Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Ushauri kwa TCRA Kuhusu zoezi la Kusitisha Matumizi ya Simu Bandia....

$
0
0
TCRA wametoa taarifa kwa umma miezi michache iliyopita juu ya kusudio la Mamlaka hiyo kusitisha matumizi ya simu bandia ifikapo mwezi Juni mwaka huu.

Ni hatua nzuri na ya kupongeza lakini kwa bahati mbaya,kwa mtazamo wangu,naona imetolewa tu kama "briefing" pasipo kuwa na msisitizo wa kutosha pengine kwasababu mwezi June bado ni mbali kitu ambacho si sahihi.

Ushauri:
Viongozi wa Mamlaka,ikiwa imebaki takribani miezi mitatu kutekeleza zoezi hili,nawashauri muongeze utoaji wa elimu na taarifa kwa umma juu ya zoezi hili na pia mtoe tahadhari kwa umma kuacha kuendelea kununua simu hizi bandia maana bila shaka bado ziko sokoni na huenda nyingine ziko kwenye meli zinakuja.

Cha kufanya:
Mamlaka kwa kushirikiana na makampuni ya simu,mnaweza mkaanda ujumbe mfupi wa maneno(sms) kuhusu zoezi hili ambao kila mtumiaji wa simu atalazimika kuupata ujumbe huo kwanza kabla hajaweza kuongeza salio kwenye simu yake au kabla ya kupata salio la simu yake pale mtumiaji atakapotaka kupata huduma hizo.

Pia,ujumbe huu ambao pia utamuelekeza mteja namna ya kugundua kama simu yake ni bandia au laa,unaweza pia kuja kama ujumbe wa awali pale mteja atakapotaka kutumia huduma za m-pesa,tigo pesa,airtel money,n.k.

Njia nyingine ni kuanzia sasa kutumia vyombo vya habari kueneza ujumbe huu na zaidi kutahadharisha umma kuacha kuendelea kununua simu hizi za bandia na pia ikibidi mshirikiane na Shirika la Viwango Nchini(TBS) kufanya ukaguzi wa kushitukiza katika maduka mbalimbali ya simu na kuchukua hatua kwa watakaokuwa wanaendelea kuuza simu hizi za bandia ila mjue nanyi hapa hamtakwepa lawama kwa kuacha simu hizi ziingizwe nchini.

Sababu za ushauri huu:
Muda uliobaki ni mchache na jambo hili linaonekana kutopewa uzito wa kutosha licha ya athari kubwa za kiuchumi na kijamii zitakazokuja kujitokeza hapo baadae endapo zoezi hili litatekelezwa kwa muda uliopangwa.

Ni wazi simu za bandia zilizoko katika matumizi ni nyingi kuliko simu original lakini ndio hizi hizi zinazotumika katika shughuli za kibiashara,kiuchumi na kijamii.

Kwa mfano,ukisitisha matumizi ya simu bandia,ni wazi utaathiri kwa kiasi kikubwa wale waliojiajiri kwa kufungua vibanda vya m-pesa,tigo pesa, n.k.

Hatari nyingine iwapo umma utakuwa kama umeshitukizwa katika utekelezaji wa zoezi hili,itakuwa ni kupanda kwa ghafla kwa bei za simu original due to sudden increase in demand baada ya simu bandia kuzuiwa.

Kwa mtazamo wangu,hapa patakuwa na athari ya ziada ambapo watu wengi kushindwa kumudu bei za simu original ambazo kwa kawaida huwa ziko juu ukiachilia mbali ongezeko la bei litakolotokana na ongezeka la mahitaji ya bidha hiyo(increase in demand).

Athari nyingine itakayotokana na kupanda kwa bei ni kuwafanya watu wengi washindwe kununua simu hizi kwa uharaka kufidia pengo litakalokuwa limejitokeza na hivyo kuchukua muda mrefu zaidi kwa hali kurejea katika hali ya kawaida.

Mbali na sababu hizo,TCRA kwa kuanza kutoa elimu hii mapema na kuhamasisha umma juu ya zoezi hili ,itakuwa imejivua lawama kwa kutimiza wajibu wake mapema kabisa maana watanzania wengi hungoja dakika za majeruhi kutekeleza wanayopaswa kuyafanya na hili kila mtu ni shahidi na tuna mifano mingi tu kama vile watu kujiandikisha dakika za mwisho kwenye daftari la mpiga kura,n.k.

Ni mtazamo na ni ushauri pia.

Meya wa Jiji Dar es Salaam Atia Kiwewe vigogo

$
0
0
DAHIRA ya Isaya Mwita, Meya wa Jiji la Dar es Salaam kukamata wakwepa kodi na kuwafikisha mahakani inatia kiwewe vigogo wengi, anaandika Happyness Lidwino.
Amesema, amepanga kukamilisha mambo mengi katika kipindi cha miaka mitano kwenye nafasi hiyo lakini donda ndugu la ukwepaji kodi atashughulika nalo kwa kuwa, limeota mizizi ndani ya jiji hilo.

Akizungumza na mtandao huu jana Mwita ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Vijibweni (Chadema) amesema, vigogo wakwepa kodi wanapaswa kujua kuwa “huu ni utawala mpya wenye lengo la kurudisha maendeleo kwa watu wote bila upendeleo.”

Amesema, licha ya jiji hilo kuwa na vyanzo vingi vya mapato bado wananchi wake wanaishi maisha duni kutokana na baadhi ya vigogo wenye biashara nyingi kutolipa kodi ipasavyo.
“Nasubiri tu wiki ijayo niapishwe ili nianze kuwafuatilia wote wenye viporo vya kodi na wanaokwepa.

