Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live

Diamond, Wizkid, Flavour Kutumbuiza Barclays Center, New York, July 22

$
0
0
Ni ukumbi wa ndani kwa ndani maarufu mno jijini New York, Marekani nyumbani kwa wasanii wakubwa wakiwemo Jay Z, Beyonce, Justin Bieber, Rihanna, Drake, taja kila msanii mkubwa wa Marekani, amewahi kutumbuiza hapo.

Na sasa Diamond, Wizkid na Flavour, watakuwa wasanii wa kwanza wanaofanyia muziki Afrika kuwahi kutumbuiza kwenye ukumbi huo. Mastaa hao watatumbuiza kwenye tamasha la muziki la One Africa July 22, 2016 kwenye ukumbi huo wenye uwezo wa kujaza watu 20,000.

“We are about to Make a History America!!!…. Platnumz Diamond with my Fellow African brothers and Sisters will be Shutting the Barclays Center Down! On the 22nd Jully 2016 in New York!…. 20k Seat Capacity!…Now make sure you tell your Friend to tell a Friend,” ameandika Diamond.


Barclays Center ni ukumbi unaotumika kwa shughuli mbalimbali na upo Brooklyn, New York City. Pia hutumika kama uwanja wa nyumbani wa timu ya kikapu ya Brooklyn Nets pamoja na New York Islanders ya National Hockey League.

Show ya kwanza kufanyika kwenye ukumbi huo ilikuwa ya Jay Z, September 28, 2012.

SUKARI Tani 133 za Sukari iliyoingizwa Kimagendo Yagawiwa Bure

$
0
0
Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imegawa Sukari yote ya Magendo Mifuko 5,319 yenye thamani ya Zaidi ya Shilingi Milioni 373.5 kwa Taasisi mbali mbali Mkoani Lindi baada ya kuthibitishwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA kuwa ni Salama kwa matumizi.

Sukari hiyo ilikamatwa mwezi Februari mwaka huu katika bandari ya Lindi ndani ya meli ya MV Hassanat ikiingizwa kinyume cha Sheria ikitokea nchini Brazil kupitia Zanzibar.

Sukari hiyo ilipaswa kulipiwa Kodi zaidi ya shilingi Milioni 246.

Sukari hiyo imegawiwa kwa taasisi 31 mkoani humo baada ya TFDA kuthibitisha kuwa sukari iko salama kwa matumizi ya binadamu.

Akizungumza wakati wa ugawaji wa sukari hiyo Mkurugenzi wa huduma na Elimu kwa mlipakodi TRA Richard Kayombo amesema baada ya kukamatwa kwa bidhaa hizo TRA kwa kushirikiana na taasisi nyingine za serikali ikiwemo ofisi ya mkuu wa mkoa wa Lindi, iliamriwa sukari hiyo kuigawa kwa watu wenye uhitaji katika mkoa huo zikiwemo taasisi za elimu, Afya, kambi za wazee na Jeshi la magereza.

Chanzo: TBC

Rais Magufuli Awagomea Wabunge Nyongeza Ya Mikopo Ya Magari

$
0
0
Katika kile kinachoonekana amedhamiria kuendelea kubana matumizi ya serikali, Rais John Magufuli amekataa ombi la kuongeza fedha za ununuzi wa magari kwa wabunge pamoja na fedha za mfuko wa bunge.

Baada ya kuchaguliwa, wabunge walipatiwa milioni 90  za mkopo kwa ajili ya ununuzi wa magari, lakini baadhi yao walieleza kutoridhishwa na kiasi hicho, wakidai hakitoshelezi na kutaka kiongezwe hadi sh. milioni 120.

Taarifa za kuaminika zinaeleza kuwa wabunge waliwasilisha ombi kwa Rais Magufuli kuongezwa fedha lakini ombi hilo limekataliwa.

Chanzo cha kuamini kimedokeza kuwa mmoja wa wabunge wa CCM alimkumbushia Rais Magufuli ombi hilo wakati wa kikao cha chakula cha jioni, kilichofanyika wiki iliyopita mjini Dodoma.

Chanzo hicho kilieleza kuwa Rais Magufuli alikataa kuwaongezea wabunge fungu hilo kwa madai kuwa serikali yake haina fedha.

