Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

IDRIS Sultan Ampiga Dongo Diamond, Adai Amepoteza Control Kwa Wanawake zake Mpaka Mambo Yanamwagika Ovyo

$
0
0
Kama huwezi utani basi jiweke mbali na Idris Sultan kwa kuwa ipo siku unaweza kujikuta ukifanya kitu usichokitarajia.


Mchekeshaji huyo ameandika ujumbe wa utani kwa Diamond na Zari kwenye mtandao wake wa Instagram baada ya hivi karibuni kusambaa kwa taarifa kuwa First Lady huyo wa WCB alikuta hereni kwenye chumba cha Diamond ikionekana kuwa alimsaliti na mwanamke mwingine.

Ameweka picha ya Remote Control iliyoandikwa Woman Control na kuandika haya:

“Ndio imeingia na DHL @diamondplatnumz nakupitishia hapo maana umepoteza control mambo yanamwagika hovyo mara hereni ulizisimamia kama kangaroo,” ameandika Idris kwenye picha ya remote aliyoiweka kwenye mtandao huo.

Hakuishia hapo Idris amempongeza Zari The Bosslady kwa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kuweka picha ya hereni kwenye mtandao huo na kuandika ujumbe unaosomeka, “Happy birthday @zarithebosslady 😅.”

Nay wa Mitego Afunguka Kwa Mara ya Kwanza Toka Shamsa Ford Kuelewa na Mwanaume Mwingine...Adai Alimwambia Anaenda Kuolewa

$
0
0
Akizungumza katika kipindi cha XXL cha Clouds FM Ijumaa hii, Nay Wa Mitego amesema Shamsa ni ‘wife material’ hivyo anamtabiria kudumu katika ndoa yake.

“Ndoa ni kitu cha heri lakini sometime watu wanaweza wakaoana kwa kutafuta experience za ndoa zinakuwaje, watu wakioana inakuwaje, ukishapata experience kila mtu anaendelea kupuyanga,” alisema Nay. “Sasa mimi sijajua kama wao wanatafuta experience za ndoa ili kujua watu wakioana wanakuwaje,”

Aliongez, “Kwa jinsi ninavyomjua Shamsa ni mwanamke kweli, kwa sababu ni mwanamke ambaye anastahili kuwa mke kwa sababu amekaa ‘kiwife material’ kiukweli kabisa, sijui mtu ambaye ameenda kuolewa naye na kuna vitu yeye mwenyewe anatakiwa kubadilika,”

Rapper huyo amedai Shamsa kabla hajaolewa alimwambia kwamba anaenda kuolewa na akampatia baraka zote.

Shilole Asema Chupu Chup Awe Salome Kwenye Video ya Diamond...Adai Ingepata Views Mil 2 Ndani ya Siku Mbili

$
0
0
Mwanadada mwenye mvuto kupita wote ndani ya gemu ya maburudani Afrika Mashariki na Kati ameendelea kugonga headlines za vyombo vya habari baada ya kusema Diamond platnumzs alitaka yeye ndio HAWE video Queen wa nyimbo ya Salome na walikubaliana kabisa.... Sema siku ya kushoot alipata zalula hivyo nafasi yake akamwachia hamisa mobeto.... Ila anaamini hangekuwa yeye ndio video Queen basi video hiyo ya Salome ingepata views milioni 2 ndani ya siku mbili

Jokate: Bado Nafanya Muziki, ila Nahitaji Menejimenti

$
0
0
Mwanamitindo na mwanamuziki nchini Tanzania, Jokate Mwegelo ambaye amekuwa kimya katika masuala ya muziki kutokana na kuwa busy na biashara, amesema bado anafanya muziki.

Jokate ambaye wimbo wake wa mwisho kuutoa ulikuwa ‘Leo Leo’ aliomshirikisha Ice Prince kutoka Nigeria, alikuwa akihojiwa Ijumaa hii kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM.

