Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Mchezaji Ibrahim Ajib wa Tanzania Afuzu Majaribio Afrika Kusini

$
0
0
Mshambuliaji wa Simba SC, Ibrahim Ajib amefuzu majaribio katika klabu ya Lamontville Golden Arrows FC ya Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini.

Hata hivyo, klabu hiyo haiko tayari kumnunua mchezaji huyo bali inataka kumchukua kama mchezaji huru na kumsainisha Mkataba.

Kwa sababu hiyo, klabu hiyo imemuambia Ajib arejee Dar es Salaam kuangalia kama mkataba wake umekwisha apeleke uthibitisho Afrika Kusini ili apewe Mkataba Arrows.

Wakala wa mchezaji huyo, Juma Ndabila amesema kuwa Ajib amefuzu majaribio, lakini kuna suala la mkataba ambapo Simba wanasema bado ana mkataba ingawa mkataba wake umeisha.
Aidha, wakala huyo amesema kuwa wanarejea leo Dar es Salaam pamoja na Ajib.

Kwa upande wake, wakala aliyemuunganishia majaribio Hajib Afrika Kusini, Rodgers Mathaba amesema kwamba mchezaji huyo amepewa fursa ya kurudi Arrow wakati wowote akiwa mchezaji huru.

Madee Adai Muziki wa Hip Hop Unapendwa na Wahuni Ambao Hawawezi Kununua Kazi za Wasanii

$
0
0
Msanii wa muziki kutoka Tip Top Connection Madee amefunguka na kueleza ni kwanini wasanii wengi wa muziki wa Hip Hop nchini wanashindwa kufanya vizuri licha ya nyimbo zao kupendwa mitaani.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na video yake ya wimbo, Migulu Pande, ameiambia Times Fm kuwa Hip Hop inapendwa na kundi la ‘wahuni’ wachache na machizi mtaani ambao ni ngumu kwenda dukani kununua kazi anayoipenda.

Katika hatua nyingine, Mdee amesema kama yeye angeendelea kudumu na staili yake ya kurap kama zamani mpaka sasa, angekuwa amekwisha potea kwenye ‘Game’ na ulimwengu wa muziki.

“Watu wanataka changes, kama biashara haikulipi kwanini uendelee kufanya inakuingizia hasara kila kukicha, ningekuwa narap mpaka leo nisingekuwepo kwenye game ningepotea, dunia yenyewe inabadilika sasa kwa nini wewe usibadilike” alisema Madee.

Wosia wa Le Mutuz kwa Wanaowaza Kwenda Kuishi nje ya Nchi..

$
0
0
Leo i want to touch this very sensitive subject ya wanaodai kuwa inapokuja kwenye diaspora huenda nina wivu na chuki na wanaoishi majuu kwa sababu nilirudi, ha! ha! ha! kwa wale ambao hamjafika majuu naomba kusema hivi:- mungu alinijalia sana confidence in myself na everything i do, nilipofika majuu kwa mara ya kwanza nilikuta wabongo karibu wote pale New York wanafanya kazi za kulinda na kutunza wazee na mataharia, siku moja mbongo mmoja alinipeleka kwenye kazi ya kutunza mataahira nilikaa kama lisaa limoja tu sikurudi tena, nikaenda shule kutafuta leseni ya cdl ya kuendesha malori makubwa sana ambayo hapa bongo hayapo, kazi ambayo inalipa haswa nikahangaika mpaka nikapata ile leseni nikiwa ninafanya kazi gas station mchana na usiku Kentucky Fried Chicken. Nilipopata leseni nikaanza kuendesha malori America nzima. Wale wabongo niliowakatalia zile kazi zao wakaanza kunizushia maneno kwamba ninauza unga, ha! ha! ha! ha!,

Kabla ya kwenda New York nilishakuwa baharia Belgium so Ulaya haikuwa kitu kigeni kwangu, ndio maana siku moja nikaamua kurudi Bongo mwenyewe bila kulazimishwa na mtu. Cha kwanza nilipofika tu bongo nikaanza kunenepa, why? Kwa sababu ni kwa mara ya kwanza katika miaka 30 ya maisha yangu nimeweza ku-relax na maisha. Majuu ni kufanya kazi tu na kulipia madeni, wazungu sio wajinga wameitengeneza system yao to the point wewe unaenda kuchangia uchumi wao tu hauwezi kuwa tajiri maana uwezekano haupo, wewe ni kazi tu, social life hamna ni kazi tu kila ukikaa unawaza kazi, mabebez hamna, wachache wabongo waliopo ni hasara tupu wengi wao hawajitambui. Kwenye uzungu hawapo kwenye ubongo hawapo wapowapo tu ole wako uwaguse, i mean kila kitu majuu ni perfect lakini gharama yake haikupi nafasi wewe kuwa na pesa extra, ndio unagundua kwamba majuu sio kama ulivyotegemea maisha ni mazuri lakini magumu sana kurudi bongo nako huwezi maana ni noma zaidi so you are stuck, i was stuck too mpaka nilipoamua kwa hiari yangu kurudi home.

Hapa sina deni kwa mara ya kwanza katika maisha yangu, sidaiwi na mtu kila nilichonacho, kama ni gari ni langu, apartment ni yangu, shamba na nyumba ni vyangu sidaiwi na mtu, nafanya kazi ya kujiajiri, nakuja kazini saa ninayotaka, ninatoka saa ninayotaka, kwa mara ya kwanza ninamiliki simu za usd $ 1000 a piece majuu ningekuwa nayo ya kukopa na sikuwahi kuwanazo, bongo maisha baada ya kazi hayana mfano, marafiki kila kona kule unakuwa huna marafiki, bongo heshima kila kona majuu mweusi atakuheshimu nani? i mean kwenye kujiajiri nikipiga deal moja ikaitika millions zinakuwa zangu sio kulipia madeni, ninasafiri bongo na nje ya bongo anytime i want majuu nisingeweza maana ni kazi tu all the times.

Sasa naomba kuuliza jamani kweli niwaonee wivu na chuki waliobaki majuu kwa kisa gani? nasema hivi majuu wanatuzidi bongo kwa one thing matibabu wao wakiumwa kule ni rahisi sana kupona kuliko hizi hospitali zetu bongo, ni hilo tu mengine hapana bongo kuna maisha asikudanganye mtu, again mungu alinijalia moyo wa kujali yangu zaidi na sio ya wengine so kwa wale mnaolia lia kwamba nawaonea wivu eti mko majuu ha! ha! ha! ha! please!!, ninafanya biashara na wabongo wengi huko nje inapokuja kwenye kulipa ni kivumbi na patashika lakini hapa bongo ni tofauti watu wanalipa mara moja tena mpaka kwa dola za kimarekani, jamani kwa wale ambao hamjafika huko majuu na unaweza kula milo mitatu bongo bila tatizo tulieni hapa hapa jamani huko majuu kusikieni tu!!, ninamshukuru mungu kila siku kwa kunipa akili ya kwenda majuu na pia ya kurudi home ontime kabla sijachelewa, ndugu zangu huko rudini huku bongo maisha ni sawa ila tu ujipange kabla ya kuja na muhimu kuliko yote soma shule kwanza, huku bongo bila elimu utachekesha maana hela ukijanazo zitaisha kama huna elimu. jamani samahani kwa maelezo marefu lakini i hope nimemsaidia somebody out there!! - Le mutuz.

Rais Magufuli Atishia Kuwatumbua JIPU Mawaziri Wawili......Wenzao Wabaki Vinywa Wazi Kikaoni

$
0
0
Operesheni ya kutumbua majipu ya Rais John Magufuli nusura iwaangukie Mawaziri wawili ambao  pia walikuwa  manaibu  mawaziri katika Serikali ya Awamu ya Nne.

Taarifa kutoka katika chanzo cha kuaminiwa zimeeleza kuwa Rais Magufuli alionesha kutoridhishwa na utendaji wa Mawaziri hao na kuwafokea mbele ya mawaziri wenzao  kwa kuwataja majina katika kikao maalum cha mawaziri kilichofanyika hivi karibuni.

"Ni mazingira ambayo mawaziri hawakuyazoea kwamba Rais anawaambia moja kwa moja kwa majina, anafoka akisema anaweza kuwafukuza wakati wowote.....

"Mawaziri wamezoea mara kwa mara wanapofanya kosa au uzembe wanaonywa kwa staili tofauti, ni kama ya kistaarabu hivi. Sasa huyu bwana mkubwa hana mchezo, aliwataja kabisa, tena mbele ya wenzao ambao walibaki vinywa wazi.

“Wewe (anataja jina la Waziri) na mwenzako (anamtaja jina pia) nitawatumbua,” Chanzo cha gazeti la Rais Mwema kinamkariri Rais Magufuli.

Mawaziri hao ambao ni wabunge wa kuchaguliwa majimboni kwa upande wa Tanzania Bara, wanaongoza wizara nyeti ambazo zinasimamia sekta mtambuka, wizara ambazo zinagusa sehemu ya ahadi za mabadiliko alizonadi Magufuli wakati akigombea urais katika kampeni za mwaka jana.

Chanzo hicho kilieleza kuwa Rais Magufuli aliwaonya pia mawaziri wengine ambao alionesha kutoridhishwa na utendaji wao kwakuwa hawaendani na kasi yake ya kuwaletea wananchi maendeleo.

“Magufuli alitaka atoe mfano kwa mawaziri wengine kwamba wao si watu maalum sana. Kama wanavyotumbuliwa watu wengine na wao pia wanaweza kutumbuliwa,” kiliongeza chanzo hicho

Rais Magufuli aliunda Baraza lake la Mawaziri mwishoni mwa mwaka jana na kuwashauri wasifanye sherehe ya kuteuliwa kwakuwa wakifanya vibaya hatawaonea haya atawaondoa mara moja bila kujali majina yao.

Utendaji wa Rais Magufuli umeendelea kusifiwa kila kona hususan katika kuwawajibisha viongozi wa ngazi zote na kuonesha nia ya dhati ya kuwahudumia watanzania huku akipambana na uzembe na ufisadi.

IMEVUJA:Wema Sepetu na Petitman ndani ya bifu

$
0
0
 Imevuja! Urafiki wa muda mrefu wa muigizaji nyota, Wema Sepetu na mshika kamera wake, Petit Man umeingia dosari baada ya kudaiwa kuwa wawili hao wako ndani ya bifu, Risasi Mchanganyiko linakujuza.

Chanzo makini kililiambia gazeti hili kuwa Wema na Petit ambao hapo awali walikuwa wakiambatana kama kumbikumbi, kila kona walipoonekana, hivi sasa ni kama paka na panya kwani hakuna mawasiliano kati yao.


“Wema na Petit hali ya hewa imechafuka, kwa sasa hawaongei kabisa kwa sababu Muna ambaye ni rafiki yao wote anadaiwa kumwambia maneno yaliyomkasirisha madam kuhusu mpigapicha huyo na kusababisha bifu hilo kali,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kupata ubuyu huo, gazeti hili liliwatafuta wahusika na wa kwanza kupatikana alikuwa Petit Man, aliyekiri kuchafuka kwa hali ya hewa.

“Unajua mimi na Wema nipo naye kwa miaka tisa sasa na ni kama familia moja, hivyo tatizo lililopo kati yetu litaisha tu na kumalizwa kifamilia kwa hiyo watu wasilivalie sana njuga,” alisema.