Kilieleza pia kuwa Rais Magufuli alikataa kuongeza fungu la mfuko wa jimbo kwa kuwa serikali haina fedha huku akiwataka wabunge kufanya kazi kwa bidii.

"Rais alisema kwa sasa hali si nzuri, amekumbana na changamoto mbalimbali na kutuahidi kulichukua ombi letu, endapo hali itatengemaa atatuangalia kwa sababu hata yeye analitambua hilo kwa sababu alikuwa mbunge."Kilisema chanzo hicho

Kauli ya Msemaji wa Yanga Baada ya Simba Kufungwa na Mwadui na Kuipa Yanga Ubingwa hii Hapa

$
0
0
"Tunawashukuru sana wa matopeni kwa kutubeba, hii inadhihirisha ni jinsi gani wanatupenda, bahati nzuri hata sisi tunabebeka, unajua unapobebwa, yule anayekubeba sharti achutame halafu unayebebwa unampandia juu, juu ya mgongo, Simba wametubeba kwa kutupa ubingwa"

Je, unakubaliana na kauli hii ya msemaji wa Yanga?

Bush Asema Hatampigia Kura Donald Trump

$
0
0
Aliyekuwa mgombea wa urais wa tiketi ya chama cha Republican nchini Marekani, Jeb Bush amesema hatampigia kura Donald Trump katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika nchini humo Novemba mwaka huu.

Bush alisema kuwa Trump hana tabia wala mienendo ya kuwa Rais wa Marekani.

‘‘Marais wa Marekani wanasifa zao na wanakubalika kwa watu, lakini huyu jamaa hana sifa hata moja ndiyo maana kila siku namkana na kusema hafai kabisa kuwa rais wa nchi hii, ’’alisema Bush

Jeb ni mojawapo wa wanachama mashuhuri wa Republican kutanganza hadharani kuwa hatampigia kura Trump kwa sababu ya kampeni yake ya kiburi ambayo imegawanya Chama cha Republican.

Juzi Spika wa Bunge, Paul Ryan alisema hatamuunga mkono mfanyabiashara huyo tajiri ingawa atakutana naye wiki ijayo.

Hata hivyo, Trump aliungwa mkono na mgombea urais wa zamani wa nchi hiyo, Bob Dole aliyeshindwa katika uchaguzi na Bill Clinton wa Chama cha Democratic mwaka 1996.

Wiki iliyopita Seneta wa Texas, Ted Cruz alijitoa katika kinyang’anyiro cha kuwania uteuzi wa kugombea urais kwa Republican baada ya kushindwa katika uchaguzi wa awali dhidi ya mpinzani wake huyo.

Cruz aliwaambia wafuasi wake katika mji wa Indianapolis kwamba: “ Njia hii kuelekea ushindi imefungwa” na kusema kuwa wapiga kura wamechagua njia nyingine.

Alitoa shukrani kwa wafuasi wake wote. Trump alipata ushindi mkubwa Indiana huku Cruz akishika nafasi ya pili na gavana wa Ohio John Kasich akiwa katika nafasi ya tatu.

Trump alisema huo ni ushindi mkubwa kwake na kumpongeza Cruz akimuita yeye na wagombea wengine 15 waliokuwa wanagombea uteuzi wa Republican kuwa ni werevu na wenye nguvu.Alitoa wito wa kuwa na umoja ndani ya chama hicho.

Kwa upande wa Democratic seneta wa Vermond, Bernie Sanders ameshinda katika jimbo la Indiana dhidi ya Hillary Clinton

Wagombea hao wawili walibadilishana ushindi kabla ya Sanders kuibuka mshindi kwa asilimia saba ya kura. Hata baada ya ushindi huo wa Sanders katika jimbo la Indiana, Hillary anaongoza katika idadi ya wajumbe ikionyesha kwa mahesabu ni vigumu kwa Sanders kuteuliwa kuwa mgombea wa Democratic

Kocha Julio Adai Timu ya Simba Ina Laana Kubwa Sana

$
0
0

Kocha mkuu wa Mwadui FC Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ameiambia timu ya Simba kwamba inalaana ndiyo sababu ya kushindwa kufanya vizuri kwenye michuano ya ligi kuu Tanzania bara kwa muda mrefu.

