Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live

Updates..Kilichosababisha Sintofamu Kivuko cha Kigamboni leo Asubuhi Kutaka Kuzama Hichi Hapa

$
0
0
Updates -  Kivuko cha MV Kigamboni mapema leo kilikaribia kuzama baada ya kuzidisha abiria na mizigo, baadhi ya abiria wajitosa na kuogelea.
Kilipoteza mwelekeo na kuacha njia yake hali ilozua taharuki kwa abiria.

Mwanamke wa Kikurya Apokonya Majambazi Matatu Bunduki Aina ya SMG

$
0
0
Mwanamke wa kitongoji cha Buriba, kata ya Sirari, wilayani Tarime, anayejishughulisha na biashara ya kuuza kibanda cha duka, Sophia Manguye (46), amefanikiwa kuwanyang'anya majambazi watatu bunduki moja aina ya SMG yenye risasi 27, baada ya kupambana nao ndani ya kibanda chake cha biashara.

Majambazi hayo kabla ya kunyang'anywa bunduki, yalifanya uporaji katika vibanda kadhaa vya maduka na kufanikiwa kujikusanyia zaidi ya Sh. 180,000, pamoja na vocha za simu za mkononi kutoka maduka matatu tofauti.

Jambazi aliyeporwa bunduki hiyo na Sophia ni Gesanta Matinde (19), mkazi wa kijiji cha Kebeyo, kata ya Mbogi, ikiwa na risasi 27.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tarime/Rorya, Gemini Mushi, jana alisema tukio hilo la uvamizi na unyang'anyi kwa wafanyabiashara lilitokea juzi saa 2:00 usiku katika kitongoji cha Buriba, mji mdogo wa Sirari, baada ya majambazi watatu waliokuwa na silaha aina ya SMG namba UK 5115 kuwavamia wafanyabiashara hao.

“Awali majambazi hao waliingia duka la Zaituni Magasi lililopo jirani na la Sophia na kupora fedha taslimu Sh. 100,000 kabla ya kuingia dukani kwa Sophia na kupora 80,000 za mauzo, lakini hawakuridhika na kiasi hicho, hivyo kuingia ndani na kuanza kutafuta fedha nyingine,” alisema Kamanda Mushi.

Hata hivyo, Kamanda Mushi alisema wakati wakiendelea kupekua kutafuta fedha nyingine, mwanamke huyo alimvamia jambazi aliyekuwa na silaha kisha kumng’ang’ania kwa nguvu, huku akipiga kelele za kuomba msaada hadi walipojitokeza wananchi na polisi waliokuwa karibu kutoa msaada.

Kamanda Mushi alisema baada ya tukio hilo, majambazi wawili walifanikiwa kutoroka, huku mwanamke huyo akipata majeraha usoni na mikononi wakati wa kupambana na majambazi hao.

Alisema Jeshi la Polisi limempongeza mwanamke huyo kwa ujasiri aliouonyesha pamoja na wananchi waliojitokeza na kuongeza nguvu na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa na bunduki hiyo ambayo ingeleta madhara makubwa kwa wananchi.

Aliwaomba wananchi kushiriki ulinzi shirikishi kwa kutoa taarifa za uhalifu kwa jeshi hilo mapema kabla ya matukio.

Alisema kwa sasa wanaendelea kumhoji mtuhumiwa na wengine wawili waliotoroka wakitafutwa ili waweze kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Nay wa Mitego Akanusha Wimbo Wake Kufungiwa na Basata...Adai Hata Kama Wakiufungia Wamechelewa Kwani Mpaka Panya Wanaujua Tayari

$
0
0
Nay wa Mitego Amafunguka Haya Katika Ukurasa wake wa Instagram:
"Pale unaposikia eti kuna wasiopenda kuambiwa Ukweli wamezusha Eti Wimbo wa ShikaAdabuYako Basata wamefungia. 
Guys Wimbo haujafungiwa na Basata awajafungia Wimbo ila wale wenye Team zao kwenye mitandao wamechanwa kwenye #ShikaAdabuYako ndio wameufungia kwenye Masikio Yao sababu ya hawataki kusikia fact wame publish habari za kufungiwa. Ata ingekua kweli umefungiwa wamechelewa sanaaa coz mpaka Panya wanajua tayari #TrueBoy keshakiwashaaaaa" 
Nay wa Mitego

Agness Masogange Aibuka na Kusema Haya ' Mnapoteza Muda Wenu Kunijadili Mimi'

$
0
0

Video Queen maarufu Bongo, Agness Jerald ‘Masogange’ amewataka watu kufanya kazi na kuacha kumjadili kwani kwa kufanya hivyo wanapoteza bure muda wao.

