Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live

Mwanamziki Colonel Mustapha Atoboa Siri Adai Amelala na Huddah Mara 50 "Ni Mtamu Amepelekwa Unyagoni"

$
0
0
Staa wa muziki kutoka nchini Kenya, Colonel Mustafa amedai kuwa amesha fanya mapenzi na Huddah Monroe zaidi ya mara 50 kwa penzi lililodumu kwa muda wa wiki mbili pekee.

Akizungumza katika kipindi cha Friday Night Live cha East Africa Television Ijumaa hii, Colonel alizungumzia uhusiano wake na Huddah Monroe.

Nilikuwa na mahusiano na Huddah, tuli sex hata mara 50. Huddah she’s fine kitandani, Nafikiri amepelekwa unyagoni kidogo” Alisema Mustafa.

Hata hivyo, mrembo Huddah aliwai kukanusha kutoka kimapenzi na Colonel huku akidai msanii huyo alikuwa anatafuta kiki kupitia jina lake.

Katika hatua nyingine Mustafa alisema anamkubali Diamond , AY, pamoja na Navy Kenzo na anawish siku moja angefanya kolabo na mmoja kati ya hao.

Director Adam Juma Aingilia Malumbano ya Washabiki Wanaosema Video Mpya ya Ali Kiba ni Mbaya

$
0
0
Siku moja baada ya staa wa bongofleva Alikiba kuiachia video ya ngoma yake ‘Lupela‘, leo Director wa long time Tanzania Adam Juma ameyatoa yake ya moyoni kupitia account yake ya instagramn baada ya kuona comments za watu wengine wakiikosa video yenyewe.

Adam Juma

“Lupela @officialalikiba , this is art, watanzania hatujui kuidadavua art. Hatujui thamani ya kitu, tunachukulia kiurahisi urahisi tu, kila mtu anajifanya anajua kitu ambacho sio sawa. Hii sio video tu, tulia basi angalia kwa umakini utapata ujumbe usipoelewa inawekana tatizo lipo kwenye level yako ya kuchanganua ujumbe ktk picha, btw sio fan wa alikiba ni mwana tu. Ningependa kusema video ni A one, haifanani na kitu ambacho tumezoe!!! Go kiba…...” – Adam Juma

Angalia Video Hiyo na Wewe Utoe Maoni yako Hapa:

Nuhu Mziwanda Afunguka ' Shilole Hakuwa Mke Mzuri Kwangu Ndio Maana Nimefuta Tattoo yake'

$
0
0

Msanii Nuh Mziwanda amefunguka baada ya kuachana na mwandani wake Shilole, na kusema kuwa Shilole hakuwa mtu mzuri kwake, ndiyo maana ameamua kufuta hata tatoo ya jina lake aliyoichora.

Nuh ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kwamba wakati yupo kwenye mahusiano na Shilole alishindwa kuonesha undani wake, ambao amekuja kuujua baada ya kuachana na penzi kuisha.

“Baada ya mapenzi kuisha mi nimekuwa adui yake, amehack acount yangu ya instagram najaribu kuwacheki wa kurudisha acount yangu wanashindwa kunirudishia anabana kila sehemu, kuna vitu ananifanyia vidogo vidogo ambavyo nimefanya kugundua kuwa hakuwa mwanamke mzuri kwangu, alikuwa anashindwa kuonesha true colour yake nimekuja kuijua baada ya kuachana naye”, alisema Nuhu.

Pia Nuh Mziwanda amesema iwapo wangeachana kwa amani na Shilole asingelazimika kuifuta tatoo hiyo, kwani ni ukweli usiopingika kwamba amemsaidia katika maisha yake.

“Mi ningeiacha tatoo kama Shishi ningeachana nae poa, kila mtu na maisha yake fresh tukionana tunasalimiana hakuna noma, lakini mwenzangu kwenye interviews anasema, akiitwa kwenye interview anaongea hiki kwamba mimi sina kitu, sijui nashindwa kusurvive nakula magengeni, anaongea vitu vingi ambavyo anajaribu kutoa fan base yangu, angekuwa mtu mzuri baada ya kuachana naye tatoo ningeiacha kwa sababu ningejua bado kabaki kuwa rafiki yangu na ni mtu ambaye alinisaidia”, alisema Nuh.

Pamoja na hayo Nuh amesema yeye binafsi hana chuki na msanii huyo ambaye alikuwa naye kwenye mahusiano, na kwa sasa ana mahusiano mengine ambayo asingependa kuyaweka wazi.

Mimi sina ubaya na Shishi , sina ugomvi naye na wala sitaki kufikiria kuja kuwa na bifu naye, nipo kwenye mahusiano lakini siwezi kuweka wazi mahusiano kwenye mitandao ya kijamii, sababu ni mke wangu yuko kwenye moyo wangu, hayupo instagram wala kwenye mitandao ya kijamii”, alisema Nuh.

