Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Zitto Kabwe afunguka yake kuhusu Oparesheni UKUTA...Adai ni Haki Yao Kuandamana

$
0
0
Wakati viongozi wa dini wakiendelea na jitihanda za kusaka suluhu kati ya upande wa Serikali na Chadema kuhusu namna ya kuzuia kwa amani kufanyika kwa Operesheni ya chama hicho iliyopewa jina la UKUTA, Septemba 1, Kiongozi Mkuu wa Chama Cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe ametoa maoni yake.

Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini amesema kuwa haoni haja ya kufanyika kwa vikao hivyo vya kusaka maridhiano kwani Chadema wanachotaka kufanya kiko kikatiba.

“Sioni ni kwanini tunahangaika na vikao vya maridhiano na tahariri nyingi kuhusu shughuli ya CHADEMA kufanya operesheni yao ya UKUTA. Kuandamana ni Haki ya KIKATIBA. Tuache watu watimize Haki yao Kwa amani. Kuzuia watu kufanya jambo lao la kikatiba ndio kuvunja amani. Wanaotaka kuandamana waandamane na wanaotaka kufanya Kazi zao nyingine tuendelee na Kazi zetu. Kwanini kutekeleza Haki ya kikatiba iwe ni kuvunja amani? Kwanini?,” Zitto ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Hata hivyo, vikao vya maridhiano vinavyoendelea tayari vimeonesha kuzaa matunda kwenye suala la mgogoro wa Bunge ambapo wabunge wa vyama vya upinzani wameridhia kurejea Bungeni katika vikao vitakavyoanza mapema mwezi ujao.

Serikali imeendelea kuwaonya watu wote wanaopanga kuandamana Septemba 1 huku viongozi wa Chadema wakisisitiza kuwa siku hiyo watafanya maandamano kama walivyopanga.

Hali hiyo imepelekea kumtoa hadharani Kingunge Ngombale Mwiru ambaye ameomba marais wastaafu kumshauri Rais Magufuli ili kuruhusu Serikali kukaa na Chadema kusaka muafaka wa masuala ya kisiasa nchini.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa ya Agosti 26, Ikiwemo ya Ukawa, ACT Wataka Magufuli Afute Siasa

$
0
0


Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa ya Agosti 26, Ikiwemo ya Ukawa, ACT Wataka Magufuli Afute Siasa

Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema Adaiwa Kukamatwa na Polisi Leo Asubuhi

$
0
0
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema(CHADEMA) anadaiwa kukamatwa na Jeshi la Polisi leo alfajiri na anashikiliwa kituo cha kati.
Sababu za kukamatwa kwake bado hazijawekwa wazi

Tabia Tatu Kubwa Zinazoleta Tofauti Kati Ya Tajiri Na Maskini

$
0
0
Kila kitu kinapoanza kwenye hii dunia huwa kinaanza sawa na kitu kingine. Kwa mfano mimea inapoanza kuchipua yote huanza pamoja lakini utofauti hujitokeza katika kukua kwake kwa kadri siku zinavyokwenda, kwa mingine kuwa mikubwa sana na mingine midogo ya kawaida.

Pia hata wanyama wengine wanapozaliwa iwe swala au simba wote huzaliwa wote wakiwa na nguvu sawa lakini utofauti huanza kujitokeza kwa jinsi wanavyoendelea kukua. Wengine hujikuta wana nguvu zaidi kuliko wengine na wengine hubaki wanyonge wanyonge.

Halikadhalika linapokuja suala la mafanikio mambo pia huwa yapo hivyo hivyo. Hii ikiwa na maana kwamba, kila binadamu amezaliwa sawa na binadamu mwingine. Hakuna binadamu ambaye atasema alikuja duniani akiwa na mafanikio na mwingine akiwa hana. Wote tulizaliwa tukiwa hatuna kitu.
Kama mambo yako hivi, ni nini kinacholeta tofauti hizi kubwa? Kwa nini wengine wawe matajiri na wengine wawe maskini? Je, matajiri wanakipi cha ziada kinachowafanya wafanikiwe? Kimsingi, huwa yapo mambo mengi kidogo yanayosababisha wengine wawe matajiri na wengine kuwa maskini.

Lakini katika makala haya tutaongelea mambo matatu ambayo yanahusiana na tabia ambazo zinaleta utofauti kati ya maskini na tajiri. Ni kweli zipo tabia ambazo matajiri wanazo na huwafanya wao kuwa matajiri kila kukicha. Ni tabia ambazo huwatenga kabisa na maskini na kuwaacha matajiri waendelee kufanikiwa.

