Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live

Mtangazaji Diva wa Clouds FM Acharuka Baada ya Tetesi Kuwa Anatoka Kimapenzi na Mwanamuziki Ali Kiba

$
0
0
Mtangazaji wa Clouds FM, Diva the Bawse amekanusha tetesi zilizosambazwa na gazeti moja la udaku kuwa ana uhusiano na Alikiba.

Kupitia Instagram, Diva ameandika:

Kuna gazeti Nimetumiwa limeandika nina Mahusiano na Ali Kiba. bila aibu wametumia Picha tumepiga studio. really? Since when ? Ali he is My good friend. he is sucha great heart and soul sina mahusiano nae sijawahi Wallahi kuwa na Mahusiano nae hata mara 1. na focus sana na Kazi yangu nina Plan zangu kibao sitaki niandikwe mambo ya Mahusiano. nafanya interviews hizo zina trend africa nzima na nje ya Africa mbona hamuandiki? nina Diva Beautyy Product pia straight from the UK . mbona hamuandiki? come on now.. My main focus is to get on my grind and pursue my career. y’all leave me alone. S/O to @jacob_mbuya and @kyarwendafrj for always Being there .. well about Gk pia mmeandika right? Gk is sucha great heart. a very Special man. amma cherish him forever .naomba mniandike kuhusu Interview zangu za Levels baby levels maana zinakiki hatarious. das matter to me sawa eeh? ntawashukuru sana. #busywitmashit

Washitakiwa Watatu wa TRA Wanaohusika na Utoroshaji Makontena Wapewa Dhamana.......Yupo Masamaki na Wenzake Wawili

$
0
0
Mahakama kuu ya Tanzania imeridhia dhamana kwa washitakiwa watatu wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA wanaokabiliwa na mashitaka ya kutoa makontena 329 bandarini bila kulipiwa kodi na kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 12.7.

Maamuzi hayo ya mahakama kuu ya Tanzania yametokana na ombi lililowakilishwa mahakamani hapo na washtakiwa watatu wakiongozwa aliyekuwa Kamishina wa Forodha wa TRA Bw Tiagi Masamaki.

Jaji wa mahakama hiyo Bi Wilfrida Koroso, alisema dhamana kwa washitakiwa hao watatu iko wazi kama watatimiza masharti sita yakiwemo ya kulipa hundi ya shilingi bilioni 2.6 kila mmoja huku pia wakitakiwa kuwasilisha hati zao za kusafiri na kutakiwa kuwa na wadhamini watakaokuwa na uwezo wa kusaini hundi ya shilingi milioni 20 kila mmoja.

Mshitakiwa namba moja katika kesi ya kuhujumu uchumi, aliyekuwa Naibu Kamishna wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), Tiagi Masamaki (Kulia) akiwa na wenzake aliyekuwa Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Habibu Mponezya na Bulton Mponezya wakiwa katika Mahakama Kuu Tanzania jijini Dar es Salaam jana wakisomewa shtaka linalowakikabili  la makosa ya jinai na uhujumu uchumi.

Nafasi za Kazi

Mawakala wa Forodha Waibua Mapya Ya Utoroshaji Wa Kontena Bandarini

$
0
0
CHAMA cha Mawakala wa Forodha nchini (TAFFA) kimesema kuwa wizi wa kontena bandari ya Dar es Salaam na kusababisha serikali kukosa mapato ni tatizo la muda mrefu ambalo ni limekuwa likisababishwa na watumishi wa bandari.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Rais wa TAFFA, Steven Ngatunga alisema tatizo lilojitokeza ya uondoshaji wa kontena 329 katika bandari Kavu ya Azam ilitokana na baadhi ya watumishi wa baadhi ya benki na Bandari kuingilia taarifa katika mfumo na kusababisha serikali kukosa mapato.

Ngatunga alisema kuwa tatizo la serikali kukosa mapato katika bandari ya Dar es Salaam walishagundua lakini serikali ilishindwa kuchukua hatua mpaka serikali ya awamu ya tano kugundua hilo na hatua zimechukuliwa kwa wale waliohusika.

