Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Jinsi Ya Kumwacha Mpenzi Wako Kwa Amani.....

$
0
0
Ziko njia mbili tu ambazo uhusiano baina ya wapenzi wawili utaandika historia. Ama uhusiano utadumu hadi kifo kiwatenganishe ama utavunjika. Hata hivyo uzoefu unaonyesha kuwa kwa walio wengi hawajaweza kuwa kwenye uhusiano wa kudumu, wanakuwa wamepitia katika mahusiano mengine na hivyo kupitia awamu Fulani Fulani za kuvunja mahusiano.Na kuna namna mbili ambazo uhusiano utavunjika. Ama kwa amani ama kwa ugomvi.


Kumaliza mahusiano si kitu rahisi sana hata kama ni hakika umemchoka mwenzi wako na hata kama uhusiano wenu si mzuri kiasi kwamba uko tayari kuwa huru. Kwa hiyo basi, kuvunja mahusiano ya kimapenzi ni jambo ambalo haliwezi kuepukika. Hata hivyo kumaliza mahusiano kwa amani ni vizuri na inapendeza kuliko kuumaliza kwa ugomvi na jazba. Kumbuka "The Golden Rule": Kwamba ungekuwa ni wewe ungependa uachwe vipi? Kama upo katika mahusiano yasiyo na tija na unafikiri kwamba imefika wakati unahitaji uhusiano wenu uvunjike, basi dondoo zifuatazo zitakusaidia kumaliza mahusiano na mpenzi wako kwa amani. Kitu kimoja kikubwa cha kuzingatia ni kuweka Jazba pembeni:


1. Kuwa Na Uhakika Na Unachotaka Kufanya: Kama huna uhakika juu ya hisia zako kwa mwenzi wako unapotaka kuvunja uhusiano bora usifanye hivyo maana utafanya moyo wako usiwe na maamuzi dhabiti aka "Maamuzi magumu". Kama una hisia naye pia itamfanya achanganyikiwe na ajisikie kuwa bado anayo nafasi ya kuwa na wewe ama anaweza akaamua na yeye kukukomoa na kukuacha kabisa wakati kumbe bado una hisia za mapenzi na yeye . Hata hivyo kama una uhakika kwamba ni kweli hauutaki uhusiano uliopo basi kuwa tayari kukata kabisa mahusiano yenu la sivyo kuwa tayari kukiona cha moto . . . maana utakuwa unachezea hisia zako.

2. Fikiria Sababu za Kuvunja Uhusiano: Uhusiano unapovunjika mara nyingi ndugu, jamaa na marafiki wanapenda kujua sababu. Unapojua sababu zinazopelekea wewe kuvunja mahusiano itakusaidia kutoa majibu ya uaminifu pale unapoulizwa. Pia itakusaidia kumaliza mahusiano katika namna njema. Hata kama mwenzi wako hataamini au ataamini juu ya kuvunjika kwa uhusiano wenu, kuwa honest au mkweli ni muhimu. Mweleze unahitaji kusonga mbele na maisha yako bila yeye na mjibu maswali yote kwa uaminifu. (Fikiria huko nyuma kama uliwahi kuachwa bila sababu ulivyojisikia)

3. Maliza Mahusiano Wewe Binafsi: Kama umekuwa na mpenzi wako kwa muda mrefu au kuipindi chochote ambacho uliwekeza muda na nguvu zako za kujenga mapenzi, basi ni busara mahusiano hayo yakamalizwa na mwenyewe binafsi. Usitumie njia yoyote ile zaidi ya wewe mwenyewe, usitumie SMS, usitumie IM "Chat", usitumie simu au email au barua au mtu yeyote kufikisha ujumbe. Ukitaka kumaliza mahusiano kwa amani, tafuta muda wa kukaa na mwenzi wako in person au face to face ili kuumaliza uhusiano huo katika hali njema.


4. Chagua Mahali Panapofaa. Mahali pazuri panapofaa ni pale ambapo wewe unayetaka kumwacha mwenzako ungekuwa wewe unaachwa ungependa iwe mahali gani ili uelezwe? Be on his/her shoes. Public Places si mahali pazuri sana kwani mwenzi wako anaweza kujisikia kadhalilishwa. Kama ukiweza chagua mahali patakapomfanya mwenzi wako awe confortable na kurelax kama yuko nyumbani kwake.

Angalizo: Kama una uhakika kuwa mwenzi wako anaweza kuleta ukorofi, basi chagua Public Place kama kwenye restaurant ambapo wapo watu wengine. Hii itasaidia kuondoa uwezekano wa kuleta vurugu. Public Place patakufanya ujiamini. Pale mambo yatakapochachamaa unaweza kuondoka tu bila tishio la ugomvi kwa kuwa kuna watu. Ukiona hali si shwari ni vema uanze kuondoka wewe kuliko yeye kuondoka kwanza.


