Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104803 articles
Browse latest View live

Mrembo Gigy Money Amjibu Mwanamuziki Tekno..Adai Ana Kibamia na Hata Hakumkuna Kunako Sita Kwa Sita...

$
0
0
Baada ya Siku ya Jana Mwanamuziki Tekno kutoka Nigeria Kukanusha Kutembea Kimapenzi na Mrembo Gigy Money na kudai kuwa Gigy Anatafuta Kiki...Mrembo huyo Ameibuka na Kuandika Haya Hapa


Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne Ya Januari 5, Ikiwemo ya Ugunduzi wa Dawa ya Ukimwi..

$
0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne Ya Januari 5, Ikiwemo ya Ugunduzi wa Dawa ya Ukimwi..

Lulu Michael Akanusha Kula Uroda na Tekno, Atoa Maelezo ya Kina

$
0
0
Elizabeth ‘Lulu’ Michael amelazimika kuandika maelezo marefu kukanusha tetesi zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii kuwa alivunja amri ya sita na hitmaker wa Duro, Tekno aliyekuwepo Dar siku ya mwaka mpya.

Haya ni maelezo yake aliyoandika kwenye Instagram:

Okay…naona watu Mnatafutaga Topic Na mkipata picha story mnatungaga mnazozijua NI hivi….naomba heshima Na busara vitumike Nilikutana Na Tekno Kwenye show yake Na alikuja kunisalimia kwenye meza Yangu,picha zote zilizopigwa Na yeye au mtu mwingine yoyote zilipigwa kwenye meza yangu by the time amekuja kunisalimia,Na sio mm tu niliyepiga nae picha NI watu wengi.

Kuhusu issue yake Na whoever called Gigy me cjui Coz hata sikuwepo wakati wanapigana picha zao…Kwahyo mni exclude kwenye hyo issue Yao Nilikuwa najua akili Za watu wengi NDO maana hata sikuthubutu kupost picha yangu Na Tekno B4 this issue Mnachotakiwa kujua….nilienda kwenye show as a fan n nothing else [blush] Na NDO maana hata Post alopost Na mm ka post Kwa heshma Na Taadhima Hakuna Mahusiano Mengine zaidi ya Hapo hata Tekno anajua….au Kama kuna mtu ana picha yangu Na Tekno yenye Utata nje ya eneo la show yake Anisaidie hapa sshv..!

Hebu jaribuni Kuwa mnaongelea vitu mnavyovijua Kwa kina Na sio kunganisha unganisha tu..! Sijaeleza maelezo mengi kwaajili ya KIMA yoyote alosema/kusambaza habari uongo…nijieleza ili wale wachache wenye akili zao wasiendelee kupotoshwa…. Gotta Sleep wth Bae now… #InstagrambilaLuluInawezekana

Makamu Wa Rais Mama Samia Nae Ameanza Kazi Rasmi ......Jana Kaanza na haya Baada ya Kutua Geita.

$
0
0
Makamu wa Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan jana jioni aliwasili  mkoani Geita  na akakutana na uongozi wa mkoa huo ambapo alisisitiza suala la  wananchi kunufaika na mgodi wao wa dhahabu wa Geita Gold Mine.…

"Wakati nilipopita kwenye kampeni nilipita kwenye mgodi wa Geita Gold Mine nikaangalia hali ya watu wa Geita nikawa na majonzi makubwa…sikuridhika kuwa na mgodi mkubwa kama ule na hali ya watu wa Geita iko ilivyo hivi nikawa sikuridhika nilikuwa mkali kidogo." Alisema Mama Samia  na  kuongeza;

"Wakati naangalia presentation nimeona amount nzuri kidogo inatolewa kwenda kwa watu ingawa bado ninamaswali yangu ambayo nitayafanyia kazi ili tuone ni kiasi gani sahihi kinatakiwa kutolewa na mgodi kwenda kwa wananchi, dhahabu iliyopo niyawana Geita Mungu amewaumbia katika ardhi yao

"Hatukatai kuwa na wawekezaji wachimbe lakini uchimbaji uwe na faida kote wao wapate na wananchi wapate kwa hiyo hatunabudi kusimamia vizuri na kuhakika kwamba wananchi wa Geita wanafaidika na rasilamali ambayo Mwenyezi Mungu amewapangia."
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Geita Mhe. Fatma Mwassa wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa GGM Mkoani Geita jana Januari 04,2016 kwa ajili ya kuanza ziara ya siku mbili ya kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo Mkoani humo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na baadhi ya wawekezaji wa Mgodi wa GGM Mkoani Geita alipowasili Uwanja wa ndege wa GGM Geita jana Januari 04, 2016 kwa ajili ya kuanza ziara ya siku mbili ya kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo Mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa Geita Mhe. Fatma Mwassa akizungumza wakati akitoa Taarifa ya Maendeleo ya Mkoa wa Geita, kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia), katika kikao kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo, jana Januari 4, 2016. Katikati ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Injiani Gerson Lwenge.

Madaktari Watangaza Kungundua Dawa ya Kutibu Ugonjwa wa Ukimwi...

$
0
0
Wakati dunia ikiwa na zaidi ya watu 34 milioni wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU), madaktari nchini Hispania wametangaza kugundua tiba ya ugonjwa huo wanayodai ni uhakika.

Kwa kutumia damu ya kupandikiza kutoka kwenye kitovu mwana (umbilical cord) cha mtu ambaye ana vinasaba ambavyo havipokei virusi hivyo vya Ukimwi, wataalamu hao wa tiba wa Hispania wanaamini kuwa wanaweza kutibu ugonjwa huo baada ya mafanikio waliyopata kwa mgonjwa mmoja.

