Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Alikiba Ana Mziki Mzuri Lakini Kuna Walakini Mahali...Hivi Hana Timu ya Kuhakikisha Kila Kitu Kipo Sawa?

$
0
0
Ule usemi wa kwenye miti hakuna wajenzi nimeliona kwenye hiyo Show ya Mombasa hasa baada ya Ali Kiba kuhojiwa na kipindi cha Mseto... kwa kweli huyu msanii anahitaji Management. Anajisikia sana anategemea mashabiki sana anasahau hata mitume walisalitiwa na watu "Eti sallam alikuwa backstage" Swali la kujiuliza hapo timu yake ilikuwa inafanya nini mpaka Sallam Akafanya yake kuzima mziki?

Huyu jamaa hayupo kibiashara amejidhalilisha sana kwa kuonyesha team ya Diamond ipo vizuri sana kiasi cha kumdhalilisha. Hivi huyo msanii wa Marekani na Alikiba mbona wapo sawa tu? Hakupaswa kurudi jukwaani kuimba.

Ni muda umefika akapata management amabayo inajua ataongea nini atavaa nini alale wapi. Na kama anayo management awafute kazi. Nadhani Alikiba anahitaji msaada haiwezekani aende Kenya bila mtu backstage.

By Pascal Ndege


Je, Kujamiiana Huondoa Msongo wa Mawazo Kwa Wanawake?

$
0
0
UTAFITI uliofanywa na Chuo Kikuu cha State cha jijini New York nchini Marekani unaeleza kuwa manii ni nzuri kwa wanawake kwani huwaondolea msongo wa mawazo.

Pia, watafiti hao wamesema wanawake wanaofanya tendo la ndoa mara kwa mara bila kutumia kinga (mapenzi salama) wanakuwa na kiwango kidogo cha msongo wa mawazo na hufanya vizuri katika vipimo vya akili.

Hali hii wamesema wataalam hao kuwa inatokana na manii kuwa na kemikali ambazo humfanya mtu kuwa vizuri kihisia, huongeza upendo/unyenyekevu, huchochea mtu kupata usingizi na huwa na angalau aina tatu za kemikali za kuondoa msongo wa mawazo (anti-depressants).

Utafiti huo uliofanywa kwa kuwahoji wanawake 293 kwa kufuatilia maisha yao ya kujamiana dhidi ya afya za akili zao. Manii huwa na mchanganyiko wa kemikali aina ya cortisol ambayo huongeza upendo, kemikali aina ya esterone na oxytocin ambazo zote humfanya mtu kuwa vizuri  kihisia.

 Pia, huwa na homoni aina za ‘thyrotropin releasing hormone’, ambayo huondoa msongo wa mawazo, melatonin ambayo huchochea usingizi na serotonin ambayo ni homoni inayoondoa msongo wa mawazo.


Kutokana kuwapo kwa mchanganyiko wa kemikali na homoni hizo kwenye manii

Matokeo ya utafiti

Matokeo muhimu ya utafiti huu ambao umechapishwa katika jarida la ‘Archives of Sexual Behaviour’ ni kwamba hata baada ya baadhi ya watafitiwa kuongeza kiwango chao cha kujamiana, wale ambao walikuwa hawatumii kinga yoyote walikuwa na kiwango kidogo cha msongo wa mawazo tofauti na wale ambao walikuwa wakitumia kinga kama kondomu wakati wa kujamiana.

 Pia, wanawake hawa ambao hawakutumia kinga walikuwa na kiwango kidogo cha msongo wa mawazo tofauti na wale ambao hawakushiriki tendo la ndoa kabisa.

Watafiti hao wamesema siyo tu kujamiana huongeza furaha kwa mwanamke na hivyo kumwondolea msongo wa mawazo, bali kiwango cha furaha pia huendana na wingi wa manii katika mili yao.


Hata hivyo, ushauri wa kitaalamu ni kuwa utafiti huu usiwe chanzo cha watu kufanya mapenzi bila kinga bali uwe chanzo cha kufanya mapenzi salama na mwenza unayemwamini.

Pia, tunakemea na kupinga wale wote wanaofanya vitendo vya usagaji kwani ni hatari kwa afya zao kwani ni chanzo kimojawapo cha magonjwa ya akili. Wiki ijayo tutakuletea mengi kuhusu uhusiano kati ya usagaji na ugonjwa wa akili.