Alisema TAFFA itatoa ushirikiano kwa kile ambacho wanakiona katika bandari ya Dar es Salaam juu ya watu wanaosababisha serikali kukosa mapato kwa maslahi yao binafsi.

Aidha alisema kuwa kuna kampuni zilionekana kuwa zipo kwa ajili ya kukwepa kodi ya serikali ambazo chama kiliona na kupeleka malalamiko ambayo mwisho wa siku kukawepo urasimu wa kukutana viongozi ambao wanaweza kushughilikia hilo.

Alisema baadhi ya mawakala walilipia kontena lakini wanaambiwa malipo hayakufanyika huku wakiwa na kumbukumbu za malipo na kusababisha kutilia shaka juu ya uadilifu wa watumishi wa benki pamoja na bandari.

TAFFA imesema haiko tayari kwenda na mawakala ambao wanaharibu taaluma hiyo na kusababishia serikali kukosa mapato ambayo ndio ya kufanyia maendeleo nchini.

Alisema kuwa kuna kampuni 73 zimefungwa wakati hawahusiki katika  uondoshaji wa kontena katika bandari na bandari kavu kutokana na kampuni hizo kuwa kulipia kontena zinazodaiwa kukwepa kodi.

Nafasi za Ajira

TFDA Yateketeza Shehena ya Vipodozi

$
0
0
Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Kanda ya Kati imetekeza shehena ya vipodozi vyenye viambata vya sumu vya thamani ya Sh49 milioni.

Vipodozi hivyo tani mbili na nusu, viliteketezwa mbele ya maofisa polisi, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), usalama wa Taifa na wamiliki wake baada ya kukamatwa vikisafirishwa kwa njia za panya hivi karibuni.

Mkaguzi wa Chakula na Dawa wa TFDA, Dk Endrybet Mbekenga alisema jana kuwa kazi hiyo itakuwa mwendelezo wa uteketezaji wa bidhaa nyingine zenye kemikali ambazo zina madhara kwa binadamu.

Alisema shehena hiyo ilikutwa ikishushwa kutoka kwenye lori la mafuta.

Dk Mbekenga aliwataka wafanyabiashara kuacha kuendelea kuingiza bidhaa hizo nchini zilizopigwa marufuku na Serikali kwa sababu zina sumu.

Alisema vipodozi hivyo athari zake ni kubwa kwa matumizi ya binadamu, ikiwamo wanawake kuota ndevu, kupata saratani ya ngozi na kuathiri figo.

Alionya kuwa wafanyabiashara watakaokiuka kanuni za mamlaka hiyo, watachukuliwa za kisheria.

Ofisa wa Forodha wa TRA, Mohamed Mnonda alisema watashirikiana na polisi na TFDA kuzuia bidhaa zote zinazoingizwa nchini kinyemela kwa kukwepa kodi.

Kwa mujibu wa Sheria ya Kodi, ni makosa kwa gari linalosafirisha bidhaa kwenda nje ya nchi kurudi nchini na bidhaa nyingine kutoka nchi iliyopelekewa mzigo.

Nafasi za Ajira

Wema Sepetu Adata na Wimbo Mpya wa Diamond Platnumz (Video)

$
0
0
Ameachana na Diamond lakini Wema Sepetu bado ni shabiki mkubwa wa nyimbo za ex wako huyo.

Malkia huyo wa filamu, amedhihirisha kuwa hana kinyongo na Diamond baada ya kuonekana akiimba wimbo mpya wa msanii huyo, Utanipenda!

Muigizaji huyo aliwahi kunukuliwa akisema ingawa ameachana na Diamond bado ataendelea kupenda muziki wake.

Video yake inayomuonesha akiuimba wimbo huu ilisambaa kutoka kwenye mtandao wa Snapchat.