Watu Tisa Waliotungua Helkopta na Kumuua Rubani Wakamatwa na Bunduki 29 na Meno ya Tembo 3

$
0
0

Watu 9 wakiwa na bunduki 29, meno ya tembo 3 wamekamatwa, yadaiwa walihusika kutungua chopa na kumuua rubani Rogers Gower.

Walimuua rubani huyo katika pori la Maswa

Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda Apata Ajali Mbaya ya Gari

$
0
0

Mtu mmoja amefariki dunia na wengine wanne wamejeruhiwa akiwemo mke wa waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda Mama Tunu Pinda baada ya gari walilokuwa wakisafiria kumgonga mwendesha pikipiki wakati akikatisha barabara katika eneo la Mkundi barabara ya Morogoro Dodoma manispaa ya Morogoro.


Ajali hiyo imetokea majira ya saa nane mchana katika eneo la Mkundi ikihusisha gari lenye namba za usajili STK 9242 gari la mke wa waziri mstaafu Mizengo Pinda likitokea Dodoma kwenda jijini Dar-es-Salaam  na pikipiki


Majeruhi wengine wa ajali hiyo ni dereva wa gari hilo Bw Anjelo Mwisa, mlinzi wa mke wa waziri mkuu mstaafu Gaudensi Tembo na kijana wa familia ya Mama Tunu Pinda Bwana Gilbert Sampa.


Kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro Dr Rita Liamuya amesema hali ya mke wa

waziri mkuu mstaafu na majeruhi wengine zinaendelea vizuri na kueleza kuwa  majeruhi hao wanatarajia kuhamishiwa jijini Dar-es-Salaam kwa matibabu zaidi

Vicent Kigosi ‘Ray’ Awacharukia Wanaosema Tasnia ya Filamu Imekufa Baada ya Kanumba Kufariki...

$
0
0
Msanii mkongwe wa filamu nchini, Vicent Kigosi ‘Ray’ amewataka mashabiki wa filamu kuwapuuza watu wanaodai tasnia ya filamu imekufa baada Steven Kanumba kufariki.
Ray Kigosi

Akizungumza na Bongo5 Ijumaa hii, Ray alisema huu ni wakati kwa wadau wa filamu pamoja na mashabiki kusupport wasanii waliopo kwa nunua kazi zao.

“Mimi nataka mashabiki wa filamu wajue hii tasnia inaendeshwa na wao, sisi wasanii tunategemea support yao kwa kununua kazi zetu. Mimi binafsi naukubali mchango wa Kanumba lakini ufike wakati tujue ya Kanumba yalishapita, tuwaandae akina Kanumba wengine, na wanaosema tasnia ya filamu imekufa baada ya Kanumba kufariki sio kweli na wapuuzwe.” Alisema Ray.

Aliongeza, “Mimi naamini tuna wasanii wengi wenye vipaji ambao tukiwasupport tutafika mbali zaidi. Mbona kwenye muziki leo kuna Diamond, lakini hapo nyuma kulikuwa na akina MB Dog, Matonya, TID na wengine wengi. Mimi naamini hata Diamond wakati wake ukipita watakuja wengine wakali. Kwahiyo nawaambia mashabiki wa filamu tuna wasanii wengi bado wanafanya vizuri, kinachotakiwa ni kuwasupport alafu tuone kama watashindwa.”.

Aidha, Ray amewakata mashabiki wa filamu kuisubiria filamu yake mpya ‘Tajiri Mfupi’ ambayo inatarajia kutoka hivi karibuni.

Salam Jabir Nae Aibuka Kwenye Malumbano ya Video Mpya ya Ali Kiba Baada ya Baadhi Kuiponda...Asema Haya

$
0
0
Mtangazaji wa kipindi cha Mkasi ambacho kinarushwa kupitia ting'a namba moja kwa vijana (EATV) Salama Jabir amefunguka na kuwataka watanzania kuthamini na kuheshimu watu ambao wanajituma kufanya mambo katika kazi zao.

Salama amesema kuwa kazi ya msanii siku zote ni sanaa ambayo unaweza kuipenda au kutoipenda.
Salama Jabir amesema hayo kupitia Account yake ya Twitter kufuatia baadhi ya maoni ya mashabiki ambao wamekuwa wakiwaponda wasanii wa bongo pindi wanapokuwa wanatoa kazi zao hususani video huku mashabiki wengine wakienda mbali na kuponda au kuzungumzia jambo kama wao wana maarifa ya jambo hilo.

