Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live

Zitto Utapotea, Achana na Rais Magufuli!!

$
0
0
Namkumbuka Zitto Zuberi Kabwe wa 2005-2010 na ninamlinganisha na huyu wa sasa mmmmhhh hadi inauma sana tukiendelea kupoteza vijana kama huyu wengine miaka ijayo kuna kazi kubwa sana ya kuja kulikomboa taifa hili!!

Nimekuwa nikijiuliza hivi Zitto ni nini kimempata??
Yuko wapi Zitto aliyeibua sakata la mgodi wa Buzwagi?
Yuko wapi zitto aliyekuwa akipigania masilai ya wanyonge bungeni kupitia ununuzi wa Rada??

Zitto aliyeungana na Dr slaa juu ya Richmond yuko wapi??
Zitto huyu huyu anayetuhumiwa kwa kuwa na mali zisizolingana na kipato chake ??
Zitto huyu huyu ambaye milija yake imezibwa pale NSSF?
Zito amekuwa mtu tena wa kupiga dili na kuakikisha kila kitu amekipata kanunua majumba mazuri ,Magari mazuri,kila kitu kamiliki leo hii kabaki na kazi moja tu ya !!

Kila siku kuiponda selikari ya Rais magufuli!!!
Hivi hakuna mazuri ya kumpongeza Rais magufuli ni kumponda tu ? Hata akipongeza anapongeza kwa unafiki!!
Kama kweli Wewe ni mzalendo unapigania masilai ya watanzania njoo ujibu maswali yafuatayo!!

Wewe si dictator??
Na ulivyo dictator ulipofika tu ACT wazalendo ukapewa cheo cha kiongozi mkuu wa chama hivi uoni kwamba ilo ni tatizo la kupenda madaraka?
Kwani kulikuwa hakuna watu wengine mpaka upewe wewe hicho cheo uligombea na nani?

Sasa hivi professor Mkumbo anawashauri wapinzani mbadilishe njia za kupambana na selikari ya Rais magufuli lakini hata ushauri usikii imekuwa sikio la kufa!
Na juzi tu mama Anna ametofautiana na wewe waziwazi kuusu mwaliko uliotolewa Dodoma !!

Mbili kwanini uliondoka chadema kwa kutaka uwe mwenyekiti uoni hapo kuna tatizo la udikiteta kutaka cheo kwa nguvu? Kwanini ukusema wazi wazi ila ukaanzisha mtandao ndani ya chama?

Ulishamsikia magufuli anagomea cheo ndani ya chama toka amejiunga na CCM hata cha mwenyekiti wa shina??
Leo hii unatoka na kumfananisha rais magufuli na Putin wa Russia hivi hoja yako ya Jana kwamba watu wamsome Putin ina faida gani kwa taifa?

Kuna faida gani kwa wananchi wa Ujiji??
Hivi unafikiri wananchi wa vijijini wanaweza kaa wasome vitabu au wapekue Internet kwa vifulushi vipi hivi hivi vya wanyonyaji Voda,Tigo na Airtel?
Baada ya kuishauri selikari ilifufue shirika letu la TCCL ili tupate affordable bundle wananchi waweze kupata Internet ilivyo bora na kuepukana na makampuni ya wanyonyaji upo tu kukosoa !!

Mkuu Zitto tulikuheshimu sana lakini sasa your politically finished!!
Baada uungane na Magufuli mpeleke kiwanda cha nyavu za kuvulia Dagaa ujiji ??unaangaika eti wananchi wamsome Putin Hivi mwananchi wa kawaida wa ujiji atakuelewa kweli??


Kwanza tu nikufaamishe taarifa nyingi unazozisoma kwenye mitandao kuusu Putin kama hazitoki Russia ni za kupika kutoka nchi za magaribi!!
Nchi za magaribi hazimpendi Putin kwa sababu analeta mabadiliko ya kweli uko Russia!!
Ni kiongozi imara asiyeteteleka kama alivyo Magufuli hivyo vyombo vya habari vya magaribi haviwezi kumpamba hata kidogo Putin ni kiongozi imara kama alivyo Magufuli!!

