Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Agizo la Rais la Kugawia Wananchi Mawe ya Dhahabu laanza Kutekelezwa Mgodi wa Geita

$
0
0
Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mkoani Geita la kuwagawia wananchi mabaki ya mawe maarufu kama Magwangala kutoka mgodi wa dhahabu wa Geita GGM umeanza kutekelezwa.

Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Sospeter Muhongo yupo katika ziara ya kikazi katika mgodi huo kwa kutafuta sehemu ambayo wachimbaji watayaweka na kuyachenjua kwa ajili ya kuyagawa kwa wananchi.

Akiongea mara baada ya ziara hiyo Mhe. Muhongo amesema kuwa agizo la Rais lilikuwa ni baada ya wiki tatu lakini kwa kuwajali wananchi wa eneo hilo wameamua kuanza zoezi hilo mapema kwa ajili ya utekelezaji wa agizo la rais.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Emanuel Kiunga, amesema kuwa serikali ya Mkoa kwa kushirikiana na wabunge wa mkoa huo na baadhi ya viongozi wametafuta maeneo ya kuweka Magwangala hayo kwa ajili ya kuyahifadhi.

Wakizungumzia maeneo hayo yaliyotengwa kwa ajili ya zoezi hilo baadhi ya wabunge wa mkoa huo akiwemo Mbunge wa viti Maalum kwa tiketi ya CHADEMA, Upendo Peneza, na Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Kasheku Musukuma wamesema serikali lazima iwe makini na mawe hayo pamoja na kuwajali wananchi wa maeneo yaliyotengwa.

Dk Magufuli Ataja Majipu CCM

$
0
0
Licha ya kupokelewa na umati mkubwa wa wana-CCM na kusindikizwa na msafara mrefu hadi ofisi ndogo za CCM, Rais John Magufuli ametaja majipu yaliyopo ndani ya chama hicho akitaka wanachama na viongozi kumvumilia katika kipindi ambacho anataka kurejesha heshima, imani na maadili yaliyopotea.

Magufuli alikuwa mgombea pekee kwenye uchaguzi maalumu wa mwenyekiti wa CCM uliofanyika Julai 23 mjini Dodoma alioshinda kwa kupata kura 2,398 na tangu wakati huo alikuwa kwenye makao hayo makuu ya nchi hadi alipokwenda mikoa ya Kanda ya Ziwa kushukuru wananchi kwa kumchagua kuwa Rais.

Mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius  Nyerere na kupokelewa na vikundi vya ngoma, matarumbeta na mamia ya wanachama, msafara wa magari madogo na mabasi ulielekea ofisi hizo ndogo za CCM zilizoko Lumumba ambako Rais Magufuli alitoa hotuba fupi iliyotaja baadhi ya majipu ndani ya CCM.

“Mahali nitakapoamua kunyosha nitanyooshea hapo hapo,” amesema Magufuli katika hotuba yake iliyochukua takribani dakika 50. “Inawezekana ujio wangu ndani ya CCM usiwafurahishe baadhi ya watu, lakini nina uhakika wanachama wetu zaidi ya milioni nane watafurahi. Nimeamua kufanya kazi kwa uwazi ili kila pato la chama lionekane.”

Rais Magufuli alisema CCM ilianza kupoteza dira na kuwa ya matajiri na kwamba anataka kukifanya kiwe cha aina yake.

Akizungumza baada ya viongozi wa CCM kuhutubia wakipiga vijembe vyama vya upinzani, Rais alisema hata vigogo wa chama hicho watakaokwenda kinyume na taratibu, watang’oka.

Akitaja baadhi ya majipu ndani ya CCM, Magufuli alisema jijini Dar es Salaam chama hicho kina viwanja zaidi ya 410 na kuhoji fedha zinazopatikana kutokana na mali hizo zinakwenda wapi.

“Kulikuwa na (Shirika la Uchumi na Kilimo la CCM)Sukita. Fedha za Sukita zinakwenda wapi? Kuna jengo la ghorofa la vijana wa CCM, naambiwa baadhi ya viongozi wa chama wamejigawia vyumba,” alisema huku akionyesha kwa kidole lilipo jengo hilo huku sauti ikitoka kwa wanachama ikisema “wengine umekaa nao hapo mbele, tunao ushahidi tutakuletea”.

“Hizi fedha zinakwenda kwenye mfuko wa nani? Haya ndio nitayachambua kituo kwa kituo, koma kwa koma, nukta kwa nukta mpaka kieleweke.”

Alisema hata Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) na Jumuiya ya Wazazi wana majengo na vitega uchumi vingi, lakini fedha hazionekani.

“Viwanja vya mpira vya CCM navyo; kipo cha Mwanza, Songea; kuna viwanja sijui wapi na kila kiwanja kimezungushiwa maduka,” alisema.