5. Msikilize Mwenzi Wako: Hata kama umeshaamua huwezi kubadili mawazo juu ya kuvunja mahusiano yenu haina maana kuwa usimsikilize mwenzi wako. Kumsikiliza mwenzi wako kutamfanya mwenzi wako atoe yote aliyokuwa nayo moyoni kitu ambacho kwa uhakika kitasaidia kumaliza mahusiano kwa amani. Pia unaweza kujifunza baadhi ya mambo ambayo yatakusaidia katika mahusiano yako yanayofuata.


6. Kuwa Mpole Na Dhibiti Hisia Zako: Moja ya sababu kubwa ya mahusiano kuvunjika ni pamoja na wahusika wote kutokuwa na furaha na amani na mwenzi wako. Wakati wa kuvunja mahusiano hayo pia yanaweza kujitokeza hasa pale mtakapoanza kulaumiana na kuonyeshana vidole ni nani mwenye makosa. Hakikikisha unadhibiti hasira hisia zako na hasira hata kama anachoongelea mwenzio kitakutia hasira. Ukifanya hivyo utafanikisha kuwa na mazungumzo ya amani.


7. Kuwa Mtulivu na Makini: Unahitaji kuumaliza uhusiano na kuondoka mahali mlipo. Hata hivyo ni busara kuwa mtaratibu na mpole. Kama kuvunjika kwa uhusiano wenu kutakuja kama Suprize kwa mwenzio, basi bila ya shaka atahitaji muda wa kuyameza unayomwambia, kuyatafakari ili aende sambamba na wewe katika mazungumzo yenu. Inaweza ikawa si habari njema kwa mwenzi wako kwa hiyo utulivu wako na upole katika maongezi yenu kutamfanya apunguze maumivu.


8. Mkimaliza Maongezi Ondoka Haraka: Iko hivi: Kwa kiasi kikubwa anayeachwa anaweza kuwa alikuwa hajui kuwa ataachwa kwa hiyo hatakuwa na furaha kwa yeye kuachwa. Anaweza akakulaani sana na kukuita majina yote mabaya anayoyajua na hivyo kukufanya na wewe uwe na hasira. Tulia. Jizuie. Kwa kuwa umeshaongea na pia umemsikiliza kistaarabu, huna haja ya kuendekeza ugomvi au malumbano. Ondoka. Hakuna faida utakayoipata kwa kuendelea kutoa maelezo yoyote ya ziada. Kama ni mwelewa na mmemaliza maongezi kwa amani basi mwage na nenda zako.


Je, ni nini uzoefu wako kuhusu kuacha au kuachwa katika mahusiano mbalimbali uliyopitia? Na je, kuna lolote la kujifunza?

Manji na Sanga Wapeta Uchaguzi Yanga

$
0
0
Matokeo ya awali yanaonyesha kuwa Mwenyekiti wa Yanga anayetetea nafasi yake, Yusuph Manji anaongoza kwa kura 1,468, na hakuna zilizomkataa, huku mbili zikiharibika.

 Akizungumzia uchaguzi huo ambao kura zimeendelea kuhesabiwa hadi asubuhi ya leo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha klabu hiyo, Jerry Muro amesema Clemence Sanga anaongoza katika nafasi ya Makamu mwenyekiti kwa kujikusanyia kura 1,428 dhidi ya mpinzani wake, Tito Osoro aliyekuwa amepata kura 80.

 Hadi taarifa hizi zinapatikana kutoka Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam, klabu hiyo ilikuwa inaendelea na mchakato wa kuhesabu kura za wajumbe.Hata hivyo, Muro amesema matokeo kamili yatatolewa leo.

Mwanamuziki 2 Face Ampa Shavu Vanessa Mdee....

$
0
0
MWANAMUZIKI mwenye jina kubwa Afrika, 2 Face Idebia amempa shavu la mwaliko diva anayekimbiza kwenye Tasnia ya Muziki Bongo, Vanessa Mdee ‘V Money’ kwenye tamasha lake litakalofanyika leo jijini Nairobi, Kenya huku wasanii mbalimbali kutoka kila kona ya Afrika wakitarajia kufanya makamuziki ya ukweli.

