Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli Aagiza Fedha Zilizochangwa Kwa Ajili ya Sherehe ya Kumpongeza Zipelekwe Hospitali ya Taifa Muhimbili

$
0
0
Baada ya kulihutubia na kulizindua bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt JOHN POMBE MAGUFULI amehudhuria hafla fupi iliyoandaliwa kwa ajili ya wabunge katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma na kuagiza fedha zilizochangwa kwa ajili ya kugharamia hafla hiyo zipelekwe Katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kununulia vitanda vya wagonjwa.

Mheshimiwa Magufuli ametoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa kuwa wadau mbalimbali wamechanga kiasi cha shilingi milioni 225 kwa ajili ya kugharamia hafla ya wabunge katika siku ya uzinduzi wa Bunge.

Dkt Magufuli amesema alipata taarifa za kuwepo kwa michango hiyo ya fedha na kutoa maelekezo kuwa zitumike kwa kiasi kidogo kwa ajili ya hafla hiyo na sehemu kubwa zipelekwe katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili zikatumike kununulia vitanda na hivyo kupunguza tatizo la wagongwa wanaolala chini kutokana na uhaba wa vitanda unaikabili hospitali hiyo.

“Nilipoambiwa kwamba zimechangwa shilingi milioni 225 zimekusanywa kwa ajili ya sherehe, nikasema fedha hizo zipelekwe katika hospitali ya Taifa Muhimbili zikasaidie kununua vitanda” alisema Dkt Magufuli na kusisitiza kuwa “kwa kufanya hivyo tutakua tumejinyima sisi wenyewe lakini tutakua tumewanufaisha wenzetu ambao wanamatatizo makubwa yanayoweza kutatuliwa kwa fedha hizo”.

Awali akitoa taarifa ya michango hiyo Ofisa wa Spika wa Bunge Bwana SAID YAKUBU amesema jumla michango iliyopatikana na shilingi milioni 225 na kwamba fedha zilizotumika katika hafla hiyo ni shilingi milioni 24 tu baada ya kuzingatia maagiza ya Rais Magufuli.

Katika Hafla hiyo Rais Magufuli amekabidhi vyeti vya kutambua mchango wa wadau waliochangia fedha wakiwemo Benki za NMB, CRDB na Benki ya Afrika pamoja na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya PSPF na PPF.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano IKULU
November 20, 2015

Looks Like it's True! TMZ is Reporting That Kylie Broke Up With Tyga

$
0
0

MTO reported it earlier but I didn't believe...lol.. but since TMZ is also reporting it...it could be true! .
Kylie Jenner and Tyga have broken up, and it was sudden and nasty ... TMZ has learned. Sources connected with the couple tell us they split Thursday, just after Kylie returned from Australia. One source says, "It's something Tyga did," but the source would not be specific. Sources connected with Tyga say Kylie's the one who pulled the plug and it had something to do with "pressure from the Kardashians." Kendall was out Thursday night at dinner and we're told she was upset and had harsh words about Tyga.


UKAWA Wasimulia Kilichowafanya Walete Vurugu Na Kumzomea Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein

$
0
0
UMOJA wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umesema mipango yao ya kutomruhusu Rais Dk. John Magufuli kulihutubia Bunge akiwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, imefanikiwa.

Mwenyekiti wa Umoja huo, Freeman Mbowe, alisema  jana kuwa walimua kuzuia Rais Magufuli asihutubie Bunge kwa vile Dk. Shein, muda wake wa kuwa rais ulikwisha tangu Novemba 2 mwaka huu kwa hiyo hakustahili kuhudhuria Bunge hilo.

Alisema kuwa waliamua kufanya vile wakiamini kuwa ilikuwa sehemu muafaka ya kufikisha kilio chao kutokana na wageni mbalimbali waliohudhuria mkutano ule, wakitokea katika nchi za jumuiya ya kimataifa.

“Tulishangaa kumuona Dk. Shein, Pandu Amiri Kificho na Makamu wa Pili wa Rais wakiwa ndani ya Bunge wakati kikatiba hawana uhalali,” alisema Mbowe.

