Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live

Mashabiki wa Diamond Washerehekea Tangazo hili la MTV Base

$
0
0
Seems like Diamond Platnumz amewapa taarifa muhimu MTV Base.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, kituo hicho cha runinga kiliandika kuwa staa huyo anakuja na collabo na Chris Brown.

“@diamondplatnumz working on a future project with #chrisbrown,” wameandika.

Taarifa hiyo ilipokelewa kwa furaha kubwa na mashabiki wake waliomwaga lundo la comments takriban 900. Comments nyingi ni za mashabiki wanaobishana na kutukanana hata hivyo, SMDH!

Video ya Wema Akidendeka Yamweka Pabaya

$
0
0
Kipande cha video kilichosambaa kwenye Mitandao ya Kijamii ya Instagram, Facebook na WhatsApp kikimuonesha staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘akidendeka’ chumbani na mwanaume kimemuweka pabaya baada ya Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fisoo kusema kuwa kama ni sehemu ya filamu haina maadili ya Kitanzania.

wema (1)  Akizungumza na Wikienda kwa njia ya simu akiwa nje ya nchi wikiendi iliyopita, Fisoo alisema kuwa kama ni filamu mpya ya mwanadada huyo, ikiingizwa sokoni ikiwa haina maadili yanayotakiwa kamwe hawawezi kuruhusu kusambazwa popote na wala hawawezi kuipitisha.
Kipande hicho cha filamu hiyo kinamuonesha Wema akiwa anadendeka kikwelikweli na jamaa huyo jambo ambalo bodi hiyo imeliangalia kwa upande wa pili na kwamba haitaingia sokoni ikiwa hivyo.
wema (2)Baadhi ya mashabiki wa Wema waliokiona kipande hicho walikuwa na maswali lukuki kichwani kutokana na kile walichokuwa wakikiona kwenye kipande hicho cha filamu hiyo.

“Jamani hata kama ni filamu, hapana, imezidi, kwa kweli ni hatari sana maana kama Wema angekuwa mwanamke wangu hata hiyo filamu angeacha kuicheza kabisa,” alisema mmoja wa mashabiki hao.

wema (3)Kwa upande wake mpenzi wa Wema ambaye ni Mshindi wa Big Brother Africa 2014, Idris Sultan alisema kuwa na yeye anatamani kupata nafasi ya kucheza filamu, tena apewe vipande kama hivyo hata kama ishirini, atacheza kwa uangalifu.

“Yaani na mimi napenda sana nicheze filamu vipande kama hivyo ishirini hivi tena nitacheza vizuri sana maana najua kila mtu anaweza kuigiza kama hivyo,” alisema Idris.
Kwa upande wake Wema hakutaka kusema chochote juu ya kipande hicho.

Chanzo:GPL

Aika: Nina Wivu Hatari Kwa Nahreel Acha tu

$
0
0
Memba wa Kundi la Navy Kenzo, Aika Mareale amefunguka kuwa ana wivu wa kupindukia kwa memba mwenzake ambaye ni mpenzi wake, Emmanuel Mkono ‘Nahreel’ wanaotamba na wimbo wao wa Kamatia Chini kwani kuna kipindi huwa anapata wakati mgumu hasa warembo wanapokatiza mbele ya jamaa huyo.

Aika aliliambia Wikienda kuwa kila mwanadamu ana moyo na kuna watu wengine wanaweza kuwaona kuwa wapo tu wala hawaoneani wivu lakini ukweli ni kwamba ana wivu na mpenzi wake huyo.
“Watu wanadhani sina wivu lakini ninao kinoma lakini nagugumia kimoyomoyo,” alisema Aika
Chanzo:GPL

Serikali yazidi kumg'ang'ania Zombe, yafufua kesi yake kivingine

$
0
0
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) amemuondolea kosa la mauaji aliyekuwa mkuu wa upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abdallah Zombe na sasa inataka ajibu mashtaka ya kuficha wahalifu.

DPP amefanya mabadiliko hayo kwenye rufaa aliyoikata Mahakama ya Rufani dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu wa kumuachia huru Zombe, ambaye alikuwa Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) katika mashtaka ya mauaji.

Awali, DPP alikata rufaa akipinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyomwachia huru Zombe na wenzake tisa, katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge mkoani Morogoro na dereva mmoja wa teksi wa Manzese jijini Dar es Salaam.

Katika rufaa hiyo, DPP alikuwa anaiomba Mahakama ya Rufani iwatie hatiani washtakiwa hao kwa kosa la mauaji ya kukusudia, kama ilivyokuwa kwenye kesi ya msingi, kosa ambalo adhabu zake ni pamoja na kunyongwa hadi kufa.

Hata hivyo, DPP amebadili msimamo huo dhidi ya Zombe na badala yake anaiomba Mahakama hiyo imtie hatiani kwa kosa la kuwalinda wahalifu ambao walitenda kosa la mauaji ya wafanyabiashara hao na dereva wa teksi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Timoth Vitalis, ambaye ni Wakili Mkuu wa Serikali (PSA) na Richard Rweyongeza, ambaye ni wakili wa kujitegemea anayemtetea Zombe katika rufaa hiyo, walisema mtu anayepatikana na hatia kwa kosa hilo adhabu yake ni kifungo jela kisichozidi miaka saba.

Kwa maana hiyo, hata kama Mahakama ya Rufani itakubaliana na hoja za rufaa za DPP na kumtia hatiani Zombe kwa kosa hilo jipya ambalo hata hivyo, hakuwa ameshtakiwa nalo kwenye kesi ya msingi, atakuwa ameepuka adhabu ya kitanzi.

DPP alibadili msimamo wake huo dhidi ya Zombe siku ya usikilizwaji wa rufaa hiyo Mahakama ya Rufani mbele ya jopo la majaji watatu, Bernard Luanda, Sauda Mjasiri na Semistocles Kaijage, hivi karibuni.

