Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live

Barakah Da Prince: Mr Blue anapotaka twende sasa tutafika

$
0
0
Series ya sinema ya Mr Blue na Barakah Da Prince inayomhusu Naj imeendelea, ni zamu ya hitmaker wa Siwezi kuongea.

Akiongea na 255 ya Clouds FM Alhamisi hii, Barakah da Prince amesema kuwa hajawahi kuongea kuhusu Blue kumpigia simu Naj na kwamba ni kitu kipya kwake.

“Namuona kabisa yule mwana anataka kukosa heshima, ananikosea heshima halafu anashindwa kurespond heshima ambayo mimi huwaga nampa. Kwahiyo anapotaka twende sasa tutafika huko anapotaka yeye,” amesema muimbaji huyo.

Kuna Kitu Ninacho Moyoni Mwangu Lakini.. – Wema Sepetu

$
0
0
Tangu malkia wa filamu nchini, Wema Sepetu aachane na mpenzi wake Idris Sutlan kuna mengi yamekuwa yakizungumzwa katika mitandao ya kijamii.

Muigizaji huyo hakuwahi kuzungumza sababu ya kuachana na mshindi huyo wa shindano la Big Brother Africa Hotshots 2014 hali ambayo imekuwa ikiibua maswali mengi kwa mashabiki wake.

Alhamisi hii Wema amewataka mashabiki wake katika mitandao ya kijamii kukaa mkao wa kula kwa ajili ya kuyasikia mengi ambayo yanaukabili moyo wake.

“Kuna muda mtu unaweza ukakaa na ukasema na moyo wako, Ila moyo mara nyingi huwa unazidi nguvu nyingine zozote. Kuna kitu kiukweli ninacho kwa moyo wangu,” aliandika mwigizaji huyo kupitia ukurasa wa instagram.

Aliongeza, “Lakini siwezi kusema leo wala kesho, but ipo siku isiyo na jina wala tarehe nitakisema tu, maana mnanijua kukalfisha nafsi huwa sipendi, but all in all tuseme Inshallah,”

Wiki iliyopita aliyekuwa mpenzi wake, Idris Sultan aliamua kufuta akaunti yake ya instagram yenye followers zaidi ya milioni 1 baada ya kushindwa kuvumilia yale yanayoendelea katika mitandao ya kijamii.

Waondoeni Machinga Kwenye Barabara za DART; Waziri

$
0
0
Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene ameuagiza uongozi wa mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha wanawaondoa wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama wamachinga wanaofanya shughuli za kibiashara kwenye maeneo ya barabara ya mabasi yaendayo haraka.

Sehemu ya Barabara za mabasi yaendayo haraka
Mhe. Simbachawene ametoa agizo hilo leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kupokea ripoti ya tathmini ya awali ya utekelezaji wa mradi wa mabasi yaendayo haraka kutoka kwa kamati ya kudumu ya bunge ya tawala za mikoa na serikali za mitaa, baada ya wabunge ambao ni wajumbe wa kamati hiyo kutaja uwepo wa wafanyabiashara hao kama changamoto kubwa kwa mradi huo.

Naye Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Mwanne Nchemba amesema maboresho yaliyopendekezwa na kamati hiyo yafanyiwe kazi kwa muda muafaka na kuleta manufaa kwa watumiaji.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa DART Bwana Ronald Rwakatare amesema kwa sasa wanajikita katika awamu ya pili ya usafiri huo kuelekea Mbagala ambapo utekelezaji wake utaanza mapema mwakani.

Cheyo Awataka Watanzania Waungane Kuyakataa Maandamano ya Chadema

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha UDP John Cheyo amewataka Watanzania kupaza sauti na kukataa maandamano ya Septemba Mosi mwaka huu ambayo yameandaliwa na Chama cha Demokrasia (CHADEMA).

Cheyo ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu msimamo wake juu ya maandamano hayo.

“Watanzania wenzangu jambo la kuwaacha watoto wetu kwenda kupambana na Polisi si jambo zuri, wote tupaze sauti zetu na kusema hapana kwa maandamano ya Septemba Mosi,” alisisitiza Cheyo.

Alisema kuwa, ziko njia mbalimbali ambazo Chadema wanaweza kuzitumia kutatua migogoro, kama vile meza ya mazungumzo na kuachana na maandamano ambayo yanachochea vurugu na hata kutishia amani ya nchi.

Aliongeza kuwa Jeshi la Polisi linapotoa katazo la maandamano ni lazima utii uwepo, kwani Polisi wapo kwa mujibu wa Sheria na Katiba. Ikiwa Chama hicho hakikuridhika na katazo hilo basi wanatakiwa kuonana na Waziri anayehusika na Jeshi la Polisi.

