Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live

MZIKI ya Darassa ilivyogeuka Wimbo wa Taifa Ndani ya Wiki Moja

$
0
0
Hii hutokea kwa nadra sana na tena kwa wasanii wachache tu wenye ngekewa zao. Kama ni soka, basi Darassa amepiga hat-trick. Kama Utanipenda, Too Much na Muziki ni nyimbo zilizobadilisha upepo katika maisha ya muziki ya Darassa.

Kama Utanipenda na Too Much zilikuwa ni kama mvua za rasha rasha zilizoashiria kuwa kuna mvua kubwa inataka kunyesha. Bila promo kubwa, Novemba 23, Darassa aliachia wimbo wake Muziki ambao ungekuja kuwa gia ya mwisho wa kuashiria kuwa gari limeondoka rasmi.

Hii hutokea kwa nadra sana na tena kwa wasanii wachache tu wenye ngekewa zao. Kama ni soka, basi Darassa amepiga hat-trick. Kama Utanipenda, Too Much na Muziki ni nyimbo zilizobadilisha upepo katika maisha ya muziki ya Darassa.

Kama Utanipenda na Too Much zilikuwa ni kama mvua za rasha rasha zilizoashiria kuwa kuna mvua kubwa inataka kunyesha. Bila promo kubwa, Novemba 23, Darassa aliachia wimbo wake Muziki ambao ungekuja kuwa gia ya mwisho wa kuashiria kuwa gari limeondoka rasmi.

Naye mrembo mwingine, Elizabeth ‘Lulu’ Michael amepost video akifurahia wimbo huo na kuandika: Mama Micah on the One n Two…Shikamoo @laviemakeup Sio Simba,Sio Chui,Sio Mamba….Kazi Yangu Tu inatosha kujigamba 💃Nasikia huu ni Wimbo wa Taifa😝.”

“Mimi Wakazi nasema hivi, Ndio Kwa sasa DARASSA is one of the hottest rap artist in the country, period. (Nilikuwa Dodoma na Wimbo wake mpya unafanya vizuri kuliko hata wa Wasafi mpya,” aliandika Wakazi.

Naye producer Jors Bless ameandika: Jamaa ameula bana……. I’m happy he found a style na sound ya kumtambulisha, you listen to nyimbo za Darassa from ile alofanya na Blue I think Heya haye or whatever it’s like from there aliamza kutembea na template ya muziki wake, he found himself….. That’s what wasanii wengi wanafeli, hawajijui wanafit wapi, at the end of the day they want to do everything hence a confusion because there is no identity, darassa found his.”

Ndani ya wiki na nusu, video ya wimbo huu imeshavutia views zaidi ya 788,000 – kitu ambacho ni nadra kwa msanii anayefanya Rap. Umma umeukubali wimbo huu na ni kweli kuwa kile alichokisema katika miongoni mwa nyimbo zake za mwanzo kabisa, ‘Sikati Tamaa’ kimemsaidia kufika hapo alipo leo.

Naamini kuwa Darassa anaelekea kuanza kuifaidi fedha ya muziki ambayo ni wasanii wachache wapo kwenye nafasi hiyo. Kwakuwa kama alivyosema Jors Bless kuwa ametambua sound yake, rapper huyu ataendelea kukwea ngazi na kama ataendelea kutengeneza hits zaidi, Tanzania inaenda kupata msanii mwingine wa rap mwenye ushawishi mkubwa siku za usoni.

Nauona muziki ukitumika kwenye kampeni na matangazo ya biashara ya matangazo makubwa. Kwa jinsi wimbo wake unavyofanya vizuri, rapper huyu hakwepeki kwenye kila tamasha kubwa. Shabiki mmoja anadai kuwa muitikio wa kushangaza wa wimbo wake, unadhihirisha kuwa woga uliopo kuwa timu zinadidimiza muziki wa Tanzania hauna maana. Anaamini kuwa kila msanii atakayeweza kufanya muziki mzuri ana nafasi ya kumega mkate wa tasnia hiyo.

Fredrick Bundala

NISHA: Mimba Hii Ingekuwa ya Baraka The Prince Inge.........

