Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

WIMBO WA DIAMOND WASHIKA NUMBER MOJA TRACE TV....

$
0
0
Diamond Platnumz hashikiki kwa sasa. Kwa mujibu wa Trace TV, My Number One Remix ft Davido, ndio wimbo namba moja kwa sasa barani Afrika.

Wimbo huo umekamata nafasi ya kwanza kwenye Top 10 ya chart ya kituo hicho cha runinga cha kimataifa. “Need i say More…???? My Prayers are slowly been answered… Trust me! we getting there… S/O to @trace_inter for keeping that pace of promoting African Music Constant,” ameandika Diamond kwenye Instagram kuelezea furaha yake.

RAPPER WA SOMALIA K'NAAN NDIO MPENZI WA LUPITA NYONG'O

$
0
0
Zile speculation kuwa huenda star mpya wa Hollywood Lupita Nyong’o ana uhusiano wa siri na mwigizaji mwenzake Jared Leto zimezikwa na speculation mpya kuwa huenda rapper na mwimbaji wa Somalia aitwaye K’naan ndiye mpenzi wa Lupita.
lupi knaan-4
Picha mbalimbali zilizosambaa siku moja baada ya Tuzo za Oscar zikiwaonesha Lupita na rapper K’naan mwenye asili ya Somalia, wakiwa katika pozi zinazoashiria ukaribu mkubwa ndio zimezua speculation hizo.
lupi knaan-3
Katika picha hizo K’naana anaonekana pia amembebea tuzo yake ya Oscar.
lupi knaan-5
Keinan Abdi Warsame a.k.a K’naan ambaye amewahi kuhit na single yake ‘Waving Flag’ mwaka 2010, walionekana wakiwa pamoja siku ya Jumatatu wakati Lupita akitoka kufanya mahojiano na Live.
lupi knaan-6
Ripoti zinasema kuwa K’naan pia alikuwepo katika matukio ya awali kabla ya siku ya Tuzo za Oscar kumpa support Lupita, na Lupita amekuwa akisema jinsi anayopenda muziki wake kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii, na mwezi uliopita (February 27) alihudhuria show yake Hotel Café, huko Los Angeles ambayo pia alimsaidia kumfanyia promo.
lupi knaan-2
Hii ni picha waliyopiga Ava DuVernay, K’naan na Lupita december 2013 wakisheherekea nomination za SAG Awards
lupi knaan-1
Moja ya post za K’naan ambazo inathibitisha ukaribu wao

BEN POL AINGIA KATIKA KASHFA NZITO..

$
0
0
Huu ni mtiririko wa matukio yanayomfikia Gossip Cop Soud Brown,leo tukio lililofikishwa mezani kwake ni la Ben Pol kuchukua pesa ya show na kisha kutoonekana kwenye show yenyewe iliyokuwa imeandaliwa na wanachuo kutoka Dodoma,sikiliza kupitia 104.4 Clouds Fm Dodoma.
Bonyeza play kusikiliza.

MOYES AAMUA KUWAANDIKIA MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED

$
0
0
Kocha wa Manchester United David Moyes ameandika barua ya wazi kwa mashabiki wa klabu hiyo akielezea kwamba msimu wake wa kwanza ndani ya klabu umekuwa mbovu zaidi kuliko ilivyotegemewa.
Akiwasifu mashabiki kwa uvumilivu wao Mscotish huyu ambae aliteuliwa na Sir Alex Ferguson amekiri kwamba matokeo yao mabovu yanamshangaza mpaka yeye lakini ana uhakika kila kitu kitakaa sawa mbeleni.
‘Wakati nilifahamu hii kazi ingekuwa na changamoto nyingi ni wakati nilipopewa jukumu hili, lakini msimu mgumu tulionao hakikuwa kitu ambacho nilikifiria, jambo ambalo nina uhakika mashabiki wote hawakudhani hali ingekuwa hivi,” aliandika Moyes.
‘Wachezaji wangu na makocha wenzangu wanajaribu kwa kila namna kuhakikisha timu inarudi katika kufanya vizuri,
wote tumezoea kuiona Manchester United inayofanikiwa na sapoti mliyowapa wachezaji na mimi katika kipindi chote cha msimu ni kubwa sana’
‘Tunapocheza ugenini mashabiki wetu waliosafiri wameendelea kuwa bora kabisa katika nchi hii na wakati tunapokuwa Old Trafford imani yenu kwenye timu imekuwa ikionekana wazi, kuisapoti timu yenu wakati inashinda ni rahisi lakini ni ngumu sana wakati mambo yanapokuwa mabaya, nyinyi mmekuwa nasi katika kipindi chote’
‘Kila magumu tunayopitia yatatufanya tuwe bora zaidi, timu imara na klabu bora huko mbeleni, kwa miaka mingi sasa mmekuwa mkishuhudia vikosi vya ushindi na kwa muda fulani, nina uhakika kabisa tutaiona Manchester United tuliyoizoea.”
Source:shaffihdauda.com

WAANDISHI WA HABARI WAFUNGIWA NJE BUNGE LA KATIBA

$
0
0
Bunge la Katiba limeamua kuweka kitanzi kwa uhuru wa wananchi kupata habari za mchakato wa Katiba Mpya, kwa kuwazuia waandishi wa habari kuingia kwenye Kamati 12 za wajumbe wa Bunge hilo zitakazojadili Rasimu ya Katiba.

Mjadala mkali ulizuka kwa juzi na jana kwenye Bunge hilo, huku baadhi ya wajumbe wakitaka uhuru wa wananchi kupata habari uwapo kwa waandishi kuruhusiwa kuingia kwenye kamati na wengine wakiwamo wajumbe wa Kamati ya Kanuni na Kumshauri Mwenyekiti wakipinga vikali kwa kutaka waandishi wapewe taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa kamati husika.

Kifungu cha 57 fasili ya kwanza ya Kanuni za Bunge Maalum la Katiba, kinaeleza kuwa vikao vyote vya kamati vitakuwa vya faragha na hakuna mtu yeyote asiyekuwa mjumbe wa kamati, mtumishi wa Bunge au mtaalam aliyeitwa na Mwenyekiti wa Bunge Maalum atakayeruhusiwa kukaa katika sehemu yoyote ya ukumbi wa mikutano ya kamati wakati kikao cha faragha kinaendelea.