Akifafanua zaidi alisema kuwa Rais Magufuli amekuwa akichukua hatua za makusudi za kutatua matatizo mbalimbali kama vile kupambana na ufisadi, ambapo viongozi wengi wa Serikali wamesimamishwa kazi au kufukuzwa kutokana na kujihusisha na masuala ya rushwa.

Mwenyekiti huyo wa UDP amewataka watanzania kumuunga mkono Mhe. Rais Magufuli ili aweze kutimiza ndoto zake na yale ambayo ameyaahidi kwa ajili ya nchi ya Tanzania.

Aidha Cheyo aliwasifu viongozi wa Dini ambao walikaa na Viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na kukubali kurudi bungeni bila pingamizi lolote.

Amewataka viongozi hao wa dini kuendelea kuzungumzia suala la amani kwa Watanzania na Viongozi wa kiasa ili kudumisha amani ya nchi.

Hali Ngumu ya Maisha, Afisa wa Polisi Ajiua Kwa Kujipiga Risasi Jomo Kenyatta (JKIA)

$
0
0
Afisa wa polisi Caudencia Wausi alimejiua kwa kujipiga risasi kichwani katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta (JKIA) muda mfupi baada ya kuchapisha ujumbe wa kuashiria kuwa na mahangaiko maishani.

Koplo Caudencia Wausi alitumia bastola yake aina ya Jericho kujifyatulia risasi kichwani ndani ya choo dakika 13 tu baada ya kuchapisha ujumbe katika mtandao wake wa Facebook.

"Maisha ni magumu unapoishi katika ulimwengu ambapo kila mtu anapanga kukufanyia maovu.. na utafanya nini wakati ambapo huwezi kuvumilia au hauna uwezo wa nguvu za kuwatia nguvu wapendwa wachache katika maisha yako.!? hauna lingine la kufanya ila... kwa hivi nisadie Mungu "aliandika kwenye Facebook.

Kwa mujibu wa mkubwa wake, Bi Wausi alikuwa amerudi kazini kutoka mapumzikoni kabla ya kujiua baada ya kujifungia chooni, JKIA.

Inadaiwa alijifungua mkanda wake wa polisi na kuuacha katika chumba cha Control Room pamoja na fimbo yake kabla ya kujifungia chooni.

"Tulisikia tu mlio wa risasi na baadaye tukampata juu ya choo huku bastola yake ikiwa mkononi, alikuwa tayari ameaga dunia "alisema kamanda wa polisi katika uwanja wa ndege Rono Bunei.

Bwana Bunei alisema kisa hiki kimeshtua wenzake kwasababu afisa huyo hakuwa na dalili za kusongwa na mawazo.

" Alikuwa anapiga gumzo na wenzake asubuhi na nilimuona mwenye furaha, hakuonyesha dalili zozote za kuwa na mahangaiko "alisema Bw Bunei na kuongeza kuwa uchunguzi umeanza kubaini kilichosababisha afisa huyo kujiua.

DC wa Morogoro amefuta vibali vyote vya mikusanyiko isiyo ya lazima

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Morogoro Bi.Regina Chonjo ametangaza hali ya hatari katika wilaya hiyo baada ya kupokea tarifa za kiintelijensia za kuwepo matukio ya uhalifu yanayoshabihiyana na vitendo vya ugaidi katika maeneo tofauti ya wilaya hiyo na hivyo kufuta vibali vyote vya mikusanyiko isiyo ya lazima hadi itakapo tangazwa hali ya amani.

Mkuu wa wilaya Bi.Chonjo ametoa tarifa hiyo wakati wa wito wa dharura kwa waandishi wa habari ambapo amewataka wananchi wote wa wilaya ya Morogoro kutoa tarifa katika vyombo vya dola wanapoona watu wasiowafahamu na matukio yanayoashiria uvunjifu wa amani.

Aidha amewataka wamiliki wa vyumba za kulala wageni na kumbi za starehe kuwa makini na wageni wanaoingia na kutoka huku akiwataka wenyeviti wa vjiji,mitaa pamoja na watendaji wote kufanya jitihada za kuwatambua wageni wote walioko katika maeneo yao.

Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa wilaya Morogoro wameomba Jeshi la Polisi kuimarisha ulinzi katika kituo cha mabasi cha Msamvu pamoja na maeneo ya sokoni kwani ndiyo maeneo yenye mikusanyiko ambayo haiwezi kuzuiliwa.

Gharama ya Video ya Saka Hela ya Nay ni Sawa na Passo 7 Mpya!

$
0
0
Baada ya kukaa kimya bila kutaja kiasi cha fedha alichotumia kushoot video yake ya ‘Saka Hela’ Nay Wa Mitego amefunguka rasmi kwa mara ya kwanza.

Rapper huyo amekiambia kipindi cha ‘Ngaz kwa Ngaz’ kinachoruka kupitia EATV kuwa ametumia kiasi cha $25,000 kushoot video yake hiyo ambazo kwa hela za kibongo ni zaidi ya shilingi milioni 50. Kiasi hicho cha fedha kinaweza kununua gari aina ya Passo mpya kutoka show room, saba na chenji inabaki!

