Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

MO Kukabidhiwa Simba SC Hali Bado Tete

$
0
0
Baada ya mkutano mkuu wa klabu hiyo uliofanyika leo katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oyesterbay, ambao ulikuwa na ajenda 10, moja kati ya ajenda hizo ilikuwa ikizungumzia taarifa ya kamati ya maboresho ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo.

Katika ajenda hiyo ndipo lilipojitokeza suala zima la MO ambapo wanachana hao wa Simba zaidi ya 700 waliojitokeza kwenye mkutano huo walitaka bilionea huyo apewe timu hiyo kutokana na hali mbaya ya kiuchumi iliyopo klabu hapo ambapo imekuwa ikijiendesha kwa hasara kila mwaka.
Katika msimu wa 2014/15 klabu hiyo ilifanikiwa kujikusanyia Sh bilioni 2, 096, 721, 493  kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali vya mapato lakini ikatumia Sh bilioni 2,101,100,303 na kujikuta ikidaiwa 4, 378,810.

Lakini pia katika bajeti yake ya msimu ujao wa 2016/17 uongozi huo unatarajia kukusanya kiasi cha Sh bilioni 3, 583, 000,000 kutoka katika vyanzo vyake vya mapato lakini matumizi yake yanatarajiwa kuwa Sh bilioni 4, 411,025, 000, hivyo itakuwa ikidaiwa Sh milioni 828, 025, 000.

Kutokana na hali hiyo wanacha hao waliutaka uongozi huo, kukubali kumpatia Mo timu  kwani wanataka mabadiliko na wamechoshwa na hali hiyo ya ukata wa kila wakati ambao umekuwa ukiwatesa na kuwakosesha amani kila siku.

Hata hivyo uongozi wa klabu hiyo chini ya rais wake, Evans Aveva haukuwa tayari kufanya hivyo licha ya kelele za wanachama hao ambao kila wakati walikuwa wakiimba na kulitaja jina la MO.

MICHEZO Bilionea anayetaka kuinunua Simba, ametaja kilichomsikitisha katika mkutano wa Simba

$
0
0
Siku moja baada ya mkutano mkuu wa Simba kufanyika na kukubali kupitisha maadhimio ya mabadiliko ya kiuongozi ili klabu iendeshwe kwa mfumo wa hisa, bilionea wa 21 Afrika ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) Mohammed Dewji ameelezwa kusikitisha na taarifa za upotoshwaji.

Mohammed Dewji amesikitishwa kutokana na taarifa zilizotolewa katika mkutano mkuu Simba uliofanyika jana July 31 2016, kuwa yeye ambaye aliomba kununua asilimia 51 ya hisa za Simba kama mfumo ukibadilishwa, hajaandika barua kwa uongozi wala kukutana nao ila amekuwa akiongea kupitia vyombo vya habari kitu ambacho sio kweli.

“Kiukweli nimesikitishwa kwa wanaosema dhamira yangu ya kutaka hisa Simba nimeomba kupitia vyombo vya habari na wala sijaandika barua, ukweli nimekutana na Rais wa Simba Evans Aveva zaidi ya mara tatu, ameshakuja ofisi kwangu zaidi ya mara tatu”

“Kuhusu kuandika barua nilikuwa sijaandika kwa sababu mfumo wa hisa niliokuwa nahitaji ulikuwa haupo sasa utaombaje kitu ambacho hakipo, ila leo baada ya mkutano mkuu kukubali nimeandika barua rasmi kwenda kwa uongozi wa Simba na tayari tumeshaituma”

Mbowe: Mpango wa kuhamia Dodoma ni wa kukurupuka

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema hakitotekeleza mpango wa kuhamia Dodoma kwani ni wa kukurupuka.

Msimamo huo umetolewa jana na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alipozungumza na gazeti hili wakati wa kutoa heshima za mwisho za aliyekuwa mpigapicha mwandamizi wa gazeti la Tanzania Daima, Joseph Senga ambaye anatarajiwa kuzikwa leo huko Kwimba, Mwanza.

“Serikali inaendeshwa kwa kukurupuka. Ni mpango usiotekelezeka,” alisema Mbowe.

Alisema uhamaji unaotekelezwa sasa haukuwa na maandalizi wala mkakati kwenye ilani ya chama tawala wala Bajeti ya Serikali hivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kukwama huko mbele.