Fasili ya tatu, inaeleza kuwa bila kuathiri masharti ya kanuni hii Mwenyekiti wa Kamati ya mjumbe yeyote kwa idhini ya Mwenyekiti anaweza kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu mambo yaliyojitokeza kwenye kikao cha kamati.
Baadhi ya wajumbe waliiomba kuwasilisha mapendekezo yao kwenye kifungu hicho, walitaka waandishi wa habari kuruhusiwa kwani kwa kuwazuia ni kwenda kinyume cha ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inayotaka kuwapo kwa uhuru wa kupata taarifa.

OLUOCH

Ezekiel Oluoch alisema anashauri vikao viwe wazi kwani hakuna jambo la siri la kujifungia kwani wananchi wana haki ya kujua kinachojadiliwa kwenye kamati na kwamba ni vyema kamati zikawa huru.

HALIMA MDEE

Halima Mdee alisema wenye jukumu la kuzitengeneza kanuni ni wajumbe na kwamba awali kamati ya kanuni na kumshauri mwenyekiti baada ya majadala mkubwa kamati ilipendekeza waandishi waruhusiwe kuingia kwenye vikao, na ikakubaliwa kwenye vikao vya kamati ambavyo vitakuwa na mijadala mikubwa na watakapokuja kwenye Bunge watafanya majumuisho kwenye manbo yaliyojadiliwa.

“Tulikubalina watu watakaokatazwa ni wananchi wa kawaida kutokana na
udogo wa kumbi, ila waandishi wa habari wakubaliwe, sisi ndiyo tunaopitisha kanuni na sisi tuliridhia ilikuwa ni matarajio yetu,”
alisema.

Alisema waliotajwa kwenye kanuni waruhusiwe kuingia na utaratibu utakaotumika uamuliwe na mwenyektii wa kamati kushauriana na makamu mwenyekiti.

“Waandishi wa habari waingie mnaogopa nini, mnaficha nini?…hii Katiba ni ya wananchi wana haki ya kujua kila kinachoendelea ndani ya kamati na nje ya kamati na kwenye ukumbi wa Bunge,” alisema Mdee.

MOSES MACHALI

Moses Machali alipendekeza fasili ya tatu ya kifungu hicho, ifutwe kwa kuwa inaweka kitanzi kwa uhuru wa wananchi kupata habari na hakimlazimishi mwenyekiti au makamu kutoa taarifa kwa waandishi wa habari.

Alisema vikao vyote vifanyike kwa uwazi bila kuzuia mtu ingawa hawataruhusiwa kushiriki kwenye mjadala wa kamati.

“Hao wanaosisitiza kura ya wazi halafu mnaogopa na kuwakataa waandishi wa habari mnaficha nini, sioni sababu ya msingi,” alisema Machali.

MARIA SARUNGI

Maria Sarungi alisema vikao vya kamati viwe wazi kwa waandishi wa habari kwa kuwa Rasimu ya Katiba itakwenda kwao kwa ajili ya kuipigia kura.

“Mwanzo wa Rasimu ya Katiba unasema kwakuwa sisi wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua…Katiba hii si ya kwetu tuliokaa humu ndani bali ya wananchi wa Tanzania, mchakato ulivyoanza ilianza kwa wananchi hadi tulipofika,” alisema.

FREEMAN MBOWE

Freeman Mbowe alisema Katiba inayotungwa ni ya wananchi na wanaowakilishwa ndani ya Bunge hilo wanataka kujua kila kinachoendelea ndani ya Bunge hilo.

“Tusifikiri tunahitaji kuridhiana sisi wenyewe tulioko ndani ya Bunge hili kuna Watanzania kwa mamilioni wa vyama na taasisi mbalimbali wanatisikiliza,” alisema.

Wakati wajumbe huyo anazungumza, baadhi ya wajumbe walipiga kelele na kuzomea hali iliyomlazimu kuacha kuzungumza na mwenyekiti kumsihi kuendelea, lakini Mbowe alisema: “Siwezi kuendelea wakati wajumbe wanapiga kelele.”

MAHALU

Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni na Kumshauri Mwenyekti wa Muda,Prof. Costa Mahalu, alisema kamati yake inapeleka mapendekezo kwa wajumbe na wenye maamuzi ni wajumbe na baadaye wanaagizwa kurekebisha mwafaka uliofikiwa na kuonyesha msimamo wao kwa pamoja.

Mjumbe wa Kamati, Bakari Khamis Bakari, alisema hakuna uhuru usiokuwa na kinga kulingana na maelezo ya maeneo husika na kwamba kamati italichukua suala hilo na kujadailiana ili kupata namna bora ya kuruhusu waandishi wa habari kuchukua habari.

George Simbachawene, mjumbe wa Kamati ya Kanuni na Kumshauri Mwenyekiti, alisema maoni ya kamati ni kuwa hisia na sababu wanazotoa wajumbe hao zilikuwapo kwenye kamati yao na walipenda waandishi waruhusiwe ili mchakato huo uonekane kwa umma wote.

“Kilichotushinda na kufikia uamuzi wa maoni hayo ni utekelezaji wake…kwa busara yetu tukaliwekea utaratibu kwenye fasili ya tatu, vyombo vyetu vya habari ni vingi, kamati iko ukumbi wa Msekwa asubuhi anakuja mwandishi anachukua anapeleka, habari zitakazokwenda juu ya hoja moja jambo moja zitakuwa hazijakamilika zitawachanganya wananchi na si kuwasaidia,” alisema.

Alisema waandishi watachukua habari kivyao na kuwachanganya wananchi na ndiyo maana wameamua mwenyekiti wa kamati atoe taarifa kwa waandishi.

DK. MWAKYEMBE

Dk. Harrison Mwakyembe alisema kitaaluma ni mwandishi wa habari na mwanasheria na kwamba anaona hakuna haja ya waandishi wa habari kuruhusiwa kuwepo kwenye kamati na badala yake wapewa taarifa na mwenyektii wa kamati husika.

Hata hivyo, baadhi ya watoa hoja, walipinga hatua hiyo huku wanaopinga waandishi kuingia kwenye ukumbi wakishangilia kwa kupiga meza kusisitiza waandishi kunyimwa kuingai kwenye kamati hizo, huku wachache wa vyama wa upinzani wakipinga uamuzi huo.

