Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli atimiza ahadi yake kwa Balozi Omben Sefue...Amteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi Chuo cha Diplomasia

$
0
0
Hatimaye Rais John Magufuli ametimiza ahadi yake kwa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue baada ya kumteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Cha Diplomasia.

Balozi Sefue amepata uteuzi huo jana ikiwa ni miezi kumi tangu Rais Magufuli atengue uteuzi wake [kama Katibu Mkuu Kiongozi]kwa sababu ambazo hazikutajwa huku akiahidi kumpangia kazi nyingine na nafasi yake ikajazwa na Balozi John Kijazi, .

Aidha, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Waziri wa wizara hiyo, Balozi Augustine Mahiga amewateua wajumbe sita wa Bodi ya chuo hicho cha Diplomasia.

Wajumbe hao ni Balozi Begum Taj, Balozi John Haule, Juma Salum, Profesa Mohamed Bakari, Profesa Innocent Zilihona na Mathias Abias.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza rasmi Oktoba 6 mwaka huu.

Leo ni Siku ya Kumbukumbu ya Kuzaliwa Kwa Aliyekuwa Rais wa Tanzania, Mh. Jakaya Mrisho Kikwete

$
0
0
Leo ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa aliyekuwa Rais wa Tanzania, Mh. Jakaya Mrisho Kikwete.

Neno moja kwake kumtakia heri huku ukimtakia maisha marefu zaidi

Diamond Apata Shavu Nono , Kutumbuiza na Neyo United Kingdom Katika Miji Sita

$
0
0

Diamond platnumz ameendelea kukuza mziki wake baada ya kupata shavu kubwa la kutumbuiza kwenye majukuu makubwa nchi Uingereza akiwa na mkali kutoka marekani Neyo.
Mtandao wa Revolt Africa umetoa taarifa hiyo.
Diamond mwenyewe kwenye kipindi cha playlist cha Times FM alisema amekuwa karibu na Neyo na kuna mambo makubwa anajifunza na wanafanya pamoja
Ziara hiyo itafanyika kwenye miji 6 uko United Kingdom

Mboto Afungukia Kubanjuka Na Aunt Ezekiel

$
0
0
KAMA kawa Mtu Kati ipo ‘live’ leo tena, ambapo baada wiki iliyopita kukuletea mwanadada mkongwe anayefanya vizuri kwenye Tasnia ya Filamu Bongo, Halima Yahaya ‘Davina’ wiki hii inakusogezea mvunja mbavu mwenye jina kubwa katika ardhi ya JPM, Haji Salum ‘Mboto.’

Huyu ni mchekeshaji mkongwe kidogo aliyeanzia sanaa yake katika Kundi la Kaole Sanaa Group mwishoni mwa miaka ya tisini, akiigiza na kina Max (marehemu), Zembwela, Bambo na wengine wengi.
Kuhusu mafanikio, maisha binafsi, anatoka na staa na demu wa aina gani pamoja na mengine mengi ambayo huyafahamu kutoka kwa mkali huyu, katika Mtu Kati ya leo anafunguka kila kitu, tena kwa kujiachia, ungana naye;

mboto2-1Komediani kiraka Bongo, Haji Salum almaarufu Mboto.

Mtu Kati: Mashabiki wako wangependa kufahamu matumizi yako ya pesa kwa siku yanakuaje? Unatumia kama shilingi ngapi?
Mboto: Siku hazilingani, inategemeana siku hiyo nitakuwa nahitaji kupata mahitaji gani. Kwa hiyo sina kiwango kamili ambacho naweza kusema huwa ninatumia, lakini kama unavyofahamu maisha ya Bongo ni ghali kwa hiyo mfuko huwa unatoboka sawasawa.



KUOA VEPEE?
Mtu Kati: Umeoa na una watoto wangapi?
Mboto: Ahhaaa haaa! Bado sijaoa, ila niko mbioni kufanya hivyo kuhusu mtoto ndiyo ninaye mmoja tu.
Mtu Kati: Miaka miwili nyuma umewahi kufanya mahojiano na sisi na ukadai kuwa uko mbioni kuoa lakini mpaka sasa bado upoupo, imekaaje hapo?
Mboto: Ni kweli lakini ndiyo kujipanga kwenyewe, miaka miwili nyuma si mingi, sihitaji kukurupuka juu ya hili ndiyo maana nafanya mambo taratibu.