“Mchezo uliopo; kila kibanda kwenye viwanja wanasema wanalipwa Sh30,000 lakini ukweli walikuwa wanalipwa Sh500,000 au milioni moja. Zile tofauti walikuwepo watu wakubwa ndani ya chama wanazimega. Hao n’talala nao mbele.”

Amesema kuwa anataka CCM yenye lengo la kutawala na si kubembeleza kutawala.

“Haiwezekani kila ukikaribia uchaguzi, tunakwenda kuombaomba kwa wafanyabiashara. UVCCM wenye maghorofa unakwenda kuomba; UWT nao hivyo hivyo na wakati mwingine mnawaomba hata waliohama CCM. Hawa UWT wanawafuata kwa kuvaa baibui usiku, yaani asubuhi ni CCM na usiku ni Chadema. Nasema uongo  UWT?” alihoji na kuitikiwa “kweliii”.

“Hivi kwanini Redio Uhuru haina fedha na haipati matangazo? Kwanini kikundi cha TOT kina shida? Kwanini CCM haina hata televisheni? Lazima tujipange vizuri, tubadilike na kukubali changamoto. Asiyekubali kubadilika tutajitahidi kumbadilisha na asiyeweza kubadilika tutamwacha pembeni.”

Alisema katika uongozi wake anataka kuondoa kero za wananchi, huku akieleza jinsi anavyotekeleza ahadi yake ya elimu bure, kukusanya kodi, kujenga viwanda, kuimarisha miundombinu ya usafiri na kuimarisha sekta ya afya.

Kuhusu uchaguzi mkuu wa CCM utakaofanyika mwakani, Rais alisema atahakikisha wanapatikana viongozi wenye sifa na ambao hawatatoa rushwa.

“Atakayetoa fedha, jina lake halitarudi maana hata mimi nimepatikana bila rushwa,”

Amesema ilikuwa vigumu kuwania nafasi ya uongozi ndani ya CCM na kushinda akifananisha na ngamia kupenya kwenye tundu la sindano.

Katika hotuba hiyo, Rais Magufuli amesema wapo mafisadi waliosalia licha ya baadhi yao kukimbia baada ya kutoswa katika mchakato wa urais ndani ya CCM.

Chadema Wagawana Bendera za Ukuta

$
0
0
Chadema imeanza maandalizi ya operesheni ya kupinga uvunjaji wa katiba na sheria nchini iliyopangwa kufanyika Septemba Mosi kwa kugawa bendera za chama hicho kwa viongozi mbalimbali wa Kanda ya Pwani.

Kanda ya Pwani ya chama hicho inajumuisha mikoa ya Dar es Salaam na Pwani. Bendera hizo ni kwa ajili ya kuweka kwenye ofisi, kwenye nyumba na maeneo ya biashara na kupeperusha kwenye magari.

Katibu wa Kanda ya Pwani, Casimir Mabina amewaambia waandishi wa habari kwamba wanafanya hivyo kama ishara ya kuunga mkono tamko la Kamati Kuu ya Chadema ya kufanya maandamano ya amani na mikutano nchi nzima.

“Chadema Kanda ya Pwani tunaunga mkono kauli na tamko la Kamati Kuu ya Chadema la kupinga kwa nguvu zote, msimamo wa utawala huu wa awamu ya tano wa kukandamiza demokrasia. Sisi Kanda ya Pwani tutashiriki kikamilifu katika operesheni hiyo,” amesema Mabina.

Amewataka wafuasi wa chama hicho kanda hiyo kutundika kila eneo bendera watakazopewa katika kile alichokiita amshaamsha kuelekea Septemba Mosi.

“Mwenye gari aweke bendera, mwenye ofisi, mwenye duka, kila kona tandazeni bendera za chama kama ishara ya kuunga mkono uamuzi wa chama chetu wa kupinga uminywaji wa demokrasia unaofanywa na serikali ya awamu ya tano,” alisema.

Hata hivyo, Rais John Magufuli ameonya mara kadhaa kwamba asijaribiwe, mikutano ya siasa hadi mwaka 2020. Mikutano pekee aliyoruhusu ni ya ndani na wabunge katika majimbo yao lakini si ya wanasiasa.

Chadema inasema tamko hilo la Rais Magufuli ni kinyume cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano, Sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992, na Kanuni za maadili ya vyama vya siasa za mwaka 2007, kwani zinaruhusu mikutano na maandamano kwa ajili ya kutafuta wanachama na kunadi sera mradi watoe taarifa polisi kwa ajili ya ulinzi. Katika siku za hivi karibuni, mikutano kadhaa ya Chadema imesambaratishwa na Jeshi la Polisi.

Katika mkutano huo na waandishi wa habari, Mabina amesema anashangaa wakati Rais Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM anakataza wapinzani kuandamana, wafuasi na wanachama wake wameonekana wakifanya maandamano kutoka uwanja wa ndege kuelekea yalipo makao makuu ya chama chao.

