Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Wema Sepetu Adaiwa Kufulia na Kutembelea Usafiri wa Bajaj..Mwenyewe Afunguka Haya

$
0
0
STAA mwenye nyota ya kipekee Bongo, Wema Sepetu amewafungukia wanaomsema vibaya kuwa siku hizi kafulia mpaka anatembelea usafiri aina ya Bajaj na kudai kuwa hayo ni maisha yake binafsi ambayo hayamhusu mtu yeyote.

Akizungumza na gazeti hili juzikati, Wema alisema kuwa anashangazwa sana na watu ambao wanafuatilia maisha yake kila kona kwa kuwa yeye ni binadamu kama walivyo wengine na maisha yote anastahili kuishi.

“Jamani sijui mijitu mingine ikoje? Bajaj ni usafiri kama usafiri mwingine, sasa cha ajabu nini mimi kuutumia? Mniache na maisha yangu,” alisema Wema.

Chanzo:GPL

Tamko la ACT Wazalendo Baada ya Wabunge wa Upinzani Kufungiwa

$
0
0
Baada ya Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge kuwatia hatiani wabunge saba kwa makosa mbalimbali ikiwemo kudharau madaraka ya bunge ambapo wabunge Easther Bulaya na Tundu Lissu wameadhibiwa kutokuhudhuria vikao vilivyobaki vya mkutano wa tatu na vikao vyote vya mkutano  wa nne.

Wabunge Pauline Geku, Halima Mdee, Zitto Kabwe, Godbless Lema wamepewa adhabu ya kutokuhudhuria vikao vyote vilivyobaki vya mkutano wa tatu na Mbunge John Heche hatohudhuria vikao kumi vya mkutano wa tatu. Makosa hayo waliyafanya mkutano wa pili mwezi January.

Baada ya adhabu hiyo kwa wabunge, ACT Wazalendo wametoa tamko lao ambapo wameyazungumza haya……

’Chama cha  ACT Wazalendo kimesikitishwa na kitendo cha ugandamizaji wa demokrasia kilichofanywa na wabunge wa CCM kwa kuwasimamisha ubunge wabunge wa upinzani akiwemo kiongozi wa chama chetu  Zitto Kabwe’

’Katikati ya masikitiko hayo tunafarijika kuona wabunge hao wameondolewa kwa sababu ya misimamo yao ya kutetea maslahi ya wananchi’

’Tungesikitishwa zaidi kama mashujaa wetu hawa wangeondolewa bungeni kwa sababu ya ulevi au wawe sehemu ya wagonga mihuri ya masuala ya hovyo hovyo yanayosimamiwa na serikali ya chama cha Mapinduzi (CCM)’

’Kwa sababu hiyo ya kusimamia maslahi ya wananchi sisi kwetu ni mashujaa na kwa maana hiyo Chama chetu kinaandaa maandamano makubwa jijini Dar Es Salaam kuwapokea mashujaa wa wananchi’

VIDEO: Freeman Mbowe Kazungumza Baada ya Wabunge Kutolewa Tena Bungeni

$
0
0
Headline za Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi ilitangaza kuwafukuza jumla ya wanafunzi 7802 kutoka Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) kufuatia mgomo wa Walimu unaoendelea hivi sasa zimeendelea kuchukua nafasi Bungeni Dodoma.

Asubuhi ya May 30 2016 Baadhi ya Wabunge kutoka vyama tofauti walisimama Bungeni kuomba suala hilo kujadiliwa lakini ombi hilo halilikubalika mbele ya Naibu Spika Tulia  Akson. Baada ya kipindi cha pili kurudi mjadala ukakataliwa kwa mara nyingine.

Nakukutanisha na  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Freeman Mbowe akiongea na Waandishi wa habari.

Mke wa Trafiki Kinyogori Adaiwa Kukiri Kumuua Mumewe

$
0
0
MKE wa askari polisi wa kikosi cha usalama barabarani (trafiki), Sajenti Ally Salum (Kinyogori) aliyeuawa hivi karibuni, inadaiwa amekiri kuhusika kwenye mauaji hayo, akidai ilitokana na mumewe kumuacha na kuoa mke mwingine.

Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa mwanamke huyo anashikiliwa na polisi kwa mauaji hayo yaliyofanyika nyumbani kwa Kinyogori, Mkuranga mkoani Pwani.