Mkurugenzi huyo wa mashtaka alifikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha kuwa hakuna ushahidi wa kumtia hatiani Zombe kwa kosa hilo la mauaji. Akizungumzia uamuzi huo wa DPP kumuondoa kwenye shtaka la mauaji kama alivyokuwa akidaiwa tangu awali na sasa kupewa shtaka la kuwalinda wahalifu, Zombe alisema kwanza alikuwa ameonewa kwa kuhusishwa na hatimaye kushtakiwa kwa kosa la mauaji.

Alisisitiza kuwa hakutendewa haki wakati wa kumfungulia shtaka hilo la mauaji kwa kuwa sheria hazikufuatwa.
"Kwanza ni mambo ya ajabu sana. Nimedhalilishwa sana kwa muda wote huo na kuonekana kuwa mimi ni muuaji kila ninakopita, kwa kufunguliwa shtaka ambalo sikuhusika nalo," alisema Zombe.

"Mimi sikuwapo eneo la tukio na wala nilikuwa siwafahamu watu hao na hata Tume (iliyoundwa na Rais kuchunguza mauaji hayo iliyoongozwa na Jaji Mussa) Kipenka ililiridhika kuwa sikuwepo eneo la tukio. Sasa nilihusikaje na mauaji hayo?"

Zombe aliongeza kuwa washtakiwa wote walihojiwa na kuandika maelezo yao na kwamba huo ndiyo utarartibu wa kisheria. Zombe alisisitiza kuwa yeye alikuwa mwendesha mashtaka kwa muda mrefu na mkuu wa upelelezi wa mkoa, hivyo anajua taratibu kwa kuwa alikuwa akiandika majalada mengi kwenda kwa Mwanasheria wa Serikali na mengine yalikuwa yakienda mahakamani kama alivyoyaandika.

Kuhusu kosa alilobadilishiwa na DPP wakati wa usikilizwaji wa rufaa hiyo, Zombe hakuwa tayari kulizungumzia kwa kuwa bado Mahakama haijatoa hukumu. Kabla ya kumbadilishia shtaka hilo, wakati wa usikilizwaji wa rufaa, DPP alitaka kumuongezea Zombe shtaka hilo kama shtaka mbadala, wakati wa usikilizwaji wa kesi ya msingi.

Hata hivyo, DPP aligonga mwamba baada ya Jaji Massati kumkatalia kwa maelezo kuwa alitakiwa ashtakiwe tangu mwanzo kwa kosa hilo. Kabla ya kumuondoa Zombe katika kosa la adhabu hiyo ya kunyongwa, kwanza DPP, aliwaondolea washtakiwa wengine watano, baada ya kubaini kuwa ushahidi aliokuwa nao hauwagusi katika rufaa hiyo. Walioondolewa ni Jane Andrew, Emmanuel Mabula, Michael Shonza, Abineth Salo na Festus Gwabisabi. Lakini ameendelea kuwang'ang'ania Zombe na wenzake watatu ambao ni Christopher Bageni, Ahmed Makelle na Rajabu Bakari.

Source: Mwananchi
SIGNATURE

KUTOKA BUNGENI: Hotuba ya Lema yazuiliwa kusomwa mpaka Kamati ya kanuni iipitie

$
0
0
Hotuba ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani ya Msemaji Mkuu wa Wizara ya Mambo Ndani ya Nchi, Godbless Lema imezuiliwa kusomwa.

Imezuiliwa kusomwa mpaka kwanza kamati ya Kanuni ya Bunge iipitie hotuba hiyo kabla ya kusomwa bungeni ili kuangalia kama hotuba hiyo imekiuka kanuni za Bunge.

Watu 11 Wakamatwa Mkoani Morogoro Kwa Tuhuma za Kumbaka na Kumdhalilisha Binti wa Miaka 21

$
0
0
WATUHUMIWA wawili Zuberi Thabiti (30) na Iddy Adamu (32) wanaodaiwa kushirikiana kufanikisha tukio la kumbaka na kumdhalilisha binti mkulima (jina limehifadhiwa), mkazi wa Kata ya Dakawa, wilayani Mvomero, mkoani Morogoro, wamekatwa na kohojiwa na jeshi la polisi mkoani humo.

Watuhumiwa hao wanadaiwa kufanya tukio hilo la kinyama usiku wa Mei 4, mwaka huu katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Titii iliyoko Dakawa ambapo Zuberi aambaye ni dereva, mkazi wa Mbarali Mbeya anadaiwa kumbaka binti huyo huku Iddy ambaye ni mkulima, mkazi wa Makambako akirekodi picha za video kwa kutumia simu yake ya mkononi.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, baada ya kurekodi katika simu yake, baadaye Iddy alizituma picha hizo kwa mtu aliyefahamika kwa jina la Rajabu Salehe (26), mkazi wa Dakawa ambaye naye alizisambaza picha hizo katika mitandao mbalimbali ya kijamii kwa watu mbalimbali.
Taarifa ya polisi imeeleza kuwa, chanzo cha tukio hilo ni kwamba, binti huyo alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Zuberi ambapo siku hiyo mtuhumiwa alimpigia simu binti huyo na kumwambia aende katika nyumba hiyo ya wageni.

Taarifa hiyo ya polisi imezidi kueleza kuwa, baada ya kufika katika chumba husika ndipo Iddy alipoingia kisha kumtaka binti huyo afanye atakachomuelekeza huku akimshikia kisu ili asipige kelele na baada ya kutekeleza ukatili huo (ubakaji), walimtaka asitoe siri hiyo vinginevyo atauawa.
Aidha, baada ya tukio hilo kuripotiwa kituo cha Polisi Dakawa Apliri 5, mwaka huu, polisi walianza uchunguzi mara moja ambapo walifanikiwa kuwakamata jumla ya watuhumiwa 11 wakiwemo Zuberi na Iddy pamoja na walioshiriki kuzisambaza picha hizo za udhalilishaji ambao ni;

Rajabu Salehe (26), Saidi Athumani (26),  Musini Ngai (36), Saidi Mohamedi (24), John Peter (24), Hassani Ramadhani (27), Ramadhani Ally (26), Lulu Peter (38) na Magreth Njonjome (30), wote wakazi wa Dakawa ambapo kwa pamoja wamefunguliwa shitaka la PICHA ZA UTUPU (PONOGRAFIA) chini ya kifungu cha 14 (1) (a) cha sheria ya makosa ya mtandao.

