Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live

Dili la Mbwana Samatta Kuhamia Klabu ya Genk Laipa Ulaji wa Mamilion Timu ya Simba....

$
0
0
Mbwana Samatta
BAADA ya dili la mshambuliaji, Mtanzania, Mbwana Samatta kujiunga na Klabu ya Genk ya Ubelgiji kutimia, habari nzuri kwa klabu yake ya zamani ya Simba ni kuwa inatarajia kuvuna Sh milioni 200 kutokana na kipengele ambacho kiliwekwa na uongozi wa timu hiyo wakati unamuuza kwa Klabu ya TP Mazembe ya DR Congo, miaka mitano iliyopita.


Samatta ambaye anashikilia Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika kwa Wachezaji wa Ndani, wiki iliyopita alitua rasmi ndani ya Genk inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji kwa mkataba wa miaka minne akitokea TP Mazembe huku akikabidhiwa jezi namba 77.

Kipengele ambacho uongozi wa Simba wa wakati huo uliokuwa unaongozwa na mwenyekiti wake, Ismail Aden Rage, kinasema kuwa klabu hiyo itapata asilimia 20 za fedha ambazo mshambuliaji huyo atauzwa kwenda klabu yoyote akitokea Mazembe.

Habari za uhakika ambazo Championi Jumatatu linazo ni kuwa, Samatta ameuzwa kutoka Mazembe kwenda Genk kwa euro laki saba (zaidi ya sh bilioni moja za Kitanzania) ambazo kwa kipengele walichokiweka Simba cha asilimia 20, basi watapata milioni 200.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Said Tully ameliambia Championi Jumatatu, kuwa wanatambua kuwa wao wanatarajia kupewa fedha hizo kutokana na mkataba ambao waliingia na Mazembe.

“Tunajua kuwa baada ya Samatta kuuzwa kwenda Genk sisi tunapata asilimia 20 za fedha zitakazopatikana kutokana na makubaliano maalumu yaliyowekwa wakati kijana huyo anaingia mkataba na timu ya TP Mazembe.

“Kwa sasa tumeshaanza kufanya mipango kuona kuwa tunafuatilia fedha hizo na kuzipata kwa wakati ambapo zitakuja kuweka sawa mambo mengine,” alisema Tully.

Tafuteni Umaarufu Bungeni Kwa Kujenga Hoja si Vurugu

$
0
0

Ni wiki nyingine muhimu katika ulingo wa siasa za hapa nchini. Mkutano wa pili wa Bunge la 11 unatarajiwa kuanza tena. Tunasubiri kushuhudia kasi ya Bunge hili ndani ya Serikali ya Awamu ya Tano. Bila shaka litaendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya kaulimbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’.

Matamanio yangu ni kuona kasoro zilizowahi kujitokeza katika mikutano iliyopita, hususani vurugu zinazoambatana na zomea zomea, vijembe, matusi na kususa, zikiwekwa kando katika Bunge hili. Naomba Mungu, Bunge hili lenye watu wa rika na taaluma mbalimbali, lioneshe nidhamu, weledi, busara na utendaji uliotukuka.

Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) , wabunge wenye umri kati ya miaka 21 na 35 wako 47, wenye umri kati ya miaka 36 na 50, wako 112 na walio na umri wa zaidi ya miaka 51, wako 91.Natamani damu changa iliyoingia katika Bunge la sasa, iwe chachu ya kufanya kile ambacho wananchi wamewatuma wawafanyie. Kwa kuwa tunaambiwa ‘utu uzima dawa’, pia wabunge wenye umri mkubwa, wawe chachu siyo tu ya utendaji uliotukuka, bali pia wawe mfano bora wa maadili na nidhamu bungeni.

Idadi kubwa ya vijana iwe chachu ya kufanya vizuri na iondolee jamii dhana potofu iliyojengeka kwamba wanaweza kugeuza Bunge uwanja wa kujipima ubavu wa kuongea badala ya kujenga hoja.Upo ukweli kwamba, baadhi ya wabunge bila kujali rika, wamekuwa wakitafuta sifa na umaarufu kwa gharama yoyote ikiwemo kufanya vitendo visivyofaa bungeni.

Matokeo yake, huligeuza uwanja wa mapambano, jazba, mipasho na matusi. Kwao kutukana, kubeza na kudhalilisha wengine, huchukulia ndiyo umahiri wa siasa jambo ambalo si sahihi. Huwa inashangaza kuona mtu mzima, msomi, mwenye familia na aliyeaminiwa na wananchi, anafanya mambo ya kitoto na ya ajabu.

Ukiuliza sababu za kufanya hivyo, utajibiwa eti hizo ndizo siasa na sifa ya mabunge ya mfumo wa vyama vingi! Baadhi ya wabunge huona sifa kutajwa tajwa bungeni kwa kuonywa na Kiti cha Spika au na wabunge wenzake.

Wengine huona sifa kuondolewa bungeni au kutakiwa kuondoa kauli za kudhalilisha dhidi ya wenzao. Bahati mbaya, chini ya siasa za vyama vingi, wabunge wa aina hiyo wakibanwa na kanuni, hutafuta huruma kwa kuhamishia suala hilo kwenye ushabiki wa vyama.Kwa mfano, unakuta mbunge wa chama tawala anatoa lugha isiyo ya staha dhidi ya upande mwingine na wenzake hawako tayari kumkosoa. Vivyo hivyo wa upinzani, anapofanya hivyo, anabaki akikingiwa kifua na wabunge wa kambi yake.

Jamii pia huziba macho na masikio juu ya utovu wa mbunge husika, na kuchukulia suala hilo kwa mtazamo wa siasa za vyama.Wakati macho na masikio ya Watanzania yakielekezwa bungeni mjini Dodoma, chonde Kiti cha Spika kiwe macho na wabunge wanaochafua chombo hicho kwa kusaka sifa na umaarufu kwa utovu wa nidhamu.

Kiti cha Spika kihakikishe kanuni na taratibu za Bunge zinaheshimiwa na kila mmoja bila kujali chama anachotoka wala nafasi yake. Spika adhibiti mihemko inayoambatana na lugha zisizo za staha ndani ya Bunge kwa kuhakikisha wanaokwenda kinyume wanaadhibiwa kwa mujibu wa kanuni.

