Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live

Mashabiki Waguswa na Kukatwa Kwa Jina la IRENE UWOYA Viti Maalumu CCM, Wamtaka Arudi Kwenye Uigizaji

$
0
0
Baada ya Irene Uwoya kushindwa kupata nafasi ya vitu maalumu kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) baadhi ya mashabiki wa ukurasa wa facebook wa EATV wamemshauri msanii huyo kuachana na masuala ya siasa na kurudi katika tasnia ya filamu na kuendelea na kazi yake hiyo ya sanaa ambayo imempa jina kubwa na heshima zaidi.

Mashabiki hao wamepokea tofauti taarifa ya kukatwa kwa jina la Irene Uwoya katika katika vitu maalumu, wapo ambao wameonyesha kuguswa na kuumia Irene Uwoya kushindwa ingawa lipo kundi lingine ambalo linaonyesha kufurahia taarifa ya kushindwa kwa msanii huyo ambaye alikuwa moja ya watu ambao walikuwa wakifanya kampeni za uchaguzi kupitia Kundi la Kibajaji.

Yafuatayo ni maoni mbalimbali ya mashabiki wa ukurasa wa facebook wa EATV kwa Irene Uwoya.
Neema Mgwale: “Hahahaa afadhali kashindwa maana alivyokuwa anashoboka na kuwatukana wasanii wa UKAWA na nilimuona anawaambia wasanii wa UKAWA eti wamemsaliti Jakaya Kikwete kwani alikuwa anawaita Ikulu kila siku yaani hapo ndo nilimwona hafai sababu anathamini kula na rais Ikulu kuliko maisha magumu ya watanzania aendage tuu siasa haimfai”.

Kwa upande wa shabiki mwingine alikuwa na haya ya kusema. “Amshukuru Mungu wake na aamini kuwa kila likuepukalo lina kheri na yeye, kwa sababu CCM inahitaji kubadilisha muelekeo wa bendera yake na kwa sababu hiyo watu wa mzaha mzaha mwaka huu hawana nafasi miaka hii 5 ndio Interview ya CCM kuangalia kama tuwape tena au tusiwape kabisaa na ukumbuke kwenye Interview hatumwi mtoto” ameandika Enock Kayagambe Yahaya.

Zitto Kabwe Yamemfika Hapaa! Ataka Zanzibar Itangaze Matokeo ya Uchaguzi na Mshindi Aapishwe...

$
0
0
Mbunge mteule wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya Chama Cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar yatangazwe na mshindi aapishwe.Zitto Kabwe amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Facebook na kudai kuwa suala la Zanzibar lisidharauliwe kabisa kwani hawawezi kutazama Katiba ikikanyagwa, vinginevyo amesema Maalim Seif apate Jaji amwapishe na aunde Serikali mara moja.

"Suala la Zanzibar lisidharauliwe kabisa. Matokeo yatangazwe na mshindi aapishwe. Hatuwezi kutazama tu Katiba inakanyagwa. Vinginevyo Maalim Seif apate Jaji amwapishe na aunde Serikali mara moja na kuanza kuwatumikia Wazanzibari, Serikali ya Umoja wa kitaifa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar" Amesema Zitto Kabwe

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha. Mnamo tarehe 28 Oktoba alitangaza kufuta matokeo ya Uchaguzi Zanzibar, uliofanyika Oktoba 25, 2015.


Jecha alisema kuwa, ZEC imefuta matokeo ya uchaguzi kutokana na kukiukwa kwa sheria na taratibu mbalimbali za uchaguzi wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo. Na kutangaza Uchaguzi huo kurudiwa.

Masanja Aangukia Pua Kwenye Kura za Maoni ya Ubunge Ludewa

$
0
0
Mchekeshaji, Masanja Mkandanizaji ameangukia pua katika kura za maoni za ubunge katika jimbo la Ludema baada ya kupata kura chache.

Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi, Deo Ngalawa aliwashinda makada wenzake tisa waliokuwa wakiwania nafasi hiyo kwa kupata kura 537 akifuatiwa na mdogo wa marehemu Filikunjombe, Philip aliyepata kura 501.

Makada wengine ni Edgar Lugome, Johnson Mgimba, Emmanuel Mgaya maarufu Masanja Mkandamizaji (19), James Mgaya (72), Jackob Mpangala (3), Evaristo Mtitu (21) na Zephania Chaula (38).

Mwanamuziki Mr Nice Atoa Kali..Aelezea Sababu za yeye Kunywa Pombe Sana Mpaka Kuwa Analala Bar

$
0
0
Msanii ambaye yuko kwenye orodha ya wasanii wakubwa wa Tanzania waliowahi kufanya vizuri sana miaka ya nyuma, Lucas Mkenda maarufu kama Mr Nice amethibitisha kwamba ni kweli huwa anakunywa pombe na kulala bar.