"Kazi ya msanii ni Sanaa... Usingiingilie!! ni aidha utaipenda au hutaipenda simple!! Kama rahisi fanya na wewe tuone Respect kwa wanaojituma" Amesema Salama

Imekuwa ni kawaida kwa mashabiki kuponda kazi za wasanii na kuwatusi kupitia mitandao yao ya kijamii jambo ambalo linakuwa linakatisha tamaa baadhi ya wasanii na kuwaumiza kwani maneno ambayo mashabiki huwa wanatumia ni makali na ya kukatisha tamaa.

Hali hii mara nyingi imekuwa ikisababishwa na makundi ya mashabiki maarufu kama Team, kuna watu wanaweza kuponda jambo ili mradi tu kwa sababu yeye si shabiki wa msanii fulani na wapo wengine wanafanya hivyo kwa lengo ya kukomesha, huku wengine wakitaka wasanii waendelee kuleta video za aina fulani pekee na ukifanya vinginevyo wanaona umekosea kwa sababu ndicho kitu walichozoea kifupi hawataki kukutana na kitu cha iana mpya.

Kulikoni Dkt Magufuli Kutohudhuria Karamu ya Mabolozi Ikulu?

$
0
0
Nimeshangazwa kidogo kwa kitendo cha Rais Dkt Magufuli kuwaandalia karamu ya kuukaribisha mwaka mpya, mabalozi na Maafisa wa kimataifa waliopo nchini na kisha yeye mwenyewe kumtuma waziri wake wa mambo ya nje kumwakilisha.

Kwa maoni yangu naamini hili ni kosa la kiufundi hasa ikizingatiwa kuwa Magufuli ndio ameanza tenure yake kama Raisi na hivyo angepaswa kutumia fursa hiyo kikamilifu ili kujenga taswira yake vema kimataifa kupitia kile anachokiamini na kusimamia.

Taarifa iliyorushwa na vyombo vya habari haikusema ni dharura gani aliyokuwa Mhe Rais ilihali yupo nchini.\

Source:Jamii Forums

Mwanamke Kuwa Juu ya Mwanaume ni Mtindo Hatari Wakati wa Tendo la ndoa

$
0
0
Wanasayansi nchini Brazil wamefanya utafiti ili kubaini ni mtindo upi katika ufanyaji tendo la ndoa ulio hatari zaidi kwa mwanaume.
Kwa mujibu wa utafiti huo, mtindo ambao mwanamke anakuwa juu ya mwanaume ndio hatari zaidi na huwa na risk kubwa zaidi ya kusababisha hata kuvunjika kwa uume.

Wanasayansi hao wanasema:

Pindi mwanamke anapokuwa juu, mara zote hucontrol movement na uzito wote wa mwili wake ukitua kwenye uume uliosimama na kushindwa kuzuia pale uume unapokuwa umeingia vibaya kwasababu madhara huwa ni madogo kwa mwanamke bila maumivu lakini ni mabaya kwa mwanaume.
“Pindi mwanaume anapokuwa akicontrol movement, ana nafasi kubwa ya kuzuia kutokana na uume wake kuwa sehemu mbaya na hali inayopelekea kusikia maumivu na hivyo kupunguza hatari.
Hivyo inashauriwa kuepuka staili hiyo....

Rais Magufuli Apigilia Msumari Sakata la Zanzibar..Adai Hakuna Jinsi zaidi ya Kurudia Uchaguzi

$
0
0

Rais John Magufuli amesema kuwa hana mamlaka yoyote ya kuingilia suala la uchaguzi wa Zanzibar.
 

Rais Magufuli aliyaeleza hayo  jana katika hotuba yake kwa mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania iliyosomwa kwa niaba yake na waziri wa mambo ya nje, ushirikiano wa Afrika Mashariki, kikanda na kimataifa Balozi Augustine Mahiga  jana ikulu jijini Dar es salaam.

 

Katika hotuba hiyo, Rais Magufuli aliwaeleza mabalozi hao kuwa licha ya Tanzania kuwa nchi moja, Zanzibar ina mfumo wake wa siasa, ina serikali yake, Katiba yake na pia tume yake ya uchaguzi inayojitegemea.

Alisema tume hiyo ilifuta uchaguzi kutokana na mapungufu yaliyojitokeza kisiwani Pemba, na kwamba tayari tarehe mpya ya uchaguzi wa marudio imekwisha tangazwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar.

 

Alosema mazungumzo ya kutatua mgogoro huo yalifanyika bila mafanikio ambapo chama kikuu cha upinzani (CUF) kimeendelea kupinga uchaguzi wa marudio huku vyama vingine kikiwemo chama tawala vikionesha uhitaji wa uchaguzi huo wa marudio.

 

Alisema kwa hali ilivyo, busara inahitajika ili kunusuru suala hilo, na kwamba kususia uchaguzi siyo suluhu bali kutumia nafasi iliyopo sasa kujadili namna ya kuufanya uchaguzi wa marudio kuwa huru na wa haki.