Akiteta na GPL, Masogange alisema watu wamekuwa hawafanyi mambo yao binafsi bali kujadili mambo ya watu wengine kitu ambacho siyo sahihi.

“Mimi naona wanapoteza muda tu kunijadili, wangefanya mambo yao wangeweza kuendelea kuliko kunijadili mimi hapa naona watachelewa kwenye mafanikio yao,” alisema Masogange.

Kasi ya Magufuli Yainufahisha Hospital ya Muhimbili Kwa Mapato Kuongezeka...

$
0
0

Hospitali ya Taifa ya rufaa Muhimbili, imesema baada ya kuongeza kasi ya usimamizi wa wafanyakazi katika hospitali hiyo, imeongeza mapato na yamefikia Bilioni 4.3 kwa mwezi Januari pekee

Ongezeko hilo limetokana kutengenezwa kwa mashine za MRI na CT-SCAN, mashine ya CT-SCAN imeshapima wagonjwa 1,000 na MRI imepima wagonjwa 2,200

SIRI ya Urembo wa Zari Yabainika...Hufanya hivi ili Aendelee kuwa Mbichi Japo Ana Watoto Wanne

$
0
0

Mtu wa karibu wa Zari Hassan Ametupenyezea siri ya Zari kuendelea kuwa mrembo japo ana watoto wanne kuwa ni mazoezi na kula vizuri...Anasema kila asubuhi na jioni lazima aingie Jimu japo bado ananyonyesha na kuzingatia vyakula anavyokula

Jac Wolper na Mkongo Wake Watimkia Sauzi Afrika.....

$
0
0
Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper na mpenzi wake Mkongo, wamedaiwa kuuza magari yao na kutimkia nchini Afrika Kusini ‘Sauz’.


Chanzo makini kilichoomba hifadhi ya jina, kimepenyeza ubuyu kuwa miezi kadhaa iliyopita, maisha ya Wolper na Mkongo huyo yalibadilika na kuwa magumu hivyo katika kusaka suluhisho la kujikwamua, wakaamua kuuza magari yao na kwenda kuanzisha maisha mapya Sauz.

“Jamani mambo hapa kati hayakuwaendea vizuri Wolper na mpenzi wake hivyo waliamua kutimkia Sauz lakini waliuza magari yao na kwenda kuendelea na maisha mengine huko maana Mkongo alikuwa pia na makazi kule,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kuinyaka habari hiyo gazeti hili liliwasiliana na Wolper kwa njia ya simu ambapo alikiri kuwa yupo Sauz na mpenzi wake Mkongo lakini akakana vikali suala la wao kuuza magari.

“Jamani kwa nini watu wako hivyo mimi sijauza gari langu lolote kama huamini nenda nyumbani utayakuta watu wanapenda sana kuzungumza vitu ambavyo hawana uhakika navyo kabisa.

“Tuliamua tu na mpenzi wangu tubadili maisha, tuhamie huku Sauz na si kwamba maisha Bongo yalikuwa magumu,” alisema Wolper.

Chanzo:GPL

Baada ya Kuachana na Shilole… Nuh Mziwanda Adaiwa Kufulia

$
0
0
IMEVUJA! Zikiwa zimepita siku chache tangu wasanii waliokuwa wapenzi, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ na Naftar Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ kuachana, imedaiwa kuwa mwanaume huyo amefulia na kujikuta akila kwa mama lishe huku akidaiwa kodi ya chumba anachoishi.

Chanzo makini kimeiambia Showbiz Xtra kuwa wawili hao wakati wakiwa katika uhusiano wa kimapenzi, Shilole ndiye aliyemlipia kodi ya chumba ambacho Nuh anaishi mpaka sasa kilichopo maeneo ya Sinza-Kwa Remmy hivyo muda ukiisha kuna uwezekano akatolewa vitu vyake nje kwani hawezi kumudu kulipa kodi.