$
0
0
Nyota wa filamu nchini ambaye siku za karibuni amekuwa akihaha na ujauzito alionaonao bila kumuweka wazi muhusika, amekanusha kuwa ujauzito huo ni wa msanii Baraka The Prince.

Nisha Baby amefunguka kuhusiana na hilo akiwa katika kipindi cha FNL cha EATV, na kusema kuwa endapo ujauzito huo ungekuwa wa Baraka kama inavyosemwa na wengi basi ungetoka wenyewe mapema sana kwa kuwa Baraka ni miongoni mwa wanaume asiowapenda kabisa duniani.

"Kama hii mimba ingekuwa ya Baraka, ingetoka yenyewe, wala isingesubiri" Alisema Nisha.
Kuhusu muhusika wa ujauzito huo, Nisha ameendelea kufanya siri na kuapa kutomtaja kabisa hata siku moja licha ya watu kutaja baadhi ya majina ya watu maarufu ambao amekanusha kuwa siyo wahusika.

Katika hatua nyingine Nisha aliweka wazi kuwa anatarajia kujifungua mtoto wa kiume, licha ya kuwa bado hajamtafutia jina.

Kuhusu mazingira aliyopata ujauzito huo, Nisha ambaye alijikuta akimwaka chozi studio, alisema mwanaume aliyempa ujauzito alimlazimisha kufanya naye mapenzi, na kwamba ahaikuwa ridhaa yake na ndipo ikatokea hivyo.

Kuhusu hoja za baadhi ya mashabiki kuwa ni kwanini hakuitoa kama hakuwa tayari, Nisha alisema imani yake ya dini haimruhusu kutoa mimba.
"Ingawa kuzidi ni dhambi, lakini kutoa mimba pia ni dhambi na dini zote haziruhusu kutoa mimba"

Situmii Dawa za Kutunisha Misuli - Young Dee

$
0
0
Msanii wa hip hop nchini Paka Rapa (Young Dee) amesema hatumii dawa zozote za kukuza misuli yake na mwili wake bali anafanya mazoezi kila siku na bado hajafikia katika kiwango ambacho anataka kufikia.

Hata hivyo akiongea kupitia eNewz, Young Dee amesema anazingatia chakula, muda  wa mazoezi na muda wa kupumzika na pia anazingatia sana chakula  chenye protini na mahali pazuri pa kulala, hizo ndizo sababu ambazo zinampelekea kuwa na mwili mkubwa kwa sasa.

Pia Yong Dee amemalizia kwa kusema kwamba hajawahi kuachana na mpenzi wake Tunda hivyo hata sasa Tunda anavyomposti katika mitandao yake na kumshukuru Young Dee ni kutokana na ushauri ambao alimpa hivi karibuni kuhusiana na maisha yake.

TAZAMA VIDEO MPYA: Vanessa Mdee Ametuletea Hii Inaitwa ‘Cash Madame’

$
0
0
Muimbaji wa Bongofleva Vanessa Mdee leo Jumatatu ya December 5 2016 ameamka na good news kwa mashabiki wake, Vanessa ameamua kuiachia video yake mpya inaitwa ‘Cash Madame’ director ni Justin Campos, enjoy dakika 3 za video yenyewe mtu wangu. VIDEO:

SERIKALI yatangaza Adhabu Mpya Kwa Wala Rushwa

$
0
0
Serikali imeeleza dhamira yake ya kuongeza adhabu kwa watu wanaobainika kuhusika na rushwa ili wawe wanalipa fidia ya hasara iliyojitokeza mbali na kutumikia kifungo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mh. Angellah Kairuki amesema kuwa adhabu zinazotolewa kwa wala rushwa ni ndogo ikilinganishwa na hasara wanayoisababishia serikali, hivyo marekebisho ya sheria hizo itamtaka mlarushwa kulipa fidia ya hasara iliyojitokeza

Akiongea na waandishi wa habari, mara baada ya kuzinduliwa kwa wiki ya kupokea malalamiko ya wananchi, katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Mhe Angella amesema serikali itahakiki mali za viongozi wa serikali wapatao 500 na kuwataka wananchi kujitokeza kuhakiki mali za viongozi wao pamoja na kutoa taarifa ambazo serikali haikufanikiwa kuzipata.