“Nasema haya kutokana na taarifa iliyotolewa na Ole Sendeka kuwa Rais alikuwa akifanya ziara ya chama ambayo ilianzia Dodoma makao makuu ya CCM baada ya kuchaguliwa kushika wadhifa wa mwenyekiti wa Taifa… leo (jana) amemalizia mtaa wa Lumumba zilipo ofisi ndogo za chama,” alisema

Kwa mazingira hayo, Mabina alisema Chadema Kanda ya Pwani inaunga mkono operesheni hiyo iliyopewa jina la Ukuta na kuwa watahakikisha inafanyika kama ilivyokusudiwa na kwamba kwa umoja wao watasimama imara.

“Kutokana na Serikali ya awamu ya tano kuonekana kukandamiza demokrasia nchini, sisi Chadema Kanda ya Pwani tumeazimia kushiriki kwa nguvu zote kwenye operesheni Ukuta” alisema.

Aliongeza kuwa nia yao ni kuungana na wenzao nchi nzima kupinga ukandamizaji wa demokrasia na uhuru wa vyama vya upinzani kufanya siasa kama Katiba na sheria za nchi zinavyoruhusu.


Mzee Yusuf Afanya Maamuzi Magumu

$
0
0
Gwiji wa mziki wa taarabu nchini Mzee Yusuf amethibitisha kuwa ameachana na kazi hiyo takribani miezi miwili iliyopita.

Taarifa zilizoenea katika mitandao ya kijamii zimeeleza kuwa mwanamziki huyo ameachana na mziki na kuamua kumrudia Mungu.

Akizungumza na Mwananchi Digital kwa njia ya simu usiku huu, mmiliki huyo wa bendi ya Jahazi Modern Taarab amethibitisha kuwa taarifa hizo ni kweli na kuongeza:

“Nashangaa taarifa hizi zinasemwa leo. Ni suala la muda mrefu….takribani miezi miwili iliyopita na sababu ni kuwa nimeamua kumrudia Allah,”

Mwanamziki huyo mzaliwa wa Zanzibar alipoulizwa kuwa ni suala gani lililomsukuma hata achukue maamuzi hayo magumu, alijibu kwa kifupi, “ndivyo tunavyofundishwa na viongozi wa dini.”

Yusuph aliyetamba na vibwagizo kama “Nichumu, nikisi….mwaaaa,” katika baadhi ya nyimbo zake, amesema familia yake imeupokea uamuzi wake kwa mtazamo chanya na kwamba inamuunga mkono.

“Kwa sasa nitaimba kaswida zenye mafundisho ya dini,” amesema nyota huo huku akiahidi kufanya mkutano rasmi kuelezea suala hilo.

Mfalme huyo aliyeonekana kuwa ni gwiji wa taarabu ya kisasa (modern taarab) amezaliwa visiwani Zanzibar mwaka 1977. Aidha amejihusisha na sanaa nyingine kama maigizo.


Magufuli: Kuna Viongozi wa UVCCM Wamegawana Magorofa ya Vitega Uchumi ya Umoja Huo

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM Mh. John Pombe Magufuli akihutubia wanachama wa chama hicho leo kwenye ofisi ndogo ya CCM Lumumba amesema, ana taarifa viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM UVCCM wamejigawia vyumba vya magorofa ya vitega uchumi wa umoja huo yaliyojengwa karibu na jengo la umoja wa vijana.

Amesema viongozi hao wamekuwa wakikusanya kodi za majengo hayo na kodi hizo kuishia mifukoni mwao.

Kazi ya kutumbua majipu ya chama ndio kwanza inaanza.

Source: ITV.

Rais Magufuli: Ikulu ya Magogoni Haitauzwa Serikali ikihamia Dodoma, itabaki Kama Makumbusho

$
0
0
Rais Dkt.John Pombe Magufuli amesema kwamba serikali haina mpango wa kuiuza Ikulu ya Rais jijini Dar es salaam kama ambavyo baadhi ya watu walisema kufuatia utekelezaji wa mpango wa serikali kuhamia Dodoma.

Akizungumza kwenye ofisi ndogo ya CCM jijini Dar es salaam leo akitokea mkoani Mwanza Rais Magufuli amesema kwamba mpango wa serikali kuhamia Dodoma uko pale pale ikiwa ni ahadi yake mara baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM mkoani Dodoma mwezi uliopita.

Rais Magufuli alisema serikali pamoja na watumishi wote wa watahamia Dodoma ila Ikulu ya Rais jijini Dar es salaam itabaki kama Makumbusho.

“Hatuwezi kuuza ikulu, Ikulu itabaki pale kama makumbusho” Alisema Rais Magufuli huku akishangiliwa na baadhi ya wanachama chama cha Mapinduzi.