PAUL Makonda Awajibu Mawaziri Wanaohoji Anatafuta Nini

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Dar Paul Makonda amesema kuna watu wanaohoji wakiwemo mawaziri kuwa anatafuta nini?
Yeye amesema hawezi kujizuia na anawajibu kuwa anatafuta kutimiza kusudi la Mungu kwenye nafasi aliyopewa, na kingine ni kuwapa heshima waliompa nafasi aliyonayo
Amesema kuna watu wengi walikuwa wanaongea kuhusu yeye kupewa nafasi ya ukuu wa mkoa wakati yeye ni mdogo na hataweza lakini licha ya hayo rais akamuamini na kumteua
Lingine amesema anataka aache alama kuwa kuna mtu alikuwa mkuu wa mkoa wa Dar na akafanya mambo kadhaa

Angalia Video

Hizi Ndio Sababu Zinazowafanya Wanaume Kufa Mapema Kabla ya Wanawake

$
0
0
Utakubaliana na mimi kwamba wanaume wengi walioko kwenye ndoa wanakufa mapema na kuwaacha wake zao, ingawa swali linabaki kuwa ni kwanini?

Zifuatazo ni sababu 6 za wanaume wengi walioko kwenye ndoa kufa mapema na kuwaacha wake zao.


1. Ugumu katika kufunguka.
Utakubaliana na mimi kwamba wanaume ni wagumu sana ten asana kufunguka na kushirikisha mambo yao, wao wako tayari wafe na tai shingoni wakijifanya hawaumii au hawasikii shida. Mkiwa na ishu kwenye ndo mkaitwa sehemu muyaongee yeye kamwe hamumpati, anakwambia
mambo yetu tutasuluhisha wenyewe wakati ndani yanamla na kummaliza.


2. Ugumu katika kusamehe.
Kusamehe sio tu kwa faida ya anayesamehewa bali pia kwa afya yaw ewe unayesamehe. Mzigo unaotokana na kusamehe hutuumiza sana mioyo yetu, hata kama mara nyingine tunajifanya hatuna shida yeyote.
Unaposamehe unaachilia mzigo mkubwa, wanaume wao ni wagumu sana kusamehe. Wako tayari wakubebe moyoni miaka, na tena watakukumbusha uchungu wao kila wanapokuona. Hii inawala sana bila wao kujua.

3. Tabia hatarishi.
Wanaume wengi kwenye ndoa ndio wanaoongoza kushiriki tabia hatarishi kama vile ulevi, anasa, ngono holela na hii huwaweka karibu zaidi na jeneza kuliko wake zao
waliowaacha nyumbani wakiwadanganya kuwa wako mkutanoni mkoani.

4. Ugumu katika kujali afya.
Ni rahisi sana mwanaume akajisikia vibaya lakini asiende hospitalini kuangalia afya, hata pale anapohimizwa kwenda bado anaweza kukwepa au kubisha au hata kusema kuwa ameshakwenda au ameshakunywa dawa kumbe mwongo.
Wako pia ambao wanaweza kupewa dawa na wasizitumie.

5. Msongo wa mawazo.
Wanaume ndio wabebaji wakubwa wa shehena za msongo wa mawazo “stress” ingawa kwa nje wanajitahidi sana kuonyesha kuwa mambo yako shwari wakati wanatafunwa ndani. Kaulize hospitalini, wanaokufa kwa presha ya kupanda au ya kushuka, stroke, kusimama kwa
moyo, kupasuka kwa mishipa ya damu, matatizo ya mifupa, au kuumwa sana kichwa, halafu uliza ni jinsia gani.

Kuwa open, roho safi and less agressive

CUF Tanga Wamgomea Profesa Lipumba

$
0
0
CHAMA cha Wananchi (CUF) wilayani hapa kimetoa tamko la kutomtambua Mwenyekiti wa Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba, na kwamba hakitampokea katika ziara yake.

Lipumba anatarajia kuanza ziara mkoani Tanga kesho  huku uongozi wa chama hicho ukisisitiza kutambua uamuzi wa  Mkutano Mkuu uliomwondoa madarakani na wa Baraza Kuu kumvua uanachama.