“Nina mipango mingi ya kimaendeleo lakini yote inahitaji pesa ambazo ni lazima zipatikane kwa njia ya kodi na kuongeza vyanzo vya mapato,” amesema Mwita.
Amesema kwamba, kwa muda mrefu amekuwa akitamani kuwa meya wa jiji ili aweze kuweka wazi uozo wa utawala uliopita.

“Mimi pia ni mmoja kati ya wananchi waliotoka katika familia ya kimaskini, kwa hiyo ninatambua shida za wananchi ambapo nikianza kazi kwa kushirikiana na mameya wa wilaya, zitatatuliwa,’’ amesema.

Changamoto nyingine kubwa katika jiji hilo Mwita anataja kuwa ni uchafu uliokithiri. “Nina mpango wa kujenga dampo kubwa kila wilaya ili kuondoa taka zinazozagaa jijini kwa kusubiri kukusanywa na kupelekwa dampo kubwa la pugu.

“Ninaamini kwa kufanya hivyo suala la taka kuzagaa kila mahali itakuwa ni ndoto,” amesema Mwita.
Hata hivyo ameahidi kutatua kero ya foleni ya magari kwa kujenga maeneo ya maegesho ya magri katika kila wilaya ili kusaidia wafanyakazi huegesha magari yao nyumbai na kwenda katika shuguli zao kwa daladala.

Akizungumzia uhaba wa vyoo vya umma Mwita amesema asilimia kubwa katika sehemu muhimu zinazokaliwa na watu wengi hakuna vyoo vya bure.

“Hii nayo ni kero kwa namna moja ama nyingine kwani vipo vya kulipia tu hakuna vya bure na hata kama vikiwepo havina ubora. Na kuna wengine pia hawana uwezo wa kujilipia huduma hiyo. Hili litakuwa ni jambo la haraka kushuhulikiwa,” amesema Mwita.

Shein Tumbua Majipu Kama Rais Magufuli..Ni Bora Ufe Kwa Kujali Wengine Kuliko Kujinufaisha- Askofu

$
0
0
Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein ametakiwa afuate nyayo na dhana ya utumbuaji majipu ya Rais John Magufuli kwa kuwa imegusa maisha ya wananchi wanyonge.

Wito huo ulitolewa juzi na Askofu mstaafu wa Kanisa la Anglikana, Jimbo la Tabora Francis Ntiruka katika mahubiri ya Ijumaa Kuu katika Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu mjini Dodoma.

Askofu huyo alisema Yesu Kikristo aliteseka hadi kuuawa kwa ajili ya kutetea haki za wanyonge na vivyo hivyo lazima viongozi wawatetee wanyonge.

Alisema kifo chake kiliambatana na vipigo vya mateso ya dhihaka nyingi kutoka kwa watawala waliotaka kujinufaisha wao binafsi pasipo kujali wengine.

“Ni bora ufe kwa ujali wengine kuliko kujinufaisha, alisema askofu huyo ambaye pia ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha St John.

Alimtaka Dk Shein aliyeapishwa juzi kuwa Rais wa Zanzibar ajipange kuhakikisha analeta umoja na amani ya Wazanzibari na kutumbua majipu kama anavyofanya Rais Magufuli.

Alisema Watanzania wana mateso mengi kama ya umaskini, magonjwa, kuporwa haki na rasilimali zao jambo alilosema bila kutafutiwa ufumbuzi, malalamiko yao hayataisha.


Kijana Aliye Fariki Mwaka 2013 Akutwa Akiwa Hai Katika Nyumba ya Mfanyabiashara Mkubwa

$
0
0
Kijana Aliye Fariki Mwaka 2013 Akutwa Akiwa Hai Katika Nyumba ya Mfanyabiashara Mkubwa

Sikiliza Hapa:

Vanessa MDEE Yuko Kipesa Zaidi na Sio Mapenzi!

$
0
0

Kwenye kipindi cha Friday Night Live ambacho kinarushwa na East Africa Television na East Africa Radio, Vanessa ametoa jibu kuwa yeye anapenda pesa zaidi, kuliko mapenzi, na kuibua hisia kuwa huenda hata kwa mwandani wa ambaye pia ni msanii anayefanya poa kwenye bongo Fleva Juma Jux, yupo kipesa zaidi na si Mapenzi.

Mtangazaji wa kipindi hiko alisikika akimuuliza vanessa maswali ambayo alitakiwa kujibu ndani ya sekunde, na ndipo alipotoa jibu hilo kuwa anapenda pesa zaidi.

Sam: Unachukua muda gani kuvaa getting ready?
Vanessa: 30 minutes
Sam: Diamond au pulse?
Vanessa: Diamond
Sam: Hils au sneakers?
Vanessa: Sneakers
Sam:Dresses au trousers?
Vanessa:Trouser
Sam: Icecream au chocolate?
Vanessa:Chocolate
Sam:Nyama au Salad?
Vanessa:Nyama
Sam: Diamond au Alikiba?
Vanessa: Vanessa
Sam: Bags au purses?
Vanessa: Bags
Sam: Ugali au wali?
Vanessa: Ugali
Sam: Mapenzi au pesa?
Vanessa: Pesa

Pia katika maswali hayo Vannesa Mdee alishindwa kuweka wasi ni msanii yupi anamkubali zaidi kati ya Diamond na Alikiba, baada ya kuulizwa kuhusu wao na kuamua kujitaja mwenyewe.

Mwanamuziki Malaika Amefunguka Kuhusu Tetesi za Kuhongwa Gari Aina ya Ranger Rover...