 

Aliwaeleza mabalozi hao kuwa serikali pamoja na watanzania walio wengi wangependa kuona CUF inathibitisha madai yake ya kushinda uchaguzi huo kupitia sanduku la kura katika uchaguzi wa marudio.

 

“Tunakiasa chama cha CUF kama ambavyo watanzania wengi wangependa kuona, kuthibitisha madai ya ushindi wao katika sanduku la kura, hakuna jinsi nyingine ya kutatua suala hili zaidi ya kukubali kufanya uchaguzi wa marudio”ilisema sehemu ya hotuba hiyo.

 

Magufuli amewahakikishia mabalozi hao kuwa nchi ni salama na hali ya amani na utulivu ni ya kuridhisha katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi wa marudio.

Kimenuka..Mhifadhi wa hifadhi ya Ngorongoro Akamatwa Katika Majangili Tisa Walio Waliotungua Helkopta na Kuua Mzungu Pori la Akiba Maswa

$
0
0

Siku chache baada ya kutokea tukio la majangili katika pori la akiba Maswa wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu, kuitungua ndege (helikopta) iliyokuwa doria na kuaawa kwa rubani wake Rodgers Gower (37),  watu 9 wamekamatwa kuhusika na tukio hilo. 


Katika watuhumiwa hao mmoja niMhifadhi wa hifadhi ya taifa ya Ngorongoro kitengo cha Interejensia, ambaye alitajwa kuwa mhusika Mkuu wa kufanikisha tukio hilo sambamba na kukamatwa mganga wa jadi.



Akitoa taarifa mbele za waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa polisi Mkoani Simiyu Lazaro Mambosasa alisema kuwa kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumetokana na jeshi hilo kufanya kazu usiku na mchana  kwa kushirikiana na wananchi, pamoja na uongozi wa TANAPA.


Kamanda Mambosasa alisema watuhumiwa wote walikamatwa na kukiri kuhusika na tukio hilo, huku akieleza kuwa msako mkubwa uliofanywa na jeshi hilo mara baada ya tukio kutokea chini ya Mkuu wa upelelezi Mkoa Jonathan Shana.


Alisema katika msako huo baadhi ya watuhumiwa walibainika kuwa kiungo kikubwa kufanikisha tukio hilo kwa kutoa mbinu za uharifu, huku wakijihusisha na matukio ya ujangili kwa muda mrefu.


Aliongeza kuwa baadhi yao walibainika kuwa waganga wa jadi, ambapo walikuwa wakitoa dawa kwa majangili za kuosha silaha, ikiwa ni pamoja na  kuosha na kusafisha miili yao ili wasiweze  kukamatwa.


Mambosasa aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Shija Mjika (38), Njile Gonga (28) Mhazabe, Masasi Mandago (48) pamoja na Dotto Pangali (41) , ambao ndio walihusika kutungua helkopta hiyo.


Wengine ni Iddi Mashaka (49) ambaye Kamanda Mambosasa alimtaja kuwaMhifadhi wa hifadhi ya taifa ya Ngorongoro Kitengo cha Intelijensia na ndiye alikuwa kiungo Mkuu wa tukio hilo.


Aliwataja wengine kuwa ni Mapolu Njige (50) ambaye ni mganga wa jadi aiyekuwa anatumika kutoa dawa za kutokamatwa kwa majangili hao, Mwigulu Kanga (40) , Dotto Huya (45) , Pamoja na Mange Balumu.


Aidha Mambosasa alisema kuwa Mtuhumiwa Dotto Pangali alikamatiwa katika wilaya ya Kishapu Mkoa wa Shinyanga mnamo tarehe 7/02/216 na kufanyiwa upekuzi nyumbani kwake ambapo alikutwa na bunduki aina ya Riffle yenye namba .7209460 CAR Na.63229.


Mkuu huyo wa polisi alisema Mtuhumiwa huyo alikiri bunduki hiyo kutumika katika tukio la kuuawa kwa rubani huyo, ambapo ilibainika kuwa bunduki hiyo inamilikiwa na Mange Magima ambaye pia amekamatwa.


Alisema msako uliendelea nyumbani kwa Pangali na kufanikiwa kukamatwa kwa bunduki nyingine aina ya Riffle Na3478 CAR 458 ikiwa na risasi 6 ambayo ilibainika kumilikiwa na Nghomango Jilala ambaye mpaka sasa hajakamatwa.


Alieleza kuwa jeshi hilo liliendelea kupata taarifa ambapo mnamo tarehe 29/01/2016 walikamatwa Shija Mjika, Njile Gonga, pamoja na Masasi Mandago wakiwa na meno ya tembo 2 yakiwa na uzito wa Kilo 31 yakiwa yamefichwa chini ya daraja katika kijiji cha Itaba.