Mwenyekiti wa CUF wa Wilaya ya Tanga, Rashid Jumbe alitoa tamko hilo jana akieleza kuwa hawatakuwa tayari kukaidi Katiba ya Chama chao na kwamba hawatampokea na hakuna maandalizi yatakayofanyika kumpokea.

"Tumeambiwa Lipumba ana dhamira ya kufanya ziara mkoani hapa. Sisi kwa uamuzi wa Baraza hatumtambui, wala hatujaandaa maandalizi ya kumpokea.

“Wilaya za Korogwe na Muheza ndizo zimesema atazitembelea, lakini sisi hatuko pamoja nao na watakaompokea wataingia kwenye mgogoro mwingine kwa sababu hatambuliki," alisema Jumbe.

Mwenyekiti huyo pia alizungumzia mgogoro baina yao na CCM kutokana na sakata la umeya ambapo alisema  hatima ya mgogoro huo itajulikana baada ya mkutano mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29.

Alisema kutokana na sakata hilo walitoa malalamiko kwa viongozi mbalimbali lakini hakuna hatua zozote zinazoendelea, hivyo Kamati ya Utendaji iliwataka madiwani wa chama hicho kutohudhuria kikao chochote cha Halmashauri hadi itakapotoa uamuzi.

"Tumetoa malalamiko yetu kwa viongozi wa CCMna lengo letu ilikuwa tuonane na  Rais lakini tulimpata Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa aliyetwambia kuwa atalifanyia kazi, lakini sasa tumeamua kupeleka malalamiko yetu kwa wenye chama na wao ndio watakaotoa uamuzi juu ya mgogoro huo.

“Hivyo tumeitisha mkutano ambao utakuwa na wajumbe 440 ambapo tuna imani kuwa tatizo letu litakwisha Oktoba 29,” alisema Jumbe.

DOWNLOAD SIASA APP Kwenye Smart Phone Yako Kupata Habari na Matukio ya Siasa Kirahisi

$
0
0

Install Android Application ya Siasa Huru Sasa Ipo Google Play Store , Fanya Kuinstall Kwenye Smart Phone yako kupata habari na Matukio ya Siasa kwa wakati...

Bonyeza HAPA Kuinstall 

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya SIASA HURU Kwenye Simu yako ili Kupata Habari zetu Haraka

Wema Sepetu Awashushua Wanaomsema Aunt na Zari

$
0
0
Imelda Mtema, Risasi
SUPA-STAA Wema Isaac Sepetu ‘Madam’, amefunguka kuwa anachukizwa na watu wanaomtolea matusi muigizaji mwenzake, Aunt Ezekiel, baada ya kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa ya mzazi mwenza wa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.


Akizungumza na Za Motomoto News, Wema alisema unatakiwa ufike wakati watu waelewe na waongozwe kwa akili zao za kuzaliwa kwa sababu hakuna kitu kibaya ambacho amekifanya Aunt, kwa kuwa staa mwenzake huyo kwa sasa ni mmoja wa familia hiyo.


“Jamani hebu naomba kwanza wamuache Aunt, hana kosa lolote, hata kama ningekuwa mimi hapa nisingeweza kuacha kwenda kwa sababu tayari ni familia na hawezi kumuacha mumewe aende peke yake maana vitu vingine ni vya kujiongeza tu, nachukizwa sana na jinsi wanavyomrushia maneno ya kashfa,” alisema Wema.

Meneja wa Alikiba Afunguka Mkasa Mzima wa AliKiba Kushushwa Stejini Ghafla Huko Mombasa.

$
0
0
American Superstar Chris Brown, Jumamosi ya juzi ali rock kwenye tamasha la Mombasa Rocks Festival, ambalo tamasha hilo lilifanyika kwenye hoteli kubwa inayoitwa Mombasa Golf Hotel.

Mombasa Rock Festival lilikuwa na wasanii wengi wa ku-perform kutoka ndani na nje ya Kenya. Kutoka Bongo tuliwakilishwa na King Kiba pamoja na Vee Money.

Lakini kuna video zinasambaa zikionesha kuwa wakati anaperform Kwenye tamasha hilo, Kiba alipanda juu ya speaker, alitumbuiza nyimbo mbili tu kabla ya mic aliyokuwa anaitumia kuonekana kupata mushkeli/kuzimwa na kumlazimu kuondoka jukwaani na kupandishwa Chris Brown.

