Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live

RAYVANNY Amshukuru Mungu Kwa Kumkutanisha na Diamond...Adai Mpaka Nguo Anazofanyia Video ni za Diamond

$
0
0

Ray Vanny Ameandika Haya Kupitia Ukurasa wake wa Instagram:

Rayvanny - Kwenye Video ya #KWETU Nguo zote Ulinipa wewe!!! #MUGACHERERE Nguo zote ulinipa zako... kiukweli Nimepata tabu nyingi Sana Kwenye Mziki wangu Lakini Niliamini Ipo Siku Namimi Nitaonekana.Nashukuru Mungu Sana Kunikutanisha nawewe Brother Naseeb Asante kwa Moyo Wako wa Upendo Kwangu Ulithamini kwa kidogo nilichonacho Nakuamini Nitaweza kufanya.Safari Bado Ndefu Tutafika Tunapotaka!!!

KWA Hili Lady Jaydee na Clouds Media Group Wanastahili Pongezi

$
0
0
Najua hakuna aliyetarajia kuona hili likitokea lakini kwa uwezo wa Mungu limefikia mwisho.

Nakumbuka Machi 21 ya mwaka huu kaka yangu Fredrick Bundala aliandika makala iliyokuwa na kichwa cha habari kinachosomeka “Ninachotamani: Lady Jaydee na Clouds Media Group wamalize tofauti zao” hatimaye hilo limesikika na kila kitu kimeonekana kuwa sawa kutokana na pande zote mbili kuamua kufukia mabaya yote yale yaliyowahi kutokea.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, napenda kumpongeza Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kwa busara yake aliyoitumia ya kujibu swali aliloulizwa kwenye kipindi cha XXL kuhusu kumaliza ugomvi wao na malkia wa muziki wa Bongo Fleva, Jaydee.

“Tatizo ni kwamba hakuna ambacho hatujamaliza, tulimaliza, tunasubiri order. Unajua kimsingi ulipopewa order ya kwamba ‘nyimbo zangu usipige, jina langu usiseme kwenye chombo chako, vyovyote itakavyokuwa mimi sitaki kusikia hiyo kitu’ hiyo ndio order. Kwahiyo labda tukikutana, nimuombe tena [Lady Jaydee] kama tutaruhusiwa kufanya hiyo kitu,” alisema Ruge kwenye kipindi hicho.

Aliongeza kwa kusema kuwa ni muda mrefu hajawahi kukutana na Lady Jaydee, japo alidai ‘hata leo nikipata nafasi ya kahawa nitashukuru sana kwa huo mwaliko.’

Hatimaye ujumbe ule ulimfikia Jaydee na nampongeza hakutaka kuliacha jambo hilo lipite kwa kuwa limedumu kwa muda mrefu na hakuna jipya lililotokea kwa kuwa kila mtu bado anafanya kazi zake huku mashabiki ndio wakibaki njia panda wakishindwa cha kufanya.

Jumatano hii uongozi wa Jide ulitoa taarifa yake rasmi kuwa wapo tayari kufanya kazi tena na kituo hicho cha redio. “Hatuna tatizo na Clouds Media Group kuanza kupiga nyimbo za Lady Jaydee. Wanaweza kuanza kupiga wakati wowote watakapokuwa tayari kwakuwa chochote kilichotokea hapo nyuma kimefikia tamati, la msingi sasa ni amani na upendo vitawale. Kuanzia leo wana uhuru wa kupiga na kutaja jina la Lady Jaydee kadri wawezavyo,” yalisema maelezo yake.

Kitendo hicho kilichofanywa na pande zote mbili kitawarudisha upya tena baadhi ya mashabiki waliogawana upande pamoja na kuwapa nafasi wasanii ambao walikuwa wakitamani kufanya kazi na Jide kwa muda mrefu lakini walikuwa wakihofia nyimbo zao kutochezwa kwenye kituo hicho.

Kama hili limewezekana basi natamani pia kuona siku moja wasanii wengine ambao hawapatani na kituo hicho na vituo vingine vya habari wakiyamaliza matatizo yao na kuendelea kuufanya muziki wetu kusonga mbele kwa kuwa wote tupo kwenye safari moja na kila mtu anamtegemea mwenzake ili kuhakikisha hilo linatimia.

By Salum Kaorata

GIGY Money 'Nawashauri Wadada Wasivae Nguo ya Ndani Kama Mimi'

$
0
0
Baada ya video queen, Gigy Money kusemwa katika mitandao ya kijamii kwamba havai nguo ya ndani, mrembo huyo amesema ni kweli havai na ni maisha anayopenda kuishi.

