Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104808 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli: Ningejua Kama Urais Ndio Hivi, Nisingegombea

$
0
0
Wakati Muheshimiwa JPM akiwa mapumzikoni kule Chato aliwasiliana na Kardinal Pengo kwa njia ya simu, muheshimiwa JPM inaonekana alifunguka mambo mengi sana ambayo Pengo ameyaminya, ila kubwa alilomueleza ni kuwa kama angejua kazi ya Urais ilivyo ngumu hivi, wala asingethubutu kugombea.

Kardinali Pengo aliishia kumtuliza kwa kumwambia kuwa ni afadhali mtu mmoja afe lakini taifa lisiteketee.

Swali ni, kuna nini kinaendelea nyuma ya pazia huko Magogoni??
Nini maana ya maneno "ni afadhali mtu mmoja afe kuliko taifa kuteketea"?

Diva Ajibu Tuhuma za Jokate na Lulu Kuwatukana Instagram Kupitia Akaunti Feki (Video)

$
0
0
Kuna wakati Jokate na Lulu waliwahi kumshutumu Diva kuwa amekuwa akifungua akaunti zingine za Instagram na kuwatukana.

Diva amezungumza na Bongo5 kujibu tuhuma hizo na kusema mambo makubwa ikiwa ni pamoja na kumuita Jokate ‘feki.’ Amesema ugomvi wao umetokana na Alikiba ambapo Jokate alikuwa akihisi Diva anatembea na mpenzi wako huyo. Anadai yote hayo ni kutokana na wivu alionao Jokate kwa Alikiba.

Anadai marafiki zake na Jokate walikuwa wakimshambulia kwenye Instagram wakimshutumu kuwa anatembea na Alikiba kitu anachosema si kweli na kwamba akitaka kutembea na muimbaji huyo wa ‘Nagharamia’ ni dakika moja tu lakini hawezi kufanya hivyo.

Pia amezungumza kuhusu Lulu kumwandikia tweet kuwa amekuwa akimtukana hivyo hivyo kwa akaunti feki za Instagram.

Mtazame zaidi hapo:

Chanzo:Bongo5

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Tanesco, William Mhando Aachiwa Huru Baada ya Mahakama Kukosa Ushahidi wa Kumfunga Jela

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo imewaachia huru aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), William Mhando na mkewe Eva Mhando .

Mhando na wenzake walikuwa wanashitakiwa kwa makosa sita likiwemo la matumizi mabaya ya ofisi, kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Mhando alikuwa anatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka kwa kuipa zabuni Kampuni ya Santa Clara Supplies Ltd huku akijua ana maslahi nayo na kwamba anaimiliki yeye, mke na watoto wake.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Hellen Riwa kwa niaba ya Hakimu mwenye kesi hiyo Kwei Lusema amesema  upande wa mashtaka umeshindwa kuthibisha juu ya matumizi mabaya ya ofisi kwani Mhando alikuwa haingii kwenye vikao vya maamuzi ya bodi ya Tanesco kwa hiyo alikuwa hana ushawishi wa moja kwa moja kushawishi kampuni  ya Santa Clara ambayo ni ya mke wake ipatiwe tenda

Imebainika Watumishi Hewa Mwanza Walikuwa Wakikopa Hadi Pesa Bank....Takururu Wafunguka Makubwa

$
0
0
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Mwanza, imebaini kuwepo kwa watumishi hewa zaidi ya watano ambao uongozi wa mkoa huo haukuyawasilisha majina yao kwa Rais Dk. John Magufuli huku yakionekana kukopa fedha benki.

Pia Takukuru imesema kuwa majina ya watumishi hewa hao baada ya kufanya uchunguzi wamebaini hukopeshwa fedha kwa kisingizio kwamba wao ni watumishi wa Serikali kitendo ambacho ni cha uongo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mwanza, Ernest Makale wakati akitoa taarifa ya robo mwaka kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu, ambako alisema  majina yaliowasilishwa kwa Mkuu wa Mkoa huo, John Mongella sio kamilifu.

Amesema watumishi hao hewa wamekuwa wakikopa fedha kutoka benki mbalimbali kwa kutumia nyaraka za kughushi jambo ambalo alidai kwamba kuna baadhi ya watumishi wasio waaminifu wanaohusika kufanya udanganyifu huo.

Amesema pia katika uchunguzi wao unaonesha kuwa majina ya watumishi yaliowasilishwa na baadhi ya halmashauri za mkoa huo sio kamilifu kwani kuna watumishi wengine ambao hawajaorodheshwa.

