Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104796 articles
Browse latest View live

Umoja wa Mataifa Wamsifu Rais Magufuli Kwa Kupambana na Rushwa na Kukusanya Mapato Mengi

$
0
0
SHIRIKA la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), limeeleza kuridhishwa kwake na utendaji wa Rais John Magufuli katika mapambano ya rushwa, kuongeza uwajibikaji na ukusanyaji wa mapato.

Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Alvaro Rodriguez, alisema hayo jana katika semina ya wabunge kuhusu Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia.

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano, imekuwa ikipambana na rushwa na kusimamia kwa karibu ukusanyaji mapato, hali aliyosema itasaidia maendeleo kwa kuwa hakuna nchi iliyoendelea bila kuchapakazi.

Rodriguez alisema mbali na kuona maendeleo katika baadhi ya mikoa na mitaa, ameona jitihada hizo za Serikali na amefurahishwa na kuridhika nazo.

Mwakilishi huyo pia alisema Serikali ya Tanzania na Ofisi ya Umoja wa Mataifa (UN), zimekuwa zikifanya kazi pamoja katika harakati za usambazaji wa malengo ya dunia kwa Watanzania.

Alisisitiza umuhimu wa malengo hayo kueleweka kwa wabunge, ili katika jukumu lao la kuisimamia Serikali, wawe mabalozi wa utekelezaji wa malengo hayo katika ufuatiliaji kwenye ngazi zote za utawala.

Awali akifungua semina hiyo, Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson aliwataka wabunge kuoanisha malengo hayo na malengo ya Dira ya Taifa ya 2025 pamoja na malengo ya Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano wa 2016/2017 mpaka 2020/2021 ambao ulishafikishwa bungeni.

Dk Tulia aliwataka wabunge kila mmoja kuyaelewa vizuri malengo hayo ili kila mmoja ashikilie mahali atakapofuatilia Serikalini wakati wa utekelezaji wake.

Miongoni mwa malengo hayo ni pamoja na kutokomeza umasikini wa kila aina, kufuta njaa kwa kuhakikisha kuna kuwa na uhakika wa chakula bora kwakuboresha kilimo endelevu, kuhakikisha watu wote wanakuwa na afya bora nakupata huduma za afya na kupunguza utofauti wa kipato.

Akitoa mada katika semina hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Paul Kessy, alisema Tanzania imeshiriki kwa kiasi kikubwa katika maandalizi ya malengo hayo na hivyo mchango wake kuwa sehemu ya maudhui ya malengo hayo endelevu kwa maslahi mapana ya taifa na watu wake.

Kwa mujibu wa Kessy, sehemu ya mchango wa Tanzania katika kuunda malengo hayo, ilikuwa ni kutaka malengo hayo yahakikishe kuwa baadhi ya masuala ambayo hayakukamilika katika utekelezaji wa Malengo ya Milenia yanazingatiwa katika malengo endelevu.

Baadhi ya mambo hayo ni pamoja na kupunguza umasikini, upatikanaji wa ajira na kukuza uwezo wa nchi masikini hasa katika maendeleo ya teknolojia.

Video : Ali Kiba Akubali Kua ni Kweli Hajui Kingereza

$
0
0
Ni mara chache sana unakutana na msanii na anakubali kua lugha ya kiingereza inampiga chenga. Nakumbuka msanii AY alikubali kua miaka kama 13 nyuma hakua akiiongea kugha hiyo kwa ufasaha lakini baada ya mazoezi mengi kwa sasa yupo vizuri.

Siku chache zilizopita msanii Ali Kiba alikubali kua pamoja na kukaa katika gemu mda mrefu na kukutana na wasanii wengi wa nje lugha hiyo bado ni tatizo kwake. Japo anaweza kuongea kidogo sana kwa Kingereza ila si mtaalamu sana. Msikie hapa akifunguka kuhusiana na swala hilo....

Tanzania Imetolewa na Misri Michuano ya AFCON 2017

$
0
0
June 4 2016 ilikuwa ni siku ambayo timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars itacheza mchezo wake wa tatu wa Kundi G wa kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika 2017 AFCON, kwa kucheza na timu ya taifa ya Misri The Pharaos uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Huu ni mchezo ambao Taifa Stars alikuwa anahitaji ushindi wa aina yoyote ile.


Huu ulikuwa ni mchezo wa tatu kwa Taifa Stars, lakini ulikuwa ni mchezo wa marudiano na timu ya taifa ya Misri baada ya mchezo wa kwanza kuchezwa Misri June 14 2015 katika mji wa Alexandria na kumalizika kwa Taifa Stars kufungwa jumla ya magoli 3-0, hivyo huu ulikuwa ni mchezo wa kulipa kisasi kwa Taifa Stars, lakini pia ulikuwa ni mchezo wa kutengeneza mazingira ya kufuzu AFCON 2017.


Hata hivyo timu ya Taifa ya Tanzania licha ya kuwa nyumbani imekubali kipigo cha goli 2-0, , magoli ya Misri yalifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea anayeichezea klabu ya AS Roma ya Italia Mohamed Salah dakika ya 43 na 58, kwa upande wa Tanzania Mbwana Samatta alikosa penati iliyopatikana baada ya Himid Mao kufanyiwa faulo ndani ya 18.

Kwa matokeo hayo Taifa Stars wanakuwa wametolewa rasmi katika michuano ya kuwania kufuzu AFCON 2017, lakini imebakiza mchezo mmoja wa kukamilisha ratiba itakayocheza September dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles, Misri imefikisha jumla ya point 10, Taifa Stars point moja na Nigeria ina point 2.

Mbeya: Watumishi 11 Wasimamishwa Kazi Kwa Kuwa na Vyeti Feki vya Kidato cha Nne

$
0
0
Watumishi 11 mkoani wa idara ya afya mkoani Mbeya wamesimamishwa kazi baada ya kukutwa na kosa la kughushi vyeti vya kidato cha nne hilo limefanyika baada ya zoezi la kuhakikisha vyeti kwa kushirikiana na baraza la mitihani NECTA ikiwa ni mwitikio wa agizo alilotoa rais John Magufuli.

Amesema waliwakilisha vyeti vingi NECTA na hivyo 11 ndio vikabainika vilikuwa vya kughushi ambao karibia wote ni wanawake Tazama Hapa:

Prof. Mwandosya Atoa Ufafanuzi Juu ya Elimu yake

$
0
0
Mwaka 1967 Serikali, kupitia Wizara ya Elimu ya Taifa ilianzisha sera ya kuwa na shule ambazo zingechukua wanafunzi wenye vipaji, waliofanya vizuri na kupata alama za juu kwenye masomo ya sayansi na hisabati katika mitihani ya kidato cha nne.

