Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Baada ya Bei ya POGBA Kuwa Gumzo Duniani, Scholes Ametoa Kauli yake

$
0
0
Paul Scholes anaamini kwamba Manchester United hawatakuwa wanatenda haki endapo watatoa kiasi cha paundi mil 92 (euro mil 110) kuinasa saini ya Paul Pogba kutoka Juventus, ada ambayo inaelezwa kuvunja rekodi ya usajili duniani.

Scholes ni shabiki mkubwa wa Pogba lakini amesema kwa bei hiyo inaaminisha kwamba uwezo wake ni sawa na Lionel Messi and Cristiano Ronaldo huku akisema haamini kwamba Mfaransa huyo ana thamani sawa na wakali hao wawili.

“Alikuwa ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa, Nimewahi kucheza naye mara nyingi tu,” Scholes aliwaambia wanahabari.

“Ni kweli amekuwa kwenye kiwango bora lakini bado siamini kama ana thamani ya paundi milioni 100 kwa sasa.”

“Kwa bei kama hiyo, ungehitaji mchezaji ambaye anaweza kufunga magoli zaidi ya 50 kwa msimu, kama Ronaldo au Messi, Pogba bado hajafika huko kabisa.”

Fredrick Sumaye Na Kisa Cha Mchimba Kisima..!

$
0
0
Ndugu zangu,
Bila shaka, mmoja wa ' Wana- CCM' wa zamani waliofuatilia kwa karibu sana Mkutano Mkuu wa CCM leo ni Fredrick Tluway Sumaye.

Huyu ni mmoja wa wanasiasa walioshindwa sana kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Ni heri ya Lowassa na Kingunge kulikoni Sumaye. Nilibaki nikimshangaa Sumaye aliposimama majukwaani na kuiponda CCM huku akilaumu pia Katiba inayovikandamiza vyama pinzani.
Katika uchaguzi wa mwaka jana yumkini wapiga kura waliwaadhibu watu wa aina ya Sumaye na kuwaonyesha, kuwa wao wapiga kura si wajinga.

Nilimshangaa Sumaye na Kingunge kusimama majukwaani na kulaumu mfumo ambao wao walishiriki kuujenga na kuulinda. Kwa Sumaye na Kingunge wanapolaumu Tume ya Uchaguzi na Katiba ya Nchi ya mwaka 1977 wanasahau, kuwa wao wakiwa madarakani walikuwa na nafasi ya kuweka mazingira ya kufanyiwa mabadiliko.

Ona Fredrick Sumaye, ukiacha mapendekezo ya Jaji Francis Nyalali ya mwaka 1992 ambayo yaliainisha sheria 40 kandamizi, na hata Sumaye alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu mwaka 1995, sheria hizo 40 kandamizi alizikuta, hakufanya lolote.

Mwaka 1998, Ben Mkapa aliunda Tume ya Jaji Kissanga iliyomkuta Sumaye akiwa Waziri Mkuu. White Paper ile ya Jaji Kissanga, mbali ya mambo mengine, ilipendekeza pia Rais achaguliwe kwa kupata 50 plus asilimia za kura zote.

Ikaenda mbali kupendekeza pia Serikali tatu katika muundo wa Muungano. Nakumbuka pale Diamond Jubilee Hall, Ben Mkapa akiongea na wazee wa darisalaam aliinanga ripoti ya Jaji Kissanga akidai pia haikufuata adidu za rejea. Sumaye alikuwepo kama Waziri Mkuu, alikuwa na nafasi ya kuweka mazingira ya kurekebishwa kwa sheria hizo, lakini, wakati huo, alikaa kimya.
Sumaye alikuwa bize akichimba kisima ambacho leo ameingia mwenyewe.

Niwe mkweli kwa nchi yangu, Fredrick Sumaye wa leo, kama alitaka mabadiliko ya kweli, alipaswa kuendelea kubaki CCM na kuifanya kazi hiyo ndani ya CCM- kama ' Born Again Sumaye' . Si nje ya CCM kama anavyofanya sasa.