Kwa upande wake Muna ambaye ni rafiki wa wote wawili, alisema anasikia watu wakizungumza kuhusu kuwagombanisha Petit na Wema, kitu ambacho alidai siyo kweli, kwani hawezi kuwagombanisha watu ambao ni kama ndugu na kwamba yupo tayari kusawazisha matatizo kati yao badala ya kuchochea.

“Mimi kwa kweli nawashangaa watu wanaosambaza hayo maneno ni kwa vile tu hawajui, mimi siwezi kuwagombanisha wale ni familia moja, waligombana kwa ishu zao wenyewe, sihusiki nazo na mara nyingi ninachofanya kama wana tatizo huwaweka sawa ili waendelee na uhusiano mzuri na si kuwagombanisha,” alisema Muna.

Lakini jitihada za gazeti hili kupata kauli ya Wema zilishindikana baada ya simu yake ya mkononi kuita bila kupokelewa hadi linaingia mitamboni.

Hii Ndio Hotuba ya Mbunge Godbless Lema iliyokataliwa Bungeni..Isome Hapa

$
0
0
HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KATIKA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI, MHE. GODBLESS JONATHAN LEMA (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAONI YA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA YA WIZARA HIYO, KWA MWAKA WA FEDHA 2016/2017

Inatolewa chini ya Kanuni ya 99 (9) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, toleo la Aprili, 2016.

______________________


1.0 UTANGULIZI


Mheshimiwa Spika, Kwa dhati namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kunijalia afya njema , nawashukuru pia Mke wangu Neema, Watoto wangu Allbless, Brilliant, Terrence na Precious Mawazo, pamoja na Wazazi wangu kwani wamekuwa msaada mkubwa sana kwangu katika shughuli zangu zote kwa maombi na sala . Kwani kufanya kazi ya Siasa za Mabadiliko Tanzania ni kazi ngumu na iliyojaa mateso, vitisho na hata kifo, lakini kwa ajili ya siku zao njema za baadae, ninapaswa kuendelea na kuvumilia katika kazi hii na wajibu huu muhimu ili kutafuta mwanga mpya wa Taifa letu katika siku za usoni.


Mheshimiwa Spika, Namshukuru Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Mhe. Freeman Aikael Mbowe kwa busara, ujasiri na maamuzi yake katika kuamua mambo yenye mwelekeo chanya katika Chama chetu na Nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, Nawapongeza pia wale wote waliojiunga na Chama chetu na Ushirika wetu wa Ukawa katika mwaka ule wa Uchaguzi hasa katika hatua za mwisho, nampongeza Mhe. Edward Ngoyai Lowassa na mke wake Mama Regina Lowassa ambaye ni mfano wa kuigwa, Mhe. Fredrick Tulaway Sumaye ambaye kwa sasa ni Mjumbe wa Kamati kuu wa CHADEMA na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru na wengine wengi kwa ujasiri na maamuzi mazito waliyofikia.


Mheshimiwa Spika, nina washukuru wananchi wa jimbo la Arusha Mjini kwa imani yao kubwa kwa Chama chetu na kwangu kwa kuweza kutupa madiwani 24 kati ya 25 na kufanikisha kuongoza Halmashauri ya Jiji la Arusha.


2.0 HALI YA USALAMA NA AMANI YA NCHI YETU


2.1 MAADILI YA FAMILIA


Mheshimiwa Spika, Taifa lolote Duniani msingi wake ni familia , hivyo njia sahihi ya Taifa kuwa na usalama wa kweli katika Jamii ni muhimu Serikali ikajua kuwa Jamii ni Familia, kuongelea hali ya usalama na amani ya Nchi yetu bila kuongelea maadili ya familia zetu ni kupotosha fikra zetu.


Mheshimiwa Spika, ukweli ni kwamba familia yenye maadili, wajibu na inayomcha Mungu ni jamii bora itakayozalisha Raia wema wenye wajibu na tija kwa Taifa, hatuwezi kuwa na Nchi yenye nidhamu na ustawi pasipo kuwa na familia zenye wajibu katika malezi .


Mheshimiwa Spika, Wazazi wengi leo tukiwemo Waheshimiwa Wabunge na Jamii ya kada mbali mbali tunafikiri kuwa tumekosa nafasi ya kukaa na familia zetu, na hivyo tumeamua ku- out source malezi ya Watoto wetu na familia zetu, hivyo watoto wengi wanao kuwa katika karne hii, ni watoto wanaolelewa ama na wasaidizi wa shughuli zetu majumbani, mitandao ya jamii, Shule, na makundi mengine tusiyoyajua, ambayo hayajui mila, utamaduni, desturi na maadili ya Jamii zetu.


Mheshimiwa Spika, hii ni hatari kwa usalama wa Taifa, unapokuwa na Taifa lenye familia ambazo hazina malezi mazuri ni ukweli usiopingika kuwa, ni lazima utegemee kizazi kisichokuwa na mwelekeo wa kimaadili. Hivyo ni muhimu Wazazi na Taifa likajua wajibu wa usalama na amani ya Nchi unaanzia kwenye malezi bora katika ngazi ya familia .


3.0 AMANI NI TUNDA LA HAKI.


Mheshimiwa Spika, hali ya Amani katika Nchi yetu iko katika mashaka makubwa na kwa bahati mbaya Serikali inaufahamu ukweli ila kwa sababu inazozijua yenyewe imeamua kupuuza ukweli huo wa kushindwa kutofautisha kati ya amani na utulivu katika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika , Taifa hili lina utulivu unaosabishwa na hofu inayojengwa kwa mabavu na silaha na sio amani, kuna mateso makubwa wanayoyapata wananchi wa Taifa hili kila siku, umasikini, njaa, ukandamizwaji, ubaguzi, uonevu, udhalilishwaji na mateso ya jinsi mbali mbali kutokana na kukosa uongozi unaojali maisha ya Watu.


Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni baada ya uchambuzi na tathimini ya “Hali ya Usalama na Amani ya Nchi yetu” kabla wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2015, tumebaini kuwa nadharia na mwenendo wa demokrasia ya vyama vingi hapa nchini iliwekwa kando, na badala yake sura nzima ya uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2015, uligeuka kuwa “Military Operation” yaani “Operesheni ya Kijeshi” kwa kisingizio cha kulinda amani.


Mheshimiwa Spika, tarehe 25 Oktoba 2015 siku ambayo wananchi walipiga kura, Katika Jengo la Mlimani City, CCM na timu yao ya Kampeni ya Rais John Pombe Magufuli walifanya zoezi la kuhesabu kura za mawakala wao kutoka vituo mbalimbali nchini yaani “Parallel Voter Tabulation” bila kubughudhiwa na Jeshi la Polisi, wakati huo huo UKAWA wakifanya zoezi kama hilo la “Parallel Voter Tabulation” katika vituo vitatu vya ICT ndani ya Jiji la Dar es Salaam, na vituo vyote hivyo kuvamiwa na Jeshi la Polisi ambalo lilizuia zoezi hilo kufanyika, kuvunja na kuharibu baadhi ya vifaa vilivyotumika kama vile laptop, kuwanyang’anya simu na laptops vijana zaidi ya 160 waliokuwa wanajitolea kufanya zoezi hilo, kuwasweka rumande kwa muda wa siku tatu mfululizo bila kuwafungulia mashitaka, kuwatishia kuwa wanatuhumiwa kwa makosa ya kufanya biashara haramu ya kusafirisha binadamu (human trafficking) na kuwafungulia mashitaka ambayo hayana msingi.


Mheshimiwa Spika, mnyonge anayelia moyoni kwa huzuni ya kuonewa ni hatari kwa usalama wa Nchi na Dunia , vikundi vingi vya uhalifu Duniani kwa asilimia kubwa vimesababishwa na utawala wa kibabe, uonevu na ukandamizwaji usiovumilika na huko ndiko tunakoelekea kama Taifa.


Mheshimiwa Spika , matendo mabaya haya yaliofanyika wakati wa uchaguzi mkuu uliopita Zanzibar na Tanzania bara ni ishara ya watawala kuelekeza Nchi yetu katika mapigano ya sisi kwa sisi katika siku za usoni .


Mheshimiwa Spika, unapokuwa na Jamii inayoamini kuwa mfumo wa demokrasia hauwezi kuwapa wananchi viongozi wanaowataka , maana yake ni dhahiri kwamba unaanza kuifundisha jamii hiyo kufikiri njia mbadala ya mabadilko katika Nchi .


Mheshimiwa Spika , kuwa na Tume ya Uchaguzi inayotiliwa mashaka na Jamii ni hatari kwa usalama wa Nchi yetu. Ni muhimu sasa kama Taifa kutafakari uwepo wa katiba ya wananchi na Tume Huru ya Uchaguzi itakayorudisha imani ya Wananchi katika Uchaguzi wa Kidemokrasia.


Mheshimiwa Spika , Mungu adhihakiwi apandacho Mtu ndicho avunacho, utulivu mnaouona Zanzibar na kwingine kokote kule kuliko na ukandamizaji ni nafsi zinazojadili mwelekeo mpya wa maisha yao katika utawala wa Nchi yao.


Mheshimiwa Spika , Zanzibar mmeshinda uchaguzi kwa hila na sio kwa haki, wekeni kumbu kumbu maneno ya Kambi Rasmi ya Upinzani leo kuwa, ipo siku Zanzibar itakuwa ni sehemu ngumu ya kuishi Binadamu kama hamtachukua hatua sasa ya kurekebisha mlichokifanya Zanzibar na Tanzania Bara katika uchaguzi uliopita .


Mheshimiwa Spika , kwani tunajiuliza maswali mengi , je tutarudi tena kwenye uchaguzi wa mwaka 2020 kwa njia ya demokrasia ? au tutafakari njia nyingine mbadala, kwani demokrasia katika Taifa hili imethibitisha kuwa tunaweza kushinda uchaguzi lakini tukaporwa matokeo na tusitangazwe kuwa washindi.





4.0 MAUAJI YA VIONGOZI WA KISIASA.


Mheshimiwa Spika , Viongozi wa kisiasa hasa wale wa Upinzani wamekuwa wakiishi kwa kubaguliwa na kwa mateso makubwa sana hata wengine kuuwawa kwa sababu ya kazi na wajibu wao katika siasa na jamii.


Mheshimiwa Spika , nikianza kueleza wale wote waliopatwa na madhara ya vipigo , kusingiziwa kesi , na wengine kuuwawa , ninaamini kwamba hotuba hii haitoshi isipokuwa labda tuandike vitabu.


Mheshimiwa Spika ,Rafiki na ndugu yetu mpendwa Alphonce Chemu Mawazo, Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita aliuawa kinyama kule Katoro- Busanda - Geita , mchana , hadharani , tena karibu na kituo cha Polisi.


Mheshimiwa Spika, sisi tulilia sana na kuhudhunika sana hata mpaka leo, na tulipohitaji kumzika kwa heshima anayositahili kama rafiki na Kiongozi wetu hatukuruhusiwa na Polisi , tulipigwa sana mabomu na wengine kama Mwenyekiti wetu wa Vijana Taifa Patrobas Katambi walipewa kesi ya kushambulia jambo ambalo ni la kutunga na uzushi.