Wakati huo huo, Kamanda Sirro amezungumzia pia mauaji ya Anathe Msuya yaliyofanyika hivi karibuni Kigamboni na kusema polisi inaendelea kumtafuta msichana wa kazi za nyumbani aliyetoroka siku moja kabla ya kifo cha mwanamke huyo.

Anayetuhumiwa kuua mumewe
Akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu matukio mbalimbali ya uhalifu yaliyojitokeza jijini Dar es Salaam, Sirro alisema katika mahojiano ya awali mke wa Kinyogori amekiri kuhusika.

Kwa mujibu wa kamanda, mwanamke huyo ambaye hata hivyo hakutaja jina lake kwa sababu za kipelelezi, aliamua kumtuma mtu kutekeleza mauaji hayo baada ya mumewe kumwacha na kuoa mke mwingine.

“Ni jambo la kusikitisha kuona mtu anatoa uhai wa mtu sababu ya kuachwa. Tunawasihi wananchi kuepuka kujihusisha na matukio kama haya, eti sababu tu ya kuachwa wanawake wapo wengi na wanaume wapo wengi unaweza kuachwa na ukaolewa na ukaoa kuliko kuondoa uhai wa mtu,” alisisitiza Sirro.

Hata hivyo, Sirro alisema wanaendelea kuwahoji watuhumiwa hao ili waweze kuwataja watu wengine walioshirikiana nao kutekeleza tukio hilo baada ya kuonekana kuwepo kwa wahusika wengine.

‘Hausigeli’ asakwa
Kuhusu mauaji ya Anathe aliyechinjwa nyumbani kwake Kibada, Kigamboni, Kamanda Sirro alisema wanaendelea na jitihada za kumtafuta msichana huyo ahojiwe kuhusu tukio hilo.

Aidha alisema mtu mmoja anashikiliwa akituhumiwa kuhusika na tukio hilo huku polisi ikiwa imeandaa timu ya upelelezi itakayoshughulikia tukio hilo kufanikisha kuwakamata wote waliohusika na tukio hilo.

Sirro alisema msichana huyo aliondoka siku moja kabla ya tukio hilo la mauaji hivyo kupatikana kwake, kunaweza kusaidia polisi kujua kama kuondoka kwake kulikuwa salama au kuna kitu kimejificha.

“Msichana huyu tunaendelea kumsaka tujue kama aliondoka salama na kumhoji zaidi juu ya kuondoka kwake siku moja tu, tukio linatokea nina imani tutafanikiwa kumpata na wote waliohusika na kukomesha matukio haya,” alisema Sirro.

Mamia wajitokeza msibani
Vilio na simanzi jana vilitawala wakati mamia ya wakazi wa Kibada Kigamboni na Salasala walipokuwa wakiuaga mwili wa marehemu Anathe Msuya (30), aliyeuawa Mei 25 nyumbani kwake kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana.

Mwili ulichukuliwa jana asubuhi kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili na kupelekwa nyumbani kwake Kibada, kwa ajili ya kuagwa na majirani zake kabla ya kusafirishwa kwenda kuzikwa mkoani Arusha leo.

Akizungumza baada ya mamia kumuaga nyumbani kwa marehemu, mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Nyakwale Kibada, Said Pazi alisema kuwa wao kama majirani waliomba familia wapate fursa ya kumuaga jirani yao ambaye tangu ahamie ana muda wa miezi sita.

“Baada ya kuambiwa msiba upo Salasala tuliomba kama majirani na sisi tupatiwe fursa ya kuuaga mwili wa ndugu yetu ambaye alihamia mwaka jana… kwa kweli msiba wake umetusikitisha sana” alisema.

Akizungumzia tukio hilo alisema kuwa mtoto wa marehemu huyo, Allan Kimario (4) aliwataarifu majirani kuwa mama yake haamki na ndipo walipofika wakakuta ameuawa.

Mwenyekiti huyo alitoa pole na kusema atahakikisha wanaimarisha ulinzi na kuhimiza wenye viwanja ambavyo havijajengwa, wavifanyie usafi ili kuondoa vichaka ambavyo ni hatari kwa usalama.

Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) Profesa Tunus Mgaya Aliyesimamishwa Kazi na Waziri wa Elimu Afunguka Mambo Mazito

$
0
0
ALIYEKUWA Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Profesa Tunus Mgaya amesema amesikitishwa na taarifa zilizoandikwa katika vyombo vya habari za kukosoa maamuzi ya serikali ya kuwasimamisha kazi kuwa hayakuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa.

Mgaya ambaye hakuwa tayari kueleza kama taratibu za kusimamishwa kwao zilifuata utaratibu au la, amewataka waandishi wa habari kuwa na vyanzo vya uhakika katika habari zao.

“Mimi nikiwa miongoni mwa watendaji waliopumzishwa kazi, napenda kueleza kuwa sihusiki na taarifa hizo, suala hili limeshapita na kutolewa uamuzi na serikali na tuiache Tume iendelee kufanya kazi,” alisema Profesa Mgaya alipozungumza na waandishi wa habari jana mara baada ya kukabidhi ofisi.

Aidha, Profesa Mgaya aliweka wazi kuwa, anaunga mkono jitihada za Rais John Magufuli katika kuhakikisha kuwa watanzania wengi zaidi wanapata elimu ya msingi bure na kutolewa kwa elimu inayokidhi viwango stahiki kitaifa na kimataifa na kusema jambo hilo ni jema na linapaswa kuungwa mkono kwa nguvu zote.

Katika hatua nyingine, alimtaka Waziri wa Elimu, Sayansi,Teknolojia na Ufundi , Profesa Joyce Ndalichako kuendeleza jitihada za kuinua ubora wa elimu katika ngazi zote ili kuwa na taifa lenye watu walioelimika vizuri na lenye mchango mkubwa katika kuendeleza taifa.

Baada ya Nay wa Mitego Kuchepuka na Msichana wa Kihabeshi… Lulu Diva Aliyekuwa Mpenzi Ahamia Kwa Belle 9

$
0
0
SIYO siri tena! Baada ya mkali wa Muziki wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kuchepuka kwa msichana wa Kihabeshi mwenye asili ya Ethiopia, aliyekuwa mpenzi wake Lulu Abass ‘Lulu Diva’ naye ameamua kugeukia kwa staa wa muziki, Abedinego Damian ‘Belle 9’.

Akizungumza na Over Ze Weekend Lulu ambaye ni muuza nyago kwenye video za Kibongo alidai kuwa, Nay hajatulia na badala yake anahitaji kuwa na mtu asiye na skendo za kutembea na wanawake ovyo na Belle 9 ndiye tulizo lake.

“Ni ukweli Nay nilikuwa naye kwenye uhusiano nikifahamu alishawahi kuwa na msururu wa wanawake lakini siyo siri yamenishinda na sasa nahitaji kujiweka kando. Sasa hivi feelings zangu zote zipo kwa Belle na analijua hilo,” alisema Lulu

Maalim Sief Matatani Tena, Atakiwa Kurepoti Polisin Kwa Mahojiano

$
0
0
Baada ya Jeshi la Polisi Zanzibar kuahirisha kumhoji Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, hatimaye hatua hiyo sasa imeelekea kutekelezwa.

Taarifa rasmi ya jeshi hilo visiwani Zanzibar, imemtaka Maalim Seif afike katika Ofisi za Makao Makuu ya Polisi, Ziwani mjini hapa leo saa 4.00 asubuhi.

Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Uhusiano kwa Umma wa CUF, Salim Bimani alithibitisha Maalim Seif kupokea barua hiyo jana wakati akiwa njiani kuelekea Dunga, Wilaya ya Kati Unguja, akiendelea na ziara yake katika majimbo ya Unguja.

“Ni kweli Maalim amepokea taarifa hiyo na ametakiwa afike Ziwani (mjini hapa) kesho (leo) saa nne asubuhi,” alisema Bimani

Bimani aliongeza kuwa hatua hiyo ya sasa imekuja baada ya jeshi hilo kuahirisha hatua ya wito wa kumhoji Maalim Seif, Ijumaa iliyopita.

Barua hiyo ya kuahirisha iliyosainiwa  na Msangi kwa niaba ya Kamishna wa Polisi Zanzibar Mei 26, yenye kumbukumbu namba PHQ/ Z/C.5/4/4/TEMP/34 kwenda kwa Maalim Seif ilikuwa na kichwa cha habari ‘Kuahirisha mahojiano’.