Maana, Sumaye angelikuwa na jukwaa pana zaidi na angeaminika zaidi. Nitakuwa mtu wa mwisho kushangaa, pale Sumaye atakapoyashindwa hata maisha ya kila siku ya kisiasa, uko aliko sasa.
Ni mtazamo wangu.
Maggid,
Iringa.

Magufuli Ashindwa Kumtumbua Kinana

$
0
0
ABDULRAHAMAN Kinana, amekubali kuendelea na wazifa wake wa katibu mkuu.
Taarifa zinasema, Kinana ataendelea kutumikia wazifa huo hadi kufanyika uchaguzi mkuu ujao, Novemba mwaka kesho.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa wa gazeti hili, wengine watakaobaki kwenye nyazifa zao, ni Philip Mangula na manaibu makatibu wakuu wote- Bara na Zanzibar.

Habari zinasema, “uamuzi wa kumbakisha Kinana kwenye nafasi yake, haukuwa wa Magufuli. Ni shinikizo la viongozi wakuu wa CCM wakiongozwa na Benjamin Mkapa,” anaeleza mmoja wa viongozi wandamizi wa chama hicho.

Chanzo:Mwanahalisionline

David Moyes Ametangazwa Kuwa Kocha Mpya wa Sunderland

$
0
0
Kocha wa zamani wa Everton na Man United, David Moyes ametangazwa kuwa mrithi wa Sam Allardyce, David Moyes ambaye ana umri wa miaka 53 amesaini mkataba wa miaka minne wa kuitumikia Sunderland.
Sam Allardyce maarufu kama Big Sam ambaye ametangazwa kuwa kocha mkuu mpya wa England.

LULU:Mimi na Mama Kanumba Tupo Vizuri!

$
0
0
STORI zilivuma na bado vuguvugu linaendelea kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusu uhusiano wa staa wa kike katika filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na mama Kanumba, Flora Mtegoa kuwa siyo mzuri kama zamani.

Watoa habari wa mjini, wanadai kuwa mama Kanumba na Lulu kwa muda mrefu sasa hawapikiki chungu kimoja kama ilivyokuwa zamani.

Lulu alikuwa mchumba wa mwigizaji wa filamu za Kibongo, marehemu Steven Kanumba ambaye alifariki dunia Jumamosi ya Aprili 07, 2012, nyumbani kwake, Sinza – Vatican jijini Dar es Salaam.

Mbali na mitandao ya kijamii kukuza kinachoitwa bifu kati ya mtu na mkwewe huyo, magazeti mbalimbali yalipata kuripoti kuhusiana na kuwepo kwa kutokuelewana baina yao.

Katika mahojiano na My Style ya Swaggaz ndani ya Mtanzania Jumamosi, Lulu alifunguka mengi kuhusiana na madai ya bifu hilo, akikiri kuwepo lakini akasema kuwa kwa sasa imebaki stori tu.

Akizungumzia hilo anasema: “Ni kweli kuna wakati  kulitokea kutoelewana kidogo na naweza kusema ni jambo la kawaida. Jamani binadamu kutofautiana mitazamo wakati fulani si kitu cha kushangaza.

“Lakini hayo mambo yalishaisha kabisa. Mimi na mama Kanumba tupo vizuri sana kwa sasa. Sina ugomvi naye,  tunaelewana na tunaishi vizuri kabisa. Mikwaruzano ya mwanzo iliisha na tunaendelea vyema.”

Lulu anawaangushia lawama watu wenye tabia za kukuza mambo mitandaoni ambao hawamtakii mema kwa kuzusha kuwa bado wana bifu.

“Tatizo kuna watu hawana kazi za kufanya, kazi yao kushinda mitandaoni na kutunga habari za uongo au kukuza mambo ambayo hayapo. Watu waache, mimi sina tatizo na mama Kanumba.

