Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104803 articles
Browse latest View live

Mtoto wa Wilson Kabwe AGOMA Kupokea Mkono wa Pole Toka Kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda

$
0
0
Anna Kabwe, binti wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe amegoma kumpa mkondo Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam

Tukio hilo la aina yake lilimfika Makonda aliposhiriki shughuli ya kuaga mwili wa Kabwe katika Viwanja vya Karimjee alipokuwa akitoa mkono wa pole kwa familia ya Kabwe.

Wakati Makonda akimpa mkono, Anna aliendelea kuchezea simu yake huku akipuuza mkono wa kiongozi huyo. Anna alifanya hivyo akiwa amekaa huku ndugu zake wengine wakiwa wamesimama wakati wakipokea mkono huo wa pole.

Kitendo hicho kimetafsirika kwamba, Anna alikumbuka tukio lililofanywa Aprili 19 mwaka huu wakati wa uzinduzi wa Daraja la Kigamboni ambapo Makonda alimtuhumu marehemu Kabwe (baba yake) kwamba amehusika na kusaini mikataba iliyoikosesha mapato serikali.

Kabwe alifariki tarehe 19 Mei mwaka huu kutokana na tatizo la ini. Mauli yalimkuta akiwa katika Hospitali ya Mama Ngoma jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu. Ameacha mjane na watoto watano; wanne wa kiume na mmoja wa kike.

Nay wa Mitego Amnasa Mchumba Mhabeshi

$
0
0
Miezi michache tu baada ya staa wa Hip Hop Bongo, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’  kuripotiwa kutoka na msichana anayejulikana kama Chaga Baby, imedaiwa kuwa hivi sasa, yupo na mrembo raia wa Ethiopia (Mhabeshi) anayejulikana kwa jina la Addi na ameapa kufunga naye ndoa.

Chanzo makini kililiambia gazeti hili kuwa, Nay na mwanadada huyo ambaye ni msanii wa filamu, kwa sasa ni mahaba niue na wanapoelekea ni pazuri tofauti na wapenzi wengine waliopita, kwani huyu humzungumzia kila wakati.

Nay alitafutwa na alipopatikana alikiri kuwa na uhusiano na raia huyo wa Ethiopia, huku akikazia kuwa baada ya kurukaruka sana ana mpango wa kumuoa kabisa.

“Nimesharukaruka vya kutosha, sasa nimetulia na mchumba wangu huyu Addi tuliyekutana uwanja wa ndege huko Afrika Kusini wakati nikiwa narudi Bongo na yeye anarudi kwao, tangu hapo tulianza uhusiano na tunae-ndelea vizuri.

“Sija-wahi kusema kuhusu kuoa, lakini kwa huyu ndiye mke wangu ajaye maana tulipofikia ni pazuri, anawapenda sana watoto wangu, sitaki Wabongo wamzoee maana wataniharibia na maneno yao,” alisema.

Staili ya kukutana kwa wapenzi hao, inafanana na ilivyokuwa kwa Diamond na Zari, ambao pia walikutana ndani ya ndege nchini humo, lakini wenyewe wakiwa na uelekeo mmoja wa Dar es Salaam.

Chanzo;GPL

Young Dee Afunguka Kuhusu Madawa ya Kulevya na Pombe

$
0
0
Young Dee amekanusha tena uvumi ulioenea mtaani kuwa anajihusisha na matumizi ya dawa za kulevya.

Akiongea kwenye kipindi cha Harakati cha Clouds FM kinachoendeshwa na Kalapina, rapper huyo amesema tokea akiwa mdogo amekutana na mambo mengi ya kuzushiwa.

“Hata mimi nasikia sana,” alijibu alipoulizwa kuhusu tetesi za kutumia unga. “Unajua mimi nimekuwa kwenye muziki tokea niko mdogo maana tokea nipo shule nimekutana na mengi sana. Nina imani mti wenye matunda ndio hupigwa mawe, unajua sometimes wanavyosema ukifuatisha ndio unaweza kukuta kweli unaingia huko. Lakini situmii madawa ya kulevya, mimi ndio najua maisha yangu, mimi najua natumia pombe tu,” alisema Young Dee.

Alipoulizwa kwanini aliamua kuandika ujumbe kuhusu Babutale kumsaidia Chid Benz na kama hakukubaliana na Tale haya ndio yalikuwa majibu yake:

“Mimi nilihisi kitu tofauti kabisa maana Chid ni msanii mkubwa sana na haikutakiwa kumweka vile, ilitakiwa umchukue umweke sawa kimya kimya na sio vile kila mtu aone. Kama unamsaidia huo ndio ulikuwa mtazamo wangu wa tofauti, hayo mambo mengine yaliyotokea na mimi ni binadamu.”