Alisema, baada ya kitendo kile hivi sasa umoja wa vyama hivyo, unatarajia kukutana ili kupeana mikakati ya kuendeleza mapambano ya ndani na nje ya nchi ya kudai haki.

“Uchaguzi wa Zanzibar hauwezi kutenganishwa kikatiba au kisiasa na uchaguzi mkuu wa Jamhuri ya muungano,” alisema Mbowe.

Mbowe alisema Ukawa hawako tayari kuinajisi Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuruhusu viongozi wasio halali kuingia bungeni.

Aidha, Mbowe alisema walitaka shughuli ya ufunguzi rasmi wa Bunge isitishwe kwa sasa na kuahirishwa hadi hapo Rais halali aliyechaguliwa na wananchi wa Zanzibar, Seif Sharrif Hamad, atakapotangazwa rasmi na kuapishwa.

Naye Mwenyekiti Mwenza, James Mbatia, alisema haijawahi kutokea katika historia ya Bunge tangu nchi hiyo ilipopata uhuru kwa vyombo vya dola kuingia ndani ya bunge na kuwatoa wabunge kwa nguvu.

“Wakati sisi tunatafuta majadiliano mezani ilikumaliza mgogoro huu wenzetu Chama Cha Mapinduzi (CCM), wameamua kutumia majeshi kukandamiza demokrasia,” alisema Mbatia.

Mbatia alisema kuwa hawatakaa kimya bali wataendelea kupigania matakwa ya wananchi hususan kwa upande wa Zanzibara.

“Kuna mambo mengi yanafanywa hovyo na CCM na wapinzani wamekuwa wakivumilia kwa sababu ya kumpenda mama Tanzania lakini hivi sasa wasijaribu kuharibu amani, utulivu na mshikamano uliopo,” alisema.

Mbatia, alisema kwa kawaida mtu anapodhulumiwa haki yake kila mara matokeo yake anachoka kwa hiyo kuna siku ataifuta haki yake hata kwa kusababisha kumwaga damu.

Naye Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu alisema Umoja wa Katiba ya Wanachi (Ukawa ) wamesikitishwa na kitendo cha serikali ya CCM kuonesha wazi jinsi walivyobaka na kuikanyaga demokrasia nchini.

Alitoa kauli hiyo aipokuwa akizungumza na mwandishi wetu muda mfupi baada ya kutoka bungeni baada ya kufukuzwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai baada ya wabunge wa umoja huo kupinga kitendo cha kuruhusiwa kwa Rais wa Zanzibar kuwa sehemu ya Bunge.

Lissu alisema imeonesha wazi kuwa serikali ya CCM ilivyo kuwa ikitumia mabavu ya kuvunja sheria waziwazi sambamba na kuvunja kanuni za bunge jambo ambalo ni hatari kwa afya ya nchi.

Akizungumzia kutoka kwao nje ya ukumbi wa Bunge alisema serikali ya CCM kwa kutumia kiti cha Spika walionekana kupanga mbinu chafu za kuwazima wabunge wa Ukawa ili wasiweze kufikisha hoja zao mbele za wananchi kupitia bunge hilo.

“Unaweza kuona kwamba serikali ya CCM inavyoweza kuvitumia vibaya vyombo vya dola, kwa utaratibu jinsi ulivyo ili kuruhusu watu waingie katika ukumbi wa bunge ni lazima kutengua kanuni ili watu waeze kuingia lakini kutokana na uovyo na ujinga mkubwa wa serikali ya CCM, ambayo haizingatii sheria na katiba imeweza kuleta askari wengi pamoja na majeshi kwa ajili ya kukabiliana na upinzani.

“Jambo kubwa na baya zaidi na la ajabu ni pale ambapo askali waliovaa magwanda ya polisi na jeshi wakiwa na silaha za moto walivyoweza kuingia katika ukumbi wa bunge kwa misingi ya kutaka kukabiliana na wabunge wa upinzani.