$
0
0
STAA wa Ngoma ya Zogo, Diana Exavery ‘Malaika’ kwa mara ya kwanza amefungukia gari jipya la kifahari analodaiwa kumiliki aina ya Range Rover Sport kuwa hajahongwa kama watu wasemavyo.

Akichonga na Showbiz, Malaika aliyewahi kubamba pia na Ngoma ya Sare Sare na Mwamtumu alisema kuwa katika picha ambayo aliachia kwenye ukurasa wake wa Instagram hivi karibuni ni kweli gari lake na kwamba hajahongwa na mtu.


“Ni kweli lile gari ni la kwangu na nipo katika utaratibu wa kulishughulikia litoke bandarini, sijahongwa na mtu jamani hao wanasema tu ila mimi nimesema nilichosema inatosha,” alisema Malaika.

Baada ya Timu ya Taifa ya Chad Kujitoa AFCON 2017, Haya ndio Maamuzi ya CAF......

$
0
0
Jumatatu ya March 28 timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ilikuwa inajiandaa kushuka dimbani kucheza mchezo wake wa nne wa kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika 2017 dhidi ya Chad, habari zilizotoka March 27 kutoka shirikisho la soka Afrika CAF ni kuwa Chad wamejitoa.

Baada ya Chad kujitoa kwa sababu za kutokuwa vizuri kiuchumi, CAF wamekumbushia sheria iliyowekwa January 15 2015, inaeleza kuwa kundi lolote litakalo salia na timu tatu, halitakuwa na best looser na badala yake kinara wa kundi ndio atakuwa anafuzu michuano hiyo pekee.

Kwa sheria za CAF michezo ya Chad inafutwa na msimamo wa Kundi G unabakia kuongozwa na Misri kwa point 4, Nigeria point 2 na Tanzania kubakia mkiani kwa kuwa na point moja, ikumbukwe kuwa Taifa Stars ilicheza na Chad March 23 N’Djamena na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu Ya March 28, Ikiwemo ya Siri ya Kikwete na IPTL Zafichuka

$
0
0

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu Ya March 28, Ikiwemo ya Siri ya Kikwete na IPTL Zafichuka

Ofisa Elimu Dar es Salaam Amchokoza Wazi wazi Rais Magufuli Sera ya Elimu Bure

$
0
0
Katika kile kinachoonekana kuwa ni kumchokoza waziwazi Rais John Magufuli, Ofisa wa Elimu wa Manispaa ya Kinondoni ametoa agizo la kuwataka wakuu wote wa shule za sekondari kwenye manispaa yake kukata Sh. 1,500 kwa kila mwanafunzi kutoka katika fedha wanazopokea kwa ajili ya uendeshaji wa shule zao na kisha kuzipeleka kwenye manispaa hiyo.

Katika barua ya Februari 4, 2016 iliyosambazwa kwenda kwa walimu wakuu wa shule za sekondari za Kinondoni na Ofisa wa Elimu wa Manispaa hiyo aitwaye Rogers Shemwelekwa, inaelezwa kuwa fedha hizo zinapaswa kutolewa na kila mkuu wa shule ili kugharimia michuano ya sekondari, inayoandaliwa chini ya mwavuli wa Umoja wa Michezo kwa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA). Amri iliwataka wakuu wote wa shule za sekondari Kinondoni zikiwamo pia zinazomilikiwa na taasisi binafsi kuwasilisha michango hiyo ifikapo Februari 28 kupitia akaunti namba 0150259059100, katika benki ya CRDB  kwa jina la KMC Miscellaneous deposit Account na stakabadhi zote zipelekwe kwa Ofisa Elimu wa Sekondari. Michezo hiyo ya UMESSETA inatarajiwa kuanza Mei.

Uchunguzi wa Nipashe umebaini kuwa agizo hilo linakwenda kinyume cha waraka wa serikali kuhusu matumizi ya fedha za ruzuku zinazotolewa kila mwezi kwa ajili ya kufanikisha utoaji wa elimu bure iliyoahidiwa na Rais Magufuli wakati wa kampeni za kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015. 

Kwa mujibu wa waraka wa kufanikisha elimu bure, fedha zilizoguswa kupitia agizo la Ofisa Elimu wa Kinondoni zipo katika fungu la pili ambalo lililotengewa asilimia 30 ya fedha zote za ruzuku kwa lengo la kuziwezesha shule siyo kugharimia michezo peke yake bali pia ukaguzi na vifaa vya kujifunzia.

Tangu Januari mwaka huu, serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli imekuwa ikisambaza fedha za kufanikisha utoaji wa elimu bure kwa kila shule kuanzia msingi hadi kidato cha nne, lengo likiwa ni kuwaondolea wananachi kero ya kukabiliana na rundo la michango kwa visingizio mbalimbali vikiwamo vya michezo, madawati, ulinzi, uji, nembo ya shule, majengo karatasi, maandalizi ya mitihani, umeme, maji na masomo ya ziada marudu kama ‘tuition’. Katika mgawo wa kwanza uliotolewa Januari, serikali iligawa Sh. bilioni 18.77 kwa ajili ya kugharimia elimu bure nchini kote huku Rais Magufuli akionya kuwa ole wake atakayekiuka maelekezo na kubadilisha matumizi ya fedha hizo.

Wakizungumza na Nipashe mwishoni mwa wiki, baadhi ya walimu wakuu wa shule za sekondari katika manispaa ya Kinondoni wamelalamikia hatua hiyo ya kutakiwa walipe Sh. 1,500 kwa kila mwanafunzi kwa madai kuwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume cha agizo la Rais kuhusiana na utoaji wa elimu bure.

