Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale akamatwa na Polisi leo asubuhi

$
0
0

Meneja wa mwanamuziki wa kimataifa Diamond Platnumz, Hamis Tale Tale maarufu kwa jina la ‘Babu Tale’ hivi sasa yupo mikononi mwa polisi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Babu Tale amekamatwa leo na kufikishwa mahakamani hapo ili ajieleze ni kwa nini asifungwe kwa kushindwa kutekeleza hukumu ya Mahakama iliyomwamuru alipe fidia ya Sh250 milioni kwa makosa ya kuvunja sheria ya Hakimiliki.

Babu Tale anatakiwa alipe fedha hizo kutokana na kuvunja mkataba kati yake na Shekhe Mbonde, kwa kuuza na kusambaza nakala za mawaidha (DVDs) bila ridhaa ya shekhe huyo, jambo ambalo ni kinyume na haki miliki.


Msigwa apewa kibali kufanya mkutano wa hadhara, Tundu Lissu Akoleza Moto Oparesheni UKUTA Mahakamani

$
0
0
Peter Msigwa Akibebwa na Wananchi katika moja ya mikutano
Hatimaye Jeshi la Polisi limetoa kibali cha kufanya mkutano wa hadhara kwa Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, lakini limeweka mlolongo wa masharti ambayo atalazimika kuyatii kuepuka rabsha.

Wakati Jeshi la Polisi likitoa masharti hayo, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu amesema vyama vya upinzani vitaendelea kuendesha mikutano ya hadhara licha ya kufungua kesi Mahakama Kuu ya kupinga zuio la shughuli hizo, huku akisema amri ya kuzuia wanasiasa kufanya mikutano nje ya maeneo yao imetolewa bila ya kusoma sheria.

Mkoani Iringa, Jeshi la Polisi lilitoa masharti hayo baada ya Msigwa, ambaye anaongoza Jimbo la Iringa Mjini kwa kipindi cha pili mfululizo, kutaarifu kuwa atafanya mkutano wa hadhara kuanzia Septemba Mosi, siku ambayo Chadema imepanga kuanza operesheni ya nchi nzima inayoiita “ya kupinga udiktekta Tanzania”.

Katika barua aliyomwandikia Mchungaji Msigwa juzi, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Iringa (OCD), Y. Z Mjengi amerejea barua ya mbunge huyo yenye kumbukumbu namba MB/IR/M/05 ya Agosti Mosi mwaka huu, inayohusu mikutano ya hadhara kuanzia Agosti 3 hadi 22, ikianza saa 8:00 mchana hadi 12:00 jioni.

Kupitia barua hiyo, ambayo Msigwa alithibitisha kuipokea, Jeshi la Polisi limesema limeridhia kwa sababu lengo la mkutano wake ni kuhamasisha maendeleo na kupokea kero za wananchi, kazi ambayo inatakiwa kufanywa na mbunge wa eneo husika.

“Natarajia mkutano wako (Msigwa) utakuwa wa amani na utulivu bila kumkashifu mtu wa chama kingine,” anasema Mjengi katika barua hiyo.

“Mikutano yote hiyo kibali kimetolewa kwako kama mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini. Sitarajii mtu mwingine kutoka nje ya Mkoa wa Iringa kuja kukusemea kuhusu maendeleo ya jimbo lako au kuja kupokea kero za wananchi wako na kuzijibia wakati hiyo ni kazi ya mwenye himaya ambaye ni wewe.

“Kashfa, kejeli, matusi na maneno ya uchochezi kwa viongozi wa Serikali vitahesabiwa ni uvunjifu wa amani na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yako na zitapelekea kuzuiliwa kufanya mikutano yako inayoendelea.”

Barua hiyo inaishia kwa maneno yaliyoandikwa kwa herufi kubwa. “Kumbuka: Amani ya Tanzania italindwa na kila Mtanzania kwa hiyo ni jukumu lako wewe Mhe. Mbunge kutekeleza jukumu la ulinzi wa amani. Kwa pamoja tutaweza,” inasema barua hiyo.

Alipoulizwa kuhusu masharti hayo, Mchungaji Msigwa alisema hayo ni ya kwanza lakini hakutaka kuzungumza zaidi kwa maelezo kuwa alikuwa kwenye kikao.

Shamsa Ford Amuweka Wazi Mpenzi wake Mpya

$
0
0
Msanii wa filamu nchini Shamsa Ford amefunguka na kusema kuwa baada ya kuachana na mpenzi wake wa zamani Nay wa Mitego ambaye alimuweka wazi kwa jamii na kuja kuachana baada ya muda mfupi alikuwa mwoga tena kumuweka wazi mpenzi wake mpya.

Shamsa Ford alisema hayo kupitia kipindi cha eNEWZ na kusema kuwa alikuwa mwoga kumuweka wazi kwa jamii mpenzi wake mpya lakini kwa kuwa mapenzi yamemzidi imebidi sasa amuweke wazi, kwani anasema mapenzi huwezi kuyaficha.

“Mwanzo kweli nilikuwa naogopa lakini mapenzi yakizidi huna namna inabidi tu ujiachie, ni kweli mpaka sasa tayari ameshanitolea mahari nyumbani” alisema Shamsa Ford

Katika kusherehekea siku ya kuzaliwa Shamsa Ford alitumia nafasi hiyo kumtambulisha mpenzi wake mpya ambaye anafahamika kwa jina la Chid Mapenzi ambaye mara kadhaa alikuwa akisema ni mtu anayeshirikiana naye kwenye biashara tu.

eatv.tv

Wema Sepetu: Niacheni jamani Nimechoka

$
0
0
Wema Sepetu 
Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu ameonesha kuchoka na maneno mbalimbali kutoka kwa watu hususani kwenye mitandao ya kijamii kiasi cha kuamua kutoa yake ya moyoni kwa watu wote ambao wamekuwa wakimfuatilia maisha yake.