Makale amesema kuwa kutokana na kuonekana kwa hali hiyo Takukuru inaendelea kufanya uchunguzi wa kina kuwabaini watumishi hewa wengine na watumishi wengine wanaoshirikiana nao.

“Kuna dalili za wazi ambazo zinaonesha kuna watumishi wasiokuwa waaminifu wa halmashauli ambao wanahusika kufanya vitendo hivi vya udanganyifu, atakaebainika atafikishwa mahakamani,” amesema Makale.

Watumishi wadakwa kwa utapeli
Makale pia amesema kuwa Takukuru Mkoa wa Mwanza katika kipindi cha miezi hiyo tayari imewakamata aliyekuwa Meya wa Ilemela, Henry Matata, Justine Lukaza (Mhandisi wa Manispaa ya Ilemela) na Mfanyabiashara, Hemed Hamad kwa kosa la kutoa zabuni feki ya kutoza ushuru kwenye stendi ya mabasi ya Buzuruga jijini hapa.

Watumishi wengine waliokamatwa kwa makosa ya kutumia vibaya madaraka yao ni pamoja na aliyekuwa Mganga wa Wilaya ya Magu, Patrick Mwindunga, Afisa Ugavi wa Wilaya ya Misungwi, Zabron Marwa, anaetuhumiwa kuingia manunuzi feki.

Wengine ni wauguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Misungwi, Masalu Kangalukwi na Amon Shija wanaotuhumiwa kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa wagonjwa.

TAMISEMI yaongoza kwa Rushwa
Katika taarifa hiyo, Mhandisi Makale amebainisha kuwa Takukuru imepokea jumla ya malalamiko 45 yanayohusiana na vitendo vya rushwa kutoka kwa wananchi ambapo katika malalamiko hayo, 27 yameelekezwa kwa watumishi wa idara za Serikali za Mitaa (TAMISEMI) hiyo ikiwa ni sawa na asilimia 60. Kati ya malalamiko hayo 27, malalamiko 13 yameelekezwa katika idara ya ardhi.

Amesema idara zinazofuata kwa kulalamikiwa ni Mahakama yenye malalamiko tisa, polisi malalamiko sita na idara ya afya malalamiko matatu.

Mhandisi Makale amesema kesi 33 zinaendelea Mahakamani kutokana na vitendo vya rushwa Mkoani Mwanza huku kesi sita zikiwa ni mpya katika kipindi cha miezi mitatu na nyingine zikiwa katika upelelezi.

Jeshi la Polisi Latoa Tamko Kuhusu Matapeli Wanaodanganya na Kujipatia Pesa Kwa Kujifanya ni Waajiri wa Makampuni

$
0
0
Katika siku za hivi karibuni katika maeneo mbalimbali hapa nchini, kumejitokeza makundi ya watu ama mtu binafsi kutumia mwamvuri wa taasisi fulani kujipatia kipato kwa njia za udanganyifu (utapeli) kwa kuwaahidi vijana kwamba watawapatia ajira katika taasisi hizo.

Makundi haya ya kihalifu imebainika kwamba yapo katika maeneo mbalimbali, hivyo, ni suala ambalo linahitaji ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi ili kukomesha vitendo hivyo.

Juhudi za makusudi zinaendelea kufanyika na jeshi la polisi ili kuwatia mbaroni watu wote wanaojihusisha na vitendo hivyo vya kitapeli.

Aidha, kufuatia kuibuka kwa vitendo hivyo, tayari Jeshi la Polisi limewakamata matapeli wawili wakiwa wamekusanya vijana katika mikoa ya Kilimanjaro na Mbeya, uchunguzi dhidi yao unaendelea na pindi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabiri.

Jeshi la Polisi likishirikiana na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama, kimsingi, kazi yetu kubwa ni kuhakikisha Tanzania inakuwa na Ulinzi na Usalama imara.

Tutaendelea  kupambana na makundi haya ya kihalifu na utapeli ili nchi yetu iendelee kuwa salama.

Tunawasihi wananchi kufuatilia taarifa kwenye vyanzo sahihi juu ya jambo lolote wanalotaka kulifanya ili kuepuka utapeli unaoweza kufanywa na baadhi ya watu kwa lengo la kujipatia vipato.

Aidha, wananchi watoe taarifa kwenye vyombo vya usalama kuhusu tabia na mienendo yoyote wanayoitilia mashaka.

Jeshi la Polisi na vyombo vingine vyote  vya Ulinzi na Usalama viko imara, makundi ya kiuhalifu na wahalifu wote wajue hawana pa kukimbilia, watakamatwa.

Imetolewa na:
Advera John Bulimba – SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Makao Makuu ya Polisi.

