Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104808 articles
Browse latest View live

Uchu wa Kufanya Mapenzi na Wanyama..Wataka Sheria Kuwaruhusu Kujamiana na Wanyama

$
0
0
Walalmishi wawili wameshindwa katika jaribio lao la kuishinikiza mahakama ya kikatiba nchini Ujerumani kuangazia madai yao dhidi ya sheria inayopiga marufuku kujamiana na wanyama.

Watu hao ambao majina yao hayakutajwa wanasema kwamba wana uchu na wanyama.
Walitaka kuishinikiza mahakama hiyo iliopo Karlsruhe kufikiria iwapo sheria hiyo ni kinyume na katiba.

Hatahivyo mahakama hiyo ilitupilia mbali madai yao ikisema kuwa ni haki kwa sheria hiyo kuendelea kufuatwa.

Mahakama ilisema kuwa kuwalinda wanyama dhidi ya unyanyasaji wa kingono ni jukumu la sheria ,ambayo haikubadilishwa kufuatia uamuzi wa mahakama hiyo.

Sheria za kuwalinda wanyama nchini Ujerumani zimeweka faini ya $27,700 kwa wale watakaowalazimisha wanyama kushiriki katika tabia mbaya.

Mgogoro wa Wamasai na Wamang’ati Wamalizwa Wilayani Kondoa

$
0
0
Juhudi za viongozi wa serikali wanasiasa na viongozi wa mila kutoka mikoa ya Manyara na Dodoma wakiongozwa na naibu waziri wa kilimo mifugo na uvuvi William Ole Nasha wamefanikiwa kumaliza mapigano ya watu wa jamii ya kifugaji kutoka makabilia ya Masai na Mang'ati (Tatoga) waliyokuwa wanagombania Ng'ombe na kusababisha vifo vya watu wawili katika mpaka wa wilaya za Kondoa na Simanjiro.

Kikao hicho kilichofanyika kwa zaidi ya masaa tisa viongozi hao wakiongozwa na naibu waziri Ole Nasha iliwabidi kutumia busara kubwa kumaliza mgogoro huo ambapo kabla ya muafaka hali ilikuwa hivi.

Baada ya kikao viongozi wa kisiasa kutoka katika kabila hizo mbili mbunge wa Simaniro James Milya mbunge wa Hanang Mary Nagu Flatei Maasai wa Mbulu vijijini na mwenyekiti wa halmashauri ya Simanjiro Jackson Sipitek wakatoa kauli zao.

Baadae naibu waziri wa kilimo mifugo na uvuvi William Ole Nasha aliongoza muafaka huo akaitimisha kwa kueleza walicho afikiana hadi kufikia makubaliono ya kusitisha mapigano hayo.

Papa Francis, Donald Trump wavutana kuhusu ukristo wa Mgombea huyo

$
0
0
Papa Francis na mgombea wa Republican mwenye matamshi tata, Donald Trump wameingia kwenye mvutano kuhusu ukristo wa mgombea huyo kufuatia matamshi yake kuwa akichaguliwa kuwa Rais wa Marekani atajenga ukuta mpakani mwa Mexico na Marekani ili kuzuia wahamiaji kuingia nchini humo.

Trump alieleza hivi karibuni kuwa atachukua hatua hiyo ikiwa ni sehemu ya jitihada za kulinda usalama wa Marekani ikiwa ni pamoja na kuzuia Watu wenye imani ya Kiislamu kuingia nchini humo.

Kauli hiyo ya Trump imeonekana kumkwaza Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis ambaye amesema kuwa mtu anayepanga kujenga ukuta kati ya Marekani na Mexico badala ya kujenga daraja ‘sio Mkristo’.

“Mtu anayefikiria kujenga ukuta, kokote walipo, na sio kujenga madaraja, sio mkristo. Hii sio injili,” Papa Francis aliwaambia waandishi wa habari.

Papa Francis alitoa kauli hiyo katika siku yake ya mwisho ya ziara ya Mexico. Alisema kuwa hawalazimishi wakristo kumchagua au kutomchagua mtu fulani, lakini wampime kauli zake kabla ya kufanya maamuzi katika sanduku la kura.

Trump amejibu kauli hiyo ya Papa akieleza kuwa Kiongozi huyo hana haki ya kumhukumu mtu yeyote kuwa ni Mkristo au sio Mkristo.

“Hakuna kiongozi, hususan kiongozi wa dini, mwenye haki ya ya kuhoji  imani ya kidini ya mtu mwingine,” Trump alisema.

“Kama Vatican itashambuliwa na ISIS, ambapo kila mmoja anajua kuwa ni tuzo muhimu ya ISIS, ninawaahidi kuwa Papa atatamani na kuomba kuwa Donald Trump angekuwa Rais,” aliongeza Trump.

Wema Sepetu Afunguka...Baada ya Tetesi za Mkongo Man na Idris Sultan Kupigwa Kibuti

$
0
0
Baada ya Tetesi za Kumpiga Idris Kibuti na Kuruka na Mkongo man leo kuzagaa huko mitandaoni, Wema Sepetu ameandika Haya....