“Tafadhali rejea barua yangu PHQ/Z/C.5/4/4/TEMP 26 ya tarehe 22/5/2016 ambapo tulikuita hapa Makao Makuu ya Polisi Zanzibar kwa mahojiano maalumu ya masuala mbalimbali yanayohusiana na Ulinzi na Usalama wa Visiwa hivi,” ilisomeka sehemu ya barua hiyo ya Msangi.

Kadhalika, barua hiyo ya kuahirisha mahojiano hayo ilisema:

“Tutakujulisha mapema siku ile iliyosainiwa na DCP Salum ya mahojiano itakayofuata mara baada ya kukamilisha taratibu.”

Msangi alithibitisha wito huo wa leo baada ya hatua ya awali, kumtaka kiongozi huyo awasili mbele yao kwa mahojiano kama ambavyo walimuahidi awali.

Kilio cha Maisha Magumu: Je, Tulikuwa Tunategemea Vipato Haramu?

$
0
0
Kuna kilio cha maisha magumu kila kona. Utasikia wakina mama,wafanyakazi, vijana hata wazee wanadai kipindi hiki cha awamu ya tano pesa imekuwa ngumu sana!.

Ninajiuliza:
1:Serikali inatueleza Inazuia ufisadi, kubana matumizi yasio ya lazima, matokeo yake wananchi wanalia eti maisha yamekuwa magumu maana yake nini?

2:Makusanyo ya Kodi ya kuwahudumia wananchi yameongezeka sana lkn kilio kila kona, tatizo nini?

3:Je Maisha bora mtaani kipindi kilichopita yalikuwa matokeo ya wizi,ufisadi,matumizi mabaya ya pesa za umma na ukwepaji kodi?

4: Nasikia hotel zinakoswa wateja na taasisi nyingi zinazorota kutokana na kubana matumizi kwa serikali. Najiuliza hivi hawa jamaa walianzisha hizo taasisi/kumbi/hotel walikiwa na market strategy ya kutegemea wateja wawe serikali tu au?

5: je, unadhani nini kinakosekana ili kikiwepo Mafisadi waendelee kutumbuliwa,wakwepa kodi walipe, Gharama za maisha zishuke, Serikali iwe na pesa za kutosha, n.k na maisha ya wananchi yawe saaafi kwa matajiri na maskini kihalali? nini kinakosekana.

Najaribu kuwaza....

Madhara ya Spika na/Au Naibu Kuwa Mteule wa Rais sasa Yanaonekana

$
0
0
Sio siri tena kuwa Dr. Tulia aliteuliwa na Dr. Magufuli awe Mbunge kwa lengo la kupata nafasi ya Unaibu Spika baada ya mpango wake wa kugombea Uspika kuonekana kugonga mwamba.

Aliyemshinikiza Rais Magufuli kuwa Dr. Tulia ana weledi wa kuweza kuwa Naibu Spika hatumjui lakini ni wazi alimdanganya au Tulia mwenyewe ndiye amejisahau na kudhani kwa vile cheo hicho kapigiwa chapuo na Rais basi Spika sio chochote wala wabunge hawana cha kumfanya.

Ni wazi analivuruga bunge na litavurugika hasa. Haelewani na uongozi wa Bunge kwa kukurupuka kwake, na ana haribu mahusiano ya serikali na wabunge wa pande zote kwa kudhani anaiokoa serikali ya mteule wake.

Amesaidia kuweka wazi kuwa mteule wa Rais hapaswi kuongoza muhimili unaoisimamia serikali. Njia sahihi kabla mambo hayajaharibika kabisa ni yeye kujiuzulu.

Kosa lililowasimamisha Wabunge Saba wa Upinzani

$
0
0
Bunge jana limeazimia kuwasimamisha vikao wabunge 7 wa kambi ya upinzani kwa kosa la kukiuka sheria na kanuni za bunge na kushinikiza kujadiliwa kwa hoja ambayo imekwisha tolewa maamuzi kinyume na utaratibu wa kanuni za Bunge.

Akisoma maamuzi hayo ya Bunge Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge, George Mkuchika amesema Januari 27.01.2016 wabunge hao walikiuka sheria na taratibu za kuongoza bunge kwa walishinikiza kiti cha spika kijadili hoja ambayo ilikwisha tolewa uamuzi na kiti hicho.