Mwenendo wa Jengo la Machinga Complex umesababisha Waziri wa Magufuli kutoa maamuzi haya

$
0
0
April 14 2016 yamefanyika maadhimisho ya Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania ambapo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simbachawene amepata fursa ya kuzungumza na akatoa tamko la kuifuta na kutoitambua bodi inayosimamia jengo la machinga complex lililopo Ilala, Dar es salaam ambalo imedaiwa lilijengwa kwa ajili ya matumizi ya wafanyabiashara wadogo lakini limeonekana kutumika tofauti na kusudio hilo.

Waziri Simbachawene amelikabidhi Jengo hilo kwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kwa ajili ya kuandaa mpango wa kuwaingiza wafanyabishara bila masharti huku ukiangaliwa utaratibu mpya kwa wafanyabiashara hao pia amewataka watumishi wa jengo hilo kuondoka mara moja na kutafuta kazi nyingnine.

Aidha Waziri Simbachawene ameziagiza halmashauri zote nchini kutotoa vibali vya leseni za biashara kwa wafanyabiashara wa kigeni hadi tamko litoke Wizarani kwake. Lengo likiwa ni kuongeza nafasi kwa wafanyabiashara wa nyumbani.

Vigogo CHADEMA Ndani ya Kashfa Nzito ya Kudai Rushwa Ubunge Viti Maalum...

$
0
0
VIGOGO wa juu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wameingizwa ndani ya kashfa ya kutumia madaraka na ofisi za chama hicho vibaya. RAI lina taarifa kamili.

Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu na mmoja wa wakurugenzi wa chama hicho anayeshughulikia masuala ya Bunge (jina tunalihifadhi), wanadaiwa kuomba rushwa kwa baadhi ya makada wa chama hicho ili wawasaidie kupata nafasi ya ubunge wa jimbo na ile ya viti maalumu wakati na hata baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Tayari tuhuma hizo zimeshawasilishwa kwenye Kamati Kuu ya chama hicho na inayotarajiwa kukutana wakati wowote kuanzia sasa.

Mwalimu anatajwa kufanya hivyo katika kipindi alichokuwa akikaimu nafasi ya Ukatibu Mkuu, ambapo anadaiwa kuwaomba rushwa baadhi ya makada wao waliokuwa wakitaka ridhaa ya chama ya kuwania ubunge.

Wakati Mwalimu akipewa tuhuma hizo, mwenzake anadaiwa kuwaomba rushwa baadhi ya makada wa kike wa chama hicho ili awasaidie kupata nafasi ya ubunge wa viti maalumu.

Taarifa kutoka kwa baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu waliokutana Machi mwaka huu, jiji Dar es Salaam kabla ya kwenda jijini Mwanza kwenye kikao cha Baraza Kuu, zililiambia RAI kwamba Mwalimu anadaiwa kufanya hivyo kwa nia ya kujinufaisha.

Tuhuma hizo zilifikishwa mbele ya Kamati Kuu ya Chadema na Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.

Ilidaiwa kuwa Mwalimu aliomba kiasi cha Sh. Milioni 10 kwa Mbunge wa jimbo la Ndanda, Cesil Mwambe.

RAI lilimtafuta Mwambe kuzungumzia suala hili, hata hivyo hakukubali wala kukataa, lakini zipo taarifa zisizo na shaka zinazothibitisha mbunge huyo kuwasilisha madai yake kwa maandishi ikiwa ni sehemu ya kiambatanisho kwenye madai ya Mbilinyi.

Kiambatanisho hicho cha ushahidi kinaonyesha namna ambavyo Mwalimu, alitoa maelekezo ya kuwazuia viongozi wa Chadema kumnyima ushirikiano Mwambe, kutokana na kukaidi ombi lake.

Mbilinyi alipoulizwa na gazeti hili kuhusu malalamiko aliyopeleka kwenye Kamati Kuu, alikiri kufanya hivyo na kusema kuwa kazi hiyo ameiachia kamati hiyo kuwachukulia hatua zinazostahili viongozi hao kwa mujibu wa taratibu na katiba ya chama hicho.

“Taarifa nimeshafikisha hivyo kama hadi sasa umeona kimya ujue kabisa siku viongozi wakiamua kutoa uamuzi wa jambo hilo naamini hata ninyi (waandishi) mtajua,” alisema Mbilinyi.

Kwa upande wake Mwalimu alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa sababu kama litakuwa mikononi mwa Kamati Kuu ni wazi hana mamlaka ya kulitolea ufafanuzi.