“Jambo hapa ni kwamba hata wao wanajua kuwa Dk. Shein siyo rais halali wa Zanziba lakini kwa ubishi wao wanalazimisha kufanya hivyo na kutokana na hali hiyo ndiyo maana serikali imekuwa ikitumia vyombo vya dola kwa ajili ya kuthibiti wabunge wa Upinzania ambao wametumwa na Umma wasitoe mawazo yao,” amesema Lissu.

Mbali na hilo alisema pamoja na kuwa walizuiliwa kuendelea na bunge, kwa ajili ya kuwasilisha hoja zao kwa watanzania lakini watatumia mbinu nyingi za kufikisha ujumbe kwa jamii kwani kwa sasa kuna kila mikakati ya kuhakikisha wanataka kuuzima upinzani.

Akizungumzia kuhusu kanuni za bunge kwa sasa alisema kama ilivyo katiba ya sasa ilivyo na makosa kibao ndivyo na kanuni za bunge zinavyotakiwa kurekebishwa kwani kuna makosa mengi zaidi.

Kwa upande wao wabunge wa Zanzibar walisema ni dhambi kubwa kwa Dk. Ali Mohamed Shein kuenedelea kung’ang’ania kukaa madarakani wakati muda wake umeisha jambo ambalo linaonesha wazi kuwa ni matumizi mabaya ya madaraka na dola yake.

“Inasikisha zaidi kuona jinsi Rais wa Zanzibar alivyokuwa siyo muungwana anajua kabisa kwamba hakushinda uchaguzi, lakini ikumbukwe wakati wa kuvunja baraza la wawakirishi wabunge wa CCM walimkataa Maalim Seif Shariff Hamad kama makamu wa kwanza wa rais asiingie katika bunge.

“Lakini kwa uungwana wa kiongozi huyo aliondoka wala hakuhudhuria kikao hicho lakini jambo la kushangaza huyu Dk. Shein amekomaa sasa inafikia hatua anazomewa bila kuwa na aibu sasa huo ni uongozi gani na anamuongoza nani,” amesema.

“Tunamuuliza Rais Magufuli, ni nani akapeleka vifaru na kuongeza askari wengi katika nchi za Zanzibar na ni kwa sababu gani.

“Kwa sasa hali ya Zanzibar si shwali kwani kila jambo sasa limelala kwani hata watalii hawaji kama ilivyokuwa mwanzo, mbali na hilo kuna hali ya sitofahamu ni kwani nguvu nyingi ya vyombo vya dola inaelekezwa Zanzibar,” alisema mmoja wa wabunge wa Zanzibar.

Maguri Auzwa TP Mazembe Kwa Sh Mil 100

$
0
0
Na Sweetbert Lukonge
STAND United imekubali kumuuza straika wake Elias Maguri kwa TP Mazembe ya DR Congo kwa dau la dola 50,000 ambazo ni zaidi ya Sh milioni 100.
Timu hiyo imetoa kauli hiyo baada ya kuwepo kwa taarifa mbalimbali zinazomhusisha Maguri kujiunga na Yanga na TP Mazembe na sasa ipo tayari kumuachia straika huyo mwenye mabao 10 msimu huu.
Maguri ambaye yupo katika kikosi cha Kilimanjaro Stars kinachoshiriki Kombe la Chalenji huko Ethiopia, amefunga mabao tisa katika Ligi Kuu Bara, pia ana bao moja kwa timu ya taifa alililoifungia Taifa Stars dhidi ya Algeria katika sare ya mabao 2-2 Novemba 14, mwaka huu.
Ofisa Habari wa Stand United, Deo Makomba, ameliambia Championi Jumamosi kuwa, klabu yake imekubali kumuuza Maguri kwa dola 50,000 kwa TP Mzembe au timu nyingine ya nje ya nchi inayomtaka.
“Tupo tayari kumuachia Maguri ajiunge na TP Mazembe kwa dau la dola 50,000, kilichobaki sasa ni kufuatwa kwa taratibu za klabu na klabu ili mchezaji aweze kwenda DR Congo.
“Hii si kwa TP Mazembe pekee, timu yoyote ya nje ya nchi inayomtaka Maguri ijue hilo ndilo dau lake lakini kwa timu ya hapa nchini, inatakiwa kulipa Sh milioni 50 ili tuwaachie Maguri,” alisema Makomba.
Yanga ndiyo klabu pekee ya Tanzania iliyotajwa kumuwania Maguri na hata mchezaji mwenyewe aliwahi kunukuliwa kuwa tayari kuichezea timu hiyo badala ya Simba ambayo aliachana nayo hivi karibuni.
Hata hivyo, Maguri ameliambia gazeti hili: “Nilizungumza na Yanga kuhusu kujiunga nayo lakini sasa nimebadili mawazo na akili yangu yote ipo kwa TP Mazembe, nataka kufika mbali zaidi.
“Hata kama Yanga watakuja na dau kubwa kushinda Mazembe, nitaichagua timu hiyo ya DR Congo.”