Ameonesha kukasirishwa na baadhi ya watuwanaomsema kwenye mitandao ya kijamii hususani kuhusu mapungufu yake.

Wema Sepetu ametumia mtandao wake wa Instagram kuweka ujumbe mrefu kwa watu hao, huku akiwataka wamuache aishi maisha yake kwani hajawahi hata siku moja kwenda kuomba msaada kwao, na kusema hata siku atakapokufa atakufa mwenyewe na kama ni majibu kwa Mungu atajibu mwenyewe.

“Naomba niseme kitu na nieleweke tafadhari, sijawahi hata siku moja kwenda kwa hata mmoja wenu na kumgongea kuomba hata hela ya chumvi. Maisha yangu yananihusu mimi na hata siku nikifa nakufa mwenyewe, majibu kwa Mungu naenda kujibu peke yangu. Niacheni jamani nimechoka” aliandika Wema Sepetu

Mbali na hilo Wema Sepetu amewataka watu ambao wanakereka na aina ya maisha ambayo yeye anaishi waache kuyafuatilia kwani si lazima kufuatilia kile akifanyacho au maisha anayoishi yeye.

“Kama nakukera na maisha yangu basi usiyafuatilie siyo lazima. Nisiheme sasa jamanii. Naomba tafadhari kama mapungufu ni ya kwangu mimi. Niacheni mimi nafanya kile kinachoridhisha nafsi yangu maana sipendi kujikasirisha. Kwani nikitajirika mimi au nikiwa masikini wewe unapata faida gani. Jiulize kwanza hilo swali ndiyo uanze kutoa maneno yako” alisema Wema Sepetu

eatv.tv

Madiwani wa UKAWA Wasusia Kikao cha Paul Makonda Kwa Madai Kwamba Anawadharau

$
0
0
Madiwani wa Ukawa wa Manispaa ya Kinondoni wamesusa kikao kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa madai kiongozi huyo hana uhusiano mzuri na viongozi wa upinzani.

Jana, Makonda aliitisha kikao cha wakuu wa wilaya, wakurugenzi, wakuu wa idara za manispaa za Temeke, Ilala na Kinondoni na madiwani wote, wakiwamo wabunge wanaounda halmashauri hizo.

Kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Arnaoutoglou kililenga kuzungumzia masuala mbalimbali, kama maeneo yaliyovamiwa na uboreshaji wa elimu mkoani Dar es Salaam.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, meya wa Kinondoni, Boniface Jacob alisema Makonda amekuwa na tabia ya kudharau na kutoheshimu viongozi wenzake, hasa wa upinzani akiwaona hawatendi kazi vizuri.

Pia, Jacob alidai kuwa Makonda amekuwa na tabia ya kuingilia kazi zinazofanywa na viongozi wengine kwa kutumia cheo cha ukuu wa mkoa, jambo ambalo meya huyo alisema ni kinyume cha sheria.

“Akitaka tumpe ushirikiano, Makonda abadilike la sivyo mtindo utakuwa huuhuu, mambo yatakuwa hivi. Huu ni mwanzo na ndiyo maana leo (jana) Ukawa Kinondoni tumekuwa na msimamo mmoja,” alisema Jacob.

Jacob, ambaye pia ni diwani wa Ubungo (Chadema), alisema hawakuona umuhimu wa kwenda katika kikao hicho kwa sababu kiongozi wa mkutano huo anawadharau.

Akijibu tuhuma hizo, Makonda alisema madiwani waliohudhuria kikao hicho maeneo yao yalikuwa na shida na yanahitaji kushughulikiwa, hivyo si kazi yake kuhesabu watu na kubaini nani hakufika mkutanoni.

Alisema ajenda kuu ya kikao hicho ilikuwa ni kujadiliana namna bora ya kuvirudisha viwanja vilivyochukuliwa na kuvirejesha kwa matumizi yaliyokusudiwa.

“Huyo anayelalamika mwambie huo anaoufanya ni utoto akikua ataacha. Narudia tena siyo kazi yangu kuangalia nani hajaja kwenye kikao,” alisema.

Kwenye kikao hicho, meya wa Ilala (Chadema), Charles Kuyeko alikuwapo kwenye mkutano huo pamoja na madiwani wenzake, sambamba na wale wa Temeke.

Makonda si mgeni wa tuhuma .Aliteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Kionondoni katika kipindi ambacho alikuwa akituhumiwa kuhusika kwenye sakata la kupigwa kwa Waziri Mkuu wa zamani, Jaji Joseph Warioba kwenye mdahalo wa Katiba uliofanyika Hoteli ya Blue Pearl.

Katika kipindi hicho, Makonda pia alikuwa akituhumiwa kumrushia tuhuma za ufisadi Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akiahidi kuwa CCM isingempitisha kugombea urais.

Akitoa majumuhisho ya kikao cha jana kilichoanza saa 2:00 asubuhi hadi saa 5:00 asubuhi, Makonda aliwataka watu waliovamiwa na kujenga kwenye maeneo yasiyoruhusiwa, kuanza kubomoa majengo yao kabla ya Serikali kuwafikia.

Kabla ya kutoa majumuisho hayo, Makonda alitoa nafasi kwa madiwani wa manispaa hizo kueleza kero zinazowakabili, hususan zinazohusu ardhi.

“Najua mchakato huu utawagusa hadi vigogo, lakini mimi siogopi vita kwa sababu ndani yangu ninaongozwa na Mungu pekee,” alisema Makonda.

Mbali na hilo, Makonda alisema endapo mtendaji wa ardhi atayebainika kuhusika katika kuchezea michoro na ramani ili aachie ardhi na kujipatia fedha, atashughulikiwa kwa mujibu sheria.

Katika hatua nyingine, Makonda amemwagiza kamishna msaidizi wa ardhi wa Kanda ya Dar es Salaam, Mathew Nhange kumwambia Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi awaondoe maofisa ardhi na mipango miji wa Kinondoni na Ilala baada ya kushindwa kutoa taarifa za kuridhisha katika mkutano huo.