“Siwezi kutolea ufafanuzi taarifa ambazo mnasema zimeshafika kwenye Kamati Kuu, kwa sababu Mwenyekiti ndiye mwenye mamlaka wa kuzungumzia jambo hilo. Hata hivyo siamini kama kweli nimemuomba Mwambe hizo fedha,” alisema Mbilinyi.

RAI liliwasiliana na Mkurugenzi aliyehusihwa katika tuhuma hizo bila mafanikio, mara zote alizokuwa akipigiwa simu alikuwa akiikata na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi, hakujibu.

Alipotafutwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ili kuzungumzia madai hayo, nae hakuweza kupatikana si ofisini kwake wala kwenye simu.

Chanzo: Rai

VIDEO: Uhuru Attacks Raila for Embarrasing Him in International Media

$
0
0
President Uhuru Kenyatta has sharply criticised CORD leader Raila Odinga for supposedly tainting his image and that of his Deputy William Ruto in international media.

Speaking in Nyandarua, Kenyatta attacked Odinga following his remarks on France24 and AFP where he commented that failure by the International Criminal Court (ICC) to try top Kenyan leaders for crimes against humanity spelt "doom" on global efforts in fighting impunity.

The President condemned the former Prime Minister for telling the international community that the ICC suspects, who included Uhuru, 'should have been arrested'.

“Lakini yako ni kwenda kuharibu jina yetu huko nje na mambo haina [sic] Your business is to drag our names in the mud while abroad, speaking about things that do not add up,” Kenyatta indicated.

An enraged Kenyatta firmly told off the Opposition leader highlighting that dirty and abusive politics would not take Kenya anywhere.

He further urged Odinga to be satisfied with the ruling and come back and develop the country with the Jubilee Government.

“The ICC declared that we have no case to answer. Who are you to start questioning that?” Kenyatta questioned.

The Head of State expressed that instead of the Opposition leader trying to scheme his way into power and wishing others evil, he should present his policies and vision to Kenyans in order to be elected.

“It is God who gives people authority and one does not need to falsely accuse others to ascend to power. When I tried and failed the first time in 2002, I accepted defeat and waited and by God’s grace I am now leading the nation." Kenyatta said.

DP Ruto who was also in the meeting critised the former Primier stating: “There is no greater impunity than that by those who plan to jail innocent people for political reasons".

Meno ya Rais Magufuli Yang'ata Tena..Atengua Uteuzi wa Kigogo Huyu wa Magazeti ya Serikali

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Bw. Gabriel Nderumaki.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 14 Aprili, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi, imeeleza kuwa Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kuanzia tarehe 18 Machi, 2016.

Kufuatia kutenguliwa kwa uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua Bi. Tuma Abdallah kukaimu
nafasi hiyo.

Bi. Tuma Abdallah ni Mhariri Mtendaji Msaidizi wa Magazeti ya Serikali (TSN)

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam-14 Aprili, 2016

Dj Rommy Jones Kwenye Kashfa ya Ubakaji Sweden...

$
0
0

Inasmekana alimbaka mdada wakibongo aishie sweden anaitwa Deborah
Shutuma hizo zimewekwa Instagram katika page mbali mbali zinasema Rommy alikuwa na dada huyu nyumbani kwake na kumuwekea kilevi kwenye kinywaji chake akasinzia na jamaa kufanya yake...
Wadaku wanadai Rommy Jones hakumaliza ziara ya chibu chibude huko ulaya kwani alikimbia soo na chat sms zimewekwa hadharani akiomba msamaha
wambeya wanadai meneja wa diamond aitwaye salaam alikuwa radhi kutoa euro 10,000 ili kuua soo ila bidada akakataa....

Kwa Habari zaidi Ingia Page ya Dougie masta huko insta...
or Jamii Forums

Mwanamuziki MR BLUE Akata Shauri..Aamua Kumuoa Kabisa Mama wa Mtoto Wake...Picha

$
0
0
Hatimaye Mr blue kaachana na ukapera kaamua kumuoa mama watoto wake Wyder!!! Hongera sana Mr Blue kwa hatua uliyofikia!!!

Mr blue simbaaa akiwa na mke wake halali kabisaaa Wyder !!! Hakika Blue nayeye ameingia katika list ya wasanii mifano ya kuigwa katika maswala ya ndoa.. tupia neno la kumtakia kheri katika maisha ya ndoa...!!!bado baba Tiffah 


Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Yatahadharisha Mvua Kubwa za Upepo Mkali

$
0
0
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya kunyesha mvua kubwa inayozidi milimita 50 wiki hii.