FILAMU ZINAMLAZA NJAA!!
Mtu Kati: Vipi, kutokana na mdororo wa kiwanda cha filamu Bongo, pesa unayopata kwa kuuza filamu inajitosheleza kumudu mahitaji yako?
Mboto: Ndiyo inajitosheleza. Unajua japo soko limedorora inategemeana na muvi unatengenezaje, kwa hiyo kwa upande wangu ninatengeneza muvi bora ambazo zinapata soko na kuniingizia mkwanja.
Mtu Kati: Muvi gani ambayo imekuingizia mkwanja kuliko zote?
Mboto: Nampenda Mke Wangu, iliuza sana lakini siwezi kutaja iliniingizia shilingi ngapi.
Mtu Kati: Kwa muvi unaigiza kwa shilingi ngapi na kwenye nyimbo vepe?
Mboto: Kwenye muvi naanzia kuchukua shilingi milioni 3 na kwenye nyimbo naanzia laki tatu.

KUBANJUKA NA AUNT EZEKIEL JE?
Mtu Kati: Kuna madai kuwa huwa unatumia ukaribu wako na Aunt Ezekiel kubanjuka naye na si kuigiza hiyo vepe?
Mboto: Ha! Ha! Haaa! Hayo madai hayana ukweli, Aunt ni mtu wangu wa karibu, nampenda sana kwa sababu ni mtu ambaye tumefanya kazi nyingi na tunaelewana!
Mtu Kati: Huo ukaribu wenu vepe?
Mboto: Ni wa kazi tu, halafu kitu ambacho watu hawakijui, Aunt anafahamu udhaifu wangu wote na mimi ninafahamu tunapokuwa kwenye kazi. Kwa hiyo kuna muda unakuta tunapokuwa lokesheni naweza kusahau kitu yeye akanikumbushia katika mwendelezo bila mtu yeyote kufahamu, na mimi hivyohivyo.

KAPITIA WAREMBO KIBAO BONGO MUVI?
Mtu Kati: Inasemekana pia miongoni mwa wasanii viwembe, wewe pia umo. Kwamba umepitia warembo wengi Bongo Muvi!
Mboto: Si kweli. Sijawahi kuwa hata na mmoja wao. Mimi ni mtu ambaye sipendi kuwa na mpenzi sehemu ninapofanyia kazi, kwa hiyo madai hayo ni ya uongo.
Mtu Kati: Kwani mpenzi wako ni wa aina gani?
Mboto: Mwanamke wa kawaida tu ambaye hata hayupo kwenye sanaa, anapenda kuwa mtazamaji tu na anafanya ishu zake zinginezingine.

HEE! ANAIKUMBUKA IVETA?
Mtu Kati: Kati ya nyimbo nyingi ulizoigiza, wimbo gani unaukubali kazi uliyoifanya?
Mboto: Iveta ya Sajna. Unajua wakati ule teknolojia ilikuwa chini, lakini jambo la kufurahisha ile kazi ilikuwa bora na ilitokea kupendwa mno hapa Bongo na Afrika Mashariki kwa jumla. Hata hivyo, kazi nyingine ni kazi ya Tunda Man iitwayo Mama Kija.

WANAWAKE WANAMSHOBOKEA?
Mtu Kati: Wewe ni mtu maarufu, upande wa usumbufu kutoka kwa kina dada vepe?
Mboto: Usumbufu upo, hata hivyo nafahamu namna ya kukabiliana nao.
Mtu Kati: Ushawahi kutongozwa na mrembo yeyote Bongo Muvi?
Mboto: Mmmmh! Hapana!