Bifu la Harmonize na Team Wema Lachafua Hali ya Hewa

$
0
0
Kuna bifu kubwa sana limeibuka kati ya msanii wa Wasafi Harmonize na team Wema baada ya Harmonize kutoa freestyle yenye maneno ya kumkashifu Wema Sepetu.

Kijana Harmonize mpaka sasa anaoga matusi yote ya dunia hii kutoka kwa team Wema.

"sista duu usitoe mimba ukaja kulia kama Sepetu " - Harmonize

Wolper Afungukia Penzi Lake na Harmonize, Adai Hakujua kama ‘Mkongo’ Ana Mke

$
0
0
Mwigizaji Jackline Wolper jana amefanya mahojiano na Zamaradi Mketema kwenye kipindi cha TakeOne na kuzungumzia mambo mengi kuhusu yeye na aliyekuwa mpenzi wake Putin ‘Mkongo’ aliyemvisha pete, na uhusiano wake na msanii Harmonize.


‘Ni kweli Raj (Harmonize) ni mpenzi wangu,ukweli nilimjua siku nyingi nilikuwa nikimchukulia kama mwanamuziki tu, tuna mwezi mmoja na wiki mbili sasa’’ alisema Jack.

’Nisingependa kumuongelea mwanaume niliyekuwa naye ‘Putin’, nikiona picha zake,nikisikia jina lake yaani kuna vitu nikiviona kuhusu yeye naumia sana , na mimi nikimpenda mwanaume nampenda kutoka moyoni, nilijuana naye mwaka 2012 nilikuwa namzungusha kwasababu watu walikuwa wakiniambia kabila lao ni waongo, sasa kipindi alivyorudi hapa nchini alinikuta nipo singo, nilikuwa sipo sawa’’

‘’Katika maisha yangu sijawahi kumpeleka mwanaume kwa wazazi wangu nilimuamini nikampeleka kwetu na unajua mwanaume yeyote unayempeleka kwenu hutokubali kuachana naye kwasababu utakuwa unawaangusha wazazi wako na familia yako na ikiwa wamempokea vizuri lakini kwanini nimekubali kumuacha’’(analia)

‘’Ni kweli alikuwa mume wa mtu, baadhi ya watu walikuwa wakiniambia na kunitumia picha siku ambayo alinivisha pete, n asiku ambayo alinivisha pete nilikuwa sijui ilikuwa ni sehemu ambayo tulikuwa tunapenda kukaa na kunywa kila siku ananivisha pete nikakubali baada ya kunivalisha watu wakawa wananiambia kwanini nimevishwa pete na mume wa mtu sikutaka kumuamini mtu kwa sababu mahusiano yangu mengi yamekuwa yakiharibika kwa sababu kuwasikiliza watu, niliziona picha za harusi lakini nilihisi ni harusi tu, sikuelewa kwa sababu nilikuwa kwenye mapenzi’’

‘’Putin alikuwa akinidanganya kuhusiana na mke wake na niliamini ndoa nyingi watu wanaoana na kuachana na aliniambia ni kweli alikua na mwanamke lakini waliachana, lakini mwanamke aliyekuwa naye ni tofauti na watu walivyokuwa wakiambia yeye aliniambia kuwa hawajaoana na mwanamke huyo ila walitaka kufunga ndoa, kiukweli ni mtu ambaye anaweza sana kujielezea alinidanganya sana, nilimuamini sana kuliko wale watu zaidi ya kumi waliokuwa wakinieleza ukweli kuhusu yeye sikuwaamini, na wale waliokuwa wananiambia ukweli hawakuwa wabaya lakini sikuwaelewa kwa sababu nilikuwa kwenye mapenzi tayari’’ (analia).

‘’Nilitoka naye hapa tukaenda South Afrika(analia) tulienda kwa ajili ya kusoma nakumbuka ilikuwa mwezi wa 12 mwaka jana akaniambia ameshalipa kila kitu na ameninulia gari ya kuendea shule,nikakaa miezi mitatu sikusoma lakini wazazi wangu walikuwa wanajua nasoma ilikuwa ni lazima nimsitiri mchumba wangu kwa wazazi wangu nikawadanganya kuwa nasoma, mama yangu alikuwa anampenda sana mchumba wangu lakini baba yangu hakukubaliana na naye, alikuwa akisema kuwa kama atanichukua kunipeleka South Afrika basi akamilishe ishu ya kunivisha pete na kunioa kabisa, akanivisha pete mbele ya wazazi wangu wakakubaliana baada ya mwezi wangeleta mahali ’’ alisema  Jack.