Ushauri kwako kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo!!
Watu unaotakiwa kubishana nao ni Mkuu wa mkoa Kigoma,Mkuu wa willaya jimboni kwako,Mkurugenzi jimboni kwako na spika wa ubunge Hao ndio size yako!! Hakuna mtu anayeupata Urais kwa kumponda Rais aliyeko madarakani hapa Afrika nikukumbushe lazima tuambiane ukweli!!

Tanzania- Professor Lipumba aliponda ameenda,
Kenya-Raila Odinga aliponda huyo anakwenda,
Uganda-Kiza Besige aliponda anakwenda,
Zimbabwe- Morgan Shangelai aliponda amekwenda !!

Mifano ipo mingi tu ila nikushauri pigania masilai ya wananchi wako wa ujiji na Tanzania!!
Nasikitika tunapoteza nguvu kazi za Taifa hasa vijana tuliokuwa tunawategemea wanatoweka taratibu.

Asanteee.

By technically/JF

Madai: Aliyemuweka Mbongo rehani akamatwa!

$
0
0

Mtanzania aitwaye Juma (jina lake la pili tunalihifadhi kwa sababu maalum) anayedaiwa kumuweka rehani ughaibuni Mbongo mwenzake Adam Akida Mwinyimkuu, mkazi wa Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam ambaye ametekwa na kushikiliwa na watu wanaoaminika kuwa ni ‘Wazungu wa Unga’ , amekamatwa na polisi jijini Dar.


Uchunguzi wa kina uliofanywa na waandishi wetu wiki iliyopita umebaini kuwa, Juma alikamatwa na polisi mwishoni mwa wiki iliyopita Tegeta na anahojiwa kuhusiana na kutuhumiwa kumuweka dhamana kijana Adam kisha kumtelekeza ughaibuni huku ikidaiwa kuwa yeye alikuja na shehena ya unga.

Habari zinasema ili Adamu awe huru, Juma anatakiwa kupeleka fedha shilingi trilioni moja ambazo ni gharama ya unga aliopewa, huku akimfanya mwenzake huyo kuwa ‘bond’ ya mzigo huo haramu.

“Fedha anazodaiwa Juma ni nyingi ni shilingi trilioni moja. Ni kwamba mzigo wenyewe (unga) hakufanikiwa kuuza kwani alikamatwa na askari wakamnyang’anya na sasa sijui atafanya nini ili kumuokoa mwenzake aliye ughaibuni,” kilisema chanzo chetu.

Habari zaidi zinasema kuwa licha ya Juma kuwa korokoroni, baba wa Adamu mzee Akida Mwinyimkuu naye alishikiliwa kwa muda na polisi katikati ya wiki iliyopita lakini hakuwa na msaada wowote kwa vyombo vya dola.

“Mzee Akida alikamatwa na polisi lakini badala ya kusaidia akawa anapotosha ukweli. Yeye aliwaambia polisi kuwa mtoto wake Adam hakwenda Pakistani bali alikwenda Afrika Kusini na ndivyo anavyojua. Alipooneshwa video ya mwanaye akiwa chini ya ulinzi, alishangaa na hakuwa na la kusema,” kilisema chanzo chetu.

Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, SACP Mihayo Msikhela (pichani) alipoulizwa na gazeti hili kuhusu kukamatwa kwa mzee Akida na Juma hakukiri wala kukataa.

“Unajua hili jambo bado lipo kwenye uchunguzi, hatuwezi kusema chochote hadi tumalize uchunguzi wetu lakini wote wanaotuhumiwa tunawasaka na tukiwakamata tutawahoji. Tukimaliza upelelezi wetu tutatoa taarifa kwa umma,” alisema kamanda huyo.

