Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live

Mlinzi wa Mfalme wa Qatar Atiwa Mbaroni Moshi Kwa Tuhuma za Kusafirisha Fuvu la Twiga

$
0
0
Kikosi kazi maalumu kilichoundwa na Jeshi la Polisi kupambana na ujangili, kimemtia mbaroni mlinzi wa mfalme wa Qatar, kwa tuhuma za kusafirisha fuvu la twiga kwenda Uarabuni.

Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Fulgence Ngonyani jana alithibitisha kukamatwa kwa mlinzi huyo wa mfalme na kwamba utaratibu wa kumfikisha mahakamani ulikuwa ukifanyika.

“Ni kweli tuna mtu kama huyo tulimkamata pale (Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro) Kia, akapelekwa Arusha lakini amerudishwa Moshi na mchakato wa kumfikisha mahakamani hapa Moshi unaendelea,” alisema Ngonyani.

Habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi, Idara ya Uhamiaji na Idara ya Wanyamapori zimemtaja mlinzi huyo kuwa ni Jasim Mbarakke Alhkubaisi (43).

Mlinzi huyo amekamatwa wakati mtuhumiwa muhimu aliyepatikana na hatia ya kusafirisha wanyama hao wakiwamo twiga wanne kwenda jijini Doha, Qatar, Kamran Ahmed akiwa hajapatikana licha ya kushtakiwa na kuhukumiwa kifungo baada ya kupatikana na hatia.

Mlinzi huyo alikamatwa Kia, ambako Novemba 26, 2010 walipitishwa wanyamapori 152, wakiwamo twiga.

Taarifa zilizopatikana jana mjini Arusha na Kia, zilidokeza kuwa mlinzi huyo wa Mfalme wa Qatar alikamatwa na kikosi kazi hicho Desemba 18.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, mtuhumiwa huyo alikutwa akiwa na fuvu la twiga, ambalo anatuhumiwa kuwa alitaka kulisafirisha kwenda Qatar kwa kutumia ndege ya Qatar Airways ya nchi hiyo.

“Hii issue (suala) ni nyeti. Kuna maofisa wa ubalozi wa Qatar walikuja hapa Arusha juzi na jana wakijaribu kufanya kila njia asishitakiwe lakini imeshindikana,” alidokeza afisa mmoja wa Uhamiaji.

Taarifa nyingine za uhakika zilisema kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa amelazwa katika hospitali moja jijini Arusha na polisi inaangalia uwezekano wa kulipeleka shtaka lake mahakamani ili asomewe shauri lake akiwa hospitalini.

Kukamatwa kwa mlinzi huyo, kumekuja wiki moja tangu Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, limtie mbaroni raia wa Vietnam, Hoang Nghia Trung (49), akiwa na kucha 261 na meno 60 ya simba.

Kamanda Ngonyani, alikaririwa akisema raia huyo wa Vietnam alikamatwa Desemba 14 saa 10 alasiri kwenye uwanja huo wa Kia.

Kwa mujibu wa Kamanda Ngonyani, mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya polisi wa uwanjani hapo kumtilia shaka na alipopekuliwa alikutwa na nyara hizo za Serikali.

Taarifa hizo zinadai kuwa wakati akikamatwa, kulitokea ubishani baada ya mlinzi huyo kujitetea kuwa alilichukua fuvu hilo kwa ajili ya utafiti, lakini akashindwa kufafanua ni utafiti gani.

Kwa mujibu wa vyanzo, mlinzi huyo alikuwa na hati mbili za kusafiria, moja ikiwa na hadhi ya kidiplomasia na nyingine ya kawaida lakini katika safari hiyo alitumia pasi ya kawaida.

Desemba 5, 2014, Kamran ambaye ni raia wa Pakistan, alihukumiwa kifungo cha miaka 60 jela baada ya kupatikana na makosa manne ya kusafirisha wanyamapori hao kwenda Arabuni bila kibali.

Mbali na kuhukumiwa kifungo hicho, pia Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa, Simon Kobero aliamuru kutaifishwa kwa mali zote za mtuhumiwa huyo zilizopo Tanzania.

Hata hivyo, hukumu hiyo ilitolewa bila ya mtuhumiwa kuwapo mahakamani kwa kuwa alitoroka nchini Februari 2014.

Twiga hao na wanyama wengine walitoroshwa kwenda Arabuni Novemba 26, 2010 kupitia Kia kwa kutumia ndege kubwa ya Jeshi la Qatar.

Wanyama waliotoroshwa kwenda Doha wenye thamani ya Dola 113,715 za Marekani (Sh170.5 milioni), walisafirishwa kwa kutumia maboksi marefu.  


Angalia Picha za Nyumba Mpya ya Wema Sepetu Baada ya Habari Kuzagaa Jana Kuwa Amefukuzwa Kwa Ile Nyumba ya Kijitonyama

$
0
0

Angalia Picha za Nyumba Mpya ya Wema Sepetu Baada ya Habari Kuzagaa Leo Kuwa Amefukuzwa Kwa Ile Nyumba ya Kijitonyama....