Miongoni mwa vitu vinavyoufanya mpango huo usitekelezeke kwa ufanisi, kwa maoni yake, alisema miundombinu ya kutosheleza watendaji wote na wadau wengine muhimu ambao watalazimika kufuata huduma muhimu za wizara na idara za Serikali.

“Huku ni kuwaumiza wananchi. Watumishi wa Serikali, wanahabari na wadau wengine wakihama wote watapata wapi malazi katika mji ule?”

Muda mfupi baada ya kukabidhiwa majukumu ya kuiongoza CCM, Julai 23, Rais John Magufuli alieleza nia yake ya kutekeleza uhamisho wa makao ya Serikali kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma na kwamba atahakikisha, ndani ya miaka minne anatimiza ndoto hiyo ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ya tangu mwaka 1973.

Siku moja baadaye, akihutubia kwenye hafla ya Siku ya Mashujaa mjini Dodoma, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alitangaza kuhamia mjini humo Septemba na kusema kuwa wizara nyingine zitamfuata.

Tangu kutolewa kwa matamko hayo ya viongozi waandamizi wa Serikali; wizara, taasisi, mashirika ya umma, idara na baadhi ya ofisi binafsi, mabalozi na wanadiplomasia zimeanza kuandaa mazingira ya utekelezaji huo.

Lakini, Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni alionyesha wasiwasi wake juu ya umakini wa Serikali kutekeleza azma hiyo akisema kutakuwa na usumbufu mkubwa kwa watumishi na familia zao suala linaloweza kupunguza morali yao ya kazi. “Watu wana familia zao. Watoto wanasoma... Dodoma hakuna shule za kutosha watoto watakaohama na wazazi wao.”

Alisema wakati wazo hilo linatolewa na kuungwa mkono enzi za Mwalimu Nyerere kulikuwa na sababu za msingi lakini hivi sasa kuna mabadiliko makubwa yaliyochagizwa na maendeleo ya sayansi na teknolojia. Alisema wakati huo mindombinu ya mawasiliano haikuwa rafiki tofauti na iliyopo sasa inayowezesha watu walioko New York, Marekani kufanya mkutano na wenzao waliopo popote duniani kwa kutumia miutano kwa njia ya masafa. “Sababu zimepitwa na wakati,” alisisitiza.

Alishauri, mpango huo ungetekelezwa kwa utaratibu maalumu, akitoa mfano kwa wizara moja au mbili kuhama kwa kila mwaka mpaka zitakapokamilika ili kupunguza gharama zisizo na ulazima.

Alisema kuhamisha wizara siyo waziri au katibu mkuu pekee, bali ni watumishi wote na miundombinu yote iliyopo ambayo ni muhimu kwa utekelezaji wa majukumu yake: “Kwa mfano, Wizara ya Kilimo ina watumishi 2,000 na maelfu ya mafaili yenye taarifa za kiutendaji… unawahamishaje watu wote hawa na mindombinu iliyopo unaifanyaje? Namshangaa IGP anaposema anahama wakati mifumo yote ya uchunguzi na taarifa imejengwa hapa kwa kutumia mabilioni ya fedha za wananchi.”

Wiki iliyopita, Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Polisi, Nsato Marijani alisema jeshi hilo litahamia Dodoma mwezi huu na watakaohusika ni Inspekta Jenerali na baadhi ya makamishna.

Chanzo: Mwananchi

Article 7

$
0
0
MWENYEKITI wa Yanga, Yusuf Manji, amevunja ukimya na kusema Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Jerry Muro yupo huru na anaendelea na kazi zote za klabu kama kawaida.
Manji ameliambia Championi Jumatatu kwamba, klabu hiyo haina taarifa yoyote rasmi ya kufungiwa kwa Muro.
“Kama taarifa tumesikia kwenye magazeti na redio, kweli taasisi kama Yanga, msemaji wake anasimamishwa kwa njia hiyo?
“Hao waliomsimamisha pia ni taasisi, vipi wafanye hivyo. Yanga tunawezaje kuamini hilo? Muro bado yuko kazini na anaendelea na shughuli zake kama kawaida,” alisema Manji.

Kenya :Mchungaji awapachika mimba wasichana 20

$
0
0
Nchini Kenya amewapachika mimba wasichana 20.
Mchungaji huyo amesema hiyo ni Baraka amewasambaza wanadada hao.
Chanzo :CRI kiswahili

Shetta asema ushindani uliopo kwenye muziki umemfanya aogope kutoa ngoma mbaya

$
0
0
Hit maker wa wimbo ‘Namjua’ Shetta amefunguka kwa kusema kuwa yeye ni mmoja kati ya wasanii ambao hawajawai kutoa ngoma mbaya katika maisha yake ya muziki.
prima

Akiongea na Bongo5 Jumapili hii, Shetta amesema biashara ya muziki imefanya afanye muziki wa kushindana kila siku ndio maana kila akitoa ngoma anahakikisha ni kali.

