Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Waraka wa Wazi Kwa Rais Magufuli Toka Kwa Mbunge Godbless Lema "Haki Huinua Taifa"

$
0
0
Mh Rais nakusalimu, sasa ni usiku wa manane nimeamka nikiwa natafakari mambo mengi lakini zaidi sana ni kuhusu mwenendo wa demokrasia katika Nchi yetu, nimekosa usingizi kabisa nikifikiri ni namna gani ninaweza kusaidia kwa mawazo yangu kufanikisha nia yako njema katika ustawi wa Nchi yetu.

Mheshimiwa Rais na kabla sijaanza kuandika waraka huu kwako, nimesali nipate hekima ya kutosha juu ya maandishi haya ninayoandika na wewe pia nimekuombea sana kwa Mungu, kwani baada ya mimi na Wabunge wenzangu kufukuzwa Bungeni kwa kudai matangazo ya Bunge live nilikwenda kijijini kwetu kusalimia wazazi wangu, na nilipokuwa nawaelezea kwanini nimefukuzwa Bungeni matamshi yangu yalikuwa na laumu nyingi dhidi ya Serikali yako, Mama yangu aliniuliza kama huwa nakuombea kwa Mungu kama Rais wa Nchi, sikuwa na jibu la uaminifu kwake na hivi ndivyo alivyoniambia “ KAZI YA URAIS NI NGUMU, KILA MARA UNAPOSALI USIACHE KUMWOMBEA RAIS WA NCHI, MUNGU AMAJILIE AFYA NJEMA, HEKIMA NA BUSARA KWANI RAIS AKIKOSEA KUAMUA NI NCHI IMEKOSEA SAFARI YAKE YA MAFANIKIO NA USTAWI, KWA HIYO MUOMBEE RAIS SIKU ZOTE “

Mheshimiwa Rais, ulikuwa ni husia muhimu sana kwangu lakini mgumu sana kwa wakati huo, lakini baada ya kutafakari, kuanzia siku hiyo mimi na Familia yangu tumekuwa tukikuombea sana kwa Mwenyezi Mungu ili Nchi yetu isikosee safari yake ya mafanikio yaliyojaa Ustawi bora na Uhuru.
Mheshimiwa Rais, kama ambavyo naamini Watu wengi wanakuombea na Sisi pia tunaomba utuombee, Mungu atujalie hekima, busara na uvumulivu juu ya maumivu tunayopitia wakati tunapojaribu kutekeleza wajibu wetu wa kidemokrasia katika Nchi yenye msingi wa demokrasia lakini kwa bahati mbaya sana kazi zetu za siasa zimekuwa ngumu sana na mashaka kuliko hata wakati ule wa ukoloni.

Mheshimiwa Rais, Ukimchukua ndege porini ukamfuga nyumbani ,ukamtengenezea kiota cha pamba na sufi, ukampa chakula chake kwa ufasaha na asikose maji ya kunywa tena masafi ya chupa ya Kilimanjaro, ukamfungia ndani asipate tabu juani, hakika siku ukiacha mlango au dirisha wazi ataondoka na hatarudi, atakwenda porini akatafute asili yake na Uhuru wake, atakwenda kutafuta chakula kwa shida, maji kwa shida, lakini lengo muhimu ambalo ni Uhuru litampa faraja kubwa ya kwamba ameondoka kizuizini.

Mheshimiwa Rais, unaweza ukatupa chakula, elimu, afya, na mambo mengi muhimu, lakini ukitunyima Uhuru wa kusema, tukaishi kwa hofu kama tuliyonayo sasa, Mheshimiwa Rais nakuhakikishia siku ukiacha dirisha wazi tutatoroka na kamwe hatutarudi. Aliyekuwa Rais wa Libya Hayati Muhamar Gaddafi, alifanya kazi kubwa ya kujenga Libya hata mahari watu walilipiwa na Serikali walipotaka kuoa, watu walipewa nyumba na mambo mengi muhimu, lakini Gaddafi alisahau kuwa hakuna zawadi kubwa kwa Binadamu zaidi ya Uhuru.

Mheshimiwa Rais, ruhusu Watu waseme, acha Watu wapige kelele, ruhusu mioyo yao ipumue, wacha Watu wakosoe jambo hili halitakuwa balaa kwako bali Baraka. Kama kweli unayo nia njema, njia pekee na muhimu tu unayoweza kuthibitisha nayo nia yako njema ni kuruhusu mfumo wa demokrasia wa Vyama vingi kukua, umekuwa ukipigana sana na mambo mengi machafu yaliofanywa na Serikali ya Chama chako huko nyuma, umethibitisha kwetu kwa kiwango fulani na kwa umma wote hali mbaya uliyoikuta Serikalini baada ya kuingia Ikulu, hili funzo tosha kwako kwamba namna pekee ya kusaidia Taifa hili ni kujenga demokrasia ya dhati na kufufua matumaini ya Watanzania kwa kuwapa Katiba bora waliyoitaka, ambayo hata kama uwepo wako hautakuwepo Watanzania watakuwa salama na watasonga mbele.

Mheshimiwa Rais, mamlaka uliyonayo yanatokana na Katiba , Wewe ni Kiongozi Mkuu wa Nchi kwa sababu ya Katiba, Majeshi yote yanakutii wewe ni kwa sababu ya Katiba, uteuzi wote unaofanya wa Viongozi katika utawala na unaowatumbua, mamlaka hayo pia umepewa na Katiba, mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa pia ni matakwa ya Katiba na tumepewa na Katiba ,na wote sisi kwa dini zetu mbali mbali na makabila yetu wote tunakutana na kuunganishwa na Katiba na kuheshimu Katiba kama msingi mkuu wa uendeshaji wa Nchi.