Akizungumza na gazeti hili, V-Money anayetamba na Wimbo wa Niroge kwa sasa amesema shavu hilo kwake ni kitu kizuri maana kimeonesha ni jinsi gani wasanii wa nje wanavyothamini kazi zake hata kuamua kumpa mwaliko ambao mbali na kutangaza ngoma yake ya Niroge atapata fursa ya kukutana na wasanii wengi ambao anaweza kupata wa kufanya nao kazi.

“Namshukuru Mungu kazi zangu zinaheshimika, mwaliko wa 2 Face ni muhimu kwangu na nimeuchukulia kwa uzito kutokana na tamasha lenyewe litakavyokuwa kubwa, nina uhakika sitaondoka bure, lazima nitapata lolote la kufanya kwa mashabiki wangu,” alisema V- Money.

Watumishi 12,246 Waondolewa Kwenye Mfumo wa Malipo ya Mishahara Serikalini

$
0
0
WATUMISHI 12,246 wameondolewa kwenye mfumo wa malipo ya mishahara kwa sababu mbalimbali, ikiwemo umri wa kustaafu kwa lazima, kufukuzwa kazi, vifo na kumalizika kwa mikataba.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora), Angela Kairuki alisema kuondolewa kwa watumishi hao kumeokoa Sh bilioni 25 ambazo zingelipwa kwa watumishi hao.

Alisema kuwa fedha hizo zingepotea endapo watumishi wasingeondolewa kwenye mfumo, ikilinganishwa na watumishi 10, 295 walioondolewa kwenye mfumo kuanzia Machi 15 hadi Aprili 30 mwaka huu.

“Jumla ya Sh bilioni 23.2 ziliokolewa kwa kipindi cha Machi 15 hadi Aprili 30 mwaka huu baada ya Rais John Magufuli kutoa maagizo ya kuwaondoa watumishi hao kwenye malipo,” alisema Kairuki. Alisema pia kuwa watumishi hewa 1,951 wameongezeka ikiwa ni pamoja na Sh bilioni 1.8.

Alifafanua kuwa ofisi hiyo ilitoa maelekezo kwa Makatibu Wakuu, Wakuu wa taasisi za umma na Mamlaka za Serikali za Mitaa, kuwasilisha taarifa ya watumishi hewa ifikapo juzi (Juni 10 mwaka huu).

Alisema kuwa walielekeza taarifa zibainishe majina, namba za hundi za watumishi hewa, tarehe walizotakiwa kuondolewa kwenye mfumo, kiasi cha fedha kilichopotea na kilichookolewa.

Akizungumzia maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, Waziri huyo alisema kuwa maadhimisho ya mwaka huu yatakuwa na dhana ya mchango wa watumishi wa umma katika uchumi.

Kidumu Asema Wakenya Wanadhani yeye ni Mtanzania, Azungumzia Kolabo Mpya na Wasanii TZ

$
0
0
Mwanamuziki kutoka nchini Burundi, Kidumu, amefunguka kwa kusema kuwa Wakenya wengi wanadhani kwamba yeye ni Mtanzania kutokana na kuonyesha uwezo mkubwa wakuimba kwa lugha ya Kiswahili.

Muimbaji huyo ambaye aliwahi kufanya kazi na Lady Jaydee, ameiambia BBC Ijumaa hii kuwa yeye ni Mburundi lakini kuwa karibu na Watanzania kumemfanya aonekane na yeye ni Mtanzania.

“Tanzania ni nyumbani pia, nilikuwa nikienda Tanzania kila mwisho wa mwezi, hata Wakenya wengi wanadhani mimi ni mtu wa Tanzania, walikujakujua baadae kama mimi ni Mburundi, lakini kwa sababu ya Kiswahili changu bado wanasema mimi ni Mtanzania” alisema Kidumu.

Pia muimbaji huyo alizungumzia mpango mpya wa kufanya kazi na wasanii wa Tanzania.

“Mpango upo kwa sababu nilishauanza, niliimba na Lady Jaydee, niliimba na Msechu wote ni Watanzania, na bado na mpango wa kufanya kolabo zaidi,” alisema Kidumu.

Breaking News:Uongozi Mpya Wa Yanga Watangazwa Baada Ya Kura Zote Kuhesabiwa, Mwenyekiti ni Yusuf Manji, Makamu wake ni Clement Sanga

$
0
0
Yusuf Manji ameshinda nafasi ya uenyekiti wa Yanga kiulaini kutokana na kutokuwa na mpinzani kwenye nafasi hiyo hivyo kupita bila kupingwa kwenye nafasi ambayo alikuwa akiitetea.

Clemen Sanga nae amepenya katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti kwa kumbwaga mpinzani wake Titus Osoro.

