Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Anne Makinda Aukimbia Uspika.....Aingia Mitini Dakika za Mwisho Licha ya Kufanya Kampenj

$
0
0
Anna Makinda
Aliyekuwa Spika wa Bunge la Kumi, Anne Makinda ameamua kukaa kando ya mbio za Uspika wa Bunge la 11, siku chache baada ya kufanya kampeni kuwania nafasi hiyo kwa mara nyingine.

Taarifa za kuaminika zimeeleza kuwa Mama Makinda aliamua kuchukua uamuzi huo wa kujiweka kando ya mchuano huo baada ya kushauriwa na watu wake wa karibu kufuatia dalili walizoziona kwenye mchakato huo pamoja na mambo mengine.

Awali mama Makinda alidaiwa kuanza kampeni kupitia ujumbe mfupi alioutuma kwa wabunge wateule kupitia simu za mkononi akiwapongea na kuwaomba kumuunga mkono kuwa Spika wa Bunge la 11.

“Mimi ndugu yako kwa unyenyekevu na heshima kubwa kwa ko kama mbunge wangu, naomba kugombea uspika kwa mara nyingine, kwa msaada w Mwenyezi Mungu nakutegemea sana naomba uniunge mkono. Asante kwa ukarimu wako,” ilisomeka sehemu ya ujumbe unaoaminika kuwa ulitumwa na Anna Makinda kwa wabunge wateule.

Hata hivyo, hadi pazia la kuchukua na kurudisha fomu za kuwania Uspika wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linafungwa, Mama Anna Makinda alikuwa hajarudisha fomu yake hivyo kuonesha dhahiri kuwa ameachana na mpango huo.

Makada 21 wa CCM wamejitokeza kuwania nafasi ya Uspika wa Bunge.Dkt. Emmanuel Nchimbi, Samwel Sitta, Dkt Didas Masaburi, Balozi Philip Marmo, Mussa Hassan ‘Zungu’, Job Ndugai, Abdallah Mwinyi ni miongoni mwa majina ya makada wa CCM waliojitokeza kuwania nafasi hiyo.

Naipongeza Rasmi UKAWA Mpaka Hapa ilipofikia...Naiona CCM Kama Chama cha Upinzani Miaka Ijayo

$
0
0
Kwakweli kwa mtanzania anayefikiri kwa kina ataungana na mimi kwamba, pamoja na hujuma na figisufigisu nyingi zilizofanyika ambazo ziko wazi japo ukweli hausemwagi Tanzania, UKAWA kwakweli wameimarisha upinzani.

Ninachokiona mimi ni CCM kuwa chama cha kawaida cha upinzani siku za usoni.. Sasa hii itawezekanaje? Twende pamoja nitoe yangu ya moyoni

1. Niwakati sasa wakutambua kwamba kwakuunganisha nguvu ndo dawa pekee itakayosaidia kummaliza mtawala CCM. Kwa hili naomba niseme viongozi wa UKAWA zitambueni fitna zinazotimiwa na CCM kuwachonganisha na kuwagawa, naomba muwe werevu muwazidi akili zaidi shikamaneni.

2. Hakikisheni mnapigania kwa udi na uvumba kupatikana kwa katiba mpya yenye dira na muelekeo sahihi, itakayoweza kusema fulani kashinda mpeni haki yake,

3. Jikiteni Sasa kutoa elimu vijijini ambao wengin kwasababu hawazijui changamoto kali za maisha na wengine wakiamini kuwa CCM ni ile ile ya nyerere y ujamaa basi wa
naipa kura tu,

4. Dumisheni Democrasia kwa vyama vyote vya "UKAWA" viwe na haki sawa ya kutangazwa na kuimarishwa,

5. Tofauti na chama tawala nyie wekeni uwazi wa kila kitu kinachofanyika ili kuongeza imani za wafuasi

6. La mwisho kwa sasa, dumisheni kwa pamoja na kwa uhalisia kumtegemea Mungu aliyeumba majira na nyakati.

By H.T.

Kila Wikiendi Anataka Nimgegede Bure...Ataki Kitu Chochote Kutoka Kwangu zaidi ya Dushelele...Ushauri Tafadhali

$
0
0
Binti mmoja (jina kapuni) mzuri wa viwango, nilimtongoza kanizungusha balaa. Kidume nikapotezea nikajua nimechezea za Uso. Baada ya wiki kupita, kanitafuta kwa Simu, akaomba tuonane ana kwa ana kuwa analo jambo la muhimu.
Nikaitikia wito. Stori aliyonipa ni kwamba yeye, hakuwahi kumpenda mtu, zaidi ya kutolewa bikra kwa nguvu (forced sex) na kijana mmoja waliyeishi nae jirani zamani hizo.
Hivyo akaomba mahusiano yangu na yeye yawe ya pole pole na si haraka kwani bado ana chuki na wanaume. Aliongea kwa uchungu, huku machozi yakimtoka. Baada ya kumbembeleza tulijikuta tukifanya mapenzi mimi na yeye bila kupanga tena kavu kavu. Baada ya tendo hilo hakuamini kilichotokea na aliondoka kwa uchungu mkubwa akidai na Mimi ni wale wale. Kiufupi sikumsoma. Iweje aingie King halafu ananilaumu.

Anyway nikapotezea, coz hata Simu zangu akawa hapokei, waka text hajibu. Nikatulia zangu. Baada ya wiki mbili akanipigia Simu, akiomba msamaha eti hakujielewa. Nikaona haina haja kuweka bifu na binti, nikapotezea. Maisha yakaendelea.

Sasa kila wikiendi akawa anakuja kwangu, tunagegedana, nikimpa mshiko anaukataa, hata nikimtumia vocha hazitaki wala Zawadi yoyote hataki zaidi ya mgegedo. Basi tumekuwa tukifanya hivyo kwa muda mrefu sana. Kitu kinachonishangaza hapa ni huo ujasiri wa binti kukataa tip kutoka kwa dume unatoka wapi?