Mheshimiwa Rais, Mungu adhihakiwi kwani apandacho Mtu ndicho avunacho,Wazazi wengi wanalia sana siku hizi juu ya tabia ya kwamba watoto wao wamekuwa walevi na wenye adabu mbaya, lakini ukifanya utafiti karibu nyumba zote za kisasa zinazojengwa siku hizi ramani ya nyumba hizo hazikosi baa ndogo ndani ya nyumba hizo, kama hatuwezi kufanya tunayo ruhusiwa na Katiba na anayetuzuia kufanya hivyo mamlaka yake yanatokana na Katiba, hakika mbegu inayopandwa hapa ni hatari kwa ustawi wa Taifa, iko siku amri ya utekelezaji juu ya masuala muhimu haitachukuliwa kwa sababu umuhimu wa kuheshimu Katiba na utawala wa sheria hautakuwepo.

Mheshimiwa Rais, Haki huinua Taifa,tuanapoelekea tarehe 1/09/2016, CHADEMA imeitisha mikutano ya hadhara kote Nchini pamoja na maandamano, tayari kauli yako na viongozi wengine wa juu wa Serikali wameonya juu ya Mikutano hiyo na kusema hatua kali zitachukuliwa bila huruma dhidi ya watu wote watakaojitokeza kuunga mkono harakati hizo.

Mheshimiwa Rais, tunafahamu Jeshi la Polisi liko imara kupambana na kuzuia haki hii ya Kikatiba, pengine Watu wataumia na wengine watakufa, je ni kweli tunahitaji kufika huko? je hatuoni kuwa matakwa ya Katiba yakizingatiwa risasi wala bomu havitatumika, maandamano haya yameitishwa kushinikiza haki yetu ya Kikatiba ya kufanya mikutano, Uhuru huu wa Katiba ukizingatiwa kwa kuruhusu mikutano ya hadhara hakika ni kwamba maandamano hayatakuwepo na kusema kwamba Sasa ni Kazi tu, na mikutano yote ya Siasa isubiri 2020, je ni halali Mkristo kusali siku ya Noeli (Christmas ) tu ? au Mwislamu kuingia Msikitini siku ya Idd tu?

Mheshimiwa Rais, Siasa ni Kazi na ndio maana wewe ni Rais kwa sababu ya Siasa na Mimi ni Mbunge kwa sababu ya Siasa, tena ni kazi muhimu sana tu kwani ndio mfumo pekee unaotafuta utawala wa ngazi mbali mbali na wa juu kabisa katika Nchi.

Mheshimiwa Rais, lakini pia kufuatia kauli yako ya kwamba kila Mtu afanye mkutano kule alikochaguliwa ni hatari kwa ustawi wa Taifa letu na mshikamano kwani tunajenga siasa za ukanda na ukabila katika Nchi yetu. Mkoa wa Kilimanjaro ccm ina majimbo mawili tu, maana yake CCM hawatakiwi kufanya mikutano ya hadhara na siasa sehemu nyingine za Mkoa wa Kilimanjaro? Mkoa wa Geita hauna hata Jimbo moja la Upinzani, je huko nako vyama vyetu havitakiwi kwenda kufanya mikutano na ujenzi wa chama? Je, ikiendelea hivi huoni kuwa tutaanza kujenga misingi ya kugombania nafasi za siasa kule ambako ni asili za makabila yetu tu?

Mheshimiwa Rais, jambo hili litaleta mpasuko katika Taifa letu ni kauli inayopaswa kerekebishwa haraka , hivi Karibuni Msemaji wa ccm Ole Sendeka alifanya Mkutano Longido, je Ole Sendeka ni Mbunge wa Longido? au Polisi wa Mkoa wa Arusha hawakusikia tamko lako?

Mheshimiwa Rais, nakuomba sana utambue kwamba, unyenyekevu sio utumwa wala uzembe, ukizingatia matakwa ya Katiba hakuna mwenye hekima hatakaye kudharau, wewe ni Binadamu unaweza ukufanya makosa usiruhusu mikono yako ikashika damu pasipo sababu ya msingi ni laana kwa Taifa na Kizazi chako.

Mheshimiwa Rais, na kama jambo hili ambalo liko wazi katika Katiba yetu halitaweza kupata fikra yako na mwelekeo mpya wa mawazo yako, basi itakuwa ni dhahiri kwamba unachokitafuta katika utawala wako sio haki ya Watanzania bali ni utukufu binafsi. Na suala lolote kuhusu utukufu ni suala linalomuhusu Mungu na sio Binadamu

Mheshimiwa Rais, Polisi wanajiandaa kwa sababu ni muhimu wakatii amri ya Amiri Jeshi Mkuu, wasipofanya hivyo watakuwa wanafanya uhaini, lakini ni vyema ikajulikana kwamba, dhamira ikichoka huwa inatamani mauti, tukikaa kimya huku dhamira zetu zikiumia ni hatari kuliko kupiga kelele kwa sauti kuu, ni maombi yangu kwa Mungu kwamba muufaka wa utata huu wa Uhuru wa Vyama vya Siasa unaotokana na Katiba uwe umepatikana mapema iwezekanavyo ili kuepusha hatari inayoweza kutokea na kusabibisha maumivu , hasara, vifo na utengano katika Taifa letu.