“Yule ni mtu mzima, nawezaje kuwa na bifu naye? Ninachoweza kusema ni kwamba kulikuwa na kupishana kauli kidogo, lakini hayo mambo yameshaisha, watu wasijaribu kuendelea kukuza,” anasema Lulu ambaye ni mshindi wa Tuzo ya  Africa Magic Viewer’s Choice Awards katika kipengele cha Filamu Bora ya Afrika Mashariki kupitia filamu yake ya Mapenzi ya Mungu ambayo mama Kanumba pia ameshiriki.

MY STYLE: Unapenda kuishi vipi wewe kama staa?

LULU: Kama binti napenda maisha mazuri ndiyo maana najituma ili niweze kufanikiwa. Kama nilivyosema huwa sipendi uzushi na ugomvi, ndiyo maana ninapozushiwa au kutukanwa mara nyingi huwa nanyamaza kwa kuwa sipendi malumbano na watu. Napenda amani.

MY STYLE: Unajivunia nini katika sanaa yako?

LULU: Nimefanikiwa kimaisha nashukuru, pili najivunia kupata tuzo ya kimataifa kule Lagos, Nigeria. Kwangu ni mwanzo mwema na mwanga mzuri mbele yangu.

MY STYLE:  Lulu ana tofauti gani na waigizaji wengine wa Bongo?

MY STYLE: Lulu ni Lulu hawezi kuwa mtu mwingine na mtu mwingine hawezi kuwa Lulu, nadhani hiyo ndiyo tofauti.

MY STYLE: Unazungumziaje skendo zinazokuandama katika mitandao ya kijamii na wale ambao hukushushia matusi?

LULU: Nachukulia kama changamoto tu katika kazi kwani kuna mambo mengine nahusishwa nayo ila siyajui. Ila ninachojua, hao wanaonitukana ndiyo haohao mashabiki wangu, sema wanajibalaguza tu lakini moyoni wananikubali.

MY STYLE: Wewe ni shabiki wa chama gani cha siasa?

LULU: Mimi sina chama, ndiyo maana hata katika kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka jana, sijaonekana kwenye jukwaa lolote. Miye naamini kura ni siri na nilifanya hivyo ili nisifungamane na upande wowote.

MY STYLE: Una ushauri gani kwa mastaa wenzako?

LULU: Tushirikiane na kufanya kazi kwa ufanisi, tuongeze juhudi ili tuweze kurudisha hadhi ya soko la filamu kama lilivyokuwa awali.

Mtanzania

CHADEMA 'Hatuna Muda wa Kuwazungumzia Hao Waliohama Chama Jana'

$
0
0

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimedai hakina muda wa kuwazungumzia Fredy Mpendazoe na Mgana Msindai waliotangaza rasmi kukihama chama hicho jana na kurejea Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa maelezo kuwa kuna mambo mengi ya maana zaidi ya kufanya kwa sasa.

Nini maoni yako, na ungependa kuwaambia nini wawili hawa?

Lulu Michael Afunguka Kuhusu Chama Anachokifagilia Bongo.....

$
0
0

Alipoulizwa yeye shabiki wa chama gani cha siasa?, Elizabeth Michael ‘Lulu’ alijibu hivii; "Mimi sina chama, ndiyo maana hata katika kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka jana, sijaonekana kwenye jukwaa lolote. Miye naamini kura ni siri na nilifanya hivyo ili nisifungamane na upande wowote." Alifanya vizuri au alichemka?

Kauli ya CHADEMA baada ya wanachama wake kutangaza kujiunga CCM

$
0
0
Wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM jana mjini Dodoma, Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) kiliwapoteza wanachama wake watatu baada ya kutangaza rasmi kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Wanachama hao waliokihama chama hicho ni Fred Mpendazoe ambaye alikuwa mwanachama wa CCM pia aliwahi kuwa Mbunge wa Kishapu mwaka 2005 hadi 2010 kupitia CCM, Mgana Msindai aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida na mbunge wa zamani wa Iramba Mashariki na mwigizaji wa filamu nchini Tanzania Jackline Wolper.