“Muziki bado nafanya ila bado nahitaji menejimenti ambayo ipo vizuri,” alisema. “Sitaki kufanya muziki niwe kama najaribu, nahitaji kuwa na timu ambayo tutafanya kazi ya serious kama ilivyo kwenye brand ya Kidoti. Bado natafuta timu ambayo itanisimamia katika muziki vizuri, sijaacha nimesimama tu hadi hapo nikapopata menejimenti nzuri,” alisema Jokate.

Diamond Hongera Kwa Kumpata Zari Lakini Nina Duku Duku Moyoni

$
0
0
Jamani tunajua Dada zetu wabongo kichwani Hamna kitu, wanawaza starehe tu na hawapendi maendeleo wala kujituma kama zari, tunajua zari yupo smart kichwani anajielewa, pengine kutokana na malezi na exposure aliyoipata ya kutembelea nchi mbali mbali, hivyo ni dhahiri upeo wake wa kufikiri ni mkubwa zaidi kuliko Dada zetu hawa bongo movie na bongo flavor, na namsifu zari kwa kweli japokua Ana ka cv kabaya ila sijawahi kumsikia akiwa na scandal za wanaume toka kawa na diamond, achilia mbali mashauzi na dharau ambayo yanaweza kutokana na malezi au hali ya kimaisha, kwa hilo tu nampongeza zari kwa kuficha aibu ya kaka yetu ambaye alikua akiitwa tasa kila siku(ikiwemo Mimi)

Tukija upande wa pili, ina maana diamond wanawake wote wa bongo ni ****** kiasi hicho mpaka uende ng'ambo?? Sitaki kuamini ujue, mi roho inaniuma ujue?? Mjengo wote ule umeenda kwa waganda? Maana mama teeh hataki ujinga Yule na hacheki ovyo na watu, hata kuja kwako mashabiki tutashindwa ujue maana mwanamke hana ushoga wala ujirani na mtu khaaa ,kama Salome tu alisahau hereni wakati mkifanya shooting kaumbuliwa vile hadharani haya sie majirani ya madale tukija tukasahau viatu si ndo vitatangazwa snapchat nzima?? Waah hapana kwa kweli

By Warumi/JF

Hawa Hapa Ndio Watoto wa Mwanamuziki Shilole Kiuno

$
0
0
Kwa wale ambao mlikuwa hamuwajui watoto wa Shilole aka Shishi basi hawa ndio watoto wake, sema chochote

Rekodi Nyingine iliyovunjwa na Diamond Platinumz Youtube

$
0
0
Najua inaweza kua sio jambo geni ukisikia wimbo wa msanii kutoka Marekani umetazamwa mara nyingi kupitia Youtube, Lakini leo hii niko na hii kutoka Tanzania mtu wangu, Diamond Platinumz amefanikiwa kuweka rekodi ya kufikisha Views zaidi ya Milioni moja na nusu kwenye mtandao wa Youtube baada ya Video ya hit single ya Salome kuwekwa ndani ya siku nne tu.

Diamond Platinumz anafuatana kwa views nyingi na wasanii mapacha kutoka kundi la PSquare na video yao ya Bank Alert iliyotazamwa zaidi ya mara milioni moja na laki moja ndani ya wiki moja tangu ilipowekwa Youtube.

Jipatie Dawa Asili za Kutengeneza Shepu, Kuondoa Michirizi Chunusi, Kurefusha Nywele Toka Markson Beauty Products

$
0
0
HABARI NJEMA MARKSON BEAUTY PRODUCTS
Baada ya kupata cheti cha bidhaa bora kwa mwaka 2015-2016, Sasa kampuni hii inasambaza huduma zake ndani na nje ya nchi kwa vibali maalum. Bidhaa zetu zimetengenezwa kwa mimea na matunda na kudhibitishwa. Hazina kemikali wala madhara. DAWA ZETU NI YA:-