Mheshimiwa Rais, wakati Polisi wanajiandaa kukabiliana na waandamanaji wanaodai haki yao ya kweli, chuki kubwa inaendelea kujengwa kati ya walinzi hawa wa amani na raia, mashaka yangu ni kwamba kunaweza kutatokea mpasuko mkubwa huko mbele ya safari kati ya Polisi na raia, maisha ya visasi yataanza mitaani na mwelekeo mbaya wa Taifa letu unaweza kutokea.

Mwisho, Mheshimiwa Rais, nakutakia kila la kheri na Mungu akubariki sana katika kazi zako na maamuzi yako ya kila siku , ila siku zote kumbuka" Haki huinua Taifa"

Never forget that justice is what love looks like in public“ Cornel West
“injustice anywhere is a threat to justice everywhere” Martin Luther JR“
“Peace and justice are two sides of the same coin“ Dwight D.Eisenhower
“All the great things are simple , and many can be expressed in a single word, freedom , justice, honor, duty, mercy, hope” Winston Churchill
Godbless J Lema (MB)

King Kaka awalaumu mapromota wa Kenya kwa kuwalipa zaidi Alikiba na Diamond

$
0
0
Rapper King Kaka wa Kenya, amewatupia lawama mapromota wa nchini humo kwa kuwalipa fedha nyingi wasanii wa nje kwenye show na kuwapa kiduchu wasanii wa ndani.

Ametoa malalamiko hayo kwenye mtandao wa Facebook na kuwatolea mfano Diamond na Alikiba ambao wamekuwa wakilipwa mamilioni ya shilingi kila wakitumbuiza nchini humo.

“Sazile Alikiba anakam na analipwa hiyo 2million sio mbaya, Diamond anakam analipwa hiyo 2 Million, Na Nani pia anakam analipwa 2 Million, na Nani pia 2 million but on the same performance utaona wameweka legends wa hapa Kenya na trust me wamepewa 300k, 400k ata unaweza Pata mi 100k (shame, what a shame) sahizo bado yule amekupa show anataka cut yake which sio mbaya but what do fans expect. Hii kitu yote iko connected,” aliandika Rabbit.

Amedai kuwa wasanii wa Kenya hawapewi heshima wanayostahili na hivyo kudidimiza muziki wa nchi hiyo.

Soma post yake nzima hapa:

'Respect your elders, I started doing this $**t while you were still in diapers' I think Nameless akiandika hiyo line alikuwa ananiongelea na hawa marapper wote wanajiita Kings na Ma Queens na hii Generation yote mpya ya musicians. But kile mimi inaniuma ni Kitu inaitwa RESPECT ama RESPEK, just put some respect on these guys (kama sijakuweka kwa list jiweke tu ama mafans wakuweke).

Sazile Alikiba anakam na analipwa hiyo 2million sio mbaya, Diamond anakam analipwa hiyo 2 Million, Na Nani pia anakam analipwa 2 Million, na Nani pia 2 million but on the same performance utaona wameweka legends wa hapa Kenya na trust me wamepewa 300k, 400k ata unaweza Pata mi 100k (shame, what a shame) sahizo bado yule amekupa show anataka cut yake which sio mbaya but what do fans expect. Hii kitu yote iko connected.

Fact 1: pay an Artiste 100k unaexpect aende South Africa kushoot video (yet by the way mimi uona ni ufala, huku Kuna Enos, Kyalo, J Blessing, Wallace na ni wanoma) so atalipa ndege na album yake ama???? So don't expect many Godfather Campos videos huku any time soon.

Fact 2: Less play kwa stations, na hii mimi nakuwanga advocate (kwanza kama Kuna stations ulikuwa unaniona na sikuhizi haunioni, hao walicatch wale wananipa airplay Big Up but good Thing mafans wangu wako tight na Mimi kwa MA mathree na kejani zao, Hauwezi zima moto ya Mungu, aje??? Ha ha ha)

Fact 3: mafans unajua tunawapenda sana na sana, but Si twende concert za Wasanii wakenya pia vile sisi uenda za nje, vile Sauti Sol wako na album Si twende Supermarket tukabuy (ata mimi nijitete, niko na album nne niko itunes na hizo ma Mziiki na kadhalika ukitaka physical niko na jeshi yangu itakuletea) anyway we as artists are very thankful but let's show more support that's the only way we will get Nameless and Wyre walipwe 2 million, let's vote kwa wale wako nominated let's watch their links kwa youtube let's get entertained (na nyinyi pia Wasanii make more effort just alittle more, mdogo mdogo)

Fact 4: mimi kwanza ni fan mnoma sana wa Kenyan Music from tene sana and na msee aliniInspire was and still is Chiwawa (najua hii generation ya KuDab hamjui mtu kama huyu, well Google is your friend) anyway hizi ma MCSK, PRISK, CMO'S, PRSP get your act right tafadhali. Msanii anaingia studio anafanya kazi yake, wewe Si ufanye kazi yako. bado unataka atoke studio akuje demonstration bado unaexpect aishi kwa hao poa, bado tunaexpect aDrive gari nzuri ati hasipande mat, bado unaexpect aende SA, bado unaexpect amake statement aje. Ataenda studio saa ngapi na ataenda demonstration saa ngapi???