Mpaka sasa wimbo huo una zaidi ya miezi mitatu tangu alipouachia mwezi Mei mwaka huu kwa kushtukiza na umefanikiwa kutazamwa kwa zaidi ya mara laki nne kwenye mtandao wa Youtube.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya Agosti 27

$
0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya Agosti 27

KIMENUKA..Kauli ya Paul Makonda ya Kutaka Polisi Iwapige watu Wakiwakuta Msituni Yasababishwa Aitwe na Tume za Haki za Binadamu

$
0
0
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imesikitishwa na matamshi ya Mhe. Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam yanayokiuka misingi ya utawala bora aliyoyatoa tarehe 25 Agosti, 2016 wakati wa kuaga miili ya askari Polisi watatu waliouawa Mbande, Mkoani Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Bahame Tom Nyanduga, leo (Agosti 26, 2016) Mhe. Makonda ametumiwa barua ya wito inayomtaka afike makao makuu ya Tume mtaa wa Luthuli, tarehe 30 Agosti, 2016 ili kujadili kile Tume ilichokiona kuwa ni kejeli kwa Tume pamoja na jumuiya yote ya watetezi wa haki za binadamu.

Aidha, Tume imeona kuwa maagizo aliyoyatoa Mkuu huyo wa Mkoa kwa Jeshi la Polisi hayana msingi wa kisheria na hayako ndani ya mamlaka ya Mkuu wa Mkoa.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 6(1)(f) na (i) pia Kifungu cha 27(1) na (2) (a) vya Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Sura Na. 391 ya Sheria za Tanzania 2002, THBUB ina mamlaka ya kuchunguza mwenendo wa mtu au taasisi yoyote kuhusiana na utendaji wa kazi zake zinapokiuka mipaka ya madaraka yake, ili kuchukua hatua za kurekebisha ukiukwaji huo.

Imetolewa na:

(SIGNED)
Idara ya Elimu kwa Umma na Mafunzo

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Agosti 26, 2016

Serikali yaagiza Mabasi Mapya 165 ya Mwendokasi

$
0
0
Serikali imeanza mchakato wa kuagiza mabasi mapya 165 ya mwendokasi yatakayotoa huduma za usafiri kwa wakazi Dar es Salaam kwenye maeneo yasiyo na huduma hiyo.

Tayari imeshatangaza zabuni ya kununua mabasi hayo na mwezi Desemba, mwaka huu itasaini mkataba na mzabuni.

Mtendaji Mkuu wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi (Dart), Ronald Rwakatare amewaeleza wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa waliotembelea mradi huo kuwa wanatarajia mabasi hayo yataanza kazi Aprili mwakani.

“Mabasi haya yatahudumia maeneo ya Morocco, Tegeta, Masaki, Makumbusho na mengine yasiyofikiwa, wakati tukiendelea na ujenzi wa awamu ya pili ya mradi huo,” amesema.

Waliokaa Kituo Kimoja Miaka Mitano TRA Wahamishwe-Waziri

$
0
0
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango ameagiza kuhamishwa kwa watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) sehemu mbalimbali nchini ambao wameshakaa kwenye kituo kimoja kwa zaidi ya miaka mitano.

Alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na watumishi wa TRA wa Mkoa wa Kigoma mjini hapa jana na kuelezea alivyokasirishwa na tuhuma za rushwa zinazotajwa kuwafanya wasafirishaji wa shehena kuvusha bidhaa zao bila kulipa kodi katika forodha ya Manyovu, wilaya ya Buhigwe iliyopo katika mpaka wa Tanzania na Burundi.

Kutokana na hilo, ameagiza watumishi wote kituo hicho wahamishwe, akisema taswira mbaya inayoonekana kwa watumishi wa TRA inawafanya wafanyabiashara kutokuwa tayari kulipa kodi kwa hiari na kuipunguzia serikali uwezo wa kukusanya mapato, hivyo kukwamisha mipango ya serikali katika kuwahudumia wananchi.

Alisema anazo taarifa za vitendo vya rushwa vya watumishi hao, jeuri, ulevi na utoro kazini kwa kila mtu na jina lake na kwamba kuhamishwa huko ni hatua ya awali ya kujenga upya taswira nzuri ya TRA.

Aidha, waziri huyo ameitaka mamlaka hiyo kukusanya kodi kila penye fursa ya kuwepo kwa mapato na kwamba wasiogope kuingia gharama katika kusimamia hilo ili mradi wahakikishe malengo wanayoweka ya ukusanyaji yanafikiwa.