Julio anadai laana hiyo inatokana na uongozi wa Simba kumfukuza yeye pamoja na kocha mkongwe Abdallah Kibadeni ‘Kin Kibadeni Mputa’ bila kuwalipa stahiki zao.

“Wakati mimi na King Kibaden tunafukuzwa Simba, niliwaambia kwamba ,mnatufukuza huku tunadai mishahara yetu na hiyo itakuwa laana kwasababu sisi tunafamilia kubwa ambazo zinatutegemea lakini wao walitufukuza hihuni”, anasema Julio ambaye ameshawahi kuitumikia Simba kama mchezaji na baadaye kama kocha.

“Niliweka nadhili kwenye ligi hii baada ya kuipandisha Mwadui lazima niifunge Simba, mechi ya kwanza tulitoka sare, walichomoa goli. Haji Manara akasema kuna goli walitufunga likakataliwa, safari hii tumekuja kwenye uwanja wao waliouzoea na tumewafunga.”

“Tukubali kwamba timu ya Simba mbovu na mimi nitoe wito kwa viongozi wa Simba, kama wanataka timu ifanikiwe lazima wawe wanatoa nafasi kwa waalimu wasajili wachezaji. Haya mambo ya mtu mwenye nguvu ya pesa ndiyo asajili wachezaji ni makosa kwasababu kitaalamu hata Mungu kazi nyingine hazitaki ndiyo maana kazi ya kuua kampa Israel.”

“Nimefurahi sana kuifunga Simba kwasababu wanapokuwa hawana kocha wananiita, wakipata kocha mzungu wa kumlipa pesa nyingi wananitimua tena kwa matusi.”

Maneno hayo ya Julio yamekuja mara baada ya Mwadui kuichapa Simba kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa VPL uliochezwa Jumapili kwenye uwanja wa taifa.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe atinga Nigeria kwa Nabii TB Joshua

$
0
0
Ninatazama Emmanuel tv hapa nimemuona mhe. Freeman Mbowe akiwa kwenye ibada katika kanisa la The Synagogue Church of All Nations linaloongozwa na Prophet T.B Joshua

SUMATRA yatangaza nauli kwa mabasi yaendayo kasi

$
0
0
Baada ya Kampuni ya UDA-RT kuwasilisha maombi ya nauli zitakazotumika kwa mabasi yaendayo haraka kwa Mamlaka ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA), leo hii (May 09 2016) SUMATRA imetangaza nauli hizo.

SUMATRA imesema kuwa njia ya pembezoni (Freeder Route) nauli ya mtu mzima ni 400 na mwanafunzi 200 na njia kuu (Trunk Route) ni 650 na mwanafunzi 200 na kwa abiria atakayetumia kusafiri njia kuu (Freeder Route) na kuendelea na safari kwa njia ya pembezoni nauli yake itakuwa ni 800 na mwanafunzi 200.

Huduma hiyo itatolewa kuanzia kesho bure kwa wananchi kwa siku mbili mfululizo na ifikiapo May 12 2016 zitaanza kutozwa nauli zilizotajwa.

Msimamizi wa mradi kutoka DART, Injinia Ronald Lwakatare amesema haya wakati akiongea na waandishi wa habari mchana huu;

‘Wakati huo tunafanya majaribio tutakuwa tunaangalia mfumo unavyofanya kazi kwa hiyo tutawabeba abiria kwa siku kadhaa bila kulipa nauli’.

Rais Mugabe Apigwa Kibao na Mkewe Hadharani...

$
0
0

Rais wa Zimbabwe Bw. Robert Mugabe amepigwa kibao hadharani na mkewe Grace Mugabe. Mlinzi wa rais huyo amemlaumu Grace kwa kitendo hicho cha kumpiga Mh Mugabe hadharani na kudai kuwa alipaswa kufanya kitendo hicho wakiwa chumbani.

Kwa upande wake Grace anadai hawezi kufuata taratibu kwa kusubiria mpaka afike chumbani kutokana na ukweli kwamba yeye pia ni boss wao kwa kuwa ni mke wa rais.


