Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Vanessa Mdee Aelezea Changamoto Kubwa zaidi Waliyonayo Wasanii wa Kike

$
0
0
Baadhi ya waigizaji wa kike wa filamu nchini Marekani waliwahi kulalamika utofauti wa malipo kati yao na wanaume.

Kinachowaumiza zaidi ni kuwa wanaume hulipwa malipo makubwa zaidi kuliko wao hata katika uhusika unaofanana. Kwa mujibu wa Vanessa Mdee, hilo ni tatizo kubwa pia lililopo kwenye muziki wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.

“Kubwa zaidi ni masuala ya bookings msanii wa kike kupewa kile anachostahili, mwanaume atalipwa zaidi siku zote japo msichana ana hit song anaweza kuvuta wale wale atakaovuta akinakaka,” Vanessa aliiambia 255 ya XXL kupitia Clouds FM.

Exclusive VIDEO: Mbunge Agness Marwa Akisema na Walioisambaza CV yake Mitandaonia

$
0
0
Alianza kuongelewa kwenye mitandao ya kijamii Tanzania baada ya video yake kusambaa akichangia bungeni kwenye bunge la bajeti Dodoma na kusema haoni sababu ya bunge kurushwa live lakini apia kauli yake nyingine iliyosambaa ni ile aliyosema anatamani hata kulia.

Baada ya hapo watu wakaitafuta CV yake na kuisambaza mitandaoni ikionyesha alianza Form One akiwa na miaka 30, amekuwa mkurugenzi wa kampuni ya Aggy Classic Entertainment bado akiwa ni mwanafunzi wa kidato cha pili, yote hayo ameyaona na anayajibu kwenye hii video hapa chini

Video:

AUDIO: Kauli ya Kwanza ya Mkwasa Baada ya Kumuita Cannavaro ‘Taifa Stars’

$
0
0
Kocha wa timu ya Tanzania Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa ameeleza amejibu kwa nini amemuita Nadir Haroub Cannavaro katika kikosi licha ya staa huyo kutangaza kuwa amestaafu kuichezea Taifa Stars.

“Labda niseme tu mimi sijapata taarifa za yeye kujiuzulu timu ya taifa wala ofisi kunipa barua yoyote, mimi nimeona uzoefu wake bado unahitajika katika timu nimeona nimuite, kuhusu kustaafu lazima astaafu kwa heshima sio kienyeji tu hatuwezi kumfanyia hivyo”

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Nadir Haroub Cannavaro alitangaza kustaafu kucheza timu ya Taifa ya Tanzania, baada ya kuvuliwa unahodha pasipo taarifa rasmi na uongozi kumpatia nafasi hiyo Mbwana Samatta.

Miaka Miwili Baada ya Kutekwa Wasichana 276 na Boko Haram, Mmoja Apatikana Akiwa Mjamzito

$
0
0
Kama unazikumbuka story za kundi la Kigaidi la Boko Haram kuteka wasichana 276 Nchini Nigeria, sasa leo taarifa zilizopatikana ni kwamba binti mmoja amepatikana baada ya miaka miwili.

Binti huyo kwa jina la  Amina Ali amepatikana akiwa na ujauzito kwenye msitu wa Sambisa huko kaskazini mwa  Nigeria ambapo ndipo walikuwa wamefichwa wasichana hao.

Wasichana hao ambao huitwa ‘chibok girls‘ ambao ni wanafunzi wa shule ya bweni walitekwa na magaidi hao wakiwa shuleni.

Zitto Kabwe, Halima Mdee na John Heche Wawekwa Kitimoto, Wahojiwa Kwa Dadkia 90 Kwa Kufanya Fujo Bungeni

$
0
0
MBUNGE wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto (ACT-Wazalendo) na wenzake wawili, jana wamehojiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge, George Mkuchika kwa kufanya fujo bungeni kuhusu suala la Bunge kutorushwa ‘live’.

Mbali na Zitto, wengine waliohojiwa ni pamoja na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche (Chadema). Wabunge hao walihojiwa kwa tuhuma za kufanya fujo bungeni wakati ilipotolewa hoja ya Bunge kutorushwa moja kwa moja ‘live’, akiwa pamoja na wabunge wawili; Mdee na Heche.