Naye Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amemhakikishia Rais kuwa watatekeleza kwa ukamilifu maagizo yake ikiwa na pamoja na Mpango wa serikali kuhamia Dodoma.

Kwa upande mwingine Rais Dkt. John Magufuli hivi karibuni alitangaza kuuza majengo ya wizara Dar es Salaam, atakapohamia yeye katika makao makuu ya nchi mkoani Dodoma.

Rais Magufuli alisema hayo hivi karibuni kwenye mkutano wa hadhara mkoani Singida, katika siku ya kwanza ya ziara yake ambapo alisisitiza kuwa atahakikisha anauza baadhi ya majengo hayo kwa mnada, ili wale wasiotaka kuhama, wahame kwa lazima.

Kafulila: Rais Magufuli Anazidi Kudidimiza Uchumi

$
0
0
DAVID Kafulila, aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Kigoma Kusini (2010-2015) amesema takwimu za kiuchumi zinaonyesha hali ya Tanzania inaendelea kuwa mbaya zaidi chini ya Serikali ya awamu ya tano, anaandika Pendo Omary.

Kafulila ambaye alipoteza ubunge katika mazingira ya kutatanisha katika uchaguzi Mkuu wa mwaka jana ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam katika kongamano lililoandaliwa na Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) ili kuadhimisha siku ya vijana duniani.
Kafulila amesema kuwa kwa sasa Tanzania ndiyo nchi inayoongoza kwa deni kubwa Afrika Mashariki ambapo deni la taifa la Tanzania ni 40% ya pato la taifa hali inayoliweka taifa pabaya zaidi kiuchumi.

“Wakati hali ikiwa hivyo kwetu, deni la taifa la Kenya ni 25% ya pato la taifa lao na deni la taifa la Uganda ni 20 ya pato la taifa na bado Rais John Magufuli anaendelea kukopa kwa kasi ya ajabu,” amesema na kufafanua zaidi kuwa;

“Kwa mujibu wa ripoti ya robo mwaka ya Benki ya Dunia katika kipindi cha robo mwaka tu cha utawala wa Rais Magufuli tayari serikali yake imekopa zaidi ya 900 milioni dola za kimarekani ambazo ni zaidi ya Sh. 2 trilioni za kitanzania.”

Kafulila ametahadharisha kuwa kwa kasi ya ukopaji ya Rais Magufuli na serikali yake suala la serikali kujiendesha yenyewe kwa kujitegemea ni ndoto ambayo haiwezi kufikiwa katika miaka ya hivi karibuni.

“Wakati makusanyo yote ya mapato ya serikali hapa nchini kwa mwezi ni 1.2 trilioni, malipo ya mishahara peke yake ni zaidi ya 570 bilioni kila mwezi lakini wakati huo huo serikali ya Tanzania inalipa deni la Shilingi 500 bilioni kila mwezi. Ameeleza.

Kafulila pia amesema licha ya tambo za serikali ya Tanzania kuwa imeongeza ukusanyaji wa mapato lakini fedha katika shughuli za msingi zinazochochea ukuaji wa uchumi kama kilimo zinazidi kufyekwa na serikali.

Ametoa mfano kuwa; Katika sekta ya kilimo Mwaka 2015 serikali ilitoa 78 bilioni kama ruzuku katika mbolea lakini mwaka huu serikali imetoa 10 bilioni tu kama ruzuku katika mbolea.

Lakini pia akisema mwaka jana akiba ya taifa ya chakula ilikuwa zaidi ya tani laki 4 (400,000) lakini mwaka huu akiba ya chakula ni tani elfu sitini na nane pekee (68,000) na wakati huo huo riba katika mikopo ya benki imepanda kutoka 14% ya 2005 hadi 25% kwa mwaka 2015.

Kongamano hilo lenye mada, “kupiga vita umasikini ili kufanikisha uzalishaji na matumizi endelevu” linaendelea muda huu.

Sauti ya Diamond Kwenye wimbo wa Dully Sykes feat Harmonize - INDE

$
0
0
Mimi si timu alikiba wala mavi kunuka gani sijui wala chama sina. Nakosoa panapohitajika.

Diamond hapa unachemka, atakayeiskia hii nyimbo atajua direct we ndio unayeimba, sauti yako tayari iko common, it doesnt make sense unapoenda kumtuma huyu dogo mayonaise kutoa video anarukaruka tu kapwaya.

Hapo ukiangalia Dully kafunika mbaya, mmeiga jina INDE MONIE-KANDA BONGOMAN, bado muigane sauti kucheza, mavazi, style na kila kitu.

Bwa'mdogo wa Mbagala jaribu japo kutengeneza muziki wako unaotambulika kimataifa,
mfano mdogo Chameleone.