Source: Global Publisher

Breaking News: Kambi kuu ya Amisom yavamiwa Mogadishu

$
0
0

Washambuliaji wa kujitoa mhanga wameshambulia kambi kuu ya wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika (AU) mjini Mogadishu.

Milipuko miwili mikubwa imesikika karibu na lango la kambi hiyo ifahamikayo kama Halane na baadaye kukatokea ufyatuaji wa risasi.

Makao makuu ya wanajeshi hao yamo karibu na uwanja wa ndege wa Mogadishu, eneo ambalo pia lina afisi nyingi za ubalozi za mataifa ya Magharibi na Umoja wa Mataifa.

Mlipuko wa kwanza ulipasua vioo vya majumba katika uwanja wa ndege.

Taarifa zinasema mshambuliaji wa kwanza alilipua bomu lililotegwa kwenye gari na wa pili akajaribu kuingia ndani ya kambi hiyo kwa miguu lakini akapigwa risasi na akalipuka akiwa karibu na lango.

Kundi la al-Shabab limedai kuhusika, na kusema watu zaidi ya 12 wameuawa kwenye shambulio hilo. Msemaji wa kundi hilo ambaye ametambuliwa kama Abdiasis Abu Musab amesema washambuliaji wote wawili walilipua mabomu ya kutegwa kwenye magari.

TCU yakanusha taarifa za kuvifungia udahili wa kozi tofauti vyuo 22 zilizozagaa juzi

$
0
0

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imewatoa hofu wanafunzi waliohitimu katika vyuo vilivyozuiwa hivi karibuni kufanya udahili, huku ikikanusha taarifa za kuzifungia udahili wa kozi tofauti vyuo 22 zilizozagaa juzi.


Hivi karibuni TCU ilitangaza kusimamisha kufanya udahili  vyuo vitano baadhi vikiwamo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo Kikuu cha Mtakatifu Francis cha Ifakara Morogoro, Chuo cha Mtakatifu Joseph cha Dar es Salaam na Chuo cha IMTU cha Dar es Salaam vyote kwa kozi ya udaktari.


Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana, Kaimu Katibu Mtendaji wa TCU, Eliuther Mwageni alisema kufungiwa kwa vyuo hivyo ni kwa muda mpaka vitakapokabidhi vigezo vinavyotakiwa.


"Kuna vigezo vinavyotakiwa kufikiwa ili chuo kiweze kusajiliwa  na hivi vyuo hatujavifungia ila tumevisimamisha kwa muda mpaka vikidhi vigezo vyetu.


Kuhusu taarifa za vyuo 22 kusimamishwa kudahili wanafunzi katika kozi mbalimbali zilizozagaa kwenye mitandao juzi na jana, Mwageni alisema taarifa hizo ni za uzushi, zina lengo baya hivyo hazina ukweli wowote.

Afande Sele afunguka adai hakuna rapper zaidi yake

$
0
0
Rapper wa Morogoro, Afande Sele amesema hadi sasa hajapatikana rapper mbadala wake anayeweza kuifanya hip hop kwa mwelekeo aliokuwa nao yeye.

Amesema amegundua hilo hata kwenye mitandao ya kijamii ambapo licha ya kuongelea vitu vingine, bado mashabiki wanamuuliza kuhusu lini atarejea tena na kudai kuwa hiyo inamaanisha kuwa mbadala haujapatikana.

“Ina maana mpaka sasa hivi hawajapata mbadala, wasanii wengi wanatoka lakini hawana uimbaji wa aina yangu ndio maana wanataka nitoke mimi mwenyewe,” amesema.

Afande ambaye mwaka jana aliingia kwenye siasa na kugombea nafasi ya uongozi kupitia tiketi ya chama cha ACT- Maendeleo, amemweleza mtangazaji wa Jembe FM, JJ kuwa muziki wa sasa umekuwa rahisi sana kuliko zamani.