Diamond Afanya Kufuru Kariakoo Karume..Atoa Show ya Bure na Kusema "Njooni Dar Live Siku ya X-mas, Sitawaangusha"

$
0
0
Funga Mwaka Concert 2015 (7)Funga Mwaka Concert 2015 (9)
Diamond Platnumz akiwasalimia mashabiki wake waliofurika katika eneo la Karume leo kwenye mkutano na wanahabari kuhusu shoo yake itakayofanyika Dar Live kwenye Sikukuu ya Krismasi.
Funga Mwaka Concert 2015 (10)
Diamond akiimba wimbo wake mpya wa Utanipenda sambamba na mashabiki waliofurika Karume leo.
Funga Mwaka Concert 2015 (8)
Mashabiki wakiwa wamepagawa wakati Diamond akiimba wimbo wake mpya wa Utanipenda.
Funga Mwaka Concert 2015 (1)
Meneja Masoko wa Global Publishers na Dar Live, Innocent Mafuru (mwenye tisheti nyeupe aliyesimama kulia) akiwakaribisha wanahabari, wasanii na mashabiki wa burudani katika mkutano na wanahabari kuelekea shoo ya Funga Mwaka itakayofanyika Dar Live kwenye Sikukuu ya Krismasi.
Funga Mwaka Concert 2015 (2)
Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho akielezea jinsi walivyojipanga kwa shoo hiyo ya Krismasi.
Funga Mwaka Concert 2015 (3)Meneja Uhusiano Msaidizi wa Airtel Tanzania, Jane Matinde akionyesha kadi ya Airtel Money Tap Tap inayomuwezesha mteja kufanya malipo mahali popote na watakaohudhuria shoo ya Diamond kununua tiketi kwa punguzo la shilingi 5000 kwa wateja 1000 wa kwanza.
Funga Mwaka Concert 2015 (4)
Mratibu wa Burudani Dar Live, Juma Mbizo akiongea na wanahabari pamoja na mashabiki (hawapo pichani) kuhusu walivyojipanga kuwapa burudani mashabiki siku ya Krismasi.
Funga Mwaka Concert 2015 (5)
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Staric ambaye naye atapanda jukwaani siku hiyo akiongea na mashabiki.
Funga Mwaka Concert 2015 (6)
Diamond akizidi kuwapagawisha mashabiki wake.
Funga Mwaka Concert 2015 (18)Funga Mwaka Concert 2015 (19)
Baada ya kuongea na mashabiki wake Diamond aliamua kugawa CD na DVD za nyimbo zake kwa mashabiki waliohudhuria.
Funga Mwaka Concert 2015 (20)
Diamond akiwaaga mashabiki na kuwataka wakutane Dar Live katika Sikukuu ya Krismasi.
Funga Mwaka Concert 2015 (21)
Mashabiki wakiwa wamemzingira Diamond wakati akiondoka eneo la mkutano na wanahabari leo.
Funga Mwaka Concert 2015 (22)Funga Mwaka Concert 2015 (23)Mashabiki wakiwa wamezingira gari la Diamond wakati akiondoka.

Polisi Sita Mbaroni kwa Tuhuma za Mauaji ya Washukiwa Dar es Salaam

$
0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linawashikilia askari polisi sita, wawili wakiwa askari wa kawaida na wanne wa Idara ya Wanyamapori kwa tuhuma za kusababisha vifo vya watu wawili wanaodaiwa kujihusisha na ujangili.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana,  Kamanda wa Kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova, aliwataja askari hao wa kawaida kuwa ni Bonny Mbange ambaye ni mkaguzi wa polisi E.909D/SGT na mwingine aliyemtaja kwa jina moja la Filbert.

Kwa upande wa Askari wa Wanyamapori aliwataja kuwa ni Emmanuel Mbaga, Deogratias Mwageni, Joseph Jimmy na Asubile Mwakyusa.

Kamishna Kova aliwataja watuhumiwa waliofariki kuwa ni Yasin Rashidi (46) na Samson Michael (46) mkazi wa Mbezi jijini Dar es Salaam.

Aidha, Kamishna Kova alisema awali waliwakamata askari saba walioshiriki katika mauaji hayo, lakini wakati wanahojiwa mmoja kati yao aitwaye Issa Kazimoto mwenye namba F.5371D/C alifanikiwa kutoroka.

Alisema taarifa za awali zinaonyesha kuwa askari hao na wenzao wa Idara ya Wanyamapori kutoka kikosi maalum cha kuzuia ujangili walikuwa wanafuatilia watu wawili kwa tuhuma za ujangili.

Alisema Desemba 9, mwaka huu, zilitolewa taarifa Kituo cha Polisi Magomeni kutoka kwa askari waliokuwa katika operesheni maeneo ya Sinza kuwa watuhumiwa waliokuwa wanawafuatilia wamefariki dunia katika harakati za kuwakamata.