Taarifa hiyo ya polisi pia imeeleza kuwa jeshi hilo linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine huku jeshi hilo likitoa onyo kwa wananchi wote kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii kwa kutoshiriki makosa ya uhalifu wa kimtandao kwani sheria itachukua mkondo wake.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu leo alikemea suala hilo bungeni na kueleza masikitiko yake makubwa kwa watu hao kutekeleza unyama huo na kusisitiza kuwa watuhumiwa hao wafikishwe mahakamani haraka.

Penzi la Diamond, Kiba Lamtesa Jokate

$
0
0
Siri imevuja kuwa penzi la vinara wawili wa Muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond PlanumZ’ na Ali Saleh Kiba ‘King’ linadaiwa kumtesa mlimbwende Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ ambaye amekuwa akijutia kujiingiza kwenye uhusiano na wasanii hao.

TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa Jokate, hivi karibuni alitupia mashairi ya Wimbo wa Ndi Ndi Ndi wa Mwanamuziki Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo baadhi ya mashabiki wake walimtaka kuwaahidi kuwa hatarudia kujiingiza kwenye penzi la mastaa hao (yaani Diamond na Kiba) kwani ishu hiyo ilimfanya atafsiriwe vinginevyo tofauti na ilivyokuwa awali.
kiba jokate

Ilisemekana kuwa kauli hizo za mashabiki hao zilikuwa kama kugongelea msumari wa moto kwenye kidonda kwani ishu hiyo imekuwa ikimsumbua na kumsababishia maumivu yanatokana na kujutia uamuzi wake huo kwa kuwa hakudumu nao.
“Unajua Jokate alijijengea na ana heshima sana kwenye jamii yetu kwa uwezo na upeo wake (IQ) na hata kujitambua, sasa anapokuwa na uhusiano na msanii kisha baada ya muda mfupi akaachana naye kama ilivyokuwa kwa Diamond na sasa Kiba, inaweza kumshusha hadhi, na hiyo ndiyo inamfanya Jokate ajute kujiingiza kwenye mapenzi na mastaa hao,” kilifunguka chanzo hicho.


ALIPASWA KUWA BUNGENI?
Hata hivyo, baadhi ya watu wake wa karibu walikwenda mbele zaidi na kusema kwa muonekano wake alipaswa kuwa mjengoni (bungeni) akitema madini, kwani hawana hofu na elimu yake ila tatizo ni hilo tu la ‘kurukaruka’ na wasanii.
 “Kiukweli Jojo (Jokate) anastahili kuwa bungeni akitafuta njia mbadala ya kutatua matatizo ya wananchi wake wa jimbo lake f’lani hivi.
“Au kama anataka kuendelea na mapenzi kwa kuwa ameachana na Kiba basi atafute mtu wake na kutulia naye kwani kuna baadhi ya warembo wenye majina wana watu wao na wametulia wanafanya mambo ya kujenga taifa,” alisema mmoja wa watu hao.

HUYU HAPA JOKATE
Baada ya kunyetishiwa ‘ubuyu’ huo, Wikienda lilimtafuta mlimbwende huyo na kumfikishia madai hayo kisha kumweleza mabadiliko wanayotaka mashabiki na watu wake wa karibu ambapo alikuwa na haya ya kusema:

 “Siku zote ninavyojua mimi mapenzi hayachagui, suala la kumpenda nani kwa maana ya staa, kiongozi, fukara, mwenye elimu au asiyekuwa nayo na wengineo ni matakwa ya moyo wangu kutokana na ulipodondokea.
“Kama ni ishu ya kuwa bungeni ni suala la muda, wakati ukiwadia basi kila kitu kitakuwa sawa. Kama ni mchumba wasubiri watamuona siku ya ndoa lakini hao wengine wala sijatoka nao!”

KABLA YA DIAMOND, KIBA
Ukiachilia mbali Diamond na Kiba, pia Jokate aliwahi kukiri na kuripotiwa kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Mbongo anayekipiga kwenye Ligi ya Kikapu ya Marekani, NBA, Hasheem Thabeet.

Upinzani Bungeni, Wagoma Kusoma Hotuba Baada ya Kushinikizwa Kufuta Maneno

$
0
0
Godless Lema:Baada ya kamati ya kanuni na uongozi wabunge kuifanyia kazi na kuondoa vipengele hotuba ya kambi ya upinzani mambo ya ndani kama mauwaji ya kisiasa. Nyumba za serikali, Mkataba wa Lugumi, uchaguzi wa Zanzibar sakata la NIDA na Wizi wa Rada.Tumeamua kuiondoa hotuba Yote.


Makosa ya Mwanaume yanayosababisha Mke Amsaliti

$
0
0
Kuna sababu anuai zinazomfanya mwanamke amsaliti mumewe. Ni muhimu kutambua kuwa mwanamke ni kiumbe mwenye hisia kali na daima ahisi raha na amani. Baadhi ya nyakati hufanya usaliti ili kuziba pengo la upungufu unaotokea katika maisha yake. Zifuatazo ni sababu kubwa ambazo zinamfanya amsaliti mumewe:

1. KUTOMPA KIPAUMBELE NA KUTOMTHAMINI

Tunatambua kuwa mke anafanya kazi kubwa sana ambayo lau kama ingekuwa ni kampuni basi pangehitajika watu zaidi ya 10 kuzifanya. Atamtunza mume, watoto, nyumba na familia kwa ujumla.

Wakati fulani mume anaweza akampuuza na asimthamini, licha ya kujitoa kwa moyo wote kumtunza na kuihudumia familia. Hivyo, kutotoa kipaumble kwa mke ni kosa kubwa ambalo linaweza likamgharimu mume, mke akipata mtu anayempa kipaumbele na kumuonesha thamani hakika hataacha kuitumia hiyo fursa.

2. UKOSEFU WA MAHABA

Kwa asili mwanamke ana silika ya hitajio la kupendwa, mwanamke anahitaji kupendwa, mwanaume yeye ana silika ya kupenda ngono, ukimpa ngono tu basi anaridhika.