Swali..Je kupanda juu ya speaker ndio kulisababisha waandaaji wamshushe Kiba au ?

Kupitia perfect255 ikaona isiwe kesi.. nakumvutia waya moja kwa moja Meneja wa AliKiba, Aidan Charlie nakufunguka haya.

“Hapana kwanza Ilo la kupanda juu ya speaker haikuwa sababu, kwa sababu Wizkid nilimuona pia alipanda na hakushushwa.” aliendelea Aidan

“Issue kubwa iliyokuepo nitime, show ilitakiwa ianze saa 8 mchana na kumalizika usiku kama saa 6 lakini kutokana na wenyewe maorganizer walivyojiorganize mambo haya kwenda kama yalivyopangwa, kwa hiyo baada ya kuanza show saa 8 ikaanza saa 3 usiku.”

“But the time show inaanza wakaperform Navio, Vanessa hata nazizi akaondolewa..” alisema Meneja Aidan.

Chris Brown Hakuwa Kwenye Mood na Hakutaka Kuongea na Mtu – Vanessa Mdee

$
0
0
Mara nyingi wasanii wa nje wanapokuja kwenye show Afrika, hupenda kujichanganya na wasanii wanaotangulia kwenye show yake na kuchukua selfie na vitu kama hivyo. Lakini kwenye tamasha la Mombasa Rocks lililofanyika Oktaba 8 mjini Mombasa ambalo Chris Brown alitumbuiza, hakuna picha yeyote iliyoonekana akiwa na wasanii waliomsindikiza – Wizkid, Vanessa Mdee na Alikiba.

Kwa mujibu wa Vanessa, Chris hakuwa kabisa kwenye mood katika siku hiyo nzima na hakutaka kuongea na mtu. “To be honest, Breezy was not in a good mood,” Vanessa aliwaambia watangazaji wa XXL ya Clouds FM Jumatano hii.

“Tangia tumefika hadi tumeondoka hata ku.. sijui labda mazingira yalikuwa hayamfurahishi. Amepokelewa vizuri sana, sijui, alikuwa hana mood ya kusocialize na mtu yoyote,” ameongeza.

Kwa upande mwingine Vanessa alizungumzia sakala ya Alikiba kuzimiwa mic kwenye show hiyo.

“Mimi nilikuwa namsubiria Alikiba kama wewe ulivyokuwa unamsubiria, mimi nilikuwa nataka kuona show yake maana Mombasa wanamkubali sana but kilichotokea ni kwamba nadhani muda ulikuwa umeshatimia na Chis Brown muda wake wa kupanda stejini ulikuwa umeshafika, so that’s what happened, that’s what I know hayo mengine mimi siyajui,” alisisitiza.

“Halafu kibaya ni kwamba walikuwa wamesubiri kwa muda sana, kulikuwa na delay baada ya performance yangu mpaka alipopanda Wizkid, long time walikuwa wamesubiri na yeye [Chris Brown] alikuwa ameshaanza [kulalamika], ni kama nilivyosema alikuwa in a very bad mood. Kwahiyo walikuwa wanajaribu kumridhisha yeye ili apande muda ambao anataka yeye.”

Vanessa Mdee Afichua Sababu za Ali Kiba Kuzimiwa Mic Mombasa

$
0
0
Vanessa mdee ambaye pia ali pafomu Mombassa ametaja sababu iliyosababisha Ali Kiba kuzimiwa mic ni kuwa Chris Brown aliingia akiwa hana mood nzuri, kwa hivyo ili kumfurahisha wale waandaji ikabidi wakatishe shoo ya Ali Kiba wampe muda wa kupanda jukwaani atakapojisikia yeye

Baraka da Prince Amtukana Ney wa Mitego

$
0
0
Baada ya Nay wa Mitego kudai kuwa muimbaji huyo wa ‘Nisamehe’ na Stan Bakora ni watoto na kwamba huenda wanatafuta kiki, ameibuka na kudai kuwa rapper huyo hana akili na ni mp*mbavu.

“Nay hana akili, yaani Nay wa Mitego ni mp*mbavu tu,” Barakah alimwambia mtangazaji wa kipindi cha Mdundo Bando cha Lake FM, JR Junior. “Yeye ndio anaishi kwa makiki ndio maana mpaka alifungiwa kwa kupiga madada za watu picha za uchi, sio mwanamuziki mzuri,” alisisitiza msanii huyo.