Katika mfumo huo taasisi/shule mbili, Chuo cha Ufundi Dar es Salaam, na Sekondari ya Kibaha, zilichaguliwa kudahili wanafunzi waliopata alama za juu katika hisabati, fizikia, na kemia, kuchukua masomo ya Hisabati, Hisabati, na Fizikia (Pure Mathematics, Applied Mathematics, and Physics) kidato cha tano na cha sita(Advanced Level au A-Level).

Chuo cha Ufundi Dar es Salaam kilichaguliwa kuanzisha masomo ya kidato cha tano na cha sita mbali na mafunzo ya kawaida ya cheti(Full Technician Certificate). Kozi hizi mbili zilienda sambamba lakini zilikuwa tofauti. Masomo ya kidato cha tano na sita yalilenga katika kuwatayarisha wanafunzi ambao baada ya kumaliza na kufaulu wangeenda vyuo vikuu kusomea uhandisi.

Mbali na mchepuo wa Hisabati, Hisabati na Fizikia, wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita Chuo cha Ufundi Dae es Salaam walichukua masomo ya ziada ya Uchoraji katika Uhandisi (Engineering Drawing) na mazoezi ya karakana (Workshop Practice).

Masomo haya yalitolewa katika azma ile ile ya kuwatayarisha wanafunzi kuchukua uhandisi vyuo vikuu lakini hawakutahiniwa katika masomo haya ya ziada. Mchepuo huu ulianza mwaka 1968 na pamoja na mafanikio makubwa ulihitimishwa mwaka 1972.

Baadhi ya wanafunzi waliopitia mchepuo huo ni Profesa Mathew Luhanga, Profesa Lunogelo Mwamila, Profesa Mark Mwandosya, Eric Mugurusi, Majani(RIP), Profesa Maurice Mbago, Kassim Mpenda, na wahandisi na wataalamu wengi mashuhuri.

Kwa kumalizia, si kweli kwamba Profesa Mwandosya alipata cheti cha ufundi halafu akaenda Chuo Kikuu cha Aston Uingereza, bali alipata alama za juu kidato cha sita katika mchepuo wa Hisabati, Hisabati, na Fizikia (Pure Mathematics, Applied Mathematics, and Physics), msingi uliomwezesha hatimaye kupata shahada ya uhandisi umeme daraja la kwanza( First Class Honours), Chuo Kikuu cha Aston, Uingereza, na hivyo kuruhusiwa kufanya shahada ya uzamifu (PhD), Chuo Kikuu cha Birmingham, Uingereza, moja kwa moja bila kupitia shahada ya uzamili(Masters).

Rafiki yangu yeyote wa fb anayemfahamu Ndugu Malisa GJ,mwandishi na mchangiaji wa makala katika mitandao ya kijamii, tafadhali mpatie taarifa hii. Shukrani.

Mark Mwandosya.

Waliotimuliwa Udom Waibuka, Watoa ya Moyoni

$
0
0
Jana wawakilishi wa wanafunzi hao ambao waliambatana na viongozi wa

Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), walisema wanapinga pia hatua ya kutimuliwa chuoni.

Dar/Dodoma. Sakata Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) limezidi kupanuka baada ya wanafunzi waliorudishwa nyumbani kupinga kuitwa vilaza.

Jana wawakilishi wa wanafunzi hao ambao waliambatana na viongozi wa

Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), walisema wanapinga pia hatua ya kutimuliwa chuoni.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Gibson Johnson alisema wanasikitika kuona wanavyozushiwa tuhuma mbalimbali kuhusiana na wao kujiunga na chuo hicho.

Alisema wamekuwa wakijiuliza sababu za Serikali zinazotaka kuhalalisha kutimuliwa kwao chuoni kuwa hawakuwa na sifa, jambo ambalo si la kweli.

“Siyo kweli kwamba sisi ni vilaza (wanafunzi wasiofanya vizuri darasani) na waliofeli na kupata daraja sifuri.

“Sisi ni wanafunzi tuliofaulu kwa viwango vilivyohitajika kwa daraja la kwanza hadi la tatu na tulipangiwa shule za kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita, lakini tulibadili na kuamua kujiunga Udom, hivyo tunaomba Serikali itumie busara zake.

“Hatuwezi kwenda kusoma kidato cha tano na sita kwa kuwa tumepoteza muda wetu.”

Alisema wanamshauri Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako na Rais John Magufuli kutumia busara kuwarudisha chuoni kumalizia masomo yao.

Katibu Mkuu wa TSNP, Alphonce Lusako aliitaka Serikali ichukukue hatua kwa waliohusika kudahili wanafunzi wasio na vigezo na kuwawajibisha.

“Lakini pia wanafunzi wafidiwe fedha na muda waliopoteza kwa wakati wote waliokuwa chuoni, kama hawatapewa haki zao, sisi tutashirikiana na wadau wa elimu zikiwamo asasi za utetezi wa kisheria kutafuta haki mahakama,” alisema Lusako.



Udom yazungumza

Ofisa uhusiano wa Udom, Beatrice Baltazali alisema wanafunzi hao wote walifaulu vizuri wakiwa na daraja la kwanza, pili na wachache daraja la tatu.

“Wanafunzi wote walikuwa na nafasi ya kwenda kidato cha tano, lakini kwa kuwa waliahidiwa ajira, waliona wapitie huku kwa kuwa watapata ajira ya moja kwa moja,” alisema.

Beatrice alisema walimu wa Udom walikuwa wanalipwa fedha za ziada kuwafundisha wanafunzi wa programu hiyo kwa kuwa walikuwa wanatumia muda mwingi zaidi ya kiwango walichokuwa wamepangiwa.

“Kutokana na madai ya malipo hayo, mkaguzi wa ndani aligundua kuna tatizo, ndiyo walimu nao wakaamua kugoma, wanafunzi wakawa hawafundishwi Serikali ikaamua warudishwe nyumbani,” alisema Beatrice.

My take; mh raisi tuelewe lipi na aliangalia wapi mpaka ukajilizisha hawa wanafunzi kufukuzwa ndani ya masaa 24?

Diamond Platnumz Afunguka Kuhusu Wema Sepetu

$
0
0
Akiwa kwenye kipindi cha Friday Night Live cha EATV, Diamond Platnuzm amesema kitendo alichofanya Wema kupost kazi zake anadhani imefika wakati labda Wema Sepetu ameona hakuna sababu yeye kuendelea kumchukua Diamond Platnumz na ndiyo maana ameonyesha upendo kwa kusupport kazi zake na za wasanii kutoka kwenye Label yake.