Mheshimiwa Spika , Mwili wa Marehemu Alphonce Mawazo ulizuiwa kuagwa kwa ubabe na Jeshi la Polisi bila sababu za msingi mpaka Mahakama ilipotoa haki ya mwili kuagwa kule jijini kwao Busanda Geita.


Mheshimiwa Spika, Marehemu Mawazo ameacha Binti yake mzuri na mwenye akili nyingi Precious akiwa darasa la nne, Baba yake ameuwawa si kwa sababu alikuwa mwizi , bali aliamini katika siasa tofauti na demokrasia kwa maslahi ya Taifa.

Mheshimiwa Spika, wakati mioyo yetu ikilia ndani kwa huzuni, kwa dhuluma, uonevu, ukandamizwaji, vipigo hata vifo vya marafiki zetu na ndugu zetu katika kazi zetu za siasa tunazofanya, nyie mnaona mambo haya ni ya kawaida.

Mheshimiwa Spika, hii ni hatari kwa usalama wa Taifa, kwani subira na uvumilivu vitakapoishiwa nguvu, kuna dalili ya mauaji ya ulipizaji visasi kuanza na itakapofika hapo usalama na amani ya Taifa letu utakuwa mashakani sana.


Mheshimiwa Spika, Kama Rais Magufuli anaweza kuanzisha Mahakama ya Mafisadi ambao wapo hai, Kambi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kutoa majawabu kwa nini mpaka dakika hii bado tume ya kimahakama ya kuchunguza vifo tata (Judicial Commission of Inquiry) haijawahi kuundwa, ili kutoa haki kwa Watanzania. Japo kuwa ilikuwa ni ahadi ya Waziri Mkuu katika katika Serikali ya awamu ya nne.




5.0 MIKATABA TATA YA JESHI LA POLISI.


5.1 Mkataba tata wa Lugumi na Jeshi la Polisi.


Mheshimiwa Spika, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali , ilihoji utekelezaji wa mkataba wenye utata wa vifaa vya Mfumo wa Alama za Vidole (AFIS) ulioingiwa kati ya Jeshi la Polisi Tanzania na Kampuni ya Lugumi Enterprises.


Mheshimiwa Spika, kumetokea majibishano na malumbano mengi kwenye vyombo vya habari na miongoni mwa wabunge wa Bunge lako tukufu, hasa pale walipoanza kuhoji utekelezaji wa mkataba huo hasa kuhoji juu endapo vifaa hivyo vinafanya kazi.

Mheshimiwa Spika, Kufuatia majibishano na malumbano yaliyojaa utata ambao lazima upatiwe majibu yasiyo na shaka yoyote, hivyo basi, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inaitaka Serikali kutoa majibu ya moja kwa moja bila kupepesa macho. Tunataka Maswali yafuatayo yajibiwe hapa bungeni;


Mheshimiwa Spika,

1) Kwa kuwa mikataba ya serikali kwa mujibu wa sheria lazima ufuate sheria za manunuzi na kuthibitishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Je, Utaratibu huu ulifuatwa?

2) Je Mkataba huu wa LUGUMI ENTERPRISES na JESHI LA POLISI umetekelezwa ama haukutelezwa, na kama ulitekelezwa ni kwa kiwango gani, na ikiwa kulikua na tatizo la utekelezaji, Je, Jeshi la Polisi lilichukua hatua zipi?

3) Je, ni kampuni ngapi ambazo zinahusika na hatua za utekelezaji wa Mkataba kati ya Lugumi Enterprises na Jeshi la Polisi, kwa kuwa kampuni ya INFOSYS ambayo mmoja wa wamiliki wake ni Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mhe. Charles Kitwanga inatajwa kufunga vifaa hivyo (AFIS).

4) Ni kwanini C.A.G katika ukaguzi wake hakuhoji kuhusu uhalali na ulinganishi wa thamani ya pesa ya manunuzi na faida ya vifaa hivyo?

5) Kampuni ya INFOSYS (inayomilikiwa na Mhe. Kitwanga) imedai kulipwa na Jeshi la Polisi, takribani Dolla za Marekani 74,000, Je fedha hizi Kampuni ya Mhe. Kitwanga ililipwa kwa kazi ipi iliyofanya na Jeshi la Polisi?

6) Ni kwanini mpaka sasa , Rais Magufili hajachukua hatua dhidi Said Lugumi, na aliyekuwa IGP Said Mwema / Emmanuel Nchimbi aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na kuwasimamisha kazi wale wote ambao bado wako kazini juu ya mkataba tata wa Lugumi ?

7) Tunamtaka Rais , kutengua mara moja uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mathias Chikawe na kumrudisha nchini mara moja , kwani alihudumu kama Waziri wa Mambo ya Ndani na ni imani ya Kambi rasmi kuwa alijua mambo yote yanayoendelea ya mkataba wa Lugumi



Mheshimiwa Spika , Ni imani ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuwa Mhe.Waziri Charles Kitwanga, anazo taarifa za Mkataba huu na utekelezaji wake aidha kutoka kwenye Kampuni yake ambaye yeye ni Share holder ( Mbia ) ambayo ilifunga vifaa hivi au anazo taarifa ya utekelezaji wa Mkataba huu kutoka Jeshi la Polisi ambalo liko chini yake kwa kiwango chote kuhusu mambo yote ya Mkataba huu.


Mheshimiwa Spika, Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) , alinukuliwa na vyombo vya habari pale alipoulizwa kuhusu sakata la Lugumi na Mikataba yake na Jeshi la Polisi kutotekelezwa, alijibu majibu mafupi Katika gazeti la Raia Mwema la tarehe 27/04/2016 namnukuu “siyo kweli, watu wana ugomvi wao kibiashara, lakini nakueleza wazi kwamba, tembelea vituo vyote tulivyokubaliana, utakuta mashine zipo. Inawezekana zingine hazifanyi kazi kwa sababu ya kukosekana kwa internet” Mwisho wa kunukuu.

Mheshimiwa Spika, kulingana na maswali ambayo tumeuliza hapo juu na uchambuzi wetu, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inashauri kama ifuatavyo;


Mheshimiwa Spika,

1. Kwa vile Waziri wa Mambo ya Ndani anahusika kwa karibu katika Mkataba huu kupitia Kampuni yake ya INFOSYS na vile vile Jeshi la Polisi liko chini yake , je ? haoni kuwa ni busara kwa yeye kujiuzulu ili kutoa nafasi ya Uchunguzi kuepusha mgongano wa maslahi ndani ya Jeshi la Polisi na kwenye Kampuni ambayo yeye ni mmoja wa wamiliki ?



Mheshimiwa Spika,

2. kwa vile inaonekana kupitia vyombo vya habari na kauli za viongozi mbali mbali kuwa upo uwezekano wa Polisi kuwa wametapeliwa na vifaa hivyo havijafungwa, Kambi ya Upinzani Bungeni inautaka uongozi wote wa juu wa Jeshi la Polisi kujiuzulu mara moja, kwani kama wao wameshindwa kujua ukweli wa vifaa vilivyofungwa kwenye vituo vyao vya Polisi ama vipo au havipo, watawezaje kuchunga na kulinda mali na usalama wa raia wengine?


Mheshimiwa Spika,

3. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inataka majibu yote yanayohusu Mkataba wa Lugumi na Jeshi la Polisi kuhusu utekelezaji wake uwekwe wazi hapa bungeni na wizara husika.


5.2 Sakata la Kuuzwa kwa ardhi ya Polisi Oysterbay


Mheshimiwa Spika, Sakata la Kuuzwa kwa ardhi ya Polisi Oysterbay limeleta mashaka makubwa ndani ya jamii na baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi, pamoja na Rais Magufuli kutilia mashaka jambo hili.


Mheshimiwa Spika, Kwa vile kuna ukakasi na mashaka ya rushwa, tunaliomba bunge liazimie na kuitaka Serikali kuleta mara moja mkataba huu na mingine yote yenye sura kama hii ndani ya Bunge lako tukufu, ili ipitiwe na kufanyiwa tathimini endapo mikataba hiyo ilifuata utaratibu na ina tija kwa Taifa na hii iwe ni kwa mikataba yote iliyofanyika wakati wa Serikali ya awamu ya nne ya Mh Jakaya Kikwete , pamoja na ule wa ununuzi wa boti

( Mv Dar es salaam ) uliofanywa wakati Rais wa sasa Mh Dr Magufuli akiwa Waziri wa Ujenzi.


Mheshimiwa Spika samba samba na hilo Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka pia Serikali kuleta mikataba ya uuzwaji wa Nyumba za Serikali kazi ambayo aliisimamia Rais Magufuli mwenyewe wakati huo .


Mheshimiwa Spika , kwa vile Rais wa sasa alihusika kuuza nyumba za Serikali ni imani yetu kuwa Kambi rasmi ya Upinzani itapata ushirikiano wa kutosha juu ya utata wa mikataba hii tete ya uuzaji wa nyumba hizi.


6.0 RUSHWA, SURA YA SERIKALI NA BUNGE TISHIO LA HALI YA USALAMA.


6.1 Rushwa na Bunge kutumika kuwalinda wahalifu nchini


Mheshimiwa Spika , Mh Andrew Chenge (MB)ametuhumiwa na imethibitika hapa Bungeni na katika taasisi za Uchunguzi za Kimataifa (SFO) kuwa alihusika kwa karibu na kwa ufanisi katika sakata la kashfa ya ununuzi wa rada ya Taifa.


Mheshimiwa Spika , Mwandishi Andrew Feinstein , Colonel .U.S. Army (retired) katika Kitabu chake “ THE SHADOW WORLD - Inside the Global Arms Trade, katika ukurasa wa 188-196, amefanya uchambuzi wa kina jinsi Andrew Chenge alivyofanikiwa kukwapua fedha za Wananchi kiasi cha pesa za Kimarekani dolari 1.2 milioni kupitia Kampuni yake ya Franton Investment Ltd Jersey na Kampuni hii ya Andrew Chenge ikampa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dr. Idrissa Rashid pesa za Kimarekani dolari $600,000 kupitia Kampuni ya Gavana huyu inayojulikana kwa jina la Langley Investment Ltd.


Mheshimiwa Spika, Lakini kwenye utawala huu wa utumbuaji majipu, Andrew Chenge ni Mkiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkiti wa Kamati ya sheria ndogo, jambo hili lina sura ya dharau na fedhea kwa Bunge lako tukufu na kwa jamii.


Mheshimiwa Spika, Wako wengi wenye sura hizi za Mh Chenge na wengine ni Mawaziri ambao wamekuwa na kashfa mbali mbali kwenye Serikali iliyopita lakini wameonekana kwenye madaraka tena katika Serikali hii ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais aneyeamini katika utumbuaji majipu , wakati kuna majipu mengine asiyoweza kuyatumbua ndani ya baraza la Mawaziri.


Mheshimiwa Spika , Taifa linapokuwa na huzuni juu ya utawala unaopuuza na kudharau Wananchi , kwa vyovyote vile hali ya amani na usalama inakuwa mashakani na kuwatia moyo watumishi wengine wa Umma katika masuala yanayohusu ufisadi, rushwa na ubadhirifu kwamba sio mambo mabaya. Ndio maana imekuwa ni vigumu kukemea rushwa katika ngazi mbalimbali za utawala wa nchi hii ikiwemo Jeshi la Polisi.