Madaktari hao wa Kitengo cha Taifa cha Upandikizaji (ONT) cha Hispania walichukua damu ya vitovu mwana vya watu wenye vinasaba ambavyo havipokei VVU na kuipandikiza kwa mtu anayeishi na virusi hivyo. Baada ya miezi mitatu, mgonjwa huyo alipimwa na kuonekana hana virusi.

Daktari wa Programu ya Upandikizaji kutoka Taasisi ya Tiba ya Catalan, Barcelona, Rafael Duarte alisema mgonjwa aliyetibiwa kwa njia hiyo, Timothy Brown (37), alikuwa anaishi na VVU tangu mwaka 2009 na madaktari hao walithibitisha kuwa amepona baada ya kupandikizwa damu hiyo. Mgonjwa mwingine aliyefanyiwa majaribio ya tiba hiyo alipona VVU, lakini miaka mitatu baadaye alifariki kwa ugonjwa wa saratani.

Timu ya madaktari wa Hispania ililiambia gazeti la kila siku nchini humo la El Mundo kuwa wana uhakika kuwa wameleta mapinduzi katika mapambano ya Ukimwi na magonjwa yanayofanana na hayo.

Dk Duarte alisema mwaka 2015 umekuwa wa kujivunia ugunduzi huo mkubwa duniani, ingawa alitahadharisha kuwa tiba kamili haiwezi kupatikana katika siku za usoni.

Kaimu mkurugenzi wa mwitikio wa Taifa wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids), Dk Morris Lekule alisema utafiti kama huo hauna budi kufuata taratibu zote na kuthibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kabla ya kutangazwa kuwa ni tiba sahihi.

“Kila mara taarifa zinakuja zikisema tiba ya Ukimwi imepatikana, lakini tiba kupata uthibitisho kwamba ni sahihi, ni mchakato mrefu unaotakiwa kuhakikisha kama kweli dawa hiyo inatibu na ni lazima WHO wathibitishe hilo,” alisema. Alisema ni vizuri kama wataalamu hao wakapata uhakika kutoka WHO badala ya kuwapa watu matumaini kuwa kuna tiba na baadaye matumaini hayo yanapotea.

Daktari wa kitengo kinachoshughulika na masuala ya Ukimwi cha WHO, Richard Banda alisema hana taarifa za tiba hiyo.


Tiba inavyofanya kazi

Madaktari wa ONT walitumia damu ya mtu mwenye vinasaba vya ‘CCR5Delta’ ambavyo seli zake haziathiriwi na VIRUSI hivyo vya Ukimwi.

Dk Duarte alisema kwanza huziua seli za damu ya mgonjwa kwa kutumia mionzi halafu seli mpya (kutoka kwenye damu ya mtu mwenye seli zisizoathiriwa na VVU hupandikizwa.

Damu hiyo ilipandikizwa kwa mgonjwa mwenye virusi hivyo na saratani ya damu.

Baada ya seli hizo kupandikizwa, Virusi vya Ukimwi vilivyo kwenye damu ya mgonjwa hushindwa kujipenyeza katika seli mpya zilizopandikizwa. “Siku 11 baada ya upandikizaji, mgonjwa wa Barcelona alianza kupata nafuu na baada ya miezi mitatu, tulimpima na kukuta hana VVU,” alisema.


Zitto: Rais Magufuli Ameshaipotezea Nchi Mapato ya Bilioni 8 Tangu Aingie Madarakani

$
0
0
Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe ameilalamikia serikali ya Magufuli kwa kitendo chake cha kukaa kimya kuhusu ufisadi unaoendelea kufanywa na Harbinder Singh Seth, mmiliki wa IPTL, ambaye huvuna kiasi cha malipo ya bilioni 4 kila mwezi kama malipo ya kuliuzia umeme shirika la ugavi wa umeme nchini, Tanesco.

Zitto ambaye ni mmoja wa wabunge walioibua na kusimamia kidete sakata la ufisadi wa Tegeta Escrow bungeni mwishoni mwa mwaka juzi (2014), amesema hayo kufuatia tangazo la serikali kuhusu kashfa ya Commodity Import Support ya miaka ya miaka 1980 na 1990s, ambapo ameisifu serikali kwa hatua hiyo na kuhoji iweje ikomae na kashfa hiyo tu, huku ikisita kuchukua hatua kwenye sakata la IPTL linaloigharimu serikali kiasi kikubwa cha fedha kila mwezi isivyostahili?

Kampuni ya IPTL imeshalipwa fedha mara mbili tangu Rais Magufuli aingie rasmi madarakani, hivyo kufanya hesabu zitimie bilioni 8 kwa kipindi cha miezi miwili mpaka sasa.

Msome;

"Nimeona tangazo la Serikali kuhusu kashfa ya Commodity Import Support. Hii ni kashfa ya miaka ya 1980s na 1990s. Ni hatua nzuri. Lakini ina maana gani wakati Serikali inavuta miguu kwenye suala la IPTL? Harbinder Singh Seth na genge lake wanavuta tshs 4bn kila mwezi. Kwa kutochukua hatua kuhusu IPTL, Rais Magufuli ameshaipotezea nchi mapato ya tshs 8bn tangu aingie madarakani. ‪#‎TegetaEscrow‬ ndio baba la mtandao wa ufisadi nchini kwetu" - Zitto Kabwe.

Shule za Sekondari Nchini Kuanza Kufundisha Lugha ya Kichina

$
0
0
WIZARA ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi imeteua shule sita za sekondari nchini kuingia katika mpango maalumu wa wanafunzi wake kufundishwa somo la lugha ya Kichina kuanzia mwaka huu.

Kutokana na uamuzi huo, walimu 12 kutoka China wamekamilisha utaratibu wa mpango kazi wa namna ya ufundishaji wa somo hilo kwa shule zilizoteuliwa mara zitakapofunguliwa rasmi mwezi huu.