MWANAUME Ongeza Ukumbwa wa Umbile (Cassava) lako Kwa Kutumia Kifaa cha Handsome Up....

$
0
0

Handsome up ni kifaa chenye uwezo wa 99% kuongeza uume kwa uhakika na bila madhara. Inapatikana kwa @170,000/=tu. PIA kuna Gely ya kupaka @ 120,000/= na Vidonge maalum kwa ajili ya kuongeza nguvu na hamu ya tendo la ndoa @120,000/=.
Wasiliana nasi kwa no (+ 255 ) 0767447444 au
0714335378.
Follow us
@Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr

DONALD Trump Amteua Ben Carson Kuwa Waziri wa Makazi

$
0
0
Donald Trump amemteua mmoja wa washindani wake kuwa Waziri wa makazi na ustawi wa miji.
Rais huyo mteule amesema amefurahishwa sana kumteuwa Dkt. Ben Carson ambae amemtaja kama aliye na uwezi wa kuimarisha masuala ya jamii.

Ben Carson alistaafu kama daktari wa upasuaji wa kichwa.

Mwandishi wa BBC mjini Washington Marekani amesema bwana Trump na Carson wananuia kuwavutia wafuasi wa chama cha Republican ambao wametaka uwongozi uwepo kwa watu wasio ya uzoefu wa kisiasa.

Dkt Ben Carson ana ushawishi mkubwa miongoni mwa Wamarekani wa madhehebu ya kiinjilisti.

ROMA Awachana Warembo Bongo Movie, Amtahadharisha Darasa

$
0
0
Kweli bongo movie mmedharaulika sana, mkoje nyie lakini? Mbona miaka fulani waimbaji walikuwa wanakimbilia kwenu leo wanawacheka?

Hata Marekani Jay Z hawezi kumdharau Denzel au Tom Cruise hata kama kamzidi hela. Filamu ni tasnia inayoheshimika sana kasoro hapa kwa nyie wa Bongo Movie.

Jisomee Hapa Alichosema Mwanamuziki ROMA:


VIDEO: Dereva wa Basi la Abiria Apagawishwa na Nyimbo Mpya ya Darasa..Aachia Usukani na Kuanza Kucheza Wimbo Huo Huku Basi Linaenda

$
0
0
Dereva huyo ambaye ameonekana kwenye video akiwa anaendesha gari aina ya Coster ambayo inafanya safari zake Dodoma kwenda itigi akiwa anafanya kitendo cha hatari cha kuacha gari likiwa kwenye mwendo na kisha yeye kusimama na kuanza kucheza muziki huo 
TAZAMA VIDEO:

AUDIO:Kijana Mzalendo Atoa Sababu za Kufungwa Kwa Kiwanda cha Dangote

$
0
0
Sikiliza Hapa Audio Kijana Mzalendo Akitoa Sababu za Kufungwa Kwa Kiwanda cha Dangote
Bonyeza Hapa Chini:

FUNDI Pancha Atupwa Jela Miaka 30 Kwa Kukutwa na Misokoto 601 ya Bangi

$
0
0
Fundi wa kuziba pancha, Harson Solomon (38), mkazi wa wilayani hapa amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kutiwa hatiani kwa kupatikana na misokoto 601 ya bangi.

Kifungo hicho kimeangukia sheria mpya ya udhibiti wa dawa za kulevya iliyosainiwa Mei 11, 2015 na aliyekuwa Rais wakati huo, Jakaya Kikwete. Imeelezwa Solomon ni miongoni mwa washtakiwa wa mwanzo kufungwa kwa sheria hiyo.

Awali, sheria ilikuwa inatoa mwanya wa faini na mtu anaposhindwa kulipa ndipo hutumikia kifungo jela lakini hivi sasa anayepatikana na hatia ya kukutwa na kiwango kikubwa hutupwa jela.