6.2 Kuingiliwa kwa Uhuru wa Bunge na Mhimili wa Dola


Mheshimiwa Spika , tishio lingine la hali ya usalama Nchini ni Serikali kuingilia Uhuru wa Bunge , ni ajabu kubwa kwamba chombo kinachopanga matumizi ya fedha za Serikali ni Bunge , lakini kwa wakati huu tumeona Serikali ikiondoa matangazo ya moja kwa moja ya Bunge kwa kisingizio cha kubana matumizi , kazi ambayo hata hivyo kama ingekuwa ni hoja basi jambo hilo lingefanywa na Bunge na sio Serikali.


Mheshimiwa Spika, Wananchi kupata habari na kujua wanachojadili wabunge wao ni hitaji la lazima la Kikatiba na sio hisani ya Serikali, malumbano yetu dhidi ya hoja mbali mbali ndani ya Bunge yalikuwa ni muhimu kwa ustawi wa usalama wa Nchi yetu.


Mheshimiwa Spika, Wananchi , walipotuona kupitia vyombo vya habari mbali mbali , tukilumbana juu ya maisha na maendeleo yao , jambo hili lilikuwa linasidia kupunguza tension na uchungu kwa jamii kwani walikuwa wanashuhudia tukipigana na kulumbana juu ya ustawi wa maisha yao , walipata matumaini waliposikia majibu ya Serikali hata kama yalikuwa ni uongo.


Mheshimiwa Spika , Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni inasikitishwa na jinsi Bunge letu linavyoendelea kukosa nguvu na kuingiliwa na mihimili mingine ya dola kwa kuelekezwa ni kipi cha kufanywa na kipi si cha kufanywa. Ni wazi sasa bila chenga kuwa Bunge hili limeingiliwa na dola na sasa ni Bunge kibogoyo jambo linalohatarisha usalama na amani ya nchi, kwa kuwa Dola sasa inaweza kufanya chochote na isionekane kukemewa na Bunge ambalo kazi yake ni kuisimamia Serikali, badala yake sasa hivi Serikali ndio inalisimamia Bunge.


Mheshimiwa Spika , kisingizio cha gharama kubwa za kurusha matangazo ni uongo mkubwa ambao hata shetani anaushangaa, kwani hata vyombo vingine vya habari vilivyokuwa vinarusha matangazo ya “live” kwa gharama zao navyo vimezuiwa sio na Serikali bali na uongozi wa Bunge uliodhibitiwa na Serikali ya Dkt. Magufuli.

6.3 Tabia ya Rais Magufuli na Usalama wa Nchi.


Mheshimiwa Spika, wakati Taifa letu linapita kwenye changamoto nyingi Kama vile ukosefu wa sukari, umeme, umasikini, mizigo kupungua bandarini , madini ya Tanzanite kuanguka bei na ubadhirifu uliokithiri katika mfumo wa utawala. Rais mwenyewe ameonekana kufuatilia na kufanyia kazi habari za kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa tabia hii ya Rais Magufuli, kama Taifa tunahitaji maombi haraka, kwani Rais ataumiza watu wengi sana kwa kufuatilia maneno ya mitaani kwa njia mbali mbali , kwani kwa madaraka aliyonayo Rais bila shaka ataumiza watu wengi. Mfano, Sakata la Mke wa Waziri Mahiga na Trafiki barabarani. Ni jambo dogo sana na la karaha kuona linazingatiwa na Rais .


Mheshimiwa Spika, haikuwa busara Rais kukemea familia ya Waziri wake mbele ya vyombo vya habari na kuagiza askari huyu kupandishwa cheo bila kujua historia ya utumishi wake .


Mheshimiwa Spika , kwa nini mambo haya ni muhimu kuyasema na kwa nini ni hatarishi kwa usalama wa Nchi, tulipoonza vikao vya Kamati za Bunge, vyombo vya habari vilimnukuu Rais akielezea mpango wake wa kuanza kurekodi Mawaziri wake wanaolalamika juu ya staili yake ya uongozi. Kwa hiyo leo ukienda kwenye ofisi za Mawaziri, unaona, hofu, mashaka, kutokujiamini, mambo yatakayo punguza ufanisi, ubunifu na uhuru katika utendaji wao, jambo linalopeleka Taifa kuzorota katika Nyanja zote kwa utumishi wa umma jambo ambalo ni hatari kwa Taifa.


7.0 UGOMVI KATI YA WAKULIMA NA WAFUGAJI


Mheshimiwa Spika, Ugomvi kati ya Wakulima na Wafugaji ni tatizo kubwa na ambalo lisipotatuliwa kwa makini na haraka , Nchi yetu itaendelea kushuhudia mauaji kwa raia wake .


Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani inashauri Serikali kutenga mara moja na kupima maeneo kwa ajili ya wakulima na wafugaji , tatizo hili haliwezi kutatuliwa kwa bunduki na mabomu ya machozi isipokuwa mipango maalumu ya upimaji ardhi na ushauri wa kitalamu juu ya ufugaji wa kisasa na ukulima wa kisasa unaweza kuwa njia ya kupunguza tatizo na kuliondoa kabisa.


Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya upinzani inaishauri Serikali kuanzisha mfumo wa mauzo ya wanyama kwa kuzingatia vipimo vya uzito na kuuza kwa mizani yaani kilogramu na si kuuza kwa kutazama mifugo kwa macho na kupanga bei. Kwa kufanya hivyo wafugaji watajali zaidi na kuona tija ya kuwa na mifugo michache na kuwanenepesha kuliko kuwa na mifugo mingi isiyo na afya.


8.0 HALI YA UHALIFU NCHINI


Mheshimiwa Spika, Hali ya Uhalifu nchini bado ni mbaya na kasi ya kupunguza uhalifu hairidhishi, taarifa za Takwimu za Hali ya Uhalifu Januari-Juni, 2015 zilizotolewa na ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi zimeonesha kuwa kuna ongezeko la asilimia 9.8 ya makosa ya jinai hapa nchini. Taarifa hiyo imeonesha kuwa matukio madogo ya makosa ya usalama barabarani yakiongezeka kwa asilimia 16.4 kutoka mwezi Januari – Juni, 2014 mpaka kufikia Januari – Juni, 2015.


Mheshimiwa Spika, ikumbukwe kuwa mara zote ndani ya muda wote wa Bunge la 10, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ilikuwa ikiishauri Serikali juu ya hatua mbalimbali za kuchukua dhidi ya matukio ya ajali za barabarani ambazo zinagharimu maisha ya wananchi wa Taifa hili ambao ni nguvu kazi inayopotea, na kuwaacha vijana wengi wakipoteza wazazi wao na kubaki mayatima. Taarifa za Takwimu za Hali ya Uhalifu Januari-Juni, 2015 zimebainisha kuwa “Jumla ya watu 1,849 walifariki kutokana na ajali za barabarani ikilinganishwa na watu 1,777 waliofariki Januari hadi Juni, 2014. Hili ni ongezeko wa watu 72 sawa na asilimia 4.1”.


Mheshimiwa Spika, Ubunifu pekee wa Serikali katika Jeshi la Polisi ilikuwa na kuwapatia mashine za EFD ili wasiendelee kufanya kazi ya kuhakikisha usalama barabarani na badala yake “kudandia” kazi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ya kukusanya mapato. Ni aibu kubwa sana kwa Jeshi letu la polisi kujisifia kwa ukusanyaji wa mapato kutokana na makosa ya barabarani badala ya kutoa taarifa za namna gani Jeshi hilo limepunguza uhalifu wa makosa ya barabarani. Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro alikaririwa na vyombo vya habari akidai kuwa “Kikosi cha usalama barabarani kanda ya Dar es Salaam kimekusanya kiasi cha shilingi bilioni 1.9 kama faini za makosa ya barabarani kuanzia Februari 1 hadi 22, mwaka huu”


Mheshimiwa Spika, Itoshe tu kusema kuwa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haijaridhishwa na mbinu na weledi hafifu unaotumiwa na Serikali ndani ya Jeshi la Polisi kupambana na uhalifu hapa nchini. Taarifa ya Hali ya UhalifuJanuari-Decemba, 2014 imeonesha ongezeko kubwa sana, (substantial increase) ya uhalifu nchini kwa asilimia 32.5, kutoka makosa milioni 1.2 mpaka makosa milioni 1.6.


Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaishauri Serikali kuzingatia ushauri wote uliotolewa na Kambi kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita. Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali itoe maelezo ya kina juu ya mpango mkakati wa kupunguza kiwango cha uhalifu hapa nchini na kueleza ni kwa kiwango gani wanafanya kazi ya Usalama wa Raia na Mali zao.




9.0 UKOMESHAJI BIASHARA HARAMU YA DAWA ZA KULEVYA NCHINI


Mheshimiwa Spika, Ifahamike kuwa kwa zaidi ya muongo mmoja uliopita Kambi Ramsi ya Upinzani Bungeni, imekuwa ikiishauri Serikali juu ya hatua za kuchukua katika kukomesha matumizi na biashara haramu ya dawa za kulevya nchini.


Mheshimiwa Spika , ushauri wetu juu ya jambo hili nikuitaka Serikali ikatafute ushauri wetu wote wa huko nyuma katika hansard na kuuzingatia mara moja , kwa ajili ya kuokoa Taifa letu.





10.0 HALI ZA MAHABUSU NA WAFUNGWA MAGEREZANI

10.1 Kuondoa adhabu ya Kifo iliyo kinyume na Katiba ya Tanzania

Mheshimiwa Spika, Mwaka 2015, inakaridiwa kuwa watu 472 walipatikana na hatia na kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa, kati ya hao wanaume ni 452 na wanawake 20, ambapo wafungwa 228 wanasubiria kunyongwa hadi wafe kwa mujibu wa sheria, na wafungwa 244 wanasubiria kusikilizwa kwa rufaa zao, hii ni kwa mujibu wa Ripoti ya Haki za Binadamu (LHRC, 2015).

Mheshimiwa Spika, adhabu ya kifo inakiuka misingi ya Kikatiba, ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema kuwa “Kila mtu anayo Haki ya Kuishi na kupata kutoka katika Jamii hifadhi ya maisha yake kwa mujibu wa katiba hii” Lakini pia hajaanza kutumiza masharti ya katiba yetu kwa kuwa bado hukumu za vifo zinatolewa. Hata hivyo bado Serikali ya Tanzania haijatia saini makubaliano ya sehemu ya pili ya mkataba wa International Convention on Civil and Political Rights wa mwaka 1966, ambapo Second Optional Protocol to the International Convention on Civil and Political Rights, ya mwaka 1989 ambayo inataka nchi wanachama kukomesha adhabu ya kifo.

Mheshimiwa Spika, inaishauri Serikali kusaini na kuridhia mkataba wa Second Optional Protocol of the International Covenant on Civil and Political Rights, ili kuilinda katiba yetu na kutimiza matakwa ya kikatiba ya kulinda uhai wa kila Mtanzania.