Alisema uchunguzi wa awali wa tukio hilo unaonyesha kuna utata tangu wakati wa ukamatwaji hadi vifo vya marehemu hao wawili na ndiyo sababu askari hao  wanashikiliwa ili kupata ukweli wa vifo hivyo na uhalali wa nguvu iliyotumika.

Aliongeza kuwa ukaguzi wa miili ya marehemu hao unaonyesha kuwa walipata majeraha ya risasi, hivyo uchunguzi wa kisayansi utafanyika ikiwa ni pamoja na kuwahusisha  madaktari bingwa wa uchunguzi wa miili.

Aidha, Kamishna Kova aliwataka wananchi wenye taarifa zaidi kuhusu tukio hilo walisaidie Jeshi la Polisi ili sheria ichukue mkondo wake.

Shamsa Amvulia Kofia Irene Uwoya na Kumwagia Misifa Kedekede

$
0
0
MSANII wa filamu nchini, Shamsa Ford, amesema katika wasanii ambao anawakubali kutokana na ubora wa kazi zao mmojawapo ni Irene Uwoya.

Shamsa alisema msanii huyo anajua nini anachofanya na anapenda kupeana ushauri na kushirikiana katika mambo mbalimbali na wenzake.

Shamsa aliyasema hayo alipokuwa akimkabidhi zawadi Irene katika sherehe yake ya kuzaliwa iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwake Sinza, Dar es Salaam.

“Tabia yangu na ya Irene inaendana kwani tumekuwa tukifanya vitu kwa ushirikiano, nampenda sana na tumekuwa tukishauriana vitu vya msingi kwani ni yeye aliyenishauri na mimi nizae,” alisema.

Diamond Afunguka Kutotokea Kwenye Zari All White Party, Adai Hamwogopi Ivan

$
0
0
Diamond Platnumz alikuwepo, Kampala, Uganda usiku ambao Zari alikuwa akifanya party yake ya All White lakini hakutokea. Ex wa Zari, Ivan Ssemwanga na wapambe wake walikuwepo. Watu walihisi kuwa Diamond aliogopa kwenda kumpa kampani mama wa mtoto wake Tiffah ili kuepusha shari na kambi ya Rich Gang ya Ivan.


Hata hivyo muimbaji huyo wa Utanipenda amedai kuwa hakukacha party hiyo bali makubaliano aliyokuwa nayo na promota wa show yake ya Ijumaa (siku moja baada ya all white party) yalimtaka asiende kwenye show hiyo ili kutengeneza uspesho kwenye show yake na Patoranking na sio ukweli kuwa alimgwaya Ivan.

“Halafu sasa watu wanasema namuogoa [Ivan], mimi siwezi kumuogopa, hii code chafu kabisa kutoka Tandale mimi nimuogope mtu!,” alisema kwenye mahojiano ya jana kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM.

Diamond amesema ameshawahi kukutana na Ivan mara kibao japo walipigiana mikausho kama kawa!

Sijawahi kuwa na matatizo naye, nshakutana naye wakati naenda kwenye MTV alikuwepo, mara nyingi tulikuwa tunapishana hivi na hivi kabisa. Hatujawahi kusalimiana sababu sijawahi kuwa na mahusiano naye niseme nimsalimie ni uongo. Halafu nilikuwa nikipita, nipo na crew, security, yeye anakuwa anapita tu maskini ya Mungu.”

Chanzo: Bongo5

Rais Magufuli amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli Tanzania (RAHCO)

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (RAHCO) Mhandisi Benhadard Tito ili kupisha uchunguzi wa kina kufuatia ukiukwaji mkubwa wa taratibu za manunuzi uliobainika katika mchakato wa utoaji wa zabuni ya ujenzi wa reli ya kati.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema, Rais Magufuli amefikia uamuzi huo baada ya kuitisha kikao cha wataalamu kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za serikali ambazo zinahusika katika utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Reli ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani "Standard Gauge"

Amesema pamoja na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO, Rais Magufuli ameivunja bodi ya RAHCO baada ya kujiridhisha kuwa haikutekeleza ipasavyo wajibu wake katika kusimamia mchakato wa zabuni hiyo na badala yake imeonekana kutetea kilichofanyika

Aidha Rais Magufuli amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO Mhandisi Benhadard Tito kutoa ushirikiano kwa vyombo vya serikali vitakavyofanya uchunguzi zaidi kuhusu mchakato wa Zabuni hiyo.

Pia ameiagiza Mamlaka ya udhibiti wa manunuzi ya umma (PPRA) kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya kampuni za ukandarasi zilizopewa zabuni ya ujenzi huo endapo itathibitika kuwa zimeshiriki katika ukiukwaji wa sheria.