Akiongea na Planet Bongo ya EATV amesema watu wanaosema kuwa amefulia ni waongo tu na kuhusu tetesi kuwa ni mlevi wa kutupwa na analala Bar, Mr Nice ameweka wazi kuwa yeye anakunywa na kulala Bar sababu ana pesa za kuweza kufanya hivyo na anakunywa mpaka pale anapotosheka.

Mkali huyo wa Takeu amewataka wasanii wa kibongo wanaojisifia kwa mali na mbwembwe wawe wakweli na kuonyesha mali zao za ukweli kama ambavyo yeye ameonyesha nyumba ambayo anadai ni yake na kukanusha ile taarifa ya kuwa kwa sasa hana hata sehemu ya kuishi.

Source: Eatv.tv

Ubovu wa Fifaa Hospitali ya Muhimbili..Mtaalamu Aongea Kuhusu Sakata Zima na Nani Anapashwa Kuwajibika

$
0
0
Ukweli usemwe na wakuwajibika na kuwajibishwa na wawajibike kwa haki!

Niseme tu sipingi na kamwe sitapinga kasi ya Magufuli katika kufanya maamuzi...maamuzi yote magumu lazima yawe na setbacks na regrets lakini yanaheshimika kuwa ni maamuzi magumu.

Kiongozi ni yule anayechukua maamuzi hata kama atakosea au kuumiza wengi.

Hii ndio kasi inayohitajika kwenye mfumo mbovu unaoficha maovu yake chini ya mwamvuli wa 'utaratibu'

Ubovu wa CT SCANNER NA MRI Muhimbili ni rflection ya tatizo kubwa na la msingi katika hospitali nyingi au zote nchini.

Kwa uelewa wangu hadi jana ni kwamba wizara ya afya iliingia mkataba na kampuni flani (sitaitaja jina) kufanya matengenezo ya vifaa tiba aina ya CT scan na X rays na Ultra sounds na vinginevyo.

mkataba huu ulifanyikia huko huko wizarani.

Mojawapo ya kipengele cha mkataba ni kwamba vifaa hivi haviruhusiwi kutengenezwa na mwingine yoyote zaidi ya yule aliyepewa tenda huko wizarani.

Yoyote au taasisi yoyote itakayokiuka kipengele hiko kwa kutengeneza vifaa hivyo na kwa bahati mbaya vikafa kabisa basi itakuwa imekula kwake.

Kipengele hiki kinaweza kuwa sababu ya uongozi wa MNH au hospitali nyingi kutozigusa vifaa hivi kwa matengenezo ya kawaida au dharura.

Tetesi zilizopo ni kuwa malipo ya huyu mzabuni hayakwenda sawa kwa muda mrefu kwa hiyo walivisusa au kuvitekekeza vifaa hivi .

Kwa hiyo kwa mkurugenzi anayeamini katika 'taratibu' angeweza kuendelea kusubiri wizara na mzabuni wamalizane ili mashine hizo zije kutengenezwa.

Ni common practise kuwa viongozi wa mahospitali wakijaribu kuwasilisha tatizo hili wizarani au kwa mzabuni kupewa majibu ya tunashughulikia...

KOSA LA DIRECTOR WA MNH!

Kama kiongozi wa 'zahanati' kuu alitakiwa kulichukulia tatizo la CT SCAN NA MRI kutokufanya kazi kuwa ni tatizo kuu na la kutisha na linalohitaji special attention

Alitakiwa kutokulala,kuumizwa na kulihangaikia toka siku ya kwanza.

Alotakiwa kulipresent kwa wadau wote ikibidi hata kulifikisha Ikulu na kulielezea umuhimu wake kama ukosefu wa umeme nchini.sidhani kama alifanya enough katika hili...pia sidhani kama wakuu wengi wa hospitali nyingi za serikali wana hulka hii ya kuyaelezea matatizo ya hospitali zao.
Hilo ndilo kosa pekee kama hukumu yake ilibase katika ukosefu wa huduma za ct scan na MRI!!

WANAOTAKIWA KUWAJIBISHWA KWENYE SAKATA HILI...ukiacha ditector wa MNH!

Kama nilivyoekeza hapo juu...mkataba huu wa maintanance uliingiwa juu kwa juu huko huko wizarani.

Kwa hiyo wapo wengi tu ambao wanaotakiwa kuwajibishwa...

Kuna Director wa Diagnostics yaani anayehusika na mambo ya vipimo hospitalini.

Kuna watu wa procurement aka wazee wa michakato na 10%...

Kuna watu wa hazina waliopeleka B3 jana na sio miezi miwili iliyopita.

Kuna wahasibu wa Muhimbili nikiamini kuwa kuna makusanyo ya fedha za kuweza kutengeneza hiyo mashine.

Kuna maafisa wa procurement hapo muhimbili na wizarani ambao mara nyingi hawajui umuhimu wa vifaa hivi kufanya kazi.

Kuna bodi ya Muhimbili kwa bahati nzuri ilikuwa imemaliza muda wake.