Aidha Mambosasa alieleza kuwa baada ya kukamatwa kwa wahusika wote ilibainika kuwa bunduki zilizotumika katika tukio hilo zinamilikiwa kihalali na watu ambao waliomba kuzimiliki kwa ajili kujilinda.


“Mbali na tukio hilo bunduki nyingi wamiliki wake wanawaazimisha majangili kwa ajili ya kutumika kwa uhalifu pamoja na kuua wanyama ndani ya hifadhi…lakini na hao wamiliki wanalipwa pesa baada ya uhalifu kufanyika” ,alisema.


Alisema baada ya kubaini hilo kulifanyika msako mwingine kwa wanaomiliki silaha, ambapo alisema asilimia kubwa wanaishi karibu na hifadhi, na jumla ya bunduki 27 zimekamatwa na mara baada ya uchunguzi wamiliki watarudishiwa.


“Tunajiandaa kupeleka zuio la silaha mahakamani ili kubaini kama wana sifa za umiliki…lakini mbali na hilo sasa kutaanzishwa oparesheni kwa watu wote wanaomiliki silaha hasa maeneo ya hifadhi kwa ajili ya kuwanyanganya”, alisema.

 

Mkuu huyo wa polisi alisema kuwa upelelezi juu ya tukio hilo umekamilika na watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani leo Jumanne ili kujibu tuhuma zinazowakabili, ambapo alioomba mahakama kuharakisha hukumu kwa vile uchunguzi umekamilika.


Kwa upande wake Mhifadhi mkuu wa Serengeti William Mwakilema amelipongeza jeshi la polisi ambapo amesema tukio hilo lilipotokea liliwasikitisha sana kwani hasara ilipatikana kutokana na kutunguliwa kwa helkopta.


Mnamo tarehe 29/01/2016 saa 11:30 jioni katika eneo la Gululu lililopo ndani ya hifadhi ya Maswa kata ya Mwangudo wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu, majangili waliipiga risasi ndege (helkopta) 88HFCG iliyokuwa doria na kusababisha kifo cha rubani wake Rodgers Gower (37) raia wa uingereza huku Mwenzake Nicholas Beste (43) raia wa Afrika Kusini akinususrika kifo. 

Mimba ya Wema, Idriss Sultan Apachikwa Jina la Dk. Mwaka Baada ya Wengi Kushindwa Kumpa Ujauzito Wema

$
0
0

MIMBA ya Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu inazidi kuzua ya kuzua kila kukicha baada ya hivi karibuni, Mshindi wa Big Brother Africa Hot Shots 2015, Idriss Sultan ambaye anajigamba kuwa ndiye mwenye ujauzito huo kupachikwa jina la Dk. Mwaka.

Idriss amepewa jina hilo kwa vile Tabibu wa Tiba Mbadala Tanzania, Juma Mwaka Juma JJ Mwaka au ‘Dk. Mwaka’ amekuwa akisifika kwa kuwatibu wanawake wenye matatizo ya kutoshika mimba.

Mitandao mbalimbali ya kijamii wiki iliyopita ilimwita Idriss ni Dk. Mwaka huku ikimsifia kuwa, wameshindwa wanaume wengi, akiwemo Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ aliyewahi kuwa mpenzi wa Wema lakini yeye ameweza kumpa furaha mrembo huyo kwa kumpachika ujauzito.

“Kweli wewe Idriss ni Dk. Mwaka. Maana Mwaka amekuwa akiwasaidia wanawake kupata watoto. Wema ametoka na wanaume kibao, lakini wewe dogo umeweza, big up!” ulisomeka mtandao mmoja.
Gazeti hili lilimtafuta Dk. Mwaka kwa njia ya simu ili kumuuliza amelichukuliaje tukio la Idriss kuitwa kwa jina lake.

“Pengine uwezo wangu wa kazi umesababishwa aitwe hivyo. Lakini mimi bado nabaki kuwa Dk. Mwaka orijino na kazi yangu inajulikana,” alisema Dk. Mwaka.
Idriss hakupatikana hewani juzi kuzungumzia ishu hiyo lakini kwa nyakati tofauti amewahi kucheka tu kwa watu kumwita jina hilo.

Mnyonge Mnyongeni Rais Magufuli Ndio Rais Tuliyokuwa Tunamtaka Tanzania...Ukweli Utabaki pale pale

$
0
0

Mungu ni mwema hatuna budi kumshukuru kwa anayotufanyia katika nchi yetu.
Baada ya kusema hayo niseme bila kumung’unya maneno kwamba Rais Dk. John Pombe Magufuli ndiye rais tuliyekuwa tunamtaka kutokana na anachokifanya sasa.