Ingawa wabunge watakuwa wamepewa semina elekezi, Kiti cha Spika kisichoke kuendelea kuwafunda wote wapya na wa zamani juu ya heshima, nidhamu, uadilifu katika kuwasilisha ujumbe bungeni kuepuka kuligeuza gulio. Kiwafunde watambue kwamba wao ni viongozi wa nchi ambao hawakufika mahali hapo kwa bahati mbaya, bali wameaminiwa na umma wa Watanzania. Spika asiogope kutumia rungu lake kwa yeyote atakayekwenda kinyume na kanuni.

Rungu hilo litue kwa yeyote bila kujali chama, umri, jinsi na wadhifa wake . Kiti cha Spika kihakikishe Mkutano huu wa Pili wa Bunge la 11, hauwi mwendelezo wa jukwaa la uchaguzi . Nafahamu wazi kwamba, Spika atakapoamua kushusha rungu lake kwa mujibu wa kanuni na taratibu, wapo watakaoona kana kwamba wanaonewa. Lakini Kiti, chini ya Spika Job Ndugai, kisiangalie uso wa yeyote. Atakayepanda vurugu na lugha zisizo na staha bungeni, naye avune adhabu stahiki.

Yale mazoea ya kusema wabunge (hasa wapya) bado wanajifunza kwanza, yasipewe nafasi tena kwani ndicho chanzo cha matatizo. Kanuni za Bunge zizingatiwe tangu siku ya kwanza. Zikitumika vizuri, wabunge wataka sifa, umaarufu na wanaojifanya wapambanaji kwa kufanya vitendo visivyo na staha, hawatapata nafasi kuvionesha. Nasisitiza, umma wa Watanzania unataka maendeleo ndiyo maana ukawatuma bungeni. Wanataka kusikia hoja zenye maslahi kwao.

Kwa upande wa wabunge wasomi, onesheni uwezo wenu kwa kutoa hoja na kuuliza maswali yenye ‘akili’. Hata wabunge wasio na kisomo, wajisomee kuepuka kupoteza muda wa vikao kwa maswali mepesi mepesi. Kwa ujumla, umaarufu wa wabunge unapaswa utokane na hoja wanazotoa na si kwa kuwa vinara wa vurugu na vitendo vya ajabu bungeni.

Anna Makinda na Zungu Tutawakumbuka Daima Kwa Kinachoendelea Bungeni Sasa

$
0
0
Binafsi hua sipendi kummwagia mtu misifa hovyo hovyo lakini Leo hii acha hawa watu nisiwanyime haki zao pamoja na mapungufu walivyokua nayo kama wanadamu wengine.Ni wanasiasa wazoefu, watulivu, wastahamilifu na wenye kuongozwa na busara na hekima zaidi.Hawa viongozi waliliongoza bunge kwa ubunifu wa hali ya juu sana mpaka kufikua kujenga heshima ndani ya bunge.

Ni viongozi ambao walitambua kwamba kua njia pekee ya kuendesha mambo vizuri ni mawasiliano mazuri ama maridhiano katika pande mbili zinazokinzana! Ni viongozi waliojua kua utatuzi pekee wa migogoro ndani ya bunge ni majadiliano inapotokea kutokuelewana baina ya pande mbili kinzani, ni viongozi waliosoma vizuri mwenendo wa bunge na mazingira yaliyokuepo na wakati wake pia badala ya kutumia ubabe.

Ndio kuna mahali walijaribu kutumia ubabe lakini ni pale ambapo mambo yalionekana kua magumu sana kufikia kukosa maamuzi mengine zaidi ya kutumia nguvu kiasi.Ukiwa kiongozi bila kuangalia na kuwasoma surbodinates wako, bila kusoma wakati, bila kusoma mazingira uliopo kwa hakika uongozi utakushinda! Utatumia sana ubabe lakini lakini itafika mahali utashindwa na dhamira yako itakusuta kufikia kuikimbia nafasi yako ya uongozi.

Ni washauri tu ndugu zangu Chenge, Ndungai pamoja na Dkt Tulia kwamba bado ni mapema sana kwao watumie muda huu kujirekebisha mapema wasianze vibaya! Watumje zaidi njia ya majadiliano kila inapotokea kutoelewana baina ya pande kinzani ndani ya bunge, watumishi kamati za bunge kurekebisha mambo mfano kàmati ya uongozi na kamati ya maadili. Inapotokea serikali inakosolewa wachukulie kua ndio kazi ya bunge kufanya hivyo kuliko kutanguliza ukada zaidi, unapokua kiongozi wa pinde mbili kinzani lazima uwe neutral bila kupendelea upande wowote.

Waliovamia Shamba la Sumaye Watii Amri ya Paul Makonda

$
0
0
Paul Makonda
Wananchi wanaodaiwa kuvamia shamba la Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye, lililopo Kinondo, mtaa wa Mji Mpya, kata ya Mabwepande, Manispaa ya Kinondoni, wametii agizo la Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (pichani), la kuwataka kuacha kuendelea na ujenzi katika maeneo waliyogawiana.

Katikati ya wiki iliyopita, mkuu huyi wa wilaya alifanya mkutano na wananchi hao pamoja na Sumaye na kuwataka kutoendelea na ujenzi katika maeneo hayo hadi baada ya wiki mbili atakapokuwa amekutana na viongozi kwa ajili ya kuangalia jinsi ya kuwasaidia wananchi hao.

Pia Makonda alitaka nyumba zote zilizokwishajengwa katika eneo hilo zihesabiwe halafu apelekewe orodha ya nyumba hizo pamoja na wamiliki wake.

Wananchi hao wakizungumza mwishoni mwa wiki katika mkutano wa kujadiliana kuhusu agizo la Makonda, walisema hawataendelea na ujenzi wa nyumba zao hadi hapo watakapopata maelekezo mengine kutoka kwa mkuu huyo wa wilaya kama alivyowataka.

Mmoja wa viongozi wa wananchi hao, Athuman Hassan, alisema wanaheshimu kauli ya mkuu wa wilaya, hivyo hawataendelea na ujenzi wa nyumba zao hadi hapo watakapopata maelekezo mengine.