Chanzo cha uhakika kutoka ndani ya kamati hiyo, kimesema Zitto alihojiwa na kamati hiyo kwa muda wa zaidi ya saa moja kwa makosa mbalimbali, ikiwamo kufanya fujo bungeni Januari 27, mwaka huu.

Taarifa hizo zilieleza kuwa Zitto alifanya fujo hizo baada ya Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge, kuahirisha kujadili hoja ya serikali iliyowasilishwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, kuhusu Bunge kutorushwa ‘live’.

Hatua hiyo inatokana na hoja iliyowasilishwa na Zitto aliyetaka kuahirishwa kujadili hotuba ya Rais kutokana na kauli ya Waziri Nape ya kutorushwa matangazo ya moja kwa moja ya Bunge.

Zitto, alihojiwa na kamati hiyo ya Mkuchika kwa kilichoelezwa alisimama na kuomba mwongozo kuhusu jambo ambalo limekwishatolewa uamuzi kinyume na Kanuni ya 72 (1) na 68 (10 ya Kanuni za Kudumu za Bunge toleo la Januari 2016.

Mbali na hilo pia anadaiwa kusimama na kuzungumza bila utaratibu kinyume na Kanuni ya 60 (2) na 12 ya Kanuni za Kudumu za Bunge, jambo ambalo lilileta fujo na kuvunja shughuli za Bunge.

Katika barua za mwito zilizosainiwa na Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah, Mei 12, mwaka huu, inaelezwa kwamba pamoja na mambo mengine na Mwenyekiti wa Bunge kumsihi mbunge huyo bado aliendelea kuzungumza na kusimama ikiwa ni kuonesha dharau kwa mamlaka ya Spika na shughuli za Bunge kinyume na kifungu namba 24 (d) na (e) cha Sheria ya Kinga na Haki za Bunge.

Barua hiyo ilieleza kuwa kutokana na vitendo hivyo vinavyokiuka Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge, Sura namba 296 na Kanuni za Bunge, wabunge hao walionywa kuwa endapo wasingefika mbele ya kamati hiyo jana hatua za kisheria zingechukuliwa dhidi yao kwa mujibu wa kifungu cha 15 na 31 (1)(a) na sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge.

Edward Lowassa na Fredrick Sumaye Watajwa Katika Sakata la Uuzwaji wa Nyumba za Serikali.......Mbowe Atoa Ufafanuzi

$
0
0
Uuzwaji wa nyumba za serikali umegeuka mwiba huku wabunge wakiendelea kuhoji hatua zilizochukuliwa kutokana na kadhia hiyo

Hatua hiyo iliyotekelezwa mwaka 2002  hadi 2004 ilizusha malalamiko mengi tangu wakati huo na sasa imeibuka tena bungeni

Akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na mawasiliano jana, mbunge wa Nachingwea, Hassani Masala (CCM) alihoji mfumo uliotumika kuuza nyumba za serikali

Alisema haungi mkono kwa vile umesababisha viongozi wapya wa serikali wanaoteuliwa kujikuta wakiishi katika nyumba za wageni.

Mjadala huo uliibuliwa juzi na msemaji wa kambi ya upinzani Bungeni kupitia kwa waziri kivuli wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Godbless Lema kabla ya Mwenyekiti wa Bunge Mussa Azzan Zungu kumtaka kuondoa baadhi ya maneno katika hotuba yake likiweo suala la uuzwaji wa nyumba za serikali.

 Ritha Kabati Amvaa Lowassa
Akichangia mjadala huo jana, Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Ritha Kabati alimtaja aliyekuwa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa kuwa alinunua nyumba ya serikali iliyouzwa mwaka 2002 yenye jengo namba 68.

Alisema hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ilisema nyumba za serikali 7,921 ziliuzwa tangu mwaka 2002 hadi 2004 na kutaka serikali ya awamu ya tano kurejesha nyumba hizo kutokana na walionunua kukiuka mikataba na malengo ya mauzo.