DK. TULIA ACKSON

Mjumbe wa Kamati ya Kanuni na Kumshauri mwenyekiti, Dk. Tulia Ackson, alisema hakuna uhuru usiokuwa na mipaka na kwamba kamati inapendekeza kifungu hicho kubaki jinsi kilivyo.

Hoja hiyo ilimalizika kwa wajumbe kupitisha kifungu jinsia kilivyo kuwa waandishi hawataruhusiwa kuingia kwenye kamati na badala yake watapewa taarifa na mwenyektii wa kamati.

CHANZO: NIPASHE

KENYA NAO WATAKA SHERIA YA USHOGA

$
0
0
Nairobi. Mbunge Irungu Kang’ata anaongoza juhudi za kundi lililoundwa la kupinga wapenzi wa jinsia moja nchini  Kenya. Sheria zilizopo zinasema ni hatia kwa watu kujiingiza katika tabia za ushoga na adhabu yake ni kifungo cha miaka 14 jela.

Huenda ikawa nchi inayofuata kwenye utata unaohusiana na haki za wapenzi wa jinsia moja, huku wabunge wakipanga kuwasilisha muswada bungeni kushinikiza Serikali kufanya juhudi zaidi kutekeleza sheria zilizomoza kupiga marufuku ushoga.

Kwa upande wao wanaharakati wa kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja wanasema shinikizo limeongezeka tangu nchi jirani ya Uganda ilipopitisha sheria dhidi ya mashoga mwezi uliopita.

Irungu Kang’ata ambaye ni mbunge kwa mara ya kwanza anaongoza juhudi za kundi lililoundwa majuzi la kupinga wapenzi wa jinsia moja nchini Kenya. Katika kampeni za wazi kabisa, mbunge huyo ameomba chama tawala kuelezea Serikali inachukua hatua gani kutekeleza sheria zilizopo dhidi ya mashoga.

Sheria zilizopo nchini  Kenya zinasema ni hatia kwa watu kujiingiza katika tabia za ushoga na adhabu yake ni kifungo  cha miaka 14 jela.

Kundi hilo linalopinga wapenzi wa jinsia moja  liliundwa majuzi wakati Rais wa nchi jirani ya Uganda Yoweri Museveni alipotia saini sheria dhidi ya wapenzi wajinsia moja mwezi Februari, licha ya shinikizo kutoka kwa nchi za Magharibi asitie saini.

CCM WAANZA KUVIZIANA BUNGENI

$
0
0
Wabunge wa CCM wamedaiwa kupokea vitisho, kama watakwenda kinyume na msimamo wa chama.
Dodoma. Mpasuko miongoni mwa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM), umechukua sura mpya, baada ya kuelezwa kuwa wabunge 90 wameorodheshwa kwa lengo la kuhojiwa kwa tuhuma za kukisaliti chama.
Wajumbe hao wengi wao wakiwa ni wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, wamekuwa wakiitwa na mmoja wa viongozi waandamizi wa Serikali ya CCM na kuelezwa wazi kuwa chama hakiridhiki na mwenendo wao.
 Wengi wa wajumbe hao ni wale waliotamka hadharani kuunga mkono muundo wa Muungano wa Serikali tatu, badala ya Muungano wa Serikali mbili ulioboreshwa, ambao ndiyo msimamo wa chama hicho tawala.
Wengine ni wale wanaotajwa kuunga mkono upigaji wa kura wa siri katika kupitisha vifungu vya rasimu ya Katiba Mpya, ikiwa ni kinyume na msimamo wa CCM wa kutaka kura ya wazi.
“Ni kweli hata mimi niliitwa na (akimtaja jina) na kuniambia ametumwa aniletee ujumbe kuwa niko kwenye orodha hiyo na nikiendelea na msimamo huo nitachukuliwa hatua,” alidai mbunge mmoja.
Hata hivyo, mjumbe huyo alidai kuwa kinachofanywa na CCM ni sawa na kumpa mgonjwa wa saratani dawa ya kutuliza maumivu, lakini mwishowe ugonjwa alionao uko palepale.
“Mimi msimamo wangu ambao naamini ndiyo msimamo wa wabunge wengi ni kutaka kura ya siri na Serikali tatu. Nitasimamia msimamo huo, kwani ndiyo dhamira yangu kwa masilahi ya Watanzania,” alidai.
Mbunge mwingine anayetajwa kuwapo kwenye orodha hiyo (jina tunalo) alipoulizwa jana kama ana taarifa hizo alisema, “Ni kweli kuna orodha hiyo ya wabunge 90, lakini mimi sijaulizwa chochote.”
Mbunge huyo alisema, wabunge hao 90 wamewekwa katika orodha nyeusi (Black list) iliyoandaliwa na CCM kimeandaa kama njia mojawapo ya kuwatesa kisaikolojia ili waachane na msimamo wao.
Tayari CCM kupitia kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye kilishaweka wazi msimamo wake kuhusu suala la muundo wa Serikali na kutaka wajumbe wake watetee kwa nguvu zote muundo wa Serikali mbili.