MAFANIKIO NAYO?
Mtu Kati: Mpaka sasa umevuna nini kwenye sanaa?
Mboto: Mambo mengi. Umaarufu unaonisaidia kwenye biashara zangu. Nina vyombo vya usafiri barabarani vinavyopiga kazi ambavyo sidhani kama kuna umuhimu wa kuvitaja, naendesha maisha yangu na mambo mengine mengi.
Mtu Kati: Lolote kwa wapenzi wa kazi zako.
Mboto: Wazidi kunipa sapoti, sitawaangusha.

Waandaaji wa Show ya Chriss Brown Mombasa Washindwa Kuelewana na Vanessa Mdee, Atangaza Kutofanya Show Hiyo

$
0
0

Mwambaji Vanessa Mdee Ametangaza kuwa hatakuwepo kwenye show kubwa ya Mombasa ambayo awali ilitangazwa atakuwepo sambamba na Chriss Brown, Ali Kiba na Wengine..Sababu alizozitoa ni kuwa waandaaji wa Show hawakutimiza makubaliano yao ya mwanzo.

Ameandika haya kupitia ukurasa wake wa Instagram:

Video: Mabusu ya Ruby na Kijana Anayedaiwa Kuwa Mpenzi wake

$
0
0
Mkali wa wimbo ‘Na Yule’ Ruby ameshare video mbele ya mashabiki wake zaidi ya 260,000 katika mtandao wa instagram akibusiana na kijana anadaiwa kuwa ni mpenzi wake.

Muimbaji huyo alikuwa msiri kwenye mahusiano yake. Wiki hii amepost picha taofauti tofauti za kijana huyo huku akiandika ujumbe wa kimahaba hali ambayo imewafanya mashabiki wake kuhisi huwenda ni mpenzi wake.

Katika moja ya picha muimbaji huyo aliandika: Comedian wangu 👑 @_mantogoro love you baba 💋😘nyakunyaku stay away. Katika picha nyingine aliandika “My world” huku akimtag kijana huyo.

Muimbaji huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake ‘Wale Wale’ aliouachia wiki chache zilizopita.
Bongo5

Sababu ya Rais Magufuli Kutishia Kumfukuza Kazi Mtoto wa Dada yake

$
0
0
Rais Dkt John Pombe Magufuli ametishia kufukuza kazi mtoto wa dada yake kutokana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kutopeleka umeme katika kiwanda kipya cha kusindika matunda cha Bakhresa.

Rais Magufuli alisema jana alipokuwa akifungua rasmi kiwanda cha kusindika matunda cha Bakhresa kilichopo Mwandege, Mkuranga mkoani Pwani.

Wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi, kiongozi mmoja wa kiwanda hicho akieleza changamoto wanazokumbana nazo alisema kuwa tatizo la umeme ambapo wameongea na TANESCO lakini hadi leo umeme haijafikishwa kiwandani hapo hivyo kuwalazimu kutumia jenereta kuendesha mitambo kitu kinachopelekea kuongezeka kwa gharama za uzalishaji.

Aliposimama kuhutubia Rais Magufuli aliuliza kama kuna kiongozi yeyote wa TANESCO mkoa wa Pwani ndipo akasimama mtoto wa dada yake. Rais Magufuli akamwambia anafahamu kuwa amefanya kazi nzuri alipokuwa Kagera na Tanga na kuwa anataka ahakikishe umeme unafika katika kiwanda hicho la si hivyo ataanza kumtumbua yeye ambaye ni mtoto wa dada yake.

Rais Magufuli alielekeza maswali mawili kwa TANESCO wakati wa hotuba yake, kwanza, kama TANESCO wanania ya kufanya biashara, kwanini hawapeleki umeme kiwandani hapo kwa sababu ni fursa ya kibiashara, pili aliuliza kama TANESCO wanania ya kuona Tanzania inakuwa ya viwanda, kama wanania, kwanini hawapeleki umeme kiwandani hapo.

Rais Magufuli ametoa miezi miwili kwa TANESCO kuhakikisha kuwa wanafikisha umeme kiwandani hapo kama wanataka kuendelea na kazi zao.