"Sisi tunaheshimu maelekezo ya mkuu wetu wa wilaya, tumeamua kusimamisha ujenzi wa nyumba hadi hapo tutakapopata maelekezo mengine, hivyo wananchi mnatakiwa kuwa wavumilivu katika kipindi cha wiki tulizoambiwa nina imani na DC wetu atatusaidia kama alivyotuahidi, " alisema Hassan.

Aidha, aliwataka wananchi ambao wameshakamilisha ujenzi wa nyumba zao na kuanza kuishi kuendelea kuishi kwa amani na utulivu katika nyumba zao hizo.

"Wenzetu ambao mmeishakamilisha ujenzi wa nyumba zenu endeleeni kuishi kwa amani na utulivu wakati tukisubiri maelekezo mengine kutoka kwa mkuu wetu wa wilaya kwa ajili ya ambao tulikuwa

Ikulu Yafafanua Magufuli Kumtuma Samia Mkutano wa Marais wa Afrika.

$
0
0
Rais Dk. John Magufuli ameendelea kukacha safari za nje ya nchi, baada ya jana kumtuma Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, kumwakilisha katika Mkutano wa wakuu wa Nchi za Afrika unaojadili masuala ya usalama barani Afrika, mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Hata hivyo, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa, aliieleza Nipashe kuwa  kutumwa kwa Makamu kwa Rais ni sawa na uwapo wa Rais katika mkutano huo.

Alisema Rais anapokuwa hayupo nchini, Makamu wa Rais ndiye anayeongoza nchi na kusema kuwa Rais Magufuli ana miaka mitano ya uongozi mbele, hivyo kuna mikutano mingi atakayotakiwa kuhudhuria.

Alisema serikali inawatendaji wengi, hivyo si kila mkutano Rais anatakiwa kwenda.

“Katika serikali kuna Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na mabalozi, hivyo si kila mkutano Rais aende. kuna  watendaji wengi,” alisema Msigwa.

Msigwa alisema itakapotokea Rais Magufuli anasafiri kwenda kuhudhuria mkutano wowote nje ya nchi, Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu itatoa taarifa kwa umma.

Akiwa nchini humo katika mkutano huo wa masuala ya usalama barani Afrika, Samia alikutana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Viwanda la Umoja wa Mataifa (UNIDO), Li Yong, na kuzungumzia juu ya kuendeleza ushirikiano kwenye maendeleo ya viwanda utakaotolewa na UNIDO kwa serikali ya Tanzania na kuwa moja ya nchi za viwanda kuanzia mwaka 2015/2020
Tangu aingie madarakani Novem,ba 5, mwaka jana, Rais Magufuli  amekuwa akikacha safari za nje ya nchi kuhudhuria mikutano na badala yake amekuwa akiwatuma viongozi wa kiserikali kumwakilisha.

Mojawapo ya safari ambazo hakwenda ni Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Madola (CHOGM), uliofanyika visiwa vya Malta Novemba 27, mwaka jana.

Rais John Pombe Magufuli
Katika mkutano huo, Rais alimtuma aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Peter Kallaghe, kumwakilisha akiwa pamoja na maofisa wengine watatu.

Pia Novemba 29, mwaka jana, Rais Magufuli alitakiwa kuwapo Paris, Ufaransa, katika mkutano wa kimataifa wa 21 kujadili mabadiliko ya tabianchi duniani (COP21) ambao takriban wakuu wa nchi 150 kutoka  nchi 195 walishiriki, wakiwamo marais Barack Obama wa Marekani na Xi Jinping wa China.

Desemba 5, 2015, Rais Magufuli hakwenda Johannesburg, Afrika Kusini kulikokuwa na mkutano wa tano wa wakuu wa nchi za Afrika na Rais wa China, Xi Jinping, kupitia Jukwaa la Nchi za Afrika na China (FOCAC). Katika mkutano huo, Rais Magufuli aliwakilishwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.

Wakati akizindua Bunge, Rais Magufuli alisema safari za nje zimeligharimu taifa Sh. bilioni 356.3, ambazo kati yake Sh. bilioni 183.1 zilikuwa kwa ajili ya tiketi za ndege, Sh. bilioni 68.6 ziligharamikia mafunzo na Sh. bilioni 104.5 zilikuwa za posho, ambazo zingeweza kujenga kilometa 400 za barabara ya lami.

UHUSIANO WA TANZANIA NA AU
Waziri Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), sasa Umoja wa Afrika (AU).

Miongoni mwa viongozi 30 ambao walikuwa waasisi wa OAU ni Hayati Mwalimu Julius Nyerere. Pia katika  bara la Afrika, miongoni mwa nchi zinazoheshimika kutokana na mchango wake katika ukombozi wa bara hilo ni Tanzania kwa kusaidia mataifa mengi kupata uhuru na kujitawala.

Aidha, Nyerere kupitia OAU, alipewa heshima ya pekee na kuenziwa kwa kuamua Jengo la Baraza la Amani na Usalama la Umoja huo kuitwa Julius Nyerere.

Kadhalika, Kamati ya Ukombozi Kusini mwa Afrika iliyokuwa chini ya OAU, makao makuu yake yalikuwa Dar es Salaam na  Katibu Mtendaji wake alikuwa Brigedia Jenerali Hashim Mbita (sasa marehemu) ambaye alikuwa Mtanzania.

Licha ya rekodi ya Rais Magufuli ya kutosafiri kwenda Ulaya na nchi nyingine za nje ya Tanzania hata mara moja tangu aingie madarakani kuwavutia wengi, baadhi ya watu waliozungumza na Nipashe wamedai  hatua hiyo ni nzuri.

Mkufunzi wa Chuo cha Mlimani kilichoko Mbezi kwa Musuguri jijini Dar es Salaam, Vedasto Malima, alisema Rais Magufuli anafanya jambo la maana na la kuigwa kwa watendaji wengine.

Alisema Rais Magufuli ameonesha nia na dhati ya kuwasaidia Watanzania kuliko kupenda kusafiri nje ya nchi kama watangulizi wake walivyofanya.

Mtuhumiwa wa Kutorosha Wanyamapori Alikuwa na Vibali vyote Halali Kutoka Serikalini

$
0
0
RAIA wa Pakistan, Kamran Ahmed, aliyetuhumiwa na kisha kutiwa hatiani katika kashfa ya kutorosha wanyamapori hai 130 wa aina 14 tofauti, alikuwa na vibali vyote halali kutoka serikalini, Raia Mwema linaweza kuthibitisha.