“Kuna wakati inafika watu mnakuwa mmekuwa labda, mtu anaona hana sababu ya kuendelea kukuchukia au kuwa na vita na wewe, sababu mwanzo mwanzo mkiwa bado mnaenda mnaona kuna vitu mko navyo ndiyo maana kuna kuwa na chuki kubwa, lakini ikifika wakati kila mtu amesonga mbele na maisha yake, ameridhika na maisha yake anaona kwanini nimuwekee vita mtu fulani hivyo nadhani labda wakati huo ndiyo huu maana mwenyewe nimeona kweli amepost BET, amepost promo ya Rich Mavoko kwangu mimi nafurahi kwa sababu naona haina faida kwa sisi wasanii kuwekeana vita” alisema Diamond Platnumz

Mbali na hilo Diamond Platnumz alidai toka ameachana na Wema Sepetu hana namba yake ya simu, hajawahi hata siku moja kumpigia simu wala Wema Sepetu hajawahi kumpigia simu Diamond Platnumz.

Kajala Amwanika Bwana Mpya!

$
0
0
Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu, staa wa filamu Bongo, Kajala Masanja juzikati alimwanika bwana’ke mpya, kufuatia kupigana kibuti na Mbongo Fleva, Quick Raca, Risasi linakujuza.

Kajala (picha ya kushoto) na mwamme anayedaiwa kuwa bwana wake mpya
Katika Pool Party ya staa mwenzao, Shilole, iliyofanyika katika uwanja wa ofisi ya BKT iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam, Kajala alimtambulisha mwanaume huyo bila kumtaja jina, akisema ndiye mtu wake rasmi kwa sasa.

“Naona unanitolea macho na kunitamani muda mrefu na unavyopenda umbeya unataka kujua hawa nilionao ni kina nani, naomba ufahamu kuwa huyu ndiye mchumba wangu wa sasa, ndiyo maana unaniona niko naye,” alisema msanii huyo.

Kajala, ambaye pia alimuonya bwana’ke huyo kuwa makini na paparazi wetu, alithibitisha usemi huo baada ya kuondoka pamoja na mtu wake huyo katika viwanja hivyo kuelekea Coco Beach kabla ya baadaye kuonekana tena pamoja wakinywa kinywaji kimoja ndani ya Ukumbi wa Club Billicanas.

Kabla ya kuwa pamoja na Quick Raca, Kajala alikuwa na mumewe, Faraji Chambo ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka saba gerezani, Machi 2013 baada ya kupatikana na hatia ya utakatishaji pesa, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu.

Chanzo: GPL

Wema Sepetu Adai Mwaka 2006 Ulikuwa Mwisho wa Miss Tanzania

$
0
0
Staa wa bongo movie,  Wema Sepetu ambaye pia aliwahi kuwa Miss Tanzania 2006 amesema hajui lolote kuhusu mashindano hayo zaidi ya kuwa mwaka alioshinda yeye ndiyo ulikuwa wa mwisho kwa mashindano hayo.

Hawa ndiyo walikuwa washindi watatu wa Miss Tanzania 2006,kulia ni Lisa (Mshindi wa 2),Kati ni Wema Sepetu (Mshindi wa 1) na Jokate (Mshindi wa 3).
Hawa ndiyo walikuwa washindi watatu wa Miss Tanzania 2006,kulia ni Lisa (Mshindi wa 2),Kati ni Wema Sepetu (Mshindi wa 1) na Jokate (Mshindi wa 3).
Mwaka jana mashindano ya Miss Tanzania yalifungiwa na BASATA kutokana na tuhuma za upangaji wa matokeo uliosababisha kupoteza msisimko na mvuto wa mashindano hayo. Hata hivyo mashindano hayo yamerejea tena.

Akiongea na Times FM, Wema alisema, “Sijui ni nini hasa kimetokea, maana mimi sifuatilii kabisa Miss Tanzania kwa sasa wala sijui Miss Tanzania mwaka huu anaitwa nani, nimeamua kuachana nayo kabisa sijui lolote, ila ninachojua mimi 2006 ndio mwaka wa mwisho wa Miss Tanzania.”

Bongo5

Baada ya kuoa mwanamke mwingine, Isabella adai ni yeye ndiye alimpiga chini Kalama, adai ni mwanaume asiye na future

$
0
0
Baada ya rapper wa kundi la Gangwe Mobb, Luteni Kalama kuoa mwanamke mwingine na kumwacha mchumba wake aliyemvisha pete, Isabella ameibuka na kudai kuwa ni yeye ndiye aliyemwacha baada ya kumuona ni mwanaume asiye na future.

“Mimi na Kalama tulikuwa tumeshaachana muda mrefu kwasababu nimeona ni mwanaume ambaye hana future hawazi chochote, kwahiyo nikaona kwanini nijipotezee muda. Mwanaume anaamka saa saba, kwahiyo nikaona niachane naye,” Isabela alimuambia mtangazaji wa Jembe FM, Natty E.

“Lakini watu wameona ilivyotokea gazeti wanahisi labda Kalama aliniacha mimi kitu ambacho sio kweli, hana uwezo wa kuniacha, mimi ndio nilimuacha. Na nafikiri stress zake ndio zimemfanya aende akamuoe rafiki yangu sasa si ni uchizi. Halafu mwanamke unaoa unaenda kukaa kwa mwanamke tena, yeye si ndio anakuwa ameolewa, kwahiyo yeye ni mwanaume ambaye ni kilaza,” aliongeza Isabela.

Babu Tale asema ni bahati kwa wasanii wa ‘WCB’ kupata wanawake wenye umri mkubwa zaidi yao (Video)

$
0
0
Baada ya kambi ya WCB kuonekana wasanii wake wanapenda kutoka kimapenzi na wanawake wenye umri mkubwa zaidi yao, uongozi wa kambi hiyo umelizungumzia swala hilo.
Diamond, Harmonize

Akizungumza na waandishi wa habari Alhamisi hii, Mmoja kati ya viongozi wa juu wa kambi hiyo, Babu Tale, amesema ni bahati kwa wasanii wake kupata wanawake waliowazidi umri.

“Sisi tunameneji wasanii hatumeneji hisia zao, lakini ikitokea msanii fulani amempenda mwanamke fulani tunamuacha kwa sababu ni mapenzi yake,” alisema Tale. “Tunaona ni bahati kwa wasanii wetu kupata wanawake waliowazidi umri, hiyo ni bahati (anacheka) kwa sababu wanamuenzi Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alimuoa Bi Khadija ambaye alimzidi umri,”

Hata hivyo, Tale alisema ndani ya WCB hawameneji mapenzi bali wanammeneji msanii pamoja na kazi zake.

Mwanamuziki Mwana FA Amefunga Ndoa na Mchumba wake Aitwaye Helga

$
0
0
Mwana FA unaona lini? Hatimaye jibu lake limepatikana. Rapper huyo amefunga ndoa Jumapili hii.

Hitmaker huyo wa Asanteni kwa Kuja amefunga ndoa na mchumba wake aitwaye Helga.

Ndoa hiyo ya kiislamu imehudhuriwa na ndugu na marafiki zake wa karibu wakiwemo AY, Hermy B, Ommy Dimpoz, Sallam, Dully Sykes, Alberto Msando na wengine.