Kuhusu ombi la uongozi wa kiwanda hicho kutumia  gesi asilia inayopita jirani na kiwanda hicho, Rais Magufuli alisema kuwa watakaa na Wizara ni Nishati na Madini na Wizara ya Viwanda na Biashara kuona namna wanaweza kulishughulikia hilo.

Diamond Afunguka Asema Zari Ndiye Model Aliyewahi Kumlipa Hela Nyingi

$
0
0
Mkali wa wimbo ‘Salome’ na Mkurugenzi wa WCB, Diamond Platnumz amesema katika ma Model ambao amewahi kuwalipa hela nyingi ni Zari ambaye ni mpenzi wake na Mama watoto wake pia.

Diamond Platnumz akiongea katika kipindi cha The play list cha Radio Times Fm na mtangazaji Lil Ommy baada ya kuulizwa ni model gani amewahi kumlipa hela nyingi.

“Zari ndo mtu ni mlipa hela nyingi katika video ya “Utanipenda” unajua hata kama ni Family ni mpenzi wangu lakini inapokuja kazi lazima iwe kazi japo kuwa nilicho mlipa haikuwa thamani yake japo alifanyia kidogo fever lakini nilimlipa zaidi ya Milion kumi ndo model ambaye nimewahi kutoa hela nyingi tokea nimeanza kufanya muziku” alisema Diamond.

KIM Kardashian Aapa Kutoonesha Tena Mali zake Kwenye Mitandao ya Kijamii

$
0
0
Kim Kardashian ameapa kutoonesha tena mali zake kwenye mitandao ya kijamii.

Hiyo ni baada ya watu wengi kudai kuwa ndio chanzo cha kuvamiwa Jumatatu hii jijini Paris na kuporwa mali zenye thamani za dola milioni 11 kwa mtutu wa bunduki.

Vyanzo vimeuambia mtandao wa TMZ kuwa Kim amekubali ni kweli alikuwa amezidisha kuringishia mali zake kwenye mitandao hiyo. Muda mfupi kabla ya kuvamiwa, Kim aliionesha pete ya $4.5m aliyonunuliwa na mume wake Kanye West. Pete hiyo ilikuwa miongoni mwa vitu vilivyoibwa.

TMZ imedai kuwa Kim atakuwa mapumzikoni mwa mwezi mmoja na akirejea atakuwa na mabadiliko makubwa katika jinsi anavyotumia mitandao ya kijamii.

Jerry Muro arudi tena TBC kutangaza

$
0
0
Yule msemaji mkuu wa Yanga African hatimaye amerudi tena kwenye kazi yake ya utangazaji aliyokuwa akifanya hapo awali katika television ya Taifa.

Chanzo: TBC

Meneja wa Diamond Apanda Ndege Kumfuata Chriss Brown Mombasa Kukamatia Fursa...

$
0
0
Wadau wa muziki wa bongofleva nadhan wote mnaelewa kuhusu ushindani unaoendelea kati ya wanamuziki machachari kabisa nchini..katika pitapita zangu kwenye mitandao ya kijamii nimeona meneja wa gwiji wa huu muziki Diamond platnumz ameandika kwamba anaelekea mombasa ambako gwiji Alikiba atapafomu akiwa pamoja na Chris brown kutoka America na wizkid,na kwa maoni ya watu wengi wanasema kwamba Sallam anaenda kumnasa Chris brown ili afanye kolabo na Chibu kama kipindi kile kwa Neyo..Nikiwa kama mpenzi bongofleva naomba kingkiba afanye kitu kuhusu kolabo na CB na asichezee bahati..

Vanessa Mdee awalegezea waandaaji wa show ya Chris Brown Mombasa, akubali kutumbuiza

$
0
0
Waandaji wa Mombasa Rocks Music Festival walitikiswa na Vanessa Mdee – wakatikisika. Muimbaji huyo amekubali kupanda jukwaani kutumbuiza Jumamosi hii, shukrani kwa jitihada zilizofanywa na gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho.