Read full story here...Source: NEWS SA


Harare – Police deputy commissioner general and close relative of president Robert Mugabe Innocent Matibiri is being blamed for failing to protect the dictator as details emerge of the embarrassing altercation in which the president was beaten up by his wife Grace Mugabe.

Footage of the incident shows Grace Mugabe slapping her husband in a fit of rage. Matibiri, Mugabe’s chief police guard, rushes in and tries to calm the situation, telling Grace Mugabe that if she wants to fight her husband she must do it in their bedroom, not in public.



Grace Mugabe slaps Matibiri hard in the face and he withdraws in shame, leaving Mugabe to face further abuse from his wife, who is 40 years younger than the 92 year-old despot now afflicted with poor health.

The beating left Mugabe and his aides shell-shocked. Mugabe has previously complained of abuse from his wife, who harbours presidential ambitions and has declared: “Who has more right than me to be president?”

The failure by Mugabe’s guards to restrain his violent wife has left the president exposed and allowed Grace Mugabe to institute a reign of terror within Zanu PF where her entry as the women’s league chairperson has sparked chaos amid allegations of sex scandals.

Grace Mugabe has declared that she will not follow protocol because she is ‘superior’ to all of Mugabe’s aides by virtue of being “their boss’s wife”.

Source: News SA

BEKI wa Simba Hassan Kessy Asaini Kuichezea Klabu ya Yanga kwa Miaka miwili

$
0
0
Beki wa kulia wa Simba SC, Hassan Ramadhani Kessy atimae ameasaini kuichezea Klabu ya Yanga kwa mkataba wa miaka miwili, Hii ni baada ya mkataba wake na Simba wa miaka miwili kumalizika.

Zoezi hilo lilifanyika juzi usiku mjini Dar es Salaam. Akiwa na Meneja wa Kessy, Tippo Athumani na katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit Kessy ataanza kuitumikia Yanga kuanzia mwezi ujao.

TAZAMA Hapa Video ya Jinsi Mtangazaji Gadner G Habash Alivyomzalilisha Lady Jay Dee Hadharani..

$
0
0
Wikiendi iliyoisha imesambaa video mtandaoni ikimuonesha mtangazaji huyo akiongea kwenye tamasha alilokuwa mshereheshaji: "My name is Captain Gardner G Habash all the way from Clouds FM, Jahazi hatari sana. Na sina neno na yule mtoto wa kike. Nimeshamkojoza kwa miaka kama 15 hivi.”

Video hiyo imesababisha hasira kubwa kwa mashabiki wa Jaydee na watu wengi kwa ujumla.

Itazame Hapa chini:

Tazama Video ya Msanii Mpya wa The Industry Anayeitwa Seline..Wimbo Unaitwa Njoo

$
0
0
The Industry, label ya Nahreel imeanza kuwatoa wasanii wake. Jumamosi walitambulishwa wasanii wake watatu akiwemo Seline ambaye leo ameachia kazi yake mpya, Njoo. 

Tazama video ya wimbo huo.

WEMA Sepetu "Sipendi Watu Wanavyonitukana Mgumba Instagram..Saa Zingine Nashindwa Kuvulimia"

$
0
0
Wema Sepetu amefunguka na kusema kuwa hapendi watu wanavyomwita mgumba ama kuendelea kumuongelea kuhusu uwezo wake wa kupata mimba huko Instagram kwani saa zingine anashindwa kuvumilia, ameongeza na kusema pia hiyo ndo ilikuwa sababu moja wapo ya yeye kutangaza  sana kuwa anamimba kipindi kile kwani ilikuwa nafasi yake ya kuwa prove wrong watu wanaosema kuwa ni mgumba lakini mungu hakupenda iwe hivyo na mwisho mimba kuharibika....

Jamani Punguzeni Kidogo

Mose Iyobo asema kuwa na mahusiano ya mapenzi na Aunt Ezekiel kumemsaidia sana

$
0
0
Dancer wa Diamond, Mose Iyobo amesema kuingia kwenye mahusiano ya mapenzi na Aunt Ezekiel kumemsaidia mambo mengi katika maisha yake.
Aunt na Mose

Akizungumza na Bongo5, Mose amesema hasa hasa amenufaika sana na umaarufu wa Aunt Ezekiel ambae ni staa mkubwa katika tasnia ya filamu.