Wako watumishi wengine wadogo wadogo ambao sitawataja.

WAY FOWARD NI NINI?

Bado nakubali hii nginjanginja ya Magufuli ili watumishi wa umma waamke!

Viongozi waliopewa dhamana waelewe kuwa hakuna tatizo dogo au kubwa au la mazoea.

Sheria za manunuzi zilizopo zipitiwe na kuenenda kulingana na sekta mbalimbali...kuna sekta zilizo na uharaka au dharura kwa muda wote.

Rais awawajibishe watendaji wa wizara sio wa taasisi pekee.

Wanasiasa na bodi mbalimbali zifanye kazi kutikana na ushauri wa wataalamu.

Maamuzi mbalimbali yatoke kwa wataalamu walioko 'site' na sio wapigaji wa wizarani.

Wananchi waendelee kupigia kelele huduma mbovu sio tu kwa kuilenga taasisi bali hata executives kwa maana ya wizara.

MWISHO:

Tumekubaliana na Slogan ya #HAPAKAZITU basi tukubaliane kuumizana sana tu mpaka pake tutakapokaa sawa kama taifa.

WASALAAM...HII SIO SIASA NI USHAURI WA #HAPAKAZITU

Breaking News : Hawa Ndio Vigogo Wanne Wanao Wania Nafasi ya Uspika wa Bunge

$
0
0
Mchuano wa kuwania nafasi ya Spika wa Bunge la 11 imebaki kwa vigogo wanne wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), huku vikao vya chama vya kupitisha jina moja vikisubiri Mwenyekiti, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete.
Chanzo cha uhakika ndani ya CCM kimeieleza  kuwa, walioonyesha nia ya kuwania nafasi hiyo ni aliyekuwa Spika wa Bunge la 10 Ni  Anne Makinda, aliyekuwa Naibu Spika wa Bunge hilo, Job Ndugai, aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa, Samuel Sitta, aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge la 10, Mussa Azzan Zungu na Mjumbe wa Kamati kuu Dk. Emmanuel Nchimbi.

Mmoja wa wanaotajwa kugombea nafasi hiyo, Job Ndugai ameithibitishia Nipashe kuwa atawania nafasi hiyo na anaomba wabunge wote kumuunga mkono kwa kuwa uzoefu, uwezo na elimu yake vinamuwezesha kushika nafasi hiyo nyeti.

Alisema anasubiri chama chake (CCM) kikamilishe taratibu zake na kuruhusu wagombea wa nafasi hiyo kuchukua fomu ndipo atafanya hivyo kwa kuwa ana sifa zote za kuwania nafasi hiyo.
Ndugai ambaye ni Mbunge Mteule wa Jimbo la Kongwe, alisema wabunge wa Bunge la 11 wana uwezo, hivyo ni wazi hawatahitaji Spika kutoka nje yao na mwenye uwezo wa kuongoza Bunge hilo ni yeye.

Alisema iwapo Spika wa Bunge la 10, Makinda atasimama kuwania tena nafasi hiyo hana tatizo naye na kumuomba kumuunga mkono iwapo jina lake (Ndugai) litapenya ndani ya chama na kufika bungeni.

“Naamini kuanzia kesho (leo) chama changu kitatoa utaratibu wa uchunguaji fomu, ni kweli nina nia ya dhati kabisa ya kugombea nafasi hiyo ya juu katika muhimili wa Bunge na ninaomba niungwe mkono,” alisema.

Naye, Dk. Nchimbi, alipopigiwa simu na Nipashe, alimweleza mwandishi kuwa CCM bado haijatangaza nafasi zilizo wazi zinazostahili kugombewa.
Hata hivyo, alipoulizwa kama atagombea nafasi hiyo hakukubali wala kukataa na kumtaka mwandishi kusubiri utaratibu utakaowekwa na chama.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajabu Luhwavi, alipoulizwa kuhusiana na mchakato wa kumtafuta mgombea wa uspika, alimtaka mwandishi kuzungumza na Katibu wa Sekretarieti ya CCM, Anamringi Macha, ambaye alisema vikao vya CCM kujadili na kumpanga suala hilo bado havijafanyika.
“Vikao vinamsubiri mwenyekiti ndiyo wataamua fomu zianze kutoka lini na mchakato mzima kwa ujumla,” alisema Macha.
Ndani ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) unaoundwa na Chadema, NLD, NCCR Mageuzi na Cuf, bado haijajulikana vikao vya kujadili suala hilo vitafanyika lini.
Wenyeviti wenza wa umoja huo, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema wala James Mbatia, Mwenyekiti NCCR-Mageuzi hawakupatikana kuzungumzia suala hilo.

