Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

SWALI KWA WADADA...HIVI WANAUME WAREFU NA WEUSI WANA NINI CHA ZIADA KWENYE MAPENZI?

$
0
0
Swali langu kwa wadada na wataalam wengine wa mambo ya mahusiano,wanaume warefu,weusi wana nini cha ziada tofauti na wanaume wengine? 

Nimepata kuwauliza wadada wengi,ambao nimekutana nao maeneo tofauti wangependa waolewe au wawe na mahusiano na wanaume wa aina gani,wengi na karibu sehem kubwa hujibu kua wanapenda wanaume warefu ,weusi.

Mi naomba kujua wanaume warefu,weusi wana nini cha ziada hadi wapendelewe hivyo?

Karibuni sana.

KAJALA APANGUA SKENDO YA KUJIUZA

$
0
0

Stori: Imelda Mtema

UZUSHI! Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ameitolea mbavuni skendo ya kujiuza nchini China inayowatafuna mastaa wengi wa kike Bongo.
Kajala ambaye mara kwa mara amekuwa akisafiri kwenda nchini China, alipozungumza na paparazi wetu aliruka viunzi na kufafanua:
“China nakwenda kwa pesa zangu, nalipa dola 5000 (business class), nina dili zangu za kikazi na si kujiuza kama wapo wanaofanya hivyo ni wao lakini si mimi.”
GPL

PROF ISSA SHIVJI NA UBAKAJI WA MATAKWA YA UMMA KWENYE MUUNDO WA MUUNGANO

$
0
0
Sijawahi kufundishwa na Profesa huyu anaeishi Amerika akighani sheria zake katika uga wa Pwani ya Azania, nimjenzi mzuri wa hoja za kisheria vilevile jamii ya kiswahili inamuamini kwa misimamo yake,


Baada ya Tanzania kuanza mchaato wa kupata katiba mpya ya Muungano, Prof Shivj alikuwa miongoni mwa watu wanaotazamiwa kulisaidia taifa kupata katiba bora kabisa ya "KIRAI", lakini katika hali isiyotegemeka, mamlaka zote za nchi zikamtelekeza, akawa sasa ni deiwaka tu msako wa katiba mpya, akionyesha kuheshimu misimamo ya uuma.

Mnyukano wa kimaslahi kati ya Chama cha Mapinduzi na UMMA wa Watanzania, umemrejesha tena Issa Shivji mbobevu wa sheria za kiutawala, lakini akija kwa nadharia ya kusigina matakwa ya umma,

Yule Issa Shivji aliyekuwa mtetezi wa matakwa ya umma, leo amekuwa mpiga zumari wa Lumumba. Issa Shivji anafikiri Watanzania ni wajinga kiasi cha kumfuata kila akifanyacho, vikao vyake vya ikulu wiki jana kwamalengo ya ghiriba wa umma havita saidia Watanzania kudai Muungano wao BORA kabisa wa Serikali TATU.


Hebu tujirejeshe kidogo kuitazama Nadharia ya Muungano.


Hoja za muudo wa serikali zinatafsiriwa na sababu kuu mbili ambazo ni hoja za kisheria na hasira za kisiasa.

1.HOJA ZA KISHERIA

Hoja za kisheria ni kwamba zinapoungana serikali mbili ni lazima pawepo na katiba ya serikali moja au tatu na wala sio mbili tena kisheria.Kwa mfano ni kwamba tume zote mbili zilizoundwa na Rais chini ya wasomi wa kisheria chini ya JAJI FRANSISI NYALALI na ile ya JAJI ROBERT KISANGA zote zilipendekeza serikali 3 na sio mbili.

Kwa mfano endapo utampa msomi wa kisheria kazi ya kukuandalia katiba ya serikali mbili zinazotakiwa kuungana atakuandalia katiba ya serikali ama 1 au 3 lakini sio mboli kwani hazipo kisheria.

