Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Utafiti: Watz Wengi Wameajiriwa Kwenye Ulinzi

$
0
0
Wanzania haiwezi kupiga hatua kimaendeleo na kupunguza tofauti ya hali ya maisha na kipato kwa watu wake iwapo idadi kubwa ya nguvu kazi ipo kwenye sekta ambazo hazina umuhimu mkubwa katika uzalishaji.


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa taasisi ya Society for International Development - SID ya nchini Canada na yenye ofisi zake jijini Nairobi nchini Kenya Bw. Arthur Muliro, amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa ripoti ya hali ya kipato kwa wakazi wa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki, ripoti iliyotolewa jijini Dar es Salaam hii leo.

Katika maelezo yake, Bw. Muliro amesema utafiti umeonyesha kwamba zaidi ya Watanzania milioni moja wameajiriwa kwenye sekta ya ulinzi na masuala ya usalama, idadi aliyodai kuwa ni tofauti na katika sekta nyingine muhimu kama za uhandisi na wataalamu ambao kwenye baadhi ya sekta idadi yao haizidi watu elfu kumi na sita.

Ameshauri kuwa juhudi kubwa zinahitajika kuongeza wataalamu kwenye sekta zilizoajiri watu wengi kama kilimo ambacho takribani asilimia themanini ya watanzania ndiyo wanayoitegemea kwa ajili ya kuendesha maisha yao.

Ripoti hiyo imetolewa na taasisi inalojihusisha na uboreshaji mazingira ya biashara, uchumi na uwekezaji kwa nchi za Afrika Mashariki ya Trade Mark East Africa ambapo SID ndiyo iliyofadhili utafiti huo uliohusisha nchi za Tanzania, Uganda, Rwanda, Kenya na Burundi.

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu ya Agosti 8

$
0
0


SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu ya Agosti 8

Polisi Wazuia Ghafla Mkutano wa CHADEMA Chalinze, Mbowe Asema Wapo Tayari Kufa Kwa Kupigania Demokrasia

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limefuta mkutano wa hadhara wa Chadema uliopangwa kufanyika katika Uwanja wa Miembe Saba mjini Chalinze.

Mkutano huo uliokuwa ufanyike jana, ulikuwa uhutubiwe na Waziri Mkuu mstaafu na mjumbe wa kamati ya Chadema, Frederick Sumaye.

Mwenyekiti wa Chadema, Mkoa wa Pwani Baraka Mwago alisema jana kuwa alishangazwa na hatua hiyo ya ghafla ya polisi kwa kuwa mkutano huo ulifuata taratibu zote na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Chalinze, aliruhusu kufanyika kuanzia saa 6.00 mchana hadi saa 12.00 jioni.

Alisema wakati maandalizi yote yakiwa tayari, ilipotimia saa nane mchana waliitwa polisi na kuelezwa kuwa mkutano huo umezuia kwa maelezo kuwa intelijensia ya polisi imeonyesha kuwa ungehudhuriwa na viongozi wengi wa kitaifa, hivyo polisi Chalinze haijajipanga kutoa ulinzi kwa viongozi hao.

“Hii sababu imetushangaza kwa sababu kiongozi wa kitaifa ambaye angehudhuria ni Sumaye peke yake."

Kwa mujibu wa Katiba ya Chadema kipengele cha 7.5.3 (f) inamtambua mjumbe wa kamati kuu au baraza kuu anayeishi katika mkoa kuwa ni mjumbe wa baraza la mkoa husika.

“Kutokana na kipengele hicho, Sumaye ana sifa za kuhudhuria mkutano huu kwa sababu anaishi Kiluvya wilayani Kisarawe,” alisema Mwagu.

Alisema lengo la mkutano huo, lilikuwa ni kuutambulisha uongozi mpya wa Chadema kwa wananchi baada ya kufanyika uchaguzi mdogo Juni 4, mwaka huu wilayani Mkuranga.

Katibu wa Chadema mkoani humo, Halfani Milambo alisema waliandika barua kuwataarifu polisi na likakubali, lakini walishangazwa kuzuiwa baada ya kufika katika Uwanja wa Miembe Saba walikotakiwa kufanya mkutano.

“Tuliwaandikia barua tarehe Agosti 4 na siku iliyofuata Agosti 5 tulikubaliwa na Mkuu wa Polisi Chalinze (OCD), SSP J. Magomi kufanya mkutano kwa masharti,” alisema.
Alitaja masharti ambayo jeshi hilo liliwapa kuwa ni pamoja na kutokuwapo kwa maandamano ya bodaboda, ya miguu au magari, kutokukashifu chama au utawala wa kiongozi yeyote na kuzingatia muda wa kuanza na kumaliza mkutano.