Angalia Video Hapa Chini:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Disemba 16, Ikiwemo ya Magufuli Amekuwa Mwiba kwa JK

$
0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Disemba 16, Ikiwemo ya Magufuli Amekuwa Mwiba kwa JK

MBOWE Afunguka Kuhusu Kasi ya Magufuli..Adai Ameanza Vizuri Kutekeleza Hoja zilizokuwa Zikipigiwa Kilele na Chadema Bungeni

$
0
0
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amezungumzia kasi aliyoanza nayo rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli pamoja na baraza lake la mawaziri.

Akizungumza jana na mwandishi wa habari wa Azam TV, Mbowe alisema kuwa rais Magufuli ameanza vizuri kiutendaji na kwamba ameanza kuzifanyia kazi hoja zilizokuwa zikihubiriwa na Chadema ndani na nje ya Bunge.

Hoja ya kubana matumizi ya serikali, hoja ya kupunguza sherehe za kitaifa, hoja ya kupunguza safari za nchi za nje kwa viongozi wetu, hoja ya kupunguza watumishi wa umma ambao hawana umuhimu, hoja ya kuwa na serikali ndogo. Haya mambo tulizungumza siku zote na hawa hawa wa Chama cha Mapinduzi ndio waliokuwa wanayapinga haya,” alisema Mbowe.

Mbowe alieleza kuwa dhana ya upinzani sio kupinga kila kitu kinachofanywa na serikali hivyo chama chake hakitakuwa tayari kupinga mambo mema yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano kama baadhi ya watu wanavyotarajia, bali kitajikita katika kujadili na kuibua hoja za msingi.

Kuwa mpinzani sio kupinga kila jambo linalofanyika hata kama likiwa jema. Sasa sisi kama kambi rasmi ya upinzani bungeni na hata nje ya bunge ni wajibu wetu katika wakati wote ule kuhakikisha tunaisimamia serikali ili anachokisema rais kweli kitekelezwe kwa vitendo na isiwe hoja ya rais pekee,”alisema.

Hata hivyo, Mbowe alikosoa uteuzi wa baadhi ya mawaziri katika baraza la serikali ya awamu ya tano hususan Dk. Harison Mwakyembe ambaye wizara ya Uchukuzi aliyokua akiiongoza awali imekumbwa na sakata la upotevu wa makontena bandarini na Profesa Sospeter Muhongo ambaye amerudishwa katika wizara ya Nishati na Madini baada ya kujiuzulu katika nafasi hiyo wakati wa serikali ya awamu ya nne kufuatia sakata la Escrow.

Chama Changu CHADEMA, Kwa Mwendo Huu Tutachokwa

$
0
0
Toka jana nimefutilia mijadala na kauli za Mnyika kuhusu kuhamishwa kwa TAMISEMI na leo tena kuibua inshu ya ESCROW.

Pia nimeendelea kuona matamko yanayofuatana tu kutoka kwa Tumaini Makene.Chama changu CHADEMA, staili tunayoitumia saiv tutachokwa sana mapema,tuache siasa za matukio tufuate siasa za hoja. Lipumba naye leo katupiga dongo, saiv tumekazania mambo ya Makonda...hayatatusaidia hayo, tunaomba tuendelee sera zetu za kuibua ufisadi.

Nashukuru Mnyika amesema ataibua hoja ya Escrow,ni vizuri sana ila naomba pia na Richmond irudishwe, Kubenea mpambanaji wangu naomba upeleke hoja binafsi kuhusu Richmond kamanda ili wahusika wawajibishwe..

Asanteni..

Nafasi za Ajira
Bofya www.ajirayako.com

Tanesco Bado Mnafungulia Maji Usiku Katika Mabwawa Yenu? Mvua ni Nyingi Mgao Ukome Basi!