Imesema mvua hizo ambazo zitanyesha katika mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Morogoro pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba zitakuwa kubwa na kuweza kusababisha madhara.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agness Kijazi ilisema mvua hizo zilitarajia kunyesha kuanzia Aprili 13, mwaka huu hadi Jumamosi Aprili 16, mwaka huu.

Dk Kijazi alisema kiwango cha uhakika wa mvua hizo ni kwa asilimia 70 na hali hiyo imetokana na kuimarika kwa ukanda wa mvua sambamba na uwepo wa kimbunga cha Fantala katika Bahari ya Hindi.

Hivyo aliwataka wananchi wanaokaa maeneo yaliyotajwa kuchukua hadhari na kuchukua hatua stahili ili kuepukana na madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na mvua hizo kubwa.

Hivi karibuni, TMA ilisema mvua za masika katika ukanda wa Pwani zilizoanza wiki ya kwanza ya mwezi huu kutakuwa na vipindi vifupi vya mvua kubwa zitakazoweza kusababisha mafuriko.

Aidha, kwa wakati huo hali ya joto kali itaendelea kuwepo nyakati za usiku huku ikipungua nyakati za mchana.

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya April 15

$
0
0
 

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya April 15

Serikali Kuchukua Hatua za Kisheria Kwa Waliofunga Mita za Kupimia Mafuta Bandarini na Kuacha zisifanye Kazi Kwa Miaka Mitano

$
0
0
Kamati ya Miundombinu imeitaka Serikali kuchunguza kwa kina na kuchukua hatua za kisheria kwa yeyote aliyehusika na kufungwa mita za mafuta zilizopo Bandari ya Dar es Salaam, bila kufanya kazi kwa miaka mitano.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk Norman Sigala alisema kuna haja ya Serikali kujiridhisha kwa umakini lengo la kufungwa kwa mita hizo na sababu ya kufungwa kwake, kisha ichukue hatua.

“Kamati yetu inatambua wajibu wake ikiwamo kuielekeza Serikali, kuishauri na kuikosoa bila uoga tulitembelea tukaona zile mashine moja ya mafuta ya dizeli tayari ilifungwa na inaendelea kufanya kazi, sasa hiyo nyingine Serikali inapaswa kwenda ndani zaidi kiuchunguzi na kuchukua hatua kali kwa yeyote aliyehusika,” alisema.

Februari 12, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alifanya ziara ya ghafla kwenye Kitengo cha Upimaji Mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam na kukuta mita zimejaa kutu baada ya kutelekezwa kwa miaka zaidi ya mitano.

Kutokana na hali hiyo, alimpa saa nne Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Magdalena Chuwa aandike barua ya kujieleza ni kwa nini aliamua kufunga mita hizo zisitumike kwa zaidi ya miaka mitano iliyopita.

Akizungumzia kiwango cha fedha za bajeti ya Sh4 trilioni iliyotengwa kwa ajili ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, alisema kamati yake inaridhishwa na kiwango hicho.

Hata hivyo, alisema Serikali inapaswa kuongeza upembuzi katika uteuzi wa watendaji wa idara na taasisi zake, ili kuepusha vitendo vya ufisadi ambavyo vimekuwa vikigharimu fedha nyingi kutafunwa ama kupotea katika mazingira ya kutatanisha, hivyo kukwamisha juhudi za maendeleo.

“Serikali ifanye uteuzi vyema wa watendaji wake kigezo cha uadilifu na uwezo wa kazi kiangaliwe kwa makini, huwezi kuzuia rushwa mahali ambapo kiongozi si mwadilifu, kamati inaishauri Serikali nafasi hizo zisitolewe kama zawadi,” alisema.

Alisema wameridhishwa na utendaji wa baadhi ya viongozi wanaokaimu nafasi za ukurugenzi wa taasisi hivyo na wameishauri Serikali pia iwathibitishe watu hao ili waweze kuwa na moyo wa kufanya kazi vizuri zaidi.

Akizungumza kuhusu bajeti, Dk Sigala alisema kamati yake imeridhishwa na mipango ya Serikali iliyoweka kwa mwaka huu wa fedha 2016/17 kwa wizara hiyo inayolenga kuboresha miundombinu muhimu.

“Serikali imetenga mafungu ya fedha kwa ajili ya kuboresha reli, barabara, viwanja vya ndege pamoja na kununua ndege nne, na kwa kuanzia imetenga Sh250 bilioni kununulia mbili za kuanzia katika mwaka huu wa fedha,” alisema.

