Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Diamond Platnumz Kutambulisha Kichwa Kingine Kutoka Wasafi Wiki Hii

$
0
0
Lebel ya Diamond Platnumz ‘Wasafi’ imetangaza rasmi kumtambulisha msanii mpya baada ya mafanikio makubwa ya Harmonize.

Kupitia twitter Diamond Platnumz ametufahamisha haya.



VIDEO: EXCLUSIVE: Paul Makonda Kaongea nini Baada ya Kupewa Ukuu wa Mkoa Dar?

$
0
0
Headline zilizoongoza kwenye magazeti ya Tanzania March 14 2016 ni kuhusu uteuzi wa wakuu wa mikoa nchini, miongoni mwa waliozikamata zaidi headline hizo ni aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda.

Sasa baada ya hayo yote, Paul Makonda akatangazwa kwamba ndio Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es salaam, wakati akitangazwa hakuwa akijua kwamba atatangazwa kuwa Mkuu wa Mkoa.

‘Leo nilikuwa natimiza mwaka mmoja tangu kuteuliwa kwangu kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, pia nilienda kuzindua  na kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa jengo laupasuaji katika hospitali ya Mwananyamala‘

Alizipata vipi taarifa za kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa? ‘Sina uhakika zaidi kwasababu mtu hata akipiga simu mimi nilikuwa najua ni utani, lakini nilikuja kuamini baada ya kuliona jina langu kwenye karatasi yenye nembo ya Serikali ‘ ;-Paul Makonda

Baraka Da Prince na Mrembo Najma Hawa Hapa...Sasa Mapenzi yao Sio Siri Tena

$
0
0
Baada ya kuficha ficha sana mahusiano yao sasa Baraka Da Prince na Najma wameanza kuonekana pamoja kwenye sehemu tofauti na bila kujificha.

Nafasi za Kazi Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma, Mwisho wa Kutuma Maombi Tarehe 24 March

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/9 11 Machi, 2016
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa  mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 188 kwa ajili ya Wizara, Taasisi zinazojitegemea na mamlaka za Serikali za Mitaa kama inavyoonyesha hapa chini.

1.0 MHANDISI NISHATI II NAFASI 5 (LINARUDIWA)

1.1 MAJUKUMU YA KAZI

•    Kuratibu miradi ya nishati katika ngazi zote,
•    Kufuatilia maendeleo ya teknolojia mbalimbali na matokeo ya uvumbuzi na utafiti katika fani zao
•    Kutoa ushauri wa kitaalam kuhusu matumizi bora ya nishati kutokana na maendeleo ya teknolojia,
•    Kufanya ukaguzi wa shughuri za nishati ikiwa ni pamoja na kuhakiki viwango vya ubora wa huduma za nishati zitolewazo, uingizaji wa petrol na utunzaji wa nishati,
•    Kusimamia utendaji wa kazi wa wahandisi nishati waliopo chini yake.

1.2 SIFA ZA MWOMBAJI

•    Shahada/Stashahada ya juu ya Uhandisi wa Nishati (Energy Engineer) kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali.

1.3 MSHAHARA

•    Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.

=========



2.0 MHANDISI MITAMBO II MKUFUNZI (METAL TECHNOLOGY) (LINARUDIWA) NAFASI - 1

Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Wahandisi hawa watafanya kazi ya kufundisha somo la Ufundi Mitambo katika vyuo vya maendeleo ya Jamii Tanzania Bara

2.1 MAJUKUMU YA KAZI

•    Kufundisha somo la ufundi mitambo katika vyuo vya Maendeleo ya Jamii.
•    Kutayarisha mpango wa kazi wa Mafunzo
•    Kupima Maendeleo ya Wanachuo katika nadharia na vitendo
•    Kutunza vifaa vya kujifunzia na kufundishia
•    Kufanya na kutoa taarifa za Utafiti
•    Kutoa ushauri wa kitaalam kuhusu somo la uhandisi maji.
•    Kutunga na kusahihisha Mitihani ya wanachuo.
•    Kufanya utafiti utakosaidia kutoa majibu kwa matatizo/changamoto mbalimbali
•    katika jamii inayozunguka chuo
•    Kutoa ushauri juu ya kuboresha Taaluma chuoni

2.2 SIFA ZA MWOMBAJI

•    Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha sita waliofuzu Mafunzo ya Shahada/ stashahada ya juu katika fani ya Uhandisi Mitambo (Metal Technology) kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

2.3 MSHAHARA

•    Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.

==========


3.0 MKUFUNZI MSAIDIZI DARAJA LA II –HOME ECONOMICS/ DOMESTIC SCIENCE (LINARUDIWA)- (NAFASI 6)

•    Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto. Wakufunzi wasaidizi hawa watafanya kazi ya kufundisha somo la ushonaji, ufumaji, kudarizi, upishi na lishe katika vyuo vya maendeleo ya wananchi Tanzania Bara

3.1 MAJUKUMU YA KAZI

•    Kufundisha masomo ya ushonaji, ufumaji, kudarizi na upishi na lishe katika vyuo vya maendeleo ya wananchi.
•    Kutayarisha mpango wa kazi wa Mafunzo
•    Kupima Maendeleo ya Wanachuo katika nadharia na vitendo
•    Kutunza vifaa vya kufundishia
•    Kufanya na kutoa taarifa za Utafiti
•    Kutoa Ushauri wa kitaalam
•    Kuandaaa kanuni na taratibu za kusimamia Mitihani chuoni
•    Kutunga na kusahihisha Mitihani
•    Kufanya Utafiti utakosaidia kutoa majibu kwa matatizo/changamoto mbalimbali katika jamii inayoizunguka chuo
•    Kutoa Ushauri juu ya kuboresha Taaluma chuoni na kuendeleza Mafunzo nje ya chuo

3.2 SIFA ZA MWOMBAJI

•    Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne/sita waliofuzu mafunzo ya stashahada ya ufundi katika fani za ushonaji, ufumaji, kudarizi, upishi na lishe kutoka vyuo vya ufundi vinanvyotambuliwa na Serikali.

3.3 MSHAHARA

•    Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi.

=========


4.0 MUUNDA BOTI DARAJA II (BOAT BUILDER II) – NAFASI 3

4.1 MAJUKUMU YA KAZI (LINARUDIWA )

•    Kusaidia kuunda boti za uvuvi
•    Kuwashauri wavuvi juu ya utunzaji na matumizi ya boti
•    Kufanya matengenezo ya boti.
•    Kusaidia kutafsiri/kusoma michoro ya kiufundi ya boti.
•    Kuandaa vifaa kwa ajili ya ujenzi wa boti.

4.2 SIFA ZA MWOMBAJI

•    Kuajiriwa wenye stashahada ya Uundaji boti kutoka chuo cha Mbegani au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

4.3 MSHAHARA

•    Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C kwa mwezi

============

5.0 DEREVA DARAJA LA II (DRIVER II) – NAFASI 31

5.1 MAJUKUMU YA KAZI (LINARUDIWA)

•    Kuendesha magari ya abiria, magari madogo na malori
•    Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote, na kufanya uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu unaohitaji matengenezo,
•    Kufanya matengenezo madogo madogo katika gari,
•    Kutunza na kuandika daftari la safari “Log-book” kwa safari zote.

5.2 SIFA ZA MWOMBAJI

•    Kuajiriwa wenye Cheti cha Mtihani wa Kidato cha IV, Wenye Leseni daraja la “C” ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miaka mitatu bila kusababisha ajali na wenye Cheti cha Majaribio ya ufundi Daraja la II (Trade test II).

5.3 MSHAHARA

•    Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGOS. A kwa mwezi.


6.0 MPISHI DARAJA LA II (COOK II ) NAFASI – 7(LINARUDIWA)

•    Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Wapishi hawa watafanya kazi ya kuwapikia wanachuo katika vyuo vya maendeleo ya wananchi

6.1 MAJUKUMU YA KAZI

•    Kuandaa chakula cha wanachuo kulingana na Menyu na idadi ya wanachuo
•    Kupika chakula cha wanachuo
•    Kutoa ushauri kwa uongozi wa chuo kuhusu chakula cha wanachuo.
•    Kusimamia jiko.

6.2 SIFA ZA MWOMBAJI

•    Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne/sita waliofuzu mafunzo ya cheti yasiyopungua mwaka mmoja katika moja ya fani ya “food Production” yatolewayo na vyuo vya Forodhani (Dar es Salaam),Masoka (Moshi), Arusha Hotel, Y.M.C.A (Moshi), VETA (mikumi) na Vision Hotel (Dar es Salaam) kutoka vyuo vinavyotambuliwa na serikali.