Shughuli pevu ilikuwa kwa wagombea nafasi ya ujumbe ambapo jumla ya wagombea 20 walikuwa wakiwania nafasi 8 za ujumbe.

Mwenyekiti
Yusuf Manji ameibuka mshindi wa nafasi ya uenyekiti akipenya bila kupingwa na kupata idadi ya kura 1468 zilizopigwa na wanachama, huku kura 2 pekee zikiwa zimeharibika.

Makamu Mwenyekiti
Clement Sanga amemgaragaza mpinzani wake baada ya kupata kura 1428 wakati mpinzani wake Titus Osoro akiambulia kura 80 pekee.

Wajumbe
Ayoub Nyenzi (889), Salim Mkemi (894), Bakar Malima (577), Godfrey Mheluka (430), David Ruhago (582), Lameck Nyambaya (655), Sylvester Haule (197), Pascal Laizer (178), Samwel Lukumay (818), Hashim Abdallah (727), George Manyama (249), Hussein Nyika (770), Siza Lyimo (1027), Beda Tindwa (452),Tobias Lingalangala (889), Athumani Kihamia (558), Mchafu Chakoma (69), Edgar W  Chibura (72), Ramadhani M. Kampira (182), Omary S. Amei (1069)

Kwa Matokeo hayo, uongozi mpya wa Yanga uliochaguliwa na wanachama unaundwa na Mwenyekiti Yusuf Manji, Makamu Mwenyekiti Clement Sanga huku wajumbe wakiwa ni Omary S. Amei, Siza Lyimo, Salim Mkemi, Tobias Lingalangala, Ayoub Nyenzi, Samwel Lukumay, Hussein Nyika na Hashim Abdallah

Wapinzani Wataka Wabunge wa CCM Wasioongea Bungeni Nao Wanyimwe Posho

$
0
0
KAMBI Rasmi ya Upinzani Bungeni, imelitaka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwafutia posho wabunge wa CCM  wanaofika kwenye vikao vya Bunge hilo na kukaa kimya bila kuchangia jambo lolote hata kwa maandishi kwa maelezo kuwa hawafanyi kazi.

Msemaji Mkuu wa Kambi hiyo, ambaye ni Mbunge wa Momba, David Silinde (Chadema), alitoa pendekezo hilo jana bungeni mjini hapa muda mfupi kabla ya kuwasilisha maoni ya Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni, kuhusu hotuba ya Mapendekezo ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali katika mwaka wa Fedha 2016/17.

Hotuba hiyo ya Bajeti iliwasilishwa bungeni Juni 8, mwaka huu na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango. Silinde alisema;

“Kabla ya kutoa maoni ya Kambi ya Upinzani, ninaomba niweke sawa taarifa zinazopotoshwa na kiti cha Naibu Spika kuhusu posho na kueleza kuwa sisi ndio kila wakati tumetaka posho ziondolewe na kupelekwa kwenye shughuli za maendeleo, lakini Serikali imekuwa ikisuasua kutekeleza jambo hilo.”

Kwa mujibu wa Silinde, suala kwao sio posho kwa sababu hata wakati wa Bunge la Katiba kila Mbunge wa upinzani aliacha Sh milioni 30.

Akizungumzia wabunge wa CCM wakaa kimya, Silinde alisema wapo na wanapokea posho kama kawaida ilhali hakuna kazi yoyote wanayoifanya na kwamba umefika wakati sasa Bunge liongeze umakini zaidi kwa kuwadhibiti wabunge wa aina hiyo kwa kuwakata posho za vikao.

Alipendekeza kuwa Hansard (kitabu cha taarifa rasmi za Bunge) zitumike kuwabaini kwa sababu wapo na wanajulikana.

Hata hivyo, kabla ya kueleza suala hili, Silinde alivunja utaratibu kwa kumtaja Naibu Spika kwa jina ‘Kiti cha Spika’ badala ya Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lililosababisha alazimishwe kutumia busara kuheshimu kiti hicho na hatimaye kutii.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu), Jenister Mhagama, ndiye aliyesimama kuomba mtoa hoja (Silinde), aheshimu utaratibu wa Bunge hilo.

Quick Racka Afunguka Haya Kuhusu Yeye na Kajala

$
0
0

Mkali wa Bongo fleva Quick Racka amefunguka juu ya uhusiano wake na msanii wa Bongo muvi Kajala Masanja.

Akizungumza na Enewz Quick Racka alisema kuwa yeye na bongo muvi star huyo ni washikaji wa karibu sana na urafiki wao una miaka miwili sasa, huku kila mtu akiwa na kazi zake.