Mpakistan huyo alitoweka akiwa chini ya dhamana, akahukumiwa bila kuwapo mahakani na sasa imedhihirika kwamba kutoweka kwake kulikuwa ni kuficha ushiriki wa vigogo katika mpango wa kuuziana wanyama hao.

Uchunguzi wa muda mrefu wa Raia Mwema, umebaini kwamba Kamran Ahmed alikuwa na vibali vyote muhimu vya kusafirisha wanyama hao pamoja na hati ya makubaliano (MoU), kati yake na Idara ya Wanyamapori ya Tanzania.

Wanyama hao hai wenye thamani ya shilingi milioni 170 za Tanzania walisafirishwa Novemba 26, 2011, kwa Ndege ya Jeshi la Qatar (Emir Air force) kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Hati ya makubaliano (MoU) ambayo Raia Mwema inayo nakala yake, inaonyesha kuwa kulikuwa na makubaliano kimaandishi baina ya Kamran, kama Wakala wa Halmashauri ya Jiji la Karachi nchini Pakistan (CDGK) na Erasmus Tarimo, kama mwakilishi wa Serikali ya Tanzania.

Tarimo alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Wanyamapori kati ya mwaka 2007 na 2011, kabla ya kustaafu kwa mujibu wa sheria. Alitia saini hati hiyo Mei 28, 2009 kwa niaba ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

Aidha, imebainika kuwa kabla kutiwa saini makubaliano hayo, ofisa wa Serikali ya Tanzania aliyetambulika kwa jina moja la Midele alikwenda Karachi-Pakistan kukagua bustani ya kutunzia wanyama (zoo) ambako wangepelekwa wanyama hao kutoka Tanzania.

Kwa mujibu wa picha zilizopatikana kutoka vyanzo vya uhakika vya habari vya gazeti hili, Midele anaonekana akiwa mbele ya lango la kuingilia katika bustani wakati nyingine zinamwonyesha akiwa na maofisa kadhaa wa Serikali ya Pakistan katika “miondoko” tofauti.

Taarifa zinadai kuwa Midele alikwenda Pakistan kwa kulipwa gharama zote na Kamran, ikiwa ni pamoja na posho za kujikimu, nauli ya ndege na gharama ya malazi. Baada ziara hiyo, hati hiyo ya makubaliano ndipo ilipotiwa saini.

Hati hiyo yenye kurasa nne ina vipengele 16 na imeainisha kuwa wanyama watakaokamatwa na kusafirishwa hawatatumika kwa shughuli za kibiashara.

“Malengo ya Hati (MoU) hii ni kujulisha ridhaa ya Wizara ya Malialisili na Utalii kuipatia Halmashauri ya Jiji la Karachi nchini Pakistan (CDGK) tembo watoto wanne (4), kwa ajili ya Zoo (bustani ya kuhifadhia wanyama) ya Karachi na hifadhi, kwa madhumuni ya kutoa elimu na uhifadhi,” inasema sehemu ya kwanza ya hati hiyo.

Hata hivyo, haikufahamika mara moja iwapo bustani ya wanyama ya Karachi ni ya kibiashara au kwa ajili ya huduma za kijamii.

Nyaraka zaidi zinabainisha kuwa katika kashfa hiyo, maofisa wa Idara ya Wanyamapori Tanzania ndiyo waliohusika kuwakamata twiga hao na wanyama hai wengine, wakilipwa posho na Kamran.

Aidha, pia vitendo hivyo vimefanyika kinyume cha Sheria ya Tanzania ya Wanyamapori (Wildlife Conservation Act) ya mwaka 2009, ambayo inazuia biashara ya wanyamapori hai.

Sura ya 5 kifungu cha (2) kipengele (a) (b) na (c) kinafafanua kuwa mtu au taasisi itaruhusiwa kukamata mnyama wa aina yoyote kwa sababu tu za utafiti, elimu, kiutamaduni na si kwa sababu za kibiashara.

Uchunguzi unaonyesha kuwa katika kipindi chote wakati biashara hiyo ikifanyika nyaraka za serikali zilitumika tu kwa malengo ya kujikinga na mkono wa sheria pale mambo yatakapoharibika.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari, Kamran alikuwa anawalipa maofisa wote wa serikali waliofanikisha mipango hiyo kwa fedha za kigeni kati ya dola za Marekani 20,000 na 50,000 kama “huduma ya kuwanunua” wanyama hao.

“Katika kipindi cha miaka miwili kabla ya kufichuliwa kwa kashfa hiyo maafisa wa Idara ya Wanyapori walipokea fedha kutoka kwa Kamran kama rushwa na wao walimtengenezea nyaraka za kiserikali ili wanyama wafike salama huko sokoni,” anadai mmoja wa watu wa karibu wa Kamran.

Kwa mujibu msiri huyo, Kamran alikuwa na mtandao mpana wa usafirishaji wanyama hai duniani kiasi cha kuwekwa katika orodha maharamia 139 waliokuwa wanatafutwa na Polisi wa Kimataifa (Interpol) katika nchi 36 dunia kote.

Operesheni ya kuwatafuta watu hao ilipewa jina la “infra terra” na ilizinduliwa Oktoba mwaka 2014 na Kamran alikuwa mtu wa 17 katika orodha hiyo.

Mtandao wa Kimataifa wa Interpol unamtaja Kamran kuwa ni raia wa Pakistani, aliyezaliwa mwaka 1985, anatafutwa na Serikali ya Tanzania kwa kosa la kusafirisha wanyama hai kutoka Tanzania kwenda Qatar. Interpol wanaeleza kuwa Kamran alilipa gharama za usafiri wa ndege ya kijeshi iliyopakia twiga na swala kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwenda Qatar.

Kwa mujibu wa Mfuko wa Wanyamapori Duniani (World Wildlife Fund - WWF), utoroshaji wa wanyama hai ni biashara kubwa inayoendeshwa na mtandao hatari wa kimataifa.