Ofisa Elimu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Salum Salum, alitaja shule zilizoingizwa kwenye mpango huo katika awamu ya kwanza ni Benjamin Mkapa na Chang’ombe (Dar es Salaam), Msalato na Dodoma (Dodoma), Morogoro na Kilakala za mkoani Morogoro.

Salum alitoa taarifa hiyo juzi wakati akifungua mafunzo ya kazi na mipango mikakati iliyoandaliwa na Taasisi ya China inayojihusisha na lugha ya Kichina kwa walimu wake walioteuliwa kufundisha somo la lugha ya kichina katika shule hizo.

Alisema kabla ya kufunguliwa kwa shule, viongozi wa China wamekutana kwa siku mbili mjini Morogoro kufanya mafunzo ya kazi ya kujiandaa kuingia darasani baada ya shule kufunguliwa.

Mafunzo kazini ni ya kujiandaa na kupeana mikakati na nini kifanyike kabla ya shule kufunguliwa ili kuingia madarasani kufundisha wanafunzi wa kitanzania lugha ya kichina,” alisema Ofisa Elimu Mkuu.

Alisema wanafunzi watatahiniwa somo hilo la lugha ya kichina katika mitihani yao na watakapohitimu watahesabiwa alama za ufaulu sawa na yalivyo masomo mengine yanayofundishwa katika shule za sekondari kama ilivyo kwa Kifaransa na Kijerumani.

Alisema wizara inaona ni njia nzuri kwa vijana wa Kitanzania kuwa na lugha ya mawasiliano katika kuwasaidia kujifunza zaidi na kutumia fursa zitakazopatikana China ikiwemo kujiendeleza na elimu ya juu zaidi.

Mkurugenzi wa Taasisi ya China ya lugha ya kichina, Ambar Zheng, kutoka katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), alisema walimu 12 wa China wameshapatiwa mafunzo ya namna ya kufundisha somo hilo kwenye shule husika.

Alisema kila shule ya sekondari iliyoteuliwa katika mikoa hiyo ya Dodoma, Dar es Salaam na Morogoro, zitapangiwa walimu wawili kila moja kwa ajili ya kufundisha somo hilo kuanzia mwaka wa masomo unaoanza mwezi huu.

Alipongeza ushirikiano mzuri uliooneshwa kati ya Serikali ya Tanzania na China na wizara husika kuwezesha kuanzishwa kwa somo hilo katika baadhi ya shule za sekondari nchini. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Waislamu cha Morogoro, Profesa Hamza Njozi alipongeza Serikali ya China kwa kuendeleza ushirikiano katika nyanja mbalimbali, ikiwemo elimu ya vyuo vikuu.

Wananchi Waliobomolewa Nyumba zao Wacharuka..Watumia Mabango Kufikisha Ujumbe Kwa Rais Magufuli...

$
0
0

Wakati muda wa `mapumziko’ ya bomoabomoa ukimalizika leo huku jaribio la kupata zuio la muda likiwa limewekwa kiporo, wakazi wa Jangwani ambako nyumba zitaanza kubomolewa leo, jana waliweka mabango barabarani yanayotuma ujumbe wa aina mbalimbali kwa Rais John Magufuli.

Bomoabomoa hiyo ilianza Desemba mwaka jana likilenga nyumba zilizojengwa kwenye Bonde la Mto Msimbazi, lakini lilisitishwa kwa siku 14 na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi hadi Januari 5, mwaka huu kuwapa nafasi wakazi kuondoka kwa hiari yao kuokoa mali zao.

Wakazi wa Jangwani walitumia mwanya huo wa kusitisha ubomoaji, kufungua kesi Mahakama ya Ardhi kupinga kuondolewa maeneo hayo bila ya kupatiwa sehemu nyingine na kuwasilisha ombi za zuio la ubomoaji, lakini chombo hicho cha sheria kilikataa kubariki mambo hayo ya kutaka sitisho la bomoabomoa liendelee wakati kesi ikiendelea mahakamani.

Wakati wawakilishi wa wakazi hao wakiwa mahakamani katikati ya jiji, watumishi wa halmashauri za jiji waliendelea kuweka alama nyumba zinazotakiwa kubomolewa wakiwa wamesindikizwa na ulinzi mkali wa polisi.

Hakukuwepo na wakazi waliojitokeza kuzuia uwekaji alama hiyo ya “X” inayotaarifu kuwapo kwa ubomoaji, lakini mabango ya maboksi yaliyosimikwa kwenye vifusi na maeneo mengine ya jangwani, yanatosha kuelezea hisia za wakazi hao wanaoishi maeneo ambayo yametangazwa kuwa hatarishi.


Rais Magufuli Alidanganywa na Huyu Mgonjwa Hospitali ya Muhimbili...Mazito yaibuka

$
0
0
DAR ES SALAAM: Yule mgonjwa anayeaminika ndiye aliyetoa siri ya kuharibika kwa mashine za CT Scan na MRI Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa Rais Dk. John Magufuli na wiki iliyopita kudai amelazwa chini, Chacha Makenge, amesababisha mapya kuibuka.

Wakizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita, maofisa uhusiano wa Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (Moi), Frank Matua na Patrick Mvungi kwa nyakati tofauti, walisema kuwa, mgonjwa huyo hakuwa na tatizo lolote la kiafya na alisharuhusiwa kuondoka hospitalini hapo.