‘’Tulivyofika South Afrika nilikuwa namfanyia kila kitu kama mke wa mtu, nilikuwa namdanganya mama nasoma lakini baada ya hapo nikaona mambo hayaendi kwa sababu kuna siku nilienda salun nikasikia kuwa mke wake naye yupo kule Sauz na alikuwa ananiaga sana anasafiri anaweza akakaa siku mbili au tatu nikamuuliza akaniambia sio kweli yupo Kongo’’ alisema Jack.

‘’Siku iliyofuata alikuja nyumbani akiwa amechelewa, nilikuwa chumbani yeye alikuwa sebuleni ana’preview’ picha nikataka kumpora simu nikamwambia nimeona picha ukiwa na mke wako, na mtoto wako, akaniambia alimkuta mwanamke wake kwa kaka yake akataka kupiga picha naye ndo akapiga, halafu alikuwa anavaa pete ya ndoa nikamwambia siitaki hiyo pete akaiuza, lakini kuna siku alirudi akiwa ameivaa ile pete nikakasirika nikamwambia naondoka akanitupia ile pete kitandani akaniambia nikaitupe chooni’’ alisema Jack.

‘’Kuna kipindi nilikuwa nalewa sana kutokana na stress, kuna siku nilikuwa ‘location’ nilikuwa nimelewa hadi nikazima akapigiwa simu akanifuata akanipeleka nyumbani akanivua nguo zote akaanza kunirekodi na kunipiga picha, lakini nilifanikiwa kuzifuta, lakini baada ya wiki mbili alinitumia meseji na kunitisha kuwa kitu atakachonifanya watanzania watafunga macho na sitoamini’’ Alimalizia Jack

Cloudsfm

Meneja wa Wema Afungukia Ugomvi wa Mirror na Petiti Man

$
0
0
Wema Sepetu na Martin Kadinda
Mwanamitindo na Meneja wa Wema Sepetu, Martin Kadinda amefunguka juu ya ugomvi wa Mirror na Petiti Man.

 Akizungumza na Enewz Kadinda alisema kuwa ugomvi wa Mirror na Meneja wake anayesimamia kazi zake za muziki yaani Petit man ni utoto tu unawasumbua.
“Petiti bado yupo Endles Fame kwakuwa bado hajaiandikia barua kampuni kuwa anatoka na yote yaliyotokea kati ya petit na Mirror ama Wema ni tofauti zao tu kawaida ambazo si mara ya kwanza kutokea”,alisema Kadinda.

Hapo awali Mirror aliiambia Enewz kua hasimamiwi tena na Petit katika kazi zake huku Petit akitaka tumuulize Meneja wa kampuni ambaye ni Kadinda juu ya swala hilo kwakuwa yeye ndo msemaji wa kampuni hiyo.

Video : Lulu Michael Afunguka Kuhusu Mimba yake, Kuolewa na Kutengana kwa Wazazi wake

$
0
0
Miezi michache iliyopita mwanaBongomovie Lulu aliamua kumtangaza mpenzi wake hadharani kua ni Majay, mkurugenzi wa Efm. Na maswali ya mashabiki wengi yakawa ni kweli watadumu au ndo atakua kafika na kuamua kuolewa????

Lulu aliamua kujibu maswali hayo pale alipoamua kujibu maswali aliyokua akiulizwa na mashabiki wake kwa njia ya video. Katika video hiyo Lulu aliamua kufunguka mambo mengi sana ikiwemo ufafanuzi wa picha aliyopost ikionyesha kua ana mimba, kama ataolewa au la, na mengine mengi. Unaweza mskiza katika video hii hapa chini ....

 TAZAMA VIDEO HAPA:

Video : Mama Wema Sepetu Kawalaani Wanaomsema Vibaya Wema Sepetu

$
0
0
Ukitaja orodha ya wasanii wa Bongo ambao wanasemwa au kuandikwa na magazeti vibaya basi hutaacha kumtaja Wema Sepetu. Kwa mwaka huu tu keshaandikwa na stori nyingi sana ila kubwa zaidi ni kuhusu habari yake ya kubeba mimba ya mapacha  na kisha kudaiwa kutoka.