“Tunashauriana yaani kama washikaji na nampenda kama mshikaji wangu kama hamuelewi hata picha hamuoni”,alisema Quick Racka huku akiongezea kuwa kwasasa studio yao ya switch inafanya kazi ya kumsimamisha producer wao Rufe ajulikane ndipo watakaporudi kujihusisha na msanii mmoja mmoja”, alisema Quick Rocka.

Rapper Quick Rocka ambaye kwa sasa anafanya kazi na Switch Records, pia ameelezea mipango yake ya kufanya muziki wa aina tofauti tofuti, huku tetesi zikisema sasa anataka kufanya muziki wa bolingo

Wanafunzi 316 Waliofukuzwa Chuo Kikuu cha St. Joseph Wafungua Kesi Mahakamani

$
0
0
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetoa kibali cha kufungua kesi ya uwakilishi, kwa wanafunzi wanne, waliofukuzwa katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph kwa madai ya kutokuwa na sifa za kudahiliwa kwenye vyuo vikuu.

Jaji Eliezer Feleshi alitoa kibali hicho baada ya wanafunzi hao kuwasilisha maombi ya kibali cha kuwakilisha wenzao mahakamani pamoja na kusitisha masomo wakati kesi ya msingi ikiendelea kusikilizwa.

Wanafunzi hao, walisimamishwa masomo baada ya kutolewa amri ya Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Joyce Ndalichako kwamba kutokana na tatizo la ufundishaji wa Stashahada ya Elimu (Sayansi, Hisabati na Teknolojia) wanafunzi wote wanatakiwa kurejea nyumbani.

Akiwasilisha maombi ya wanafunzi hao, Wakili Emmanuel Muga aliomba wanafunzi 316 waliofukuzwa chuo, wapewe kibali cha kufungua kesi ya uwakilishi pia Mahakama itoe amri ya kusitisha masomo wakati wa usikilizwaji wa kesi.

Akitoa uamuzi, Jaji Feleshi alisema Mahakama imekubali ombi hilo, isipokuwa la kusimamishwa masomo wanafunzi wote na kufafanua kuwa “masomo yataendelea kusimama kwa wanafunzi 316 waliosimamishwa”.

Aidha alisema wanafunzi hao wanatakiwa kuwa na wawakilishi wanne tu, badala ya 316, kwa sababu idadi yao ni kubwa. Baada ya uamuzi huo, Wakili Muga aliwataja wanafunzi wanne watakaowawakilisha wenzao mahakamani hapo kuwa ni Innocent Peter, Ramadhan Kipenya, Oswald Mwinuka na Faith Kyando.

Jaji Feleshi alisema Mahakama imetoa kibali na itapanga tarehe ya kusikilizwa kwa kesi baada ya walalamikaji hao kufungua kesi yao. 

Katika madai yao, wanafunzi hao wanadai fidia ya miaka mitatu waliyokaa chuoni hapo dhidi ya Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) iliyowakilishwa na Wakili Rose Lwita na Judith Misokia na Chuo cha Mtakatifu Joseph, kikiwakilishwa na wakili Jeromah Msemwa.

Nisha na Wolper Wavutana, Kisa Viserengeti Boys vya Bongo Flava...

$
0
0
Mastaa wa bongo muvi, Salma Jabu ‘Nisha’ na Jacqueline  Wolper wamejikuta wakivutana mtandaoni baada ya Nisha kuandijka kitu ambacho Wolper alijibu na kusababisha Nisha kuibuka tena na kutoa ufafanuzi.

Nisha aliandika haya; kwenye hicha hii
“Mmoja kati ya hawa amejaa kwenye galary ya simu yangu na moyoni mwangu,otea A B C AU D? enhe. hivi sasa siweki hadharani maana nna phd ya kunyakuliwa.
sa hivi ni kumpost kwa mwendo kasiii yaani wengi wengi simtaji ng’ooo.
RAMADHAN QAREEM...sasa andika matusi ufungulie.
nimesubiri siku hii muda jmn dah watu wakiwa wamefungwa makufuli midomoni na mwezi(waislam/waikristo wote wanauheshimu”

Baada ya ujumbe huo wa Nisha ndipo Wolper alitoa maoni yake kwenye picha hiyo kwa kuandika hivi

Kisha Nisha Akajibu;