Mtandao huo husafirisha wanyama hai na viungo vya wanyama kama ilivyo kwa dawa za kulevya na silaha.
Kutokana na jinsi biashara hiyo inavyoendeshwa, mfuko huo unakiri kuwa ni vigumu kujua kwa uhakika gharama halisi ya biashara hiyo haramu.

Lakini wataalamu mbalimbali wanakadiria thamani ya biashara hiyo kuwa Dola za Kimarekani bilioni 20, na kuifanya kuwa ni biashara haramu ya nne inayoingiza pesa nyingi duniani, ikitanguliwa na dawa za kulevya, noti bandia na usafirishaji wa binadamu.

Source: Raia Mwema

Dk. Shein: Ni hiyari chama kushiriki au la uchaguzi wa marudio Zanzibar

$
0
0

Wakati Chama cha Wananchi (CUF), kikiwa kimetangaza rasmi kutoshiriki uchaguzi mkuu wa marudio visiwani hapa, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, amesema suala la chama cha siasa kushiriki au kutoshiriki ni jambo la hiyari katika misingi ya demokrasia.

Kauli hiyo aliitoa alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara uliyofanyika katika Uwanja wa ndani wa Makao Mkuu ya CCM Kisiwanduwi katika uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi.

Alisema Uchaguzi Mkuu wa marudio Zanzibar hakuitishwa na CCM, CUF au Chadema, bali Tume ya Uchaguzi ndiyo walioitisha baada ya kujiridhisha kuwa Uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka jana ulikuwa na kasoro.

Alisema mujibu wa Katiba ya Zanzibar na Sheria ya uchaguzi namba 11 ya mwaka 1984, Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec)ndiyo yenye mamlaka ya kuratibu na kusimamia uchaguzi Zanzibar.

“CCM tumeshakubali kushiriki uchaguzi wa marudio na suala la kushiriki au kutokushiriki ni jambo la hiyari katika demokrasia,”alisema Dk. Shein.

Alisema uchaguzi wa Zanzibar umelazimika kurudiwa ili kukidhi matakwa ya demokrasia na kuwataka wananchi kutumia nafasi hiyo kukamilisha haki yao ya kuchagua viongozi wanaowataka.

Aidha, Dk. Shein aliwataka wananchi kudumisha na kuimarisha amani ya Zanzibar lakini alionya serikali haitofumbia mtu yeyote ambaye atajaribu kuvuruga amani na mshikamano kwa wananchi wake.

Alisema vyombo vya dola vipo makini kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarishwa na kuwataka wananchi kuendeleza utamaduni wa Zanzibar wa kuiishi katika mazingira ya amani kwa manufaa ya Zanzibar na watu wake.

Alisema kurejewa kwa uchaguzi Zanzibar isiwe sababu ya kuchafua amani ya nchi na kuonya kuwa kwa mwenye ubavu ajaribu kufanya na kwamba atakiona cha moto.

Dk. Shein alisema uchaguzi utafanyika kwa amani na salama na kwamba sio kweli kama kutakuwa na sitofahamu kama inavyodaiwa na watu na kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini.

Upande wake mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, alisema wana-CCM wasibabaike na kauli ya CUF ya kutoshiriki uchaguzi wa marudio wa Machi 20, mwaka huu.

Ray C Awashukia Global Publishers Kwa Kutoa Habari Amerudia Madawa ya Kulevya..Adai Atapambana Nao Mahakamani

$
0
0
Yule mdada kiuno bila mfupa! Rehema Chalamila a.k.a Ray c Ameahidi kupambana na Global publishers mahakani kwa madai ya kuzushiwa habari katika ukurasa wake wa insta ameandi haya

"Seriously kwa kweli huwa naumia sana sana kuona binadamu mwenzangu anadiriki kuni niharibia jina langu ili yeye apate kula! Hamjui mnaniathiri kiasi gani na hizi habari zenu? Hivi unadirikije kuandika usengwile kama huu bila hata ya aibu bila hata ya picha ya kuisapoti habari hiyo yaani ni ujinga ujinga tuu umeunganishwa na picha yangu yaani bila hata woga mmechukua picha yangu kwenye insta page yangu tayari mmeshapata story ilimradi mniharibie tu maisha yangu nyie mpate pesa mimi nife maskini! Kama kweli mnauhakika na mlicho kiandika kwanini hamkuweka picha yangu ni kivuta hayo maunga badala yake mnaweka picha ya kituo cha mkunguni cha daladala,mmepiga picha ya kituo cha daladala cha mkunguni bado mkaona haitoshi mkaaingia kwenye page yangu insta mkachukua picha nilio jipiga mimi mwenyewe na kuitungia story kulichafua jina langu tena ndio kwanza nahangaika kurudi kwenye kazi yangu haki amungu sijawahi kusikia nyie global mmeandika story kuhusu faundation yangu na mambo mazuri nilio fanya japo mnajua kabisa nimewaokoa vijana zaidi ya sabin kutoka kwenye madawa ya kulevya na wanatumia methadone na wako fit je mnajua hilo? Sijawahi ona mmenichangia hata nauli ya kwenda kila siku kwny dose japo kila siku inatakiwa niende na ukikosa ni mateso makali huu ni mwaka wa tatu natumia dawa tuu its not easy ni mateso makalo lakini am fucking hard working kuhakikisha sikosi kwenda kuchukua dawa! Mimi ni mwanamke jasiri naparangana na haya madawa kuhakikisha nayapinga vikali na kamwe sitarudi nyuma hizi nuksi mzipeleke kwenye familia zenu! WEWE SHIGONGO UNAMKOSEA SANA MUNGU UNAJIFANYA MLOKOLE Lakini kazi yako ni kuharibia maisha ya wengine unasahau kuwa malipo ni hapa hapa duniani,mimi ni kapuku tu sina mbele wala nyuma mbele yako lakini bado unanichimbia kaburi angali ni mzima na wewe Mayasa Marwata ni mpuuzi usie jua kazi yako nimesoma habari yako nimejua ni mvivu wa kufuatilia habari chimbo langu la unga lajulikana sasa kwanini hukunipiga picha nikiwa navuta unga unaenda kupiga picha kituo cha daladala bwege wewweee! NITAPAMBBA NA NYIE MAHAKAMANI"Ray C

KIMENUKA..Mume wa Zari na Wenzake Wakamatwa Afrika Kusini

$
0
0
Kuna Habari Kuwa Mme wa zari ambaye pia ni mganga wa kienyeji (sangoma) amekamatwa huko South Africa pamoja na wenzake kwa sababu ambazo hazijulikani ila najua umeshajua ni kwa nini?