Akiongea na Bongo5 Jumamosi hii, Gigy Money amesema anajisikia vizuri akivaa nguo bila kufuli kwani anajiona yupo huru zaidi. “Hata hapa nilipo sijavaa ch**i na nikweli sipendi kuvaa ch**i ila napenda kuvaa ch**i yenyewe bila kuvaa nguo juu yake,” alisema Gigy Money.

“Ch*pi nayo ni nguo na ni vazi la ndani, nivae ch*i nisivae hayo hayawahusu, hapa nilipo sijavaa c**i kwanza c**i inaharibu shepu, kama hii nguo niliyovaa leo nikivaa na c**i si naharibu nguo yangu, vitu ninatakiwa kuonekana. Tena ningewashauri wadada wenzangu wabane matumizi kwa sababu ch**i zinapanda bei kila kukicha,” aliongeza.

Katika hatua nyingine Gigy amesema kwa wasanii wachanga ndio watu ambao wanamtafuta zaidi ili ashiriki kwenye video zao.

MWAMVITA Makamba Atapeliwa na Sheria Ngowi......

$
0
0
Katika pitapita zangu Twitter nimekumbana na Tweet moja ya Mwanadada Mwamvita Makamba akidai yeye kama Mwekezaji binafsi katika tasnia ya Fashion ametapeliwa na Mbunifu wa Suti matata Bwana Sheria Ngowi.

Hapo alikuwa akimpa taarifa jamaa anayeendesha kipindi kipya mjini cha Papo Kwa Papo na Papi kinachoruka kila jumatano saa 3 kamili usiku kupitia YouTube na kinakuwa Mubashara.

HATIMAYE Rolls Royce la Diamond Liko Njiani Kuja Tanzania.....

$
0
0
The Rolls Royce musician from east africa aka diamond hatimaye amekamilisha ndoto zake za siku nyingi baada ya order yake ya gari aina ya rolls royce kukamilia na gari hilo liko njiani kuwasili mikononi mwake punde... Gari hilo aina ya rolls royce Drop Head coupe 6.7 litre V-12 ambalo limeagizwa kupitia kampuni ya Newline Luxury Motors ambalo order yake ina waiting time ya six months kuanzia unapolipia hadi litengenezwe hadi likufikie mteja..

PENDEZA na Markson Beauty Products...Kukuza Makalio, Kungarisha Ngozi na Kwa Wanaume Kukuza Cassava

$
0
0

HABARI NJEMA
MARKSON BEAUTY
PRODUCTS

Baada ya kupata cheti cha bidhaa bora kwa mwaka 2015-2016, Sasa kampuni hii inasambaza huduma zake ndani na nje ya nchi kwa vibali maalum. Bidhaa zetu zimetengenezwa kwa mimea na matunda na kudhibitishwa. Hazina kemikali wala madhara.

DAWA ZETU NI YA:-
1. kurefusha nywele na kuzuia kukatika ovyo @100,000/=
2. Kuongeza shepu (hips na makalio) kwa/= (a)Dawa ya kunywa au kupaka @150,000/=
(b)Vidonge @170,000/=
3. Kuwa mweupe na softi mwili mzima kwa:- (1)Mafuta @100,000/=
(11)Vidonge @150,000/=
4. Kupunguza unene na manyama uzembe @120,000/=
5. Kuongeza uume pamoja na nguvu za kiume kwa:-
(a) Gely ya kupaka @120,000/= (b) Vidonge maalum @120,000/= (c) Handsome up original @170,000
6. Kuondoa mvi milele zisiludi tena @100,000/=
7. Kuongeza unene wa mwili mzima na uzito @120,000/=
8. Kupunguza tumbo (kitambi) na nyama za pembeni kwa:-
(a) Dawa ya kunywa au kupaka @120,000/= (b) Mkanda wa kawaida @100,000/= (c) micro-computer belt unaovaibret @200,000/=
9 .Kupunguza maziwa na kuyasimamisha @90,000/=
10. Kushepu miguu na kuwa minene @100,000/=
11. Kuondoa mipasuko mwilini (michirizi) @90,000/=
12. kubana uke na kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa mwanamke @100,000/=
13. Taiti za hips na makalio @150,000/=
NB: Hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii kwa bidhaa halisi.
Wasiliana nasi :-
(+255) 0767447444 na
0714335378
Google MARKSON BEAUTY.
Follow us @Markson_beauty_pr
@Markson_beauty_pr

VIDEO:Wadada wa Kitanzania Wanaswa Wakinunua Mashine Bandia za Majamboz, Wanaume Hakuna?