UKAWA Wamkimbia Naibu Spika nje ya Bunge

$
0
0
MSIMAMO wa wabunge wa upinzani wa kususia kushiriki vikao vya Bunge vinavyoongozwa na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson umechukua sura mpya.

Jana wabunge hao walitoka ndani ya ukumbi wa Pius Msekwa uliopo bungeni mjini Dodoma  baada ya kiongozi huyo kupewa nafasi ya kufungua semina ya wabunge kuhusu Malengo Endelevu ya Dunia.
 
Semina hiyo ilikuwa imeandaliwa na Umoja wa Mataifa kupitia mpango wake wa kufanya kazi pamoja (Delivering as One).

Wabunge wa upinzani wanaotoka vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), walitoka ndani ya ukumbi huyo baada ya Naibu Spika huyo kupewa nafasi ya kufungua semina hiyo iliyoanza saa nne asubuhi.
 
Wabunge hao walirejea ukumbini na kushiriki semina hiyo baada ya Dk. Ackson kumaliza kuwasilisha hotuba yake.
 
Kususa kwa wabunge hao jana kulikuja baada ya kuwa walikuwa wamesusa kuhudhuria vikao vya Bunge vilivyoongozwa na Dk. Ackson kwa siku nne mfululizo mpaka Ijumaa.
 
Kambi ya Upinzani Bungeni imekuwa ikifanya hivyo dhidi ya Naibu Spika huyo tangu uongozi wa kambi hiyo utangaze kutokuwa na imani naye Jumatatu.
 
Tayari wabunge hao wamewasilisha hoja ya azimio la kutaka kumng'oa madarakani yenye sababu sita.
 
Jumanne iliyopita, kambi hiyo ilianza utaratibu huo wa kutoka kwenye ukumbi wa Bunge mara tu baada Naibu Spika kuingia.
 
Upinzani unachodai kutoridhishwa na uendeshwaji wa chombo hicho cha kutunga sheria chini ya Naibu Mwanasheria Mkuu huyo wa zamani wa serikali.
 
Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, alitangaza Jumatatu kuwa upinzani hauna imani na Naibu Spika na hautakuwa tayari kushiriki vikao vinavyoongozwa na kiongozi huyo wa Bunge hadi pale "haki itakapopatikana".
 
Kutokana na msimamo huo, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe, aliuomba uongozi wa Bunge kutolipa mishahara na posho za wabunge wa kambi hiyo waliosusa Jumanne.
 
Hata hivyo, Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa, aliponda pendekezo hilo .
 
"Kama tuliacha posho ya Sh. milioni 30 za Bunge la Katiba, itakuwa hii ya vikao vya Bunge la Bajeti ambayo haifiki hata milioni tano?” Alihoji Mchungaji Msigwa.
 
"Hoja hapa si fedha, hoja ni misingi ya uendeshaji wa Bunge.
 
"Hatuwezi kukubali kuburuzwa eti kwa sababu tunapewa posho.

Diamond Asema ‘WCB’ Imeajiri watu 42, Azungumzia Issue ya Kulipa Kodi

$
0
0
Mkali wa muziki na CEO wa label ya WCB, Diamond Platnumz amesema label yake mpaka sasa tayari imeajiri watu 42.

Muimbaji huyo ambaye pia anamiliki, studio ya picha pamoja na studio ya muziki ‘Wasafi Record’, aliwaambia waandishi wa habari hivi karibuni kuwa kila anachokipata anagawana na team yake.

“Tunashukuru mungu kile tunachokipata tunagawana na wengine, mpaka sasa tayari WCB imeajiri watu 42, hii ni hatua kubwa sana katika tasnia ya muziki wetu,” alisema Diamond.

Katika hatua nyingine, Diamond amesema ni swala la kiungwana kulipa kodi katika kile anachopita.

“Unajua katika kila penye biashara ni lazima na ni haki kulipa kodi ili pato la taifa liingie, namna ya mapato maana yake nini, serikali inatambua kazi na inailinda. So serikali ipo na inafanya hivyo, lakini labda kuna nyanja nyingine hawazioni, kwa hiyo sisi kama tunataka kazi zetu zichangie pato la serikali, lazima tuwe mstari wa mbele katika kuonyesha nyanja zote za mapato, kwamba tunafanya hichi na hichi, ridhiki zetu zinatokea hapa na hapa, mishahara yetu tunagawa hivi na hivi, na kama serikali inavyoagiza katika kiasi hichi tunatakiwa kutoa kiasi hichi kwa ajili ya serikali. Kwa hiyo tusilalamike tu serikali haifanyi kazi wakati sisi tunaweza kuwa wa kwanza kuirahisishia serikali kutekeleza majukumu yake,” alisema Diamond.

 Bongo5

Mwanamke Kumkimbia Mume Maisha yakiwa Magumu na Kurudi yanapokuwa Mazuri.

$
0
0
Nimeleta mada hii tujadili tuone ni wapi mtu anapokuwa sahihi na wapi mtu anakosea.

Mkataba wa ndoa unawataka wanandoa kuvumiliana katika SHIDA na RAHA.

Sasa chukulia mmeoana halafu inafikia mahali maisha yanakuwa magumu hata milo miwili inashindikana, hivyo mwanamke anaamua kumkimbia mumewe.

Mwanaume anapobaki mwenyewe anaparangana japo maisha yanarudi kwenye mstari, na hapo mwanamke anaanza kutaka kurudi tena kwa nguvu kwakuwa bado ni mke halali.

Usahihi wa huyu mwanamke ni upi. Kabla hajaingia kwa nyumba, mwanaume alikuwa vizuri na pengine mwanamke alichangia ufukara katika familia hiyo kwani alipoondoka, mali zilirejea, na yeye akataka kurejea tena. Je kama wewe ndo mwanaume utampokea tena? Tuangalie pande zote.

Karibu tuchangie.

Mwanamuziki Shetta Apangua Tuhuma za Kubebeshwa Madawa ya Kulevya

$
0
0
Star wa Bongo Fleva Shetta anayefanya vizuri na wimbo wake mpya wa ”Namjua” ameweka wazi juu ya mafanikio yake baada ya kuwa na tetesi nyingi kuwa siku hizi na yeye anabeba mabegi ya unga.

Akizungumza na Enewz Shetta alikanusha tuhuma hizo na kudai kuwa yeye shughuli yake kubwa ni mziki na hata anaposafiri kwenda nchi nyingine watu huwa wanaona yeye anachokifataga huko kama kushuti video nzuri pamoja na show.

“Mimi sifanyi hiyo biashara nafanya mziki kuna vitu vingi vya kutuingizia pesa sisi wasanii tunauza video zetu yutubu,matukio miito ya simu,endorsement na nimeshakuwa balozi wa kampuni kubwa kwahiyo ninavitu vingi vya kuniingizia pesa”,alisema Shetta.