Wemasepetu 
Nilizaliwa peke yangu... Na siku nikifa nadhani hakuna mtu atakaeingia kaburini na mimi... Nitazikwa Peke yangu.... So i guess we good...!!! Gnyt now....!!! I was born ALONE... And when I die I dont think anyone is gon give me company in my Grave... Means Il be buried ALONE.... Nadhani tumeelewana...!! Adios for now... Mpaka kesho...!!!

Jack Pemba (Ex Mume wa Aunty Ezekiel) Aonyesha Jeuri ya Fedha Uganda...

$
0
0
Aliyekuwa mume wa super star aunty ezekiel, aitwaye Jack Pemba pesa imeonekana ikizidi kumtembelea baada ya hivi karibuni kuonekana nchini Uganda akifanya kufuru ya aina yake , ambapo alikuwa akiosha moja kati ya magari yake ya kifahari aina ya range rover kwa kutumia Mvinyo wa bei mbaya huku akitumia ma dolali kufuta gari lake hilo, hali iliyozua gumzo jijini Uganda na kuwaacha watu midomo wazi.

Mume wa msanii huyo inadaiwa anafanya biashara nchini Uganda ikiwemo ya kumiliki makampuni kadhaa ya magari pamoja na maduka mbali mbali nchini humo

Zitto Kabwe Ampa Laivu Rais 'Wanaokusifia tu Hawakusaidii'

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa watu wanaomsifia tu Rais Magufuli hawawezi kumsaidia katika kufikia malengo yake ya kuleta maendeleo na mabadiliko kwa taifa hili.

Zitto Kabwe aliweka wazi hayo kupitia ukurasa wake wa Facebook na kusema anashukuru kuona Rais Magufuli anawasikiliza PIA watu ambao wanamkosoa kwa malengo mazuri kwani wana nia njema na wanatumia uzalendo wao wa hali ya juu kukosoa.

"Rais Wanaokusifia tu hawakusaidii. Umefanya vema kusikiliza tunaokukosoa. Tuna nia njema na tunatimiza uzalendo wa hali ya juu ambao ni kukosoa. Hatusemi wasikusifie, hapana. Wawe na kiasi" Aliandika Zitto Kabwe.

Siku za karibuni Zitto Kabwe aliandika Makala ya mambo kumi ambayo Rais Magufuli hajafanya ndani ya siku 100 na katika makala yake, jambo la nne alizungumzia suala la uingizwaji wa sukari kutoka nje na kusema ni jipu ambalo limeiva na linatakiwa kutumbuliwa.

"Tanzania bado inaagiza Sukari kutoka Nje na serikali haina mpango wowote ule wa kuondoa tatizo hilo. Hata katika mpango wa maendeleo serikali haisemei sukari kabisa. Uagizaji wa sukari ni jipu" Zitto Kabwe

Lakini Rais Magufuli ni kama amesikia kilio cha Mh Zitto Kabwe kwani tayari ametangaza kufutwa kwa vibali vya uingizwaji wa sukari nchini, jambo ambalo Mh Zitto amemshukuru Rais kwa kuliona na kulifanyia kazi na kumuomba pia aliangalie suala la IPTL/PAP nalo bila kulionea kigugumizi chochote.

"Rais Magufuli nakupongeza kwa kuona tusemayo wapinzani wa chama chako. Umetekeleza jambo 1/10 niliyoeleza kuwa hujafanya. Naomba utekeleze na hayo mengine kwa manufaa ya nchi yetu. Hili la IPTL/PAP mbona unalipatia kigugumizi ndugu Rais?
Umetoa agizo kuhusu hili. Shukrani sana" Aliandika Zitto Kabwe.

Picha ya Wema Sepetu na Mkongo Man Yazua Balaaa Mtandaoni...Tetesi za Idriss Sultan Kutemwa zaibuka...

$
0
0
Mpya mjini hapa leo ni habari ya Mkongo ajulikanae kama Apocalypse na Wema Sepetu, Wawili hawa inasemekana wako pamoja kimapenzi kiasi cha kupiga picha na video na kuziweka mitandaoni huko Instagram na Snapchat...Tetesi hizi zinasema kwa sasa Idriss Sultan hana chake baada ya mimba kutoka, mkongo huyo inasemekana ana mavumba ya kutosha na alishawahi kutoka na mrembo Huddah Monroe wa Kenya.....

Toka habari za mimba kutoka Idriss Sultan ama Wema Sepetu hawajawahi kuweka picha zao kwenye page ya Instagram kama walivyokuwa wanafanya zamani kitu ambacho kinaongeza tetesi za kuachana kwao....Leo Idris amempost demu mwingine ambani ni rafiki yake kwa kile kinachoonyesha kama kupoza machungu ya Wema na Mkongo kupost ma video yao.....

Huyu Ndio Mukongo Anayesemekana kuwa yupo na Wema Sepetu Kwa Sasa, Hapo akiwa katika Hotel ya Hyatt Regency baada ya kuwasili jana...

Ni tetesi tu......

Dogo Janja Azungumzia Uhusiano Wake na Uongozi wa Tip Top Baada ya Kudai Unambania

$
0
0
Msanii wa muziki wa Hip Hop, Dogo Janja baada ya kusambaa audio yenye sauti yake katika mitandao ya kijamii akidai uongozi wake Tip Top Connetion unambania, amefunguka na kueza hali ilivyo.