Baada ya kuenea habari hizo za mimba kutoka wengi waliongea huku wengi wakimsema kwa mabaya. Maneno hayo yalimfikia mama mzazi wa Wema na kuamua kuwafungukia kwa kuwachana na kuwalaani wale wote wanaomsema vibaya mtoto wake.

Hapa chini nimeweka video ambayo mama Wema ameongea mengi na kubwa zaidi amewalaani wote wanaomsema vibaya mtoto wake.

Tazama video hapa chini

Ester Bulaya Achafua Hali ya Hewa Bungeni Baada ya Kumfananisha Waziri Maghembe na TISHU

$
0
0
Mbunge wa Bunda Mjini (Chadema), Ester Bulaya jana alichafua hali ya hewa bungeni baada ya kusema kwamba Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe ni mzigo na mwepesi kama ‘tishu’ kwa sababu hana uwezo wa kusimamia mambo mazito yaliyopo katika wizara hiyo, kama vile migogoro ya wananchi na hifadhi za Taifa.

“Huyu waziri ni mzigo kama alivyowahi kusema (Abdulrahman) Kinana. Mimi nasema yeye ni mwepesi kama tishu, hawezi kuisaidia wizara hii nyeti,” alisema mbunge huyo jana wakati akichangia hotuba ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

Hata hivyo, Waziri wa Nchi, Sera, Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama alisimama na kuomba mwongozo wa mwenyekiti juu ya mbunge huyo kutumia maneno ya kuudhi ambao uliungwa mkono na Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge aliyemtaka Bulaya kufuta neno mwepesi kisha aendelee na hotuba yake. Hata hivyo, Bulaya alikataa kufuta neno hilo na kusema wabunge hawaamuliwi maneno ya kutumia.

Chenge aliendelea kumsihi mbunge huyo kufuta neno hilo na katika mabishano hayo yaliyodumu kwa dakika tatu, baadaye, Bulaya alikubali kuondoa neno ‘tishu’ na kuliacha neno mwepesi na kuruhusiwa kuendelea kuchangia.

“Mwenyekiti sitafuta neno mwepesi, kama neno ‘tishu’ linawakera basi naliondoa libaki mwepesi,” alisema Bulaya.

Katika mchango wake, Bulaya alisema wananchi wanaoishi katika hifadhi zilizopo jimboni mwake wananyanyaswa na askari wanyamapori wakati Serikali imeshindwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya kuishi.

Alimtaka waziri huyo kushughulikia kero zote zinazowakabili wananchi wa Bunda akisema Serikali haiendeshwi kwa maneno matupu, bali vitendo na dhamira ya dhati ya kuwahudumia wananchi.

“Tatua matatizo jimboni kwangu ili niweze kukupima kama wewe ni mzito au mwepesi,” alisema mbunge huyo akimwambia Profesa Maghembe.

Baada ya Bulaya kumaliza muda wake, mbunge aliyefuatia alikuwa Abdallah Ulega wa Mkuranga (CCM) ambaye alisema kuna haja ya wabunge kupimwa kama wamelewa getini ili kujua akili zao.

“Kijana aliyefunzwa vizuri hawezi kumtukana mzee kama yule (Maghembe). Kama suala ni uwaziri basi aangalie hata umri wake kabla ya kuzungumza... Naungana na aliyesema wabunge tupimwe vilevi kabla hatujaingia humu ndani. Unaweza kujenga hoja yako bila kutukana, huhitaji kutukana ili waziri atekeleze madai yako,” alisema mbunge huyo.

Silaa Adai Wafuasi wa Chadema walitishia Kuchoma Nyumba yake

$
0
0
ALIYEKUWA mgombea ubunge wa Ukonga, Jerry Silaa (CCM) amedai kuwa wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walimtishia kuchoma moto nyumba yake wakati wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka jana.

Silaa alieleza hayo jana katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, wakati akitoa ushahidi wa kesi ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi mbunge wa jimbo hilo, Mwita Waitara (Chadema).

Alitoa ushahidi huo kwa njia ya kiapo baada ya Jaji Fatuma Msengi kutupilia mbali pingamizi la upande wa walalamikiwa waliokuwa wanapinga kupokewa kwa kiapo hicho kwa kuwa kina mapungufu kisheria.

Katika kiapo hicho, Silaa anaeleza kuwa, Oktoba 27 mwaka jana katika kituo cha kujumlishia kura cha Pugu Sekondari, kulikuwa na idadi kubwa ya wapiga kura wa Chadema wakiwa wamesimama mita 20 kutokea usawa wa kituo hicho.