Hotuba ya Zitto Kabwe leo katika Mkutano wa 'Linda Demokrasia' Mbagala Dar

$
0
0
Ndugu Wananchi, Nawashukuru sana kwa kujitokeza kwenu kuitikia wito wetu wa kuja kutusikiliza. Tumewaita hapa ili kuwaeleza kinachoendelea katika nchi yetu hivi sasa na madhara makubwa yanayoweza kutokea iwapo hatutosimama kidete dhidi ya mbinu zozote za kufifiza na kuminya demokrasia na misingi ya uwajibikaji katika nchi yetu.

Mwaka 2015 tulikwenda kwenye uchaguzi kuchagua madiwani, wabunge na Rais. Baada ya Uchaguzi kumalizika Serikali mpya iliundwa na Serikali za Mitaa (Halmashauri) kuundwa. Nawapongeza wananchi wote kwa kuendesha zoezi la uchaguzi kwa amani na kuweka heshima ya nchi yetu mbele.

Baada ya uchaguzi tumeona viongozi wapya wakichukua hatua mbalimbali nzuri na mbaya, zenye kujenga na kubomoa, zenye kuimarisha demokrasia na zinazobomoa demokrasia. Tumeshuhudia maamuzi mengine ambayo yanatia khofu, kwamba ingawa tunaona dhamira ya dhati ya kupambana na Ufisadi, lakini pia tunaona mbinu za chini chini za kutokomeza Demokrasia ya nchi yetu ambayo tumeijenga kwa jasho na damu.

Mkutano wetu wa leo utagusia baadhi ya maeneo ambayo tunadhani ni vihatarishi vya ustawi wa wananchi wetu na ambavyo lazima tuanze kuvipinga mapema sana kabla havijaota mizizi. Ndugu Wananchi, Baadhi ya maeneo tutakayozungumza leo ni pamoja na;

• Wabunge kusimamishwa kazi za Bunge

• Maamuzi ya Serikali kuhusu Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma

• Hali ya Zanzibar

• Mwelekeo wa Bajeti ya Kwanza ya Serikali ya Rais Magufuli

• Tishio la Nchi kuelekea kwenye Utawala wa Imla wa MTU mmoja

Wabunge Kusimamishwa Kazi

Ndugu Wananchi, mnamo tarehe 30 Mei, 2016 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Naibu Spika lilipitisha Azimio la Bunge la kuwasimamisha kazi wabunge 7 kwa vipindi mbalimbali. Wabunge wawili, ndugu Esther Bulaya na ndugu Tundu Lissu walisimamishwa Mikutano miwili ya Bunge. Wabunge Wanne, ndugu Halima Mdee, Ndugu Pauline Gekul, Ndugu Godbless Lema na Mimi ninayezungumza nanyi tulisimamishwa mkutano mmoja, huu unaoendelea wa Bajeti, na mbunge mmoja ndg John Heche Suguta amesimamishwa vikao 10 vya mkutano huu wa tatu unaoendelea.

Sababu iliyoelezwa na Bunge ni kwamba wabunge hawa walifanya fujo siku ya tarehe 27 Januari, 2016 kufuatia hoja niliyoitoa Bungeni ya kutaka mjadala kuhusu sababu za hovyo na za uongo zilizotolewa na Serikali kuhusu uamuzi wa kuzuia Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) pamoja na televisheni binafsi (Star tv na Azam) kuonyesha moja kwa moja mikutano ya Bunge.

Ndugu Wananchi, mimi binafsi pamoja na wabunge wengine 6 hatukufanya fujo yeyote ndani ya Bunge. Kosa letu kubwa ni kutaka kuhoji maamuzi ya Serikali ambayo kwa maoni yetu hayana msingi wowote. Serikali inasema ninyi Wananchi hamfanyi kazi kwa sababu Bunge linaonyeshwa wakati wa kazi. Hata hivyo Serikali hiyo hiyo inatwambia kuwa katika kipindi cha miaka 10 iliyopita uchumi wa Tanzania ulikua kutoka tshs 16 trilioni mwaka 2005 mpaka tshs 99 trilioni mwaka 2015. Kipindi chote hiki Bunge lilikuwa linaonyeshwa moja kwa moja na televisheni ya Taifa (TBC) na televisheni ya StarTV.

Kama mngekuwa hamfanyi kazi Uchumi usingekua kwa kiwango hicho cha asilimia 600 ndani ya Muongo mmoja wa uongozi wa Rais Jakaya Kikwete. Utawala wa Rais John Magufuli unataka kutuaminisha kuwa ukiwa na Bunge ‘live’ watu hawafanyi kazi lakini uongozi uliopita umedhihirisha kwa ushahidi kuwa ukipanua demokrasia na kuwaonyesha wananchi kila kinachoendelea Bungeni uwezo wa kazi unaongezeka na uwezo wa wananchi kuwajibisha viongozi wao unaongezeka.

Hivyo Serikali kuamua kuficha Bunge ni mbinu za kuendesha Serikali kwenye giza ili kufanya maamuzi ambayo baadaye ionekane Serikali tu au Rais tu ndiye mfanya kazi. Ndio maana mikutano yote ya Rais anapohutubia huonyeshwa moja kwa moja lakini sio Bunge.

Wananchi, Wabunge wamesimamishwa kwa sababu ya kukataa Bunge kuendeshwa kwenye giza. Wabunge waliosimamishwa walisimama kidete kuhoji sababu za Serikali kufikia maamuzi hayo. Walitaka kujua kwanini Serikali imekuwa kigeugeu kwa kubadilisha badilisha sababu zake za kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya Bunge.

Wakati mmoja Serikali ilisema sababu ni gharama, kama ni hivyo ni kwanini walizuia StarTV na AzamTV kuonyesha moja kwa moja? Ni dhahiri wananchi Serikali inataka kuendesha mambo yake kwa uficho kwa sababu kuna maamuzi inataka kufanya na haitaki wananchi mjue mapema maamuzi hayo. Serikali inaturudisha nyuma badala ya kwenda mbele.

Wananchi, wabunge waliosimamishwa ni wabunge wenye uwezo wa kujenga hoja. Kuna wengine wamebaki Bungeni wenye uwezo mkubwa tu wa kujenga hoja, lakini hawa saba waliosimamishwa ni wabunge waliojidhihirisha kwa muda mfupi kwa baadhi yao kama ndugu Heche, kwamba wanaweza kusimamia hoja zao bila woga. Swali la kujiuliza ni, tukio ambalo limetokea mwezi Januari ni kwanini lifanyiwe mwezi Juni tena wiki moja tu kabla ya Waziri wa Fedha kuwasilisha Bungeni Bajeti ya Serikali?

Katika waliosimamishwa ni pamoja na Waziri Kivuli wa Fedha, ndg. Halima Mdee na Waziri Kivuli wa zamani wa Fedha ambaye anazungumza nanyi leo (Zitto Kabwe). Kuna nini? Nitawaeleza katika hoja ya Bajeti. Kimsingi Utawala wa Rais Magufuli umepanga kupandisha kodi za wananchi masikini na uliona uwepo wetu bungeni utatibua mipango yao.