2.HASIRA ZA KISIASA

Hasira za kisiasa ni sababu nyingine ya kuwa na serikali tatu,Kwa mfano mwaka 1984 aliyekuwa rais wa Zanzibar ABDU JUMBE aliasisi hoja ya kuwa na serikali 3 na ikamgharimu kunyang'anywa kadi ya CCM na kupoteza urais wa Zanzibar na nafasi yake kuchukuliwa na MZEE ALI HASAN MWINYI 1984-1985 kabla ya kuchukuliwa na IDRISA ABDUL WAKIL 1985-1990.

Mwaka 1993 paliibuka kundi la G55 liliokuwa na nia ya kuifufua Tanganyika kundi ambalo lilipelekea baraza la mawaziri kuvunjwa mwaka 1994 na baadhi ya mawaziri akiwemo waziri mkuu na makamu wa kwaza wa Rais kupoteza wadhifa wake.

Mwaka huo huo 1993 Zanzibar ilitaka kujiunga na OAC wakakataliwa kwamba hawana mamlaka ya kufanya hivyo ndipo aliyekuwa Rais wa wakati huo DR SALIMIN AMOUR JUMA akasema Zanzibar imedharauliwa na kuzidi kupandisha homa na hasira za Wazanzibar kudai mamlaka kamili ya Zanziabar.

Hata mwalimu Nyerere alikuwa na nia kwamba waunde serikali moja lakini kwa kuanzia alipendekeza kwamba waanze na serikali mbili ili wazanzibar wasiseme wamemezwa japo baadae alishindwa kuunda serikali moja.

Kwahiyo hizo ndio sababu za mkanganyiko uliopo Tanzania katika mchakato wa katiba mpya.

By Yericko Nyerere

JIDE: MIMI NA GARDNER TUNAISHI KAMA KAKA NA DADA!

$
0
0
Kumbe! Super woman katika Afro-Pop, Judith Wambura a.k.a Lady Jaydeee au Jide amefunguka kuwa yeye na mumewe, Gardner Habash ‘Kapteini’ kwa sasa wanaishi kama kaka na dada hivyo kuibua swali kivipi?

Akizungumza na Ijumaa Wikienda katika mahojiano maalum yaliyofanyika kwenye mgahawa wa staa huyo wa Nyumbani Lounge uliopo Ada Estate, Kinondoni jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita, Jide alisema kuwa yeye na Gardner wamefikia hatua ya kuishi katika staili hiyo kutokana na mapenzi yao yaliyopitiliza.

“Gardner ananipenda sana na mimi pia vilevile nampenda sana mume wangu. Mapenzi yetu yamepitiliza hadi tunajiona kama vile tumezaliwa tumbo moja na ndiyo maana nawaambia kuwa mimi na yeye tunaishi kama kaka na dada,” alifunguka Jide.

Akiendelea kuzungumza kwa kujiamini, Jide alisema kuwa hadi simu ya mkononi wanatumia moja kwa ajili ya mawasiliano.

“Mimi hapa sina simu, anayo mume wangu lakini wakati mwingine nakuwa nayo mimi ila muda mwingi anakuwa nayo Gardner,” alimalizia Jide.

Kwa makala zaidi kuhusu usichokijua juu ya maisha ya Jide, nenda kurasa za nane na tisa za gazeti hili.

MVUA YAVUNJA NYUMBA NA GARI LA BABU AYUBU

$
0
0
Mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia siku ya Ijumaa 28 March 2014 imeleta maafa maeneo Kimara na Kuvunja Nyumba ya msanii wa Sauti na Muziki wa Kizazi Kipya maarufu kama Babu Ayubu, yeye mwenyewe anasema siku hiyo alirudi saa saba usiku na kujifungia ndani kwake lakini ilipofika mida ya saa kumi usiku akaskia kishindo Puup kushusha mguu wake kutoka kitandani akaona maji yapo kimo cha ugoko wake akajaribu kufungua mlango ukawa haufunguki kumbe ukuta ulikua umeangukia mlangoni na kuzuia usifunguke ndipo alipopiga makelele kwa majirani, wakafika na kumpa msaada lakini alipotoka nje akakuta gari lake limepondwa na matofali 1200, Babu anasema Gari hilo haliwezi tena kukaa barabarani so itabidi auze kwenye vyuma chakavu na kuhusu kulala amesema atalala katika nyumba yake nyingine kwasababu alikua amejenga nyumba tatu katika eneo moja na iliyoathirika ni moja tu. - See more at: http://www.makorokocho.co/2014/03/you-heard-mvua-yavunja-nyumba-na-gari.html#sthash.fNDXNdIU.dpuf