“Shetta sasa hivi ni mfanyabiashara, muziki wangu ni bidhaa adimu ndio maana mimi sijawai kutoa ngoma alafu isifanye vizuri, ni hit baada ya hit na ndo maisha yangu kwa sasa, na nitaendelea kufanya hivyo,” alisema Shetta.

Rapper huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kubiria surprise ya wimbo wake mpya baada ya ‘Namjua’ kufanya viruri.

Huyu Ndio Mwanamke Anayemuumiza Kichwa Zari Hassan wa Diamond Kwa Sasa...Check Video

$
0
0
Hamisa Mobeto Kwa sasa amekuwa Kirusi Kwenye Penzi la Mwanamuziki Diamond na Zari Hassan Hasa tetesi zinazosema Kuwa anatoka kimapenzi kwa siri na Diamond....
Leo Ametupostia hii Video kwenye page yake ya Instagram
Angalia Video Hapa chini:

Baraka Da Price na Najma Watupia Video Wakifanya Yao Kitandani..Video Hii Hapa

$
0
0
Penzi kati ya Baraka da Prince linazidi kuwa Gumzo mitandaoni Baada ya Jana Baraka Kuposti Video Akifanya yake Kwa Najma Huku Naj Akiwa katika Usingizi mzito
Nimekuwekea Video Hapa Chini:


Mbowe na CHADEMA, Lini Mtatuomba Radhi Watanzania Kuwa Mlidanganya Lowassa sio Fisadi

$
0
0
Ndani ya miaka nane na zaidi wananchi tumeimbishwa na kuaminishwa usiku na mchana kuwa Lowasa ni Fisadi mkubwa wa uchumi wa Tanzania.

Na mbaya zaidi mkasema mnaushaidi wa ufisadi wa Lowassa kama anabisha aende mahakamani.

Wengi tuliamini na mpaka sasa tumesimama kwenye misingi ya uaminifu kuhusu Chadema kuwa Lowasa ni Fisadi na hafai kupewa nchi.

Lakini wengi wetu mmeshindwa kutushawishi kwa hoja kwa nini Lowassa awe msafi sasa.

Ni vema mtuombe radhi hadharani kuwa ndani hiyo miaka mlikuwa mnatudanganya na kutulaghai ili kuwalaghai na ccm wamteme Lowassa.

Bado nipo kwenye misingi ya awali ya Chadema kupinga ufisadi na mafisadi na naamini Lowassa ni fisadi mpaka pale viongozi wa Chadema mtakapokiri wazi kuwa mlitupotosha Lowassa sio fisadi na ushahidi mlikuwa hamna.

Mrema Aanza Kazi Aliyopewa na Magufuli..Ataka Boda Boda Wampe Majina ya Polisi Wanaolazimisha Rushwa

$
0
0
Mwenyekiti wa bodi ya Parole nchini, Agustino Lyatonga Mrema, amewataka madereva wa Bodaboda wasijihusishe na maandamano ya kisiasa.

Pia amewaagiza waendesha bodoboda Kinondoni wampe majina ya polisi wanaowalazimisha kutoa rushwa, atayakabidhi kwa Rais Magufuli

Chid Benz: Mpaka sasa hivi Babu Tale ameshatumia zaidi ya milioni 40 kwa ajili yangu

$
0
0
Moja kati ya watu anaowaheshimu rapa Chidi Benz, ni Babutale, kwasababu meneja huyo wa Diamond ametumia fedha nyingi hadi sasa kwaajili yake.

“Huwezi amini mpaka sasa hivi ninavyoestimate kwamba Tale anaweza akawa ametumia kama milioni 45, 50, 60. Sio kuwekeza, vitu ambavyo vimefanyika tayari, lakini sijasaini wala nini,” alisema Chidi kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM.

“Tale anachokifanya anaonesha kwamba ‘nia yangu mimi sio lazima tukabane kwenye suala la hela, nia yangu wewe uwe sawa, uwe okay, uwe poa.’ Kwahiyo ina maana mimi sijasaini lakini nachukulia kwamba yeye aone kusaini inawekana nikasaini ukaniletea mkataba wa miaka miwili but mimi sasa naishi na wewe kabisa,” aliongeza.