Hii ni taarifa rasmi kutoka kwa waandaji:

Vanessa Mdee Management announces that the Tanzanian songstress, Vanessa Mdee (Vee Money), will be performing at the anticipated Mombasa Rocks Music Festival (Saturday, 8th October), alongside Chris Brown and Wizkid in Kenya, Mombasa.

Contrary to previous reports highlighting disagreement between her and the festival’s management, Vanessa Mdee management would like to now confirm that both parties have reached an understanding thanks to Mombasa Governor Ali Hassan Joho’s involvement.

Ahead of her anticipated arrival and performance in Kenya, Vanessa Mdee says, “Calling out all the Vee Money fans around East Africa, Kenya and Mombasa to come dance to their favourite hits like “Niroge” and “Hawajui”. I am very excited to be performing in Mombasa for the first time! It will be special for my fans!

Taarifa Kuhusu Mama na Watoto Wake Wanne Waliyofariki Dunia Baada ya Kula Chakula Kilichokuwa na Sumu

$
0
0
Mama na watoto wake wanne wakazi wa Kijiji cha Nyamilanda, Kata ya Kyebitembe, Wilaya ya Muleba, mkoani Kagera, wamefariki dunia jana baada ya kula ugali unaosadikiwa kuwa na sumu.

Kumekuwapo na taarifa za kukanganya juu ya tukio hilo, wakati nyingine zikidai kuwa unga uliotumiwa kupikia ugali huo ulitoka kwa mama mkwe wa mama huyo anayeishi jirani naye, nyingine zilidai kuwa alitengeneza mwenyewe na kabla ya kupika alikuwa ameuanika na kisha kuuchekecha.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Damasen Kalori, aliitaja familia iliyofikwa na tukio hilo la kusikitisha kuwa ni ya mke mdogo wa Julius Gerald. Aliwataja waliokufa kuwa ni Yulitha Julias (35) ambaye ni mke wa Gerald na mama wa watoto; Aujen Julius (14) Siteus Julius (10) Gebora Julius (4), Pascal Julius (miezi mitano). Na inasemekana kwamba walikula ugali huo saa tisa mchana na mara baada ya kula wakaanza kutapika mfululizo.

Kwa mujibu wa taarifa hizo watu hao walifariki wakati wakipelekwa Kituo cha Afya cha Kimeya kilichopo jirani na kijiji hicho.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinadai kuwa kabla ya kufikwa mauti hayo, mama huyo aliandaa mboga aina ya dagaa na kisha kuchekecha unga ambao alikuwa ameuanika kwa ajili ya kupika ugali.

Hata hivyo, taarifa nyingine zinadai kuwa baada ya kuandaa mboga alikwenda kwa mama mkwe wake nyumba jirani kwa ajili ya kuchukua unga wa muhogo ambao aliutumia kupika ugali huo.

“Walipoanza kula wakatapika na kuanza kuhangaika hatimaye wananchi wakafika lakini juhudi za kuokoa maisha yao hazikuzaa matunda, nilipofika nilikuta hali ni mbaya walikuwa wakitapika sana na tulitoa taarifa polisi lakini walipofika wakati wanawakimbiza hospitali ndogo ya Kimeya kwa bahati mbaya wakafariki,” alisema mmoja wa majirani.

Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kyebitembe, Mohamed maarufu kama ‘Mabomu’, alisema baada ya kupata taarifa hizo alifika katika nyumba hiyo na kukusanya vielelezo vyote ikiwa ni pamoja na kuimarisha ulinzi kwa hofu ya kutokea vurugu.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera, Agustino Olomi, alikiri kupokea taarifa ya tukio hilo.

Olomi alisema hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa kutokana na tukio hilo ambalo alisema tayari limefikishwa kwa wataalamu kwa ajili ya uchunguzi.

“Uchunguzi wa wataalamu wa afya unaendelea ili kujiridhisha na kutambua aina ya sumu iliyotumika hadi watu hao wakapoteza maisha yao.”

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Mhandisi Richard Ruyango, alisema uchunguzi umeonyesha watu hao walikula chakula chenye sumu.

Kwa mujibu wa Runyango, hata hivyo sumu hiyo haikubainika kwa haraka hivyo sampuli imechukuliwa na kupelekwa ofisi ya Mkemia Mkuu Dar es Salaam.