Alisema kuwa cha kushangaza jana baada ya kukamilisha maandalizi yote ikiwamo kufanya matangazo na kufunga vyombo vya muziki, baadhi ya viongozi waliitwa kwenye Ofisi ya Polisi Wilaya ya Chalinze na kuambiwa wasifanye mkutano huo.

Alisema walielezwa kuwa ujumbe ambao unaenea kwenye mtandao unasema mkutano huo utaleta watu wengi sana, hivyo usalama utakuwa mdogo.

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Boniventura Mushongi alisema lengo la Polisi si kuwakataza kufanya mkutano, lakini kilichoonekana ni kuwa walikiuka maelekezo kwani awali walipaswa kufanya mkutano wa ndani na si wa nje.

“Sisi hatuwakatazi kufanya mikutano yao, lakini ni vema wafuate makubaliano, maana sisi Jeshi la Polisi tuliwaruhusu wafanye mkutano wa ndani lakini tulishangazwa kuona wanaanza kufanya nje huku wakipiga muziki,” alisema.

Mushongi alisema pia polisi inazuia mikutano yote ambayo haina madiwani wala wabunge katika eneo husika, jambo ambalo halikuwa kwenye maelekezo ya OCD.

“Chadema katika eneo la Chalinze hawana diwani wala mbunge, hivyo wamekosa sifa za kufanya mkutano huu. Kama ni kikao cha ndani hatuna tatizo wafanye hata wakialika watu 200,” alisema Mushongi.

Hata hivyo, Mushongi alisema Chadema Pwani walipopeleka barua ya maombi mkutano huo walipewa masharti hayo.

Mbowe: Tuko tayari kwa lolote
Wakati hayo yakiendelea, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema yeye na makamanda wake wako tayari kwa lolote kwa ajili ya kutetea misingi thabiti ya utawala bora unaoheshimu utawala wa sheria.

Akizungumza  jana, Mbowe alisema hakuna mtu wa kuwafundisha makamanda wa Chadema, hivyo mikutano ya Ukuta itafanyika nchi nzima kuanzia Septemba Mosi.

“Ambao hawako tayari warudi nyuma, hakuna aliyelazimishwa, watuache sisi tutangulie wa kufa wafe na wa kupona wapone. Haiwezekani mtu apuuze sheria, avunje katiba halafu taifa linyamaze,” alisema.

“Sisi tumeamua kuchukua mzigo huo kwa niaba ya wananchi wote. Kama ataua wacha aue tu, kama atatufunga wacha atufunge tu lakini tutakuwa tumeacha legacy (kumbukumbu) duniani,” alisisitiza.

Mbowe alisema sifa ya kiongozi bora anayeheshimu misingi ya kidemokrasia ni kuheshimu utawala bora unaoheshimu utawala wa sheria.

Kwa mujibu wa Mbowe, Rais anakiuka Katiba na sheria za nchi zinazoruhusu vyama vya siasa kuendesha mikutano ya hadhara na hakuna mtu ndani ya CCM anayezungumzia hilo.

Mbowe alisema Rais amejisahau kuwa yeye (Mbowe) ni mwenyekiti wa taifa kama alivyo Rais, hivyo anastahili kuzunguka nchi nzima kujenga uhai wa chama.

“Rais anazunguka kwenye mikoa anavisema vyama vya upinzani na kutoa amri mbalimbali lakini sisi (upinzani) hatuna jukwaa la kujibu au kutoa ufafanuzi. Anasema tusubiri hadi 2020,” alilalamika Mbowe.

“Rais anatoa amri, wakuu wake wa mikoa wanatoa amri, wakuu wa wilaya wanatoa amri, watu wanafukuzwa kazi ovyo. Nchi haiwezi kwenda kwa staili hii,” alisema.

“Wewe unanyanyuka tu na kusema watu wahamie Dodoma kivipi? Issue ya kuhamia Dodoma ni suala la kitaifa siyo mamlaka ya mtu mmoja tu kwa kuwa ni Rais.”

 “Hata Nyerere 1973 alipopitisha hoja ya watu kuhamia Dodoma kilikuwa ni kikao cha NEC ya Tanu. Mpaka leo hakuna sheria ya kuhamia Dodoma na nchi hii inaoongozwa kwa sheria.”