Wabunge waliosimamishwa kuhudhuria vikao hivyo ni Zitto Kabwe, John Heche, Halima Mdee, Tundu Lissu, Godbless Lema, Pauline Gekul na Esther Bulaya.

Azimio la adhabu kwa wabunge hao limetolewa na Bunge chini ya Kifungu cha 30A (1) cha sheria ya Haki Kinga na Madaraka ya Bunge Sura ya 296 na kanuni ya 74 (4) na (6).

Kufuatia uchunguzi huo Bunge kupitia kamati hiyo limeazimia kuwa Ester Bulaya naTundu Lisu wasihudhurie vikao vyote vya mkutano wa tatu wa Bunge la Kumi na Moja vilivyobaki kuanzia tarehe 30 Mei , 2016 pamoja na vikao vyote vya Mkutano wa Nne Spika wa Bunge la Kumi na Moja kwa kuwa walipatikana na makosa ya ukiukwaji wa Kanuni na kuonyesha dharau kubwa kwa mamlaka ya Bunge.

Aidha, Bunge limeazimia kuwa Mhe. Pauline Gekul, Mhe.Godbless Lema, Mhe.Zitto Kabwe na Mhe Halima Mdee wasihudhurie vikao vyote vya mkutano wa tatu wa Bunge kuanzia tarehe 30 Mei 2016.
Adhabu hizo Bunge limeazimia Mhe.John Heche asihudhurie vikao kumi mfululizo vya Mkutano wa Tatu wa Bunge hilo kuanzia Mei, 30, 2016 kwa kuwa alipatikana na kosa moja

Baadhi ya Wabunge Wapongeza Wenzao Kusimamishwa

$
0
0
Baadhi ya wabunge wa chama tawala wamepongeza uamuzi wa bunge wa kuwasimamisha wabunge 7 wa upinzani kwa kutofuata sheria za bunge kwa kutaka kushinikiza kujadiliwa kwa hoja ambayo ilikuwa imeshatolewa maamuzi kuhusu bunge kurushwa live.

Baadhi ya wabunge hao ni Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ambaye ameupongeza uamuzi wa Bunge na kusema kwamba ni lazima ifike sehemu adhabu itawale bungeni. Wabunge 7 waliosimamishwa wamepewa kitu wanachostahili kwa kuvunja kanuni.

Mbunge wa Geita vijijini Joseph Kasheku Msukuma amesema kwamba adhabu hiyo ni sawa kwa wabunge hao ili iwe fundisho kwa wabunge wapya.

Kwa upande wake Mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga amesema kwamba kusimamishwa huko kutajenga heshima ya Bunge na kuwa fundisho kwa wengine.

Aidha Wabunge waliosimamishwa ni Tundu Lissu na Ester Bulaya vikao vya mkutano wa tatu na wanne, Godbless Lema, Zitto Kabwe, Paulin Gekul, na Halima Mdee vikao vyote vya mkutano wa tatu na John Heche vikao 10 vya mkutano unaoendelea sasa.

Siri Nne za Shilole Kupenda ‘Vitoto’

$
0
0
MSANII nyota wa Muziki wa Kizazi Kipya, Zuwena Mohammed maarufu kama Shilole, baada ya kusemwa kwa muda mrefu, hatimaye amefunguka na kutoa sababu nne za yeye kupenda kutoka na wanaume wanaotajwa kuwa ni wadogo kwake kiumri.

Akizungumza na Ijumaa, nyota huyo ambaye pia hufahamika kama Shishi Baby, alisema maneno ya watu juu ya jambo hilo siyo sahihi, kwani historia ya maisha aliyopitia ndiyo inayomfanya aonekane mkubwa, wakati yeye ni binti mdogo aliyezaa mapema.

Aidha, mkali huyo wa kibao cha Paka la Baa, alisema yeye hivi sasa ana umri wa miaka 30, ‘size’ kabisa kwa wanaume anaotoka nao kimapenzi, kwani hata hao nao, siyo watoto ‘kihiiivyo’ kama maneno ya watu yanavyosema.
Sababu nyingine ni;
.
1: KUOGOPA KUZEESHWA
“Mimi ni kijana kutembea na wazee siwezi, naweza kujikuta nimezeeshwa bure kitu ambacho sikitaki hata kukisikia, kwani naamini bado nina uhitaji kama kijana.
“Angalia wasichana wengi wadogo wanaotoka kimapenzi na wazee hujikuta nao wanakuwa na mambo ya kizee, unadhani atafanya nini wakati ameshakubali kuzeeshwa?”