Katika hatua nyingine Balozi Sefue amesema, Rais Magufuli amevunja bodi ya Mamlaka ya Reli Tanzania (TRL) kutokana na kutoridhishwa na jinsi bodi hiyo ilivyoshughulikia ripoti ya uchunguzi wa mchakato wa ununuzi wa mabehewa ya treni.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

22 Desemba, 2015

Sababu Sita Kwanini Hutakiwi Kuacha Kujichua ikiwa Bado Hujaoa(Single)

$
0
0
Watu wengi Walio jaa uzandiki wamekuwa wakijitokea na kubeza kuwa kujichua kuna madhara,hii si kweli bali ni milengo ya kihafidhina ambayo inataka kuendekeza ukaha na umalaya kwa vijana wanaobarehe,kujichua kumekuwepo tangu enzi ,hivyo mtu hapaswi kupinga tendo hili ambalo ni takatifu na sio haramu~

Faida za mtu (Mme&Mke) kujichua

1.Humfanya mtu kuwa salama hivyo kuepuka hatari ya kuambukizwa magonjwa ya ngono kama vile UKIMWI
2.Haina gharama,huhitaji pesa za kupoteza kumuhonga mwanamke/mwanamme ili kupata burudani
3.Humfanya mme achelewe kufika kileleni wakati wa tendo la ndoa akiwa na mke wake
4.Hupunguza misongo ya mawazo kwa kukataliwa/pindi migongano ya kimapenzi inapotokea hivyo kumfanya mtu kuishi huru
5.Husaidia ubongo kuwaza na kutafakari vyema na kwa usahihi,mfano mtu anapotaka kujichua itambidi achukue picha/taswira(avute hisia) ya binti au mme anayemvutia ili kukidhi haja yake.kitendo hiki husaidia ubongo kuwa active.
6.Ongeza na wewe msomaji ..

COSOTA Yataja Kiasi Atakacholipwa Msanii Kwa Kila Wimbo Au Video itakayochezwa Kwenye Redio au TV

$
0
0
Miongoni mwa maswali mengi ambayo yanaendelea kuulizwa kuhusiana na utaratibu mpya wa vyombo vya habari kuanza kuwalipa wasanii kwa kucheza nyimbo zao kuanzia mwakani, ni pamoja na kiasi gani msanii atakuwa analipwa.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama cha Hakimiliki Tanzania (Cosota), Doreen Sinare alisema kuwa wanamuziki, watunzi na maproducer watalipwa asilimia 60 kwa kila wimbo au video itakayochezwa katika redio na televisheni yoyote ndani na nje ya nchi kwa kutumia vifaa bora vilivyowekwa na kampuni ya CMEA.

Doreen alisema kuwa mwanamuziki, msanii alitakiwa kupata asilimia 70 ya kazi yake, lakini asimilia 10 itakatwa katika malipo hayo na kuingia katika mifuko ya jamii kwa mahitaji yake ya baadaye.

Alisema kuwa wanamuziki ni sawa na wafanyakazi wengine na asilimia 10 hiyo itamwezesha kujipatia kipato chake kama ilivyo kwa wafanyakazi wengine katika taasisi mbalimbali.

COSOTA kwa kushirikiana na kampuni ya kusimamia kazi za wanamuziki nchini Copyrights Management East Africa Limited (CMEA) wataanza kulipa mirabaha ya wanamuziki na wadau wake kuanzia mwakani.

Sherehe za Kumuombea Lowassa Uvumilivu na Hekima Nusura Zivunjike

$
0
0
Wananchama na viongozi wa vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa mjini Morogoro wamefanya sherehe zenye lengo la kumuombea hekima na uvumilivu aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa.

Taarifa kutoka mjini Morogogoro zinaeleza kuwa sherehe hizo nusura zivunjike baada ya kutawaliwa na majonzi kwa hali ya juu huku baadhi ya wahudhuriaji wakidondosha machozi kutokana na maelezo yaliyokuwa yakitolewa na viongozi wa vyama hivyo.

Mmoja kati ya waandaaji wa sherehe hizo, Bi. Bertha Kombe alieleza katika sherehe hizo kuwa vijana wengi walitupa kadi zao za kupigia kura baada ya matokeo ya urais huku afya za akina mama wa chama hicho zikidhoofu kutokana na kutoridhishwa na muenendo wa uchaguzi huo.

“Vijana wengi mitaani wamevunjwa mioyo na kutupa shahada zao za kupigia kura, kina mama tumejikuta tukikonda na kushindwa kula kwa sababu tunatumia muda mwingi kutafakari kilichotokea,” alisema Bi. Kombe.

Viongozi wa Chadema waliwashukuru wananchi kwa kuitikia wito na kuwataka kuanza harakati za kuomba kura kwa ajili ya mwaka 2020.

Nini Kimemkuta Ommy Dimpoz? Nyimbo zake za Sasa Zimekosa Ladha

$
0
0
Mimi ni mshabiki wa Ommy Dimpoz kitambo kidogo tangu anatoa nainai lakini siku hizi ananiangusha sana tangu wanjera na hii mpya ya sasa achia body ambayo kimsingi nyimbo imekosa ubunifu, nyimbo imefanana na shikorobo ya Shetta hasa beat, melody nyepesi mno haivutii...Nyimbo zake kwa sasa zinabebwa na Video na si Kingine.......