Anyway I am thankful to all the stations zinacheza more Kenyan (endeleni hivyo hivyo) All the Djs who push for more Kenyan (kwanza nyinyi hapo mnacheza role Kubwaaaaaaaa sana BIG UP , we appreciate, all the fans wale wameenda sahii kucheki album yangu iTunes na kama ushawai buy any Kenyan Music BIG UP, wale wote ubuy tiko za show na wanaenda manze nyinyi ni shujaa (wakireWrite history mnafaa muwekwe -my opinion), wale event organizers upush msanii apewe more money BIG up (sababu music is art and it's not even equivalent to that 2 million nasema, but gets the art growing) , kama uko na mix ya Kenyan kwa keja yako ama more songs za Kenya kwa simu yako BIG UP wewe ni shujaa.
All I am saying let's start by putting some RESPECT on our Legends akina Nameless, akina WYRE, (wale wanaPut in work) list ni Refu you know them. (mimi ntajitetea baadaye, but we have to start somewhere) na you can quote me.
Mafans wangu tuendele,
Back to regular programming, my new video is out 'Besha Shigana ' icheki youtube na uiDownload legally (hizo maTubidy na waptrick hazifikishi doh kwa msanii)
Ni hayo tu kwa sasa. Have a Beautiful day ata naenda studio.
‪#‎TheKing‬'sSpeech3

‪#‎Mistarillionaire‬ powered by GOD


Bongo5

Mahakama Kuu Yampunguza MAKALI Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP)

$
0
0
MAMLAKA ya kugomea dhamana za watuhumiwa aliyokuwa nayo Biswalo Mganga, Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), sasa imeondolewa na mahakama kuu.

Awali, DPP alikuwa na uwezo wa kuzuia  dhamana za baadhi ya watuhumiwa kwa namna alivyoona inafaa licha ya kuwepo kwa malalamiko ya uhalali wa kuzia dhamana hizo.

Miongoni mwa sababu ambazo zimekuwa zikitolewa na DPP  ni maslahi ya umma hivyo kusababisha haki ya kupata dhamana kuwa ngumu.

Kwa kuwa hatua hiyo inakiuka Katiba ya Tanzania, Mahakama Kuu imefikia uamuzi wa kumwondolea mamlaka hayo DPP.

Kifungu kilichokuwa kikimpa mamlaka DPP ya kuzuia dhamana ni 148 (4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) na kwamba, kinakwenda kinyume na Ibara ya 13 (6) (a) ya Katiba ya Tanzania.

Uchambuzi wa udhaifu wa kifungo hicho kilichokuwa kikitumiwa na DPP ulitolewa na Majaji Sekieti Kihiyo na Dk. John Ruhangisa wakiongozwa na Jaji Kiongozi Shaaban Lila.

“Imeamriwa mtuhumiwa aliye chini ya ulinzi wa polisi au mtuhumiwa yoyote, anatakiwa kupewa haki yake ya kujitetea kabla ya haki hiyo haijazuiliwa na mkurugenzi wa mashitaka kwa pingamizi la kuwanyima dhamana,” sehemu ya taarifa ya majaji hao imeeleza hivyo.

Kifungu cha 148 (4) kinasema; “bila kujali kitu chochote kilichopo kwenye kifungu hiki, hakuna afisa polisi wala mahakama atakayeweza, baada ya mtu kukamatwa na wakati anasubiri shauri au rufaa, atathibitisha kwa maandishi kwamba kuna uwezekano kwa usalama au maslahi ya Jamhuri.

“…na cheti kilichotolewa na Mkurugenzi wa Mashitaka chini ya kifungu hiki kitaanza kutumika kuanzia terehe kitakapowasilishwa mahakamani au kutaarifiwa kwa afisa msimamizi wa kituo cha polisi na kitaendelea kutumika hadi mwenendo utakapohitimishwa ama mkurugenzi wa mashitaka atakapokiondoa.”

Kuondolewa kwa mamlaka ya DPP kuzuia dhamana za watuhumiwa kulitokana na kupelekwa pingamizi la kikatiba lililowasilishwa na Jeremiah Mtosebya, Mkazi wa Jiji la Dar es Salaam ambaye amesema kifungu hicho kinakiuka Katiba ya Tanzania.

Linah aeleza kwanini watu wanahisi anatoka kimapenzi na Billnas

$
0
0
Msanii wa muziki, Linah Sanga amekanusha tetesi ambazo zilisambaa katika mitandao ya kijamii kuwa anatoka kimapenzi na rapper Billnas.
linnah

Muimbaji huyo ambaye ameachia wimbo ‘Raha Jipe Mwenyewe’ hivi karibuni, amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio kuwa Billnas ni mshkaji wake.