Ikiwa utaamua kujifunza na kuzifatilia tabia hizi kwa karibu, uwe na uhakika utajiri utakuwa mikononi mwako muda sio mrefu. Nasema hivyo nikiwa na maana hii, ukitaka kuwa tajiri fanya yale ambayo matajiri wanafanya nawe utafanikiwa na kuwa kama wao.

Hebu kwa pamoja bila kupoteza muda, tuangazie nukta kadhaa, zinazoweza kutuonyesha tabia zinazowatenga kati ya  matajiri na maskini.

1. Kuwekeza.
Watu wenye sifa ya utajiri ndani mwao hata kama bado hawajafika huko kwenye utajiri halisi ni wawekezaji wazuri sana. Si watu wa kuridhika na chanzo kimoja cha mapato. Wana vitega uchumi vingi sana ambavyo vinawasaidia kuingiza mapato kwa wingi hata kama wamelala.

Kwa mfano uatakuta wamewekeza kwenye mashamba, mafuta, migodi na maeneo mengine mengi. Hii ni sifa mojawapo kubwa inawatenga maskini na matajiri. Ukiona una kitega uchumi kimoja ujue unajizibia nafasi mwenyewe ya kuelekea kwenye utajiri mkubwa.

2. Kuweka akiba.
Suala la kuweka akiba kwa watu matajiri sio suala la hiari, kwao ni lazima. Angalau huweka asilimia kumi ya kile wanachokipata. Wanajua vizuri akiba hizo ni msaada mkubwa kwa baadae katika suala zima la kuwekeza. Wao katika kuweka akiba ni lazima, na pia hawana mchezo katika hilo.

Kutona na tabia hii, huwafanya wazidi kufanikiwa kila siku na kuwaacha maskini wakibaki kuwa maskini. Ni kitu ambacho unatakiwa kujifunza na kuelewa kwamba, akiba ni jambo la msingi sana kujiwekea kama unataka kuwa tajiri. Vinginevyo acha kuweka akiba, uendelee kubaki kwenye umaskini.

3. Kutoa.
Tabia nyingine inayowatenga watu matajiri na maskini ni ile hali ya kutoa. Watu matajiri ni watoaji wazuri sana wa pesa na mali zao. Hufanya hivi si kwa sababu wanazo nyingi, bali kutoa ni moja ya kanuni kubwa ya mafanikio walioamua kuitumia. Huwezi kufanikiwa sana kama hutoi.

Ieleweke hivi, maskini wanaendelea kubaki kuwa  maskini kwa sababu ya uchoyo walionao. Hukumbatia sana walivyonavyo na kusahau kutoa. Kosa hilo huwafanya wazidi kuendelea kuwa maskini siku zote za maisha yao. Ili kuwa tajiri ni lazima kutoa.

Kumbuka, tabia ya kuwekeza, kuweka akiba na kutoa ni moja ya tabia kubwa zinazo watenga matajiri na maskini. Matajiri wanajikuta wakiwa ni watu wakuzifanyia kazi tabia hizo na kuwafanya kuwa matajiri na maskini hubaki na umaskini wao kwa sababu ya kutokuzifanyia kazi tabia hizo. Chukua hatua ya kutenda ili kubadili maisha yako.

Bosi wa TPDC Asimamishwa Kazi

$
0
0
BODI ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) imemsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Dk James Mataragio.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya shirika hilo na wadau mbalimbali wa masuala ya mafuta na gesi, zimeeleza kuwa kusimamishwa kazi kunatokana na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu (CAG) ya mwaka jana iliyoeleza kuwa, TPDC ilikiuka taratibu za manunuzi ya umma kwa kuipa upendeleo kampuni ya Marekani kutafiti mafuta na gesi katika maeneo ya kaskazini na magharibi mwa Ziwa Tanganyika, Songosongo, Mandawa na Eyasi.

“Shirika kwa sasa si salama, kwani mkurugenzi amepewa barua kutoka kwa mwenyekiti wa bodi kusimamishwa kazi kuanzia jana (Jumatano) kutokana na ripoti ya ukaguzi,” alisema mmoja wa watoa taarifa.

Hata hivyo, mpaka jana jioni hakukuwa na taarifa rasmi kuhusu kusimamishwa kazi kwa mkurugenzi huyo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa alipoulizwa kuhusu hatua hiyo, alisema anafahamu suala la kusimamishwa kazi kwa Dk Mataragio, lakini akaongeza kuwa, maelezo zaidi kuhusu maamuzi hayo anayo Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Profesa Sufian Bukurura.