$
0
0
Wadada wa Kitanzania wamenaswa na camera ya mdau kwa siri wakinunua sehemu za kiume dukani, nashangaa kilichowasukuma kufannya hivyo ni nini?
Tazama Video:

DIAMOND Akiri Bob Junior Anamchango Mkubwa Sana Kwenye Maisha yake ya Muziki....

$
0
0
Diamond hafanyi tena kazi na Bob Junior, lakini hawezi kusahau ukweli kuwa producer huyo wa Sharobaro Records ndiye aliyemfungulia njia ya mafanikio kimuziki. Akizungumza kwenye kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz Alhamis hii kupitia EATV, Diamond alikiri kuwa Bob Junior ana mchango mkubwa kwenye maisha yake.

“Kiukweli Bob Junior ana mchango mkubwa sana katika katika maisha yangu kwasababu ukiangalia nyimbo zangu zote zilizonitoa ni yeye ndiye alikuwa ametengeza,” alisema Diamond.

“Japokuwa hata kipindi ambacho nilikuwa nazitengeneza inawezekana watu walikuwa hawajamuona kama anaweza kuwa producer mzuri sana. Lakini mimi nilikuwa naona mbona huyu natoka naye, nakufa naye mimi yaani huyu natoa nyimbo na inahit,” aliongeza.

“Nakumbuka tulifanya nyimbo kama sita, Nenda Kamwambie, Mbagala, Nitarejea, Binadamu, nyimbo tofauti tofauti. Kila nyimbo alikuwa akinitengenezea akinipa beat nikifika nyumbani naandika vibaya sana. Na mpaka nakumbuka ilifika time niliweka kama chuki fulani kwa wasanii waliopo pale wakaona mbona unampendelea mtu fulani, yeye akasema mimi ni producer, natengeneza beat nikimpa msanii kaandikie kitu kikali, akasema huyu nikimpa analeta beat kali.”

Kwa upande mwingine staa huyo alidai kuwa Mbagala ni moja ya nyimbo zake anazozipenda sana kwakuwa aliuandika kwa ufanisi mkubwa.

MZEE Yusufu Kumtema Mkewe Baada ya Kugoma Kuacha Kuimba Taarabu Kama Alivyofanya

$
0
0
Aliyekuwa nguli wa muziki wa Taarabu nchini Mzee Yusufu inadaiwa na dada yake kuwa atampa mkewe talaka baada ya kugoma kuacha kufanya muziki wa taarabu na kumrudia mungu kama mumewe alivyofanya. maana sheria za dini ya kiislam zinataka mume akifanya jambo na mke amfuate Video:

SAKATA Kufungwa Kwa Kiwanda cha Dangote Bei ya Simenti Yapanda

$
0
0

BEI ya simenti imeanza kupanda katika baadhi ya maeneo nchini, imefahamika.

Uchunguzi uliofanywa na MTANZANIA unaonyesha kuwa bei hiyo imepanda zikiwa ni siku chache baada ya kiwanda cha simenti cha Dangote kilichoko mkoani Mtwara, kusimamisha uzalishaji kutokana na gharama kubwa ya uzalishaji.

Taarifa zilizopatikana mkoani Mtwara   zinasema mfuko wa simenti umepanda kutoka Sh 11,500 hadi Sh 17,000.

Mmoja wa wafanyabiashara wa simenti mjini Mtwara, Abdallah Said, aliiambia MTANZANIA, kwamba kupanda kwa bidhaa hiyo kumesababishwa na Kiwanda cha Dangote kusimamisha uzalishaji.

Said alisema kuna haja Serikali kuangalia namna ya kutatua mgogoro uliopo kati yake na mmiliki wa kiwanda hicho.

DODOMA

Mjini Dodoma, bei ya jumla ya mfuko mmoja wa simenti hadi jana ni Sh 12,500 na rejareja ni kati ya Sh 13,500 na 14,000.

Akizungumza na MTANZANIA katika eneo la Uwanja wa Jamhuri, mfanyabiashara wa jumla ambaye ni wakala mkuu wa kusambaza simenti mkoani Dodoma, Fred Mushi wa Kampuni ya Priscus Alexander Company Limited (PACL), alisema bei ya jumla ya mfuko mmoja wa saruji ni Sh 13,500 hadi Sh 14,000.