Mbowe alisema kwa kutambua kuwa hakuna sheria ya kuhamia Dodoma, ndiyo maana Ilani ya CCM (2015-2020) imeeleza kutengeneza sheria ya kuhamia makao makuu Dodoma.

“Hakuna sheria. Rais hawezi kuamua matakwa yake binafsi yakawa ni sheria ya nchi. Alipaswa apeleke muswada wa sheria bungeni na ipitishwe na Bunge siyo kauli ya mtu mmoja,” alisisitiza Mbowe.

Lissu: Tutafuata sheria
Wakati huohuo, mwanasheria Mkuu wa Chadema na mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amesema katika utekelezaji wa Ukuta watafuata sheria kwa kupeleka barua za taarifa ya mikutano kwa wakuu wa polisi nchi nzima saa 48, kabla ya kuanza mikutano hiyo Septemba Mosi mwaka huu.

Akizungumza juzi katika mahojiano na Redio ya Sauti ya Ujerumani (DW), Lissu alisema mikutano hiyo itafanywa kwa kufuata sheria na taratibu ikiwamo kutoa taarifa kwa wakuu wa polisi wa wilaya.

Lissu ambaye aliachiwa na mahakama juzi kwa dhamana, alitoa kauli hiyo baada ya kuulizwa kwanini chama chake kisitafute njia mbadala ya operesheni Ukuta ambayo Serikali imesema itakabiliana nayo kwa njia yoyote ile.

“Tumesema hatutafanya mkutano wowote usiokuwa na taarifa.Tutapeleka taarifa kwa wakuu wa polisi wilaya wote Tanzania nzima kama inavyotakiwa. Sasa hiyo hatuvunji sheria, tunatekeleza sheria,” alisema Lissu.

Mbunge huyo, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya uchochezi na kuidharau mahakama, alibainisha kuwa mikutano ya hadhara kuanzia Septemba Mosi, itafanyika kwa mujibu wa sheria za nchi kama Katiba ya nchi na sheria ya vyama vya siasa inavyoeleza.

Alisema sheria inasema chama cha siasa ambacho kimeandikishwa kikitaka kufanya mkutano wowote wa hadhara wa siasa, kinatakiwa kupeleka barua ya taarifa kwa mkuu wa polisi wa wilaya saa 48 kabla ya mkutano huo.

“Sheria inasema huyo ambaye tunampelekea taarifa atupe ulinzi kwenye mikutano yetu. Ndicho tunachotaka,” alisema Lissu.

Alipoulizwa kama ni sawa iwapo polisi ikisema haiwezi kuwapa ulinzi na wasifanye mkutano katika eneo husika kwa wakati huo, Lissu alijibu, “(OCD) Ana uwezo wa kutuambia msifanye leo, msifanye kwenye eneo hili au msifanye saa hii, lakini hana uwezo wa kukataa katakata.”

Mbunge huyo alisema kilichotokea nchini na kinachofanyika sasa si mikutano kudhibitiwa bali inakatazwa.

“Hakuna sheria inayokataza au inayowapa mamlaka ya kukataza mikutano moja kwa moja kama hakuna tangazo la hali ya hatari,” alisema Lissu.

Alisema kama Magufuli hataki mikutano atangazie dunia kwamba Tanzania ina hali ya hatari.

“Akitangaza hali ya hatari tutamwelewa na wengine tutamuuliza kilichotokea ni kitu gani mpaka kuwe na hali ya hatari,” alisema Lissu.

Sikia Mkwara Huu wa Banana Zorro

$
0
0
Mkali kunako muziki wa kizazi kipya, Banana Zoro amejigamba kuwa hahofii kuimba bila kutumia vyombo kwani uwezo wake kwenye muziki ni mkubwa haswaa.

Akiongea hivi juzi Banana amesema wasanii wengi wanashindwa kuimba bila kutumia vyombo kwasababu hawajitumi katika kazi hiyo. “Mimi naweza kuimba bila kupiga vyombo au midundo na watu wakaelewa nini ninafanya kwani nipo kwenye muziki muda mrefu na najua ninachokifanya” alimalizia.

KRC Genk ya Samatta Imepoteza Mechi Dakika ya 90 Dhidi ya KAA Gent

$
0
0
Usiku wa August 7 2016 Ligi Kuu Ubelgiji iliendelea tena kwa klabu ya KAA Gent kuikaribisha KRC Genk katika uwanja wa GHELAMCO wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 20,000 ili kucheza mchezo wao wa pili wa Ligi Kuu Ubelgiji.