  1. kurefusha nywele na kuzuia kukatika ovyo @100,000/=
  2. Kuongeza shepu (hips na makalio) kwa/= (a)Dawa ya kunywa au kupaka @150,000/=(b)Vidonge @170,000/=
  3. Kuwa mweupe na softi mwili mzima kwa:- (1)Mafuta @100,000/= (11)Vidonge @150,000/=
  4. Kupunguza unene na manyama uzembe @120,000/=
  5. Kuongeza uume pamoja na nguvu za kiume kwa:-(a) Gely ya kupaka @100,000/= (b) Vidonge maalum @120,000/= (c) Handsome up original @170,000
  6. Kuondoa mvi milele zisiludi tena @100,000/=
  7. Kuongeza unene wa mwili mzima na uzito @120,000/=
  8. Kupunguza tumbo (kitambi) na nyama za pembeni kwa:- (a) Dawa ya kunywa au kupaka @120,000/= (b) Mkanda wa kawaida @100,000/= (c) micro-computer belt unaovaibret @200,000/=
  9. Kupunguza maziwa na kuyasimamisha @90,000/=
  10. Kushepu miguu na kuwa minene @100,000/=
  11. Kuondoa mipasuko mwilini (michirizi) @90,000/=
  12. kubana uke na kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa mwanamke @100,000/=
  13. Taiti za hips na makalio @150,000/=           
NB: Hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii kwa bidhaa halisi. Wasiliana nasi :-(+255) 0767447444 na 0714335378 Google MARKSON BEAUTY.
Follow us
@Markson_beauty_pr
@Markson_beauty_pr

Vanessa Mdee Aeleza Collabo Yake na Trey Songz….

$
0
0
Ni Headlines za Vanessa Mdee ambae amekuwa ni moja kati ya wasanii wa Africa waliochaguliwa kurekodi wimbo na mshindi wa Grammy na mwimbaji wa RNB nchini Marekani, Trey Songz kupitia msimu wa 4 kipindi cha Coke Studio Africa.

Akizungumza na millardayo.com & Ayo TV  Vanessa Mdee aliyaongea haya:
Niko Kenya nikifanya msimu wa Coke Studio Africa ambapo msimu huu tumemkaribisha msanii wa kimarekani Trey Songz kuja kufanya collaboration na waafrika nikiwemo na mimi’
‘Ni experience ya kipekee sana nimefuraha sana kuwa katika nafasi hii ya kufanya collabo nae kwani ni hatua nzuri kwangu pia kuitangaza nchini yangu’

Ruby Asema Wimbo wa Wale Wale Sio Dongo Kwa Clouds FM na Ruge Kusaga

$
0
0
Msanii wa muziki ambaye ni zao la Fiesta Super Diva 2014, Ruby, amesema wimbo ‘Wale Wale’ sio dongo kwa mtu yeyote bali amemwimba shetani.

“Mimi sijaimba huu nyimbo kwa ajili ya mtu yeyote kama ambavyo watu wanaweza kufikiria,” alisema Ruby. “Hii ni inspirational song, sijaimba mapenzi kabisa humo ndani kama ambavyo watu wanavyomuongelea Ruby anaimba mapenzi tu. Halafu sijamwongelea mtu nimemwongelea shetani, sifa za shetani,”

“Shetani siyo mtu wala hajafanana na mtu ila ni roho ambayo inaweza ikamwingia mtu yeyote. Hiyo roho inaweza ikaplay part mbili tofauti, hiyo roho inaweza ikakuletea kitu kizuri kumbe inataka ikitawale halafu ikuharibie, lakini kitu kizuri na chakudumu nichamungu.

Na hivyo hivyo hivi vitu vinatokeaga kwa mabosi wetu, pengine bosi akakutaka kimapenzi ili akupandishe cheo, lakini ile hali siyo hali nzuri, kwa hiyo mimi sijamwongelea mtu yeyote bali ni shetani ambaye mara nyingi anataka kutuaribia maisha yetu,” aliongeza.

Wimbo ‘Wale Wale’ ni wimbo wake wa kwanza kuuandika mwenyewe toka aanze kufanya muziki.