Katika maelezo yake, Mushi alisema bei hiyo imepanda kutoka Sh 12,500 iliyokuwa ikiuzwa hivi karibuni.

Kauli hiyo ya Mushi iliungwa mkono na mfanyabiashara, Muhommed Fahkim wa Kampuni ya Fasam General Supply.

MOROGORO


Mjini Morogoro, bei ya mfuko mmoja wa simenti nayo imepanda kutoka Sh 12,000 na Sh 12,500 hadi Sh 13,000 na Sh 13,500 kufikia jana.

Mmoja wa wafanyabiashara wa bidhaa hiyo wilayani Gairo, mkoani Morogoro, Samuel  Kivanda, alisema bei hiyo ni katika wilaya za Kilombero, Ulanga na Kilosa.



TANGA

Mkoani Tanga, bei ya mfuko mmoja wa simenti uliokuwa ukiuzwa kwa Sh 13, 000 hadi Sh 14,000, imeshuka hadi Sh 11500.

Baadhi ya wafanyabiashara mjini hapa waliozungumza na MTANZANIA jana, walisema bei hiyo imeshuka kutokana na viwanda viwili vya  simenti mjini hapa kuzalisha bila kusimama.

Mmoja wa wafanyabiashara hao, Shaban Ally kutoka Barabara ya 20  Tanga, alisema mjini hapa saruji iliyokuwa ikiuzwa kwa Sh 14, 000 na Sh 15,000 sasa inauzwa kwa Sh 13, 000 hadi Sh 12,500.

MBEYA

Jijini Mbeya nako bei ya bidhaa hiyo kwa mfuko mmoja imeshuka kutoka Sh 18,000 hadi Sh 14,500.



Kwa mujibu wa baadhi ya wakazi wa jijini hapa waliozungumza na MTANZANIA, mfuko mmoja wa simenti ya Tembo inayozalishwa mjini hapa iliyokuwa ikiuzwa  kwa Sh 15,000, kwa sasa inauzwa  Sh 14,500 kwa mfuko mmoja.



Mmoja wa wafanyabiashara hao, mkazi wa Soweto mjini hapa, Nsaji Mwakilili, aliiambia MTANZANIA, kwamba mfuko wa simenti aina ya Nyati uliokuwa ukiuzwa   Sh 18,000, umeshuka na kuuzwa kati ya Sh 16,000 na Sh 17,000.



ARUSHA

Jijini Arusha, bei ya mfuko mmoja wa saruji imeendelea kuuzwa kwa Sh 13,500 na bei hiyo imeelezwa kuwa imeendelea  muda mrefu bila kubadilika.

Akizungumza na MTANZANIA mjini hapa jana, mmoja wa wauzaji wa simenti eneo la Mji mpya la Burka City, Abdallah Rashid, anashangaa bei hiyo kutobadilika kwa muda mrefu sasa.

KILIMANJARO

BEI ya bidhaa hiyo katika maduka ya rejareja  mkoani hapa, imeshuka kutoka Sh 12,500 hadi Sh 11,900 kwa mfuko mmoja wa kilo 50.

Baadhi ya wafanyabiashara waliozungumza na MTANZANIA kwa nyakati tofauti, walisema simenti iliyoshuka bei ni ya kampuni  zinazozalisha bidhaa hiyo katika mikoa ya kaskazini.

TIC NA DANGOTE

Wakati hayo yakiendelea, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), kimevunja ukimya na  kuzungumzia hatua ya Dangote kusimamisha uzalishaji wa simenti kwa kinachoelezwa kuwa ni kupanda kwa gharama za uzalishaji.

Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Meneja Uhusiano kwa Umma wa Kituo hicho, Pendo Gondwe, alisema    wamekwisha kukutana na uongozi wa Kiwanda cha Dangote na kuzungumzia madai yao.

Kwa mujibu wa Gondwe, uwekezaji uliofanywa na Dangote ni mkubwa hivyo  Serikali siyo rahisi kukubali asimamishe uzalishaji kwa sababu zozote zile zikiwamo  gharama kubwa za uzalishaji.

“Kampuni ya Dangote ilipokewa na kituo hiki na ikapewa huduma zote za kuiwezesha kufanikisha uzalishaji.

“Hiyo ni kampuni kubwa ambayo ina uwezo wa kuzalisha ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja zinazofikia 6,000 kama itafanya uzalishaji kwa kiwango kilichokusudiwa.