Mwanamke anahitaji kupetiwapetiwa, anahitaji kudekezwa, anahitaji aambiwe maneno yenye ladha adimu yaliyochanganywa na vionjo vya ndimu, mwanamke anataka hivyo, anataka aone kama anapendwa, anataka aone mtu anamwambia vile alivyo, alivyo maridhawa, amueleze hisia zake, ampe lugha ya kimajnun, mwanamke anamtaka Majnun. Sasa akimpata mtu wa aina hiyo, tofauti na mumewe, huwa ni balaa tupu, mnanipata hapo?

3. USALITI WA MUME

Miongoni mwa mambo ambayo huibadilisha roho ya mwanamke ni pale anapogundua kuwa mumewe kipenzi anamsaliti. Hapo mwanamke anaweza akabadilika kabisa. Wapo wanaosamehe, lakini wapo wanaolipiza kisasi.

4. KUTOJIAMINI

Mwanamke anahitaji mwanaume anayemfanya ajiamini iwapo mumewe hatekelezi jukumu hilo, akimpata mtu anayemfanya ajiamini, yanaweza kutokea mengine kabisa. Hivyo, nasaha zangu kwa kaka zangu kuyaangalia kwa makini mambo haya.

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya May 17, Ikiwemo Siri ya Kuzuia Hotuba ya Upinzani Bungeni

$
0
0

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya May 17, Ikiwemo Siri ya Kuzuia Hotuba ya Upinzani Bungeni

Aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue Sasa Amestaafu Bila Kupangiwa Kazi Nyingine!

$
0
0
Aliyekuwa Katibu mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue sasa amestaafu bila kupangiwa kazi nyingine kama alivyoahidiwa na Rais John Magufuli siku aliyomteua Balozi Injinia John Kijazi kushika wadhifa huo na hivyo Balozi Sefue kutolewa kwa madai ya kupangiwa kazi nyingine.

Tarehe 6 mwezi Machi Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli alimteua John William Kijazi kushika wadhifa wa Katibu Mkuu kiongozi wadhifa ambao hapo kabla ulikuwa ukishikiliwa na Balozi Ombeni Sefue.Balozi Sefue alieteuliwa tena na Rais Magufuli Desemba 20, 2015 kuendelea kushika wadhifa huo kwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya utumishi wake wa umma kuisha sambamba na makatibu wakuu na manaibu 50.

Katika uteuzi ule wapo makatibu wakuu na manaibu walioachwa akiwemo Dkt.Donald Mbando (Afya),Balozi Liberata Mulamula (Mambo ya Nje), Omari Chambo (Nishati na Madini), Jumanne Sagini(Tamisemi) na Joyce Mapunjo (Afrika ya Mashariki).Balozi Sefue alirudishwa tena lakini ghafla Machi 6 alisimamishwa na kumpisha Kijazi kwa maelezo kuwa atapangiwa kazi nyingine.

Lakini sasa imethibitika kuwa Balozi Sefue hatapangiwa kazi nyingine na kwamba muda wake wa kustaafu ulifika na hivyo hawezi kuendelea tena na utumishi wa umma.Akijibu maswali ya mwandishi wa gazeti la Mwananchi juu ya hatma ya makatibu wakuu na manaibu makatibu wakuu walioahidiwa kupangiwa kazi nyingine ,Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) Dkt Laurean Ndumbaro alisema kuwa makatibu wakuu wote wamepata barua zao na hakuna ambae hana kazi isipokuwa kwa wale waliostaafu kwa mujibu wa sheria kama Balozi Sefue, Balozi Mulamula na Chambo ambao hana uhakika kama wanaweza kupangiwa majukumu mengine.

Swali ni je kama aliongezewa mwaka mmoja wa mkataba katika utumishi wa umma alipotolewa kwenye nafasi ile mara baada ya ueuzi kutenguliwa na Kijazi kuchukua nafasi yake mkataba wake ulivunjwa?Kama haukuvunjwa analipwa mshahara mpaka sasa kwa kazi gani anayoifanya?Kama ulivunjwa je Rais alimdanganya?

Chanzo: Tanzania Investiment Adventures

Lema Amwaga Sumu Bungeni Kuhusu Staili ya Utawala wa Rais Magufuli..Adai Taifa Linahitaji Maombi

$
0
0
GODBLESS Lema, Mbunge wa Arusha (Chadema) leo amemwaga sumu bungeni kuhusu staili ya utawala wa Rais John Magufuli, anaandika Faki Sosi.

Amesema, kwa namna Rais Magufuli anavyoendesha nchi, taifa linahitaji maombi ya haraka kuhakikisha anarudishwa kwenye mstari wa maadili kwa manufaa ya nchi.

Akisoma Makadirio na Mapato katika Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Lema ambaye ni msemaji wa kambi ya upinzani kwenye wizara hiyo amesema, Rais Magufuli ataumiza  watu wengi.

“Wakati Taifa letu linapita kwenye changamoto nyingi kama vile ukosefu wa sukari, umeme, umasikini, mizigo kupungua bandarini, madini ya Tanzanite kuanguka bei na ubadhirifu uliokithiri katika mfumo wa utawala. Rais mwenyewe ameonekana kufuatilia na kufanyia kazi habari za kwenye mitandao ya kijamii.

“Kwa tabia hii ya Rais Magufuli, kama Taifa tunahitaji maombi haraka, kwani Rais ataumiza  watu wengi  sana kwa kufuatilia  maneno ya mitaani kwa njia mbalimbali , kwani kwa madaraka  aliyonayo  Rais bila shaka ataumiza watu wengi.

“Mfano, Sakata la Mke wa Waziri Mahiga na Trafiki barabarani. Ni jambo dogo sana na la karaha kuona linazingatiwa na Rais,” amesema Lema.

Amesema, haikuwa  busara Rais Magufuli kukemea familia ya waziri wake mbele ya vyombo vya habari na kuagiza askari  huyu kupandishwa cheo bila kujua historia ya utumishi wake.