2: HATAKI KUBURUZWA
“Mimi napenda kuchakarika ndiyo maana sipendi kabisa penzi la wazee ambao ukiwa tegemezi kwao wanakuburuza. Wanawake wengi wanaotoka na wazee huwategemea kwa sababu ya uvivu wao wa kutafuta, kwangu mimi kazi tu!

3: ANASAKA PENZI LA KWELI
“Wasichana wengi wa mjini wamekuwa wakijiingiza kwa wazee lakini hawana mapenzi nao ya kweli, wanakwenda kuchuna pesa kisha wana viserengeti, mimi mwenzao nafuata penzi kwa hao vijana, wanajua kupenda na kwa sababu hobi yangu ni wao siwezi kuwa na wazee kwa kweli.”

4: VIJANA WANA NGUVU, WANAVUTIA
“Na uweke pia hii, kwamba vijana wana nguvu, damu changa na wanavutia, siwezi kutoka na wazee hawana mvuto.”
Baada ya kutaja sababu zake hizo, Shilole alihoji ni yupi mwenye afadhali kati yake na wasichana wenzake wanaotoka na wazee lakini wakiwa wavivu kutafuta?

Mwalimu Atiwa Mbaroni Kwa Tuhuma za Kumkuwadia Mwanafunzi Wake

$
0
0

Mwalimu wa Shule ya Msingi Nyaigabo iliyopo Kijiji cha Musati wilayani Serengeti, Mkoa wa Mara anatuhumiwa kumkuwadia kijana anayemuuzia duka kwa kumpelekea mwanafunzi na kusababisha apate ujauzito.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhani Ng’hazi alisema mwalimu huyo, Agness Matiko amekamatwa na kuhojiwa kwa tuhuma hizo.

Ng’hanzi alisema binti huyo mwenye umri wa miaka 16 alimaliza darasa la saba mwaka jana kwenye shule anayofundisha mwalimu huyo.

Alisema mwalimu huyo alikuwa akimtoa darasani mwanafunzi na kumpeleka nyumbani kwake na kumkutanisha na kijana wake huyo kwa ajili ya kufanya naye ngono.

Binti huyo alikuwa anasoma kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Ikorongo kabla ya kufukuzwa baada ya kubainika kuwa na mimba ya miezi sita.

“Mwaka jana nikiwa darasa la saba mwalimu alinipeleka nyumbani kwake ili nikamsaidie kukamua ng’ombe maziwa, siku ya pili wakati wa mapumziko alinichukua nikamuoshee vyombo tulimkuta huyo kijana baadaye mwalimu alinisihi nibaki naye ndani,” alidai.

Alidai licha ya kukataa kufanya naye ngono, lakini mwalimu alimwambia: “Mimi ni mwalimu wako, kama lingekuwa jambo baya nisingekushauri, hivyo wewe kubali, akatufungia kwa nje. Huyo kijana akanipeleka chumbani kwake akanilaza kitandani na kuniingilia.”

Kwa mujibu wa mwanafunzi huyo baadaye mwalimu huyo alikwenda kufungua mlango na kumchukua na kumpeleka darasani na huo ukawa mwendelezo wa kumkutanisha na kijana huyo.

Alidai kila mara alimpeleka nyumbani kwake na kuwakutanisha huku akimwambia anataka waoane.

“Baada ya kubainika nina ujauzito walimtorosha huyo kijana na kudai kuwa walimfukuza kwa madai aliwatia hasara dukani,” alidai.

Akizungumza baada ya kupata dhamana, licha ya kukiri kukamatwa kwa tuhuma hizo, mwalimu Matiko alisema hajawahi kumfanyia ukuwadi mwanafunzi huyo.

Alisema kijana aliyekuwa akiishi kwake walimpata kijijini hapa akiwa anatafuta kazi. “Ndipo tulimpatia kazi ya kuuza duka tangu Aprili hadi Oktoba 2015 nilipomfukuza kwa kunisababishia hasara na alisema kwao ni Mabatini mkoani Mwanza,” alisema.