“Watu wanatakiwa wajue tu kuwa mimi na BillNas si wapenzi ila sisi ni watu wa karibu sana,” alisema Linah “Saizi mimi na Bill Nas ni washikaji sana maana siri yake ndiyo siri yangu,”

Aliongeza, “Bill Nas ndiye aliyenishauri nibadilike kwenye muziki na kunipa ‘connection’ na ‘Producer’ T Touch, yeye ndiye aliniambia nibadili mfumo mzima wa muziki wangu na ndiyo nikafanya hivyo,”

Tundu Lissu Afunguka.. 'Hakuna Mtu Anayetaka Kumjaribu Rais Magufuli, Mahabusu Sio Pazuri Niulizeni Mimi'

$
0
0
Baada ya Kutoka mahabusu kwa dhamani Tundu ameongea haya mbele ya waandishi wa Habari:

"Hakuna mtu anataka kumjaribu Rais Magufuli, hakuna anayetaka kukamatwa, mahabusu sio pazuri, niulizeni mimi." - Tundu Lissu
Toa maoni yako

Habari Njema Kwa Wapenda Supu ya Pweza...Utafiti Umeonyesha ni Kweli Inaongeza Nguvu ya Kufanya Mapenzi Kwa Mwanaume

$
0
0
Wafamasia katika Chuo Kikuu cha Muhimbili wamedai kuthibitisha kisayansi kuwa 'Supu ya Pweza' inaweza kuchochea hamu ya kufanya mapenzi kwa wanaume. "Sio kitu cha imani tena, sasa hivi tuna ushahidi wa awali unaotupa mwanga wa matumaini kuthibitisha matokeo hayo katika mwili wa binadamu," amesema Profesa Eliangiringa Kaale.

Nini maoni yako?

Mtoto Aliyewekewa Betri Kwenye Moyo Kuruhusiwa Kupita Kwenye Viwanja vya Ndege Bila Kukaguliwa na Mashine

$
0
0
Kadi ya kumtambulisha mtoto Happiness John (5) kimataifa baada ya kufanyiwa upasuaji na kuwekewa betri ndani ya moyo inatengenezwa nchini Afrika Kusini. Happiness ambaye alifanyiwa upasuaji huo Julai 15 na kuruhusiwa kutoka hospitalini wiki moja iliyopita, anatakiwa kuwa na kadi tambulishi ambayo itamuwezesha kutofanyiwa ukaguzi wa kielektroniki. Kwa sasa mtoto huyo amepewa kadi ya muda ambayo inamruhusu kutopita katika maeneo yenye mionzi kwa ajili ya ukaguzi, ikiwamo viwanja vya ndege na majengo yenye ulinzi mkali.

Tuendelee kumtakia heri mtoto huyu

Binti Miaka 19 Afunguka Kuwa ni Msagaji, Ametembea na Wake za Watu 20

$
0
0
Dunia imekwisha! Ndiyo sentensi pekee inayoweza kukutoka baada ya kusikia kisa cha binti huyu aliyejitambulisha kwa jina la Malkia Said a.k.a Malkies, mwenye umri wa miaka 19, mkazi wa Magomeni jijini Dar ambaye amekiri kujihusisha na vitendo haramu vya usagaji akieleza alivyotembea na wanawake wenzake wasiopungua 40 wakiwemo wake za watu zaidi ya 20 hadi kufikia hatua ya kufumaniwa na kunyolewa nywele.

KABLA YA KUFUNGUKA
Kabla ya kufunguka yote hayo, awali habari zake zilivuma kutoka pande mbalimbali jijini Dar na kwenye mitandao ya kijamii ikidaiwa kwamba, mrembo huyo ni hatari kwa wake za watu hivyo wenye ndoa zao wakae chonjo.
Baada ya kuvuma kwa jina hilo la Malkies na sifa zake tajwa hapo juu huku ikidaiwa kuwa alifumaniwa na mke wa mtu ndipo gazeti hili likajipa kibarua cha kumtafuta binti huyo ili kujua mbivu na mbichi za msichana huyo.

HUYU HAPA MALKIES
Akizungumza na waandishi wetu ndani ya ofisi za gazeti hili, Bamaga-Mwenge, Dar, mapema wiki hii, huku akiwa macho makavu, Malkies alisema kuwa, alianza mchezo huo tangu akiwa mdogo kutokana na hisia za mapenzi zilizokuwa zikimsukuma kwa kasi kujihusisha na kitendo hicho haramu.

“Nilipokuwa mdogo, kuna binamu yangu mara kwa mara alikuwa akinivizia akitaka kunibaka lakini nikawa ninamchenga, sasa baba yangu alipofariki dunia nikiwa darasa la nne ndipo nikapelekwa shule moja ya boarding iliyopo jijini Mwanza.
“Muda mwingi nilikuwa na watoto wa kike wenzangu huku msukumo wa kufanya nao mapenzi ukinitesa.

“Kwa kuwa yule binamu yangu alisababisha niwe na hisia kali za mapenzi, nikawa navumilia. Mwisho, nilihamishiwa shule nyingine ya boarding ipo Kibaha (Pwani).
“Huko kuna siku nikawa naumwa, rafiki yangu Mzanzibari akataka kunichumu shavuni. Ndipo tukajikuta tumeingia kwenye mchezo huo rasmi. Nakumbuka hiyo ilikuwa mwaka 2010,” alisimulia Malkies huku akilengwalengwa na machozi.

ASHTUKIWA SHULENI
Alisema, baada ya hapo ilifikia hatua uongozi wa shule ukajua na kuwaambia ndugu zake, akiwemo mama yake lakini walipuuza kwa kuhisi anasingiziwa.
Alisema kadiri siku zilivyosonga ndivyo alivyokubuhu na kupata uraibu uliomfanya kutotamani kuuacha mchezo huo ambao aliamini ndiyo furaha pekee kwake kwani baada ya muda, mama yake naye alifariki dunia.

AJARIBU KUWA NA WANAUME
Alidai kuwa, kutokana na maneno ya kila kukicha watu wakimkemea juu ya ishu hiyo, Malkies aliona bora ajaribu kuwa na mwanaume labda anaweza kuacha, lakini kila mwanaume aliyekuwa naye ambao wanaweza kufikia ishirini, hakuwa akihisi msisimko kama anapokuwa na wanawake wenzake.