Mwanamuziki Trey Songz na Vanessa Mdee Mambo Safi..Trey Asema Haya

$
0
0
Trey Songz amefunguka kuhusu kufanya kazi na Vanessa Mdee wakati akijibu swali la shabiki.

Wakati akijibu swali hilo muimbaji huyo wa Marekani amesema wametengeneza wimbo mzuri pamoja.

“Vanessa is great, we got a great song together, has a great chemistry, she loves to laugh and joke even when we was performing having a good time,” alisema.

Kuna uwezekano mkubwa Vanessa na Trey Songz wakaka kutengeneza wimbo wa pamoja nje ya Coke Studio.

Breaking News: Lipumba ni Mwenyekiti Halali wa CUF

$
0
0
Profesa Ibrahim Lipumba aingia ndani ya ofisi za CUF makao makuu jijini Dar es salaam kama mwenyekiti wa chama hicho baada ya barua ya Msajili wa vyama vya siasa kutoa barua ya kumtambua kuwa bado ni mwenyekiti halali wa CUF.

Akizungumza na waandishi wa habari Jumapili hii akiwa ofisini kwake Buguruni jijini Dar es salaam, Lipumba amesema huu ndio wakati wake wa kuzungumza na wanachama wake juu ya kukijenga upya cha hicho.

“Sasa hivi mimi nitafanya kazi kama mwenyekiti na kuna mambo yanabidi yarekebishwe ndani ya chama na nitayafanyia marekebisho yanayohitajika. Lakini pia tutafuata katiba na kanuni za chama kuhakikisha nakijenga chama chetu,” alisema Lipumba.

Alipoulizwa kuhusu hali hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF, Julius Mtatiro alikiri kupokea barua ya msajili.

Hata hivyo, Mtatiro amesema kwa vyovyote vile msajili wa vyama vya siasa hana mamlaka ya kuingilia maamuzi ya vikao vya chama chochote cha siasa.

Tamko la CUF baada ya Prof.Lipumba kuchukua ofisi

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

The Civic United Front (CUF – Chama Cha Wananchi) kimepokea kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kile kinachoitwa “Msimamo na Ushauri wa Vyama vya Siasa kuhusu Mgogoro wa Uongozi wa Kitaifa wa
Chama cha Civic United Front (CUF)” ambao uliwasilishwa Ofisi Kuu ya Chama, Buguruni, jana usiku.

Baada ya kupokea Ushauri huo, The Civic United Front (CUF – Chama Cha Wananchi) kinapenda kueleza yafuatayo:

1. Sheria ya Vyama vya Siasa (Political Parties Act, No. 5 of 1992) haimpi mamlaka wala uwezo wowote Msajili wa Vyama vya Siasa kutoa ushauri, msimamo au mwongozo kwa vyama vya siasa kuhusiana na maamuzi
ya vikao vya Chama.

2. Msimamo huo wa kisheria wa nchi hii umetiliwa nguvu na kuthibitishwa na Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia UAMUZI wa tarehe 9/5/2005 wa Jaji T.B. Mihayo katika kesi ya Emmanuel Nyenyemela na Magnus Msambila v/s Registrar of Political Parties & Others (Civil Case No. 6 of 2003) ambapo Jaji Mihayo aliamua kwamba:

“… I do not see anywhere in the Political Parties Act where the Registrar has power to bless or condemn meetings of political parties
or decisions that they make.”

Tafsiri ya uamuzi huo ni kwamba, “… Sioni popote katika Sheria ya Vyama vya Siasa ambapo Msajili ana madaraka ya kubariki au kupinga vikao vya vyama vya siasa au maamuzi ambayo vikao hivyo vinafanya.”