“Yaani sasa hivi Nuh amefulia vibaya kwani anakula kwa mama lishe tofauti na zamani alikuwa haonekani akila hapa mtaani, unajua Shilole ndiye aliyekuwa msaada mkubwa kwake sasa wameachana itakuwa ni shida sana kwake maana ndiye aliyemlipia kodi ya chumba anachoishi,” kilisema chanzo.

Baada kuzinyaka habari hizo paparazi wetu alimtafuta Nuh ambaye alisema kuwa siyo kweli bali Shilole amekuwa akimsema maneno mengi ya uongo
“Mdomo ni jadi yake lakini ukweli ni kwamba hiki chumba ninachoishi nimelipa kodi mwenyewe kwa fedha ambazo nilipata kwenye kampeni na sijalipiwa na mtu, wakati tuko wapenzi mara nyingi alikuwa akija kulala hapa.

“Kuhusu kufulia jamani sijafulia nakula kwa mama lishe kwa sababu ndiyo maisha yetu Watanzania, zamani nilikuwa nakula nyumbani ndiyo maana nilikuwa sionekani kwa mama lishe.”

Kwa upande wa Shilole alipoulizwa kuhusiana na madai hayo ya kumpangia chumba alikuwa na haya ya kusema;
“Sitaki kusikia habari za huyo mtu kwa sababu nilishamtoa kwenye mawazo yangu, sina muda wa kumzungumzia huyo mtu kabisa.”

Chanzo:GPL

Sweet Ways To Present A Rose On Valentine's Day

$
0
0
As Val's day is just a few days away, millions around the world are getting ready to present roses, a charming stamp of affection and fondness to their lovers. Monsieur rose is very excited as it will find its way into different hands this month of love.



It is one thing to buy a rose, it is another thing entirely to present the rose in a romantic and passionate way to your partner. If you have ordered this resplendent looking rose but you are in a dilemma on how to present it to your spouse, you do not need to worry anymore as Jovago.com, Africa's No. 1 hotel booking portal share five romantic ways to present a flower to your lover. It will definitely give him or her goosebumps.

♦ Don't send the roses in a bouquet

The norm is to present roses as a bouquet on Valentine's day. It is time to take a break from this trend. How do you do this? Buy five colourful boxes or any  number you can afford and send the flowers one stalk at a time to your partner over the course of valentine's day. Also, ensure that you do not use the same dispatch person for delivery. Aside from the fact that you love him or her, it also adds fun to the rose presentation. Don't forget to drop the reasons you love your partner in each of the boxes.



♦ Deliver the rose a day before Val

Your heart is pounding as you look forward to a quixotic outing with your partner as you cannot wait to tell him or her how much you love them. In other cases, you may not be jittery but you  are just an incurable romantic. To achieve this, send the roses before valentine's day and ensure that the roses will be staring at their face when they arrive at their table. Although, you may miss the surprise reaction but you will not miss the kiss of gratitude and love.



♦ Let her best friend give her the rose

You have been together for months now, then it is right to think you are familiar with her friends. If not all them but her best and close pals. Of course, friends are very influential when it comes to a lady agreeing to date a man. She must have probably put in a word for you.

So, do not hesitate to request her to help you deliver flowers to your woman. You can only imagine how they will gossip about you the whole day. You can knock your lover out with affection by picking her up for a Valentine's day dinner. You can present another rose to her if you want.

♦ Leave flowers at unexpected places

The little things that lovers do in a relationship are more significant. For example, helping your partner pick up his or her laundry, clearing the plates off the table after dinner and buying him or her chocolate. This goes a long way.

For Val's day, you can buy a vase of roses and secretly place it at different spots where you don't expect him or her to find them. It may be in her purse, car, bathtub, closet, refrigerator or anywhere you can think of.



♦ Present the flowers yourself

There is nothing like delivering roses you bought for him or her yourself. During break time, go to her table with the bouquet of flowers, and give it to her. Nobody will narrate how she felt when she received the flowers. You will have a firsthand experience of the blushes and excitement. Don't forget to spice it up with a bit of romance.

Sasa Udaku Special Blog Ipo Play Store..Unaweza Kuinstall Kwenye Smart Phone yako Hapa

$
0
0

Good News! Sasa Blog yako ya Udaku Special Ipo Google Play Store.