Kifungu cha 11(1) D cha sheria hiyo mpya, kinaeleza wazi mtu anayezalisha, kumiliki, kuuza, kununua au kusafirisha dawa za kulevya ikiwamo bangi, adhabu ya chini ni kifungo cha miaka 30 jela.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Joachim Tiganga baada ya kuridhishwa bila kuacha shaka na ushahidi wa upande wa mashtaka.

Wakili wa Serikali, Ignas Mwinuka alidai kortini kuwa Desemba 1, 2015 katika maeneo ya Mwika Kimangara, Moshi Vijijini mshitakiwa alipatikana na kiasi hicho cha bangi.

 Pia, anadaiwa kuruhusu eneo lake kutumika kuuza bangi na gongo.

Akisoma hukumu, Hakimu Tiganga alisema matumizi ya dawa za kulevya yanazidi kuongezeka nchini na kuathiri jamii, hivyo Mahakama inatoa adhabu hiyo iwe fundisho kwa wengine.

Katika kipindi chote tangu afikishwe kortini kwa mara ya kwanza Desemba 11 mwaka jana, mshtakiwa alikana mashtaka hadi alipotiwa hatiani na kuhukumiwa jana.

TOP 5 ya Wasanii wa Bongo Waliomake Mkwanja Mrefu Kwa Huu Mwaka 2016

$
0
0
1.Diamond
Huu jamaa katengenza hela nyingi sana mwaka kuanzia kwny endorsement zake, show, kuuza mziki kwny digital platform plus label yake inayomwingzia mkwnja day after day

2.A.Y
Japo jamaa hategemei sana kwenye mziki kwa asa ivi ila kutokana na miladi yake kwa mfano ana kipindi eatv ambacho kwa mtazamo tu wa kawaida kinamwingizia mpunga wa kutosha kabisa

3.Weusi
Hawa jamaa nao kwa huu mwaka ulikuwa poa sana kwako maana wametoa ngoma Kali sana ambazo zimewapatia show za kutosha na zenye mkwanja mwingi

4.Navy kenzo
Hawa jamaa ni kati ya makundi yanoyofanya vizuri sana kwny huu mziki wa bongo flava na wamewaza kupata endorsement airtel ambayo nahisi iliwatengenezea mkwanja mwing sana plus wana studio yao the industry ambayo nayo inaingiza mpunga wa kutosha

5.Lady Jay dee
Binti machozi ukipenda mwite komando au anaconda, tokea arudi na ngoma yake ya ndi ndi ndi baada ya kukaa kimya takriban mwaka mmoja imemuweka pazuri kufanya show za kutosha tena zake yeye mwenyewe plus show kali kabisa aliyoifanya pale mlimani city ambapo kiingilio cha chini ilikuwa 50,000Tsh.

Huwo ndo mtazamo wangu
By Isho_boy

DEREVA Aliyeachia Usukani wa Basi Huku Akicheza Wimbo wa Darasa Mikononi Mwa Polisi Kwa Kuhatarisha Maisha ya Abiria

$
0
0
Yule Dereva aliyepagawa na nyimbo Mpya ya Darasa na kisha kuacha kuendesha Gari na kisha kuanza kucheza mziki huo huku gari hilo likiwa kwenye mwendo akamatwa na Polisi..

Hawa ndio wahusika walio kuwepo kwenye tukio hilo..


Dereva huyo ambaye ameonekana kwenye video akiwa anaendesha gari aina ya Coster ambayo inafanya safari zake Dodoma kwenda itigi akiwa anafanya kitendo cha hatari cha kuacha gari likiwa kwenye mwendo na kisha yeye kusimama na kuanza kucheza muziki huo akamatwa na Polisi na kesho atapandishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazo mkabili yeye pamoja na wenzake ambao alikuwa nao kwenye Gari hilo.
Kama Hujaona Hiyo Video Hii Hapa Chini:

IRENE Uwoya Afunguka Haya Baada ya Gazeti Moja Kudai Anamchukia Wema Sepetu

$
0
0
Baada ya gazeti la Ijumaa kutoka na stori “Uwoya: Simpendi Wema” katika ukurasa wake wa mbele, muigizaji wa filamu Irene Uwoya amekanusha madai hayo kupitia ukurasa wake wa instagram.