Katika dakika zote 90 KRC Genk walicheza na kumiliki mpira kwa asilimia 40 wakati wenyeji wao KAA Gent walikuwa wameutawala mchezo kwa asilimia 60, licha ya KRC Genk kufanya mabadiliko katika safu ya ushambuliaji kwa kumtoa Nikolaos Karelis na kumuingiza mtanzania Mbwana Samatta dakika ya 66, walifungwa goli  1-0.

KRC Genk kutokana na kuwa ugenini na kushambuliwa kwa kiasi kikubwa, hali ilikuwa mbaya dakika ya 90 baada ya KAA Gent kupata goli la ushindi na kujichukulia point tatu kupitia kwa mshambuliaji wao aliyeibuka mfungaji bora msimu uliopita Jeremy Perbet, Genk itacheza nyumbani August 13 2016 dhidi ya W. Bevern.

Mama Mwenye VVU Pamoja na mtoto wake wakutwa wamekufa mlimani

$
0
0
MKAZI wa wilayani Chato mkoani Geita, Rose Joseph (32) aliyekuwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi na mtoto wake mwenye umri wa miaka kati ya minne na mitano, wamekutwa mlimani wakiwa wamekufa katika mazingira ya kutatanisha katika kijiji cha Nafuba kilichoko ndani ya Ziwa Victoria wilayani Bunda mkoani Mara.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Nafuba, Zakaria Kachimu alisema tukio hilo liligundulika juzi saa 9:00 mchana katika eneo la mlima huo, baada ya wananchi waliopita katika eneo hilo kuona kwanza mwili wa mwanamke huyo.

Alisema baadaye wananchi walifanikiwa kumtafuta mtoto wake na kumkuta pia akiwa amekufa katika eneo lingine.

Kachimu alisema mwanamke huyo alifika kisiwani hapo Julai 25, mwaka huu, akiwa na mtoto mdogo wa kiume aitwaye Kababu, akiwa anatafuta kazi ya kuhudumia kwenye mgahawa.

Alisema kuwa kulingana na afya ya mwanamke huyo kudhoofika, kila sehemu alikokwenda kutafuta ajira hiyo alikataliwa. Baada ya kukosa ajira hiyo mwanamke huyo alikwenda kwa jamaa yake ambaye pia ni mwanamke aliyeko kisiwani hapo na kuishi nyumbani hapo.

Baadaye mwanamke huyo alikwenda kutibiwa katika zahanati moja iliyoko kisiwani hapo na ikagundulika kuwa ana mambukizi ya virusi vya Ukimwi na kuambiwa aende katika Kituo cha Afya Kisorya kwa ajili ya kujiunga kwa kupewa dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi (ARVs).

Hata hivyo ilielezwa kuwa mwanamke huyo hakwenda kwenye kituo hicho kama alivyoshauriwa na mganga wa zahanati hiyo.

Aidha, Ofisa Mtendaji huyo alisema siku ya tukio wananchi waliopita katika eneo hilo walikuta mwili wa mwanamke huyo katika mlima huo na kuamua kutoa taarifa, ambapo tena walianza kutafuta mtoto wake na kukuta pia akiwa amekufa katika eneo lingine.

Alisema kuwa chanzo cha vifo hivyo ni cha kutatanisha na kwamba huenda mtoto huyo alikufa kwa njaa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhani Ng’anzi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo. Alisema upelelezi unafanyika kujua chanzo cha vifo hivyo.

Mwigulu Nchemba 'Atangaza Vita' Kwa Wauza Madawa ya Kulevya Nchini

$
0
0
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ametoa siku 14 kwa maofisa wanaohusika na udhibiti wa dawa za kulevya kwenye mpaka wa Tunduma mkoa wa Songwe, kuwakamata watu wanaohusika na uvushaji wa dawa hizo kutoka nchini kwenda nchi jirani ya Zambia na nyingine zilizopo ukanda huo.

Nchemba alitoa agizo hilo jana, alipofanya ziara ya kukagua mpaka huo, ambapo alisema ni jambo lisilofichika kuwa kwa sasa Tanzania imechafuka kutokana na dawa za kulevya.

Alisema kutokana na Watanzania wengi kukamatwa katika nchi mbalimbali duniani, wakijihusisha na usafirishaji wa dawa za kulevya, imefikia hatua kwa baadhi ya nchi kufikiria kuongeza masharti zaidi kwa kila atakayejitambulisha kuwa Mtanzania.