Chidi anadai kuwa anamchukulia Tale kama familia yake.

“Kwasababu hata sasa hivi nakaa kwake, bado niko kwao so yaani kwahiyo hata ukija mkataba labda aniandikie miaka 20 kwamba haina maana.”

Tale alimsaidia rapper huyo kumsaidia kuepukana na uraibu wa madawa ya kulevya ikiwa pamoja na kumpeleka rehab na baada ya kutoka kuingia studio kurekodi nyimbo mpya. Hivi karibuni aliachia wimbo wake mpya ‘Chuma’ aliomshirikisha Raymond.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne ya Agosti 2

$
0
0




Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne ya Agosti 2

​Picha za utupu za kisagaji za mke wa Donald Trump zasambaa

$
0
0
Gazeti la New Daily News limechapisha picha za utupu za mke wa mgombea urais wa Marekani kupitia chama cha Republican, Donald Trump, Melania.


Limeandika kuwa miaka mitatu kabla ya kukutana na mume wake, Donald Trump, Melania alipiga picha za utupu na mrembo mwingine kwaajili ya jarida la Ufaransa.

Picha hizo za kisagaji zilipigwa huko Manhattan mwaka 1995, kipindi hicho akiitwa Melania Knauss, mwenye umri wa miaka 25 na alikuwa akitumia jina la “Melania K.”


Baadhi ya picha hizo ziliwekwa kwenye jarida la Max la Ufaransa, zaidi ya miaka 20 iliyopita. Baadhi yake hazijawahi kuchapishwa hadi sasa.

Picha kali zaidi inamuonesha Melania akiwa amelala kitandani na mlimbwende aitwaye Emma Eriksson, akiwa mtupu pia nyumba yake.

Alipoulizwa kuhusu picha hizo, Donald Trump alisema: Melania was one of the most successful models, and she did many photo shoots, including for covers and major magazines. This was a picture taken for a European magazine prior to my knowing Melania. In Europe, pictures like this are very fashionable and common.”

Mrembo huyo raia wa Slovenia, mwenye miaka 46 sasa, alikutana na Trump kwenye hafla ya Fashion Week mwaka 1998. walioana January 2005 na wana mtoto mmoja, Baron, 10.

Serikali: Mende hakubaliki kama chakula kwa jamii ya Watanzania

$
0
0
Baada ya utafiti wa siku chache kubaini wingi wa protini katika maziwa yanayoweza kutolewa kutoka aina mpya ya mende, Serikali imesema haina mpango wa maziwa hayo kwa sasa.

Kauli hiyo ya Serikali imekuja baada ya timu ya kimataifa ya wanasayansi kubaini chembechembe za protini ndani ya mende aina ya diploptera puntuate ambaye huzaa watoto tofauti na aina nyingine.

Mratibu wa kitaifa wa uongezaji wa virutubisho katika chakula kutoka taasisi ya chakula na lishe (TFNC), Celestine Mgoba alisema “Wala hatuna mpango wa mende kwenye matumizi ya vyakula. Ni mpaka utafiti ufanyike na Serikali itoe kibali. Inawezekana tu mtu amefanya utafiti wake, ni mpaka uthibitishwe “.

“Kitu chenyewe mende? Ukiwaambia watu kuhusu ubora wa maziwa ya mbuzi tu inakuwa shida, wengi wanataka maziwa ya ng’Ombe, ndiyo utakuja kusema mende? Halafu hao mende watatoa kiasi gani, maana yatatakiwa mengi,”alisisitiza

Mratibu wa taasisi hiyo alisema licha ya kutofahamu utafiti huo., bado mende hakubaliki kwa jamii ya Watanzania kama chakula.

BY: EMMY MWAIPOPO

Taarifa Toka Ikulu: Rais Magufuli Katoa Maagizo Mazito Kwa Viongozi Wote Hapa Nchini, Pia Katoa Onyo Kali Kwa Walimu

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaagiza viongozi wote wa kuanzia ngazi ya Mkoa hadi Kitongoji hapa nchini kufuatilia matumizi ya fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya kutoa elimu bila malipo kwa lengo la kudhibiti mianya ya matumizi mabaya ya fedha hizo.

Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo tarehe 01 Agosti, 2016 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mnadani na kuwajumuisha wananchi wa Katoro na Buseresere Mkoani Geita.