Awali, Meneja wa TRA Mkoa wa Kigoma, Thadeo Kaliza alisema mikakati ya ukusanyaji mapato iliyowekwa na maofisa wake imeiwezesha mamlaka hiyo kuongeza mapato kwa asilimia 17 kwa karibu miaka mitatu sasa.

Hata hivyo, alisema wigo finyu wa kodi, uchache wa watumishi na baadhi ya wilaya kutokuwa na ofisi kunakwaza jitihada za ukusanyaji kodi na kwamba mamlaka hiyo inazifanyia kazi changamoto hizo ili kuongeza maradufu ukusanyaji mapato.

Mufti: Bakwata Haitishwi na Maneno Kuhusu Paul Makonda

$
0
0
MUFTI wa Tanzania, Shehe Mkuu Abubakar Zubery (pichani), amesema Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) halitishwi na maneno yanayoendelea mitandaoni kuhusu kujengewa jengo katika Makao Makuu na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye ni Mkristo.

Mufti alisema kumekuwa na maneno mengi, yanayozungumzwa katika mitandao ya kijamii baada ya Makonda kusema atajenga jengo hilo katika makao makuu ya Bakwata, Kinondoni jijini humo, huko wengi wakisema kwa nini baraza hilo limekubali kujengewa na mtu ambaye sio Muislamu.

Alitoa kauli hiyo jana wakati Mkuu wa Mkoa huyo, akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo hilo ambalo litatumia Sh bilioni tano hadi kukamilika kwake.

Mufti Zubery alisema maneno hayo, hayawasumbui na wapo Wakristo wengi waliowahi kuchangia maendeleo kwa Waislamu, lakini hayakutokea maneno kama yanayotokea sasa.

“Kwa nini Rais wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa alipotupa Chuo Kikuu hamkusema? Wapo wadau wengi tu Wakristo walitoa… leo Makonda katoa maneno yamekuwa mengi.

Acheni jamani, mbona hayo ni maneno ya husda na choyo, Waislamu wametoa na sasa Wakristo. Hata Mtume amewahi kupokea misaada kama hiyo,” alisema Mufti.

Kwa upande wake, Makonda alisema hashangazwi na maneno yanayoendelea, kwani Watanzania wamekuwa wakibeza kila jambo zuri linalofanywa na viongozi. Alisema jengo hilo linatarajiwa kujengwa kwa udhamini wa Kampuni ya GSM Foundation, ambao walikubali kujenga kwa gharama zao mpaka kukamilika.

“Wengi waliuliza fedha nitatoa wapi, lakini wanasahau mimi ni mtu wa watu, nimezungumza na wadau wangu, wamekubali kujenga jengo hilo ambalo nimewataka wajenge kwa muda wa miezi kumi na nne,” alifafanua Makonda na kuwataka viongozi wa serikali kutoa kipaumbele kwa viongozi wa dini wanaotaka kupata huduma katika ofisi zao kwani ni watu muhimu na wanapaswa kuwa mbele wanapohitaji huduma.

Jose Mourinho: Ni Vigumu Sana Bastian Kupata Nafasi

$
0
0
Kocha wa Manchester United Jose Mourinho alipo kuwa akiongea na waandishi amesema kuwa hafiriki na ni vigumu sana Bastian kupata nafasi ya kucheza msimu huu, sijasema haiwezekani , nimesema ni vigumu sana.

Kama tatizo lolote litatokea au nafasi , nina vijana katika Academy, nitafurahi kuwapa nafasi ya wao kuendelea.

Wanyama Waliowahi Kushinda Nyadhifa Uchaguzini

$
0
0
Mbwa kwa jina Duke amechaguliwa kwa mara ya tatu kuwa meya wa mji wa Cormorant jimbo la Minnesota, tunaangazia wanyama wengine ambao wamewahi kuchaguliwa kushikilia nyadhifa mbalimbali au kufanya kazi nyingine za binadamu.
Mbwa achaguliwa tena kuwa meya Minnesota, Marekani

1. Mbwa waliowahi kuchaguliwa kuwa mameya
Kuna Junior Cochran, mbwa mweusi aina ya Labrador, aliyechaguliwa kuwa meya mji wa Rabbit Hash, Kentucky, mwaka 2004.

Na hatuwezi kumsahau Bosco mbwa aliyehudumu kama meya wa Sunol, California, kuanzia 1981 hadi 1994.
Hata kuna sanamu ya ukumbusho wake.

Sanamu ya mbwa aliyejulikana kama Bosco

2, Paka waliochaguliwa kuwa mameya
Paka kwa jina Stubbs alichaguliwa meya wa Talkeetna, Alaska, mwaka 1997.
Kuna hata akaunti ya Twitter yenye jina lake. Kwenye maelezo imeandikwa: "Mimi ni paka. Nilichaguliwa Meya wa Alaska. Karibuni, nitakuwa rais."