Ommy rudi kwenye identity yako utakuwa zaidi hata uko kimataifa unakota kwenda, umemtoa Vanessa mdee na amepiga hatua kuliko wewe, wake up Dimpoz.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Disemba 23

$
0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Disemba 23

Mpekuzi blog
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

January Makamba Atema Cheche Kuhusu Wavamizi wa Ardhi.....Asema Kuwa na Vibali vya Ujenzi Hakuizuii Bomoa Bomoa Kuchukua Nafasi Yake Mpekuzi blog

$
0
0
Taarifa ya Hali ya Mazingira Nchini inaonyehsa kwamba mwenendo wa uharibifu wa mazingira nchini ni wa kutisha. Mito mingi nchini inakauka.

Vyanzo vingi vya maji vinakufa. Miti na misitu ya asili inapungua kwa kasi kubwa – kila mwaka, tunapoteza zaidi ya ekari milioni moja za misitu. Viwanda vingi havijaweka udhibiti wa kuzuia umwagaji wa kemikali zenye sumu.
 
Uharibifu wa mazingira unaathiri sekta zote muhimu (kama vile kilimo, mifugo, uvuvi, utalii, uzalishaji umeme, makazi, miundombinu) na kupunguza uwezo wa nchi kupata maendeleo endelevu.

Tukiendelea na mwenendo wa sasa wa uchafuzi wa mazingira, ndani ya kipindi kifupi, mifugo na wanyamapori watakosa malisho (tumeshaanza kuona viboko wanakufa kwenye Mto Ruaha kutokana na kukauka kwa mto), watu watakosa maji ya kutumia, kilimo kitashindikana. Tunayo Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004 ambayo inaweka makatazo mahsusi kwa nia ya kuepusha uharibifu wa mazingira.

Serikali ya Awamu ya Tano itahakikisha kwamba Sheria hii inatekelezwa kwa ukamilifu wake. Pia, mapema mwakani, Serikali italeta mpango kabambe wa kupambana na uharibifu wa mazingira, ambao utatoa wajibu kwa kila mwananchi na kila taasisi ya umma na binafsi.

Kwasasa, kwa kuanzia, tunaanza na operesheni ya kuwaondoa watu wanaoishi na kufanya shughuli kwenye maeneo ya kingo za mito na maziwa, fukwe za bahari, maeneo oevu (swampy) na maeneo ya wazi (Open spaces).

Kwa hapa Dar es Salaam, zoezi la kuwaondoa wananchi waliojenga au kufanya shughuli kwenye maeneo haya kinyume cha sheria na taratibu lilianza rasmi tarehe 17/12/2015 likilenga kuwaondoa wananchi wote waliojenga na wanaofanya shughuli kwenye maeneo hayo kinyume cha sheria.

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kwa kushirikiana na mamlaka za Serikali za Mitaa kwa pamoja wanaratibu na kusimamia zoezi hili linaloendelea.

Zoezi hili limeanzia mtaa wa Mkwajuni, Kata ya Hananasifu Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam. Mpaka sasa zaidi ya nyumba 353 zimebomolewa katika mkondo wa Mto Ng’ombe unaomwaga maji yake Mto Msimbazi. Wanaoishi au kufanya shughuli kwenye mabonde na kingo za mito ya Mlalakuwa, Mbezi/Kawe na Nyakasangwe nao pia wanatakiwa kuhama.

Sheria zinazosimamia suala hili.
Zoezi hili linasimamiwa na Sheria za Ardhi, Sheria za Mipango Miji na Sheria ya Mazingira Sura ya 191 (Environmental Management Act Cap 191) ya mwaka wa 2004 kwa Mujibu wa kifungu cha 55 inaelekeza kuwa maeneo ya kingo za mito, miambao ya maziwa na bahari yanalindwa kisheria – na shughuli zinazohusu ujenzi, kufukua, kuchoronga, kutoboa na kuharibu kingo au mwambao ni kosa.

Kifungu cha 57 cha Sheria ya Mazingira pia kinazuia shughuli zozote zinazoweza kuhatarisha au kuathiri mazingira kutofanyika ndani ya mita 60 katika kingo za mito, miambao ya ziwa na bahari ili kulinda maeneo hayo.

Athari za ujenzi kwenye Kingo za Mito
Kutokana na ongezeko la watu jijini Dar es salaam, na maeneo mengine ya miji yetu, uvamizi wa maeneo ya kingo za mito, mikondo ya bahari, maeneo oevu umeongezeka.
 
 Shughuli zinazofanyika kutokana na uvamizi huu ni pamoja na ujenzi wa nyumba, kilimo, ufugaji, utupiaji taka na uchimbaji mchanga.