Walimu hao, kwa nyakati tofauti walisema kuwa wao hupokea fedha moja kwa moja kutoka Hazina zikiwa zimewekewa maelekezo, lakini wanashangaa kuona Shemwelekwa anawapa maagizo yanayokiuka maelekezo ya Hazina kwa kuwaagiza kwamba wakishazipata, wahakikishe wanazipeleka Manispaa  kwa ajili ya kugharimia michezo, tena kwa kiwango mahsusi cha Sh. 1,500 kwa kila mwanafunzi.

Baadhi ya walimu wakuu walisema ingawa idadi ya wanafunzi kwa kila shule ndiyo kigezo cha kupokea mgawo mkubwa au kidogo, lakini kwa wastani, asilimia 30 ya ruzuku wanayopewa na serikali na ambayo hujumuisha pia shughuli za michezo na ununuaji wa vifaa vya kujifunzia huwa haifiki Sh. 600,000 kwa mwezi.

Mmoja wa walimu alitolea mfano wa shule yenye wanafunzi 1,000, akisema kwamba endapo wakitii agizo la Ofisa Elimu Shemwelekwa, maana yake shule ya aina hiyo inapaswa kulipa Sh. milioni 1.5 kwa ajili ya michezo na kiasi chote kinapaswa kulipwa kwa wakati mmoja.

Mwalimu mwingine aliiambia Nipashe kuwa kwa ujumla, shule moja hupata wastani wa Sh. 1,700,000 kila mwezi kugharimia elimu bure na hivyo, ikiwa fedha hizo zitatolewa kwa wakati mmoja, maana yake uendeshaji wa shule zao utasimama kwa mwezi mmoja kwa sababu kiasi cha fedha kitakachobaki kitakuwa ni kidogo na kamwe hakiwezi kufanikisha utoaji wa elimu pasi na kuhitaji michango kutoka kwa wazazi.

OFISA ELIMU AKIRI, ARUSHA MPIRA
Akizungumza na Nipashe kuhusu barua anayodaiwa kuiandika kwenda kwa walimu wakuu wa manispaa yake kuhusiana na makato ya Sh. 1,500 kwa kila mwanafunzi, Shemwelekwa alianza kwa kukiri kuandika barua hiyo,  lakini akakataa kutoa maelezo zaidi kwa madai kwamba anayepaswa kuulizwa ni mkurugenzi wa manispaa yake.

"Siwezi kuzungumza na wewe. Ukitaka maelezo zaidi nenda kamuulize Mkurugenzi wa Manispaa,'' alisema Shemwelekwa.

Hata hivyo, alipoulizwa, Mkurugenzi wa manispaa hiyo anayetajwa kwa jina la Kagurumjuli Titus, alisema (yeye) hana taarifa ya kuandikwa kwa barua hiyo ambayo Nipashe inayo nakala yake.

Aidha, Mkurugenzi huyo alisema kama walimu wakuu hawakuridhika na barua iliyowataka kukata fedha hizo kwa kila mwanafunzi, wangepaswa kufika kwake ili awaweke meza moja na ofisa huyo wa elimu (Shemwelekwa) na kufikia muafaka badala ya kukimbilia kwenye chombo cha habari. 

Licha ya mkurugenzi kudai kuwa haijui barua hiyo, nakala mojawapo ambayo Nipashe inayo inaonyesha kuwa miongoni mwa waliotumiwa nakala kwa tarifa ni pamoja na yeye (Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni) na pia Ofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam.


20 Watiwa Mbaroni Wakituhumiwa Kumpiga Mawe Ofisa wa JWTZ Aliyemgonga Mtembea Kwa Miguu

$
0
0
Polisi mkoani Ruvuma inawashikilia waendesha bodaboda 20 Manispaa ya Songea wanaodaiwa kumshambulia askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Kikosi cha 411 KJ Ruhuwiko, kwa kupiga mawe gari alilokuwa akiendesha baada ya kumgonga mtembea kwa miguu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Zubeir Mwombeji alisema tukio hilo lilitokea Machi 24 saa 3.00 usiku maeneo ya Shule ya Msingi Mfaranyaki, karibu na Kituo Kikuu cha Polisi Songea Mjini.

Mwombeji alimtaja mwanajeshi huyo aliyejeruhiwa kwa kushambuliwa na waendesha bodaboda kuwa ni Luten Samweli Nginila (32), ambaye amelazwa Hospitali ya Rufani Mkoa.

Alisema Luteni Nginila alijeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili na kupoteza fahamu baada ya kushambuliwa na waendesha bodaboda, ambao walivunja kwa mawe vioo vya gari alilokuwa akiendesha.

Aliendelea kuwa chanzo cha tukio hilo, inadaiwa kutokea ajali maeneo ya majengo ambako askari huyo alikuwa akiendesha gari aina ya Nissan XTRAIL akitokea Bar ya Ramour .

Alisema alipofika eneo la majengo, Bahati Mbero alikatisha ghafla barabarani hivyo askari huyo kushindwa kumudu gari na kusababisha ajali.

Kufuatia hali hiyo, waendesha bodaboda waliokuwa karibu walikusanyika kwa lengo la kumshambulia, hali iliyomlazimu kuwasha gari kukimbia ili kuokoa maisha.

Hata hivyo, bodaboda hao walimkimbiza na alipofika Shule ya Msingi Mfaranyaki tairi la gari lake lilichomoka, hivyo walimzingira na kumshushia kipigo wakiwamo abiria watatu aliokuwa nao.

Mwombeji aliwataja waliokuwamo ndani ya gari hilo kuwa ni Kaumbya Kateka (24) mkazi wa Majengo, Joyce Edson (24) mkazi wa Mpambalyoto na Jackline Mwita (22) mwanafunzi wa Chuo cha Uuguzi Peramiho. Alisema katika vurugu hizo baadhi ya vitu vilipotea ambavyo ni mali ya askari huyo.