Nape: Huu ni uwongo
Nape alipoulizwa jana kuhusu kuwapo kwa orodha hiyo, alikanusha na kusema huo ni uongo ambao hata shetani ataona aibu kuusema. Chama hakina mpango wa kuwahoji, alisema na kuongeza;
“Msimamo wa Serikali mbili siyo wa mtu mmoja mmoja, ni msimamo wa CCM na msimamo wa Watanzania wengi…. Kama kuna haja ya kuwahoji wanaounga Serikali tatu watahojiwa na wapiga kura wao.”
Ngoma nzito kura ya siri
Wakati CCM wakifanya uamuzi huo, Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalumu la Katiba, Pandu Ameir Kificho, ameunda kamati ya maridhiano itakayosaidia kufikia mwafaka wa kanuni zenye utata na zilizua mabishano makali bungeni, ikiwamo upigaji kura na Muundo wa Muungano.
Akizungumza bungeni mjini jana, Kificho alisema kamati hiyo imeundwa kwa ajili ya kutafuta maridhiano katika maeneo ya kanuni ya 32 hadi 43 ambayo yamekuwa na tofauti kubwa.
“Kamati hiyo itakuwa imejumuisha wawakilishi kutoka maeneo mbalimbali ya vyama vya siasa na makundi 201.  Kamati hiyo kamili natarajia  nitaitangaza baadaye saa 9:30 leo (jana), watakutana,”alisema.
Alisema makundi mbalimbali katika kamati za vyama vyao na makundi mbalimbali yanayotokana na uteuzi wa Rais kwenye wajumbe 201, ambapo kutokana na wingi wao walipewa nafasi ya kukutana katika Ukumbi wa Pius Msekwa.
“Kamati ya maridhiano inaweza kusaidia kuwajulisha wawakilishi wao nini ambacho tumefikia katika kamati ile ya mashauriano ili iwe rahisi na wao wawe wamepata ile taarifa. Kimsingi ili tuwe na mtazamo wa pamoja kuifanya kazi ya kumaliza kanuni hizo kwa wepesi,” alisema.
Kificho alisema amefikia uamuzi huo ili wiki ijayo waanze kazi ya kupitia na kuichambua rasmi Rasimu ya Katiba.
Hata hivyo, baada ya kauli hiyo, wajumbe kadhaa waliibuka wakiomba miongozo akiwemo, Dk Ave Maria Semakafu, aliyeshauri uteuzi wa Kamati ya Maridhiano kuzingatia usawa wa kijinsia katika upande wa kundi la watu 201.
“Ningeomba busara hiyo kuanzia siku tulipojadili iwe inaongoza uteuzi wote kwa kuhakikisha katika kila kitu ambacho tunakiweka watu tulioko humu ndani tuweze kuwakilishwa kihalali,” alisema Dk Semakafu.
Hali hiyo ilimfanya Kificho kuwataka wajumbe kumpendekeza mwakilishi ambaye anayewakilisha wajumbe 201 walioteuliwa na Rais Jakaya Kikwete ambapo baadhi yao walipaza sauti wakitaka Dk Semakafu kuwawakilisha.

ACCOUNT FAKE YA FACEBOOK YA KALA JAREMIAH YAZIDI KUDHALILISHA WANAMUZIKI SASA ZAMU YA LADY JAY DEE

$
0
0
Hii akaunt sio akaunti halisi ya kala Jeremiah na hiki kinachoendelea katika akaunt hiyo ni wizi tena utapeli mkubwa, Ikiwa kama ww ni shabiki wa kala Jeremiah hiyo akaunt uta unlike maana imekaa kuchonganisha na kugombanisha wasanii


VIDEO YA D KNOB - NISHIKE MKONO FT. MWASITI ILIYOFANYWA NA NICK DIZZO

$
0
0
Video hii hapa chini imefanywa na Focus Media inayomilikiwa na Nick Dizzo Ambae zamani alikuwa E-media

FLORA LYMO AMWAGIA SIFA KEDE KEDE MANGE KIMAMBI

$
0
0
Flora Lymo ameamua kufunguka kwenye Blog yake kuhusu Mange Kimambi na Haya ndio Aliyoandika:

"Mama na Mwana'' Yani hii ndiyo sababu sana sana nikamuweka Mange kwenye hii Blog yenu ya maukweli matupu leo'Flora Lyimo Fashion Police Blog' Yani Im so PROUD of you Mange'' kwa kuweza kutokumkataa mwanao kwa sababu umeolewa na Mzungu au Mwanaume Mwengine wa aina yoyote aliekukuta wewe ukiwa na Mwanao au wanao ''yani Wanawake /Dada wengi huwakataa watoto wao kisa ni wamempata Mzungu au Mme wa kuwaowa'' Why do that jamani ?''Just take a look at Mange hapa na mwanae wanavyopendezeana yani is the Best think you can ever do to your Child'' Love them hata kama umempata Mme wa dhahabu au Gold'' Please Igeni Mfano wa Mange hapa'' Be Bless Mange na familia yako '' Yani huwa ni lazima ukiwa unakizuri ninachokijua Moyoni mwangu nitakisema na vile vile kibaya'' hiyo ndiyo habari ya mujini always say the truth''

Sasa hebu ona Jamani wanavyopendeeana ,alafu wewe uwe umemkana mwanao unajilia maraha yako mwenyewe na tena bila hata haya unazaa na watoto wengine na huku ukiwakataa wanao wengine''yani wenyewe tabia hizo wacheni mara moja please'' is not nice ,just take a look of hii Familia ya our Star Mange Kimambi na Familia yake''so lovely ''Yani naona aisee hata Mimi my Birthday mwaka huu niifanye hivi ''Just me and my Family ''wacha nijipange fasta fasta maana yakaribiaaaaaa''Ruwa Mangi'' Anyway''Hope nyie mnao wakana watoto wenu mnaisoma hii na kumuiga Mange Kimambi hapa''
Again Happy Birtday and wishing you All the Best utuzalie Mtoto wetu salama'' 
Flora Lyimo Fashion Police Blog

MASTAA WENYE NYOTA ZA NGONO!