Mmoja wa wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA alipohojiwa jana wakati kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kinaendelea alisema kuwa, hawana muda wa kukaa na kuanza kumjadili mtu mmoja mmoja anayesemekana kuhama chama hicho.

"Kamati Kuu ni kikao kizito sana, hatuwezi kuacha kujadili masuala ya msingi na kuanza kuwajadili hao wanaosemekana kuwa wamehama chama," alisema mjumbe huyo.

Kamati Kuu ya CHADEMA imekutana jana na leo katika vikao vya dharura ikiwa na lengo kubwa la kujadili mwenendo wa hali ya kisiasa nchini.


Mabasi ya Mwendo Kasi Yaanza Kutumika Visivyo..Ona Tukio Hili...

$
0
0
Bado haijafahamika vizuri nini kiliendelea mpaka wahusika wa Mabasi ya Mwendo kasi pamoja na dereva kuruhusu piki piki kuingia kwenye basi la mwendo kasi sambamba na Abiria...
Picha hii leo umekuwa ikizunguka sana mitandaoni na kila mtu kuuliza kunani?

Ali Kiba Afunguka Sababu za Kuwatosa Wanawake Watatu Alio zaa Nao....

$
0
0
Alikiba ameitaja sababu iliyomfanya ashindwe kumuoa mwanamke yeyote kati ya watatu aliozaa nao.

Hitmaker huyo wa Lupela alikiambia kipindi cha Chill na Sky kuwa hakupenda kulazimisha iwe hivyo.“Unajua hauwezi kumuoa mtu kama hamuelewani.

 Nia yangu ilikuwa ni kustick na kila mama wa mmoja toka nilipoanza. Lakini mambo yanaenda tofauti, huenda mnagombana anapata mtu mwingine,” anasema Kiba.“Kwahiyo hautakiwi kuforce mapenzi, mimi nataka nikae na mtu ambaye tutaelewana,” ameongeza.

Alikiba ana watoto wawili wa kike, Amiya Kiba, Chamy Kiba na mmoja wa kiume, Sameer Kiba. Wote ni watoto wa mama tofauti.

Pamoja ya Yote Lakini Kuna Kubwa la Kujifunza Toka CCM

$
0
0
Kwanza niseme tu kuwa mimi naunga mkono upinzani, lakini nimeona kuandika uzi huu baada ya kuona kuna kitu ambacho sisi wapinzani tunachakujifunza toka kwa CCM. Pamoja na mapungufu mengi ya chama tawala lakini bado angalau wana mifumo ya kidemocrasia hata kama haijakamilika lakini kitendo cha kubadirisha viongozi wakuu kwenye chama ni kitu cha kuigwa. Hivi ndani ya vyama vyetu hakuna watu wengine wanaoweza kuongoza?? Kwamba lazima wawe ni wale wale tu. Lini Mbowe atapumzika, Lini Maalim Seif atapumzika, lini Mbatia atapumzika du, na isingekuwa mvutano pengine na Lipumba angekuwemo mpaka leo. Tunahitaji fikra mpya ndani ya vyama vya upinzani kama ni kweli tunahubiri democrasia. Inawezekana nikawa kinyume na wengi lakini, nimeona niwe muwazi kutoa maoni yangu.

JE Mwanamke Hutokwa Shahawa Wakati wa Tendo?

$
0
0
Ndio, Wanawake wanakojoa wanapofika kileleni katika tendo la ndoa. Hii inaitwa fe.male ej.aculation au squ.irting. Wakati male eja.culation inaweza kuwa na ujazo wa kijiko 1 au 2, ya wakina mama inaweza kufikia ujazo wa kikombe na zaidi.