Pia muigizaji huyo amedai yeye hana tatizo na Wema na sio mtu wa kuwekeana chuki na msanii mwenzake.

Kupitia instagram, Irene aliposti kipande cha gazeti hapo juu na kuandika

“Jamaniii sijawah sema simpend wema… Sina sababu ya kumchukia mim na mpenda kila Mtu na sinaga adui na wala sipend Kuwa na maadui na penda sana kuishi na watu vizuri… Hivo Ndivo nilivyo.”

Pia muigizaji huyo amedai wakati mwingine bifu huanzisha na waandishi wa habari pamoja na mashabiki.

DIAMOND na Mrembo Huyu wa Zimbabwe Wateka Vichwa vya Habari (Video)

$
0
0
Kwenye interview niliyofanya na Diamond hivi karibuni, nilimuuliza kuhusu kuandamwa na tetesi za kumsaliti mchumba wake Zari na jinsi anavyozichukulia. Katika moja ya majibu yake, staa huyo alisema, “There is no way simba akapita katika zizi la swala akaondoka watu wakasema hakula swala hata mmoja, watasema tu alikula hata kama hakula.”


Na sasa maneno yake huenda yakawa yametimia. Ni kwasababu, Simba anasingiziwa kula swala mzuuuuri wa Zimbabwe, jina lake wa kuitwa Jackie Ngarande.


Ilianza kama utani baada ya Diamond kuita msichana wa kujumuika naye wakati akiimba wimbo wake Kamwambie kwenye ukumbi wa HICC wa Harare mbele ya mashabiki zaidi ya 7,000 waliokuwa wakitazama show hiyo.



Kwa mujibu wa mshiriki wa shindano la Big Brother Afrika, Pokello Nare aliyeipost video hiyo juu kwenye akaunti yake ya Instagram, walimchagua Jackie kwenda kumpa kampani fupi Diamond juu ya steji hiyo kwakuwa waliamini kuwa ni chumaa haswaaa!

“When @diamondplatnumz asked if Zim had sexy women.We sent in a representative😄😄😄 @jackiengarandeofficial on shift for #TeamSexyZimWomen,” aliandika Pokello.

Muda mfupi baadaye, zikazuka tetesi kwenye blog mbalimbali za Zimbabwe kuwa Diamond na mrembo huyo walionana kabla. Page ya Instagram ya TZShaderoom, ilikuza zaidi tetesi hizo kiasi cha kumfanya mrembo huyo kuzungumza yake na kukanusha yanayosemwa.

“I am not sure were you got this information ,but well .I think as a gossip blogger sometimes its good to do your own research before you attach people’s name’s on lies and stories that can cause malicious damage’s and bad reputation on one’s name,” aliandika Jackie.

“The problem is that i don’t understand Swahili so it took me time to look for a translater so i could reply you. My main worry is that you are more interested in lies than the truth. Nothing is permanent in this wicked world not even your gossip or lies will not last forever. Im sure the person who feeding you all this is up for my downfall but Guess what ,I serve a bigger GOD. I had to leave my throne to address a peasant like you ..because you know what I usually do not leave the throne ..👑👑👑👑👑👑,” aliongeza.

“Divert this energy you waste writing gossips into things that are productive and beneficial to you and your future .Unless you are a gettting paid to write lies i will say Madam /Sir @tzshaderoom
Continue doing your work for your salary is going to deposited into your bank account.Other than that Sorry for you 😢😢😢😢.”