Paka kwa jina Stubbs

3. Kifaru 'taka' aliyechaguliwa kuongoza Sao Paulo
Mwaka 1959, kifaru wa umri wa miaka mitano kwa jina Cacareco alichaguliwa meya wa mji wa Sao Paulo kwa kura nyingi sana.

Cacareco, jina ambalo maana yake ni "taka" kwa Kireno, aliandikishwa kwenye kura kama hatua ya kulalamikia ufisadi miongoni mwa wanasiasa.
Hakuchukua mamlaka hata hivyo kwani uchaguzi ulirudiwa.

4. Mbuzi kiongozi wa New Zealand
Iwapo bado umeshangaa, tulia. Eneo la Whangamomona nchini New Zealand, mbuzi kwa jina Billy Gumboot mwaka 1999 alichaguliwa kuwa rais.

Alikuwa mnyama wa kwanza kuchaguliwa katika wilaya hiyo lakini hakuwa wa mwisho, baada yake kuondoka madarakani, mrithi wake alikuwa mbwa aina ya Poodle aliyepewa jina Tai.
Kwa sasa eneo hilo linaongozwa na rais wa kwanza mwanamke, Vicki Pratt.

5. Sokwe wa Rio de Janeiro
Sokwe kwa jina Tiao alipata kura nyingi, ingawa hazikutosha kabisa kumfanya meya wa mji wa Rio de Janeiro. Kauli mbiu yake ilikuwa: "Mpigie kura tumbili - upate tumbili."
Lakini alipata sanamu.

Sanamu ya Tiao
6. Penguini brigadia
Penguini kwa jina Nils Olav alipewa hata cheo cha Brigadia katika jeshi la Norway, na hata akakubaliwa kutekeleza majukumu rasmi, mfano kukagua gwaride.

Hauhitaji Media PlayerPata usaidizi kuhusu Media PlayerBonyeza 'Enter' kuendelea au kurejea mwanzoni
Penguini akikagua gwaride Norway

7. Paka kiongozi wa chama cha kisiasa Uingereza
Paka kwa jina Mandu, kutoka Uingereza, alihudumu kama kiongozi mwenza wa chama cha Official Monster Raving Loony Party kuanzia 1999 hadi 2002.
Ndiye paka pekee aliyewahi kuongoza chama cha kisiasa.

Tovuti ya chama hicho inasema: "Kilikuwa kinyang'anyiro kikali kati ya Howling 'Laud' Hope na
Paka Mandu.

"Walikaribiana sana kwa kura. Wote walipata kura 112 kila mmoja na ikaamuliwa washikilie wadhifa huo kwa pamoja."

Thierry Henry Kuwa Kocha Msaidizi wa Timu ya Taifa ya Ubelgiji Kuungana na Roberto Martinez

$
0
0
Kocha mpya wa timu ya taifa ya Ubelgiji Roberto Martinez amesema mchezaji wa zamani wa klabu za Arsenal na Barcelona, Thierry, ambaye aling’aa sana wakati akichezea timu ya taifa ya Ufaransa, atakuwa mmoja wa wasaidizi wake.

Henry alikuwa mmoja wa wakufunzi wa timu ya vijana Arsenal lakini akajiuzulu Julai baada ya meneja Arsene Wenger kumwambia kwamba hawezi kufanya kazi hiyo akiwa bado anaendelea kuwa mchanganuzi wa soka kwenye runinga.

Wakati wa Euro 2016 Henry alikuwa akifanya kazi ya kuchambua soka katika vituo vya Sky Sports na pia alifanya kazi na BBC Sport.

Thierry Henry alikuwa kwenye kikosi cha Ufaransa kilichoshinda Kombe la Dunia mwaka 1998 nyumbani.

Kuna Nini Kati ya Orijino Komedi na Mpoki?

$
0
0
Kumekuwa na sintofaham kwa mashabiki wa kundi la vichekesho la original comedy la hapa nchini linaloundwa na vijana sita akiwemo Mpoki, Masanja, Joti, Mark Regan kipara na wengineo kwa kuwataja wachache kwamba huenda hilo kundi limevunjika na pengine kuna beef kati ya kutokana na mfululizo wa matukio ya hivi karibu.

1. Kutokutoa kazi mpya kwa muda mrefu
Kubwa ni ukimya wa hili kundi wa kutoa kazi mpya. Wamekuwa kimya sana hawa wasanii kwenye kutoa kazi mpya kupelekea watu kujiuliza pengine limekufa.

2. Kila mtu anafanya kazi yake
Kwa sasa kila mtu anafanya kazi yake kwa Mpoki yeye ni muajiriwa kituo cha radio cha E fm. Masanja amejiajiri kwenye miradi kadhaa ikiwemo ule aliofungua muda si mrefu wa uuzaji mgahawa.