“Alipimwa, tena alikuwa mgonjwa wa kwanza kupimwa kwenye CT Scan baada ya kutengenezwa na kugundulika uti wake wa mgongo uliumia miaka mitatu iliyopita. Alipoulizwa alikiri kuumia Stakishari… Kwanza haiwezekani mgonjwa wa uti wa mgongo kumlaza chini,” alisema Matua.
Akaongeza kuwa, baada ya kuonekana hana tatizo, aliruhusiwa kwenda nyumbani lakini anakataa akidai hana pa kwenda. Ndipo alipowaeleza maofisa hao kuwa ana familia ipo Mugumu, Serengeti mkoani Mara.

“Tulimtafutia tiketi ya basi na fedha za matumizi ili aende kwao lakini siku ya safari alikataa kwenda akisema anakwenda msibani. Pia akaelekeza kuwa fedha tulizomtengea kwa safari wapewe wagonjwa wengine ziwasaidie.

“Baada ya siku kadhaa, akarudi hapa Moi. Tulipomkumbusha kuwa amesharuhusiwa, alikataa kuondoka, hatukumshusha kitandani.

Wagonjwa wanaokataa kwenda makwao baada ya kuruhusiwa hapa hospitali wapo wengi na hatuwafukuzi, in humanitarian ground (kibinadamu), tunawapa huduma zote za chakula na malazi kwa gharama za serikali hadi utaratibu mwingine utakapofanyika,” alisema Matua.
Alifafanua kuwa, baada ya kuona Chacha anawasumbua kwa tabia zake mbalimbali, walimchunguza, wakagundua alishawahi kuwa na jalada katika wodi ya wagonjwa wenye matatizo ya akili Muhimbili, hivyo sasa wanafanya utaratibu mwingine wa kumsaidia.

Wiki iliyopita, gazeti hili lilikwenda Muhimbili, Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (Moi) na kumkuta Chacha akiwa amelala chini na akadai ameshushwa kitandani.

Kwa kuona kuwa uwepo wake pale unaweza kusababisha kumchafua Rais Magufuli aliyesimamia zoezi la kupatikana kwa vitanda, gazeti hili liliandika habari zake ili uongozi wa hospitali hiyo uchukue hatua bila kujua kwamba huko nyuma mgonjwa huyo aliwahi kufunguliwa jalada kwenye wodi ya wagonjwa wa akili.

Hata hivyo, maofisa uhusiano wa taasisi hiyo hawakupatikana wakati huo kuzungumzia tukio hilo lililowaacha midomo wazi watu walioingia wodini humo siku hiyo ya tukio.

Magufuli Afuta Hati ya Hekta 1,870 Kapunga

$
0
0
Rais John Magufuli amemaliza mgogoro wa ardhi baina ya wananchi wa Kapunga na mwekezaji wa Kapunga Rice Project Limited na sasa hekta 1,780 zitakuwa mali ya wananchi.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alitangaza jana katika mkutano wa hadhara ambao licha ya mvua kubwa, wananchi walimsikiliza kwa makini na kushangilia baada ya kupokea taarifa hiyo. Kijiji cha Kapunga kina wananchi 4,500.

Lukuvi alisema hatua hiyo ni zawadi ya kwanza ya Rais kwa wananchi Tanzania kwa kutatua mgogoro wa siku nyingi.

“Rais amedhamiria kuwasaidia wananchi, hivyo naomba (Mkuu wa Mkoa), uandae orodha ya watu wote wanaomiliki mashamba yasiyoendelezwa ingawa wanapata mikopo kupitia hati za mashamba hayo ili kazi ya Serikali kuwapatia maeneo ya kulima na wananchi wa kawaida iweze kufanikiwa,” alisema.

Lukuvi alikwenda kwenye kijiji hicho kutangaza jambo ambalo aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, Profesa Anna Tibaijuka alilishindwa Januari 7, 2013.

Meneja wa Mradi Kapunga Rice Project, Sumil Tayic alisema viongozi wake wameafiki uamuzi wa Rais bila kinyongo na sasa wataimarisha ushirikiano mzuri na wananchi.

Mwakilishi wa wananchi, Sekela Sandube aliishukuru Serikali hususan Rais Magufuli na Waziri Lukuvi kwa kumaliza mgogoro ambao uliwashinda wengi kwa sababu za roho mbaya.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kapunga, Brighton Mwinuka alisema hatua ya Rais Magufuli kuwapatia eneo hilo kutakifanya kijiji kiwe na mipango ya maendeleo.

Kabla ya kwenda wilayani Mbarali jana, Lukuvi alikutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya kuanzia saa 2.24 hadi saa 3.57 kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Habari kutoka kwenye kikao hicho zilisema waziri aliwaeleza kinagaubaga kuhusu msimamo wa Serikali ya Awamu ya Tano katika kutatua kero za wananchi na kwamba lazima viongozi wote wabadilike kiutendaji.

Alipoulizwa kilichozungumzwa Waziri Lukuvi alisema yalizungumzwa mambo mengi ya kiutendaji na baadhi angeyatoa Kapunga.

Mgogoro wa Kapunga
Mwaka 1995, wanakijiji walitoa hekta 5,500 za ardhi kwa Kampuni ya Taifa ya Kilimo (Nafco), huku eneo la hekta 1,870 likiwa la wakulima wa kawaida.

Lakini katika mazingira ya kutatanisha, Serikali ilichukua hati moja iliyojumuisha hekta 5,500 na nyingine 1,870 bila kuwajulisha wananchi, hivyo mwekezaji aliponunua eneo la Nafco alikabidhiwa hati ya eneo lote.

Serikali ilibaini kwamba Nafco ilisajili na kupata hati moja kwa eneo lote likiwamo la kijiji lakini kwa miaka yote imeshindwa kutoa uamuzi.

Mwaka 2013, mwekezaji huyo alidaiwa kumwaga sumu kwenye mashamba ya mpunga yaliyokuwa na mgogoro na Serikali ilimtuma Profesa Tibaijuka kuulimaliza.