Rapa huyo ambaye hajatoa ngoma yoyote kwa kipindi cha mwaka mmoja, ameiambia Bongo5 kuwa amejaribu kumtafuta bosi wake Madee ili amweleze kwanini aliongea vile lakini bado hajampata.

“Kiukweli siwezi kukataa ile sauti ni yangu, na aliyezingua ni msichana na sijui alinirekodi kwa nia gani,” alisema Dogo Janja.
“Mpaka sasa hivi sijaweza kuongea na Madee, nimekuwa nikimtafuta kwenye simu lakini amekuwa hapokei simu zangu, pia nimejaribu kumtumia meseji hajibu. Kama jana tulipata bahati ya kwenda kwa Mh Magufuli na yeye pia nilimuona, lakini sikuweza ongea nae, nilivyosema nimtafute kusema kweli akawa ameshaondoka na sikuweza kumfuta wakati waheshimiwa wako pale ningeonekana msumbufu. Siwezi sema ameichukilije kauli yangu mpaka nipokutana ane ndipo nitazungumza,” aliongeza.

Team Wema Sepetu..Wamfariji Idriss Sultan Baada ya Wema Kuonekana Anatesa na Mwanaume Mwingine..Wengine Wahama Team

$
0
0
Baadhi ya page maarufu zilizokuwa zinamtetea Wema Sepetu kwa liwalo na liwe huko mitandaoni hasa Instagram wajulikanao kama Team Wema naona baada ya tukio la jana wengi wamekata tamaa na kumua kuhama team na Wengine kuondoa picha za Wema Sepetu kabisa kwenye page zao wakidai Wema Anawachanganya.

Huyu Matikiboko ya kwa muda mrefu amekuwa akimsupport Wema na kufikia kutukanana na watu mitandaoni hadi kufikishwa polisi kwa kumtetea Wema, Jana Amefuta picha zote za Wema Katika Account yake na kuweka za Nick Minaj....


Wengi leo Wameonekana kwenye page zao wakimfariji Idris Sultan baada ya Kupigwa kibuti...

Baadhi ya Comments kutoka Team Wema

iamneez25
@sarahmwakinyuke we na mm atuna tofaut mi siko team wema ila i love her bt matendo yake yanakera sana sio sir mpaka kina mati kufika huku ujue yamewachosha wanamtetea mpaka wanaonekana wehu mati ad police kakaa kisa wema inauma kwakwel inamuuma sana, ila yataisha haya na watarud kua kama zaman


matikibokoyao 
@idrissultan nakupenda sanaa baba

katunzi_ 
Yan wema kajua kutuvuruga lujichanganya kwa yule Osama hatosahau mana keshaxoea ATA akiyakoroga tunamtetea this time hapana bwana tunampenda iddy wallah Kama nikupe mdogo Wangu vile mlokole @idrissultan team idriss Miller

kimongat 
 I'm no longer team wema anadhalilisha sana sitakiiiii

mefmi
 hahaahaa nimekubali insta bila wema hapanogi yaani kumekuwa kimyaaaa! mi nasubiri atoe tamko tu ni delete account yangu maana nilimpenda yeye na idrissa basi! tena nitashukuru niendelee na shughuli zangu maana nilikuwa kama chizi kila mda nachungulia wamepost nini
Read more at http://websta.me//n/matikibokoyao#LSWefSsoloGiCl2C.99

Rwanda Wampongeza Rais Magufuli Kwa Kutumbua MAJIPU Bandarini.

$
0
0
WAFANYABIASHARA wa Rwanda wamepongeza hatua zinazochukuliwa na Rais John Magufuli katika Bandari ya Dar es Salaam, kwa kuimarisha ufanisi wa bandari, kukuza biashara baina ya Tanzania na nchi jirani.

Aidha wamesema tangu Rais Magufuli aanze kuchukua hatua hizo, mizigo yao imekuwa salama zaidi na wamefanikiwa kuipata kwa urahisi tofauti na zamani ambapo mingi ilikuwa ikipotea.

Hayo yalielezwa jana na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Akizungumza baada ya kutua nchini akitokea Kigali, Rwanda, Balozi Mahiga alisema pia Rais wa nchi hiyo, Paul Kagame amemhakikishia kuwa ataendelea kushawishi wafanyabiashara wake kutumia Bandari ya Dar es Salaam, ili kukuza uhusiano wa kibiashara uliopo.

“Nilipata bahati ya kuzungumza na wafanyabiashara wa kule... wamepongeza sana hatua zinazochukuliwa na Rais Magufuli pale bandarini kwa sababu wanasema sasa hivi itawasaidia sana kuhakikisha usalama wa mizigo yao,” alisema Blozi Mahiga.

Alisema wafanyabiashara hao pia wameomba mkutano wa pamoja na wenzao wa Tanzania, ili kujadili masuala mbalimbali, ikiwemo fursa za uwekezaji ndani ya Rwanda na Tanzania.

Alisema Rais Kagame anaunga mkono ujenzi wa reli itakayotumika kusafarisha mizigo kwa kuwa ni njia mojawapo ya kukuza uchumi wa nchi hizo mbili rafiki.