Huku akiwataja maofisa hao wanaotoka Kinondoni na Ilala, Makonda alisema alishakutana na wakuu wa idara kwenye vikao vilivyopita, hivyo alitegemea kuwa watumishi hao wangetoa taarifa zilizokamilika.

“Kamishna naomba umwambie katibu mkuu mimi siwataki watumishi hawa katika manispaa hizi. Mwambie awatoe na kuwapangia kazi nyingine,” alisema Makonda.

Kamishna Nhange alisema agizo hilo analifanyia kazi na kwamba atampa katibu mkuu taarifa za watumishi hao jana.

AUDIO: Kitu Diamond kasema kuhusu yeye kuwa mapenzini na Hamisa Mobetto

$
0
0
Ukaribu wako kwenye mitandao ya kijamii siku za karibuni unaweza kuwa ulikukutanisha na stori Diamond Platnumz amekua na uhusiano wa kimapenzi na mwanamitindo wa bongo Hamisa Mobetto.

Stori zilianzia kwenye birthday party ya mama Diamond baada ya Hamisa kuonekana kuwa karibu na familia hiyo hasa dada wa Diamond lakini pia kuna picha iliyosambaa inaonyesha wawili hao kila mmoja amepiga picha kwa wakati wake lakini kwenye mazingira ya chumba yanayofanana.

Sasa August 2 2016 Leo Tena ya Clouds FM Diamond Platnumz ametolea ufafanuzi hiyo ishu na kusema “Hamisa nimeanza kumjua zamani sana kwasababu yupo katika industry hizi za kufanya fashion, nimekua nikimjua muda mrefu kidogo na sikuwahi kuwa na matatizo nae yoyote sababu tumekuwa ni watu tu ambao tunaheshimiana …..”

‘Sina uhusiano wa kimapenzi na yeye, juzi kati alikua kwenye video yangu mpya nimefanya na Ray Vanny na nafikiri hiyo imechangia kuingiza hayo maneno, kufanya video Tanzania mara nyingi huwa inaleta manenomaneno’

kupata full story ya Diamond akiongelea pia kuhusu picha iliyounganishwa wote wakiwa wametumia chumba kimoja bonyeza play hapa chini kumsikiliza akihojiwa na Geah Habib na Dahuu‘

Diamond na Zari Wataja Mwezi Ambao Wanatarajia Kupata Mtoto wa Pili...

$
0
0
Mkali wa wimbo ‘Kidogo’, Diamond Platnumz amethibitisha ujio wa mtoto wa pili kutoka kwa mpenzi wake Zari.

Muimbaji huyo amesema yeye na mpenzi wake Zari wanategemea mtoto wa kiume.
“Yah kweli mimi ni baba kijacho,” Diamond alikiambia kipindi cha Leo Tena “Natarajia Mama Tiffa anipatie tena mtoto mwingine, atakuwa wa kiume,”

Aliongeza, “Na itakuwa mwezi Disemba mwaka huu! Baada ya hapo sitaongeza tena mtoto mwingine, ni muda wa kula bata sasa ndio unafata na watoto wetu wawili”
Diamond na Zari tayari wana mtoto mmoja wa kike, ‘Tiffa’ ambaye hivi karibuni atatimiza mwaka mmoja.

Kufanya Kazi na Chid Benz ni Bahati - Raymond

$
0
0
Msanii Raymond ameelezea furaha yake baada ya kufanya kazi na msanii wa hip hop Chid Benz, na kusema kuwa kwake ni bahati kubwa sana.

Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Raymond amesema yeye kufanya kazi na Chid Benz ni heshima kubwa, kwani msanii huyo ana uwezo mkubwa na yeye bado ni mchanga kwenye game.

"Nilifurahi kupata nafasi ya mimi kufanya ngoma na Chid Benz, kwa sababu ni brother ambaye alikuwa anafanya vizuri kitambo, ni msanii mzuri kwa hiyo mimi kufanya naye ngoma naona ni nafasi ambayo nimeipata inanionyesha kabisa kwamba muziki wangu unaenda kwenye nuru, kwa sababu mpaka kaka zako ambao walikutangulia wanakubali kufanya kazi na wewe, ina maana wanakubali kazi zako", alisema Raymond.

Raymond aliendelea kusema kuwa kazi hiyo ambayo ameifanya na Chid Benz ni wimbo aliotokea kuupenda sana, na kuahidi video mashabiki wake hivi karibuni.

"Ngoma ya chuma ni ngoma ambayo naipenda sana achilia mbali mtu ambaye nimefanya naye, namshukuru sana mungu na napata coments nyingi na soon video inakuja", alisema Raymond.

Lowassa, Sumaye Hatarini Kushtakiwa

$
0
0
KAMISHNA wa Sekretarieti ya Maadili kwa Viongozi wa Umma, Jaji mstaafu Salome Kaganda, amewataka viongozi wastaafu kuacha kutoa siri za serikali kwani bado wapo kwenye kiapo na kuonya wakikaidi, watachukuliwa hatua.

Bila kuwataja kwa majina wala siri walizotoa, Jaji Kaganda alisema: “Tusiweke maslahi binafsi mbele kwa kutoa siri za mikataba kwa kuangalia manufaa binafsi, jambo ambalo limelifikisha taifa pabaya. Viongozi wastaafu wafunge midomo yao kwani bado wako ndani ya kiapo hata kama wamestaafu.”

Jaji Kaganda alisema wapo wastaafu ambao wameingia kwenye nyanja mbalimbali ikiwamo siasa, ambapo hutumia majukwaa kutoa siri za serikali na kwamba wanapaswa kukumbuka wanaweza kuchukuliwa hatua za kisheria.

Jaji Kaganda aliyasema hayo juzi alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na Kituo cha Runinga cha ITV.