Alifika akiwa na msimamo wa kutaka kumshauri Rais wa Awamu ya Nne afute hati ya eneo linalozidi ambalo ni hekta 1,870, lakini baada ya kupata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji, Justin Vermaak alisema anawashangaa wananchi kudai kwa nguvu eneo ambalo ni la mwekezaji kisheria.

“Baada ya kuzunguka nimeona mwekezaji hana matatizo, chanzo cha mgogoro ni Serikali, hivyo itaendelea kuzungumza na mwekezaji na wananchi ili kumaliza mgogoro,” alisema.

Mahakama ya Mafisadi na Wahujumu Uchumi Inafanyiwa Kazi- Mwakyembe

$
0
0
WAZIRI wa Katiba na Sheria,Dk.Harrison Mwakyembe amesema kuwa suala la kuanzisha mahakama ya mafisadi na wahujumu uchumi wanafanyia kazi na muda sio mrefu watatoa taarifa juu ya hatua walizofikia.

Dk.Mwakyembe ameyasema hayo leo wakati alipotembelea Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP),amesema kuwa suala mahakama linafanyiwa kazi kwa karibu na ofisi yake kutokana na ahadi ya Rais Dk.John Pombe Magufuli wakati wa kampeni.

Mwakyembe amesema kuwa watu ambao wanaweza kuleta maendeleo ya nchi ni vyombo vilivyo katika maamuzi ya kisheria hivyo lazima viweze kufanya kazi kwa wananchi kwa kutenda haki.

Amesema kuwa baadhi ya watendaji wa taaluma ya sheria sio waaminifu kwa kujihusisha na rushwa na kufanya watendaji wote kuharibika kwa sababu ya mtu mmoja.

Mwakyembe amesema yeye ni mwanasheria na kuongeza kuwa kuna’ majipu’katika tasnia ya taaluma ya sheria na kuwataka majipu hayo yatumbuliwe kabla ya Rais Dk.John Pombe Magufuli hajayatumbua bila sindano ya kupunguza maumivu (Ganzi).

Mwakyembe amesema kuwa wanajua changamoto ya mawakili wa serikali wanazokumbana nazo ikiwemo miundombinu pamoja na mfumo wa maisha wanayoishi hivyo serikali itafanya uwezeshaji kadri ya uwezo wao.

Mkurugenzi wa Mashitaka nchini,Buswello Mganga amesema katika mafanikio walioyapata ni pamoja kushinda kesi nane za dawa za kulevya kwa watuhumiwa kuhukumiwa kifungo cha miaka 20 hadi 30.

10 Signs To Know An Immature Guy [Must Read]

$
0
0

So many reasons have been adduced for why romantic relationships between a guy and a girl don't end up in marriage these days. One of them is Incompatibility!

For this reason, here is a list of tips on how you could get to know if a guy or that guy you are in a relationship with is immature:

1. You’re his first real relationship: He had a girlfriend or two in high school, but has not dated since. If you’re his first girlfriend in the “real world” you’re probably going to have to teach him a few basics. The only thing he has to compare this relationship to are the hormone and puberty induced ones he had when he was seventeen. In his head, when things get rough you’re going to act like his psychotic high school girlfriend, and he’s going to treat you as such. Bottom line: if you’re his first real girlfriend, you’re going to have to teach him a lot, and most of that will be the difference between girls and women.

2. He doesn’t know how to communicate: Communication is key to any relationship. There are going to be confrontations, fights, and near-breakups, but how these are handled are what determines if the couple is going to make it or not. If your boy/man-child isn’t willing to listen to you, or he readily dismisses your feelings, he’s not mature enough to be with you in the long run.

3. He loves his pride more than the relationship: There is a certain amount of give and take in relationships. If your man loves being right more than he loves you, he’s no man at all—he’s just a stubborn boy. Everyone has to swallow their pride at some point, and boys aren’t willing to do this yet.

4. He doesn’t own his flaws: This one is about placing blame, and when something happens in a relationship it’s hardly ever just one person’s fault. If you’re willing to accept what you did wrong, and he isn’t, he essentially thinks he’s always right. Not only is that immature, it’s egotistical.

5. He doesn’t want to be depended on: When poo hits the fan, he’s nowhere to be seen. You might get some sympathy from him, but he puts minimal effort into being the person you can rely on. This is because immature boys retreat when things are too difficult for them. Simply put: men are strong, boys are weak.

6. You’re his girlfriend when it’s convenient for him: You had plans for a nice weekend together? Too bad something else came up and he bailed on you. Sometimes, nothing at all comes up, but he just can’t be bothered and would rather sleep in that day. Men are committed to a relationship and put you before themselves at least some of the time. Boys do whatever they want despite you.

7. He gets lazy: He stopped putting in effort months ago. You no longer get the cute texts you use to screen-shot. You have to fish for compliments because he doesn’t offer them up anymore. And “just-because” phone calls are so few and far-between you begin to doubt their existence all together.

8. He’s a hypocrite: Remember when he got mad at you because you texted him “K” that one time? Now he does it when he’s upset just to spite you. All those things you swore never to do again, and he can’t see the irony in the doing them exactly the same way.

9. He has no ambition: He’s unhappy with his present condition but won’t make any steps to fix it. I don’t think every man needs to know what he wants to be in life, but a lack of motivation in his personal life will definitely transfer over to your relationship.

10. Instead of breaking up with you, he’ll be a jerk until you break up with him: This is something only a spineless boy does. When the relationship reaches its expiration date, instead of being honest about it with you, he’d rather hang in there until you leave him. Thus, he doesn’t have to be the bad guy, and you’re the one stuck doing his dirty work.