Download Udaku Special Blog Android Application CLICK HERE From Play Store

Au Bonyeza hii picha hapa chini

Huddah Monroe Amjibu Mustapha Colonel Amtaka Aseme Lini na Wapi Walifanya nae Mapenzi Mara 50

$
0
0
Week iliyopita mwanamuziki kutoka Kenya Mustapha Colonel akiwa anahojiwa na chombo kimoja cha habari alijitamba kuwa ameshawahi kulala na Mrembo Huddah Monroe kutoka Kenya Mara Hamsini..na akamsifia kuwa anajua sana mambo kunako sita kwa sita...

Sasa Huddah Monroe Amejitokeza na kujibu kama ifuatavyo:



Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yakamata Shehena Kubwa ya Bidhaa za Magendo

$
0
0
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikiwa kukamata bidhaa za magendo kwenye maeneo mbalimbali ya Ukanda  wa Bahari ya Hindi, Ziwa Victoria na mipakani.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi (TRA) Bw. Richard Kayombo wakati akifanya mahojiano na Mwandishi wa Idara ya Habari (MAELEZO) ofisini kwake Jijini Dar es Salaam kuhusu juhudi za operesheni ya kutokomeza bidhaa za magendo nchini.

Bw. Kayombo ameeleza kuwa, mkoani Lindi TRA imefanikiwa kukamata mashua katika bandari ya Lindi ambayo ilisheheni bidhaa za magendo zenye thamani ya shilingi 159,361,046.

Ameongeza kuwa katika operesheni hiyo, TRA imefanikiwa kukusanya kodi ya jumla ya shilingi 10,500,678 kutoka katika bidhaa zilizokuwa katika nyaraka za forodha (manifest) ambapo pia inategemea kukusanya kodi ya shilingi 19,529,500 kutoka katika bidhaa ambazo zilikuwa katika nyaraka za forodha lakini thamani yake ilikuwa chini ya bei halisi.

Akitaja bidhaa hizo za magendo zilizokamatwa katika mashua hiyo ni mifuko 3,725 ya sukari yenye thamani ya shilingi 127,070,562, betri katoni 50, mchele mifuko 3,087, mafuta ya kula madumu 80, majokofu manne ya mtumba, baiskeli 4 za mitumba pamoja na katoni 20 za hamira.

“Mashua hiyo ilikamatwa katika bandari ya Lindi tarehe1 Februari, 2016 baada ya wasamaria wema kutoa taarifa ya kuwepo bidhaa za magendo ndani ya mashua hiyo ambapo upakuaji wa shehena hiyo ulianza mara moja.’’Alisema Kayombo.

Ameongeza kuwa,  Jijini Dar es Salaam, TRA kwa kushirikiana na kikosi cha doria cha Jeshi la Wanamaji wameweza kukamata Jahazi lenye jina la ‘Takbiri’ lenye usajili wa namba Z-875 likiwa limesheheni lita 19,700 za dizeli ambapo thamani yake bado haijapatikana kwakuwa imepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya Uchunguzi zaidi.

Aidha, majahazi mengine matatu yamekamatwa katika eneo la Kigombe mkoani Tanga ambayo yalikuwa na bidhaa za magendo yenye thamani ya shilingi 99, 682, 273, 48 ambapo ndani kulikuwa na magunia ya sukari, mchele, mafuta ya kula, matairi ya magari, nyavu za kuzuia mbu, jokofu, jiko la umeme, rangi za kupuliza, betri na biskuti.

Majahazi hayo yalitaifishwa baada ya wahusika kujitosa ndani ya maji na kutoroka.

TRA kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi inafanya doria saa 24 kila siku katika maeneo yote yaliyoshamiri upitishaji wa bidhaa za magendo pia imeunda Kanda Maalum katika maeneo ya Mbweni, Msasani, Kunduchi pamoja na Kigamboni.

Waziri Mkuu Afanya Tena Ziara Ya Ghafla Bandarini.........Aibukia kitengo cha mita za kupimia mafuta Kurasini,akuta zimejaa kutu Ataka barua ya maelezo.

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara ya ghafla kwenye kitengo cha upimaji mafuta bandarini (Oil Flow Metres) na kukuta zimejaa kutu baada ya kutelekezwa kwa miaka zaidi ya mitano. Pia alitembelea mita za kupimia mafuta zinazoendelea kujengwa Kigamboni.