“Naomba niwaambie usiangalie boriti lililo katika jicho la mwenzako wakati kwako lipo, kwani hata mgombea wao wa urais Edward Lowassa alihusika kwa kununua nyumba ya plot namba 68 na Fredrick Sumaye alikuwa Waziri Mkuu na kuhusika kuuza nyumba hizo,” alisema Kabati.

Baada ya kueleza hayo, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema) aliomba kumpa taarifa mbunge huyo kuwa taarifa hiyo ni kwa maslahi ya taifa, hata kama mhusika atakuwa katokea kambi ya upinzani sheria itachukua hatua.

"Kambi ya upinzani tunapoibua jambo huwa linakuwa kwa maslahi ya Taifa, hivyo ni vyema wabunge wote mtambue kuwa kosa likifanywa na kiongozi  ni lazima hatua zichukuliwe bila kujali ni wa Chadema, CUF au CCM.

"Tunapokuwa tunatoa uamuzi kama kambi ina maana sheria ifuate mkondo wake." Alisema Mbowe huku akishangiliwa na wabunge wa UKAWA

Awali katika michango mbalimbali ya wabunge wa upinzani wamekuwa wakilalamikia kuuzwa nyumba hizo za serikali na kudai kuwa watumishi wapya wengi walioajiriwa, wamekuwa wakikosa maeneo ya kuishi.

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) akichangia mjadala huo alilalamikia kuuzwa kwa nyumba hizo pamoja na nyingine za Tazara zipatazo 500 na kuamua kumpatia Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano ripoti aliyodai inaonesha nyumba hizo zilivyouzwa.

Ndege ya Kivita ya Marekani Yaanguka na Kuungua na Moto Vibaya....

$
0
0

Ndege ya kivita ya Marekani aina ya B-52 imeanguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka kwenye kambi ya taifa hilo eneo la Guam.

Jeshi la Marekani limesema wanajeshi wote saba waliokuwa kwenye ndege hiyo walifanikiwa kuruka salama kutoka kabla ya ndege hiyo kuteketea.

Ndege hiyo ilikuwa imepaa kutoka kituo cha jeshi cha Andersen.

Picha zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zimeonesha moshi mkubwa ukitanda angani kutoka kwa vifusi vya ndege hiyo.

Ndege hiyo, ambayo hutumiwa kuangusha mabomu, ilitumwa Guam kutoka jimbo la North Dakota na ni sehemu ya juhudi za Marekani za kuendeleza uwepo wake kijeshi katika bahari ya Pasifiki.

Gavana wa jimbo la Guam amenukuliwa na tovuti ya habari ya Kuam akisema kwamba halikuwa shambulio.

Ndege aina ya 5-52 zimetumiwa na Marekani kwa miaka 60 sasa, na zilichangia sana vita Vietnam na Afghanistan.

Guam ni jimbo linalomilikiwa na Marekani eneo la Micronesia, Pasifiki magharibi na hupatikana kilomita 6,000 magharibi mwa Hawaii.

Mwaka 2008, wanajeshi sita walifariki baada ya ndege aina ya B-52 kuanguka karibu na Guam.

Wapiganaji wa Kiislamu Wadai 'Wamo Tanzania'

$
0
0

Aliyesambaza video hiyo anasema wana uhusiano na Islamic State

Kundi la watu wanaojidai kuwa wapiganaji wa Kiislamu limeweka video mtandaoni likidai uwepo wa wa wapiganaji wa Kiislamu nchini

Video hiyo inawaonesha wanaume hao wakiwa wamejifunika nyuso zao kwa vitambaa na barakoa.
Wanadai wamo katika mji wa Tanga na kuwahimiza Waislamu katika taifa hilo la Afrika Mashariki kujiunga na kampeni yao.

Ukurasa wa Twitter ambao unasambaza video hiyo ya dakika tano unasema wanaume hao ni tawi la Afrika Mashariki la kundi linalojiita Islamic State (IS).

Mwandishi wa BBC anayeangazia masuala ya usalama Afrika, Tomi Oladipo, anasema hakuna ushahidi wa uhusiano wa moja kwa moja kati ya wapiganaji hao na kundi la Islamic State.