Shughuli hizi katika maeneo hayo husababisha uharibifu na madhara makubwa ya mazingira hasa kipindi cha mvua ambapo maji hukosa uelekeo kutokana na njia zake za asili kuzibwa na hivyo kutawanyika hovyo na kusababisha mafuriko, uharibifu mkubwa wa miundombinu hasa madaraja ambayo huvunjika, kukatika kwa barabara na vifo.
 
Athari zingine za kuvamia maeneo hayo ni kusambaa kwa magonjwa ya mlipuko yasiyoisha hasa kipindupindu kutokana na maeneo hayo ya mikondo ya mito kutokua na mfumo wa utoaji wa maji taka.

Serikali ya Awamu ya Tano haitakubali kuacha hali hii iendelee. Tumeamua, kwa kushirikiana na wenzetu wa Wizara ya Ardhi na Mamlaka za Serikali za Mitaa kote nchini, kuchukua hatua kurekebisha hali hii.

Kama alivyosema Waziri wa Ardhi, kwasasa, zoezi hili litasimama kwa muda kutoa nafasi ya mwisho kwa wale wanaofanya shughuli na kuishi katika maeneo haya kuondoka kwa hiari yao kwa kuwa taarifa na notisi rasmi walikwishazipata mara nyingi siku za nyuma. Baada ya mwaka mpya zoezi hili litaendelea.

Vilevile, kwa taarifa hii, naelekeza na kukumbusha kwamba zoezi hili litaendelea nchi nzima. Kwa maana hiyo, yoyote yule aliyejenga na anayefanya shughuli zinazoharibu mazingira kwenye kingo za mito, vyanzo vya maji, miambao ya maziwa na fukwe za bahari kinyume cha sheria, ajiondoe mara moja kwakuwa kuanzia mwakani tutatimiza matakwa ya Sheria bila kusita.
 
Kuwa na vibali vingine vya ujenzi au shughuli katika maeneo haya, hakuondoi uwezo wa kutekelezwa kwa Sheria ya Mazingira.

January Makamba (MB)
Waziri wa Nchi, OMR – Muungano na Mazingira
22.12.2015

Mrithi Wa Dk. Willbrod Slaa Chadema Huyu Hapa

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinafanyia kazi uteuzi wa Katibu Mkuu wa chama hicho kufuatia aliyekuwa Katibu Mkuu wake, Dk. Willbrod Slaa kujivua wadhifa huo baada ya kujitoa kwenye siasa za vyama.

Pamoja na kutokuwa tayari kumtaja mrithi wa Dk. Slaa, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe anatarajiwa kuteua jina la mwananchama ambaye atashika wadhifa huo.

Katika majina yanayochomoza miongoni mwa wana-CHADEMA kushika mikoba hiyo ni jina la Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya tatu, Frederick Sumaye na aliyekuwa mgombea mwenza wa CHADEMA, akiungwa mkono na UKAWA, Duni Juma Haji maarufu kama "Babu Duni'.

Duru za kisiasa zinaeleza kuwa uamuzi wa hivi karibuni wa Frederick Sumaye kujiunga na CHADEMA ni moja katika mchakato mzima wa kumwezesha kuteuliwa kushika nafasi hiyo ya juu katika utendaji katika CHADEMA.

Chama hicho kinaona haja ya kumpa wadhifa huo Sumaye ili aendelee kuwepo katika medani za kisiasa na hivyo kumweka katika haiba nzuri ya kuendelea kuwa mpiga debe wa CHADEMA katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 na chaguzi zote ndogo zitakazojitokeza kufuatia rufani za wagombea ubunge wa CHADEMA waliokata rufaa kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika okroba 25, 2015.

Kwa upande wa Duni Juma Haji, ambaye awali alisemekana kuwa na mpango wa kurudi CUF ambako anadaiwa kuwa na kazi maalum, ameendelea kuwepo CHADEMA kimahesabu kwa matarajio kwamba endapo Seif Sharrif Hamad atafanikiwa kuwa Rais wa SMZ basi Babu Duni atafaa kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA ili kudumisha mahusiano kati ya CHADEMA na CUF.

Hili nalo limekaa katika mfumo ule ule wa mahesabu ya kisiasa kwani CHADEMA wanamwona Babu Duni kuwa ni mtaji wa uhusiano huo kati ya vyama hivyo vikuu vya upinzani nchini ambapo mtaji huo utwawezesha CHADEMA kuingia Ikulu ya Magogoni katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Hatimaye Samwel Sitta Akubali Yaishe Aamua Kustaafu Rasmi Siasa

$
0
0
Hatimaye mzee Samwel Sitta atangaza kustaafu rasmi siasa, hajasema kama atarudi kijijini kulima kama ilivyo kwa wanasisa wengi ambao Mara nyingi wanapostaafu hutangaza kurudi kijijini na kuwa wakulima, lakini pia kilimo kwanza ilikuwa ndiyo Sera ya chama chake katika Serikali ya awamu iliyopita.