Je, kazi yangu ni kugegeda tu na matumizi anatoa mwingine?
Au, nini kipo nyuma ya pazia

Nawasilisha, nisaidiwe kujua tabia hii maana yake nn?

Ombi Kwa Rais Mstaafu Dr. Kikwete MPE Nafasi Rais Magufuli Ajitangaze..

$
0
0
Nakumbuka Mkapa baada ya kumaliza muda wake alipotea kabisa kwenye media kwa takriban mwezi nzima hadi tukawa na hamu naye, hii inatoa nafasi kwa rais aliye madarakani kujiamini kujenga confidence, na kutoa nafasi kwa wananchi kumjua vizuri rais wao mpya.

Majuzi uliita waandishi wa habari nyumbani kwako Msoga ukaongea juu ya Taifa stars, TV zinakuonyesha mara nyingi kuliko hata rais.

Juzi ulisahau kumkabidhi JPM kitabu tukakuona sambamba na rais, jana tena umeonekana ukiwa na rais mkihani msiba.

Leo utakuwa uwanja wa taifa sambamba na rais Magufuli tutawaona kwenye TV, dah!

Ombi langu kwa rais wetu mstaafu najua bado una hamu ya kuendelea kuonekana maarufu sawa, lakini muda wako umekwisha mpe nafasi successor wako naye ajulikane.

Kulikuwa hakuna sababu yeyote leo wewe na rais kubanana uwanjani.

Nawasilisha.

Maalim Seif azugumza na Balozi wa EU na viongozi wa UKAWA....Atoa Msimamo Mzito

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amerejea kauli yake ya kutotambua kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika tarehe 25 mwezi uliopita.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya kikao cha mashauriano na viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA, Maalim Seif amesema Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Bw Jecha Salim Jecha hana mamlaka ya kufuta uchaguzi huo, na kinachohitajika na kuendelea na mchakato wa kuhakiki kura zilizobakia na mshindi kutangazwa.

Kuhusu tamko lililotolewa na serikali juu ya kufutwa rasmi kwa uchaguzi huo kupitia tangazo lililochapishwa kwenye gazeti rasmi la serikali tarehe sita mwezi huu, Maalim Seif amesema tamko hilo limekosa uhalali tangu lilipotolewa na Mwenyekiti wa ZEC.

Maalim Seif ambaye pia ni Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CUF amesema Chama chake hakijalizingatia tamko hilo na wala hakijadili uwezekano wa kurejewa kwa uchaguzi huo, kwa madai kuwa uchaguzi ulikamilika bila ya kuwepo malalamiko kutoka chama chochote cha siasa na wala Tume ya Uchaguzi.

Mapema akizungumza baada ya kikao hicho cha mashauriano, aliyekuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chadema Mhe. Edward Lowassa amesema kikao hicho kilichojadili Mkwamo wa kisiasa Zanzibar kimekwenda vizuri.

Hata hivyo amesema ufafanuzi zaidi utatolewa Jumapili ijayo ambapo viongozi hao wanakusudia kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Kabla ya kikao hicho Maalim Seif alifanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) Bw. Filberto Seregondi katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam na kuelezea hatua zinazochukuliwa kukwamua mkwamo wa kisiasa Zanzibar.

Balozi Seregondi ambaye anamaliza muda wake wa utumishi hapa nchini,aliambatana na ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi mkuu wa Tanzania kutoka Umoja huo.

Watanzania Wasiwekeze Kila Kitu Kwa Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu

$
0
0
Mbwana Samatta (kushoto) pamoja na Thomas Ulimwengu (kulia)

Stars inatoka katika kambi ya wiki moja na siku kadhaa nchini Afrika Kusini itawakabili ‘Mbweha wa Jangwani’ baada ya kufuzu hatua ya kwanza kwa ushindi wa jumla wa magoli 2-1 dhidi ya Malawi mwezi uliopita.

Kwa mara ya kwanza Stars itaingia uwanjani kucheza na timu bora zaidi Afrika ikiwa na mfungaji bora wa ligi ya mabingwa Afrika, namzungumzia kijana wa miaka 22, Mbwana Samatta.

Sina shaka kuhusu uwezo wa Samatta ambaye nilimshuhudia Jumapili iliyopita akiipa ubingwa wa Afrika upande wa vilabu timu ya TP Mazembe ya DR Congo.

Sitazungumzia sana mechi yenyewe lakini ningependa kuwaambia Watanzania wenzangu kuwa hatupaswi kuamini moja kwa moja katika uwezo wa mchezaji mmoja au wawili katika timu na ili kuishinda Algeria wachezaji wote kuanzia kwa golikipa hadi mchezaji wa mwisho katika safu ya ushambuliaji wanapaswa kucheza katika kiwango cha kufanana.

Samatta anazungukwa na nahodha wa timu ya taifa ya Zambia ambayo Jumatano hii iliifunga Sudan 1-0 jijini, Khartoom. Namzungumzia kiungo mshambuliaji Rainford Kalaba, pembeni ya Samatta pale TP Mazembe anacheza na mchezaji pekee wa timu ya Taifa ya Ivory Coast anayecheza barani Afrika, Roger Assale, Mghana, Solomon Asante, n.k

Kiujumla, Samatta anazungukwa na ‘rundo’ la wachezaji wenye vipaji ambao wanajituma sana ndani ya uwanja kwa muda wote wa mchezo. Huduma ambayo ‘Samagoal’ amekuwa akiitoa klabuni kwake ni tofauti kidogo na ile ambayo Watanzania wamekuwa wakitaraji kutoka kwa mchezaji huyo ambaye ni miongoni mwa wachezaji 10 bora wanaocheza ndani ya Afrika kwa mwaka huu wa 2015.

Kwa nini Samatta wa TP Mazembe ni tofauti na huyu anayeichezea Stars? Ubora wake ni uleule, tofauti ni kwamba, akiwa TP anakutana na wachezaji wenye vipaji kama yeye ambao pia hucheza kwa nidhamu, kujituma na kufuata maelekezo ya benchi la ufundi.