Source: BBC

Wabongo Wataja Njia 3 za Kumaliza Sakata la Lugumi

$
0
0

Sakata la Kampuni ya Lugumi Enterprises inayomilikiwa na Said Lugumi (pichani) kudaiwa kuingia mkataba tata wa mabilioni ya shilingi wa kufunga mashine za kutambua alama za vidole kwenye vituo vya polisi nchini, limeingia mitaani huku baadhi ya Wabongo wakitaja njia 3 za kumaliza ishu hiyo.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, baadhi ya wananchi walionesha shaka yao kuhusu sakata la Lugumi kuwa gumzo likiumiza vichwa vya wabunge kama vile mhusika amekwenda Ulaya, hivyo wakatoa maoni yao.

Shida Waziri, mkazi wa Ubungo External, Dar alisema: “Lugumi mwenyewe tunaambiwa hayupo mbali, anaendelea kuishi kwa amani hapahapa Tanzania. Mimi nashauri aitwe, ahojiwe mbele ya jopo la watu maalum, wakiwemo Usalama wa Taifa.

“Hii itasaidia sana kwani ataweza kuanika kila kitu. Mkataba ulivyokuwa, ulivyokwenda, nani na nani walihusika.”


John Joseph, mkazi wa Kigogo, Luhanga, Dar: “Mimi nashauri serikali iunde jopo nje ya wabunge, ila wawepo Usalama wa Taifa. Wapite kituo hadi kituo cha polisi na kutaka kuziona kwa macho hizo mashine, basi.

“Baada ya siku kumi na nne tu jopo litajua kituo gani kilifungwa, kituo gani hakikufungwa. Maana tunahisi kuna mzunguko mkubwa pasipo sababu.”

Mwanahawa Ally, mkazi wa Ilala, Dar: “Njia pekee ya kumaliza sakata la Lugumi ni kuwaita wachunguzi wa kimataifa kama wale New Scotland Yard ya Uingereza. Wale ni wapelelezi wa kila jambo hata liwe la siri kwa kiasi gani.

“Wamebobea katika kuchunguza shaka yoyote ile. Kwa hiyo naamini wakitumika wale wanaweza kuleta majibu. Huwa wanaitwa katika nchi mbalimbali duniani kwa ajili ya kuchunguza mambo magumu.”

Wakati huohuo, baadhi ya wananchi wamesema hawaoni sababu ya baadhi ya wabunge kumsakama Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga kuwa anahusika na mkataba wa Lugumi bila kuweka ushahidi usio na shaka.

“Mimi nawasikia wabunge wakisema Kitwanga ajitetee sakata la Lugumi. Ajitetee nini wakati ushahidi wenyewe wanaouweka ni wa kuungaunga tu. Hata Mahakama haihukumu jambo bila kupata ushahidi usio na shaka,” alisem Jumanne Mshindo, mkazi wa Buguruni, Dar.

TUJIKUMBUSHE
Mwaka 2011, Kampuni ya Lugumi ilipewa zabuni ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo vya polisi 108 nchini ambapo inadaiwa imeshalipwa Sh. bilioni 34 kati ya bilioni 37, sawa na asilimia 99 ya malipo yote.

Hata hivyo, kuna madai kwamba ni vituo 14 tu vilivyofungwa mashine hizo huku mashine moja pekee ikiwa ndiyo inayofanya kazi.

Vifaa hivyo vingeweza kutambua alama za vidole kwa wahalifu hasa wale wanaofanya uhalifu sehemu moja na kukimbilia nyingine.

Kufuatia sakata hilo, Aprili 21, mwaka huu, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Aeshi Hilary aliunda kamati ndogo yenye wabunge tisa, kuchunguza kwa kina mkataba huo na kupewa siku 30 za kufanya kazi hiyo kisha taarifa itatolewa bungeni.

Kamati hiyo itawahoji mawaziri, viongozi wa jeshi la polisi waliopo na waliostaafu, wafanyabiashara waliotajwa pamoja na kampuni zilizoshiriki kufunga mashine hizo.