3. Kwa msingi huo, CUF hatukuomba ushauri kwa Msajili na hivyo tunamwambia ushauri wake abaki nao mwenyewe.

4. Kwa msingi huo huo, tunawataka wanachama wa CUF na wananchi wote
kutambua kwamba Msajili hana uwezo kisheria wa kusikiliza mashauri yanayohusiana na malalamiko dhidi ya maamuzi ya vikao vya vyama vya siasa na na kuyatolea uamuzi. Uwezo huo ni wa Mahakama. Hivyo tunawataka wanachama wa CUF na wananchi wote kupuuza ushauri huo wa Msajili na wamwachie mwenyewe ndoto zake na propaganda za kitoto.

5. Ni fedheha na aibu kwa Msajili wa Vyama vya Siasa mwenye hadhi ya Ujaji kukubali kutumiwa kiasi hicho na kushindwa hata kufanya rejea kuhusu uamuzi wa Mahakama Kuu tulioutaja hapo juu ambao umeweka bayana kwamba hana madaraka na uwezo aliojifanya anao. Itakumbukwa kwamba
Wabunge wa CUF walifanya mkutano na waandishi wa habari mjini Dodoma tarehe 15 Septemba, 2016 na kumtahadharisha Msajili asikubali kutumiwa kufanya alichokuwa anatakiwa kukifanya. Ni bahati mbaya sana kwamba amefanya kile kile ambacho Wabunge wa CUF walieleza kwamba walikuwa na taarifa kuwa ameagizwa kukifanya.

6. Tunajua kwamba baada ya hatua hiyo ya Msajili kufanya kazi asiyo na uwezo wala mamalaka nayo na katika kutimiza malengo ya wanaotuma, mchana wa leo Prof. Ibrahim Lipumba na kikundi chake cha wahuni
kimevamia Ofisi Kuu ya CUF, Buguruni, Dar es Salaam na kupiga watu na kufanya uharibifu wa mali. Tunamwambia Msajili wa Vyama vya Siasa atabeba dhamana kwa yote yaliyofanywa na yatakayofanywa na kikundi
hicho ikiwemo watu watakaoumizwa na uharibifu wa mali utakaofanywa kutokana na tamko lake hilo ambalo halina msingi wa kisheria.

7. Tunatambua yote haya yanafanywa kwa sababu watawala wameingiwa kiwewe kutokana na hatua kubwa ambazo zimefikiwa na CUF katika kupigania haki yake ya ushindi ulioporwa katika uchaguzi mkuu wa Zanzibar wa tarehe 25 Oktoba, 2015. CCM haijakaa sawa tokea iliposhindwa vibaya na CUF katika uchaguzi wa Rais, Wawakilishi na Madiwani mwaka 2015 na sasa imepata mfadhaiko kutokana na jinsi jumuiya ya kimataifa ilivyosimama kidete kutetea maamuzi hayo ya
kidemokrasia na haki za binadamu za Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla. Ni vyema watawala na kibaraka wao Prof. Ibrahim Lipumba na kikundi chake pamoja Msajili anayewatumikia wakatambua kwamba CUF haiyumbishwi na michezo yao ya kitoto na itaendelea kusimamia malengo yake ya kupigania haki za kidemokrasia za wananchi wa Zanzibar na Tanzania kikamilifu.

8. Chama kinasisitiza tena kwamba maamuzi ya Mkutano Mkuu Maalum wa Taifa wa tarehe 21 Agosti, 2016 na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la tarehe 28 Agosti, 2016 ni halali na yako pale pale na kwamba Prof.
Ibrahim Lipumba si Mwenyekiti wa CUF na wanachama waliosimamishwa au kufukuzwa wataendelea kubakia wamesimamishwa au kufukuzwa isipokuwa tu iwapo vikao vya Chama vitakapofanya maamuzi mengine.

9. Chama kinawataka viongozi wake wote na wanachama wake katika ngazi zote kuanzia Taifa hadi Tawi kuendelea na kazi zao za ujenzi wa Chama kama kawaida na kuendelea kufuatilia harakati za Chama chao kupigania ushindi wetu wa tarehe 25 Oktoba, 2015.