“Kwa hiyo, tayari tumezungumza  nao, tumejiridhisha na tumefikia hatua ya kuamua kwenda kutembelea kiwanda chake baada ya siku 10 kuanzia sasa kwa kuwa uzalishaji utakuwa umerejea.

“Lengo letu la kwenda huko ni kuangalia changamoto zilizopo zinazoweza kuathiri uzalishaji wake,” alisema Gondwe.

Akizungumzia taarifa zilizosema mwekezaji huyo alipewa baadhi ya vivutio na Serikali ya awamu ya nne ambavyo vimeondolewa na Serikali iliyoko madarakani, Gondwe alisema kwa mwekezaji wa aina ya Dangote, lazima apewe vivutio.

“Wako wawekezaji na wawekezaji mahiri ambao kwa utaalamu hufahamika kama ‘strategic investors’. Kampuni ya Dangote ni moja ya wawekezaji mahiri na ambao kwa kawaida hupewa vivutio maalumu.

“Kwa taarifa yako ni kwamba wanaopewa vivutio hivyo ni wawekwzaji wenye mtaji unaofikia Dola za Marekani milioni 50 na Dangote uwekezaji wake unafikia Dola za Marekani milioni 500.

“Katika kutoa vivutio hivyo, pia huwa tunaangalia ajira zinazoweza kuwapo kutokana na uwekezaji huo na pia uwekezaji ambao hufanyika maeneo ya vijijini na umbali kutoka eneo yanapopatikana masoko makubwa, nao hupewa vivutio.

“Kwa kuwa tumekuwa na nia njema kwa wawekezaji, tumekuwa tukishirikiana na sekta binafsi  kuondoa changamoto zinazowakwamisha uwekezeji katika sekta mbalimbali nchini,” alisema.

Dangote ambaye ni kati ya matajiri wakubwa duniani, amesimamisha uzalishaji wa simenti katika kiwanda chake cha  Mtwara akidai kutoridhishwa na mazingira ya uwekezaji wake.

Serikali kwa upande wake imekuwa  ikisema kuwa madai ya mwekezaji huyo hayana msingi wowote.

Hata hivyo, uongozi wa kiwanda hicho nao umejitahidi kueleza upande  wake    jambo ambalo limesababisha   mvutano kati ya pande hizo mbili.

WAKENYA Wapewa Kazi ya Kukusanya Malipo ya Packing Jijini Dar, Malipo Yapanda

$
0
0

VIWANGO vya malipo ya maegesho ya magari katikati ya Jiji la Dar es Salaam yamepanda kutoka Sh 300 kwa saa moja hadi Sh 500, na kuanzia jana malipo hayo yatakuwa yanakusanywa na kampuni kutoka Kenya.

Hata hivyo, baadhi ya maegesho mengine ya jiji hilo malipo hayo yamebaki yakitozwa kwa gharama ya Sh 300, huku viwango vipya vikipokewa kwa malalamiko na watu ambao hutumia maegesho hayo, wakidai kupanda ghafla kwa viwango hivyo bila kutolewa taarifa za kutosha kwa umma.

Akizungumza na gazeti hili jana, Msemaji wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Gaston Makwembe alisema viwango hivyo vipya vilipitishwa na Baraza la Madiwani tangu mwaka 2014, hata hivyo havikuanza kutumika kwa sababu mbalimbali.

“Viwango hivi sio vipya kabisa, Baraza la Madiwani lilipitisha toka mwaka 2014, lakini sasa ndio tumeamua kuanza kuvitumia, kwanza tulikuwa tunaainisha maegesho yetu, tumeangalia pia uwezo wa wananchi kumudu viwango hivyo,” alieleza Makwembe.

Alisema kampuni ambayo inakusanya tozo ya maegesho ni Kenya Airport Parking System (KAPS) ambayo ilishinda zabuni hiyo na imepewa mkataba wa mwaka mmoja.

Aidha, alisema Kariakoo awali ilikuwa makazi ya watu hivyo walikuwa wakilipa Sh 100, lakini kwa sasa limekuwa ni eneo la kibiashara ndiyo maana imepandishwa na kuwa Sh 500 pamoja na eneo la katikati ya jiji.

“Lengo letu pia ni kupunguza msongamano wa magari katikati ya jiji, magari mengine yanapaki pembezoni tu mwa barabara na kwenye maegesho ya daladala,” alifafanua Makwembe na kuongeza kuwa taratibu zote za kupata kampuni hiyo zilifanyika kwa zabuni kutangazwa, kushindanisha wazabuni mpaka kupatikana kampuni hiyo ambayo ilianza kazi jana.