Africa’s 50 Richest (Forbes): Dewji ni Namba 21, Aongoza Tanzania

$
0
0
Forbes wametoa orodha ya watu 50 matajiri zaidi barani Afrika.

Nafasi ya kwanza imeendelea kushikiliwa na bilionea wa Nigeria, Aliko Dangote mwenye utajiri wa dola bilioni 16.7.

Mwenyekiti Mtendaji wa METL, Mohammed Dewji amekamata nafasi ya 21 kwenye orodha hiyo akiwa na utajiri wa dola bilioni 1.1. Dewji anaendelea kuwa tajiri namba moja nchini Tanzania.

Rostam Aziz amekamata nafasi ya 25 kwa utajiri wa dola milioni 900 huku Said Salim Bakhresa akikamata nafasi ya 36 kwa kuwa na utajiri wa dola milioni 600.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi Ya Novemba 21, Ikiwemo ya Diamond na Kajala Katika Mahaba Niue

$
0
0

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi Ya Novemba 21, Ikiwemo ya Diamond na Kajala Katika Mahaba Niue

BBA 2014 Winner Idris Sultan Break Up With South African Girlfriend Samantha Jansen

$
0
0

Big Brother Africa Hotshots winner Idris Sultan is arguably one of the hottest men in East Africa.Apart from that he has been very successful even after his win in 2014 at the reality show.His new show is set to start showing in December.

The Tanzanian  has recently revealed that he is a single man after breaking up with his BBA Hotshots flame Samantha Jansen of South Africa.

Speaking during an interview on The playlist show on Times TV in Tanzania,Idris confired that indeed he and Samantha were no longer together.

"It's over,its done me and her" said Idris.

The two had made headlines with their relationship with Samantha travelling to Tanzania to stay with Idris for awhile.

Idris has however been also rumoured to be in a relationship with top Tanzanian actress and foemer beauty queen turned politician Wema Sepetu.

Rais Magufuli Awateka Jokate na Lulu Michael Angalia Kauli Walizotoa Baada ya Hotuba yake


Kauli ya Zitto Kabwe Baada ya Kilichotokea Jana Wabunge wa Ukawa Kutoka nje na yeye Kutokusimama Wakati Dk Shein Anaingia Bungeni

$
0
0
"Simtambui Dkt. Shein kama Rais wa Zanzibar 
Nataka tu kuweka rekodi sawa. Nilimpinga Dkt. Ali Mohamed Shein hadharani na jana bungeni. Alipoingia Shein bungeni sikusimama kama inavyotakiwa. Nilikaa chini kupinga uhalali wake. 
Alipoingia Rais John Magufuli nilisimama na kumpa heshima yake kama Rais na kukaa kumsikiliza. Kuendelea kuzomea wakati Rais halali kaingia Bungeni kuzindua Bunge ili wabunge waanze kazi ni kutokuwa na mikakati sahihi. Ilitosha kumzomea Shein na kukaa chini bila kusimama alipoingia kama tulivyofanya. Wenzangu hawakujua pa kuishia. 
Magufuli anapambana na rushwa. Mimi napambana na rushwa. Namwunga mkono katika vita dhidi ya rushwa. 
Anayempinga Magufuli kwa vyovyote vile anatetea wala rushwa na mafisadi. Anayempinga Magufuli ni yule anayeogopa viwanda na mashamba yaliyobinafsishwa kurudishwa Kwa umma".
-Zitto Z Kabwe

Full Time ya Burundi Vs Zanzibar Heroes CECAFA Challenge 2015 …

$
0
0
Michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika Mashariki na kati maarufu kama CECAFA Senior Challenge Cup yameanza leo November 21 mjini Addis Ababa Ethiopia, ikiwa ni michezo miwili ilikuwa inatarajia kuchezwa leo November 21, timu ya Zanzibar Heroes dhidi ya timu ya taifa ya Burundi ndio zilikuwa timu za kwanza kufungua dimba kabla ya wenyeji Ethiopia watakaocheza dhidi ya Rwanda.