ANGALIA VIDEO JINSI REMIX YA WIMBO WA NUMBER 1 ULIVYOKUWA UNATENGENEZWA NA TUDDY

$
0
0
Angalia 'My number One Remix''Diamond' akiwa na msanii wa Nigeria 'Davido' jinsi wanavyoitengeneza kwenye studio za Ngoma Records chini ya producer Tuddy Thomas.

ONA SHOW YA DIAMOND ILIYOJAZA UWANJA KAMA VILE NI SIMBA NA YANGA..WATU WAKANYAGANA

$
0
0
Hii ilikuwa Pande za Mwanza...Dahhh huyu Jamaaa Noma embu jionee mwenyewe kwenye video hapa:

DOWNLOAD WIMBO ULIYOIMBWA NA NA WASANII ZAIDI YA 19 AKIWEMO DIAMOND, AY, FALLY IPUPA, D-BANJ NA WENGINE WENGI

$
0
0
Zaidi ya wasanii watano kati ya wale 19 waliojumuika kutengeneza wimbo na video ya wimbo "Cocoa na Chocolate" kwa ajili ya kuhamasisha kilimo kwa vijana na kuwa kiimo kinalipa, wamekutana Lagos nchini Nigeria
KODOWNLOAD BOFYA HAPO CHINI

TREY SONGZ AIKANA TWEET ALIYOANDIKA NA KUSEMA YEYE NI SHOGA

$
0
0
March 25, ilisambaa picha ya tweet inayoonesha kuwa wamei-screenshot kutoka kwenye akaunti ya mwimbaji wa R&B, Trey Songz na kuonesha amejitangaza kuwa yeye ni shoga.

“I think it’s time to finally tell my fans. All games and jokes aside…I’m gay.” Ilisomeka picha ya tweet hiyo.

Hata hivyo, mwimbaji huyo aliikana tweet hiyo mapema asubuhi na kuonesha kuchukizwa kwake na kitendo kilichofanywa na watu ambao wanaonekana walitumia teknolojia ya kuchezea picha maarufu kama Photoshop na kuichora tweet hiyo.

Trey Songz alionesha masikitiko yake kwa tweets tatu zilizofuatana.

“The things you people craft up with hatred in your hearts. The things people believe without question, or validity, all baffles me.

“Photoshop and a retweet is all people need to believe, any and everything. I feel bad for the impressionable, no minds of their own.

“If I’m gay then Tupac bringing me a ounce for this session wit Biggie tomorrow. No weapon. #LOVE.”

MUME WANGU JOGOO HALIWIKI, WIKI YA TATU SASA, YANI HATA NI MTEGE VIPI, NISAIDIENI PLZ

$
0
0
Nimeishi na mume wangu mwaka wa tatu sasa, amekua akipiga kazi mpaka nafurahi, ananifiki kilele hata mara nne kwa siku moja, lakini sasa hivi ni wiki ya tatu hasimamishi yani mpaka hata yeye mwenyewe anakosa amani kabisa, najaribu kumtega kwa kila mikao na visa visa vywa kimahaba lakini imeshindikana. Naombeni ushauri jamani  kama kuna namna nikamsaidia mume wangu, nampenda sana, sitaki kumsaliti. 

DIAMOND AKIWA NDANI YA RADIO KUBWA NIGERIA BEAT 99.9 FM KWA MAHAOJIANO...