Katika agizo hilo Dkt. Magufuli amewaonya walimu ambao wameanza kufanya udanganyifu kwa kuandikisha idadi kubwa ya wanafunzi kuliko idadi halisi kwa lengo la kupata mgao mkubwa wa fedha za ruzuku na amesema Serikali itachukua hatua kali dhidi ya yeyote atakayebainika kufanya hivyo.

"Ninafahamu mgao wa fedha hizo hutolewa kulingana na idadi ya wanafunzi waliopo, wapo baadhi ya walimu ambao wameanza kuandika wanafunzi hewa katika shule zao, ili kusudi aletewe hela nyingi kuliko idadi ya wanafunzi waliopo, wanafunzi kama wapo laki nne yeye anasema shule yangu hii ina wanafunzi laki tano, ili kusudi hela zikija za wanafunzi laki tano, za wanafunzi laki moja wagawane.

"Napenda nitoe wito kwa walimu Tanzania nzima, mnatafuta matatizo, narudia mnatafuta matatizo, msijaribu kula hela ya Serikali" Amesema Rais Magufuli.

Pamoja na agizo hilo, Rais Magufuli pia ametaka viongozi wa ngazi zote katika Mikoa kuhakikisha wana takwimu za idadi ya wanafunzi katika shule zote zilizopo katika maeneo yao ili kurahisisha ufuatiliaji wa fedha hizo na amesema kuwa kuanzia sasa ataanza kutembelea shule kwa kushitukiza na kwamba kiongozi atakayeonekana kutojua takwimu itakuwa ni uthibitisho kuwa hatoshi kuendelea na wadhifa alionao.

"Na nitoe wito kwa viongozi wa Mikoa, Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Makatibu Tarafa, Watendaji wa Kata, Wenyeviti wa Vijiji, kila mmoja awe na idadi ya wanafunzi waliopo katika shule zao, hatutaki kuwapunja wanafunzi hela ambayo wanatakiwa kupata, lakini pia hatutaki kutoa hela ambayo haitakiwi" Amesisitiza Rais Magufuli.

Mhe. Rais Magufuli ambaye ametumia mkutano huo kueleza juhudi mbalimbali zilizofanywa na Serikali yake ya Awamu ya Tano, kutekeleza ahadi yake ya kujenga Tanzania Mpya pia amewataka viongozi na watendaji wa Serikali kutekeleza wajibu wao kwa kutembelea wananchi wanaowaongoza badala ya kukaa muda mwingi ofisini huku akisisitiza ofisi hizo kuwepo katika maeneo yenye shughuli husika.

Aidha, Dkt. Magufuli amekosoa utaratibu unaotumiwa na Halmashauri nyingi za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya kutumia mawakala katika ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri akisema mawakala hao wamekuwa wakitumia utaratibu huo kukusanya fedha nyingi na kisha kuwasilisha kiasi kidogo katika Halmashauri husika.

"Hivi kwa nini Halmashauri msingekuwa na maafisa wenu wazuri na mkawa na mashine za kielektroni kwa ajili ya kukusanya fedha? Amehoji Dkt. Magufuli na kuongeza kuwa;

"Tena mawakala wengine ndio hao hao wamekuwa wakikusanya kodi hata kwa wananchi wanyonge wenye vibiashara vidogo vya kuuza mchicha bila hata kuwaonea huruma"

Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli amemaliza ziara yake ya siku nne katika Mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga na Geita na yupo nyumbani kwake Chato Mkoani Geita kwa mapumziko mafupi.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Chato

01 Agosti, 2016

Trump Amuita Hillary Clinton ni ‘Shetani’

$
0
0
Mgombea wa chama cha Republican nchini marekani Donald Trump amemtaja mshindani wake wa chama cha Democratic Hillary Clinton kuwa ‘shetani’.

Akizungumza kwenye mkutano huko Pennsylvania bwana Trump alimshambulia Bernie Sanders kwa kumuachia nafasi Bi Clinton.

Tajiri huyo alisema kuwa Sanders alifanya makubaliano na ‘shetani’ .

Wanachama wa Democrat na Republican wememkosoa bwana Trump kutokana na matamshi yake kuhusu wazazi wa mwanajeshi M’marekani muislamu aliyeuawa vitani nchini Iraq.

Source: BBC

Miss World Kenya Apokonywa taji lake Kama Miss Sitti Mtemvu

$
0
0
Aliyekuwa mshindi wa tuzo la Miss World Kenya 2016 , Roshanara Ebrahim, amepokonywa taji lake baada ya kukumbwa na sakata .