There’s a reason girls tend to date older guys: they’re hoping to find someone who has grown out of these tendencies.


Wanaume Wana Shida! This Kenyan Guy Embarrassed Himself Badly as He Was Seducing a Lady.

$
0
0

Some Kenyan men needs to be taught how to seduce a lady and if you doubt this, see how this idiot embarrassed himself badly as he was trying to sweet talk  a lady.


With such boring vibes, he may die single.

See The Conversation Below:



Kwa Haya Anayonifanyia Shemeji Ananitaka au Mawazo Yangu Tu?

$
0
0
Wadau nipo nyumbani kwa takribani mwezi sasa baada ya kumaliza mkataba wangu na kampuni flani.sasa hapa nyumbani ninaishi na wife na kidi wangu wa miaka 3..na nimekuta wife kamleta mdogo wake wa kike ambaye amemaliza chuo mwaka jana anasubiria ajira,sasa wadau wife wangu ni mfanyakazi so mida mwingi anashinda job,mimi nipo tu home na shemeji yangu,kid anapelekwa shule asubuh mpska jioni.shem huyu wadau ni mrembo sana ana figure matata sana na ni mzuri kwa kweli..yani mitihani ninayoipata ni mikubwa sana..mana nguo anazo vaa zinaonenya umbo lake namba 8 lilivyo,juzi asubuh nilikuwa nimelala akagonga chumbani kwangu anatafuta kitu wakati kavaa khanga tu.jamani naombeni ushauri wenu nifanyaje je?maana uzalendo unaelekea kunishinda asee.maana sasa imefika wakati naliota umbo lake na uzuri wake nimechanganyikiwa.naombeni ushauri weni wadau.

Asanteni

By Fukara

Kwanini "Service Charge" ya TANESCO ni Tatizo Linalohitaji Utatuzi Haraka...!

$
0
0
Najua watu wengi wameandika kuhusu Tanesco na naomba kwa wasimamizi wa Jukwaa hili wauache uzi huu kama ulivyo ili wahusika (ambao nina hakika watausoma) wapate kujua kwa kina.

Kwanza kabisa kwa wale wanaotumia umeme wanajua kwamba tulikuwa na mfumo wa zamani ambao Tanesco walitembelea nyumba zetu na kufanya matengenezo na ukaguzi wa mambo mbalimbali ikiwamo mita za umeme. Sina hakika kama hichi ndio chanzo cha haya makato, lakini ni dhahania yangu kuwa ndizo "service" tulizolipia nyakati hizo.

Sasa ni nyakati mpya. Ukitaka LUKU unalipia, na umeme unaotumia pia unalipia. Sasa service charge ni za nini? Service ipi hasa ambayo unatozwa wakati mwingine mpaka 5000/= au zaidi kwa mwezi?

Hebu tulinganishe makato haya kuona tatizo hili jinsi lilivyo kubwa:
Ukiwa na akaunti ya kawaida benki unalipia kama 700/= kwa mwezi. Ukiwa na akaunti ya kampuni, unalipia kama 7000/= kwa mwezi. Ukiwa na LUKU unalipia kama 5000 kwa mwezi.

Nadhani hata neno LUKU halina maana hapa. Kwa sababu LUKU ni lipia kadri unavyotumia. Naomba niweke mifano miwili tu hai kuonyesha tatizo hili sio dogo kama wengi wanavyolichukulia:
Kuna watu wawili hawakuwepo nyumbani kwa miezi 6. Mmoja alinunua umeme wa elfu 60 na mwingine elfu 50. Wa elfu 60 alipata unit 0 na wa pili alipata unit zisizofika 10.

Kumbuka hawa watu hawakuwa wanatumia umeme husika kwa miezi yote sita. Iko wapi hapo concept ya Lipia Kadri unavyotumia?

Lakini katika makato hayo kuna makato ya REA. Ni makato yenye lengo jema kabisa, kusaidia kupeleka umeme vijijini ili kusukuma maendeleo. Hivi tukiwa wakweli, watu wangapi vijijini wataweza kulipia 5000/= au zaidi kwa ajili ya "service charge"?

Kabla sijamalizia naomba kuelimishwa kwa nini umeme una makato mengi hivi ilhali ndiyo primer energy kwa maendeleo yetu? Kwanza bei ya umeme wenyewe kwa unit ni mkubwa sana (295/= kwa unit). Hapo bado kuna VAT (18%), EWURA (1%), REA (3%) na service charge (5000+/= @month).

Nadhani ni wakati wa kutuondolea haya makato. Mtu anayehitaji Tanesco service na ailipie kwa wakati huo atakapoihitaji. Haya makato ya kiujumla jumla tu yanaumiza sana wananchi. Niisihi serikali iliangalie hili kama moja ya mambo yanayorudisha nyuma sana maendeleo yetu. Umeme ni nishati muhimu sana na hivyo ni vyema ikaangaliwa kwa ukaribu kabisa ili kuleta mapinduzi ya kiteknolojia.

By Stefano Mtangoo

Udaku Special Blog

Wasanii Watoa Mapendekezo Haya Kwenye Kikao Chao cha Leo

$
0
0
Katika Kikao cha Wanamuziki kinachoendelea leo jijini Dar, wasanii wametoa mapendekezo makuu matatu :
(1) kutokuwa na imani na CMEA
(2) kuvunjwa kwa bodi ya COSOTA kutokana na kutokuwa utaratibu mzuri wa kudhibiti na kusimamia mirabaha ya kazi zao na
(3) Radio stations ziendelee kupiga nyimbo zao hadi watapotoa tamko.

Hivyo wameomba rais wa shirikisho (Ado Novemba) kupeleka maombi kwa Waziri mwenye dhamana ‘Mh. Nape Nnauye’ Waziri wa habari, michezo, sanaa na wasanii.