3. Kutokushirikiana kwenye shughuli za kijamii
Kwa sasa baadhi ya hawa wasanii wamekuwa hawahudhurii kwenye baadhi ya shughuli za kijamii ikiwemo harusi na sherehe. Mfano hivi karibu mmoja kati ya hawa wasanii Masanja alikuwa anaoa. Wengi walihudhuria lakini Mpoki hakuonekana kwenye shamrashamra za harusi hiyo kuweza kutia hofu kwa mashabiki zao.

Je kundi limekufa?

Wabunge CUF Waunga Mkono UKUTA

$
0
0
WABUNGE wa Chama Cha Wananchi (CUF), wametangaza kuunga mkono maandamano yaliyoitishwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), chini ya Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania (Ukuta), anaaandika Shabani Matutu.

Riziki Shari Mngwali, Mwenyekiti wa wabunge wa CUF amewambia wanahabari leo kuwa, upotoshaji kwamba wabunge wa chama chake hawaungi mkono maandamano hayo yanayotarajiwa kufanyika Septemba Mosi unapaswa kupuuzwa.

“Upotoshaji ambao umekuwa ukihusisha wabunge na chama kwa ujumla kwamba, hatupo tayari kushiriki katika maandamano hayo ya kupinga udikteta au hatuyaungi mkono ni taarifa zisizo na ukweli,” amesema.
Mngwali ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, amesema zaidi kuwa;

“tamko lilitolewa na Chadema ambao ni washirika wetu katika Ukawa, hivyo sisi tunaunga mkono mapambano yao na mtindo watakaotumia.
CUF tutakuja na mtindo wetu pia baada ya kufanikiwa kuziba nafasi za uongozi wa juu.”
Alisema kwamba, iwapo Chadema watawaomba CUF kushiriki kwenye shughuli zingine za Ukuta zinazoendelea watakuwa tayari kushiriki.

Mbarara Maharagande, mmoja wa maofisa wa CUF Makao Makuu, aliyekuwa ameongozana na kiongozi huyo amesema;

“Ukawa tumekuwa tukishirikiana katika mambo mengi ya msingi, hili la Ukuta tunaliunga mkono ila haibadilishi ukweli kuwa yale ni maazimio ya Kamati Kuu ya Chadema na si Ukawa.”

Amesema wanaopotosha kuwa CUF haiungi mkono Ukuta wanashindwa kuelewa kuwa, operesheni Ukuta ni maazimio ya Chadema ambayo pia yanaungwa mkono na vyama washirika wa Ukawa.

Viongozi Mbalimbali wa Chadema Waendelea Kutiwa Mbaroni Kwa Uchochezi

$
0
0
Zikiwa zimesalia siku nne kabla ya maandamano yanayodaiwa yatafanywa na Chadema, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amekuwa kiongozi wa 26 wa chama hicho kukamatwa na polisi kwa tuhuma za uchochezi ndani ya kipindi kifupi.

Kukamatwa kwa viongozi hao kunatokana na kauli zao zinazosisitiza kufanyika kwa maandamano yaliyopewa jina la Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta), yaliyopangwa kufanyika nchi nzima Septemba Mosi.

Hata hivyo, Serikali kupitia Jeshi la Polisi imezuia maandamano hayo na mikusanyiko yoyote ya kisiasa hadi mwaka 2020 kwa lengo la kuipa nafasi Serikali iliyopo madarakani kuwaletea wananchi maendeleo.

Baadhi ya viongozi wa Chadema waliokamatwa na kuhojiwa mpaka sasa ni Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu Visiwani, Salum Mwalimu, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ambaye kesi yake iko mahakamani.

Lissu alikamatwa Agosti 3, mkoani Singida baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Ikungi uliopo jimboni kwake kwa tuhuma za uchochezi.

Agosti Mosi, Mbowe alijisalimisha Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam na kuhojiwa kwa saa tatu. Kiongozi huyo aliitwa kwa mahojiano maalumu kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kauli za chama hicho kukinzana na agizo la Rais John Magufuli la kuzuia shughuli zozote za kisiasa ikiwapo mikutano kufanyika nchini.

Lema alikamatwa juzi alfajiri nyumbani kwake Njiro kwa Msola na makachero wa polisi kwa tuhuma za uchochezi ikiwa ni siku moja tangu kuachiwa kwa dhamana Diwani wa Chadema wa Kata ya Sombetini, Ally Benanga aliyefunguliwa mashtaka ya uchochezi mahakamani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo jana alithibitisha kukamatwa kwa Lema na kueleza kuwa uchunguzi unaendelea wa tuhuma za kutoa lugha za uchochezi mitandaoni.

Alisema mbunge huyo alitoa kauli za uchochezi na kuzisambaza kwenye mitandao, mapema wiki hii.

Polisi walisema ujumbe wa Lema kwenye mtandao ulisisitiza wito wa kufanyika mikutano na maandamano ya Ukuta, kwamba Mkoa wa Arusha umejiandaa kwa lolote na yeye atakuwa mstari wa mbele.