Kwa siku za karibuni, mbali na watumishi wa umma walioacha kazi zao na kushiriki siasa ikiwa ni pamoja na kuwania ubunge, Mawaziri Wakuu wastaafu, Edward Lowassa na Frederick Sumaye, walihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho ni chama tawala na kwenda Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita.

Viongozi hawa katika kipindi chao cha uongozi walikula kiapo na kuingia kwenye vikao vya Baraza la Mawaziri, ambavyo majadiliano yake kwa kawaida huwa ni siri.

Hata hivyo, baada ya kujiunga na upinzani, wamekuwa wakipanda jukwaani kunadi sera za chama chao cha Chadema.

Akizungumzia maadili ya viongozi, Jaji Kaganda alisema kiongozi mwadilifu anatakiwa kutojihusisha na mambo ya rushwa, ulevi, kuiba saa za kazi za serikali au kwenda ofisini kupanga safari za kujipatia fedha na kumwibia mwajiri.

Jaji Kaganda alisema taifa likiwa na viongozi waadilifu, halitapata shida kupambana na rushwa.
Alisema pia baadhi ya viongozi wamekuwa wakikiuka Sheria ya Maadili kwa kutotangaza zawadi zinazozidi kiasi cha Sh. 200,000 wanapopewa wakiwa kazini, ambazo walipaswa kuwasilisha kwa ofisa masuhuli, ambaye hutakiwa kutoa maelekezo ya matumizi yake baada ya kuwasiliana na Sekretarieti ya Maadili.

“Kama umepewa gari, ataamua ipelekwe kwenye wizara au kama ni kinyago cha dhahabu, basi kinatakiwa kitumike kwa maslahi ya umma au kiwekwe kwenye jumba la makumbusho ya serikali ili tujue kiongozi fulani alitembelea nchi fulani na kupewa zawadi ya nchi.

“Tatizo kubwa wengi hawakabidhi zawadi kwa ofisa masuhuli, wengi wakishapokea kama ni wanyama, unasikia zizi linaongezeka, sasa tutafuatilia tukisikia kiongozi kapewa zawadi fulani, tunakwenda kwa ofisa masuhuli kujua kama amekabidhi au la,” alieleza Jaji Kaganda.
Jaji huyo alisema viongozi wanatakiwa kutambua anayepewa zawadi siyo kiongozi, bali nafasi aliyonayo na kwamba haihusiani na zawadi za kimila.

“Tutawafuatilia na kuwafikisha kwenye Baraza la Maadili na hatua zichukuliwe,” aliongeza Jaji Kaganda.
Alisema kuna viongozi 15,265 ambao wanaguswa na kiapo na kwamba sekretarieti ina kanda saba nchini, ambapo hushirikiana na vyombo vya dola na mamlaka za kiserikali kupokea taarifa kutoka kwa wananchi na mashirika yasiyo ya kiserikali kuhusu vitendo vyao.

Jaji Kaganda aliwataka viongozi waliopewa madaraka kutambua wajibu wao kwa kuepukana na vishawishi na kuunga mkono nia na malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli.

Alisema Mungu amesikia kilio cha Watanzania kwa kumleta Rais Magufuli ambaye amekuwa mstari wa mbele kusimamia maadili ikiwamo kuhakikisha viongozi anaowateua wanaoheshimu sheria na kanuni za utumishi wa umma.

“Tufanye kazi kwa uadilifu, tujizuie na tamaa, tujiheshimu, tuache ubinafsi, kwa kupendelea ndugu na rafiki, tujitume na kutekeleza majukumu yetu kwa kuzingatia misingi ya uadilifu na umahiri. Viongozi wazingatie Sheria ya Maadili watoe matamko yao kwa wakati na kutunza siri za serikali,” alifafanua Jaji Kaganda.

Alisema maadili kwa viongozi wa umma na katika jamii kwa ujumla, yalikuwa yamedorora mno na ndiyo maana yalikuwapo malalamiko kila kona.

“Ukienda msikitini, kanisani, ofisini, kwenye jamii, unasikia maadili yameporomoka. Kweli asilimia kubwa ya viongozi walikuwa hawazingatii maadili,” aliongeza Jaji Kaganda.

Alisema kuporomoka kwa maadili ndani ya serikali kuliifanya Sekretarieti kuanza kutoa elimu kwa viongozi wa umma katika makundi mbalimbali, lengo likiwa ni kukumbushana majukumu na wajibu.
“Kwa sasa naweza kusema hali ya uadilifu inaanza kurudi vizuri na hasa Rais alivyokuja na msisitizo wa kutaka kuona watumishi wa umma na viongozi wanazingatia sheria na kauni. Yeye (Rais), ni mwadilifu hata katika uteuzi anazingatia hilo,” alisema.

Jaji Kaganda alisema pale Rais anapochuja wateule wake, hufuata usemi wa kiutawala unaosema, ‘ikiwa kuna magogo yanaliwa mchwa na mengine hayajaliwa na wadudu hao, ni vibaya kuyaweka karibu, mchwa watatoka kwenye magogo yale na kwenda kwenye mazima’ na ndiyo maana kuna mchujo kwenye uteuzi.

Alisema msisitizo wa kuzingatia uadilifu kwenye uongozi haujaanza sasa, bali tangu Azimio la Arusha lilipotangazwa mwaka 1967 ambalo liliainisha miiko ya uongozi, lakini Azimio la Zanzibar la lilipopitishwa na Halmashauri Kuu ya CCM liliondoa baadhi ya mambo baada ya viongozi kulalamika walikuwa wamebanwa.

“Walilelegeza kanuni ya miiko ya uongozi bila kuweka mwongozo baada ya kuondoa baadhi ya vipengele vya Azimio la Arusha, matokeo yake wakajisahau na ndiyo ikawa chanzo cha kuporomoka kwa maadili ya uongozi.