Akizungumzia safari yake hiyo, Balozi Mahiga alisema, alienda nchini humo kujadiliana masuala mbalimbali aliyoagizwa na Rais Magufuli kwa Rais wa nchi hiyo, ambapo walijadili masuala matatu, ikiwemo machafuko yanayoendelea Burundi.

Alisema kuhusu machafuko ya Burundi, Rais Kagame alikanusha tuhuma zinazotolewa na nchi hiyo pamoja na jumuiya za kimataifa kuwa anahusika katika kuchochea machafuko hayo.

Kwa mujibu wa Balozi Mahiga, maandamano ya nchi nzima yaliyofanyika wiki iliyopita nchini Burundi ya kuishutumu Rwanda kuhusika na machafuko nchini mwao, yalishitua nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kutokana na baadhi ya maneno ya chuki yaliyokuwa yakitolewa na wananchi hao dhidi ya nchi hiyo.

Alisema hali hiyo, ilihofiwa kwamba ingeweza kuvunja mazungumzo ya kutafuta suluhu yanayoendelea. “Nilimuuliza Rais Kagame kuhusu hili suala, akasema hatachukua hatua yoyote licha ya kwamba wananchi wake wamemlazimisha kufanya kitu."

 Lakini alisema atashiriki katika majadiliano ya kutafuta suluhu ya Burundi. “Sisi tulikuwa tunahofia kuwa huenda akachukua hatua ambazo zingeweza kuleta matatizo na hata mazungumzo yanayoendelea kuvunjika, lakini ameniambia hatachukua hatua yoyote inayoweza kusababisha kuvunjika kwa uhusiano,” alisema Balozi Mahiga.

Hata hivyo, alisema Rais Kagame alilalamikia nchi yake kushutumiwa kwa kutoa mafunzo ya kijeshi kwa wakimbizi wa Burundi, ili kuipindua Serikali ya nchi hiyo na kutaka Jumuiya za Kimataifa, kuwaondoa wakimbizi zaidi ya 70,000 na kuwahamishia nchi nyingine za jirani.

“Aliniambia kuwa kuendelea kuwa na hawa wakimbizi katika nchi yake, kunaweza kumletea matatizo makubwa, kwa sababu amekuwa akilaumiwa sana. Hivyo kuliko lawama, ni bora hizi Jumuiya za Kimataifa zikawaondoa wakimbizi,” alisema.

Alisema kwa mujibu wa Rais Kagame, Rwanda itaendelea kushiriki katika mijadala mbalimbali ya kutafuta suluhu ya Burundi na itahakikisha Burundi inakuwa salama.

Jambo lingine walilozungumza na Rais Kagame ni mkutano wa marais wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, unaotarajiwa kufanyika mwisho wa mwezi nchini Tanzania, ambapo pia alikuwa katika hatua ya mwisho katika kukamilisha ajenda na watakaoshiriki mkutano huo.

Ben Pol Asema Kuchora Tattoo, Kuvaa Hereni na kufuga Rasta ni Mwiko Kwenye mwili wake

$
0
0
Msanii wa muziki wa R&B Benard Paul ‘Ben Paul’, amesema hapendi kuchora tattoo, kuvaa hereni pamoja na kusuka rasta kama baadhi ya wasanii wanavyofanya kwa kuwa ana uheshimu sana mwili wake.
ben-pol

Akizungumza na gazeti la Mtanzania, Ben Paul alisema imekuwa ni kawaida kwa idadi kubwa ya wasanii kujichora ‘tattoo’ na kuwa na mwonekano wa tofauti na watu wengine, lakini kwake jambo hilo halina nafasi.

“Japo ni msanii lakini sipendi kuwa na mwonekano wa tofauti kama kufuga rasta, kuvaa hereni au kujichora mwilini kwa sababu nauheshimu mwili wangu, ndiyo maana nipo kawaida kila wakati,” alisema Ben Pol.

Ben Pol na Jux hivi karibuni wameachia wimbo wao mpya uitwao ‘Nakuchana’.

Waziri Mkuu Atinga Bandari Ya Tanga....Akutana Na MADUDU Kibao

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa jana jioni (Ijumaa, Februari 19, 2016) alikagua bandari ya Tanga na kumtaka Mkuu wa Bandari ya Tanga (Port Master), Bw. Henry Arika amletee maelezo juu ya ukiukwaji wa manunuzi ya tishari ifikapo leo (Jumamosi) saa 6 mchana.

Waziri Mkuu ambaye aliwasili Tanga jana mchana ili kushiriki mazishi ya baba mzazi wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi. Ummy Mwalimu yaliyofanyika kwenye makaburi ya Mchukuuni, Tanga, aliamua kuzuru bandari hiyo kabla ya kuelekea uwanja wa ndege akiwa njia njiani kurejea Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo fupi, Waziri Mkuu alikataa kuingia ofisini (bandarini) na akataka apelekwe mahali tishari tatu za bandari hiyo zilipo. 

Katika maswali aliyoulizwa na Waziri Mkuu, Bw. Arika alikiri kuwa matishari hayo hayafanyi kazi kama inavyotakiwa kwa sababu yanasubiri kusukumwa na tugboat  (meli ndogo).