“Hatuwezi kuacha nchi ikachafuka kwa sababu tu ya watu wachache.Ukienda China Watanzania zaidi ya 200 wanashikiliwa kwa dawa za kulevya, Pakistan wapo, India, Afrika Kusini ni Watanzania. Hili linatuchafua sana,” alisema Nchemba.

Aliutaja mpaka wa Tunduma kuwa miongoni mwa maeneo yanayoongoza kwa kupitisha dawa hizo na kutaka nguvu kuongezwa zaidi ili kuwezesha misako.

Alisema wapo watu ambao si makondakta wa mabasi wala abiria, lakini wamekuwa wakisafiri kila siku kwenye mabasi, hatua inayodhihirisha kuwa ndiyo wanaojihusisha na usafirishaji wa bidhaa hizo haramu.

Alisema watu hao wamekuwa na ushirikiano na watu wengine katika miji ya jirani, kabla ya kufika mpakani ikiwemo kijiji cha Mpemba wilayani Momba mkoani Songwe, ambapo wakifika hapo basi husimamishwa na mzigo kushushwa, kisha kusafirishwa kwa njia za panya hadi ng’ambo ya nchi.

“Wakati ninyi mnafanya utaratibu wa kawaida wa kupitisha gari husika hapa mpakani, wao wanavusha kupitia njia za panya. Basi likishavuka na mzigo unakuwa umefika Zambia wanakutana na kuupakia tena kisha wanaendelea na safari.

“Na katika hili ni lazima mzungumze pia na wenzenu wa upande wa pili, wadhibiti pia mji unaofuata baada ya huo wa mpakani maana huko ndiko wanakopakia tena. Kama mtashindwa katika wiki mbili, nitakuja mimi mwenyewe na nitawakamata tu,” alisisitiza.

Habari Njema Kwa Mashabiki wa Man United Kuhusu Usajili wa Mchezaji Paul Pogba Hii Hapa

$
0
0
Headlines za kiungo wa kimataifa wa Ufaransa aliyekuwa anaichezea klabu ya Juventus ya Italia Paul Pogba kuhusishwa kujiunga na Man United, zinaelekea kumalizika kwa kiungo huyo kurudi Man United toka aondoke mwaka 2012.

Leo August 7 2016 klabu ya Juventus ambayo ilikuwa inahitaji rekodi ya dunia ya usajili ya pound milioni 100 kama ada ya usajili wa staa huyo, imemruhusu staa huyo kufanya vipimo vya afya Man United.

Pogba ambaye ana umri wa miaka 23 aliondola Man United 2012 na kujiunga na Juventus kwa dau la pound milioni 1.5, Pogba amefanikiwa kushinda mataji manne ya Ligi akiwa na Juventus. Pogba atakuwa staa wa nne kusaliwa Man United chini ya Jose Mourinho baada ya  Eric Bailly, Ibrahimovic na Henrikh Mkhitaryan.

Video Queens wa Bongo na Skendo za Picha Chafu!

$
0
0
Video Qeen Tunda Akiwa Chooni Akijisaidia na Kujipiga Picha, Picha Imekatwa Kwa maadili
Hivi karibuni vijana wengi wa kike wanaotumiwa na wasanii wetu katika utengenezaji wa video zao wamekuwa na mtindo mchafu wa kupiga picha za nusu uchi na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii,swali la kujiuliza hapa je ni lazima vijana hawa kukaa nusu uchi ndo wapate kazi au kuna biashara zingine wanazifanya kwa mgongo wa kuwa video queens?maana sasa imekuwa kero kila ukiingia kwenye mitandao ya kijamii unakutana na picha zao kwa kweli ndo maana kumekuwa na

Msukuma: Sijawahi Kuwa Rafiki wa Edward Lowassa

$
0
0
Akizungumza asubuhi hii kupitia star tv,Joseph Kasheku (msukuma )amesema hajawahi kuwa rafiki wa Lowassa na alichokuwa anakifanya mwaka jana ni umamluki kama wanavyofanya askari kwenye vita.

Amesema wazi kuwa alitumwa kumpeleleza Lowassa kipindi hicho.Pia amesema hajawahi kuchukua hata senti moja ya Lowassa,na kama kuna mtu anajua alichukua hela ya Lowassa aseme na yupo tayari kuzirudisha.