Hata hivyo, aliyekuwa Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzania Bunge la 10, Tundu Lissu, aliieleza Nipashe kuwa hakuna kikao chochote cha Ukawa kilichokaa kujadili suala hilo hivyo ni vigumu kuzungumzia.
CHANZO: NIPASHE

Membe: Tulikuwa Tunagongana Angani Utadhani Nyumbani Kuna Moto

$
0
0
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amempongeza Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kwa kupiga marufuku safari za nje ya nchi, akisema mawaziri na watendaji wa Serikali walikuwa wakigongana angani na ndege utadhani Tanzania ilikuwa ikiwaka moto.

Mbunge huyo wa zamani wa Mtama alisema uamuzi huo utaokoa fedha nyingi za Serikali na kumtaka Rais kushusha rungu hilo hadi kwenye mashirika.

Wakati Membe akieleza hayo, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue alisema kila safari ya nje ina gharama yake na kila safari itakayofutwa zitapatikana fedha kusaidia masuala mengine ya maendeleo katika jamii.

Juzi, Dk Magufuli alipiga marufuku safari za nje ya nchi kwa watendaji na kwamba shughuli ambazo wangekwenda kuzifanya, kuanzia sasa zitahitaji kibali kutoka kwake au zitafanywa na mabalozi wa Tanzania walioko katika nchi husika.

Jana Membe alisema: ?...Tulikuwa tunagongana huko hewani utadhani huku nyumbani kunaungua moto. Tunapobaki huku ndani tunaokoa hela nyingi na nina hakika (Dk Magufuli) ataingilia hata kwenye mashirika. Kuna wakuu wao wanasafiri kila siku, nina hakika wataguswa katika hili. Lazima kuziokoa pesa za kufanyia shughuli nyingine mimi naunga mkono mia moja kwa mia hili.?

Alisema kitendo cha Rais Magufuli kufuta safari za nje hakina maana kwamba uhusiano wa Tanzania na nchi hizo unakufa. ?Hajakataza wageni, wafanyabiashara wa dunia wala wawekezaji kuja Tanzania, hata wawekezaji hawawezi kukataa kuja Tanzania waache gesi, dhahabu, almasi au tanzanite.?

Alisema wapo watu wanaodhani kuwa kauli ya Rais Magufuli itamhusu hadi Waziri wa Mambo ya Nje ?... atakwenda nje maana ukishamuita waziri wa mambo ya nje lazima aende nje. Dk Magufuli hawezi kusema hivyo. Hutasikia amekatazwa maana ndiyo wizara yenyewe na inashughulika na dunia.?

Alisema kauli hiyo pia haina maana kwamba Wizara ya Mambo ya Nje imefutwa kwa kuwa balozi za Tanzania zilizopo nje zipo chini ya wizara hiyo.

CHANZO: Mwananchi

Kama Umeona Picha Mbaya Kwenye Account ya Ray C Instagram, Kilichomkuta ni hiki..

$
0
0
Kumeenea picha mbaya na stori kuhusu Ray C na kilichotokea jana kwenye account yake ya Instagram, leo Soudy Brown kampata na kajibu yote ilivyokuwa.

Ray C amesema zile picha ni zake private ambazo alizihifadhi kwenye simu yake, lakini kwa bahati mbaya simu yake imepotea na aliyeiba simu ndio aliamua kuanza kupost picha alizokuta kwenye simu ya Ray C.

Ray C amesema alituma email kwa wamiliki wa Instagram ili waifungie account hiyo, lakini anaomba radhi kwa kilichotokea kwa sababu sio yeye aliyepost picha hizo.

Niombe tu msamaha maana sijui hata naanzaje kuelezea… naomba tu waelewe kwamba simu nimeibiwa na mtu ambaye amefanya hivyo namjua na nimeripoti Polisi.. naomba tu msamaha“- hii ni sehemu ya maneno ya Ray C alipokuwa kwenye U Heard na Soudy Brown leo.

Baada ya Magufuli Kutembelea Muhimbili Kwa Kushtukiza..Hii ni Habari Mpya ya Kufurahisha Kuhusu Mashine ya MRI

$
0
0
Siku ya tatu baada ya Rais Dk Magufuli kuingia Ikulu na kuanza kazi alifanya ziara za kushtukiza katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ikiwa ni baada ya kumaliza ziara katika Wizara ya Fedha siku moja baada ya kuapishwa.

Baada ya kutembelea hospitali ya Muhimbili alifanya mabadiliko ikiwa kumsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo Hussein Kidantu sambamba na kutaka mashine za CT Scan na MRI zifanyiwe ukarabati baada ya kukaa miezi miwili bila kuhudumia wagonjwa kutokana na ubovu wake.

Kamati mpya tendaji ya hospitali hiyo ilikutana jana na mara moja kuitisha wataalam ambao leo walianza kazi ya utengenezaji wa mashine hizo.

Taarifa mpya kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya umma Aminiel Eligaisha amesema ni kweli mashine za MRI tayari zimeanza kufanya kazi na mashine za CT Scan bado zipo katika matengenezo na zitaanza kufanya kazi wakati wowote kuanzia sasa.