Wetness kwenye uke ni muhimu ili tendo la ndoa lisimuumize. Lakini mwanamke anapofika kileleni anatoa haya maji zaidi ili spe.rms zipate medium ya kuogelea zinapotafuta yai.

Wakina mama wanatofautiana na kiasi gani cha haya maji wanayatoa. Kuna light squi.rters na wale super (niagara) squi.rters. Ukikutana na super-squi.rter utajua tu kwa sababu itabidi muweke mataulo ili muweze kulala. Wanawake pia wana uwezo wa kuwa na multiple-ejaculations kama umemuandaa vizuri.

Somo:
Ili mpenzi wako (mke) aweze ku-squ.irt, ni lazima umuandae vizuri. Haya mambo ya "slam-bam thankyou-maam" uta-clim.ax wewe lakini sio yeye. Ukiweza kumfanya mpenzi wako a-squ.irt ni dalili kuwa umemridhisha vya kutosha.

Wakina mama msione aibu kama utalowesha shuka kwa gharika utakalolishusha kwani hii inamuashiria mwenzio kuwa kibarua ulichompa amekitimiza.

Wakina baba kila siku lengo lako katika tendo la ndoa ni kumfanya mwenzio a-squi.rt. Ukiweza kufanya hivi kila mara huyo mama atakufunga kamba kwenye tendegu usitoke.

Jitibu Magonjwa 300 Kwa Kutumia Mti wa Mlonge

$
0
0
Mlonge au moringa oleifera kwa kiingereza umekuwa ukijulikana kama mti wa miujiza kwa karne nyingi katika baadhi ya nchi za Afrika, Asia na katika nchi za Caribbean. Mti huu umeripotiwa kutibu zaidi ya magonjwa 300 ikiwemo magonjwa mbalimbali sugu.

Karibu kila sehemu ya mti huu hutumika kama dawa. Majani ya mlonge yanaweza kutafunwa mabichi, yaliyochemshwa kama mboga au yaliyokaushwa na kusagwa kuwa unga. Unga wa mlonge unaweza kuhifadhiwa kwa miezi kadhaa bila kupoteza ubora na faida zake za kiafya.

Mbegu za mlonge zimekuwa dili kubwa duniani kwa sasa, zinahitajika kwa kiasi kikubwa katika nchi ya Marekani na China na kwa mujibu wa taarifa ni kuwa zinauzwa mpaka 45000 ya Tanzania kwa gramu 500. Walikuja pia wachina kuzinunua kwa wingi na walikuwepo hapa bei ya mbegu za mlonge ilifika mpaka 11000 kwa kg kwa bei ya jumla yaani kwa anayechukua kg 100 au 500 au 1000 na kwenda juu. Taarifa zisizo rasmi zinadai wachinja hawa walikimbia nchini baada ya serikali kuanza kufuatilia na kuwakamata wakwepaji kodi bandarini. Isingekuwa hivi mpaka leo mlonge ungekuwa umeshatowka wote Tanzania.


Faida za mlonge zimeandikwa na majarida ya afya na lishe kadhaa duniani. Kile ulikuwa hujui ni kuwa viwanda na makampuni mengi ya dawa za hospitalini yamekuwa yakitumia virutubishi vilivyomo kwenye mti huu kutengenezea madawa kwa ajioli ya binadamu na wanyama.

Mlonge una:

Kalsiumu mara 17 zaidi ya ile ya maziwa ya ng’ombe

Potasiamu mara 15 zaidi ya ile ya kwenye ndizi

Una vitamini A mara 10 zaidi ya ile ya kwenye karoti

Una protini nyingi mara 9 zaidi ya ile ya kwenye mtindi

Una klorpfiti (kemikali ya rangi ya kijani ipatikanayo katika mimea) mara 4 zaidi ya ile ya kwenye nyasi au majani ya ngano (wheatgrass)