6.3 MSHAHARA

•    Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGSC kwa mwezi.

===========


7.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI MITAMBO YA MAJI– NAFASI 30 (LINARUDIWA)

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.

7.1 MAJUKUMU YA KAZI

Kufanya kazi kwa kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi sanifu aliyesajiliwa ili aweze;
•    Kufunga mfumo wa umeme unaohitajika kwa ajili ya uendeshaji wa mitambo ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
•    Kufunga mota na vifaa vingine vya umeme vya aina mbalimbali vya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
•    Kufanya usafi na ukaguzi wa mfumo wa umeme, mota na vifaa vingine vya umeme na miradi ya maji na usafi wa mazingira kwa ajili ya kukidhi uendeshaji nadhifu wa pampu na kuzuia uharibifu;
•    Kuendesha mitambo inayotumia umeme ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
•    Kufanya matengenezo ya kawaida, ya vipindi na ya kuzuia uharibifu kwenye mfumo wa umeme, mota na vifaa vingine umeme kwa kufuata miongozo ya uendeshaji, na inapohitajika kwa dharura.
•    Kunakili, kutayarisha, kukusanya, kutunza na kuziwasilisha takwimu za uendeshaji na matengenezo ya mitambo inayotumia umeme ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
•    Kumsaidia Fundi Sanifu katika kazi za kiufundi.

7.2 SIFA ZA MWOMBAJI

•    Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka mmoja kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali ambao wana Cheti cha ufundi Daraja III (Plants Technician Electrical).

7.3 MSHAHARA

•    Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.

========


8.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI - (ASSISTANT TECHNICIAN WELDING) NAFASI 4 (LINARUDIWA)

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.

8.1 MAJUKUMU YA KAZI

•    Kufanya kazi kwa kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi Sanifu aliyesajiliwa ili aweze;
•    Kufunga pampu na injini za aina mbalimbali za miradi ya maji na usafi wa mazingira;
•    Kufanya usafi na ukaguzi wa pampu na injini za miradi ya maji na usafi wa mazingira kwa ajili ya kukidhi uendeshaji nadhifu, endelevu na kuzuia uharibifu;
•    Kuhudumia uendeshaji wa pampu na injini za miradi ya maji;
•    Kufanya matengenezo ya kawaida, ya vipindi nay a kuzuia uharibifu wa pampu na injini kwa kufuata miongozo ya uendeshaji na matengenezo na inapohitajika kwa dharura;
•    Kunakili, kutayarisha, kukusanya, kutunza na kuziwasilisha takwimu za uendeshaji na matengenezo ya pampu na injini za miradi ya maji;
•    Kumsaidia Fundi Sanifu katika kazi za kiufundi.

8.2 SIFA ZA MWOMBAJI

•    Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka mmoja kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali ambao wana Cheti cha ufundi Daraja III katika fani ya Welding na fiter turner.

8.3 MSHAHARA

•    Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.


9.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI ( UJENZI – CIVIL TECHNICIAN ) – NAFASI 27 (LINARUDIWA)

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga.

9.1 MAJUKUMU YA KAZI

•    Kufanya kazi za ujenzi wa kuta za nyumba na kupaka rangi na kufunga mabomba,
•    Kuchonga vifaa vya nyumba za serikali ikiwa ni pamoja na samani “furniture”,
•    Kufanya kazi za upimaji (Survey) wa barabara, majengo na mifereji kama atakavyoelekezwa,

9.2 SIFA ZA MWOMBAJI

•    Kuajiriwa waliomaliza kidato cha IV katika masomo ya Sayansi na kufuzu mafunzo ya mwaka mmoja katika Fani ya Ufundi wa Ujenzi (Civil Technician) kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali,

Au
•    Kuajiriwa waliomaliza kidato cha IV wenye cheti cha Majaribio ya ufundi hatua ya II (Civil Technician) kutoka chuo cha ufundi katika mojawapo ya fani za ufundi Ujenzi.

9.3 MSHAHARA

•    Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
.
===========


10.0 DOBI DARAJA LA II – NAFASI 1 (LINARUDIWA)

10.1 MAJUKUMU YA KAZI
•    Kufanya uchambuzi wa nguo kwa ajili ya kuosha, kukausha, kunyoosha na kuzifungasha.

10.2 SIFA ZA MWOMBAJI

•    Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliofuzu mafunzo ya miaka miwili au mitatu katika fani ya Dobi (Laundry Services) kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

10.3 MSHAHARA

•    Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS. C kwa mwezi.

=========


11.0 MPOKEZI (RECEPTIONIST) – NAFASI 3 (LINARUDIWA)

11.1 MAJUKUMU YA KAZI

•    Kupokea wageni na kuwasaili shida zao.
•    Kutunza rejesta ya wageni wa ofisi na kufanya uchambuzi wa wageni wanaoingia ili kutoa ushauri juu ya utaratibu bora wa kupokea wageni.
•    Kupokea na kusambaza maombi ya simu za ndani.
•    Kutunza na kudumisha usafi wa “Switchboard” na ofisi zake.
•    Kuwaelekeza wageni wa ofisi kwa maafisa/ofisi watakakopewa huduma.
•    Kuhakikisha kwamba wageni wanaoingia ndani wanamiadi (Appointment) au wamepata idhini ya maafisa husika.
•    Kupokea simu kutoka nje na kuzisambaza kwa maofisa mbalimbali ofisini.
•    Kupokea simu kutoka “Extension” za ndani na kupiga nje ya ofisi.
•    Kutunza rejesta ya simu zinazopokelewa kutoka nje ya ofisi na zinazopigwa kwenda nje.

11.2 SIFA ZA MWOMBAJI

•    Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha IV waliofaulu masomo ya Kiingereza, Kiswahili na Hisabati na kufuzu mafunzo ya Mapokezi na Upokeaji Simu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

11.3 MSHAHARA

•    Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B kwa mwezi


============

12.0 MTUNZA BUSTANI DARAJA LA II - NAFASI 3 (LINARUDIWA)

12.1 MAJUKUMU YA KAZI

•    Kupanda maua katika maeneo yanayohusika.
•    Kupanda na kukata majani na kumwagilia maji.
•    Kupanda mboga, matunda katika bustani.
•    Kupalilia mazao katika bustani.
•    Kufanya kazi zingine zitakazoelekezwa na Viongozi wa Kitengo chao.

12.2 SIFA ZA MWOMBAJI

•    Kuajiriwa wenye Cheti katika fani ya utunzaji bustani za maua, mboga na upandaji majani kutoka chuo cha Maendeleo ya Wananchi, VETA, au JKT au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.

12.3 MSHAHARA

•    Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi.

===========


13.0 AFISA UFUGAJI NYUKI DARAJA LA II (BEEKEEPING OFFICER II) – NAFASI- 5

13.1 MAJUKUMU YA KAZI

•    Kusimamia uanzishaji wa hifadhi za nyuki na manzuki.
•    Kutangaza Sera na Sheria za ufugaji nyuki.
•    Kufundisha masomo ya fani ya ufugaji nyuki.
•    Kukusanya takwimu za rasilimali na ufugaji nyuki.
•    Kupanga na kupima ubora wa mazao ya nyuki.

13.2 SIFA ZA MWOMBAJI

•    Kuajiriwa wenye Shahada katika fani ya Ufugaji Nyuki au Sayansi ya Elimu ya Mimea, Elimu ya Wadudu au Elimu ya Wanyama kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.

13.3 MSHAHARA

•    Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi


=========


14.0 MFUGAJI NYUKI MSAIDIZI DARAJI LA II – NAFASI – 5

14.1 MAJUKUMU YA KAZI

•    Kusimamia manzuki.
•    Kutunza hifadhi za nyuki.
•    Kukusanya takwimu za ufugaji nyuki.
•    Kutunza kumbukumbu za kazi za utafiti.
•    Kuondoa nyuki wanaodhuru binadamu na mifugo.
•    Kutoa leseni za biashara ya mazao ya nyuki.
•    Kutoa ushauri wa kitaalam kwa wananchi juu ya ufugaji endelevu wa nyuki na matumizi bora ya mazao ya nyuki.
•    Kutunza makundi ya nyuki wanaouma na wasiouma.

14.2 SIFA ZA MWOMBAJI

•    Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne au Sita wenye Astashahada (Cheti) au Stashahada (Diploma) ya Ufugaji Nyuki kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

14.3 MSHAHARA

•    Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B na TGS kwa mwezi.