Hata hivyo, Mwenyekiti huyo alipotafutwa kwa simu kutoa taarifa rasmi za kusimamishwa kazi kwa mkurugenzi huyo, hakupatikana kwani mara zote simu yake ilisema inatumika.

Watanzania wengi wapo gerezani Afrika Kusini kwa ‘unga

$
0
0
WAZIRI wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga amesema Watanzania wengi wanashikiliwa katika magereza ya Afrika Kusini kwa makosa ya kujishughulisha na biashara ya dawa za kulevya.

Alisema hayo wakati akifafanua suala la Watanzania wanaoishi nje ya nchi, hasa vijana na kusema wamekuwa wakijishughulisha na uuzaji dawa za kulevya badala ya kuwa raia wema.

Aliwataka kuacha kujishughulisha na mambo yanayoweza kuwaweka kwenye wakati mbaya na kutii sheria za nchi waliko.

Alisema Watanzania wengi waliopo Afrika Kusini wanafanya kazi ya kusafirisha dawa za kulevya na wengine wanasubiri ‘kuzamia meli’ mjini Durban.

Alisema suala hilo ni moja ya mambo ambayo yamekuwa yakijadiliwa na Serikali ya Afrika Kusini ambapo Tanzania imejulishwa tatizo hilo na Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Afrika Kusini pamoja na Rais Jacob Zuma.

“Ni kweli lipo tatizo kubwa la Watanzania waliopo Afrika ya Kusini kujishughulisha na biashara ya dawa za kulevya. Serikali ya Afrika Kusini imetujulisha jambo hilo nasi tunalishughulikia kuiepusha nchi kuwa na uhusiano mbaya wa kidiplomasia na nchi nyingine.

Wasanii Wapenda Amani Waungana Kupinga Maandamano UKUTA Ya Chadema

$
0
0
WASANII mbalimbali wanaopenda amani wameungana kwa pamoja kupinga maandamano ya UKUTA yanayotarajiwa kufanyika Septemba Mosi, mwaka huu.

Akizungumza jana mbele ya Waandishi wa Habari, Mwenyekiti wa Wasanii hao wapenda amani, Steve Nyerere alisema hamna haja ya maandamano bali tunahaja ya kufanya kazi hususan kwa vijana.

"Vijana ndio muhimili mkubwa kulinda amani ya nchi,tusiwaze maandamano bali tuwaze je Akinamama na Watoto wanapata huduma hospitali"alihoji Steve Nyerere.

Kwa Upande wa Makamu Mwenyekiti wa Wasanii hao, Asha Baraka alisema wameamua kupaza sauti zao kwa niaba ya Wasanii wote wanaopenda amani.

Alisema Tanzania ni nchi ya Amani sio nchi ya vita hivyo wanapofanya shughuli za UKUTA shughuli zote za kijamii zitasimama.

Hatahivyo aliomba Septemba 1,  UKUTA wasimamishe maandamano hayo, pia watafute njia muafaka ya kuweza kuongea Vyama kwa Vyama na wakapata muafaka ili nchi iweze kwenda mbele.

Nafasi za Kazi Zilizotangazwa leo CVPeople Africa..Apply Here


Kimenuka...Mapigano Makali Yaendelea Kati ya Polisi na Majambazi Mkuranga Vikindu

$
0
0
Mapigano makali yanaendelea kati ya polisi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi eneo la Vikindu, wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani.

Timu ya Mwananchi iliyo eneo la tukio imeshuhudia magari ya polisi (defenda) zaidi ya 16 yakifika eneo la tukio huku polisi wakiwa wameshika silaha zao kwa umakini mkubwa.

Kadhalika, magari yanayokwenda maeneo ya Vianzi Mkurang, Malela, Pemba Mnazi, Mfuru zimefungwa kutokana na mapambano hayo.

Jaji Warioba na Cleopa Msuya wamjibu Kingunge Ngombale-Mwiru.

$
0
0
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, Kingunge Ngombale-Mwiru aliwataka Marais wastaafu na Mawaziri Wakuu wastaafu nchini kuingilia mvutano wa kisiasa unaoendelea sasa kuhusu Ukuta kutafuta muafaka kwa Rais Magufuli.

Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba akizungumza na gazeti hili jana kwa njia ya simu alisema viongozi wakuu wastaafu ambao ni marais na mawaziri wakuu wamekuwa wakimshauri Rais katika masuala mbalimbali.