Kulingana na gazeti la The Standard nchini Kenya,Roshanara mwenye umri wa miaka 23, alishinda taji la mwaka uliopita na alikuwa anatarajiwa kuiwakilisha Kenya kwenye mashindano ya Miss World, mwishoni mwa mwaka huu.

Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, wasimamizi wa Miss World Kenya, kampuni ya bidhaa za urembo, Ashleys imeandika,

'Kuanzia sasa, Roshanara hatoiwakilisha Kenya nchini na hata kimataifa kama Miss World. Tumefahamishwa kuhusu sakata kubwa inayomkumba Roshanara Ebrahim, ambayo inakiuka sheria na masharti ya Miss World Kenya. Tunatekeleza sheria zetu na tunatarajia wanamitindo wetu kusimamia maisha yao ya kibinafsi.

Kulingana na gazeti hilo , Roshanara ameandika kukubaliana na uamuzi huo na kuwasihi warembo wenye umri mdogo kuhakikisha maisha yao ya kibinafsi, hayaathiri jukumu lao la Miss World.

''Nakaribisha uamuzi wa ofisi ya Miss World Kenya kunipokonya taji la Miss World Kenya kwa masikitiko makubwa, namtakia atakayechukua nafasi yangu kila la heri.

Kabla ya uamuzi wa ofisi ya Miss World Kenya, Roshanara alilazimika kujitetea dhidi ya madai yaliomhusisha kuwa na uhusiano na mwanasiasa mashuhuri.

Tayari ofisi ya Miss World Kenya, imeahidi kumtangaza mwanamitindo atakayejaza pengo lililoachwa na Roshanara Ebrahim siku chache zijaazo.

Roshanara anayesomea uwakili, anatarajiwa kuendelea na shughuli zake za kuwasaidia watoto walio na mpasuko wa mdomo, yaani 'cleft.

Diamond Asema Zari Atajifungua Mwezi Disemba

$
0
0
Mkali wa wimbo ‘Kidogo’, Diamond Platnumz amethibitisha ujio wa mtoto wa pili kutoka kwa mpenzi wake Zari.
Diamond

Muimbaji huyo amesema yeye na mpenzi wake Zari wanategemea mtoto wa kiume.

“Yah kweli mimi ni baba kijacho,” Diamond alikiambia kipindi cha Leo Tena “Natarajia Mama Tiffa anipatie tena mtoto mwingine, atakuwa wa kiume,”

Aliongeza, “Na itakuwa mwezi Disemba mwaka huu! Baada ya hapo sitaongeza tena mtoto mwingine, ni muda wa kula bata sasa ndio unafata na watoto wetu wawili”

Diamond na Zari tayari wana mtoto mmoja wa kike, ‘Tiffa’ ambaye hivi karibuni atatimiza mwaka mmoja.

Mwanamuziki Patoranking Aanza Ziara ya Uzinduzi wa Album yake Tanzania

$
0
0


Toka kulia, Meneja bidhaa wa Spice Africa Mariam Nnauye, Msanii maarufu wa miondoko ya reggae kutoka Nigeria Patrick Nnaemeka Okorie aka Patoranking na Meneja Mkuu Masoko wa kampuni ya Spice Africa Joan Nkuzi wakipiga “Selfie” kabla ya kuanza kwa mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa Paparazzi jijini Dar es salaam siku ya jana ambapo msanii huyo alikuwa akiitambulisha albamu yake mpya ya “God over everything” kwa mashabiki wake kwenye ziara ya siku moja nchini Tanzania
Albamu iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu inayoitwa“God over Everthing” (GOE) kutoka kwa nyota wa mtindo wa reggae/dancehall wa kinigeria Patrick Nnaemeka Okorie a.k.a Patoranking hatimaye imekemilika.

Mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu nyerere (JNIA) jana jioni, msanii huyo wa miondoko ya reggae pamoja na timu yake iliyopokelewa na Spice Africa, kampuni ambayo inayofanya kazi na Patoranking katika kutangaza mziki wake na usambazaji wa albamu mpya ya msanii huyo kwa nchini Tanzania.