HAKI SAWA KWA WOTE

NASSOR AHMED MAZRUI
NAIBU KATIBU MKUU - CUF

Mtu Anayefanana na Mchezaji Zlatan Ibrahimovic Avamia Uwanjani Kwa Nguvu Kutaka Kumsalimia Zlatan Original

$
0
0
Mtu mmoja ambaye anafanana na Zlatan Ibrahimovic ameibuka uwanjani kwa kuwalaghai walinzi na kwenda hadi alipokuwa Zlatan mwenyewe wakati akiitumikia timu yake dhidi ya Leicester City.

Mtu huyo alifanikiwa kumvaa Zlatan na kusababisha watu kuangua kicheko wakiwemo wachezaji wa Man United waliokuwa benchi.

Mwisho, walinzi walimuwahi mtu huyo na kumuondoa katika eneo la uwanja.

Fahamu Umuhimu wa Kumfanyia Mtoto Massage

$
0
0
Mtoto anapozaliwa kuna vitu vingi anatakiwa kufanyiwa ili apevuke vizuri na nimekutana na hili moja kati ya hayo ambalo nsingependa likupite mtu wangu, Kituo cha habari cha Kenya ‘Citizen’ kimeripoti kuwa ukandaji wa mtoto mdogo unamanufaa mengi ambayo yametajwa kama kumtuliza mtoto, kumsaidia kuimarisha viungo vyake na kumpa usingizi mnono mtoto mchanga.

Nakusogezea video hapa chini inayoelezea zaidi ukandaji wa namna gani unatakiwa kwa mtoto unaoelezewa na mhudumu wa afya wa hospitali moja Malindi mjini, Kenya.

Kama Wewe Mwanaume Una Tatizo la Kufika Kileleni Haraka Kabla Mpenzi Wako Hajaridhika Hii Inakuhusu

$
0
0
Pre mature ejaculation ni nini?
Hii ni hali ambayo mwanaume anatoa mbegu mapema sana kipindi cha tendo la ndoa na mara nyingi huambatana na kushindwa kumridhisha mpenzi wake.

Tatizo hili limekua likiwapata wanaume wengi na kujisikia aibu mbele za wenzi wao pale wanaposhindwa kuendelea kabisa baada  ya hali hii kutokea.

Kimsingi  mwanaume anatakiwa achukue dakika nne mpaka nane kabla ya kutoa mbegu za kwanza lakini watafiti wanasema tatizo hili hugundukiwa mtu anapotoa mbegu ndani ya dakika moja au kabla ya dakika moja.

Tatizo hili huweza kutokea mara tu baada ya kubalehe,{primary pre mature ejaculation} mda mrefu baada ya kubalehe{secondary PE} au kutokana na aina ya mwanamke uliompata.{situational PE}

Chanzo ni nini?
Tatizo hili halina sababu za kitaalamu zilizofanyiwa utafiti zikakakubalika ila wanasayansi wanaamini sababu zifuatazo zinaweza kua chanzo kikuu cha tatizo hilo.

Kupiga punyeto au kujichua; 
mara nyingi watu wanaopiga punyeto hua wanafanya haraka kwa kujificha ili wasikutwe na mtu. tabiaile ya kulazimisha mbegu zitoke haraka huweza kuleta tatizo hili.

Kukaa muda mrefu bila kushiriki tendo la ndoa;
kukaa mda mrefu sana bila kushiriki tendo la ndoa husababisha mkusanyiko mkubwa wa mbegu za kiume ambazo zinaleta msisimko mkubwa na ukichelewa sana kushiriki tendo la ndoa zitatoka kwenye ndoto nyevu. kawaida mwanaume anatakiwa ashiriki tendo angalau mara nne kwa wiki.

Kuwa na wasiwasi wakati wa tendo la ndoa; 
mtu akiwa na historia ya kupata  hali hii kabla, hua hajiamini na kua na wasiwasi kwamba litatokea tena na matokeo yake hulipata kweli.