Meya wa jiji la Arusha, Calist Lazaro alithibitisha kukamatwa kwa Lema na kueleza kuwa bado walikuwa hawajajua tuhuma zake.

“Ni kweli mbunge anashikiliwa na tunaendelea kuhangaika apate dhamana leo (jana), ama afikishwe mahakamani,” alisema.

Salum Mwalimu na wenzake 17 watiwa mbaroni
Wakati Lema anakamatwa Arusha, Naibu Katibu Mkuu Visiwani, Salum Mwalimu na wenzake 17 walikamatwa wakati wakijiandaa kufanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mwandoya wilayani Meatu Mkoa wa Simiyu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Onesmo Lyanga alisema kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 25, saa 10 jioni katika kijiji hicho.

Lyanga alisema watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa wanajiandaa kufanya mikutano ya hadhara yenye lengo la uchochezi.

Alisema baada ya kupata taarifa kutoka katika vyanzo vyao, walifika eneo la tukio na kuwakamata kwa kuwa hata kibali cha kufanya mkutano hawakuwa nacho.

Jana, Mwalimu na wenzake walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Bariadi na kusomewa mashtaka ya kuwashawishi wananchi kufanya vitendo viovu na uchochezi.

 Viongozi hao walinyimwa dhamana na kurudishwa rumande hadi Agosti 30.

Agosti 23, Diwani wa Chadema, Kata ya Sombetini, Ally Bananga (40), alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha kujibu tuhuma za kuhamasisha uchochezi.

Akisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mfawidhi Augustino Rwezire, diwani huyo alidaiwa kuhamasisha wananchi kufanya maandamano yasiyo halali, Septemba Mosi.

Diwani huyo alifikishwa mahakamani hapo Agosti 23, ambapo Wakili wa Serikali Charles Kagirwa, alidai alitenda kosa hilo Agosti 13, wilayani Karatu Mkoa wa Arusha.

Pia, alisema kuwa siku ya tukio Bananga akiwahutubia wananchi katika mkutano wa wazi uliofanyika eneo la Hosteli ya Karatu, aliwahamasisha wananchi hao washiriki katika kusanyiko lisilo halali Septemba Mosi.

Agosti 25, viongozi wengine wanne wa Chadema Jimbo la Kigoma Mjini, walikamatwa na polisi wakidaiwa kujihusisha na vitendo vya uchochezi.

Waliokamatwa ni mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Kigoma, Ally Kisala, Katibu wa Baraza la Vijana Chadema Mkoa (Bavicha), Omary Gindi, Katibu wa chama jimbo la Kigoma mjini, Frank Ruhasha na Mwenyekiti wa mtaa wa sokoni katika Kata ya Katubuka, Moses Bilantanye.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma, Kamishna Msaidizi wa Polisi (DCP), Ferdinand Mtui alikiri viongozi hao wanne kushikiliwa kituoni hapo kwa muda lakini walipata dhamana, hivyo kuruhusiwa kuondoka na kutakiwa kuripoti kituoni hapo jana.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Kigoma, Shaaban Madede aliwaomba Polisi kwamba chama hicho kimejipanga kuandamana kwa amani na kufanya mikutano kila pembe ya mkoa, lengo ikiwa ni kufikisha ujumbe kwa wananchi juu ya kilio chao dhidi ya Serikali kukandamiza demokrasia.

Wabunge CUF  Waunga Mkono UKUTA
Wakati wabunge wa Chadema wakikamatwa, wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF), wamesema wanaunga mkono Ukuta, kwa sababu imelenga kupambana na uvunjaji wa demokrasia unaodaiwa kufanywa na Serikali ya Awamu ya Tano.

Msimamo huo ulitolewa jana na Mwenyekiti wa Wabunge wa CUF, Riziki Mngwali alipozungumza na wanahabari kufuatia taarifa zilizosambaa kuwa wabunge hao wanapinga Ukuta.

Riziki ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani, alisema wabunge wa chama hicho hawana tatizo na Ukuta na wanaunga mkono, hivyo tofauti na propaganda zinazoenezwa kuwa wanaupinga.

“Chadema ni washirika wetu kwenye Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), hivyo hatuna sababu ya kutowaunga mkono.

 “Tunachosubiria ni taratibu za uongozi wa juu kukamilika kisha watupe mwongozo nini cha kufanya kwenye Ukuta. Lakini wabunge tupo pamoja na operesheni hii, hatuipingi kwa sababu ina lengo ya kudai haki na demokrasia inayominywa,” alisema Riziki.

Lowassa na Magufuli wakutana Uso Kwa Uso Jubilei ya ndoa ya Mkapa

$
0
0
Hafla ya Jubilei hiyo imefanyika nyakati za mchana katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa uliopo kando ya kanisa la Mtakatifu Petro-Oysterbay na imetanguliwa na Misa ya shukrani iliyofanyika katika kanisa hilo majira ya asubuhi.