Mafanikio ya Samatta na ‘patna’ wake Thomas Ulimwengu ndani ya klabu yao wiki iliyopita ni ya ‘mfanowe’. Ni wachezaji wa kwanza wa Kitanzania kucheza mchezo wa fainali wa ligi ya mabingwa Afrika. Katika michezo miwili ya fainali kati ya TP Mazembe na USM Algers ya Algeria, Samatta amefanikiwa kufunga magoli mawili kati ya manne ya TP na kutengeneza goli lingine moja.

Ushindi wao wa taji la mabingwa Afrika umewafanya Watanzania wengi kujenga imani kwamba, Stars inaweza kuishinda na kuitoa Algeria! Kila kitu kinawezekana katika mchezo wa soka, lakini ukitazama aina ya wapinzani ambao tunakwenda kucheza nao ni sawa na ‘mlima mrefu’ ambo tunapaswa kuupandaa.

Ulimwengu anacheza kwa kupambana sana akiwa klabuni kwake TP Mazembe na amekuwa akicheza hivyo hivyo hadi timu ya Taifa Stars. Lakini Samatta anahitaji ‘muunganiko’, anahitaji wachezaji wenzake wacheze kwa asilimia ya juu. Anahitaji wachezaji ambao wana uwezo wa kuusoma mchezo. Kila Mtanzania ukimuuliza hivi sasa kwanini anaamini Stars itashinda dhidi ya Algeria anakwambia “Mbwana Samatta”.

Lakini mchezo wa mpira wa miguu si kama mchezo wa ngumi au tenis, mtu anapambana mwenyewe. Akiwa mzuri anapata matokeo. Lakini mchezo wa mpira wa miguu unahitaji sana uwezo wa kiuchezaji wa mchezaji mwingine. Ukitaka kuuona uwezo halisi wa Samatta katika timu ya Taifa ni lazima, Shomari Kapombe, Nadir Haroub, Kelvin Yondan, Ally Mustapha wote wacheze inavyotakiwa katika idara zao.

Timu ambayo Samatta aliifunga magoli mawili katika fainali ya CAF Champions league haina hata mchezaji mmoja katika timu ya Taifa ya Algeria! Inamaanisha kuwa wanategemea zaidi mkusanyiko wa wachezaji wao wanaofanya vizuri barani Ulaya. Algeria ina wachezaji wanaofanya vizuri katika ligi kuu England, Hispania, Ureno na kwingineko.

Algeria wamekuja na ‘timu kabambe’, Rais M’Bolhi (Antalyaspor/Uturuki), Azzedine Doukha (JS Kabylie), Malik Asselah (CR Belouizdad). Viungo: Mehdi Zeffane (Rennes/Ufaransa), Mohamed Khoutir Ziti (JS Kabylie), Faouzi Ghoulam (Napoli/Italia), Djamel Mesbah (Sampdoria/Italia), Carl Medjani (Trabzonspor/Uturuki),Aïssa Mandi (Reims/Ufaransa), ukweli itakuwa mechi ngumu kwa Stars kuliko Algeria.

Dr Magufuli Aifumua Ikulu.....Aipanga upya Kwa kupunguza Ofisi na Watendaji

$
0
0
Rais John Magufuli amezifumua na kuziunda upya baadhi ya ofisi za Ikulu ya Magogoni, Dar es Salaam pamoja na kuwaondoa baadhi ya watumishi ambao hawana ulazima katika mfumo wa utumishi wa Ikulu.

Taarifa za uhakika zilizotufikia kutoka ndani ya Ikulu zimeeleza kuwa Rais Magufuli alianza kufanya ukaguzi wa ofisi moja baada ya nyingine zilizo Ikulu huku akitaka maelezo ya kina kuhusu shughuli zake na aina ya watendaji waliopo.

Mmoja wa maofisa waandamizi wa Ikulu aliyezungumza  kwa sharti la jina lake kuhifadhiwa, alisema katika ukaguzi huo, Rais Magufuli aliamuru kufungwa mara moja kwa baadhi ya ofisi alizobaini kuwa hazina tija na kwamba zina watumishi ambao ni mizigo.

Ofisa huyo alizitaja baadhi ya ofisi zilizofungwa kuwa ni pamoja na iliyokuwa ikishughulikia chakula cha rais na ile iliyokuwa ikijihusisha na kupokea wageni binafsi wa rais.

“Rais Magufuli alipoingia tu Ikulu alifanya ziara ya kukagua ofisi zote zilizopo Ikulu, alitaka kujua utendaji kazi wa ofisi hizo lakini alipofika kwenye kitengo maalumu cha lishe ya rais alisema haoni umuhimu wa kuwepo kwa ofisi hiyo kwa sababu suala la lishe yake siku zote linasimamiwa na mkewe Janeth. Akaamuru ifungwe na watumishi wake warejeshwe walikotoka.

"Ofisi nyingine aliyoamuru ifungwe ni kupokea wageni binafsi wa rais. Alisema haoni tija ya kuwepo kwa ofisi hiyo kwa sababu mgeni anatakiwa kufika Ikulu baada ya kutoa taarifa, nayo aliamuru ifungwe,” alisema ofisa huyo.

Taarifa zaidi zimeeleza kuwa aliyekuwa mkuu wa kitengo cha lishe Ikulu amerudishwa katika ajira yake ya awali Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, huku watumishi wengine wakipelekwa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Alipotafutwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue kupitia simu ya kiganjani kuzungumzia hatua hiyo, simu yake iliita muda mrefu bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno ulionyesha kupokelewa kwenye simu yake lakini haukujibiwa.

Alipoulizwa Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi, Premi Kibanga kuhusu kuwepo kwa hatua hizo alisema ni kweli Rais Magufuli alipoingia ofisini alianza kuipanga upya Ikulu kulingana na matakwa yake wakati wa utawala wake.

Premi ambaye alizungumza kupitia simu yake ya kiganjani alisema wakati wa utawala wa Serikali ya awamu ya nne kulikuwa na ofisi maalumu ya lishe Ikulu ambayo hata hivyo ilikuwa haihusiani na uandaaji wa chakula cha rais.