"Nataka kesho saa 6 mchana uniletee barua yenye maelezo ni kwa nini mlinunua tishari tatu ndogo badala ya mbiili kubwa wakati mnajua Serikali ilitenga Dola za Marekani milioni 10.113 kwa ajili ya kununua tishari mbili zenye uwezo wa kujiendesha zenyewe  (self propelled) "

“Nataka maelezo ni kwa nini mlizinunua tangu mwaka 2011 lakini zimekaa bila kufanya kazi hadi Novemba mwaka jana? Na kwa nini mnaendelea kutumia hela ya Serikali kwa kukodisha tishari kutoka Mombasa badala ya kutengeneza za kwenu au kufundisha vijana wa Kitanzania? Kwani tunao wahitimu wangapi wa fani hii?" alihoji Waziri Mkuu.

"Taarifa nilizonazo ni kwamba moja ya tishari lilidondoka baharini mkaenda kutafuta huko na kulivuta hadi hapa ndiyo maana yameshindwa kufanya kazi inavyotakiwa," aliongeza.

Katika majibu yake, Bw. Arika alisema wao waliagiza tishari hizo kupitia ofisi ya Bandari makao makuu ambayo iko Dar es Salaam. 

"Pia wakati zinaagizwa sikuwepo hapa Tanga. Nimekuja mwishoni mwa mwaka jana," alisema Mkuu huyo wa Bandari ambaye inaelezwa alitokea Mamlaka ya Bandari Dar es Salaam.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Bibi Mwantumu Mahiza awaite watu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Mamlaka ya Bandari na Jeshi la Polisi wakae na kutafuta mbinu za kudhibiti njia za panya zinazotumika kupitisha sukari ya magendo.

"Mkuu wa Mkoa simamia hawa watu, msaidiane kudhibiti uingizaji wa sukari kwa njia za panya. Kuna majahazi yanaleta sukari kutoka Brazil. Mheshimiwa Rais amepiga marufuku uingizaji wa sukari kutoka nje ili viwanda vyetu vya ndani viweze kuongeza uzalishaji. Dhibitini bandari zote ndogondogo hadi Pangani," alisema Waziri Mkuu.

Alisema changamoto inayoikabili Serikali ni kwamba hata Shirika la Viwango Tanzania (TBS)  au Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) hawawezi kuzikagua sukari hizo na hazijulikani ubora wake licha ya kuwa zinafika kwa walaji.
Waziri Mkuu, Kssim Majaliwa akiongozwa na Mkuu wa Bandari ya Tanga , Henry Arika (kulia kwake) kukagua bandari hiyo Februari 19, 2016.
Matishari matatu ambayo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametaka apewe maelezo kwa maandishi kuwa ni nani aliyeidhinisha mchakato wa manunuzi yake bila kuzingatia viwango na ubora uliokusudiwa na serikali. mheshimiwa Majaliwa alifanya ziara katika bandari ya Tanga Februari 19, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

Mange Kimambi Amshukia Wema Sepetu Tena...Adai Wema Anapoteza Muda tuu Kwa Huyo Mkongo Afadhali ya Idris

$
0
0

Mange Kimambi Afunguka tena.....

"Jamani nimechokaaaaaaaaaaa kuulizwa kuhusu Wema na hili njemba, sijui terrorist atajijua mwenyewe...

I don't know anything.And I don't want to know.... All I can do is pray kuwa sio Kweli maana hapa Wema ndo atakuwa kapoteaaaaaaaa.Janaume mishow off tu, upuuzi mtupu! Yani jinga flani... .
Team Wema mmepanick Mpaka , listen hamuwezi kumpangia Mtu Maisha yake Ana akili zake Yule!!!!!! Mnaosema Wema hawezi kutulia sijui Malaya , Hana umalaya wowote anaweza kutulia vizuri. Kila mwanamke Ana Mtu wake wa kumtuliza. Nyie wenyewe mlihangaika Na boyfriend wangapi kabla hamjatulia Kwa waume zenu?

Hivi mmesahau enzi za CK, Wema Mbona Alitulia Kama maji ya mtungini, she was private miaka watu hawajui yuko Na Nani , media ilibidi ichokonoe Kweli Kweli ku found out..Yani love life yake ilikuwa private.Watu tulikuwa tu nashangaaa anakula bata hatuelewi. That's how it should be. That means Wema anaweza sana kutulia Na Mpaka tukamsahau... Enzi za CK alikua business woman Hana drama wala nini ni yeye Na kampuni yake...... Alivyo rudi tu Kudate vijana wenzie , wasaniiiii wenzie balaaa likarudi pale pale... .seriously nyie Kumbukeni tofauti ya Wema enzi za CK na alivyo rudi Kwa Watoto wenzie. The difference is huge!