Source: Magazeti ya leo

Nafasi za Kazi Dangote Industries Limited Tanzania, Apply Here

$
0
0
DANGOTE INDUSTRIES LIMITED TANZANIA
JOB OPPORTUNITIES

We invite you to be part of a very large State-of-the-Art Cement Manufacturing Plant?

Dangote Group, one of Africa's largest conglomerates, producing diversified products and rendering services aimed at meeting the basic human needs of Food, Shelter and Clothing, is on a rapid industrialization plan across African continent.
As part of our investment in Tanzania, we are setting up a centrally computerized controlled Cement Manufacturing Plant near Mtwara, Tanzania with its own clinker manufacturing facility.

We are looking for Seasoned, Experienced and Qualified Professionals in following disciplines to be members of our Group and grow with us.

Bonyeza HAPA Kuapply

Au Tembelea www.ajirayako.com

Sumatra Yatoa Vibali vya Muda Kwa Mabasi Kuwapeleka Wachaga Kilimanjaro, Matapeli Kibao Wavamia Ubungo Wauza Ticket Feki

$
0
0
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) imelazimika kutoa vibali vya wiki moja kwa mabasi ya mikoa ambayo haina abiria wengi kufanya safari za Kaskazini na Kanda ya Ziwa.

Imeamua kufanya hivyo kutokana na hali ya usafiri katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi cha Ubungo (UBT) kuwa mbaya hasa kwa abiria wanaokwenda katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Mwanza, Kagera na Kigoma kwa sherehe za Krismasi na Mwaka Mpya kuongezeka.

Jana saa 12.20 asubuhi katika kituo hicho, abiria walikuwa ‘wakipambana’ kupata tiketi lakini karani wa Basi la Meridian Mustafa Mussa alisema hakuna aliyekuwa akiuziwa tiketi zaidi ya tatu. Baadhi ya wasafiri walilazimika kupanga foleni mara mbili ili kufikisha idadi ya tiketi walizohitaji.

Sijui kwa nini wanatufanyia hivi, wanatulazimisha tukate tiketi tatu.. mimi nasafiri na familia yangu yote watu saba naambiwa nikate tiketi tatu hivi kweli inakuja?” alilalamika Joyce Munisi.

Ngenka Eliachim alisema kuna watu wanapanga foleni mara mbili, wanakata tiketi nyingi halafu wanaziuza.

Wanatunyima haki sisi abiria, tumekuja tangu jana, tumelala hapa tunasubiri tiketi na tunaambiwa zimebaki za siku mbili,” alilalamika Eliachim.

Meneja Usalama Barabarani na Mazingira wa Sumatra, Geoffrey Silanda alisema wanatoa vibali kwa mabasi ambayo hayako kwenye ratiba ya kusafirisha abiria.

 Matapeli kibao

Ugumu huo wa usafiri umesababisha pia ongezeko la matapeli ndani ya kituo hicho na kuwalaghai abiria. Jana, abiria aliyekuwa akisafiri kuelekea Mwanza, Neema Mussa alitapeliwa Sh50,000 baada ya kuuziwa tiketi feki.

Nilikuwa nasafiri kwenda Mwanza ,nimefika hapa nikakosa tiketi, baadaye wakaja vijana wawili wakiwa na makaratasi, wakaniambia niwape Sh50,000 wanitafutie” alisema.

Alisema kutokana na shida aliyokuwa nayo aliwapa na matapeli hao walimwachia leseni ya gari kama dhamana lakini vyote vilibainika kuwa feki.


Mchungaji na Mkewe Wasota Gerezani Kwa Kumfungia Mtoto wao Ndani Miaka 12 Bila Kuona Jua

$
0
0
Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste katika Kijiji cha Itaga mkoani Singida, David Mtipa (59) na mkewe, Maria Phillip (45), wanasota katika Gereza la Singida baada ya kushindwa masharti ya dhamana kufuatia kufikishwa mahakamani Ijumaa iliyopita kwa madai ya kumfungia ndani kwa miaka 12, mtoto wao, Timotheo (30).

Watuhimiwa hao walipandishwa kizimbani kwa madai ya kushindwa kumpatia huduma muhimu mtoto huyo kwa kipindi cha miaka 12, tangu akiwa na umri wa miaka 18.
Mwanasheria wa Serikali, Patrisha Mkina alidai mbele ya Hakimu Mwandamizi wa Mahakama ya Singida, Faisal Kahamba kuwa, kati ya mwaka 2003 mpaka 2015, kwa makusudi, Mchungaji David akishirikiana na mkewe Maria walishindwa kumpatia Timotheo huduma muhimu za kibinadamu.
“Wanandoa hao walitenda kosa hilo huku wakijua kuwa kitendo hicho ni kinyume cha sheria,” alisema mwanasheria huyo.