Burundi ambao walikuwa na nyota wao kadhaa akiwemo Didier Kavumbagu anayekipiga katika klabu ya Azam FC ya Tanzania walikuwa wakiutawala mchezo kwa wastani kumiliki mpira kwa asilimia 56 katika kipindi cha kwanza wakati Zanzibar walikuwa na asilimia 44 za umiliki wa mpira kwa dakika zote 45 za kwanza.


Mchezo huo ambao Burundi walikuwa wakifika sana langoni kwa Zanzibar Heroes hadi wanaenda mapumziko walikuwa wanaongoza kwa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na Didier Kavumbagu dakika ya 38. Licha ya kipindi cha pili Zanzibar kutafuta nafasi ya kusawazisha goli hilo haikuwezekana.

Huyu Ndio Mshindi wa Shindano la Urembo la Miss Universe 2015 TZ , Akiwa na Mshindi wa Pili na Watutu Waliopatikana Usiku wa Jana

$
0
0
Usiku wa November 20 2015 ulimwengu wa urembo Tanzania umeandika historia nyingine kubwa na nzuri ambapo mrembo mmoja aliibuka na ushindi wa taji la Miss Universe 2015 !! anahesabu siku chache tu kugusa stage ya Miss Universe duniani !

List ya warembo waliogusa TOP 3 ya Miss Universe 2015 ilikuwa hivi:


Washindi wenyewe kwenye ubora wao, Lilian Loth (mshindi wa pili kushoto), Lorraine Marriott (mshindi wa kwanza katikati) na Willice Donald (mshindi wa tatu kulia)

KIMENUKA..Kinje Afunguka Kwa Mara ya Kwanza Kuhusu Tuhuma Anazozushiwa na Mange Kimambi Kuwa Anajihusisha na Uuzaji wa Madawa ya Kulevya

$
0
0

Kinje Akiwa na Familia yake...
Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Kinje ambaye ni mtoto wa Mwanasiasa Maarufu Tanzania Ameamua Kumjibu Mange Kimambi Ambaye Mara Kwa Mara Amekuwa Akimtuhumu kuwa Anahusika na uuzaji wa Madawa ya Kulevya....

Kinje Ameandika Haya:

"Poor you @mangekimambi_ ,let me tell you something Serikali ya Tanzania itaanza nawewe na hao wanaokutuma ili Upoteze Jamii Maboya, wanaokutuma wengine ni familia yako so @mangekimambi_ unaweza kundangaya watu wachache tu Lakini ukweli ni kwamba Wewe Unatumwa Na wahusika wakuu WA madawa ya kulevya ili Upoteze lengo Lkn Serikali ya awamu ya 5 haidanganyiki na itakunyorosha Wewe Na hao wanaokutuma...Alafu as I told you last time Peleka ushaidi wako kwenye kitengo Cha madawa ya kulevya Tanzanian Na Kama uwezi hapo USA wapi CIA,DEA Na FBI you can give them your evidence Other wise shut the fuck off and leave me Alone..| Kinje

Shilole Atoboa Sababu ya Kuuza Nyumba Yake Aliyokua Anajenga Kimara

$
0
0
Msanii Shilole aliwai kuingia kwenye headlines baada ya ku-post kwenye instagram picha ya nyumba yake ambayo alikua bado anaijenga. Caption ya picha hiyo ilikua inasomeka hivi, “Mungu nisaidie nimalize hii kitu ili watoto wangu wasije kupata tabu”.