$
0
0
Baada ya Wimbo wa number One kumpa chat kubwa Nigeria na Africa kwa ujumla ..leo Radio kubwa kuliko zote Nigeria Beat 99.9 FM walikuwa wakimuhoji nguli huyo...hii ni kutokana na wimbo wake kukaaa number moja katika top chat za radio hiyo kwa zaidi ya week moja

MCHUNGAJI MTIKILA ADAI AMEZUIWA KUCHANGIA BUNGENI

$
0
0
Mjumbe wa Bunge la Katiba, Mchungaji Christopher Mtikila amedai hataweza kuchangia tena katika mjadala wa Katiba kwa kuwa Ofisi ya Bunge imempiga marufuku kutokana na kauli zake.

Hata hivyo, Katibu wa Bunge Maalumu la Katiba, Yahaya Khamis Hamad alisema kuwa taarifa hiyo kwake ni mpya na haamini kuwa jambo hilo lipo.

“Hili kwangu ni jipya na sidhani kuwa linawezekana na lipo,” alisema Hamad.

Awali Mtikila aliliambia gazeti hili kuwa amepewa barua hiyo Jumatano iliyopita, ikiwa ni majibu ya barua yake aliyoandikia ofisi hiyo ya Bunge kutaka ufafanuzi wa kile alichoeleza kuwa amekuwa akinyimwa haki ya kuchangia bungeni.

“Nilianza kuhisi baada ya kuona kuwa nanyimwa kuchangia, nikaandika barua kuomba maelezo kwa nini ninakosa nafasi ya kuchangia bungeni,” alisema Mtikila na kuongeza;

“Lakini juzi nilipokea barua kutoka kwa Katibu wa Bunge ikinikataza kuchangia tena bungeni kutokana na statement (taarifa) zangu za kukosewa kwa mchakato.”

Alisema kuwa alipomuuliza katibu kulikoni akatazwe kuchangia katika Bunge hilo alijibiwa kuwa ni maagizo kutoka kwa mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta.

Mchungaji Mtikila alisema kutokana na katazo hilo atamwona Sitta ili amfafanulie tatizo lake.

“Hii imeniathiri sana mimi. Bunge hili limepotoka wanachoangalia ni masilahi yao na si ya nchi,” alisema.

Alisema mchakato wote umekosewa kwa kuwaweka wabunge na wawakilishi kuwa sehemu ya Bunge badala ya wananchi kuchagua wajumbe wa Bunge hilo.

“Hakuna nchi yoyote ambayo imefanya hivyo, wanaharibu mabilioni ya fedha ambayo hayataleta Katiba yenye uhalali yoyote,” alisema.

Alisema endapo Sitta atashindwa kutatua jambo hilo anakusudia kuunganisha katika ushahidi wake kwenye kesi inayopinga mchakato wa Katiba.

PATA BREAKING NEWS NA HABARI ZA MASTAA KUTOKA UDAKU SPECIAL KWA KUPITIA SIMU YAKO

$
0
0

Jiunge na UDAKU SPECIAL BREAKING NEWS Kupata Habari Mbali Mbali za Mastaa Kwenye Simu yako kwa Kutuma Neno "UDAKU" Kwenda Namba 15678 ...Fanya sasa Hivi Usipitwe...
Note:Mitandao yote

MASKINI:MBWA WA UBALOZI WAMLA MTOTO!

$
0
0
NI vigumu kuamini kilichotokea lakini ndivyo ilivyokuwa! Mtoto Christian Alex (6) ameuawa kikatili kwa kuliwa na mbwa wanaodaiwa kuwa ni wa Ubalozi wa Qatar nchini  Tanzania unaoongozwa na Balozi Jassim Mohammed Mubarak Daruwesh.