Alisema kwa miaka 12, washitakiwa walimnyima Timotheo malazi, chakula, nguo, matibabu na uhuru wa kikatiba kitendo ambacho kimechangia apate madhara ya kudumu ya afya.
Washitakiwa walikana mashitaka hayo na kesi hiyo itatajwa tena, Desemba 28, mwaka huu. Washitakiwa walipewa masharti ya dhamana ya wadhamini wawili ambao wangeweka dhamana ya shilingi milioni moja kila mmoja, wakashindwa kutimiza.

Wiki iliyopita, Jeshi la Polisi mkoani Singida lilimshikilia nchungaji huyo na mkewe kwa tuhuma za kumfungia ndani kwa miaka 12 mtoto huyo mwenye ulemavu wa viungo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Tobias Sedoyeka alisema tukio hilo la kusikitisha liligunduliwa na wasamaria wema ambao walitoa taarifa serikalini.
Kamanda Sedoyeka alisema Timotheo alikuwa akipata huduma zote chumbani zikiwemo chakula, haja ndogo na kubwa.

“Wazazi hao walisema, kijana wao alizaliwa mwaka 1984 akiwa mzima. Akiwa darasa la 6, mwaka 2003, alianza kuugua ugonjwa usiojulikana, akawa anaanguka na kutoa povu mdomoni huku mwili wake ukibadilika rangi kuwa wa njano na akatibiwa bila mafanikio.
“Walisema baada ya Timotheo kutibiwa bila mafanikio, ndipo wao waliamua kumfungia ndani wakiona kuonekana kwake mitaani kunawafedhehesha katika jamii,” alisema.

Serikali Yafuta ‘Semina Elekezi’ Kwa Madiwani

$
0
0
John Magufuli
Serikali imesema mafunzo kwa ajili ya madiwani wote hayatakuwepo na badala yake wenyeviti na makamu wa wenyeviti kote nchini ndio watapatiwa mafunzo ya namna ya kusimamia halmashauri zao.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) anayeshughulikia Utumishi na Utawala Bora, Selemani Jafo alisema hayo wakati alipofanya ziara ya kutembelea Chuo cha Serikali za Mitaa cha Hombolo mjini Dodoma.

“Madiwani ni wengi wote kuwapatia mafunzo haiwezekani kila halmashauri itatoa mwenyekiti na makamu mwenyekiti, meya na naibu meya” alisema Jafo.

 Alisema mafunzo hayo yatahusisha wenyeviti wa halmashauri na makamu wao kutoka halmashauri 185 nchini na kuwaagiza wakurugenzi kuhakikisha viongozi hao wanafika Chuo cha Hombolo tayari kwa ajili kwa mafunzo hayo.

Alisema miaka ya nyuma kulikuwa na utaratibu wa kuwapatia mafunzo madiwani waliochaguliwa baada ya Uchaguzi Mkuu, lakini sasa ni wenyeviti na makamu wenyeviti wa halmashauri ndio watapatiwa mafunzo hayo.

Alisema halmashauri 185 zilizopo nchini zitapeleka watu wawili kila halmashauri na waliopata mafunzo hayo watakwenda kuwafundisha wengine.

 Naibu Waziri alisema kulikuwa na changamoto nyingi katika Uchaguzi Mkuu uliopita na madiwani walichaguliwa kutokana na sifa zao na wengine wananchi walifanya uchaguzi wa hasira, lakini mwisho wa siku kiongozi aliyetakiwa alipatikana.

Alisema madiwani wapya waliopatikana wapo wafanyabiashara, wanafunzi na watu wa kada mbalimbali ambao wote walitakiwa kufundishwa namna ya kutenda kazi zao.

 Hata hivyo, alisema mafunzo kwa ajili ya madiwani wote hayatawezekana, bali viongozi wa madiwani hao ndio watapatiwa mafunzo hayo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa, Dk Emmanuel Gibai alisema maandalizi kwa ajili ya mafunzo hayo yamekamilika.

Awali yalipangwa kutolewa kwa madiwani wote, lakini kutokana na maelekezo hayo wahusika watakaotakiwa kupatiwa mafunzo hayo watayapata.

Kova: Krismasi, Mwaka mpya Disko Toto Marufuku

$
0
0
Disco Toto
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amepiga marufuku disko toto na milipuko ya baruti katika kusherehekea sikukuu za krismass na mwaka mpya.

Kamanda Kova amesema hayo ikiwa zimebaki siku mbili kusherekea Sikukuu ya Krismasi na siku tisa kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya wa 2016 ambazo mara nyingi huwa na shamrashamra na mfululizo wa matukio ya hatari yanayotokana na namna mbaya ya usherehekaji.

Amesema kuwa, anawahakikishia usalama wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakati wa kusherehekea sikuu za maulidi, krismass na mwaka mpya hivyo wananchi wanatakiwa kusherehekea kwa amani sikukuu hizo.

Kamanda Kova amesema kuwa jeshi hilo litadhibiti wahalifu watakaotumia siku hizo kufanya matukio ya kihalifu na kudhuru watu bila ya sababu.
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>