============


15.0 MPIGA CHAPA DARAJA LA II (PRINTER GRADE II) – NAFASI 7

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Ofisi ya Waziri Mkuu

15.1 MAJUKUMU YA KAZI

•    Kufuatilia utekelezaji wa kazi zinazoendelea na kutoa taarifa kwa msimamizi wa kazi
•    Kutayarisha vielelezo (job jacket lay out) kuhusu mtiririko wa kazi (Plan of Production)
•    Kupanga ratiba ya kazi
•    Kuandaa vifaa vya kufanyia kazi
•    Kugawa kazi kwa watumishi walio chini yake

15.2 SIFA ZA MWOMBAJI

•    Kuajiriwa wenye Stashahada(Diploma) ya kawaida ya Kupiga Chapa,kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
MSHAHARA
•    Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi

===========

16.0 MPIGA CHAPA MSAIDIZI (ASSISTANT PRINTER) - NAFASI 10

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu.

16.1 MAJUKUMU YA KAZI

•    Kukunja karatasi ngumu na kutengeneza „covers‟ za vitabu, majarida, madaftari katika mahitaji mbalimbali kwa kugandisha, kuweka pamoja au kushona katika hali mbalimbali za ubora.
•    Kukarabati vitabu, kumbukumbu mbalimbali au majarida kwa kuyawekea gamba jipya, au kurudisha katika hali yake ya mwanzo kutegemea na kifaa hicho kilivyoharibika.
•    Kupanga vifaa vilivyotengenezwa katika makasha kwa vipimo vyake au katika seti.
•    Kuendesha mashine za kukata karatasi/kupiga Chapa/Mashine za Composing, kushona au kugandisha vitabu, majarida, madaftari na vifaa vingine vinavyokuwa vimetakiwa kwa mtindo na ubora wake.
•    Kupanga karatasi zitakazochapwa kwa hesabu ya kila kitabu, jarida, daftari na vinginevyo kwa kushonwa au kugandishwa pamoja.

16.2 SIFA ZA MWOMBAJI

•    Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha IV au VI katika masomo ya Sayansi, au Sanaa, wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi Daraja la I (Trade Test Grade I) katika Lithography/Composing/Binding/Machine Minding, au waliohitimu mafunzo ya miaka miwili ya Kupiga Chapa.

16.3 MSHAHARA

•    Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.Bkwa mwezi

=========


17.0 MHANDISI II MITAMBO I (MECHANICAL ENGINEER) – NAFASI 5

17.1 MAJUKUMU YA KAZI

•    Kufanya kazi chini ya uangalizi wa Mhandisi aliyesajiliwa na bodi ya usajili wa Wahandisi kama Professional Engineer ili kupata uzofu unaotakiwa.
•    Kufanya kazi kwa vitendo katika fani ya Mekanika ili kumwezesha kupata sifa za kutosha kusajiliwa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi.
•    Kukusanya taarifa na takwimu kuhusu magari na mitambo mbalimbali, bei za magari na mitambo na vifaa vya umeme ndani na nje ya nchi.
•    Kupitia mapendekezo ya miradi (project proposals) mbalimbali ya Ufundi .

17.2 SIFA ZA MWOMBAJI

•    Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu ya Uhandisi (Mechanical Engineering) kutoka vyuo vikuu vinavyotambulika na Serikali.

17.3 MSHAHARA

•    Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.


========

18.0 24

19.0 BI DARAJA LA II – NAFASI 1

19.1 MAJUKUMU YA KAZI

•    Kupanga ratiba ya kazi kwa watumishi walio chini yake
•    • Kuhakikisha kuwa maktaba ni safi
•    Kufanya kazi nyingine za maktaba atakazopangiwa na Mkuu wa kituo

19.2 SIFA ZA MWOMBAJI

•    Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza katika fani ya ukutubi au sifa inayolingana na hiyo kutoka katika vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali

19.3 MSHAHARA

•    Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.


20.0 AFISA MISITU DARAJA LA II (FORESTRY OFFICER GRADE II) –NAFASI- 1

20.1 MAJUKUMU YA KAZI

•    Kusimamia upandaji na uhudumiaji wa miti na misitu.
•    Kusimamia uendelezaji wa misitu ya kupandwa isiyozidi hekta 5,000 au ya asili isiyozidi hekta 10,000.
•    Kufanya utafiti wa misitu.
•    Kutekeleza Sera na Sheria za misitu.
•    Kuendesha mafunzo ya Wasaidizi Misitu.
•    Kukusanya takwimu za misitu.
•    Kufanya ukaguzi wa misitu.
•    Kupanga na kupima madaraja ya mbao.
•    Kudhibiti leseni na uvunaji wa miti.
•    Kutoa ushauri na mafunzo kwa wananchi juu ya uendelezaji na matumizi endelevu ya miti kwa wananchi.
•    Kufanya ukadiriaji wa rasilimali za misitu.
•    Kupima maeneo na kuchora ramani za misitu.

20.2 SIFA ZA MWOMBAJI

•    Kuajiriwa wenye Shahada ya Misitu kutoka chuo Kikuu cha kilimo cha Sokoine au Vyuo Vikuu vingine vinavyotambuliwa na Serikali.

20.3 MSHAHARA

•    Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi.

==========


21.0 MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA II – NAFASI- 5

21.1 MAJUKUMU YA KAZI

•    Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi na mbuga za wanyamapori.
•    Kusimamia utekelezaji wa taratibu za uwindaji na utalii.
•    Kutekeleza kazi za maendeleo katika Mapori ya Akiba.
•    Kuhakiki ulinzi wa nyara za Serikali.
•    Kuhakiki vifaa vya doria.
•    Kudhibiti usafirishaji wa wanyamapori na nyara nje na ndani ya nchi.
•    Kudhibiti matumizi ya magari ya doria.
•    Kuratibu uingiaji wa wageni katika Mapori ya Akiba.
•    Kusimamia uwindaji wa kitalii.
•    Kudhibiti na kusimamia umilikaji wa nyara.
•    Kuweka mikakati ya kudhibiti moto mkali.
•    Kukusanya takwimu za wanyamapori na mimea.

21.2 SIFA ZA MWOMBAJI

•    Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au Kidato cha VI, wenye stashahada ya Uhifadhi wa Wanyamapori Mweka au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

21.3 MSHAHARA

•    Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B na C kwa mwezi.

===========


22.0 AFISA UGAVI MSAIDIZI II (ASSISTANT SUPPLIES OFFICER) – NAFASI 1

22.1 MAJUKUMU YA KAZI

•    Kutunza ghala la vifaa lenye thamani ndogo.
•    Kupokea vifaa vipya vitakavyoletwa na wazabuni mbalimbli na kupokea vifaa ambavyo vimetumika lakini vinahitaji kutunzwa kabla ya kufutwa.
•    Kufungua na kutunza “Bin Card” kwa kila kifaa kilichopo ghalani.
•    Kufungua “Ledger” ambayo itatunza kumbukumbu ya vifaa vinavyoingia, kutunzwa na kutoka kwa nyaraka mbalimbali.
•    Kutoa vifaa kwa wateja na watumiaji wengine.
•    Kuhakikisha kwamba ghala na vifaa vilivyomo vinatunzwa katika hali ya usafi na kwa usalama.
•    Kuandaa hati za kupokelea vifaa.
•    Kufanya kazi zingine atakazopangiwa.

22.2 SIFA ZA MWOMBAJI

•    Kuajiriwa wenye cheti cha “National Store-Keeping Certificate au “Foundation Certificate” kitolewacho na Bodi ya Taifa ya Usimamizi wa Vifaa au wenye Cheti kinachotambuliwa na Bodi ya Taifa ya Usimamizi wa Vifaa.

22.3 MSHAHARA
•    Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.A kwa mwezi

===========


23.0 MSAIDIZI WA OFISI – NAFASI- 10

23.1 MAJUKUMU YA KAZI

•    Kufanya usafi wa ofisi na mazingira ya nje na ndani ikiwa ni pamoja na kufagia, kufuta vumbi, kupiga deki, kukata majani, kupalilia bustani, kumwagilia maji bustani, kupanda maua au miti na kusafisha vyoo.
•    Kuchukua na kupeleka majalada na hati nyingine kwsa maofsa waoaohusika na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
•    Kusambaza barua za Ofisi kama jinsi atakavyoelekezwa.
•    Kutayarisha chai ya ofisi.
•    Kupeleka mfuko wa posta na kuchukua barua kutoka Posta.
•    Kuhakikisha kwamba vifaa vya ofisi vinaweka sehemu zinastahili.
•    Kufungua Milango na Madirisha ya Ofisi wakati wa Asubuhi na Jioni kuyafunga baada ya Saa za Kazi.
•    Kudurufu barua au machapisho kwenye mashine za kudurufia.
•    Kuweka katika majalada nakala za barua zilizochapwa katika ofisi walizomo.
•    Kutunza vifaa vya ofisi na kutoa ripoti kila vinapoharibika.