Una madini chuma mara 25 zaidi ya yale ya kwenye Spinach

Una vitamini A mpaka Z

Una omega 3, 6 na 9

Una asidi amino zile muhimu zinazohitajika na mwili

Una kiasi cha kutosha cha madini ya zinc ambayo ni madini muhimu katika kuongeza homoni za kiume na nguvu za kiume kwa ujumla

Mlonge ndicho chakula chenye afya zaidi juu ya ardhi:

Mlonge una jumla ya virutubishi 92, mmea au mti mwingine wenye virutubishi vingi basda ya mlonge una virutubishi 28. Mlonge una vionsa suku 46 na viondoa uvimbe mbalimbali mwilini 36, una asidi amino 18 na asidi amino muhimu zaidi 9 ambazo miili yetu haina uwezo wa kuzitengeneza.

Unga wa majani ya mlonge unao uwezo wa kutibu magonjwa zaidi ya 300 mwilini, magonjwa hayo ni pamoja na :

1. HUko Afrika magharibi madaktari hutumia mlonge kutibu kisukari.

2. HUko India mlonge hutumika kutibu shinikizo la juu la damu

3. HUtibu matatizo u maumivu ya mishipa

4. Hutuliza mapigo ya juu ya moyo

5. Hutibu kansa

6. Pumu

7. Hutuliza wasiwasi

8. Kikohozi

9. Maumivu ya kichwa

10. Inazuia na kushusha ile lehemu hata ile ya juu zaidi

11. Inapunguza mafuta tumboni

12. Inaweza sawa homoni

13. Inatibu maumivu wakati wa hedhi

14. Unasafisha ini

15. Inasafisha mkojo na kibofu cha mkojo

16. Inarekebisha matatizo kwenye tezi

17. Unatibu kipindupindu na kuharisha

18. Kifua kikuu

19. Kichwa kizito

20. Uchovu

21. Mzio

22. Vidonda vya tumbo

23. Maambukizi kwenye ngozi

24. Maumivu mbalimbali mwilini

25. Huondoa madoa doa meusi kwenye ngozi

26. Husafisha damu

27. Hutibu matatizo kwenye koo

28. Huondoa makohozi mazito kooni

29. Huondoa taka na msongamano kifuani

30. Hutibu kipindipindu

31. Huondoa moto wa jicho au uvimbe kwenye jicho

32. Hutibu maambukizi kwenye macho na kwenye masikio

33. Unatibu homa

34. Maumivu kwenye maungio

35. Huondoa chunusi

36. Hutibu matatizo karibu yote ya ngozi na kinga ya mwili

37. Matatizo kwenye mfumo wa upumuaji

38. Inatibu kiseyeye

39. Huongeza uwingi wa mbegu za kiume na nguvu kwa ujumla

40. Inatibu minyoo

41. Huongeza maziwa kwa wingi kwa mama anayenyonyesha

42. Huondoa uvimbe kwenye utumbo mpana

43. Inatibu ugonjwa wa kuvimba mwili

44. Inatibu kuhara damu

45. Inatibu kisonono

46. Unatibu tatizo la kukosa usingizi

47. Unatibu homa ya manjano

48. Unatibu malaria

49. Unatibu U.T.I na matatizo mengine kwenye mfumo wa mkojo

50. Unasaidia pia kujenga na kuimarisha misuli

51. Unatibu magonjwa ya mifupa

Mlonge uansafisha mwili wako wote, unasafisha ini, figo, moyo, macho, unaimarisha meno, ngozi na nywele. Wakati unatumia mlonge unakufanya ujisikie vizuri, ujisikie mpya na mwenye nguvu. Watu wengi wanaotumia mlonge huwa ni wenye afya nzuri hata kwa muonekano tu hata wanapokuwa na umri mkubwa zaidi ya miaka 90.

Majani ya mti wa mlonge pia yanaweza kutumika kutengeneza biogas. Hutumika pia kama chakala cha wanyama kama sungura , mbuzi, ng’mbe. Mbwa n.k. Sungura wanaonekana kupenda zaidi mlonge kuliko wanyama wote.