My take: Kabla ya mtu kuwa na rafiki au sponser mchunguze vya kutosha.

Nay wa Mitego kuachia video ya wimbo ‘Pale Kati’ Jumatano hii

$
0
0
Rapper Nay wa Mitego amedai ametimiza katakwa aliyopewa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) baada ya kufungiwa kwa wimbo wake wa ‘Pale Kati’, ambapo Jumatano hii taachia version ya kwanza ya video ya wimbo huo.

Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii, Nay amewataka mashabiki wake wa muziki wa kimataifa kukaa mkao wa kula.

“Mimi na BASATA tulishamalizana, wao walinipa maazimio na mimi nimeshayatekeleza, kwa hiyo na mimi naendelea na issue zingine,” alisema Nay. “Jumatano hii mashabiki wangu Wakimataifa pamoja na wa kwenye mitandao ya kijamii wakae mkao wa kula, naachia video,”

Rapper huyo alisema wimbo wa ‘Pale Kati’ una nguvu kubwa sana na unafanya vizuri katika baadhi ya nchi kama Kenya, Uganda pamoja na Ghana, na ndio maana ameamua kuanza kutoa video kwa ajili ya kimataifa kwanza.

Pia amewataka mashabiki wa muziki wake kuendelea kusubiria mambo mazuri kwani wimbo huo una video nne.

Mwenge Wamtia Matatani DC Mwanza

$
0
0
MARY Tesha, Mkuu wa Wilaya (DC) Nyamagana mkoani Mwanza, anadaiwa kuhusika kuzuia shughuli zote za kijamii na kiuchumi katika wilaya yake ili wananchi wote wakaimbe wimbo wa Taifa na kuupokea mwenge wa uhuru, anaandika Charles Mseti.

Mwenge wa uhuru utawasili leo Nyamagana ukitokea Sengerema mkoani Mwanza na tayari umeibua hisia kali baada ya wananchi kutakiwa kutoendelea na shughuli zao za kujiingizia kipato na kuhudhuria mapokezi yake.

Gari la Jiji la Mwanza limepita asubuhi ya leo na kuwatangazia wananchi wote kusitisha shughuli zao kwa madai kuwa leo ni sikukuu ya Nanenane na mwenge wa uhuru huku barabara ya Nyerere inayounganisha Jiji la Mwanza ikifungwa kabisa.

Amri ya kusitisha shughuli zote ili kuhudhuria mapokezi ya mwenge wa uhuru inadaiwa kutolewa na DC Tesha huku gari mali ya jiji la Mwanza ikizunguka kutoa matangazo hayo.

Julai 3, mwaka huu, DC Tesha pia anadaiwa kuwaita ofisini kwake walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari wilayani humo na kuwataka kuhudhuria mapokezi ya mwenge wa uhuru huku akiahidi kuchukua hatua kali za kinidhamu kwa wasiohudhuria.

“Wasiwasi wa DC Tesha ni watu wachache kujitokeza kutokana na watu wengi kutokuwa na mwamko na mwenge kama zamani ndiyo maana ameamua kuita walimu ofisini kwake na kuwatisha,” ameeleza mwalimu mmoja huku akiomba jina lake lihifadhiwe.

DC Tesha alipotafutwa na mtandao huu ili kuzungumzia suala hilo ikiwemo vitisho dhidi ya walimu, simu yake ya mkononi iliita pasipo kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno (SMS) hakuweza kujibu.

James John mwandishi wa vikao vya jiji la Mwanza akiwa katika gari la jiji asubuhi ya leo ametangaza kuwa mwenge huo utalala wilayani Nyamagana na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo na wananchi wakitakiwa kushiriki na kujitokeza kuimba wimbo wa uhuru wa Tanzania.

Mkurungenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, kufuatia gari la Jiji kupita na kuwatangazia wananchi kusitisha shughuli zao, simu yake haikupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno (SMS) hakujibu.

Wanaume Kwa Hili Mnatutesa Mnatuvurugia Wengi

$
0
0
Jamani wanaume wa kizazi hiki cha nyoka sjui mpoje, mkianza mahusiano na mtu mkapeana namba utasikia "bby una watsup" Imo n.k ili uanze kudai picha za uchi na kufanya video calls.Kiukweli wadada wengi tumestukia hilo, na tunapinga vikali no video calls, no sex pictures at all.

Kama hutaki sauti pita hivii!Kingine msitupangie matumizi ya simu zetu, hujainunua wewe sa kiherehere cha nini, kila saa umenuna"bby simu ipo busy kila saa" haikuhusu!Nunua yako nipe kisha nipangie wakuchati nao.