“Nay wa Mitego ni rapper anayeungaunga, yaani huwezi kumweka miongoni kwa rappers wakali Bongo, huwezi kunitajia Nay wa Mitego nikakuambia kwamba ni rapper mkali. Kwahiyo naye akija akaongea shit about me yaani
nitamshangaa.”

VIDEO:Waziri January Makamba Atembelea Studio ya Diamond Platnumz

$
0
0

VIDEO:Waziri January Makamba Atembelea Studio ya Diamond Platnumz

Governor wa Mombasa Kumleta Nicki Minaj Baada ya Chris Brown

$
0
0
Inavyoonekana kaunti 001, au ukipenda kaunti ya Mombasa inatarajiwa kupata masupastaa mpwito mpwito mwaka huu.

Baada ya kumleta Chris Brown Mombasa, Gavana wa Mombasa, Gavana 001, almaarufu Sultan au ukipenda Ali Hassan Joho aliwapa ahadi mashabiki waliohudhuria tamasha la #MombasaRocks, kuwa atamleta Nicki Minaj kuperform Mombasa.

Chini ya ministry ya Tourism, kaunti ya Mombasa imekuwa mstari wa mbele kukuza jina lake kupitia matamasha mbalimbali yanayoandaliwa ili kuipa sifa kaunti hii kwenye sekta ya Utalii.
Hivyo basi, wapenzi wa Nicki Minaj kaeni tayari.

Baada ya Young Dee Kukana Kutoka Kimapenzi na Amber Lulu...Amber Atoboa Siri Nzito

$
0
0
Ukimwaga mboga wenzio wanamwaga ugali.
Ukweli wafahamika baada ya mara kadhaa Rapper Young Dee
kukanusha kuwahi kuwa na mahusiano na video vixen
kutoka kwenye kiwanda cha Bongo Fleva, Amber Lulu.

Akiongea na U-Heard ya Clouds FM, Amber Lulu amefunguka
ukweli kwa kusema kuwa amekuwa na mahusiano na rapper
huyo kwa tangu miaka minne iliyopita wakati akiwa mkoani
Mbeya.

“Marafiki zangu wanajua ni jinsi gani nilivyokuwa naishi
naye, mara ya mwisho alikamatwa na polisi mimi ndio
nilienda kumtoa ndugu zake wote walikataa kwenda, Mimi
nimeenda. Matatizo yangu yeye anayafurahia ina maana.Sikuwa nimefanya vile kwa kuwa alikuwa ni mpenzi wangu ni
mtu ninayemfahamu siku nyingi na ambaye tupo wote,”

Amesema Amber.

DUME Condom Washtushwa ‘Scorpion’ Kushtakiwa..Wadai Hawana Uhusiano Naye Kwa Sasa

$
0
0
Taasisi ya T.Marc Tanzania, ambayo iliendesha mashindano ya Dume Challenge imeeleza kushtushwa na kusikitishwa na taarifa za kukamatwa kwa Salum Njwete, maarufu kwa jina la Scorpion.

Taasisi hiyo pia imethibitisha kuwa Njwete alishiriki na kushinda mashindano ya Dume Challenge Season 1 mwaka 2012 na kuwa balozi wa kondomu za taasisi hiyo chapa ya Dume kuanzia mwaka 2012 hadi 2014.

Njwete alikamatwa na kushtakiwa kwa uporaji wa kutumia silaha na kumjeruhi baada ya wananchi kulalamika kwenye vyombo vya habari kuwa kuna mtu anayeitwa Scorpion aliyekuwa akipora na kujeruhi wananchi, akiwemo kinyozi Said Ally wa Mabibo Hosteli aliyeporwa fedha na kutobolewa macho.

“Hata hivyo, tangu mwaka 2014, Bwana Njwete hajakuwa na uhusiano na chapa hiyo,” inasema taarifa ya T-Marc iliyosainiwa na mkurugenzi mkuu, Diana Monika Kisaka.

“T-Marc pia inapenda kuthibitisha kuwa Bwana Njwete alikuwa balozi wa programu ya kuwezesha wasichana ya “Hakuna wasichoweza” mwaka 2014 ambayo imeisha muda.