Alikiba Ala Shavu Kubwa....Asaini mkataba na Sonny Music Huko South Africa

$
0
0
Alikiba baada ya kusaini mkataba huo amewashukuru mashabiki wake kwa support waliompa toka aliporudi na wimbo wake wa 'Mwana' mpaka leo hii na kusema atafanya sherehe na mashabiki zake ili kufurahi nao baada ya kuweza kusaini mkataba na 'Sony Music'

"Nataka kukumbuka nilivyorudi kwenye game 2014 toka nimepumzika, nimepiga hatua kubwa sana na hii ni kutokana na support kutoka kwa mashabiki, mtanisamehe mashabiki pale nilipokosea, ila kwa furaha niliyonayo leo kusaini mkataba huu naomba nikirudi nifanye party ili nifurahi pamoja na mashabiki zangu ambao walikuwa na mimi mwanzo mpaka sasa" alisema Alikiba.

Mbali na hilo Alikiba amewashukuru waandishi wa habari na vyombo vya habari ambavyo vilikuwa vikimpa support kwenye kazi zake za muziki siku zote.

"Msiumizwe Komando Nipo Napigana"- Lady Jaydee

$
0
0
Jay dee ameyasema hayo alipokuwa akiongea East Africa Televishion, na kusema kuwa muziki ni kila kitu kwake, na hajioni yeye bila muziki.

"Mafanikio yangu mpaka kufika hapa naweza nikasema ni nidhamu niliyonayo kwenye kazi yangu, nauheshimu sana muziki, kwani ni kila kitu kwangu, sijioni mimi bila muziki, hivyo nauthamini sana", alisikika Lady jay dee akisema.

Jay dee ambaye kwa muda alikuwa kimya kwenye muziki na kuibuka na wimbo wa NdiNdiNdi ambao umepokelewa vizuri, amesema hakutarajia kama NdiNdiNdi ungekuwa wimbo mkubwa, kwani hakuwa kabisa na hisia za kutoa kazi yoyote kwa muda huu.

"Unajua baada ya kukaa kimya, sikuwa na hisia ya kuandika wimbo wowote, nikakaa na watu Seven, akaandika, na kuna mtu mwingine kutoka Uganda nae akaandika, lakini waliandika mashairi ambayo walijua nitauvaa uhusika ipasavyo, zikaandikwa na nyingine lakini NdiNdiNdi ndo ikapitishwa itoke, hata sikufikiria ingekuwa kubwa, lakini nashukuru watu wameipokea vizuri sana", alisema jay dee.
Pamoja na hayo Jaydee ambaye amejielezea yeye ni mwanamke mpole lakini ana hasira pale anapokosewa, amewataka mashabiki wake wasiwe na wasi wasi na wasiumizwe na lolote, kwani komando wao yupo vitani anapigana.

Majaliwa: Rais Magufuli hakukosea kuzuia sukari kuingia nchini kiholela2

$
0
0
Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema kauli ya Rais John Pombe magufuli ya kuzuia kuingizwa kwa sukari kiholela nchini ilikuwa ni katika kulinda viwanda vya ndani.

Aidha Majaliwa amesema kuingia kwa sukari Tani 70,000 toka nje ya nchi hakutaathiri uzalishaji wa viwanda unaotarajiwa kuanza mapema mwezi julai.

Akijibu swali la kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni na mbunge wa jimbo la Hai, Freeman Mbowe, Majaliwa amesema uhaba wa sukari ni tani 100,000 na uwezo wa viwanda kuzalisha ni tani 320,000 huku mahitaji ya sukari kwa mwaka mzima ni tani 420,000.

Amesema katika kukabiliana na uhaba uliopo Serikali kupitia bodi ya sukari imeagiza sukari nje ya nchi na tayari Serikali imeshaanza kupanga mikakati ya kudumu ya kumaliza tatizo la sukari kwa miaka ijayo.

Akiuliza swali la nyongeza Mbowe alimtaka waziri mkuu kuwahakikishia watanzania kuhusu bei elekezi na kutaka kujua ni lini uraismu wa uanzishwaji wa shamba/kiwanda eneo la bagamoyo utakavyo malizwa.