Aidha, Waziri Mkuu amempa saa nne tu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo nchini (WMA), Bi. Magdalena Chuwa aandike barua ya kujieleza ni kwa nini aliamua kufunga mita hizo zisitumike kwa zaidi ya miaka mitano iliyopita na amletee barua hiyo ofisini kwake ifikapo saa 11 leo jioni.

“Nataka unieleze ni kwa nini ulitoa maelekezo ya kufunga mita hizo, na kwa nini jana uliamua kubadili uamuzi huo? Ni kwa nini umeamua kuchukua maamuzi haya baada ya kupokea ujumbe wa simu ya mkononi (sms) wakati mita zimekaa bila kufanya kazi kwa miaka mitano? Ni kwa nini umeamua kufanyia kazi ujumbe wa sms wakati unajua Serikali inafanya kazi kwa maandishi rasmi?” alisema Waziri Mkuu.

“Umesema mlikuwa mnatumia utaratibu wa kupima kwa kijiti. Huu hauna uhakika na huwezi kutegemea taarifa ya mtu mwingine au kuingia kwenye meli ya mtu na kuanza kuchukua vipimo hadi ujiridhishe. Nataka kujua ni kwa nini mlikuwa na utaratibu wa ku-bypass mafuta ili yasipite kwenye mita za kupimia mafuta? Ni kwa nini umetoa amri zianze kutengenezwa jana na siyo mwaka 2012 au 2013?” alihoji Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu alisema mita hizo za Kurasini zilinunuliwa na Serikali kwa gharama za dola za marekani milioni 1.2 (wakati huo) na haiwezekani kuacha kuzitumia wakati watu wanachezea mifumo na kuongeza mianya ya kupoteza mapato kwa Serikali. Ameagiza mita hizo zianze kufanya kazi mara moja.

Wazir Mkuu alisema matumizi ya mita hizo yaliafikiwa na Serikali baada ya kubaini upotevu mkubwa wa kodi kwenye mafuta yanayoingizwa nchini na baada ya kuona hakuna tija ya kuendelea na ukadiriaji au kupokea taarifa za waagizaji peke yao.

Waziri Mkuu ambaye aliwasili Kurasini leo saaa 4: 30 asubuhi (Alhamisi, Februari 11, 2016) kwenye kitengo hicho kilichopo Kurasini (Kurasini Oil Jetty), alikagua mita hizo na kisha kwenda kukagua meli iliyokuwa ikishusha mafuta bila kutumia mita hiyo ya kupima mafuta yanayopokelewa kwa sababu mafundi walikuwa bado wanaendelea na ukarabati.

Akiwa Kurasini, Waziri Mkuu alielezwa na Bibi Chuwa kwamba mita hizo zilianza kufanyiwa ukarabati jana na leo asubuhi moja imekamilika ambayo ni ya kupokelea mafuta ya petroli. Ya dizeli ilikuwa inafunguliwa na mafundi na kukutwa imejaa kutu sababu ya kutotumika kwa muda mrefu.

“Hii ya dizeli imefunguliwa leo na ile ya mafuta ya kula, haijawahi kufanya kazi tangu ilipofungwa mwaka 2011,” alielezwa Waziri Mkuu na Kaimu Mkurugenzi wa Bandari, Eng. Aloyce Matei.

Alipoulizwa ni kwa nini aliamua kuzifungia mita hizo ziisifanye kazi, Bi. Chuwa alijibu kuwa alifikia uamuzi huo baada ya kupokea malalamiko kwamba zinawapunja wateja. Hata hivyo, hakufafanua ni wateja gani au wa aina gani.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa, ametembelea na kukagua mita mpya za kupimia mafuta ambazo zinajengwa Kigamboni. Mita hizo zimegharimu dola za marekani milioni 6 (sawa na sh. bilioni 12.96/- za sasa).

Akiwa hapo, Waziri Mkuu alielezwa kwamba ujenzi huo ambao ulianza miezi nane iliyopita, unatarajiwa kukamilika ifikapo katikati ya mwezi Machi, 2016. “Tunajitahidi kazi hii ikamilike ifikapo katikati ya mwezi ujao,” alisema Eng. John Bura, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya BQ Contractors Ltd ambayo inasimamia ujenzi wa mita hizo.