“T-Marc haina tena uhusiano wa aina yoyote, rasmi au kwa njia yoyote ile na Njwete. T-Marc inaamini kuwa haki itatendeka katika shauri ambalo Njwete anatuhumiwa.”

Taasisi hiyo imesema inaendelea kujikita katika kutoa huduma kwa maisha ya Watanzania kwa kutoa bidhaa na programu bora.

MASKINI: Saida Karoli Aelezea Alivyotumiwa Kuwatajirisha Watu Huku Akibaki Maskini

$
0
0
Muimbaji nguli wa Tanzania aliyetamba na vibao kama Mapenzi Kizunguzungu, Kitobero na nyingine nyingi amesema kuwa ana hofu ya kuwa na meneja kwa sasa kutokana na yaliyomsibu miaka kadhaa nyuma.

Najua, kuna mameneja wazuri katika muziki wa bongo kama meneja wa Diamond Platnumz hata wa Ali kiba. Lakini kuna baadhi ya mapromota na mameneja kwa kweli nina wahofia sana. Alisema Saida Karoli.

Saida Karoli ameeeleza kuwa wakati wake alifanya vizuri sana kimuziki lakini hakuona mafanikio hayo kifedha. Hayo yote ni kutokana na uongozi wake.

Amesema kuwa hata sasa akipata meneja mwingine atahakikisha anajiridhisha kwanza kama anaweza kazi ndio aingie nae mkataba. Saida Karoli amesema jina lake kwenye jukwaa ni kubwa sana kuliko mafanikio aliyonayo, na hii humfanya aamini kuwa alitumika kuwanufaisha watu wengine.

Nilikuwa nikilipwa fedha kidogo sana kutokana na kazi zangu za muziki. Kama mwandishi akitembelea ninapoishi Watanzania wataweza kuelewa ni nini ninazungumzia.

Muziki wa Saida Karoli bado unaendelea kuishi na kuvutia watu mbalimbali licha ya kuwa uliiimbwa miaka mingi nyuma. Diamond Platnumz aliurudia wimbo wake wa Salome na kuongeza vionjo ili kuuboresha na Saida Karoli atapata asilimia 25 ya mauzo yote ya wimbo huo.

Hakuna Beef kati ya Ali Kiba na Diamond ila Kuna Beef kati ya Ali na Sallam

$
0
0
Hii kitu sio mara ya Kwanza kutokea malumbano kati ya Ali na Sallam.

1.Show ya Tigo Dar es salaam

mwaka jana kwenye show ya Tigo ambayo wasanii A List wa bongo flava wote walikuwemo ila baada ya ile show ambayo Ali kama kawaida yake alikimbiza Sallam kesho yake alishinda huko Twitter akimkashifu na kumtukana Ali kuwa ni mchawi na muoga akitoa madai kuwa Ali na timu yake waliruka ukuta kuingia back stage na Ali akumsalimia msanii yoyote kule back stage japo walikuwepo wakina A.Y,Mwana da,Barnaba boy,Ben Pol,Ommy Dimpozi,Diamond na wasanii wengine Kibao.

Hapo ndio utashikwa na mshangao mambo ya Ali kuruka ukuta na kutomsalimia msanii yoyote ikiwa kweli au ni uongo yeye Sallam inamuhusu nini?!
Na mbona wasanii wengine au mameneja wao hawakuzungumzia ile kitu kwanini yeye imuume namna ile na kuropoka kwenye social network kwa kiasi kule??

2.Show ya ODM-Mombasa

Kukawa na Show nyingine Mombasa..Show ambayo haikuwa ya diamond lilikuwa ni Tamasha la Chama cha Siasa ODM cha bwana Raila Odinga na wasanii Kibao wa Mombasa walikuwepo na Diamond alienda pale kama msanii mualikwa.
Kumbuka kuwa Tamasha sio la Diamond ni la Chama cha ODM wenye tamasha Lao wakaamua kumualika na Ali kwa sababu Ali ndio msanii anaekubalika zaidi Kutoka afrika pale Mombasa.