Mungu, hata hivyo, alisikia maombi yetu wakati wa uchaguzi na kutupa mtu anayekazania maadili,” aliongeza Jaji Kaganda.
CHANZO: NIPASHE

KUBET Ama Kamari Janga Jipya Kwa Vijana....

$
0
0
Ndivyo unavyoweza kusema, kutokana na kundi kubwa la vijana wakiwamo wazee na wanawake kugeukia mchezo wa kubahatisha ambapo kila kukicha vituo vya kamari ya soka na michezo mingine maarufu kama ‘kubeti’ vimekuwa vikiongezeka.

Mchezo huo ambao umekuwa ukikusanya idadi kubwa ya mashabiki hutumia fedha kwa kubashiri mechi za mpira mbalimbali za mataifa ya nje na kushinda kiasi kikubwa cha fedha.

Kushamiri kwa mchezo huo kumekuja miezi michache baada ya tamko la Rais Dk. John Magufuli, kupiga marufuku mchezo wa ‘Pool Table’ asubuhi huku akitaka vijana watafute shughuli za kufanya ikiwemo kilimo, badala ya kupoteza muda katika mchezo huo.

Agizo hilo la Rais Magufuli, alilitoa Mei 16, mwaka huu alipokuwa akiwaapisha wakuu wa mikoa, ambapo kwa sasa makundi hayo yamegeukia mchezo wa ‘kubeti’.

Kamari hiyo kwa sasa imekuwa ikiwateka watu wa jinsi na rika zote na sasa imeshika kasi, huku vituo vya kuchezesha vikichipuka kama uyoga katika maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam na mikoani.

Takwimu za Bodi ya Michezo ya Bahati Nasibu Tanzania, zinaonesha kuwa kwa nchi nzima kuna vituo vya kubeti 2,684 huku Mkoa wa Dar es Salaam pekee ukiwa na vituo 1,344.

Kundi kubwa la wanafunzi, vijana na wafanyakazi wamekuwa wakicheza kwa kutumia simu zao za mkono au mitandao jambo ambalo linaweza kuwa hatari kwa nguvu kazi ya taifa.

Vituo maarufu ni Premier Betting na Meridian Betting, ambavyo vyote vipo katika ushindani mkubwa wa kuchezesha mchezo huo na kuvuta watu wengine jijini.

Gazeti hili lilifanya utafiti kwa zaidi ya wiki moja na kutembelea maeneo ya Mwenge, Magomeni, Kariakoo, Tandale, Tandika, Manzese, Mikocheni, Msasani na Temeke na kukuta makundi ya watu wa jinsia zote na rika mbalimbali wakiwa na makaratasi huku wakibashiri mechi mbalimbali kwa viwango tofauti vya fedha.

Pamoja na hatua hiyo inaelezwa kuwa zaidi ya asilimia 45 ya watu hushiriki mchezo huo kwa njia mbalimbali ikiwemo kununua katarasi maalumu maarufu kwa jina la ‘mkeka’, mitandao na hata kwa njia ya simu.

Alipotafutwa kwa siku juzi na jana Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abbas Tarimba, alimtaka mwandishi wa habari hizi kufika ofisini kwake akiwa na kitambulisho ndipo anaweza kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu suala hilo.

Mabilioni yakusanywa

Hivi karibuni Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abbas Tarimba alinukuliwa na mtandao wa Blog ya Jaizmela Leo pamoja na gazeti la Nipashe ambapo alisema kuwa michezo hiyo imekuwa chanzo kikubwa cha mapato kwenye bodi hiyo na kuongeza mzunguko wa fedha unaozidi Sh bilioni 1.4 kwa mwezi.

Alisema michezo hiyo ya kubahatisha inafanya vizuri, kwani mapato yake kwa bodi hiyo hufikia Sh bilioni 14 kwa mwaka.

“Huu mchezo umekuwa na mchanago mkubwa katika pato la Taifa kwa mwaka 2012/13 hadi Desemba 2015 Shilingi bilioni 14.0 zilikusanywa na pia kutoa ajira zaidi ya 7,000 kwa watu wa rika mbalimbali,” alisema Tarimba.

Mkurugenzi huyo wa michezo ya kubahatisha, alisema kuwa sheria ya michezo ya kubahatisha inakataza mtoto chini ya umri wa miaka 18 kushiriki mchezo huo.

Kutokana na hali hiyo aliwataka wamiliki wa vituo vya kamari hizo kufuata kanuni zilizoainishwa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini.

Tarimba alisema matatizo kadhaa yanayojitokeza kwenye michezo hiyo ni pamoja na malalamiko ya kutotendewa haki kwa wachezaji.

Bajeti ya Serikali

Akiwasilisha bajeti ya mwaka 2016/17 katika Bunge la Bajeti Juni 9 mwaka huu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, alisema Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania,  inatarajia  kukusanya  kodi itakayofikia Sh bilioni  34.72,  sawa  na  ongezeko  la  asilimia  26.35 ikilinganishwa  na  Sh bilioni  27.48  inayotarajiwa  kukusanywa  katika  mwaka  wa 2015/16.

Kutokana na hatua hiyo bodi hiyo imejipanga  kuendelea  kusimamia  vema  sekta  ya  michezo  ya  kubahatisha  nchini  na  kuhakikisha  kwamba  inaendelea  kuendeshwa  kwa  mujibu  wa sheria.

“Bodi inatarajia kuchangia kiasi cha Shilingi bilioni 2.17 kwenye Mfuko Mkuu wa  Hazina  katika  mwaka  2016/17  hii  ikiwa  ni  sawa  na  ongezeko  la  asilimia  50.69  ikilinganishwa na Shilingi bilioni 1.44  ya mwaka wa 2015/16,” alisema Waziri Dk. Mpango

Kauli za wachezaji

Mmoja wa wachezaji wa mchezo huo aliyehojiwa na gazeti hili, Said Simion mkazi wa Magomeni Mwembe Chai, alisema alianza kucheza mchezo huo mwaka jana na amefanikiwa kushinda mara nyingi.