“Kweli tuko kimya lakini ukimya huo usitafsiriwe kuwa hatumshauri Rais sisi kama viongozi wastaafu, lakini haifanyiki kwenye vyombo vya habari,” alisema Jaji Warioba.

Jaji Warioba alisema badala ya kumjibu Kingunge ni vyema kumuachia Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi awakutanishe viongozi wa vyama vya siasa kujadili hali hiyo kwa lengo la kupata muafaka.

Hata hivyo, alisema ni wajibu wa Watanzania wote kuhakikisha wanalinda hali ya amani nchini badala ya kuliona jambo hilo linamhusu Rais John Magufuli pekee au mtu mwingine yeyote. “Tumsaidie msajili katika hili, hili sio tatizo la mtu mmoja bali ni la nchi nzima tusimuachie Rais,” alisema Jaji Warioba.

Aidha, alisema jambo ambalo linafanywa na Msajili wa Vyama vya Siasa la kuandaa majadiliano ni jambo jema zaidi na kwamba yakifanyika mambo mengine yanaweza kuleta madhara kwa wananchi.

Jaji Mutungi hivi karibuni alipozungumza na vyombo vya habari aliwatoa hofu wananchi kuwa hakutakuwa na uvunjifu wa amani kutokana na sintofahamu inayoendelea nchini baina ya vyama vya siasa.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu mstaafu Cleopa Msuya alisema serikali imetoa mwongozo wake watu wauzingatie na siyo kufanyika mazungumzo.

Alisema viongozi wa vyama vya upinzani waliotangaza operesheni hiyo kama wana hoja za msingi waseme ili zipatiwe ufumbuzi, lakini siyo kuvunja miongozo iliyowekwa makusudi.

“Tukae tuzungumze na Rais tunazungumza nini? Kama una watoto wako umeweka miongozo wengine hawataki kufuata mnazungumza? Kama wana tatizo waseme kuna moja, mbili, tatu, sasa waache wapambane na dola,” alisema Msuya na kuongeza kuwa Rais Magufuli anatosha, aachwe afanye kazi zake kwa uhuru bila kuingiliwa na watu wengine.

Naye Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema ambaye pia alikuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa alipozungumza na gazeti hili jana alisema mazungumzo ni jambo zuri kuliko maandamano. Lowassa alisema ushauri wa Kingunge wa viongozi wastaafu kufanya mazungumzo na Rais Magufuli kwa lengo la kumshauri juu ya hali ya kisiasa inavyokwenda ni wa busara.

“Ushauri wa Mzee Kingunge ni wa busara sana na mimi naona viongozi wa zamani tukae tufanye mazungumzo na Rais kuliko kufanya maandamano,” alisema Lowassa.

SOURCE: Habarileo

‘CCM Inaongoza Uvamizi wa Viwanja Kinondoni’

$
0
0
MANISPAA ya Kinondoni imesema viwanja vya wazi vipatavyo 160 vimevamiwa na kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaongoza katika uvamizi huo kwa asilimia zaidi ya 70.

Akizungumza na waandishi wa habari   Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji na Mazingira wa Manispaa hiyo, Mustapha Muro, alisema itafanyika operesheni kubwa   kuyarudisha maeneo hayo kwa umma.

Muro alisema katika ripoti za manispaa hiyo, Chama cha Wananchi (CUF), nacho kimevamia kwa asilimia zipatazo 2.3 na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa asilimia moja.

“Viwanja vya wazi 160 (asilimia 80) ambavyo ni mali ya manispaa vimevamiwa ingawa wapo pia watu binafsi waliofanya hivyo lakini vyama vya siasa navyo vimo.

“Manispaa tumepanga kuvirejesha katika umiliki wa umma kuanzia leo (jana) tumeanza operesheni maalumu ambayo itakuwa endelevu ya kuyapitia maeneo yote na kuyatwaa,” alisema Muro.

Alisema manispaa hiyo itasimamia operesheni hiyo kwa mujibu wa sheria ikizingatiwa inaruhusiwa kusimamia ardhi yote.

“Kwa hiyo wataalamu wetu watapita na kuweka alama na muhusika atapewa notisi ya mwezi mmoja wa kujitetea kabla ya manispaa kulitwaa eneo husika,” alisema

Alisema  jambo hilo linatekelezwa kwa kushirikisha  wanasheria wa manispaa  kuhakikisha linafanyika kwa usahihi   na kwamba ni lazima maeneo hayo yote yarudi.