Ok guys kuna picture niliweka saa 4 asbh leo,za wasanii kadhaa wa music ambao niliweka na caption yangu kwa furaha zangu tu.
ila baada ya lisaa limoja ikaja coment hiyo ya msanii mwenzangu sikudhungumza chchte,i was like ok nikacheka tu.
then zikaja comments nyingi za kumuuliza kulikoni kuandika hivyo.
masaa mawili yaliyopita ukaandikwa waraka mzito mrefu unaosema. “Nisha aandaa show mtwara ya kumnasa Harmonize ila Wolper akagundua hilo akaamua kuongozana naye Harmo hadi huko kukwepa hilo (NA MANENO MENGI YA ZIADA YA UONGO.
ikimbukwe show imeshapita km week na haya maneno yamezuka leo baada ya hiyo coment.
guyz tuje kwenye point KWANZA KABISA SIJAMLENGA YYTE KWA NILIYEANDIKA NILIANDIKA KWA MAPENZI YNG KM NILIVYOANDIKA JANA STATUS YA VIDONDA VYA TUMBO,TENA HADI WADOGO ZNG NIKAWAAMBIA TAZAMA NACHEZA NA AKILI ZA WATU.
NIMESHANGAA HABARI ZA UONGO KUSAMBAZWA ZIDI YANGU TENA BAADA YA COMENT HII KWANGU.
POINT YA PILI KWA YYTE ANAYEULIZA NIMEANZA LINI UPROMOTA guyz mimi ni mfanyabiashara na kwenye pesa nipo,show ya MTWARA imenigharimu si chini ya ml.18 unadhani naweza poteza pesa zote hizo kisa mapenzi?sina ujinga huo wa akili.
NA SIJAWAHI KUMTAKA NA SITOTARAJI KWANZA SIJAZOEA KUPITA ANAPOPITA MTU HASWA NNAYEMJUA.
TATU nimeandaa show ingine ramadhan ya 13 DAR-ES-SALAAM inahusu ramadhan.
na nna SHOW SKUKUU YA IDD MOSS NA IDD PILI MIKOANI ZOTE MM NDO MUANDAAJI NA KUNA WASANII WAKUBWA TU JE HAO PIA NATAKA KUWANASA? HE.
IFIKE HATUA TUSIWE TUNABALANCE MTU MMOJA NA PIA SIO KILA ASIYEDHUNGUMZA NI MNYONGE SANA ILA KUNA WKT DRAMA HAZINA MUDA INABIDI UPIGE KAZI MAANA MAISHA YANAENDA MBELE HAYARUDI NYUMA.
NB:SHUKRAN KWA WEWE UNAYESAMBAZA UJUMBE HUU WA UONGO SINA CHA KUKWAMBIA NIMEPITIA MENGI MAKUBWA SO HILI KM NACHEZA MDAKO. (mwenye uelewa kaelewa chanzo cha story inayosambaa imetoka wapi,nimeandika hapa kwa manufaa ya mashabiki zangu wote watakaobahatika kusoma habari hizo za uongo.

Wanawake wa Kichagga na Kihaya Mtatumaliza Wanaume

$
0
0
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Wanawake wa kichagga na kihaya wanatumalizia ndugu zetu. Yaani hawa wanawake ni so strategic, wananyatia wanaume (hata simba na ufundi wake wa kuwinda hawafikii) wenye mafanikio au dalili ya kufanikiwa tu! Wanaume waliosoma, wenye hela au biashara kubwa kubwa. Mbaya zaidi wakishaolewa wanawaendesha hao wanaume mpaka wengine wanakufa vifo vya ghafla kama vile kwa presha! Mrengo wao kimaisha ni kujenga kwao.

Ndugu zangu na rafiki zangu asilimia kubwa wenye mafanikio na elimu wote wameoa wachagga au wahaya, yaani badala ya kuwapenda hawa wanawake kwa sababu ni shemeji zangu, badala yake sina amsha amsha nao kabisa. Mwaka jana kulikuwa na harusi kama 18 hivi ambazo nilihusishwa kwa sababu ya ukaribu au undugu, yaani kati ya hizo 16 mchagga au mhaya anaolewa! Niligoma mgomo baridi, vikao wala michango sikutoa! Mbaya zaidi kuna jamaa nimesom naye UDSM rafiki wa damu, tuliapa viapo vyote, tukae mbali na wanawake wa kichagga na kihaya, cha ajabu juzi ananitumia ujumbe wa simu kuwa anaoa na nilivyohoji shemeji ni wa wapi, akaniambia mchagga. Yaani anamezwa na zimu tulilolikwepa kwa zaidi ya miaka kumi!

Wakuu hii hali ikoje kwa jamaa/ndugu zenu? Wanawake wa kihaya na kichagga muwe na uungwana japo kidogo.

By Simplicity.