23.2 SIFA ZA MWOMBAJI

•    Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliofaulu vizuri katika masomo ya Kiingereza, Kiswahili na Hisabati.

23.3 MSHAHARA

•    Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS.A

===========


24.0 MLINZI - NAFASI- 5

24.1 MAJUKUMU YA KAZI

•    Kuhakikisha kwamba mali yoyote ya ofisi inayotolewa langoni (nje ya ofisi) ina hati ya idhini.
•    Kuhahikisha kuwa mali yote inayoingizwa langoni inazo hati za uhalali wake.
•    Kulinda usalama wa majengo, ofisi na mali za ofisi mchana na usiku.
•    Kuhakikisha kwamba milango na madirisha yote yamefungwa ipasavyo mwisho wa saa za kazi.
•    Kuhakikisha kwamba wageni wote wanaoingia katika eneo la ofisi wana idhini ya kufanya hivyo.
•    Kupambana na majanga yoyote yatakayotokea katika sehemu ya kazi kama vile, moto, mafuriko n.k na kutoa taarifa katika vyombo vinavyohusika kama vile, moto, mafuriko n.k na kutoa taarifa katika vyombo vinavyohusika.
•    Kutoa ushauri wa jinsi ya kuboresha huduma ya ulinzi mahali pa kazi.

24.2 SIFA ZA MWOMBAJI

•    Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne waliofuzu mafunzo ya mgambo/polisi/JKT au Mafunzo ya Zimamoto kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali.

24.3 MSHAHARA

•    Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS.A


==========


25.0 BARAZA LA SANAA LA TAIFA (BASATA)

Baraza la Sanaa la Taifa ni shirika la Umma lililoundwa kwa Sheria ya Bunge Na. 23 ya mwaka 1984. (Sheria ya kuunda upya Baraza la Sanaa la Taifa kwa kuunganisha Baraza la Sanaa la Taifa na Baraza la Muziki la Taifa na kufuta Sheria ya Baraza la Sanaa la Taifa ya mwaka 1974 na Sheria ya Baraza la Muziki la Taifa ya mwaka 1974 na kuweka utaratibu kuhusiana na mambo hayo. Kazi za Baraza la Sanaa la Taifa ni Kufufua, kukuza na kuendeleza kazi za sanaa ikiwa ni pamoja na Uhamasishaji, Usimamizi, Uimarishaji, Uratibu, Utafiti, na Ushauri wa kazi mbalimbali za Sanaa.

25.1 MKURUGENZI WA UTAFITI NA UKUZAJI WA STADI ZA WASANII – NAFASI - 1 (LINARUDIWA)

25.1.1 MAJUKUMU YA KAZI

•    Kuongoza Idara ya Utafiti na ukuzaji wa stadi za Sanaa.
•    Kuandaa mpango wa Utafiti na kusimamia utekelezaji.
•    Kuandaa mpango wa kukuza stadi za wasanii na kusimamia utekelezaji.
•    Kuwasiliana na watafiti mbalimbali na kushirikiana nao.
•    Kuandaa na kusimamia makubaliano na watafiti wanaojiajiri kwa muda kufanya tafiti maalum
•    Kubaini na kuteua wawezeshaji wa ukuzaji wa stadi za wasanii.
•    Kusimamia uchapishaji wa majarida na vitabu vya Baraza.

25.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI

•    Kuajiriwa wenye Shahada ya Uzamili katika fani za Sanaa (Master of Arts in either Performing Arts, Theater Arts or Cultural and Heritage kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
•    Uzoefu wa kazi usiopungua miaka nane (8) ambapo miaka mitano (5) kati ya hiyo ikiwa ni kwenye nafasi ya uongozi katika idara mbalimbali zilizo chini ya taasisi za umma.

25.1.3 MSHAHARA

•    Mshahara PGSS 14

NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.

i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
v. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
vi. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
vii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
viii. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
ix. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
x. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 24 Machi, 2016
xi. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xii. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza..
i. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo;
http://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa‘Recruitment Portal’)
ii. MUHIMU: KUMBUKA KUWEKA (TO ATTACH) BARUA YAKO YA MAOMBI KWENYE SEHEMU YA ‘OTHER ATTACHEMENTS’.
iii. VYETI NA WASIFU (CV) VITAKAVYOTUMWA BILA BARUA YA MAOMBI HAVITAFIKIRIWA.
iv. WAOMBAJI WANATAKIWA KUANDIKA MAJINA YA VYUO VYAO NA KOZI KWA KIREFU (Eg. Bachelor of Science with Computer Science, University of Dar es Salaam, na msiandike, BSc. Computer Science UDSM)

X. M. DAUDI KATIBU SEKRETARIETI YA AJIRA

Siri Imefichuka...CUF Watoa Sababu za Maalim Seif Sharif Hamad Kuishi Serena Hoteli Pamoja na Gharama Iliyotumika Hadi sasa

$
0
0
SIRI imefichuka kuhusu hatua ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar (SUK), Maalim Seif Sharif Hamad, kuishi hotelini jijini Dar es Salaam.

Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), amekuwa akiishi katika Hoteli ya Serena jijini Dar tangu aliporuhusiwa kutoka Hospitali ya Hindu Mandal Machi 8, mwaka huu alipokuwa amelazwa kwa matibabu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mmoja wa ofisa wa ngazi za juu wa CUF, alishangazwa na hatua ya baadhi ya watu kuhoji kiongozi huyo kuendelea kuishi hotelini hapo.

Alisema hatua ya kiongozi huyo kuishi hotelini ni matokeo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), kushindwa kutekeleza ahadi ya kumpa nyumba pindi anapokuwa Dar es Salaam katika shughuli zake.

Alisema kutokana na hali hiyo imekuwa ni utaratibu kwa kiongozi huyo kufikia katika hoteli hiyo na gharama za kuishi hotelini hapo hulipwa na SMZ kwa mujibu wa sheria.

“Tangu mwaka 2010 Maalim aliahidiwa atapewa nyumba na Serikali ya SMZ lakini hilo halijafanyika, hiyo nyumba hajapewa hadi leo ndiyo maana mara zote akija Dar hufikia hotelini.

“SMZ ndiyo wenye jukumu la kulipa na si vinginevyo, kwani hata kama kama kuna viongozi wa SMZ wamepewa nyumba kwa muda wote, lakini Maalim Seif hajapewa, sasa kama unataka kujua kwa undani unaweza kuwauliza viongozi wa Serikali wao ndiyo wenye majibu zaidi,” alisema ofisa huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe

Gharama zilizotumika kwa siku 7
Kwa mujibu wa chumba anachoishi kiongozi huyo chenye hadhi ya rais ambacho hutozwa kwa Dola za Marekani 2,801.50, ambapo dola moja ni sawa na Sh 2,180. Hivyo kwa siku saba hadi kufikia leo Serikali imemlipia Maalim Seif,  Sh milioni 42.946.

Kauli ya CUF
Alipotafutwa Kaimu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa CUF, Hamad Masoud Hamad, alisema hatua ya Maalim Seif kuishi hotelini inatokana na maagizo ya daktari wake ambaye amemtaka apumzike kwa sasa.

Alisema kutokana na hali hiyo baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali alipokuwa akipatiwa matibabu alikwenda katika Hoteli ya Serena anapofikia kila mara anapokuwa jijini Dar es Salaam.

Alipoulizwa ni nani anayelipa gharama za kuishi hotelini hapo, Hamad alisema wanaoweza kuzungumzia suala hilo ni viongozi wa SMZ.

“Magufuli (Rais), alipokwenda kumwona alimuuliza ni nani anayemlipia gharama za hoteli na Maalim alisema wazi ni SMZ, lakini ninachotaka kuwaambia Maalim Seif hana nyumba Dar es Salaam.

“… kama wapo viongozi waliopewa nyumba wa SMZ ni hao lakini si Maalim Seif, tangu mwaka 2010 hana nyumba na hufikia hotelini, hana nyumba ya Serikali wala yake binafsi,” alisema Hamad.

