2004, baada ya kukutwa na hatia katika kesi hiyo, Babu Seya, Papii Kocha na wakili wao, Mabere Marando walikata rufaa ya pili ambayo ilitupiliwa mbali.

Mwaka 2010 waliomba tena rufaa ambayo marejeo yake yalisikilizwa na kutolewa hukumu Februari 2010.

Mahakama iliridhia hukumu ya kifungo cha maisha kwa Babu Seya na Papii Kocha huku ikiwaachia huru watoto wake wawili, Nguza Mbangu na Francis Nguza.

Credit:Mtanzania

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu Ya Novemba 9, Ikiwemo ya Wema na Idriss Kuonyesha Mahaba Laivu Ikulu

$
0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu Ya Novemba 9, Ikiwemo ya Wema na Idriss Kuonyesha Mahaba Laivu Ikulu





















ANNE KANSIIME Strips Half Nak3d For Men, This Will Drive You Crazy (PHOTOs)

$
0
0

Celebrated Ugandan comedian, Anne Kansiime, has decided to prove that besides her amazing talent on the mic, she has also been blessed with a body to die for.

Below are s3xy photos as she flaunts her goodies in a bikini.


Rais Magufuli Afanya Ziara Ya Kushtukiza Muhimbili..Akuta Hali ya Kusikitisha....Avunja Bodi Ya Uongozi Wa Hospitali, Ateua Uongozi wa Muda

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli , leo mchana amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kukutana na hali ya kumsikitisha.

“ Rais  amesikitishwa na kuhuzunishwa na hali ya huduma kwa wagonjwa hususan wanaolala chini. Pia amekasirishwa na hali ya kutokujali wala kushughulikia vifaa vya kufanyia kazi ambapo amekuta mashine muhimu za uchunguzi wa magonjwa kama vile MRI na CT-SCAN zikiwa hazifanyi kazi kwa muda wa miezi miwili sasa, ilihali mashine kama hizo katika Hospitali za binafsi zinafanya kazi na wagonjwa wanaelekezwa kwenda kutafuta huduma huko”.  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema na kutoa maelekezo yafuatayo :

Rais amevunja Bodi ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambayo ilishamaliza muda wake na amemteua Prof. Lawrence Mseru , kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Muhimbili kuanzia kesho tarehe 10 Novemba, 2015.

Dkt. Hussein L. Kidanto ambaye ndiye anayekaimu hivi sasa, amehamishiwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambako atapangiwa kazi nyingine.

Balozi Sefue pia amesema,   Rais ametoa wiki moja na kwa vyovyote si zaidi ya wiki mbili kwa uongozi mpya wa Muhimbili kuhakikisha kuwa mashine zote za uchunguzi wa magonjwa ambazo hazifanyi kazi zinafanya kazi na kuhudumia wananchi kama ipasavyo.

Tayari Wizara ya Fedha imetoa shilingi bilioni 3 kwa ajili ya kazi hiyo na kulipa madeni ya ukarabati wa mashine za uchunguzi wa magonjwa nchini.

Hata hivyo Katibu Mkuu Kiongozi amesema kuanzia sasa hospitali zote nchini zinatakiwa kutenga fedha kutoka kwenye mapato yao wenyewe na kuhakikisha mashine na vifaa vyote vya kazi vinafanya kazi wakati wote (Regular Maintenance).

Balozi Sefue pia metumia nafasi hii kuwaagiza watendaji na viongozi wote katika sehemu za kazi kuhakikisha wananchi wanahudumiwa ipasavyo na kazi za umma zinatekelezwa ipasavyo.

“Hakutakuwa na huruma kwa watumishi wa Umma wasiojali wananchi na mahitaji yao” Amesisitiza Balozi Sefue.

Imetolewa na;

Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam.
9 Novemba, 2015
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live




Latest Images