Baba wa binti huyo, Marwa Nchama (53) alisema baada ya kubaini ana mimba alifuatilia na kubaini mwanaye alikuwa akifanyiwa vitendo vya unyanyasaji na kijana huyo.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Turuka Samwel alikana kulifahamu tukio hilo likiwamo suala la walimu kuwafanyisha kazi wanafunzi majumbani mwao.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Maftah Ally, alisema watumishi wanaohusishwa na tuhuma za kuwapa mimba wanafunzi licha ya kufikishwa mahakamani, watawachukulia hatua za kinidhamu.

Diamond Platnumz Aonyesha Hadharani Bastola Yake

$
0
0
The CEO of Wasafi Records, Diamond Platnumz, has now joined the list of celebrities who are believed to be walking around with guns.
Well this comes days after he shared a photo on his gram posing with a gun in what looks like a photo studio.
This has left many wondering whether he is a licensed gun holders or he was just posing with it for fun and giggles.

Wanafunzi Chuo Kikuu UDSM Wagoma..Kisa Hichi Hapa

$
0
0

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) leo wamegoma wakiishinikiza Bodi ya Mikopo(HESLB) kuwapatia fedha zao za kujikimu.

Kwa kawaida wanafunzi hupewa fedha za kujikimu kila baada ya miezi miwili



Majambazi Yauwa na Wananchi Baada ya Kumpora Mfanyabiashara Sh Laki Tano

$
0
0

Watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, wameuawa na mwingine mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kujihusisha na ujambazi jijini Dar es Salaam.Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Simon Sirro wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema tukio hilo lilitokea Mei 28 mwaka huu baada ya polisi kupata taarifa kuwa maeneo ya Mburahati kuna majambazi watatu, ambao walikuwa wanafukuzwa na kundi la bodaboda huku wakifyatua risasi.Sirro alisema katika ufuatiliaji askari walifika katika eneo hilo na kukuta jambazi mmoja akishambuliwa na wananchi baada ya silaha aliyokuwa akiitumia kuishiwa risasi.
Jambazi huyo alikutwa na silaha moja, bastola LLA yenye namba 649440. Alisema majambazi wengine wawili, walikimbia wakiwa na bodaboda yenye namba za usajili MC 444 BFY.
Polisi waliwakimbiza wakishirikiana na madereva bodaboda hadi kufika katika eneo la Kisukuru, ambako majambazi hao walianguka na kuangusha bastola yao aina ya Chinese Star, ndipo wananchi walianza kuwashambulia kwa mawe na fimbo.
Aliongeza kuwa majambazi hao, walishambuliwa baada ya muda mfupi walifariki dunia huku mwingine alifanikiwa kukimbia na begi dogo jeusi lililokuwa na fedha.Sirro alisema awali majambazi hao, walikuwa watatu wakiwa kwenye pikipiki maeneo ya Buguruni, ambapo walifanya tukio la uporaji wa Sh 500,000 mali ya Mushi Bakari, aliyekuwa na gari namba T 786 CZI Toyota IST ambaye walimjeruhi mkono wa kulia.


Msamaha wa Jakaya Kwa Baadhi ya Watuhumiwa wa Ufisadi wa EPA Waleta Utata

$
0
0

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe amesema Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete hakutumia ibara ya 45 ya Katiba kutoa msamaha kwa baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu (BoT), wanaoelezwa kuamriwa kurejesha fedha walizochukua.Aidha, alisema pale ambapo kuna makosa, Rais anaweza kumsamehe mtu ambaye tayari amehukumiwa au kupewa adhabu kwa kutumia ibara hiyo.Alisema, “Mimi kwa taarifa nilizonazo Mheshimiwa Rais mstaafu hakutumia kifungu hicho,” Dk Mwakyembe alisema bila kueleza kifungu kilichotumiwa.Alisema hivyo jana bungeni mjini hapa, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji (CUF) aliyetaka kujua endapo Rais aliyepita alitumia madaraka yake vibaya, alikosea au alikuwa sahihi kuruhusu baadhi ya watuhumiwa walipe fedha walizodaiwa kuzifanyia ubadhirifu kupitia akaunti ya EPA (Hawakutajwa).Pia, mbunge huyo katika swali lake la pili la nyongeza alitaka kujua ni lini watafikishwa mahakamani akieleza kuwa msamaha waliopewa haukuwa wa kikatiba na kwamba wanastahili kushitakiwa.Katika swali lake la msingi, Haji alitaka kujua iwapo Rais ana mamlaka ya kisheria kutoa msamaha kwa watuhumiwa wa uhalifu wa aina yoyote ambayo mashauri yake yapo katika vyombo vya dola kwenye hatua za uchunguzi, upelelezi au mahakamani.