Rais na wenzake ndani ya CCM hawapendi kusikia hoja zinazowapinga, hawana uvumilivu wa kukosolewa na hivyo walipanga kuhakikisha kuwa baadhi yetu hatutakuwepo kwenye mjadala wa Bajeti ili kufanikisha malengo yao ya kufanya maamuzi yatakayowandamiza wananchi. Nitaeleza vizuri hili baada ya muda kidogo. Hivyo nataka Watanzania wajue kuwa kusimamishwa kwetu ni ajenda maalumu ya Serikali ya Rais Magufuli kufunika mjadala wa Bajeti kwa sababu inajua kuwa tunajua inachopanga kufanya dhidi ya mafukara wa nchi yetu.

Sisi hatutakaa kimya, tutatumia wenzetu waliopo Bungeni kuyasema haya na pia tutazungumza na wananchi kuwaeleza pia. Tutatumia mikutano yetu mbalimbali bila kujali itikadi za vyama vyetu kuhakikisha kuwa Wananchi wanajua kila kinachoendelea na kuwataka kuunganisha nguvu kukataa udikteta unaonyemelea nchi yetu.

Wanafunzi 7800 Kufukuzwa Chuo Kikuu Cha Dodoma

Ndugu Wananchi, mmesikia sakata la Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma waliokuwa wanasomea programu maalumu ya Ualimu wa Sayansi. Hawa ni watoto wa Watanzania masikini waliokubali kuacha kwenda Kidato cha Tano na cha Sita (A level) na kukubali kusomea diploma ya Ualimu ili wakawafundishe watoto wa masikini wenzao. Wanafunzi hawa hawakuanzisha wao program hii, ilianzishwa na Serikali na kupitishwa na Baraza la Mawaziri ambalo Rais Magufuli alikuwa mjumbe na alishiriki kikao hicho kwa mujibu wa kumbukumbu za Baraza la Mawaziri.

Rais Magufuli hakupinga mpango huu na aliubariki kama Wenzake walivyofanya na kuanza kutekelezwa. Lengo na program hii ni kuondoa tatizo la walimu wa masomo ya Sayansi. Tanzania ina uhaba wa walimu wa Sayansi 26,000 (Kwa Utafiti wa Mwaka 2014) na tukienda kwa utaratibu wa kawaida tutahitaji miaka 20 kuziba pengo hilo.

Program hii ilianzishwa ili kuziba pengo hili kwa muda mfupi, na vijana waliitikia wito huu wa kizalendo kuhakikisha wadogo zao hawakosi walimu siku za usoni. Serikali ya awamu ya Tano imewafukuza vijana hawa 7800 kutoka chuoni ndani ya masaa 24 kwa makosa ambayo sio yao.

Wananchi, hatusemi kuwa program haikuwa na kosoro. Zilikuwepo ikiwemo kudahili wanafunzi wengi zaidi ya ilivyotarajiwa na kudahili wanafunzi 88 kati ya 7800 ambao walikuwa na daraja la nne (Div 4) katika masomo yao. Lakini aliyedahili sio watoto hawa bali ni Serikali yenyewe, kwanini waadhibiwe watoto?

Bunge lilipotaka kujadili hoja hii au hata kuipeleka kwenye kamati ya Bunge kuifanyia uchunguzi na kutoa mapendekezo Naibu Spika alizuia hoja ya mbunge Joshua Nasari bila sababu za msingi. Wabunge wote bila kujali vyama vyao walitaka hoja ijadiliwe na kuweza kupata majawabu. Mbona wakati wa Uongozi wa awamu ya 4 tulijadili hoja ya mgomo wa madaktari na kisha kupelekwa kwenye kamati ya husika ya bunge kupata suluhisho la kudumu? Kwanini Utawala wa Rais Magufuli hautaki Bunge lifanye kazi yake? Mbona yeye Rais kaenda kujadili jambo hilo huko Chuo Kikuu mlimani?

Wananchi, Rais Magufuli anafikia kuita watoto wetu Vilaza? Rais huyu anayesema yeye ni Rais wa masikini anaita watoto wa masikini Vilaza. Vijana hawa Wazalendo waliojitoa muhanga kuacha kwenda kidato cha Tano ili wasome kuwa Walimu na kulea kizazi kijacho Rais wao anawaita vilaza. Rais sifa zimempanda kichwani. Rais Magufuli hana budi kuwaomba radhi vijana hawa na wazazi wao.

Kitaaluma Rais ni Mwalimu, anajua madhara ya kisaikolojia kufuatia maneno aliyoyasema. Ni sawa na Jenerali wa Jeshi anayetukana askari wake walio Mstari wa mbele. Hata Baba wa Taifa hakuthubutu kamwe kuita wanafunzi Vilaza hata kama walimuudhi kiasi gani.

Rais Magufuli anaongea mno, sio sawa kwa Kiongozi. Rais ajue kuweka akiba ya maneno. Yeye ni Kiongozi wa wote, wenye akili na Vilaza. Yeye anapaswa kuwa wa mwisho kuongea ili watu waweze Kukata rufaa kwake. Yeye akishaongea wananchi ‘aggrieved’ (walioonewa Au kukosewa) waende kwa nani? Waende kwa mungu?

Tunamtaka Rais awarudishe wanafunzi Hawa Chuoni mara moja na wale wanafunzi ambao itaonekana hawakuingia kwenye programu kihalali (ambao Ni 88 Tu) waondolewe badala ya kuadhibu watoto wote kwa makosa ya wachache ambao ni asilimia 5 tu ya wote. Makosa madogo ni mambo ya kawaida katika Jamii. Yeye Rais ni mfano mzuri wa hili kwani naye mbona aliteua Waziri mlevi na kurekebisha kwa kumfukuza peke yake?, mbona hakufukuza Baraza zima la mawaziri kwa ulevi wa Waziri mmoja?

Zanzibar

Ndugu Wananchi mnajua mara baada ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar kufutwa chama chetu kiliweka msimamo wa wazi kwamba kinatambua ushindi wa Maalim Seif Sharif Hamad kama Rais aliyechaguliwa na Wazanzibari na anayepaswa kula kiapo na kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Tuliandika pia masuala 10 muhimu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuyafanyia kazi, na moja ya jambo tulilomtaka Rais Magufuli Kulifanyia kazi ni suala la demokrasia ya Zanzibar. Rais hakusikia wito wetu na aliruhusu ufutwaji usio halali, kisiasa wala kisheria wa uchaguzi mkuu wa Zanzibar wa Oktoba 25, 2015.

Tunarudia kusisitiza kuwa Chama chetu cha ACT Wazalendo hakiutambui uchaguzi wa marudio wa Zanzibar uliofanyika mwezi Machi mwaka 2016 pamoja na matokeo yake yote. Kwa maana hiyo hatutambui Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, Baraza la Mawaziri la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, na Pia Rais wa Zanzibar.