Eneo ambalo alilokua anajenga nyumba hiyo ni Kimara jijini Dar es Salaam lakini Shilole amesema kwamba ameuza nyumba hiyo ambayo ilikua bado haijaisha vizuri.

Akiongea na millardayo.com Shilole ametoa sababu za kuuza nyumba hiyo kama hivi, “Nyumba yangu niliyokua naijenga maeneo ya Kimara nimeiuza kwenye hatua iliyofikia kama ilivyokua inaonekana kwenye picha. Sababu ya msingi iliyonifanya kuiuza ni kwamba pale eneo nililokua najenga ni nimegundua kwamba ni njia ya maji. Hivyo basi sitaki kupata tabu msimu wa mvua ukianza maji yakiwa yanapita nje ya nyumba yangu. Pia hakuna tatizo nimeuza nitajenga kwingine mambo ni mazuri”

Picha ya Zitto Kabwe Akipongezwa na Rais Kwa Kitendo cha Kubaki Bungeni...

$
0
0

Zitto kabwe akipongezwa na Rais kwa kitendo cha kubaki bungeni...Iwekee Maneno hii Picha ...

Hapa Kazi Tu Inaendelea..Vitanda na Magodoro Yamwagwa Muhimbili Hospital...Ni Baada ya Rais Magufuli Kusema Haya

$
0
0
Jumla ya vitanda 500 na magodoro 500 vimeshushwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jana Baada ya Rais Magufuli Kuamuru hela za kufanyia Sherehe yake zaidi ya mil 200 zitumike kununulia vitanda vya wagonjwa.
.
kuna watu wengine bhana kila kitu kupinga hata Yale yanayofanyika na tunaona yanastahili kupongezwa. Nani angeweza kuliko Tinga tinga


Magufuli Awakuna Wanachama 115 wa CHADEMA na CUF Wilayani Handeni Mkoani Tanga Waamua Kufanya Maamuzi Magumu

$
0
0
Wanachama 115 wa Chadema na CUF wilayani Handeni Mkoa wa Tanga, wamejiunga na CCM kwa madai kuwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umeshindwa kuelewana hadi kipindi cha Uchaguzi Mkuu.

Wakirudisha kadi na bendera juzi mbele ya Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Tanga, Mathew Mganga walisema walikuwa na nia ya kweli ya kuunga mkono Ukawa unaoundwa na vyama vyao lakini kutokana na kutokuwa na msimamo wameamua kuhama.

Katibu wa Chadema Kata ya Kwenjugo, Rajabu Vuli, alisema alifanya hamasa kuhakikisha chama chao kinapata ushindi lakini viongozi wa wilaya hawakuonyesha ushirikiano na watu wa chini.

Mwingine aliyehama ni Katibu wa Vijana wa Chadema wa kata hiyo, Ramadhani Dawa.

Dawa alisema ahadi zisizotimia za viongozi ikiwamo kuwadharau viongozi wa kata ndiyo sababu kubwa iliyosababisha kuhamia CCM.

Alisema kama wasingedharauliwa na mawazo yao kufanyiwa kazi wangebaki Chadema na kukiendeleza chama hicho ambacho amedai kimekuwa na mvuto mkubwa na Watanzania ambao walitaka kuleta mabadiliko ya kweli.

Mganga alisema wamepokea wanachama hao bila wasiwasi kwani tayari hizo ni kura.

Hivi sasa chama hicho kipo kwenye kampeni za kumuombea kura mgombea ubunge Jimbo la Handeni Mjini (CCM), Omari Kigoda.

Alisema wameridhika na uamuzi wa wanachama hao wapya kwa kuona CCM inajali ngazi zote za uongozi kuanzia wa chini hadi juu.

Alisema baada ya uchaguzi huo mdogo, watahakikisha yale walioahidi kwa wananchi yanafanyiwa kazi haraka hasa yanayowagusa moja kwa moja ikiwamo elimu, afya, maji na masuala ya miundombinu.

Mgombea ubunge huyo, aliahidi endapo atapewa ridhaa ya kuongoza jimbo hilo, atawaleta maendeleo.