Baada ya lile tamasha Sallam akulala alilalama usiku kucha kwanini hawakuambiwa kuwa Ali angekuwemo kwenye hilo tamasha..basi kama kawaida yake akamtukana Ali kumwita muoga mwenye kusafiria nyota ya Diamond na kusahau kabisa lile tamasha alikuwa la kwao wao bali ni Chama cha Siasa ODM na wote walikuwa waalikwa tu.

3.Coke Studio,Nairobi

Mwaka jana Ali alikuwa Coke studio na kina Neyo kule Kenya na Neyo alikuwa yupo tayari kufanya Solo project na Ali nje ya coke studio..Sallam akulala alifunga safari usiku usiku mpaka Nairobi akaenda kumtia maneno maneno Neyo na kuvuruga mipango yote ya Ali na Neyo...mwisho wa siku Neyo akafanya Solo project na Diamond badala na Ali Kiba kama Neyo mwenyewe alivyotaka.

4.Show ya Chriss Brown,Monbasa

Juzi tena show sio yake haimuhusu ila alishinda Back stage kutoa figisu figisu...Ali alitakiwa afanye live show..na kufunga vifaa vya live show ingechukua zaidi ya Dakika 30 pale jukwaani alafu Ali ndio apande na hilo alikuwa tatizo la Ali bali ni la waandaaji wa show na fundi mitambo walichelewa kufunga mitambo yao.

Wizkid afanyi live show Anafanya semi live show ambayo Inawekwa CD yenye beat tupu na yeye anaimba juu yake.
Ali akamshauri kwa kuwa kufunga mitambo itachukua muda mrefu basi ni bora Wizkid apande afanye semi live show kwa maana mpaka Wizkid akimaliza show yake wale mafundi watakuwa washamaliza kazi yao na Ali atapanda kupiga Live show sasa kilichotokea Sallam akamwambia Meneja wa Wizkid Mr.Sande kuwa asikubali hapo ndio ulipotokea mzozo kati ya Ali na Team ya wizkid wakiongozwa na mfitini Sallam.

Mwisho wa siku walipoteza zaidi ya Dakika 40 yote kutaka kumkomoa Ali kwa kitu ambacho kipo wazi kabisa.

Mpaka Ali alipopanda muda ulikuwa ushapita na kupelekea kuzimiwa Mic na team ya Chris Brown kwa sababu ndege ulikuwa inawasubiri Airport kuwarudisha marekani.

Mwisho wa siku hakuna Bifu kati ya Ali na Naseeb ni washkaji ila kuna Beef kati ya Ali na Sallam.

Babu Tale Atoboa Siri ya Usambazaji wa Nyimbo za Wasafi Records

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, January Makamba wiki hii alitembelea ofisi za WCB na kuonyeshwa mambo mbalimbali ambayo yanafanyika katika kila kitengo.


Moja kati ya sehemu ambayo muheshimiwa alipekekwa ni sehemu ambayo huwa mikutano kuhusu usambazaji wa kazi za wasanii wa WCB hufanyika.


Akiongea katika utambulisho huo, Babu Tale alisema wao katika usambazaji wa kazi za wasanii wao huanza kwa watu wa chini ambao wanapatikana mtaani.

“Hii ni ofisi ya watu wa creative,” alisema Tale katika ubambulisho huo. “Wakati wa kunatoa nyimbo mpya lazima tunakaa na kuwaza tunafanya nini na tutatoa kwa style gani ili tuanze kuukamata mtaa tunafanyaje kuhusu mtaa. Kwa hiyo tunapotoa nyimbo tunahakikisha kila mtu mtaani anayo halafu ndio tunaiachia redioni. Kwahiyo ikienda redioni watu wa mtaa watakuwa wanaisukuma ile ya redio,”

Pia Diamond alisema wanaitegemea mitandao ya kijamii kwa kiasi kikubwa katika kusambaza nyimbo zake kwa uharaka zaidi.

Kwa upande wa Waziri January Makamba alimmwagia sifa Diamond pamoja na team yake kwa kufanya kazi nzuri.

Said Ally (Aliyetobolewa Macho) Apewa Pikipiki 5, Bajaji 2 na Kuahidiwa Nyumba

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha vitu alivyoviahidi kwa kijana Said Ally aliyetobolewa macho maeneo ya Buguruni Sheli jijini Dar es Salaam anavipata. Alhamis hii, ametimiza yote aliyoahidi na mengine.