Kamati hiyo ilitembelea maeneo ya kata za Makuburi    na Makurumla ambako   uvamizi umefanyika.

“Katika eneo la Makuburi watu wamevamia eneo la soko na sasa limekuwa la makazi jambo ambalo si sahihi kwa mujibu wa sheria,” alisema.

Mohamed Paze ambaye ni mkazi wa eneo hilo tangu 1979, alisema eneo hilo lilivamiwa baada ya kuachwa kwa muda mrefu bila kuendelezwa.

Mfanyabiashara Ataka Kujirusha Daraja la Ubungo

$
0
0
Katibu wa Chama cha Wafanyabiasha za Mezani katika maeneo ya Stendi ya Mkoa, Ubungo jijini Dar, John Shayo amekusanya umati baada ya kupanda juu kabisa ya daraja jipya lililopo eneo hilo na kutaka kujirusha, akihitaji Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda afike hapo kwani hakutendewa haki.

Tukio hilo lililovuta hisia za wengi lilijiri kwenye Daraja la Ubungo ambapo katibu huyo alitaka afe kwa kuwa anadai hajatendewa haki na alitaka Makonda afike amwelezee shida zake katika suala zima la ufanyaji biashara ndipo aweze kushuka la sivyo angejirusha.

Kundi kubwa la watu lilikusanyika eneo hilo huku polisi na gari lao la zima moto wakitanda wakimshangaa akiwa anazungukazunguka akisema yeye ni Mtanzania anahitaji haki ndipo walimsubiria alipokuwa akimpa mkono ndugu yake kama ishara ya kumuaga wakamvuta na kufanikiwa kumshusha.

Baada ya kushushwa, aliwekwa chini ya ulinzi wa polisi kisha akapelekwa katika Kituo cha Polisi cha Ubungo ambapo wafanyabiashara wenzake  walidai kwamba alikuwa na mgogoro na mwenzake waliyekuwa wanafanya biashara pamoja. Hata hivyo, hadi mwandishi wetu anaondoka kituoni hapo, jamaa huyo alikuwa akitoa maelezo.

Stori/picha: Gladness Mallya/GPL

Mbwana Samatta Aipeleka Timu ya Genk Hatua Nyingine Ligi ya Europa League

$
0
0
Mtanzania mshambuliaji wa Kimataifa, Mbwana Ally Samatta amepata nafasi ya kucheza hatua ya makundi ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League.

Hii ni baada ya klabu yake ya KRC Genk ya Ubelgiji kupata ushindi wa jumla ya mabao 4-2 dhidi ya wapinzani wao Lokomotiva Zagreb ya Croatia.

Genk walipata ushindi wa 2-0 mechi iliyochezwa jana jioni.

Klabu hizo mbili zilitoka sare 2-2 mechi ya mkondo wa kwanza.

Samatta alifungia klabu yake bao la kwanza dakika ya pili naye mwenzake Leon Bailey akafunga la pili muda mfupi baada ya mapumziko.

UPDATE KUTOKA VIKINDU: Wamekamatwa jumla ya majambazi 14 na wengi wao ni askari wastaafu.

$
0
0
Inadaiwa wamekamatwa majambazi 14 na wengi wao ni askari wastaafu. Kiongozi wa wahalifu wao anadaiwa kuwa Kanali wa Jeshi mstaafu.

Apewa talaka baada ya kulitaja jina la msanii Chameleone wakati akifanya mapenzi

$
0
0
Mwanamke nchini Uganda amepewa talaka baada ya kulia jina la Chameleone wakati akishiriki mapenzi na mumewe

– Chameleone ameweka kisa hicho kwenye Instagram baada ya kuchapishwa na gazeti moja la Uganda

Mwanamke mmoja Uganda amepewa talaka baada ya kuliita jina la msanii msifika Jose Chameleone wakati wakishiriki mapenzi na mumewe.

Habari hizo zimeenea kote Uganda baada ya mume huyo kuapa kumfurusha mkewe alipomlia mwimbaji huyo wa kibao maarufu Valu Valu.

Chameleone alionekana kufurahishwa na tukio hilo kiasi cha kupiga picha za habari zenyewe kwenye gazeti moja la hapo.


“Mume amfukuza mke kwa kumite Chameleone wakati wakishiriki mapenzi,” msanii huyo aliandika kwenye maelezo ya picha hiyo.

Kisa hicho kinajuia siku chache tu baada ya mwimbaji huyo maarufu wa Uganda kushirikiana na kundi la Elani katika kolabo ya “My Darling”, wimbo unaoangazia mapenzi, changamoto na kutoelewana kunakowakumba wapenzi.