From the Source;
Reliable sources have told us that first to be arrested was Lawrence Kiyingi aka King Lawrence.

Other members of The Rich Gang include; Ivan Semwanga, Shafiq Katumba (Katsha) and Eddie Kyeyune (Ed Chuene) among others.

“King Lawrence was arrested early this week. However; the reason for his arrest is scanty” a source privy to this information intimated to us.

Much as we are informed that only Lawrence Kiyingi aka King Lawrence has been arrested, fears are that all other members of ‘The Rich Gang’ have also been arrested on the same offense.

“These guys stay together and do similar jobs. They have a lot in common not only here in Uganda, but in South Africa and so, if King Lawrence is arrested, so are others.

Interpol Director Asan Kasingye in an interview with this reporter on Thursday confirmed the arrest of Lawrence Kiyingi but quickly said the reason for his arrest is being gathered.

“Somebody called me early last week and told me King Lawrence has been arrested” He confirmed adding, “We have sent information to our colleagues in Pretoria to find out the truth of his arrest in South Africa”

He however added: “There could even be more arrested along with King Lawrence”

Kasingye also noted that the arrest of The Rich Gang members-does not get him by surprise regarding the numerous accusations on the quadruple at his desk both from South Africa and within by members of the public.

“It won’t come to me as a surprise. I have these accusations from South Africa and other members of the public here in Uganda but i want to get proper facts about their arrest”

Nikifa Nichomwe Moto Sihitaji Kuwa Binadamu Tena Nataka Kuwa Malaika - Afande Sele

$
0
0
Msanii Afande Sele ambaye anawakilisha mkoa wa Morogoro katika muziki amefunguka na kusema kuwa hataki kuja kuwa binadamu tena bali anahitaji kuwa Malaika.

Afande Selle alisema hayo kupitia kipindi cha Planet bongo cha East Africa Radio na kusisitiza kuwa siku atakayo kufa anaomba achomwe moto kwani yeye anaamini katika moto na si kuzikwa kawaida.
Afande Sele alidai kuwa amechoka kuwa binadamu bali anataka kuwa Malaika ndio maana anahitaji kuchomwa moto ili siku ya ufufuo arudi kama Malaika na si binadamu, imani yake inamtuma kuwa akizikwa kwenye udongo siku ya ufufuo atarudi kuwa binadamu tena jambo ambalo yeye hataki kusilisikia tena.

Kufuatia imani hiyo Afande Sele amesema mpaka sasa ameacha wosia kuwa siku atakayokufa achomwe moto na si kuzikwa.

Picha Mpya za Zari Zilizowaacha Team Wema Midomo Wazi na Kukubali Yaishe

$
0
0
Jana Zari Ameshare Nasi Picha hizi Ambazo Zimezua gumzo mtandaoni kwa wengi kusema amezidi kuwa mcharo utazani binti wa miaka 21 ....Yaani Huwezi Amini kama ni Mama wa watoto wanne mmoja akiwa ni wa Mwimbaji Diamond Platnumz.....

Zitto Kabwe Akomaa na Ufisadi Uliyofanyika Benki ya Stanbic..Ataka Serikali Ichukue Hatua

$
0
0
MBUNGE wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT- Wazalendo) ameitaka serikali kumwagiza Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) ili kubaini wizi wa Sh. 608 trilioni zilizokopwa kupitia Benki ya Stanbic yenye tawi lake nchini hapa.

Ametoa kauli hiyo leo bungeni wakati akiuliza swali la nyongeza kutaka kujua ni hatua gani ambazo zinachukuliwa kutokana na ufisadi mkubwa wa fedha hizo ambazo ni trilioni 6.8.

“Jumla ya fedha ambazo serikali ilizikopa nje kwa mfumo wa namna hiyo ni shilingi trilioni 6.8 na katika taarifa ya hukumu inaonesha mtindo huo wa kutumia vikampuni kwa ajili ya kupata mikopo imekuwa ikitumika na mabenki mengi ya kibiashara hapa nchini.

“Serikali haioni kwamba umefika wakati CAG aweze kufanya ukaguzi maalum wa mikopo yote ya kibiashara ambayo serikali imechukua katika kipindi hicho ili kuweza kujua kama pia kulikuwa kuna aina za rushwa za namna hiyo ambazo zimekuwa zinafanyika,”amehoji Zitto.

Zitto amesema DFA (Hukumu ya Uingereza) ilikuwa ina lengo la kuilinda Benk ya Uingereza ambayo ndiyo ilitoa hongo kwa maofisa wa Tanzania ili iweze kupata biashara ambapo alihoji, serikali haioni kwamba ni wakati muafaka sasa kufungua kesi dhidi ya benki hiyo ya Uingereza ili iwe fundisho kwa kampuni za nje zinazohonga kwa lengo la kupata biashara katika nchi za kiafrika

Akijibu maswali hayo Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji George Masaju amesema CAG anayo majukumu ya kikatiba na hilo ni jukumu ambalo anaweza kulitekeleza wakati wowote ili kujiridhisha kama mikopo hiyo ambayo imekuwa ikipatikana kwa namna ambayo inaifanya nchi iingie kwenye hasara.

Amesema, kama Zitto anazo taarifa zozote zinazoweza kuisaidia serikali ama kufungua shauti la madai ama jinai ashirikiane na vyombo husika ikiwemo Ofisi ya AG na kuliangalia ili kuona kama linakidhi sifa na sheria na kwa kuzingatia pia uhusiano uliopo kwa nchi ya Uingereza ili kuona kama kesi ya jinai inaweza kufunguliwa.

Aidha amesema serikali imepokea ushauri wa Zitto na itaufanyia kazi kwa kuzingatia sheria za ndani ya nchi na uhusiano wa kisheria katika Jumuiya ya Kimataifa.

Awali katika swali la msingi la Zitto alitaka kujua serikali inaichukulia hatua gani Stanbic Bank ili walipe fidia zaidi.