We unaiga kila kitu, ndio maana yule nani sijui Davido alisema `"he will make you famous". We mwanamuziki unaalikwa matamasha ya kimataifa you dnt even know what to say there.

Kila muziki wako unakuja na kolabo na wanaijeria, mpaka siku hizi wabongo nje tunaitwa kollabo. Bado miziki yako ya zamani its my favourite km muziki gani, nataka kulewa, Kizaizai, Mbagala.

Jitahidi kutunga na uimbe mwenyewe. Kiuhalisia huyo dogo hapo anarukaruka tu kuuza sura na sauti haimkai kabisaaaa.

Kalaghabahoooo

Katarina Karatu, mchekeshaji wa kike namba 1 Tanzania

$
0
0
Asee sikuwahi kudhani kwamba kuna wanawake wenye kipaji cha comedy nimeona kwa Katarina yaani huyu Dada ni shidaa kila nikiangalia vipande vyake vya video nacheka mbavu sina. Alafu cha ajabu haendani na comedy kabisa, ukimuona mtoto mrembo kabisa aisee

Jukwaa la Wahariri lapinga Mseto kufungiwa

$
0
0
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limepinga hatua ya Serikali kulifungia gazeti la Mseto kwa mtindo wa yenyewe kujifanya mlalamikaji, mwendesha mashtaka na hakimu.

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limepokea kwa mshituko taarifa za kufungiwa kwa miezi 36 gazeti la Mseto kwa kutumia kifungu cha 25(1) cha Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976.

Katika maelezo ya Waziri, Nape Nnauye anasema tangu Mwaka 2012 wamekuwa wakiwaonya Mseto bila gazeti hilo kubadilika.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Halihalisi, Saed Kubenea amekana kupata maonyo kutoka Serikalini.

Sisi TEF tunapinga utaratibu wa Serikali kuwa mlalamikaji, mwendesha mashitaka na Hakimu katika kesi inazohusika.

Tunataka mchakato wa kubadili Sheria ikaanzisha chombo cha kitaaluma cha kusimamia wanahabari na vyombo vya habari uende haraka kwa nia ya kumaliza kadhia hii.

Serikali imeahidi muda mrefu kubadili Sheria hii mbaya ya Magazeti lakini miaka yote utekelezaji umekuwa sifuri.

Tunasisitiza kuwa hatukubaliani na wala hatuungi mkono utaratibu huu wa Serikali kufungia au kufuta vyombo vya Habari.

Kwa upande mwingine tunapenda kuvitahadharisha vyombo vya Habari katika matumizi ya nyaraka ili kuepuka kuingia katika migogoro na Serikali, Jamii au mtu mmoja mmoja.

Pamoja na taarifa hii, TEF itafanya uchunguzi na uchambuzi wa adhabu iliyotolewa kwa Gazeti la Mseto pamoja na habari iliyosababisha gazeti hilo kufungiwa, kwa manufaa ya waandishi wa habari na vyumba vya habari.

Makonda Aumbuka, Azomewa Mbele ya Magufuli

$
0
0
PAUL Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amezomewa na wafanyabiashara wadogowadogo (wamachinga) mbele ya Rais John Magufuli, anaandika Faki Sosi.

Tukio hilo lilitokea jana katika ofisi ndogo za Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizopo Mtaa wa Lumumba, jijini Dar es Salaam baada ya Rais Magufuli kutoka mikoani kwa ziara yake ya kuwashukuru Watanzania.

Wafanyabiashara hao walifika kwenye ofisi hizo wakiwa na mabango yalio na maandishi yenye ujumbe wa malalamiko kwa rais dhidi ya Mgambo wa Jiji wanaowazuia kufanya biashara zao.
Wakati Rais Magufuli akizungumzia suala la mama lishe, wauza mbogamboga na wamachinga kuhusu kusumbuliwa na Mgambo wa Jiji, alisema ameteua viongozi wazuri akiwemo Makonda kama Mkuu wa Mkoa.

Lakini alipotajia jina la Makonda, sauti kutoka kwa wamachinga zilipiga kelele na kusema ‘jipu hilooooo baba,’ kelele hizo ziliendelea.
Rais Magufuli alisita kidogo kuongea kupisha zomea hiyo na baada ya muda mchache aliendelea kuzungumza.

Pamoja na Makonda kuzomewa, Rais Magufuli alisema, hataki kuona makundi hayo yakibaguliwa na kuagiza kuandaliwa kwa utaratibu mwingine.

Wamachinga hao walifika kwenye hadhara hiyo na mabango mbalimbali ambayo moja ya jumbe zilizoonekana kwenye mabango hayo ni pamoja na ‘Kilio chetu kwa Rais JPM ulituahidi ukiingia Ikulu mgambo watafute kazi nyengine…’ na ‘wamachinga tumekosa uhuru’ ambapo Rais Magufuli. Hata hivyo Rais Magufuli aliwataka watulie.