Cloudsfm.com

Mauaji ya ‘Tajiri Mtoto’ Yaendelea Kuzua Utata

$
0
0
Mtandao wa kikundi kinachozalisha pombe kali bandia kinachodaiwa kuwa na uhusiano na baadhi ya watumishi wasiowaaminifu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), unahusishwa na mipango ya kumuua mfanyabiashara Joseph Mahole maarufu ‘Tajiri Mtoto’.

Mfanyabiashara huyo aliuawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia Desemba 30, mwaka jana nyumbani kwake eneo la Katanini, Wilaya ya Moshi Mjini.

Mauaji hayo ambayo yameibua utata hasa baada ya wauaji hao kudaiwa kuondoka na bastola tu iliyokuwa ikimilikiwa na marehemu na hawakuchukua kitu kingine chochote.

Habari kutoka kwa marafiki wa karibu na marehemu, zinadai huenda njama za kumuua zilifanywa na baadhi ya watumishi wa TRA na wafanyabiashara wanaozalisha pombe kali bandia.

Kwani baada ya upekuzi uliofanyika nyumbani kwa Mahole, Polisi waligundua kuwapo kwa malighafi ya kutengenezea pombe kali pamoja na vifungashio vyake. Pia, walizikuta stika zenye nembo ya TRA zinazobandikwa kwenye chupa za pombe kuonyesha kuwa bidhaa inayouzwa imelipiwa kodi.

Baada ya Mahole kuwagomea, watu hao walihofia kama angekamatwa angeweza kuwataja, hivyo wakaamua kumuua.

Hata hivyo, bado utata unaendelea kugubika tukio hilo kwani inadaiwa kuwa marehemu hakuwahi kufanya biashara ya pombe, bali alikuwa akifanya biashara ya vifaa vya ujenzi na alikuwa akisafiri mara kwa mara kwenda China kununua bidhaa hizo.

Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Ramadhan Mungi jana alisema wanaendelea kuchunguza mazingira ya kifo pamoja na vitu vilivyokamatwa baada ya upekuzi kufanyika nyumbani kwa marehemu zikiwamo stika hizo za TRA kama ni za mamlaka hiyo.

“Ni kweli kulikutwa hizo stika na sisi kazi yetu ni kuchunguza ili kubaini zilifikaje nyumbani kwa marehemu,” alisema Mungi.

Meneja wa TRA Mkoa wa Kilimanjaro, Abdul Mapembe alisema wao kama TRA hawajapewa taarifa kamili juu ya kupatikana kwa stika hizo nyumbani kwa Mahole.

“Tunasikia taarifa hizo mitaani, lakini polisi bado hawajatueleza chochote,” alidai Mapembe.

Alisema watawasiliana na Polisi kama inawezekana, watakwenda kuzitambua kama ni mali ya TRA ama la.


Naibu Waziri wa Afya Dkt. Hamisi Kigwangala Akerwa na Kitendo cha Hospitali Binafsi Kumfanyia Vipimo vya Ziada Mgonjwa......Asema ni Matumizi Mabaya Ya Pesa

$
0
0
Serikali imepiga marufuku tabia ya baadhi ya hospitali au taasisi binafsi za afya kuwapima wagonjwa wanaotoka hospitali za Serikali vipimo ambavyo hawakuagizwa kuvipima na madaktari kutoka hospitali hizo kwani kufanya hivyo ni kuiongezea Serikali gharama  zisizo la lazima.

Tamko hilo limetolewa na Naibu  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi  Kigwangala wakati alipofanya ziara ya kutembelea leo kwenye Taasisi ya Saratani ya Ocean Road iliyopo jijini Dares Salaam.

Waziri Kingwangala alitoa agizo hilo baada ya kukutana na mgonjwa ambaye alitakiwa kufanya kipimo cha MRI katika hospitali moja  ya binafsi jijini Dar es Salaam, lakini hospitali hiyo ilimpima mgonjwa huyo vipimo vingine ambayo havikupaswa kupimwa.

Alisema fedha zilizotumika kulipia vipimo hivyo vya ziada vingetumika kununulia dawa na vifaa tiba ambavyo vingetumika kuwahudumia wananchi wengi zaidi.

Aidha Naibu Waziri huyo aliwataka watendaji wa afya kutumia utaalamu  na ujuzi wao  kuaanda mipango ya kuweza kukabaliana na changamoto za sekta ya afya nchini.

Ni lazima tutumia utaalamu tulioupata katika kupunguza shida  za watu katika sekta ya afya. Tumumie elimu tuliyoipata shuleni na vyuoni ili kuboresha maisha ya Watanzania na tumsaidie Rais John Pombe Mafuguli tusisubiri hadi tuambiwe tufanye nini,”alisisitiza.

Mgonjwa huyo  matibabu yake yanalipiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Kitendo cha hospitali hiyo kilionesha kumsikitisha Naibu Waziri huyo kwa kuwa fedha za Serikali ndizo zinazotumika kugharamia vipimo ambavyo, taasisi hiyo haikumwandikia mgonjwa huyo.

Hospitali hii imetumia nafasi hiyo ya kupima mgonjwa huyo vipimo ambayo hakuandikiwa na daktari aliyemwona katika taasisi hii. Chakushangaza baadhi ya vipimo ambayo amepimwa vipo katika taasisi hiyo. Hospitali hii imetumia vibaya mfumo wa mfuko huo kwa kumpima mgonjwa huyo vipimo vya ziada,"alisema Naibu Waziri Kigwangala.