Vilevile, Waziri Mkuu alitembelea sehemu ya kuchukulia mafuta yanayotoka bandarini (TPA Manfold) iliyoko Kigamboni na kukagua mitambo ya kusambazia mafuta kwenye matenki ya mafuta ya kampuni ya TIPER yaliyoko Kigamboni yanayomilikiwa kwa ubia bainaya Serikali na kampuni ya Oryx Energies.

Katika ziara hiyo ilibainika kuwa Kampuni ya TIPER imejiunganishia bomba la moja kwa moja kutoka kwenye bomba kubwa la mafuta linalotoka bandarini hali iliyomlazimu Waziri Mkuu kuagiza kwamba bomba hilo litolewe kwenye maungio hayo ndani ya mwezi mmoja.

“Natoa mwezi mmoja hili bomba liondolewe kwenye mfumo huu na kama yapo mabomba mengine pia yaondolewe,” alisema huku akionyesha karatasi iliyokuwa mfukoni kwake yenye mchoro unaobainisha kuwa kuna bomba jingine la inchi 10 limeungwa kinyemela kwenye bomba kuu.

“Kila mmoja anapaswa aje kuchukua pale kwenye manfold ili tujue nani kachukua nini. Msajili wa Hazina hili ni eneo lako na wewe unamiliki TIPER kwa asilimia 50, hebu simamia hili. Ninyi TPA leteni mapendekezo yenu Serikalini ili tuone tunaweza kudhibiti vipi vitendo kama hivi,” alisema Waziri Mkuu.

Pia alimtaka Msajili wa Hazina, Bw. Lawrence Mafuru awasiliane na Mwanasheria Mkuu ili waangalie upya mkataba na umiliki wa matenki hayo uwe chini ya Serikali kwa asilimia 100 ili mafuta yanayoagizwa na Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (Petroleum Bulk Procurement Agency) yaweze kuhifadhiwa huko.

Mapema, Waziri Mkuu ambaye alifuatana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, alikagua eneo la manfold ya Mamlaka ya Bandari iliyopo Kigamboni na kukuta ni kampuni nne tu zenye matenki Kigamboni ambazo zinachukua mafuta yao hapo.

Kampuni hizo ni HASS, WORLD OIL, LAKE OIL na MOIL. TIPER haikutaka kufuata mfumo huo licha ya kuwa nafasi ya kufanya hivyo ipo. Kampuni nyingine zenye matenki yake nchi kavu, zinachukulia mafuta kwenye manfold ya Kurasini.

Rais wa South Africa Jacob Zuma Acopy na Kupaste Anachofanya Magufuli kwa Tanzania...

$
0
0
Zuma yupo analihutubia Bunge, amechukua hatua za kukata matumizi ya serikali sawasawa kabisa na alivyofanya Magufuli , mfano safari za nje lazima zizipate kibali, sherehe za kibunge, kusafiri nje na delegation kubwa marufuku na mengine mengi.

Ama kweli Magufuli ni mfano duniani!

Majangili Waliotungua Helikopta na Kumuua Rubani Mzungu Wahukumiwa Jela Miaka 70 Leo

$
0
0


Watuhumiwa wanne kati ya tisa wanaotuhumiwa kuhusika na tukio la kutungua helikopta iliyokuwa ikifanya doria kwenye pori la akiba la Maswa wilayani Meatu Mkoani Simiyu na kumuua rubani wake, wamehukumiwa kifungo kwenda jela miaka 70.

Watuhumiwa hao wamehukumiwa adhabu hiyo katika mahakama ya wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu kwa kesi ya tatu inayowakabili watuhumiwa saba ambayo ni kukutwa na silaha kinyume cha sheria iliyokuwa chini ya Hakimu mfawidhi wa Mahakama hiyo Mary Mrio.

Baada ya maelezo ya wakili huyo mahakamani hapo, watuhumiwa wote wanne kati ya saba walikiri kutenda makosa hayo, ambapo wote waliiomba mahakama kuwapunguzia adhabu kwa kile walichoeleza kuwa ni mara yao ya kwanza kutenda makosa kama hayo.

Hata hivyo wakili Mlekano aliitaka mahakama kutoa adhabu kali kwa watuhumiwa wote ili kuwa fundisho kwa watu wengine wenye nia ya kutenda makosa kama hayo.