Nichukue nafasi hii kumpongeza kwa hatua anazochukua ili kuwafanya wananchi wanufaike na rasilimali za nchi hii, hivyo namtakia kila la heri katika kazi yake ya kututumikia. Naomba kukiri kwa uwazi kwamba Watanzania tulifanya chaguo sahihi, hatukukosea.

Tanzania ina vyama 23 vya siasa vilivyosajiliwa na vinavyofanya kazi sasa, tutake tusitake Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilimuona Dk. Magufuli kuwa ni tunu ya taifa na leo anadhihirisha hilo kwa kupigania wananchi wake na kuwa adui kwa mafisadi.

Kila Mtanzania sasa anaamini kwamba Dk.Magufuli anaweza kurejesha bila wasiwasi usimamizi thabiti wa serikali na nidhamu ya utendaji ndani ya serikali. Naamini kuwa serikali ya Magufuli itakuwa ya kiusimamizi na yeye mwenyewe anaweza kulifanya jambo hilo bila kusita. Tumeona.

Katika nyadhifa nyingi alizopitia hadi sasa ameijenga taswira hii kila alikopita na bado inambeba katika awamu hii ya tano.Hakuna siri, kama kuna jambo ambalo lilikuwa haliendi sawa nchini ni la utendaji ndani ya serikali. Tunafahamu kuwa wafanyakazi ndani ya serikali ukiachilia mbali matatizo waliyonayo kwa maana ya vipato, hata mambo madogo ambayo wangeweza kuyasimamia ndani ya dakika au saa chache yalichukua wiki hata miezi kadhaa.

Utaratibu wa utoaji huduma ulikwama sana lakini kwa spidi ya Rais Magufuli atafanikiwa kutatua changamoto hiyo kubwa na ya siku nyingi. Ikiwa utendaji wa serikali unaimarika na huduma zinatolewa kwa wakati, tutaweza kujenga taifa linalokwenda mbele kimaendeleo.

Taswira bora ya pili ya serikali ya Dk. Magufuli ni misimamo katika masuala ya msingi na kutoyumba. Magufuli muda wote ambao amekuwa kiongozi anaonesha njia, ndiyo maana alipoanza tu kazi, alianza na tabia ya ziara za kushtukiza. Hii alikuwa akifanya hata alipokuwa waziri wa ujenzi.

Moja ya mambo ambayo serikali iliyopita ilikosa ni pamoja na kukosa misimamo na kuwa na Double standard. Mfano mdogo tu ni kwenye mchakato wa Katiba Mpya ambapo rais anayeondoka alisimamia uanzishwaji bora wa mchakato huo, akaunga mkono katika hatua zote na rasimu zote, lakini akaja kuwageuka wajumbe wa tume hiyo na rasimu yao ya pili alipolihutubia Bunge Maalumu la Katiba.

Naamini Magufuli si mtu wa kugeuka na kuna masuala mengi anaweza kuyasimamia kwa dhati na kila mmoja wetu akakubali kuwa, huyu ni kiongozi anayesimamia haki na ana uchungu na wananchi wake.
Amekuwa akitetea wanyonge hadharani mara nyingi na anaonekana wazi kwamba anaumizwa na watu wanaoibia serikali bila kujali kuwa kuna watu wanakosa mlo mmoja kwa siku.

Wote tumuunge mkono, ni rais anayestahili sifa hizo, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Kwa kufanya hivyo naamini tutashinda.
Jipu limepasuka siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.

Haya Sasa Maigizo Mwalimu Mkuu wa Shule Avuliwa Cheo Chake Baada ya Kuchelewa Mkutano wa Mkuu wa Wilaya

$
0
0

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Butinzya, amevuliwa wadhifa huo kwa madai ya kuchelewa kuhudhuria kikao kilichoitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Amani Mwenegoha.


Utekelezaji wa kumvua madaraka mwalimu huyo, Mathias Mazuri, ulifanywa na Ofisa Elimu Shule za Msingi wa wilaya hiyo, Shadrack Kabanga.


Mwalimu Mazuri alichelewa kikao kilichoitishwa na Mwenegoha Februari 6, kikiwa na lengo la kudhibiti fedha za ruzuku ya Serikali na kwamba adhabu hiyo ni fundisho kwa watumishi wengine.


Akitangaza kumvua wadhifa huo mbele ya walimu wakuu wenzake, Kabanga alisema Shule ya Butinzya ipo karibu na eneo la mkutano na wezake waliotoka mbali walifika saa 3:00 asubuhi yeye saa 6:00 mchana.


“Sikubali, huu ni muda wa kubadilika siyo kuleana, nakuvua wadhifa kuanzia sasa siyo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Butinzya,” alisema.


Mwalimu Mazuri alijitetea kuwa kuchelewa kwake kulitokana na pikipiki yake kuharibika njiani, utetezi huo ulitupiliwa mbali na ofisa elimu.