Tukio hilo la kusikitisha lilijiri Machi 26, mwaka huu Jangwani Beach, Kunduchi jijini Dar es Salaam ambapo mtoto huyo alishambuliwa na mbwa wa kigogo huyo alipokuwa na baba yake jirani na nyumba hiyo ya kupanga yenye nyumba nyingine mbalimbali (apartment).
MAELEZO KWA UFUPI
Inaelezwa kuwa, baba wa marehemu pia anaishi kwenye moja ya nyumba hizo akifanya kazi ya kutunza mazingira endapo mpangaji mmoja anahama. Wote wanaoishi humo wanatumia mageti mawili tu, kuingia na kutoka.
Mama wa mtoto Christian Alex akiwa amezimia wakati mwili wa mwanae unazikwa
BABA WA MAREHEMU ASIMULIA
Akizungumza na gazeti hili kwa majonzi  kwenye msiba uliogubikwa na vilio na simanzi, baba wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina la Alex, alisema siku ya tukio yeye alikuwa akitoka nje ya nyumba anayoishi katika ‘apartment’ hizo, lakini  ghafla nyuma yake alisikia kelele za mwanaye.
“Kwa kawaida ili utoke lazima uwe makini, kwanza ujue mbwa wako wapi? Nilipotoka nikiwa nawaangalia walipo, mara nikasikia kelele mtoto wangu analia, nilirudi haraka, nikamkuta mwanangu anashambuliwa na mbwa watatu huku tayari akiwa na majeraha makubwa.
Mazishi ya Mtoto Christian Alex (6).
“Ilibidi nimng’ang’anie mtoto ili kumwokoa ambapo pia niliokota jiwe kutaka kuwapiga, wakataka kuondoka lakini wakarudi tena na kumvamia.
“Hapo ndipo ilikuwa shughuli kwani walimfumua utumbo, wakazinyofoa sehemu zake za siri na kuziingiza midomoni huku kisogoni wakimtia kucha kali mpaka kumtoa ngozi.
“Wakati kitendo hicho kinaendelea huku nikishuhudia kwa macho, yule balozi akawa anaingia ndani, akawaamuru mbwa wake waache, walitii amri hiyo lakini hali ya mtoto wangu ilikuwa mbaya sana, akawa hasemi wala hapigi kelele tena za kuomba msaada,” alisema baba huyo huku akimwaga machozi. Inauma sana!
Mtoto Christian Alex  baada ya kujeruhiwa na mbwa wa ubalozi wa Qatar.
Akaongeza: “Mpaka sasa siamini kilichotokea, nashindwa hata niongee nini, ninachoweza kusema ni kwamba mwanangu Christian nilikuwa nampenda sana kama vile ninavyompenda mwanangu mwingine, Sabina.
“Nahisi ukiwa baada ya kupoteza mtoto wa kiume niliyekuwa namtegemea. Itanichukua muda mrefu sana kusahau kile nilichokiona kwa macho yangu. Nimeshuhudia mwanangu akishambuliwa na wala sikusimuliwa na mtu.”
Mazishi yakiendelea.
KUMBE TAHADHARI ILITOLEWA
Baba anaendelea kusimuliza: “Kinachoniuma zaidi ni kwamba, nilishatoa angalizo tangu mwanzoni wakati huyu bwana anahamia kwenye nyumba hii. Nilimwambia mwenye nyumba  amwambie huyu awajengee banda  mbwa wake lakini wakapuuzia.”
ADAKTARI WALIVYOSEMA
Baadhi ya majirani walifika eneo la tukio na kukuta sakata hilo limefikia hatua ya mbwa kutii amri ya bosi wao na kurudi kwenye maskani yao.
Walimchukua mtoto huyo na kumkimbiza kwenye Hospitali ya IMTU iliyopo Mbezi, Dar  ambapo madaktari walisema alishafariki dunia kitambo.
VILIO VYATAWALA 
Baada ya kuzinyaka taarifa hizo, haraka mwandishi wetu alifika eneo la tukio muda mfupi baada ya mtoto huyo kupelekwa hospitali na kushuhudia vilio vikitawala kwa kila jirani aliyepata taarifa za kifo hicho cha kusikitisha.
MAJIRANI WASIMULIA
Wakionesha jinsi walivyoumizwa na tukio hilo, baadhi ya majirani walisimulia jinsi mbwa hao wanavyowatishia amani katika nyumba hiyo ambapo tangu kigogo huyo ahamie ndani ya nyumba hiyo wamekuwa watu wa kujifungia siku nzima wakihofia mbwa hao wakali.
“Jamani huyu mtoto kafa kifo kibaya sana, mbaya zaidi mbwa hawa wamekuwa tishio kiasi cha watu kushindwa kufanya shughuli zao za kila siku.
“Mbwa huwa hawafungiwi kwenye banda, labda ingekuwa hivyo wasingefanya hivi,” alisema jirani mmoja huku akilia bila kikomo.
POLISI WALIVYOFANYA
Paparazi wetu alipojaribu kuingia ndani na kwenda kuongea na balozi huyo, askari waliodaiwa ni wa Kituo cha Polisi Kawe jijini Dar walitia ngumu huku ikidaiwa kuwa maelezo waliyoyaandika ni mmiliki wa mbwa kuwa mzembe kwa kuwaachia mbwa kudhuru binadamu.
MAMA MZAZI AZIMIA
Maria Mvile, mama mzazi wa marehemu Christian kwa sasa yupo katika hali mbaya tangu mkasa wa kushambuliwa mwanaye na mbwa hao utokee ambapo amekuwa akizimia mara kwa mara.
Mwandishi wetu alimshuhudia mama huyo akishindwa kuweka shada la maua katika kaburi la mwanaye kwa kuanguka na kuzimia.
MAZIKO
Safari ya mwisho ya mtoto Christian ilifanyika kwenye Makaburi ya Mburahati, Dar es Salaam ikitanguliwa na misa iliyosomwa na Katekista wa Kanisa Katoliki Mburahati, Owen Hokororo.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Camillius Wambura amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kukiri kuwa ni nyumbani kwa balozi wa Qatar nchini.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.
GPL