“Mwaka 2013 serikali ilizuia hatifungani ya thamani ya dola za Kimarekani milioni 600 (USD 600.0 mili) kupitia Benki ya Sdandard yenye tawi hapa nchini (Stabic).

“Shirika la Corrupition Watch la Uingereza kwa kutumia vyombo kama IFM imeonesha kuwa hatifungani hiyo imeipa Serikali ya Tanziania hasara ya Dola za Marekani miliono 80 na serikali imelipwa fidia Dola za Marekani milioni 6.

“Je kwa nini serikali haichukulii hatua Stanbic Bank ili ilipe fidia zaidi?”amehoji Zitto.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashantu Kijaju amesema, serikali imefuatilia taarifa za hasara kwa Serikali ya Tanzania ya Dola za Marekani 80 iliyotajwa na Zitto lakini haikupata ushahidi wake.

Hata hivyo Dk. Kijaju amesema Benki Kuu ya Tanzania imeiandikia Benki ya Stanbic barua ya kusudio la kuitoza faini ya Sh. 3 bilioni kwa kosa la kufanya miamala inayokiuka sheria na kanuni za mabenk na taasisi za fedha.

Kutoka Bungeni...Wauguzi Wanaotoa Lugha Chafu Kwa Wagonjwa Kuchukuliwa Hatua Kali

$
0
0
Hamisi Kigwangala
Serikali imejipanga kutoa huduma bora za afya kwa wananchi kwa kuwawezesha kila mwananchi kupata Bima ya Afya itakayosaidia kupata huduma bora za afya katika zahanati na hospitali mbalimbali.

Hayo yamesemwa leo Bungeni na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee Mhe.Hamis Adrea Kigwangalla wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Faida Mohammed Bakar(CCM)

Mh. Faida alitaka kujua namna serikali ilivyojipanga kutokomeza tabia mbaya ya wahudumu wa afya hasa kutoa lugha chafu kwa wagonjwa hususani kwa kinamama wajawazito na kwamba  bado kuna ukiukwaji wa huduma za afya, haki za afya na haki za uzazi katika baadhi ya vituo vya kutolea huduma za afya  hapa nchini.

Akijibu swali hilo,Naibu Waziri wa Afya, Hamis Kingwala alisema  katika kuhakikisha kuwa haki hizo za mgonjwa zinapatikana,Serikali kwa kupitia mifumo yake, ikiwa ni pamoja na mabaraza ya weledi, kurugenzi ya uhakiki na ubora wa huduma za afya na idara mbalimbali zilizo chini ya Waziri zinatoa mafunzo kwa watoa huduma za afya kuhusiana na haki za wateja.

Mhe. Hamis Adrea Kigwangalla amesema katika kutekeleza hili vituo vyote vya kutolea huduma za afya vina masanduku ya maoni na ofisi za malalamiko ambazo ni sehemu muhimu ambapo wateja wanaweza kupeleka malalamiko yao ili hatua zaidi zichukuliwe kukomesha na kutokomeza ukiukwaji wowote wa haki za wateja.

“ Tutawachukulia hatua wale wote watakaobainika kukiuka haki za wateja kwa kupitia baraza la wauguzi na wakunga ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora zinazostahili ili kuokoa maisha ya wananchi hasa maisha ya mama na mtoto” Alisema Mhe.Kigwangalla na kuongeza;

''Ni marufuku kwa wauguzi kutoa lugha chafu kwa wagonjwa na wana bodi zao za taaluma zao hivyo kila mgonjwa anaehudumiwa aangalie anahudumiwa na nani na atoe maoni yake katika eneo husika ili sheria ichukue mkondo wake''

Aidha Mhe. Hamis Adrea Kigwangalla amesema Wizara yake imeandaa rasimu ya Sheria ya Bima ya Afya ambayo itamuwezesha kila mwananchi kupata bima ya afya itakayomsaidia kupata huduma bora za afya katika maeneo yao.

Serikali kupitia Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee inatoa mafunzo kwa  Wakunga wa Jadi ambao wamekuwa wakitumika sana sehemu ambazo huduma za afya zipo mbali ili kuwezesha wananchi hao kupata huduma bora za afya kutoka kwa wakunga hao hasa katika afya ya mama na mtoto.

Rais Magufuli Uso Kwa Uso na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Waongelea Suala la Zanzibar

$
0
0
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi hapa nchini Mheshimiwa Jaji Damian Lubuva amemhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa tume hiyo ipo huru na haijawahi kuingiliwa kimaamuzi na Rais wala kiongozi yoyote.

Jaji Lubuva amesema hayo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Rais Magufuli ambapo alikuwa akimpa taarifa juu ya yaliyojiri katika kikao cha Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofanyika Mjini Kampala, Uganda na kujadili kuhusu uchaguzi Mkuu wa Uganda unaotarajiwa kufanyika tarehe 18 mwezi huu.

Amesema katika kikao hicho ambacho yeye alikuwa mwenyekiti, wamezungumzia umuhimu wa tume ya uchaguzi kuwa huru huku wakichukulia mfano wa Tanzania ambayo imetoka katika uchaguzi mkuu miezi michache iliyopita.

Jaji Lubuva amefafanua kuwa tume ya uchaguzi inapaswa kuwa huru katika maamuzi yake na kwamba jambo hili limekuwa likifanyika wakati wote hapa nchini.

Amebainisha kuwa wanaosema Rais anapaswa kuingilia kati masuala ya uchaguzi iwe Tanzania bara ama Zanzibar wanafanya makosa, kwani kwa namna yoyote Rais hana mamlaka hayo na hivyo hawezi kuingilia maamuzi ya tume hizo

“Unaposikia kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano aingilie hilo suala la uchaguzi wa Zanzibar, yeye kwa kweli hana mamlaka kabisa. Pili ni kama kujikanganya, huku unasema tuwe na tume huru isiyoingiliwa halafu huku unasema aingilie kati maamuzi ya tume” alisema Jaji Lubuva

Jaji Lubuva amesisitiza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kikatiba hana mamlaka ya kuingilia maamuzi ya tume ya uchaguzi ya Zanzibar na hata huku bara pia hana mamlaka ya kuingilia maamuzi ya tume.