“Kipindi hiki muziki umekuwa mwepesi watu hawafikiri, hakuna challenge ndio maana watu wanataka wamuone Afande Sele akija upya, wamuone Profesa, wamuone Jay Moe akija upya.”

Afande amedai kuwa kwenye kazi zake zijazo amewashirikisha Linex na Bonta na kwamba ana wimbo uitwao Kisu ambao amepanga kumshirikisha Alikiba.

Raymond: ‘Natafuta Kiki’ inakwamishwa na wasanii niliowataja katika wimbo

$
0
0
Msanii wa muziki kutoka WCB, Raymond aka RayVanny ameitaja sababu kubwa ya kuchelewa kwa video ya wimbo wake ‘Natafuta Kiki’ kuwa ni baadhi ya wasanii aliowataja kwenye wimbo huo kushindwa kuonesha ushirikiano.

Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Clouds E cha Clouds TV kuwa baadhi ya wasanii aliowataja kwenye wimbo wake ‘Natafuta Kiki’ wamekuwa wagumu kupatikana.

Aidha Raymond ameongeza kuwa menejimenti yake ilimleta director kutoka nje lakini baada ya baadhi ya wasanii kushindwa kuonesha ushirikiano wakamruhusu kurudi kwao kwanza.

Kutokana na mashabiki wengi kuwa na hamu ya kuiona video ya wimbo huo, Raymond ameachia video ya wimbo huo ikiwa ni Guitar Version. Hata hivyo Raymond amedai video hiyo itafanyika japo hajataja itachukuwa muda gani.

Ufafanuzi kuhusu ile pikipiki iliyopakizwa kwenye basi la mwendokasi

$
0
0
Baada ya picha iliyosambaa ikionyesha pikipiki iliyokuwa ndani ya basi liendalo kwa haraka jijini Huu hapa ufafanuzi kama jambo hili linaruhusiwa.

Afisa habari wa UDART, Deus Bugaywa, ametoa ufafanuzi huo na kusema….

Tumefuatilia iliingia wapi? kwa sababu gani na mahali gani? tunadhani picha itakuwa imetengenezwa kwa sababu tumefuatilia kwenye vituo vyetu na ni jambo ambalo haliruhusiwi kabisa na hakuna namna kwamba utabeba pikipiki au baiskeli yako ya kawaida isyo ya mlemavu unasafirisha mle ni jambo ambalo haliwezekani kabisa’

Koffi Olomide Akamatwa Nyumbani Kinshasa

$
0
0
Mwanamuziki maarufu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC amekamatwa akiwa nyumbani kwake mjini Kinshasa.

Wiki iliyopita Olomide alitimuliwa kutoka nchini Kenya baada ya video kuonyesha akimpiga teke mnenguaji wake wa kike katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta baada yake kuwasili nchini humo.

Lengo la ziara ya Kenya alipangiwa kutumbuiza mashabiki wake Bomas of Kenya siku ya Jumamosi lakini tamasha hiyo lilifutwa na mamlaka.

Koffi amekamatwa kwa agizo la mwendesha mashtaka huku kukiwa na matamshi ya wanaharakati wa haki za kibinadamu wakitaka afunguliwe mashtaka kufuatia kitendo chake cha kumpiga ‘stage show’ wake.

Aidha baada ya show ya Kenya kusitishwa alikamatwa na maafisa wa polisi na siku iliyofuata asubuhi akaingizwa kwenye ndege na kurejeshwa Kinshasa.

Chanzo BBC.

Hatimaye Petitman 'atubu' kwa Esma Platnumz

$
0
0
Utata uliokuwepo kati ya wapenzi wawili Petitman na mama watoto wake umekwisha baada ya vuta nikuvute ya familia hizo mbili. Mama mzazi wa Petitman amewahi kusikika akisema kuwa hamtaki Esma kuwa mkwe wake kutokana na vitendo vyake.