Wananchi, Hivi karibuni kumekuwa na kuongezeka kwa sintofahamu huko Zanzibar kufuatia Mgombea Urais aliyeshinda na kunyanganywa ushindi wake kwenda kwa wananchi kuzungumza nao. Hali hii imepelekea jeshi la polisi kumhoji Maalim Seif na siku mbili baadaye Dkt. Shein kutamka kuwa hamwogopi Maalim Seif kwa sababu "Hana vifaru na mizinga".

Tunalaani kauli hii ya Dkt. Shein ya kutisha kwa vifaru na mizinga. Kamwe huwezi kuzima haki za Wananchi kwa vifaru na mizinga. Dkt Shein akumbuke kuwa Sultan alikuwa na jeshi, vifaru na mizinga na ulinzi wa Dola kubwa kama Uingereza lakini aliangushwa na wananchi wa Zanzibar mwaka 1964.

Dkt Shein akumbuke kuwa nchi kadhaa duniani zilikuwa na madikteta wenye vifaru na mizinga lakini waliondoka. Dkt Shein afute kauli yake hii na kuacha vitisho badala yake aanze mchakato wa kupata maridhiano ya jamii ya Zanzibar. Hatutaki kurithi damu, tunataka kurithi nchi yenye amani, haki na demokrasia.

Wananchi, sisi ACT Wazalendo, tunajua hali mbaya ya kisiasa iliyopo Zanzibar na mkwamo uliopo hivi sasa Kisiasa, Kijamii na Kiuchumi. Hata hivyo ni lazima tupate jawabu kupitia sanduku la kura. Tunapendekeza kuwa Vyama vikuu vya siasa Zanzibar vikubali ‘kufa kidogo’ yaani ‘to die a little’, kwa vyote kukubali kuwa Chaguzi zote Mbili, wa Mwaka 2015 na ule wa mwaka 2016 zilikuwa batili, zifutwe na Uchaguzi Mkuu mpya uitishwe.

Uchaguzi huo utanguliwe na Serikali ya Mpito itakayohusisha vyama vyote vya siasa na baadhi ya wanajamii wanaoheshimika na Wazanzibari wote ili kujenga kuaminiana. Tunadhani hii itatupa nusra kwa Zanzibar. Tunawaomba Wazanzibari watumie mwezi mtukufu wa Ramadhani kutafakari maoni haya na wote kwa pamoja baada ya Ramadhani kuja na jawabu ya hali ya kisiasa. Tunatamani Zanzibari irudi kwenye hali ya kawaida na ishamiri. Zanzibar ikiingia kwenye mtafuruku Tanzania nzima itakuwa kwenye mtafaruku. Ni dhahiri kuwa Rais Magufuli ameshindwa kutoa uongozi kwenye suala hili na hivyo ni wajibu wa Wazanzibari wenyewe kukaa na kupata mwafaka wa kijamii na kusonga mbele.

Bajeti ya 2016/17

Wananchi, kuanzia tarehe 8 mwezi Juni, 2016 Bunge litakuwa kwenye mjadala wa Bajeti ya kwanza ya Serikali ya Rais Magufuli. Rais ameleta mapendekezo ya Bajeti ya shilingi 29.5 trilioni. Katika makadirio haya vyanzo vya ndani ni shilingi 18.5 trilioni na misaada ni shilingi 3.6 trilioni. Serikali inatarajiwa kukopa jumla ya shilingi 7.4 trilioni.

Mwaka 2015/16 Serikali ilitarajiwa kukusanya jumla ya shilingi 13.8 trilioni, hivyo ndani ya mwaka mmoja wa fedha Utawala wa Rais Magufuli unataka kukusanya shilingi 4.7 trilioni zaidi sawa na ongezeko la asilimia 25. Kwa ufupi ni kwamba Serikali haina budi kuongeza kodi kwa kiwango cha asilimia 25 ili kuweza kutimiza malengo yake ya makusanyo.

Wananchi, mtakumbuka kuwa mara baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani tulikuwa tunaelezwa kodi iliyokusanywa kila mwezi na tuliona wafanyabiashara wakikabwa koo kwa kukwepa kodi. Hata hivyo ongezeko la Makusanyo lilikuwa kwa miezi 2 tu ya Novemba na Disemba kwani kuanzia mwezi Janauri makusanyo yalianza kuendana na hali halisi ya uchumi wa nchi yetu na ndio maana mbwembwe za makusanyo hazisikiki tena hapa nchini.

Ukweli ni kwamba Rais alikuwa anakusanya ‘arrears’ na hapakuwa na hapajakuwa na mbinu mpya za kukusanya mapato ya Serikali. Maeneo muhimu yanayopoteza mapato kama vile makampuni ya nje kutumia mbinu za kihasibu kukwepa kodi hayajatazamwa kabisa na Rais na wasaidizi wake.

Hivyo, Serikali imeamua kurudi kwa wanyonge kuwaminya na kodi ikianzia kuchukua kodi zote za Majengo kutoka kwenye Halmashauri zetu. Kodi za majengo ndio chanzo kikuu cha mapato ya Halmashauri zetu za Miji, Manispaa na Majiji. Uamuzi wa Serikali kuchukua chanzo hiki cha mapato utapelekea Halmashauri zetu kushindwa kuzoa taka na hata kutoa huduma kwa wananchi.

Hata hivyo wananchi uamuzi huu ni kwa sababu Halmashauri nyingi za Miji zinaongozwa na vyama vya Upinzani kama vile Manispaa ya Kigoma Ujiji, Manispaa ya Iringa, Arusha jiji, Ilala, Kinondoni, Mbeya Jiji nk. Utawala wa Rais Magufuli unataka kuhakikisha kuwa Manispaa zinaoongozwa na vyama vya upinzani zinashindwa kutoa huduma. Duniani kote kodi za majengo hukusanywa na Serikali za Mitaa. Katika Bajeti ya mwaka huu kodi hizi zitaongezwa maradufu.

Wananchi, Serikali inatarajia kupandisha ushuru kwenye soda, vilevi na sigara pia kwa mujibu wa vitabu vya Bajeti vilivyogawiwa kwa wabunge. Hata kodi kwenye gharama za kupiga simu zitaongezwa kwa zaidi ya asilimia 10. Eneo la ushuru peke yake Serikali inataka kukusanya shilingi 1.2 trilioni kutoka shilingi bilioni 900 za mwaka uliopita. Hii ni nyongeza ya shilingi 300 bilioni zaidi kutoka Bajeti ya mwaka 2015/16.

Maeneo haya mawili peke yake (kodi za majengo na ushuru wa bidhaa) yataongezewa kodi kiwango cha kuumiza sana wananchi wa kawaida. Hii ndio sababu Serikali imefukuza baadhi ya wabunge mahiri bungeni ili kulainisha upitishwaji wao wa viwango hivi vya kodi. Hata hivyo tutatumia wabunge waliobakia Bungeni kuhakikisha kuwa kodi kwa wananchi masikini haziongezwi kiholela.