Alisema hata hivyo katika kuboresha utendaji wa Mamlaka ya Bandari wameishauri Serikali kupunguza baadhi ya gharama ambazo zinakuwa zinatozwa na mamlaka hiyo, nia ikiwa ni kuwezesha wavutia wafanyabiashara na kumudu ushindani na bandari za nchi nyingine

Soma Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Katika Magazeti Leo.....


Msanii Mpya wa Diamond Platnumz Anaitwa Raymond Ameachia Video ya Wimbo wake Itazame Hapa....

$
0
0
Video ya ngoma ya msanii wa WCB, Raymond ‘Kwetu.’ Imeongozwa na Godfather Productions.
Tazama Video Hapa Chini Alafu Utoe Maksi zako Kwenye Comment Box....

Kajala Masanja Amtolea Chozi Kigogo wa Wema Sepetu Aliyefulia Mpaka Kuonekana Akiuza Chips

$
0
0
Siku chache baada ya gazeti dada na hili, Risasi Jumamosi kuandika juu ya aliyekuwa kigogo wa msanii Wema Sepetu, Clement Kiondo ‘CK’ kunaswa akiuza mishikaki, tukio hilo limemliza shosti wa Wema, Kajala Masanja.

Kumwaga chozi kwa Kajala kumetokana na maelezo yake kwamba, baada ya kuiona habari hiyo hakuweza kuamini kama kweli ni CK yule aliyewahi kumtolea shilingi milioni 13 kama faini ili asiende jela kutokana msala aliokuwa nao.


Akizunbumza na Ijumaa kwa majonzi, Kajala alisema: “Kiukweli nililia sana, nilishindwa kuamini kama kweli CK amefikia hali hiyo,” alisema Kajala ambaye pia aliwahi kudaiwa kutoka kimapenzi na jamaa huyo.

Akasema stori hiyo isingekuwa imeambatana na picha asingeamini lakini alipoona zile picha zinazomuonesha CK akiwa jikoni akimhudumia mtu, alishindwa kujizuia na kujikuta akibubujikwa na machozi.

Tukio la kunaswa kwa CK akiuza mishikaki lilinaswa na mapaparazi wetu juzikati kwenye baa moja iliyopo maeneo ya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar, jambo lililozua maswali mengi kutokana na jeuri ya fedha aliyokuwa nayo kigogo huyo.

GPL

Wastara Amshikia Kisu Mbunge...Afunguka A-Z ya Kuachana Kwao...Adai Hakuwahi Kumpenda Mbunge Huyo...

$
0
0
Untold story! Staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma ambaye hivi karibuni ndoa yake na Mbunge wa Jimbo la Donge, Zanzibar, Sadifa Juma iliingia kwenye mgogoro mkubwa, alijikuta akimshikia kisu mumewe huyo, kitendo ambacho kilimtisha jamaa huyo ambaye hakutarajia kama mwanamke anaweza kumfanyia hivyo.

NI SIMULIZI YA KUSHANGAZA
Chanzo kilicho karibu na wawili hao kimenyetisha simulizi hiyo ya kushangaza ambapo kilidai kwamba, Wastara si mwanamke wa kumchezea ndiyo sababu kubwa iliyomfanya mbunge huyo kunyoosha mikono na kumuacha aende zake.
Kilisema kuwa, wakiwa katikati ya ugomvi wao wa kindoa, Sadifa alishtushwa na kitendo cha Wastara kumshikia kisu, jambo ambalo lilikuwa ni mapema mno akipiga hesabu za huko mbele itakuwaje?

MAMBO MENGI
Chanzo hicho kilitiririka kwamba, katika ndoa hiyo iliyodumu kwa muda wa takriban miezi mitatu, kulikuwa na mambo mengi nyuma ya pazia na kushukuru kuwa bora hata imevunjika kwani kati yao huenda kungetokea jambo kubwa zaidi, aidha mmoja wao kumwaga damu au hata kuaga dunia kwani kila mmoja alikuwa akijihami kwa jinsi anavyojua namna ya kutumia silaha kali.

WASTARA AMSHIKIA KISU
“Siku ya mwisho hadi Wastara akaamua kuondoka kwenye ndoa yake, mheshimiwa alitaka kumpiga ndipo Wastara akaamua kumshikia kisu kwa madai kuwa yeye huwa hapigwi, kiufupi wale wasingewezana,” kilidai chanzo.Sadifaaaaaaaa

WASTARA ABANWA
Baada ya madai hayo mazito na ya kushtua, mwanahabari wetu alimwendea hewani Wastara na kumbana kuhusiana na habari hiyo ambapo mwanamama huyo alifunguka mazito zaidi.
Ijumaa: Wastara kwanza pole na kuvunjika kwa ndoa yako, hivi ni kweli uliwahi kumshikia kisu mbunge kwenye mgogoro wenu wa ndoa?
Wastara: Dah! Nimechoshwa na hizi habari jamani kwa sababu
zinanisononesha sana kwani nimekuwa mimi ndiye naonekana muovu.