SMZ wazungumza
Alipotafutwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Aboud ili kupata ufafanuzi wa suala hilo, alisema Maalim Seif anastahiki zake kama kiongozi wa SMZ ikiwemo kupatiwa haki ya matibabu pamoja na mahala pa kuishi.

“SMZ ni wajibu wake kuwahudumia viongozi na wananchi wake kwa ujumla, Maalim Seif bado ni Makamu wa Kwanza wa Rais hivyo ana wajibu wa kuhudumiwa.

“Na katika hili anahudumiwa na SMZ ikiwemo kulipiwa hoteli pindi awapo nje ya Zanzibar na si hilo tu pia tunahusika kumpa stahiki zake zote ikiwemo matibabu.

“Kwa kawaida pindi kiongozi yoyote wa kitaifa anapokuwa Dar es Salaam na kama hana nyumba SMZ hulipa malazi ya kiongozi wake na Maalim bado ni kiongozi na hata kama akiondoka kwenye uongozi bado anazo stahiki zake ikiwemo kuhudumiwa kama kiongozi mstaafu,” alisema Waziri Aboud.

Alisema pamoja na hali hiyo kwa sasa Serikali ya Muungano ndiyo inayolipa gharama za Maalim Seif kuishi hotelini kwa agizo la Rais Dk. John Magufuli.

Alisema ahadi ya Rais Magufuli ya kusaidia kulipia hoteli anayoishi Maalim Seif inaonesha ni namna gani Serikali zote mbili ya Muungano na ile ya Zanzibar zinavyoshirikiana kwa dhati.

“Kwa ubinadamu wake Rais Magufuli tunamshukuru sana kwani inaonesha namna gani kiongozi huyo wa Jamhuri ya Muungano alivyo na mapenzi mema  na Zanzibar pamoja na viongozi wake.

“… ila pamoja na yote SMZ bado ina wajibu wa kutekeleza wajibu wake wa kuwatunza viongozi wake wote wakiwemo waliokuwa ndani ya Serikali pamoja na wale waliostaafu,” alisema Aboud

Msomi Prof Baregu Aibuka na Kudai Utawala wa RAIS Magufuli ni wa Kejeshi...Kuwapo Kwa Wanajeshi Wengi Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa Wamtisha

$
0
0
SIKU moja baada ya Rais Dk. John Magufuli kuteua wakuu wa mikoa wapya, mtaalamu wa sayansi ya siasa, Profesa Mwesiga Baregu, ameibuka na kusema kuwa kuwapo kwa wanajeshi wengi wastaafu katika uteuzi huo inadhihirisha wazi kuna dalili za utawala wa kijeshi nchini.

Profesa Baregu amesema kuwa  wanajeshi huwa hawana hulka ya kidemokrasia.

“Kitu kimoja kinachojitokeza kwenye uteuzi huu ni kuwepo kwa wanajeshi wastaafu, na mimi ninavyoelewa wanajeshi huwa hawana hulka za kidemokrasia. Hii inaonyesha wazi kwamba utawala huu ni wa kijeshi,” alisema.

Profesa Baregu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alisema haileti picha nzuri kuwapo kwa wanajeshi wengi katika utawala kwa sababu tawala za mikoa na wilaya ni saula la kiraia na demokrasia zaidi.

Alisema rasimu ya katiba ambayo yeye alikuwa mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ilipendekeza kupitia upya tawala za mikoa na kupunguza idadi yake.

“Kutokana na hilo, mamlaka ya wananchi inamezwa kwa sababu wakuu wa mikoa na wilaya ni wengi na kunakuwepo na mgongano mkubwa,” alisema.

Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Bashiru Ali, alisema uteuzi wa wakuu wa mikoa na wilaya ni wa rais na wanaoteuliwa ni watu mchanganyiko.

Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ruaha (Ruco), Profesa Gaudence Mpangala, alisema kila anapoingia kiongozi mpya anaunda timu ambayo anaona ataendana nayo.

Msaga Sumu: Sikunufaika na Wimbo Wangu wa Kampeni Niliomwimbia Edward Lowassa....Wanaosema Nilijengewa Nyumba Waongo

$
0
0
MSANII wa nyimbo za Uswahilini ‘Kigodoro’, Seleman Jabir ‘Msaga Sumu’, ameweka wazi kwamba licha ya kupata jina kubwa katika kampeni za urais na wabunge mwaka 2015, lakini hakunufaika na wimbo aliowatungia wagombea hao.

msaga sumu
Msaga Sumu aliweka wazi hayo jana alipotembelea ofisi za Kampuni ya New Habari (2006) Ltd inayochapisha magazeti ya Mtanzania, Rai, Bingwa, Dimba na The African zilizopo Sinza Kijiweni jijini Dar es Salaam.

Msanii huyo alilalama kwamba licha ya kutunga wimbo uliomtaja aliyekuwa mgombea urais wa Chadema kupitia mwavuli wa Ukawa, Edward Lowassa, lakini hakunufaika nao kama watu wanavyodhani.

“Wimbo haukuninufaisha chochote kama baadhi ya watu wanavyosema kwamba nimejengewa nyumba na nimenunuliwa gari, nilichopata ni fedha ya mboga na kufahamu baadhi ya mikoa ya Tanzania ambayo sikuwa
nikiifahamu ukiwemo Mwanza, Mbeya, Tabora na mingineyo.

“Nilipoona hakuna maslahi nikamweleza Mzee Lowassa tulipokutana naye mkoani Morogoro katika kikao cha pamoja na wasanii wengine, hapo nilimweleza dukuduku langu hilo na ndipo tukakubaliana upya kwa mikoa mitano nikalipwa kwa mikoa hiyo tu.

“Kwanza watu wajue kwamba wimbo wa Lowassa niliuimba kipindi alipokuwa CCM, lakini sikutaja chama
chochote ila alipohamia Chadema alihama nao wakaniita nikatie maneno ya Chadema,” alieleza Msaga Sumu.

Katika hatua nyingine mkali huyo wa ‘Kigodoro’ alisema yupo mbioni kuachia wimbo wa timu anayoipenda kwa Tanzania, Yanga Africans ili kulipa fadhili ya wimbo aliowaimbia mashabiki wa Simba.
“Mimi ni mwana Yanga lakini niliimba wimbo wa Simba kwa kuwa Simba walikuwa bora kwa kipindi kile lakini kwa sasa nimeandaa wimbo mpya wa Yanga ambao utakuwa mkali kuliko ule wa Simba, naomba mashabiki wangu wakae mkao wa kusubiri kwa hamu wimbo huo,’’ alieleza.

Mtanzania

MAKALA:Kupanda, Kushuka na Kuibuka Tena Kwa Mwigizaji Mrembo Lulu Michael.....

$
0
0
Alikuwa anatambulika kutokana na uigizaji wake tangu akiwa binti wa miaka mitano na umahiri wa kuvaa vyema uhalisia wa nafasi anazopewa kuigiza, jambo lililomtengenezea mashabiki wengi.

Umaarufu hauna tofauti na mvua za masika ambazo zinaweza kuleta neema au maafa kwa mafuriko. Wanaomfahamu Lulu tangu akiigiza kama mtoto katika tamthilia za Kundi la Kaole Sanaa Group hawahitaji kusimuliwa. Wengine wanasema majina yanaponza kwa maana ukiwa maarufu jambo lako dogo litashupaliwa lionekane kubwa. Kuna wakati Lulu alikuwa habari ya mujini kwa Kiingereza tungesema She was on top of her game.

Uigizaji na utangazaji wa Kipindi cha Watoto Wetu kilichokuwa kikirushwa na kituo cha ITV mwanzoni mwa miaka ya 2000 vilimjengea umaarufu.

Awali alipamba vichwa vya habari kwa kufanya vema katika maigizo na filamu, baadaye alipamba vichwa hivyo kwa habari nyingine ambazo hazina uhusiano kabisa na filamu na sasa amerejea akiwa na habari kubwa kuliko zote ambazo waigizaji wengi wameshindwa kufikia lengo hilo.

Pengine mwenyewe aligundua nini kilikuwa kinatokea katika maisha yake ndiyo maana akaamua kuachia filamu aliyoibatiza jina la “Foolish Age”. Huyu si mwingine bali ni Elizabeth Michael ambaye anafahamika zaidi Afrika Mashariki na Kati kwa jina moja la Lulu.

Jina la Lulu alipewa na Chiki Mchome ambaye mbali na kumtaka alitumie katika filamu yake, alimsihi alitumie kibiashara kwani litamfungulia milango ya neema siku za usoni.