Barua ilisomeka hivi…

Dkt. Slaa Aibuka na Kutoa Tathmini ya Maamuzi Ya Rais Magufuli

$
0
0
Aliyekuwa katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Wilbroad Slaa ametoa tathmini yake kwa siku chache za Rais John Magufuli alizoanza kazi katika Serikali ya Awamu ya Tano na maamuzi aliyoyafanya.

Dkt. Slaa ambaye alikuwa mgombea urais kupitia Chadema mwaka 2010, ameeleza kuwa maamuzi ya kufuta safari za nje kwa watendaji wa serikali yaliwahi kuchukuliwa na Rais wa Serikali ya Awamu ya kwanza, Mwalimu Julius Nyerere.

Alisema kuwa hata wapinzani walikuwa wakilalamikia gharama zinazotumika kwenye safari za nje na kwamba yeye pia aliwahi kupendekeza safari hizo kufutwa na badala yake watendaji waende vijijini kuchagiza maendeleo.

Tulilamikia safari za JK nje ya nchi. Na mimi niliwahi kusema kuwa tufute safari za njena kuanza kwenda zaidi vijijini.  Tuone naye kama katufa tu… na badala yake tufanye nini. Ni siku mbili (Jumamosi) ofisini huwezi kufanya tathmini ya maana,” alisema.

Tathmini hii kwa kawaida hufanywa baada ya siku 100. Mwalimu alifanya hivyo. Rais wa watu ni vyema akifanya hivyo. Ndiyo namna pekee ya kujua hali halisi. Kwa Magufuli si ya kwanza, amefanya sana akiwa Waziri.”

Imebainika Sababu za Mshirika wa Lowassa, Bashir Awale Kukamatwa na Polisi..Kumbe si Mtanzania

$
0
0
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji nchini, wanafanya uchunguzi kuhusu tuhuma zinazomkabili mwanaharakati na mshirika wa aliyekuwa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa, Bashir Awale anayetuhumiwa kuwa Mkenya.

Awale aliyekuwa mwanaharakati wa Lowassa katika mchakato wa kuelekea Ikulu, alikamatwa Novemba 9, mwaka huu, akituhumiwa kwa utata wa uraia wake na jinsi alivyokuwa akijihusisha na siasa nchini. Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Kova alisema baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo, alipekuliwa nyumbani kwake maeneo ya Mikocheni, na alikutwa na cheti cha kuzaliwa chenye namba D 063711 kwa jina la Bashir Ally.

Alisema cheti hicho kinaonesha kuwa alizaliwa Julai 11, 1969 katika Hospitali ya Serikali mkoani Dodoma. Aidha, alisema pia mtuhumiwa alikutwa na hati ya kusafiria ya Kenya yenye namba C 000529 ambayo ilionesha kuwa alizaliwa Nairobi tarehe hiyo hiyo kwa jina la Bashir Awale.

“Kumbukumbu hizo zinakinzana na zinaleta utata, hivyo tunashirikiana na Idara ya Uhamiaji kumhoji mtuhumiwa kwani hilo ni kosa chini ya sheria za uhamiaji,’’ alisema Kova. Alifafanua kuwa zipo tuhuma zinazoonesha mtuhumiwa huyo akiwa raia wa Kenya, amekuwa akijihusisha na siasa za Tanzania hususan wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka huu.

“Kitendo hicho ni kinyume cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambayo haimpi nafasi raia wa kigeni haki ya kuchagua, kuchaguliwa na kushiriki katika kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani,” alifafanua Kova.

Kova alisema kuwa mtuhumiwa huyo anachunguzwa na kwamba akibainika kuwa alijihusisha na siasa wakati sio raia, itakuwa ni kinyume cha Katiba, hivyo atachukuliwa hatua za kisheria. Alisema mtuhumiwa huyo hivi karibuni alipeleka maombi ya uraia katika Idara ya Uhamiaji, na hajakubaliwa.

Alisisitiza kuwa Watanzania wasiwe warahisi kukaribisha wageni kwani ni lazima kuwa na viwango kwa sababu ni hatari kwa usalama wa nchi. “Tuwe na kiasi kwani nchi za wenzetu hawana utaratibu wa kuruhusu wageni kuingia pasipo kuwa na kibali.

Tuige mfano huo ili tuendelee kuwa salama,’’ alisema Kova. Alisema hawamuonei mtuhumiwa huyo, bali sheria inawataka kufanya uchunguzi wa kina kuhusu tuhuma mbalimbali zilizoelekezwa kwake.

Wizara Ya Mambo ya Nje Kutekeleza Agizo la Rais Magufuli ‘kijeshi’

$
0
0
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imesema imeanza kutekeleza agizo la Rais John Magufuli kwa haraka kama jeshi juu ya kuiwakilisha Serikali katika masuala mbalimbali nje ya nchi baada ya kusitishwa safari za nje kwa maofisa wote wa ndani.
 
Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Balozi Liberata Mulamula alisema jana kuwa atawapelekea mwongozo mabalozi wote kutekeleza majukumu hayo kwa kasi inayoendana na Serikali ya Awamu ya Tano.
 
Wiki iliyopita, Rais Magufuli alitangaza kufutwa kwa safari za nje kwa maofisa wake na kusema kuwa safari nyingi zielekezwe vijijini kuwahudumia wananchi na kwamba kazi za nje zifanywe na mabalozi ili kupunguza matumizi ya Serikali.
 
Hata hivyo, Balozi Mulamula alisema utekelezaji wa agizo hilo la Rais utachukua muda kidogo kutokana na balozi nyingi kukosa rasilimali fedha na wataalamu wa kutosha kufanikisha malengo hayo kwa ufanisi na tayari wameshamweleza tatizo hilo.

“Kwa sasa ikitokea unawaagiza mabalozi wakawakilishe kwenye kongamano la biashara, hatuna maofisa wa biashara wa kutosha au ikitokea kuna kongamano la nishati sisi hatuna wataalamu hao.

“Pia, uteuzi wa mabalozi nao itabidi uwe makini kuhakikisha balozi anayeteuliwa eneo husika ana uwezo wa kutosha kufanya kazi,” alisema.
 
Akizungumza katika hafla ya miaka 40 ya ushirikiano wa Tanzania na EU, Balozi wa umoja huo, Filiberto Sebregondi alisema wametumia Euro 3 bilioni sawa na Sh6.93 trilioni katika miradi mbalimbali ya maendeleo nchini ambazo zilielekezwa zaidi katika sekta za miundombinu, elimu, usambazaji umeme vijijini, maji, utawala bora na utetezi wa haki za binadamu.

Balozi huyo ambaye pia aliaga jana baada ya kumaliza muda wake, alisema EU itaendelea kusaidia Tanzania miradi ya maendeleo katika nchi ambayo ni mfano wa kuigwa Afrika katika kulinda amani, utulivu na demokrasia.

“Uchaguzi uliopita pamoja na kuonyesha ushindani mkubwa, umeonyesha utulivu wa hali ya juu kwa Watanzania. Hivyo, tunasubiri kuona hali inayoendelea Zanzibar inatatuliwa kwa mazungumzo na kwa kuheshimu matakwa ya Wazanzibari,” alisema Sebregondi.

Udaku Specially

Katibu UVCCM Wilaya Ateuliwa Kuwa Mbunge Viti Maalum Chadema

$
0
0
Katika hali isiyotarajiwa na wengi, Katibu wa UVCCM wilaya ya Mbulu mkoani Manyara, Bi. Anna Gideria ameteuliwa na Chadema kuwa mbunge wa viti maalum.

Bi. Gideria amejiuzulu nafasi ya ukatibu na kukabidhi barua yake kwa mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Manyara, Bi. Regina Ndege baada ya kutangazwa majina ya viti maalum na jina lake kuwa katika orodha ya wabunge wa Chadema.

Akizungumzia hatua hiyo, Bi. Ndege alieleza kuwa Bi. Gideria alipoteza imani na CCM muda mfupi baada ya jina la waziri mkuu wa zamani, Frederick Sumaye kukatwa katika kinyang’anyiro cha kumtafuta mgombea urais kwa tiketi ya CCM.

Mwenyekiti huyo alieleza kuwa Bi. Gideria alikuwa ‘Team Sumaye’ na aliomba likizo ya mwezi mmoja baada ya jina la waziri mkuu huyo wa zamani kukatwa.

“Baada ya Sumaye kutoswa, alipoteza imani na CCM na ilipofika wakati wa kampeni mwezi Agosti aliandika barua ya kuomba likizo na kukabidhi ofisini kwa mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya UVCCM wilaya ya Mbulu,” alisema Bi. Ndege.

Tukio hilo limewashtua wananchi wengi wa Wilaya ya Mbulu ambao walikuwa wanamuona Bi. Gideria kama kiongozi na mpambanaji wa CCM kuteuliwa kuwa mbunge wa Chadema.
 
 Zipo hisia za wananchi wengi kuwa huenda alikuwa anatumiwa kuihujumu CCM wakati wa kampeni.