$
0
0
Kuna mkuu mmoja aliwatuhumu Tanesco kwamba huwa wanafungulia maji usiku ili mabwawa yaonekane hayana maji, Mgao uanze wapige dili za mafuta na Jenereta,Mwaka huu mvua ni nyingi sana, hatutarajii muendelee kutukatia umeme kama mnavyofanya katika mikoa ya Arusha na Mwanza...natoa wito kama kuna wanaofungulia maji bado wakamatwe.....

Nafasi za Ajira

LEMUTUZ Afunguka Tena Kuhusu Dr Mwaka...Adai Anaamini Kuwa Dr Mwaka Hajavunja Sheria yoyote....

$
0
0

Lemutuz Ameandika haya Kwenye Ukurasa wake wa Instagram:

Ok niliahidi kusema ukweli kama ulivyo on this ishu bila longo longo na mpaka nione mwisho wake:- ......ni kwamba KWANZA Hospitali zote za Dr. Mwaka @dr.mwaka leo zilikuwa zimefunguliwa zinaendelea na kazi kama kawaida na PILI:- Alikwenda Wizarani kama alivyoamriwa na kinachosubiriwa ni majibu ya Wizara ili wote tujue ukweli upo wapi.....ingawa nilitegemea by now kwa tuhuma nilizozisikia jana akirushiwa Dr. Mwaka majibu yangekuwa rahisi sana kutolewa na Wizara lakini sina haraka nitaendelea kusubiri....ninasema hivi MNYONGE MNYONGENI .....wote tunapenda HAKI na UKWELI.....binafsi I have worked kumtangazia matangazo Dr. Mwaka nikiamini 100% in nilichokuwa namtangazia na in the process he became a Friend ni mtu mstaarabu sana na hata wake zake 2 ninawafahamu ni wastaarabu sana....mengi yametokea jana ambayo KISHERIA HAYAKO SAWA SANA lakini then tunaangalia wahusika kwa vile wengine tunawafahamu tunaishia kuyaacha hoping watakuwa wamejifunza kwamba FACTS sio mchezo na wala sio lelemama mtu anaweza akakurupuka na maneno mengi sana lakini in the end inakuja SHERIA na FACTS huwa wengi wanakwama...now ninasema nitaendelea kufuatilia mpaka mwisho wa hii ishu cause imetugusa wengi sana na ni kwa nia njema ninachotaka ni kuona HAKI INATENDEKA mimi sio mtu wa kukurupuka Hospitali ya Dr. Mwaka ni PRIVATE sio ya Serikali na besides ni Hospitali inayoongozwa na SHERIA za DAWA ZA ASILI kuna tofauti kubwa sana na Hospitali kama Muhimbili so guys kama nilivyoahidi ninaendelea kusubiri na nitasema ukweli kila siku mpaka tufikie kwenye THE TRUTH OF THIS MATTER! ...BADO NASISITIZA DR. MWAKA NI RAFIKI YANGU NA SIAMINI KWAMBA AMEVUNJA SHERIA YOYOTE ILE YA JAMHURI KWA KAZI ZAKE ZA KILA SIKU MPAKA NAIBU WAZIRI ATAKAPONIHAKIKISHIA TOFAUTI! - le Mutuz

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu Afanya Ziara ya Kushtukiza Hospitali ya Muhimbili Leo na Kukuta Mashine za CT Scan na MRI Zimeharibika Tena

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Ummy Mwalimu amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili leo na kukuta mashine za CT Scan na MRI hazifanyi kazi.

Katika ziara hiyo aliyoifanya asubuhi ya leo, alikutana na mzee wa miaka 90 ambaye alikuwa akisubiri huduma hiyo tangu jana.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Wa Hospitali hiyo, Lawrence Museru, mashine hizo ziliharibika tangu juzi na hivyo huduma zilisimama tangu jana asubuhi.

Tatizo kubwa katika machine ya CT Scan picha hazisomeki vizuri na MRI imeharibika spea ambazo kwa mujibu wa uongozi wa hospitali hiyo, matengenezo yanaanza leo.

Hata hivyo, Mwalimu ameagiza uongozi wa hospitali hiyo ya rufaa kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha kuwa mashine hizi zinarudi katika hali yake ya kawaida.