$
0
0
Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya
Makubwa! Mtabiri maarufu Bongo, Maalim Hussein Yahya ameanika nyota za baadhi ya mastaa wa Bongo katika kipengele cha mapenzi au ngono, Risasi Jumamosilimesheheni.
Mtabiri maarufu Bongo, Maalim Hussein Yahya.
Akizungumza na mapaparazi wetu katikati ya wiki hii ofisini kwake Magomeni-Mwembechai jijini Dar, Maalim alitumia saa kadhaa kuangalia nyota ya mmoja baada ya mwingine na kueleza sifa zao katika sekta ya uhusiano na tendo la ndoa.
Wema Sepetu.
Baadhi ya mastaa alioweza kuwasoma nyota zao kirahisi ni pamoja na ‘kichaa’ wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, waigizaji Wema Sepetu, Vincent Kigosi ‘Ray’, Aunt Ezekiel, Steven Jacob ‘JB’, Jacqueline Wolper, Blandina Chagula ‘Johari’ na wengine.
ALIANZA NA WEMA
Akimzungumzia Wema aliyezaliwa Septemba 28, Maalim alisema nyota yake ni Mizani hivyo ana tabia zifuatazo katika masuala ya mapenzi:
“Kwanza yeye (Wema) na Diamond nyota yao ni moja hivyo mambo yao mengi yanafanana.
“Wanapenda kuwa kwenye ulimwengu wa mapenzi na mahaba wakati wote. Wanathamini sana masuala ya ngono kuliko maisha mengine.”
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Wema Sepetu katika pozi la kimahaba.
NDOA NA DIAMOND
“Hawa watakuwa watu wa kuachana na kurudiana mpaka watakapofunga ndoa ya kifahari hapo baadaye.
“Kuhusu mambo mengine kinyota ni kwamba wana sifa ya uongozi, wanapenda kuwa huru na kujitegemea. Wanapenda kuheshimika kwenye jamii na ni wacheshi, wana hekima na diplomasia.”
Vincent Kigosi ‘Ray’.
KUHUSU RAY
Kwa upande wake Ray ambaye amezaliwa Mei 28, Maalim alisema nyota yake ni Mapacha.
Akimchambua kinyota kuhusu masuala ya mapenzi, alisema:
“Akimpenda mwanamke ana uwezo wa kumpa chochote, kimawazo na kila kitu, anaweza hata kuhamia nyumbani kwa mwanamke huyo.
Vincent Kigosi ‘Ray’ akiwa na mpenzi wake Chuchu Hans.
“Ila ni mtu anayechoka haraka na hawezi kudumu kwa muda mrefu kwenye penzi na mwanamke mmoja tu.
“Pia anapenda kuwa na mapenzi ya siri siku zote. Hata akioa ni lazima ataendelea kuwa na mwanamke wa nje ‘nyumba ndogo’.
“Mbali na masuala hayo, ni mtu mwenye hisia kali sana ambapo hukasirika upesi. Ni mtu mwenye uwezo wa kujieleza na kuzungumza, ana ushawishi mbele za watu.”
Aunt Ezekiel.
AUNT EZEKIEL NAYE
Akimchambua Aunt Ezekiel ambaye alizaliwa Oktoba 27, mtabiri huyo alisema nyota yake ni Nge.
“Kinyota, ni mtu mwenye ‘muwashawasha’ wa mapenzi, anapokuwa na hasira tu hupenda kuzimaliza kwa kufanya tendo la ndoa.
“Ni msiri sana. Ana wapenzi wengi lakini kwa siri. Kwake tendo la ndoa ni ishu muhimu sana katika maisha yake hasa ikizingatiwa kuwa, nyota ya Nge inatawala sehemu za siri.
“Kwa mwenye moyo mdogo, asifanye mapenzi na mtu mwenye nyota hii kwani atajuta maisha yake yote. Lakini hayumbi na hakubali kushindwa hata kwa jambo ambalo halitamharibia popote.”
Jacqueline Wolper.
JB & WOLPER
Kwa upande wa JB aliyezaliwa Desemba 4, Wolper aliyezaliwa Desemba 6, Maalim alisema wote wana nyota moja inayofanana ya Mshale. Anaichambua nyota hiyo hivi:
“Wanapenda kufanya ngono kwa muda mrefu, hivyo mwanamke au mwanaume atakayekuwa nao kimapenzi lazima awe amekula akashiba vizuri kabla ya tendo lenyewe.
Jacob Steven ‘JB’.
“Wapenzi wao wanapowaonesha dalili ya kuwapenda sana basi wao huwa wanajiondoa kwa hofu.
“Wanapoingia katika mapenzi wanakuwa waaminifu na wanakolea vilivyo. Mara nyingi wanapenda sana kuwa na wapenzi wapya, lakini hawapendi mapenzi ya kudumu kwa sababu yanawanyima uhuru.
Blandina Chagula ‘Johari’.
NYOTA YA JOHARI SASA
Akimzungumzia Johari aliyezaliwa Agosti Mosi, mtaalam huyo alisema nyota yake ni Simba. Anasema:
“Kinyota ana tatizo la kujiamini katika mapenzi lakini kwa ndani ni mtu anayeumia.
“Mara nyingi hujipa hisia za kupendwa na mpenzi wake kama anavyompenda yeye.
“Ni mkarimu lakini ni jeuri, anapenda sana kuonea wenzake. Anapenda kujionesha na humharibu mpenzi wake.”
Credits:Global Publishers

OLE SENDEKA AMSIFIA TUNDU LISSU BUNGENI..AMSHAURI RAIS JK AMPE UWAZIRI WA KATIBA NA SHERIA

$
0
0
Wadau ole sendeka amemsifu mh tundu lissu kwa uwezo aliounyesha kwenye haya masuala ya kikanuni bungeni. Ameenda mbali zaidi kwa kumshauri rais Jakaya Kikwete ampe uwaziri wa sheria na katiba!

Uzalendo kwanza vyama baadae! Kama mtu anapiga kazi vizuri basi mpeni sifa na nafasi inayomfaaa......


YALIYONIKUTA JANA SIWEZI RUDIA KUMPIGIA SIMU MWANAMKE YOYOTE USIKU

$
0
0

Yaliyonikuta jana siwezi rudia kumpigia simu mwanamke yoyote usiku

Kuna msichana nilikuwa namchukulia kama dada kwa sababu ni dada wa rafiki yangu na tumekuwa tukipigiana simu ata usiku yeye pia amekuwa akinitumia ujumbe ata usiku ikawa mazoea.

Jana usiku wa saa nne nikampigia simu nimwambie wikend njema,akapokea simu mwanaume anaongea kama watu wa Arusha.

Alivyosikia sauti ya kiume tu bila kuuliza mi ni nani alinifulumishia matusi ya nguoni sana na kuniambia yeye anaenjoy kifuani mimi naangaika kupigia simu wake za wengine.

Akanitukania mama yangu,na matusi mengine makali, nilijitahidi kumwambia siwez rudia kupiga simu sababu sikujua kama ana mwanaume.Na pia nikamwambia uyo ni kama dada yangu lakin hakunielewa .uyo rafik yangu amekuwa akiniambia yuko single hana mtu.

Siwezi rudia kumpigia simu rafik yangu yoyote wa kike usiku.mwisho itakuwa saa 12 jioni.Matusi niliyotukanwa ni makubwa.