Maandalizi, ujasiri, kujitambua , kujituma kumemfanya aibuke kidedea katika tuzo kubwa za filamu barani Afrika za Africa Magic Viewers’ Choice (AMVCA), kupitia filamu yake ya “Mapenzi ya Mungu”. Filamu ambayo kwa madai ya mwigizaji huyo kisa na hadithi yake inaendana na maisha yake.

Kwa nini alilia?

Maneno machache yalisikika wakati akitoa neno la shukrani baada ya kupokea tuzo yake, mengi yalimezwa na kilio alichokitoa.

Sikulia kwa uchungu, nililia kwa furaha na huzuni pamoja, kama nilivyohuzunika wakati wa kuigiza filamu ya “Mapenzi ya Mungu” ambayo maarufu Mapenzi ndivyo nilivyolia wakati nachukua tuzo.

Kushinda tuzo kubwa kama ile siyo kitu kidogo, nilikuwa nina kila sababu ya kulia ukizingatia nimekuwa msanii wa kwanza wa kike kuipata, ahsanteni Watanzania na mashabiki wangu kwa kuniunga mkono.

 2016

Mwaka ambao Lulu amejitofautisha na waigizaji wengine wa kike kutokana na kunyakua tuzo ya kubwa Afrika katika kipengele cha filamu bora Afrika Mashariki kupitia filamu yake ya “Mapenzi ya Mungu”. Ameibuka kuwa mwigizaji wa kwanza kutoka nchini Tanzania kushinda tuzo hiyo na kuwapiku magwiji wa filamu nchini.

2015

Mwaka huu ndiyo ulikuwa msingi wa mafanikio ambayo Lulu anayofurahia leo. Huu ndiyo mwaka aliotoa filamu yake ya Mapenzi ya Mungu ambayo ndiyo ilimtoa kimasomaso katika tuzo hizo. Hii ilikuwa ni kazi yake ya tatu baada ya kutoa “Foolish Age” zote zikiwa chini ya Kampuni ya Usambazai Filamu ya Proin Promotion.

Mwigizaji huyo alidhamiria kusimama na kuonyesha kuwa amejifunza kitu kutokana na misukosuko aliyopitia, baada ya kujiunga na Chuo cha Utumishi wa Umma Magogoni Jijini Dar es Salaam.

2014

Lulu ana cha kujivunia katika mwaka huu pia kutokana na kuibuka kidedea katika Tuzo za Watu, ambapo alishinda kipengele cha msanii bora wa kike anayependwa. Kutokana na kupata tuzo hiyo alizidi kujiongezea umaarufu na kuwa gumzo huku akifanya mambo yake kimya kimya na kujiondoa kwenye makundi ya wadada wa mjini.

Aliweza kujitofautisha na wasanii wengine kwa kuishi maisha ya kistaa, mpangilio wa mavazi, nywele, viatu na mikoba hivyo vyote vilitosha kumfanya Lulu avute mashabiki wengi kwenye ukurasa wake wa Instagram.



2012/13

Aliiibuka kinara katika kinyang’anyiro cha mwigizaji bora wa kike katika Tamasha la Zanzibar International Festival (ZIFF), kutokana na umahiri alioonyesha wakati akiigiza filamu ya “Women of Principles”.

Kama nyota imeng’aa, mwaka huo huo alifanya uzinduzi wa kishindo wa ujio wake mpya baada ya kutoka katika mikasa ya kusota rumande, alifanya uzinduzi wa filamu yake mwenyewe iitwayo “Foolish Age” na “Family Curse”.

Alianza lini kuigiza?

Elizabeth Michael lulu akiwa na miaka mitano.Muigizaji Mahsein Awadh, “Dk. Cheni”ndiye aliyemuibua kupitia bonanza la kuibua vipaji lililoandaliwa na nyota huyo aliyekuwa akiigiza katika kundi la Kaole.

By Kalunde Jamal, Mwananchi

Picha : Rais Magufuli Awaapisha Wakuu Wapya Wa Mikoa Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Jeshi la Polisi,Zelote Steven Zelote kuwa mkuu wa mkoa wa Rukwa,Hafla hiyo fupi ya kuwaapisha Wakuu hao wa Mikoa imefanyika leo Ikulu,jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu kuwa mkuu wa mkoa wa Kagera,Hafla hiyo fupi ya kuwaapisha Wakuu hao wa Mikoa imefanyika leo Ikulu,jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Meja Jenerali Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga  kuwa mkuu wa mkoa wa Katavi,Hafla hiyo fupi ya kuwaapisha Wakuu hao wa Mikoa imefanyika leo Ikulu,jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga kuwa mkuu wa mkoa wa Geita,Hafla hiyo fupi ya kuwaapisha Wakuu hao wa Mikoa imefanyika leo Ikulu,jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Meja Jenerali Mstaafu Emmanuel Edward Maganga kuwa mkuu wa mkoa wa Kigoma,Hafla hiyo fupi ya kuwaapisha Wakuu hao wa Mikoa imefanyika leo Ikulu,jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Paul Christian Makonda kuwa mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam,Hafla hiyo fupi ya kuwaapisha Wakuu hao wa Mikoa imefanyika leo Ikulu,jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mh.Anne Kilango Malecela kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Hafla hiyo fupi ya kuwaapisha Wakuu hao wa Mikoa imefanyika leo Ikulu,jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.

Kuna Uwezekano Babu Seya, Papii Kutoka Jela Ndani ya Saa 72 zijazo....

$
0
0
Hatimaye rufaa ya wanamuziki maarufu nchini, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’, imesikilizwa katika Mahakama ya Haki za Binadamu Afrika (AfCPHR) jijini Arusha Machi 11, mwaka huu na sasa zimebaki saa 72 tu kujua hatima yao, yaani Machi 18, 2016, UWAZI linakupa zaidi.

Rufaa hiyo ilisikilizwa na mahakama hiyo yenye majaji 11 kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) ambapo rais wao ni Jaji Augustine Ramadhani wa Tanzania ambaye pia aliwahi kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.

MAJAJI WENYE SIRI MOYONI
Baadhi ya majaji waliotajwa kusikiliza rufaa hiyo na nchi zao kwenye mabano ni Ben Kioko (Kenya), Solomy Balungi Bassa (Uganda), Duncan Tambala (Malawi), Angelo Vasco Matuse (Msumbiji), Sylvain Ore (Ivory Coast), El Hadji Guisse (Senegal) na Rafaa Ben Achous (Tunisia).

KUTOKA MAHAKAMANI
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika kutoka katika mahakama hiyo, rufaa hiyo ilisikilizwa kwa faragha na hakuna mwandishi wa habari yeyote aliyeruhusiwa kuingia kupata mwenendo.
Chanzo kilizidi kusema kuwa rufaa ya mwanamuziki huyo na mwanaye, ilisikilizwa kwa karibu saa tatu tangu ianze na matokeo au hukumu wanayo wahusika.

SABABU ZAFICHWA
Hata hivyo, si Rais wa Mahakama ya Afrika, Jaji Ramadhani au mtu mwingine yeyote aliyeeleza sababu za kesi ya Babu Seya na mwanaye Papii Kocha isikilizwe faragha.

HATA JAJI RAMADHANI HAJUI
Wakati akichukua madaraka ya urais wa mahakama hiyo, Jaji Ramadhani alisema: “Kesi yoyote inayohusu nchi yangu mimi sitakiwi kuhudhuria kutokana na sheria zetu za mahakama hii…”
Kutokana na maneno hayo, kumezuka utata kwani haikujulikana mara moja kama wakati shauri la Babu Seya na mwanaye linasikilizwa, Jaji Ramadhani alikuwepo au la kwani rufaa ilipitiwa kwa faragha na kama alitoka nje basi itakuwa imepitiwa na majaji 10.

WATOA UAMUZI
Habari zaidi zinasema kuwa mara baada ya rufaa hiyo kupitiwa na majaji hao, shauri lao linapelekwa kwenye Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu ambako huko ndiko kutakakotolewa uamuzi ndani ya saa 72 zijazo.

WANACHODAI
Wanamuziki hao wamekata rufaa dhidi ya adhabu waliyohukumiwa mwaka 2004 ya kutumikia kifungo cha maisha jela ambapo mpaka sasa, wapo Gereza la Ukonga, Dar wakitumikia kifungo chao.

Kupitia shauri lao lililowasilishwa mahakamani na jalada lake kupewa namba 006/2015, wawili hao wanaiomba mahakama hiyo kutoa uamuzi kuwa haki zao zilikiukwa na wanaomba waachiwe huru na kulipwa fidia.