10.2 MSONGAMANO WA MAHABUSU NA WAFUNGWA MAGEREZANI.

Mheshimiwa Spika, Kwa zaidi ya muongo mmoja uliopita, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imekuwa ikiitaka Serikali kuchukua hatua ya kupunguza msongamano wa wafungwa na mahabusu Magerezaji sambamba na kuboresha lishe na huduma za afya kwa Wafungwa na Mahabusu.

Mheshimiwa Spika, Mwaka wa fedha 2015/2016, aliyekuwa Waziri wa mambo ya Ndani wakati huo, Mhe. Mathias Chikawe, alisema kuwa uwezo wa magereza yetu ni kubeba wafungwa 27,653, wakati mpaka kufikia mwaka 2015 mwezi machi magereza ilikuwa na wafungwa 33,027.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haijaridhishwa na hatua ambazo Serikali ilizichukua kwa mwaka wa fedha uliopita katika harakati za kupunguza msongamano wa magereza. Hatua za Parole, Msamaha wa Rais na Kifungo cha nje bado hazitoshi kwa kuwa hatua hizo zinalenga kupunguza msongamano bila kuangalia hali ya mazingira ya mahabusu na wafungwa wanaobakia ndani ya magereza. Tuliendelea kuisisitiza Serikali kuwa huduma za afya, uchakavu wa miundombinu ya vyoo na mabafu, na ufinyu wa vyumba vya kulala, ukosefu wa matandiko na magodoro pamoja na lishe kwa mahabusu na wafungwa zimeendelea kuwa duni.

Mheshimiwa Spika, Mwaka wa fedha 2015/2016, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni iliishauri Serikali kuwa ili kupunguza msongamano wa mahabusu magerezani iandae utaratibu kwa Jeshi la Polisi kuwa kabla halijawakamata watu na kuwaweka mahabusu basi uchunguzi wa kina ufanyike, tofauti na sasa ambapo mtu anayehisiwa tu kuwa ni mhalifu anaweza kuwekwa mahabusu na kukaa huko hadi miaka zaidi ya mitano na baadae kuambiwa kuwa hana hatia, huu ni uvunjaji wa haki za Binadamu.

Mheshimiwa Spika , hata hivyo sababu nyingine mojawapo inayofanya mahabusu kujaa katika magereza zetu , zinachangiwa na matumizi mabaya ya Sheria ya mwenendo wa Makosa ya Jinai kifungu cha 91 ambacho kinampa mamlaka Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP) kuondoa Shauri la jinai Mahakamani lakini kuondolewa kwa shauri hilo hakuzuii mamlaka kumshtaki tena kwa kosa lile lile mtuhumiwa.

Mheshimiwa Spika, Jeshi la Polisi wamekuwa wakitumia vibaya masharti ya kifungu hiki ambapo mara baada ya mtuhumiwa/watuhumiwa kuachiwa wamekuwa wakikamatwa tena na Jeshi la Polisi mara nyingi ikiwa katika maeneo ya Mahakama.

Mheshimiwa Spika, kambi rasmi ya upinzani Bungeni inashauri mbali na uwepo wa parole, na vifungo vya nje ni vema magereza zikaimarisha na kuwa kitengo maalumu cha wafungwa watakao fanya kazi za huduma za jamii na Kitengo cha mazingira na upandaji miti hasa kwa kifungo chini ya mwaka mmoja au na zaidi ili kunusuru uharibifu wa mazingira unaohatarisha Taifa letu kuwa jangwa . Kazi yao kubwa iwe kuhudumia idadi miti kwa kuipanda na kuitunza adhabu zao ziwe na manufaa kwa jamii na sura ya Taifa.

11.0 HATIMA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA

Mheshimiwa Spika, Katika hotuba yangu ya mwaka wa fedha 2015/16 nikiwasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, niiliitaka Serikalikutoa ukomo wa muda, ambapo kila raia wa Tanzania atapatiwa Kitambulisho chake cha Taifa na kuainisha gharama zilizotumika katika mchakato mzima wa kutengeneza vitambulisho vya Taifa.

Mheshimiwa Spika, Rais Magufuli alitengua uteuzi wa Bwana Dickson E. MAIMU, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kuanzia, tarehe 25 Januari, 2016 kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu tarehe 26 Januari 2016. Katika taarifa ile ilibainika kuwa “Taarifa zilizomfikia Rais zinaonesha kuwa NIDA hadi sasa imetumia Sh.179.6 bilioni.”

Mheshimiwa Spika, Katika taarifa ile, Rais aliagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) wafanye ukaguzi maalum wa manunuzi yote yaliyofanywa na NIDA. Sasa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inaitaka Serikali kuliambia bunge hili tukufu kuwa ni lini inatarajia kuileta bungeni ripoti ya Ukaguzi Maalumu ulioagizwa kufanyika na Rais Magufuli, ili bunge sasa liweze kutimiza majukumu yake yaliyoanishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 63 ibara ndogo ya (2)

Mheshimiwa Spika, Ripoti hiyo ya uchunguzi maalumu wa NIDA itakapowasilishwa ndani ya Bunge hili, wabunge kwa niaba ya wananchi tutaweza kufahamu mbivu na mbichi na kujua hatma ya vitambulisho vya Taifa, hatma ambayo mpaka sasa Serikali imekosa majibu yake.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni pamoja na masuala mengine kuhusu ushauri tuliotoa katika vitambulisho vya Taifa, bado tunaona kuwa mfumo mzima wa kuwatambua Watanzania upo “shaghala bagara” kutokana na kuwepo kwa vitambulisho vya aina nyingi kama vile Leseni za Udereva na Kadi ya Mpiga kura, hivyo kulifanya Taifa kuingia hasara kubwa ya kutengeneza vitambulisho kwa watu wale wale. Huku ni kukosa ubunifu.

Mheshimiwa Spika, Gazeti la Mtanzania la tarehe 2 Machi 2016, liliripoti kuwa “mchakato wa utoaji wa vitambulisho vya Taifa unatarajiwa kuanza upya, kutokana na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), kukiri kuwapo kwa upungufu katika vitambulisho vya sasa.” Huu ni udhaifu mkubwa wa Serikali kukosa ubunifu, kitendo kinachopeleka hasara kwa Taifa bila watu kuwajibishwa.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kutoa maelezo ya kina kuwa ni kwa sababu gani ilifanya uzembe mpaka vitambulisho vya Taifa vikaanza kutolewa huku kukiwa na udhaifu uliobainika baada ya zoezi la kuvigawa kuanza.

Mheshimiwa Spika, Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni tunaishauri Serikali kuunganisha mfumo wa vitambulisho vya Taifa na vitambulisho vya aina nyingine kama vile leseni za udereva, Utambulisho wa Namba ya Mlipa Kodi, Vitambulisho vya Bima za Afya, Hati za Kusafiria na Kadi za Mpiga kura ili kuwa na “National Database” ambayo inajumuisha taarifa zote za Watanzania, jambo ambalo litaepusha upotevu wa kumbukumbu na kurahisisha michakato ya kutoza kodi na kuongeza ufanisi katika ufuatiliaji wa wapi wananchi wapo, wanafanya nini na wanaweza vipi kuisaida Serikali kutimiza majukumu yake kama vile ulipaji kodi kwa wakati na ufuatiliaji wa ulinzi wa Raia wetu wanasafiri nje ya nchi.

11.1 UKIUKWAJI WA TARATIBU ZA KUSITISHA AJIRA ZA WAFANYAKAZI 597 WA NIDA

Mheshimiwa Spika, Tarehe 7 Machi 2016, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa alisitisha ajira za vijana 597 waliokuwa wanafanya kazi kwa mkataba, bila kufuata taratibu za kusitisha ajira. Watumishi hao hawadai kurudishwa kazini, lakini wanachodai ni kulipwa stahiki zao kwa mujibu wa mkataba wao wa ajira.

Mheshimiwa Spika, waliokuwa watumishi wa NIDA waliositishiwa mikataba yao ya ajira wana madai ya zaidi ya bilioni 2.3. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA alitoa tangazo tarehe 11 April 2016, katika gazeti la Mwananchi ukurasa wa 16 kuwa NIDA itaanza kufanya malipo ya madai yao kuanzia Jumatano tarehe 13 April 2016 saa 3.00 asubuhi, lakini Mheshimiwa Spika, Taarifa zilizoifikia Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ni kuwa mpaka dakika hii ninavyoongea hakuna fedha zozote zilizolipwa kwa waliokuwa waajiriwa hao 597 wa NIDA waliositishiwa ajira zao.

Mheshimiwa Spika, huu ni ukiukwaji wa haki za binadamu wa kumfukuza mtumishi kinyume cha sheria kiholela na hatimaye kutomlipa stahiki zake ipasavyo jambo ambalo ni kinyume na misingi ya utawala bora.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ina taarifa na imebaini kuwa mamlaka hiyo haikuwahi kupeleka makato ya wafanyakazi katika Mfuko wa Kijamii wa GEPF kuanzia mwezi Julai 2015 mpaka tarehe 7 Machi 2016 ambapo ajira zilisitishwa.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kulieleza bunge hili sababu za Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA kushindwa kulipa madai ya wafanyakazi wapatao 597 walioachishwa kazi tangu mwezi Disemba 2015 ambapo hawakulipwa stahiki zao kwa miezi mitatu mfululizo tangu mpaka ilipofika tarehe 7 Machi 2016 ambapo ajira zao zilisitishwa rasmi.




12.0 UMUHIMU WA JESHI LA POLISI KATIKA KUBORESHA MAISHA YAO.


Mheshimiwa Spika, Serikali yoyote makini Duniani inaweza kujenga ustawi wa maisha ya raia wake kwa kutambua umuhimu wa Ulinzi na Usalama katika Taifa. Lakini kuhitaji ulinzi kwa walinzi ambao huwapi ulinzi wa maisha yao kama mishahara bora na masilahi mengine ni sawa na kumeza dawa ya tumbo kwa kutumia konyagi.


Mheshimiwa Spika, Watumishi wote wa umma wanahitaji ungalifu bora kutoka Serikalini , lakini watumishi wetu wanaolinda amani na usalama wa raia wanahitaji upendeleo kwa kiwango fulani zaidi , kwani kazi ya ulinzi ni kujitoa maisha kwa ajili ya wengine .


Mheshimiwa Spika, mishahara ya Polisi na posho zao zote bado ni ni ndogo sana , na ndio maana kuondoa rushwa ndani ya jeshi la Polisi kwa kuendesha warsha , semina elekezi , kutoa miongozo , na vipeperushi ni jambo ambalo haliwezi kufanikiwa , katika sala ambayo Bwana Yesu aliwafundisha wanafunzi wake, kuna mahali sala hiyo inasema na nukuu “ USITUTIE MAJARIBUNI BALI UTUOKOE NA YULE MWOVU “


Mheshimiwa Spika , rushwa ndani ya Jeshi la Polisi imejengwa na utawala wa Serikali ambao umeshindwa kujali masilahi bora ya Walinzi wetu hawa ikiwa ni pamoja na Jeshi la Magereza , kwa hiyo Serikali ndiyo inayowatia Askari wetu majaribuni katika suala la kuomba na kupokea rushwa kwa kuwalipa fedha kidogo sana kwa ajili ya maisha yao .


Mheshimiwa Spika, hakuna Polisi wala Askari magereza anayeweza kujenga nyumba kwa mshahara na marupurupu anayopokea , wanaishi maisha magumu na ya taabu sana , ndio maana wakiona kosa wanaona fedha badala ya uwajibikaji na na kutenda haki.