Makonda awafungukia walionukuu kauli yake vibaya

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amefafanua juu ya kauli yake aliyoitoa hivi karibuni ambayo imekuwa ikinukuliwa vibaya na vyombo vya habari ikiwemo gazeti la leo la Mwananchi.

Kwenye ukurasa wa tatu, gazeti hilo limeandika habari yenye kichwa kinachosomeka, “Makonda ataka wahalifu wagongwe, wapigwe.”

Akiongea na Clouds 360 ya Clouds FM, Makonda amesema kuwa kuna baadhi ya watu wanapenda kuwagombanisha wananchi na viongozi wao kutokana na kauli wanazozinukuu kutoka kwao.

“Unajua kuna baadhi ya wenzetu wana agenda zao tofauti na agenda ya kujenga taifa, watu ambao wangependa kuwatengenezea mazingira wananchi wasielewane na viongozi wao,” amesema Makonda.

“Kwa sababu ukiangalia hii stori ilivyoandikwa kuna kitu kimewekwa ambacho hakipo kabisa lakini kimewekwa kwa tafsiri ya kumsaidia mwenye kusudi la kufikisha ujumbe tofauti na ule uliotolewa,” ameongeza.

Aidha Makonda ameendelea kwa kufafanua kauli yake hiyo iliyonukuliwa vibaya kwa kudai kuwa, “unapokuwa msituni ni sawa na mapambano lazima upambane kwa kuwalinda polisi wako, majambazi siyo watu wazuri kutokana na tukio lililotokea la kuuawa kwa polisi wanne hivi karibuni.”

Waziri mkuu amwakilisha Rais Magufuli mkutano wa wakuu wa nchi

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasili Nairobi, Kenya kuhudhuria Mkutano wa Mkuu wa Sita wa Wakuu wa Nchi wa TICAD (TICAD VI) utakaofanyika Agosti 27 -28, mwaka huu.

Waziri Mkuu anahudhudia mkutano huo kwa niaba ya Rais, John Pombe Magufuli.

Leo asubuhi Waziri Mkuu amekutana na viongozi wakuu mbalimbali wa makampuni ya kibiashara kutoka Japan ambao wamekuja kuhudhuria mkutano huo

Dudubaya Amfundisha Mwanaye Kuvaa Condom

$
0
0
Msanii Godfrey Tumaini au Dudubaya ameonesha mfano jinsi ya kuwa baba bora, kwa kuzungumza na mtoto wake kuhusu maambukizi ya magonjwa ya zinaa, na jinsi ya kujikinga na magonjwa hayo kwa kutumia condom.

Akizungumza na Planet Bongo ya East Africa Radio, Dudubaya amesema huwa anazungumza na kijana wake kwa kuwa hataki apate magonjwa ya zinaa na kufa mapema kabla yake.

"Mwezi wa 12 mwaka jana ndiyo nilikuwa naye alikuwa amefunga shule kwa hiyo kujiandaa kwenda form one, nilichomwambia siku moja mpaka washkaji walicheka maskani, nikamwambia dogo sikiliza, najua sasa hivi we unajisikia, sasa kama unajisikia unajua kuna kitu kinaitwa condom!?

akaniambia yah, unajua kuitumia!? akasema hapana, nikamwambia unajua kuna magonjwa kama gono, kuna kaswende na UKIMWI, na sipendi utangulie wewe kufa mimi nikabaki, ni bora mimi nife wewe ndo uje kuwa mrithi wangu", alisema Dudubaya.

Dudubaya aliendelea kusema kuwa wazazi wengi sasa hivi hawazungumzi na watoto wao na hatimaye watoto wanaingia kwenye mambo yasiyofaa, na mwisho wazazi huwalaum na kuwachukulia hatua watoto, kwa makosa ambayo wameyasababisha wenyewe.

"Mtoto anapofikia kujisikia haina sababu ya kumfungia geti, na ndiyo maana unakuta kuna watoto wanapata maambukizi ya magonjwa kama UKIMWI, kumbe we mzazi hukuongea na mwanao,

mzazi unatakiwa uzungumze na mwanao umwambie hivi na hivi, kwa mfano kama mjini hapa watoto kibao wanaharibika na madawa ya kulevya, kwa sababu mzazi huzungumzi na mtoto", Alisema Dudubaya.