LULU KATIKA SKENDO YA KUPORA BWANA WA MTU

$
0
0
E LIZABETH Michael ‘Lulu’ anayetesa katika filamu za Kibongo, yupo kwenye bifu zito na mshiriki wa Miss Tanzania mwaka 2012, Husna Maulid ambaye anadai amempora bwana’ke.

Habari zinaeleza bifu lao limefikia hatua ya kuanikana waziwazi hadi kumwagiana matusi kwenye mitandao ya kijamii, hasa Instagram lakini huondoa majibizano yao machafu kila baada ya muda mfupi.

Chanzo cha habari hizi kinapasha kuwa ugomvi wa Lulu na Husna ni juu ya mwanaume huyo ambaye anaishi jijini Arusha aliyetajwa kwa jina moja la Seki anayeelezwa kuwa na pesa za kutosha kusumbua mjini. “Hao wanamgombea jamaa fulani wa Arusha, anaitwa Seki, ana mawe (pesa) mbaya.

Lakini wa kwanza kuwa na Seki ni Husna na Lulu alijua, sema Husna na huyo jamaa walikuwa wanagombana na kumwagana mara kwa mara. Sijui sasa nini kilimfanya Lulu kwenda kutembea tena na huyo jamaa wakati anajua ni wa shoga yake, labda ni baada ya kujua wamemwagana,” kilipasha chanzo hicho.

Baada ya kupata habari hizi, mwandishi wetu aliwatafuta Lulu na Husna kwa ajili ya kuthibitisha madai hayo. Lulu alikuwa wa kwanza kupatikana ambapo alisema: “Jamani mimi simjui kabisa Husna Maulid wala hata katika fikra zangu hayupo... yaani kifupi simjui.”

Husna alipopatikana na kuelezwa mkanda mzima, kwanza alishangaa Lulu kutomjua, akasema: “Hakuna mtu asiyejua kuwa Lulu kanipora mwanaume wangu. Lakini anajifanya mjanja, tutaoneshana tu. Anajidai sana, anajifanya wa mjini hanijui mimi, lakini mimi ni wa mjini zaidi yake.”
GPL

KUHUSU TUKIO LA WANA NDUGU 12 KUPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI YA BARABARANI WAKIENDA MSIBANI HUKO KILIMANJARO

$
0
0
Lori la mizigo aina ya Fusso likiwa limegongana na  gari ndogo aina ya Toyota Hilux Pick Up katika eneo la Hedaru, wilayani Same, Kilimanjaro, juzi  na kusababisha vifo vya watu 12.