Manyika Jr na Naima wapanga Kufunga ndoa, Aeleza Misukosuko Waliyopitia

$
0
0
Mlinda mlango wa Simba, Peter Manyika Jr na mchumba wake Naima wanatarajia kufunga ndoa hivi karibuni.
12081027_1651638835115791_2014890630_n
Wawili hao wamepitia misukosuko mingi kwenye uhusiano wao ikiwa ni pamoja na kuwa kwenye hatari kuvunjika kwa uhusiano wao kutokana na shinikizo la wazazi na uongozi wa Simba.
Klabu ya Simba iliwahi kumuonya mchezaji huyo baada ya kuwashambulia mashabiki wa soka kwenye mtandao waliodai kuwa Naima ni chanzo cha kushuka kwa kiwango chake uwanjani.
12093349_1679673918915048_223428952_n
Akiongea kwenye kipindi cha Uhondo cha EFM kinachoendeshwa na Dina Marious na Swebe, Jumatano hii, Manyika alisema ni mama yake ndiye aliyemvusha kwenye mapito hayo na anamchukulia kama shujaa wake.
Alisema maneno hayo yalimsumbua kisaikolojia na kuathiri mchezo wake uwanjani lakini mama yake alimsaidia na kumpa moyo.
Aliongeza kuwa baba yake, Peter Manyika pia alikuwa hajaupa baraka uhusiano wao lakini mama yake alimshawishi mume wake ampe support mwanae na kumwacha achague maisha yake mwenyewe hasa mwanamke wa kuwa naye.
10946694_1513089505650753_818605591_n
Kuhusu tetesi kuwa alimpokonya Naima kwa Aslay wa Yamoto Band, Manyika alisema alimkuta msichana huyo akiwa single.
Bongo5

Maneno ya Masanja Baada ya Kushindwa Kura za Maoni Ludewa..

$
0
0
List ya mastaa wa Bongo Tanzania ambao walijitosa na kujipanga kwenye foleni ya kuusaka Ubunge iliongezeka baada ya mchekeshaji kutoka Kundi la Orijino Komedi, Masanja Mkandamizaji nae kujitosa kwenye foleni hiyo.

Masanja alithibitisha kwamba kazi ya Ubunge anaiweza   “Orijino Komedi ipo, mimi sio member wa kundi, mimi ni mwanzilishi.. siwezi kuacha Komedi, mbona nilikuwa Mchungaji na sikuacha Komedi.. nitakuwa Mbunge, Komedi na Church…” Hii ni siku chache zilizopita kwenye exclusive interview na millardayo.com pamoja na  Amplifaya.

Kura hazikutosha kwake, maana yake ni kwamba kwenye Kura za maoni upande wa makada wa CCM Ludewa, Masanja hajafanikiwa kupita… lakini aliahidi pia hata kama akishindwa bado ataendela kumpa support yule atakaepita.
Kwenye ukurasa wake wa Twitter, Masanja ameandika haya kukubali matokeo  “Ludewa ….. Dah! Najipanga nitarudi tena. Sasa ni muda wa kumpigia kampeni aliyepita ili akatuwakilishe Bungeni. HapaKaziTu”  @mkandamizaji

Kwenye ukurasa wake instagram ameandika
Jamani uchaguzi wa kura za maoni umeisha.
nimepata kura jumla kwa zoooote ukihesabu nimebeba jumla kabisa kabisa kura ukijulisha vizuri kabisaaa utulie nimepata kura hiziiiiì 19

Udaku Specially

Wanawake wa CHADEMA Arusha, Kufanya Maandamano Wakiwa Uchi

$
0
0
Mfano wa Wanawake Hawa wa South Africa Walipo Andamana Kuishinikiza Serekali kukubali Mapenzi ya Jinsia Moja
Mwenyekiti wa Baraza la wanawake CHADEMA Mkoani Arusha, amesema watafanya maandamao wakiwa uchi iwapo watahujumiwa au kama NEC wataleta mambo ya Goli la Mkono katika Uchaguzi mdogo wa Ubunge unategemewa kifanyika.

Hatua hiyo imekuja baada ya kusikia CCM wakisema lazima washinde Jimbo la Arusha Mjini kwa sababu ni jimbo muhimu sana.

Hivi Kweli Watanzania Tunamsifia Magufuli Kwa Kuvamia Maofisini? Naomba Soma Hii Alafu Jiulize Maswali Haya

$
0
0
Kwanza tujiulize saivi kilo ya nyama ni bei gani na mkakati gani madhubuti wakuliokoa taifa.

Pili kabla ya kushabikia tujiulize JK alianzaje? Alimsimamisha mkurugenzi Muhimbili akamteua Mwanamama! Huyu naye kafanya vilevile au tumesahau?

Yaani kwa kweli mi ninapoangalia hali ya uchumi wa Tanzania, maisha duni ya wafanyakazi, ukisefu wa ajira ukosefu, wa maji safi ni salama karibia nchi nzima!

Namshangaa sana mtu anayemshabikia Mh Pombe kutembea na vyombo vya habari kwenye maofisi!

Kwanza jiulize huko kote alikovamia amehoreshaje mazingira ya utendaji wa wafanyakazi ili kuwapa morally ya kufanya kazi?

Hizi sio zama za dictatorship style ni zama za democratic leadership ambapo ku win minds za wafanyakazi ni kuwatendea vile inavyopasa na sio kuwakimbiza na viboko.

Tanzania tunahitaji kuona wanafunzi wa vyuo vikuu wanapata mikopo yao kwa ufasaha na kwa utoshelevu.