Kadhia ya kuzomewa Makonda mbele ya Rais Magufuli inamfika siku chache baada ya John Mongella, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kuzomewa mbele ya rais huyo.
Mongella alikumbana na kasheshe hiyo wakati akitoa taarifa fupi ya hali ya usalama na shughuli za maendeleo Mkoa wa Mwanza.

Akiendelea kusoma ghafla wananchi hao walianza kumzomea, hatua ya kuzomea ilianza pale Mongella alipodai kwambwa, hakuna njaa katika mkoa huo.

Mongella amedai kuwa, katika mkoa huo wa Mwanza, wamefanikiwa kuvuna chakula kingi na hakuna tatizo la njaa, kitendo ambacho kilipingwa na wananchi hao ambao walisikika wakidai, “acha uongo’ tuna njaa, hakuna chakula.”

Source:Mwanahalisi

Picha:Ujauzito wa Zari Sasa Unaonekana...Diamond Platnumz Aomba Ushauri wa Jina la Mtoto Wake wa Kiume

$
0
0
Bongo fleva super staa Diamond Platnumz ameweka wazi kuwa anatarajia kupata mtoto wa kiume na kwamba angependa mashabiki wake watoe mitazamo yao juu ya jina gani ampe mtoto wake.

Mpaka sasa tunafahamu kuwa mwezi Decemba ndio Zari atajifungua mtoto huyu wa pili.

Kupitia instagram yake Diamond aliandika hivi… “Looking so sexy, my Beautiful and cute Wife @zarithebosslady???? ????!!!… Please tell what would you like me to name my Upcoming Son?…(Tafadhali niambie Mtoto wangu wa kiume unadhani akija nimwite jina gani…?)”

Chadema Yaanza Kugawa Vifaa vya Operesheni UKUTA

$
0
0
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Pwani kimeanza kugawa vifaa zikiwemo bendera kwa ajili maandalazi ya Umoja wa Kupinga Udikteta ( Ukuta) ambayo yanatarajia kufanyika Septemba mosi mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Katibu wa Kanda ya Pwani wa Chadema, Casimir Mabina, alisema kuwa bendera hizo zitaanza kupeperushwa kuanzia kesho kutwa kwa ajili ya kuunga mkono azimio la Kamati Kuu ya kufanyika oparesheni Ukuta.

Alisema oparesheni Ukuta ni lazima ifanyike nchi nzima na kwamba hawako tayari kuona ukandamizaji wa demokrasia unaoendelea kufanywa na serikali ya awamu ya tano ambayo imeonyesha viashiria vya utawala wa kidikteta.

Alisema Rais John Magufuli, anajaribu kuua demokrasia ya vyama vingi kwa kukataza na kuzuia mikutano ya kisiasa ya vyama vya upinzani huku CCM ikiendelea na mikutano yake kama kawaida.

“Tumeona jinsi Rais alivyopiga marufuku wapinzani kukutana kwenye mikutano ya hadhara huku akiwatishia kuwa wakikaidi atawashughulikia na kweli amewaamuru polisi watekeleze amri hiyo ya kuwakamata viongozi wa Chadema na kuwafungulia mashtaka,” alisema

Aliongezea kuwa mbaya zaidi Jeshi la Polisi linazuia hata mikutano ya ndani ya vyama vya upinzani na makongamano na hata mahafali ya wanafunzi wenye itikadi za upinzani licha ya kutambua kuwa mikutano ya ndani haiwezi kuleta uvunjifu wa amani kwa walio ndani ya ukumbi.

Alisema licha ya kwamba Mwenyekiti wa CCM Rais Magufuli. amekataza mikutano hiyo kufanyika chama tawala, kinafanya mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali kwa kisingizio cha shughuli za serikali.

Mabina alisema juzi CCM ilisema itakuwa na maandamano kutoka uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere ya kumpokea Rais Magufuli hadi Makao Makuu ya CCM yaliyopo Lumumba.

“Tunahoji haki ya kufanya siasa ni kwa CCM tu na siyo kwa vyama vingine? Hili jambo hatuwezi kukubali Jeshi la Polisi lituambie inakuwaje vibali vinatolewa kwa CCM halafu upinzani tunyimwe tunasema lazima tufanye oparesheni Ukuta ya kupinga ukandamizaji wa demokrasia,” alisema Mabina

Naye Katibu wa Wabunge wa Upinzani Mkoa wa Dar es Salaam, Mbunge wa Viti Maalum, Anatropia Theonest, alisema lengo la oparesheni ya Ukuta ni kupinga ukandamizaji unaofanywa na serikali.