Mashine hizo zimeendelea kuwa changamoto kwa hospitali hiyo licha ya Rais John Magufuli kufanya ziara ya kushtukiza na kukuta hali kama ya leo.

Rais John Magufuli Amfuta Kazi Mkurugenzi wa Takururu Dr Edward Hosea..Sababu Hizi Hapa

$
0
0

Rais Magufuli leo ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Dr. Edward Hoseah kwa kutoridhishwa na utendaji wake. Nafasi yake itakaimiwa na Valentino Mlowola

Pia amewasimamisha kazi watumishi wanne wa TAKUKURU kwa kukiuka agizo lake la kutosafiri nje ya nchi, awataka watumishi wote wa Umma kutii agizo lake

Navykenzo Wamtambulisha Msanii Mpya wa The Industry...

$
0
0
Wanamziki Nahreel na Aika wa Navykenzo Wamemtambulisha rasmi msanii mpya ambae atakuwa chini ya lebel yao inayojulikana The Industry, Msanii huyu mpya ni Rapper wa Kike anayejulikana kama Rosa Ree....

Navykenzo Wameandika Kwenye Page yao hivi:

Navykenzoofficial 
Stoop!!! Anaitwa @rosa_ree ni rapper anaeletwa kwenu na mtayarishaji mahili na mmiliki wa studio @theindustrytz michael jordan wa beats @nahreel tunaomba mumpokee kwa mikono miwili kwasababu anajua pia kaeni mkao wa kula hivi karibuni mtaanza kumsikia masikioni mwenu.....
#AboveInAMinute #GameGame #GoodMusicFamily



Nyimbo 5 za Diamond zilizopo Store Zitaendelea Kumuweka Kileleni kwa Miaka 10 – Asema Mpiga Picha Wake

$
0
0
Diamond Platnumz ni msanii ambaye (angalau kwa sasa) haoneshi dalili za kushuka kimuziki hivi karibuni. Tunayo mifano mingi ya wasanii wa Bongo ambao waliwahi kufanya vizuri sana na baadaye kupotea kabisa kwenye ramani ya muziki.

Diamond ambaye ameachia ngoma mpya ‘Utanipenda’ wiki iliyopita ambayo imekuwa gumzo kwa watu wa kila rika, ana akiba ya hits na collabo za maana, ambazo kwa mujibu wa mpiga picha wake zinampa uhakika wa kuendelea kukaa kileleni kwa miaka mingine kumi ijayo.

Japo zipo collabo kubwa za kimataifa alizoisha fanya, ameamua kufunga mwaka kwa kuachia wimbo mwingine kabisa ambao hakuna aliyefahamu kama upo wala utafanya vizuri, hii inathibitisha silaha zilizosalia kwenye ‘benki’ yake ya nyimbo huenda yakawa ni mabomu makubwa zaidi.

Collabo zinazosubiriwa kwa hamu ni pamoja na ile ya Diamond na Ne-yo, Diamond na P-Square, Diamond na Usher na zingine.

Rais Magufuli: Kwa Mara ya Kwanza Serikali Inakusanya Takribani Trilioni 1.3 Kwa Mwezi

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli amesema kwa mara ya kwanza Serikali itakusanya takribani trilioni 1.3 kwa mwezi.

Pia amewahakikishia watanzania kuwa ahadi yake ya kutoa elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne ni lazima itekelezwe.

Amempongeza Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kazi nzuri ya ukusanyaji wa kodi.

Mama Diamond, Wolper Wafunika Kwenye Video ya Je Utanipenda?