Pia wanataka mahakama hiyo iteue wataalam watakaotoa ufafanuzi wa hoja za kesi yao na kuisaidia kufikia wajibu wake.

Miongoni mwa hoja za Babu Seya na mwanaye zilizosikilizwa mahakamani hapo, ni pamoja na kwamba mwenendo wa shauri lao haukufanyika kwa kuzingatia haki, vilevile wanadai hati ya mashitaka dhidi yao ilikosewa kuandikwa tarehe ambayo tuhuma za makosa yao zilidaiwa kufanywa hivyo wakashindwa kutayarisha utetezi wao.

Pia wanadai mahakama iliyowatia hatiani, ilijielekeza katika ushahidi wa upande wa mashitaka pekee usioshirikisha ushahidi mwingine.

WANAISEMA SERIKALI
Wanadai kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia maofisa wake, ilivunja misingi ya haki za binadamu na sheria za kimataifa kwani ilivunja Ibara 1, 2, 3, 5, 7(1) b, 13 na 18 (1) ya Mkataba wa Afrika wa Ubinadamu na Haki za Binadamu.
Wanadai kwamba mashitaka dhidi yao yalitungwa na hivyo hukumu iliyotolewa haikujikita katika ushahidi wenye nguvu katika sheria.


Oktoba 12, mwaka 2003, Nguza na wanaye watatu, Mbangu, Johnson na Francis walikamatwa na kufikishwa Kituo cha Polisi cha Magomeni, Dar wakidaiwa kubaka na kulawiti watoto 9, maeneo ya Sinza Palestina, Dar.

Oktoba 16, mwaka huohuo walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma hizo huku wakitetewa na Wakili Mabere Marando ambaye juzi hakupatikana alipotafutwa na gazeti hili ili kutoa ufafanuzi kupitia simu yake ya kiganjani.

Juni 25, 2004, Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Addy Lyamuya aliwatia hatiani Babu Seya na wanaye kwa hatia ya kubaka na kulawiti.

Januari 27, mwaka 2005, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Thomas Mihayo alitupilia mbali rufaa yao iliyokuwa ikipinga hukumu dhidi yao.

Awali mwaka 2004, baada ya kukutwa na hatia katika kesi hiyo, Babu Seya, Papii Kocha na wakili wao, Mabere Marando walikata rufaa ya pili ambayo ilitupiliwa mbali.

Mwaka 2010, waliomba tena rufaa ambayo marejeo yake yalisikilizwa na kutolewa hukumu Februari 2010. Mahakama iliridhia hukumu ya kifungo cha maisha kwa Babu Seya na Papii Kocha huku ikiwaachia huru watoto wake, Mbangu na Francis.

Chanzo:Global Publishers

Rais Magufuli Awataka Wakuu wa Mikoa Kuwaweka Ndani Hata Masaa 48 Viongozi Wanaonyanyasa Wananchi

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Magufuli akihutubia Wakuu wa Mikoa wapya 26 na Watumishi wengine wa Serikali walioapishwa leo amesema; "Nimewateua ninyi (Wakuu wa Mikoa) muende mkawatumikie Wananchi na sio kwenda kufanya siasa. 

"Ilinichukua muda sana kuteua kwa sababu nilitaka kujihakikishia kuwa ninateua watu makini.

"Mkienda Mikoani nataka  mkatatue kero za Elimu, Ajira, Ujambazi na nyingine kwa kushirikiana na viongozi wengine na Mumtangulize Mungu naye atawasaidia.

"Kuna viongozi huko wananyanyasa wananchi, unakuta katibu tarafa, mtendaji wa kata ananyanyasa  tu  wananchi  bila  sababu.

"Ninyi  mna mamlaka  ya  kumuweka  mtu  ndani  hata  masaa 48. Kawawekeni wengi ili kusudi wajue kwamba wananchi wanatakiwa kuheshimiwa." Amesema Rais

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Atapeliwa Million 10 Kupitia Mtandao Kwenye Simu yake ya Mkononi....

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Fadhili Nkulu ameibiwa kiasi cha shilingi milioni 10 na wezi wa mtandao ambao waliteka mawasiliano yake ya simu za mkononi kwa muda wa saa 3 na kutumia namba hizo kuomba fedha kwa watu wa karibu na kiongozi huyo.

Akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake ,Nkulu amesema kuwa jana majira ya saa 10:00 alasiri simu zake zilikua hazipatikani hewani mpaka majira ya saa 3:00 usiku ndipo aliposhtuka na kuanza kufuatilia na kugundua kuwa mawasiliano yake yalitekwa kwa muda.

Mkuu huyo wa Wilaya amelaani vitendo vya wizi wa mtandao vinavyofanywa na watu wenye nia ovu huku akiwataka wananchi na wamiliki wa makampuni ya simu kuwa makini juu ya wizi huo wa kimtandao ambao umeshamiri miaka ya hivi karibuni.

Msaidizi wa Mkuu wa Mkoa Yoitham Ndembeka ambaye alitumiwa ujumbe wa kumtaka atume fedha kupitia namba ya mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa baada ya kusumbuliwa na matapeli hao ambao hawakutaka kupokea simu aliamua kuachana nao huku akitafuta namna ya kuonana ana kwa ana na Mkuu huyo wa Wilaya.

Kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya Simu ya Airtel kanda ya Kaskazini alipotafutwa kujibu madai hayo simu yake haikupatikana hewani.

Wizi wa mitandao umeshamiri na kushika kasi hasa katika kipindi hiki ambacho teknolojia imekua kwa kiasi kikubwa ,hivyo makapuni ya simu,mamlaka za kusimamia teknolojia ya mawasiliano TCRA pamoja na polisi wanapaswa kuchukua hatua kupambana na uhalifu huo

Polisi Wafumua Kituo cha Wauza na Watumia Unga Jijini Dar es Salaam..Vijana 90 Mbaroni....

$
0
0

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, jijini Dar limekifumua kituo cha watumiaji wa madawa ya kulevya ‘unga’ na kuwakamata vijana zaidi ya 90 waliokutwa eneo hilo lililopo Mwembeyanga, Tandika.

Jumatano iliyopita mchana, polisi wakiwa na magari yao sita walivamia eneo hilo na kuwazunguka bila kutarajia kisha kuwashika na kuwapeleka Kituo cha Chang’ombe.

Gazeti hili lilishuhudia kamatakamata hiyo ambayo ilitokana na malalamiko ya wakazi wa eneo hilo ambao waliwatuhumu vijana hao kuwa licha ya kuvuta unga, lakini pia hufanya vitendo vingine vya kihalifu.

Zoezi hilo la kamatakamata linasemekana kuwa ni nguvu mpya ya kamanda mpya wa polisi wa mkoa huo ACP Gilles Muroto (pichani), ambaye amechukua nafasi ya ACP Andrew Satta aliyehamishiwa Kanda Maalum ya Polisi Tarime-Rorya.

Akizungumza na gazeti hili, Kamanda Muroto alisema msako huo mkali unaendelea katika mkoa mzima ikiwa ni pamoja na kuwasaka majambazi na akinadada wanaojiuza kwa jina maarufu machangudoa.

Mzee wa Miaka 75 Amepigwa na Mpangaji Wake Hadi Kufa Kisa Bili ya Umeme.....

$
0
0
Mzee wa miaka 75 mkazi wa Ondo State nchini Nigeria, ameripotiwa kupigwa hadi kufa na mpangaji wake kisa bili ya Umeme.

Mtandao wa Naija Gists umeripoti kuwa, Baba mwenye nyumba huyo ambaye ni mstaafu wa shirika la maji Nigeria, aliwapa masharti wapangaji wake kuwa endapo bili ya umeme ikitoka basi hela ichangwe na ilipwe ndani ya masaa 24.

Taarifa inazidi kudadavua kuwa mpangaji mmoja alichelewa kutoa fedha hiyo, mwenye nyumba akaanza kumkoromea ndipo jamaa alipoamua kumshushia kipigo kilichompelekea umauti.

Mshitakiwa anashikiliwa katika kituo cha polisi cha Ondo kwa mahojiano zaidi

Zanzibar Kimenuka...Bomu Larushwa na Kulipua nyumba ya Kamishna wa Polisi Hamdani Omar Makame

$
0
0
Habari kutoka visiwani Zanzibar zinaeleza kwamba, nyumba kadhaa ikiwemo  ya Hamdani Omar Makame ambaye  ni Kamishna wa Polisi Viswani Zanzibar  zimelipuliwa kwa mabomu.