Picha za uchi BIG NO, USINITUMIE WALA SIKU TUMII. TUKIPANGA MIADI YA KUKUTANA NITAANDAA SEHEMU MIMI NA SIO WEWE, POTELEA MBALI KULIKO UKAFUNGE MI KAMERA ILI UNIREKODI.

KINYWAJI NI JUICE TU, POMBE SITAKII

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Agosti 9

$
0
0


SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Agosti 9

Q Chief Azungumzia Ujio Wake Mpya Baada ya Kuweka Kambi ya Wiki Moja South Africa

$
0
0
Mwimbaji Q Chief amerejea nchini akitokea Afrika Kusini baada ya kuweka kambi nchini humo kwa wiki kadhaa kwa ajili ya kuandaa video yake mpya aliyoshoot na director mashuhuri, Justin Campos.

Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii, Q Chief amesema alienda kushoot video ya wimbo wake mpya Afrika Kusini ili kupata kitu kizuri.

“Mashabiki wasione ukimya, kuna mambo mazuri soon yanakuja, videos pamoja na mambo mengi mapya,” alisema Q Chief. “Nimetoka Afrika Kusini hivi karibuni kwa ajili ya video yangu mpya, nimefanya na Justin Campos, kwa hiyo mashabiki wakae mkao wa kula,”

Pia mwimbaji huyo amewashukuru mashabiki wake pamoja na media kwa kuendelea kusupport muziki wake.

Kayumba wa BSS Katoa Ufanunuzi Juu ya Milioni 50 zilivyotumika…

$
0
0
Msanii kutoka zao la Bongo Star Search 2015, Kayumba Juma amefunguka kueleza namna milioni 50 alizoshinda kwenye shindano la Bongo Star Search zilivyotumika.

Msanii huyo aliipata heshima millardayo.com na Ayo TV na kuyaongea haya:
’Kiasi nilichokichukua kilikuwa ni milioni 50 ambazo zimetumika katika matumizi yangu ambapo sasa hivi niko kwenye ujenzi wa nyumba yangu mpya iliyopo maeneo ya Mbagala na pia nimenunua usafiri wangu mpya wa kuzunguka hapa na pale kwenda studio na sehemu zingine’- Kayumba

Madee Afunguka Kuhusu Mkanganyiko wa Nani Anamsimamia Dogo Janja Tip Top

$
0
0
Msanii Madee leo ameweka wazi mkanganyiko ambao wengi walikuwa nao kuhusu msanii anayemsimamia Dogo Janja, mbaye pia yuko chini ya Tip Top ambayo inamsimamia yeye Madee.

Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Madee amesema ingawa Dogo Janja yupo chini yake, lakini iwapo kuna kazi anatakiwa kuifanya, lazima afanye mawasiliano na Babu Tale, na kufikia uamuzi kwa pamoja, tofauti na wengi wakivyofikiri kuwa yeye ndio ana uamuzi na Dogo Janja.

“Mtu akitaka collabo na Dogo Janja tunawasiliana na Babu Tale, na kama ishu ya kazi hawezi kukataa, lakini lazima tujadili, kwetu hatuishi kibosi bosi, kama ni jambo la msingi linawekwa mezani kila mtu anatoa maoni yake, kama afanye au asifanye”, alisema Madee.

Madee ambaye pia alianza kwa kumtoa msanii Raymond mpaka akachukuliwa na wasafi ambako yuko sasa, amesema anajivunia mafanikio ya msanii huyo, kwani tayari yupo kwenye historia yake.

Mwanaume Ajitokeza na Kudai Ameporwa Demu na Nuhu Mziwanda

$
0
0
Ubuyu wa mjini unanyetisha kuwa, mkali wa Bongo Fleva anayetamba na wimbo wake wa Jike Shupa aliomshirikisha Ali Kiba, Natfal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, anadaiwa kupora demu wa jamaa ambaye naye ni msanii wa wa Bongo Fleva, Valentino Michael ‘Vale wel’.
Mrembo anayedaiwa kuporwa kwa Vale ni yule Nawali ambaye kwa sasa Nuh anamnadi kuwa ni mpenzi wake wa kiyama.

Ubuyu ulionaswa na Wikienda ulidadavua kuwa mwenye demu wake alipigwa na butwaa alipomuona Nuh akimnadi Nawali kwenye mitandao ya kijamii ndipo akang’atwa sikio kuwa kwa sasa hana chake kwani ‘mtoto’ yupo mikononi mwa Nuh.