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya July 25

$
0
0



SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya July 25

Rais wa Zanzibar Dr Shein Afuata Nyayo za Magufuli...Aanza Tumbua Tumbua Majibu Uchungu

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein, amefuta uteuzi wa Naibu Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), Hafidh Ussi Haji huku akimteua Khadija Shamte Mzee, kuchukua nafasi hiyo.

Pia, taarifa ya Ikulu inaonyesha Dk Shein, amemteua Amour Hamil Bakari kuwa Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar kuchukua nafasi ya Abdi Khamis Faki ambaye anastaafu kwa mujibu wa sheria.

Vilevile, Dk Shein amemteua Umi Aley kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Magazeti ya Serikali; Said Bakar Jecha na Sebtuu Mohammed Nassor wameteuliwa kuwa Makamishna wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, wakati Ali Saleh Mwinyikai ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utangazaji Zanzibar.Wengine walioteuliwa ni Maryam Hamdan kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Sanaa na Sensa ya Filamu na Utamaduni, wakati Maryam Abdulla Yussuf ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani Zanzibar na Profesa Ali Seif Mshimba, ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Viwango Zanzibar. Uteuzi huo unaanza Julai 25.



Askofu Josephat Gwajima Amjibu Yusuf Makamba Kistaili.....

$
0
0
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amemjibu Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Yusuf Makamba aliyemtuhumu kuwa ni mwongo, akisema leseni yake ni ya kuendesha magari makubwa siyo vibajaji na maguta.

Akihubiri katika kanisa lake jana, Gwajima bila kutaja jina la Makamba, alisema: “Siwezi kushughulika na vigari vidogovidogo nyie mnanifahamu, nina leseni ya kuendesha semi trailer …nadhani mmenielewa,” alisema huku waumini wake wakimshangilia.

Juzi, Makamba aliwaeleza wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM kuwa, Askofu Gwajima ni kiongozi wa dini lakini ni mwongo na kuwa uongo huo unawaudhi hata waumini wake ambao ni wanachama wa chama hicho.


Diwani Moshi Akwepa Risasi Sita, Apambana na Majambazi Mwanzo Mwisho....

$
0
0
Hii ni kama filamu lakini ndio ukweli, Diwani wa Kata ya Kiborlon Manispaa ya Moshi, Frank Kagoma (Chadema) ameonyesha ujasiri wa hali ya juu alipopambana na majambazi waliokuwa na silaha za moto.

Alinusurika kuuawa baada ya majambazi hao waliokuwa na bunduki na bastola, kumfyatulia risasi sita alipokuwa akiwafukuza ambazo hata hivyo, hazikumpata.

Tukio hilo ambalo lilionekana kama sinema, lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya majambazi hayo kuvamia duka la jumla la kuuza mitumba linalomilikiwa na Menti Mbowe na kupora Sh10 milioni.

Katika tukio hilo lililotokea saa tano asubuhi eneo la Kiborlon, majambazi hayo walimjeruhi kichwani mfanyabiashara huyo anayemiliki pia mabasi ya Machame Safaris. Hali ya majeruhi huyo inaendelea vizuri.

Polisi Yasema Trafiki Aliyeuwawa Kijitonyama sio Yule Mwenye Mbwembwe

$
0
0
Usiku wa July 22 2016 ilisambaa taarifa ya kupigwa risasi Askari wa kikosi cha usalama barabarani wa kituo cha Polisi Oysterbay Kinondoni Dar es salaam ambapo alipigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni wahalifu wakati akiwa kazini katika eneo la Sayansi Kijitonyama.

Kutokana na mauaji hayo kutokea kwenye eneo la Sayansi taarifa zilizosambaa mitandaoni zilianza kumuhusisha na tukio hilo Askari mwingine wa barabarani aitwae Ashraf ambaye wengi ndio wamezoea kumuona kwenye eneo hilo kwa mbwembwe zake za kukimbiza foleni.