“Kuwa na mahusiano na mama Cookie kumenisogeza sana,” alisema Mose. “Kwa sababu ni star wa filamu toka kitambo sana. Mimi nilikuwa najulikana lakini siyo kivile, lakini nilivyokutana na Mama Cookie kuna vitu vingi vimeongezeka katika maisha yangu,” alisema Mose.

Pia Mose amesema mwanae Cookie ataonyeshwa hadharani rasmi kwa mara ya kwanza tarehe 21 mwezi huu baada ya kutimiza mwaka mmoja

Chanzo:Bongo5

Serikali Kujenga Kituo cha Michezo Manyara

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye amesema serikali itajenga kituo cha michezo katika Mkoa wa Manyara ili kuacha kutumia kituo cha hifadhi ya mbuga ya Tarangire Mkoani humo.

Waziri Nape ameyasema hayo leo Bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Martha Umbula aliyetaka kujua kuhusiana na ni lini serikali itajenga kituo cha mkoa cha michezo kitakachoweza kuwakusanya wanamichezo wengi kwa wakati mmoja kuliko ilivyo sasa.

''Serikali itajenga kituo hicho baada ya kupata eneo la kutosha kwani kujengwa kwa kituo hicho kutarahisisha upatikanaji wa ajira pamoja na biashara''Amesema Waziri Nape.

Aidha kufuatia swali hilo Mbunge wa Mbulu Lazaro Massey (CCM) amesema kwamba kuna uwezekano wa kupata ardhi bure kama serikali itaridhia kujengwa kwa kituo hicho katika wilaya ya Mbulu.

Waziri Nape akijibu swali hilo amesema kwamba kama ardhi ipo serikali itajenga kituo hicho wilayani humo ili kuweza pia kumuenzi kazi nzuri ya riadha aliyofanya Filbert Bay katikakuipatia heshima Tanzania.

Swala la Sukari lisitu Sahaulishe Lugumi na Ripoti ya CAG..... Tusiwe Wepesi Wakutolewa Kwenye Reli-Henry Kilewo

$
0
0
Hivi ile kamati ya PAC imeishia wapi na ishu ya Lugumi? Mbona hapa pako kimya? Na tukizingatia ni ishu inayogusa jeshi letu la polisi? Hapa jipu halitumbuliki?

Nimejiuliza maswali hayo nikasema nilini Watanzania tutalazimisha Watawala wajue tumechoka na kusikia ishu zikiibuliwa na kuishia njia.... Au huko Bungeni wanaliongelea na sisi huku hatusikii wala kuona kwakuwa Bunge halipo live?

Swala la Sukari lisitu sahaulishe Lugumi na Ripoti ya CAG..... tusiwe wepesi wakutolewa kwenye Reli, Lugumi na Ripoti ya CAG imeishia wapi ama inaendeleaje?

HUU MCHEZO HAUHITAJI HASIRA

By Henry Kilewo

Ankal Issa Michuzi wa Issa Michuzi Blog Afiwa na Mtoto wake

$
0
0
Ankal Issa Michuzi anasikitika kutangaza kifo cha mwanae Maggid Muhidin kilichotokea jana Jumapili huko Durban, Afrika Kusini, alikokuwa masomoni.

Mipango ya kuusafirisha mwili wa marehemu inafanywa, msiba utakuwa Tabata Mawenzi jijini Dar es salaam ambako ratiba ya mazishi itatoka mara tu baada ya mwili kuwasili.

Habari ziwafikie ndugu, jamaa, majirani na marafiki popote pale walipo.

Innalillah wa inna ilayhi raajiun

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne Ya May 10, Ikiwemo Sukari Yamshinda Magufuli

$
0
0

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne Ya May 10, Ikiwemo Sukari Yamshinda Magufuli

Wachungaji Wawili wa KKKT Wafikishwa Mahakamani Kwa Tuhuma za Mauaji.......Mmoja wa Moravian Mbaroni kwa Kukutwa na Meno 11 ya Tembo Kanisani

$
0
0
Wakati mchungaji wa Kanisa la Moravian akikamatwa na meno ya tembo 11 ndani ya kanisa, huko Moshi wachungaji wawili wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji.