Ulinzi mkali kwa Naibu Spika waimarishwa

$
0
0
Naibu Spika wa bunge, Dk Tulia Ackson ameongezewa ulinzi hasa kipindi hiki ambacho wabunge wanajadili Bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/17. Tangu Serikali ilipowasilisha bajeti, idadi ya walinzi kwa ajili ya Dk. Tulia iliongezeka hadi watano idadi ambayo ni kubwa kuliko awali.

Jambo hilo limesababisha hata wabunge wa CCM na wa upinzani kushangaa huku wengine wakihoji sababu. Wapo baadhi ya wabunge waliodhani huenda ulinzi wa Dk. Tulia umeongezwa baada ya kutoa mwongozo mwishoni mwa wiki wa wabunge wa upinzani kutolipwa posho za vikao vyote walivyotoka nje.

Rais Magufuli waite wapinzani wako ujue wanachotaka

$
0
0
Tangu raisi ameingia madarakani,ameshakutana na kada za watu tofauti na ameongea nao isipokuwa kwa upande wa wanasiasa bado,najua si lazima lakini kibusara kidogo angewaita akasikia maoni yao,nafikiri wanafikira nzuri tu ya kuisogeza nchi mbele ila wanapata hasira unapowapuuza,labda tatizo vyombo vya habari vimekuwa ni wapinzani kuliko wapinzani wenyewe,mpaka sasa mazuri mengi umefanya ila kubwa ni hilo,kama ulivyokwisha sema wewe ni raisi wa vyama vyote basi waite hawa mabwana sidhani kama watakataa wito

Serikali Yatangaza Vita Dhidi ya Majambazi na Watu Wanaojihusisha na Mauaji

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni ametangaza vita dhidi ya majambazi na watu wanaojihusha na mauaji.

Alisema Serikali imelazimika kutangaza vita hivyo baada ya kutokea matukio 41 yaliyohusisha mauaji ya kinyama tangu Januari hadi mwezi uliopita.

“Serikali ipo kazini, sasa inatangaza vita dhidi ya watu wanaojihusisha na ujambazi, watakaobainika hakika wataangamizwa hatuwezi kukubali watu wazidi kupoteza maisha pasipo na sababu za msingi,” alisema Masauni.

Waziri huyo alitembelea Msikiti wa Rahman Mtaa wa Utemini Kata ya Mkolani wilayani Nyamagana, Mwanza na kusema matukio hayo yanapaswa kutokomezwa na kukemewa kwa nguvu zote.

 “Mauaji hayo yalikuwa ya kutisha hivyo ilikuwa ni lazima watuhumiwa wakamatwe, hata hao waliokimbia wanapaswa kutiwa mbaroni,” alisema.

Pia, alionya tabia ya baadhi ya polisi kujihusha na vitendo vya uhalifu na kupoteza imani na uaminifu kwa wananchi.

 Aliwataka polisi wanaofanya vitendo hivyo kuacha na badala yake wapambane na wahalifu.

Masauni alisema nia ya Serikali ni kuhakikisha Watanzania wanaishi kwa utulivu, hivyo haitakubali watu wachache kuvuruga amani iliyopo

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella alisema vyombo vya usalama vipo imara kwani baadhi ya wahalifu wameuawa na wengine kukamatwa na wanaendelea kuhojiwa.

Mjumbe wa baraza la masheikh Wilaya ya Nyamagana, Saidi Darwesh alisema tukio la mauaji ya msikitini limesababisha hofu kwa waumini, hususan kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani kwani wengine hawaendi msikitini kuswali.

 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Utemini, Jukael Kiula alisema wakazi wa Kata ya Mkolani wamejitolea kujenga kituo cha polisi katika mtaa huo ili kudhibiti uhalifu unaotokea mara kwa mara.

Maneno ya Ruby na Aslay yanayoashiria Kuwa ni Wapenzi

$
0
0
Kama wewe ni mmoja wa watu wanaotumia mitandao ya kijamii hususani instagram, najua huenda ukawa umekutana na post za mastaa wa Bongofleva Ruby na Aslay ambazo zinatafsirika kama wapo kwenye mahusiano. Haijajulikana kwa mara moja kama ni kiki au ni serious ni wapenzi ila hii ndio ishu inayo trend kwa sasa.


Polisi Wauzuia Mkutano wa Chama cha ACT Wazalendo, Millenium Tower DSM

$
0
0
Tunasikitika kuwataarifu Wananchi Na Umma Kwa Ujumla kuwa Polisi katika Mkoa wa Dar es Salaam wametuzuia kufanya Kongamano letu lililolenga kuchambua Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2016/2017. Polisi wamezingira eneo la ukumbi wa Kongamano (LAPF Millenium Towers) tangu saa 12.00 asubuhi.