Mkuu huyo wa wilaya amewataka wananchi katika Tarafa ya Kimwani kuwa makini na vyakula wanavyokula kwani hilo ni tukio la tatu la familia kula vyakula vyenye sumu na kupoteza maisha.

“Kitendo hiki kinasikitisha na si mafundisho ya Mungu licha ya waliofanya hivyo kuwa miongoni mwa waumini wa kiroho kwani wangetumia sheria kushtakiana kama hakuna usalama,” alisema Ruyango.

Ruyango alisema Jeshi la Polisi na kamati za ulinzi na usalama za kijiji na kata zimepewa jukumu la kufanya uchunguzi na kubaini waliohusika ili wachukuliwe hatua za kisheria kwani wametenda kosa kubwa la mauaji kinyume cha sheria.

Wakati mkuu huyo wa wilaya akisema hayo, taarifa kutoka eneo la tukio zinadai kuwa mke huyo mdogo kabla ya kufikwa na mauti hayo alikuwa na mgogoro na mke mwenzake kuhusiana na fedha ambazo zimekuwa zikitolewa na Tasaf katika kaya za watu masikini.

“Mke mdogo ndiye alikuwa ameandikishwa kuchukua fedha za Tasaf  na mgogoro ulianza pale mgawo wa kwanza ambapo mke mkubwa alilalamika kupata fedha kidogo, lakini baadaye mke mdogo aligundua kuwa mke mwenzake hahusiki katika mgawo huo hivyo fedha zilizofuata za mwezi wa tisa hakumpa,” alisema Mwenyekiti wa kijiji hicho, Damasen Kalori ambaye pia ni kaka wa marehemu.

Tukio kama hilo lilitokea mwaka jana Kata ya Kasharunga, Tarafa ya Kimwani Jimbo la Muleba Kusini ambapo watu wanne wa familia moja walifariki dunia baada ya kula chakula chenye sumu.

Katika tukio hilo watu watatu walisalimika baada ya kukimbizwa kituo cha afya na kupatiwa matibabu. – MTANZANIA

Bodi ya Mikopo (HESLB ) Yasitisha Mikopo Ya Walimu Wanafunzi Waliompiga Mwanafunzi Mbeya

$
0
0
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inautaarifu umma kuwa imesitisha mikopo ya elimu ya juu iliyokuwa ikitolewa kwa walimu-wanafunzi wanne waliosimamishwa masomo kwa kuhusika katika tukio la kumshambulia na kumuumiza mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kutwa ya Mbeya. Walimu hao walikuwa katika mafunzo ya vitendo.

1. Frank Msigwa - Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE)

2. John Deo- Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE)

3. Evance Sanga - Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE)

4. Sante Gwamaka - Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)

Kwa utovu huo wa nidhamu, wanafunzi hao wamesimamishwa masomo na mamlaka husika kwa hiyo wamepoteza sifa za kuendelea kupokea mikopo.

Mikataba inayosainiwa na wanufaika wa mikopo inawataka wanufaika kuzingatia masharti kadhaa ikiwa ni pamoja na nidhamu na kufuata sheria na taratibu za vyuo na mamlaka halali.

Aidha, kwa mujibu wa taratibu za kukopeshwa, wanafunzi hawa watatakiwa kuanza kurejesha kiasi walichokopeshwa mara moja.

Bodi ya Mikopo inawakumbusha wanufaika wanaoendelea masomo kuzingatia masharti ya ukopeshwaji na kuheshimu sheria, kanuni taratibu na kuwa mfano mwema katika jamii. Mikopo na ruzuku zinazotolewa na Serikali ni kwa ajili ya kuwaandaa kuwa raia wema, waadilifu, na wachapa kazi ili kujenga uchumi imara na ustawi kwa wote.