TAFSIRI:

Sina uhakika ni wapi umepata hizi taarifa, lakini sawa. Nadhani kama blogger wa udaku wakati mwingine ni vizuri ukafanya utafiti wako mwenyewe kabla ya kuambatanisha majina ya watu kwenye habari za uongo ambazo zinaweza kusababisha madhara na sifa mbaya kwa jina la mtu. Tatizo ni kwamba, sielewi Kiswahili hivyo ilinichukua muda kutafuta mtu wa kutafsiri ili niweze kukujibu. Hofu yangu kubwa ni kwamba unavutiwa zaidi na uongo kuliko ukweli. Hakuna kitu cha muda wote kwenye ulimwengu huu katili; hata umbea wako au uongo utaweza kukaa milele. Ninaamini mtu anayekulisha yote haya anataka nianguke lakini, ninamhudumia Mungu mkubwa. Imebidi niache kitI changu cha enzi ili nikujibu mkulima kama wewe sababu siku zote huwa sikiachi. Peleka nguvu hii unayopoteza kuandika udaku kwa vitu vingine vyenye maana na faida kwako na siku zako za usoni. Labda kama unalipwa kwa kuandika uongo nitasema endelea kufanya kazi yako kwakuwa mshahara wako unaenda kuweka kwenye akaunti yako ya benki. Tofauti na hayo, pole kwako

Pamoja na tetesi hizo, show ya Diamond inadaiwa kuwa ya kihistoria na ameacha heshima kubwa kwenye nchi hiyo inayotawaliwa na Robert Mugabe.

Imeandikwa na Fredrick Bundala Bongo5

Mjamzito Mbaroni Kwa Kujipasua Tumbo Ajiue

$
0
0

POLISI mkoani Ruvuma linamshikiria Eva Kapinga (20), Mkazi wa Kata ya Mateka Halmashauri ya Manispaa ya Songea, kwa tuhuma za kumuua mtoto wake, Catherine Kapinga,mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu kisha kujichoma na kisu tumboni kwa lengo la kutaka kujiua na kumsababishia jeraha kubwa na kulazwa.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji, alisema tukio hilo lilitokea Desemba 1 mwaka huu ya saa 1:30 jioni katika Mtaa wa Mateka C Kata ya Mateka Tarafa ya Songea Magharibi.


Alisema inadaiwa Catherine aliuawa na mama yake mzazi Eva.


Alisema sababu za mauaji hayo hazijafahamika licha ya taarifa za awali kudai kuwa Eva alikuwa na malumbano kati yake na mama yake mzazi, Sofia Mayunga, ambaye alikuwa akimuuliza kwanini ameamua kushika mimba wakati anajua kuwa ana mtoto mdogo wa umri wa mwaka mmoja, jambo ambalo lilimkasirisha na kuamua kujichoma kisu tumboni kwa lengo la kujiua.


Kwa mujibu wa Mwombeji, Eva baada ya kujichoma kisu tumboni inadaiwa watu waliokuwa jirani walimkimbiza kwenye Hospitali ya Mkoa na taarifa za tukio hilo zilikuwa zimeshafikishwa Polisi na kwamba askari walipofika kwenye eneo la tukio wakiwa wameongozana na mganga walikuta Catherine ameshafariki dunia na baadaye walikwenda Hospitali ya Mkoa na kumkuta Eva amelezwa akiwa na hali mbaya akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi.


Hata hivyo, Kamanda Mwombeji alisema wanaendelea na uchunguzi wa kina kuhusiana na tukio hilo na kwamba utakapokamilika mtuhumiwa Eva atafikishwa mahakamani.

Nyota Mzimabwe Jah Prayzah katika kashfa ya kukopi video ya Diamond Plutnumz

$
0
0
Nyota wa muziki maarufu nchini zimbabwe Jah Playzah amekumbwa na kashfa kubwa ya kukopi kila kitu video ya wimbo ya wimbo wake jarusarema kutoka katika video ya wimbo mdogomdogo ya mwanamuziki Diamond Plutnumz wa Tanzania. hata hivyo imekuja kugundulika baadae kabisa wakati nyota huyo mzimbabwe akiwa keshabeba tuzo mbali mbali kupitia video hiyo.

Cheki video hiyo hapo:

NAMPENDA Mume Wangu Lakini Haniridhishi Tukiwa Faragha

$
0
0
Nampenda sana mume wangu lakini nimeboreka nae! in the bedroom ndio hata usiseme! yaani hata nikikaa mwezi hatujakutana siku ikitokea mechi najua kabisa anaanzia wapi atafanya nini, hayuko creative kabisa.