Madhara ya dawa zinazofanya kazi kwenye mishipa ya fahamu; 
baadhi ya dawa za usingizi, mawazo na zingine zinazofanya kazi kwenye mishipa ya fahamu huleta tatizo hili mfano amitriptyline.

Kurithi;
baadhi ya koo au familia fulani hurithi vimelea vya kua na ugonjwa huu kwa vizazi mbalimbali vya familia husika.

Magonjwa ya mfumo wa uzazi wa mwanaume mfano prostatitis.

Diagnosis{ kuutambua ugonjwa]
Mwanaume yeyote ambaye anatoa mbegu chini ya dakika moja au mbili ni muhanga wa hili tatizo na anatakiwa apewe matibabu.
 

Matibabu
Matibabu ya ugonjwa huu yamegawanyika sehemu kuu mbili kulingana na ukali wa tatizo husika.


Non pharmacological treatment{matibabu yasiyo hitaji dawa}:  matibabu haya hupewa watu ambao wanahimili mpaka dakika tatu bila kutoa mbegu.
Pharmacological treatment{matibabu yanayohusu dawa}: matibabu haya hupewa watu ambao hutoa mbegu ndani ya dakika moja baada ya kuanza kushiriki tendo la ndoa, watu hawa hushauriwa kutumia na mbinu zote mbili za matibabu.


Yafuatayo ni matibabu yasiyohitaji dawa.

Tumia condom:
Condom ni moja ya tiba nzuri ya tatizo hili kwani hufanya kazi kwa kupunguza hisia kali za mapenzi mtu anazozipata pale ambapo hatumii condom.

Kandamiza perineum kwa kidole:
Perineum ni eneo kati ya mkundu na korodani, ile sehemu ikikandamizwa na kidole huweza kuzuia kukojoa haraka wakati wa tendo la ndoa.

Punguza wasiwasi: 
hebu lifikirie tendo hili kama njia ya kujifurahisha sio njia pekee ya kutafuta kutoa mbegu,  hii itakusaidia kuondoa mawazo ya kutafuta mbegu na kuchelewa kumaliza.

Fanya taratibu: 
picha za ngono zinadanganya sana watu kwamba kulala na mwanamke lazima ufanye kwa haraka haraka kama mbwa. HAPANA; ukifanya taratibu ndio njia nzuri ya kumfikisha mwenzako na wewe kuchelewa kufika kileleni.

Badilisha style: 
ile style ya zamani ya kumlalia mwanamke kwa juu{missionary position} inaleta msuguano mkubwa kwenye kichwa cha uuume hivyo itakufanya ufike haraka sana.

Tumia style ya wewe mwanaume kutangulia chini afu mwanamke juu au kulala kwa upande wote mnaangalia upande mmoja hii itakusaidia sana kuchelewa

Toa mawazo kwamba unafanya ngono:
hebu jaribu kufikiria mambo mengine ya kikazi au masomo wakati unafanya tendo hilo, hii itakupunguzia hisia kali za mapenzi na kuchelewa kufika.

Fanya na kuacha:
hii ni ile hali ya kuzuia msuguano pale unapoona unakaribia kutoa mbegu kwa kama sekundi 30 kisha unaanza upya. Hakikisha haufiki “point of no return”. pointi ambayo huwezi kujizuia tena kumaliza.

Kandamiza sehemu ya shingo la uume:
hii sehemu ya shingo ya uume kwa chini ambayo ukiibana itakusaidia kuanza upya tena kihisia. Nimetumia shingo la uume kwasababu najua uume hauna mabega.

Tumia kilevi:
unywaji wa pombe mfano bia mbili kwa siku kwa wanaume pombe hupunguza kidogo nguvu ya mishipa ya fahamu na kufanya mtu aliyekunywa kuchelewa sana kufika kileleni, [watu wanaokunywa pombe lazima mtakubaliana na hili] hivyo unaweza kunywa bia, wine au whisky nusu saa kabla ya tendo na kuondoa shida hii.