Katika ahadi zake, Makonda aliahidi kumchangia Said shilingi milioni 10 na leo hii amemkabidhi rasmi kiasi hicho. Pia amesema kupitia watu na taasisi mbalimbali, atapewa pikipiki tano na Bajaji mbili. Kama hiyo haitoshi, Makonda alisema kampuni ya GSM imeahidi kumnunulia nyumba kijana huyo .

“Nimeleta milioni 10 zangu siwezi kusahau lakini hili namuachia mwenyezi Mungu, naomba nikukabidhi, nashukuru na wale walioniunga mkono katika kumpatia Bodaboda 5 na Bajaj mbili ambazo zimetoka katika makampuni tofauti tofauti,” alisema Makonda.

“Jambo ambalo nilikuwa nikimlilia Mungu anipe nafasi ili niweze kulifanikisha – ni jambo ambalo lilikuwa likimsumbua kila mtu, ni jambo la Said kupata kiwanja na ukiangalia kwenye mji wetu huu kiwanja kinauzwa kwa bei ya juu sana, vinginevyo utaenda Magwepande na bado utakuwa nje ya mji,” aliongeza.


“Shughuli za kibiashara zinafanyika katika ya mji, na hili jambo ulilisema ofisini kwangu na mimi nilikuwa nikimlilia Mungu anipe nafasi ya kufanikisha ndoto yako. Tumepata mdau ambaye amekubali na kumnunulia ndugu yetu Said nyumba, ambayo ni kampuni ya GSM na nimewambia wasikupeleke Magwepande, wasikupeleke Bunju, Mbagala, Gongo la Mboto. Nataka ukae mazingira yale yale ambayo umeyazoea. Iwe Tabata unakuja tena Buguruni, Mwenge. Nataka maeneo haya haya ambayo watu wamezoea kukuona. Kwahiyo ndugu zetu wa GSM wamekubali kuniunga mkono kumnunulia nyumba. Mi nakuombea neema ya bwana iendelee kutembea katika maisha yako,” alisisitiza Makonda.

Kwa upande wake, Said alishukuru na kusema, “Ukiona mtu anatoa chozi kwaajili ya mwananchi wake ni jambo zuri, alivyosikia kwenye vyombo vya habari hakuchelewa kuja. Lakini leo nashukuru sana kwa kila kitu alichonitendea, nashukuru sana.”

“Sina cha kumlipa zaidi ya kumuombea dua siku nyingine nisikie amekuwa waziri. Nashukuru sana namuombea kila siku na watu siwezi kuwasahau sana, Clouds ni watu ambao sitawasahau sana na Diamond sitamsahau sana,” alisema.

Wakati huo huo wahenga wanasema ‘milima haikutani lakini binadamu hukutana.’ Hii likuwa kwa Said ambaye alipenda siku moja amuone mwanamuziki anayemkubali zaidi, Diamond Platunumz.

Said alishindwa kuvumilia baada ya kusikia wimbo wa Salome na video yake ambayo hajawahi kuiona na mbele ya msanii Diamond aliyekuwa akimpenda, hatimaye leo wamekutana. Amedai kukutana na Diamond wakati hana uwezo wa kumuona ni kitu kinachomuumiza lakini amefurahi.

Staa huyo anayemiliki label ya WCB, alitoa shilingi milioni mbili za kumkabidhi Said aliyezipokea kwa furaha.

Kutofanya Mapenzi Mpaka Ndoa ni Udhaifu?

$
0
0
Nina swali ambalo linanitatiza sana haswa pale ninapoulizwa na rafiki zangu

 Swali "Hivi ushamla yule demu?"

Kiukweli kwa confidence huwa najibu hapana kwa sababu tumewekeana ahadi ya kuwa hakuna hicho kitu mpaka ndoa. Sasa cha ajabu ninapojibu hivyo wenzangu huwa hawaamini kwa kuwa mara kadhaa huyu mchumba wangu ambaye tayari nishamposa na kumtolea mahari anakuja nyumbani na kushinda nami muda mwingi.

"Kama hugongi basi unagongewa"

Hayo ndio majibu ya wenzangu.

Namuamini sana huyo msichana kwa sababu i knw ni virgin sio kwa kuambiwa kwa kuiona mimi mwenyewe.

Swali langu ni ushamba au ujinga kusubiri mpaka ndoa?
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images