MAOVU MENGI
Kuna maovu mengi ya mbunge ambayo sasa nitayaweka wazi. Niliyaacha kwa sababu ya kumheshimu kama mume wangu lakini yeye alifunguka, naomba muandike yote msifiche.
Hiyo habari ni ya ukweli wala hamjakosea, nilimshikia kisu kwa sababu nilikuwa nikijihami. Katika maisha yangu kupigwa ni mwiko, yeye alijaribu kunipiga na mimi nikamshikia kisu kwa kujihami.
Ijumaa: Huoni kama ni kosa kubwa na ulihatarisha maisha yake?

WASTARA KISU, MBUNGE PANGA
Wastara: Niliamua kumshikia kisu kwa sababu kubwa ya msingi ambayo ni baada ya yeye kunishikia panga, hiyo ni kawaida yake kwani hata ndani kwake ana mapanga mawili ambayo ameyahifadhi chini ya kitanda.
Ijumaa: Kuna madai kuwa uliondoka nyumbani kwake na kufungasha kila kitu alichokununulia kama aseti, unalizungumziaje hilo?
Wastara: Kweli nilibeba kila kitu lakini hakuna chake hata kimoja.

NINI KISA NA MKASA?
Ijumaa: Nini hasa sababu ya kuachana na mumeo maana hujawahi kufunguka kama hivi?
Wastara: Ni mambo mengi na wakati naolewa naye sikuyajua, nilianza kuyaona kwenye mitandao ya kijamii siku chache baada ya ndoa. Watu walikuwa wakinionea huruma, mimi sukujua lakini baadaye ndipo nilipoyaona yote.

WASTARA NA WANAUME
Ijumaa: Kuna madai kuwa una mpango wa kurudi kwa Bond ndiyo sababu ya yote hayo je, kuna ukweli juu ya hilo maana hata michango hamjarudisha kwa sababu mtafanya harusi nyingine?
Wastara:  Hakuna ukweli, mimi sina hamu na wanaume tena. Bond naongea naye kwa sababu alinithamini na kuujua utu wangu kwa kukiri makosa aliyonitendea. Kuhusu michango hakuna msanii hata mmoja aliyetoa zaidi ya ndugu zangu.

WASTARA ATOA NENO ZITO
Ijumaa: Je, mumeo akikufuata urudi myamalize, uko tayari?
Wastara: Siwezi kurudi kwa yule mbunge. Sikuwahi kumpenda wala yeye hakuwahi kunipenda, nilijikuta tu nimeshaingia kwenye ndoa.
Ijumaa: Kwa nini unasema hajawahi kukupenda?
Wastara: Kwa sababu alikuwa akinitukana. Kiufupi alininyanyasa, mbali na hapo hakuwahi kuwapenda hata watoto wangu.

SADIFA VIPI?
Baada ya Wastara kufunguka mazito, mwandishi wetu alimtafuta Sadifa lakini simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa SMS  hakujibu.
Hata hivyo, Hivi karibuni Sadifa alitoa ufafanuzi wa ndoa yake na kuanika baadhi ya mambo kwenye magazeti yaliyopita kuwa Wastara alikuwa akimwendea kwa waganga na kuahidi kumpa talaka.

Chanzo:Global Publishers

ANNE KILANGO Ajikusanya na Kufunguka Kwa Mara ya Kwanza Kanisani Baada ya Magufuli Kumfuta Kazi

$
0
0
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango Malecela, ameibukia kanisani na kutoa ya moyoni, ikiwa siku tano baada ya Rais Dk. John Magufuli kutengua uteuzi wake.

Kilango, Jumatatu wiki hii uteuzi wake ulitenguliwa baada ya Machi 20, mwaka huu, kudai kuwa mkoa wa Shinyanga hauna mtumishi hewa wa serikali hata mmoja.

Hata hivyo, Ikulu ilifanya uchunguzi na kubaini kuwa katika taarifa za awali kuna watumishi hewa 45, huku kazi ya uhakiki ikiendelea katika wilaya za Ushetu na Shinyanga.

Rais Magufuli aliwaagiza wakuu wa mikoa wote, alipokuwa akiwaapisha kuwa wafanya uchunguzi kuhusu uwapo wa watumishi hewa katika mikoa yao na kutoa taarifa.