Lema alikumbusha kwamba, wabunge walipoanza vikao vya Kamati za Bunge, vyombo vya habari vilimnukuu Rais Magufuli akielezea mpango wake wa kuanza kurekodi  mawaziri wake wanaolalamika juu ya staili yake ya uongozi.

“Kwa hiyo leo ukienda kwenye ofisi za mawaziri unaona, hofu, mashaka, kutokujiamini, mambo yatakayo punguza ufanisi, ubunifu na uhuru katika utendaji wao, jambo linalopeleka Taifa kuzorota katika nyanja zote kwa utumishi wa umma jambo ambalo ni hatari kwa Taifa,” amesema.
Akizungumzia mashaka ya nchi Lema amesema,

Taifa letu liko katika mashaka na kuwa, serikali inaufahamu ukweli huu.
“Taifa hili lina utulivu unaosabishwa na hofu inayojengwa kwa mabavu  na silaha  na sio amani, kuna mateso makubwa wanayoyapata wananchi wa Taifa hili kila siku, umasikini, njaa, ukandamizwaji, ubaguzi, uonevu, udhalilishwaji na mateso ya jinsi mbali mbali kutokana na kukosa uongozi unaojali maisha ya Watu,” amsema na kuongeza;

“Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni baada ya uchambuzi na tathimini ya “Hali ya Usalama na Amani ya Nchi yetu”  kabla wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2015,  tumebaini kuwa nadharia na mwenendo wa demokrasia ya vyama vingi hapa nchini iliwekwa kando.

“… na badala yake sura nzima ya uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2015, uligeuka kuwa ‘Military Operation’ yaani ‘Operesheni ya Kijeshi’ kwa kisingizio cha kulinda amani.”

Lema amesema, mnyonge anayelia moyoni kwa huzuni ya kuonewa ni hatari kwa usalama wa nchi na dunia na kwamba, vikundi vingi vya uhalifu duniani kwa asilimia kubwa vimesababishwa na utawala wa kibabe, uonevu na ukandamizwaji usiovumilika na huko ndiko tunakoelekea  kama Taifa.
Amesema, “matendo mabaya haya yaliofanyika wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita Zanzibar na Tanzania Bara ni ishara ya watawala kuelekeza Nchi yetu katika mapigano ya sisi kwa sisi katika siku za usoni.

“Unapokuwa na Jamii inayoamini kuwa  mfumo wa demokrasia hauwezi kuwapa wananchi viongozi wanaowataka, maana yake ni dhahiri kwamba unaanza kuifundisha jamii hiyo kufikiri njia mbadala ya mabadiliko  katika Nchi.”

Amesema kuwa, Tume ya Uchaguzi  inayotiliwa shaka na jamii ni hatari kwa usalama wa nchi  na kwamba, ni muhimu kwa taifa kutafakari uwepo wa katiba ya wananchi na Tume Huru ya Uchaguzi itakayorudisha imani ya Wananchi katika uchaguzi wa kidemokrasia.

“Mungu adhihakiwi apandacho mtu ndicho avunacho, utulivu mnaouona Zanzibar na kwingine kokote kule kuliko na ukandamizaji ni nafsi zinazojadili mwelekeo mpya wa maisha yao katika utawala wa nchi yao.

“Zanzibar  mmeshinda uchaguzi  kwa hila na sio  kwa haki, wekeni kumbukumbu maneno ya Kambi Rasmi ya Upinzani  leo  kuwa,  ipo siku Zanzibar itakuwa ni sehemu ngumu ya kuishi binadamu kama hamtachukua hatua sasa ya kurekebisha mlichokifanya  Zanzibar  na Tanzania Bara katika uchaguzi uliopita,” amesema.

Hata hivyo amehoji kwamba, kwa namna mambo yanavyoendeshwa nchini, je kuna matarajio ya taifa kuingia kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2020 kwa njia ya kidemokrasia?

Chanzo:Mwanahalisi

Mganga wa Kienyeji Ambaka Mgonjwa wake

$
0
0
Mganga wa Kienyeji Hamza Saidi,(40) anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kumbaka mgonjwa aliyekwenda kutibiwa masikio kwenye ofisi ya mganga huyo.

Mganga huyo, Mkazi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji anatuhumiwa kumbaka msichana wa miaka 20, na kumsababishia maumivu makali.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa Kigoma SACP Fredinandi Mtui alisema, mganga huyo alifanya tukio hilo, Mei 15 majira ya saa tano asubuhi.

Inadaiwa kuwa msichana alifika  nyumbani kwa mganga huyo akiwa na lengo la kutibiwa masikio lakini mganga alimwambia ili dawa hiyo ifanye kazi ni lazima afanye naye mapenzi kwanza.

“Alimrubuni kuwa dawa ya sikio ili ifanye kazi inatakiwa afanye tendo la ngono na kwa ujanja huo , alimbaka msichana huyo,” alisema Kamanda.

Kamanda Mtui alisema kwa sasa mganga huyo anashilikiwa na polisi na atafikishwa mahakamani wakati wowote.

Katika tukio jingine, mkazi wa Mvinza,  kata ya Kagera Nkanda Josephine Ntahukisiga  (42) ambaye ni mkulima amekutwa akiwa amejinyonga ndani ya nyumba ya baba yake kwa kutumia shuka.

Tukio hilo lililotokea Mei 14, 2015 inaelezwa kuwa  Ntahukisiga alivizia ndugu zake wakiwa wamelala ndipo alipoenda sebuleni na kujinyonga kwa kutumia shuka kwa kulifunga juu ya dari.

Kwa  mujibu wa baba wa marehemu, Andrew Ntahukisiga alisema marehemu alikuwa na msongo wa mawazo tangu watoto wake walipofariki kwa ajali ya moto mwaka 2015.

Kiongozi wa Upinzani Uganda Besigye Ashtakiwa Kwa Uhaini

$
0
0
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda,  Kizza Besigye ameshtakiwa kwa kosa la uhaini baada ya kujitangaza mshindi wa uchaguzi uliofanyika hivi karibuni.