Pia walakini mwingine wa mapenzi haya ulikuwa mgumu pale Madam Wema Sepetu alipotengana na Diamond Platnumz kipindi kile na kupelekea kukosa ushirikiano kwa kutokea makundi mawili kati ya Petiti na madam na upande wa Diamond Platnumz na mdogo wake Esma

Wadau wengi wanasema kurudiana kati ya Petitman na mdogo wa Diamond ni kwa sababu sasa hivi Petit hayupo tena na Wema kitendo kilichomfanya Esma kurudiana kiurahisi na baba watoto wake kwa kuwa hakukuwa na kipingamizi tena.

Hata hivyo Petitman usiku wa juzi mbele ya camera za eNewz na umati wa watu alisema “sioni haja ya kuendelea kuchepuka na wanawake wengine kwa kuwa nimeona kuwa na mademu wengine ni kujipa stress tu, kwa kifupi nimezima simu feki na nimerudiana na mzazi mwenzangu ili tuweze kumlea mweznetu kwa pamoja”.

Kutana na Mtandao Mpya wa Kijamii Kwa Ajili ya Kukuza Secta ya Utalii Tanzania 'EZYLINC '

$
0
0
Ezylinc ni mtandao mpya wa kijamii, ambapo watu binafsi na makampuni wanaweza kuweka
picha na kuandika makala kuhusu vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Mtu yeyote anaweza kujiunga na mtandao huu wa kijamii bure kabisa kwa kujisajili
www.ezylinc.com , baada ya hapo anaweza kuweza picha, kuandika makala kuhusu vivutio vya
utalii, kutengeneza magroup, kukutana na marafiki wengi zaidi kutoka sehemu mbalimbali
duniani na mengine mengi.

Ezylinc inaunganisha makundi mawili. Upande mmoja tuna watalii, na kwa upande mwingine
watu wanaofanya kazi zinazoendana na shughuli za kitalii.

Hapa Tanzania kama mfano, utalii ni sekta inayoliingizia taifa fedha nyingi za kigeni. Katika mwaka
2014 sekta ya utalii, imechangia asilimia 17 katika pato la taifa na kuchangia kwa asilimia 25 ya
mapato yote ya fedha za kigeni, ambapo bilioni 2 za Kimarekani zilipatikana.

Tanzania ni nchi yenye vivutio vingi vya utalii katika bara la Afrika. Kilimanjaro mlima mrefu kuliko
yote Africa, Visiwa vya Zanzibar, hifadhi za taifa za Serengeti na Ngorongoro, Tarangire, Ziwa
Manyara, Ruaha na Selous, ni mifano hai michache ya vivutio vinavyopatikana Tanzania.

Kwa kutumia mtandao huu mpya wa kijamii tunaweza kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini
kwetu kwa urahisi zaidi, na kupata watalii wengi zaidi.

Hii ni moja ya sababu kubwa kutengeneza mtandao mpya huu wa kijamii. Tunalenga kusaidia
ukuaji zaidi wa sekta ya utalii nchini, na hiyo itasaidia watu wengi zaidi kupata ajira katika shuguli
zinazoendana na sekta hii.

Karibu - Kujiunga Ezylinc, Ingia: www.ezylinc.com

TAMASHA La Mwendokasi Festival Kuliteka Jiji la Dar es Salaam Jumamosi Ijayo Tarehe 30 July 2016

$
0
0
Tarehe 30 Mwisho wa mwezi huu wa saba Tanzania kushuhudia mapinduzi ya kiburudani. Tamasha Kubwa la MWENDOKASI FESTIVAL linatarajiwa kufanyika katika Viwanja vya Postal Kijitonyama, Wasanii Wakubwa Mbali mbali wa Bongo Flava watatoa burudani kali mbele ya maelfu ya wakazi wa Dar es salaam , Baadhi ya wasanii ambao watakuwepo ni