$
0
0
Kuna msemo usemao “experience is the best teacher”, msemo huu umekamilika kupitia mama mzazi wa msanii Diamond Platnums , baada ya kuigiza kama mama ambaye ana maisha magumu kupitiliza,huku akiwa ameuvaa uhusika vilivyo kupitia video mpya ya msanii huyo ambaye ni mwanae wa kumzaa huitwao, je utanipenda.
DIAMOND WOLPER356

Mama diamond, ni kati ya watu wachache waliotumika kwenye video hiyo na kuifanya ionekane kuwa na mvuto wa kipekee na kubeba hisia za mamilioni ya watanzania kwa uchezaji wa hali ya juu alioonyesha kwenye video hiyo.

Mbali na mama diamond, msanii wolper nae anatajwa kuhusika kwa namna moja au nyingine kuifanya video hiyo kuwa na mvuto wa aina yake kutokana na uchezaji wake wa nyodo na dharau,hulka iliyomvaa vilivyo na kuitendea haki.
mama diamond34

Mashabiki wengi waliyoiona video hiyo wamempongeza sana mama diamond kwa kuvaa uhusika, na kumtabiria kufanya vyema kwenye sekta ya uigizaji kama akiamua kuingia huko.

diamond245
Warumi-JF

Diamond Awakera Baadhi ya Mashabiki kwa Video Hii Yenye Ujumbe wa Utata!

$
0
0
Diamond na Zari ni mtu na mpenzi wake na tayari wana mtoto mmoja so wakikutana kwenye chumba kwenye hoteli ya kifahari huko Kampala, Uganda unajua nini kitatokea sio?

Yes, kitakachotokea ni kile mtu na mpenzi wake wakikutana kitandani hufanya – they make love!

Lakini Diamond amewakera baadhi ya mashabiki wake baada ya kupost video hiyo juu na kuandika: Jus love my Uganda’s Room….Can’t wait for the Dirty game with mama tee here lol!

Tembelea kwenye ukurasa wake wa Instagram ujisomee comments za kukinzana!

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Akaidi Agizo la Rais Magufuli....... Aenda Nairobi, Kenya Kwa Fedha za Serikali Bila Kibali Cha Ikulu

$
0
0
MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Juma Assad, amekiuka agizo la Rais Dk. John Magufuli, baada kusafiri nje ya nchi bila kibali cha Ikulu.

Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania, CAG aliondoka nchini Jumamosi (Desemba 12, 2015) kwenda jijini Nairobi, Kenya na kurejea nchini Jumanne wiki hii.

Taarifa hizo, zimesema CAG alikwenda kutoa mhadhara katika Chuo Kikuu cha Nairobi, kazi ambayo haina uhusiano na ofisi yake, lakini alilipiwa gharama zote na ofisi yake.

“Bosi wetu aliondoka kwenda Nairobi Jumamosi iliyopita na kurejea Jumanne, alikwenda kutoa mhadhara katika Chuo Kikuu cha Nairobi bila kibali cha Ikulu, alipaswa kupata kibali kwa sababu ofisi yake ndio ililipa gharama zote.

“Jumla ya gharama zinafika Sh milioni 15, ambazo ni pamoja na posho, tiketi ya ndege, hoteli na gharama nyinginezo,” kilisema chanzo cha gazeti hilo.

Alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusu safari hiyo, Profesa Assad hakuthibitisha wala kukanusha taarifa hizo, zaidi ya  kutishia kwenda mahakamani.

“Wewe si umesema umepata taarifa kutoka vyanzo vyako na umenipigia ‘for validation’, sasa mimi nakwambia hizo taarifa si za kweli na mkiandika tutachukua hatua,” alijibu CAG.

Baada ya muda, Profesa Assad alipiga simu kwa  mhariri akimtaka afike ofisini kwake akachukue nyaraka za kuthibitisha kuruhusiwa na kusafiri nje ya nchi na ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.

Kutokana na mhariri huyo kuwa nje ya Dar es Salaam, alimtuma  mwandishi mwingine kwenda katika ofisi ya CAG ili kuchukua nyaraka hizo. Mwandishi alipofika, CAG alikataa kumpa wala kumwonesha nyaraka hizo.