 Akitoa hukumu mbele ya watuhumiwa Hakimu huyo alisema kuwa katika kosa la kwanza, pili pamoja na kosa la nne kwa watuhumiwa wote wanne mahakama imewahukumu kifungo cha maika mitano (5) kila mmoja kwenda jela.

Hata hivyo Hakimu Mrio alieleza kuwa katika kosa la tatu ambalo watuhumiwa wawili kati ya hao saba walikiri kutenda, mahakama imewahukumu kifungo cha miaka mitano (5) jela kila mmoja au kulipa faini ya shilingi Milioni 10.

Kwa pamoja watuhumiwa wote wanne watatakiwa kutumikia kifungo jela miaka 70, huku baadhi yao wakitumikia kila mmoja kifungo cha miaka 20 na wengine kifungo cha miaka 15 kila mmoja.

Katika kesi hiyo Njile Gunga ambaye anadaiwa kutungua ndege hiyo atatumikia kifungo cha miaka 20, huku akiwa anakabiliwa na kesi mbili ikiwemo ya mauaji pamoja na uhujumu uhumi ambazo mahakama hiyo haina uwezo wa kuzisikiliza.

Taswira ya Jengo la Ghorofa 16 Linalovunjwa Dar Baada ya Kukiuka Taratibu

$
0
0

Mafundi ujenzi wakiwa kazini kutekeleza uvunjaji wa jengo hilo lililopo mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar.

KAZI ya kuvunja jengo la ghorofa 16 lililojengwa kinyume cha taratibu za kitaalam inaendelea jijini Dar es Salaam katika Mtaa wa Indira Ghandi. Amri hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar, Said Meck Sadick, kutokana ushauri wa wataalam.

Ofisi za CCM Kengeja Pemba Zachomwa Moto na Nyumba Kupigwa X Usiku

$
0
0

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimelaani vikali kitendo cha kuwekwa alama ya X nyumba kadhaa za wafuasi wake Kisiwani Pemba hivi karibuni.

Aidha, kimesikitishwa na kulaani vikali kitendo cha kuchoma moto Tawi la CCM la Kengeja, kilichofanywa na watu wasiojulikana usiku wa kumkia leo.

Hayo yamesema na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC wa Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar, Bibi Waride Bakari Jabu, alipokuwa akizungumza na Wanahabari hapo Afisini kwake Kisiwandui, Mjini Unguja.

Amesema kitendo cha kuweka alama ya X kwenye nyumba za wafuasi wa CCM pekee katika maeneo ya Mtambile, Kengeja, Minazini na Kangani Wilayani Mkoani sio tu kina lengo la kuvunja amani iliyopo nchi bali pia kinakwenda kinyume na sheria na taratibu za Taifa letu.

“Kwa niaba ya CCM nachukua nafasi hii kulaani vikali na kuwataka wale wote waliohusika na vitendo hivyo, waache mara moja, kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria na taratibu za nchi yetu” na kuongeza kusema kuwa kinapaswa kulaaniwa na kila mpenda amani na ustawi wa demokrasia ya kweli nchini”. Alidai Bi. Waride.

Ametoa wito kwa Wazanzibari hasa wafuasi wa CCM kupuuza vitendo hivyo, na badala yake waelekeze nguvu zaidi katika maandalizi ya uchaguzi wa marudio uliotangazwa kufanyika Machi 20, ili kukiletea ushindi wa kishindo Chama hicho (CCM).

Kuhusu kuchomwa moto Tawi la CCM Kengeja, Bibi Waride amesema Chama Cha Mapinduzi kimeshtushwa na kitendo hicho, kwani sio tu kinarejesha nyuma maendeleo ya chama, bali pia kinawatia hofu wana CCM wa maeneo husika.

Amesisitiza haja kwa Vyombo vya Ulinzi hasa Jeshi la Polisi kuwatafuta wale wote waliohusika na hujuma hiyo, na kuwafikisha mbele ya Vyombo vya Dola ili Sheria iweze kuchukua mkondo wake.