Vitu vilivyopotea ni simu mbili za mkononi, pochi ambayo ilikuwa imehifadhi vitambulisho mbalimbali na Sh120,00.

Alisema wanaendelea kuwabaini wengine waliohusika, taratibu za kuwafikisha mahakamani zitafuata.

Chama cha Wananchi (CUF) Kutoa Tamko Zito Kuhusu Hatima yake Kisiasa Zanzibar...Maalim Seif Apunguziwa Ulinzi

$
0
0
Chama cha Wananchi (CUF), kimesema kinajiandaa kutoa tamko zito kuhusu hatima yake kisiasa visiwani Zanzibar.

Kufuatia hatua ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zaniabar (ZEC), Jecha Salum Jecha kufuta Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana, ambao chama hicho kinaamini kuwa kilishinda, CUF iligomea uchaguzi wa marudio wa Jumapili iliyopita.

Tangu hapo, Rais Dk. Ali Mohammed Shein alishaapishwa Alhamisi iliyopita kuongoza visiwa hivyo mpaka mwaka 2020.

CUF inaamini matokeo ya uchaguzi wa mwaka jana yangeonyesha kuwa mgombea wao, Maalim Seif Hamad, ameshinda kwa kishindo.

Aidha, Chama hicho kimesema hakitababaishwa na hatua ya serikali kumwondolea walinzi Maalim Seif  kwasababu chama hicho kina walinzi wa kutosha kufanya kazi hiyo .
Akizungumza na Nipashe jana, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, Magdalane Sakaya, alisema CUF inafanya maandalizi ya vikao vya ngazi za juu ambavyo ndivyo vitakavyotoa maamuzi kuhusu mustakabali wa kisiasa visiwani humo, baada ya uchaguzi wa marudio.

Sakaya ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kaliua mkoani Tabora kwa tiketi ya CUF, alisema ingawa shughuli za chama zinaendelea kama kawaida, vikao hivyo ambavyo ni Kamati Tendaji na Baraza Kuu vitakaa ndani ya muda mfupi ujao na vitajadili na kutoa msimamo wa chama kuhusu hatma ya Zanzibar.

“Tunaendelea na maandalizi ya vikao hivyo na wiki ijayo vitakaa na kutoa mwelekeo wa nini kinaendelea na nini msimamo wa chama kuhusu siasa za Zanzibar, lakini tunaendelea kuamini kuwa mgombea wetu ndiye chaguo sahihi la Wazanzibari katika uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka jana,” alisema Sakaya.

Aidha, Sakaya alisema CCM ilishapanga siku nyingi za kuhakikisha wanashinda kwa hila kwenye uchaguzi huo ili wabadili Katiba ya Zanzibar inayozungumzia Serikali ya Umoja wa Kitaifa na hatimaye waunde serikali peke yao ambayo haitakuwa na vyama vya upinzani.

Kuhusu taarifa za Maalim Seif kupunguziwa walinzi, Sakaya alisema CUF haiwezi kubababishwa na hilo kwasababu chama chao kina walinzi wa kutosha ambao watamlinda wakati wote na aliongeza kuwa hatua ya CCM kulazimisha kumwapisha Dk. Shein ni udikteta wa kupindukia.

Alielezea kushangazwa na idadi kubwa ya askari polisi na wa JWTZ wakati wa uchaguzi wa marudio, hali ambayo iliwatisha wananchi na wengine kuogopa kwenda kwenye shughuli zao za kila siku.

“Baadhi ya wanachama wa CUF bado wako mahabusu hadi leo na wanasheria wetu wanaendelea na mchakato wa kuwatoa maana hawana kesi," alisema Sakaya.

"Wengi walipigwa na kuteswa na kubambikiwa kesi kwasababu za kisiasa na kwa kuwa wameshatimiza kile walichokuwa wanakitaka tunaamini watawaachia.”
Mwenyekiti wa ZEC Jecha alimtangaza Dk. Ali Mohammed Shein kuwa Rais wa Zanzibar Jumatatu kwa kupata asilimia 91.4 ya kura halali.

Kwa mujibu wa Jecha, Shein alipata kura 299,982 kati ya jumla ya wapiga kura waliojitokeza 341, 865. Jumla ya Wazanzibari wlaiojiandikisha walikuwa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana ambao ulifuntwa na Jecha walikuwa 503,580.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na mgombea urais wa ADC, Hamad Rashid aliyepata kura 6,734 na Maalim Seif Sharif Hamad (CUF) alishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 6,076.

Ushindi wa Dk. Shein wa asilimia 91.4 una maana vyama vingine saba vilivyoshiriki vilikosa asimilia 10, ambazo kisheria zingeliweza kukifanya kuingia kwenye serikali ya umoja wa kitaifa.

Jecha aliufuta uchaguzi wa Oktoba 25 kwa madai ya kuwepo kasoro kubwa, hatua ambayo ilipingwa vikali na CUF, ambacho aliyekuwa mgombea wake wa urais, Maalim Seif Sharif Hamad, alisema alikuwa ameshinda kwa zaidi ya 52%.

Bado haijafahamika ikiwa Dk. Shein ataunda serikali nyengine yenye muundo wa umoja wa kitaifa, kwasababu  mbali na chama chake, hakuna chama kingine kilichotangazwa na ZEC kufikia asilimia 10 ya kura za jumla wala kupata wajumbe kwenye baraza la wawakilishi, masharti muhimu kwa chama kujumuishwa kwenye uundaji wa serikali kwa mujibu wa katiba ya visiwa hivyo.