Akizungumza kwenye mkutano wa vyombo vya habari uliofanyika katika ukumbi wa Paparazi-Slipway jioni hiyo hiyo, msanii huyo alitambulisha baadhi ya vibao/nyimbo zake ambazo ziko katika albamu hiyo, baadhi ambazo tayri zinafanya vizuri katia anga za kimataifa kama “Girlie O”, “My woman”, “Make Am”, “Another Level”, “Alubarika” na wimbo wake mpya wa hivi karibuni “No Kissing Baby”aliomshirikisha msanii Sarkodie kutoka Ghana. Albamu hiyo imebeba nyimbo zilizotengenezwa katika label yake ya VP records yenye idadi ya zaidi ya nyimbo 16.

“Albamu hii ni ya kipekee; ina nyimbo kwaajili ya kila mtu, kwa watu wenye umri wowote na kila kona ya Afrika. Nilitaka kulipa fadhila/Heshima kwa asili yangu na pia kukumbatia mfumo mpya wa muziki wa kiafrika ambao unashika kasi Ulimwenguni kwa sasa. Nina furaha sana kuitambulisha albamu yangu kwa mara ya kwanza duniani kwa mashabiki wangu waTanzania”….alisema Patoranking.

Msanii huyo pia alitumia muda huo kufafanua kwanini alichagua Dar es salaam kama Jiji la kwanza kuitambulisha albamu yake mpya, “watanzania ni watu wazuri sana, nimeona wasanii wengi kutoka Nigeria na mataifa mengine wakija kufanya shoo hapa jinsi wanavyopokelewa vizuri na upendo mkubwa”. Aliwataja baadhi ya wasanii  wa Kitanzania ambao nyota huyu anapanga kufanya nao kazi akiwemo: Navy Kenzo na Vanessa Mdee a.k.a  V-Money ambao kwa maelezo yake ni kama wanafamilia.
Toka kushoto ni Meneja Mkuu Masoko wa kampuni ya Spice Africa Joan Nkuzi, Mwanamuziki maaarufu anaetambulika zaidi kwa miondoko ya dancehall na reggae kutoka nchini Nigeria Patrick Nnaemeka Okorie a.k.a Patoranking, Meneja bidhaa wa Spice Africa Mariam Nnauye pamoja na Meneja wa Msanii huyo nchini Tanzania Tom Raymond kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza shughuli ya utambulisho wa album ya msanii huyo kwa waandsihi wa habari katika hafla iliyofanyika jana usiku ndani ya ukumbi wa Paparazzi jijini Dar es salaam. Msanii huyo alikuwa nchini kwa ziara ya siku moja kuitambulisha albamu yake ya “God over everything” kwa mashabiki wake nchini Tanzania.

Aliwashukuru mashabiki wake na vyombo vya habari vya Tanzania kwa kuunga mkono mziki wake  kabla  hajabainisha kuwa atatembelea Nairobi, Kampala na Accra-Ghana kuitambulisha albamu hiyo kabla ya kurudi nyumbani.

Patoranking pia aliendelea kutaja siri ya kuwa ameanzisha lebo ya kurekodi /studio aliyoiita “his baby”, ambayo msanii wa kwanza ametokea kutoka hapa hapa Tanzania, “Jina lake ni Walid, mnaweza msimfahamu kwa sasa, lakini mtamfahamu, huyu amekusudiwa kufanya mambo makubwa” alisema Patoranking

Kwa upande wake Meneja wa Masoko wa Spice Africa Joan Nkuzi amesema, ni heshima kubwa sana kwa Msani  nyota wa Nigeria kutambulisha albamu yake kwa mara ya kwanza hapa Tanzania na ndio maana hawakusitasita kuunga mkono juhudi zake. Jukumu kubwa lab Spice Africa kupitia application yake ya Mziiki ni kupeleka muziki wa Kiafrika duniani kote kama wakusanyaji na wasambazaji walioko katika masoko zaidi ya 12 ndani ya Afrika, walitoa uhakika sio tu kufanya kazi na wasanii wenye vipaji, bali pia wasanii ambao ni wanyenyekevu na ambao wanajua malengo yao – ambapo mmoja wao ni Patoranking.