“Pia mjomba wangu alikuwa akinikuta na wanaume, ananipiga kwa sababu aliona umri wangu hauruhusu na hakujua kwa nini nafanya hivyo maana nilishindwa kumwambia,” alisema Malkies mwenye umri mdogo lakini aliyepitia mambo mengi ya kikubwa.

AFUMANIWA
Akiendelea kusimulia, Malkies alisema, kwa kuwa anajitambua na anajua nini anachokifanya, alidhani ni vyema kutoka na watu waliomzidi umri kuliko kuwapotosha vijana wa rika lake, ndipo akampata mke wa mtu.

Alisema kabla ya hapo alishakuwa na wake wengine wa watu lakini huyo wa Magomeni hali ilikuwa mbaya kiasi cha kutwangwa talaka na mumewe.

“Nimeshakuwa na wake za watu zaidi ya ishirini, wengi wamenizidi umri pia wake za watu wananitaka wenyewe, huyo mmoja alikuwa anaishi Magomeni na mumewe akawa ananishumbua kwa kipindi kirefu wakati mimi nilikuwa na mtu wangu.

“Nakumbuka ilikuwa mwanzoni mwa mwaka huu, nilipoachana na huyo mtu wangu (mwanamke mwenzake), niliamua kuwa na huyo mwanamke.

“Yeye ana umri wa miaka 30, alinidanganya anaishi na baba yake, akanipeleka hadi kwake. Baadaye aliniweka wazi kuwa anakaa na mumewe na majirani wakamfikishia habari mume wake kuwa huwa nakwenda pale akiwa hayupo.

“Kulitokea ugomvi mkubwa kati ya yule mwanamke na mumewe, yule mwanamke akadai talaka na akapewa kwa sababu yangu.

“Niliendelea naye hata baada ya mumewe kumuacha, tukawa tunaishi wote Ubungo kwa dada yake na mimi nikiwa na mtu najiachia kimahaba siwezi kuficha.
“Wiki mbili baadaye, yule dada’ke alichukia, akaita ndugu zake na yule mume, wakaja kunifumania, wakanipiga na kuninyoa nywele.

“Tuliendelea kidogo lakini sasa tumeachana kabisa,” aliongeza binti huyo ambaye pia aliwahi kushiriki kwenye filamu na muziki japokuwa hakuwika.

STAA ANAYEMZIMIKIA
Akiendelea kueleza kwa kujiamini, Malkies alisema, wanawake wengi ambao alikuwa akiwazimia ni Wazungu na chotara, lakini mbali na hao alikuwa akiumiza kichwa na staa wa filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ambaye aliwahi kumtunza Sh. milioni moja kwenye shoo huko Arusha.
“Hakuna msanii anayenivutia zaidi ya Wema na siku ile nilipomtunza ni kwa sababu tu alikuwa amelewa na mimi nililewa, lakini tungekuwa sawa ningemueleza jinsi ninavyomkubali,” alisema.

LENGO LA KUJITANGAZA
Alimalizia kuwa, suala hilo siyo jambo la kufumbia macho kwa sababu linafanywa na wanawake wengi wakiwemo mastaa na wake za watu hivyo ameamua kuanzisha shirika la kuwasaidia wengine ambao bado hawajajiingiza na waliojiingiza kwenye vitendo hivyo ili waache kwa lengo la kuokoa kizazi hiki na kijacho.

Imeandikwa na Global Publishers

Video:





Diamond: Muziki si Kitu Cha Lazima Kwangu

$
0
0
Diamond amesema kuwa hategemei muziki kuendesha maisha yake.

Hit maker huyo wa wimbo wa ‘Kidogo’ hivi karibuni kupitia kipindi maalum cha kituo cha runinga cha E!TV, E Vip aliutaja utajiri wake kuwa ni dola milioni 4 za Kimarekani ambao kwa shilingi ya Tanzania ni zaidi ya shilingi bilioni 8.6.

Kupitia kipindi cha SupaMix cha EA Radio, Diamond alisema, “Ukiachilia mbali kazi ya muziki mimi pia nina vikorokoro kibao ambavyo vinaniwezesha kuweza kupata kipato cha kila siku.”

“Siyo kwamba muziki ni kila kitu lazima kujishughulisha na Mungu anasaidia kuweza kusonga mbele,” ameongeza staa huyo.

Paul Pogba Akabidhiwa Jezi Namba 6

$
0
0
Baada ya kusajiliwa na Manchester United kutoka Juventus ya Italia kwa ada ya paundi milioni 89 kwa mkataba wa miaka mitano, Paul Pogba, amekabidhiwa jezi namba 6 ambayo pia alikuwa akivaa zamani alipokuwa Juventus kabla ya kupewa jezi namba 10. Tazama picha za staa huyo akiwa na uzi wa Man United.

Kajala 'Nilikurupuka Nikaingia Mapenzini Kwa Mwanaume Aliye Nihonga Gari 'Harrier'

$
0
0
Msanii wa filamu nchini Kajala Masanja ambaye kwa sasa yupo karibu sana na msanii Quick Racka amefunguka na kusema kuwa alikurupuka kukubaliana na mwanaume ambaye hakuweza kumfahamu vizuri tabia zake baada ya yeye kuhongwa gari aina ya Harrier.