Najaribu kufanya changes try new positions ila yeye wala. Inaniboa! yaani I can only dream mechi za stori za sinema za x hahaha! ana mashine nzuri lakini utaalam ziro. mpaka nimenunua kitabu flani cha positions hakya nani.

Hayo yote sijawahi kucheat...ivi kuna unyago for men? nakiri kwa kweli niko shy kidogo kumpa somo, jinsi ya kuhandle mwanamke. nifanyeje?

WELEDI wa Prof Rwekaza Mukandala Aongezewa Muda wa Mwaka Mmoja Kuongoza UDSM Baada ya Kustaafu

$
0
0

MKUU wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambaye ni Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete baada ya mashauriano ameafikiana na Rais John Magufuli kuongeza muda wa Makamu Mkuu wa chuo hicho wa sasa, Profesa Rwekaza Mukandala kwa muda wa mwaka mmoja.

Katika taarifa aliyoituma kwa vyombo vya habari jana, Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho, Peter Ngumbullu alisema uamuzi huo unaanza mara moja.

Ngumbullu alisema muda wa Profesa Mukandala ulimalizika Desemba 4, mwaka huu.

Profesa Mukandala aliteuliwa kwa kipindi cha sasa cha miaka mitano kilichoanza Desemba 5, 2011 na kumalizika Desemba 4, mwaka huu.

Profesa Mukandala alisema alikuwa tayari ameshajitayarisha kwamba juzi angekabidhi madaraka hayo kwa mtu mwingine, lakini kwa imani waliyokuwa nayo uongozi wa chuo hicho uliridhia aendelee kwa mwaka mwingine.

“Viongozi wa chuo hiki wakishirikiana na Rais John Magufuli wamekuwa na imani na mimi na kuniongezea mwaka,” alisema Profesa Mukandala.

Amewashukuru waliomchagua na ameahidi kuendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na viongozi wote na jumuiya ya wanachuo ili Udsm iendelee kuwa bora. Pia alisema ataendelea kuenzi na kutunza tunu ya chuo hicho iliyoachwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanataaluma (UDASA), Dk George Kahangwa alisema kuna mambo mengi Profesa Mukandala alikuwa bado anayafanyia kazi hayajakamilika, hivyo wakati anamalizia kipindi chake, ikatokea akachaguliwa mkuu mpya wa chuo hicho Kikwete.

Dk Kahangwa alisema hivyo inabidi akamilishe mambo yaliyo mezani kwake wakati wamempata mkuu huyo mpya wa chuo Kikwete.

“Hii inatoa nafasi ya kufanya utafiti mzuri ili ajaye apatikane mwenye sifa zote ambazo wahusika watakuwa wamejiridhisha,” alieleza na kuongeza kuwa wanataaluma si ajabu mtu akastaafu lakini akaongezewa muda kutokana na umuhimu wanaokuwa nao.

Alisisitiza kwao wanajumuiya ya chuo hicho lililo la muhimu ni Profesa Mukandala kuwapatia Chuo Kikuu wanachokitaka. Naye Rais wa Serikali ya Wanachuo Udsm (Daruso), Leon Erasmi alisema amefurahishwa na hilo kwa kuwa Profesa Mukandala amekuwa na ushirikiano mzuri na wanafunzi.

“Mukandala amekuwa ni kiongozi mzuri tumejifunza mengi kutoka kwake. Ofisini kwake wanafunzi kumuona ni muda wowote pia amekuwa akishughulikia changamoto tulizonazo au kutuelekeza kwa mtu mwingine huku akifuatilia kwa ukaribu,” alieleza Erasmi

Mzee wa Miaka 75 Ameweka Bango Lenye Sifa za Mke Anayemtaka, Katikati ya Mtaa Anaoishi

$
0
0

Mzee wa miaka 75 nchini Tanzania ameweka bango lenye sifa za mke anayemtaka, katikati ya mtaa anaoishi.
Athuman Bakari Mchambua mkazi wa Dar es Salaam amechukua hatua hiyo baada ya kifo cha mke wake.
Amesema hawezi kutumia njia nyingine yoyote isipokua udahili ama mahojiano kumpata mke. - BBC
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live


Latest Images