Trump Afunguka: Sera yangu Kimataifa ni 'Marekani Kwanza' Hatuta Punjwa Tena...

$
0
0
Mgombea urais kwa niaba ya chama cha Republican, Trump ambaye anaongoza hivi sasa katika kinyang'anyiro hicho, amesema siasa zake za mambo ya nje, zitaweka maslahi ya Marekani mbele.

Katika mahojiano na gazeti la New York Times amesema nia yake sio kwamba anataka kuitenga Marekani ila anasema anapanga kusitisha kupunjwa kwa Marekani na washirika wake.

Amesema anataka Marekani iache kuendelea kununua mafuta yake kutoka Saudia hadi pale waSaudi watakapokubali kupeleka majeshi yao kupigana na wanamgambo wa IS.


Aidha Trump ameongeza kusema kuwa endapo ataibuka mshindi wa uchaguzi wa urais wa Marekani, atayaondoa majeshi ya Marekani kutoka Japan na Korea Kusini kama mataifa hayo hayatailipa zaidi Marekani kwa wanajeshi hao kuendelea weko nchini humo.

Sharobaro Amlipia Mahari Mwigizaji Riyama....Mwenyewe Asema Wanaendana Kinafsi...

$
0
0
Hatimaye! Taarifa ikufikie kwamba, staa wa kitambo wa Bongo Muvi, Riyama Ally amelipiwa mahari na mpenzi wake ‘sharobaro’ ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, Haji  Mwalimu ‘Leo Mysterio’ huku mipango kabambe ya ndoa ikiendelea.

Riyama ameliambia Wikienda kuwa, anamshukuru Mungu kumpata mtu anayeona ndiye anamfaa katika maisha yake na tayari sasa ni mchumba rasmi wa mtu, tena kijana anayempenda kwa dhati.

“Sasa hapa ndiyo nimefika kwa kuwa nimekutana na mtu mwenye mapenzi ya kweli kwangu. Pia nafsi zetu zimeendana, hapa namuomba Mungu anyooshe mambo yaende kama vile tulivyopanga,” alisema Riyama ambaye amekuwa ‘singo’ kwa muda mrefu.

Kwa upande wake, Mysterio alisema kuwa anaamini safari yake ya muda mrefu imefika kwa kuwa amempata mwanamke anayempenda kutoka ndani ya uvungu wa moyo wake na kwa upande wake taratibu zote za uchumba amemaliza, anasubiri ndoa watakayofunga hivi karibuni.

Tazama Hapa Picha Alizoweka Zari Hassan Zikionyesha Jinsi Wanavyoenjoy na Diamond Katika Tour yao Inayosemakana Wametumia Million 100

$
0
0
A Tanzanian site recently revealed that Diamond Platnumz’ tour to Europe specifically Germany, Norway, Sweden, Belgium, Finland and Denmark would cost him a whopping 100 Million!

The Bongo superstar took his family including his mum Sanura Kassim, daughter Tiffah and baby mama Zari along with him for his tour. Zari has been sharing some sights and sounds from their Europe tour. But perhaps the most touching, heartwarming and even envy-inducing were these adorable photos of her family that were taken in Sweden.


Boko Haram Wailiza NIGERIA Tena...Wateka Nyara Wanawake 16

$
0
0

Wapiganaji wa Kundi la Boko Haram wamewateka nyara wanawake 16 katika eneo la mashambani, Kaskazini Mashariki mwa Jimbo la Adamawa.


Vyanzo vya habari vilisema wanawake hao walitekwa msituni, walipokuwa wakitafuta kuni na wengine walikuwa wakivua samaki kando ya mto.


Wanawake hao hadi sasa hawafahamiki mahali walipohifadhiwa na watekaji.


Kundi hilo lililoenea nchini humo, limekuwa likijihusisha na vitendo vya utekaji wa mara kwa mara. Awali, liliwateka wasichana ambao ni wanafunzi zaidi ya 200 ambao mpaka sasa hawajapatikana.


Wakati huohuo, Jeshi la Nigeria limewakomboa zaidi ya watu 800, waliokuwa wakishikiliwa na kundi hilo katika vijiji kadhaa, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.


Mateka wengine walikombolewa katika Jimbo la Borno, huku 520 wakikombolewa katika Kijiji cha Kisuma, baada ya mapambano kati ya wanajeshi hao na wapiganaji wa kundi hilo, mateka wengine 309 waliokolewa katika vijiji vingine 11 vinavyodhibitiwa na kundi hilo.


Rais wa nchi hiyo, Muhammadu Buhari alipokuwa anaingia madarakani alisema atahakikisha anapambana na kundi hilo

Makonda Aingilia kati Vurugu za makanisani.....Asema Muumini Atakayekimbilia Polisi Kulishitaki Kanisa Atamuweka Rumande

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema mkoa wake hauko salama kama watu wanavyodhani kwa sababu silaha nyingi zinamilikiwa kiholela na mafunzo ya matumizi ya silaha hizo hutolewa hata kwa watoto.


Makonda alisema hayo jana wakati wa ibada ya Pasaka iliyofanyika katika Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano na kuwataka wakazi wa Dar es Salaam kujitokeza kuhakiki silaha zao na kusalimisha zile zinazomilikiwa kinyume cha sheria.


Alisisitiza kwamba ifikapo Julai Mosi, operesheni maalumu ya kukamata silaha zinazomilikiwa kinyume cha sheria itaanza na yeye mwenyewe ndiye atakayeiongoza.