Mwenyekiti huyo wa tume ya uchaguzi amewasihi Watanzania kuwa uchaguzi umekwisha, na kuwaomba waungane na viongozi waliochaguliwa kuchapa kazi ili kujiletea maendeleo.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam.
01 Februari, 2016

Shilole Asema Kuachana na Nuh Mziwanda Hakumzuii Kuendelea na ‘Project’ ya Nyang’anyang’a

$
0
0
Nuhu Mziwanda na Shilole
Ngoma ya ‘Nyang’anyang’a’,Shilole alimuimbia aliyekuwa mpenzi wa Nuh Mziwanda kabla hawajaachana,anazungumzia kama hali hiyo inamzuia kuendelea na project yake ya wimbo huo.

‘’Hapana hainipi ugumu wowote kwasababu wimbo nimeimba bila kumtaja mtu jina ila nimesema nilimuimbia aliyekuwa mpenzi wangu Nuh Mziwanda,hakuna ambacho nishindwe kuendelea ku’promote’ wimbo wangu na hainipi ugumu wowote kabisa,’’Shilole.

Cloudsfm.com

Faiza wa ‘Sugu’ Aomba Radhi, Azindua Kipindi Chake

$
0
0
Faiza Ally
MSANII wa filamu nchini, Faiza Ally, amezindua kipindi cha runinga kiitwacho ‘Stars’ ambacho kitakuwa kikizungumzia maisha yake.

Akizungumza katika kipindi cha Friday night live kinachoongozwa na mtangazaji, Sami Misago, wakati akitambulisha kipindi hicho alisema kitaanza kuoneshwa Jumanne katika kituo cha Eatv na kitahusu maisha yake ya kila siku.

“Kipindi changu kipya kitakuwa kikiitwa ‘Stars’ na kitakuwa kikizungumzia maisha yangu ya kila siku, nataka watu waone upande wangu mwingine kwa sababu kitu mnachokiona kina utofauti mkubwa na maisha yenu, kwa hiyo nataka kuonyesha watu kuna maisha tofauti na yale ambayo wanayaona,” alisema Faiza.

Msanii huyo alitumia fursa hiyo kuwaomba radhi mashabiki wake baada ya siku chache zilizopita kutuma video ya mwanawe, Sasha iliyomwonyesha akiomba fedha za kusuka huku akilia hali ambayo ilitafsiriwa kuwa ni udhalilishaji kwa mtoto huyo

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne ya Februari 2, Ikiwemo ya Mimba ya Wema Kuwa ni Mapacha

$
0
0
m

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne ya Februari 2, Ikiwemo ya Mimba ya Wema Kuwa ni Mapacha

Sakata La Mabehewa Feki Laibuka Bungeni..Mwakyembe Akomaa, Asema Yupo Tayari Kujiuzulu Ikithibitika

$
0
0
Sakata la ununuzi wa mabehewa kwa ajili ya Shirika la Reli Tanzania (TRL) yanayodaiwa kuwa mabovu liliibuka jana Bungeni na kumuinua Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe ambaye alikuwa Waziri wa Uchukuzi katika serikali ya awamu ya nne.

Waziri Mwakyembe alikanusha madai yaliyotolewa na Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Jesca Kishoa kuwa ununuzi huo wa mabehewa mabovu uliisababishia sherikali hasara ya shilingi bilioni 238, huku akitaka ripoti ya ukaguzi wa ununuzi huo iwasilishwe bungeni.

Akitumia kanuni ya 63 (3) kuomba kutoa taarifa, Mwakyembe alikanusha kiwango cha fedha kilichotajwa na mbunge huyo wa viti maalum ambaye ni mke wa aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila.

“Mbunge aliyesimama kabla, aliyejitambulisha kama mke wa Kafulila, ameeleza kwamba serikali ilitumia zaidi ya shilingi bilioni 238 na kuleta hasara kwa kununua mabehewa mabovu. Mheshimiwa Mwenyekiti nataka kukuthibitishia kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano, kwa kununua mabehewa 274 haijawahi kutumia zaidi ya shilingi bilioni 60,” alisema Mwakyembe.

Waziri huyo alienda mbali na kueleza kuwa endapo mbunge huyo atawasilisha uthibitisho wa kiwango hicho cha fedha kutumika kununua mabehewa hayo, atajiuzulu nafasi yake ya ubunge.

“Mimi naomba athibitishe hiyo shilingi bilioni 238. Na nitashukuru sana kama akileta hapa. Na akileta hiyo, mimi nitajiuzulu hata ubunge,” alisema Mwakyembe.

Baada ya kauli hiyo ya Mwakyembe, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee naye alisimama na kueleza kuwa Waziri huyo hakutumia kifungu sahihi kutoa taarifa kwa kuwa alipaswa kutumia kifungu cha 63 (4) kutoa ushahidi wa kukanusha kwake kwanza.

Naye Kishoa aliendelea kusisitiza kuwa Serikali inapaswa kuwasilisha bungeni hapo ripoti ya ukaguzi wa manunuzi ya mabehewa hayo.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bunge, Dk. Mary Mwanjelwa alitoa siku tatu kwa mbunge huyo wa viti maalum kuwasilisha ushahidi kuhusu madai yake.

Sugu Afunguka..'Serikali Hii Inaendeshwa MIZUKA Kwa Viongozi Wengi Kukurupuka Katika Maamuzi'

$
0
0
Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA), Joseph Mbilinyi (Sugu), jana Bungeni mjini Dodoma amesema serikali hii inaendeshwa kwa mizuka kwa viongozi wengi kukurupuka katika maamuzi?
Kama unakubaliana nae comment 'YES' kama unadhani si kweli na amekurupuka comment'NO'

Mbunge Aitaka Serikali ihalalishe Bangi na Mirungi Kama zao la Biashara

$
0
0
Katika hali isiyo ya kawaida Mbunge wa Geita Vijijini"Msukuma, amesema haoni sababu ya Serikali kuzuia bangi na mirungi kuwa zao la biashara maana haoni madhara yake.

Ameenda mbali zaidi kwa kusema wasukuma wakivuta bangi wanalima zaidi na inahitaji uchunguzi ili kuhalalisha mimea hiyo kuwa zao la biashara.

Wewe Una Maoni Gani!
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live




Latest Images