Imetolewa na:
Abdul-Razaq Badru
Mkurugenzi Mtendaji

Ijumaa, Oktoba 7, 2016

Video: Donald Trump Matatani Kwa Kauli ya Kejeli Dhidi ya Wanawake Aliyoitoa Mwaka 2005

$
0
0
Mgombea wa Urais wa Marekani, Donald Trump ameingia matatani kwa mara nyingine tena baada ya kusambaa kwa video ya mwaka 2005 ambayo anasikika akiongea maneno makali ya jinsi anavyowachezea wanawake.

Kufuatia kusambaa kwa video hiyo iliyozusha hasira kali kwa Wamarekani, Trump ameomba radhi.

Kwenye video hiyo Trump anasikika akisema kuwa unaweza kufanya chochote kwa wanawake na kama ni staa hawawezi kukataa. Anasikika pia akisema jinsi alivyotaka kulala na mke wa mtu na jinsi anavyopenda kuwabusu wanawake warembo kila anapowaona.

Viongozi wa juu wa Republicans wamelaani maneno hayo. Mpinzaki wake, Hillary ameyaaita ya kushtusha.

“We cannot allow this man to become president,” aliandika kwenye Twitter.

Desmond Tutu Aomba Kusaidiwa Kufa Atakapougua

$
0
0
Askofu mkuu wa Afrika Kusini Desmond Tutu amesema katika ujumbe wake wa siku yake ya kuzaliwa katika gazeti la Washington Post kwamba angependelea kusaidiwa kufa.

Katika ujumbe huo Tutu alisema: Nimejiandaa kufa na nimesema wazi singependelea kuendelea kuishi kwa gharama yoyote.Ningependa kutibiwa na mapenzi na kuruhusiwa kufariki vile nipendevyo.Watu wanaokufa wanapaswa kuwa na haki ya kuchagua vile na lini watakavyokufa.Ninaamini kwamba,mbali na uuguzi uliopo ,chaguo lao linafaa kushirikisha kusaidiwa kufa kwa heshima.

Alitangaza hatua yake ya kuunga mkono wazo hilo baada ya kulipinga 2014.
Habari kwamba Desmond Tutu angependa asaidiwe kufa sio swala la kushangaza nchini Afrika Kusini.

Swala la kusaidiwa kufa limeigawanya nchi hiyo kwa kipindi cha muda sasa.
Mwaka uliopita mahakama kuu katika mji mkuu wa Pretoria iliamuru kwa kumpendelea mgonjwa mmoja aliyekuwa anaugua saratani kupitia kiasi, Robin Strasham-Ford ambaye alikuwa ametoa ombi la kusaidiwa kufa.

Alikuwa amesalia na wiki mbili pekee kufariki na alitaka sheria irekebishwe ili asaidiwe kufa bila ya kuwepo kwa kesi.

Sheria ilikuwa wazi,daktari yoyote ambaye angemsaidia mgonjwa kufariki angepewa hukumu ya miaka 14 jela.
Taifa hilo halina sheria ya kusaidiwa kufa,huku katiba ikilinda haki ya kila mmoja ya kuishi.

Ahukumiwa Kifungo cha Maisha Jela kwa KUMLAWITI Mgoni Wake Aliyemfumania na Mkewe

$
0
0
Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemhukumu kifungo cha maisha jela, Erick Kasila (39) baada ya kupatikana na hatia katika mashtaka matatu likiwamo la kumlawiti mwanamume kwa madai kuwa alimfumania gesti na akiwa na mke wake.

Kasila anadaiwa kumlawiti Idd Kambi katika nyumba ya kulala Wageni ya Maembe, Yombo Kiwalani, Wilaya ya Ilala na kumpiga picha za utupu na kutisha kunitumia katika mitandao ya kijamiina kumnyang’anya nguo alizovaa, fedha, laptop na viatu.

Mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo, Juma Richard (31) alihukumiwa kifungo cha miaka 14 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlazimisha mlalamikaji kumnyonya uume wake na kumtaka kusaini karatasi ya ahadi ya Sh1 milioni ili asisambaze picha walizompiga wakati wakimlawiti, ambazo hata hivyo, walizisambaza katika mitandao ya kijamii.