Akijibu swali hilo Waziri Mkuu amesema swala la kuanzisha shamba katika eneo la bagamoyo lina mchakato mrefu na halina urasimu wowote.

Amesema shamba hilo limepakana na mbuga ya saadani na kwamba linategemea sana maji ya mto Wami, lakini pia wanyama nao wanategemea maji ya mto huo.

Hivyo amesema serikali na wadau wanaendelea kuangalia suala hilo kwa umakini ili kutoa maamuzi yatakayo leta tija kwa taifa.

Kuhusu bei elekezi ya sukari amesema tayari bodi ya sukari imeshaanza kusimamiasuala hilo, ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua wale wote watakaopandisha sukari kiholela

Jerry Muro:Pesa za CAF Tutaisaidia Simba Kulipa Deni la Musoti Wasije Shushwa Daraja

$
0
0
Klabu ya Yanga kupitia kwa mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano Jerry Muro, wamesema wako tayari kuisaidia Simba kulipa deni la Musoti ili klabu hiyo ya Msimbazi isishushwe daraja.

Muro amsema, wako tayari kuichangia Simba kulipa deni lao linalowakabili ili FIFA isiishushe daraja na wao wakakosa pointi sita katika msimu ujao wa VPL.

“Tunaomba watuletee barua na karatasi za malipo za yule mchezaji ili sisi tu-process malipo kwa sababu tuliahidi tukifika hatua ya makundi ya michuano ya Afrika tutawasaidia kulipa deni lao. Sisi hatukubali Simba ishushwe daraja kwasababu pale tunapointi sita za wazi kwenye msimu ujao wa ligi”.

“Sasa kwanini tukose pointi sita ambazo tunaweza tukazitetea zikabaki. Inaweza ikashuka Simba halafu ikapanda timu ya Milambo ya Tabora halafu ikatusumbua sana, sisi tunazihitaji ponti sita za Simba na tulisema tukifika hatua ya makundin tutawalipia”.

“Ili tuweze kufanya transaction na kwakua hela hii inalipwa kupitia FIFA, tutawaandikia CAF barua ya kufanya malipo kwenda FIFA ili kuisaidia Simba isishuke daraja. Mhasibu wetu anasubiri karatasi za malipo na kwakua malipo yanafanyika kwa dollar, tutawaandikia CAF watoe kiasi cha pesa kwenda FIFA kwa ajili ya kuwasaidia ndugu zetu”.

Simba imeelezwa kupuuza kumlipa mchezaji Donald Musoti Omanua kwa wakati tangu mkataba wake uvunjwe. Musoto aliyesajiliwa na Simba msimu wa 2014/15 na kuachwa alilalamika FIFA ambayo iliona ana hoja na hivyo Simba kutakiwa kumlipa dola 29,250 (sawa na Sh 62.8 milioni) na kiasi kingine anachodai ni Dola 600 (Sh 1,290,000) zilizobaki katika usajili ambapo jumla yake ni Sh 64.2 milioni. Pia Mosoti anamlipa Mwanasheria wake dola 2,000 (Sh 4.3 milioni) kwa ajili ya kusimamia kesi hiyo.

Video:Alikiba Anakualika Kuitazama Video yake Mpya Inaitwa ‘Aje’

$
0
0
Alikiba anakualika kuitazama video yake mpya inaitwa ‘Aje’ ambayo imefanyika Cape Town South Africa ikiwa ni single yake ya kwanza kutoka chini ya mkataba na Sony Music aliousaini leo May 19 2016 Johannesburg South Africa, ukishaitazama utuachie comment yako ili akipita hapa na timu yake wajue watu wanasemaje

Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Katika Magazeti na Mitandaoni leo 19 May 2016

$
0
0

Machozi Band Imekufa Haipo Tena, Sitaki Kuitwa Binti Machozi Tena- LadyJaydee

$
0
0
Akongea na East Africa Tv Jaydee amsema ameamua kubadili jina hilo kwani hata yeye sasa hivi hatumii jina la Binti Machozi, akiamini msemo wa watu kuwa jina huzaa maana yake kwenye maisha.