Alisema wana haki ya kikatiba ya kufanya mikutano bila kuzuiliwa kama ambayo wamefanyiwa na ndio maana wameanza kugawa bendera kwa ajili ya kujiandaa na oparesheni hiyo.

Nicki Minaj Ambwaga Meek Mill..Chanzo Cha Kumwagana Hichi Hapa

$
0
0
Mastaa waliokuwa wapenzi kwa zaidi ya miaka miwili Meek Mill na Nicki Minaj wametengana.

Watu wa karibu na Couple hii wanasema Meek Mill amekuwa na maisha tofauti na Minaj huku Meek akitaka zaidi kuendelea na maisha yake ya mtaani na masela na Minaj akitaka kumbadilisha ili aishi kistaa zaidi.

Maisha ya zamani ya wasanii hawa wawili yanafanana ila Minaj hataki tena kuwa mtu wa HOOD sana ila Meek bado yuko ki HOOD sana.

Mpaka sasa wawili hawaja sema chochote kuhusu Taarifa hizi.

Mrembo wa Kenya Vera Sidika aeleza sababu na kiasi cha pesa alichotumia kuongeza maziwa yake.

$
0
0
Mrembo maarufu kutoka Kenya,Vera Sidika ameweka wazi kuwa alifanya plastic surgery ili aweze kuwa na matiti makubwa.

Vera aliyasema hayo akiwa kwenye mahojiano ya Tv na kipindi cha FNL cha EATV ambapo alieleza kuwa alifikia uamuzi huo baada ya kuona sehemu zingine za mwili wake ni kubwa kasoro matiti,hivyo akaamua kutafuta mwili wenye uwiano.

“Kipindi nakua kutoka utotoni na kuwa kijana,mwili wangu ulianza kuwa mkubwa na ukaanza kuwa mkubwa sehemu nyingine huku kwa juu nikawa kama nimenyimwa kidogo,halafu kwenye industry kama hollywood sio big deal,watu wanafanya surgery kama kawaida ila kwa Afrika ni kitu kipya..Nilifanyiwa surgery ya matiti,inaitwa boob job,nilikuwa nataka niwe na mwili wenye uwiano,nilifanyiwa Marekani mjini hollywood na iligharimu kama dola elfu 30” alifunguka vera sidika ambaye pia alidai kuwa uamuzi huo ulichangiwa na ukweli kwamba alitaka avutie zaidi kwenye show biz na kuongeza kuwa hela alizotumia kufanya plastic surgery zinarudi kutokana na madili anayopata kwenye show biz kutokana na muonekano wake ikiwemo kuonekana kwenye videos za wasanii,magazines na special appearance kwenye clubs.

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya Agosti 14, Ukuta Ngangari Wakomaa na Jiji

$
0
0



SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya Agosti 14, Ukuta Ngangari Wakomaa na Jiji 

Paul Makonda kuzichapa na bondia Francis Cheka kuhamasisha usafi

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anatarajia kupanda ulingoni Agosti 27 kuzichapa na bondia Francis Cheka katika pambano la kuhamasisha usafi jijini Dar es salaam.

Akizungumza jijini Dar, Cheka amesema kampuni yake ya Cheka promosheni imeandaa pambano hilo ili kuunga mkono jitihada za Makonda katika zoezi zima la usafi.

“Siwezi kujua mkuu wa mkoa maandalizi yake ambayo amejiandaa lakini siku zote namuogopa mtu ambaye anaamua mapambano na mtu anayejua ngumi, ila namheshimu mkuu wa mkoa, kupitia mkuu wa mkoa ambapo wao ndiyo wametangaza usafi na sisi tusupport usafi katika nchi yetu,”, alisema.

Cheka aliongeza kuwa kutakuwa na mabondia kutoka Kenya, Uganda na Malawi.

Aidha Cheka amesema zoezi la kuhamasisha mabondia kushiriki katika usafi litakuwa endelevu katika mikoa mingine ikiwa ni Arusha, Morogoro, Dodoma na Mwanza.

Kwa upande mwingine, Afisa michezo ofisi ya mkuu wa mkoa, Adolf Ally, aliwataka watu wengine kuiga mfano wa Cheka katika kampeni yao ya ‘Usijifanye mstaarabu kuwa mstaarabu.’

Mrema Ataka Mateja Wasitupwe Jela

$
0
0
MWENYEKITI wa Bodi ya Taifa ya Parole, Augustine Mrema ameshauri waathirika wa dawa za kulevya kupelekwa hospitalini kupata tiba badala ya polisi kuwakamata na kuwapeleka mahabusu au gerezani ambapo huko hujazana bila kupata msaada wowote.

Aidha, amesema atamwomba Rais John Magufuli kumrejesha kazini Mwalimu wa Sekondari, Emmanuel Roman ambaye alifukuzwa kwa ajili ya utumiaji wa dawa hizo, lakini hivi sasa ameacha baada ya kupata tiba na ushauri nasaha.