Mrembo na Mwigizaji Thea Adaiwa Kuhongwa Gari

$
0
0
STAA wa filamu Bongo, Salome Urassa ‘Thea’ sasa hivi anasukuma mkoko baada ya kutembea kwenye vumbi kwa muda mrefu lakini pia taarifa zilizo nyuma ya pazia zinadai eti kahongwa na mwanaume.

Inadaiwa baada ya Thea kumwagana na Michael Sangu, alijiweka kwa mwanaume mwenye nazo na ndiye aliyempa jeuri ya kumiliki gari hilo aina ya Toyota Passo.

“Thea sasa mambo safi, anatembelea makalio baada ya kuhongwa gari na yule bwana wake wa sasa,” kilidai chanzo hicho.

Baada ya kunyaka ‘ubuyu’ huo, Thea alitafutwa, alipopatikana alisema: “Hili gari sijahongwa na katika maisha yangu sitegemei kuhongwa na mtu yeyote, nimenunua kwa hela yangu ninayopata kwenye muvi.

Madhara ya Kujichua Kwa Mwanamke Kwa Kutumia Vifaa Haya Hapa..

$
0
0
Kama ilivyo kwa jinsia ya kiume, kuna wanawake pia ni wahanga wa kufanya punyeto kwa kutumia vifaa tofauti tofauti.

Haya ni baadhi ya madhara awezayopata mwanamke anayejichua;

1. Inaharibu kizazi

2. Inakufanya kua mvivu mara kwa mara

3. Unakuwa unakosa hamu ya tendo

4. Maumivu ukeni yasiyo na sababu

5. Uke kuwa mlegevu yaani mtepeto

6. Hupelekea uke kutoa maji maji mara kwa mara au maji yale ambayo utoka kabla ya tendo kuto kuwepo ivyo itakufanya kupata michubuko na maumivu makali wakati wa tendo.

7. Uwezi kuja kujua raha ya tendo ukizoea punyeto sana wewe dada.

8. Punyeto inafanya uke wa mwanamke kukosa ladha kabisa hiyo itapelea kukimbiwa na mmeo au mwenzako kutafuta kamchepuko kenye uke mtamu.

9. Na ukizoea punyeto itakufanya kuwa mtu wa hasira hasira kila mara

10. Punyeto ni hatari kwa afya yako pia ukiizoea sana itapekekea kufanya mapenzi ya jinsia moja.

Askari wa Kike wa Usalama Barabarani na Mpenzi wake Waungua moto Hadi Kufa Kisa Hichi Hapa

$
0
0
Picha ni ya Tukio jingine la Moto
Askari wa kike wa Usalama Barabarani, Attuganile Mwakibete (37) na mpenzi wake Sunday Mhagama (36), wameteketea kwa moto baada ya nyumba walimokuwa ndani kuungua.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alisema tukio hilo lilitokea Februari 2, mwaka huu saa 7:15 mchana katika kitongoji cha Maporomoko, Kata na Tarafa ya Laela Wilaya ya Kipolisi ya Laela.

Inadaiwa kuwa nyumba hiyo iliyoteketea kwa moto ambayo askari Attuganile alikuwa amepanga vyumba viwili, ni mali Yaiyela Mwamahonje aliyokuwa akiishi na watoto wake wawili wadogo ambao wamenusurika kufa, licha ya kuwemo ndani ya nyumba hiyo wakati wa ajali hiyo.

Taarifa za uhakika zinaeleza kuwa Mhagama aliyekuwa rafiki wa trafiki huyo wa kike, ni mkazi wa Mbeya ambako mkewe anaishi, na alikuwa na mazoea ya kumtembelea mpenzi wake huyo mara kwa mara.

Inadaiwa askari Attuganile alikuwa ameachana na mumewe wa ndoa. “Vyumba viwili yaani sebule na chumba walimokuwemo Attuganile na Mhagama viliwaka moto baada ya jenereta lililokuwa likifanya kazi likiwa sebuleni humo kulipuka na kuwajeruhi vibaya,” alieleza.

Kwa mujibu wa Kamanda Mwaruanda, Attuganile alifariki dunia Februari 8, mwaka huu saa 2:30 asubuhi akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa mjini Sumbawanga.

Mhagama alikimbizwa na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya jijini Mbeya ambako alifariki dunia Februari 9, mwaka huu. Kamanda Mwaruanda alisema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.

Viewing all 104793 articles
Browse latest View live




Latest Images