  1.  Navy Kenzo,
  2.  Ally Kiba, 
  3. Christain Bella
  4. Roma, 
  5. ManiFongo,
  6.  Snura, 
  7. Gnako, 
  8. Isha Mashauzi, 
  9. SautiSol, 
  10. Mr Blue, 
  11. Nuh Mziwanda, 
  12. Barnaba 
  13. Adamu Mchumvu
  14. Quick Rocka
  15. Juma Nature
  16. Nay wa Mitego
  17. Rucky Beby
  18. Dj D Ommy na wengine
Katika tamasha hilo patakuwa na sehemu ya kawaida ambapo kiingilio kitakuwa ni 10,000/= kwa Mtu mmoja,

Kutakuwa na sehemu maalumu ya VIP ambapo Kiingilio kitakuwa 100,000/= kwa watu wawili

Pia Kutakuwa na Sehemu maalumu kwa ajili ya VVIP ambapo Kiingilio ni 500,000/= Kwa watu wanne

Tickets zitaanza kuuzwa soon katika vituo mbali mbali ambapo tutawatajia muda si mrefu...

Usikose Mtu Wangu ...Ni pale Viwanja vya Posta Sayansi Kuanzia Saa nane mpaka Kuchweeee

Mwanaume Anaye Wabikira Watoto Kwa Kulipwa Malawi..Akamatwa Baada ya Kugundulika ana Ngoma

$
0
0
Eric Aniva aliyeripotiwa wiki iliyopita huwa huingiza fedha kwa kazi ya kuwabikiri wasichana nchini Malawi amekamatwa na polisi nchini humo.

Aniva ambaye ni maarufu kwa jina la Fisi, hulipwa kiasi cha dola 7 na wazazi wa kabila moja huko nchini Malawi kwa ajili ya kuwabikiri watoto wao wa kike wakiamini kuwa mtoto wa kike kuwa na bikira na mkosi.

Baada ya taarifa hiyo kuruka kupitia BBC, Rais wa Malawi, Peter Mutharika kupitia kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu ya nchi hiyo, Bright Molande aliamuru raia huyo akamatwe kutokana na vitendo hivyo vya uzalilishaji kwa watoto wa kike.

“And since Mr. Eric Aniva confesses to be HIV positive and that he never uses protection in his evil acts against the innocent girls and women, he should further be investigated for exposing the young girls to contracting HIV and further be charged accordingly,” alisema rais Mutharika.
“These practices not only cast a shadow on the hard-earned achievements my Government has made on issues such as violence and HIV prevention but they also go against a vision of development that seeks to ensure that the youth (and in particular young girls), are able to achieve their full potential.”
“Furthermore, these horrific practices although done by a few also tarnish the image of the whole nation of Malawi internationally and bring shame to us all,” aliongeza.
“ Children, girls and women must be cared for, protected and provided every opportunity to survive peacefully and become productive citizens.”

Aniva anakadiriwa kuwabikiri zaidi ya watoto wa kike 104 lakini kubwa zaidi amegundulika kuwa na virusi vya ugonjwa ukimwi na haijulikani ni watoto wangapi tayari amewaambukiza virusi hivyo.

Msanii wa Filamu Gabo Zigamba na Faiza Ally Wasemekani ni Wapenzi..Gabo Afunguka

$
0
0
Msanii wa filamu Gabo Zigamba, amefunguka kwa kusema kuwa hana mahusiano yoyote na msanii mwenzake wa kiwanda cha filamu Bongo, Faiza Ally.

Muigizaji huyo ambaye hivi karibuni amefanikiwa kushinda tuzo ya mwigizaji bora wa kiume kwenye tamasha la Ziff 2016, ameiambia Times FM kuwa hakuna mahusiano yoyote ya kimapenzi yatakayotokea kati yake na Faiza.

“Faiza namjua kama producer wangu, amenishirikisha kwenye filamu yake ya Baby Mama Drama. Hakuna chochote wala hayatotokea mahusiano ya kimapenzi kati yetu,” amesema Gabo.