Kutokana na kutoa taarifa hizo zisizo za kweli, Jumatatu wiki hii, Rais Magufuli alitangaza kutengua uteuzi wake, akiwa amekaa kwenye nafasi hiyo kwa siku 27. Kilango amekuwa mkuu wa mkoa wa 19 tangu kuanzishwa kwa mkoa huo.

Mbali na Kilango, Rais Magufuli pia alimsimamisha kazi Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Abdul Dachi, kutokana na taarifa hizo za kutokuwapo watumishi hewa katika mkoa.

Alivyosema Kanisani
Akiwasalimia waumini wenzake juzi, katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, mjini Shinyanga, baada ya kupewa fursa ya kusema neno, Kilango alisema anamshukuru Mungu kwa kila jambo kwa yote yaliyomtokea.

“Ndugu waumini wenzangu, hili ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu. Hata mtu unapojifungua mtoto akafariki dunia, unamshukuru Mungu kwani hayo ni mapenzi ya Mungu.
"Ukiona mzazi wako kafariki dunia pia, unamshuruku Mungu. Tunao wajibu wa kumshukuru Mungu kwa kila jambo,” alisema kwa maneno mafupi na kisha kuketi, huku akiacha simanzi miongoni mwa waumini wenzake, wakiwamo viongozi wa kanisa.

Alivyoanza Kazi
Mbele ya kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC), muda mfupi baada ya kuanza kazi, Kilango alisema Shinyanga ni mkoa wenye changamto nyingi ambazo atazishughulikia, lakini atakuwa akilazimika kukimbia Dar es Salaam kumwona mwenzi wake, Mzee John Malecela ambaye ni mgonjwa, na pindi hali yake ikiimarika wataungana naye mjini Shinyanga.

Hayo aliyasema Machi 22, mbele ya wajumbe wa kikao cha kamati hiyo na Ijumaa Machi 25, alisali kanisani hapo.

Sambamba na hayo, aliahidi kupambana na watumishi wazembe na wale wanaoendekeza rushwa na ufisadi na kurejesha hadhi ya mkoa wa Shinyanga kimaendeleo.

Kilango ambaye yuko mjini Shinyanga, akisubiri kukabidhi ofisi kwa mrithi wake kwa mujibu wa utaratibu, bado anaishi hotelini kwa vile aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Ally Rufunga, hajaondoka katika nyumba ya serikali iliyoko Ikulu ndogo, eneo la Lubaga.

Watumishi HEWA Jijini Arusha Waongezeka na Kufikia 300

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda amesema idadi ya watumishi hewa mkoani humo imeongezeka baada ya uchunguzi wa awali huku baadhi ya waliokuwa wakifuja fedha za serikali kwa kudanganya wakiomba kuzirejesha.

Aidha, amesema mkoa umepoteza Sh bilioni 1.8 kwa mwaka jana kutokana na kulipa watumishi hewa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini  Arusha, Ntibenda alisema hivi sasa mkoa huo unafuatilia akaunti za watumishi hao hewa ili fedha hizo zirudishwe serikalini huku watumishi wengine baadhi waliokuwa wakifuja fedha za serikali kwa kudanganya wakiomba kuzirejesha.

Alisema awali wakati timu ya uchunguzi aliyoiunda kuchunguza watumishi hewa ilibaini mkoa huo kuwa na watumishi hewa 270, lakini hadi jana idadi hiyo imeongezeka na kufikia zaidi ya 300.

Alisema wilaya mbili za Karatu na Arumeru ndizo ambazo watumishi hewa wameongezeka.

“Bado tunaendelea na uchunguzi na naamini wataongezeka lakini hivi sasa hao watumishi hewa wanahaha kurudisha fedha za serikali lakini hata kama wakirudisha watapelekwa mahakamani,” alisema Ntibenda.

Alisema hata kama fedha hizo watazirudisha, lakini watawafikisha mahakamani na pia wanafuatilia kujua ni kwa nini wakuu wa idara zao walifahamu udhaifu huo, lakini walikaa kimya na kuwalipa mishahara huku wakijua kuwa wanaihujumu serikali.

Alisisitiza ni vyema watu wakaacha tabia ya kujipatia fedha nyingi kwa njia isiyo halali kwani watumishi hewa wanasababisha fedha za serikali kushindwa kufanya shughuli nyingine badala yake kupata hasara.

Katikati ya mwezi uliopita, wakati akiwaapisha wakuu wa mikoa wapya, Rais John Magufuli aliagiza waende kufuatilia watumishi hewa katika mikoa yao na hadi sasa wamegundulika watumishi hewa zaidi ya 4,000.
Viewing all 104808 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>