Jubilei hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Awamu ya Sita wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume, Mke wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere, Mawaziri Wakuu Wastaafu Mhe. Cleopa Msuya, Dkt. Salim Ahmed Salim, Jaji Joseph Warioba na Mhe. Edward Lowassa.

Misa Takatifu ya Shukrani imeongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha Mhashamu Askofu Josephat Lebulu na kuhudhuriwa na Maaskofu na Maaskofu Wakuu saba akiwemo Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa Misa Takatifu Rais Magufuli amempongeza Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa kwa kutimiza miaka 50 ya ndoa na ameeleza kuwa ndoa hiyo iliyowaunganisha wanandoa wanaotoka katika madhehebu tofauti ya Kikristo imetoa fundisho kubwa kuwa binadamu wanapaswa kuwa wamoja hata kama wana tofauti mbalimbali zikiwemo za kimadhehebu ya dini, siasa na kanda.

Rais Magufuli amesema miaka 50 ya ndoa ya Mhe. Benjamin William Mkapa ambaye ni Muumini wa Kanisa Katoliki na Mkewe Mama Anna Mkapa ambaye ni Muumini wa Kanisa la Kilutheri inawafundisha watanzania wote hususani wanasiasa kuishi kwa upendo na kuilinda amani waliyonayo na ametoa wito kwa viongozi dini kuendeleza juhudi zao za kuliombea taifa na kuwaunganisha wananchi licha ya tofauti walizo nazo.
Kwa upande wake Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa pamoja na kuwashukuru Viongozi wote, ndugu, jamaa na marafiki waliohudhuria Misa ya Shukrani na Jubilei hiyo ya miaka 50 ya ndoa yake amemshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuijaalia ndoa yake umri mrefu.

Rais Mstaafu Mkapa pia ametoa wito kwa watanzania kupenda na kushirikiana huku akibainisha mafunzo aliyoyapata kutoka kwa viongozi wa dini kuwa "Kila mmoja ni zawadi kwa mwenzake"
Naye Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amempongeza Rais Mstaafu Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa kwa kuadhimisha miaka 50 ya ndoa na amewasihi watanzania kuiga mfano mwema uliooneshwa na wana ndoa hao ambao wamedumu katika imani bila kuyumba.

Kardinali Pengo amesema ndoa ya Rais Mstaafu Mkapa anaifundisha jamii kuwa tunaweza kuishi kwa imani zetu bila kubadili dini.

Polisi Yaongeza Nguvu Oparesheni ya Vikindu

$
0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeongeza nguvu kwa kutuma askari wengine 80 katika oparesheni ya kusaka majambazi inayoendelea katika maeneo ya Vikindu, wilayani Mkuranga mkoani Pwani.

Akizungumza na vyombo vya habari leo katika kituo kikuu cha Polisi Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo Kamishna Simon Sirro, amesema Jeshi hilo limeanza rasmi oparesheni hiyo usiku wa kuamkia jana, ikiwa na lengo kusaka watu wanaoshukiwa kuwa ni majambazi wanaodaiwa kufanya matukio kadhaa ya ujambazi likiwemo lile la kuuawa kwa askari wanne waliokuwa wakienda lindoni, katika benk ya CRDB, Mbade jiji Dar es Salaam.

Amesema kuwa katika oparesheni hiyo kuna watu waliouawa na wengine wanashikiliwa na jeshi hilo, lakini amekataa kutaja idadi yoyote ile ya waliouawa au waliokamatwa kwa sababu za kiusalama kwa kuwa oparesheni hiyo bado inaendelea.

Kuhusu taarifa za uwepo wa askari aliyeuawa, Kamishna Sirro amekataa kuthibitisha au kukanusha na kusema kuwa taarifa kamili kuhusu oparesheni hiyo itatolewa siku ya Jumanne ya wiki ijayo.
Amewataka wananchi kuendelea kuwa watulivu, na kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo kwa kutoa taarifa zitakazoweza kufichua wahalifu hao na kusisitiza kuwa jeshi hilo litawabaini na kuwatia nguvuni wote waliohusika.

Katika hatua nyingine, Sirro ameendelea kupiga marufuku maandamano ya aina yoyote yale katika mkoa wa Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya zuio la jeshi la polisi la kupiga marufuku mikutano ya kisiasa na maandamano nchi nzima.

Usiku wa kuamkia jana, hali ya taharuki iliwakumba wakazi wa Vikindu baada ya kikosi maalum cha askari kuvamia nyumba moja iliyoko eneo hilo, na kisha kuzuka kwa majibizano ya risasi kati ya polisi na wanaodaiwa kuwa ni majambazi waliokuwa katika nyumba hiyo.
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live




Latest Images