Alisema ofisi hiyo ilikuwa mahususi kwa ajili ya ushauri kuhusu programu ya kimataifa ya urutubishaji wa vyakula kwa lengo la kupunguza tatizo la udumavu wa watoto.

“Ofisi hiyo ilikuwa inaongozwa na mtaalamu wa masuala ya lishe hata hivyo kabla ya Rais Kikwete kumaliza muda wake mtaalamu huyo aliacha kazi yake na kwenda kugombea ubunge huko kwao sasa ukiniambia amerudishwa Wizara ya Afya sitakuwa na jibu la uhakika kwa sababu sifahamu,” alisema Premi.

Alipoulizwa kuhusu kufungwa kwa ofisi ya wageni binafsi wa Rais, Premi alisema ilikuwa na kazi ya kupokea malalamiko ya wananchi lakini Rais Magufuli ameamua kuiondoa kwa sababu ameweka utaratibu wa malalamiko ya wananchi kupokewa kuanzia ngazi za chini.

“Kama unavyojua Rais amekuja na dira yake ya ‘hapa kazi tu,’ hivyo anataka watendaji wa ngazi zote wawajibike kwa ufanisi. Wakati wa utawala wa Rais Kikwete alifungua dawati hilo kwa ajili ya kusikiliza matatizo ya wananchi, watu walitoka mikoa ya mbali kuleta kero zao hapa Ikulu lakini Rais Magufuli ameamua malalamiko ya wananchi yasikilizwe kuanzia ngazi za chini.

“Rais Magufuli anataka watendaji wote wa Serikali wawajibike kupokea kero za wananchi na kuzifanyia kazi. Zipo ofisi za madiwani, wabunge, wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa ambao wote wanalo jukumu la kuwasikiliza wananchi na kuwatatulia kero zao,” alisema Premi.

Credit:Mtanzania

Ratiba ya Uchaguzi wa Spika wa Bunge Pamoja na Uteuzi wa Waziri Mkuu

$
0
0
Spika  wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anatarajiwa kuchaguliwa mjini Dodoma Jumanne ijayo, ratiba ya Bunge hilo imeeleza.
 
Kutokana na ratiba hiyo, ni wazi Chama Cha Mapinduzi (CCM), kitalazimika kumtaja mgombea wake atakayekuwa na nafasi kubwa ya kuwa Spika kati ya kesho na keshokutwa na kumaliza mvutano wa nani anafaa kuwa spika, baada ya wanachama 22 kujitokeza mpaka jana kuwania nafasi hiyo.

“Kutokana na kuitishwa kwa Bunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk John Pombe Joseph Magufuli... Ofisi ya Bunge inapenda kuwatangazia wabunge wateule wote kuwa wanatakiwa kuwasili mjini Dodoma Novemba 13, 2015 (jana) tayari kwa ajili ya usajili utakalofanyika bungeni kuanzia siku hiyo hiyo,” imeeleza ratiba hiyo iliyowekwa katika ukurasa wa Facebook wa Bunge.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, kuanzia jana mpaka kesho, wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, watapaswa kuwa wameshawasili mjini Dodoma na kujisajili kwa watumishi wa Bunge ambao wameshaanza kazi hiyo.

Baada ya kazi hiyo, ratiba ya Bunge hilo imeonesha kuwa keshokutwa siku ya Jumatatu, wabunge wote wanatarajiwa wawe wameshajisajili ili saa nne asubuhi washiriki kikao cha maelekezo katika Ukumbi wa Bunge kitakachohusisha kutembelea ukumbi huo.

Ratiba hiyo inaonesha kuwa siku hiyo hiyo kuanzia saa 10 jioni, wabunge hao watakuwa na mikutano ya vyama vyao, ambako inatarajiwa hoja kubwa itakuwa jina la Spika na Naibu Spika.

Spika
Siku ya Jumanne wiki ijayo, Watanzania wataelekeza macho yao na masikio katika Kikao cha Kwanza cha Bunge la 11 mkoani hapa, ambacho kitatanguliwa na kusomwa kwa tamko la Rais Magufuli la kuitisha Bunge.

Mara baada ya kusomwa kwa tamko hilo, kutafuatiwa na uchaguzi wa Spika utakaofanyika kwa kura za siri na mshindi akishatangazwa, atakula kiapo siku hiyo hiyo, kisha atapigiwa Wimbo wa Taifa na dua itasomwa.

Siku hiyo hiyo, Spika huyo anatarajiwa kuanza kuapisha wabunge na kazi hiyo ataendelea nayo siku ya Jumatano na kumalizia siku ya Alhamisi asubuhi kwa wabunge watakaokuwa hawajala kiapo cha uaminifu.

Waziri Mkuu, Naibu Spika
Alhamisi ya Novemba 19, saa 10 jioni Rais Magufuli anatarajiwa kupeleka kwa Spika jina la Waziri Mkuu ambalo litasomwa mbele ya wabunge wote na kuthibitishwa na wabunge kwa kura.

Baada ya kuthibitishwa kwa Waziri Mkuu, siku hiyo hiyo Naibu Spika atachaguliwa na kula kiapo cha uaminifu na baada ya hapo wabunge watajiweka tayari kwa Hotuba ya Kwanza ya Rais Magufuli itakayotolewa Ijumaa saa kumi jioni na kufuatiwa na kuahirishwa kwa Bunge.

Lowassa Kuongea na Watanzania Leo jijini i Arusha

$
0
0
Aliyekuwa mgombea wa urais wa Chadema, Edward Lowassa anatarajia kuhutubia mkutano wa kumnadi mgombea wa ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema na kuwashukuru Watanzania kwa kura walizompa katika Uchaguzi Mkuu uliopita.

Jeshi la Polisi limeridhia mkutano huo utakaofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro, lakini limepiga marufuku maandamano yoyote.