·     
Matibabu ya kutumia dawa.
hizi hupewa iwapo tatizo lako ni kubwa sana na hizo njia hapo juu zimeshindikana...

1. Serotonin reuptake inhibitors mfano paroxetine na  clomipramine zimefanya kazi nzuri ya kuzuia kufika kileleni haraka..... humezwa saa moja kabla ya tendo la ndoa.

2. anesthetic creams: hii hupakwa kwenye kichwa cha uume saa moja kabla ya tendo la ndoa kuzuia msisimuko na kufanya mwanaume achelewe kufika kileleni wakati wa tendo.

Madhara ya Kutofanya Tendo la Ndoa Muda Mrefu

$
0
0
Habari zenu, nimeona niwaletee hili nina imani mtajifunza hasa kwa wale wasiofahamu,Ukikaa Muda Mrefu bila Kufanya tendo la Ndoa madhara yake ni kama haya:

Hasira za mara kwa mara katika mambo madogo,
kupendelea sana kuangalia picha za uchi,
Kusahausahau,
Kupendelea story za mapenzi,
Kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi (Mke),
Kupenda kurukiarukia mambo ya watu wengine (tabia ya kufuatilia mambo yasiyokuhusu),
Kuumwa na kichwa,
Kukakamaa mgongo (wanaume),
Kuingiliwa kirahisi na jini mahaba,
Kupoteza umakini ktk kazi (efficiency),
Siku ukikutana kimwili na mwenye virusi bila kinga utaambukizwa kirahisi mno,
Waweza ku-develop tabia mpya ambayo hukuwahi kuwa nayo ili iwe mbadala

kama ulevi n.k.

Balaa Jipya la Wenye Vyeti Bandia Serikalini....Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili ya Septemba 25

$
0
0


Balaa Jipya la Wenye Vyeti Bandia Serikalini....Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili ya Septemba 25

Ushahidi Huu Hapa Mungu Amekataza Mapenzi Kinyume na Maumbile

$
0
0
Kitabu cha Biblia kinaeleza waziwazi huu uchafu unaofanywa na binadamu kama matendo ya ushoga,kutembea na binamu yako pamoja na wake za watu,kupitia vifungu vifuatavyo :

USHOGA NA ULAJI TIGO MAMBO YA WALAWI 20:13 Tena mtu mume akilala pamoja na mtu mume,kama alalavyo na mtu mke,wote wamefanya machukizo hakika watauwawa

KUTEMBEA NA MKE/MUME WA MTU MAMBO YA WALAWI 20:10 Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine,na mwanamke aziniye na mtu mume hakika watauwawa

NA WALE MNAOKULA KUKU NA MAYAI YAKE [MAMA NA MWANA] MAMBO YA WALAWI 20:12 Na mtu mume akilala na mkwewe mwanamke wote wawili hakika watauwawa,Tena mtu mume akimuoa mke pamoja na mama yake ni uovu mkuu

WALE WANAOTEMBEA NA WANYAMA MAMBO YA WALAWI 20:15 Tena mtu mume akilala na mnyama, na mwanamke akimkaribia mnyama yeyote na kulala pamoja naye,mtamwua huyo mwanamke

KUTEMBEA NA BINAMU YAKO MAMBO YA WALAWI 20:19 Usifunue utupu wa umbu la mama yako wala umbu la baba yako

Tunakumbushana tuu Jamani

By Eddy Love

Faiza Ally: Nahitaji Mwanaume Anipe Ujauzito Nipate Mtoto wa Kiume

$
0
0

Mwanamama mzazi mwenza wa mheshimiwa Joseph Mbilinyi Sugu atangaza kutafuta mwanaume ili ampe ujauzito na hatimaye apate mtoto wa kiume kwa kuwa ana nguvu za kutosha za kulea

Haya sasa kazi kwenu ambao hamna mademu, toto limejitokeza hilo changamkia fursa kabla hajabadili mawazo

NB :Awe mtanashati siyo mtu wa mchezo mchezo
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images