WOLPER ACHOMOA SKENDO YA KUTELEKEZA WAZAZI

$
0
0
Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper amechomoa madai yaliyoibuka kuwa hawajali wazazi wake.Baada ya taarifa hizo za chinichini kuzagaa, Wolper aliibuka na kuzikanusha:
“Wazazi wangu ni matajiri kwa pesa gani nyingi nilizonazo za uwafikia wao kiasi cha kuwapa matunzo, bado nawategemea hivyo wanaodai nimetelekeza wazazi ni waongo tu.”
GPL

KURA YA SIRI, WAZI KAA LA MOTO BUNGE LA KATIBA

$
0
0
Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, juzi na jana wamekuwa katika mtihani mgumu wa kufikia uamuzi wa pamoja kuhusu utaratibu wa upigaji kura, kati ya kura ya wazi na kura ya siri.

Habari kutoka katika kikao cha ndani cha Chama Cha Mapinduzi (CCM), zilisema kutokana na mvutano huo, mjumbe mmoja, Chritopher Ole Sendeka, alijikuta akilia hadharani akitetea upigaji kura ya wazi.

Kikao hicho kilichofanyika juzi kati ya saa 2:00 na saa 5:30 usiku chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kilishuhudia mabishano makali kati ya wanaotaka kura ya siri dhidi ya wale wanaotaka kura ya wazi.

Habari hizo zilisema baada ya Pinda kufungua kikao hicho, alimkaribisha Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Shamsi Vuai Nahodha, ili atoe mrejesho wa kikao cha mashauriano.

Inaelezwa kuwa katika kikao hicho, Nahodha aliwaambia wajumbe kuwa kutokana na mazingira yaliyopo ndani na nje ya Bunge kwa upande mmoja na wananchi kwa upande mwingine, kura ya siri haiepukiki.

“Kilio cha Ole Sendeka kwenye party cocas kikao cha chama (party cocus) juzi usiku kilitokana na kauli ya Nahodha kwamba kura ya siri haiepukiki,” alidokeza mbunge mmoja wa CCM aliyehudhuria kikao hicho cha faragha.

Mbunge huyo alilidokeza gazeti hili kuwa ndani ya kikao kulikuwa na mabishano makali baada ya kauli ya Nahodha, huku baadhi ya wabunge wakisema wananchi wamechoshwa na msimamo wa CCM.

Ni kutokana na mabishano hayo ndipo Ole Sendeka aliposimama akipinga mapendekezo yaliyotaka CCM kulegeza msimamo na kuridhia kura ya siri na wakati alipokuwa akizungumza alipobubujikwa na machozi.

Huku akilia katika kikao hicho, inadaiwa Ole Sendeka akisema kwamba kukubali kura ya siri ni kuitosa CCM na msimamo wake wa kutaka muundo wa Serikali mbili.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho, zilidai kuwa Ole Sendeka alienda mbali zaidi na kusema endapo Pinda ataridhia kura hiyo ya siri, basi yeye (Pinda) na viongozi waandamizi wa CCM waliohudhuria watawajibishwa na CCM.

Kutokana na mtafaruku huo, kikao hicho kilishindwa kufikia mwafaka na kuahirishwa hadi jana saa 5:00 asubuhi ambapo hoja ya ama kura ya siri au ya wazi, iliendelea kuwagawa wabunge katika makundi mawili.

Wakati akifungua kikao cha jana, Pinda alisema kutokana na yaliyotokea katika kikao chao cha juzi usiku na baada ya kutafakari kwa mapana yake, chama kimeamua kibakie na msimamo wake wa kura ya wazi.
Kutokana na yaliyojitokeza jana (juzi) na hasa ukiona mtu mzima analia, tumetafakari tumeona tubaki na msimamo wa kura ya wazi,” alisema mmoja wa wabunge akimkariri Waziri Mkuu Pinda.

Kwa mujibu wa mbunge huyo, katika kikao hicho ilielezwa kuwa kukubali upigaji kura wa siri ni kuiua CCM kwa sababu wajumbe wengi wa Bunge Maalumu la Katiba, watapitisha muundo wa Serikali tatu badala ya mbili.

Katika hatua nyingine, baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, wamehoji kitendo cha Mwenyekiti wa Muda wa Bunge hilo, Pandu Ameir Kificho kuhudhuria kikao cha ndani cha wabunge wa CCM.

“Kificho ni mwenyekiti wa Bunge lenye makundi tofauti, sasa anapoingia kwenye kikao cha wabunge wa CCM kinachoweka mikakati ya kupingana na makundi mengine anatoa picha gani?” alihoji mbunge mmoja.

Taarifa za Kificho kuhudhuria kikao hicho cha jana cha CCM zilionekana kuwakera wajumbe wengine wa Bunge hilo, wanaotokana na vyama vya upinzani na wale wanaotoka katika kundi la wajumbe 201.

“Bado tunatafakari tuchukue uamuzi gani, lakini tukiona vipi, tutasusia kikao cha leo (jana) jioni, nyie njooni ndani lolote linaweza kutokea,” alidokeza mjumbe huyo anayetoka katika kundi la vyama vya hiari.

Kura ya siri, wazi yawekwa kiporo

Hata hivyo, jana mara baada ya Kificho kuanza kikao cha semina saa 10:40 alasiri badala ya saa 9:00 alasiri alisema semina hiyo imechelewa kuanza kwa sababu ya masuala muhimu.

Kificho aliwaambia wajumbe kuwa kamati ya mashauriano ilikuwa imemshauri kanuni ya 37 na 38 zinazohusu kura ya siri viwekwe kiporo kutokana na kutopatikana kwa mwafaka.

“Kamati imenishauri bado tuache kanuni ya 37 na 38 ili kamati ya mashauriano iendelee kunishauri vizuri zaidi ili baadaye tuje tuwaambie kamati ya kanuni iziandike vipi,” alisema.

Kutokana na ombi hilo, wajumbe waliafiki waendelee kupitia kanuni ya 32 hadi 36 na 39 hadi 43 ambavyo havina mvutano.
Mwananchi


TAARIFA KUHUSU KIJANA ALIYEJICHINJA NA SIME NDANI YA BASI..UNAAMBIWA BADO NI MZIMA HAKUFA

$
0
0
Hii ni habari ambayo ililipotiwa na vyombo mbalimbali vya habari kuhusu Abria aliyejichinja ambaye alikua msafiri wa kutoka Lindi kuelekea Dar es salaam,na bus alilosafiri nalo ni mali ya kampuni ya Maning Nice.
Basi hilo lenye namba za usajili T574 CQD ambalo linafanya safari zake za Dar es salaam na Mtwara saa 6 mchana,millardayo.com imepata nafasi ya exclusive interview na Dereva la basi hilo anayeitwa Rashidi Mohamed ambaye alikuwepo kazini siku ya tukio.