Huu utakuwa mkutano wa kwanza wa hadhara kwa Lowassa tangu matokeo ya uchaguzi mkuu yalipotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ambayo yalimpa ushindi mgombea wa CCM, Dk John Magufuli. Lowassa alipata kura 6,072,848, sawa na asilimia 39.97 wakati mshindi Dk Magufuli alijikusanyia kura 8,882,935 sawa na asilimia 58.46

“Tunatarajia kesho (leo) aliyekuwa mgombea wa urais wa Chadema chini ya mwavuli wa Ukawa, Edward Lowassa atahutubia mkutano wa kampeni wa kawaida akiongozana na viongozi wengine wa kitaifa,” alisema Katibu wa Chadema Wilaya ya Arusha, Lewis Kopwe, alipozungumzia kukamilika kwa maandalizi yote ya mkutano huo jana.

Kopwe alisema mkutano huo ni sehemu ya mikutano ya kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arusha Mjini na amehimiza amani na utulivu vitamalaki katika mkutano huo.

Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas jana alisema wamepiga marufuku maandamano ya aina yoyote katika mikutano ya kampeni inayoendelea.

Alionya Jeshi la Polisi halitasita kumchukulia hatua mtu yeyote ambaye ataandamana na kusababisha kuvunjika kwa amani katika Jiji la Arusha. “Kuna watu, kwa maslahi yao, wanataka kutuvunjia amani, sasa tunaonya tutachukua hatua kali kwa yeyote ambaye atavunja sharia,” alisema Kamanda Sabas.

Pamoja na onyo hilo, alisema kuwa hadi jana jeshi hilo, lilikuwa halijapata barua yoyote ya kutaka maandamano na hata ikiwapo hawatakuwa tayari kuruhusu yafanyike. Pia, alisema jeshi hilo liko vizuri na limejipanga kuhakikisha amani na utulivu vinadumu kama ilivyokuwa wakati wa Uchaguzi Mkuu Oktoba 25 mwaka huu.

Katika hali inayoonyesha kwamba Jeshi la Polisi halitanii, jana jiji la Arusha lilikumbwa na taharuki kutokana na magari makubwa ya kurusha maji ya kuwashwa kupitishwa mitaani huku yakiwa kwenye mwendo kasi.

Kamanda Sabas alisema kilichokuwa kinafanyika ni mazoezi ya kawaida ambayo yanathibitisha kuwa polisi ipo imara. “Haya ni mazoezi ya kawaida, tunajua uchaguzi bado unaendelea na tumejipanga kulinda amani ya Arusha,” alisema.

Lema, ambaye anajiandaa kutetea kiti hicho alisema kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni kwamba Lowassa atazungumza leo na Watanzania, pia kuwashukuru kwa kumpigia kura nyingi.

Naye Mbunge mteule wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi “Sugu” alisema katika mkutano huo Chadema watatoa tamko zito la kwanza mara baada ya uchaguzi huo wa madiwani, wabunge na rais kumalizika.

Raisi mstaafu,Jakaya Mrisho Kikwete Aingia Mtaani.....Afanya 'Shopping’ Mlimani City

$
0
0
Kwa mara ya kwanza tangu aondoke madarakani mwanzoni mwa mwezi huu, jana Rais Jakaya Kikwete alionekana akifanya manunuzi katika maduka yaliyopo jengo la Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

Kikwete, ambaye alikuwa amevalia suti maarufu kama ‘kaunda suti’ yenye rangi nyeusi, alionekana akiingia katika viunga vya Mlimani City saa 5:00.

Mwandishi wetu ambaye alikuwepo katika viunga hivyo vya Mlimani City alishuhudia Kikwete akiwasili katika maeneo hayo akiwa katika msafara wa magari manne na pikipiki moja.

Rais huyo mstaafu pia alikuwa ameambatana na mkewe, Salma Kikwete, aliyekuwa amevalia mavazi ya kitenge pamoja na walinzi wao wanne.

Hatua hiyo ilionekana kushangaza baadhi ya watu waliokuwepo katika maeneo hayo, huku wengi wao wakionekana kutaka kumsalimia.

Mwandishi wetu ambaye  muda wote alikuwa akimfuatilia Rais Kikwete na mke wake, alishuhudia wakiingia katika maduka ya Game na kufanya manunuzi kwa dakika zisizopungua 10 hadi 15 na  baadaye kutoka nje na walinzi wake wakionekana kubeba mifuko iliyokuwa na bidhaa walizonunua.

Kama ilivyo hulka ya Rais Kikwete alipotoka nje ya duka hilo alianza kusalimiana na mtu mmoja ambaye alionekana kufahamiana naye.

Hatua hiyo ilimpa fursa ya kuwasalimia watu wengine waliokuwa karibu na tawi la benki moja.

Baada ya hapo msafara wake uliondoka na kuelekea Barabara ya Sam Nujoma.

Tangu achaguliwe kuwa rais mwaka 2005 itifaki na majukumu yake ya urais yalikuwa yakimbana Rais Kikwete na hivyo kushindwa mambo yake binafsi kama walivyo raia wengine.

Pamoja na kwamba Kikwete sasa ni raia, lakini kutokana na wadhifa aliowahi kuushika wa urais bado halingani na raia wengine wa kawaida, ingawaje majukumu ya urais yamepungua na hivyo kumpa fursa ya kutembea katika maeneo ya wazi na kufanya matumizi ya kawaida kama alivyofanya jana.

Tangu alipoachia kiti cha urais na kumkabidhi Dk. John Magufuli baada ya kuapishwa Novemba 5, Kikwete amekuwa akiishi nyumbani kwake Msoga, mkoani Pwani.

Rais Kikwete aliondoka rasmi Ikulu na familia yake Ijumaa iliyopita Novemba 6 na kuanza maisha mapya kijijini kwake huko.

Wastara Juma Apandisha Majina na Kumshushia Kichapo Mr Bond

$
0
0
KAZI ipo! Staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma anadaiwa kumpa kichapo kikali aliyekuwa mwandani wake, Bond Suleiman baada ya kupatwa na kile kinachosemwa kuwa ni kupandisha majini.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, kupandisha majini hayo kulitokana na jinsi ambavyo mwanaume huyo amekuwa akimtendea mpenziwe huyo, ambaye inadaiwa katika kupandisha huko, alitoa maelekezo ya namna anavyotakiwa kufanya.