Habari hizo zinaeleza kwamba, Jeshi la Polisi linaendesha kamata kamata ya watu waliohusika kwenye tukio hilo  ambapo  mpaka  sasa  watu 31 wametiwa  mbaroni.

Tukio hilo limezidisha hali ya wasiwasi visiwani humo ambapo ni siku 5  tu  zimesalia  kabla  ya  uchaguzi  wa  marudio  kufanyika

Mwanaume Wangu Nadhani Anajulikana..Nyie Endeleeni Kumpa ‘Kiki’ Mkongo – Wema Sepetu

$
0
0
Staa wa filamu Wema Sepetu, amemkana raia wa Kongo ambaye watu wengi wanadai ana mahusiano naye ya kimapenzi.
Wema na Idris

Kupitia ukurasa wa instagram, Wema Sepetu ameandika.

Sijawahi na sitowahi kuwa na mwanaume Mkongo wa aina yoyote ile, sasa nashangaa watu wameona mimi ndo daraja la kuwapa umaarufu, I’m tired, huyo Apocalypse sijui kitu gani aint my man, I only know him as a friend, So please guys…. Niacheni kidogo tafadhal… Alam-siq.

And ontop of all that I think u all know me by now nikiwa na mtu sijivungi kumtangaza maana huwa I live to please my heart…

Mwanaume wangu nadhani anajulikana… Sasa endeleeni kumpa huyo baba attention sababu yeye nako naona kashaona ni kamchezo kakupatia followers… Na nyie mnampa airtime ya kutosha…. So anaendelea… Ananiudhi na mimi kiukweli hadi napata hasira… But nakaa tu kimya.

Kupitia ujumbe huo inaonyesha huwenda Wema Sepetu bado yupo kwenye mahusiano na Idris Sultan licha ya taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuzagaa kwamba wawili hao ameachana.

Taarifa ya Magufuli Kuwapunguzia Ulinzi Marais Wastaafu....IKulu Yafunguka na Kukanusha Vikali Habari Hiyo...

$
0
0
Gazeti la JAMBOLEO, toleo namba 2381 la tarehe 15 Machi, 2016 limechapisha taarifa yenye kichwa cha habari kisemacho "Magufuli awapunguzia ulinzi marais wastaafu".

Taarifa yake kamili ipo katika ukurasa wa nne, na inaeleza kuwa Mheshimiwa Rais John Magufuli amewapunguzia ulinzi Marais wastaafu na imewataja marais hao kuwa ni Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete.

Ikulu inapenda kuwataarifu watanzania kuwa taarifa hizo sio za kweli na inalitaka gazeti hilo kukanusha habari hiyo mara moja, vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Aidha, Ikulu inapenda kuwataarifu watanzania kuwa utaratibu wa ulinzi wa Marais wastaafu haujabadilishwa.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam-15 Machi, 2016

Rais Magufuli Awashukia Vijana Wacheza Pool Asubuhi Kwenye Mabaa..Atoa Tamko Kwa Wakuu wa Mikoa Ikiwezekana Wakamatwe

$
0
0
Rais John Magufuli leo amewaapisha wakuu wa mikoa wapya aliowateua hivi karibuni na katika hotuba yake amewataka wakuu wa mikoa hao wapya kuhakikisha vijana wanafanya kazi na kuacha uzembe.

Rais Magufuli amewataka wakuu wa mikoa hao kuhakikisha hakuna vijana ambao watakuwa wanakwenda kucheza pool table asubuhi na badala yake vijana hao wanatakiwa kufanya kazi kweli kweli hata kwa kulazimishwa.

"Nimeamua kuwateua wakuu wa mikoa nikiamini kwamba mtaniwakilisha vizuri katika mikoa yenu.

"Napenda niwape pole kwa sababu mtakwenda kufanya kazi kweli kweli kutatua kero za wananchi wetu.

"Lakini pia niwaombe wakuu wa mikoa mkasimamie watu wafanye kazi hasa vijana.

"Haiwezekani vijana leo hii unawakuta saa mbili asubuhi wanacheza Pool table wakati wakina mama wanalima shambani, kama hawataki kufanya kazi kwa kupenda walazimishwe kufanya kazi. Atakayekataa mpelekeni  kambini akafanye kazi" amesema Rais Magufuli

Rais Magufuli ameongelea pia suala la wafanyakazi hewa kwenye Halmashauri zote nchini ambapo  amewapa siku 15 wakuu wapya wa mikoa kuhakikisha hakuna wafanyakazi hewa katika Halmashauri zote nchini.

"Niwape grace time ndani ya siku 15 wakurugenzi wawe wamejumlisha na wamewatoa wafanyakazi hewa katika payroll

"Mshahara wa mwezi tukigundua mkurugenzi amelipa mshahara hewa ajue hana kazi na tunampeleka mahakamani

"Singida na Dodoma ina wafanyakazi hewa 202 wanalipwa mishahara hewa na kwenye data ilionyesha wengine wamefariki, wamestaafu, wamefukuzwa , wengine likizo bila malipo wote hao kumbe wanalipwa malipo ya serikali fedha ambazo zingetumika kutatua matatizo ya wananchi" 

"Nimeamua kuwateua nyinyi kama wakuu wa mikoa nikiamini mtaniwakilisha vizuri popote.


"Tusiogope kuchukua maamuzi, nafuu uchukue maamuzi hata kama ni mabaya yatarekebika huko mbele."Amesema Rais Maguful

Mrembo Naj Athibitisha Uhusiano Wake na Barakah Da Prince Kwa Picha Hii

$
0
0
Naj hataki kuficha tena penzi lake na muimbaji wa ‘Siwezi’, Barakah Da Prince.

Uhusiano wao ambao hauna muda mrefu tangu uanze, unaonekana kukolea siku hadi siku. Naj amepost picha Instagram ya kichwa cha Barakah huku mkono wake wenye kucha zilizopakwa rangi ya njano ikikikishika.

Ni hivi karibuni tu pia Barakah alidai kumpata mpenzi anayeamini kuwa ndiye aliyeushika moyo wake. Japo picha ya msichana aliyekuwa kwenye picha yake haikuonesha sura yake, msuko aliokuwa nao ulithibitisha kuwa alikuwa ni Naj.

Kamishna Wa Jeshi La Polisi Zanzibar Azungumza Na Wandishi Wa Habari Juu Ya Milipuko Ya Mabomu Inayotokea Unguja Na Pemba

$
0
0
Nyumba ya Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame imeripuliwa  na kitu kinachosadikiwa kuwa  ni bomu na watu wasiojulikana  majira ya saa 5.00 usiku huko Kijichi nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Ofisini kwake Makao Makuu ya Polisi Kilimani, Kamishna Hamdani amesema tukio hilo limeathiri sehemu ya paa la nyumba na dari na  kujeruhi baadhi ya watu  waliokuwa wamelala  na kusababisha hasara kubwa.

Amesema tukio hilo linafanana na  lile lililotokea tarehe 03 mwezi huu katika Maskani ya CCM Kisonge Unguja hivyo polisi inaendelea kufanya uchunguzi ikiwa ni pamoja na kuwasaka wahalifu wanaofanya  uhalifu huo.

Akizungumzia  matukio  mengine ya uhalifu na kuchoma moto nyumba, maskani na kituo cha Afya huko Pemba, alisema  Jeshi la Polisi limeanza msako mkali na kuwatia mbaroni watu 31 ambao wanaendelea kuhojiwa na watakaohusika watafikishwa  katika vyombo vya sheria.

Kamishna Hamdani amewatoa hofu  wananchi kuhusu usalama wao na mali zao kuelekea uchaguzi wa marudio utakaofanyika tarehe 20 mwezi huu na kuwepo kwa ongezeko la askari katika maeneo  mengi ya mijini na vijijini  ni  moja ya juhudi za kuimarisha  ulinzi  na kuhakikisha  uchaguzi huo utakuwa salama na amani.

Ametahadharisha kuwa mtu yoyote atakayejihusisha kuanzisha vurugu au kufanya kitendo chenye ishara ya  uvunjifu wa amani atapambambana na vyombo vya sheria.

Kamishna Hamdani ametoa wito kwa wananchi waliojiandikisha kupiga kura kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili waweze kutimiza haki yao ya msingi ya kikatiba bila ya woga  kwani jeshi hilo limejipanga  kuimarisha ulinzi  sehemu  zote.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images