Idris is a great guy I like him but he is too young kumtuliza Wema. I wish them the best though . Mwanaume wa kumfanya Wema atulie will be a millionaire, mkubwa na Mtu very down low dizain za Yule CK , Ila hawa watoto wenzie wa kumpa laki kwa mwenzi watakimbizana kila siku.. Ukweli ndo huo. Hamuoni kina Kyln walivyobadilika 360 degrees? Ukiwa Na Mtu mwenye heshma zake na mihela yake you become another person! Ila kumwita Malaya sijui nini wala sio, sababu woooote tunajua anajua kutulia vizuriiiii Mpaka tukamsahau yuko mjini! Sometimes tuweni wakweli tu Jamani mwanaume ukiwa Na hela utamtuliza hata Malaya wa Jollies, atavaa hata baibui. Bila hela mwanaume utasumbuliwa tu.

Hili Dudu baya la Congo hamna kitu hapo! Wastage of time ! Hana pesa yoyote! Na hata Kama ana pesa sio mwanaume wa kutulia nae.Mashauzi ya kitoto tu! Janaume halina Siri kuposti mipicha na caption za kitoto' Mange Kimambi

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi Ya Februari 20, Ikiwemo Boti ya Magufuli nayo ni Jibu

$
0
0

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi Ya Februari 20

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu Atangaza Oparesheni Kamata Bodaboda Nchi Nzima

$
0
0
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu amewaagiza makamanda wa Polisi kote nchini, kuendesha oparesheni kali ya kuwachukulia hatua za kisheria, waendesha bodaboda wasiotii sheria za usalama barabarani.

Ametaja makosa yatakayosababisha waendesha bodaboda hao kukamatwa kuwa ni pamoja na kubeba abiria zaidi ya mmoja, kupita katika taa nyekundu na kutovaa kofia ngumu.

IGP Mangu alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na maofisa wakuu wa Polisi, wakiwemo makamanda wa Polisi wa mikoa, vikosi na makao makuu katika kikao kazi kilichofanyika Dar es Salaam hivi karibuni ambacho kilifunguliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga.

Alisema waendesha bodaboda wamekuwa wakikaidi kufuata sheria za usalama barabarani, lakini sasa mwisho wao umefika na kuwataka makamanda wa Polisi wa mikoa kote nchini, kutekeleza maelekezo hayo, ili kuleta nidhamu kwa bodaboda katika kufuata sheria za usalama barabarani.

IGP Mangu alisema suala la kufuata sheria za usalama barabarani kwa bodaboda halina mjadala na kila Kamanda ahakikishe kuwa wote wasiofuata sheria na kukaidi, wanakamatwa bila kuoneana muhali kwa kuwa wamekuwa wakisababisha ajali zinazoweza kuzuilika.

“Pamoja na kuendelea kudhibiti uhalifu wa aina zote, natoa maelekezo kwa kila mkoa kuhakikisha unaendesha oparesheni kali dhidi ya bodaboda, ili kupunguza ajali zinazosababishwa na bodaboda.

 “Wengi wao hawataki kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani, tusiwaonee muhali maana maisha ya watu ni muhimu sana na jambo la msingi ni kusimamia sheria tu,” alisema IGP Mangu.

Awali akifungua kikaokazi hicho Waziri Kitwanga alilitaka Jeshi la Polisi kuendelea na mapambano yake dhidi ya uhalifu na wahalifu, ili usalama wa raia na mali zao uendelee kuimarika na Watanzania waendelee na shughuli zao za kujiletea maendeleo bila hofu ya kutendewa uhalifu.

Mbinu Mpya ya Mastaa wa Bongo Kujiuza Mtandaoni....

$
0
0

Imevuja! Siri ya maisha mazuri ya baadhi ya mastaa wa kike Bongo ambao hawafanyi filamu, Bongo Fleva wala kazi yoyote imejulikana huku aibu kubwa ikiwafuata nyuma ya siri hiyo, Risasi Jumamosi limefungasha mzigo wa kutosha!

Kwa mujibu wa chanzo chetu kikuu kikizungumza na Risasi Jumamosi, mastaa hao wamekuwa wakitumia njia ya kisasa ambayo ni Mtandao wa Kijamii wa Instagram kupata wanaume wenye fedha ambao hujitokeza na kuwataka kimapenzi, wengi wao wakiwa nje ya nchi.


 Giggy Money


NCHI ZENYE WATEJA WENGI
Chanzo hicho ambacho na chenyewe ni staa, kiliendelea kusema kuwa, nchi ambazo mastaa hao wana soko kubwa ni China, Dubai na Afrika Kusini. India ni kwa mbali sana!

INAVYOKUWA SASA
Chanzo: “Ili tuweze kuonwa na wateja wetu hao, huwa tunatupia kwenye mtandao huo, picha zetu zenye mvuto tukiwa kwenye mapozi ya ‘ki-hasarahasara’, wengine hutupia mpaka picha za nusu utupu ili wanaume wakiwaona wavutike haraka.

“Baada ya wanaume wateja kuziona picha zetu kwenye Instagram na kuvutiwa, sasa hutaka kuwasiliana kwa kutumia Insta Direct (mawasiliano ya wawili tu ‘in box’).

“Hapo sasa ndiyo huwa pazuri, kwani kama mwanaume atakuwa amekolea, atatangaza dau na kumtaka staa aliyempenda amfuate nchini mwake. Kama ni Dubai, China au Afrika Kusini,” kilisema chanzo hicho.