Alikamatwa baada ya kuandaa sherehe zake mwenyewe za kuapishwa kabla ya sherehe za kuapishwa kwa Rais Yoweri Museveni
aliyechaguliwa kwa muhula wa tano.

Kiongozi huyo amekuwa kizuizini muda mwingi tangu February mwaka huu. Rais Museveni amekanusha madai ya kuiba kura.

Ulinzi ulikuwa umeimarishwa kwenye sherehe za kuapishwa kwa Museveni Alhamis iliyopita ikiwa pamoja na kuzuiliwa kwa maandamano ya upinzani.

Serikali iliwaonya waandishi habari kutoripoti maandamano yoyote.

Mitandao ya kijamii kama vile Whatsapp, Facebook na Twitter
Ilizuiliwa kwa agizo la serikali ikidai ni sababu za kiusalama.

Zitto Kabwe amtaka Nape aziagize redio na TV za TZ zicheze asilimia 80 nyimbo za nyumbani

$
0
0
May 13 2016 ilikuwa ni siku ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwasilisha Bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2016/2017 .

Hotuba hiyo iliyosomwa na Waziri, Nape Nnauye ambapo kiwango kilichoombwa kilikuwa ni shilingi 20,326,176,000.

Wabunge mbalimbali walichangia bajeti hiyo huku Mbunge wa Kigoma, Zitto Kabwe yeye alikuwa na haya ya kusema katika uchangiaji wake wa Wizara hiyo kuhusu muziki wa nyumbani:

“Leo hii ukifungua Redio au TV za hapa nyumbani zote asilimia nyingi utakuta wanapiga nyimbo za nje tu. Leo hii ukienda nchi za watu kuna limit mfano ukienda Lagos,Nigeria ukisikia nyimbo ya msanii wa huku kwetu basi ujue lazima atakuwa amefanya na msanii wao yaani wana promote wasanii wao, sasa sisi sijui ni ulimbukeni wa ukoloni wa miaka hamsini bado haujatutoka. Nape hili lipo kwako kama unataka kuwatetea wasanii hili wala halihiitaji kubadilisha sheria na kanuni za kontenti zipo chini ya waziri. Toa kanuni TCRA wazibariki kuwa asilimia 80 ya nyimbo zitakazopigwa kwenye redio na TV zetu ziwe za wasanii wetu wa Tanzania basi,” alisema Zitto.

Utanashati Wamponza Ommy Dimpoz..Wadau Wamchana Kwa Kujipamba Sana

$
0
0
Msanii mkali wa muziki, Ommy Dimpoz amesema haumizwi kichwa na kauli mbalimbali za mashabiki wake wa kwenye mitandao ya kijamii ambao wanadai kuwa anajipamba kuzidi.

Akizungumza katika kipindi cha Sporah Show cha Clouds TV, Ommy amesema yeye haumizwi na kauli hizo kwa kuwa anajijua yeye ni mwanaume wa aina gani.

“Ndo nasema haya maneno ya kwenye mitandao mimi hayaniathiri,” alisema Ommy Dimpoz.

“Mimi siwezi sema nipo tofauti na wanaume wengine, mimi nipo kawaida. Kwahiyo suala la kujipenda linaendana na hobby, kwa mfano kuna wanaume wanafanya vitu nasema no, huwezi mwanaume ukafikia kufanya hivi,” aliongeza Ommy Dimpoz.

Muimbaji huyo wa wimbo ‘Achia Body’, amesema swala la muonekano wake linamfanya achukue muda mrefu kujiandaa ili aweze kwenda sehemu.

Ray Kigosi Apata Shavu Nchini Rwanda

$
0
0
Msanii wa filamu, Vincent Kigosi ‘Ray’ hivi karibuni ametimkia nchini Rwanda baada ya kualikwa nchini humo kwa ajili ya kuandaa filamu maalum ambayo itashirikisha wasanii wa Tanzania na Rwanda.

Kupitia instagram, Ray ameandika:
Nipo nchini Rwanda nimekuja kushoot movie inayoshirikisha nchi mbili Tanzania na Rwanda ni msanii pekee toka Tanzania niliyechaguliwa kuja kufanya movie hapa nchini Rwanda nina imani sitowaangusha Watanzania wenzangu hapa ni kazi tu.
Katika hatua nyingine leo ni siku ya kuzaliwa ya Vincent Kigosi, ambapo wasanii mbalimbali pamoja na mashabiki wake wa filamu wamekuwa wamtakia heri.

Mabasi ya Mwendo Kasi ( Dart ) Yaanza kwa Changamoto Lukuki....... Mfumo wa Kukatia Tiketi Walalamikiwa, Walimu nao Walalamika Kutotambuliwa

$
0
0
Huduma  ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka imeanza rasmi jana jijini Dar es Salaam huku yakilalamikiwa na watumiaji wakiwemo baadhi ya watu waliokuwa na msamaha wa kusafiri bila kutoa nauli, ambao sasa hawatambuliwi na mfumo mpya.

Utaratibu uliokuwa umezoeleka awali wa askari wa polisi, jeshi, magereza na walimu kutolipa nauli kwenye usafiri wa daladala, umeonekana kugonga mwamba chini ya mabasi hayo.

Jana  mwalimu ambaye hakufahamika jina lake alisikika akitaka mwongozo wa kutolipa nauli kwa kuwa yeye ni mwalimu.

“ Mama mfumo huu haumtambui mwalimu, askari,” alimjibu mmoja wa wahudumu wa UDA-RT aliyekuwa akihakiki tiketi za abiria kabla ya kupanda basi.

Akijibu hoja hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa UDA-RT, David Mgwasa alisema mwongozo uliotolewa na Sumatra, unamtambua mwanafunzi pekee ambaye anatakiwa kulipa Sh 200, wengine wote wanatakiwa kulipa nauli.

Mbali na walimu, askari, pia watu wenye ulemavu ambao walikuwa hawalipi nauli kwenye daladala, kwenye mfumo wa mabasi yaendayo haraka wanatakiwa kulipa.