Dereva Rashid anaanza kuelezea>>’Abiria wangu alikua amekaa siti namba 68 na 59 pamoja na ndugu yake,hao jamaa walipandia Lindi,cha kusahangaza baada ya kufika sehemu moja inaitwa Nangulukuru mkoa wa Lindi sehemu ambayo mabasi yote tunapaki kwa ajili ya kupata chakula’
‘Abiria wote walipoteremka dakika 3 yule jamaa akarudi tena ndani ya basi utaratibu wangu watu wote wakishuka huwa nafunga milango ya gari kwa rimoti mpaka watu wote wakimaliza kula tunaingia tena ndani ya basi kwa pamoja kwa ajili ya usalama zaidi’
‘Jamaa alivyopanda nikashangaa huyu jamaa mbona amepanda kabla ya watu kumaliza chakula nilivyoenda kumuangalia nikamkuta ana sime yuko kwenye boneti yani eneo langu la kazi yaani nikiwa na maana sehemu ya kitanda nikamkuta anajichoma kisu aina ya sime’

Home » General News » Kuhusu abiria aliyejichinja akitokea Lindi kwenda Dar es salaam.

Kuhusu abiria aliyejichinja akitokea Lindi kwenda Dar es salaam.
Posted by: TZA two March 9, 2014 General News19 views
1Hii ni habari ambayo ililipotiwa na vyombo mbalimbali vya habari kuhusu Abria aliyejichinja ambaye alikua msafiri wa kutoka Lindi kuelekea Dar es salaam,na bus alilosafiri nalo ni mali ya kampuni ya Maning Nice.
Basi hilo lenye namba za usajili T574 CQD ambalo linafanya safari zake za Dar es salaam na Mtwara saa 6 mchana,millardayo.com imepata nafasi ya exclusive interview na Dereva la basi hilo anayeitwa Rashidi Mohamed ambaye alikuwepo kazini siku ya tukio.
5Dereva Rashid anaanza kuelezea>>’Abiria wangu alikua amekaa siti namba 68 na 59 pamoja na ndugu yake,hao jamaa walipandia Lindi,cha kusahangaza baada ya kufika sehemu moja inaitwa Nangulukuru mkoa wa Lindi sehemu ambayo mabasi yote tunapaki kwa ajili ya kupata chakula’
‘Abiria wote walipoteremka dakika 3 yule jamaa akarudi tena ndani ya basi utaratibu wangu watu wote wakishuka huwa nafunga milango ya gari kwa rimoti mpaka watu wote wakimaliza kula tunaingia tena ndani ya basi kwa pamoja kwa ajili ya usalama zaidi’
‘Jamaa alivyopanda nikashangaa huyu jamaa mbona amepanda kabla ya watu kumaliza chakula nilivyoenda kumuangalia nikamkuta ana sime yuko kwenye boneti yani eneo langu la kazi yaani nikiwa na maana sehemu ya kitanda nikamkuta anajichoma kisu aina ya sime’
3‘Nikastaajabu kwa sababu sijawahi kuona vitu kama hivi naonaga tu kwenye mitandao sijawahi kuona mtu ana kwa ana anafanya vitu hivyo nilipomuuliza kwanini anafanya hivyo alinipa ishara kwamba nitulie tu wakati huo abiria wengine wako kwenye vibanda wanaendelea kula hawajui kinachoendelea ndani ya basi’
‘Baada ya kuwa naendelea kumwambia yeye ananiashiria nimuache yaani nisiendelee kumpigia kelele akawa anatoa sasa kisu tumboni anaanza  kujichinja kama kuku shingoni zaidi ya mara 3 au 4 mpaka kunaachana kama mdomo vile yaani mfano upana wa uwazi wa mdomo na damu zikaanza kutoka yaani hata kama akifoka damu zinatoka tumboni zinatokea shingoni na si mdomoni’
‘Nikaanza kupiga kelele watu wakajaa tukamuita Meneja wa hotel akapiga simu polisi baada ya nusu saa wakaja polisi lakini walikuta jamaa yuko hoi ameshalala chini na damu zimetapakaa kwenye gari’
‘Yule jamaa nilipata neno lake moja anaitwa Kulwa kwa sababu yule ndugu yake alivyokuja akaanza kupiga kelele huku akiita ‘Kulwa kwanini unajiua,kulwa kwanini unajiua’baada ya hivyo yule ndugu yake akaanza kukimbia’
‘Tulimfukuza akarudi pale akaanza kusema kuwa huyu jamaa alikuwa anafanya kazi Lindi hakuwa na cha kuzungumza pale,baada ya polisi kuja wakamchukua jamaa wakamuweka chini ya ulinzi na Yule jamaa mwingine tayari macho alikua kashaanza kugeuza geuza’
‘Sisi tuliendelea kusubiri kuanzia hiyo saa 9 Alasiri mpaka saa 11 jioni mkuu wa kituo wa Kilwa Masoko alivyokuja kunihoji,mwisho wa mchezo Yule jamaa akapelekwa Kilwa Masoko,lakini siku ya pili wakati tunarudi Mtwara tulipishana nae na gari ya polisi analetwa Muhimbili baada ya Madaktari wa Kilwa Masoko kushindwa hilo zoezi’
‘Pale hakufariki watu wote tuliamini amefariki maana macho alishafumba na alikua hana uwezo maana hatua ya mwisho wakati anataka kudondoka chini aliomba karatasi na kuandika ‘kaka’ halafu akakata kauli hakuweza kuandika tena lakini aliashiria tumkamate yule jamaa yake aliesafiri nae alikua akiashiria kwa mikono yake’
‘Humu ndani tulipakia wamasai 3 wale wamasai nahisi walivyoteremka pale Nangulukuru kula mmojawapo alikua na Sime ambayo aliiacha kwenye kiti,walikua wamekaa siti namba 6 na 9 ni karibu na mbele hapa,nafikiri walipoteremka jamaa aliliona lile sime na ndiyo maana wao walivyoteremka tu kwenda kwenye chakula yeye akarudi kwenye basi’
‘Nafikiri alilidhamiria lile sime ndiyo maana alivyoingia tu alifanya kile kitendo bila kuchelewa na wale wamasai baada ya kuja polisi wakakataa lakini wawili walikua na mapanga yao kiunoni lakini yule mmoja akakataa akasema ameliacha pale alisafiri na rungu tu’.
Tunaendelea kufatilia kujua hali ya mgonjwa ikiwa ni pamoja na Kauli ya Jeshi la Polisi mkoa wa Lindi,endelea kuwa mwanafamilia wa millardayo.com ili uendelee kupata habari za uhakika.