Akimwaga chozi mbele ya Wikienda, Vale alisema kuwa mpaka sasa hajaelewa ni kwa nini Nuh ameamua kumtangaza Nawali kuwa ni mpenzi wake wakati akijua wazi kwamba ni shemeji yake na ni mwanamke wake wa siku nyingi kwani wanafahamiana.

“Kiukweli nilikuwa sijui hili wala lile. Nilipoingia mitandaoni nilipigwa na butwaa kumuona Nuh akijitangazia ufalme kuwa mpenzi wake kwa sasa ni Nawali.
“Mwanzoni nilijua labda ni mambo ya kiki kwa sababu nijuavyo Nuh hana malengo mazuri na Nawali.

“Baadaye ndipo nikawa nahakikishiwa na watu wangu wa karibu kuwa ni wapenzi na hawafanyi kificho.
“Kinachoniumiza nilikuwa sina tatizo wala ugomvi wowote na Nawali na bado naamini ni mpenzi wangu kwa sababu hatujaachana na tukikutana huwa tuko kama kawaida,” alisema Vale.

MWENYE KISU KIKALI?
Vale alizidi kutokwa povu kuwa kwa sasa hasemi sana kwa sababu hana mkwanja wa kumpa Nawali hivyo ule usemi wa mwenye kisu kikali unamtafuna kwani inawezekana Nuh anatumia vijisenti alivyonavyo kumnyang’anya tonge mdomoni.

“Lakini ukweli ni kwamba ‘nafaiti’ na mambo yatakaponinyookea nitahakikisha nafanya kila njia kumrudisha Nawali kwenye himaya yangu kwani ndiye mwanamke wa maisha yangu.

“Najua nilipomtoa, ni mwanamke ambaye ninampenda sana na nimetumia muda mwingi kumbadilisha kimuonekano kwani mwanzoni hakuwa alivyo sasa, alikuwa mgumu hivyo nimefanya jitihada za hali ya juu kumfanya aonekane ‘soft’,” alimalizia Vale.
Mwanaume anayedai kuibiwa akiwa na niwale enzi zao

HUYU HAPA MTUHUMIWA NUH
Baada ya ubuyu huo ulionyooka kutua kwenye Wikienda, waandishi wetu walimweka ‘mtukati’ Nuh aliyedai kuwa hapendi kumuongelea mpenzi wake huyo kwa sababu kama ni maneno yameshasemwa mengi.

“Unajua kuhusu huyu demu wangu, maneno mengi sana yamesemwa hadi nimechoka. Kama huyo mwanaume yupo na anaamini ni mwanamke wake basi amchukue akakae naye,” alisema Nuh akiomba kuachwa atulize mawazo.

NAWALI ANASEMAJE?
Kwa upande wake Nawali, alipotafutwa kwa njia ya simu alisema kuwa hamjui Vale na wala hajawahi kupiga naye picha za kimahaba ambazo gazeti hili lina nakala zake.

Habari kutoka kwa Wana-Ubuyu wanaolinyaka vilivyo sakata hilo wanadai kwamba Vale ana uhakika kuwa huyo ni mpenzi wake na picha ametoa wakiwa wawili tena kimahaba hivyo inakuwaje Nawali anabisha?

HUYU NDIYE NUH
Mbali na Nawali, baada ya kufungishiwa virago na Zuwena Mohammed ‘Shilole’, Nuh alitua kwa mrembo mwingine shombeshombe ambaye hata hivyo hawakudumu

Imeandikwa na Global Publishers

Nafasi za Kazi East Africa Television EATV, Application Deadline 15 August 2016

$
0
0
East Africa Television EATV Wametangaza Nafasi za Ajira kadhaa, Kama una ndoto za kufanya kazi katika kampuni hiyo basi fanya kubonyeza HAPA : www.ajirayako.com

Unaambiwa Asilimia 61 ya Wanaomaliza Elimu ya Juu Tanzania ni Bongo lala...Wanauwezo Mdogo

$
0
0
UTAFITI: Asilimia 61 ya wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu wana uwezo mdogo, hawawezi kushindana katika soko la ajira nchini.
Kulingana na utafiti huo imegundulika kuwa vyuo Vikuu vingi vimekuwa haviangalii ubora isipokuwa hufanya Biashara tu.

Je ni Kweli ?

Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images