Alidai kuwa wafuasi hao walianza kuwatishia Mawakala na Msimamizi wa Kituo, jambo lililosababisha Polisi washindwe kufanya kitu zaidi ya kuwaonya, ndipo mjibu maombi wa pili na wenzake wakasema hawatopokea matokeo na watachoma moto nyumba yake pamoja na kituo hicho.

Silaa ambaye aliwahi kuwa, Meya wa Manispaa ya Ilala, alidai hadi Oktoba 27, baadhi ya vituo vilikuwa havijakusanya matokeo jambo lililosababisha aandike barua kwenda kwa Msimamizi wa Kituo kuomba mchakato wa kuhesabu kura urudiwe.

Video : Lulu Michael Akubali Kua Anavaa Matambala ya Kuongeza Makalio

$
0
0
Siku za hivi karibuni kumetokea mabifu mengi sana ya wasanii wetu wa kike hapa Bongo. Mabifu makubwa ambayo yamemake headline sana ni ya ya Shilole na Vanessa Mdee na upande wa pili ni Lulu na video queen Giggy Money.

Giggy Money siku za karibuni amekua akitofautiana na wasanii wengi na kwa sasa kaamua kulinukisha na kuanzisha bifu na Lulu. Giggy amekua akijitamba kua anamzidi maisha mazuri Lulu hasa katika upande wamavazi na kuvaa matambala ili aongeze tako.

Katika kauli moja Giggy alisikika akisema kua Lulu ni bingwa wa kuvaa nguo za matangazo. Baada ya Lulu kutuhumiwa hayo aliamua kufunguka kwa ufupi na kujibu tuhuma hizo.

Unaweza mskiliza kwa kutazama video yake hapa chini.


Video: Chid Benz Adaiwa Kutoroka Sober House

$
0
0
Wakati wadau wa muziki wakifahamu kuwa Msanii wa Muziki wa Hip Hop Bongo, Rashid Makwilo ‘Chid Benz’ yuko katika kituo cha kusaidia waathirika wa madawa ya kulevya ‘sober house’ kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani, inadaiwa jamaa alishatoroka kitambo na sasa yuko kitaa.

Taarifa iliyotua kwenye meza ya dawati hili ilidai kuwa, Chid alitoroka kituoni hapo baada ya kushindwa kuhimili mazingira yalikuwepo hivyo akaona bora arudi mtaani kwa staili ya liwalo na liwe.

Baada ya kupata taarifa hiyo, mwishoni mwa wiki iliyopita waandishi wetu walitinga Bagamoyo na kukutana na meneja wa kituo hicho, Tumaini Majura ambaye alithibitisha kuondoka kwa Chid akiwa bado anaendelea kupatiwa matibabu. Sehemu ya mahojiano kati ya Risasi na meneja huyo ni hii;
Chid-Beenz_fullRisasi: Kwani Chid Benz ameishi hapa kwa muda gani?
Tumaini: Ni siku 28 lakini alitakiwa kukaa kwa muda wa angalau miezi mitatu ili kurudi katika hali yake ya kawaida.

Risasi: Ilikuwaje sasa mpaka akaondoka kabla hajawa sawa?
Tumaini: Nafikiri ni uamuzi wake binafsi maana siku moja meneja wake (Babu Tale) alikuja kumjulia hali, alipotaka kuondoka aling’ang’ania kuondoka naye. Sisi pamoja na Tale tulimsihi sana kubaki lakini alikataa.

Risasi: Hali ilikuwaje kwa meneja wake wakati Chid anang’ang’ania juu ya jambo hilo?
Tumaini: Kiukweli hakuwa akitaka aondoke maana mara kwa mara alikuwa anamsihi kuwa mvumilivu ili amalize angalau miezi mitatu na ampeleke kwenye shoo za muziki ndani na nje ya nchi, lakini Chid hakujali hayo. Kwa hiyo siwezi kusema alifurahia juu ya jambo hilo.
Risasi: Maisha yake ya kawaida yalikuwaje na wenzake?

Tumaini: Hayakuwa mabaya sana japo alikuwa mzito kushiriki kwenye ishu za usafi na vitu vingine. Muda mwingi alipenda kupumzika na kuandika mistari. Lakini kuna kipindi alikuwa akijaribu kuhamasisha wenzake wagomee kitu fulani. Sisi tulikuwa tunamchukulia kama mtu wa kawaida aliyekuwa anahitaji msaada kutoka kwa viongozi.

Baada ya mahojiano hayo, waandishi wetu waliamua kumtafuta Chid Benz, alipopatikana alikataa kuzungumzia suala hilo huku akisisitiza kuwa lolote kuhusu yeye atafutwe Babu Tale.