Kikwete: Nashukuru Mungu Kwa Kuutua Mzigo Salama Huku Nikiiacha Nchi Ikiwa Salama Tulii Kabisa

$
0
0
MWENYEKITI Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt.Jakaya Kikwete amesema anashukuru Mungu Kwa kuutua mzigo salama huku akiicha nchi ikiwa salama tulii kabisa.

Amesema kuwa safari yake ya urais ilianzia Bagamoyo akitokea wilayani hapo ambapo baada ya hapo alikwenda Kibaha kutangaza nia ya kugombea urasi nakudai kuwa amejisikia furaha kurudi tena Bagamoyo akiwa salama.

Amesema wakati akielekea kutangaza nia ya kugombea urais alikuwa na mtoto wake Ridhiwani Kikwete ambapo yeye alikuwa anaandika na Ridhiwani anachapa kwenye Komputa.

Dkt.Kikwete aliyasema hayo jana wilayani Bagamoyo katika hafla ya kumkaribisha Nyumbani baada ya kuitumikia nchi Kwa miaka mingi, ambapo iliandaliwa na Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani.

Alisema anashukuru Kwa Mara nyingine kurudi mahala alipoanzia na kwamba amemaliza salama na ameacha nchi ikiwa salama na imetulia tulii kama Maji kwenye mtungi.

Akikumbuka mchakato wa mwaka jana wa kumpata Mgombea ulikuwa na mambo mengi lakini mambo yalikwenda salama na hakuna lililokuwa limeharibika .

"Ilikuwa Kazi kubwa si ndogo lakini hatimaye wa kavuka na wakaingia kwenye uchaguzi ambao ulikuwa na vurumai" alisema Dkt.Kikwete .

Aidha alisema kuwa hata hivyo katika uchaguzi huo kulikuwa hakuna mtu ambaye alipatwa na tukio la kumpiga mwezake hali ambayo iliwashangaza hata nchi jirani.

Alisema kuwa katika kipindi chake cha uongozi amefanya kazi kubwa ya kusukuma maendeleo ya wananchi Kwa mikoa yote,wilaya zote bila ubaguzi wowote ule huku akikiri kukabiliana na Changamoto ya kunyoshewa vidole hususani pale alipojaribu kupeleka maendeleo Wilayani Bagamoyo kanakamba wananchi wa Bagamoyo walikuwa hawana haki.

Aidha Dkt.Kikwete alisema kuna wakati alisimamisha fedha za ujenzi wa barabara hiyo na kupeleka fedha hizo kujenga barabara ya Geita, Sengerema,usagala ,na kulizuka na Maneno mengi dhidi yake na hadi kufikia wabunge kulumbana.

Alisema hata hivyo anashukuru kwamba amemaliza salama na Kwa bahati nzuri amepatikana rais ambaye ana ari kubwa ya kuwaletea maendelea watu huku akitaka watanzania kumuunga mkono.

Koffi Olomide akamatwa DR Congo na Kuhukumiwa Kifungo

$
0
0
KINSHASA, CONGO: Mahakama imemhukumu Mwanamuziki Koffi Olomide, miezi 18 jela kwa kumpiga mnenguaji wake wa kike wiki iliyopita.
Hukumu yake hiyo haina adhabu mbadala ya kulipa faini kwa hiyo kutumikia hiyo miezi 18 jela

Mwanamuziki wa Kenya Avril Apangua Tuhuma za Kutoka Kimapenzi na Diamond Platnumz

$
0
0
Msanii wa muziki kutoka nchini Kenya, Judith Mwangi 'Avril' ambaye alicheza kama video queen kwenye wimbo wa Diamond Platnumz 'Kesho' amefunguka na kusema hakuwahi kutoka kimapenzi na Diamond Platnumz kama ambavyo baadhi ya watu walivyokuwa wakidhani

Msanii Diamond Platnumz akiwa na msanii kutoka Kenya Avril.
huenda kuwa Diamond Platnumz baada ya video hiyo labda alitumia nafasi hiyo kutoka naye kimapenzi.