 Kidoa

UJIRA WAO
Chanzo hicho kilisema kuwa, ujira wanaolipwa mastaa hao ni wa chini sana ukilinganisha na kiwango cha muda.“Mara nyingi kama ni Dubai, unatangaziwa dola za Marekani 3,000 (kama shilingi milioni 6) ambapo ndani ya humo ni pamoja na tiketi yako ya ndege kwenda na kurudi, malazi ya kule kwa maana ya kukaa hotelini na kula.

“Siku ukirudi unapewa labda dola 500 tu ambazo ni kama shilingi milioni moja na kidogo. Sasa hizo, ndiyo utaingia madukani kufanya manunuzi mbalimbali ya vitu kama pafyumu, losheni, nguo na viatu. Ndiyo maana masta wengi wakienda nje ya nchi kwa wanaume hurudi na mabegi ya vitu walivyonunua.” Chanzo.


Jackline Wolper

HUWA WANAJAZA NAFASI
Katika hali ambayo ilishtua, staa huyo alisema kuwa, kwa tabia hiyo ya kujiuza nchi mbalimbali, baadhi ya mastaa hujikuta nafasi zimejaa!

“Utakuta staa anatakiwa kwenda Dubai mwezi huu. Mwezi ujao anakwenda China kwa mwanaume mwingine, akitoka China, Afrika Kusini mwezi Aprili. Akitokea mwanaume akamtaka aende Dubai anakuta nafasi imejaa. Pengine mpaka Mei.

“Mkifuatilia sana mtagundua ni kwa nini baadhi ya yetu hatutulii nyumbani Bongo wakati hatuna biashara kusema ndiyo inatufanya tusafiri kila wakati. Ni kujiuza tu! Mh! Mbona Instagram ina mambo!”

SIFA ZAO
“Tena nataka kukuongezea kwamba, ogopa sana mastaa ambao picha zao kwenye Instagram ni za nusu utupu! Hebu we fikiria, Instagram mimi sioni kama ni sehemu ya siri, sasa kwa nini mtu apige picha chafu halafu azitupie kule, anatafuta nini? Maana hata baba yako, mama yako, ndugu zako wanaweza kuona,” alisema staa huyo.

MASOGANGE ALITAJWA
Madai hayo yananyemeleana kwa karibu na habari iliyowahi kuandikwa na Gazeti la Ijumaa la Januari 23, 2015 ikiwa na kichwa kisemacho;

MASOGANGE AIBU TUPU SAUZI
Habari hiyo ilimhusu modo aliyetikisa Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’.
Habari hiyo ilisema Masogange yupoyupo tu, kazi kujipiga picha za utupu na kuzitupia mtandaoni kana kwamba anatafuta wanaume.

“Kimsingi hana kazi huku Sauz zaidi ya kuposti picha kwenye Mtandao wa Instagram na anachanganya sana wanaume wenye pesa zao. Si unajua tena mtoto kajaliwa shepu la maana. Ukitaka kuthibitisha hilo ingia katika akaunti yake utaona picha kibao za kihasara akiwa hotelini.”

Hata hivyo, staa huyo alikuja kukanusha kuhusu picha zake na kujiuza huko bondeni ambapo alisema:
“Mie sijui hizo picha zilisambaa vipi sababu zilikuwepo kwenye kamera yangu na mimi siku hiyo nilikuwa nimelewa. Sikuwa naelewa chochote na nilikuwa South Africa (Afrika Kusini). Kwa hiyo masuala ya kuandikwa kwamba nilikwenda kujiuza si kweli.”

KIDOA HIVI KARIBUNI
Hivi karibuni, video queen wa Bongo anayekuja kwa kasi, Asha Salum ‘Kidoa’ naye alisafiri kwenda Dubai akisema amepata dili. Lakini hakuweka wazi ni dili gani kiasi kwamba, katika toleo moja la gazeti ndugu na hili, Ijumaa liliandikwa makala yenye kichwa kisemacho; Kidoa; Dubai umeenda kula bata, kujiuza au dili za ‘sembe’? Katika makala hayo, mwandishi alitilia shaka baada ya kuona picha kwenye Instagram yake zikimuonesha msanii huyo akiwa Dubai akila bata kwenye klabu ya hoteli kubwa.

Wengi baada ya kuona binti huyo yuko Dubai walianza kujiuliza maswali mengi. Kwamba kaenda kujipumzisha na kula bata au kaenda kujiuza kama ambavyo baadhi ya mastaa wamekuwa wakifanya au ameanza kutumika katika kusafirisha ‘sembe’? yaani unga au madawa ya kulevya.

Mwandishi alisema anaandika hayo kwa sababu anajua Kidoa hana mkwanja wa kusema anakwenda kupumzisha akili Dubai.

WENGINE HUWAUZA WENZAO
Katika maelezo mengine ya staa huyo, baadhi ya mastaa hao wanapokuwa nje ya nchi na wanaume wao wa kwenye Instagram hugeuka na kuwa mawakala wa kuwauza wengine.