Kajala alitoa ushuhuda huo kwenye kipindi cha Friday Night Live ya (EATV) alipokuwa akiwapa hamasa mabinti na wasichana kutokukurupuka kwa kuangalia mali za wanaume bali wanapaswa kujisomea ili baadaye waje kuwa na maisha yao wenyewe, kwani yeye alikurupuka na kuolewa na matokeo yake aliishia kufungwa gerezani kwa sababu ya mwanaume wake.

"Ni kweli mfano mimi nilihongwa gari aina ya Harrier nikajikuta nakubaliana na mwanaume lakini baadaye nilikuja kujuta maana niliishia gerezani, hivyo nawaomba mabinti wenzangu tusikurupuke kwenye maamuzi, na wale wasichana ambao wanasoma wanapaswa kusoma ili baadaye waje kuwa na maisha ya kwao wenyewe"alisema Kajala

Kajala pamoja na wasanii wengine kama Mwasiti, Queen Darleen, Shilole wameanzisha kundi linalofahamika kama 'Sisters' ambacho lengo lake ni kutoa ushuhuda katika mambo mbalimbali ambayo yamewahi kuwatokea kwa wanafunzi wa kike wa shule za sekondari wakiwa na lengo la kuwahamasisha wanafunzi hao kusoma kwani maisha ambayo wao wamepitia hawataki wanafunzi hao nao waje kupitia.

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya Agosti 10

$
0
0

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya Agosti 10

Diamond Akiri Kupenda Bifu

$
0
0
Msanii Diamond Plutnuz amewashangaza watu baada ya kauli yake kwamba anaona bifu kwenye muziki na kitu kizuri, tofauti na wasanii wenzake wengi ambao hupinga suala la bifu.


Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Diamond amesema kwake yeye anaona ni sawa tu iwapo wasanii wanakuwa na bifu, kwani inasaidia kwa kiasi kikubwa kuinua muziki wao, kwa kuzungumziwa na vyombo vya habari na watu mbali mbali, isipokuwa inakuwa shubiri pale inapogusa familia, na kutoleana maneno machafu.

“Bifu mi naona fresh, kwangu kitu kikizungumziwa ndo naona poa tu kwanza inaniongezea, ila pale inapofikia kugusa kwenye familia na kutoleana maneno machafu ndio inakuwa sio poa”, alisema Diamond Plutnumz.

Kutokana na kauli hiyo, Diamond amekuwa amepigia mstari kuwa wasanii wa lebo yake ya WCB hutegemea ‘kiki’ zaidi kuliko kazi bora kuweza ku-hit, kama ambvyo watu wengi huwatuhumu wasanii hao.

Pia Diamond ametoa siri kuwa mashabiki wake wajiandae mkao wa kula kwani kabla mwaka huu kuisha, atatoa album ambayo itakuwa ya kimataifa.

Shilole ‘Awaka’ Kisa Penzi na Jay Moe

$
0
0
MREMBO ambaye jina lake liko juu kwa sasa kwenye gemu la Muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ hivi karibuni amewaka baada ya kubanwa maswali juu ya tetesi za uhusiano wake na Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Juma Mchopanga ‘Jay Moe’.

Akistorisha na Uwazi Showbiz, Shilole alifunguka kuwa hana uhusiano na mkali huyo wa ngoma ya Pesa Madafu na hajawahi kufikiria kutoka naye na anawashangaa watu wanaomhusisha kuwa kwenye mahaba na Jay Moe.

“Watu bwana wanashindwa kufuata yao wanakalia kuchonga yawenzao, mimi Jay Moe ni kaka yangu, tumeshibana na hatuna uhusiano wowote,” alisema Shilole.

Kwa upande wa Jay Moe amefunguka kupitia kwenye mitandao ya kijamii juu ya kuzisikia tetesi za yeye kutoka kimapenzi na Shilole, amedai pia hazina ukweli wowote maana mwanadada huyo ni mshikaji wake wa karibu tu!

Chanzo:GPL

Matabibu Mbadala waomba kibali kuishtaki Serikali kuwafutia usajili

$
0
0
MATABIBU wanne wa Tiba Asilia na Mbadala akiwemo mmiliki wa Kliniki ya Sure Herbal, Simon Rusigwa wamewasilisha maombi ya kuomba ruhusa ya kufungua kesi ya kupinga uamuzi wa kufutiwa leseni za kutoa huduma za kitabibu.

Wamewasilisha maombi hayo katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, dhidi ya Baraza la Tiba Asilia na Mbadala, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Mbali na Rusigwa, matabibu wengine waliowasilisha maombi hayo kupitia kwa Wakili Dk Lucas Kamanija, ni Abdallah Mandai wa kliniki ya Mandai Herbalist, Fadhili Kabujanja wa Fadhaget Sanitarium na John Lupimo wa Lupimo Sanitarium.

Maombi hayo yalitakiwa kusikilizwa jana mbele ya Jaji Ama–Isario Munisi wa mahakama hiyo, hata hivyo kabla ya kuanza kusikilizwa, Serikali iliwasilisha pingamizi la awali ikidai kuwa maombi hayo hayakufuata misingi ya kisheria.

Katika pingamizi hilo serikali inadai kuwa maombi hayo yana kasoro kwa kuwa waombaji hawajapita njia zote zinazotakiwa wazifuate ndipo waende mahakamani pia wanadai maombi hayana miguu ya kusimamia kwa kuwa hati ya viapo vya walalamikaji vina upungufu ya kisheria.