Mheshimiwa Spika, Serikali inapaswa kuwalipa walinzi wetu hawa vizuri ili kufanya kazi ya Jeshi la Polisi au Jeshi la Magereza / Zima moto na Uokoaji iwe ni kazi ya fahari kuanzia kwenye familia kama zilivyo kazi nyingine .


12.1 JESHI LA ZIMA MOTO NA UOKOAJI


Mheshimiwa Spika, Katika hotuba ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wakati wa Bajeti ya mwaka wa fedha 2011/2012 pamoja na mambo mengine alipendekeza kuwa kutokana na kuongezeka kwa majengo makubwa nchini ambayo ni chanzo cha mapato serikali ianzishe mamlaka ya kuyasimamia (Real Estate Regulatory Authority) kwa ajili ya kuhakikisha kuwa inapata mapato na kusimamia uzingatiaji wa miundo mbinu na kanuni za kiusalama katika ujenzi.

Mheshimiwa Spika, Aidha pamoja na masuala ya mapato tunaitaka serikali katika ihakikishe kuwa inatoa maelekezo kwa taasisi na watu binafsi ambao wanamiliki majengo au wanatarajia kuwa na majengo kuhakikisha kuwa wanajenga na kuweka visima kwa ajili ya maji ambayo yatatumika kama kutakuwa na janga la moto katika majengo yao au maeneo yao Hii itasaidia sana kuondoa tatizo la magari ya zima moto kuishiwa maji kila linapotokea janga la moto na hili ni kwa mujibu wa sheria ni bora sheria hii ikazingatiwa na kufuatiliwa.


Mheshimiwa Spika , Kambi rasmi ya upinzani Bungeni inalitaka na kulishauri Jeshi la Uokoaji na zimamoto kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani kuzipa mamlaka Halmashauri za Miji , Manispaa na Majiji uwezo wa kusimamia kikamilifu maeneo ya makazi na kuhakikisha kuwa kila nyumba inayoishi binadamu au anakofanyia kazi inakuwa na uwezo na miundo mbinu ya kuzima moto na kila nyumba iwe ni lazima kuwa na Mtungi wa kuzimia moto ( Fire extinguisher ) na kazi hizi ziachwe kwa Halmashauri za Miji , Manispaa , Majiji husika kwa kushirikiana na Jeshi la zima moto na uokoaji

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika kipindi chote cha Bunge la 10, tumekuwa tukiishauri Serikali kufanya maboresho makubwa ya Jeshi la Zima Mto na Uokoaji kwa kulipangia bajeti ya kutosha kwa ajili ya miradi ya Maendeleo ili jeshi hilo liendeshwe kisasa zaidi katika kukabiliana na majanga ya ajali za moto na matukio ya uokoaji.

Mheshimiwa Spika, Hata hizo bilioni 53 zilizoombwa na Jeshi la Zima Moto na Uokoaji inaonesha kiasi gani Wizara yenyewe na Jeshi kwa ujumla halijatambua umuhimu wa kitengo hiki. Jeshi la Zima moto linahitaji Helkopta za kisasa zenye uwezo wa kuzima moto. Jeshi hili la zima moto linahitaji kuwa na uwezo wa kuzima moto kwenye misitu mikubwa kunapokuwa na janga la moto, milima inapopata majanga ya moto kama mlima Kilimanjaro, Jeshi hili linapaswa kuwa na uwezo wa kuzima moto, vile vile Jeshi linatakiwa kuwa na uwezo wa kuzima moto katika maeneo ya nchi ambayo magari hayawezi kufika kwa urahisi.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaona umuhimu wa Jeshi hili utathibitika baada ya Chama Cha Mapinduzi kuondoka madarakani, ili uongozi wenye maono mapana uje na kutazama Jeshi hili katika sura na mfano tulioeleza hapo juu. Bilioni 53 walizoomba inapaswa kuwa bajeti ya Jeshi la Zima moto ya kufanya dhifa ya nyama choma yaani (barbecue)


13.0 UHAMIAJI HARAMU NA USALAMA KATIKA MIPAKA YA NCHI


Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeendelea kuishauri Serikali kuhusu usalama wa mipaka ya nchi yetu kuwa ipo hatarini dhidi ya matukio ya uhalifu wa kimataifa na matukio ya ugaidi, kutokana na ongezeko la wahamiaji haramu ambao wanaingia nchini kupitia mipaka yetu na wanakamatwa wakiwa ndani ya nchi tayari wakisafirishwa kwenda kwenye mataifa mengine kusini mwa jangwa la Sahara.


Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni tunaishauri Serikali kutumia mbinu za kisasa ili kuzuia wahamiaji haramu wanaotumia nchi yetu kama “transit gate” ya kuhamia kwenye mataifa mengine hasa kutoka mataifa ya Kaskazini mwa Afrika kwenda kusini mwaka bara la Afrika.


Mheshimiwa Spika , vile vile Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali iangalie namna ya kuanzisha ofisi za uhamiaji kwenye maeneo muhimu yanayotumika kama matobo kwa wahamiaji haramu .


14.0 HITIMISHO


Mheshimiwa Spika, Asilimia zaidi ya 50% ya wabunge waliomo ndani ya Bunge hili wengi ni wapya maana yake ni kwamba, michakato ya kura za maoni katika vyama vya siasa ni sehemu ya kubadilisha mwanasiasa na pia mfumo wa demokrasia unatoa uhuru wa jinsi hiyo katika uchaguzi.


Mheshimiwa Spika, Martin Niemoller alikua mchungaji wakati wa utawala wa Kinazi Ujerumani akiwa mstari wa mbele kupinga utawala wa mabavu , alichukuliwa mateka katika kambi (concentration camp) na alisema maneno yafuatayo;

“First they came for the Socialists, and I did not speak out—
Because I was not a Socialist.

Then they came for the Trade Unionists, and I did not speak out—
Because I was not a Trade Unionist.

Then they came for the Jews, and I did not speak out—
Because I was not a Jew.

Then they came for me—and there was no one left to speak for me.”

Mheshimiwa Spika, ni muhimu wabunge, viongozi wa vyama na serikali na watu wote wajue tunapoishauri Serikali juu ya sheria na sera za nchi ni busara na upendo wa hali ya juu kujua kwamba uamuzi tunaoufanya humu ndani leo ni kwa faida na maslahi ya watoto wetu na watoto wa watoto wetu. Kwa bahati mbaya itikadi za vyama vyetu zimenunua utashi, ukweli na utu wetu.


Mheshimiwa Spika, Rais Magufuli ana jambo muhimu la kufanya ili athibitishe anachokiita huruma yake kwa masikini nalo ni kuwapa masikini katiba yao (Rasimu ya Warioba) iliyobeba maoni waliyoyatoa katika Tume ya Warioba kabla ya kuchakachuliwa na Bunge la Katiba.

Mheshimiwa Spika, ni namma moja tu inaweza kumsaidia Rais kukabiliana na ufisadi , ubadhirifu wa mali za umma na mengineyo yenye sura hizi , na namna hiyo ni kuacha uhuru wa Bunge katika kazi zake za kuisimamia Serikali .


Mheshimiwa Spika, James Freeman Clarke alisema maneno haya “The difference between a politician and a statesman is that a politician thinks about the next election while the Statesman think about the next generation.”Sisi tunafikiria nini?


Mheshimiwa spika, tatizo la wanasiasa wengi wa Taifa hili kila wanapomaliza uchaguzi papo hapo, ndipo wanaanza kufikiria uchaguzi unaofuata. Ndio maana mawazo ya vikao vya vyama vyetu (Party Caucus) yanakuwa muhimu kuliko msingi wa siku za usoni za nchi yetu. Hili nalo ni tishio kubwa la usalama wa Taifa letu. Kwani wanaopaswa kushauri, kuelekeza na kusimamia wameukataa wajibu wao bila aibu.


Mheshimiwa Spika, nimalizie kwa kusema, zawadi pekee mbunge yoyote anayoweza akatoa kwa wazazi wake, watoto wake, familia yake na nchi yake ni yeye kuwa na uwezo wa kusimamia ukweli, demokrasia, utu na haki kwa gharama yoyote ile.



………………………………………..

Godbless Jonathan Lema (Mb)

MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI NA

WAZIRI KIVULI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Tarehe 16 Mei, 2016

Vanessa Mdee Vs Shilole Hali ni Tete Instagram, Wapigana Vijembe Laivu

$
0
0
Ni juzi tu tuliona video ya msanii wa kimataifa vanessa mdee akimfundisha yai local artist Shishi baby salon cha ajabu ni leo ghafla wamenza kutupiana maneno uko instagram
shilole alianza na ujumbe huu


Haikuchukua mda nae vanessa mdee v. money amendika maneno haya kupitia instagram account yake

"Nikupe KICKIII ujulikane au sio? Kila siku twanyamaza ndiyo mtugaragaze. Sit the f**k down. Mimi sio wale uliowazoea. P.s: You ain't worth this post inashushwa sasa hivi" #MessageSent

BUNGE LIVE: Ushauri wa bure kabisa kwa vyama vya upinzani

$
0
0
Ushauri wangu kwa Wabunge wa Upinzani.

Waachane kupoteza muda kuvutana juu ya bunge kuwa laivu bali waangalie plan B .Kwa kuwa hata wafanyaje hiyo itakuwa hivyo kutokana na uchache wao ndani ya Bunge.

Plan B-wawafanyie kazi watu wao kwa kuisimamia Serikali vizuri katika maeneo yao ili yale matunda ndio iwe sera yao katika vyombo vya habari.
Mfano: Tumeona bajeti ya jimbo la kinondoni ni nzuri sana na kama itaenda kama ilivyopangwa basi utakuwa mfano nzuri na watu wataona umuhimu wa upinzani kuongoza jimbo.

Kama wataendelea kuvutana na serikali huku mambo yakiwa yanaenda pasipo kuona impacts za kugoma kwa wabunge wa upinzani basi serikali ambayo ipo chini ya CCM na huu moto wa mh rais serikali itazidi kujizolea sifa kwa kuwa wanacho kifanya wananchi wanakiona .

Ni upinzani kukaa na kujitathmini mapema sana bila ya hivyo watakuja kujitathmini wakati Mh rais yeye anasema jamani wananchi katika miaka yangu 5 nimefanya 1,2,3,4,5....naombeni tena mnipe miaka 5 nifanye 1,2,3,4,5...

Wakati huo wapinzani watabaki na mabomu (tuhuma za ufisadi mbalimbali) kwenye mikoba yasiyo na madhara ambayo wananchi wamechoka kuyasikia.

Siku hazigandi kama alivyoimba mwanamuziki mmoja maarufu nchini. Muda wa wao kufanya jambo la maana ndio huu.

Besigye ashtakiwa kosa la uhaini Uganda

$
0
0

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye amefikishwa mahakamani mjini Kampala na kushtakiwa kwa kosa la uhaini.


Dkt Besigye alifikishwa katika majengo ya mahakama ya Nakawa mapema kabla ya saa tatu, muda wa kawaida wa kufunguliwa kwa mahakama, na akasomewa mashtaka.