Mji wa Hedaru uliopo wilayani Same mkoani Kilimanjaro, jana ulizizima kwa vilio na simanzi baada ya waombolezaji 12 wote ndugu, kufariki dunia kwa ajali ya barabarani.

Waombolezaji hao wanawake, walipewa lifti ya gari na Diwani wa Kata ya Hedaru, Gerard Mgwena (CCM), kwa ajili ya kuwapeleka msibani eneo la Majengo ambako mtu mmoja alifariki kwa kusombwa na maji.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro (RPC), Robert Boaz alithibitisha ajali hiyo akisema ilitokea juzi saa 2:00 usiku na kwamba ilikuwa mbaya zaidi tangu kuanza kwa mwaka 2014.
“Ni ajali iliyohusisha magari matatu kwa wakati mmoja…; watu 11 walifariki pale pale na mwingine alifariki dunia leo (jana), asubuhi Hospitali ya Rufaa ya KCMC,”alisema Boaz.
Hata hivyo, alisema hakuwa na nafasi nzuri ya kufafanua kwa undani ajali hiyo kwa vile alikuwa nje ya Mkoa wa Kilimanjaro na kuelekeza atafutwe Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa (RTO), Joseph Mwakabonga.
Akizungumza kwa niaba ya RPC, Mwakabonga alisema, lori aina ya Mitsubish Fusso lililokuwa likitokea Moshi kwenda Dar liligonga kwa nyuma gari aina ya Toyota Hilux Pick-Up.
Alisema kuwa baada ya kuligonga gari hilo lililowabeba waombolezaji hao, nalo lilisukumwa na kwenda kuligonga lori aina ya Scania lililokuwa na tela lake.
Lori hilo aina ya Scania lilikuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Moshi likiendeshwa na dereva wake, Gabriel David. Madareva wawili wa Toyota Pick-Up na Toyota Fusso wote hawajulikani waliko.
Taarifa zilizopatikana baadaye, zilisema dereva wa Fusso alikuwa amelazwa katika Hospitali ya KCMC, wakati Kigogo wa CCM aliyekuwa amewabeba waombolezaji akilazwa hospitali moja jijini Arusha.
Mwakabonga aliwataja waliofariki kuwa ni Stella John(45), Salma Kizoka (33), Marry Senzige (49), Neema Daniel (52), Rehema George (29) na Sophia Mbike (51).
Wengine ni Ritha Kalani (55), Mama Kalani Stephano (55), Kolina Mmatha(55), Bahati Daud(25) na Farida Kiondo mwenye umri wa miaka 25.
Majeruhi mmoja, Maria John (33) ambaye ni miongoni mwa watu 10 waliojeruhiwa, alifariki dunia jana asubuhi katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC alikolazwa kwa ajili ya kuokoa maisha yake.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia ajali hiyo, watu hao walipata ajali hatua 10 kutoka katika eneo ambalo ndugu yao aliosombwa na maji na kufa, ambapo maiti yake iliokotwa eneo hilo.
Alex Shirima mmoja wa mashuhuda alisimulia kuwa gari la diwani lilikwama kweye tope katikati ya Barabara ya Moshi Dar es Salaam.
Alisema, kabla ya kushuka kuangalia namna ya kulinasua gari lake, likatokea lori gari aina ya Fuso kwa nyuma ambalo liliigonga gari lake iwani na kulisukuma mita kadhaa mbele ambako lilikutana uso kwa uso na lori lingine aina ya Scania lililokuwa likitokea Dar es Salaam.
Alisimulia kuwa kutokana na ukubwa wa ajali hiyo, eneo hilo lilitapakaa viungo vya binadamu na damu.
Shirima ambaye ni dereva aliyefika katika eneo hilo dakika mbili baada ya ajali kutokea, alisema eneo hilo ni hatari kwa madereva kwa kuwa mvua zikinyesha, barabara hujaa maji na matope.
Hali ilivyo kijijini
Mmoja wa watoto ambaye mama yake mzazi amefariki katika ajali hiyo, Sebali Mkwizu alisema kuwa kijiji chao kimekumbwa na ukimya na majonzi, huku wakishindwa kuamini kilichotokea.
Alisema kuwa ajali hiyo imechukua maisha ya ndugu zake wanane na kati ya hao, saba walikuwa wakiishi kijijini hapo kwenye nyumba tofauti zinazofuatana.
“Nimepoteza mama yangu mzazi, mama mdogo, shemeji zangu watatu, mke wa ndugu yangu na watoto wawili. Hapa nyumba saba zina msiba,” alisema Mkwizu.
Alibainisha kwamba mazishi ya wanawake hao yanatarajiwa kufanyika leo katika eneo la pamoja kijijini hapo.
“Tumeambiwa watazikwa eneo moja, lakini bado hatujajua ni sehemu gani, hadi kesho (leo) ndiyo tutapata taarifa kamili,” alisema. 