“Nimeshawahi kushinda na kufanikiwa kupata Sh 200,000 mara mbili, na pia nimeshinda na kupata Sh  500,000 mara tatu lakini kwa hizi fedha ndogo za 10,000 hadi 50,000 huwa nazipata kila wakati,” alisema

George Silawa ambaye amekuwa akibeti kupitia Kampuni ya Meridian, alisema ingawa anakosa mara moja moja, lakini mara nyingine amekuwa akishinda na kujipatia fedha ambazo huziingiza kwenye biashara yake ya duka.

Mmoja wa wapiga debe katika eneo la Manzese,  Kalama Kalama (26), alisema huwa anakusanya fedha zake na kwenda kucheza kamari hiyo kwa kubashiri ‘mkeka’.

“Binafsi huu mchezo huwa naupenda sana maana kuna siku nilipata Shilingi 10,000 lakini nikafanikiwa kwa kiasi kikubwa sana na nikienda kubeti huwa napata hadi Shilingi 70,000 na nikipata hutenga hata Shilingi 20,000 kucheza tena kwa siku inayofuata kwani ninakuwa na kianzio.

“Nina miaka miwili nacheza betting, kabla hata mchezo huu haujachukua umaarufu nilikuwa nacheza karata kamari,” alisema Kalama

Muuza mitumba Ally Kisukuna ambaye ni mfanyabiashara wa Mwenge, alisema kwa miaka mingi anashiriki mchezo huyo.

“Nacheza betting nina muda ila sijawahi kushinda. Sichezi kila siku ila ninapojisia,” alisema

Namna unavyochezwa

Wakala wa bahati nasibu ya Premier, iliyopo Msasani Albert Franchesco, alinukuliwa na gazeti moja (si MTANZANIA) alieleza jinsi kamari hiyo inavyochezwa na kwamba kushinda kunahusisha bahati na kuijua soka, wachezaji na timu zao.

“Ili kushiriki, mchezaji lazima uchukue ratiba ya timu zote. Huu ni kama mtihani wenye maswali. Maswali hayo huwa na namba ambazo kwenye kamari ni kama ‘code’.

“Kwa kawaida kila timu ina ‘code’ yake, unachotakiwa kufanya ni kuangalia pointi za timu kisha unazijumlisha pointi hizo pamoja na kiasi cha fedha unachoweka.

“Baada ya kuchagua timu zako, unapeleka karatasi yako kwa wakala ambayo huchapishwa na kutolewa kitu kinachoitwa ‘mkeka’. Baada ya kupata mkeka, unasubiri timu hizo zicheze na baada ya hapo timu zako zote ulizochagua zikishinda basi utajipatia fedha ambazo ni jumla ya kiasi cha fedha na idadi ya pointi za timu ulizochagua,” alisema

Kwa upande wake Meneja Uendeshaji wa Premier Betting, Javier Diaz Del Rio, ambayo huchezesha mchezo huo hususan kwa ligi za Ulaya kama ligi ya kuu za England, Hispania, Ujerumani na Ufaransa, alisema kampuni hiyo hutoa zawadi hadi Sh bilioni 2 kwa mwezi.

“Fedha zetu huwa tunatoa papo kwa papo, mteja anaweza kuchukua kwa wakala wetu kama ni kiasi kidogo au kwenye matawi yetu mengine kama ni kiasi cha kati ila kwa kiasi kikubwa wanakuja kuchukua makao makuu,” alisema Rio

Lugha inayotumika

Ubashiri huo katika michezo hiyo unajulikana zaidi kwa jina la ‘mikeka’ itakumbukwa kwamba mkeka ni kitu kama jamvi kinachoshonwa kutokana na kili na hutumika kwa kazi mbalimbali kama vile kukalia au kutandika kitandani.

‘Sports Betting’ iliitwa mikeka kutokana na karatasi zinazobandikwa katika ukuta wa matangazo katika kituo cha michezo ya kubahatisha ikionyesha mechi mbalimbali zinazotarajiwa kuchezwa.

Kwa Tanzania kuna makampuni zaidi ya 10 ya michezo ya kubahatisha ambapo baadhi ni Premier Betting, Gaming Africa (Meridian), Gateway Gaming (M Bet), New Africa Casino, Play Master na Dunia Investiment (iPlay8).

SUDAN KUSINI: Rais Salva Kiir Amemfukuza Kazi Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mabior Garang.

$
0
0
SUDAN KUSINI: Rais Salva Kiir amemfukuza kazi Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mabior Garang.

Sababu za kufukuzwa kwake bado hazijawekwa wazi, nafasi yake imechukuliwa na Sofia A. Gai

Diamond Aitolea Ufafanuzi Picha ya Hamisa Aliyopiga Kwenye Chumba Alicholala na Zari

$
0
0

Baada ya ukaribu wa hivi karibuni wa mwanamitindo Hamisa Mobetto na familia ya Diamond kumekuwepo na sintofahamu kubwa.

Hivi karibuni kulionekana picha ambayo Hamisa amepiga kwenye chumba kile kile ambacho Diamond alilala na mchumba wake, Zari nchini Afrika Kusini.

Kupitia kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM, Diamond aliielezea picha hiyo pamoja na tetesi kuwa na uhusiano na mrembo huyo. “Hamisa nimeanza kumjua zamani sana na sina uhusiano wa kimapenzi na yeye, juzi kati alikuwa kwenye video yangu mpya nimefanya na Ray Vanny na hiyo ndo imeleta maneno maneno yote hayo.”

Na kuhusu picha iliyounganishwa wote wakiwa wametumia chumba kimoja alisema, “Pale ni South Africa sehemu ile inaitwa Capital ni apartment ambazo vyumba vyake vyote vinafanana kama unavyoona hata Madam Rita pia ana share katika hizo apartment naye anayo yake na pia wabongo wengi tunapenda kufikia hapo kidogo huwa ni rahisi.”