Alipopatikana, Babu Tale alisema: “Sitaki kusikiliza wala kuzungumza lokote kuhusu Chid, muda ukifika nitaongea ila kwa sasa niacheni tu.”


Angali Video Hapa:

Chanzo:Global Publishers

Rais Magufuli na Mkewe Waguswa na Stori ya Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Aliyepofuka Macho..Waamua Kumchangia Mil 10 Akatibiwe

$
0
0

Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DktJohn Pombe Magufuli, Mkewe Mama Janeth Magufuli na familia yake kuahidi kuchangia Milioni 10 kwaajili ya matibabu ya #Kipepeo Bernadeta Msigwa mwakilishi kutoka ofisi ya Rais Bw. Ngusa Samike amefika katika ofisi za CloudsMediaGroup na kukabidhi fedha hizo. Vilevile Mheshimiwa Rais ametoa ujumbe kwa Kipepeo Bernadeta kuwa amtumainie Mungu kwani ndiye muweza wa kila kitu. Katika upande mwingine Naibu wa Waziri wa Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira Mh. Anthony Mavunde amechangia Shilingi Milioni 1.
Kama umeguswa na unahitaji kuchangia au unataka maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kumsaidia piga namba 0742848729. Pia unaweza kuangalia story yake kamili kwenye account hii ya Instagram@BernadetaMsigwa.
Asante sana Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Wolper awajia juu wanaofuatilia penzi lake jipya na Harmonize

$
0
0

Jacqueline Wolper amewafungukia wanaomsema kuwa haendani na mpenzi wake mpya, Harmonize.

Hivi karibuni familia ya WCB imeonekana kuchafua hali ya hewa mitandaoni baada ya picha zilizokuwa zinasambaa zikionyesha couple hiyo mpya mjini kati ya Jacqueline Wolper na Harmonize huku baadhi ya mashabiki wakisema kuwa ilikuwa ni kiki lakini kwa sasa mambo yanaonekana kubadilika.

Akiongea kwenye kipindi cha Take One, kinachoruka kupitia Clouds TV, Wolper alisema kuwa anaweza akawa na mwanaume anayefanya kazi yeyote sababu haitaji pesa kutoka kwa mwanaume.

“Naweza hata nikawa na mtu anaendesha bodaboda au anaweza sijua akawa mfagia hoteli, sijui anafagia nini lakini mimi kama mimi nikambadilisha na akawa mwanaume wangu. Kwa sababu nachokihitaji mimi sihitaji pesa mimi ni mpiga kazi, mimi nafanya kazi na ndiyo maana mwanzo nimeanza like na fanya promosheni Napata hela yangu, sitaki kutegemea mtu,” aliongeza.

Wolper alianzisha uhusiano na muimbaji huyo wa ‘Bado’ baada ya kuvunja uchumba na mwanaume aliyeahidi kumsomesha nchini Afrika Kusini na ambaye alikuja kugundua kuwa ni mume wa mtu.

Lowassa Ajisafisha Tuhuma za Kukwapua ardhi Ya Wananchi na Kujimilikisha

$
0
0

Siku chache  baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kulieleza Bunge kuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa alijimilikisha shamba la Makuyuni Wilayani Monduli mkoani Arusha, Mbunge wa Monduli, Julius Kalanga amejitokeza kutoa ufafanuzi unaomsafisha.


Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dodoma, Kalanga alisema kuwa Lowassa hamiliki shamba hilo la Makuyuni kwakuwa tangu Rais wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa alipofuta hati ya umiliki wa shamba hilo kutoka kwa raia wa Kigeni aliyemtaja kwa jina la Stein, bado halijamilikishwa rasmi kwa wananchi na ndio ilikuwa hoja yake.


Alisema kuwa maelezo ya Lukuvi hayakuwa na ukweli  na kwamba alichanganya kati ya shamba hilo la Mkuyuni na shamba la Manyara Ranchi ambalo hati yake ilifutwa tangu mwaka 2000 na kukagawiwa kwa wananchi wa Monduli ambapo Lowassa alisaini hati miliki yake kama muwakilishi wa wananchi wa Wilaya hiyo kwakuwa wakati huo alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya udhamini ya Ardhi (Tanzania Land Trustee (TLCT).