Alijiwakilisha mwenyewe kortini na amesema hataki kuhusisha mawakili katika kesi hiyo.
Hakimu ameamuru awekwe rumande hadi tarehe 1 Juni.

Dkt Besigye ndiye aliyekuwa mpinzani mkuu wa Rais Yoweri Museveni kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Februari nchini humo.

Leo imekuwa mara ya pili kufikishwa mahakamani akikabiliwa na tuhuma hizo za uhaini kwani awali alifikishwa mahakani kwa mara ya kwanza siku ya Ijumaa iliyopita katika mji wa Moroto, baada yake kudaiwa kujiapisha kuwa rais siku moja kabla ya Rais Museveni, aliyetangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi huo kuapishwa..

Besigye alishikiliwa na polisi kwa muda wa siku mbili ambapo alifikishwa mahakamani huku shughuli za mahakama zikiwa zimekwisha.

Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wafuasi wake ambao wamekuwa wakisema hakuruhusiwa kuwasiliana na wanasheria wake.

Matumizi ya Mitandao ya Kijamii Kama Instagram na Facebook Kupigwa Marufuku Ofisi za Serikali

$
0
0

Serikali imeanza mchakato wa kutekeleza mpango wa kudhibiti matumizi ya mitandao ya kijamii katika ofisi za umma ili kuongeza ufanisi.

Mpango huo umelenga kuzuia mitandao ya kijamii ikiwamo Facebook, Twitter, Whatsapp na Instagram.

Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala wa Serikali Mtandao (Ega), Suzan Mshakangoto alisema mpango huo umelenga kuwadhibiti watumishi wa umma wanaotumia mitandao hiyo kuanzia saa 1.30 asubuhi hadi saa 9.30 alasiri.

Alisema sehemu kubwa ya wataalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) wa taasisi za umma wameshapewa mafunzo mbalimbali kufanikisha mpango huo.

Hatua hiyo imekuja baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue kuuagiza wakala huyo miezi mitano iliyopita kutafuta njia madhubuti ya kudhibiti matumizi ya mitandao ya kijamii ofisini ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

“Mtumishi akishaingia ofisini hataweza kutumia mitandao ya kijamii na huduma za barua pepe nje ya mfumo wa Serikali kama Yahoo na Gmail. Tunawataka watumie mfumo wa barua pepe za Serikali ili wafanye mawasiliano salama,” alisema Mshakangoto.

Utekelezaji wa mpango huo huenda ukachukua muda kidogo kuanza kwani Mshakangoto alisema taasisi zote za umma zaidi ya 500 zinatakiwa kuunganishwa kwenye Mkongo wa Taifa lakini huenda ukaanza na taasisi 72 zilizounganishwa zikiwamo wizara zote, wakala wa Serikali na idara kama Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Ega ilianzishwa miaka minne iliyopita kwa ajili ya kujenga mfumo wa mtandao wa Serikali, kuimarisha uratibu, usimamizi na uzingatiaji wa viwango vya Serikali Mtandao katika utoaji wa huduma kwa umma. Pia, kuimarisha mifumo shirikishi ya Tehama na kuboresha uwezo wa taasisi za umma katika kutekeleza Serikali mtandao.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Ega, Dk Jabiri Bakari alisema sasa wamejikita kuhakikisha mifumo yote ya taasisi za umma inaingiliana kama ilivyobainishwa kwenye miongozo ya Serikali Mtandao ili kurahisisha mawasiliano na kuongeza uwajibikaji.

Upinzani Wamtega Rais Magufuli....Watumia Njia Mbadala Bungeni Kukumbushia Uuzwaji wa Nyumba za Serikali, Wadai MV Dar es Salaam Ni Jipu Lililoiva

$
0
0

Kambi ya Upinzani imelizidi maarifa  Bunge na kurejesha sakata la kuuzwa nyumba za Serikali ambalo juzi lilisababisha kiti cha Spika kuagiza yaondolewe maneno yanayomtaja Rais katika hotuba ya maoni mbadala.

Juzi, Kamati ya Kanuni za Bunge ilihariri hotuba ya msemaji wa kambi ya upinzani wa Wizara ya Mambo ya Ndani, ikiondoa maneno yanayomtaja Rais John Magufuli na badala yake kuweka neno Serikali kwenye sakata la uuzwaji nyumba za Serikali.

Kamati hiyo pia iliondoa suala la mkataba wa Jeshi la Polisi na kampuni ya Lugumi Enterprises, rushwa, mauaji ya wanasiasa, mwenendo wa Rais na Bunge kulinda wahalifu, jambo lililomfanya msemaji wa kambi hiyo, Godbless Lema kukataa kusoma hotuba yake.

Lakini jana katika hotuba ya kambi ya upinzani kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, mbunge wa Vunjo, James Mbatia alilirejesha sakata hilo akieleza kuwa ni muda sahihi kwa Rais John Magufuli kurekebisha kasoro zilizojitokeza wakati akiwa waziri ili kurejesha imani katika jamii.

Mbali na sakata hilo, pia Mbatia alizungumzia sakata la kivuko cha Mv Dar es Salaam ambacho kinatakiwa kifanye safari kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo, akikielezea kuwa “ni jipu ambalo limeiva kwa viwango vyote na sasa linatakiwa litumbuliwe mara moja”.

Suala la Mv Dar es Salaam liliungwa mkono na Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Zitto alisema kuwa hoja ya kivuko hicho lazima ichukuliwe hatua ili iaminike kuwa kuna nia ya dhati ya kupambana na ufisadi nchini.

“Naona suala hili linakwepwakwepwa, hivyo litolewe maamuzi,” alisema Zitto.

Pia mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini alisema suala la Mv Dar es Salaam kuwa iko chini ya kiwango, liliwahi kusemwa na mbunge wa upinzani lakini Serikali ikakataa.

Hata hivyo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) amesema ukweli katika ripoti yake. “Hili suala inabidi liangaliwe kwa kuwa kuna watu wanahitaji kutumbuliwa hivyo hao watu waangaliwe,” alisema Selasini.

Akisoma hotuba ya maoni mbadala ya kambi ya upinzani, Mbatia alisema wakala wa majengo nchini ndiye muhusika mkuu katika kuhakikisha nyumba za Serikali zinakuwa katika hali nzuri kwa watumishi wa Serikali kuishi.

“Katika muktadha huo, kambi ya upinzania inalikumbusha Bunge kwamba kati ya mwaka 2002 mpaka 2004 Serikali iliuza nyumba 7,921 na mpaka mwaka 2008 ilikuwa imejenga nyumba 650 tu,” alisema Mbatia.

Alisema katika biashara hiyo ya kuuza nyumba zilizokuwa mali ya Tamisemi, Serikali ilipata Sh252 milioni lakini sasa inahitaji kusaka zaidi ya mara mbili ya kiasi hicho kujenga nyumba za fidia.

Mbatia alisema Serikali ingetumia Sh677.6 milioni kujenga nyumba mpya ili zirejeshwe Tamisemi.

“Kwa vile hata wale waliouziwa nyumba hizo, kuna taarifa kati yao wapo walioziuza na kujipatia faida kubwa kinyume na mikataba ya mauzo hayo, kambi ya upinzani inapendekeza wanyang’anywe nyumba hizo kwa kukiuka mikataba na malengo ya mauzo.”

Mbatia alisema kumbukumbu rasmi za Bunge zinaonyesha Serikali ilitoa taarifa kuwa kamati iliundwa kuchunguza mchakato wa mauzo ya nyumba hizo na ilitarajiwa kumaliza kazi Februari 2007, lakini hadi leo hakuna taarifa iliyotolewa na Serikali na kuitaka Serikali ya Awamu ya Tano izirejeshe.

Feza na Lulu Wajitosa Kwenye Bifu ya Vanessa na Shilole

$
0
0
Msanii wa filamu Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Feza Kessy wamejitosa kwenye bifu la Shilole na Vanessa Mdee ambalo linaendelea katika mitandao ya kijamii.

Chanzo cha bifu ya Shilole na Vanessa hakijatambulika, lakini wawili hao toka jana wamekuwa wakirushiana maneno makali na vitisho katika mitandao ya kijamii hali ambayo imewafanya baadhi ya wasanii kuingilia kati sakata hilo la aina yake.

Muigizaji mahiri Elizabeth Michael ‘Lulu’ alikuwa moja kati ya msanii wa kwanza kutupia neno kwenye ugomvi huo kwa namna ya kushangazwa na jinsi watu wanavyosifia uzuri wao kupitia mitandao ya kijamii.

“Hebu nikazane kusoma nianze ligi za kikubwa na dada zangu wenye madegree na ma masters kama ‘Esilovey’ hizi ligi nyingine zinasikitisha,” aliandika Lulu kupitia Twetter huku akiongeza post nyingine kwa kuandika “Watu wanashindania uzuri, makalio, followers, nguo, outings, umaarufu, umaarufu wenyewe kama network ya mtandao unaokuwaga mpya, full kukatakata,”

Pia msanii wa muziki na mtangazaji wa Choice Fm, Feza Kezzy baada ya kuona stori inakuwa kubwa katika mitandao ya kijamii, aliandika ya moyoni kuhusu jinsi watu wanavyo shabikia mambo yasiyo na maana na kuacha kushabikia mambo ya msingi.

“Yaani watu wa ajabu sana, inabidi mbadilike. Watu wakifanya mazuri or kazi nzuri hamsemi, hamsupport, lakini umbea comments karibu laki moja dah. It’s very sad, bongo we need to change and support our talents Not tear them apart, Ntawacheka sana mkigundua labda hata ma star hawa hawana beef lol,” aliandika Feza kupitia instagram.

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

$
0
0
Picha zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao kuonyesha ufahari wa hali ya juu wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa dar es salaam.

Ofisi hiyo imekuwa tofauti kabisa na ile ya Mkuu wa mkoa aliyepita bwana Sadick, ofisi ya Makonda ina kompyuta kadhaa za apple,mapambo mengi ya kila aina yanayoashiria ufahari na utukufu wa hali ya juu kuliko hata ofisi ya rais.

Nani aligharamia ufahari huu wakati hata ikulu haijabadili muonekano? Kulikuwa na umuhimu wa kuweka ufahari huo katika kipindi hiki cha kubana matumizi?
Nini kilipungua katika ofisi ya aliyekuwa Mkuu wa mkoa mpaka ufahari uongezwe katika jiji ambalo limezungukwa na wananchi wenye hali ngumu na maisha yasiyoridhisha.

By iparamasa

Hizi Hapa Aina Nne za Wanawake Michepuko…..

$
0
0
1.MCHEPUKO LAMI: Huu ni ule ambao hauombi pesa, katulia hana mapepe, uwe naye au usiwe naye maisha yake yanaendelea tu.

2. MCHEPUKO VUMBI: Huu ni ule wa vibomu!! mara ooohhh sina pesa, naomba vocha, sijui simu imekufa, oooh mara nipo saluni nadaiwa elf thelathin, naomba nauli…..n.k! Na hii ndio noma maana njia kuu lazima washtuke mana mchepuko vumbi unachafua na unasumbua full time.

3. MCHEPUKO KOKOTO: Huu ni mkali zaidi ya njia kuu maana kila mara huuliza upo wapi, Uko na nani, why hupokei simu yangu? Kama uko kwako naomba utoke nje tuongee kidogo na leo uwe na mimi tu…Yaani tabu tupu!