IS yamtangaza kiongozi mpya wa Boko Haram

$
0
0
Katika video ya Boko Haram , Abu Musab al-Barnawi ametajwa kuwa msemaji wa kundi hilo
Boko Haram

Kundi la wapiganaji wa Islamic State limetangaza kuwa kwamba tawi lake la Afrika magharibi la Boko Haram lina kiongozi mpya.

Abu Musab al-Barnawi ambaye alikuwa msemaji wa kundi hilo ndio anayeonekana kuchukua uongozi wa kundi hilo.Hatahivyo kundi halijasema nini kilichomtokea aliyekuwa kiongozi wake Abubakr Shekau.

Mara ya mwisho kusikika ni katika kanda ya sauti mwezi Agosti akisema kuwa yuko hai na kwamba nafasi yake haijachukuliwa -huku kanda ya video ya ISIS iliotolewa mwezi Aprili ikithibitisha hilo.KUndi la Boko Haram ambalo limepoteza eneo kubwa lililokuwa likidhibiti miezi 18 iliopita linapigana kuiondoa madarakani serikali ya NIgeria.

Mashambulio yake ya miaka saba yamesababisha vifo vya watu 20,000 hususan katika eneo la Kaskazini mashariki.

Vijana Wawili wa CHADEMA Wakamatwa Kwa Kudaiwa Kueneza Ujumbe wa Kichochezi

$
0
0
Vijana wawili wa CHADEMA huko Mbeya wamekamatwa na Jeshi la polisi mkoani Mbeya kwa kudaiwa kusambaza ujumbe wa kichochezi kwa kutumia simu.

Vijana hao ni Moses Ezekia Mwaifumba ambaye alikuwa ni Mwenyekiti wa BAVICHA Mbeya na mwenzake Meshack Yohana Mgaya mwenye umri wa miaka 28 ambaye polisi wamedai alikuwa anashirikiana na mtuhumiwa huyo
Video:

UTAFITI: Wasichana Wanaopenda Kuvaa Nguo Ndefu/Suruali Wana Miguu Myembamba!

$
0
0
Kwa kipindi kirefu nimejaribu kuwafuatilia wasichana wanaopenda kuvaa magauni au sekti ndefu katika karne hii ya ishirini na moja ili nijue kwamba wanavaa hivyo kutunza maadili ya Mwafrika au wana sababu zao nyingine...

Kwa utafiti wangu nimebaini kuwa zaidi ya asilimia sabini na tano ya wadada wanaovaa nguo ndefu na pia wanaovaa suruali wana usafiri mwembamba...

Orodha hii haijahusisha utafiti wa wale wanaovaa mavazi kulingana na imani zao... Imehushisha tu wale wanaovaa mavazi ya kawaida ambayo hayana muingiliano na imani yeyote...

Utafiti huu pia ukaendelea kubaini kuwa wadada wenye guu za bia hupenda sana kuvaa visketi au magauni mafupi na kuanika miguu yao hadharani...

HUYU Ndio Mwanaume Anaemzuzua Shamsa Ford Kimapenzi Kwa Sasa....

$
0
0
Mfanyabiashara wa nguo ‘Chidi Mapenzi’ yupo mbioni kufunga ndoa na mwigizaji Shamsa Ford baada ya hivi karibuni kumtolea barua mrembo huyo.

uigizaji huyo alikaririwa na gazeti la Mtanzania akisema kwamba licha ya kupita katika changamoto za wapenzi wengi, mpenzi wake huyo wa sasa ndiye aliyeonyesha ushawishi wa hadi kutaka kumuoa.

“Kwa hatua hii najivunia, hadi mwanaume akushawishi muoane huyo ana nia njema na heshima kwangu,” alisema Shamsa.

Picha: Wema Sepetu, Idris Wanaswa Wakipeana Mabusu Moto Moto Hadharani

$
0
0


Staa wa Bongo Movies, Wema Sepetu akiwa na mpenzi wake mshindi wa BBA 2014, Idris Sultan wakifanya yao

Freeman Mbowe Amtembelea na Kumjulia Hali Spika wa Bunge, Job Ndugai

$
0
0
Kiongozi wa Kambi rasmi  ya Upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe akisalimiana na Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai alipomtembelea nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam.Spika wa Bunge amerejea nchini hivi karibuni kutoka nchini India alipokwenda kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake.

Tundu Lissu Akamatwa na Jeshi la Polisi Akiwa Singida.....Msigwa Ahutubia Iringa, Adai Serikali Imekurupuka Kuhamia Dodoma

$
0
0
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amekamatwa na polisi muda mfupi baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Ikungi, Singida.

Wakati Lissu akiwa mikononi mwa polisi, Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa jana alifanya mkutano wa hadhara na kusema hakuna wa kumpangia cha kuzungumza kwenye mikutano yake.

Kukamatwa kwa Lissu
Lissu, ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema ndiye aliyetoa taarifa za kukamatwa kwake kwenye mtandao akisema: “Wakubwa sana salaam. Ninawaandikieni maneno haya nikiwa chini ya ulinzi wa polisi Singida.

" Nimemaliza kuhutubia mkutano wa hadhara mji mdogo wa Ikungi ambao ni makao makuu ya Jimbo langu la Singida Mashariki. Mara baada ya kushuka jukwaani nimefuatwa Regional Crimes Officer (RCO) wa Mkoa wa Singida aliyejitambulisha kwa jina la Babu Mollel na kunitaarifu kuwa ameelekezwa na Regional Police Commander (RPC) Singida nikamatwe apparently (dhahiri) kuna amri ya kunikamata iliyotoka Dar es Salaam.