Viongozi Wakuu wa chama wanakutana na waandishi wa Habari wa Makao Makuu ya Chama Kijitonyama kuanzia saa 7.30 Mchana kwa taarifa zaidi.

Abdallah Khamis
Afisa Habari Mkuu
Chama cha ACT-Wazalendo.

Tamko la ACT-Wazalendo Baada ya Mkutano wao Kuzuiwa na Polisi

$
0
0
Baada ya Jeshi la polisi kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa Chama Cha ACT- Wazalendo kilipanga kufanya kongamao Jumapili ya June 12 2016 kwa lengo la kujadili Bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/2017.

Taarifa iliyotolewa na chama cha ACT-Wazalendo kupitia kwa Mwenyekiti wa chama hicho Anne Mghwira imesema kwamba kongamano hilo lililenga kumpa fursa ya pekee kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe kusema yale ambayo angeyasema bungeni baada yeye na wabunge wenzake sita wa upinzani kusimamishwa kuhudhuria vikao vya bajeti bungeni.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa katika hali isiyo ya kawaida walipewa taarifa na mwenye ukumbi (LAPF Millenium Tower) kwamba polisi walikuwa wametanda katika eneo la ukumbi tangu saa kumi mbili asubuhi na ilipofika saa nne kamili asubuhi mwenye ukumbi aliwataarifu rasmi kuwa amepewa taarifa na kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kinondoni kwamba chama chao hakina kibali cha kufanya kongamano hilo na hivyo asiwafungulie ukumbi huo.

Hivyo kupitia taarifa hiyo chama ACT-Wazalendo kimesema kimesikitishwa sana na hatua hiyo ya polisi na wanaitafsri kuwa ni mwendelezo wa hatua za uhakika katika kufifisha demokrasia katika nchi.

Amber Lulu Afunguka Kupiga Picha za Utupu

$
0
0
Akiongea kwenye FNL ya EATV, Amber Lulu amesema yeye ni model hivyo picha hizo huwa zinakuwa za kazi ambazo huwa yupo assigned, ambayo pia ndio inayomlipa.

"Mimi ni model unajua, sasa kama model kuna picha kama zile napiga, zinakuwa na kazi, na sio napiga tu, ukiona nimepiga vile jua kuna kazi ambayo ipo na mtaijua", alisema Amber Lulu.

Mwanadada huyo ambaye kwa sasa amejizolea umaarufu kwenye mitandao ya kijamii, amesema kwa sasa hayupo kwenye mahusiano kutokana na ugumu anaoupata unaotokana na kazi yake hiyo, hivyo huamua kuwa mwenyewe ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza.

Hamisa Mobeto Asema Bado Kuna Watu Wanadhani mtu Kuwa Model ni Uhuni

$
0
0
Mwanamitindo Hamisa Mobeto amewataka wazazi kuuwaacha watoto kike/wakiume waingie kwenye fashion na kuachana na dhana ya kwamba kufanya modeling ni uhuni.
Mobeto

Akiongea na Bongo5 wiki hii wakati akitoa maoni yake juu ya nini kifanyike ili kuboresha tasnia ya mitindo, Hamisa amewataka wazazi kuichukulia tasnia ya fashion kama sector nyingine za ajira.

“Unajua Watanzania wengi bado hawajajua nini maana ya modeling , wengine wanadhani ni uchafu, uhuni,” alisema Mobeto. “Tanzania kuna Wanawake wazuri sana, kama wazazi wakiwaruhusu vijana wao kufanya modeling basi Tanzania tutafika mbali sana kwa sababu tuna warembo wengi sana,”

Pia mrembo huyo ameitaka serikali kuangalia tasnia ya fashion ambayo kwa sasa inatoa ajira kwa vijana wengi pamoja na kuitangaza nchi.

Taarifa ya ACT- Wazalendo Kuhusu Kupotea Kwa Zitto Kabwe Tangu Jana Jioni

$
0
0

TAARIFA KWA UMMA

Tunaujulisha UMMA kwamba Kiongozi wa Chama chetu cha ACT Wazalendo ndg. Zitto Kabwe amekuwa anatafutwa na Polisi tangu jana usiku.


Mpaka sasa hatujui Kiongozi wetu yupo wapi na yupo kwenye Hali gani. Askari kanzu wanalinda nyumbani kwake na kwa watu wake wa karibu. 


Sisi kama chama tunaliambia jeshi la Polisi kuwa lolote litakalotokea kwa Kiongozi wetu wao watajibu kwa umma.

 

Msafiri Mtemelwa, 
Kaimu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo


Viewing all 104809 articles
Browse latest View live


Latest Images