Tunahitaji kuona wafanya biashara wadogowadogo wakiboreshewa mazingira ya kazi..mfano mama ntilie na bodaboda na machinga,

Tunahitaji kuona wakulima ambao ndo uhai wa Taifa wakiboreshewa zana za kilimo na mbolea.

Tunahitaji kuona michakato ya viwanda ikianza.

Tunahitaji kuona waalimu wakiimarishiwa mishahara yao pamoja na kulipwa malimbikizi yao.

Tunahitaji kuona jiji la Dar likiokolewa kuondoka na uchafu unaosababisha vifo vya watanzania kila kukicha.

Nina mengi sana lakini ngoja nitulie kwanza, hebu jiulize vijana hawana ajira iko wapi mikakati ya viwanda?

Huko Muhimbili mkurugenzi anasimamishwa kazi wakati tunaona madactari wanagoma kwa mishahara duni iko wapi mikakati ya kuwaboreshea mishahara yao ili kuwapa ari ya kufanya kazi?

Mi nadhani cha kufanya kwa sasa kuboresha kwanza mazingira ya kazi alafu kazi ya usimamizi itakua nyepesi.

" Ukitaka Punda akubebee mzigo vizuri bila kipigo mpe majani na maji ashibe"

VIDEO:Wafanyakazi Kiwanda cha Urafiki Wagoma Wakidai Nyongeza ya Mshahara

$
0
0
Wafanyakazi wa kiwanda cha urafiki ubungo jijini Dar es Salaam wamegoma kufanya kazi wakidai nyongeza ya mshahara.

Wafanyakazi wa kiwanda cha urafiki ubungo jijini Dar es Salaam wamegoma kufanya kazi wakidai nyongeza ya mshahara.

Hali ya utulivu ni nzuri, hamna fujo, polisi wa kituo cha Urafiki wamefika eneo la tukio, wafanyakazi bado wanashikiza madai yao yasikilizwe

Wastara Afungu 'Jamani Penzi lililowahi Kunipa Raha na Kunifanya Nifurahie Maisha ni la Sajuki tu na si Mwanaume Mwingine yeyote

$
0
0
NASEMA ukweli kabisa! Staa wa ‘grade one’ kunako filamu za Bongo, Wastara Juma ameweka wazi kuwa, tangu azaliwe, penzi pekee alilowahi kulifurahia ni la aliyekuwa mumewe na msanii mwenzake, marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’.

Staa wa ‘grade one’ kunako filamu za Bongo, Wastara Juma.
Akichonga na Amani juzi, Wastara alifunguka kuwa, Sajuki ndiye mtu pekee aliyekuwa akimwelewa na kumpa mapenzi ya dhati.Aliongeza kuwa, Sajuki ndiye mwanaume aliyekuwa akimlinda siku zote na kumtetea katika jambo ambalo alikuwa akionewa

Jamani penzi lililowahi kunipa raha na kunifanya nifurahie maisha ni la Sajuki tu na si mwanaume mwingine yeyote. Hicho ndicho kitu kinachonifanya nimkumbuke sana kila wakati,” alisema Wastara.
Source:Globalpublishers

Sihitaji Pedeshee, Dansa Wangu Moses Iyobo Ananitosha Sana...Aunty Ezekiel

$
0
0
MAKUBWA! Staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel amefunguka kuwa wapo watu wanamcheka kuwa na uhusiano wa kimapenzi na dansa (Moze Iyobo) lakini ni bora aendelee kuwa naye kuliko kuwa na uhusiano na mtu mwenye pesa za kugawa hovyo (pedeshee) asiyekuwa na mapenzi ya dhati.

Staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel akiwa na mpenzi wake Moze Iyobo.
Akizungumza na Amani, Aunt alisema kuwa aangalii hela hata kama wakilala njaa lakini kama kuna mapenzi ya kweli inatosha kabisa kuliko kuwa kwenye hela akaumizwa na kunyanyaswa.
Acha niendelee kuwa na dansa wangu kuliko kuwa na pedeshee ambaye hana mapenzi ya dhati kwangu akaenda kuniumiza na nisione raha ya penzi, kwa Moo (Iyobo) nafurahia mapenzi na wala siyo pesa kwani hata njaa tunaweza kulala,” alisema Aunt.


Akizungumza na Amani, Aunt alisema kuwa aangalii hela hata kama wakilala njaa lakini kama kuna mapenzi ya kweli inatosha kabisa kuliko kuwa kwenye hela akaumizwa na kunyanyaswa.

Acha niendelee kuwa na dansa wangu kuliko kuwa na pedeshee ambaye hana mapenzi ya dhati kwangu akaenda kuniumiza na nisione raha ya penzi, kwa Moo (Iyobo) nafurahia mapenzi na wala siyo pesa kwani hata njaa tunaweza kulala,” alisema Aunt.
chanzo;globalpublishers
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live




Latest Images