 Aliwataka watendaji wa afya kuhakikisha wanawapeleka wagonjwa wanaotakiwa kupimwa vipimo vya MRI na CT- Scan katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH) kwa kuwa hospitali hiyo ina vifaa vya kisasa na vinafanya kazi  vizuri kwa gharama nafuu.

 Naibu Waziri huyo aliagiza uongozi huo kusitisha malipo ya vipimo hivyo vya ziada kwa kushirikiana na mfumo huo wa NHIF.

Sitisheni malipo ya vipimo vya ziada katika hospitali hiyo, mgonjwa ni wa taasisi hii anaingiliwa na taasisi nyingine kwa kupimwa vipimo vingine ambavyo havikupaswa kupimwa, hivi ni vijipu vidoovidogo vinatumbuliwa hapahapa,” alisema Waziri huyo.

 Katika ziara hiyo Naibu Waziri huyo alielezwa kwamba taasisi hiyo inakabiliwa na changamoto ya vipimo vya ugunduzi wa saratani na tiba ya satarani, dawa, ambapo alisema atashirikiana na uongozi ili kuweza kukabiliana na matatizo hayo.

Pia aliutaka uongozi wa taasisi hiyo na watendaji wa afya pamoja na wizara kufanya kazi kama timu ili kuweza kutatua changamoto zilizopo.

Afanyayo Magufuli Siyo Mizani na Kumkomoa Kikwete ni Wajibu Wake

$
0
0
Wale watu wenye umri mkubwa wanajua kuwa Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere alikuwa na uhusiano mbaya na Shirika la Fedha la Dunia IMF na Benki ya Dunia akiwa madarakani.

Alipoingia madarakani, Ali Hassan Mwinyi aliamua kufuata masharti yaliyowekwa na mkubwa huyo. Hali ya uchumi ikawa mbaya. Hata hivyo, Mwalimu aliwafanya Watanzania kuwa kitu kimoja.
Mzee Mwinyi enzi hizo alipolaumiwa na baadhi ya watu akasema kwamba ‘kila zama na kitabu chake.” Nyerere hakuwa mkamilifu kwa asilimia 100, Mwinyi na Benjamin Mkapa vivyo hivyo.
Bila shaka, Jakaya Mrisho Kikwete naye si malaika na alikuwa na upungufu wakati wa miaka 10 ya utawala wake. Ukosoaji wowote dhidi ya Kikwete unakubalika ingawa nitatofautiana na kinachoendelea sasa .

Kwanza, wakosoaji wa Kikwete wanafanya hivyo kwa kumlinganisha na Magufuli jambo ambalo ni kosa kwa sababu Magufuli alikuwa na maono yake wakati akitaka urais na anayofanya sasa ni wajibu wake na ni kile anachokiona ni sahihi kwa taifa letu kusonga mbele. Kama kila anachofanya kitatafsiriwa kuwa ni kijembe dhidi ya mtangulizi wake, basi hilo ni kosa.

Tangu wakati wa kampeni, Magufuli alionesha dalili ya kuwa hivi alivyo. Wakati CCM kikimpa tiketi ya kuwania urais, kilijua kinampa mtu wa namna gani, kilijua atakuwa mkali kwa wavunja sheria na alikuwa akisema hilo waziwazi.

Katika hali ya kawaida, si rahisi kwa mtu kuelewa kwa nini Kikwete alikuwa na baraza la mawaziri la watu 60 kwenye awamu yake ya kwanza ya urais. Tukumbuke kuwa aliingia madarakani wakati kukiwa na mpasuko uliosababishwa na kundi la mtandao lililomsaidia aingie madarakani.
Hivyo basi, Kikwete fikra yake ya kwanza baada ya kuwa rais ilikuwa ni kuhakikisha kuwa kila kundi ndani ya chama linawakilishwa ndani ya serikali yake.

Jakaya-Kikwete2Niwakumbushe kuwa hata Nyerere wakati anaunda serikali ya mwanzo alihakikisha baraza la mawaziri linakuwa na Waafrika, Wazungu, Wahindi, Waislamu, Wakristo, yaani walau kila kundi la kijamii.

Magufuli alipoteuliwa kupeperusha bendera ya CCM kwenye kuwania urais alikuta chama kimeungana dhidi ya mgombea wa upinzani, Edward Lowassa.

Rais Magufuli ana historia tofauti na JK. Yeye ametokea kwenye taaluma ya ualimu. Kazi kubwa ya mwalimu ni kuhakikisha anamsaidia mwanafunzi kufikiri hadi kufikia mwisho wa uwezo wake wa kiakili kwa kushauri, kuelekeza, ukali na kadhalika na ndivyo anavyofanya sasa.

Naamini Magufuli atafanya kila analoweza kuhakikisha Tanzania inafikia anapofikiria kufikia na ili kufika hapo, atatumia kila aina ya mbinu alizojifunza kama mwalimu na pia kama mwanasiasa mkongwe kwani alikuwa waziri kwa miaka 20.

Kutokana na ukweli huo ndiyo maana, sioni busara ya kuwafananisha Magufuli na Kikwete kwa kuwatia kwenye mizani. Tukumbuke kuwa Kikwete aliikuta Tanzania ikiwa moja na akaiacha ikiwa moja na alikuwa karibu na wananchi wake na aliwapenda.

Ili kumsaidia Magufuli katika ndoto zake ni vema kila Mtanzania kueleza yalipo matatizo kwa kutumia njia yoyote, hilo litatusaidia kututoa hapa tulipo.
Jipu limepasuka, siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya Januari 6, Ikiwemo ya Wema Sepetu Kutumbua Mil 300 za Mbunge

$
0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya Januari 6, Ikiwemo ya Wema Sepetu Kutumbua Mil 300 za Mbunge

Udaku Special Blog
Viewing all 104803 articles
Browse latest View live




Latest Images