Baada ya kuwasilishwa kwa pingamizi, Jaji Munisi aliahirisha shauri hilo hadi kesho saa 8 mchana, ambapo alizitaka pande zote zinazohusika ziwepo ili kusikiliza pingamizi hilo.

Katika maombi yao, matatibu hao wanadai, wameamua kupeleka maombi hayo mahakamani, kwa kuwa wanaamini walifutiwa leseni bila kufuata taratibu za kisheria.

Wamedai wanaamini uamuzi uliochukuliwa umetolewa bila kupitia Kamati ya Maadili ya Baraza la Tiba Asilia na Mbadala, huku wakidai kuwa huo si uamuzi bali zilikuwa tuhuma mpya, lakini hawakupewa nafasi ya kusikilizwa.


Gigy Money akiri kutembea Kimapenzi na Alikiba pamoja na Abdukiba

$
0
0
Katika miaka 19 aliyoishi Duniani hakumbuki idadi ya wanaume ambao ameshalala nao
Akiwa amezaliwa katika Familia ya Watoto wanne ambao kila mtu ana Baba yake, kwa upande wake HAKUWAHI KUMJUA BABA YAKE

Mama yake alimzaa pembeni ya mlango wa choo, na ni mtu aliekuwa akiwa anaamini hapendwi na Mama yake mzazi kutokana na sababu tofauti kabla hajagundua ukweli.

Aliwahi kujitoa kimwili katika umri mdogo ili apate hela ya kuweza kumnusuru MAMA yake mzazi kulipa Deni la mkopo wa Benki

Ametaja MASTAR WA KITANZANIA ambao ameshawahi kushirikiana nao kingono kama


LIST HII YAPA:

1. ALIKIBA
2. ABDU KIBA
3. CASTRO DICKSON
4. HAMED PHD
5. RICH MAVOKO
6. HARMONIZE

 Haya yote kayaeleza wakati akiojiwa katika kipindi cha Take One cha Zamaradi mtetema...



Angalia Video

Soma Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Katika Magazetini na Mitandaoni Leo 10 Aug 2016

$
0
0

A New Travelers Social Network is Here..Check It Out

$
0
0
A new interactive social network, developed mainly for travelers; backpackers, hikers, holiday
makers and those who simply enjoy exploring the world.

Anyone can join the social network freely by login to www.ezylinc.com and post photos of
World's heritage sites, Historical sites, Parks, Hotels, Restaurants, write articles about
destinations, Legends, form groups, messaging, add friends and much more.

Ezylinc connects two groups. On one side we have travelers and adventurists and on the other
side local businesses connected to travel and tourism. The social network is developed by a
Tanzanian startup.
Let’s take Tanzania as an example, where travel and tourism is one of the leading industries.
The country is harboring a diversity of an unmatched fauna and flora, a unique destination on
the African continent. Kilimanjaro, the highest free standing snow-capped mountain in Africa,
the Islands of Zanzibar, the national parks of Serengeti, Ngorongoro Crater, Tarangire, Lake
Manyara, Ruaha, Selous and the Marine Park of Mafia Island are few of the living examples
found in Tanzania.

In 2014 The tourism sector in Tanzania, contributed 17 per cent to the country’s GDP and
accounted for 25 per cent of all the foreign exchange earnings, with 2 billion USD in revenues.
The country ranks 5th among African countries with the highest growth in the tourism
industry.

This is why we have created a new social network. We want to support travel, local
businesses, and create more jobs in tourism along the way.
Join Ezylinc by login to http://ezylinc.com/`

Mwigulu Nchemba Awaonya Polisi Wanaowabambikiza Kesi Raia

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba amewaambia askari wa jeshi la Polisi mkoani Katavi kufanya kazi kwa taratibu na sheria bila kumuonea mtu yeyote hasa wanyonge.

Waziri Mwigulu ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kutembelea makazi ya watanzania wapya pamoja na kuzungumza na askari wa jeshi la polisi, Magereza pamoja na Uhamiaji.

Mhe. Mwigulu amesema kuwa Askari hao waondokane na tabia ya matukio ya kuwabambikizia kesi raia kwa maslahi binafsi na kuwaonea na kusema kuwa serikali kali ya awamu ya tano haitamfumbia macho askari atakayebainika kufanya hivyo.

Aidha Waziri Mwigulu amechukua fursa hiyo kuwapa hamasa Askari hao kwa kusema kuwa serikali itawaboreshea maslahi yao kadri bajeti itakavyoruhusu ili waweze kufanya kazi kwa weledi zaidi.

Muigizaji wa filamu Bongo, Jada apoteza kumbukumbu baada ya ajali akiwa location

$
0
0
Muigizaji wa filamu Bongo, Jada amepoteza kumbukumbu baada ya kupata ajali ya kujigonga ukutani akiwa location.

Taarifa hiyo imetolewa na muongozaji wa filamu aliyokuwa anashoot, Leah Richard Mwendamseka maarufu kama Lamata kupitia kipindi cha Magic Style cha CG FM ya Tabora.

Leah amesema Jada anaendelea na matibabu ya kumsaidia kurudisha kumbukumbu zake zote. Amedai kuwa tatizo hilo lilitokea baada ya wiki tatu akiwa ameshamaliza kushoot filamu hiyo na kwamba mashabiki wamuombee.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images