Mkuu wa wilaya hiyo, Mwenegoha aliwataka walimu kutumia vizuri fedha za ruzuku na kwamba, wasichangishe wazazi kutokana na uhaba wa posho za madaraka.


Mwenegoha alipiga marufuku kuwadai wanafunzi fedha za masomo ya ziada.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda Abanwa Kisawasawa na Wakili wa Kubenea Mahakamani

$
0
0

PAUL Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, amebanwa kwa maswali kutoka kwa Wakili Peter Kibatara anayemtetea mteja wake Saed Kubenea. Anaandika Happyness Lidwino.

Makonda amebanwa kwa maswali na wakili huyo kutokana na ushahidi alioeleza mbele ya mahakama kuhusu kesi yake ya madai aliyoifungua tarehe 15 Desemba mwaka jana dhidi ya Kubenea ambaye ni Mbunge wa Ubungo.

Ikiwa ni siku ya Makonda kujitetea, Wakili Kibatara alimuhoji kwanini aliamua kupeleka kesi hii mahakamani?, Makonda alishindwa kujibu.

Baada ya Makonda kushindwa kujibu, hakimu anayesimamia kesi hiyo Thomas Simba alimweleza Wakili Kibatara aulize swali la pili.

Wakili Kibatara alimuuliza Makonda kwamba alichukua muda gani kwenda katika gari yake baada ya Kubenea kuanza kumtolewa lugha za matusi?

Makonda aliieleza mahakama kwamba, alitumia muda wa dakika 15, Wakili Kibarata alimuhoji kwamba, je katika dakika hizo hakujibu matusi kutoka kwa Kubenea?

Makonda alijibu kwamba, katika muda huo hakumjibu chochote Kubenea. Wakili Kibatara alihoji kwamba inawezekanaje katika dakika zote 15 Makonda asizungumze chochote.

Hata hivyo, hakimu alimtaka Wakili Kibatara kuuliza swali lingine ambapo aliuliza je polisi waliokuwa katika eneo la tukio walichukua hatua gani?

Makonda alisema, polisi walichukua hatua ya kumkamata Kubenea baada ya Kubenea kuendelea kutoalugha ya matusi.

Na hata alipoulizwa aliyetoa amri ya kumkamata Kubenea, Makonda alikana na kudai si yeye isipokuwa polisi ndio walimkamata.

Wakili Kibatara alimuuliza Makonda, “Je, unayajua majukumu ya Mbunge? Je ulijibizana na Kubenea eneo la tukio? Je, unajua ni vigezo gani vilitumika kukuchagua kuwa Mkuu wa Wilaya? Je unafahamu maana ya neno mjinga na mpumbavu?

Maswali hayo ya mtego yalionekana kumpandisha hasira Makonda kutokana na majibu yake kuwa mafupi na kutomridhisha wakili.

Hata hivyo, hakimu aliingilia kati na kumtaka wakili kubadilisha namna ya kuuliza maswali hayo. Hata Wakili Kibatara baada ya kushauriwa na hakimu kubadilisha maswali, aliieleza mahakama kwamba amemaliza.

Makonda alifika mahakamani hapo leo kutoa ushahidi wake huku akifuatiwa na shaidi wake ambaye ni Askali Dc Gabriel mwenye namba F4829 kutoka katika Kituo cha Magomeni.

Makonda alifungua kesi hiyo tarehe 15 Desemba mwaka jana ikiwa ni siku moja baada ya Makonda kuagiza askari wa Jeshi la Polisi kumkamata mbunge huyo kwa madai ya kushindwa kutii agizo lake kama Mkuu wa Wilaya.

Tukio la kukamatwa Kubenea lilitekelezwa Tarehe 14 Desemba mwaka jana jijini Dar es Salaam, baada ya viongozi hao kukutana katika mgogoro wa wafanyakazi wa Kiwanda cha nguo cha Tooku Tanzania.

Kwenye mahakama hiyo, Makonda amefungua madai matatu dhidi ya Kubenea ambayo ni lugha ya matusi, kuitwa mpumbavu, mjinga pamoja na cheo cha kupewa.

Jaji Mihayo Afunguka Kuhusu Wanaosema Rais Magufuli ni Dikteta.....

$
0
0

Mwenyekiti wa Majaji wastaafu, Jaji Mihayo amesema Rais Magufuli sio dikteta kwani hajafanya lolote linalomfanya awe juu ya sheria.

Amesema “Wanaosema Magufuli ni dikteta hawawajui madikteta. Hakuna kiongozi dikteta Afrika Mashariki isipokuwa Idi Amin tu,” Jaji Mihayo, ambaye ni mwenyekiti wa majaji wastaafu, alihoji inawezekanaje kiongozi ambaye mataifa mengine wanatamani akaongoze nchi yao angalau kwa miezi miwili, aonekane kuwa ni dikteta. “Magufuli anafuata sheria kwa sababu hajafanya jambo lolote ambalo linamfanya awe juu ya sheria. Sijawahi kusikia kasema mfunge huyu au kusema sheria hii isitumike na hii itumike” alisema.