“Jambo la kushangaza ni pale Waziri alipochanganya shamba hilo na lile la Manyara Ranchi ambalo hati yake ilifutwa tangu mwaka 2000 na kugawiwa kwa wananchi. Hati miliki ya shamba hilo la Manyara Ranchi ilisainiwa na Lowassa ambaye wakati huo alikuwa mwenyekiti wa Bodi ya Tanzania Land Trustee(TLCT),”alisema


Awali, Waziri Lukuvi alieleza kuwa Shamba hilo la Mkuyuni linapaswa kumilikishwa kwa wananchi lakini nyaraka zinaonesha kuwa hati yake imesainiwa na Lowassa na kwamba Serikali itamnyang’anya na kulirejesha kwa wananchi.


Juzi, Lowassa aliahidi kuwasiliana na Mbunge huyo ili kufuatilia kauli aliyoitoa Waziri Lukuvi dhidi yake kuhusu kujimilikisha shamba hilo ili aweze kutoa ufafanuzi kwani hakuna ardhi anayoimiliki kinyume cha taratibu.

Dudu Baya Aongea haya Baada ya Chidi Benz Kudaiwa Kutoroka ‘Sober House’

$
0
0
Msanii wa muziki wa Hip Hop, Dudu Baya amesema kauli yake ya ‘Chidi Benz ni mtu wa kuachwa afe’ ambayo ilichuliwa vibaya na baadhi ya wadau imedhihirika hivi karibuni baada ya rappa huyo kudaiwa kutoweka sehemu ambayo alikuwa akipatiwa matibabu ya kuachana na matumizi ya Madawa ya kulevya.
Dudu Baya

Miezi miwili iliyopita katika kipindi kimoja cha runinga, rappa Chidi Benz alikiri kutumia Madawa ya kulevya na kuhitaji msaada ambapo Babu Tale pamoja na Kalapina walimsaidia kwa kumpeleka Bagamoyo Sober House ambako anadaiwa alitoroka siku 28 baadae.

Kupitia instagram, Dudu Baya ameandika:
Habari zilizopo ni kwamba msanii mwenzangu Chidi Benz ametoroka rehab aliyopelekwa ya Bagamoyo sober house. Miezi miwili iliyopita nilifanyiwa mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari pamoja na blogs na websites mbalimbali. Na kila walipokuwa wananiuliza kuhusu swala la Chidi Benz kusaidiwa na Babu Tale kupelekwa rehab, nilikuwa nawajibu kuwa msanii Chidi Benz ni mtu wa kuachwa AFE!! Kwani kwa tatizo alilonalo ni ngumu kwa mtu yeyote (hata mama yake mzazi) kuweza kumsaidia na kupona bila ya yeye mwenyewe Chidi Benz moyo wake haujaridhia kuacha madawa ya kulevya. Baadhi ya wasanii wenzangu, watu maarufu, wanasiasa,wafanyabiashara n.k waliweza kuniponda na kunipinga waziwazi kutokana na kauli yangu hii na waliniona kuwa mimi sio mtu mzuri ninayetaka kumsaidia CHID BENZ apone. Lakini ukweli wa yale maneno niliyosema umekuja kudhihiri hivi majuzi baada ya yeye msanii mwenyewe CHID BENZ kutoroka rehab kwa kukataa kusaidiwa kuondokana na matatizo yake!! So kinachofanyika sasa hivi ni kuweza kumtafuta CHID BENZ sehemu aliyokimbilia ili akipatikana aweze kuludishwa Rehab. Sina tatizo lolote na CHID BENZ na wala simuombi mabaya kwani mimi ni kama kaka yake na huwa ninamuombea kwa Mungu aweze kutoka na kupona haraka kwa haya matatizo yaliyompata. Ila narudia tena kusema kuwa tatizo alilonalo mwenyewe CHID BENZ @chidbenz ni mbaka hapo yeye mwenyewe moyo wake uridhie kuachana na matatizo hayo na sio kuweza kusaidiwa na watu kuondokana na matatizo hayo (CHID BENZ my best rapper hakuna wa kukuokoa, JIOKEE!!) Msaada wangu kwako, naendelea kumuombea.

Mambo 15 ya Kufanya Kama serikali ya Magufuli Inataka Kuendeleza Viwanda Tanzania

$
0
0
Pengine sio yote yanafaa... lakini mengi yatasaidia

1. Kwa miaka 5 serikali ielekeze nguvu kuinua viwanda vya bidhaa za chakula, hivyo...

2. Serikali itoe ruzuku kwa uendelezwaji wa viwanda vya chakula kwa miaka 5, mathalani...

3. Serikali iondoe kodi zote katika vifungashio vya bidhaa za chakula kwa miaka 5, kwa mfano...

4. Makopo ya metal na plastiki, chupa za plastiki na glass, karatasi za nylon na za kawaida ihakikishwe zinazotengenezwa nchini au kuagizwa zipatikane kwa bei rahisi, kufanikisha hilo...