Tukio la wilayani Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro linawahusisha wachungaji wawili wa KKKT, Rodrick Mlay (52) na Godbess Mamkwe (38) pamoja na wananchi watatu ambao jana walipanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini humo kwa madai ya kuua kwa kukusudia.

Wakati wachungaji hao wawili wakipanda kizimbani, Polisi mkoani Katavi kwa kushirikiana na askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi wanawashikilia watu wawili akiwamo mchungaji wa Kanisa la Moravian kwa tuhuma ya kunaswa wakiwa na meno ya tembo 11 wakiwa wameyahifadhi ndani ya kanisa.

Akizungumzia meno hayo, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda alisema watuhumiwa hao walikamatwa juzi katika Kanisa la Moravian lililopo Kijiji cha Usevya, Wilaya ya Mlele.

Nyanda alisema mchungaji huyo akiwa na mwenzake ambao wote majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za upelelezi, walikamatwa kufuatia taarifa zilizolifikia jeshi hilo na askari wa hifadhi kuwa, watu hao wanajihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo na wamekuwa wakiyahifadhi ndani ya kanisa.

Baada ya taarifa hizo, polisi na askari hao walifanya uchunguzi kuhusiana na taarifa hizo kwa kufika katika kanisa hilo na kufanya upekuzi uliofanikisha kukamatwa kwa meno hayo yakiwa yamehifadhiwa kwenye tenga la kubebea mizigo.

Kaimu kamanda huyo alisema katika matukio mengine mawili tofauti yaliyotokea Mei 8, saa mbili usiku kwenye maeneo ya Mgolokani, Kata ya Sitarike wilayani humo, polisi kwa kushirikiana na askari wa hifadhi hiyo walimkamata mtu mmoja akiwa na jino moja la tembo.

Nyanda alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya askari kufanya upekuzi ndani ya nyumba yake na kukamata jino hilo na lingine la simba.

Alisema wote waliokamatwa kwenye matukio hayo wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote ili kujibu tuhuma zinazowakabili.

Katika tukio la wachungaji waliofikishwa mahakamani mjini Moshi, Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Julieth Mawole alisema wakiwa na wananchi watatu aliowataja kwa majina ya Fadhili Mkenda (36), Jackson Ruben (45) na Mathayo Moses (27), Mei 4 katika eneo la Kilema Pofo wanadaiwa kumuua kwa makusudi Frank Peter (19).

Hakimu Mawole aliwataka watuhumiwa hao kutojibu lolote na kesi dhidi yao itasikilizwa Mei 23 katika Mahakama Kuu Kanda ya Moshi na wote walipelekwa rumande kwa sababu shtaka waliloshtakiwa nalo halina dhamana kisheria.

Katika hatua nyingine, raia wa Marekani, Mbaraka Mtambo (50) amekamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akiwa na maganda mawili ya kobe bahari aliyokuwa ameyafichwa kwenye begi la nguo.

Kamanda wa Polisi wa JNIA, Martin Otieno alisema raia huyo mwenye asili ya Tanzania, alikamatwa juzi saa 3.45 usiku akijiandaa kwa ajili ya safari ya kwenda Marekani na ndege ya Shirika la KLM kupitia Uholanzi.

Sikiliza na Download Wimbo Mpya Kutoka Kwa Mwanamuziki KB, Wimbo Unaitwa Binadamu

$
0
0
Msanii mpya KB jina lake halisi ni Kulwa Bilal, ni Msanii chipukizi anayefanya vizuri sana kwenye hiii industry ya Muziki Tanzania chini ya management ya Clarence_june22 Events, amejikita  haswa kwenye mziki wa bongo flavour  hivi karibuni  ametoa single  kali sana inayoitwa BINADAMU.. Wadau wote KB anaomba sana support yenu kwa sababu bila ninyi hakuna  muziki.

 Sikiliza/Download Hapa Wimbo Wake:
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live




Latest Images