Juhudi za kumpata Balozi Sefue kuzungumzia suala hilo hazikuzaa matunda. Baada ya kupigiwa muda mrefu aliandika ujumbe mfupi wa simu ukisema. “Nimebanwa na majukumu siwezi kupokea simu yako,” ulisomeka ujumbe huo.

Tukio hilo la CAG limekuja siku mbili baada ya Rais Dk. John Magufuli kuagiza kusimamishwa kazi kwa watumishi wanne wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa kosa la kusafiri nje ya nchi bila kibali cha Ikulu.

Watumishi wa taasisi hiyo waliosimamishwa kazi ni Ekwabi Mujungu (Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu), Doreen Kapwani, Rukia Nikitas na Mary Mosha.

Profesa Assad aliteuliwa kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Novemba 5, 2014.

Kabla ya uteuzi wake, alikuwa Profesa Mshiriki, Idara ya Uhasibu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na alichukua nafasi ya Ludovick Utouh ambaye alistaafu kwa mujibu wa sheria.

Credit: Mtanzania

Nafasi za Ajira

Ziara ya Lowassa Nchi Nzima 'Yaota Mbawa' Ghafla......CHADEMA Watoa Ufafanuzi

$
0
0

Siku moja baada ya kuahirishwa ziara ya aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, chama hicho kimesema hakilitambui zuio la kufanya maandamano na mikutano ya kisiasa lililowahi kutolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali (IGP) Ernest Mangu mwezi uliopita.

Kauli ya Chadema ilitolewa jana na Ofisa Habari wa chama hicho, Tumaini Makene, baada ya kuulizwa juu ya kuwapo taarifa kuwa wameshindwa kuendelea na ziara ya Lowassa kutokana na zuio hilo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, baada ya kuahirishwa mkutano na waandishi wa habari, Makene alisema katazo hilo la mikutano ya hadhara linaendelea.

“Hatulitambui tamko la IGP, sisi tuliahirisha kutokana na kutingwa na shughuli za uchaguzi mdogo, hivyo tukimaliza kushughulikia masuala hayo ya uchaguzi, tutarudi kuendelea na ziara kama tulivyopanga nchi nzima. Hata kama IGP kakataza, mbona CCM wanafanya mikutano ya hadhara?” alisema Makene.

Akizungumzia sababu za kuahirisha mkutano ambao chama hicho kiliuitisha jana na kusababisha waandishi wa habari kusubiri kwa zaidi ya saa tatu, Makene alisema kuna masuala ya msingi ambayo yalijitokeza katika suala la umeya wa Jiji la Dar Salaam ambalo ndilo lilikuwa ajenda.

“Tumeahirisha kwa sababu kuna figisufigisu tumefanyiwa kwenye umeya, hivyo tunazifanyia kazi,” alisema Makene.

Alisema lengo la kuita waandishi wa habari ilikuwa ni kutangaza jina la mgombea wa nafasi hiyo ya umeya wa Jiji la Dar es Salaam.

Mkutano wa viongozi hao ulikuwa ukiendelea ndani ya ofisi za chama hicho, huku kila mara baadhi ya viongozi wakitoka na kutoa matumaini kwa waandishi kuwa mkutano wao utaanza punde.

Mwezi uliopita, Jeshi la Polisi kupitia msemaji wake Advera Bulimba, lilipiga marufuku maandamano na mikutano kutokana na kudai kuwa tathimini iliyofanyika ilionyesha bado kuna mihemuko ya kisiasa ambayo itasababisha uvunjifu wa amani.

Tazama Picha Zikionyesha Unyama Unaofanyika Nchini Burundi, Watu Wanauawa Kama Wanyama

$
0
0
Umoja wa Afrika(AU) umeahidi kuhakikisha mauaji ya kimbari hayatokei Burundi. Wasema kuna uwezekano wa vita ya wenyewe kwa wenyewe.
Kuanzia mwezi Aprili mwaka huu, watu takribani 400 wamepoteza maisha nchini Burundi kutokana na vurugu zinazoendelea
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live




Latest Images