“Nakuambia ilikuwa varangati siku hiyo, Wastara alipandisha majini akiwa na Bond, walikuwa wakijaribu kutatua mgogoro wao, lakini katika hali ya kushangaza, ghafla Wastara alibadilika na kuanza kusema hivyo kwa sauti tofautitofauti, kabla ya kumshushia kipigo,” kilisema chanzo chetu, kilichoomba hifadhi ya jina lake.

Wastara alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo alimtaka mwandishi wetu kuwasiliana na Bond, huku akidai hata kama ni kweli, hayo yanabaki kuwa maisha yao.
Kwa upande wake, Bond alikiri kutokea kwa sakata hilo na hadi wakati huo (Alhamisi) alikuwa Saadan, Bagamoyo katika Sober House akikamilisha zoezi la kupewa ushauri nasaha.
“Ni kweli niko huku, natekeleza adhabu niliyopewa na Wastara, ikiwemo kunyoa nywele, kupewa ushauri wa jinsi ya kuishi. Nimeachana na pombe, mirungi, shisha, kubadilisha wanawake na starehe nyingine za aina hiyo, sasa nimebadilika, sitamuumiza tena Wastara, zimebaki siku kama 6 nikamilishe zoezi hili,” alisema Bond.

GPL

Kwa Mara ya Kwanza Wastara Aonyesha Miguu Yake na Kuandika Mazito Kuhusu Kinachomsumbua

$
0
0
Kwa mara ya kwanza toka nimekatwa mguu miaka 6 iliyopita leo nimechukua nafasi hii kupost hii pic kuondoa maswali mengi yaliyopo vichwani mwa watu
Nipo kama unavyoiona pic
Huyo ndio wastara nilivyo hakuna kilichopungua zaidi ya hicho unachokiona
Kuwa mlemavu ni kitu kingine tofauti ukiwa mzima hivyo kusikia maumivu na kuumwa mguu ni kitu cha kawaida
Sasa nipo nairobi kimatibabu na tatizo ni operetion ya kwanza nilikosewa ndio sababu ya maumivu ya mara kwa mara madaktari wameshajua nini cha kunifanya ili kuondoa mateso kwangu
Jifunze kitu kupitia hii pic yangu na si kucoment ujinga jiulize ungekuwa wew mama yako dada yako mume,mke, wako ungeweza kusmile kma mimi hali ya kuwa una maumivu?
Jifunze kitu kupitia wastara
na sijajidharirisha nimetaka wewe unijue nilivyo ili usiteseke na maswali juu yangu
Sijakatwa miguu yote kma ilivyovumishwa na pia pamoja na maumivu ninaweza kutembea japo si mwendo mrefu sana na naendelea kusmile
SOTE TUSEME ALHMADULILAH
ASANTE MUNGU

Wastara Juma @wastara84 on instagram

Soma Hapa Walichoamua Watoto wa Dk Hellen Kijo-Bisimba Mkurugenzi wa (LHRC) Baada ya Kupata Ajali ya Gari

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Mkur, Dk Hellen Kijo-Bisimba anatarajia kusafirishwa kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi.

Novemba 7, mwaka huu Dk Bisimba alipata ajali ya gari katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi na kuvunjika mshipa wa paja na goti sanjari na kujeruhiwa kichwa,bega na mgongo.

Akizungumza jana akiwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es Salaam, Dk Bisimba alisema kwa sasa anaendelea vizuri na kwamba anatarajiwa kupelekwa nchini humo na watoto wake kwa matibabu zaidi.

Alisema safari yake hiyo siyo kwa sababu ya upungufu wa huduma aliyoipata kutoka MOI bali ni kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi wa mwili wake.

“Namshukuru Mungu naendelea vizuri. Tangu nimekuja hapa MOI, nimesikilizwa na kuhudumiwa vizuri. Watoto wangu wanashugulikia usafiri na siku yoyote naenda India ,”alisema.

Meneja Uhusiano MOI, Jumaa Almasi alisema kuwa Dk Bisimba bado anahitaji uangalizi wa hali ya juu katika kipindi hiki kutokana na kupata majeraha mengi kwenye mwili wake.
 
 “Hali ya Dk Bisimba imevunja rekodi. Mbali na kumshughulikia sehemu hizo mbili (paja na goti), kutokana na kuwa na kisukari na presha tumeshindwa kulazimisha matibabu ya haraka kwa viungo vyote,” alisema.

Breaking News: Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoani GEITA Auawa Kinyama Kwa Kukatwa na Mapanga na Shoka Wakati Akifanya Kampeni za Kumnadi Diwani Wake

$
0
0
Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo ameuawa leo mjini Katoro baada ya kushambuliwa kwa mapanga na shoka na kumjeruhi vibaya sehemu mbalimali za mwili wake hasa kichwani wakati akifanya kampeni za kumnadi diwani wake

Mawazo aliyewahi pia kuwa Diwani wa Kata ya Sombetini Arusha amefariki dunia akiwa hospitalini alipokimbizwa katika jitihada za kujaribu kuokoa maisha yake. Mganga Mkuu Geita amethibitisha.

Meet The Refugee Boy Of Yesterday Who Is Now A President

$
0
0

The circled child in the photo above is the current President of Gabon, Ali Bongo. That picture was taken in an orphanage years ago before he was adopted by Omar Bongo, the late Gabonese President.

President Ali Bongo Ondimba of Gabon is a Nigerian of the ethnic Igbo stock, he was one of the children flown to Gabon during the Biafran war.



Prophet Says Mugabe Has Until December 31 To Live

$
0
0

A Malawian prophet, Austin Liabunya says Zimbabwean President Robert Mugabe has only until 31st December to live.

Liabunya's prophecy, which hit the media earlier this year has been under debate as the days to Mugabe's death near.

10 months after he made his controversial prediction, the preacher has expressed no regret saying Mugabe will die by December 31, this year.

"He made these utterances at the new year during a cross over service in Lilongwe. The service was held in Area 23 at Music Cross Road tent in Malawi's administrative capital Lilongwe in the early hours of January 1st," a published report reads.