4: MCHEPUKO MATOPE: Yaani huu usiombe hata kukutana nao maana wenyewe ndio funga kazi.. Huu bana unajua kuchuna hasa ila pale unapoupa pesa na wenyewe unaenda kuzihonga zote kwa mchepuko wake mwingine yaani hatari tupu

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi ya May 19, Ikiwemo Uuzwaji Nyumba za Serikali Mwiba

$
0
0

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi ya May 19, Ikiwemo Uuzwaji Nyumba za Serikali Mwiba

EgyptAir Flight MS804 Disappears From Radar Between Paris and Cairo – Live Updates

$
0
0


Flight MS804 has now been missing for four hours: last contact was at 02.45 local time. It is now 06.45 in Cairo, where it has been daylight for close to two hours.

A further update from EgyptAir:

It confirms that 56 passengers were on board, including one child and two babies

It says the captain has 6,275 flying hours, including 2,101 on the A320; the copilot has 2,766.

The plane was manufactured in 2003.

Specialist teams and the Egyptian armed forces are still searching for the plane.

Egypt air is following the situation closely with the relevant authorities through the integrated operations centre.

The company also provides free contact numbers: 0800 7777 0000 from any landline in Egypt and + 202 2598 9320 outside Egypt or any mobile in Egypt.

Hizi Hapa Picha za Waliombaka na Kumlawiti Binti wa Miaka 21 Huku Wakimrekodi na Kusambaza Video Mtandaoni

$
0
0
WATU sita wanaodaiwa kumbaka na kumlawiti msichana kisha kumrekodi na kusambaza video hiyo, leo wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro.

Miongoni mwa watuhumiwa hao ni pamoja na Iddi Adamu Mabena (32) Mkazi wa Njombe na Zuberi Thabiti (30) Mkazi wa Mbalali, Mbeya ambapo kesi hiyo inasimamiwa na waendesha mashtaka watatu wa serikali- Grolia Rwakibalila, Edgar Bantulaki na Kalistus Kapinga.

Akisoma maelezo ya kosa katika shtaka la kwanza la kubaka na kulawiti, Wakili Rwakibalila aliwataja wahusika kuwa ni pamoja na Iddi Adamu na Zuberi Thabiti.

Mwendesha mashataka huyo amedai kuwa, washtakiwa hao kwa pamoja huku wakijua kufanya hivyo ni kosa, walimbaka na kumlawiti msichana mwenye umri wa miaka 21 na kumsababishia maumivu makali.

Wakili huyo alidai kuwa, washtakiwa hao walimbaka na kumuingilia kinyume na maumbile msichana huyo tarehe 27 Aprili, saa 1 usiku katika  nyumba  ya  kulala  wageni ya Titii iliyopo  katika Tarafa  ya  Dakawa  Wilaya  ya  Mvomero.

Hata hivyo, mawakili wote wa serikali walipinga dhamana ya washtakiwa hao kwa madai kuwa, kesi hiyo imegusa hisia za watu wengi hivyo kwa usalama wao pia kuhofia kuharibu ushahidi ni bora waendelee kushikiliwa.

Mbele ya Marry Moyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi washtakiwa hao walikana kuhusika na mashtaka hayo ambapo wamerudishwa rumande baada ya kukosa dhamana. Kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo Juni Mosi mwaka huu na kwamba, upelelezi haujakamilika.

Katika shtaka la pili washtakiwa hao wakiwa na wenzao wanne walipandishwa kizimbani katika mahakama hiyo wakikabiliwa na shtaka la kusambaza picha chafu za ngono katika mtandao wa kijamii wa whatsapp.

Edgar Bantulaki, mwendesha mashataka amedai kuwa, washtakiwa hao wamefanya kosa hilo chini ya kifungu cha sheria namba14 (1) (b) na 2 (b) cha Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015.

Bantulaki amewataja washtakiwa wengine kuwa ni pamoja na mshtakiwa namba 1 na 2 na Rajabu Salehe, (30), Ramadhani Ally (26), Muhsin Ng’ahy (36), John Peter (24) wote wakiwa ni wakazi wa Wami, Dakawa wilayani Mvomero.

Mwendesha mashtaka huyo amedai kuwa, washtakiwa wote kwa pamoja walianza kusambaza picha hizo kati tarehe 28 hadi 30 Aprili mwaka huu wilayani Mvomero na mkoa mzima wa Morogoro kupitia mtandao wa kijamii wa Whatsapp.

Hata hivyo Ignas Kunge, wakili wa mshtakiwa wa nne (Ally) aliiomba mahakama kumpa dhamana mshtakiwa wake jambo lililopingwa na mawakili wa serikali kwasababu suala hilo limegusa jamii zaidi pia kwasababu za kutoingilia na kuharibu upelelezi wa kesi hiyo.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Ivan Msaki, washtakiwa hao walikana kuhusika na shtaka hilo ambapo wamerejeshwa rumande hadi kesi hiyo itakapotajwa tena Juni Mosi mwaka huu kwa ajili ya kusikilizwa kwa kujadiliwa suala la dhamana iliyopingwa kwa kiapo na mawakili wa serikali.

Urlich Matei, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro amesema, washtakiwa hao wamepandishwa kizimbani kati ya 11 waliokuwa wakituhumiwa kuhusika na tuhuma hizo kufuatia upelelezi kutokamilika dhidi yao.

Kamanda Matei amesema, katika hatua za awali upelelezi kipolisi ulikamilika kwa watuhumiwa sita wa mwanzo ambao ndio wamefikishwa mahakamani.

Aidha amesema kuwa, vitendo vilivyofanywa na watuhumiwa ni vibaya na ambavyo kamwe haviwezi kuvumiiwa na jamii katika nchi.

Hivyo ametoa rai kwa wananchi kuacha kufanya uhalifu kwa kutumia mitandao kwani sheria yake iliyopitishwa na bunge hivi karibuni haitamwacha mtu akiwa salama.

Hata hivyo kamanda huyo ameomba polisi wapewe kifaa kama cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ili waweze kufanya kazi zao kwa uhuru na kukamilisha mwenendo wa kesi mapema.

Amesema, kwa sasa uhalifu kwa njia ya mitandao unakuwa kwa kasi duniani kote na kwamba, mtu anaweza kutenda makosa mengi yanayosumbua jamii ikiwemo wizi mkubwa na mdogo wa fedha kwenye benki, makosa ya udhalilishaji, lugha za matusi na mengine mengi.

Amesema kuwa, kupatikana na kifaa hicho kutasaidia ushahidi kuwa madhubuti na sio rahisi kumwondoa mtu katika hatia.

Pia amewataka wananchi wote hususan vijana kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo yao badala ya kutumia muda mwingi katika mitandao  ya kijamii

Zuberi Thabit mtuhumiwa wa ubakaji.
Idd Adamu mtuhumiwa wa kurekodi video za ubakaji.

TRA Yabakiza Tshs. Trilioni 2.363 Kufikia Lengo Lao

$
0
0
Na Ally Daud- Maelezo.
Mamlaka  ya mapato Tanzania (TRA) imebakiza Tsh. Trilioni 2.363 ili kufikia lengo  waliojiwekea la kukusanya mapato ya trilioni 12.363 katika  mwaka wa fedha 2015/16, ambapo hadi sasa imekusanya kiasi cha Tsh. Trilioni 10.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi  wa awamu ya pili ya mpango wa mafunzo kwa wafanyakazi waliopo kwenye fursa ya ajira za taasisi hiyo  Kamishina Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata alisema taasisi yake imefanikiwa kukusanya kiasi cha  sh trilioni 10 katika muda waliojiwekea na kuahidi kumalizia kiasi cha shilingi trilioni 2.363 kabla ya mwaka mpya wa fedha wa Serikali unaoanza mwezi Julai mwaka huu.

“Tumejiwekea malengo ya kukusanya kiasi cha fedha cha shilingi trilioni 12.363 kwa mwaka huu wa fedha na tumefanikiwa kukusanya shilingi trilioni 10 mpaka mda huu ila tunaendelea na kutimiza lengo letu hadi kufikia July mwaka huu na tutajipanga upya mwaka ujao wa fedha kufikia malengo mapema” alisema Bw. Kidata.

Aidha Bw. Kidata amesema kuwa kwa mpango huo wa mafunzo ulioanzishwa kwa  kushirikiana na Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) ni mafunzo ya mwaka mmoja yanayoendana na usaili mpya kwa wahitimu ili  kufanya Mamlaka hiyo kuwa na wafanyakazi waadilifu na wachapa kazi ili kupaisha uchumi nchi.

Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha cha Usimamizi wa Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo alisema kuwa wameamua kuanzisha mpango huo kwa kushirikiana na Mamlaka ya mapato  ili kufundisha wafanyakazi wa TRA maadili na nyenzo za utendaji kazini  pamoja na kuendesha mafunzo ya dini ili kuwafanya wafanyakazi wawe wacha mungu katika kazi zao.

Aidha Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa TRA Bw. Victor Kimaro aliwataka wafanyakazi wote wanatakiwa wafanye kazi kwa maadili hususani upande wa ukusanyaji kodi na Chuo hicho kimewafundisha wafanyakazi hao kufanya kazi kwa ushindani katika maeneo ya kazi ili kuliletea taifa maendeleo yaliyokusudiwa.

Video: Giggy Money Adai kuwa Hata Akiwa Hawara Kwa Matonya Hamna Shida

$
0
0
Story ambazo zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Matonya kwa sasa anatoka kimapenzi na Giggy Money huku wakisikika kuwa ni kick ya ngoma yao ya Supu.

Katika mahojiano waliyofanya na ENewz wote wawili walishindwa kukubali moja kwa moja kuwa wameanguka pamoja kitandani au hawajaanguka kitandani lakini walibaki kusifia Supu huku Giggy Money akisema kuwa Matonya kwake ni zaidi ya mpenzi

Mbunge wa CCM Anusurika Kupigwa na Wabunge wa UKAWA

$
0
0
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Jackline Msongozi juzi jioni alinusurika kipigo kutoka kwa wabunge wanawake wa UKAWA baada ya kuwaeleza kuwa upande huo una wabunge wawili tu wenye michango ya maana ambao ni Upendo Peneza (Viti Maalumu Chadema) na Magdalena Sakaya (Kaliua - CUF).

Akichangia mjadala wa bajeti kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Msongozi aliishambulia kambi ya upinzani akieleza kuwa kuna mlevi mmoja amechangia upande wa upinzani kuhusu uuzwaji wa nyumba za Serikali wakati waliohusika na uuzwaji huo wamehamia upinzani ambao ni Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.

Msongozi alisema hakuna mke mwenza anayeweza kumsifia mwenzake, hivyo upinzani hauwezi kuisifia CCM kutokana na kazi wanayoifanya.

Baada ya kusema maneno hayo na wabunge wengine kuchangia, Bunge lilipoahirishwa wabunge wanawake wa upinzani wakiongozwa na Sabrina Sungura na Ester Matiko walimfuata Msongozi wakitaka kumshambulia, lakini aliondoka moja kwa moja pasipo kusimama popote.

Sungura alipoulizwa alisema kuwa mbunge huyo angesimama wangemshughulikia
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images