Aidha, Makwembe alisema; “kuanzia leo wananchi wafahamu tuna wakala mpya wa kukusanya mapato na kwa katikati ya jiji, viwango ndiyo hivyo vilivyoamuliwa watu wanatakiwa kutoa ushirikiano tu.” Alisema wamefuatilia kwa siku ya jana ambapo wameona pamoja na malalamiko ya kiwango hicho cha malipo, lakini hakuna aliyegoma kulipa.

“Awali ilikuwa shilingi mia tatu ambayo ilipitishwa na Baraza la Madiwani mwaka 1998, lakini mwaka 2014 baraza lilipitisha mabadiliko hayo ya kiwango cha tozo la maegesho kwa katikati ya Jiji na Kariakoo. “Suala la kampuni hiyo ni ya kutoka nje, taratibu zote zilifuatwa na akapatikana kampuni ya KAPS tuangalie huduma zake tu, kama hazitaridhisha, zina mapungufu turekebishe na sisi tunaendelea kutoa elimu kwa umma,” alieleza Makwembe.

Alisema kabla ya kuanza kutozwa viwango hivyo vipya, matangazo mbalimbali yalitolewa kupitia vyombo vya habari na pia magari ya vipaza sauti yaliyopita mitaani. Alisema hata hivyo, mbali na katikati ya jiji ambayo ni pamoja na Kariakoo itabaki kuwa Sh 300.

Alisema mpaka sasa Jiji la Dar es Salaam lina maegesho 28,000 na kwamba wanaendelea kuainisha maegesho mengine.

Mwandishi wa habari hizi jana alipita katika baadhi ya maeneo ya katikati ya jiji ambayo ni pamoja na Mtaa wa Samora, fukwe ya mwambao wa bahari ya Hindi katika barabara ya Barack Obama na mitaa mingine na kukuta wafanyakazi wa kampuni hiyo mpya wakitoza Sh 500.

Baadhi ya madereva walilalamikia kiwango hicho, wakidai kuwa imekuwa ghafla kwao kwani hazikutolewa taarifa za kutosha.

Godbless Lema Anyimwa Dhamana Kwa Mara Nyingine Tena

$
0
0

Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imemnyima dhamana Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA) Godbless Lema. Mahakama hiyo imeeleza kuwa mawakili wamtuhumiwa huyo walipaswa kuonesha kusudio la kukata rufaa ndani ya siku10 kabla ya kukata rufaa.

Hii ni mara ya tano mbunge huyo anakosa dhamana mahakamani tangu alipokamatwa Novemba 3 mwaka huu akiwa mjini Dodoma na kusafirishwa hadi Arusha katika kesi ya uchochezi inayomkabili.

Katika kesi ya msingi lema anatuhumiwa kutoa maneno ya kichochezi dhidi ya Rais Magufuli kwa madai kuwa Mungu ndiye aliyemwambia maneno hayo wakati akiwa anaomba.

TUNDU Lissu : Tunakuja na Staili Mpya Kumkabili Magufuli

$
0
0
Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amesema kuwa vyama vya  upinzani vimejipanga vizuri kwaajili ya kukabiliana na Rais Dkt. John Magufuli .

Amesema hayo katika Semina iliyowashirikisha viongozi wa vyama vya upinzani kutoka Mataifa 16 iliyofanyika  Makao Makuu ya Chama hicho Kinondoni Jijini Dar es salaam, amesema  wanapambana kuhakikisha  uwanja wa siasa unakuwa sawa lazima wabadili staili ya kumkabili Rais Magufuli.

Lissu amesema watafanya siasa  ikiwa Magufuli anataka ama hataki, ama wanavunja Sheria ama hawavunji” Akipiga marufuku shughuli za kisiasa, hatuwezi kwenda kanisani kuomba, hapana lazima kazi ziendelee katika aina nyingine”amesema Lissu.

Aidha, Lissu ameongeza kuwa katika Uchaguzi uliopita haukuwa wa haki na huru ambapo mawakala waliokuwa wakihesabu kura walikamatwa  na kupelekwa polisi.

Hata hivyo ameongeza kuwa hali ya kisiasa ilivyo kwa sasa kiongozi yeyote atakayefanya siasa anaonekana kama mhalifu na hukamatwa na kupelekwa mahakamani, hivyo hakuna Demokrasia bali kuna udikteta mkubwa.