"Band kwa sasa haaitwi tena Machozi Band, inatwa The Band, nilibadilisha miaka miwili iliyopita na kwasababu sasa hivi mwenyewe sikutaka kuitwa binti machozi, watu wanasema jina unaloitwa linarelate na maisha yako, so nikaamua kubadili, kwa hiyo Machozi Band haipo tena imekufa, kwa sasa itakuwa ni lady jaydee and the band", alisema Jay dee.

Jaydee ambaye mwisho wa wiki hii anayatajia kufanya tamasha kubwa la 'Naamka tena', amesema tamasha hilo litakuwa ni la masaa matatu bila kupumzika, kwani ana nyimbo zaidi ya 100 ambazo zinaweza zikamfanya afanye show zaidi ya masaa matatu.

Bondia Manny Pacquiao Ashinda Nafasi ya Useneta Katika Bunge Nchini Filipino

$
0
0
Bondia mwenye jina kubwa katika ulimwengu wa ngumi Manny Pacquiao May 19 2016 ameingia kwenye headlines baada ya kufanikiwa kushinda nafasi ya Seneta katika bunge nyumbani kwao Filipino, Pacquiao amefanikiwa kushinda nafasi hiyo kwa kura milioni 16.

Pacquiao anakuwa ni miongoni mwa watu 12 waliofanikiwa kushinda nafasi ya Seneta katika bunge la Filipino, ushindi wa bondia huyo maarufu unatoa tafsiri huenda siku akapata nafasi ya kugombea nafasi za juu za uongozi wa nchi hiyo hususani Rais.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Manny Pacquiao mwenye umri wa miaka 37 amefanikiwa kushinda mataji kadhaa ya Ubingwa ngumi, Pacquiao ndio bondia aliyepigana na Mayweather na kupoteza kwa point katika pambano linalotajwa kutazamwa na mamilioni ya watu duniani kote.

Mwanamuziki JUMA JUX Ametoka na Muonekano Mpya...Tazama Picha Hapa

$
0
0
Kama wewe utakuwa mpenzi wa kufuatilia style za wasanii kuanzia mavazi mpaka Life style zao basi hii isikupite mtu wangu May 19 2016 msanii kutoka kiwanda cha bongoflevani Juma Jux amezichukua headline kutokana na muonekano wake mpya wa nywele.

Jux aliyaandika maneno haya chini ya picha aliyopost kwenye mtandao wake wa Instagram:

’Sometimes you have to believe in yourself and do what you want, uwezi kupendwa na wote na uwezi kumfuraisha kila mtu #jiamini #hapo #wivu #aftricanboy‘ Usisahau kuniachia comment yako hapa mkali huyu ataiona.

Basi la Mwendo Kasi Lagonga na Kuua Mtoto Jijini Dar es Salaam

$
0
0
Basi la mwendo kasi ( DART)  limemgonga na kumuua mtoto huku mama yake akinusurika baada ya pikipiki waliyokuwa wamepanda kushindwa kulipita basi hilo

Ajali hiyo imetoke leo katika  eneo la Shekilango jijini Dar es Sallam.

Rose Ndauka Atoa Siri ya Mambo Yake Kumnyookea

$
0
0
MKALI wa filamu Bongo, Rose Ndauka ametoa siri ya mambo yake kumnyookea kuwa imetokana na kumuhusisha Mungu kwa kila anachokifanya na wala si vinginevyo kama watu wanavyodhania.

Akizungumza na Amani, Rose ambaye kwa sasa anamiliki kampuni inayojishughulisha na kutengeneza Jarida la Rozzie, alisema kuwa Mungu ndiye aliyemtendea miujiza hiyo kwani asingemshirikisha asingekuwa hapo alipo.

“Siri kubwa ya mafanikio niliyonayo ni kumtegemea Mungu na hakuna namna yoyote kinyume na hapo niliyofanya. Kuna faida kubwa sana katika maisha yangu, nimeona na nimeshuhudia kabisa, wala sitathubutu kumuacha kamwe,” alisema Rose.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images