Waliofukiwa na Kifusi Mgodini kwa siku 41 na kuokolewa Watakiwa Kupakwa Vinyesi ili Kuwaondolea Mikosi

$
0
0
Wazee wa kimila wa makabila ya Wakurya na Waluo wamesema watu watano waliookolewa kutoka kwenye machimbo ya Nyangalata, Kahama ambao waliwekewa matanga kabla ya kuibuka wanatakiwa kufanyiwa mambo ya kimila, vinginevyo watakufa kiajabu.

Mmoja wa wazee hao, Ghati Ryoba (61) wa Mtaa wa Mwangaza, Nyamisangura – Tarime amesema: “Mtu akidaiwa kuwa amekufa lakini baadaye akaonekana, wazee wa ukoo au wa mila humfanyia matambiko kama njia ya kuondoa mikosi kwake na kwa familia yake. Wanachukua kondoo mweusi wanamchinja kisha wanamtambikia (bharamsendola).

“Kisha wanachukua kinyesi cha kondoo (ubhuhu ghwaling’ondi) na mti mmoja unaitwa (richirya) kisha kile kinyesi kinarushwarushwa ndani ya nyumba yake na mji mzima kama kuna nyumba nyingine halafu wanachukua kile kinyesi cha kondoo na kumpaka kwenye mikono na anashikana mikono na watu.”

Mzee huyo wa kimila ameongeza kusema kuwa baada ya hapo atanawa mikono kabla ya kuruhusiwa kula na kujumuika na watu.

Amesema baada ya hapo atanyolewa kisha atakwenda kuoga “... Wengine hupeleka nywele kuzizindika kwenye mlima ambako watu hawalimi.”

Kuhusu Waluo, mzee Peter Odello wa Kitembe, Rorya amesema: “Kama inatokea mtu anadaiwa kufa na watu wakafanya matanga lakini baadaye akaonekana, lazima arudi kijijini wamfanyie matambiko.”

Amesema akirudi, wazee watachinja ng’ombe na watu watakaa tena kama walivyokaa kwenye matanga kwa siku mbili au tatu watu wakila kisha kupewa dawa inayoitwa manyasi.

Agizo la Rais Magufuli kuhusu kununuliwa vitanda hospitali ya Muhimbili latekelezwa

$
0
0
Agizo alilolitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kutaka fedha zilizochangwa na wadau mbalimbali kwa ajili ya kugharamia hafla ya wabunge zipelekwe Katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kununulia vitanda na magodoro ya wagonjwa wanaolala chini limetekelezwa.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema fedha hizo zimefanikisha kupatikana vitanda 300 vya wagonjwa pamoja na magodoro yake, shuka 600, Baiskeli za kubebea wagonjwa na vifaa vingine na kwamba hivyo vyote tayari vimepelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Balozi Sefue ameuagiza uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha vitanda vyote vinafungwa  jumapili na kwamba atakwenda kuvikagua siku ya jumatatu vikiwa tayari vinatumiwa na wagonjwa waliokua wanakosa vitanda vya kulalia na kulazimika kulala chini.

Wadau mbalimbali walichanga fedha kiasi cha shilingi milioni 225 kwa ajili ya kugharamia hafla ya wabunge baada ya uzinduzi rasmi wa bunge la 11 lakini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli aliagiza fedha hizo zitumiwe kwa kiasi kidogo kisichozidi shilingi milioni 15 na nyingine zipelekwe hospitali ya Muhimbili kutatua tatizo la uhaba wa vitanda.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano IKULU,
Novemba 21, 2015.

Lol.......Check Out Obama On 4 Different Hairstyles !

$
0
0

Lol.......Check Out Obama On 4 Different Hairstyles !

Heartless! See What This Kenyan Guy Did After Having S£X with a Single Mother.

$
0
0

Some guys are just heartless, how can you have S3X with a single mother and instead of keeping it private, you go ahead and tell the whole world that you tasted her honey jar?

A guy living in Germany has been having s3x with Kenyan single mothers who have left their comfort zones to go and hustle for their families.

He claims that most of these single mothers are lonely and thirsty for s3x. He has been using them like tissue papers and shamelessly sharing his escapades with the online community.

See what he posted.


Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images