MAMBO Yanayoshusha Thamani ya Mwanaume Mbele ya Mwanamke

$
0
0
Katika uhusiano baina ya mume na mke hutokea mambo mbalimbali yanayoimarisha uhusiano baina yao au kuuharibu. Baadhi ya nyakati mwanaume hufanya baadhi ya mambo yanayomshusha thamani mbele ya mwanamke. Hivyo, wanaume wote wenye khofu ya heshima na thamani yao kuanguka, ninawaletea mambo muhimu ambayo yanashusha thamani ya mwanaume mbele ye mwanamke:

1. HADAA NA UNYONYAJI:
Baadhi ya wanaume ni wazuri sana katika kumnyonya mwanamke kwa kutumia kisingizio cha mapenzi. Wanazitumia mali zake na kuzinyonya kwa kutumia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na maneno matamu ya mapenzi au kutengeneza simulizi za uongo kuhusu matatizo ya kipesa na kiuchumi. Mwanamke akigundua kuwa analaghaiwa, basi atamshusha thamani haraka mwanaume huyo na kuamua kujitenga naye. Na iwapo ataendelea kuwa naye, basi hasara na majuto yatakuwa juu ya mwanamke huyo.

2. WANAWAKE WENGI:
Mwanamke anapenda ahisi kuwa yeye ndiye mtu pekee katika maisha ya mwanaume. Kuwa na uhusiano na wanawake wengi wasiokuwa na ukomo, husababisha katika kushusha heshima yake mbele ya mkewe. Tambua kuwa hiyo sio sifa nzuri ya kujivunia.

3. UONGO:
Urongo ni miongoni mwa mambo ambayo mwanamke huchukia sana kuyaona kwa mwanaume. Kuna wanaume hodari katika kutunga na kusema uongo. Lakini mwanamke akigundua kuwa unamuongopea, basi heshima na thamani yako itakuwa imeshuka kabisa machoni mwake hata kama ataamua kuendelea kuishi nawe.

4. UKOSEFU WA HESHIMA:
Utovu wa heshima ni miongoni mwa mambo yanayoharibu uhusiano maridhawa baina ya wanandoa hata kama kutakuwa na mambo yanayowaunganisha. Hivyo, ewe mwanaume mwenzangu, usiishushe haiba ya mkeo kwa lugha chafu au kumdhalilisha. Usishushe thamani ya vitu anavyovifanya kwa ajili yake hata kama vitakuwa vidogo. Daima jitahidi kuwaheshimu ndugu zake kwa sababu ukifanya kinyume na hivyo, thamani yako mbele yake itashuka, hata kama hatakwambia.

5. KUTOMUAMINI:
Kuaminiana ni miongoni mwa mambo mazuri ambayo yakipatikana katika mapenzi ya wawili, huwasaidia kukabiliana na vikwazo na changamoto mbalimbali. Ikiwa mume ni mtu anayetilia shaka maneno na matendo ya mke kila siku, thamani yake machoni mwa mkewe itashuka. Kuaminiana kuna mafungamano makubwa sana na upendo na kujiamini. Iwapo kutakuwa na ulegevu katika jambo hilo, mahabba yao hayatakuwa maridhawa.

GIGY Money Adai Alikiba Alikuwa Anamhonga Vizuri Kuliko Wanaume Wengine

$
0
0
Video queen Gigy Money amedai kati ya wanaume wake wote hawezi kumsahau Alikiba, kwani muimbaji huyo wa Aje ndiye mwanaume wake ambaye alikuwa anamhonda vizuri kuliko wanaume wake wengine.

Akiongea na Bongo5 wiki hii, Gigy amedai aliweza kusoma kutokana na pesa ambazo alikuwa akihongwa na muimbaji huyo.

“Mimi kuwa naye nilikuwa napata kitu sikuwa pale bure bure, na kusema kweli alikuwa ananihonga kuliko wanaume wote na nilikuwa nasoma,” alisema Gigy.

Mrembo huyo amedai anahisi Alikiba hajataka awe video queen kwenye video zake kutokana na kuwa naye kwenye mahusiano katika kipindi cha nyuma.

MBWANA Samatta Apachika Mabao Mawili...Aongelea Kuhusu Kasi yake Kupungua

$
0
0

Kwa muda wa saa 15 na dakika 11, sawa na miezi mitatu, mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta alikuwa kizani bila bao kutoka mguuni mwake.