 “Kwa hiyo niko nguvuni na ninasubiri maelekezo ya RPC juu ya wanakotakiwa kunipeleka. It’s likely (inawezekana) nitasafirishwa Dar usiku huu. In fact (hakika) ni usiku huu kwa taarifa za sasa hivi. Kwa vyovyote itakavyokuwa, there’s no turning back. There’s no shutting up (hakuna kurudi nyuma, hakuna kunyamaza).

"Nitapambana kutetea haki yetu ya kuwasema watawala popote nitakapokuwa, whether in freedom or in jail (niwe huru au jela)... Aluta continua!. "

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka  alithibitisha kukamatwa kwa Lissu lakini alikataa kutoa sababu za hatua hiyo.

Chadema jana jioni ilitoa taarifa kuhusiana na kukamatwa kwa Lissu ikisema: “Tunaweza kuthibitisha kwa vyombo vya habari kuwa Mwanasheria Mkuu wa Chama Mh. Tundu Lissu anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Singida kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi.”

Taarifa hiyo iliyotolewa na Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene ilibainisha kuwa Polisi walimkamata jana jioni baada ya kumaliza mkutano wake wa hadhara alioufanya Ikungi jimboni kwake na kueleza kuwa viongozi wa chama hicho mkoani humo walikuwa polisi kuhakikisha anapata haki zake kama inavyostahili na kwamba ofisi ya katibu mkuu inafuatilia kwa ukaribu kujua sababu hasa ya kushikiliwa kwake na kutoa msaada wa haraka kadri itakavyohitajika.

Lissu amekuwa kwenye misukosuko na Jeshi la Polisi mara kadhaa na kwa siku za karibuni alikamatwa na kufikishwa mahakamani akituhumiwa kutoa maneno ya uchochezi kwenye gazeti la Mawio.

Sambamba na kesi hiyo, Lissu alikamatwa na polisi kwa madai ya kutoa maneno ya uchochezi baada ya kupata dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Msimamo wa Msigwa
Mkoani Iringa, Msigwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa kwanza wa kibunge tangu alipochaguliwa uliofanyika kwenye viwanja vya Mwembetogwa mjini hapa, alisema hakuna wa kumpangia hoja za kuzungumza kwenye mikutano yake.

Juzi, mbunge huyo alipewa barua na Jeshi la Polisi iliyoeleza kuwa imempa kibali cha kufanya mikutano hiyo, lakini ikimuwekea masharti mbalimbali likiwamo la kutozungumzia viongozi wengine na badala yake ajikite kwenye shughuli za maendeleo na kuchukua maoni ya wananchi anaowawakilisha.

Pia, alitakiwa kuhakikisha kuwa hakuna mtu kutoka nje ya Mkoa wa Iringa au eneo lolote lililo nje ya mamlaka atakayeruhusiwa kuzungumza.

Lakini jana akihutubia alisema: “Ninaona watu wote mna nyuso za hofu na mimi nimekuja kuwaondoa hofu …hakuna mtu mwenye mamlaka ya kunipangia cha kuzungumza, sipo hapa kwa matakwa ya polisi … mimi nipo kwa matakwa ya kisheria na ninazungumza kwa mamlaka mliyonipatia.

 “Pia Katiba inaeleza wazi mad raka na kinga ya Mbunge… mbunge anayo haki ya kuitisha na kufanya mkutano wa hadhara kwa mjibu wa sheria.”

Kuhusu Rais kuzuia mikutano ya vyama vya siasa, Msigwa alisema hakubaliani na hatua hiyo kwa madai kuwa kufanya hivyo ni ukiukaji wa Katiba ya nchi na Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992 ambavyo nchi inayoongozwa chini ya utawala wa kidemokrasia inapaswa kuvifuata.

 “Ninamuunga mkono na ninampongeza Rais John Magufuli kwa kupambana na ufisadi, anapinga rushwa… lakini siungani naye kwa kitendo chake cha kukandamiza demokrasia nchini na niwaombe wananchi wa Iringa kuungana na mimi kumpinga mtu anayekandamiza demokrasia nchini,” alisema.

Kuhusu Serikali kuhamia Dodoma, mbunge huyo ambaye pia ni waziri kivuli wa Wizara ya Mambo ya Nje, alikosoa uamuzi huo akisema hajawahi kuona katika mipango yote iliyowasilishwa na Serikali bungeni inayoelekeza hilo.

“Serikali ilileta mpango wake wa miaka mitano, mwaka mmoja na Bajeti, hivi vyote vinaletwa bungeni na baada ya kujadiliwa na kupitishwa, vinatungiwa sheria ili viweze kutekelezwa hivyo vipaumbele vyake ni lazima vifiti kwenye mipango hiyo,” alisema Msigwa na kuongeza:

 “Lakini katika vyote vitatu vya mwaka huu, mpango wa miaka mitano, mwaka mmoja na hata katika bajeti ya mwaka huu sijaona mahali popote palipoandikwa kipaumbele cha Serikali ni kuhamia Dodoma.”

Msigwa alisema kuhamisha Serikali ni gharama kubwa na kuwataka wakazi wa Iringa na maeneo mengine kuhoji suala hilo kama ndicho kipaumbele cha maendeleo na mahitaji yao.

Alisema wamejipanga kufanya shughuli za maendeleo ikiwamo miradi ya barabara, kuboresha huduma za afya, usafi wa mazingira na miundombinu.

Mkutano huo ulihudhuriwa na madiwani wa halmashauri hiyo wakiongozwa na Mstahiki Meya, Alex Kimbe.

Muonekano Mpya wa Msanii Raymond wa Wasafi Record ya Diamond

$
0
0
Huu ndio muonekano mpya wa mtindo wa nywele wa kijana Raymond wa wasafi,kijana anaye hit kwa sasa na ngoma yake ya natafuta kiki, Kwa Mimi ninavyoona kiukweli kwa muonekano huu wa mtindo wa nywele aliouweka naona hajapendeza kabisa ni bora angebaki na muonekano wa kawaida ulikuwa poa sana.
Je wewe unaonaje?
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images