“Lakini pia staa anaweza kuwa mfano, Dubai halafu akakutana na staa mwenzake anakwenda mfano China, na yeye anakuwa wakala. Mimi niliwahi kukutana na staa mmoja Dubai, anakwenda China, nikampa namba za simu za mwanaume niliyewahi kuwa naye kule.

“Alipofika alimpigia, akamwambia amepewa namba na mimi, basi na mimi nikalipwa changu maana nimemtafutia soko,” alisema staa huyo.

Mama Yangu Hapendi Nihame Nyumbani Kwetu – Ray Kigosi

$
0
0
Msanii wa filamu Vincent Kigosi ‘Ray’ baada ya kuchanwa kwenye wimbo wa Nay wa Mitego ‘Shika Adabu Yako’ kuwa bado anaishi kwao, amejibu tuhuma hizo kwa kudai anaishi kwao mpaka sasa ili kuwa karibu na Mama yake.

Akizungumza katika kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM Ijumaa hii, Ray alisema yeye ni mtoto wa mwisho hivyo anahitaji kuwa karibu zaidi na Mama yake.

“Ni kweli naishi nyumbani na kuishi kwetu sio kama sina nyumba, na kuishi nyumbani sio dhambi. Uwezo wa kupanga ninao lakini mama yangu hapendi nihame nyumbani kwetu ,” alisema Ray.

“Kujitegemea ni maamuzi yako binafsi, mimi naishi nyumbani na mama yangu ni mtoto wa mwisho lakini huwa sipendi kujionyesha nina utajiri gani?, Sipendi kupost mali zangu, sinina nyumba, magari ni ishu zangu binafsi, kila msanii ana style yake ya maisha, mwingine anapenda kujionyesha kwenye mitandao ana mali gani,” aliongeza Ray.

Pia Ray alisema yeye na mpenzi wake Chuchu Hans kila mtu anaishi kwake.

“Mpenzi wangu anaishi kwake na mimi naishi nyumbani kwetu. Mama yangu alishaniambia hata nikihama atakuja kuishi na mimi nyumbani kwangu. Chuchu Hans anajua kuhusu hili hata nyumba anayoishi nimempangia mimi,” alisema Ray.

Picha: Shamsa Ford Amwaga Radhi Ukumbini

$
0
0
Msanii wa filamu Shamsa Ford juzikati alitoa kali ya mwaka baada ya kutinga kwenye Ukumbi wa Sky nightlife uliopo Masaki akiwa ametinga kigauni kifupi ambacho kila alipoinama kwa kucheza alikuwa akimwaga lazi.

Shamsa aliyekuwa kivutio ukumbini hapo alionekana kukongwa na nyimbo za msanii Belle 9 ambapo kila ulipopigwa wimbo aliinuka akiwa na glasi yake mkononi na kukata mauno kama aliyekuwa ameahidiwa zawadi nono.

Chanzo:GPL

Matokeo ya Uchaguzi wa Raisi Uganda...Huyu Ndio Rahisi wa Uganda Aliyetangazwa na Tume ya Uchaguzi

$
0
0
Tume ya Uchaguzi nchini Uganda imemtangaza Rais Yoweri Museveni kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Alhamisi hii.
MUSEVENI

Rais Museveni alipata kura 5,617,503 sawa na asilimia 60.75 ya kura zilizohesabiwa kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume hiyo Dkt Badru Kiggundu.

Mpinzani wake mkuu Dkt Kizza Besigye alipata kura 3,270,290 ambazo ni sawa na asilimia 35.37%.

Awali, waangilizi kutoka Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Madola walikuwa wamekosoa uchaguzi huo wakisema kulikuwa na kasoro nyingi.

Aidha walishutumu kukamatwa kwa mgombea wa upinzani Dkt Besigye na kuzimwa kwa mitandao ya kijamii.


Yanga Yaibuka Kidedea Leo Kwa Kufunga Simba Bao 2-0

$
0
0
Kitendawili cha nani mbabe kati ya watani wa Jadi wa Msimbazi na Jangwani kimekamilika baada ya Simba kufungwa bao 2-0 kwa mara ya pili ndani ya miaka miwili, ndani ya uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Simba ambao walicheza wakiwa pungufu baada ya mchezaji wake Abdi Banda kupigwa kadi nyekunde hatua iliyodhoofisha zaidi nguvu ya wana Msimbazi.

Uzembe wa mabeki wa Simba katika dakika ya 39 ya kipindi cha kwanza ulipelekea kupachikwa goli la kwanza na Donald Ngoma raia wa Zimbabwe. Dakika ya 72 ya mchezo, uzembe wa mabeki wa Simba ulimpa nafasi mshambuliaji Amisi Tambwe kucheka na nyavu zao.

Tambwe ameiadhibu Simba, timu ambayo alimsajili kwa mara ya kwanza alipoingia nchini na baadae kuhamia kwa wana Jangwani. Mchezaji huyo alipachika goli huku walinzi wanne wa Simba wakiwa wanalandalanda katika eneo la goli lao.

Yanga wameweka historia ya kumfunga Simba kwa misimu miwili mfululizo huku ikifuta machungu ya kushindwa kuifunga Simba kwa misimu 10 mfululizo kati ya mwaka 2000 hadi 2009.
Viewing all 104808 articles
Browse latest View live




Latest Images