UBISHOO MWISHO AIRPORT KAMA HUAMINI LOOK AT THIS MZUNGUZ

$
0
0
Mzingu akifanya yake.....Hiyo kwa Kiswahili inaitwa Nguna.....aka Ugali....Je kwa Kabila lako ugali unaitwaje?

UJANA NA KURUKA RUKA UNA MWISHO HATIMAE BISHOO HEMEDY KUOA HIVI KARIBUNI

$
0
0
Mwimbaji Bishoo na Kipenzi cha wadada hapa mjini ...Aka Bongo Hemedy au PHD ametangaza kuwa soon ataoa na huyo kwenye picha ndio ubavu wa rohoo yake ..Humwambii kitu ....kweli Ujana maji ya Moto..Sasa yamepoa....

So proud to call you my woman…..its official,” ameandika staa huyo wa filamu na muziki kwenye picha inayomuonesha akiwa na mpenzi wake aliyoiweka Facebook.
-John K

MLIPUKO WA MABOMU TENA KENYA...SITA WAFARIKI DUNIA

$
0
0
Watu sita wamepoteza maisha na wengine 25 kujeruhiwa vibaya katika shambulizi la kigaidi katika eneo la California mtaa wa Eastleig jijini Nairobi.
Kamanda wa Polisi mjini Nairobi Benson Kibue amesema kuwa milipuko miwili ilitokea wakati magaidi waliporusha milipuko katika migahawa miwili midogo.
Mlipuko wa tatu ulitokea katika kituo cha mabasi ya uchukuzi kilichopo karibu na zahanati ya mama na mtoto.
Miongoni mwa waliojeruhiwa walikuwa ni wanawake waliokuwa wanauza mboga na bidhaa nyingine za rejareja.
Kwa mujibu wa polisi watu waliouawa walikuwa wamekwama ndani ya mgahawa huo baada ya mlango wa kutoka nje kufungwa  na washambulizi waliorusha bomu ndani.
Watu hao waliopoteza maisha walikuwa wameenda kununua chakula cha usiku.

SHOGA LATISHIA AMANI ZA WANAWAKE KARIAKOO..WANAWAKE WAJIKUSANYA KUMSUTA ILI AACHE KUCHUKUA WAUME ZAO

$
0
0
Idara ya Hekaheka leo ina taarifa kuhusu shoga mmoja aliyepo Kariako0 ambaye wanawake wa Kariakoo wamejikusanya mpaka kwa shoga huyo kwenda kumkanya na sababu ni tabia ya kuchukua wanaume wao,ungana na Geah Habibu kwenye Hekaheka hii.
88.1 Clouds Fm inasikika ukiwa Mwanza.
Bonyeza play kusikiliza. Credits:Millard ayo
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images