“Spice Africa kupitia mobsite yetu na application ya “Muziki”, pamoja kwa ushirikiano na Telco’s katika Nyanja mbali mbali kama CRBT na IVR tuna lengo la kuendelea kuimarisha maudhui yetu, kwa njia ya ushirikiano na Talent kutoka Afrika  Mashariki, Kati, Magharibi na Kusini. Kazi yetu hapa ni kuhakikisha kuwa Patoranking anafanikiwa katika kutambulisha albamu yake na anapata ushirikiano anaouhitaji kama inavyowezekana.”
Toka kulia Meneja wa Msanii maaarufu toka Nigeria Patrick Nnaemeka Okorie a.k.a  Patoranking (katikati) kwa Tanzania Tom Raymond akimtambulisha rasmi msanii huyo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) ambaye alikuwa nchini kwa ziara ya siku moja ya kutambulisha albamu  yake mpya inayofahamika kwa jina la “God over everything”. Utambulisho wa album hiyo ulifanyika katika ukumbi wa Paparazzi katika hotel ya Slipway jijini Dar es salaam. (wa pili kulia ni Meneja bidhaa wa Spice Africa Mariam Nnauye na (wa kwanza kushoto) ni Meneja Mkuu Masoko wa kampuni ya Spice Africa Joan Nkuzi

Patoranking aliingia katika tasnia ya muziki mwaka 2013 akiwa na nyimbo yake ya kwanza ya ‘Alubarika’ na ameendelea na  kuwa mmoja kati ya wasanii nyota wanaoheshimika kwa mtindo wake wa kipekee wa Miondoko ya Dancehall na Reggae na Afrobeat

Kwa habari za kipekee kuhusu utambulisho wa albamu mpya ya Patoranking, Tafadhali tembelea www.mziiki.com au tufuate katika @Mziiki App katika Instagram na Twitter.

Mwanafunzi UDOM auawa kwa kupigwa na wenzake Wakati Wakitoka Baa

$
0
0
Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza, Kitivo cha Sayansi ya Jamii katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Fredrick Joseph (25), ameuawa kwa kushambuliwa kwa kipigo na watu wanaosadikiwa kuwa ni wanafunzi wenzake wakati akitoka klabu ya pombe (Bar).

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana katika eneo la chuo hicho ambapo mwanafunzi huyo alisikika akipiga kelele ndipo walinzi wakafika na kumkuta akiwa anagalagala njiani.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa, amesema mwanafunzi huyo ambaye ametokea Musoma mkoani Mara alishambuliwa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na watu wasiofahamika.

Amebainisha mwanafunzi huyo alikutwa majira ya saa 10 alfajiri katika eneo hilo la chuo hicho huku akisema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa marehemu huyo alikuwa na ugomvi na watu hao katika klabu ya pombe ya Canival Pub iliyopo chuoni hapo.

“Alipoondoka kurudi bwenini akiwa njiani alishambuliwa na watu hao wasiofahamika na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake, kipigo kilichosababisha kifo chake wakati alipokimbizwa kutibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma,” alisema Mambosasa

Amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali hiyo kwa uchunguzi zaidi na hadi sasa hakuna mtu anayeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo.

Alipoulizwa kuwa taarifa za mwanafunzi huyo kushambuliwa na wenzake, Mambosasa alisema kwasababu inadaiwa haifahamiki upelelezi bado unaendelea.

“Kwa sababu mwenye bar si yupo, kama kuna ugomvi ambao ulikuwa unaendelea tutajua tu, nimemuelekeza OCD kufuatilia ni nani waliokuwa wanakunywa kwenye hiyo bar chuoni, ni lazima tu watakuwa wanachuo ili tuwabaini,”

Kamanda huyo amesema ameelekeza uchunguzi wa kina ufanyike kama kulikuwa na ugomvi ndio hao hao walienda kumtegea njiani.

Chanzo cha habari ambacho hakikutaka kutaja jina lake kwa madai kuwa  siyo msemaji wa polisi kimesema kuwa marehemu Joseph alikuwa anakunywa pombe pamoja na marafiki zake lakini baada ya kulewa walianza ugomvi ambao hata hivyo waliamuliwa.

“Baada ya kuamuliwa ule ugomvi wa awali ndipo wenzake walipokwenda kumsubiria kwa mbele kwenye kichaka ambapo walimvamia na kumshambulia na kumwacha karibu ya kufa,” kilisema chanzo hicho.

Kiliongeza kuwa, baada ya kumwacha hapo na kutoweka ndipo walinzi wa chuo hicho waliokuwa doria walimuokota na kumfikisha kwenye kituo kidogo cha polisi kilichopo Chimwaga ambapo alikimbizwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma alipofariki wakati akipatiwa matibabu.

Chanzo hicho kimesema hakuna mtuhumiwa hata mmoja anayeshikiliwa na polisi kwa kuwa wote waliomshambulia walitoroka na hawajulikani walipo.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images