Siku zote, raha ya soka ni mabao, lakini kwa Samatta, ukame wake uliodumu kwa muda mrefu ulimalizika juzi alipoiongoza timu yake, RCK Genk kuichapa Waasland-Beveren kwa mabao 3-1 katika mchezo wa Kombe la Ubelgiji, akifunga mabao mawili.

Samatta alifunga mabao hayo kipindi cha kwanza na pia jingine la Mnigeria Onyinye Ndidi yaliiwezesha Genk kusonga mbele hadi hatua ya 16 bora ya kombe hilo.

Mara ya mwisho, Samatta alifunga bao Agosti 25 kwenye mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Ulaya (Europa League) na Genk iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Lokomotiva.

Baada ya hapo, alicheza mechi 19 za ligi na mashindano mengine Ulaya bila bao na kupoteza namba kwa mshambuliaji raia wa Ugiriki, Nicos Karelis aliyeonekana kujimilikisha kwa muda namba kwenye kikosi cha kwanza.

Moja ya sababu zilizomgharimu Samatta uwanjani ni maumivu, ingawa yeye alikiri kuwa kupata upinzani mkali kutoka kwa Karelis.

“Ninayecheza naye (Karellis) anafanya vizuri, yuko kwenye kiwango kizuri, anafunga karibu kila mechi, kwa hiyo anastahili kuanza.

“Binafsi, niliathiriwa na majeraha yaliyosababisha kasi yangu ipungue, lakini nitahakikisha najituma zaidi kuanzia mazoezini hadi nirejee kwenye kiwango changu,” alisema Samatta.

Samatta anaonekana kumhofia Karelis, ingawa kwa mfumo wa soka la kisasa, anapaswa kuwachunga pia Leon Bailey na Leandro Trossard.

Samatta amefunga mabao tisa katika dakika 1,579, wakati Karelis ana mabao 14 na dakika 2,340. Trossard ana mawili na dakika 756, huku Bailey ana manane katika dakika 2,273.

VIDEO: Watoto wa Mbunge Lema walivyoshuhudia Baba yao akirudishwa rumande

$
0
0
Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema amekosa tena dhamana leo December 2 2016 na kurudishwa rumande kwenye kesi inayomkabili ya kutoa maneno ya uchochezi kwa viongozi wa nchi akiwemo Rais.

Miongoni mwa waliokuwepo Mahakamani ni familia yake Mke na Watoto ambao walimpungia wakati akiondoka Mahakamani hapo, unaweza kutazama hii video fupi hapa chini…

Vijana 29 Huambukizwa UKIMWI Kila Saa Moja

$
0
0
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF linasema vijana 29 huambukizwa virusi vya ukimwi, VVU kila saa moja.

Katika ripoti yake mpya iliyotolewa leo, UNICEF inasema maambukizi mapya ya VVU miongoni mwa vijana yanakadiriwa kuongezeka kutoka 250,000 mwaka 2015 hadi kufikia 400,000 ifikapo mwaka 2030.

Ripoti hiyo inapendekeza mikakati ya kuongeza kasi katika kuzuia VVU miongoni mwa vijana na kutibu wale ambao tayari wameambukizwa kama vile kuwekeza katika uvumbuzi ikiwemo wa kitaifa, kuimarisha ukusanyaji wa takwimu, kutokomeza ubaguzi na unyanyasaji wa kijinsia na elimu kwa vijana.

Wakati huo huo, kumefanyika kongamano la kimataifa jijini Durban, Afrika Kusini kuhusu Ukimwi ambalo limewaleta pamoja UNICEF, wanaharakati na vijana kutoka kutoka sehemu mbalimbali Afrika kupata maoni yao.

UNICEF inasema mbali na mafanikio mengi yaliyopatikana, ufadhili wa fedha kwa ajili ya kukabiliana na Ukimwi umepungua tangu mwaka 2014.

Install APP ya Blog Hii ya UDAKU SPECIAL Kwenye Simu yako Kutoka Google Play Kusoma Habari Kirahisi

$
0
0

Download  Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu yako Kutoka Play Store Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

Bonyeza Hapa CLICK HERE 



IRENE Uwoya Aachana na Bongo Movie, Asema Haiuzi Tena Siku Hizi

$
0
0
Msanii Irene Uwoya amesema sasa hivi haigizi tena movie kwa kuwa soko lake limedoda na badala yake atakuwa anacheza series kwani ndio zinazouza
Ila amedai kuna movie walizocheza zamani zinakuwa processed zitatoka:
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live




Latest Images