5. Kwa miaka 5 serikali itoe ruzuku kwa viwanda vya kutengeneza vifungashio vya chakula, kwa mfano...

6. Kwa miaka 5 gharama za umeme kwenye viwanda vya vifungashio vya chakula ziwe nusu ya gharama za kawaida, kisha...

7. Serikali ihamasishe bidhaa zote za chakula, hasa vilivyo rahisi kusindika na kuwa packed visiuzwe bila kuwa packed, kwa mfano...

8. Unga wa mahingi, Unga wa ngano, Mchele, Maharage/kunde, Nyama, Samaki, mayai na baadhi ya matunda viuzwe vikiwa packed, ili...

9. Biashara yake iwe rasmi zaidi na uuzaji nje ya nchi uwe rahisi zaidi, na pia...

10. Serikali iendeleze masoko ya ndani ya vyakula kwa kuyaboresha kimiundombinu na kuyarasimisha, tena...

11. Serikali ihamasishe kufunguliwa na kusambaa kwa super markets, lakini pia bidhaa zote za chakula vilivyosindikwa na kufungwa nchini visilipishwe VAT kwa miaka 5, vile vile...

12. Serikali ifungue mashamba makubwa ya mazao ya chakula kama mahindi, ngano, alizeti, maharage, mtama, miwa na mpunga, kwa kuyaendeleza hadi kiwango cha kuwa tayari kupanda mbegu (kusafisha pori, kutoa visiki na inapolazimu kuweka miundombinu ya umwagiliaji), kisha...

13. Iyakodishe mashamba hayo kwa watu walioomba na kupatiwa mafunzo, huku wahitimu wa vyuo mbalimbali wakipewa kipaumbele, ambapo...

14. Watakaokodisha mashamba hayo wataingia mikataba na wenye viwanda vya kusindika na kufungasha chakula ambao nao watakuwa na mikataba na wenye super na mini super markets, bila kusahau...

15. Serikali iimarishe maabara za TFDA kuhakikisha vyakula vyote vinavyosindikwa na kufungashwa na viwanda vyetu, pia vinavyoagizwa nje ya nchi vinakuwa na ubora unaotakiwa.

Naomba kuwasilisha

Bashe: CCM ni Waoga, Wanafiki na wa Kujipendekeza, Hatuna Sababu ya Kuendelea Kubaki Madarakani

$
0
0
Akichangia kwenye bajeti ya mali asili na utalii amewaambia wabunge na serikali kuwa hawajawahi kuweka malengo haswa ya kutatua matatizo ya wafugaji na waulima, wamekuwa waoga, wanafiki na wakujipendekeza

Ameongezea CCM kwa wingi wao hawana sababu ya kuendelea kubaki madarakani kama wameshindwa kuishauri serikali kwa ukweli.

Soma Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Katika Magazetini na Mitandaoni Leo 26 May 2016

$
0
0

Niligundua Harmonize Alikuwa Ananipenda Lakini Alikuwa Anashindwa Kuniambia – Wolper

$
0
0
Msanii wa filamu Jacqueline Wolper ameweka wazi jinsi yalivyoanza mahusiano yake ya mapenzi na hit maker wa wimbo ‘Bado’ Harmonize kutoka WCB.

Akizungumza Jumatano hii katika kipindi cha Take One Cha Clouds TV, Wolper amesema alitokewa na Harmonize wakati sahihi ambapo ameshaachana na mkongo wake ambaye alivyalisha pete.

“Rajabu (Harmonize) sijamjua hivi karibuni, nimemjua siku nyingi sana na nilikuwa namchukulia kama wasanii wengine wa muziki,” alisema Wopler.

“Lakini kwa mimi nilikuja kugundua Rajabu alikuwa ananikubali siku nyingi, tukawa marafiki. Lakini katika kumbukumbu zangu na vitu ambavyo nimevipitia, naamini kwamba Rajabu alikuwa anashindwa kuniambia. Lakini alikuja kunitamkia mimi wakati nipo kwenye wakati mgumu sana, kwa hiyo tukajikuta kunakuwa marafiki na baadae wapenzi,” aliongeza.

Wopler amesema ana mwezi mmoja na wiki mbili toka aingie rasmi kwenye mahusiano ya mapenzi na Harmonize.
Viewing all 104803 articles
Browse latest View live




Latest Images