Alisema ni kawaida kwa viongozi wanaokemea uovu kuonekana kama madikteta kwa sababu wanataka kuondoa rushwa.

Kadhalika, Jaji Mihayo alisema anaupenda utendaji kazi wa Magufuli ili wanaokiuka sheria wawajibishwe na walalahoi wapate haki yao.

Taarifa Kwa Umma Kutoka Ofisi ya Makamo wa Rais Kuhusu Uzushi Unaonea Mitandaoni Kuwa Samia Suluhu Ameanzisha Saccos ya Vikoba

$
0
0
Isome Hapa Taarifa Kwa Umma Kutoka Ofisi ya Makamo wa Rais Kuhusu Uzushi Unaonea Mitandaoni Kuwa Samia Suluhu Ameanzisha Saccos ya Vikoba..

Adam Juma Aoga Matusi Baada ya Kuisifia Video ya Wimbo Mpya wa Ali Kiba ‘Lupela ’

$
0
0

Mtayarishaji mkongwe wa video za muziki nchini, Adam Juma Jumatatu hii amejikuta akishambuliwa kwa matusi katika mitandao ya kijamii baada ya kuisifia video ya wimbo mpya wa Ali Kiba ‘Lupela’.

Muongozaji huyo aliamua kumsifia Ali Kiba kwa namna kazi ya Lupela ilivyoandaliwa mpaka kukamilika.

Kupitia instagram, Adam Juma aliandika.
    Lupela @officialalikiba , this is art, watanzania hatujui kuidadavua art. Hatujui thamani ya kitu, tunachukulia kiurahisi urahisi tu, kila mtu anajifanya anajua kitu ambacho sio sawa. Hii sio video tu, tulia basi angalia kwa umakini utapata ujumbe usipoelewa inawekana tatizo lipo kwenye level yako ya kuchanganua ujumbe ktk picha, btw sio fan wa alikiba ni mwana tu. Ningependa kusema video ni A one, haifanani na kitu ambacho tumezoe!!! Go kiba

Hata hivyo baada ya ujumbe huo kukaa kutwa nzima ya jana, Adam Juma alirudi kwa mashabiki wake na kueleza kilichomkuta.

Kupitia instagram, Adam Juma aliandika : Jana nimeoga matusi mpk raha aisee….. kumbe ni hivi duu sikujua aisee.

Hashim Rungwe Akosoa kauli za Rais Magufuli Kuhusu idara ya Mahakama, asema Zinaingilia Uhuru wa Mahakama.

$
0
0

Mwenyekiti wa chama cha ukombozi wa umma CHAUMA Hashim Rungwe amesema kauli iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt John Pombe Magufuli wakati wa maadhimisho ya siku ya Mahakama nchini iliingilia uhuru wa mahakama.


Mwenyekiti wa chama cha ukombozi wa umma CHAUMA Hashim Rungwe amesema kauli iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt John Pombe Magufuli wakati wa maadhimisho ya siku ya Mahakama nchini iliingilia uhuru wa mahakama.


Akielezea utata uliojitokeza katika hotuba hiyo Rungwe amesema hotuba hiyo ilionekana kama kuifundisha mahakama wajibu wake jambo ambalo lina utata katika uongozi wa kisheria lakini hata hivyo Rungwe ameielezea hotuba hiyo kuwa itaongeza uwajibikaji katika mahakama na haki kupatikana kwa wakati.


Wakati wa siku ya maadhimisho ya siku ya mahakama Alhamisi iliyopita, Rais Magufuli aliahidi kuipatia idara ya mahakama fedha kwa ajili ya kuendesha shuhguli za mahakama na kuitaka mahakama hiyo kuharakisha kusikiliza kesi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kesi za watuhumiwa wa kukwepa kulipa kodi.

Jeshi la Polisi kikosi cha Wanamaji Lakamata Mafuta ya Wizi aina ya Diesel Katika Bandari ya Dar es Salaam

$
0
0

Jeshi la Polisi kitengo cha majini limekamata tani zipatazo 20 za mafuta ya Dizeli yaliyokuwa katika Jahazi lililokuwa kando ya bandari ya Dar es Salaam likijiandaa kwa safari ya kwenda Zanzibar.
 
Mkuu wa Kitengo hicho cha polisi cha wanamaji Bwana Mboje John Kanga amesema watu watano wanashikiliwa kuhusiana na tukio hilo na uchunguzi zaidi unaendelea.
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live




Latest Images