Wananchi, sisi tunaamini kuwa Bajeti ya shilingi 29.5 trilioni ya Utawala wa Magufuli sio bajeti halisi kwani makadirio yao hayazingatii ukuaji wa uchumi na yana lengo la kuchukua fedha kutoka kwa wananchi kupeleka Serikali jambo ambalo litadidimiza uchumi wa nchi yetu.

Tishio la Demokrasia

Wananchi jambo la mwisho ambalo ninataka kuwaeleza ni tishio lililopo mbele yetu dhidi ya demokrasia ya vyama vingi. Hatua mbalimbali ambazo Utawala wa Rais Magufuli unachukua ni ishara ya kutengeneza utawala wa Kiimla. Rais ndiye anayejua kila kitu na ndiye anayeamua kila kitu. Hii ni hatari sana kwa nchi yetu na ni lazima kuchukua hatua mahususi kumkatalia Rais mwanzoni kabisa ili asizoee.

Tunarudia kuwa tulimuunga mkono Rais toka mwanzo katika vita dhidi ya Ufisadi, kwani ni vita muhimu na lazima ipiganwe bila kujali itikadi za vyama. Hakuna namna unaweza kumlaumu Rais anapochukua hatua za kusafisha Uvundo katika nchi. Tutaendelea kumwunga mkono katika eneo hilo.

Wananchi, hata hivyo Rais anatia Khofu mno katika ujenzi wa mfumo wa uwajibikaji. Tanzania ina vyombo vya kuimarisha uwajibikaji, ikiwemo Bunge la Jamhuri ya Muungano na Pia Ofisi ya Ukaguzi ya Taifa. Rais anataka kupigana dhidi ya ufisadi nje ya mfumo jambo ambalo ni la hatari sana kwa nchi kwani akitoka yeye tutaanza upya.

Inawezekanaje Kiongozi anayepambana na rushwa akavunja nguvu ofisi ya ukaguzi ya Taifa kwa kumnyima Bajeti Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG)? Rais amediriki hata kuvunja Katiba na sheria ya ukaguzi, kwani Bajeti ya CAG haipangwi na Serikali bali hupangwa na Kamati ya Bunge. Rais ameenda kinyume na sheria na badala yake kapanga mwenyewe Bajeti ya CAG? Toka lini mkaguliwa akapanga bajeti ya anayemkagua? Kamati ya Bunge ilipanga Bajeti ya tshs 69 bilioni kwa CAG lakini Serikali (mkaguliwa) imeipiga panga mpaka tshs 32 bilioni. Hii ni moja ya mfano dhahiri kabisa wa Serikali kuanza kuvunjavunja vyombo vya uwajibikaji.

Wananchi, hivi sasa kuna Ukosefu wa Sukari nchini. Rais alisimama kwenye Vilinge vya Siasa, akatoa matamko makali kwamba kuna Wafanyabiasha wameficha sukari na tukaonyeshwa sukari hiyo. Hata hivyo baada ya siku chache vyombo kama PCCB na TRA vikasema sukari ile ni halali. Inakuwaje Rais alitamka maneno yale bila ya kushauriana na vyombo? Ni dhahiri Rais anaongea na kuropoka tu na kutaka kujenga utawala wa Kimla. Leo bado kuna shida ya sukari na sukari ambayo serikali inasema iliagiza haionekani. Ipo wapi?

Wananchi, Rais Huyu Huyu alikwenda Benki Kuu na kusema nusu ya wafanyakazi pale ni hewa. Mpaka leo hatujaona hao wafanyakazi hewa wa BoT. Rais alikwenda tu kwa kupata maneno ya kuokoteza barabarani na kutoa matamko ambayo yanashusha hadhi ya Benki, lakini Rais anashindwa kutoka mbele kusema alikosea. Tunajenga mfumo mbaya sana wa uongozi wa Nchi.

Leo tunataka kumwambia Rais kuwa aongoze, asitawale. Rais awe na Utu na wananchi wake. Rais awe anasikiliza kwanza na kuchambua mambo kabla ya kusema chochote mbele ya hadhara. Rais awe wa mwisho kusema ili kama kuna rufaa Watu waseme kwake. Vinginevyo Rais anataka kujenga utawala wa Kiimla, tutamkatalia wazi wazi.

Wananchi, nimalizie kwa kusema yafuatayo. Rais John Magufuli amesema kuwa yeye amejitoa muhanga kupambana na ufisadi. Sisi tunalazimika kujitoa muhanga Kulinda Demokrasia.

Ni imani yetu kuwa Ufisadi utapigwa vita kikamilifu sio kwa kutegemea nia ya mtu mmoja bali kwa kuboresha na kutumia misingi ya demokrasia kwa kujenga taasisi madhubuti zitakazomaliza janga la ufisadi bila ya kutegemea nia ya Rais.

Sisi tunaamini kuwa ni jukumu letu kusimama kujitoa mhanga kuzuia maafa ya kitaifa yatakayoweza kutokea kutokana na makosa ya kukandamiza demokrasia na uhuru wa mawazo kwa kuhoji, kukosoa na kurekebisha makosa hayo sasa bila kuchelewa.

Tunamwunga mkono Rais kutokomeza Ufisadi lakini TUNAMPINGA Rais Kutokomeza Demokrasia. Demokrasia yenye misingi madhubuti ya Uwajibikaji ndio jawabu sahihi dhidi ya ufisadi na unyonyaji nchini kwetu.

Nawashukuru sana.

Zitto Ruyagwa Kabwe

Dar es Salaam

Juni 5, 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya June 6, Ikiwemo ya Bosi CBRT Kutafuna Mabilioni ya Serikali

$
0
0



Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya June 6, Ikiwemo ya Bosi CBRT Kutafuna Mabilioni ya Serikali

CUF: Prof. Ibrahimu Lipumba Unaweza Kugombea Uenyekiti wa Chama.

$
0
0
Chama cha wananchi CUF kimesema kuwa, aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho Prof Ibrahimu Lipumba, anaweza akagombea tena uenyekiti wa chama hicho kwani ana uwezo mkubwa. Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu wa CUF-Bara alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Uchaguzi utafanyika 21 August 2016

Diamond Aongeza Nyumba nyingine

$
0
0
Yeye anapenda kuviita vibanda,leo tena amekamilisha manunuzi ya nyumba nyingine maeneo ya kunduchi kupitia Dalali mwanamkee.....Naona Diamond kila akimsainisha msanii katika lebo yake laZima aongeze na nyumba

Je kuna haja ya kumchukia Diamond kama wengine wapo bize kubadiri mademu yeye yupo bize na nyumba
Viewing all 104796 articles
Browse latest View live




Latest Images