Msichana wa Kazi za Ndani Afikishwa Mahakani Kwa Kuua Mtoto Mchanga

$
0
0

NAIROBI, KENYA: Msichana wa kazi za ndani mwenye miaka 20 afikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya mtoto mchanga wa miezi nane.


Wabunge wa Upinzani wametoka nje ya bunge kuonyesha kutokuwa na imani na Naibu Spika Tulia Ackson

$
0
0

Wabunge wa vyama vya upinzani leo wametoka nje kwa mara nyingine kupinga Naibu Spika Dk. Tulia Acksonkuendesha vikao vya Bunge na kumwachia Bunge yeye na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Taarifa kutoka Bungeni zinaeleza kuwa, wabunge wote wa upinzani wametoka nje kususia kikao cha Bunge ikiwa ni kutekeleza azimio lao la kutokuwa na imani na Dk Tulia.


Baada tu ya kusomwa dua ya kufungua Bunge asubuhi wabunge hao wametoka nje na kumwacha Dk. Tulia akiwa na wabunge wa CCM pekee.


Hata hivyo Dk. Tulia ameanza kupaniwa na wapinzani tangu jana. Ni kwa madai kuwa wapinzani hawamwamini tena.


Wameeleza kuwa, namna anavyoliongoza Bunge, kauli zake na kuyumba kwake katika kusimamia haki kwa wabunge wa Ukawa na wale wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumechochea kuonekana kuwa, nafasi aliyonayo haimstahili.


Kutokana na hali hiyo, Freeman Mbowe ambaye ni Kiongozi Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni jana aliahidi kuanzisha mgomo dhidi ya Dk. Tulia.


Mbowe aliwaambia hayo wabunge wenzake mjini Dodoma kwenye kikao cha dharura alichoitisha na kushirikisha waandishi wa habari.


Alisema, Dk. Tulia ndio tatizo kuu la Bunge la Kumi na Moja na kwamba, kiongozi huyo wa Bunge kila anapokuwa kwenye kiti na kuongoza Bunge, mtafaruku hutokea.


“Nitapendekeza kuwa kila kikao cha Bunge kinachoongozwa na Tulia Ackson, sote tutoke nje ili kuonesha kwamba hatuna imani naye katika kuendesha shuguli za bunge,” Mbowe alisema jana.


Utekelezwaji wa kauli ya Mbowe umeanza leo ambapo sasa Dk. Tulia amebaki na wabunge wa CCM pekee.


Wolper adai amefilisiwa na Mkongo , amejikuta hana gari wala sehemu ya kulala

$
0
0


Msanii wa filamu, Jacqueline Wolper baada ya kukiri kwamba anatoka kimapenzi na Harmonize, amefunguka na kueleza madai ya kufilisiwa na Mkongo ambaye alikuwa mpenzi wake wa zamani.

Akiongea katika promo ya kipindi kipya cha Take One ambacho kinatarajiwa kuruka Jumanne hii, Wolper amedai yeye ndiye aliyetendwa na Mkongo ambaye alikuwa mpenzi wake, kwani wakati anaanza naye mahusiano alikuwa ana gari na nyumba lakini baadae akijikuta hana hata sehemu yakulala.

Muigizaji huyo ambaye amekuwa akionyesha uwezo mkubwa katika filamu zake, amedai alikuwa anajilipia nyumba kwa dola, lakini ulifikia wakati akafilisika na kuanza kulala hoteli.

Wolper amedai mahusiano hayo yalimsababishia kugombana na baadhi ya watu wake wa karibu ambao walikuwa wakimshauri vizuri, lakini yeye alikuwa akiwaaona kama wanamfitini.

Muigizaji huyo ambaye amewahi kutamba na filamu yake Tom Boy, kwa sasa anatoka kimapenzi na hit maker wa wimbo ‘Bado’, Harmonize kutoka WCB.


Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images