Mambo mengine yaliyolalamikiwa ni mfumo wa ukataji tiketi, ambao unadaiwa kusababisha foleni ndefu huku wahudumu wakiwa hawana chenji, jambo lililosababisha baadhi ya watu kulipa kiasi kikubwa cha fedha.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya abiria walisema walilazimika kukaa zaidi ya dakika 20 vituoni kutokana na kusubiri chenji na wengine kuamua kuacha fedha zao.

“Nimetoa Sh 1,000, nimepewa tiketi na kurudishiwa Sh 200 na kuwa hana Sh 150. Hapa inaonesha nimesafiri kwa Sh 800. Nauli hii ningeitumia kupanda daladala na kuzunguka nalo ili nipate kiti, ningepandia upande wa pili ningetumia Sh 500,” alisema Kasum Swakala, mkazi wa Ubungo Bonyokwa.

“Nina haraka na siwezi kuipata hiyo 150 ambayo hawajanipa katika chenji yangu, inabidi tu kuondoka ili kuwapisha wengine lakini hali hii inatuumiza sana na siyo sawa kwa sababu kesho siwezi kurudi kuwadai chenji yangu,” alisema.

“Nimetoka Mbezi na kulipa 400, nimefika hapa wanasema hawana cheji kama nataka nilipe 800, siwezi kulipa kiasi hicho naenda kupanda daladala.”

Meneja Uhusiano wa UDA-RT, Deus Bugaywa alikiri kuwapo changamoto ya chenji na kusema asubuhi walikuwa na chenji nyingi ambazo ziliisha haraka hivyo kuleta usumbufu kwa baadhi ya abiria.

Mkazi wa Mbezi, Laurence Msuya alilalamikia hatua ya kukata tiketi mara mbili na kusema imesababisha usumbufu kwao kwa kupoteza muda. Wakala wa kukatisha tiketi katika kituo cha Mbezi alilalamikiwa kuchelewa kufika  jambo lililozidisha msongamano.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya UDA-RT, David Mgwasa alisema hali hiyo itaondoka pale mfumo wa kadi utakapoanza kufanya kazi.

“ Wananchi tuliwafundisha namna ya kutumia kadi, na siku moja kabla Serikali ikazuia matumizi yake, sasa tunasubiri maamuzi ili tuanze kuuza. Tulijua wananchi wangekuwa na kadi na wale wachache ambao ni wanafunzi na wale wanatumia mara moja moja ndio wangetumia tiketi za karatasi,” alisema Mkurugenzi wa Uendeshaji na Usimamizi wa Miundombinu wa Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart), John Shauri

Alisema mfumo wa tiketi za kadi uko katika hatua za mwisho na mazungumzo. “ Ilikuwa ni lazima tuanze tiketi za karatasi, kwani tutakuwa na mifumo miwili inayofanya kazi hii ya tiketi za karatasi na kadi, mambo yakiwekwa sawa kadi zitaanza kutumika,” alisema.

Changamoto nyingine katika huduma hiyo iliyofanywa na baadhi ya wakala wa kukatisha tiketi kuzongwa au kutakiwa kutoa ufafanuzi ni pamoja na abiria kupewa tiketi za wanafunzi wakati wamelipa nauli ya watu wazima.

Baadhi ya abiria walijikuta wakikata tiketi nyingine kutokana na za awali kuisha muda wake. Hali hiyo ilitokana na wakazi hao kukata tiketi na kwenda kwenye shughuli zao nyingine na walipofika kituoni na kukuta muda wake umeisha walilazimika kukata nyingine.

“Awali walisema hizi tiketi unaweza kupandia basi wakati wowote lakini nashangaa leo nimekata tiketi nikaamua kwenda kwenye shughuli nyingine. Nimerudi hapa wakati tiketi inakaguliwa ikagoma kusoma kwa madai kuwa muda wake wa matumizi umeisha,” alisema mmoja wa wakazi wa Kimara Mwisho.

Akijibu hoja hiyo, Mgwasa alisema tiketi za karatasi zinatakiwa kutumika kwa safari moja na kuwa zinadumu kwa saa mbili kabla ya kuisha muda wa matumizi na ametumia fursa hiyo kuwasihi wananchi kukata tiketi pale tu wanapotaka kusafiri.

Tiketi zilizokuwa zikitolewa na mawakala wanaohusika zilikuwa hazina maelezo ya nauli waliyolipa abiria zaidi ya kuonesha tarehe, muda uliokata, kituo ulichokatia jambo ambalo liliwafanya abiria kuhoji na kuona ni ujanja wa kupoteza mapato ya serikali.

Mahausigeli 15 waliokuwa wakipelekwa Oman wanaswa

$
0
0

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewakamata wasichana 15 katika nyumba iliyopo maeneo ya Ukonga, waliokuwa tayari kusafirishwa kwenda Oman kufanya kazi za ndani.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi wa kanda hiyo, Simon Sirro, alisema wasichana hao walikamatwa baada ya Polisi kupata taarifa toka kwa msiri kuwa kuna mtu amewaweka wasichana kwa ajili ya kuwasafirisha.

Sirro alisema Polisi walifuatilia na kufika katika eneo hilo na kufanikiwa kuwakuta katika nyumba ya Hadija Mohamed (40) wakiwa wamegawanywa katika vyumba viwili.

Alisema uchunguzi wa awali, umebaini kuwa mwanamke huyo anashirikiana na mwenzake Salma Habibu (43) mkazi wa Temeke kuwatafutia masoko nchini Oman na wao ni mawakala wanaoletewa kutoka mikoani na kuwapokea kwa ajili ya kuwasafirisha.

Aidha alisema watuhumiwa hao watapelekwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

Pia ametoa onyo kwa watu wenye tabia hiyo kuacha, kwani wasichana hao wakifikishwa nje ya nchi hufanyiwa vitendo vya kikatili na unyanyasaji.

Katika tukio jingine, Polisi kanda hiyo imewakamata vijana 75, ikiwa ni muendelezo wa msako wa vijana wanaofanya matukio ya wizi wa majimbani nyakati za usiku.