MWANAFUNZI WA MZUMBE AJINYONGA HADI KUFA BAADA YA KUFELI MTIHANI

$
0
0
Usiku huu nimepokea taarifa za kusikitisha toka Mzumbe kutokana na kifo cha mwanafunzi aliyejinyonga baada ya kufeli.... 

Inasemakana kuwa Mwanafunzi huyo aliyekuwa anasoma Uchumi kwa ngazi ya Masters katika chuo hicho amejinyonga mpaka kufa baada ya matokeo kutoka jana na kuonyesha amefeli.

Taarifa toka eneo la tukio zimesema kwa sasa shughuli za mazishi zinaendelea nyumbani kwao Njombe

.................RIP.......................

By Jennifer Livigha

ETOO AMTHIHIRISHIA MOURINHO KUWA YEYE NI MZEE BAADA YA KUFUNGA BAO JANA

$
0
0
It was his first goal since Jose Mourinho was caught on camera questioning just how old the Cameroon striker even is, and Eto'o did not miss the opportunity to poke fun at the resulting controversy - his celebration saw him stagger to the corner flag bent double and holding his back, as if to suggest he is an old man....HAHA SAFI SANA KIJANA

VICTORIA KIMANI AAMUA KUACHIA PICHA ZA TATOO ALIZOJICHORA MPAKA SEHEMU ZA SIRI

$
0
0


Victoria Kimani ameamua kujipamba na urembo wa Pwani kwa kujichora na tattoo za Henna. 

HOFU YA BUNGE LA KATIBA KUWEZA KUVUNJWA YATANDA

$
0
0
Mjadala wa namna ya kuamua Rasimu ya Katiba umezua hofu ya Bunge Maalumu la Katiba kuvunjika.

Bunge hilo limeangia siku ya 21 kati ya 70 likiwa katika mjadala wa kupitisha kanuni, huku kukiwa na mabishano kuhusu namna ya kupitisha ibara.  Hadi sasa Bunge hilo limeshapitisha kanuni 85 za uendeshaji wa chombo hicho, ispokuwa mbili tu, ikiwamo ya upigaji wa kura katika kupitisha vipengele mbalimbali katika rasimu, ambayo inaonekana kusababisha mgawanyiko mkubwa.

Hali ya kutokubaliana katika masuala kadhaa ilisababisha baadhi ya wajumbe kumtaka Mwenyekiti wa Muda, Pandu Ameir Kificho aeleze iwapo Bunge hilo lingeendelea au la kutokana na utata wa kisheria na kikanuni kuhusu ibara na sura zitakazokataliwa na wajumbe kwa kura.

Akichangia mjadala wa kanuni mjumbe, Dk. Francis Michael aliitaka Kamati ya Mashauriano kuhusu vipengele vyenye ushindani ikae chini na kutoa ufumbuzi kuhusu utata huo.

“Inabidi tuwe na uamuzi, hapa tunataka Katiba Mpya au hapana. Hapa tunatumia fedha za walipa kodi. Kuna hoja ambazo zinaonyesha kabisa kuwa zikifika hapa zitagonga ukuta,” alisisitiza.

Dk. Michael alipendekeza wanasheria na wakuu wa Serikali wa pande zote za Muungano kutafuta suluhisho mapema.

 “Ni afadhali tuamue kabla hatujaendelea mbele kwa sababu hakuna mantiki ya kuendelea kukaa hapa wakati tunajua kuna hoja ambazo zinaweza zisifikie ufumbuzi,” alisisitiza Dk. Michael.

“Kwa hiyo mheshimiwa mwenyekiti kama kichwa hakikupata solution (suluhisho) huko mbeleni sijui tunakwenda kujadili vipi hii rasimu… hapa ni mahali pa kuangalia sana,” alisisitiza Hassan.

Naye Christopher Ole Sendeka alisema suala hilo la kupitisha ibara kwa kuzingatia wingi wa theluthi mbili za kura halihitaji ushabiki wowote ndani ya Bunge. Kanuni inataka iwapo ibara haikupitishwa kwa theluthi mbili ya wajumbe, ipelekwe katika Kamati ya Mashauriano ili kukarabatiwa na kurudishwa na baadaye kupigiwa kura kwa mara ya pili.

Iwapo wajumbe watapiga kura kwa mara ya pili na bado ikashindwa kupita, ibara hiyo itaondolewa kabisa. “Mnajadiliana iwapo Tanzania ni Shirikisho ama Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inapigwa kura mnakosa theluthi mbili Zanzibar na Tanzania Bara, mtatakoje hapo?” Alihoji.

Kutokana na mkanganyiko huo, Sendeka alipendekeza wanasheria waliobobea wakae na Serikali na kukubaliana ikitokea hali hiyo, njia ipi itatumika kulinusuru Bunge lisivunjike. Pauline Gekul alisema kanuni inayozungumzia wingi wa kura katika upitishaji wa ibara imewaacha hewani kuhusu nini kitatokea kama ibara zitashindikana kupitishwa. Gekul alipendekeza kuwa badala ya ibara au sura ambayo haikupitishwa kuondolewa, alishauri suala hilo lipelekwe kwa wananchi kuamuliwa kwa wingi wa kura badala ya kuziondoa.

Naye Ummy Mwalimu alipendekeza wakati wa kupitisha ibara katika hatua ya kamati, suala hilo lipitishwe kwa kuzingatia uwiano wa zaidi ya asilimia 50 kutoka pande zote za Muungano badala ya theluthi mbili.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images