“Tumegundua kwamba kwenye bonde la mto unaotenganisha Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani, kuna mafunzo yanatolewa kwa watoto. Wazazi wanadhani watoto wao wamekwenda shule  kumbe wamechukuliwa huko.Hatuwezi kukubali hali hiyo iendelee."Alisema


Mkuu huyo wa mkoa aliwataka waumini waendelee kumuombea ili afanye kazi yake vizuri kwa kutenda  haki pia aliwataka pia wamwombee Rais Magufuli  kwa sababu kazi anayoifanya ni kubwa.


Alisema Rais anapotumbua jipu moja,ndani yake kuna kundi la watu wanaoathirika na hatua aliyoichukua hivyo, alisema watu wa aina hiyo hawawezi kumpenda kwa sababu amevunja mtandao wa masilahi yao.


“Ninaomba kanisa pamoja na viongozi wote wa dini mnisaidie katika kuhimiza suala la ulinzi na usalama ili amani yetu iendelee kudumu. Ninaomba tushirikiane katika hilo, Dar es Salaam haiko salama kama mnavyodhani, mengine siwezi kusema kwa sababu sijaruhusiwa na Rais,”alisema. 


Migogoro kanisani 

Akizungumzia migogoro makanisani, Makonda alisema hataki kusikia kiongozi yeyote wa dini anakimbilia polisi au mahakamani kutaka suluhisho la matatizo yao ya ndani na kuwa atamweka ndani atakayejaribu kufanya hivyo.


Alisema ni aibu kubwa kwa kanisa kukimbilia kwenye vyombo vya dola badala ya polisi na Serikali kukimbilia kanisani kuomba ushauri. Alisema kanisa ndicho chombo cha usuluhishi wa matatizo mbalimbali ya jamii.


“Serikali inahitaji msaada wa kanisa na viongozi wa dini ili iweze kufanya kazi vizuri. Sitaki kusikia polisi wanakwenda kanisani (kukamata watu) katika mkoa wangu na wale wanaotoa taarifa kutaka polisi nitawaweka ndani,” alisema Makonda ambaye kabla ya kuwa mkuu wa mkoa, alikuwa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.


 Askofu Mokiwa 

Awali, Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Dar es Salaam, Valentino Mokiwa alibainisha mambo mbalimbali aliyoyaita majipu ambayo yanafanya kanisa hilo lisiendelee katika kufundisha waumini wake yaliyo mema.


Mokiwa alitaja mambo hayo kuwa ni pamoja na mashindano ya kimadhehebu. Alisema madhehebu mbalimbali yanashindanishwa kupima kanisa lipi ni kubwa, lina waumini wangapi, linamilikiwa na nani na nguvu yake ni ipi.


Jambo jingine alisema ni maaskofu wenyewe kupigana vita. Alisema sasa ni kawaida kwa askofu mmoja kumchimba mwingine, askofu mmoja kupanga mapinduzi dhidi ya mwingine na baadhi ya maaskofu kutukanana waziwazi.

Babu Tale: Niko Tayari Kumsaidia Msanii yeyote Anayetaka Kuacha Madawa ya Kulevya

$
0
0
Meneja wa Diamond Babu Tale katamka kuwa yuko Tayari kumsaidia msanii yeyote yule ambaye yuko tayari kuacha madawa ya kulevya, kasema milango iko wazi kama ambavyo kamsaidia Chid Benzi ambaye kapelekwa sober House Bagamoyo.

Pamoja na hayo kadai haikuwa kazi rahisi kwa Chid Benzi maana pamoja na kumpeleka sober bado alikua "akistua" njiani, njia nzima alikua akivuta hii midude.

Mungu ambariki sana huyu jamaa

Baada ya Kuachwa na Mbunge na Kulazwa..Yasemekana Wastara Juma Atoroshwa Hospitalini

$
0
0
Taarifa mbaya! Staa wa Bongo Muvi, Wastara Juma ambaye mapema wiki iliyopita alidai kupewa talaka la mumewe, Sadifa Khamis Juma, Mbunge wa Donge, Zanzibar, anadaiwa kutoroshwa hospitalini kisha kupelekwa hoteli ya mafichoni huku akiendelea na matibabu.

Kwa mujibu wa chanzo makini, Wastara aliyekuwa amelazwa kwenye Hospitali ya Misheni ya St. Herry Health Center iliyopo mjini hapa, aliondolewa wodini hapa usiku mnene huku akiwa bado hali yake ya kiafya haijatengamaa tangu alipolazwa mapema wiki iliyopita akisumbuliwa na presha na kisukari na baadaye kupoteza fahamu.

Wikienda lilifika hospitalini hapo Jumamosi iliyopita na kuthibitishiwa kuondolewa kwa msanii huyo na mtu aliyedai kuwa ni babu yake aliyetajwa kwa jina la Abdulaziz Babu.
Kwa mujibu wa mmoja wa wahudumu waliokuwa zamu walioomba hifadhi ya majina, jamaa huyo alidai kuwa Wastara aruhusiwe kwani alihofia usalama wake na kwamba sehemu aliyopanga kumpeleka ni salama zaidi.

Baada ya kunusa ‘ubuyu’ huo hospitalini hapo, Wikienda lilimsaka Wastara kujua mahali alipo na hali yake lakini jitihada hizo ziligonga mwamba kwa kuwa namba yake ya simu haikuwa hewani.

Alipotafutwa mtu huyo anayedai ni babu wa Wastara alifunguka: “Ni kweli nimemuondoa Wastara hapo hospitalini kwa sababu za kiusalama. Yupo hotelini lakini siwezi kukuelekeza ni sehemu gani kwa sababu ukiandika itajulikana na tatizo litakuwa palepale.”