Mwanamke amkuta mumewe akishiriki ngono na mbwa wake

$
0
0
Mwanamke mmoja amepigwa na butwaa baada ya kumpata mumewe akishiriki ngono na mbwa wao nyumbani Spring Valley, Nairobi

–Inasemekana mwanamke huyo alikuwa amezuru mashambani kupeleka watoto ambapo alirudi nyumbani Nairobi bila kutarajiwa

Mwanamke mmoja alielezea kisa cha kushtua baada ya kumpata mumewe akishiriki ngono na mbwa nyumbani, Spring Valley, Nairobi.

Mwanamke huyo aliondoka nyumbani Jumamosi Agosti 20, kuelekea mashambani Gatanga kupeleka watoto wao.

Walikuwa wamekubaliana na mumewe kuwa angekaa wikendi na wazazi mashambani, hasa baada ya kuacha amemtayarishia chakula mwanamume huyo.

Hata hivyo, alirudi nyumbani ghafla baada ya kukumbuka alikuwa ameacha dawa za mmoja wa watoto wao.

Lakini baada ya kufika nyumbani alipigwa na butwaa baada ya kuingia ndani ya chumba chao cha kulala na kumpata mumewe akishiriki ngono na mbwa wao!

Baada ya kupatikana, mwanamume huyo alivaa nguo haraka na kuondoka nyumbani mara moja, bila kusema chochote!

Mwanamuziki Kiss Daniel Kupamba Uzinduzi wa Tamasha la 'Monte Carlo Classic' jijini Dar Kesho

$
0
0
Msanii maarufu kutoka Nigeria Anidugbe Oluwatobiloba Daniel almaarufu kama Kiss Daniel akionesha albamu yake kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kumaliza mkutano wa kutambulisha uwepo wake katika Tamasha linalozinduliwa jijini Dar es salaam siku ya kesho katika ukumbi wa Akemi ulipo katika jengo la Golden Jubilee, Posta jijini Dar es salaam.

MWANAMUZIKI KISS DANIEL KUPAMBA UZINDUZI WA TAMASHA LA ‘MONTE CARLO CLASSIC’ JIJINI DAR KESHO
Msanii maarufu kutoka Nigeria Anidugbe Oluwatobiloba Daniel almaarufu kama Kiss Daniel akiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja wake Louiza Williams wakati mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo katika hafla ya kumtambulisha msanii huyo ambae atapamba uzinduzi wa Tamasha la “Monte Carlo Classic” litakalofanyika kesho katika ukumbi wa Akemi ulipo katika jengo la Golden Jubilee, Posta jijini Dar es salaam.

Meneja Masoko wa benki ya Barclays Joe Bendera akipiga Selfie na Msanii maarufu kutoka Nigeria Anidugbe Oluwatobiloba Daniel almaarufu kama Kiss Daniel mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari katika hafla ya kumtambulisha msanii huyo atakayepamba uzinduzi wa Tamasha la “Monte Carlo Classic” litakalofanyika kesho katika ukumbi wa Akemi ulipo katika jengo la Golden Jubilee, Posta jijini Dar es salaam. Benki ya Barclays ni wadhamini rasmi wa Tamasha hilo ambalo limezinduliwa kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.

Mmoja wa washiriki katika uandaaji wa Tamasha la Monte Carlo Classic DeJurist Global kutoka Malaysia akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hafla ya kumtambulisha msanii kutoka Nigeria Kiss Daniel ambaye yupo nchini kwa ajili ya kupamba uzinduzi wa Tamasha hilo litakalofanyika kesho katika ukumbi wa Akemi ulipo katika jengo la Golden Jubilee, Posta jijini Dar es salaam. Pamoja na kulia ni Msanii kutoka Nigeria Kiss Daniel, Meneja masoko wa benki ya Barclays, Joe Bendera na Mkurugenzi wa Sta8up Vibes, waandaji wa Tamasha Sniper Montana. Benki ya Barclays ni wadhamini rasmi wa Tamasha hilo ambalo limezinduliwa kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.

Msanii maarufu kutoka Nigeria Anidugbe Oluwatobiloba Daniel almaarufu kama Kiss Daniel (katikati) akifurahia jambo na Meneja Masoko wa benki ya Barclays Joe Bendera (kulia) sambamba na Mkurugenzi wa Stra8up Vibes Sniper Mantana (kushoto) mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari wa kumtambulisha msanii huyo atakayepamba uzinduzi wa Tamasha jipya nchini la “Monte Carlo Classic” litakalofanyika kesho kwenye ukumbi wa Akemi uliopo Golden Jubilee Towers, Posta jijini Dar es salaam.