Akisoma hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Said Mkasiwa alisema ameridhishwa na ushahidi wa mashahidi watano dhidi ya washtakiwa na vielelezo vya picha zinazoonyesha mlalamikaji alikuwa analawitiwa, nyingine zikionyesha mshtakiwa akimlazimisha mlalamikaji amnyonye sehemu zake za siri.

Akipitia baadhi ya ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, Hakimu Mkasiwa alisema kulawitiwa kwa mwanamume huyo ni baada ya kukutwa na Sanifa Bakari ambaye ni mke wa Kasila.

Kabla ya hukumu hiyo, upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Silvia Mitanto uliiomba Mahakama kutoa adhabu kali dhidi ya washtakiwa hao kwa kitendo walichokifanya ambacho kimemuathiri mlalamikaji kisaikolojia.

Washtakiwa walipopewa nafasi ya kujitetea kwa nini wasipewe adhabu kali, walishindwa na badala yake waliomba nakala ya hukumu.

Wastani wa Kiasi Cha Fedha Ambacho Mwanamuziki Diamond Huingiza Kwa Siku

$
0
0
Maneno mengi sana yamesemwa kuhusu kiasi cha fedha analichonacho Naseeb Abdul a.k.a Diamondo Platnumz na vile vile unaweza kumuita Chibu Dangote au Baba Tiffah, na wengine kufikia hatua ya kusema anaweza kuwa ndiye msanii tajiri Afrika Mashariki kwa sasa.

Inasemekana kwamba, kwa kuangalia yote anayoyafanya msanii huyo unaweza kuwa na mwanga kiasi fulani wa kujua anaingiza kiasi gani.

Diamond Platnumz, kwa siku anaingiza wastani wa Sh. milioni 20 kutokana na kupakuliwa kwa nyimbo zake zilizoko kwenye mitandao: Kumbuka hii ni pembeni kabisa na shows anazofanya au malipo anayopokea kutoka kwenye makapuni anayoyafanyia matangazo kama Vodacom, Red Gold na NMB.

Na mpaka hapo utaamini sasa ule usemi wake wa siku zote kwamba muziki ni biashara! Na wasanii wengine hawana budi kumuiga Diamond Platnumz, wawe na wivu wa maendeleo na sio kutamani kumshusha alipo sasa.

PICHA:Kijana Aliyeota Mkia Mgongoni Afanyiwa Upasuaji....

$
0
0
Kijana mwenye mkia wa sentimita 20 uliyoota chini ya uti wa mgongo wake amefanyiwa upasuaji ili kuondoa mkia huo ambao Ulianza kujitokea katika mgongo wa kijana huyo mwenye miaka 18 baada ya siku yake ya 14 kuzaliwa.

Yeye na familia yake kutoka Nagpur nchini India walifanya swala hilo kua siri kwa sababu walikuwa na wasiwasi angechokozwa na wenzake, na sasa wanataka kuonana na daktari baada ya mkia huo kuendelea kukua na kuota mfupa kwa ndani.

Mkia huo unadaiwa kuwa mrefu kuwahi kutokea kwa mwanadamu licha ya kuwa kesi kama hivyo ni vichache.

Madaktari wanasema kuwa kijana huyo huenda aliota mkia huo ndani ya tumbo la mamake kutokana na kasoro katika uti wa mgongo, lakini ukaja kuonekana nje baada ya kijana huyo kuwa mkubwa.


Amber Lulu na Gigy Money Hapatoshi..Amber Adai Gigy Money Ana Fangasi Sugu

$
0
0
Baada ya tetesi kuwa Mrembo Amber Lulu amekatwa Arusha na Madawa ya kulevya Gigy Money alihojiwa na Soudbrown kwenye U Heard na Kuongea maneno ambayo hayakumfurahisha Amber lulu...Sasa Amber Lulu Ameibuka huko alipo na kuandika haya:

"Muda ambao unaangaika kutafuta kiki ungekuwa unajifunza kuosha k na kutibu izo fangasi suguu ulizo nazo @gigy_money don't compare with me iz levels chokoraaaa paka la ambiance stay away from me"

Viewing all 104795 articles
Browse latest View live




Latest Images