Baada ya kusambaa kwa taarifa kwamba aliyeuwawa ni yule Trafiki mchangamfu kwenye taa za barabarani, kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Simon Sirro kujua ukweli.

Kamanda Sirro amesema aliyeuwawa ni mwingine aitwae Mensah na sio yule Trafiki mwenye mbwembwe (Ashraf Shaban) ambaye amejipatia umaarufu hivi karibuni kutokana na uchangamfu wake barabarani na spidi yake ya kuondoa foleni akiwa kazini.

Gigy Money, Idris Mahaba Niue!

$
0
0
IMEVUJA! Baada ya hivi karibuni penzi la Wema Sepetu na Idris kusambaratika, mwanadada Gift Stanford ‘Gigy Money’ amedaiwa kuchukua nafasi na sasa ni mapenzi motomoto.

Chanzo makini kililiambia gazeti hili kwamba Gigy Money na Idris kwa sasa ni mapenzi motomoto na mwanadada huyo aliamua kutafuta kazi ya utangazaji kwenye Kituo cha Redio cha Choice FM ili amnase Idris ambaye naye ni mtangazaji wa hapo.

gigy na idris (2)“Idris na Gigy Money sasa ni mapenzi motomoto, alimfuata Choice (Choice FM) ili amnase vizuri na kweli amefanikiwa na hata kuachana kwa Idris na Wema kuna chembechembe za yeye kulivuruga penzi lao kwani baada ya kuachana ndiyo mapenzi yamekuwa motomoto sana,” kilisema chanzo.

Hivi karibuni Gigy Money alitundika picha kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram akiwa na Idris huku akisindikizia na maneno kwamba ‘Hainaga ushemeji tunakulaga, leo niweke wazi kabisa jamani huyu ni mume wangu’.

gigy na idris (3)Baada ya kupata habari hizo, Risasi Jumamosi lilimtafuta Gigy Money ili kuupata ukweli ambapo alikuwa na haya ya kusema;

“Idris ameachana na Wema na nilijitahidi kutafuta kazi kwenye redio Choice ili niweze kumnasa vizuri na kweli nimefanikiwa, kiukweli nimejikuta nampenda sana. Sioni tatizo yeye ni mwanaume, mimi ni mwanamke, acha maisha yaendelee,” alisema Gigy.

Jitihada za kumpata Idris aweze kuzungumzia penzi hilo hazikuzaa matunda kufuatia simu yake ya mkononi kuita bila kupokelewa.

Chanzo:GPL

Henry Kilewo:Dar es Salaam ipo Chini ya Chadema/Ukawa, Ndio Maana Analazimisha Serikali Kuhamia Dodoma

$
0
0
Nimesikia Mwenyekiti Mpya wa CCM Taifa ambaye alikuwa anagombea pekee ambaye pia alitangazwa na NEC kuwa Rais akisema atahamishia serikali yake Mkoani Dodoma kutoka Dar es salaam..
Ni kweli ni lazima serikali ihamie Dodoma kwakuwa Dar es salaam ipo chini ya Chadema/Ukawa na siyo CCM ndiyo maana analazimisha ihamie Dodoma.. Mkuu unasubiri nini? Ihamishie kesho maana Dar es salaam imewakataa ccm peleka sehemu ambayo Nec wamewatangaza...

Naelewa kuwa serikali kuhamia Dodoma ilikuwa ni adhima ya Mwl.Nyerere ila lilipouzwa kwakuwa Dar es salaam lilikuwa shamba la Bibi ila kwasasa kwakuwa Dar es salaam imeikataa CCM ni lazima Serikali ihamie Dodoma kama ambavyo imekuwa matakwa ya wengi na kupuuzwa... Tunakwenda kuichukua Dodoma 2020 na ndiyo mwisho wenu.....
Henry Kilewo
Katibu Greater Dsm (Chadema)
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images