Avril kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio alisema kuwa yeye na Diamond Platnumz hawakufanya project nyingine yoyote zaidi ya kutengeneza video ile ya 'Kesho' japo alimuelezea Diamond kuwa ni msanii mpole sana na mwenye kupenda kazi yake na kujituma.

"Diamond ni rafiki yangu ni mtu poa sana, tumejuana kwa muda mfupi lakini ni msanii mwenye bidii ya kufanya kazi na kukutana na msanii mwenye bidii ni jambo zuri, hi mtu mzuri mpole hana maneno na watu. Najua vyombo vya habari vinampa sifa nyingi tofauti na yeye lakini ukikutana na yeye moja kwa moja ni mtu mzuri sana. Baada ya kufanya ile video ya kesho hakuna project nyingine tulifanya" alisema Avril

Mbali na hilo Avril alitaja wasani watano kutoka Tanzania ambao anawakubali na kuanza na Diamond Platnumz, Ommy Dimpoz, Raymond, Vanessa Mdee pamoja na Linah Sanga.

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya July 27

$
0
0



SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya July 27

Zitto na Maalim Seif walivyokutana kwenye mkutano Marekani

$
0
0
Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe na katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad wamekutana Katika Mkutano Maalum wa Viongozi wa Kisiasa Ulimwenguni (International Leaders Forum) ambao umefanyika jana  ‘Kwa Saa za Marekani’ Jijini Philadelphia.

Mkutano huo ulioandaliwa na asasi ya NDI ‘National Democratic Institute’, ni Sehemu ya matukio maalum kuelekea Mkutano Mkuu wa Chama Cha Democrats (Democratic National Convention), Mkutano ambao utamthibitisha Bibi Hillary Clinton Kuwa Mgombea Urais Kupitia Chama Hicho.

Zitto Kabwe Pamoja Na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim watakuwa Philadelphia mpaka Siku ya alhamis ambapo  mkutano huo unategemewa kumuidhinisha Bi Hillary Clinton Kuwa Mgombea Urais wa Marekani kupitia Chama Hicho.

WEMA SEPETU Avunja Record Nyingine Bongo Awa Mwanamke wa Kwanza Kufikisha Followers Mil 2 Instagram

$
0
0
Baada ya Mwanamuziki Diamond Platnumz Kuvunja Record ya kuwa msanii wa kwanza kufikisha wafuasi Million mbili kwenye Instagram Africa Mashariki , sasa Wema Sepetu nae amekuwa mwanamke wa kwanza kufikisha idadi hiyo ya followers million 2 kwenye mtandao wa Instagram,


Afrika Kuongezewa Nafasi 2 zaidi Kombe la Dunia

$
0
0
Bara la Afrika litatunukiwa nafasi nyengine mbili zaidi iwapo dimba la dunia litaongeza idadi ya mataifa yanayoshiriki hadi 40 kuanzia mwaka 2026 kulingana na rais wa FIFA, Gianni Infantino.

Infantino alipendekeza kuongezwa kwa timu hizo kabla ya kuchaguliwa kwake na shirikisho hilo la soka duniani. Kwa sasa Afrika ina nafasi tano pekee katika michuano hiyo .

“Pendekezo langu limekuwa timu 40 na iwapo hilo litadhinishwa pendekezo langu ni kulipatia bara la Afrika nafasi mbili zaidi,” alisema Infantino.

Hata hivyo hatua hiyo itaidhinishwa hadi mwaka 2026 huku timu 32 zikiwa tayari zimethibitishwa kushiriki katika kombe la dunia la 2018 nchini Urusi na 2022 nchini Qatar.

Source: BBC
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live




Latest Images