Liabunya said "Mugabe's biological clock will not tick beyond this year" after which Zimbabwe will be "restored" to be one of the richest countries in Africa.

The prophet said First Lady Grace Mugabe "will never win in Zimbabwean politics" and had simply joined politics to "protect her ill-gotten wealth," for which she would be soon humiliated.

Liabunya said that it would be good for Grace to contest as she would give back wealth to the Zimbabweans during the campaign period.

The preacher says Mugabe will "certainly die as proclaimed by this oracle of God and I will be vindicated as God's humble messenger."

Rais Magufuli Afuta Kitengo cha Upishi na Kupokea Wageni Ikulu..Adai Anaepashwa Kushughulikia Anakula nini ni Mke Wake Janeth Magufuli na si Mwingine

$
0
0
RAIS John Magufuli amezifumua na kuziunda upya baadhi ya ofisi za Ikulu ya Magogoni, Dar es Salaam pamoja na kuwaondoa baadhi ya watumishi ambao hawana ulazima katika mfumo wa utumishi wa Ikulu.

Taarifa za uhakika zilizolifikia MTANZANIA Jumamosi kutoka ndani ya Ikulu zimeeleza kuwa Rais Magufuli alianza kufanya ukaguzi wa ofisi moja baada ya nyingine zilizo Ikulu huku akitaka maelezo ya kina kuhusu shughuli zake na aina ya watendaji waliopo.

Mmoja wa maofisa waandamizi wa Ikulu aliyezungumza na gazeti hili kwa sharti la jina lake kuhifadhiwa, alisema katika ukaguzi huo, Rais Magufuli aliamuru kufungwa mara moja kwa baadhi ya ofisi alizobaini kuwa hazina tija na kwamba zina watumishi ambao ni mizigo.

Ofisa huyo alizitaja baadhi ya ofisi zilizofungwa kuwa ni pamoja na iliyokuwa ikishughulikia chakula cha rais na ile iliyokuwa ikijihusisha na kupokea wageni binafsi wa rais.

?Rais Magufuli alipoingia tu Ikulu alifanya ziara ya kukagua ofisi zote zilizopo Ikulu, alitaka kujua utendaji kazi wa ofisi hizo lakini alipofika kwenye kitengo maalumu cha lishe ya rais alisema haoni umuhimu wa kuwepo kwa ofisi hiyo kwa sababu suala la lishe yake siku zote linasimamiwa na mkewe Janeth. Akaamuru ifungwe na watumishi wake warejeshwe walikotoka.

Ofisi nyingine aliyoamuru ifungwe ni kupokea wageni binafsi wa rais. Alisema haoni tija ya kuwepo kwa ofisi hiyo kwa sababu mgeni anatakiwa kufika Ikulu baada ya kutoa taarifa, nayo aliamuru ifungwe,? alisema ofisa huyo.

Taarifa zaidi zimeeleza kuwa aliyekuwa mkuu wa kitengo cha lishe Ikulu amerudishwa katika ajira yake ya awali Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, huku watumishi wengine wakipelekwa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Alipotafutwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue kupitia simu ya kiganjani kuzungumzia hatua hiyo, simu yake iliita muda mrefu bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno ulionyesha kupokelewa kwenye simu yake lakini haukujibiwa.

Alipoulizwa Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi, Premi Kibanga kuhusu kuwepo kwa hatua hizo alisema ni kweli Rais Magufuli alipoingia ofisini alianza kuipanga upya Ikulu kulingana na matakwa yake wakati wa utawala wake.

Premi ambaye alizungumza na MTANZANIA Jumamosi kupitia simu yake ya kiganjani alisema wakati wa utawala wa Serikali ya awamu ya nne kulikuwa na ofisi maalumu ya lishe Ikulu ambayo hata hivyo ilikuwa haihusiani na uandaaji wa chakula cha rais.

Alisema ofisi hiyo ilikuwa mahususi kwa ajili ya ushauri kuhusu programu ya kimataifa ya urutubishaji wa vyakula kwa lengo la kupunguza tatizo la udumavu wa watoto.

?Ofisi hiyo ilikuwa inaongozwa na mtaalamu wa masuala ya lishe hata hivyo kabla ya Rais Kikwete kumaliza muda wake mtaalamu huyo aliacha kazi yake na kwenda kugombea ubunge huko kwao sasa ukiniambia amerudishwa Wizara ya Afya sitakuwa na jibu la uhakika kwa sababu sifahamu,? alisema Premi.

Alipoulizwa kuhusu kufungwa kwa ofisi ya wageni binafsi wa Rais, Premi alisema ilikuwa na kazi ya kupokea malalamiko ya wananchi lakini Rais Magufuli ameamua kuiondoa kwa sababu ameweka utaratibu wa malalamiko ya wananchi kupokewa kuanzia ngazi za chini.

?Kama unavyojua Rais amekuja na dira yake ya ?hapa kazi tu,? hivyo anataka watendaji wa ngazi zote wawajibike kwa ufanisi. Wakati wa utawala wa Rais Kikwete alifungua dawati hilo kwa ajili ya kusikiliza matatizo ya wananchi, watu walitoka mikoa ya mbali kuleta kero zao hapa Ikulu lakini Rais Magufuli ameamua malalamiko ya wananchi yasikilizwe kuanzia ngazi za chini.

?Rais Magufuli anataka watendaji wote wa Serikali wawajibike kupokea kero za wananchi na kuzifanyia kazi. Zipo ofisi za madiwani, wabunge, wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa ambao wote wanalo jukumu la kuwasikiliza wananchi na kuwatatulia kero zao,? alisema Premi.

LOWASSA Atoa Kauli Kuhusu Mauaji ya Mwenyekiti wa Chadema Geita Aliyeuawa Kwa Kukatwa na Mapanga

$
0
0
Marehemu
Katika Ukurasa Wake wa Facebook Lowassa Ameandika Haya Kuhusu Kifo cha Mwenyekiti wa Chademe Mkoani Geita:


"Nimeshtushwa na kusikitishwa na taarifa za msiba wa kijana wetu Alphonce Mawazo, Natoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki pamoja na familia yetu ya UKAWA' Lowassa
Hakika tumeondokewa na mpiganaji.