Wastara alikumbwa na hali hiyo ikidaiwa ilitokana na mgogoro wa ndoa yake na Sadifa iliyofungwa hivi karibuni na kushindwa kudumu.

Harmonize Atoboa Siri 'Ni Kweli Zari Hassan Ndio Aliniunganisha na Huddah Baada ya Kumtamani Kwa Muda Mrefu'

$
0
0
Siri nje! Staa kutoka Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) anayejipenyeza kwa kasi kwenye Bongo Fleva, Rajab Abdulhan ‘Harmonize’ amekiri kuwa shemeji yake kwa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz;, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’,ndiye aliyemuunganisha na demu mkali kutoka Nairobi nchini Kenya, Huddah Monroe ‘The Boss Chick’.

Akizungumza ndani ya Makao Makuu ya ofisi za gazeti hili, Bamaga- Mwenge jijini Dar, wikiendi iliyopita, Harmonize alisema kuwa kwenye maisha yake hakuwahi kuwa na ndoto ya kukutana laivu na Huddah lakini bahati hiyo aliipata akiwa nchini Afrika Kusini baada ya kukutanishwa naye na Zari.

“Katika maisha yangu nilikuwa namuona tu Huddah na kumtamani ila namshukuru shemeji yangu Zari aliyenikutanisha na Huddah na kutuunganisha kuwa marafiki ambao tumekuwa tukiwasiliana utadhani tulifahamiana zaidi ya miaka hata mitano huko nyuma,” alisema Harmonize akihojiwa na Global TV Online.

SOMA Mtazamo wa Mchambuzi Shaffih Dauda Baada ya Chad Kujitoa Kuwania Kufuzu Fainali za AFCON 2017

$
0
0
Baada ya timu ya taifa ya Chad kujitoa kwenye mashindano ya kuwania tiketi ya kushiriki fainali za AFCON mwaka 2017, watu wengi wamekuwa na maoni tofauti hususan nafasi ya Tanzania kufuzu kwa fainali hizo ambazo zitafanyika nchini Gabon.

Mchambuzi wa masuala ya michezo Shaffif Dauda kutoka Clouds Media Group yeye ametoa maoni yake juu ya kujitoa kwa Chad huku akieleza athari itakayozipata timu ambazo zilikuwa kundi moja na Chad kutokana na timu hiyo kujitoa kwenye mashindano pamoja na nafasi ya Tanzania kufuzu kwenye mahindano hayo makubwa barani Afrika kwa ngazi ya timu za taifa.

Athari kwa timu za kundi G baada ya Chad kujitoa

“Athari ya kwanza kwa Chad kujitoa ni kwa timu zote ambazo zilikuwa kundi moja na Chad kwa maana ya Tanzania, Misri na Nigeria. Kwenye kundi hili, timu tatu ndizo ambazo zilionekana zinapigania nafasi yna kufuzu kwa fainali za AFCON zitakazofanyika Gabon, walitegemea Chad awe kama ‘punching bag’ kwa timu zote ili zijekuviziana zenyewe kwa zenyewe”.

“Ukiangalia hili ili kuthibitisha kauli yangu, Tanzania tayari alishampiga Chad nyumani kwao na kuchukua pointi tatu, Nigeria alishachukua poini tatu nyumbani kwa Chad na Misri tayari naye alishampiga Chad na kuchukua pointi tatu”.

“Sasa kinachotokea ni kwamba, kujiondoa kwa Chad kwenye mashindano haya kunaathiri timu zote kwa maana ya pointi zote ambazo timu tatu zilishazivuna mbele ya Chad zinafutika na michezo mingine ambayo ilikuwa inafuatia inafutika”.

“Kwahiyo kwenye msimamo wanaangalia matokeo ya timu tatu zinazobaki kwenye mashindano kwa maana hiyo, Tanzania badala ya kuwa na pointi 4 itabaki na pointi yake 1 na zile pointi 3 ambazo zilikuwa zinahesabiwa zinafutwa, kwa maana kama Tanzania ingeshinda dhidi ya Chad kwenye mchezo wake wa marudiano ingeendelea kutengeneza mazingira chanya ya kufuzu kwenye mashindano yajayo ya AFCON yanakuwa yamepotea”.

Nafasi ya Tanzania kufuzu kwenye fainali za AFCON 2017

“Kilichobaki kwa sasa ni kuona kwa namna gani Tanzania katika mechi mbili zilizosalia dhidi ya Misri na Nigeria wataweza kujitutumua na kufikisha idadi ya pointi ambazo timu hizo zitashindwa kuzifikisha ili Tanzania iweze kufuzu ikiwa kinara wa kundi G”.

“Kwa harakaharaka ukiangalia baada ya kuyafuta matokeo ya Chad, anayenufaika ni Misri ambaye anabaki na pointi nne ambazo alizipata dhidi Tanzania na Nigeria. Kwahiyo mechi inayokuja kati ya Misri dhidi ya Nigeria, kama Misri itashinda mchezo wake moja kwa moja inakuwa imekata tiketi ya kufuzu kwa fainali zijazo kwa kufikisha pointi 7 na kutengeneza mazingira mazuri”.

Nafasi ya best loser kutoka kundi G

“Nashindwa kulizungumzia hili moja kwa moja kwasababu sijajua CAF watafanyaje, ni vigumu kumpata best loser kwenye kundi hili kwasababu kupata best loser wanaangalia timu ya pili iliyofanya vizuri kwenye kundi lenye timu nne.

“Lakini kama hili kundi lingekuwa na timu tatu toka mwanzoni wakati makundi yanapangwa, kundi ambalo huwa lina timu tatu mara zote halihusishwi kwenye mchakato wa kumpata best loser”.
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images