Mrema alitoa ushauri huo jana Dar es Salaam alipokutana na waathirika wa matumizi ya dawa za kulevya katika Ukumbi wa Friends Corner, Manzese katika Manispaa ya Kinondoni.

Alisema anapopelekwa gerezani mtumiaji wa dawa za kulevya atakuwa hajasaidiwa, kwani atazidi kuharibikiwa badala ya kurekebishwa.

“Ni marufuku kukamata vijana wadogo wanaotumia kete. Sio kama nahamasisha waendelee kutumia ila wakikamatwa wapelekwe hospitali za Muhimbili, Mwananyamala na Temeke ambako kuna vituo vyao. “Ukianzisha operesheni ya kukamata wezi bila kujua historia zao inawezekana ni waathirika wa dawa za kulevya, ambao wanapoanza kutumia kuacha ni kazi sana hivyo wanalazimika kuiba ili wapate hela ya kununua dawa hizo,” alisema mwanasiasa huyo mkongwe aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Kwa upande mwingine amevitaka vyombo vya usalama kushughulikia wafanyabiashara wakubwa wa dawa hizo maarufu kama `Mapapa wa dawa za kulevya’, badala ya kuhangaika na hao wanaotumia ili kudhibiti hali hiyo.

“Hili nitalifikisha kwa Rais nimwambie taifa lako linaangamia, vijana wanaharibika kutokana na dawa za kulevya, hivyo awashughulikie mapapa wanaoleta dawa kutoka Iran, kwani wanajulikana kwa majina na wengine wanachukua na kusambaza mtaani,” aliongeza.

Alisema kutokana na janga la dawa za kulevya kuzidi kuwa kubwa nchini, atamwomba fedha Rais Magufuli za kuwasaidia waathirika hao kuunda vikundi vya kuzalisha mali.

Pia ameshauri waathirika hao ambao wameacha watumike kukomesha wizi katika Jiji la Dar es Salaam kwa kuwakamata mateja ambao wanawajua.

Naye Mwalimu Romani alianza utumiaji wa dawa za kulevya mwaka 1998 akiwa sekondari na aliendelea kutumia hadi alipohitimu kidato cha sita na kwenda chuo cha ualimu, kisha kuanza kazi ambayo aliachishwa kwa kutoonekana kazini kwa muda.

wali, mwathirika wa dawa za kulevya ambaye ni mtaalamu wa masuala ya kompyuta katika Hospitali ya Mwananyamala, Yusuph Mizito akisoma risala kwa niaba ya wenzake, alisema wamekuwa wakikabiliwa na uhaba wa vituo vya tiba, kwani kwa nchi nzima vipo katika Jiji la Dar es Salaam pekee.

Alisema watumiaji wa dawa hizo ambao wameamua kuacha dawa za kulevya husafiri kupata huduma Dar es Salaam ambako vituo hivyo vipo Mwananyamala, Muhimbili na Temeke.

Download Application ya SIASA HURU Blog Kwenye Simu yako Kupata Habari za Siasa Kwa Urahisi

$
0
0
Kama wewe ni mpenzi wa Habari za Siasa basi hii ni habari njema kwako...Download Siasa Huru Application Kutoka Google Play Store Kwenye Simu yako itakurahisishia upataji wa Habari na Breaking News za Siasa kwa urahisi....

Bonyeza HAPA Kuinstall Kwenye Simu yako fasta....

Au Nenda Google Play Store Kwenye Simu yako Alafu Search 'Siasa Huru' Kisha Install


Waziri Ajiuzulu Kwa Sababu ya Kulewa Sweden

$
0
0
Waziri wa elimu nchini Sweden amejiuzulu wadhifa wake baada ya kupatikana akiendesha gari akiwa mlevi.

Bi Aida Hadzialic, ambaye amekuwa waziri wa elimu ya sekondari na elimu ya watu wazima, amejiuzulu baada ya kukamatwa na polisi Malmo.

Kwenye taarifa iliyoonyesha hisia nyingi, Bi Hadzialic , ambaye ndiye mtu mchanga zaidi kuwahi kuteuliwa waziri nchini humo, amesema sharti awajibike kwa alichosema ni kosa kubwa zaidi alilowahi kulifanya maishani mwake.

Alipimwa na kugunduliwa kwamba alikuwa tu amepitisha kidogo kipimo kinachoruhusiwa cha unywaji pombe.

Sweden huwa na sheria kali sana za kuzuia uendeshaji gari mtu akiwa amelewa.
Bi Hadzialic, aliyehamia Sweden kama mkimbizi Mwislamu kutoka Bosnia Herzegovina akiwa mdogo, amesema alikuwa amekunywa gilasi mbili pekee za mvinyo.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images