Ratiba ya Uchaguzi wa Spika wa Bunge Pamoja na Uteuzi wa Waziri Mkuu

$
0
0
Spika  wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anatarajiwa kuchaguliwa mjini Dodoma Jumanne ijayo, ratiba ya Bunge hilo imeeleza.
 
Kutokana na ratiba hiyo, ni wazi Chama Cha Mapinduzi (CCM), kitalazimika kumtaja mgombea wake atakayekuwa na nafasi kubwa ya kuwa Spika kati ya kesho na keshokutwa na kumaliza mvutano wa nani anafaa kuwa spika, baada ya wanachama 22 kujitokeza mpaka jana kuwania nafasi hiyo.

“Kutokana na kuitishwa kwa Bunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk John Pombe Joseph Magufuli... Ofisi ya Bunge inapenda kuwatangazia wabunge wateule wote kuwa wanatakiwa kuwasili mjini Dodoma Novemba 13, 2015 (jana) tayari kwa ajili ya usajili utakalofanyika bungeni kuanzia siku hiyo hiyo,” imeeleza ratiba hiyo iliyowekwa katika ukurasa wa Facebook wa Bunge.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, kuanzia jana mpaka kesho, wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, watapaswa kuwa wameshawasili mjini Dodoma na kujisajili kwa watumishi wa Bunge ambao wameshaanza kazi hiyo.

Baada ya kazi hiyo, ratiba ya Bunge hilo imeonesha kuwa keshokutwa siku ya Jumatatu, wabunge wote wanatarajiwa wawe wameshajisajili ili saa nne asubuhi washiriki kikao cha maelekezo katika Ukumbi wa Bunge kitakachohusisha kutembelea ukumbi huo.

Ratiba hiyo inaonesha kuwa siku hiyo hiyo kuanzia saa 10 jioni, wabunge hao watakuwa na mikutano ya vyama vyao, ambako inatarajiwa hoja kubwa itakuwa jina la Spika na Naibu Spika.

Spika 
Siku ya Jumanne wiki ijayo, Watanzania wataelekeza macho yao na masikio katika Kikao cha Kwanza cha Bunge la 11 mkoani hapa, ambacho kitatanguliwa na kusomwa kwa tamko la Rais Magufuli la kuitisha Bunge.

Mara baada ya kusomwa kwa tamko hilo, kutafuatiwa na uchaguzi wa Spika utakaofanyika kwa kura za siri na mshindi akishatangazwa, atakula kiapo siku hiyo hiyo, kisha atapigiwa Wimbo wa Taifa na dua itasomwa.

Siku hiyo hiyo, Spika huyo anatarajiwa kuanza kuapisha wabunge na kazi hiyo ataendelea nayo siku ya Jumatano na kumalizia siku ya Alhamisi asubuhi kwa wabunge watakaokuwa hawajala kiapo cha uaminifu.

Waziri Mkuu, Naibu Spika
Alhamisi ya Novemba 19, saa 10 jioni Rais Magufuli anatarajiwa kupeleka kwa Spika jina la Waziri Mkuu ambalo litasomwa mbele ya wabunge wote na kuthibitishwa na wabunge kwa kura.

Baada ya kuthibitishwa kwa Waziri Mkuu, siku hiyo hiyo Naibu Spika atachaguliwa na kula kiapo cha uaminifu na baada ya hapo wabunge watajiweka tayari kwa Hotuba ya Kwanza ya Rais Magufuli itakayotolewa Ijumaa saa kumi jioni na kufuatiwa na kuahirishwa kwa Bunge.

Maalim Seif na Lowassa Wakutana Dar es Salaam, Maalim Seif Asizitiza Kuwa Msimamo ni ule ule.....

$
0
0
MGOMBEA urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amekutana na aliyekuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia Chadema, Edward Lowassa, jijini Dar es Salaam juzi na kusisitiza kuwa CUF haitarudia uchaguzi uliofutwa visiwani humo.Edward Lowassa

Akizungumza juzi jijini Dar es Salaam baada ya mkutano huo wa ndani, Maalim Seif alisema uchaguzi huo ulifutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salum Jecha binafsi.

“Msimamo wa CUF uko wazi, hatuoni sababu ya kuficha. Tangazo la mwenyekiti sisi tunaona si halali, kwa hivyo hatutashiriki…Tushiriki kwa sababu gani? Uchaguzi huu tulishashiriki, wenzetu hawataki, tuna uhakika gani kama huo mwingine watakubali?” alihoji Maalim Seif.

“Msimamo ni ule ule… hata ukisoma tangazo lile linasema mimi Salim Jecha, haikusema kama ni Serikali, limesema Jecha Salim.”

Alipoulizwa kuhusu mazungumzo yake na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, Maalim Seif alikataa kuyaweka wazi akisema muda wake bado.

Hata alipoulizwa pia kuhusu mazungumzo yake na Rais Jakaya Kikwete kuhusu mzozo huo, Maalim Seif alisema bado wakati wake wa kuyazungumza.

“Bado wakati wake, mtapata yote wakati ukifika,” alisema.

Naye Lowassa alipoulizwa kuhusu kamatakamata ya wasaidizi wake, aligoma kuzungumzia akimtaka msaidizi wake wa habari, Aboubakar Liongo aeleze.

Hata hivyo Liongo naye aliwataka waandishi wa habari kusubiri Jumapili, siku ambayo Lowassa atakutana na waandishi wa habari.

Awali Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, aliingia katika ofisi za Lowassa eneo la Mikocheni Viwandani majira ya saa 10 alasiri ambako walikuwa na kikao kilichodumu kwa zaidi ya saa nzima.

Mbali ya Lowassa na Maalim Seif, wengine waliohudhuria kikao hicho cha ndani ni pamoja na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, Kaimu Mwenyekiti wa CUF, Twah Tasilima, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu na msaidizi wa siasa wa Lowassa, Matson Chizii.
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images