Mwanamuziki maarufu wa Nigeria Anidugbe Oluwatobiloba Daniel anayefahamika kwa jina la kisanii Kiss Daniel aliyetamba hasa kwa kibao chake cha ‘Woju’ kwenye anga za muziki,  ametua jijini Dar es Salaam kwa ajili ya uzinduzi wa Tamasha la Monte Carlo Classic lililoandaliwa na Str8up Vibes wakishirikiana na DeJurist Global kwa udhamini wa Benki ya Barclays Tanzania.

Mwimbaji huyo wa Nigeria aliyejizolea mashabiki wengi tangu alipoachia kibao chake cha ‘Woju’, ataongoza uzinduzi wa Tamasha hilo Jumamosi hii jijini Dar es Salaam katika Mgahawa wa Akemi uliopo kwenye jengo la Jubilee Towers, Mtaa wa Ohio.

Akizungumza mapema leo kwenye mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Str8up Vibes, Sniper Mantana alithibitisha mbele ya waandishi kwamba maandalizi ya Tamasha hilo yamekamilika na kuwasihi Watanzania kujitokeza kwa wingi ili kujumuika na msanii huyo maarufu.
Aliongeza kwamba kabla ya Tamasha hilo tiketi zitauzwa kwa shilingi 25,000 na itakapo timu usiku tiketi zitauzwa kwa shilingi 35,000.

Alisema Tamasha la "Monte Carlo Classic" limelenga kubadilishana uzoefu baina ya Watanzania hususani kwenye sekta ya burudani.

“Kwenye miji kama vile;-Monte Carlo, New York, Los Angeles (L.A), Paris watu maarufu hushiriki kwa kupamba matukio kama haya. Hii ni sawa na ambavyo sisi tumelenga kuliimarisha tamasha la Monte-Carlo Classic jijini Dar es Salaam, ambapo kwa usiku mmoja kila mtu anakuwa mtu wa hadhi ya juu, huku akisherehekea na mtu maarufu aliyeteuliwa na kwenye eneo lenye hadhi ambalo limeandaliwa na waandaaji,” alisema.

Kwa mujibu wa Meneja Masoko wa Benki ya Bacrays Tanzania, Joe Bendera, alisema benki hiyo imekuwa ikidhamini ligi kubwa ya soka ulimwenguni jambo ambalo limeifanya kuisogeza karibu na jamii. Tunayo furaha kuwa sehemu ya uzinduzi wa Tamasha kama hili kubwa jambo ambalo litatuwezesha kukutana na wageni waalikwa mbalimbali na wateja wetu.

"Tukio hili linatupa fursa ya kutoa elimu kuhusu matumizi ya kadi zetu na kuhamasisha matumizi yake sehemu mbalimbali kwenye mashine za mauzo maeneo mbalimbali nchini. Mwezi uliopita Benki ya Barclays ilitunukiwa cheti cha ubora cha Mtoaji wa Kadi Bora za Visa nchini Tanzania.

Pia katika kubeba fedha taslimu kuna kiwango maalumu hivyo tutapata fursa ya kuwahamasisha wateja wetu kutumia kadi zetu za Debit na Cretid kwenye tukio hili," alisema

Kwa upande wake msanii huyo alisema alishtuka alipopata mwaliko kutoka kwa Str8up Vibes na kumchague yeye kuwa mgeni rasmi kwenye tukio hilo, na kwa mara ya kwanza kuja hapa nchini kama msanii.

 “Nimefuarahi sana kualikwa kwenye tukio la Monte Carlo Classic hapa jijini Dar es Salaam, ninashukuru kwa nafasi hii na ninapenda kuwashukuru waandaji kwa kutambua umuhimu wangu.”
Msanii huyo aliongeza kwamba, amekuja nchini kufurahia na kujumuika na watu hadhi tofauti, wasanii wa muziki pamoja na mashabiki zake na kuwaomba wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kufika kwa wingi siku ya Jumamosi kwenye tukio hili.

Msanii huyo alizaliwa Mei Mosi, 1994 katika mji wa State, Kiss Daniel ni mwimbaji maarufu anayetamba na kibao chake cha Woju alichokiachia mwaka 2015 a kutamba kwenye vituo mbalimbali vya runinga na redio akimshirikisha Davido na Tiwa Savage.
Kwa hivi sasa amejiunga na lebo ya G-Worldwide Entertainment iliyomwezesha kurekodi nyimbo zake tatu; Woju, Mama na aliouachia hivi karibuni wa Jombo.
Mwisho
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images