Mabasi ya Mwendo Kasi ‘Yawatema’ Askarina Walimu

$
0
0

HUDUMA ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka imeanza rasmi jana jijini Dar es Salaam huku yakilalamikiwa na watumiaji wakiwemo baadhi ya watu waliokuwa na msamaha wa kusafiri bila kutoa nauli, ambao sasa hawatambuliwi na mfumo mpya.

Utaratibu uliokuwa umezoeleka awali wa askari wa polisi, jeshi, magereza na walimu kutolipa nauli kwenye usafiri wa daladala, umeonekana kugonga mwamba chini ya mabasi hayo. HabariLeo ilishuhudia mwalimu ambaye alikataa kutaja jina lake akitaka mwongozo wa kutolipa nauli kwa kuwa yeye ni mwalimu.

“ Mama mfumo huu haumtambui mwalimu, askari,” alimjibu mmoja wa wahudumu wa UDA-RT aliyekuwa akihakiki tiketi za abiria kabla ya kupanda basi.

Akijibu hoja hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa UDA-RT, David Mgwasa alisema mwongozo uliotolewa na Sumatra, unamtambua mwanafunzi pekee ambaye anatakiwa kulipa Sh 200, wengine wote wanatakiwa kulipa nauli.

Mbali na walimu, askari, pia watu wenye ulemavu ambao walikuwa hawalipi nauli kwenye daladala, kwenye mfumo wa mabasi yaendayo haraka wanatakiwa kulipa.

Mambo mengine yaliyolalamikiwa ni mfumo wa ukataji tiketi, ambao unadaiwa kusababisha foleni ndefu huku wahudumu wakiwa hawana chenji, jambo lililosababisha baadhi ya watu kulipa kiasi kikubwa cha fedha.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya abiria walisema walilazimika kukaa zaidi ya daika 20 vituoni kutokana kusubiri chenji na wengine kuamua kuacha fedha zao.

“Nimetoa Sh 1,000, nimepewa tiketi na kurudishiwa Sh 200 na kuwa hana Sh 150. Hapa inaonesha nimesafiri kwa Sh 800. Nauli hii ningeitumia kupanda daladala na kuzunguka nalo ili nipate kiti, ningepandia upande wa pili ningetumia Sh 500,” alisema Kasum Swakala, mkazi wa Ubungo Bonyokwa. “Nina haraka na siwezi kuipata hiyo 150 ambayo hawajanipa katika chenji yangu, inabidi tu kuondoka ili kuwapisha wengine lakini hali hii inatuumiza sana na siyo sawa kwa sababu kesho siwezi kurudi kuwadai chenji yangu,” alisema.

“Nimetoka Mbezi na kulipa 400, nimefika hapa wanasema hawana cheji kama nataka nilipe 800, siwezi kulipa kiasi hicho naenda kupanda daladala.”

Dada mmoja ambaye awali alimuuliza mwandishi eneo la kukatia tiketi baada kushuka na basi la Mbezi. Meneja Uhusiano wa UDA-RT, Deus Bugaywa alikiri kuwapo changamoto ya chenji na kusema asubuhi walikuwa na chenji nyingi ambazo ziliisha haraka hivyo kuleta usumbufu kwa baadhi ya abiria.

Mkazi wa Mbezi, Laurence Msuya alilalamikia hatua ya kukata tiketi mara mbili na kusema imesababisha usumbufu kwao kwa kupoteza muda. Wakala wa kukatisha tiketi katika kituo cha Mbezi alilalamikiwa kuchelewa kufika kwa jambo lililozidisha msongamano.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya UDA-RT, David Mgwasa alisema hali hiyo itaondoka pale mfumo wa kadi utakapoanza kufanya kazi.

“ Wananchi tuliwafundisha namna ya kutumia kadi, na siku moja kabla Serikali ikazuia matumizi yake, sasa tunasubiri maamuzi ili tuanze kuuza. Tulijua wananchi wangekuwa na kadi na wale wachache ambao ni wanafunzi na wale wanatumia mara moja moja ndio wangetumia tiketi za karatasi,” alisema Mkurugenzi wa Uendeshaji na Usimamizi wa Miundombinu wa Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart), John Shauri alisema mfumo wa tiketi za kadi uko katika hatua za mwisho na mazungumzo. “ Ilikuwa ni lazima tuanze tiketi za karatasi, kwani tutakuwa na mifumo miwili inayofanya kazi hii ya tiketi za karatasi na kadi, mambo yakiwekwa sawa kadi zitaanza kutumika,” alisema.

Changamoto nyingine katika huduma hiyo iliyofanywa na baadhi ya wakala wa kukatisha tiketi kuzongwa au kutakiwa kutoa ufafanuzi ni pamoja na abiria kupewa tiketi za wanafunzi wakati wamelipa nauli ya watu wazima. Baadhi ya abiria walijikuta wakikata tiketi nyingine kutokana na za awali kuisha muda wake.

Hali hiyo ilitokana na wakazi hao kukata tiketi na kwenda kwenye shughuli zao nyingine na walipofika kituoni na kukuta muda wake umeisha walilazimika kukata nyingine.

“Awali walisema hizi tiketi unaweza kupandia basi wakati wowote lakini nashangaa leo nimekata tiketi nikaamua kwenda kwenye shughuli nyingine. Nimerudi hapa wakati tiketi inakaguliwa ikagoma kusoma kwa madai kuwa muda wake wa matumizi umeisha,” alisema mmoja wa wakazi wa Kimara Mwisho.

Akijibu hoja hiyo, Mgwasa alisema tiketi za karatasi zinatakiwa kutumika kwa safari moja na kuwa zinadumu kwa saa mbili kabla ya kuisha muda wa matumizi na ametumia fursa hiyo kuwasihi wananchi kukata tiketi pale tu wanapotaka kusafiri.

Tiketi zilizokuwa zikitolewa na mawakala wanaohusika zilikuwa hazina maelezo ya nauli waliyolipa abiria zaidi ya kuonesha tarehe, muda uliokata, kituo ulichokatia jambo ambalo liliwafanya abiria kuhoji na kuona ni ujanja wa kupoteza mapato ya serikali.
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>